:
Tafsiri ya Surat An-Najm
Tafsiri ya Surat An-Najm
Imeteremka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
: 1 - 18 #
{وَالنَّجْمِ إِذَا هَوَى (1) مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَى (2) وَمَا يَنْطِقُ عَنِ الْهَوَى (3) إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَى (4) عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَى (5) ذُو مِرَّةٍ فَاسْتَوَى (6) وَهُوَ بِالْأُفُقِ الْأَعْلَى (7) ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّى (8) فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَى (9) فَأَوْحَى إِلَى عَبْدِهِ مَا أَوْحَى (10) مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَى (11) أَفَتُمَارُونَهُ عَلَى مَا يَرَى (12) وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَى (13) عِنْدَ سِدْرَةِ الْمُنْتَهَى (14) عِنْدَهَا جَنَّةُ الْمَأْوَى (15) إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَى (16) مَا زَاغَ الْبَصَرُ وَمَا طَغَى (17) لَقَدْ رَأَى مِنْ آيَاتِ رَبِّهِ الْكُبْرَى (18)}.
1. Ninaapa kwa nyota inapotua. 2. Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea. 3. Wala hatamki kwa matamanio. 4. Hayakuwa haya ila ni ufunuo uliofunuliwa. 5. Amemfundisha aliye Mwingi wa nguvu. 6. Mwenye kutua, akatulia. 7. Naye yuko juu kabisa upeo wa macho. 8. Kisha akakaribia na akateremka. 9. Akawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi. 10. Akamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alichomfunulia. 11. Moyo haukusema uwongo uliyoyaona. 12. Je, mnabishana naye kwa aliyoyaona? 13. Na akamwona mara nyingine. 14. Penye Mkunazi wa mwisho. 15. Karibu yake ndiyo ipo Bustani ya mbinguni inayokaliwa. 16. Kilipoufunika huo Mkunazi hicho kilichoufunika. 17. Jicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka. 18. Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi.
#
{1} يقسم تعالى بالنجم عند هُوِيِّه؛ أي: سقوطه في الأفق في آخر الليل عند إدبار الليل وإقبال النهار؛ لأنَّ في ذلك من الآيات العظيمة ما أوجب أنْ أقسم به، والصحيحُ أنَّ النجم اسم جنسٍ شامل للنُّجوم كلِّها. وأقسم بالنجوم على صحَّة ما جاء به الرسول - صلى الله عليه وسلم - من الوحي الإلهيِّ؛ لأنَّ في ذلك مناسبةً عجيبةً؛ فإنَّ الله تعالى جعل النجوم زينةً للسماء؛ فكذلك الوحي وآثاره زينةٌ للأرض؛ فلولا العلم الموروث عن الأنبياء؛ لكان الناس في ظلمة أشدَّ من ظلمة الليل البهيم.
{1} Mwenyezi Mungu anaapa kwa nyota inapotua kwenye upeo wa macho mwishoni mwa usiku, wakati usiku unaondoka na mchana unaingia. Kwa sababu katika hili kuna ishara kubwa zilizomfanya kuapa kwayo. Na lililo sahihi ni kwamba jina 'nyota' kama lilivyotumika hapa ni jina linalojumuisha nyota zote. Na aliapa kwa nyota juu ya usahihi wa yale aliyoyaleta Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – ya wahyi wa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu katika hilo kuna uhusiano mkubwa. Kwani hakika Mungu Mwenyezi alizifanya nyota kuwa pambo la mbingu, basi vile vile wahyi na athari zake ni pambo la ardhi. Lau si elimu iliyorithiwa kutoka kwa Manabii, basi watu wangekuwa katika giza zaidi kuliko giza la usiku wa kiza.
#
{2} والمقسم عليه تنزيه الرسول [- صلى الله عليه وسلم -] عن الضَّلال في علمه والغيِّ في قصده، ويلزم من ذلك أن يكون مهتدياً في علمه هادياً حسنَ القصدِ ناصحاً للخلق ، بعكس ما عليه أهل الضَّلال من فساد العلم وسوء القصد، وقال: {صاحبُكم}؛ لينبههم على ما يعرفونه منه من الصِّدق والهداية، وأنَّه لا يخفى عليهم أمره.
{2} Kinachoapishwa hapa ni kwamba Mtume [rehema na amani ziwe juu yake] yuko mbali sana na upotofu katika elimu yake na hata upotofu katika nia yake. Na inalazimu kutokana na hilo kwamba ameongoka katika elimu yake, mwenye kuongoza, mwenye nia njema, mwenye kuwashauri vizuri viumbe, kinyume na waliyo nayo wana upotovu ya elimu mbovu na nia mbaya. Na Mola Mtukufu alisema: "Mwenzenu huyu" ili kuwatanabahisha juu ya yale wanayoyajua juu yake ya ukweli na uwongofu wake, na kwamba mambo yake hayafichikani kwao.
#
{3 - 4} {وما ينطِقُ عن الهوى}؛ أي: ليس نطقُه صادراً عن هوى نفسه. {إن هو إلاَّ وحيٌ يُوحى}؛ أي: لا يتَّبع إلاَّ ما أوحي إليه من الهدى والتقوى في نفسه وفي غيره. ودلَّ هذا على أنَّ السنَّة وحيٌ من الله لرسوله - صلى الله عليه وسلم -؛ كما قال تعالى: {وأنزل الله عليك الكتابَ والحكمةَ}. وأنَّه معصومٌ فيما يخبر به عن الله تعالى وعن شرعه؛ لأنَّ كلامه لا يصدُرُ عن هوى، وإنَّما يصدر عن وحي يوحى.
{3 - 4} "Wala hatamki kwa matamanio" ya nafsi yake. "Hayakuwa haya ila ni ufunuo uliofunuliwa." Yaani hafuati isipokuwa yale yaliyoteremshwa kwake ya uwongofu na ucha Mungu, yeye mwenyewe na katika watu wengine. Hili linaashiria kwamba Sunna ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwenda kwa Mtume wake – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na Mwenyezi Mungu amekuteremshia Kitabu na hekima." Na kwamba amehifadhiwa kukosea katika yale anayoyafikisha kuhusu Mwenyezi Mungu Mtukufu na sheria yake. Kwa sababu maneno yake hayatokani na matamanio yake, bali yanatokana na ufunuo uliofunuliwa.
#
{5} ثم ذكر المعلِّم للرسول [- صلى الله عليه وسلم -]، وهو جبريل عليه السلام، أفضل الملائكة الكرام وأقواهم وأكملهم، فقال: {علَّمه شديدُ القُوى}؛ أي: نزل بالوحي على الرسول - صلى الله عليه وسلم - جبريلُ عليه السلام، شديدُ القُوى؛ أي: شديد القوَّة الظاهرة والباطنة، قويٌّ على تنفيذ ما أمره الله بتنفيذه، قويٌّ على إيصال الوحي إلى الرسول - صلى الله عليه وسلم - ومنعه من اختلاس الشياطين له أو إدخالهم فيه ما ليس منه، وهذا من حفظ الله لوحيه؛ أنْ أرسلَه مع هذا الرسول القويِّ الأمين.
{5} Kisha akamtaja mwalimu wa Mtume [- rehema na amani zimshukie,-] naye ni Jibril, amani iwe juu yake, mbora zaidi wa malaika watukufu, mwenye nguvu zaidi yao wote na mkamilifu zaidi. Akasema: "Amemfundisha Aliye mwingi wa nguvu" ambaye ni Jibril, amani iwe juu yake, mwenye nguvu nyingi za dhahiri na zilizofichikana, mwenye nguvu katika kutekeleza yale aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu kutekeleza, mwenye nguvu katika kufikisha wahyi kwa Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - na kuyazuia yasiibwe na mashetani au kuyatiya yasiyokuwamo. Hili ni katika njia za Mwenyezi Mungu kuhifadhi wahyi wake. Kwamba aliutuma pamoja na mjumbe huyu mwenye nguvu na mwaminifu sana.
#
{6} {ذو مِرَّةٍ}؛ أي: قوَّةٍ وخلقٍ حسنٍ وجمال ظاهرٍ وباطنٍ، {فاستوى}: جبريلُ عليه السلام.
{6} "Mwenye kutua;" yaani, mwenye nguvu, maumbile mazuri, na uzuri wa dhahiri na wa ndani. "Basi akatulia" Jibril amani iwe juu yake.
#
{7} {وهو بالأفقُ الأعلى}؛ أي: أُفق السماء الذي هو أعلى من الأرض ؛ فهو من الأرواح العلويَّة، التي لا تنالُها الشياطين ولا يتمكَّنون من الوصول إليها.
{7} "Naye yuko juu kabisa upeo wa macho" wa mbingu ulio juu kuliko dunia. Kwani yeye ni miongoni mwa roho za juu, ambazo mashetani hawawezi kuzishika wala hawawezi kuzifikia.
#
{8} {ثم دنا}: جبريلُ من النبيِّ - صلى الله عليه وسلم - لإيصال الوحي إليه، {فتدلَّى}: عليه من الأفق الأعلى.
{8} "Kisha akakaribia" Jibril akamwendea Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - ili amfikishie wahyi, "na akateremka" juu yake kutoka kwenye upeo wa macho wa juu kabisa.
#
{9} {فكان}: في قربه منه {قابَ قوسينِ}؛ أي: قدر قوسين، والقوس معروفٌ، {أو أدنى}؛ أي: أقرب من القوسين. وهذا يدلُّ على كمال مباشرته للرسول - صلى الله عليه وسلم - بالرسالة، وأنَّه لا واسطة بينه وبين جبريل عليه السلام.
{9} "Akawa" kwa sababu ya kuwa karibu naye "ni kama baina ya mipinde miwili" inajulikana, "au karibu zaidi" kuliko mipinde miwili. Hili linaashiria kwamba alimwelekea Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – moja kwa moja kikamilifu kwa ujumbe, na kwamba hakukuwa na muunganishi baina yake na Jibril, amani iwe juu yake.
