:
Tafsiri ya Surat Dhariyat
Tafsiri ya Surat Dhariyat
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
: 1 - 6 #
{وَالذَّارِيَاتِ ذَرْوًا (1) فَالْحَامِلَاتِ وِقْرًا (2) فَالْجَارِيَاتِ يُسْرًا (3) فَالْمُقَسِّمَاتِ أَمْرًا (4) إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٌ (5) وَإِنَّ الدِّينَ لَوَاقِعٌ (6)}
1. Ninaapa kwa pepo zinazotawanya. 2. Na zinazobeba mizigo. 3. Na zinazokwenda kwa wepesi. 4. Na zinazogawanya kwa amri. 5. Hakika mnayoahidiwa bila ya shaka ni kweli. 6. Na kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea.
#
{1 - 6} هذا قسمٌ من الله الصادق قي قيله بهذه المخلوقات العظيمة، التي جعل اللهُ فيها من المصالح والمنافع ما جعل، على أنَّ وعدَه صدقٌ، وأنَّ الدين الذي هو يوم الجزاء والمحاسبة على الأعمال لواقعٌ لا محالةَ، ما له من دافع. فإذا أخبر به الصادقُ العظيم، وأقسم عليه، وأقام الأدلَّة والبراهين عليه؛ فلِمَ يكذِّب به المكذِّبون، ويعرِض عن العمل له العاملون؟! {والذَّارياتِ}: هي الرياح التي تذرو في هبوبها {ذرواً}: بلينها ولطفها وقوَّتها وإزعاجها، {فالحاملاتِ وِقراً}: هي السحاب، تحمل الماء الكثير، الذي ينفع الله به العباد والبلاد ، {فالجارياتِ يُسراً}: النجوم التي تجري على وجه اليُسر والسُّهولة، فتتزيَّن بها السماواتُ، ويُهتدَى بها في ظلمات البرِّ والبحر، ويُنْتَفَعُ بالاعتبار بها، والمقَسِّمات {أمراً}: الملائكة التي تقسِّم الأمر وتدبِّره بإذن الله؛ فكلٌّ منهم قد جعله الله على تدبير أمرٍ من أمور الدنيا والآخرة لا يتعدَّى ما حُدَّ له وقُدِّر ورُسِم ولا ينقص منه.
{1 - 6} Hiki ni kiapo kutoka kwa Mwenyezi Mungu - ambaye ni mkweli katika maneno yake kuhusu viumbe hivi vikubwa, ambavyo Mwenyezi Mungu aliweka ndani yake masilahi na manufaa - kwamba ahadi yake ni ya ukweli, na kwamba Siku ya Malipo na kuulizwa juu ya matendo bila shaka itatokea, na haiwezi kosa, wala hakuna anayeweza kuizuia. Kwa hivvyo anapojulisha juu yake Yule ambaye ndiye Mkweli Mkuu, na akaapa juu yake, na akasimamisha ushahidi na hoja mbalimbali juu yake, basi kwa nini wanaikadhibisha wale wanaoikadhibisha, na wenye kufanya matendo wakapuuza kuifanyia matendo? "Ninaapa kwa pepo zinazotawanya vumbi" wakati zinapovuma "kabisa" mara kwa ulaini, na kwa upole, na kwa nguvu, na kwa usumbufu mkubwa. "Na zinazobeba mizigo" kama vile mawingu yanayobeba maji mengi sana ambayo kwayo Mwenyezi Mungu huwanufaisha waja wake na ardhi. "Na zinazokwenda kwa wepesi." Yaani, nyota zipitazo kwa wepesi na kwa hizo mbingu zinapambika, watu wanaongoka njia kwazo katika viza vya bara na bahari, na pia zinanufaisha kwa kuzizingatia, pia zinazogawanya kwa "amri" na pia maana yake yaweza kuwa Malaika ambao wanagawanya amri na kuisimamia kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kila mmoja wao Mwenyezi Mungu amempa jukumu la kusimamia jambo fulani kati ya mambo ya dunia na akhera, na hawezi kupita mipaka aliyoekewa wala kupunguza chochote kutoka kwake.
: 7 - 9 #
{وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْحُبُكِ (7) إِنَّكُمْ لَفِي قَوْلٍ مُخْتَلِفٍ (8) يُؤْفَكُ عَنْهُ مَنْ أُفِكَ (9)}
7. Ninaapa kwa mbingu zenye njia. 8. Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayohitalifiana. 9. Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa.
#
{7} أي: {والسماء}: ذات الطرائق الحسنة، التي تشبه حُبُكَ الرمال ومياه الغدران حين يحركها النسيم.
{7} Yaani, "Ninaapa kwa mbingu" yenye njia nzuri nzuri, zinazofanana mawimbi yanayokuwa juu ya mchanga na kidimbwi upepo unapopita juu yake.
#
{8} {إنَّكم}: أيُّها المكذِّبون لمحمدٍ - صلى الله عليه وسلم -، {لفي قول مختلفٍ}: منكم من يقولُ: ساحر! ومنكم من يقول: كاهن! ومنكم من يقول: مجنون! إلى غير ذلك من الأقوال المختلفة الدالَّة على حيرتهم وشكِّهم، وأنَّ ما هم عليه باطلٌ.
{8} "Hakika Nyinyi" enyi mnaomkadhibisha Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - "bila ya shaka mmo katika kauli inayohitalifiana." Wapo miongoni mwenu wanaosema: 'Mchawi!' Na baadhi yenu husema: 'Kuhani!' Na baadhi yenu husema: 'Wazimu!' Mbali na kauli zingine mbalimbali ambazo zinazoashiria kuchanganyikiwa kwao na shaka yao, na kwamba wanayoyafanya wao ni batili.
#
{9} {يؤفَكُ عنه من أُفِكَ}؛ أي: يُصْرَفُ عنه من صُرف عن الإيمان وانصرف [قلبه] عن أدلَّة الله اليقينيَّة وبراهينه. واختلافُ قولهم دليلٌ على فساده وبطلانه؛ كما أنَّ الحقَّ الذي جاء به محمد - صلى الله عليه وسلم - متَّفق؛ يصدِّقُ بعضه بعضاً، لا تناقض فيه ولا اختلاف، وذلك دليلٌ على صحَّته، وأنَّه من عند الله؛ فلو كان من عند غير الله؛ لوجدوا فيه اختلافاً كثيراً.
{9} "Anageuzwa kutoka kwenye haki mwenye kugeuzwa" na [moyo] wake ukatoka kwenye ushahidi wa Mwenyezi Mungu na hoja zake za yakini. Na kutofautiana kauli yao kunaonyesha ubovu wake na ubatili wake. Kama vile haki aliyokuja nayo Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – inakubaliana yenyewe kwa yenyewe, na inasadikishana yenyewe kwa yenyewe, haigongani wala haitatofautiani, na huo ni ushahidi wa usahihi wake, na kwamba umetoka kwa Mwenyezi Mungu. Na lau ingekuwa imetoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, basi bila ya shaka wangelikuta ndani yake hitilafu nyingi.
: 10 - 14 #
{قُتِلَ الْخَرَّاصُونَ (10) الَّذِينَ هُمْ فِي غَمْرَةٍ سَاهُونَ (11) يَسْأَلُونَ أَيَّانَ يَوْمُ الدِّينِ (12) يَوْمَ هُمْ عَلَى النَّارِ يُفْتَنُونَ (13) ذُوقُوا فِتْنَتَكُمْ هَذَا الَّذِي كُنْتُمْ بِهِ تَسْتَعْجِلُونَ (14)}.
10. Wazushi wameangamizwa. 11. Ambao wameghafilika katika ujinga. 12. Wanauliza: 'Ni lini hiyo siku ya malipo?' 13. Hiyo ni siku watakayoadhibiwa Motoni. 14. Onjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyokuwa mkiyafanyia haraka.
#
{10} يقول تعالى: {قُتِلَ الخرَّاصونَ}؛ أي: قاتل الله الذين كَذَبوا على الله، وجحدوا آياته، وخاضوا بالباطل ليُدْحِضوا به الحقَّ، الذين يقولون على الله ما لا يعلمون.
{10} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Wazushi wameangamizwa" wale waliomdanganyishia Mwenyezi Mungu, wakakataa Ishara zake, na wakazama katika batili ili wakanushe kwayo haki, wale wanaosema juu ya Mwenyezi Mungu yale wasiyoyajua.
#
{11} {الذين هم في غمرةٍ}؛ أي: في لُجَّةٍ من الكفر والجهل والضلال، {ساهون}.
{11} "Ambao wameghafilika" ndani ya ya ukafiri, ujinga, na upotofu, "na kujisahaulisha."
#
{12} {يسألون}: على وجه الشكِّ والتكذيب: {أيَّان [يوم الدين] }: يبعثون؛ أي: متى يُبعثون؟! مستبعدين لذلك!
{12} "Wanauliza" kwa njia ya shaka na kukadhibisha na kuona kwamba haliwezekani: "Ni lini hiyo siku ya malipo" ambayo watafufuliwa?
