Ilishuka Makka.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{ق وَالْقُرْآنِ الْمَجِيدِ (1) بَلْ عَجِبُوا أَنْ جَاءَهُمْ مُنْذِرٌ مِنْهُمْ فَقَالَ الْكَافِرُونَ هَذَا شَيْءٌ عَجِيبٌ (2) أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا ذَلِكَ رَجْعٌ بَعِيدٌ (3) قَدْ عَلِمْنَا مَا تَنْقُصُ الْأَرْضُ مِنْهُمْ وَعِنْدَنَا كِتَابٌ حَفِيظٌ (4)}
1. Qaaf. Ninaapa kwa Qur-ani tukufu! 2. Bali wanastaajabu kwamba amewafikia mwonyaji kutoka miongoni mwao,
na wakasema makafiri: 'Hili ni jambo la ajabu! 3. Ati tukifa na tukawa udongo...? Kurejea huko kuko mbali!' 4. Hakika Sisi tunajua kiasi cha kila kinachopunguzwa na ardhi kutokana nao. Na kwetu kipo Kitabu kinachohifadhi vyema yote.
#
{1} يقسم تعالى بـ {القرآنِ المجيد}؛ أي: وسيع المعاني، عظيمها، كثير الوجوه، كثير البركات، جزيل المبرات، والمجد سعة الأوصاف وعظمتها، وأحق كلام يوصف بذلك هذا القرآن، الذي قد احتوى على علوم الأوَّلين والآخرين، الذي حوى من الفصاحة أكملَها، ومن الألفاظ أجزلَها، ومن المعاني أعمَّها وأحسنها.
{1} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaapa kwa "Qur’ani Tukufu." Yaani, yenye maana pana na tukufu, yenye njia nyingi, yenye baraka nyingi. Kwani maneno yanayostahiki zaidi kusifiwa hivi ni Qur-ani hii, ambayo inajumuisha elimu za wa mwanzo na wa mwisho, ambayo ndiyo yenye ufasaha kamili zaidi, maneno mengi zaidi, na maana ya kujumuisha zaidi na bora zaidi.
#
{2} وهذا موجب لكمال اتِّباعه وسرعة الانقياد له وشكر الله على المنَّة به، ولكن أكثر الناس لا يقدِّر نعمَ الله قَدْرَها، ولهذا قال تعالى: {بلْ عَجِبوا}؛ أي: المكذِّبون للرسول - صلى الله عليه وسلم -، {أن جاءَهُم منذرٌ منهم}؛ أي: يُنْذرهم ما يضرُّهم ويأمرهم بما ينفعهم، وهو من جنسهم، يمكنُهم التلقِّي عنه ومعرفة أحوالِه وصدقِه، فتعجَّبوا من أمرٍ لا ينبغي لهم التعجُّب منه، بل يتعجَّب من عَقل من تعجب منه، {فقالَ الكافرون}؛ أي: الذين حَمَلَهُم كفرُهم وتكذيبُهم لا نقص بذكائِهِم وآرائِهِم: {هذا شيءٌ عجيبٌ}؛ أي: مستغربٌ.
وهم في هذا الاستغراب بين أمرين: إمَّا صادقونَ في استغرابهم وتعجُّبهم؛ فهذا يدلُّ على غاية جهلهم وضعف عقولهم؛ بمنزلة المجنون الذي يستغربُ كلامَ العاقل، وبمنزلة الجبانِ الذي يتعجَّب من لقاء الفارس للفرسان، وبمنزلة البخيل الذي يستغرب سخاء أهل السَّخاء؛ فأيُّ ضررٍ يلحق من تعجب مَن هذه حالُه؟! وهل تعجُّبه إلا دليلٌ على زيادة جهله وظلمه ؟! وإما أن يكونوا متعجِّبين على وجهٍ يعلمون خطأهم فيه؛ فهذا من أعظمِ الظُّلم وأشنعِه.
{2} Hili linalazimu kuifuata kikamilifu, kutekeleza mambo yake haraka, na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema ya kutupa Qur-ani hii, lakini watu wengi hawazithamini neema za Mwenyezi Mungu kama zinavyostahiki,
na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Bali wanastaajabu." Yaani wale waliomkadhibisha Mtume – Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – "kwamba amewafikia mwonyaji kutoka miongoni mwao" ili awaonye dhidi ya mambo yatakayowadhuru na awaamrishe yale yatakayowafaa, naye ni wa aina sawa nao, ambaye wanaweza kujifunza kutoka kwake na kujua hali zake na ukweli wake, kwa hivyo wakastaajabia jambo ambalo hawapaswi kulistaajabia. Bali inastaajabiwa akili ya mwenye kustaajabishwa na hilo.
"Na wakasema makafiri" ambao walifanywa na ukafiri wao na kukadhibisha kwao si kwa sababu ya kuwa na upungufu katika werevu wao na maoni yao: "Hili ni jambo la ajabu!" Katika mshangao wao huu,
wako baina ya vitu viwili: ima ni wakweli katika mshangao wao huo. Na hili linaashiria ujinga wao wa hali ya juu na udhaifu wa akili zao. Wako kama mwendawazimu ambaye anashangazwa na maneno ya mtu mwenye akili timamu, na wako kama mwoga anayeshangazwa na wapiganaji hodari wanapokutana na wapiganaji wengine hodari, na ni kama bahili anayeshangazwa na ukarimu wa watu wakarimu. Ni madhara gani yatakayotokea kwa sababu ya kushangaa kwa mtu ambaye hii ndiyo hali yake? Je, kustaajabu kwake huku si isipokuwa ushahidi juu ya kuongezeka kwa ujinga na dhuluma yake? Na ima wanashangazwa kwa namna ambayo tayari wanajua makosa yao katika hilo. Basi hii ndiyo dhuluma kubwa na mbaya kabisa.
#
{3 - 4} ثم ذكر وجه تعجُّبهم، فقال: {أإذا مِتْنا وكُنَّا تراباً ذلك رَجْعٌ بعيدٌ}: فقاسوا قدرة من هو على كلِّ شئٍ قديرٌ الكامل من كلِّ وجهٍ، بقدرة العبد الفقير العاجز من جميع الوجوه! وقاسوا الجاهلَ الذي لا علمَ له، بمن هو بكلِّ شيءٍ عليمٌ، الذي يعلم {ما تَنقُصُ الأرضُ}: من أجسادهم مدَّة مقامِهم في البرزخِ ، وقد أحصى في كتابه الذي هو عنده - محفوظٌ عن التغيير والتبديل - كلَّ ما يجري عليهم في حياتهم ومماتهم. وهذا استدلالٌ بكمال سعة علمه ، التي لا يحيطُ بها إلاَّ هو على قدرته على إحياء الموتى.
{3 - 4} Kisha akataja sababu ya mshangao wao,
akasema: "Ati tukifa na tukawa udongo...? Kurejea huko kuko mbali!" Hapo walilinganisha uwezo wa Mwenye uwezo zaidi juu ya kila kitu, Mkamilifu kwa namna zote kwa uwezo wa mja mhitaji asiyejiweza kwa namna zote! Wakamlinganisha mjinga asiye na elimu na Yule anayejua zaidi kila kitu, ambaye anajua "kiasi cha kila kinachopunguzwa na ardhi," kama vile miili yao muda wa kukaa kwao kaburini, na amedhibiti katika kitabu chake ambacho kiko kwake - kilichohifadhiwa kutokana na mabadiliko na mageuzi - kila kitu kitakachowatokea katika maisha yao na baada ya kifo chao. Huku ni kutumia ushahidi wa ukamilifu wa upana wa elimu yake, ambao hakuna anayeweza kuudhibiti isipokuwa Yeye, juu ya uwezo wake wa kuwafufua wafu.
{بَلْ كَذَّبُوا بِالْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ فَهُمْ فِي أَمْرٍ مَرِيجٍ (5)}
5. Lakini waliikanusha Haki ilipowajia; kwa hivyo wamo katika mambo ya mchanganyiko.
#
{5} أي: {بل}: كلامُهم الذي صدر منهم إنَّما هو عنادٌ وتكذيبٌ للحقِّ الذي هو أعلى أنواع الصدق. {لمَّا جاءهم فهم في أمرٍ مَريجٍ}؛ أي: مختلطٍ مشتبهٍ، لا يثبتون على شيءٍ، ولا يستقرُّ لهم قرارٌ، فتارةً يقولون عنك: إنَّك ساحرٌ! وتارةً: مجنونٌ! وتارة: شاعرٌ! وكذلك جعلوا القرآن عِضين، كلٌّ قال فيه ما اقتضاه فيه رأيُه الفاسدُ. وهكذا كلُّ من كذَّب بالحقِّ؛ فإنَّه في أمرٍ مختلطٍ، لا يدرى له وجهٌ ولا قرارٌ، فترى أموره متناقضةً مؤتفكةً؛ كما أنَّ من اتَّبع الحقَّ وصدق به قد استقام أمرُه واعتدل سبيلُه، وصدق فعلُه قيلَه.