#
{10} {فأوحى} اللهُ بواسطةِ جبريل عليه السلام {إلى عبدِهِ} [محمد - صلى الله عليه وسلم -] {ما أوحى}؛ أي: الذي أوحاه إليه من الشرع العظيم والنبأ المستقيم.
{10} Basi Mwenyezi Mungu "akamfunulia" kupitia Jibril, amani iwe juu yake "mja wake" [Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake] "alichomfunulia" ya sheria kuu, na habari iliyonyooka.
#
{11 - 12} {ما كَذَبَ الفؤادُ ما رأى}؛ أي: اتَّفق فؤادُ الرسول - صلى الله عليه وسلم - ورؤيته على الوحي الذي أوحاه الله إليه، وتواطأ عليه سمعُه وبصرُه وقلبُه ، وهذا دليلٌ على كمال الوحي الذي أوحاه الله إليه، وأنَّه تلقَّاه منه تلقِّياً لا شكَّ فيه ولا شبهة ولا ريبَ، فلم يكذِبْ فؤادُه ما رأى بَصَرُه، ولم يشكَّ في ذلك. ويُحتمل أنَّ المراد بذلك ما رأى - صلى الله عليه وسلم - ليلة أسْرِيَ به من آيات الله العظيمة، وأنَّه تيقَّنه حقًّا بقلبه ورؤيته، هذا هو الصحيحُ في تأويل الآية الكريمة. وقيل: إنَّ المرادَ بذلك رؤيةُ الرسول - صلى الله عليه وسلم - لربِّه ليلة الإسراء وتكليمه إيَّاه. وهذا اختيار كثيرٍ من العلماء رحمهم الله، فأثبتوا بهذا رؤية الرسول - صلى الله عليه وسلم - لربِّه في الدنيا. ولكنَّ الصحيح القول الأول، وأنَّ المراد به جبريل عليه السلام؛ كما يدلُّ عليه السياق، وأنَّ محمداً - صلى الله عليه وسلم - رأى جبريل في صورته الأصليَّة التي هو عليها مرتين : مرةً في الأفق الأعلى تحت السماء الدُّنيا كما تقدَّم، والمرة الثانية فوق السماء السابعة ليلة أسْرِيَ برسول الله - صلى الله عليه وسلم -.
{11 - 12} "Moyo haukusema uwongo uliyoyaona." Yaani, moyo wa Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – na uoni wake uliafikiana juu ya wahyi aliompa Mwenyezi Mungu. Basi kusikia kwake, kuona kwake na moyo wake vyote vikakubaliana juu yake. Huu ni ushahidi wa ukamilifu wa ufunuo ambao Mwenyezi Mungu aliomfunulia, na kwamba alipokea kutoka kwake kupokea ambako hakuna shaka wala mkanganyiko wowote, wala kusitasita. Kwa hivyo moyo wake haukupinga kile ambacho macho yake yaliona, wala haukutilia shaka hilo. Na inawezekana kwamba maana yake ni kwamba kile alichoona Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - katika usiku wa safari yake ya usiku ni katika ishara kuu za Mwenyezi Mungu, na kwamba hakika alikuwa na yakini nazo katika moyo wake na uoni wake. Hii ndiyo tafsiri sahihi ya Aya hii tukufu. Na ilisemekana kwamba maana yake ni kwamba Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - alimuona Mola wake Mlezi katika usiku wa safari yake ya usiku na kuzungumza kwake naye. Maana hii ndiyo chaguo la wanavyuoni wengi, Mwenyezi Mungu awarehemu. Kwa hivyo wakathibitisha kwa hilo suala la Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kumuona Mola wake Mlezi hapa duniani. Lakini kauli sahihi ni ile ya kwanza, na kwamba anayekusudiwa kwayo ni Jibril, amani iwe juu yake, kama inavyoonyeshwa na muktadha kwamba Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alimuona Jibril katika umbo lake la asili mara mbili: Mara moja akiwa juu ya upeo wa macho chini ya mbingu ya chini kabisa, kama ilivyotajwa hapo awali, na mara ya pili akiwa juu ya mbingu ya saba usiku wa safari yake ya usiku.
#
{13 - 14} ولهذا قال: {ولقد رآه نزلةً أخرى}؛ أي: رأى محمدٌ جبريل مرةً أخرى نازلاً إليه، {عند سِدْرَةِ المُنتَهى}: وهي شجرةٌ عظيمةٌ جدًّا فوق السماء السابعة، سميت سدرةَ المنتهى؛ لأنَّه ينتهي إليها ما يعرج من الأرض، وينزل إليها ما ينزل من الله من الوحي وغيره، أو لانتهاء علم المخلوقات إليها؛ أي: لكونها فوق السماواتِ والأرض؛ فهي المنتهى في علومها، أو لغير ذلك. والله أعلم. فرأى محمد - صلى الله عليه وسلم - جبريلَ في ذلك المكان الذي هو محلُّ الأرواح العلويَّة الزاكية الجميلة التي لا يقربها شيطانٌ ولا غيره من الأرواح الخبيثة.
{13 - 14} Ndiyo maana akasema: "Na akamwona mara nyingine." Yaani, Muhammad alimuona Jibril kwa mara nyingine akimshukia, "Penye Mkunazi wa mwisho." Nao ni mti mkubwa sana ulio juu ya mbingu ya saba. Uliitwa Sidrat al-Muntaha kwa sababu kinachopanda kutoka katika ardhi kinaishia hapo, na kinateremkia hapo chochote kinachoteremka kutoka kwa Mwenyezi Mungu ikiwemo ufunuo na mengineyo. Au kwa sababu elimu ya viumbe inaishia hapo, kwa sababu iko juu ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayajua zaidi. Kwa hivyo, Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alimuona Jibril katika sehemu hiyo, ambayo ni makazi ya roho za juu, safi na nzuri ambazo hazikaribiwi na Shetani wala mwingineye miongoni mwa roho chafu zenye uovu.
#
{15} عند تلك الشجرة، {جنَّة المأوى}؛ أي: الجنة الجامعة لكلِّ نعيم؛ بحيث كانت محلًّا تنتهي إليه الأماني، وترغب فيها الإرادات، وتأوي إليها الرغبات. وهذا دليلٌ على أنَّ الجنة في أعلى الأماكن وفوق السماء السابعة.
{15} Kwenye mti huo, ipo "bustani ya mbunguni inayokaliwa." Yaani, bustani ya mbunguni iliyo na kila neema, kiasi kwamba hapo ndipo mahali ambapo matamanio yote yanaishia, ambapo matashi yote yanaishia hapo. Huu ni ushahidi kwamba Pepo iko mahali pa juu kabisa, juu ya mbingu ya saba.
#
{16} {إذْ يغشى السِّدْرة ما يَغْشى}؛ أي: يغشاها من أمر الله شيءٌ عظيم لا يَعْلَمُ وصفَه إلاَّ الله عز وجل.
{16} "Kilipoufunika huo Mkunazi hicho kilichoufunika." Yaani, kitu kikubwa katika amri ya Mwenyezi Mungu, ambacho hakuna anayejua maelezo yake isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
#
{17} {ما زاغ البصرُ }؛ أي: ما زاغ يمنةً ولا يسرةً عن مقصوده {وما طغى}؛ أي: وما تجاوز البصر. وهذا كمال الأدب منه صلوات الله وسلامه عليه؛ أنْ قام مقاماً أقامه الله فيه، ولم يقصِّرْ عنه ولا تجاوزه ولا حاد عنه، وهذا أكمل ما يكون من الأدب العظيم، الذي فاق فيه الأوَّلين والآخرين؛ فإنَّ الإخلال يكون بأحد هذه الأمور: إمَّا أن لا يقوم العبدُ بما أُمِر به، أو يقومَ به على وجه التفريط، أو على وجه الإفراط، أو على وجه الحيدةِ يميناً وشمالاً. وهذه الأمور كلُّها منتفيةٌ عنه - صلى الله عليه وسلم -.
{17} "Jicho halikuhangaika" si kuliani wala kushotoni kutoka pale lilipolenga "na wala halikuruka mpaka." Hili linaonyesha ukamilifu wake wa adabu ya Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, kwamba alisimama mahali ambapo Mwenyezi Mungu alimsimamisha, wala hakupunguza, wala hakupavuka wala hakukengeuka kando. Hii ndiyo hali kamili zaidi ya adabu kuu, ambayo alipita ndani yake wa mwanzo na wa mwisho. Kwani kutokuwa na adabu huwa kwa moja ya mambo haya: Ima mja asifanye alichoamrishwa, au akifanye kwa uzembe, au kwa njia ya kupita kiasi, au kwa njia ya kukengeuka kuliani na kushotoni. Mambo haya yote hayako kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
#
{18} {لقد رأى من آياتِ ربِّه الكُبرى}: من الجنَّة والنار وغير ذلك من الأمور التي رآها - صلى الله عليه وسلم - ليلة أُسْرِي به.
{18} "Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi" kama vile Pepo, Moto na mengineyo miongoni mwa mambo aliyoyaona - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - usiku ule aliosafirishwa kwenda mbinguni.
: 19 - 25 #
{أَفَرَأَيْتُمُ اللَّاتَ وَالْعُزَّى (19) وَمَنَاةَ الثَّالِثَةَ الْأُخْرَى (20) أَلَكُمُ الذَّكَرُ وَلَهُ الْأُنْثَى (21) تِلْكَ إِذًا قِسْمَةٌ ضِيزَى (22) إِنْ هِيَ إِلَّا أَسْمَاءٌ سَمَّيْتُمُوهَا أَنْتُمْ وَآبَاؤُكُمْ مَا أَنْزَلَ اللَّهُ بِهَا مِنْ سُلْطَانٍ إِنْ يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَمَا تَهْوَى الْأَنْفُسُ وَلَقَدْ جَاءَهُمْ مِنْ رَبِّهِمُ الْهُدَى (23) أَمْ لِلْإِنْسَانِ مَا تَمَنَّى (24) فَلِلَّهِ الْآخِرَةُ وَالْأُولَى (25)}.