#
{13 - 14} فلا تسألْ عن حالهم وسوء مآلهم! {يوم هم على النار يُفتنون}؛ أي: يعذَّبون بسبب ما انطووا عليه من خبث الباطن والظاهر، ويُقالُ لهم: {ذوقوا فتنتكم}؛ أي: العذاب والنار، الذي هو أثر ما افتتنوا به من الابتلاء، الذي صيَّرهم إلى الكفر والضلال. {هذا}: العذابُ الذي وصلتم إليه هو {الذي كنتُم به تستعجلونَ}: فالآن تمتَّعوا بأنواع العقاب والنَّكال، والسلاسل والأغلال، والسخط والوَبال.
{13 - 14} Basi usiulize juu ya hali yao wala maishio yao mabaya! "Hiyo ni siku watakayoadhibiwa Motoni" kwa sababu ya uovu wao wa ndani na wa nje walio nao, na wataambiwa: "Onjeni adhabu yenu!" Ambayo ni matokeo ya mtihani waliojaribiwa nao, uliowapelekea kuwa katika ukafiri na upotofu. "Haya" ya adhabu yaliyowafika "ndiyo mliyokuwa mkiyafanyia haraka." Basi sasa furahieni kila aina ya adhabu na mateso, minyororo na pingu, ghadhabu na balaa kubwa mno.
: 15 - 19 #
{إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ (15) آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَلِكَ مُحْسِنِينَ (16) كَانُوا قَلِيلًا مِنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ (17) وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ (18) وَفِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ لِلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ (19)}.
15. Hakika wacha Mungu watakuwa katika Mabustani ya mbinguni na chemchemi. 16. Wanapokea yale aliyowapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema. 17. Walikuwa wakilala kidogo tu usiku. 18. Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira. 19. Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiyeomba.
#
{15} يقول تعالى في ذكر ثواب المتَّقين وأعمالهم التي وصلوا بها إلى ذلك الجزاء: {إنَّ المتَّقينَ}؛ أي: الذين كانت التَّقوى شعارهم وطاعةُ اللهِ دثارهم، {في جناتٍ}: مشتملات على جميع أصناف الأشجار والفواكه، التي يوجد لها نظيرٌ في الدنيا، والتي لا يوجد لها نظيرٌ، مما لم تنظر العيونُ إلى مثله، ولم تسمع الآذانُ، ولم يخطرْ على قلب بشرٍ ، {وعيونٍ}: سارحة تشرب منها تلك البساتين، ويشربُ بها عبادُ الله يفجِّرونها تفجيراً.
{15} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika kutaja malipo ya watu wacha Mungu na matendo yao waliyofika kwayo katika malipo hayo, "Hakika wacha Mungu." Yaani, wale ambao ucha Mungu ulikuwa ndio nguo yao juu na utiifu kwa Mwenyezi Mungu ukawa ndio nguo yao ya ndani, "watakuwa katika Mabustani" yenye kila aina ya miti na matunda, ambayo yana yale yanayofanana nayo katika dunia hii, na yale ambayo hayana kinachofanana nayo, miongoni mwa yale ambayo macho hayajawahi kuyaona, wala masikio hayajawahi kuyasikia, wala hayajawahi kupita katika moyo wa mwanadamu yeyote. "Na chemichemi" inayotiririka, ambazo bustani hizo zinakunywa humo, na watainywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakiifanya imiminike kwa wingi.
#
{16} {آخذينَ ما آتاهم ربُّهم}: يُحتملُ أنَّ المعنى أنَّ أهل الجنَّة قد أعطاهم مولاهم جميع مناهم من جميع أصناف النعيم، فأخذوا ذلك راضين به، قد قرَّت به أعينُهم، وفرحتْ به نفوسُهم، ولم يطلبُوا منه بدلاً، ولا يبغون عنه حولاً، وكلٌّ قد ناله من النعيم ما لا يطلب عليه المزيد. ويُحتمل أنَّ هذا وصف المتَّقين في الدُّنيا، وأنَّهم آخذون ما آتاهم الله من الأوامر والنواهي؛ أي: قد تلقَّوها بالرحب وانشراح الصدر، منقادين لما أمر الله به بالامتثال على أكمل الوجوه، ولما نهى عنه بالانزجار عنه لله على أكمل وجه؛ فإنَّ الذي أعطاهم الله من الأوامر والنواهي هو أفضل العطايا التي حقُّها أن تُتَلَقَّى بالشُّكر لله عليها والانقياد. والمعنى الأول ألصقُ بسياق الكلام؛ لأنَّه ذكر وصفهم في الدُّنيا وأعمالهم بقوله: {إنَّهم كانوا قبل ذلك}: الوقت الذي وصلوا به إلى النعيم {محسنين}: وهذا شاملٌ لإحسانهم بعبادة ربِّهم؛ بأن يعبدوه كأنهم يرونه؛ فإنْ لم يكونوا يرونه؛ فإنَّه يراهم، وللإحسان إلى عباد الله ببذل النفع والإحسان من مال أو علم أو جاهٍ أو نصيحةٍ أوأمرٍ بمعروف أو نهي عن منكرٍ، أو غير ذلك من وجوه البرِّ وطرق الخيرات، حتى إنَّه يدخُلُ في ذلك الإحسان بالقول والكلام الليِّن والإحسان إلى المماليك والبهائم المملوكة وغير المملوكة.
{16} "Wanapokea yale aliyowapa Mola wao Mlezi." Inawezekana kwamba maana yake ni kuwa wakazi wa Bustani za mbinguni wameshapewa na Mola wao Mlezi katika neema za kila aina, basi wakazichukua huku wameridhia, macho yao na nafsi zao zimefurahia kwa hayo, na wala hawakuomba chochote badala yake, na wala hata hawataki kutoka katika hayo, na kila mmoja ameshapata neema ambayo haombi chochote zaidi yake. Na inawezekana kwamba hii ni sifa ya wacha Mungu hapa duniani, na kwamba wanachukua aliyowapa Mwenyezi Mungu miongoni mwa maamrisho na makatazo, kwa mikono miwili na kifua wazi, wakawa wanayatekeleza yale ambayo Mwenyezi Mungu ameamrisha yatekelezwe kwa namna kamilifu zaidi, na wakakomeka mbali na yale aliyoyakataza na kuyakemea kwa njia iliyo kamili kabisa. Kwani amri na makatazo ambayo Mwenyezi Mungu aliwapa ndicho kipawa bora zaidi ambacho kinastahiki kupokelewa kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu juu yake na kumtii. Lakini maana ile ya kwanza ndiyo inafailia zaidi kulingana na muktadha wa maneno haya. Kwa sababu alitaja sifa zao katika dunia na matendo yao kwa kauli yake: "Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya" waliyoyafikia ya neema mbalimbali, "wakifanya mema." Na hili linajumuisha wema wao katika kumuabudu Mola wao Mlezi; kwa kumwabudu kana kwamba wanamwona. Na hata ikiwa hawakumwona, basi Yeye kwa hakika anawaona, na pia kwa sababu ya wema wao kwa waja wa Mwenyezi Mungu kwa kuwafanyia ya kuwanufaisha na ihsani kama vile kuwapa mali, elimu, ufahari, nasiha, kuamrisha mema au kukataza maovu, au mambo mengineyo ya wema, kiasi kwamba yanaingia katika hili kufanya wema kwa kauli laini na pia kuwafanyia wema watumwa, mifugo inayomilikiwa na isiyomilikiwa.
#
{17} ومن أفضل أنواع الإحسان في عبادة الخالق صلاةُ الليل الدالَّة على الإخلاص وتواطؤ القلب واللسان، ولهذا قال: {كانوا}؛ أي: المحسنون، {قليلاً من الليل ما يَهْجَعونَ}؛ أي: كان هجوعهم؛ أي: نومهم بالليل قليلاً، وأمَّا أكثر الليل؛ فإنَّهم قانتون لربِّهم، ما بين صلاة وقراءة وذكر ودعاء وتضرُّع.
{17} Na miongoni mwa aina bora zaidi za wema katika kumwabudu Muumba ni Swala ya usiku, inayoashiria ikhlasi kwamba mja anamkusudia Mwenyezi Mungu peke yake, na kwamba moyo na ulimi vimekubaliana. Na ndiyo maana akasema: "Walikuwa" wafanyao wema hawa "wakilala kidogo tu usiku." Na ama muda mwingi wa usiku, wao walikuwa wakisimama kwa unyenyekevu kwa ajili ya Mola wao Mlezi, wakiswali, na kusoma, na kumtaja, na kuomba dua na kumnyenyekea sana.
#
{18} {وبالأسحار}: التي هي قبيل الفجر، {هم يستغفرونَ}: الله تعالى، فمدُّوا صلاتهم إلى السحر، ثم جلسوا في خاتمة قيامهم بالليل يستغفرون الله تعالى استغفار المذنبِ لذنبه. وللاستغفار بالأسحار فضيلةٌ وخصيصةٌ ليست لغيره؛ كما قال تعالى في وصف أهل الإيمان والطاعة: {والمستغفرين بالأسحار}.