{5} Yaani, "Lakini" maneno yao waliyoyasema si chochote ila ukaidi na kukadhibisha tu haki, ambayo ndiyo aina ya juu kabisa ya ukweli. "ilipowajia; kwa hivyo wamo katika mambo ya mchanganyiko." na wala hawakai imara juu ya kitu chochote, wala hatulii juu ya suala lolote.
Kwani wakati mwingine wanasema juu yako: 'Hakika wewe ni mchawi!' Na wakati mwingine wanasema: 'Wazimu!' Na wakati mwingine wanasema: 'Mshairi!' Kadhalika, waliifanya Qur-ani kuwa sehemu mbili, kila mmoja wao akasema juu yake yale ambayo rai yake ya upotovu ilitaka aseme. Na hali kadhalika kila anayeikadhibisha haki. Yeye kila wakati huwa katika jambo lililochanganyika, halijui wala hatulii kwa chochote. Basi utaona mambo yake yanapingana na ya uwongo, kama vile mwenye kufuata haki na kuisadiki, mambo yake huwa yamenyooka, njia yake huwa iko sawasawa, na matendo yake yakasadiki maneno yake.
{أَفَلَمْ يَنْظُرُوا إِلَى السَّمَاءِ فَوْقَهُمْ كَيْفَ بَنَيْنَاهَا وَزَيَّنَّاهَا وَمَا لَهَا مِنْ فُرُوجٍ (6) وَالْأَرْضَ مَدَدْنَاهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنْبَتْنَا فِيهَا مِنْ كُلِّ زَوْجٍ بَهِيجٍ (7) تَبْصِرَةً وَذِكْرَى لِكُلِّ عَبْدٍ مُنِيبٍ (8) وَنَزَّلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً مُبَارَكًا فَأَنْبَتْنَا بِهِ جَنَّاتٍ وَحَبَّ الْحَصِيدِ (9) وَالنَّخْلَ بَاسِقَاتٍ لَهَا طَلْعٌ نَضِيدٌ (10) رِزْقًا لِلْعِبَادِ وَأَحْيَيْنَا بِهِ بَلْدَةً مَيْتًا كَذَلِكَ الْخُرُوجُ (11)}
6. Je, hawaangalii mbingu zilizo juu yao! Vipi tulivyozijenga, na tukazipamba. Wala hazina nyufa. 7. Na ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna. 8. Yawe haya ni kifumbua macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kurejea
(kwa Mwenyezi Mungu). 9. Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji yaliyobarikiwa, na kwa hayo tukaotesha mabustani na nafaka za kuvunwa. 10. Na mitende mirefu yenye makole yaliyozaa kwa wingi. 11. Ili iwe ni riziki kwa waja wangu. Na tukaifufua kwa maji nchi iliyokuwa imekufa. Kama hivyo ndivyo utakavyokuwa ufufuaji.
#
{6} لمَّا ذكر تعالى حالة المكذِّبين وما ذمَّهم به؛ دعاهم إلى النَّظر في آياته الأفقيَّة كي يعتبروا ويستدلُّوا بها على ما جُعلت أدلةً عليه، فقال: {أفلمْ ينظُروا إلى السماءِ فوقَهم}؛ أي: لا يحتاجُ ذلك النظرُ إلى كلفةٍ وشدِّ رحل، بل هو في غاية السهولة، فينظرون {كيفَ بَنَيْناها}: قبةً مستويةَ الأرجاء ثابتة البناء مزيَّنةً بالنجوم الخُنَّس والجواري الكُنَّس، التي ضُرِبتْ من الأفُق إلى الأفُق في غاية الحسن والملاحة، لا ترى فيها عيباً ولا فروجاً ولا خلالاً ولا إخلالاً، قد جعلها الله سقفاً لأهل الأرض، وأودع فيها من مصالحهم الضروريَّة ما أودع.
{6} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja hali ya wale wanaokadhibisha na yale aliyowakashifu kwayo, akawalingania kuzitazama ishara zake za kiupeo wa macho ili wazingatie na wazitumie kuwa ni ushahidi kwa yale ambayo zilifanywa kuwa ni ushahidi wake.
Akasema: "Je, hawaangalii mbingu zilizo juu yao!" Yaani kutazama huku hakujitaji gharama yoyote wala kuandaa chochote kwa ajili ya kusafiri, badala yake ni rahisi sana, kwa hivyo waangalie "vipi tulivyozijenga" kama kuba na pande zilizowekwa sawasawa, zenye ujenzi thabiti, zilizopambwa kwa nyota zinazorejea nyuma, zinazokwenda kisha zikajificha, ambazo ziliwekwa kutoka upeo wa macho hadi upeo wa macho katika uzuri wa hali ya juu na ukamilifu, na huwezi kuona kasoro yoyote ndani yake wala nyufa wala hitilafu, Mwenyezi Mungu alizifanya kuwa dari ya wakazi wa ardhini, na akaweka humo masilahi yao ya lazima.
#
{7} وإلى الأرض كيف مَدَدْناها ووسَّعناها حتى أمكن كلَّ حيوانٍ السكونُ فيها والاستقرار والاستعداد لجميع مصالحه، وأرساها بالجبال؛ لتستقرَّ من التَّزلزل والتموُّج. {وأنبَتْنا فيها من كلِّ زوجٍ بهيجٍ}؛ أي: من كل صنفٍ من أصناف النبات التي تسرُّ ناظريها، وتُعْجِب مبصريها، وتُقِرُّ عين رامقيها لأكل بني آدم وأكل بهائمهم ومنافعهم.
{7} Na ardhi jinsi tulivyoitandaza na kuipanua mpaka kila mnyama akatulia ndani yake, na tukaandaa humo mahitaji yake yote, na tukaisimamisha sawasawa kwa milima; ili itulie na isiwe mitetemeko na kuyumbayumba. "Na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna" ambayo inawapendeza wenye kuitazama, na huwastaajabisha wenye kuiona, na hufurahisha mno macho ya wale wanaoitazama kwa makini, ili waile wanadamu na mifugo yao na kwa ajili ya manufaa yao.
#
{8 - 11} وخصَّ من تلك المنافع [بالذكر] الجنَّات المشتملة على الفواكه اللَّذيذة من العنب والرُّمان والأترجِّ والتُّفاح وغير ذلك من أصناف الفواكه، ومن النخيل الباسقات؛ أي: الطوال، التي يطول نفعها ، وترتفع إلى السماء حتى تبلغ مبلغاً لا يبلغه كثيرٌ من الأشجار، فتخرجَ من الطلع النضيد في قنوانها ما هو رزقٌ للعباد قوتاً وأدماً وفاكهةً يأكلون منه ويدَّخرون هم ومواشيهم. وكذلك ما يخرج الله بالمطر، وما هو أثره من الأنهار التي على وجه الأرض و [التي] تحتها من {حبِّ الحصيدِ}؛ أي: من الزَّرع المحصود من بُرٍّ وشعير وذرة وأرزٍّ ودخن وغيره؛ فإن في النظر في هذه الأشياء {تبصرةً}: يُتَبَصَّر بها من عمى الجهل، {وذكرى}: يُتَذَكَّر بها ما ينفع في الدين والدنيا، ويُتَذَكَّر بها ما أخبر الله به وأخبرت به رسله، وليس ذلك لكلِّ أحدٍ، بل {لكلِّ عبدٍ منيبٍ} إلى الله؛ أي: مقبل عليه بالحبِّ والخوف والرجاء وإجابة داعيه، وأمَّا المكذِّب أو المعرض؛ فما تغني الآياتُ والنُّذُر عن قوم لا يؤمنون.