19. Je, mmemuona Lata na Uzza? 20. Na Manaat, mwingine wa tatu? 21. Je, nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndio awe na wanawake? 22. Huo ni mgawanyo wa dhuluma! 23. Hayo hayakuwa ila ni majina mliyowapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati ila dhana tu na kipendacho nafsi. Na kwa yakini uwongofu ulikwisha wafikia kutoka kwa Mola wao Mlezi. 24. Ati mtu anakipata kila anachokitamani? 25. Mwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye dunia na Akhera.
#
{19 - 20} لما ذَكَرَ تعالى ما جاء به محمدٌ - صلى الله عليه وسلم - من الهدى ودين الحقِّ والأمر بعبادة الله وتوحيده؛ ذَكَرَ بطلان ما عليه المشركون من عبادة مَنْ ليس له من أوصاف الكمال شيءٌ ولا تنفع ولا تضرُّ، وإنَّما هي أسماءٌ فارغة من المعنى سمَّاها المشركون هم وآباؤهم الجهَّال الضلاَّل، ابتدعوا لها من الأسماء الباطلة التي لا تستحقُّها، فخدعوا بها أنفسهم وغيرهم من الضُّلاَّل؛ فالآلهةُ التي بهذه الحال لا تستحقُّ مثقال ذرَّة من العبادة، وهذه الأنداد التي سمَّوها بهذه الأسماء زعموا أنها مشتقَّة من أوصاف هي متَّصفة بها، فسمَّوا اللات من الإله المستحقِّ للعبادة، والعُزَّى من العزيز، ومناة من المنَّان؛ إلحاداً في أسماء الله، وتجرِّياً على الشرك به! وهذه أسماءٌ متجرِّدة من المعاني؛ فكلُّ من له أدنى مُسكةٍ من عقل يعلم بطلان هذه الأوصاف فيها.
{19 - 20} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja yale aliyoyaleta Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ya uwongofu, dini ya haki, kuamrisha kumwabudu Mwenyezi Mungu na kumpwekesha, akataja ubatilifu wa yale wanayoyafanya washirikina ya kumuabudu vile ambavyo havina sifa za ukamilifu na wala havinufaishi wala havidhuru. Bali ni majina matupu yasiyo na maana yoyote, ambayo washirikina hao na baba zao wajinga na wapotovu ndio walivitangulia majina batili ambayo haviyastahiki, kwa hivyo wakajihadaa kwayo wao wenyewe na watu wengine wapotofu. Kwa maana miungu walio katika hali hii hawastahiki hata chembe ya sisimizi kuabudiwa. Na miungu hawa waliowaita kwa majina haya walidai kwamba yalitokana na sifa ambazo vinasifika kwazo. Kwa hivyo wakamwita Al-Lat kutoka kwa neno 'Ilaah;" yaani, Mungu anayestahiki kuabudiwa. Na wakatohoa jina 'Al-Uzza' kutokana na Al-Aziz, na Manat kutokana na Al-Mannan. Walifanya hivi kwa njia ya kuvuka mipaka katika majina ya Mwenyezi Mungu, na kufanya ujasiri wa kumshirikisha! Majina hayo hayana maana hizi hata kidogo, na kila mwenye akili kidogo tu, anajua ubatili wa sifa hizi ambazo miungu hao wanasifika kwazo.
#
{21} {ألكم الذَّكَرُ وله الأنثى}؛ أي: أتجعلون لله البنات بزعمكم ولكم البنون.
{21} "Je, nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndiyo awe na wanawake?" Yaani, je, mnampa Mwenyezi Mungu watoto wa kike kama mnavyodai, na kwamba nyinyi ndio mna watoto wa kiume?
#
{22} {تلك إذاً قسمةٌ ضيزى}؛ أي: ظالمة جائرة. وأيُّ ظلم أعظم من قسمة تقتضي تفضيل العبد المخلوق على الخالق؟! تعالى عن قولهم علوًّا كبيراً.
{22} "Huo ni mgawanyo wa dhuluma!" Basi je, ni dhuluma gani iliyo kubwa zaidi kuliko mgawanyo unaohitaji kumfanya kiumbe bora zaidi ya Muumba? Mwenyezi Mungu yuko mbali mno na kauli yao hiyo.
#
{23} وقوله: {إنْ هي إلاَّ أسماءٌ سمَّيْتموها أنتم وآباؤكم ما أنزل الله بها من سلطانٍ}؛ أي: من حجَّة وبرهان على صحَّة مذهبكم، وكلُّ أمرٍ ما أنزل الله فيه من سلطانٍ؛ فهو باطلٌ فاسدٌ لا يُتَّخذ ديناً، وهم في أنفسهم ليسوا بمتَّبعين لبرهان يتيقَّنون به ما ذهبوا إليه، وإنَّما دلَّهم على قولهم الظنُّ الفاسد والجهل الكاسد، وما تهواه أنفسُهم من الشرك والبدع الموافقة لأهويتهم، والحالُ أنَّه لا موجب لهم يقتضي اتِّباعهم الظنَّ من فقدِ العلم والهدى، ولهذا قال تعالى: {ولقد جاءهم من ربِّهم الهدى}؛ أي: الذي يرشدهم في باب التوحيد والنبوَّة وجميع المطالب التي يحتاج إليها العباد؛ فكلُّها قد بيَّنها الله أكمل بيان وأوضحه وأدلَّه على المقصود، وأقام عليه من الأدلَّة والبراهين ما يوجب لهم ولغيرهم اتِّباعه، فلم يبق لأحدٍ حجَّة ولا عذر من بعد البيان والبرهان، وإذا كان ما هم عليه غايته اتِّباع الظنِّ ونهايته الشقاءُ الأبديُّ والعذاب السرمديُّ؛ فالبقاء على هذه الحال من أسفه السَّفه وأظلم الظلم.
{23} Na kauli yake: "Hayo hayakuwa ila ni majina mliyowapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo." Yaani, hoja na ushahidi juu ya usahihi wa mafundisho yenu hayo. Na kila jambo ambalo Mwenyezi Mungu hakuteremsha juu yake hoja yoyote, basi hilo ni batili na potofu na haliwezi kuchukuliwa kuwa ni dini. Na wao wenyewe hawafuati ushahidi wowote ambao wana uhakika nao juu ya yale wanayoyaamini. Bali kilichowapelekea kusema hivyo ni dhana potofu, ujinga mkubwa, na yale ambayo nafsi zao zinayatamani ya ushirikina na uzushi unaoafikiana na matamanio yao wenyewe, na chochote kile ambacho nafsi zao zinatamani kwa ushirikina na uzushi unaokubaliana na matamanio yao. Na hali halisi ni kwamba hakuna cha kuwalazimu kufuata dhana kama vile kutokuwa na elimu na uwongofu, na ndiyo maaana akasema: "Na kwa yakini uwongofu ulikwisha wafikia kutoka kwa Mola wao Mlezi." Yaani, ambao utawaongoza katika mlango wa kumpwekesha Mwenyezi Mungu, unabii, na mahitaji yote wanayohitaji waja. Hayo yote Mwenyezi Mungu aliyabainisha kwa ufafanuzi kamili, ulio wazi kabisa na wenye kuonyesha zaidi yale yaliyokusudiwa, na akayawekea ushahidi na hoja ambazo zinawalazimu wao na wengineo kumufuata Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo hakubakia yeyote na hoja wala udhuru baada ya ubainifu na kusimamishwa hoja. Na ikiwa wanachokifanya lengo lake ni kufuata dhana, na mwisho wake ni kuwa mashakani milele na adhabu ya kuendelea milele, basi kusalia katika hali hii ndio upumbavu mbaya zaidi na dhuluma kubwa zaidi.
#
{24 - 25} ومع ذلك يتمنَّون الأماني ويغترُّون بأنفسهم! ولهذا أنكر تعالى على من زعم أنه يحصلُ له ما تمنَّى وهو كاذبٌ في ذلك، فقال: {أم للإنسان ما تمنَّى. فللهِ الآخرةُ والأولى}: فيعطي منهما مَن يشاء ويمنع مَن يشاء؛ فليس الأمر تابعاً لأمانيِّهم ولا موافقاً لأهوائهم.
{24 - 25} Lakin pamoja na hilo wanatamani matamanio na kujidanganya wenyewe! Ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpinga yule ambaye anadai kwamba atapata tu kila anachokitaka ilhali ni mwongo katika hilo. Akasema: “Ati mtu anakipata kila anachokitamani? Mwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye dunia na Akhera." Humpa katika hayo amtakaye na humnyima amtakaye. Kwa sababu jambo hilo halitegemei matamanio yao wala hata yale ambayo nafsi zao zinatamani.
: 26 #
{وَكَمْ مِنْ مَلَكٍ فِي السَّمَاوَاتِ لَا تُغْنِي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئًا إِلَّا مِنْ بَعْدِ أَنْ يَأْذَنَ اللَّهُ لِمَنْ يَشَاءُ وَيَرْضَى (26)}.
26. Na wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipokuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia.
#
{26} يقول تعالى منكراً على مَن عَبَدَ غيره من الملائكة وغيرهم، وزعم أنَّها تنفعه وتشفع له عند الله يوم القيامةِ: {وكم من مَلَكٍ في السمواتِ}: من الملائكة المقرَّبين وكرام الملائكة، {لا تُغْني شفاعتُهم شيئاً}؛ أي: لا تفيد من دعاها وتعلَّق بها ورجاها، {إلاَّ من بعدِ أن يأذنَ الله لمن يشاءُ ويرضى}؛ أي: لا بدَّ من اجتماع الشرطين: إذنه تعالى في الشفاعة، ورضاه عن المشفوع له. ومن المعلوم المتقرِّر أنَّه لا يقبل من العمل إلاَّ ما كان خالصاً لوجه الله، موافقاً فيه صاحبُه الشريعةَ؛ فالمشركون إذاً لا نصيبَ لهم من شفاعة الشافعين؛ [وقد] سدُّوا على أنفسهم رحمة أرحم الراحمين.