{18} "Na kabla ya alfajiri," ambayo ni masaa ya kabla ya alfajiri, "wakiomba maghfira" kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa hivyo wakawa wamerefusha Swala zao mpaka alfajiri, kisha wakakaa mwishoni wa Swala zao za usiku wakimwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awaghufirie kwa sababu ya madhambi yao. Na kuomba msamaha katika masaa ya kabla ya alfajiri kuna fadhila na sifa maalumu zisizo katika masaa mengineyo, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuwaelezea watu wa Imani na utiifu: "Na wanaoomba maghafira kabla ya alfajiri."
#
{19} {وفي أموالهم حقٌّ}: واجبٌ ومستحبٌّ {للسائل والمحروم}؛ أي: للمحتاجين الذين يطلبون من الناس والذين لا يسألونهم.
{19} "Na katika mali yao ipo haki" ya wajibu na isiyo ya wajibu "ya mwenye kuomba na asiyeomba."
: 20 - 23 #
{وَفِي الْأَرْضِ آيَاتٌ لِلْمُوقِنِينَ (20) وَفِي أَنْفُسِكُمْ أَفَلَا تُبْصِرُونَ (21) وَفِي السَّمَاءِ رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُونَ (22) فَوَرَبِّ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ إِنَّهُ لَحَقٌّ مِثْلَ مَا أَنَّكُمْ تَنْطِقُونَ (23)}
20. Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini. 21. Na pia katika nafsi zenu - Je, hamwoni? 22. Na katika mbingu ziko riziki zenu na yale mnayoahidiwa. 23. Basi ninaapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema.
#
{20} يقول تعالى داعياً عباده إلى التفكُّر والاعتبار: {وفي الأرضِ آياتٌ للموقِنينَ}: وذلك شاملٌ لنفس الأرض وما فيها من جبال وبحارٍ وأنهارٍ وأشجارٍ ونباتٍ تدلُّ المتفكِّر فيها، المتأمِّل لمعانيها على عظمة خالقها وسعة سلطانه وعميم إحسانه وإحاطة علمه بالظواهر والبواطن.
{20} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, akiwalingania waja wake wafikirie na kuzingatia, "Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini." Hili linajumuisha ardhi yenyewe na yaliyomo ndani yake ya milima, bahari, mito, miti, na mimea ambayo inamuashiria mwenye kuvitafakari, mwenye kuangalia vyema maana zake kuwa ni ushahidi wa ukubwa Muumba wake na upana wa mamlaka yake, na ujumla wa wema wake, na kufikia kwa elimu mambo yote ya dhahiri na ya siri.
#
{21} وكذلك في نفس العبد من العِبَرِ والحكمة والرحمة ما يدلُّ على أنَّ الله واحدٌ أحدٌ فردٌ صمدٌ ، وأنَّه لم يخلق الخلق سدىً.
{21} Kadhalika, katika nafsi ya mja kuna mazingatia, hekima, na rehema ambazo zinaonyesha kwamba Mwenyezi Mungu ni mmoja, wa Pekee, Mkusudiwa, na kwamba hakuumba viumbe bure tu.
#
{22} وقوله: {وفي السماء رزقُكُم}؛ أي: مادة رزقكم من الأمطار وصنوف الأقدار؛ الرزق الدينيُّ والدنيويُّ، وما توعدونه من الجزاء في الدنيا والآخرة؛ فإنَّه ينزل من عند الله كسائر الأقدار.
{22} Na kauli yake: "Na katika mbingu ziko riziki zenu" kama vile mvua na aina mbalimbali za mipango ya Mwenyezi Mungu. Riziki ya kidini na ya kidunia, na malipo mnayoahidiwa duniani na akhera. Hayo yote yanashuka kutoka kwa Mwenyezi Mungu kama mipango yake mingineyo yote.
#
{23} فلما بيَّن الآيات ونبَّه عليها تنبيهاً ينتبه به الذكيُّ اللبيبُ؛ أقسم تعالى على أنَّ وعده وجزاءه حقٌّ، وشبَّه ذلك بأظهر الأشياء لنا، وهو النُّطق، فقال: {فوربِّ السماءِ والأرضِ إنَّه لَحَقٌّ مثلما أنَّكم تَنطِقونَ}؛ فكما أنَّكم لا تشكُّون في نطقكم؛ فكذلك ينبغي أن لا يعترِيَكم الشكُّ في البعث والجزاء.
{23} Alipozifafanua Aya na kuzibainisha kwa namna ambayo mwenye akili na mwenye kufikiri anaweza kuzingatia, Mwenyezi Mungu Mtukufu akaapa kwamba ahadi yake na malipo yake ni kweli, na akalifananisha hilo na jambo lililo dhahiri zaidi kwetu, ambalo ni kutamka, akasema: "Basi ninaapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema." Kama vile hamna shaka yoyote kwamba mnatamka, vivyo hivyo, hamfai kuwa na shaka yoyote kuhusu ufufuo na malipo.
: 24 - 37 #
{هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ الْمُكْرَمِينَ (24) إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا قَالَ سَلَامٌ قَوْمٌ مُنْكَرُونَ (25) فَرَاغَ إِلَى أَهْلِهِ فَجَاءَ بِعِجْلٍ سَمِينٍ (26) فَقَرَّبَهُ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ (27) فَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً قَالُوا لَا تَخَفْ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ (28) فَأَقْبَلَتِ امْرَأَتُهُ فِي صَرَّةٍ فَصَكَّتْ وَجْهَهَا وَقَالَتْ عَجُوزٌ عَقِيمٌ (29) قَالُوا كَذَلِكِ قَالَ رَبُّكِ إِنَّهُ هُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ (30) قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ (31) قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَى قَوْمٍ مُجْرِمِينَ (32) لِنُرْسِلَ عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِنْ طِينٍ (33) مُسَوَّمَةً عِنْدَ رَبِّكَ لِلْمُسْرِفِينَ (34) فَأَخْرَجْنَا مَنْ كَانَ فِيهَا مِنَ الْمُؤْمِنِينَ (35) فَمَا وَجَدْنَا فِيهَا غَيْرَ بَيْتٍ مِنَ الْمُسْلِمِينَ (36) وَتَرَكْنَا فِيهَا آيَةً لِلَّذِينَ يَخَافُونَ الْعَذَابَ الْأَلِيمَ (37)}.
24. Je, imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanaoheshimiwa? 25. Walipoingia kwake na wakasema: 'Salama!' Na yeye akasema: 'Salama! Nyinyi ni watu nisiowajua.' 26. Basi akaenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliyenona. 27. Akawakaribishia, akasema: 'Mbona hamli?' 28. Kwa hivyo, akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: 'Usiwe na hofu.' Basi wakambashiria kupata kijana mwenye elimu. 29. Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa! 30. Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyosema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hekima, Mwenye kujua. 31. Akasema: 'Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mliotumwa?' 32. Wakasema: 'Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu.' 33. Tuwatupie mawe ya udongo. 34. Yaliyotiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanaopindukia mipaka. 35. Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walioamini. 36. Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu! 37. Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanaoiogopa adhabu chungu.
#
{24} يقول تعالى: {هل أتاك}؛ أي: أما جاءك؟ {حديثُ ضيفِ إبراهيمَ المُكْرَمينَ}: ونبأهُم الغريب العجيب، وهم الملائكة الذين أرسلهم الله لإهلاك قوم لوطٍ، وأمرهم بالمرور على إبراهيم، فجاؤوه في صورة أضياف.
{24} Mwenyezi Mungu anasema: "Je, imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanaoheshimiwa" na habari yao geni ya ajabu, ambao ni wale Malaika aliowatuma Mwenyezi Mungu kuwaangamiza kaumu ya Lut'i, na akawaamrisha wapitie kwa Ibrahim, kwa hivyo wakamjia katika sura ya wageni.
#
{25} {إذْ دَخَلوا عليه فقالوا سلاماً قال}: مجيباً لهم: {سلامٌ}؛ أي: عليكم، {قومٌ منكَرون}؛ أي: أنتم قوم منكَرون، فأحبُّ أن تعرِّفوني بأنفسكم، ولم يعرفهم إلاَّ بعد ذلك.
{25} "Walipoingia kwake na wakasema: 'Salama!' Na yeye akasema" akiwajibu, "Salama! Nyinyi ni watu nisiokujueni." Basi napenda mujitambulishe kwangu, na hakuwajua mpaka baada ya hayo.
#
{26} ولهذا راغ {إلى أهلِهِ}؛ أي: ذهب سريعاً في خفيةٍ ليحضر لهم قِراهم، {فجاء بعجلٍ سمينٍ}.
{26} Basi ndiyo sababu akaenda kwa "ahali yake" upesi kwa hofu ili kuwaletea cha kuwakaribisha kwacho "na akaja na ndama aliyenona."
#
{27} {فقرَّبه إليهم}: وعرض عليهم الأكل، فَـ {قَالَ ألا تأكُلونَ}؟
{27} "Akamuweka karibu nao" na kuwaalika wale chakula hicho, kisha akasema, "Mbona hamli?"