وحاصلُ هذا أنَّ ما فيها من الخلق الباهر والقوَّة والشدَّة دليلٌ على كمال قدرة الله تعالى، وما فيها من الحسن والإتقان وبديع الصنعة وبديع الخلقة دليلٌ على أنَّ اللهَ أحكمُ الحاكمين، وأنَّه بكلِّ شيء عليمٌ، وما فيها من المنافع والمصالح للعباد دليلٌ على رحمة الله التي وسعت كل شيء، وجوده الذي عمَّ كلَّ حيٍّ، وما فيها من عظمة الخلقة وبديع النِّظام دليلٌ على أنَّ الله تعالى هو الواحدُ الأحدُ الفردُ الصمدُ الذي لم يتَّخذ صاحبةً ولا ولداً، ولم يكن له كفواً أحدٌ، وأنه الذي لا تنبغي العبادة والذُّلُّ والحبُّ إلاَّ له، وما فيها من إحياء الأرض بعد موتها دليلٌ على إحياء الله الموتى ليجازِيَهم بأعمالهم، ولهذا قال: {وأحْيَيْنا به بلدةً ميتاً كذلك الخروجُ}.
ولمَّا ذكَّرهم بهذه الآيات السماوية والأرضيَّة؛ خوَّفهم أخذات الأمم، وألاَّ يستمرُّوا على ما هم عليه من التكذيب، فيصيبهم ما أصاب إخوانَهم من المكذِّبين، فقال:
{8 - 11} Miongoni mwa manufaa hayo, alizitaja kwa njia mahususi bustani zenye matunda matamu kama vile zabibu, mikomamanga, michungwa, tufaha na aina nyinginezo za matunda, na mitende mikubwa, ambayo manufaa yake ni marefu, na inamea ikaenda juu mpaka ikafikia urefu ambao miti mingi haifiki. Kisha ikatoa makole yaliyozaa kwa wingi katika mashada yake vitu ambavyo ni riziki ya waja, chakula kikuu, vitoweo, na matunda wanayokula na kujiwekea akiba wao na mifugo yao. Na vile vile anachokitoa Mwenyezi Mungu kwa mvua, na matokeo yake kama vile mito iliyo juu ya uso wa ardhi na chini yake, "nafaka za kuvunwa" kama vile ngano, shayiri, mahindi, mchele, mtama, na vitu vinginevyo. Katika kuzingatia mambo haya, kuna
“kifumbua macho” kutokana na upofu wa ujinga, na “ukumbusho” ambao mtu anakumbushwa kwa huo yale yenye manufaa katika dini na dunia, na mtu anakumbushwa kwa hayo yale ambayo Mwenyezi Mungu alimjulisha na yale waliyosema Mitume wake. Hilo si kwa kila mtu, bali “kwa mja mwenye kurejea
(kwa Mwenyezi Mungu)." Yule anayeelekea kwake kwa upendo, hofu, matumaini, na kuitikia mwenye kumuomba. Na ama mwenye kukadhibisha au mwenye kupeana mgongo, basi ishara zote na maonyo hayawafai kitu watu wasioamini. Jumla ya hayo ni kwamba yaliyomo ndani yake ya uumbaji, nguvu, na ugumu ni ushahidi wa ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na yaliyomo ndani yake ya uzuri, ustadi mkubwa, ufundi na uumbaji wa hali ya juu ni ushahidi kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuhukumu vyema zaidi ya mahakimu wote, na kwamba Yeye anajua mno kila kitu, na yale yaliyomo ndani yake ya manufaa na masilahi kwa waja wake ni ushahidi wa rehema ya Mwenyezi Mungu, ambayo imeenea kila kitu, na kupeana kwake kwa wingi ambako kumejumuisha kila kilicho hai. Na viumbe vikuu vilivyomo ndani yake na mpangilio wake wa ajabu ni ushahidi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mmoja, wa Pekee, Mkusudiwa ambaye hakujifanyia mke wala mwana, wala hana anayelingana naye hata, na kwamba ni Yeye ambaye hakuna kinachostahiki kuabudiwa, kumnyenyekea, kumpenda isipokuwa Yeye tu. Ndiyo maana akasema, "Na tukaifufua kwa maji nchi iliyokuwa imekufa. Kama hivyo ndivyo utakavyokuwa ufufuaji." Na alipowakumbusha Aya hizi za kimbinguni na za kiardhini, akahofisha na adhabu walizopata umma waliotangulia, na kwamba wasiendelee katika hali yao ya kukadhibisha, yakaja yakawapata yale yaliyowapata ndugu zao waliokadhibisha.
Akasema:
{كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَأَصْحَابُ الرَّسِّ وَثَمُودُ (12) وَعَادٌ وَفِرْعَوْنُ وَإِخْوَانُ لُوطٍ (13) وَأَصْحَابُ الْأَيْكَةِ وَقَوْمُ تُبَّعٍ كُلٌّ كَذَّبَ الرُّسُلَ فَحَقَّ وَعِيدِ (14) أَفَعَيِينَا بِالْخَلْقِ الْأَوَّلِ بَلْ هُمْ فِي لَبْسٍ مِنْ خَلْقٍ جَدِيدٍ (15)}
12. Kabla yao walikadhibisha kaumu ya Nuhu na wakazi wa Rassi na Thamudi. 13. Na A'di na Firauni na kaumu ya Luti. 14. Na wakazi wa Machakani, na watu wa Tubbaa'. Wote hao waliwakanusha Mitume, kwa hivyo onyo likathibitika juu yao. 15. Kwani tulichoka kwa kuumba mara ya kwanza? Bali wao wamo katika shaka tu juu ya umbo jipya.
#
{12 - 14} أي: كذَّب الذين من قبلهم من الأمم رُسُلَهم الكرام وأنبياءَهم العظام؛ كنوح كذَّبه قومه، وثمود كذَّبوا صالحاً، وعاد كذَّبوا هوداً، وإخوان لوطٍ كذَّبوا لوطاً، وأصحابُ الأيكةِ كذَّبوا شعيباً، وقوم تُبَّعٍ - وتُبَّعٌ كل ملكٍ مَلَكَ اليمن في الزمان السابق قبل الإسلام - فقوم تُبَّع كذَّبوا الرسول الذي أرسله الله إليهم، ولم يخبرْنا اللهُ من هو ذلك الرسولُ، وأيُّ تُبَّعٍ من التَّبابعة؛ لأنه - والله أعلم - كان مشهوراً عند العرب العرباء ، الذين لا تخفى ماجرياتهم على العرب، خصوصاً مثل هذه الحادثة العظيمة؛ فهؤلاء كلُّهم كذَّبوا الرُّسل الذين أرسلهم الله إليهم، فحقَّ عليهم وعيدُ الله وعقوبته، ولستم أيُّها المكذِّبون لمحمدٍ - صلى الله عليه وسلم - خيراً منهم، ولا رسلهم أكرم على الله من رسولكم؛ فاحذروا جرمهم؛ لئلاَّ يصيبكم ما أصابهم.
{12 - 14} Yaani: kaumu za kabla yao ziliwakadhibisha Mitume wao watukufu na Manabii wakuu kama vile Nuhu watu wake walimkadhibisha, na Thamud walimkadhibisha Saleh, na 'Adi wakamkadhibisha Hud, na ndugu zake Lut'i wakamkadhibisha Lut'i, na watu wa wa Kichakani walimkadhibisha Shuaibu na watu wa Tuba' - ambaye ni kila mfalme aliyewahi kutawala Yemen hapo awali kabla ya Uislamu. Hao pia walimkadhibisha Mtume ambaye Mwenyezi Mungu aliwatumia, lakini Mwenyezi Mungu hakutuambia alikuwa ni nani Mtume huyo, na ni Tuba' yuko miongoni mwa hao Tuba', kwa sababu - na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi - alikuwa maarufu miongoni mwa Waarabu wa asili, ambao matukio yao hayafichiki kwa Waarabu, hasa tukio kubwa kama hilo. Watu wote hawa waliwakadhibisha Mitume waliotumiwa na Mwenyezi Mungu, kwa hivyo onyo likathibitika juu yao na adhabu yake, na nyinyi mnaomkadhibisha Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake - si bora kuliko wao, wala Mitume wao sio mwenye heshima zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko Mtume wenu. Basi jihadhari na uhalifu wao; Ili yaliyowapata yasije yakakupateni pia.