{26} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, akiwakemea wanaoabudu Malaika na wengineo, na kudai kuwa wao watamfaa na watamwombea kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama: "Na wako Malaika wangapi mbinguni" walioko karibu na Mwenyezi Mungu, lakini hata watukufu miongoni mwa Malaika, "uombezi wao hautafaa chochote" mwenye kuwaomba, akafungamana nao, na kuwatumainia. "Isipokuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia." Yaani, masharti mambo haya mawili yakutane: Ruhusa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili ya uombezi, na kuridhia kwake yule ambaye anaombewa. Na kama inavyojulikana na kuthibiti ni kwamba yeye huwa hakubali matendo isipokuwa yale yaliyokusudiwa uso wake tu, ambayo mwenyewe aliyafanya kwa mujibu wa sheria. Kwa hivyo washirikina hawana fungu lolote katika uombezi wa waombezi. [Na hakika] wao wenyewe ndio waliojifungia rehema za Mwenye kurehemu zaidi ya wote.
: 27 - 30 #
{إِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ لَيُسَمُّونَ الْمَلَائِكَةَ تَسْمِيَةَ الْأُنْثَى (27) وَمَا لَهُمْ بِهِ مِنْ عِلْمٍ إِنْ يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنَّ الظَّنَّ لَا يُغْنِي مِنَ الْحَقِّ شَيْئًا (28) فَأَعْرِضْ عَنْ مَنْ تَوَلَّى عَنْ ذِكْرِنَا وَلَمْ يُرِدْ إِلَّا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا (29) ذَلِكَ مَبْلَغُهُمْ مِنَ الْعِلْمِ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنْ ضَلَّ عَنْ سَبِيلِهِ وَهُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اهْتَدَى (30)}.
27. Hakika wale wasioamini Akhera bila ya shaka wao ndio wanawaita Malaika kwa majina ya kike. 28. Nao hawana elimu yoyote kwa hayo isipokuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki. 29. Basi mwachilie mbali anayeupa kisogo ukumbusho wetu, na wala hataki ila maisha ya dunia. 30. Huo ndio mwisho wao wa elimu. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anayemjua zaidi mwenye kuipotea njia yake, na Yeye ndiye anayemjua zaidi mwenye kuongoka.
#
{27} يعني: أنَّ المشركين بالله، المكذِّبين لرسله، الذين لا يؤمنون بالآخرة؛ [و] بسبب عدم إيمانهم بالآخرة؛ تجرَّؤوا على ما تجرؤوا عليه من الأقوال والأفعال المحادَّة لله ولرسوله؛ من قولهم: الملائكة بناتُ الله! فلم ينزِّهوا ربَّهم عن الولادة، ولم يكرِموا الملائكة ويُجِلُّوهم عن تسميتهم إيَّاهم إناثاً، والحال أنَّه ليس لهم بذلك علمٌ لا عن الله ولا عن رسوله ولا دلَّت على ذلك الفطر والعقول، بل العلمُ كلُّه دالٌّ على نقيض قولهم، وأنَّ الله منزَّهٌ عن الأولاد والصاحبة؛ لأنَّه الواحد الأحد، الفرد الصمد، الذي لم يلدْ ولم يولدْ، ولم يكن له كفواً أحدٌ، وأنَّ الملائكة كرامٌ مقرَّبون إلى الله قائمون بخدمته، {لا يعصون الله ما أمَرَهم ويفعلونَ ما يُؤمرون}.
{27} Maana yake ni kwamba wale wanaoshirikisha Mwenyezi Mungu, wanaowakadhibisha Mitume wake, ambao hawaiamini Akhera, na kwa sababu ya kutoiamini kwao Akhera, wakathubutu kufanya yale waliyothubutu miongoni mwa maneno na vitendo vinavyompinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kama vile walivyosema kwamba: Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu! Wala hawakumtakasa Mola wao Mlezi mbali na suala la kuzaa, wala hawakuwatukuza Malaika na kuwaheshimu dhidi ya kuwaita wanawake. Na uhakika wa mambo ni kwamba hawana elimu yoyote ya hiyo, si kutoka kwa Mwenyezi Mungu wala kwa Mtume wake, wala hata hayakuashiriwa na maumbile ya asili ya mwanadamu wala akili. Bali elimu yote inaashiria kinyume cha wanachosema, na kwamba Mwenyezi Mungu yuko mbali sana na suala la kuzaa na kuwa na mke. Kwa sababu Yeye ni Mmoja tu, wa Pekee, Mkusudiwa, ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa, na hakuna yeyote anayelingana naye, na kwamba Malaika ni watukufu na wako karibu na Mwenyezi Mungu na wanamtumikia. "Hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayowaamrisha, na wanatenda wanayoamrishwa."
#
{28} والمشركون إنَّما يتَّبعون في ذلك القول القبيح، وهو الظنُّ الذي لا يُغني من الحقِّ شيئاً؛ فإنَّ الحقَّ لا بدَّ فيه من اليقين المستفاد من الأدلَّة [القاطعة] والبراهين الساطعة.
{28} Na washirikina wanafuata katika kauli mbaya hiyo, dhana isiyokuwa na faida yoyote mbele ya Haki. Kwani Haki lazima iwe na yakini inayotokana na ushahidi [wa uhakika] na hoja zilizo wazi mno.
#
{29} ولما كان هذا دأب هؤلاء المذكورين، أنَّهم لا غرض لهم في اتِّباع الحقِّ، وإنَّما غرضهم ومقصودهم ما تهواه نفوسُهم؛ أمر الله رسوله بالإعراض عن من تولَّى عن ذكرِهِ، الذي هو الذكرُ الحكيم والقرآنُ العظيم [والنبأ الكريم]، فأعرضَ عن العلوم النافعة، ولم يُرِدْ إلاَّ الحياة الدنيا؛ فهذا منتهى إرادتِه. ومن المعلوم أن العبد لا يعمل إلاَّ للشيء الذي يريدُه؛ فسعيُ هؤلاء مقصورٌ على الدُّنيا ولذَّاتها وشهواتها كيف حصلتْ حَصَّلوها، وبأيِّ طريق سنحت ابتدروها.
{29} Na kwa vile ilikuwa hii ndiyo tabia ya watu hawa waliotajwa, kwamba hawana lengo la kufuata haki, bali malengo yao na makusudio yao ni yale ambayo nafsi zao zinatamani tu, Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake amuepuke yule aliyeupa kisogo ukumbusho wake, ambao ni ukumbusho wenye hekima na Qur’ani kuu [na habari tukufu], na akajitenga mbali na elimu zenye manufaa na hakutaka isipokuwa maisha ya dunia tu. Huu ndio mwisho wa utashi wake. Na inavyojulikana ni kwamba mja hafanya isipokuwa kwa ajili ya kitu anachokitaka. Na matendo ya watu hawa yanafungamana tu na dunia, anasa zake na matamanio yake. Kwa hivyo, hata yakipatikana vipi, wanayachukua tu, na hata yakiwaonekania kwa njia yoyote ile wanayakimbilia.
#
{30} {ذلك مبلغُهم من العلم}؛ أي: هذا منتهى علمهم وغايته، وأمَّا المؤمنون بالآخرة المصدِّقون بها أولو الألباب والعقول؛ فهمتهم وإرادتهم للدار الآخرة، وعلومُهم أفضلُ العلوم وأجلُّها، وهو العلم المأخوذُ من كتاب الله وسنَّة رسوله - صلى الله عليه وسلم -، والله تعالى أعلمُ بمن يستحقُّ الهداية فيهديه ممَّن لا يستحقُّ ذلك فيكِلُه إلى نفسه ويخذُلُه فيضلُّ عن سبيل الله، ولهذا قال تعالى: {إنَّ ربَّك هو أعلمُ بمن ضلَّ عن سبيله وهو أعلم بمنِ اهتدى}: فيضع فضلَه حيث يعلم المحلَّ اللائقَ به.
{30} "Huo ndio mwisho wao wa elimu." Yaani, hapo ndipo mahali pa mwisho kabisa inapofikia elimu yao. Na ama wanaoiamini Akhera, wanaoisadiki, wenye ufahamu mkubwa na akili nzuri zaidi, hao hima yao na utashi wao ni nyumba ya Akhera, na elimu yao ndiyo elimu bora zaidi na tukufu zaidi, ambayo ilichukuliwa kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye ajuaye zaidi yule anayestahiki uwongofu, basi humuongoa, mbali na yule asiyestahiki hilo, basi humuachia nafsi yake na kumuachilia mbali, kwa hivyo akapotea njia ya Mwenyezi Mungu, na ndiyo maana akasema: "Hakika Mola wako Mlezi ndiye anayemjua zaidi mwenye kuipotea njia yake, na Yeye ndiye anayemjua zaidi mwenye kuongoka." Anaweka fadhila zake mahali anapojua kwamba panafailia hilo.
: 31 - 32 #
{وَلِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ لِيَجْزِيَ الَّذِينَ أَسَاءُوا بِمَا عَمِلُوا وَيَجْزِيَ الَّذِينَ أَحْسَنُوا بِالْحُسْنَى (31) الَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ إِلَّا اللَّمَمَ إِنَّ رَبَّكَ وَاسِعُ الْمَغْفِرَةِ هُوَ أَعْلَمُ بِكُمْ إِذْ أَنْشَأَكُمْ مِنَ الْأَرْضِ وَإِذْ أَنْتُمْ أَجِنَّةٌ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ فَلَا تُزَكُّوا أَنْفُسَكُمْ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اتَّقَى (32)}.
31. Ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, ili awalipe wale waliotenda ubaya kwa waliyoyatenda, na wale waliotenda mema awalipe mema. 32. Ambao wanajiweka mbali na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipokuwa makosa hafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipokuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipokuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijione watakatifu. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga akawa mbali na maovu.