#
{28} {فأوجسَ منهم خيفةً}: حين رأى أيديهم لا تصلُ إليه، {قالوا لا تخفْ}: وأخبروه بما جاؤوا له، {وبشَّروه بغلام عليم}: وهو إسحاق عليه السلام.
{28} "Kwa hivyo, akahisi kuwaogopa katika nafsi yake" alipoona mikono yao haimfikii (ndama huyo), "Wakasema: 'Usiwe na hofu' wakampa habari waliyomjia nayo "na wakambashiria kupata kijana mwenye elimu" ambaye ni Is'haka, amani iwe juu yake.
#
{29} فلمَّا سمعت المرأةُ البشارةَ؛ {أقبلتْ}: فرحةً مستبشرةً {في صَرَّةٍ}؛ أي: صيحة، {فصكَّتْ وجهها}: وهذا من جنس ما يجري للنساء عند السرور ونحوه من الأقوال والأفعال المخالفة للطبيعة والعادة، {وقالتْ عجوزٌ عقيمٌ}؛ أي: أنَّى لي الولد وأنا عجوزٌ قد بلغتُ من السنِّ ما لا تلد معه النساء! ومع ذلك؛ فأنا عقيمٌ غير صالح رحمي للولادة أصلاً؛ فثمَّ مانعان، كلٌّ منهما مانعٌ من الولد، وقد ذكرت المانع الثالث في سورة هودٍ في قولها: {وهذا بعلي شيخاً إنَّ هذا لشيءٌ عجيبٌ}.
{29} Mkewe aliposikia habari njema, "akawaelekea" kwa furaha na tumaini "na huku anasema" kwa kelele "na akijipiga usoni kwa mastaajabu." Na haya ni katika yale yanayowatokea wanawake wanapokuwa na furaha na mfano wake kutokamana na maneno na matendo ambayo ni kinyume na maumbile na desturi "na akasema: 'Mimi ni mkongwe mzee na tasa!" Yaani, nitawezaje kupata mtoto nikiwa mzee na nimefika umri ambao wanawake hawawezi kuzaa! Na pamoja na hayo mimi ni tasa, ambaye tumbo lake la uzazi halifailii kabisa kuzaa. Kuna vizuizi viwili, kila kimoja kinazuia kupata mtoto. Nacho kizuizi cha tatu kimetajwa katika Surat Hud katika kauli yake: "Na huyu mume wangu ni kizee? Hakika haya ni mambo ya ajabu!"
#
{30} {قالوا كذلِكِ قال رَبُّكِ}؛ أي: الله الذي قدَّر ذلك وأمضاه؛ فلا عجب في قدرة الله [تعالى]، {إنَّه هو الحكيم العليم}؛ أي: الذي يضع الأشياء مواضعها، وقد وسعَ كلَّ شيء علماً، فسلِّموا لحكمه، واشكروه على نعمته.
{30} "Wakasema: 'Ndivyo vivyo hivyo alivyosema Mola wako Mlezi." Yaani, Mwenyezi Mungu ndiye aliyepanga hili na akalipitisha, basi hakuna la kustaajabu katika uwezo wa Mwenyezi Mungu [Mtukufu], "Hakika Yeye ni Mwenye hekima na Mwenye kujua mno." Ambaye anayeweka vitu mahali pake, na amekienea kila kitu katika elimu, basi jisalimisheni kwa hukumu yake, na mshukuruni kwa neema zake.
#
{31} {قال فما خطبُكم أيُّها المرسلونَ} ؛ أي: قال لهم إبراهيم عليه السلام: ما شأنُكم أيُّها المرسلون؟! وماذا تريدون؟! لأنَّه استشعر أنهم رسلٌ أرسلهم الله لبعض الشؤون المهمَّة.
{31} "Akasema: 'Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mliotumwa?" Yaani, Ibrahim, amani iwe juu yake, akawaambia: Mna nini enyi mliotumwa? Na mnataka nini? Kwa sababu alihisi kwamba walikuwa wajumbe waliotumwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mambo fulani muhimu.
#
{32} {قالوا إنَّا أرْسِلْنا إلى قوم مجرمينَ}: وهم قومُ لوطٍ، قد أجرموا بإشراكهم بالله وتكذيبهم لرسولهم وإتيانهم الفاحشة التي لم يَسْبِقْهم إليها أحدٌ من العالمين.
{32} "Wakasema: 'Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu." Hao walikuwa watu wa Lut'i ambao walifanya uhalifu wa kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kumkadhibisha Mtume wao, na kufanya uchafu ambao hakuna yeyote katika kaumu zilizotangulia aliwahi kuufanya.
#
{33 - 34} {لنرسلَ عليهم حجارةً من طينٍ. مسوَّمةً عند ربِّكَ للمسرفينَ}؛ أي: معلَّمة على كلِّ حجرٍ اسم صاحبه؛ لأنَّهم أسرفوا وتجاوزوا الحدَّ. فجعل إبراهيمُ يجادِلُهم في قوم لوطٍ، لعلَّ الله يدفعُ عنهم العذاب، فقيل له: {يا إبراهيمُ أعْرِضْ عن هذا إنَّه قد جاء أمرُ رَبِّك وإنَّهم آتيهم عذابٌ غيرُ مردودٍ}.
{33 - 34} "Tuwatupie mawe ya udongo. Yaliyotiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanaopindukia mipaka." Yaani, zilikuwa zimetiwa alama juu ya kila jiwe ya yule atakayepigwa kwalo. Kwa sababu walikuwa wafujaji na wakavuka mipaka. Basi Ibrahim akaanza kujadiliana nao kuhusu kaumu ya Lut'i kwamba huenda Mwenyezi Mungu atawalinda mbali na adhabu hiyo, lakini akaambiwa: "Ewe Ibrahim! Hakika imewafikia adhabu ambayo haitarejeshwa."
#
{35 - 36} {فأخْرَجْنا من كان فيها من المؤمنينَ. فما وَجَدْنا فيها غيرَ بيتٍ من المسلمين}: وهم بيتُ لوطٍ عليه السلام؛ إلاَّ امرأتَه؛ فإنَّها من المهلكين.
{35 - 36} "Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walioamini. Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu" ambao ni nyumba ya Lut'i, amani iwe juu yake. Isipokuwa mkewe; Kwa maana yeye alikuwa miongoni mwa wale walioangamizwa.
#
{37} {وتركْنا فيها آيةً للذين يخافون العذابَ الأليمَ}: يعتبرون بها ويعلمون أنَّ الله شديدُ العقاب، وأنَّ رسلَه صادقون مصدوقون.
{37} "Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanaoiogopa adhabu chungu" ili wazingatie kwa hizo na wajue kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu, na Mitume wake ni wakweli na wanaoaminika.