#
{15} ثم استدل تعالى بالخلق الأول ـ وهو النشأة الأولى ـ على الخلق الآخر ـ وهو النشأة الآخرة ـ؛ فكما أنه الذي أوجدهم بعد العدم؛ كذلك يعيدهم بعد موتهم وصيرورتهم إلى الرُّفات والرِّمم، فقال: {أفَعَيينا}؛ أي: أفعَجَزْنا وضعفتْ قدرتُنا {بالخلق الأوَّلِ}: ليس الأمر كذلك، فلم نعجز ونعيَ عن ذلك، وليسوا في شكٍّ من ذلك، وإنما {هم في لَبْسٍ من خَلْقٍ جديدٍ}: هذا الذي شكُّوا فيه والتبس عليهم أمره، مع أنَّه لا محلَّ للَّبس فيه؛ لأنَّ الإعادة أهونُ من الابتداء؛ كما قال تعالى: {وهو الذي يبدأ الخَلْقَ ثمَّ يعيدُهُ وهو أهونُ عليه}.
{15} Kisha Mwenyezi Mungu akatumia uumbaji wa kwanza kama ushahidi juu ya uumbaji wa mwisho wa akhera. Kwani kama vile Yeye ndiye aliyewaumba baada ya kutokuwa kitu, pia atawarudisha baada ya kufa kwao na kuwa kwao mapande yaliyovurugika na mifupa iliyokwisha mung'unyika, akasema, "Kwani tulichoka" na ukadhoofika uwezo wetu "kwa kuumba mara ya kwanza." Sivyo hivyo, tena hawana shaka na hilo, "Bali wao wamo katika mchanganyiko tu juu ya umbo jipya," ijapokuwa si kitu cha kuwa na mchanganyiko juu yake. Kwa sababu kurudisha ni rahisi mno kuliko kuanzisha. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na Yeye ndiye anayeanzisha uumbaji, kisha ataurudisha mara nyengine. Na jambo hili ni jepesi zaidi kwake."
{وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ وَنَعْلَمُ مَا تُوَسْوِسُ بِهِ نَفْسُهُ وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ (16) إِذْ يَتَلَقَّى الْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ قَعِيدٌ (17) مَا يَلْفِظُ مِنْ قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ (18)}.
16. Na hakika tulimuumba mtu, nasi tunayajua yanayomtia wasiwasi katika nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake. 17. Wanapopokea wapokeaji wawili, wanaokaa kuliani na kushotoni. 18. Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari.
#
{16} يخبر تعالى أنَّه المتفرِّد بخلق جنس الإنسان ذكورِهم وإناثِهم، وأنَّه يعلم أحواله وما يُسِرُّه وتوسوس به نفسه ، وأنه {أقربُ إليه من حبلِ الوريدِ}: الذي هو أقرب شيء إلى الإنسان، وهو [العرق] المكتنف لثُغرة النحر. وهذا ممّا يدعو الإنسان إلى مراقبة خالقه، المطَّلع على ضميره وباطنه، القريب إليه في جميع أحواله، فيستحي منه أن يراه حيث نهاه، أو يفقده حيث أمره.
{16} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kwamba Yeye ndiye wa Pekee katika kuumba jamii ya wanadamu, wanaume na wanawake, na kwamba anazijua hali zake na yale anayoyaficha na yale yanayomtia wasiwasi katika nafsi yake, na kwamba Yeye
“Yuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake” ambao ndio kitu cha karibu zaidi na mwanadamu, na hili ni katika mambo yanayoweza kumfanya mtu kumchunga Muumba wake, ambaye anaifahamu vyema dhamiri yake na ndani yake, ambaye yuko karibu naye katika hali zake zote, kwa hivyo akastahi amuone pale alipomkataza, au amkose ambapo alimwamuru kuwa.
#
{17} وكذلك ينبغي له أن يجعل الملائكةَ الكرامَ الكاتبين منه على بال، فيجلُّهم ويوقِّرهم ويحذر أن يفعل أو يقول ما يكتب عنه ممَّا لا يرضي ربَّ العالمين، ولهذا قال: {إذْ يَتَلَقَّى المُتَلَقِّيانِ}؛ أي: يتلقَّيانِ عن العبد أعماله كلَّها، واحدٌ {عن اليمين}: يكتب الحسنات، {و} الآخر {عن الشمال}: يكتب السيئات، وكل منهما مقيدٌ بذلك، متهيئٌ لعمله الذي أعدَّ له، ملازمٌ لذلك.
17. Vivyo hivyo na awaweke katika akili yake Malaika watukufu wanaoandika mambo yake, na awape taadhima na kuwaheshimu, na atahadhari kufanya au kusema anayoandikiwa miongoni mwa yale asiyoyaridhia Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Ndiyo maana akasema: "Wanapopokea wapokeaji wawili" vitendo vya mja vyote, mmoja wao "kuliani" akiandika mema, "na" mwingine wao "kushotoni" akiandika mabaya, na kila mmoja wao amewekewa mipaka kwa hayo, na yuko tayari kwa kazi ambayo ametayarishwa kwa ajili yake, na kila wakati anaandamana naye na wala hatengani naye.
#
{18} {ما يَلْفِظُ من قولٍ}: خير أو شرٍّ {إلاَّ لديه رقيبٌ عتيدٌ}؛ أي: مراقب له، حاضرٌ لحاله؛ كما قال تعالى: {وإنَّ عليكم لحافظينَ. كراماً كاتبينَ. يعلمون ما تفعلون}.
{18} "Hatamki neno" jema au baya "ila karibu yake yupo mwangalizi tayari," wanaomwangalia na wanajua vyema hali zake, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu. Waandishi wenye heshima. Wanayajua mnayoyatenda."
{وَجَاءَتْ سَكْرَةُ الْمَوْتِ بِالْحَقِّ ذَلِكَ مَا كُنْتَ مِنْهُ تَحِيدُ (19) وَنُفِخَ فِي الصُّورِ ذَلِكَ يَوْمُ الْوَعِيدِ (20) وَجَاءَتْ كُلُّ نَفْسٍ مَعَهَا سَائِقٌ وَشَهِيدٌ (21) لَقَدْ كُنْتَ فِي غَفْلَةٍ مِنْ هَذَا فَكَشَفْنَا عَنْكَ غِطَاءَكَ فَبَصَرُكَ الْيَوْمَ حَدِيدٌ (22)}
19. Na uchungu wa kutoka roho utamjia kwa haki. Hayo ndiyo uliyokuwa ukiyakimbia. 20. Na litapulizwa baragumu. Hiyo ndiyo Siku ya Miadi. 21. Na kila nafsi itakuja na pamoja nayo mchungaji na shahidi. 22.
(Aambiwe): 'Kwa hakika ulikuwa umeghafilika mbali na haya. Basi leo tumekuondolea pazia lako, na kwa hivyo kuona kwako leo ni kukali mno.'
#
{19} أي: وجاءت هذا الغافل المكذِّب بآيات الله، {سَكْرَةُ الموتِ بالحقِّ}: الذي لا مردَّ له ولا مناص. {ذلك ما كنتَ منه تَحيدُ}؛ أي: تتأخَّر وتنكصُ عنه.
{19} Yaani, ukamjia huyu aliyeghafilika, ambaye anakadhibisha Aya za Mwenyezi Mungu, "uchungu wa kutoka roho kwa haki," ambao hakuna kuurudisha nyuma wala kuuepuka. "Hayo ndiyo uliyokuwa ukiyakimbia."
#
{20} {ونُفِخَ في الصُّورِ ذلك يَوْمُ الوعيدِ}؛ أي: اليوم الذي يلحقُ الظالمين ما أوعدهم الله به من العقاب والمؤمنين ما وعدهم به من الثواب.
{20} "Na litapulizwa baragumu. Hiyo ndiyo Siku ya Miadi." Yaani, siku ambayo madhalimu watapata adhabu aliyowaahidi Mwenyezi Mungu, nao Waumini watapata malipo mazuri aliyowaahidi.
#
{21} {وجاءتْ كلُّ نفسٍ معها سائقٌ}: يسوقُها إلى موقف القيامة؛ فلا يمكنُها أن تتأخَّر عنه، {وشهيدٌ}: يشهدُ عليها بأعمالها؛ خيرِها وشرِّها. وهذا يدلُّ على اعتناء الله بالعباد، وحفظه لأعمالهم، ومجازاته لهم بالعدل.
{21} "Na kila nafsi itakuja na pamoja nayo mchungaji" akiipeleka mahala pa kusimamia pa Kiyama, na wala haitaweza kuchelewa kufika hapo. "Na shahidi" ambaye ataishuhudilia matendo yake, mazuri na mabaya. Hili linaashiria kwamba Mwenyezi Mungu anawajali sana waja wake, na kwamba anawahifadhia matendo yao, na kwamba atawalipa kwa uadilifu.