#
{31} يخبر تعالى أنَّه مالك الملك، المتفرِّدُ بملك الدنيا والآخرة، وأنَّ جميع ما فيهما ملكٌ لله، يتصرَّف فيهم تصرُّف الملك العظيم في عبيده ومماليكه، ينفِّذ فيهم قدره، ويجري عليهم شرعَه، ويأمرهم وينهاهم، ويجزيهم على ما أمرهم به ونهاهم عنه، فيثيب المطيع ويعاقب العاصي، {لِيَجْزِيَ الذين أساؤوا} العمل من سيئات الكفر فما دونَه من المعاصي، وبما عملوه من أعمال الشرِّ بالعقوبة الفظيعة ، {ويجزِيَ الذين أحسنوا}: في عبادة الله، وأحسنوا إلى خلق الله بأنواع المنافع {بالحُسْنى}؛ أي: بالحالة الحسنة في الدُّنيا والآخرة، وأكبر ذلك وأجلُّه رضا ربِّهم والفوزُ بالجنة وما فيها من النعيم.
{31} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatujulisha kwamba Yeye ndiye mwenye ufalme, ambaye ni wa Pekee katika ufalme wa dunia na akhera, na kwamba kila kitu kilichomo ndani yake ni milki ya Mwenyezi Mungu, anakiendesha kama Mfalme mkuu anavyofana katika waja wake na wale anaowamiliki. Anawapitishia mipango yake, na sheria yake, na huwaamrisha na kuwakataza, na huwalipa kwa yale aliyowaamrisha na kuwakataza. Basi analipwa mwenye kutii na kumwadhibu muasi, "ili awalipe wale waliotenda ubaya" kama vile ukafiri na yaliyo chini ya hilo miongoni mwa maasia, na maovu waliyoyafanya, kwa adhabu kali. "Na wale waliotenda mema" katika kumuabudu Mwenyezi Mungu na kuwafanyia wema viumbe vya Mwenyezi Mungu, kwa kuwafikishia manufaa mbalimbali, "awalipe mema" duniani na Akhera. Na kubwa na muhimu zaidi katika hilo ni radhi za Mola wao Mlezi na kupata kuingia katika bustani za mbinguni na kupata neema zilizomo ndani yake.
#
{32} ثم ذكر وصفَهم، فقال: {الذين يَجْتَنِبون كبائرَ الإثم والفواحشَ}؛ أي: يفعلون ما أمرهم اللهُ به من الواجبات، التي يكون تركُها من كبائر الذُّنوب، ويتركون المحرَّمات الكبار من الزِّنا وشرب الخمر وأكل الرِّبا والقتل ونحو ذلك من الذُّنوب العظيمة، {إلاَّ اللَّمم}: وهو الذُّنوب الصغارُ التي لا يصرُّ صاحبها عليها، أو التي يلمُّ العبدُ بها المرَّة بعد المرَّة على وجه الندرة والقلَّة؛ فهذه ليس مجرَّد الإقدام عليها مخرجاً للعبد من أن يكون من المحسنين؛ فإنَّ هذه مع الإتيان بالواجبات وترك المحرمات تدخُلُ تحت مغفرة الله التي وسعتْ كلَّ شيءٍ، ولهذا قال: {إنَّ ربَّك واسعُ المغفرةِ}: فلولا مغفرتُه؛ لهلكتِ البلادُ والعبادُ، ولولا عفوُه وحلمه؛ لسقطتِ السماء على الأرض، ولَمَا ترك على ظهرها من دابَّةٍ، ولهذا قال النبيُّ - صلى الله عليه وسلم -: «الصلوات الخمس، والجمعة إلى الجمعة، ورمضان إلى رمضان؛ مكفراتٌ لما بينهنَّ ما اجتُنِبَتِ الكبائر». وقوله: {هو أعلم بكم إذْ أنشأكُم من الأرضِ وإذْ أنتُم أجنَّةٌ في بطون أمَّهاتِكم}؛ أي: هو تعالى أعلم بأحوالكم كلِّها، وما جبلكم عليه من الضَّعف والخَوَر عن كثيرٍ مما أمركم الله به، ومن كثرة الدواعي إلى فعل المحرَّمات، وكثرة الجواذب إليها، وعدم الموانع القويَّة، والضعف موجودٌ مشاهدٌ منكم حين أخرجكم الله من الأرض، وإذ كنتم في بطونِ أمَّهاتكم، ولم يزل موجوداً فيكم، وإنْ كان الله تعالى قد أوجدَ فيكم قوَّةً على ما أمركم به. ولكنَّ الضعف لم يزلْ؛ فلعلمه تعالى بأحوالكم هذه؛ ناسبت الحكمةُ الإلهيَّة والجود الربانيُّ أن يتغمَّدكم برحمته ومغفرته وعفوه، ويغمرَكم بإحسانه، ويزيل عنكم الجرائم والمآثم، خصوصاً إذا كان العبدُ مقصودُه مرضاة ربِّه في جميع الأوقات، وسعيُه فيما يقرُبُ إليه في أكثر الآنات، وفراره من الذُّنوب التي يمقتُ بها عند مولاه، ثم تقع منه الفلتة بعد الفلتة؛ فإنَّ الله تعالى أكرم الأكرمين وأجود الأجودين، أرحم بعبادِهِ من الوالدةِ بولدِها؛ فلا بدَّ لمثل هذا أن يكون من مغفرة ربِّه قريباً، وأن يكونَ الله له في جميع أحوالِهِ مجيباً، ولهذا قال تعالى: {فلا تزكُّوا أنفسَكم}؛ أي: تخبرون الناس بطهارتها على وجه التمدُّح عندهم، {هو أعلم بمن اتَّقى}؛ فإنَّ التَّقوى محلُّها القلبُ، والله هو المطَّلع عليه، المجازي على ما فيه من برٍّ وتقوى، وأما الناسُ؛ فلا يغنون عنكم من الله شيئاً.
{32} Kisha akataja maelezo yao, na akasema: "Ambao wanajiweka mbali na madhambi makuu na vitendo vichafu." Yaani, wanafanya yale aliyowaamrisha Mwenyezi Mungu, ambayo kuyaacha ni dhambi kubwa, na wanaacha mambo makubwa yaliyoharamishwa kama vile uzinzi, unywaji pombe, ulaji riba, kuua na madhambi mengine makubwa, "isipokuwa makosa hafifu" ambayo hayasisitizwi na mwenye kuyafanya, au anayoyalaumu mja anayatumia muda baada ya muda mbele ya uhaba na uchache Kuyafanya tu hakumwondoi mja kuwa miongoni mwa wafanyao wema. Haya, pamoja na kutekeleza wajibu na kuacha yale yaliyoharamishwa, yanaingia kwenye msamaha wa Mwenyezi Mungu ambao umekizunguka kila kitu, na ndiyo maana Akasema: "Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira." Lau si msamaha; nchi na watu wangeangamia, lau si msamaha wake na ustahimilivu wake, mbingu ingeanguka ardhini, na asingebaki mnyama mgongoni mwake, ndio maana Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – akasema: “Swala tano za kila siku, Ijumaa hadi Ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani; ni kafara ya yaliyo baina yao katika madhambi makubwa.” Na kauli yake: "Naye anakujueni sana tangu alipokuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipokuwa mimba matumboni mwa mama zenu.'" Yaani, Yeye Mtukufu ndiye anayejua zaidi hali zenu zote, na unyonge na uvivu alioweka juu yenu kutokana na mengi ya aliyokuamrisheni Mwenyezi Mungu, na wingi wa makusudio ya kufanya mambo yaliyoharamishwa,wingi wa mitihani kwenu, na kutokuwepo vizuizi vikali, na udhaifu upo na unaonekana kutoka kwenu pale Mwenyezi Mungu alipokutoeni katika ardhi, na mlipokuwa matumboni mwa mama zenu na Yeye Mola hakukosekana juu yenu, ingawa Mungu Mwenyezi amekuumba ndani yako nguvu za kufanya yale aliyokuamuru kufanya, lakini udhaifu haukutoweka; hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua kuhusu hali hizi zenu. Hekima ya Mwenyezi Mungu na rehema za Mwenyezi Mungu zinafaa kwake kukufunika kwa rehema, msamaha na upole wake, na kukufunikeni kwa hisani yake, na kukuondolea dhuluma na madhambi, haswa ikiwa lengo la mja ni kumridhisha Mola wake katika kila nyakati, na anatafuta kufanya yale yatakayomkurubisha kwake katika nyakati zenye uchungu zaidi, na anakimbia dhambi anazozichukia mbele ya Mola wake Mlezi, kisha zinaanguka kutoka kwake baada ya kuteleza. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye mkarimu zaidi kati ya watu wakarimu na mkarimu zaidi, Yeye ni mwingi wa rehema kwa waja wake kuliko mama kwa mtoto wake. Ni lazima kwa mtu huyo kupata msamaha kutoka kwa Mola wake Mlezi upesi, na Mwenyezi Mungu awe ni jawabu kwake katika hali zake zote, na kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu akasema: "Basi msijione watakatifu." Yaani, unawaambia watu utakaso wao kuwa ni njia ya kuwasifu, "Yeye anamjua sana mwenye kujikinga akawa mbali na maovu." Mahali pa ucha Mungu ni moyo, na Mwenyezi Mungu ndiye anayeuona na kuulipa kwa wema na ucha Mungu ndani yake. Ama watu, basi hao hawana faida yoyote kwenu mbele ya Mwenyezi Mungu.