Sura ya kutaja baadhi ya hekima na hukumu zilizomo katika hadithi hii Miongoni mwake ni kwamba ni katika hekima kwamba Mwenyezi Mungu aliwasimulia waja wake habari za watu wema na waovu, ili wazingatie kwa hao, na iliwafikisha wapi hali yao. Na miongoni mwake ni ubora wa Ibrahim Al-Khalil, rehema na amani ziwe juu yake; ambapo Mwenyezi Mungu alianza kwa kisa chake, jambo ambalo linaashiria kwamba anakijali na kukitunza. Na miongoni mwake ni kwamba ni katika sheria ya Uislamu kuwakaribisha wageni, na kwamba hilo ni katika Sunna za Ibrahim Al-Khalil, ambaye Mwenyezi Mungu alimwamrisha Muhammad na umma wake kufuata mila yake, na katika mahali hapa, Mwenyezi Mungu akaitaja katika hali ya kuisifu. Na miongoni mwake ni kwamba mgeni anafaa kukirimiwa kwa aina tofauti tofauti za ukarimu, kwa maneno na matendo. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alielezea wageni wa Ibrahim kwamba walikuwa wenye kuheshimika. Yaani, Ibrahimu aliwakirimu, na Mwenyezi Mungu akaelezea ukarimu aliowaonyesha kwa maneno na matendo, na wao pia ni wa kuheshimika kwa Mwenyezi Mungu [Mtukufu]. Na miongoni mwake ni kwamba Ibrahim, amani iwe juu yake, ilikuwa nyumba yake ni mahali pa kuingia kwa wapita njia na wageni. Kwa sababu waliingia kwake bila ya kumuomba ruhusa, lakini walifuata njia ya uungwana katika kuanza kutoa salamu, naye Ibrahim akawajibu kwa salamu iliyokamilika na iliyotimia zaidi kuliko yao; kwa sababu alitumia sentensi inayoanza kwa nomino, nayo ni aina ya sentensi inayoonyesha uthabiti na umadhubuti. Na miongoni mwake ni kwamba ni katika sheria ya Uislamu kumjua vyema mtu ambaye amekuja kwa mtu mwingine, au wakati wanapokuwa na utangamano fulani naye. Kwa sababu katika hilo kuna faida nyingi. Na miongoni mwake ni adabu nzuri na upole wa Ibrahim katika usemi, ambapo alisema: "Watu wasiojulikana" wala hakusema: 'Sikujuini" na baina ya maneno mawili hayo kuna tofauti kubwa isiyofichika. Na miongoni mwake: kuchukua hatua na kuharakisha ukarimu kwao; kwa sababu uadilifu bora zaidi ni ule unaoharakishwa, na ndiyo sababu Ibrahim alichukua hatua ya kuleta uandazi wa wageni wake. Na miongoni mwake ni kwamba iwapo dhabihu iliyopo ikiwa ilikuwa imetayarishwa kwa ajili ya asiyekuwa mgeni aliyepo sasa, ikiwa atakaribishwa kwa hiyo, basi hajadunishwa hata kidogo. Bali ni kitendo cha heshima. Kama vile Ibrahim, amani iwe juu yake, alivyofanya, na Mwenyezi Mungu akajulisha kwamba wageni wake hao waliheshimiwa. Na miongoni mwake ni ukarimu mkubwa ambao Mwenyezi Mungu alimpa mwandani wake, Ibrahimu, na kwamba huo ulikuwepo pamoja naye na ulikuwa nyumbani kwake tayari umeshaandaliwa, na hakuhitaji kuuleta kutoka sokoni, au kutoka kwa majirani, au vinginevyo. Na miongoni mwake ni kwamba Ibrahim ndiye aliyewahudumia wageni wake, ilhali yeye ni mwandani wa Mwingi wa rehema na bwana wa wote wanaowakaribisha wageni. Na miongoni mwake ni kwamba aliwaletea karibu chakula hicho mahali walipokuwa, wala hakukiweka mahali, kisha akaawaambia, "Karibuni" au "njooni" kwa sababu hili ndilo rahisi na bora zaidi. Na miongoni mwake ni kuzungumza na mgeni kwa mazungumzo yenye upole na ulaini, haswa wakati wa kumpa chakula. Kwani, Ibrahim aliwawekea chakula mbele yao kwa upole, kisha akasema: “Mbona hamli?” Na wala hakusema, "kuleni;" na maneno mfano wa hayo ambayo yasiyokuwa hayo yanafaa zaidi badala yake. Bali alitumia neno la kumhimiza mtu, akisema: “Mbona hamli?” Kwa hivyo, inampasa mwenye kumfuata atumie maneno mazuri yanayofaa na yanayofungamana zaidi na hali aliyomo, kama vile alivyowaambia wageni wake, "Mbona hamli?" Au: "Mbona hamkaribii?" Au mnatupa utukufu, na mnatufanyia uzuri... na mfano wa hayo. Na miongoni mwake ni kwamba yeyote anayeogopa mtu kwa sababu yoyote ile, basi inamlazimu huyo mwingine amuondolee hofu hiyo, na amtajie yale yatakayoipatia amani hofu yake hiyo, na itulize wasiwasi wake, kama vile Malaika hao walivyomwambia Ibrahim alipowaogopa: “Usiogope” na wakamwambia habari hizo za kufurahisha baada ya kwamba alikuwa na hofu nao. Na miongoni mwake ni ukubwa wa furaha ya Sara, mke wa Ibrahim, mpaka yakamtokea hayo yaliyomtokea ikiwemo kujipiga usoni na kupiga makelele, mambo ambayo si kawaida yake. Na miongoni mwake ni ukarimu wa Mwenyezi Mungu kwa Ibrahim na mke wake, Sara kwa kuwapa bishara njema ya kupata mwana wa kiume mwenye elimu.
: 38 - 40 #
وقوله تعالى: {وَفِي مُوسَى إِذْ أَرْسَلْنَاهُ إِلَى فِرْعَوْنَ بِسُلْطَانٍ مُبِينٍ (38) فَتَوَلَّى بِرُكْنِهِ وَقَالَ سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ (39) فَأَخَذْنَاهُ وَجُنُودَهُ فَنَبَذْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ وَهُوَ مُلِيمٌ (40)}.
38. Na katika habari za Musa, tulipomtuma kwa Firauni na hoja wazi. 39. Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: 'Huyu ni mchawi au mwendawazimu!' 40. Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa.
#
{38} أي: {وفي موسى}: وما أرسله الله به إلى فرعون وملئه بالآيات البينات والمعجزات الظاهرات آيةٌ للذين يخافون العذاب الأليم.
{38} Yaani, "Na katika habari za Musa" na yale ambayo Mwenyezi Mungu alimtuma nayo kwa Firauni na wakuu wake, miongoni mwa ishara zilizo wazi na miujiza iliyo dhahiri ambavyo vilikuwa ishara kwa wale wanaoogopa adhabu chungu.
#
{39} فلمَّا أتى موسى فرعون بذلك السلطان المبين؛ تولَّى فرعون {بركنِهِ}؛ أي: أعرض بجانبه عن الحقِّ، ولم يلتفتْ إليه، وقدحوا فيه أعظم القدح، فقالوا: {ساحرٌ أو مجنونٌ}؛ أي: إن موسى لا يخلوا إمَّا أن يكون ما أتى به سحراً وشعبذةً ليس من الحقِّ قي شيء، وإمَّا أن يكون مجنوناً لا يؤاخَذُ بما صدر منه لعدم عقله! هذا وقد علموا ـ خصوصاً فرعون ـ أنَّ موسى صادقٌ؛ كما قال تعالى: {وجَحَدوا بها واسْتَيْقَنَتْها أنفسُهم ظلماً وعلوًّا}، وقال موسى لفرعون: {لقد علمتَ ما أنزل هؤلاءِ إلاَّ ربُّ السمواتِ والأرض بصائرَ ... } الآية.
{39} Basi Musa alipomjilia Firauni kwa uthibitisho huo ulio wazi, alipuuza Firauni "kwa sababu ya nguvu zake." Yaani, alijiepusha na haki wala hakuizingatia, na wakamsingizia maneno ya kashfa kuu, wakasema: "Huyu ni mchawi au mwendawazimu!" Yaani, Inawezekana aliyokuja nayo Musa ni uchawi na udanganyifu ambao haukuwa wa kweli kabisa, au alikuwa mwendawazimu na asingewajibishwa kwa yale aliyoyafanya kutokana na kutokuwa na akili! Walisema haya na hakika walijua - hasa Firauni - kwamba Musa alikuwa mkweli. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na waliikadhibisha, na nafsi zao zikawa na yakini nayo katika udhalimu na kiburi". Na Musa akamwambia Firauni: "Unajua ya kwamba hakuna aliyeteremsha kwa Haya ila Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ambaye ni Mwona wa yote ..." Aya.
#
{40} {فأخذْناه وجنودَه فنَبَذْناهم في اليمِّ وهو مُليمٌ}؛ أي: مذنبٌ طاغٍ عاتٍ على الله، فأخذه [اللَّهُ] أخذَ عزيزٍ مقتدرٍ.
{40} "Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa." Yaani, mtenda dhambi dhalimu aliyemuasi Mwenyezi Mungu, basi [Mwenyezi Mungu] akamshika kama anavyoshika Mwenye nguvu na Mwenye uweza.
: 41 - 42 #
{وَفِي عَادٍ إِذْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ الرِّيحَ الْعَقِيمَ (41) مَا تَذَرُ مِنْ شَيْءٍ أَتَتْ عَلَيْهِ إِلَّا جَعَلَتْهُ كَالرَّمِيمِ (42)}.
41. Na katika habari za 'Adi tulipowatumia upepo wa kukata uzazi. 42. Haukuacha chochote ulichokifikia ila ulikifanya kama kilichonyambuka.
#
{41} أي: {و} آية لهم {في عادٍ}: القبيلة المعروفة، {إذْ أرسَلْنا عليهم الريحَ العقيمَ}؛ أي: التي لا خير فيها، حين كذَّبوا نبيَّهم هوداً عليه السلام.
{41} Hiyo ni ishara kwao "katika habari za 'Adi," kabila mashuhuri, "tulipowatumia upepo wa kukata uzazi." Yaani, upepo ambao haukuwa na heri ndani yake, walipomkadhibisha Nabii wao Hud, amani iwe juu yake.
#
{42} {ما تَذَرُ من شيءٍ أتتْ عليه إلاَّ جَعَلَتْهُ كالرَّميم}؛ أي: كالرِّمم البالية؛ فالذي أهلكهم على قوَّتهم وبطشهم دليلٌ على كمال قوَّته واقتداره، الذي لا يعجِزُه شيء، المنتقم ممَّن عصاه.
{42} "Haukuacha chochote ulichokifikia ila ulikifanya kama kilichonyambuka." Kwa hivyo, Yule aliyewaangamiza pamoja na nguvu zao na ukatili wao ni ushahidi wa nguvu na uwezo wake kamilifu, ambaye hakuna kinachoweza kumshinda, ambaye analipiza kisasi kwa wale waliomuasi.
: 43 - 45 #
{وَفِي ثَمُودَ إِذْ قِيلَ لَهُمْ تَمَتَّعُوا حَتَّى حِينٍ (43) فَعَتَوْا عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ فَأَخَذَتْهُمُ الصَّاعِقَةُ وَهُمْ يَنْظُرُونَ (44) فَمَا اسْتَطَاعُوا مِنْ قِيَامٍ وَمَا كَانُوا مُنْتَصِرِينَ (45)}.