#
{22} فهذا الأمر مما يجب أن يجعله العبدُ منه على بالٍ، ولكن أكثر الناس غافلون، ولهذا قال: {لقد كُنتَ في غفلةٍ من هذا}؛ أي: يقال للمعرض المكذِّب يوم القيامة هذا الكلام توبيخاً ولوماً وتعنيفاً؛ أي: لقد كنتَ مكذِّباً بهذا تاركاً للعمل له. {فـ}: الآن {كَشَفْنا عنك غِطاءَك}: الذي غطَّى قلبَك فكثر نومُك واستمرَّ إعراضُك، {فبصرُك اليومَ حديدٌ}: ينظر ما يزعجه ويروِّعه من أنواع العذاب والنَّكال، أو هذا خطابٌ من الله للعبد؛ فإنَّه في الدُّنيا في غفلةٍ عما خُلِقَ له، ولكنه يوم القيامة ينتبه ويزول عنه وَسَنُه في وقت لا يمكِنُه أن يتداركَ الفارطَ ولا يستدركَ الفائتَ. وهذا كلُّه تخويفٌ من الله للعباد، وترهيبٌ بذكر ما يكون على المكذِّبين في ذلك اليوم العظيم.
{22} Jambo hili ni katika mambo lazima mja ayakumbuke kila mara, lakini watu wengi wameghafilika,
na ndiyo maana akasema: "
(Aambiwe), 'Kwa hakika ulikuwa umeghafilika mbali na haya.'" Yaani, maneno haya ataambiwa Siku ya Kiyama huyu mwenye kupeana mgongo na kukadhibisha kwa njia ya kumkaripia, kumlaumu na kumkemea sana. "Basi" sasa "leo tumekuondolea pazia lako" lililokuwa limefunika moyo wako, kwa hivyo usingizi wako ukawa mwingi na ukaendelea kupeana mgongo. "Na kwa hivyo kuona kwako leo ni kukali mno." Atayaona yenye kumsumbua na kumuogopesha miongoni mwa adhabu na mateso. Au haya ni maneno ya Mwenyezi Mungu akimwambia mja wake. Kwani duniani alikuwa ameghafilika mbali na aliyoumbwa kwa ajili yake, lakini siku ya Kiyama atakuwa macho sana, na usingizi wake utamwondoka katika wakati ambapo hatoweza kurekebisha yale ambayo hakuyafanya vyema wala kufanya yaliyompita. Yote hayo ni kuhofisha anakowahofisha Mwenyezi Mungu waja wake, na ni kuwatishia kwa kutaja yale yatakayowapata wale wanaokadhibisha katika siku hiyo kuu.
{وَقَالَ قَرِينُهُ هَذَا مَا لَدَيَّ عَتِيدٌ (23) أَلْقِيَا فِي جَهَنَّمَ كُلَّ كَفَّارٍ عَنِيدٍ (24) مَنَّاعٍ لِلْخَيْرِ مُعْتَدٍ مُرِيبٍ (25) الَّذِي جَعَلَ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ فَأَلْقِيَاهُ فِي الْعَذَابِ الشَّدِيدِ (26) قَالَ قَرِينُهُ رَبَّنَا مَا أَطْغَيْتُهُ وَلَكِنْ كَانَ فِي ضَلَالٍ بَعِيدٍ (27) قَالَ لَا تَخْتَصِمُوا لَدَيَّ وَقَدْ قَدَّمْتُ إِلَيْكُمْ بِالْوَعِيدِ (28) مَا يُبَدَّلُ الْقَوْلُ لَدَيَّ وَمَا أَنَا بِظَلَّامٍ لِلْعَبِيدِ (29)}
23.
Na mwenzake atasema: 'Huyu niliye naye mimi keshatayarishwa. 24. Mtupeni katika Jahanamu kila kafiri mwenye inda. 25. Akatazaye mno heri, arukaye mipaka, mwenye kutia shaka. 26. Aliyeweka mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi mtupeni katika adhabu kali.' 27.
Mwenzake aseme: 'Ewe Mola wetu Mlezi! Sikumpoteza mimi, bali yeye mwenyewe alikuwa katika upotovu wa mbali.' 28.
(Mwenyezi Mungu) aseme: 'Msigombane mbele yangu. Tayari niliwaletea mbele onyo langu. 29. Mbele yangu haibadilishwi kauli, wala Mimi siwadhulumu waja wangu.
#
{23} يقول تعالى: {وقال قرينُهُ}؛ أي: قرين هذا المكذِّب المعرض من الملائكة، الذين وَكَلَهم الله على حفظه وحفظ أعماله، فيحضره يوم القيامة، ويحضر أعماله، ويقول: {هذا ما لديَّ عتيدٌ}؛ أي: قد أحضرتُ ما جعلتُ عليه من حفظه وحفظ عمله.
{23} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Na mwenzake atasema." Yaani, yule aliyekuwa karibu na mwenye kukadhibisha huyu miongoni mwa Malaika ambao Mwenyezi Mungu amewakabidhi kumlinda yeye na vitendo vyake, basi atamjia Siku ya Kiyama na ataleta vitendo vyake,
na kusema: "'Huyu niliye naye mimi keshatayarishwa." Yaani, nimeleta yule niliyekabidhiwa kumhifadhi na kuyahifadhi matendo yake.
#
{24} فيجازى بعمله، ويقال لمن استحقَّ النار: {ألْقِيا في جَهَنَّم كلَّ كفَّارٍ عنيدٍ}؛ أي: كثير الكفر والعناد لآيات الله، المكثر من المعاصي، المتجرِّئ على المحارم والمآثم.
{24} Kisha atalipwa kwa vitendo vyake,
na wataambiwa yule atakayestahiki Moto: "Mtupeni katika Jahanamu kila kafiri mkubwa mkaidi mno" wa Aya za Mwenyezi Mungu, mwenye kufanya maasia mengi, anayeyafanyia ujasiri maharamisho na madhambi.
#
{25} {منَّاع للخيرِ}؛ أي: يمنع الخير الذي قِبَله ، الذي أعظمه الإيمان بالله وملائكته وكتبه ورسله، منَّاع لنفع ماله وبدنه، {معتدٍ}: على عباد الله وعلى حدوده، أثيم، أي: كثير الإثم، {مريبٍ}؛ أي: شاكٍّ في وعد الله ووعيده؛ فلا إيمان ولا إحسان، ولكن وصفه الكفر والعدوان والشكُّ والريب والشحُّ واتِّخاذُ الآلهة من دون الرحمن.
{25} "Akatazaye mno heri" ambayo kubwa zaidi yake ni kumuamini Mwenyezi Mungu, Malaika wake, Vitabu vyake na Mitume wake, mwenye kuzuiliwa manufaa ya mali yake na mwili wake, "arukaye mipaka" dhidi ya waja wa Mwenyezi Mungu na mipaka yake mingine, mwenye madhambi mengi, "mwenye kutia shaka" katika ahadi na tishio la Mwenyezi Mungu. Basi akawa haamini wala hafanyi wema, lakini akasifika tu kwa ukafiri, kuvuka mipaka, kutilia shaka na kusitasita, ubakhili na kumfanyia Mwingi wa rehema miungu wengine.
#
{26} ولهذا قال: {الذي جَعَلَ مع اللهِ إلهاً آخر}؛ أي: عبد معه غيره ممَّن لا يملك لنفسه ضرًّا ولا نفعاً ولا موتاً ولا حياةً ولا نشوراً، {فألقياه}: أيُّها المَلَكان القرينان {في العذابِ الشديدِ}: الذي هو معظمها وأشدُّها وأشنعُها.
{26} Ndiyo maana akasema: "Aliyeweka mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu" miongoni mwa wale wasiojimilikia uwezo wa kudhuru, wala kunufaisha, wala kifo, wala uhai, wala kufufua. "Basi mtupeni" enyi Malaika wawili wa karibu naye "katika adhabu kali" na mbaya zaidi.
#
{27} {قال قرينُهُ}: الشيطان متبرِّئاً منه حاملاً عليه إثمه: {ربَّنا ما أطْغَيْتُه}: لأنِّي لم يكن لي عليه سلطانٌ ولا حجةٌ ولا برهانٌ، {ولكن كانَ في ضلالٍ بعيدٍ}: فهو الذي ضلَّ وبَعُدَ عن الحقِّ باختياره؛ كما قال في الآية الأخرى: {وقال الشيطانُ لَمَّا قُضِيَ الأمرُ إن الله وَعَدَكم وَعْدَ الحقِّ ووعدتُكم فأخْلَفْتُكم ... } الآية.