: 33 - 62 #
{أَفَرَأَيْتَ الَّذِي تَوَلَّى (33) وَأَعْطَى قَلِيلًا وَأَكْدَى (34) أَعِنْدَهُ عِلْمُ الْغَيْبِ فَهُوَ يَرَى (35) أَمْ لَمْ يُنَبَّأْ بِمَا فِي صُحُفِ مُوسَى (36) وَإِبْرَاهِيمَ الَّذِي وَفَّى (37) أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَى (38) وَأَنْ لَيْسَ لِلْإِنْسَانِ إِلَّا مَا سَعَى (39) وَأَنَّ سَعْيَهُ سَوْفَ يُرَى (40) ثُمَّ يُجْزَاهُ الْجَزَاءَ الْأَوْفَى (41) وَأَنَّ إِلَى رَبِّكَ الْمُنْتَهَى (42) وَأَنَّهُ هُوَ أَضْحَكَ وَأَبْكَى (43) وَأَنَّهُ هُوَ أَمَاتَ وَأَحْيَا (44) وَأَنَّهُ خَلَقَ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنْثَى (45) مِنْ نُطْفَةٍ إِذَا تُمْنَى (46) وَأَنَّ عَلَيْهِ النَّشْأَةَ الْأُخْرَى (47) وَأَنَّهُ هُوَ أَغْنَى وَأَقْنَى (48) وَأَنَّهُ هُوَ رَبُّ الشِّعْرَى (49) وَأَنَّهُ أَهْلَكَ عَادًا الْأُولَى (50) وَثَمُودَ فَمَا أَبْقَى (51) وَقَوْمَ نُوحٍ مِنْ قَبْلُ إِنَّهُمْ كَانُوا هُمْ أَظْلَمَ وَأَطْغَى (52) وَالْمُؤْتَفِكَةَ أَهْوَى (53) فَغَشَّاهَا مَا غَشَّى (54) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكَ تَتَمَارَى (55) هَذَا نَذِيرٌ مِنَ النُّذُرِ الْأُولَى (56) أَزِفَتِ الْآزِفَةُ (57) لَيْسَ لَهَا مِنْ دُونِ اللَّهِ كَاشِفَةٌ (58) أَفَمِنْ هَذَا الْحَدِيثِ تَعْجَبُونَ (59) وَتَضْحَكُونَ وَلَا تَبْكُونَ (60) وَأَنْتُمْ سَامِدُونَ (61) فَاسْجُدُوا لِلَّهِ وَاعْبُدُوا (62)}.
33. Je, umemwona yule aliyegeuka akaenda zake? 34. Na akapeana kidogo, kisha akajizuia? 35. Je, anayo huyo elimu ya ghaibu, basi ndiyo anaona? 36. Au hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa? 37. Na vya Ibrahimu aliyetimiza ahadi? 38. Ya kwamba hakika nafsi iliyobeba madhambi haibebi madhambi ya mwengine? 39. Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyoyafanya mwenyewe? 40. Na kwamba vitendo vyake vitaonekana? 41. Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa hayo kwa ukamilifu. 42. Na kwamba kwa Mola wako Mlezi ndiyo mwisho. 43. Na kwamba Yeye ndiye anayeleta kicheko na kilio. 44. Na kwamba Yeye ndiye anayefisha na kuhuisha. 45. Na kwamba Yeye ndiye aliyeumba jozi, dume na jike 46. Kutokana na mbegu ya uzazi inapomiminwa. 47. Na kwamba ni juu yake ufufuo mwengine. 48. Na kwamba ni Yeye ndiye anayetosheleza na kukinaisha. 49. Na kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya Shii'ra. 50. Na kwamba Yeye ndiye aliyewaangamiza 'Adi wa kwanza. 51. Na Thamudi hakuwabakisha. 52. Na kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhalimu zaidi, na waovu zaidi. 53. Na miji iliyopinduliwa, ni Yeye aliyeipindua. 54. Vikaifunika vilivyofunika. 55. Basi neema gani ya Mola wako Mlezi unayoifanyia shaka? 56. Hili ni onyo katika maonyo yale yale ya zamani. 57. Kiyama kimekaribia! 58. Hapana wa kukifichua isipokuwa Mwenyezi Mungu. 59. Je, mnayastaajabia maneno haya? 60. Na mnacheka, wala hamlii? 61. Nanyi mmeghafilika? 62. Basi msujudieni Mwenyezi Mungu, na mumuabudu.
#
{33 - 35} يقول تعالى: أفرأيتَ قُبْحَ حالة من أُمِرَ بعبادة ربِّه وتوحيده فتولَّى عن ذلك وأعرض عنه؟! فإنْ سمحتْ نفسُه ببعض الشيء القليل؛ فإنَّه لا يستمرُّ عليه، بل يبخل ويُكْدي ويمنعُ؛ فإنَّ الإحسان ليس سجيَّةً له وطبعاً، بل طبعه التولِّي عن الطاعة وعدم الثبوت على فعل المعروف، ومع هذا؛ فهو يزكِّي نفسه وينزلها غير منزلتها التي أنزلها الله بها. {أعنده علم الغيب فهو يرى}: الغيبَ فيخبر به؟! أم هو متقوِّلٌ على الله متجرِّئ عليه جامعٌ - بين المحذورين الإساءة والتزكية؟! كما هو الواقع؛ لأنَّه قد عُلِمَ أنَّه ليس عنده علمٌ من الغيب، وأنَّه لو قدِّر أنَّه ادَّعى ذلك؛ فالإخبارات القاطعة عن علم الغيب التي على يد النبيِّ المعصوم تدلُّ على نقيض قوله، وذلك دليل على بطلانه.
{33 - 35} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Je, umeona ubaya wa hali ya yule aliyeamrishwa kumwabudu Mola wake Mlezi na kumpwekesha, lakini akayapa mgongo hayo na akajiepusha nayo? Ikiwa nafsi yake itamruhusu kidogo, hawezi kudumu katika hilo. Bali hufanya ubahili na kujizuia na kuacha kutoa. Kwani kufanya wema si sifa yake au hali ya maumbile yake. Bali hali ya maumbile yake ni kuupa utiifu mgongo na kutokuwa thabiti katika kutenda mema. Na pamoaj na hayo, anajitakasa na kujiweka katika nafasi tofauti na ile ambayo Mwenyezi Mungu amemuweka. "Je, anayo huyo elimu ya ghaibu, basi ndiyo anaona" mambo ya ghaibu, kisha akawajulisha wengine juu yake? Au anamsingizia tu Mwenyezi Mungu na kufanya ujasiri dhidi yake katika hilo. Basi akawa amekusanya kati ya mambo mawili yaliyokatazwa: kufanya mabaya na kujitaksa? Na hii ndiyo hali halisi. Kwa maana inajulikana kwamba hana elimu ya ghaibu, na hata ikiwa atachukuliwa kwamba anadai hivyo, habari za uhakika kuhusu elimu ya ghaibu kupitia mikon ya Nabii aliyehifadhiwa kukosea zinaashiria kinyume cha aliyoyasema, na huo ni ushahidi wa ubatili wake.
#
{36 - 37} {أم لم يُنَبَّأْ}: هذا المدَّعي {بما في صُحُف موسى. وإبراهيم الذي وَفَّى}؛ أي: قام بجميع ما ابتلاه الله به، وأمره به من الشرائع وأصول الدين وفروعه.
{36 - 37} "Au hakuambiwa yaliyomo" huyu mwenye kudai hivi "katika Vitabu vya Musa? Na vya Ibrahimu aliyetimiza ahadi?" Yaani, aliyetekeleza yale yote ambayo Mwenyezi Mungu alimjaribu kwayo na akamwamuru kuyafanya ya sheria, misingi ya dini na matawi yake.
#
{38 - 41} وفي تلك الصحف أحكامٌ كثيرةٌ، من أهمِّها ما ذكره الله بقوله: {أن لا تزِرَ وازرةٌ وِزْرَ أخرى. وأن ليس للإنسان إلاَّ ما سَعى}؛ أي: كلُّ عامل له عمله الحسن والسيئُ؛ فليس له من عمل غيره وسعيه شيء، ولا يتحمَّل أحدٌ عن أحدٍ ذنباً، {وأنَّ سعيَه سوف يُرى}: في الآخرة، فيميَّز حسنُه من سيِّئه، {ثم يُجْزاه الجزاءَ الأوفى}؛ أي: المستكمل لجميع العمل، الخالص الحسن بالحسنى، والسيئ الخالص بالسوأى، والمشوب بحسبه؛ جزاء تُقِرُّ بعدله وإحسانه الخليقة كلها، وتَحْمَدُ الله عليه، حتى إنَّ أهل النار ليدخلون النار، وإنَّ قلوبهم مملوءةٌ من حمد ربِّهم والإقرار له بكمال الحكمة ومقت أنفسهم، وأنَّهم الذين أوصلوا أنفسهم وأوردوها شرَّ الموارد. وقد استدل بقوله [تعالى]: {وأن ليس للإنسان إلاَّ ما سعى}: من يرى أنَّ القُرَب لا يجوز إهداؤها للأحياء ولا للأموات، قالوا: لأنَّ الله قال: {وأن ليس للإنسان إلاّ ما سعى}؛ فوصول سعي غيره إليه منافٍ لذلك. وفي هذا الاستدلال نظرٌ؛ فإنَّ الآية إنما تدلُّ على أنه ليس للإنسان إلا ما سعى بنفسه، وهذا حقٌّ لا خلاف فيه، وليس فيها ما يدلُّ على أنَّه لا ينتفع بسعي غيره إذا أهداه ذلك الغير إليه ؛ كما أنَّه ليس للإنسان من المال إلاَّ ما هو في ملكه وتحت يده، ولا يلزم من ذلك أن لا يملِكَ ما وَهَبَه الغير له من مالِهِ الذي يملِكُه.