43. Na katika habari za Thamudi walipoambiwa: 'Jifurahisheni kwa muda mdogo tu.' 44. Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi ukawanyakua moto wa radi nao wanaona. 45. Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea.
#
{43} أي: {وفي ثمودَ}: آيةٌ عظيمةٌ حين أرسل الله إليهم صالحاً عليه السلام، فكذَّبوه وعاندوه، وبعث الله له الناقة آيةً مبصرةً، فلم يزدْهم ذلك إلاَّ عتُوًّا ونفوراً، {قيل لهم تمتَّعوا حتى حينٍ}.
{43} Yaani: "Na katika habari za Thamudi" kuna ishara kubwa pale Mwenyezi Mungu alipowatumia Saleh, amani iwe juu yake, lakini wakamkadhibisha na kumfanyia uadui. Na Mwenyezi Mungu akamtumia ngamia awe ni Ishara ya kufumbua macho, lakini hayo hayakuwazidishia isipokuwa kiburi na kujiweka mbali. "Walipoambiwa: Jifurahisheni kwa muda mdogo tu."
#
{44} {فعَتَوْا عن أمرِ ربِّهم فأخَذَتْهُمُ الصَّاعقةُ}؛ أي: الصيحة العظيمة المهلكة، {وهم ينظرونَ}: إلى عقوبتهم بأعينهم.
{44} "Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi ukawanyakua moto wa radi" wenye kuangamiza, "nao wanaona" adhabu yao hiyo kwa macho yao.
#
{45} {فما استَطاعوا من قيامٍ}: ينجون به من العذاب، {وما كانوا منتصِرينَ}: لأنفسهم.
{45} "Wala hawakuweza kusimama" ili waokoke kutokana na adhabu hiyo, "wala hawakuweza kujitetea" wao wenyewe.
: 46 #
{وَقَوْمَ نُوحٍ مِنْ قَبْلُ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ (46)}.
46. Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu.
#
{46} أي: وكذلك ما فعل الله بقوم نوح حين كذَّبوا نوحاً عليه السلام وفَسَقوا عن أمِر الله، فأرسل الله عليهم السماء والأرض بماءٍ منهمرٍ ، فأغرقهم عن آخرهم، ولم يُبْقِ من الكافرين ديَّاراً. وهذه عادة الله وسنَّتُه فيمَن عصاه.
{46} Yaani, na kama hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu alivyowafanyia watu wa Nuhu, walipomkadhibisha Nuhu, amani iwe juu yake, na kuasi amri ya Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu akawateremshia mbingu na ardhi kwa maji yanayomiminika, na yakawangamiza hadi wa mwisho wao, na wala hakubakishwa katika ardhi mkaazi yeyote katika wale waliokufuru. Na hii ni desturi ya Mwenyezi Mungu na Sunnah yake kwa wale wanaomuasi.
: 47 - 51 #
{وَالسَّمَاءَ بَنَيْنَاهَا بِأَيْدٍ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ (47) وَالْأَرْضَ فَرَشْنَاهَا فَنِعْمَ الْمَاهِدُونَ (48) وَمِنْ كُلِّ شَيْءٍ خَلَقْنَا زَوْجَيْنِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ (49) فَفِرُّوا إِلَى اللَّهِ إِنِّي لَكُمْ مِنْهُ نَذِيرٌ مُبِينٌ (50) وَلَا تَجْعَلُوا مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ إِنِّي لَكُمْ مِنْهُ نَذِيرٌ مُبِينٌ (51)}.
47. Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio wenye uwezo wa kuzitanua. 48. Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi! 49. Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie. 50. Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake. 51. Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.
#
{47} يقول تعالى مبيِّناً لقدرته العظيمة: {والسماءَ بَنَيْناها}؛ أي: خلقناها وأتقنَّاها وجَعَلْناها سقفاً للأرض وما عليها، {بأيْدٍ}؛ أي: بقوَّةٍ وقدرةٍ عظيمةٍ، {وإنَّا لَموسعونَ}: لأرجائها وأنحائها، وإنَّا لموسعون أيضاً على عبادنا بالرِّزق الذي ما ترك دابَّة في مهامه القفارِ ولُجج البحارِ وأقطار العالم العلويِّ والسفليِّ إلاَّ وأوصل إليها من الرزق ما يكفيها، وساق إليها من الإحسان ما يُغنيها. فسبحان من عمَّ بجوده جميع المخلوقات، وتبارك الذي وسعتْ رحمتُه جميع البريَّات.
{47} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, akieleza uwezo wake mkuu: "Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo." Yaani, tumeiumba vizuri kabisa na tukaifanya paa la ardhi na vilivyo juu yake "kwa nguvu na uwezo, na hakika Sisi bila ya shaka ndio wenye uwezo wa kuzitanua" kwenye pembezoni mwake na sehemu zake, na hakika pia tunawapa waja wetu riziki, ambaye hakumuacha mnyama katika sehemu ya ndani mno jangawi wala katika vilindi vya bahari na maeneo ya ulimwengu wa juu na wa chini, isipokuwa anamfikishia riziki ya kumtosha, na kumfikishia wema wa kumtosheleza. Basi ametakasika Yule ambaye wema wake umevijumuisha viumbe vyote, na ni Mwingi wa baraka Yule ambaye rehema yake imevienea viumbe vyote.
#
{48} {والأرضَ فَرَشْناها}؛ أي: جعلناها فراشاً للخلق يتمكَّنون فيها من كلِّ ما تتعلَّق به مصالحهم من مساكنَ وغراسٍ وزرعٍ وحرثٍ وجلوسٍ وسلوكٍ للسُّبل الموصلة إلى مقاصدهم ومآربهم. ولمَّا كان الفراشُ قد يكون صالحاً للانتفاع من كلِّ وجهٍ، وقد يكون من وجهٍ دون وجهٍ؛ أخبر تعالى أنه مَهَدَها أحسنَ مهادٍ على أكمل الوجوه وأحسنها، وأثنى على نفسه بذلك، فقال: {فنعمَ الماهِدونَ}: الذي مَهَدَ لعبادِهِ ما اقتضتْه حكمتُه ورحمتُه.
{48} "Na ardhi tumeitandaza." Yaani, tumeifanya kuwa ni tandiko ili viumbe waweze kutulia juu yake na kufikia kila kitu kinachohusiana na masilahi yao, kama vile nyumba, upandaji mimea, ukulima, kukaa na kufuata njia zinazoelekea kwenye makusudio na malengo yao. Na kwa kuwa tandiko linaweza kuwa nzuri kwa kila njia, na linaweza kuwa na manufaa kwa njia moja bila nyingine, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kuwa aliitandaza kwa ufundi ulio bora zaidi na mkamilifu zaidi na akajisifu kwa hilo, akasema: "Basi watandazaji wazuri namna gani Sisi!" Ambaye amewatandazia waja wake kile ambacho hekima yake na rehema zake vinahitaji.
#
{49} {ومن كلِّ شيءٍ خَلَقْنا زوجين}؛ أي: صنفين ذكرٍ وأنثى من كلِّ نوع من أنواع الحيوانات، {لعلَّكم تذكَّرونَ}: لنعم اللهِ التي أنعم بها عليكم في تقدير ذلك وحكمتِهِ؛ حيث جعل ما هو السبب لبقاء نوع الحيوانات كلها؛ لتقوموا بتنميتها وخدمتها وتربيتها فيحصل من ذلك ما يحصل من المنافع.
{49} "Na kila kitu tumekiumba kwa jozi." Yaani, aina mbili, dume na jike, katika kila aina ya wanyama, "ili mzingatie" neema za Mwenyezi Mungu alizokupeni na kukadiria hilo na hekima yake ndani yake; ambapo aliweka humo visababu vya kufanya aina zote za wanyama ziendelee kuishi; ili muwakuze, muwatumikie, na kuwakuza, ndiyo yapatikane kwayo yanapatikana miongoni mwa manufaa.
#
{50} فلما دعا العبادَ إلى النظر إلى آياته الموجبة لخشيته والإنابة إليه؛ أمر بما هو المقصود من ذلك، وهو الفرارُ إليه؛ أي: الفرار مما يكرهه الله ظاهراً وباطناً إلى ما يحبُّه ظاهراً وباطناً، فرارٌ من الجهل إلى العلم، ومن الكفر إلى الإيمان، ومن المعصية إلى الطاعة، من الغفلة إلى الذِّكر؛ فمن استكمل هذه الأمور؛ فقد استكمل الدين كلَّه، وزال عنه المرهوب، وحصل له غايةُ المراد والمطلوب. وسمى الله الرجوع إليه فراراً؛ لأنَّ في الرجوع إلى غيره أنواعَ المخاوف والمكاره، وفي الرجوع إليه أنواعَ المحابِّ والأمن والسرور والسعادة والفوزِ، فيفرُّ العبدُ من قضائه وقدره إلى قضائه وقدره، وكلُّ مَنْ خِفْتَ منه فررتَ منه إلاَّ الله تعالى؛ فإنَّه بحسب الخوف منه يكون الفرارُ إليه، {إنِّي لكُم منه نذيرٌ مبينٌ}؛ أي: منذرٌ لكم من عذاب الله ومخوِّفٌ بيِّن النذارة.