{27} "Mwenzake aseme" yaani Shetani huku alijitenga mbali naye,
akimbebesha dhambi zake: "Ewe Mola wetu Mlezi! Sikumpoteza mimi," kwa sababu sikuwa na mamlaka juu yake, wala sikuwa na ushahidi wala hoja.
"Bali yeye mwenyewe alikuwa katika upotovu wa mbali" kwa hivyo yeye mwenyewe akapotea na akajiweka mbali na haki kwa hiari yake; Kama alivyosema katika Aya nyingine: "Na Shetani atasema itakapokatwa hukumu: Hakika Mwenyezi Mungu aliwaahidi ahadi ya kweli. Nami naliwaahidi; lakini sikuwatimizia..." hadi mwisho wa Aya.
#
{28} قال الله تعالى مجيباً لاختصامهم: {لا تَخْتَصِموا لديَّ}؛ أي: لا فائدة في اختصامكم عندي، {و} الحال أني {قد قدَّمْتُ إليكم بالوعيدِ}؛ أي: جاءتكم رسلي بالآيات البيِّنات والحجج الواضحات والبراهين الساطعات، فقامت عليكم حجَّتي وانقطعت حجَّتُكم، وقدمتُم إليَّ بما أسلفتم من الأعمال التي وَجَبَ جزاؤها.
{28} Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema akijibu kubishana kwao huko: "Msigombane mbele yangu." Yaani, hakuna faida katika kugombana kwenu mbele yangu, "na" hali ni kwamba hakika Mimi "tayari niliwaletea mbele onyo langu." Yaani, Mitume wangu waliwajia na Aya zilizo wazi, hoja zilizo wazi, na ushahidi unaong'aa, basi ikathibitika hoja yangu juu yenu na ikakatika hoja yenu, na mkanijia na matendo mliyoyatanguliza ambayo inalazimu mlipwe juu yake.
#
{29} {ما يُبَدَّلُ القولُ لديَّ}؛ أي: لا يمكن أن يخلف ما قاله الله وأخبر به؛ لأنَّه لا أصدق من الله قيلاً، ولا أصدق حديثاً. {وما أنا بظلاَّمٍ للعبيد}: بل أجزيهم بما عملوا من خيرٍ وشرٍّ؛ فلا يزاد في سيئاتهم، ولا ينقص من حسناتهم.
{29} "Mbele yangu haibadilishwi kauli." Yaani, haiwezekani kuvunja yale ambayo Mwenyezi Mungu aliyasema na kujulisha. Kwa sababu hakuna mkweli zaidi kwa usemi kuliko Mwenyezi Mungu, wala msema kweli kuliko Mwenyezi Mungu. "Wala Mimi siwadhulumu waja wangu." Bali ninawalipa mema na mabaya waliyoyafanya. Kwa hivyo, haitazidishwa katika maovu yao, wala haitapunguzwa katika mema yao.
{يَوْمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ امْتَلَأْتِ وَتَقُولُ هَلْ مِنْ مَزِيدٍ (30) وَأُزْلِفَتِ الْجَنَّةُ لِلْمُتَّقِينَ غَيْرَ بَعِيدٍ (31) هَذَا مَا تُوعَدُونَ لِكُلِّ أَوَّابٍ حَفِيظٍ (32) مَنْ خَشِيَ الرَّحْمَنَ بِالْغَيْبِ وَجَاءَ بِقَلْبٍ مُنِيبٍ (33) ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ ذَلِكَ يَوْمُ الْخُلُودِ (34) لَهُمْ مَا يَشَاءُونَ فِيهَا وَلَدَيْنَا مَزِيدٌ (35)}
30.
Siku tutakapoiambia Jahanamu: 'Je,
umejaa?' Nayo itasema: 'Je, kuna ziada?' 31. Na Bustani ya mbinguni italetwa karibu mno kwa ajili ya wacha Mungu, haitakuwa mbali. 32. Haya ndiyo mnayoahidiwa kwa kila mwenye kurejea mno kwa Mwenyezi Mungu na akajilinda vyema. 33. Mwenye kumwogopa mno Mwingi wa rehema hali kuwa hamwoni, na akaja kwa moyo uliotubia. 34.
(Ataambiwa) ingieni humo kwa salama. Hiyo ndiyo siku ya kudumu daima dawamu. 35. Humo watapata wakitakacho, na kwetu yako ya ziada.
#
{30} يقول تعالى مخوِّفاً لعباده: {يومَ نقولُ لجهنَّم هلِ امتلأتِ}: وذلك من كثرةِ ما ألقيَ فيها، {وتقولُ هلْ مِن مَزيدٍ}؛ أي: لا تزال تطلبُ الزيادة من المجرمين العاصين؛ غضباً لربِّها، وغيظاً على الكافرين، وقد وعدها الله ملأها؛ كما قال تعالى: {لأملأنَّ جهنَّم من الجِنَّة والنَّاس أجمعينَ}: حتى يضعَ ربُّ العزَّة عليها قدمه الكريمة المنزَّهة عن التشبيه، فينزوي بعضُها على بعضٍ، وتقول: قط، قط ؛ قد اكتفيت وامتلأت.
{30} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema kwa kuwaogopesha waja wake: "Siku tutakapoiambia Jahanamu, Je, umejaa?" Hayo ni kwa sababu ya wingi wa wale waliotupwa humo,
"Nayo itasema: 'Je, kuna ziada?" Yaani, utaendelea kuitisha nyongeza kutoka kwa wahalifu wasiotii; kutokana na kuwa na hasira kwa ajili ya Mola wake Mlezi, na kuwa na hasira juu ya makafiri, na Mwenyezi Mungu aliiahidi kwamba itajaa.
Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Kweli kweli nitaijaza Jahanam kwa majini na watu pamoja" mpaka Mola Mtukufu atakapoweka mguu wake mtukufu juu yake, ambao hauwezi kufananishwa na chochote,
kisha baadhi yake itazudiana na itasema: "Imetosha, imetosha. Hakika nimetosheka na nimejaa."
#
{31} {وأزلِفَتِ الجنةُ}؛ أي: قرِّبت بحيث تشاهَد ويُنْظَرُ ما فيها من النعيم المقيم والحبرة والسرور، وإنما أزْلِفَتْ وقُرِّبَتْ لأجل المتَّقين لربِّهم، التاركين للشرك كبيره وصغيره ، الممتَثِلينَ لأوامر ربهم، المنقادين له.
{31} "Na Bustani ya mbinguni italetwa karibu mno" kiasi kwamba vitaweza kuonekana vilivyo ndani yake miongoni mwa neema ya milele, raha na furaha. Hiyo italetwa karibu kwa ajili ya wanaomcha Mola wao Mlezi peke yao, ambao waliacha ushirikina mkubwa na mdogo, ambao walitii na kutekeleza amri za Mola wao Mlezi.
#
{32} ويقال لهم على وجه التَّهنئة: {هذا ما توعدون لكلِّ أوَّابٍ حفيظٍ}؛ أي: هذه الجنة وما فيها مما تشتهيه الأنفس وتلذُّ الأعين هي التي وعدَ اللهُ كلَّ أوابٍ؛ أي: رجَّاع إلى الله في جميع الأوقات؛ بذكرِه وحبِّه والاستعانةِ به ودعائِه وخوفِه ورجائِه. {حفيظ}؛ أي: محافظ على ما أمر الله به؛ بامتثاله على وجه الإخلاص والإكمال له على أتمِّ الوجوه، حفيظ لحدوده.
{32} Na wataambiwa kwa njia ya kuwapongeza: "Haya ndiyo mnayoahidiwa kwa kila mwenye kurejea mno kwa Mwenyezi Mungu na akajilinda vyema." Yaani, Bustani hii ya mbinguni na vyote vilivyomo ndani yake miongoni mwa vitu vinavyotamaniwa na nafsi, na vinavyofurahisha macho, navyo ndivyo ambavyo Mwenyezi Mungu alimuahidi kila mwenye kurejea mno kwa Mwenyezi Mungu katika kila wakati, kwa kumtaja, kumpenda, kutafuta msaada wake, kumuomba dua, kumhofu na kumtarajia. "Na akajilinda vyema" kwa kulinda yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu, kwa kuyatekeleza kwa njia ya kumkusudia Yeye tu, na kuyakamilisha kwa njia kamili zaidi, na akalinda mipaka yake.