{38 - 41} Na katika Vitabu hivyo zimo hukumu nyingi, muhimu zaidi kati yake ni ile aliyoitaja Mwenyezi Mungu katika kauli yake: "Ya kwamba hakika nafsi iliyobeba madhambi haibebi madhambi ya mwengine? Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyoyafanya mwenyewe?" Yaani, kila mtendaji ana matendo yake mazuri na mbaya, wala hana chochote katika metendo na bidii ya mtu mwingine, wala hakuna atakayembebea mwingine dhambi zake. "Na kwamba vitendo vyake vitaonekana" huko Akhera? Kisha ya heri yake yatapambanuliwa mbali na maovu yake. "Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa hayo kwa ukamilifu." Yaani, malipo makamilifu kwa matendo yote: matendo mazuri halisi yatalipwa kwa mazuri zaidi, nayo maovu halisi pia yatalipwa kwa maovu, nayo yaliyochanganyika yatalipwa kulingana na namna yalivyochanganyika. Yatakuwa malipo ambayo wakakiri uadilifu wake na wema wake viumbe vyote, na kumsifu Mwenyezi Mungu juu yake, hadi wana Motoni wataingia Motoni ilhali nyoyo zao zimejaa sifa nzuri kwa Mola wao Mlezi na kukiri kwamba ni Mwenye hekima kamilifu, na kujichukia wenyewe, na kwamba wao wenyewe ndio waliozifikisha nafsi zao humo na kuziingiza mahali paovu zaidi kuingia. Na kauli yake [Mtukufu]: "Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyoyafanya mwenyewe," ilitumika kama ushahidi kwa mwenye kuona kwamba hairuhusiki kumpa sadaka ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kilicho hai wala kilichokufa. Walisema kwamba: ‘Kwa sababu Mwenyezi Mungu alisema: "Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyoyafanya mwenyewe?" Kwa hivyo, bidii ya mwingine kumfikia yeye inapingana na hili. Lakini ushahidi huu unafaa kuangaliwa vyema. Kwani Aya hii inaashiria kwamba mtu hatapata ila anachojifanyia bidii mwenyewe, na hili ni haki isiyokuwa na hilafu yoyote juu yake, lakini hakuna kitu ndani yake kinachoashiria kuwa hawezi kufaidika na jambo la mtu mwingine ikiwa huyo mwingine atampa kama zawadi. Kama vile mtu hana mali isipokuwa ile iliyo katika miliki yake na chini ya udhibiti wake, lakini hili halilazimu kwamba hawezi kumiliki kile ambacho amepewa na wengine kutoka katika mali yake anayoimiliki.
#
{42} وقوله: {وأنَّ إلى ربِّك المنتهى}؛ أي: إليه تنتهي الأمور، وإليه تصير الأشياء والخلائقُ بالبعث والنُّشور، وإلى الله المنتهى في كلِّ حال؛ فإليه ينتهي العلم والحكم والرحمة وسائر الكمالات.
{42} Na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na kwamba kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho." Yaani, kwake ndiko mambo yote yanaisha, na kwake Yeye ndiko vitu na viumbe vitaenda kwa kufufuliwa uhai na na kutalewa makaburini. Na kwa Mwenyezi Mungu ndiko mwisho katika kila hali. Kwani kwake ndiko mwisho wa elimu, hekima, rehema na mambo yote makamilifu.
#
{43} {وأنَّه هو أضحكَ وأبكى}؛ أي: هو الذي أوجد أسباب الضحك والبكاء، وهو الخير والشرُّ والفرح والسرور والهمُّ والحزن، وهو سبحانه له الحكمة البالغةُ في ذلك.
{43} "Na kwamba Yeye ndiye anayeleta kicheko na kilio." Yaani, Yeye ndiye aliyeweka visababu vya kucheka na kulia. Navyo ni heri, maovu, furaha, wasiwasi na huzuni, na Yeye Mtukufu ana hekima kubwa katika hayo.
#
{44} {وأنَّه هو أماتَ وأحيا}؛ أي: هو المنفرد بالإيجاد والإعدام، والذي أوجد الخلق وأمرهم ونهاهم، سيعيدُهم بعد موتهم، ويجازيهم بتلك الأعمال التي عملوها في دار الدُّنيا.
{44} "Na kwamba Yeye ndiye anayefisha na kuhuisha." Yaani, Yeye pekee ndiye mwenye kuumba na kuondoa, ambaye ndiye aliyewaumba viumbe, akawaamrisha na akawakataza, na atawarudisha baada ya kufa kwao, na atawalipa kwa matendo yao waliyoyafanya katika nyumba ya dunia.
#
{45 - 46} {وأنَّه خَلَقَ الزوجين}: فسَّرهما بقوله: {الذَّكَر والأنثى}: وهذا اسمُ جنس شامل لجميع الحيوانات ناطقها وبهيمها؛ فهو المنفرد بخلقها {من نُطفةٍ إذا تُمنى}: وهذا من أعظم الأدلَّة على كمال قدرته وانفراده بالعزَّة العظيمة؛ حيث أوجد تلك الحيوانات صغيرها وكبيرها من نطفةٍ ضعيفةٍ من ماءٍ مَهينٍ، ثم نمَّاها وكمَّلها حتى بلغت ما بلغتْ، ثم صار الآدميُّ منها إمَّا إلى أرفع المقامات في أعلى عليين، وإمَّا إلى أدنى الحالات في أسفل سافلين.
{45 - 46} "Na kwamba Yeye ndiye aliyeumba jozi" ambazo alizifasiri katika kauli yake, "dume na jike." Hili linajumuisha wanyama wote, wenye kuzungumza na wasiozungumza. Yeye pekee ndiye aliyewaumba. "Kutokana na mbegu ya uzazi inapomiminwa." Na hili ni katika ushahidi mkubwa kabisa juu ya ukamilifu wa uwezo wake na upweke wake katika utukufu wake mkubwa. Ambapo aliwaumba wanyama hawa wadogo na wakubwa kutokana na mbegu dhaifu ya maji yenye kudharauliwa. Kisha akawakuza na kuwakamilisha mpaka wakafika walivyofikia. Kisha mwanadamu miongoni akawa ima kwenye daraja za juu kabisa katika wale walio juu zaidi, au akawa katika hali ya chini zaidi, katika walio chini zaidi.
#
{47} ولهذا استدلَّ بالبداءة على الإعادة، فقال: {وأنَّ عليه النشأةَ الأخرى}: فيعيد العباد من الأجداث، ويجمعهم ليوم الميقات، ويجازيهم على الحسنات والسيئات.
{47} Ndiyo maana akatumia suala la kuanzisha (viumbe) kuwa ni ushahidi juu ya kurudisha (viumbe). Akasema: "Na kwamba ni juu yake ufufuo mwengine." Hapo, atawarejesha waja kutoka katika makaburi yao, na atawakusanya kwa ajili ya Siku ya Kiyama, na atawalipa kwa matendo mema na matendo mabaya.
#
{48} {وأنَّه هو أغنى وأقنى}؛ أي: أغنى العباد بتيسير أمر معاشهم من التِّجارات وأنواع المكاسب من الحِرَف وغيرها، {وأقنى}؛ أي: أفاد عباده من الأموال بجميع أنواعها ما يصيرون به مقتنين لها ومالكين لكثيرٍ من الأعيان، وهذا من نعمه تعالى؛ أنْ أخبرهم أنَّ جميع النعم منه، وهذا يوجب للعبادِ أنْ يشكُروه ويعبدُوه وحدَه لا شريك له.
{48} "Na kwamba ni Yeye ndiye anayetosheleza na kukinaisha." Yaani, aliwatosheleza waja wake kwa kuwarahisishia mambo ya maisha yao kama vile biashara na aina mbalimbali za mapato ya kiufundi na mambo mengineyo, "na kukinaisha." Yaani, aliwapa waja wake mali za kila aina, ambazo wameziweka vizuri na wanamiliki vitu vingi sana. Na hii ni katika neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwamba aliwaambia kuwa neema zote zinatoka kwake, jambo ambalo linawahitaji waja kumshukuru na kumwabudu Yeye peke yake bila mshirika yeyote.
#
{49} {وأنَّه هو ربُّ الشِّعرى}: وهو النجم المعروف بالشِّعْرى العبور، المسماة بالمرزم، وخصَّها الله بالذِّكر وإن كان هو ربُّ كلِّ شيء؛ لأنَّ هذا النجم مما عُبد في الجاهلية، فأخبر تعالى أنَّ جنس ما يعبد المشركون مربوبٌ مدبَّرٌ مخلوقٌ؛ فكيف يُتَّخَذُ مع الله آلهة؟!
{49} "Na kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya Shii'ra." Nayo ni nyota inayojulikana zaidi na ambayo pia huitwa Al-‘Abuur, na pia inaitwa Al-Marzam. Na Mwenyezi Mungu ameitaja hapa kwa jina ijapokuwa Yeye ndiye Mola Mlezi wa kila kitu, kwa sababu nyota hii ni vitu vilivyoabudiwa katika zama za kabla ya Uislamu, kwa hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akatuambia kuwa aina ya vitu wanavyoviabudu washirikina ni vitu vinavyolelewa, vinavyoendeshwa, vilivyoumbwa. Basi vipi Mwenyezi Mungu atafanyiwa miungu wengine?
#
{50} {وأنَّه أهلك عاداً الأولى}: وهم قوم هودٍ عليه السلام حين كذَّبوا هوداً، فأهلكهم الله بريح صرصرٍ عاتيةٍ.
{50} "Na kwamba Yeye ndiye aliyewaangamiza 'Adi wa kwanza." Hao walikuwa watu wa Hud, amani iwe juu yake, walipomkadhibisha Hud, basi Mwenyezi Mungu akawaangamiza kwa upepo mkali usiozuilika.
#
{51} {وثمودَ}: قومُ صالح عليه السلام؛ أرسله الله إلى ثمود، فكذَّبوه، فبعث الله إليهم الناقة آية، فعقروها وكذَّبوه، فأهلكهم الله [تعالى]، {فما أبقى}: منهم أحداً، بل أبادهم عن آخرهم.
{51} "Na Thamud" ambao ni watu wa nabii Saleh, amani iwe juu yake. Mwenyezi Mungu alimtuma kwa Thamud, lakini wao wakamkanusha, basi Mwenyezi Mungu akawatumia ngamia jike kuwa ni Ishara. Wakamchinja na wakamkadhibisha. Basi Mwenyezi Mungu [Mtukufu] akawaangamiza. “Kwa hivyo hakuacha" yeyote miongoni. Bali aliwaangamiza hadi wa mwisho wao.
#
{52} {وقومَ نوح من قبلُ إنَّهم كانوا هم أظلمَ وأطْغى}: من هؤلاء الأمم، فأهلكهم الله وأغرقهم.
{52} "Na kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhalimu zaidi, na waovu zaidi" hata kuliko kaumu waliokuwa kabla yao. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawaangamiza na akawazamisha majini.