{50} Alipowaita waja kuzitazama ishara zake zinazowataka wamche na kumrudia; akaamrisha yanayokusudiwa katika hayo, nayo ni kumkimbilia. Yaani, kukimbia kutoka kwa yale anayochukia Mwenyezi Mungu, kwa nje na ndani, na kuyapenda anayoyapenda, kwa nje na ndani. Pia kukimbia kutoka kwa ujinga kwenda kwenye elimu, na kutoka kwa ukafiri hadi katika imani, na kutoka kwa uasi hadi katika utii, na kutoka katika kughafilika hadi kwenye kukumbuka. Kwa hivyo, atakayekamilisha mambo haya, basi atakuwa ameikamilisha dini yote, na ataondokewa anayohofu yote na atapata malengo yanayohitajika. Mwenyezi Mungu aliita kurudi kwake kwamba ni kukimbia; kwa sababu katika kurejea kwa wengine kuna aina za hofu na machukizo, na katika kurudi kwake kuna aina za mapenzi, usalama, raha, furaha na ushindi. Kwa hivyo mja atakuwa amekimbia kutoka kwa mapitisho yake na mipango yake hadi kwenye mapitisho yake na mipango yake, na kila unayemhofu, utakimbia kutoka kwake isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwani kwa kiasi cha kumhofu, utakimbia kwenda kwake. "Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake" kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na anayekutieni hofu wa wazi mno.
#
{51} {ولا تَجْعَلوا مع الله إلهاً آخرَ}: هذا من الفرار إلى الله، بل هذا أصلُ الفرارِ إليه: أنْ يَفِرَّ العبدُ من اتِّخاذ آلهةٍ غير الله من الأوثان والأندادِ والقبورِ وغيرها مما عُبِدَ من دون الله، ويخلِصَ [العبدُ] لربِّه العبادة والخوف والرجاء والدعاء والإنابة.
{51} "Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu." Hii ni namna ya kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu, bali huu ndio msingi wa kukimbilia kwake: kwamba mja akimbie suala la kujifanyia miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu kama vile masanamu, makaburi, na vitu vingine vinavyoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, na [mja] amkusudie Mola wake Mlezi tu katika ibada, hofu, matumaini, dua, na toba.
: 52 - 53 #
{كَذَلِكَ مَا أَتَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ مِنْ رَسُولٍ إِلَّا قَالُوا سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ (52) أَتَوَاصَوْا بِهِ بَلْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ (53)}.
52. Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema: 'Huyu ni mchawi au mwendawazimu.' 53. Je, wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi.
#
{52} يقول الله مسلياً لرسوله - صلى الله عليه وسلم - عن تكذيب المشركين بالله، المكذِّبين له، القائلين فيه من الأقوال الشنيعة ما هو منزَّه عنه، وأنَّ هذه الأقوال ما زالتْ دأباً وعادةً للمجرمين المكذِّبين للرسل؛ فما أرسل اللهُ من رسول؛ إلاَّ رماه قومُه بالسحر أو الجنون.
{52} Mwenyezi Mungu anamwambia Mtume wake – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – juu ya kumkadhibisha washirikina Mwenyezi Mungu, wale ambao pia wanamkadhibisha yeye pia, wale wanaosema maneno mabya juu yake ambayo yuko mbali nayo, na kwamba maneno haya bado ni tabia na desturi ya wale wanaokadhibisha Mitume. Kwani Mwenyezi Mungu hakumtuma Mtume yeyote, isipokuwa watu wake walimtusi kwa uchawi au wazimu.
#
{53} يقول الله تعالى: هذه الأقوال التي صَدَرَتْ منهم ـ الأولين والآخرين ـ هل هي أقوالٌ تواصَوْا بها، ولقَّن بعضُهم بعضاً بها؛ فلا يُستغرب بسبب ذلك اتِّفاقهم عليها؟! أم {هم قومٌ طاغونَ}؛ تشابهتْ قلوبُهم وأعمالهم بالكفر والطُّغيان، فتشابهت أقوالُهم الناشئة عن طغيانهم؟! وهذا هو الواقع؛ كما قال تعالى: {وقال الذين لا يعلمون لولا يُكَلِّمُنا الله أو تأتينا آيةٌ كذلك قال الذينَ من قَبْلِهِم مثلَ قولِهِم تشابهتْ قلوبُهم}، وكذلك المؤمنون لمَّا تشابهتْ قلوبُهم بالإذعان للحقِّ وطلبه والسعي فيه؛ بادروا إلى الإيمان برسُلِهم وتعظيمهم وتوقيرهم وخطابهم بالخطاب اللائق بهم.
{53} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Je, maneno haya yaliyotoka kwao - ya mwanzo na ya mwisho - ni maneno ambayo waliusiana wao kwa wao na wakafundishana wao kwa wao? Basi haishangazi kwamba wote wanakubaliana juu yake? Au "Bali hawa ni watu waasi," nyoyo zao na vitendo vyao vilifanana na ukafiri na dhuluma, kwa hivyo maneno yao yaliyotokana na dhuluma yao yakafanana pia? Huu ndio ukweli; kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na walisema wale wasiojua kitu: 'Mbona Mwenyezi Mungu hasemi nasi au zikatufikia Ishara?' Kama hivyo walisema wale waliokuwa kabla yao mfano wa kauli yao hii. Nyoyo zao zimefanana." Na vivyo hivyo Waumini, ilipofanana mioyo yao kwa kuinyenyekea haki, na kuitafuta, na kujitahidi kupata, waliharakisha kuwaamini Mitume wao, kuwatukuza, kuwaheshimu, na kuwaongelesha kwa maneno yanayowafailia.
: 54 - 55 #
{فَتَوَلَّ عَنْهُمْ فَمَا أَنْتَ بِمَلُومٍ (54) وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَى تَنْفَعُ الْمُؤْمِنِينَ (55)}.
54. Basi waachilie mbali, nawe hulaumiwi. 55. Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini.
#
{54} يقولُ تعالى آمراً رسولَه بالإعراض عن المعرضين المكذِّبين: {فتولَّ عنهم}؛ أي: لا تبالِ بهم، ولا تؤاخِذْهم، وأقبِلْ على شأنك؛ فليس عليك لومٌ في ذنبهم، وإنَّما عليك البلاغُ، وقد أدَّيت ما حملتَ وبلَّغتَ ما أرسلت به.
{54} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, akimuamrisha Mtume wake awaepuke makafiri na wale wanaokadhibisha: "Basi waachilie mbali." Yaani usiwajali, usiwachukulie ubaya, na fanya mambo yako mwenyewe; Wewe si wa kulaumiwa kwa dhambi zao, bali wajibu wako ni kufikisha ujumbe, na umeshatekeleza uliyobebeshwa na umefikisha uliyotumwa nayo.
#
{55} {وذكِّرْ فإنَّ الذِّكْرى تنفعُ المؤمنين}: والتَّذكير نوعان: تذكيرٌ بما لم يُعْرَفْ تفصيله مما عُرِفَ مجملُه بالفِطَر والعقول ؛ فإنَّ الله فطر العقول على محبَّة الخير وإيثاره وكراهة الشرِّ والزُّهد فيه، وشرعُه موافقٌ لذلك؛ فكل أمرٍ ونهيٍ من الشرع؛ فهو من التذكير، وتمامُ التذكير أن يذكر ما في المأمور من الخير والحسن والمصالح، وما في المنهيِّ عنه من المضارِّ. والنوع الثاني من التذكير: تذكيرٌ بما هو معلومٌ للمؤمنين، ولكن انسحبتْ عليه الغفلةُ والذُّهول، فيذكَّرون بذلك، ويكرَّر عليهم؛ ليرسخ في أذهانهم، وينتبهوا، ويعملوا بما تَذَكَّروه من ذلك، وليحدثَ لهم نشاطاً وهمَّة توجب لهم الانتفاع والارتفاع. وأخبر الله أنَّ الذِّكرى تنفع المؤمنين؛ لأنَّ ما معهم من الإيمان والخشية والإنابة واتِّباع رضوان الله يوجب لهم أن تنفع فيهم الذِّكرى وتقع الموعظة منهم موقعها؛ كما قال تعالى: {فذكِّرْ إن نفعتِ الذِّكرى. سَيَذَّكَّرُ مَن يَخْشى. وَيَتَجَنَّبُها الأشقى}، وأما من ليس معه إيمانٌ ولا استعدادٌ لقبول التذكير؛ فهذا لا ينفع تذكيره؛ بمنزلة الأرض السبخة التي لا يفيدها المطر شيئاً. وهؤلاء الصنف لو جاءتهم كلُّ آية؛ لم يؤمنوا حتى يروا العذاب الأليم.