#
{33} {مَنْ خَشِيَ الرحمنَ}؛ أي: خافه على وجه المعرفة بربِّه والرجاء لرحمته، ولازم على خشية الله في حال غيبه؛ أي: مغيبه عن أعين الناس. وهذه الخشية الحقيقيَّة، وأمَّا خشيتُه في حال نظر الناس وحضورهم؛ فقد يكون رياءً وسمعةً؛ فلا يدلُّ على الخشية، وإنما الخشية النافعة خشيته في الغيب والشهادة، [ويحتمل أنّ المراد بخشية اللَّه بالغيب، كالمراد بالإيمان بالغيب. وأنّ هذا مقابل للشهادة حيث يكون الإيمان والخشية ضرورياً لا اختيارياً حيث يعاين العذاب، وتأتي آيات اللَّه وهذا هو الظاهر.] {وجاء بقلبٍ منيبٍ}؛ أي: وصفه الإنابة إلى مولاه، وانجذاب دواعيه إلى مراضيه.
{33} "Mwenye kumwogopa mno Mwingi wa rehema" kwa kumjua Mola wake Mlezi na kutaraji rehema yake, na akaendelea kumcha Mwenyezi Mungu hata anapokuwa peke yake mbali na watu. Hii ndiyo hofu ya kweli. Ama kumhofu kwake Mwenyezi Mungu watu wanapomwona au mbele yao, hilo linaweza kuwa kujionyesha na kutaka sifa, na wala halionyeshi hofu. Lakini hofu yenye manufaa ni kumhofu mbali na watu na hata anapokuwa kwa watu. Na inawezekana kwamba kinachomaanishwa na kumhofu Mwenyezi Mungu katika ghaibu ni sawa na kusema kuamini katika ghaibu, na kwamba hili ni kinyume cha kufanya hivyo katika hali ya dhahiri ambayo hapo kuamini na kuhofu vinakuwa ni kitu cha lazima si vya hiari wakati atakapokuwa ameshaona adhabu na zikaja ishara za Mwenyezi Mungu, na maana hii ndiyo ya dhahiri] "Na akaja kwa moyo uliotubia mno" na ukawa umeelekea kwenye mambo anayoridhia Mwenyezi Mungu.
#
{34} ويقال لهؤلاء الأتقياء الأبرار: {ادْخُلوها بِسلامٍ}؛ أي: دخولاً مقروناً بالسلامة من الآفات والشرور، مأموناً فيه جميع مكاره الأمور؛ فلا انقطاع لنعيمهم ولا كدر ولا تنغيص. {ذلك يومُ الخُلودِ}: الذي لا زوال له ولا موت ولا شيء من المكدِّرات.
{34} Na wataambiwa hawa wacha Mungu na wema: "Ingieni humo kwa salama" kutokana na balaa na maovu, ambamo hakuna mambo mabaya yoyote. Hakuna kukatiziwa furaha yao, wala machukizo wala huzuni. "Hiyo ndiyo siku ya kudumu daima dawamu" isiyokuwa na mwisho, wala mauti, wala machukizo yoyote.
#
{35} {لهم ما يشاؤون فيها}؛ أي: كلُّ ما تعلَّقت به مشيئتهم؛ فهو حاصلٌ فيها، {ولدَينا}: فوق ذلك {مَزيدٌ}؛ أي: ثوابٌ يمدُّهم به الرحمن الرحيم، ممَّا لا عين رأت ولا أذن سمعت ولا خطر على قلب بشرٍ، وأعظم ذلك وأجلُّه وأفضله النظر إلى وجهه الكريم، والتمتُّع بسماع كلامه، والتنعُّم بقربه، فنسأله من فضله.
{35} "Humo watapata wakitakacho" miongoni mwa kila kitu ambacho matamanio yao yanaambatana nacho. "Na kwetu" juu ya hayo kuna "ziada" ambayo Mwingi wa Rehema, Mwingi wa kurehemu atawapa, miongoni mwa yale ambayo jicho halijapata kuyaona, wala sikio haliljapata kuyasikia, na hakuna moyo wa mwanadamu uliowahi kuyafikiria, na kubwa zaidi ya hayo na utukufu zaidi na bora zaidi ni kuutazama uso wake mtukufu, kufurahia kusikia maneno yake, na kupata raha ya kuwa karibu naye. Basi tunamuomba katika fadhila zake.
{وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُمْ مِنْ قَرْنٍ هُمْ أَشَدُّ مِنْهُمْ بَطْشًا فَنَقَّبُوا فِي الْبِلَادِ هَلْ مِنْ مَحِيصٍ (36) إِنَّ فِي ذَلِكَ لَذِكْرَى لِمَنْ كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ (37)}
36. Na kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao, waliokuwa na nguvu zaidi kuliko hawa! Nao walitanga tanga katika nchi nyingi. Je, walipata pa kukimbilia? 37. Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.
#
{36} يقول تعالى مخوفاً للمشركين المكذِّبين للرسول: {وكمْ أهْلَكْنا قبلَهم من قرنٍ}؛ أي: أمماً كثيرة {هم أشدُّ منهم بَطْشاً}؛ أي: قوةً وآثاراً في الأرض، ولهذا قال: {فَنَقَّبوا في البلاد}؛ أي: بنوا الحصون المنيعة والمنازل الرفيعة، وغرسوا الأشجار، وأجروا الأنهار، وزرعوا، وعمَّروا، ودمَّروا، فلما كذَّبوا رسل الله وجحدوا آياته ؛ أخذهم الله بالعقاب الأليم والعذاب الشديد. {هل من مَحيصٍ}؛ أي: لا مفرَّ لهم من عذاب الله حين نزل بهم ولا منقذ، فلم تغن عنهم قوَّتُهم ولا أموالهم ولا أولادهم.
{36} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema kwa kuwahofisha washirikina wanaomkadhibisha Mtume: "Na kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao?" Yaani,
mataifa mengi sana "waliokuwa na nguvu zaidi kuliko hawa!" Ndiyo maana akasema: "Nao walitanga tanga katika nchi nyingi." Yaani, walijenga ngome za nguvu sana, na majumba yaliyoinuka juu, wakapanda miti, wakapitisha mito, wakalima, wakakaa imara na wakaharibu walivyoharibu. Na pindi walipowakadhibisha Mitume wa Mwenyezi Mungu na kuzikataa ishara za Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu akawachukua kwa adhabu chungu na kali sana. "Je, walipata pa kukimbilia" kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu ilipowafikia? La hasha, hata hawakupata wa kuwaokoa, na nguvu zao, na mali zao, na watoto wao havikuwasaidia kitu.
#
{37} {إنَّ في ذلك لَذِكْرى لِمَن كان له قلبٌ}؛ أي: قلبٌ عظيمٌ حيٌّ ذكيٌّ زكيٌّ؛ فهذا إذا ورد عليه شيء من آيات الله؛ تذكَّر بها وانتفع فارتفع، وكذلك من ألقى سمعه إلى آيات الله واستمعها استماعاً يسترشد به وقلبُه {شهيدٌ}؛ أي: حاضرٌ؛ فهذا أيضاً له ذكرى وموعظةٌ وشفاءٌ وهدى، وأمَّا المعرض الذي لم يصغِ سمعه إلى الآيات؛ فهذا لا تفيده شيئاً؛ لأنه لا قبول عنده، ولا تقتضي حكمةُ الله هداية من هذا نعته.
{37} "Hakika katika haya upo ukumbusho kwa mwenye moyo." Yaani, moyo mkuu, ulio hai, wenye werevu na ulio safi. Huo, unapojiwa na kitu katika Ishara za Mwenyezi Mungu, unakumbuka, na unanufaika na kuinuka juu. Na kadhalika yule ambaye anasikiliza Aya za Mwenyezi Mungu kwa njia ya kutafuta mwongozo ndani yake ilhali moyo wake "unashuhudia," huyu pia hayo kwake ni ukumbusho, na mawaidha, ponya, na uwongofu. Na ama mwenye kupeana mgongo ambaye hakuzipa Aya sikio lake, basi huyu hizo hazimnufaishi kitu, kwa sababu hawezi kuzikubali, na wala hekima ya Mwenyezi Mungu haihitaji kumwongoza yule ambaye sifa yake ni hii.
{وَلَقَدْ خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَمَا مَسَّنَا مِنْ لُغُوبٍ (38) فَاصْبِرْ عَلَى مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ الْغُرُوبِ (39) وَمِنَ اللَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَأَدْبَارَ السُّجُودِ (40)}.