#
{53 - 54} {والمؤتفكةَ}: وهم قومُ لوطٍ عليه السلام، {أهوى}؛ أي: أصابهم الله بعذابٍ ما عذَّب به أحداً من العالمين، قلب أسفل ديارهم أعلاها، وأمطر عليهم حجارة من سجِّيل، ولهذا قال: {فغشَّاها ما غَشَّى}؛ أي: غشيها من العذاب الأليم الوخيم ما غشي؛ أي: شيءٌ عظيمٌ لا يمكن وصفه.
{53 - 54} "Na miji iliyopinduliwa." Nao ni watu wa Lut'i, amani iwe juu yake; "ni Yeye aliyeipindua." Yaani, Mwenyezi Mungu aliwaadhibu kwa adhabu ambayo hakuwahi kumuadhibu kwayo yeyote katika walimwengu. Alizigeuza sehemu ya chini ya makazi yao ikawa juu, kisha akawanyeshea mawe ya udongo wa Motoni, na ndiyo maana akasema, "Vikaifunika vilivyofunika." Yaani, walifunikwa na adhabu kali ya kuangamiza, ambayo haiwezi kuelezewa.
#
{55} {فبأيِّ آلاءِ ربِّك تتمارى}؛ أي: فبأيِّ نعم الله وفضله تشكُّ أيُّها الإنسان؛ فإنَّ نعم الله ظاهرةٌ لا تقبل الشكَّ بوجه من الوجوه؛ فما بالعباد من نعمةٍ إلاَّ منه تعالى، ولا يدفع النِّقَم إلاَّ هو.
{55} "Basi neema gani ya Mola wako Mlezi unayoifanyia shaka" ewe mwanadamu? Kwani neema za Mwenyezi Mungu ziko wazi na haziwezi kukubali shaka kwa njia yoyote ile. Hakuna neema waliyo nayo waja ila ni kutoka kwake Mtukufu, wala hakuna anayezuilia adhabu isipokuwa Yeye.
#
{56} {هذا نذيرٌ من النُّذُر الأولى}؛ أي: هذا الرسول القرشيُّ الهاشميُّ محمد بن عبد الله ليس ببدع من الرسل، بل قد تقدَّمه من الرسل السابقين، ودعوا إلى ما دعا إليه؛ فلأيِّ شيءٍ تنكر رسالته؟! وبأيِّ حجَّة تبطل دعوته؟! أليست أخلاقه أعلى أخلاق الرسل الكرام؟! أليس يدعو إلى كلِّ خير وينهى عن كل شرٍّ ؟! ألم يأت بالقرآن الكريم الذي لا يأتيه الباطلُ من بين يديهِ ولا من خلفه تنزيلٌ من حكيمٍ حميدٍ؟! ألم يُهلك الله مَن كَذَّب مَن قبله من الرسل الكرام؟! فما الذي يمنع العذابَ عن المكذِّبين لمحمد سيِّد المرسلين وإمام المتَّقين وقائد الغرِّ المحجَّلين؟!
{56} "Hili ni Onyo katika maonyo yale yale ya zamani." Yaani, Mtume huyu wa Kiquraishi wa kabila la Haashimii, Muhammad mwana wa Abdullah, si kitu kigeni miongoni mwa Mitume. Bali alitanguliwa na Mitume waliotangulia, na wakawa wanalingania kwa kile anacholingania yeye. Basi ni kwa sababu gani mnaukataa ujumbe wake? Na ni kwa hoja gani mnaubatilisha wito wake? Je, maadili yake si ndiyo maadili ya juu kabisa ya Mitume watukufu? Je, yeye halinganii kila la heri na kukataza kila maovu? Je, hakuileta Qur-ani Tukufu, ambayo haiwezi kufikiwa na upotovu kwa mbele yake wala kwa nyuma yake. Imeteremshwa na Mwenye hekima, Msifiwa mno? Je, Mwenyezi Mungu hakuwaangamiza wale waliokadhibisha Mitume waliokuwa kabla yake? Basi ni nini kinachozuia adhabu kuwafika wale wanaomkadhibisha Muhammad, bwana wa Mitume, Imamu wa wachamungu na kiongozi wa wenye alama nyeupe za kung’aa kwenye nyuso na miguu (siku ya Kiyama).
#
{57} {أزِفَتِ الآزفةُ}؛ أي: قربت القيامة ودنا وقتُها وبانت علاماتها، {ليس لها من دونِ الله كاشفةٌ}؛ أي: إذا أتت القيامة وجاءهم العذابُ الموعود به.
{57} "Kiyama kimekaribia!" Yaani, muda wa Kiyama uko karibu na ishara zake zimekwisha bainika "Hapana wa kukifichua isipokuwa Mwenyezi Mungu."
#
{58} ثم توعَّد المنكرين لرسالة الرسول محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -، المكذِّبين لما جاء به من القرآن الكريم، فقال:
{58} Kisha akawatishia adhabu wale wanaokadhibisha ujumbe wa Mtume Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, - na wale wanaokanusha yale aliyoyaleta katika Qur-ani Tukufu. Akasema:
#
{59} {أفمِنْ هذا الحديث تعجبونَ}؛ أي: أفمن هذا الحديث الذي هو خير الكلام وأفضله وأشرفه تتعجبون، وتجعلونه من الأمور المخالفة للعادة، الخارقة للأمور والحقائق المعروفة؟! هذا من جهلهم وضلالهم وعنادهم، وإلاَّ؛ فهو الحديث الذي إذا حَدَّث صَدَق، وإذا قال قولاً فهو القول الفصل، ليس بالهزل، وهو القرآن العظيم، الذي لو أُنْزِل على جبل لرأيتَه خاشعاً متصدعاً من خشية الله، الذي يزيد ذوي الأحلام رأياً وعقلاً وتسديداً وثباتاً وإيقاناً وإيماناً، بل الذي ينبغي العَجَبُ من عقل من تعجَّب منه وسفهه وضلاله.
{59} "Je, mnayastaajabia maneno haya?” Yaani, je, mnashangazwa na maneno haya ambayo ndiyo maneno mazuri, bora na yenye heshima kubwa zaidi, na mnayachukulia kuwa ni kinyume na desturi, kinyume na mambo ya uhakika yanayojulikana? Hili ni kutokana na ujinga wao, upotofu wao na ukaidi wao. Vinginevyo, hii ni hadithi ambayo ikisema, inasadikiwa. Na ikisema neno, basi hilo ndilo la uamuzi wa mwisho wa kupambanua, wala siyo mzaha, nayo ni Qur-ani tukufu ambayo lau kuwa ingeteremshwa juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeliuona ukinyenyekea, ukipasuka kwa kumhofu Mwenyezi Mungu. Nayo inawaongezea wale wenye ufahamu mkubwa, maoni, akili, kunyooka sawa, uthabiti na imani. Bali kile ambacho kinafaa kustaajabiwa ni akili ya mwenye kuistaajabia, upumbavu wake na upotofu wake.
#
{60} {وتضحكون ولا تبكونَ}؛ أي: تستعجلون الضَّحك والاستهزاء به، مع أنه الذي ينبغي أن تتأثَّر منه النفوس وتلين له القلوب وتبكي له العيون؛ سماعاً لأمره ونهيه، وإصغاءً لوعده ووعيده، والتفاتاً لأخباره الصادقة الحسنة.
{60} "Na mnacheka, wala hamlii?” Yaani, mnakimbilia kucheka na kuifanyia mzaha, ilhali hiyo ndiyo zinapaswa kuathirika kwayo nafsi, na nyoyo kulainika kwayo na macho kulia kwa sababu yake; kwa sababu ya kusikia maamrisho na makatazo yake, kuitekea sikio ahadi yake na vitisho vyake vya dhabu, na kuzigeukia habari zake za ukweli na nzuri mno.
#
{61} {وأنتُم سامدونَ}؛ أي: غافلون لاهون عنه وعن تدبُّره ، وهذا من قلَّة عقولكم وأديانكم؛ فلو عبدتم الله وطلبتم رضاه في جميع الأحوال؛ لما كنتُم بهذه المثابة التي يأنف منها أولو الألباب.
{61} "Nanyi mmeghafilika?" Yaani, mmeghafilika na mnafanya pumbao mbali na kuizingatia, kutokana na upungufu wa akili na dini zenu. Kwani lau mngemwabudu Mwenyezi Mungu na mkatafuta radhi zake katika hali zote, hamngekuwa katika hali hii ambayo wenye uelewa mkubwa wanachukizwa nayo?
#
{62} ولهذا قال تعالى: {فاسجُدوا لله واعبدوا}: الأمر بالسجود لله خصوصاً يدلُّ على فضله، وأنَّه سرُّ العبادة ولبُّها؛ فإنَّ روحها الخشوع لله والخضوع له، والسجود [هو] أعظم حالة يخضع بها [العبد] ؛ فإنَّه يخضع قلبه وبدنه، ويجعل أشرف أعضائه على الأرض المهينة موضع وطء الأقدام. ثم أمر بالعبادة عموماً الشاملة لجميع ما يحبُّه الله ويرضاه من الأعمال والأقوال الظاهرة والباطنة.
{62} Ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Basi msujudieni Mwenyezi Mungu, na mumuabudu." Amri ya kumsujudia Mwenyezi Mungu hasa inaashiria fadhila zake, na kwamba ndiyo siri na msingi wa ibada. Kwani roho yake ni kumnyenyekea Mola, nako kusujudu ndiko hali kuu zaidi ambayo [mja] ananyenyekea kwayo. Kwa maana huunyenyekesha moyo wake na mwili wake, na hukiweka kiungo chake cha heshima zaidi kwenye ardhi ya kufedhehesha hamali ambapo miguu ya mtu inakanyaga. Kisha akaamuru ibada kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na yote ambayo Mwenyezi Mungu anayaridhia na anapenda, iwe ni matendo na maneno ya wazi na yaliyofichikana.
Imekamilika tafsiri ya Surat An-Najm. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu [ambaye hatuwezi kuhesabu na kudhibiti sifa zake. Bali Yeye ni kama alivyojisifu Mwenyewe na zaidi ya vile wanavyomsifu waja wake. Na rehema na amani nyingi za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Muhammad].
******