{55} "Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini." Ukumbusho ni ya namna mbili: Ukumbusho wa yale yasiyojulikana kwa undani, yanayojulikana kwa ujumla tu kwa umbile asili na akili. Kwani Mwenyezi Mungu aliziumba akili kupenda wema, kuupendelea, kuuchukia uovu, na kujiepusha nao, na sheria yake inakubaliana na hayo. Kwa sababu kila amri na katazo katika Sheria nii aina ya ukumbusho. Na ukumbusho kamili ni kutaja heri, mazuri na manufaa yaliyo katika maamrisho, na madhara yaliyo katika maharamisho. Na aina ya pili ya ukumbusho ni ukumbusho wa yale yanayojulikana kwa Waumini, lakini yameghafilika mbali nayo na wakayasahau, basi wanakumbushwa hayo na inarudiwa kuwakumbusha. Ili yawe imara katika akili zao, na wawe makini, na watende kwa yale wanayokumbuka katika hayo, na ili yawake utanashati na hima yenye kuwasababishia kunufaika na kuinuka juu. Mwenyezi Mungu alituambia kuwa ukumbusho huwanufaisha Waumini. Kwa sababu yale waliyo nayo ya imani, hofu, toba, na kufuata radhi za Mwenyezi Mungu yanawasababishia kukumbuka na kunufaika na mawaidha, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa. Atakumbuka mwenye kuogopa. Na atajitenga mbali nayo mpotovu." Na ama yule asiye na Imani wala hayuko tayari kukubali ukumbusho, basi huyu hakuna faida katika kumkumbusha. Naye ni kama ardhi ya chumvi ambayo mvua haiinufaishi kwa chochote. Na watu hawa, hata ikiwa zitawajia ishara zote, hawangeamini mpaka waione adhabu chungu.
: 56 - 58 #
{وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنْسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ (56) مَا أُرِيدُ مِنْهُمْ مِنْ رِزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَنْ يُطْعِمُونِ (57) إِنَّ اللَّهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ (58)}.
56. Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi. 57. Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe. 58. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti.
#
{56} هذه الغاية التي خَلَقَ الله الجنَّ والإنس لها، وبعث جميعَ الرسل يدعون إليها، وهي عبادتُه المتضمِّنة لمعرفته ومحبَّته والإنابة إليه والإقبال عليه والإعراض عما سواه، وذلك متوقِّف على معرفة الله تعالى ؛ فإنَّ تمام العبادة متوقِّف على المعرفةِ بالله ، بل كلَّما ازداد العبد معرفةً بربِّه ؛ كانت عبادته أكمل؛ فهذا الذي خلق الله المكلَّفين لأجله؛ فما خَلَقَهم لحاجة منه إليهم.
{56} Hili ndilo lengo ambalo Mwenyezi Mungu amewaumbia majini na watu, na akawatuma Mitume wote wakiita kwalo, nalo ni kumuabudu Yeye, jambo linalojumuisha kumjua, kumpenda, kurejea kwake, kumuelekea, na kuvipa mgongo vyote visivyokuwa Yeye, na hayo yanategemea kumjua vyema Mwenyezi Mungu. Kwani ukamilifu wa ibada unategemea kujua vyema Mwenyezi Mungu. Bali kila anapozidisha mja kumjua Mola wake Mlezi ndivyo ibada yake huwa kamilifu zaidi. Kwa hivyo, hii ndiyo sababu Mwenyezi Mungu akaumba viumbe wanaojukumishwa, wala hakuwaumba kwa sababu anahitaji chochote kutoka kwao.
#
{57} فما يريد {منهم من رزقٍ وما} يريدُ {أن يطعمونِ}: تعالى الغنيُّ المغني عن الحاجة إلى أحدٍ بوجه من الوجوه، وإنَّما جميع الخلق فقراءُ إليه في جميع حوائجهم ومطالبهم الضروريَّة وغيرها.
{57} Basi hataki "kwao riziki wala" hataki "wanilishe" Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mkwasi, na hana haja yoyote kwa chochote, lakini viumbe vyote vinamhitaji katika mahitaji yao yote muhimu, matakwa, na mambo mengineyo.
#
{58} ولهذا قال: {إنَّ الله هو الرزَّاقُ}؛ أي: كثير الرزق، الذي ما من دابَّةٍ في الأرض ولا في السماء إلاَّ على الله رزقُها، ويعلمُ مستقرَّها ومستودَعَها، {ذو القوَّةِ المتينُ}؛ أي: الذي له القوة والقدرةُ كلُّها، الذي أوجد بها الأجرام العظيمة السفليَّة والعلويَّة، وبها تصرَّف في الظواهر والبواطن، ونفذت مشيئته في جميع البريَّات؛ فما شاء الله كان، وما لم يشأ لم يكن، ولا يعجِزُه هاربٌ، ولا يخرج عن سلطانه أحدٌ، ومن قوَّته أنه أوصل رزقه إلى جميع العالم، ومن قدرته وقوَّته أنه يبعث الأموات بعدما مزَّقهم البِلى، وعصفت بهم الرياحُ، وابتلعتْهم الطيور والسِّباع، وتفرَّقوا وتمزَّقوا في مهامه القفار ولُجج البحار؛ فلا يفوته منهم أحدٌ، ويعلم ما تَنْقُصُ الأرضُ منهم؛ فسبحان القويِّ المتين.
{58} Ndiyo maana akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuruzuku." Yaani, Mwenye riziki nyingi, ambaye kwa hakika hakuna kiumbe kilicho hai katika ardhi wala mbinguni isipokuwa riziki yake iko juu ya Mwenyezi Mungu kukipa. Naye anajua makao yake na mapitio yake. "Mwenye nguvu, Madhubuti." Yaani, Yeye ndiye mwenye nguvu na uwezo wote, ambaye kwa hayo aliumba miili mikubwa ya chini na ya juu, na kupitia hayo akaendesha mambo ya nje na ya ndani, na mapenzi yake yalifanyika kwa viumbe vyote. Chochote akitakacho Mwenyezi Mungu kinakuwa, na asichotaka hakiwi, wala hamshindi mwenye kukimbia, na hakuna anayeweza kutoka katika mamlaka yake. Na katika nguvu zake ni kwamba alifikisha riziki Yake kwa ulimwengu wote, na katika nguvu zake ni kwamba atawafufua wafu baada ya kutawanywa na kuoza, na kupeperushwa na upepo, na kumezwa na ndege na wanyama wa porini, na kutawanywa na kukatikakatika vipande ndani ya majangwa na vilindi vya bahari. Basi hakuna hata mmoja wao anayeweza kumkwepa, na anajua kiasi cha kila kinachopunguzwa na ardhi kutokana nao. Basi ametakasika Mwenye Nguvu Madhubuti.
: 59 - 60 #
{فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا ذَنُوبًا مِثْلَ ذَنُوبِ أَصْحَابِهِمْ فَلَا يَسْتَعْجِلُونِ (59) فَوَيْلٌ لِلَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ يَوْمِهِمُ الَّذِي يُوعَدُونَ (60)}.
59. Hakika wale waliodhulumu wana fungu lao la adhabu kama fungu la wenzao. Basi wasiniharakishe. 60. Basi ole wao wale walioikanusha siku yao waliyoahidiwa.
#
{59} أي: {فإنَّ للذين ظلموا}: بتكذيبهم محمداً - صلى الله عليه وسلم - من العذاب والنَّكال {ذَنوباً}؛ أي: نصيباً وقسطاً، مثل ما فُعِلَ بأصحابهم من أهل الظُّلم والتكذيب، {فلا يستعجلونَ}: بالعذاب؛ فإنَّ سنة الله في الأمم واحدةٌ؛ فكلُّ مكذِّب يدوم على تكذيبه من غير توبةٍ وإنابةٍ؛ فإنَّه لا بدَّ أن يقع عليه العذابُ ولو تأخَّر عنه مدَّة.
{59} Yaani, "Hakika wale waliodhulumu" kwa kumkanusha Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie - watapata adhabu na mateso "fungu lao la adhabu" kama walivyofanyiwa wenzao waliodhulumu na kukadhibisha. "Basi wasiniharakishe" kuwaletea adhabu. Kwani hakika desturi ya Mwenyezi Mungu katika umma zote ni moja. Nayo ni kwamba kila mwenye kukadhibisha na akaendelea na kukadhibisha bila ya toba wala kurejea kwa Mwenyezi Mungu, basi hapana budi ataadhibiwa hata kama itachelewa kumfikia kwa muda.
#
{60} ولهذا توعَّدهم الله بيوم القيامة، فقال: {فويلٌ للذين كفروا من يومهمُ الذي يوعَدون}: وهو يومُ القيامةِ، الذي قد وُعِدوا فيه بأنواع العذاب والنَّكال [والسلاسل] والأغلال؛ فلا مغيثَ ولا منقذَ لهم من عذاب الله. نعوذ بالله منه.
{60} Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akawatishia kwa Siku ya Kiyama, akasema: "Basi ole wao wale walioikanusha siku yao waliyoahidiwa." Nayo ni siku ya Kiyama ambayo wameahidiwa ndani yake adhabu mbalimbali na mateso [na minyororo] na pingu, na wala hakutakuwa na wa kuwasaidia wala kuwaokoa mbali na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na adhabu hiyo.
******