38. Na bila ya shaka Sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita; na wala hayakutugusa machofu yoyote. 39. Basi vumilia kwa hayo wasemayo, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa. 40. Na katika usiku pia mtakase, na baada ya kusujudu.
#
{38} وهذا إخبارٌ منه تعالى عن قدرته العظيمة ومشيئته النافذة، التي أوجد بها أعظم المخلوقات؛ {السمواتِ والأرضَ وما بينَهما في ستَّة أيامٍ}: أولها يوم الأحد، وآخرها يوم الجمعة؛ من غير تعبٍ ولا نصبٍ ولا لغوبٍ ولا إعياءٍ؛ فالذي أوجدها على كبرها وعظمها قادرٌ على إحياء الموتى من باب أولى وأحرى.
{38} Huku ni kujulisha ambako Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu uwezo wake mkuu na utashi wake yenye kutekelezeka, ambao kwa huo aliumba kiumbe kikuu zaidi ambacho ni "Mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita." Ya kwanza ni Jumapili na ya mwisho ni Ijumaa. Bila taabu wala uchovu wala kunyong'onyea wala kuemewa. Kwa hivyo, aliyeziumba, licha ya ukubwa na ukuu wake, ana uwezo kwa njia ifaayo zaidi kuwahuisha wafu.
#
{39 - 40} {فاصبرْ على ما يقولونَ}: من الذمِّ لك والتكذيب بما جئتَ به، واشتغلْ عنهم والْه بطاعة ربِّك وتسبيحه أول النهار وآخره وفي أوقات الليل وأدبار الصلوات؛ فإن ذِكْرَ الله تعالى مسلٍّ للنفس مؤنسٌ لها مهوِّنٌ للصبر.
{39 - 40} "Basi vumilia kwa hayo wasemayo" ya kukukashifu na kukukadhibisha katika hayo uliyokuja nayo, na ujishughulishe na mengine mbali nao na abudu kwa kumtii Mola wako Mlezi na kumsifu mwanzoni wa mchana na mwisho wake, na nyakati za usiku na baada ya Sala zote. Kwani kumkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu kunaburudisha nafsi, huituliza, na humrahisishia mtu suala la subira.
{وَاسْتَمِعْ يَوْمَ يُنَادِ الْمُنَادِ مِنْ مَكَانٍ قَرِيبٍ (41) يَوْمَ يَسْمَعُونَ الصَّيْحَةَ بِالْحَقِّ ذَلِكَ يَوْمُ الْخُرُوجِ (42) إِنَّا نَحْنُ نُحْيِي وَنُمِيتُ وَإِلَيْنَا الْمَصِيرُ (43) يَوْمَ تَشَقَّقُ الْأَرْضُ عَنْهُمْ سِرَاعًا ذَلِكَ حَشْرٌ عَلَيْنَا يَسِيرٌ (44) نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَقُولُونَ وَمَا أَنْتَ عَلَيْهِمْ بِجَبَّارٍ فَذَكِّرْ بِالْقُرْآنِ مَنْ يَخَافُ وَعِيدِ (45)}
41. Na sikiliza siku atakaponadi mwenye kunadi kutoka mahali karibu. 42. Siku watakaposikia ukelele wa haki. Hiyo ndiyo siku ya kufufuka. 43. Hakika Sisi tunahuisha na tunafisha, na kwetu Sisi ndio marejeo. 44. Siku itapowapasukia ardhi mbio mbio! Mkusanyo huo kwetu ni mwepesi. 45. Sisi tunajua kabisa wayasemayo. Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari. Basi mkumbushe kwa Qur-ani anayeliogopa onyo.
#
{41} أي: {واستمعْ}: بقلبك نداء المنادي، وهو إسرافيل عليه السلام، حين ينفخُ في الصور {من مكانٍ قريبٍ}: من الأرض.
{41} Yaani, "na sikiliza" kwa moyo wako mwenye kunadi, ambaye ni Israil, amani iwe juu yake, atakapopuliza katika baragumu "kutoka mahali karibu."
#
{42} {يوم يسمعونَ الصَّيحَةَ}؛ أي: كلُّ الخلائق يسمعون تلك {الصيحة}: المزعجة المهولة {بالحقِّ}: الذي لا شكَّ فيه ولا امتراء. {ذلك يومُ الخروج}: من القبور، الذي انفرد به القادر على كلِّ شيء.
{42} "Siku watakaposikia" viumbe vyote "ukelele" wa kusumbua na wa kuwatisha, "kwa haki" ambayo haina shaka wala utata. "Hiyo ndiyo siku ya kufufuka" kutoka makaburini, suala ambalo ni lake yeye Mwenye uwezo tu.
#
{43 - 44} ولهذا قال: {إنَّا نحن نحيي ونميتُ وإلينا المصيرُ. يومَ تَشَقَّقُ الأرضُ عنهم}؛ أي: عن الخلائق {سراعاً}؛ أي: يسرعون لإجابة الدَّاعي لهم إلى موقفِ القيامة. {ذلك حشرٌ علينا يسيرٌ}؛ أي: سهل على الله ، لا تعبَ فيه ولا كلفةَ.
{43 - 44} Ndiyo maana akasema, "Hakika Sisi tunahuisha na tunafisha, na kwetu Sisi ndiyo marejeo. Siku itapowapasukia ardhi mbio mbio" wakienda kumuitikia yule anayewaita kwenda mahali pa kisimamo cha Kiyama. "Mkusanyo huo kwetu ni mwepesi" na hauna taabu ndani yake wala gharama.
#
{45} {نحنُ أعلمُ بما يقولون}: لك مما يحزنك من الأذى، وإذا كنَّا أعلم بذلك؛ فقد علمت كيف اعتناؤنا بك وتيسيرنا لأمورك ونصرنا لك على أعدائك؛ فليفرح قلبك، ولتطمئنَّ نفسُك، ولتعلم أنَّنا أرحم بك وأرأف من نفسك، فلم يبق لك إلا انتظار وعد الله والتأسِّي بأولي العزم من رسل الله، {وما أنت عليهم بجبَّارٍ}؛ أي: مسلَّط عليهم، {إنَّما أنت منذرٌ ولكلِّ قومٍ هادٍ}، ولهذا قال: {فذكِّر بالقرآن من يخاف وعيد}، والتذكير هو تذكير ما تقرَّر في العقول والفطر من محبَّة الخير وإيثاره وفعله ومن بغض الشرِّ ومجانبته، وإنما يتذكَّر بالتذكير من يخاف وعيد الله، وأما من لم يخفِ الوعيد ولم يؤمنْ به؛ فهذا فائدة تذكيره إقامة الحجَّة عليه لئلا يقول: ما جاءنا من بشيرٍ ولا نذيرٍ.
{45} "Sisi tunajua kabisa wayasemayo" wakikuambia miongoni mwa mambo ya kukuhuzunisha ya kukuudhi. Na ikiwa tunajua kabisa hayo, basi hakika umeshajua jinsi tunavyokutunza, na kukurahisishia mambo yako, na kukupa ushindi dhidi ya adui zako. Hebu moyo wako ufurahi, na nafsi yako itulie, na jua kwamba tunakurehemu zaidi na tunakufanyia upole sana hata kuliko unavyojifanyia mwenyewe. Kwa hivyo, hakuna unachobakisha isipokuwa kusubiri ahadi ya Mwenyezi Mungu na kufuata mfano wa wale wenye stahamala kubwa miongoni mwa Mitume wa Mwenyezi Mungu. "Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari.
" Na pia alisema: "Hakika wewe ni Mwonyaji, na kila kaumu ina wa kuwaongoza.
" Na ndiyo maana akasema: "Basi mkumbushe kwa Qur-ani anayeiogopa ahadi ya adhabu." Na kukumbusha huko kunahusiana na yale yaliyothibiti katika akili na maumbile asili ya kupenda heri, kuipendelea na kuifanya, na kuuchukia uovu na kujiepusha nao. Lakini anakumbuka tu kwa ukumbusho yule anayeogopa onyo. Ama yule ambaye haogopi ahadi ya adhabu ya Mwenyezi Mungu wala hata hakuiamini,
basi huyu faida ya kumkumbusha ni kumsimamishia tu hoja ili asije sema: 'Hatukujiwa na mbashiri wala mwonyaji.'
Mwisho wa tafsiri ya Surat Qaf. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, mwanzoni, mwishoni, nje kwa hadharani na kwa siri.
* * *