:
Mshairi alisema: Ewe mwenye kuangalia ndani yake, omba rehema kwa Mwenyezi Mungu...juu ya mtunzi wake na umuombee msamaha mwandishi wake Na ujiombee heri unayojitakia nafsi yako... na baada ya hayo, msamaha kwa mwenye kitabu hiki Juzuu ya nane ya Taysir Al-Karim Ar-Rahman fi Tafsir kalaam Al-Malik Al-Mannan Cha mwandishi wake, masikini, Abdur-Rahman bin Nasir bin Abdullah, anayejulikana kwa jina la Ibn Saadi, Mwenyezi Mungu amsamehe yeye na Waislamu wote.
Tafsiri ya Surat Hujurat
Tafsiri ya Surat Hujurat
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
: 1 - 3 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيِ اللَّهِ وَرَسُولِهِ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ (1) يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَرْفَعُوا أَصْوَاتَكُمْ فَوْقَ صَوْتِ النَّبِيِّ وَلَا تَجْهَرُوا لَهُ بِالْقَوْلِ كَجَهْرِ بَعْضِكُمْ لِبَعْضٍ أَنْ تَحْبَطَ أَعْمَالُكُمْ وَأَنْتُمْ لَا تَشْعُرُونَ (2) إِنَّ الَّذِينَ يَغُضُّونَ أَصْوَاتَهُمْ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ أُولَئِكَ الَّذِينَ امْتَحَنَ اللَّهُ قُلُوبَهُمْ لِلتَّقْوَى لَهُمْ مَغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌ (3)}
1. Enyi mlioamini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia mno, Mwenye kujua zaidi. 2. Enyi mlioamini! Msinyanyue sauti zenu kuliko sauti ya Nabii, wala msiseme naye kwa kelele kama mnavyosemezana nyinyi kwa nyinyi, visije vitendo vyenu vikaharibika, na hali hamtambui. 3. Kwa hakika wale wanaoteremsha sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, hao ndio Mwenyezi Mungu amezisafisha nyoyo zao kwa ucha Mungu. Hao watakuwa na maghfira na ujira mkubwa.
Hili linajumuisha kuwa na adabu mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake - na kumpa taadhima, kumtukuza. Basi Mwenyezi Mungu akawaamrisha waja wake Waumini kufanya yale ambayo kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake kunahitaji kama vile kutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kuepuka makatazo yake, na kwamba watembee nyuma ya maamrisho ya Mwenyezi Mungu, na kufuata Sunna za Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake. Katika mambo yao yote, na kwamba wasitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kwa hivyo, wasiseme chochote mpaka aseme, wala wasiamrishe mpaka aamrishe, kwani huu ndio uhakika wa kuwa na adabu ya wajibu mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na ndicho kichwa cha furaha na mafanikio ya mja, na kwa kukosa hilo anakosa furaha ya milele na neema ya milele. Katika hilo liko katazo kali juu ya kutanguliza maneno ya asiyekuwa Mtume – rehema na amani ziwe juu yake – mbele ya maneno yake. Kwa hivyo, kila inapobainika Sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake, inakuwa lazima kuifuata na kuitanguliza mbele ya mambo mengineyo, hata yakiwa ni ya nani.
#
{1} ثم أمر الله بتقواه عموماً، وهي كما قال طَلْق بن حبيب: أن تعملَ بطاعة الله على نور من الله ترجو ثواب الله، وأن تترك معصية الله على نور من الله تخشى عقاب الله. وقوله: {إنَّ الله سميعٌ}؛ أي: لجميع الأصوات، في جميع الأوقات، في خفيِّ المواضع والجهات، {عليمٌ}: بالظواهر والبواطن، والسوابق واللواحق، والواجبات والمستحيلات والجائزات. وفي ذكر الاسمين الكريمين بعد النهيِ عن التقدّم بين يدي الله ورسوله والأمر بتقواه حثٌّ على امتثال تلك الأوامر الحسنة والآداب المستحسنة وترهيبٌ عن ضدِّه.
{1} Kisha Mwenyezi Mungu akaamrisha ucha Mungu kwa ujumla, ambao ni kama Talq bin Habib alivyosema: 'Kumtii Mwenyezi Mungu kwa nuru itokayo kwa Mwenyezi Mungu, kwa kutaraji malipo ya Mwenyezi Mungu, na kuacha kumuasi Mwenyezi Mungu kwa nuru itokayo kwa Mwenyezi Mungu, kwa kuogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu.' Na kauli yake: ''Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia mno.'' Yaani, sauti zote, katika kila wakati, katika mahali pa siri zaidi na pande zote. ''Mwenye kujua zaidi'' ya dhahiri na ya siri, yaliyotangulia na yajayo, ya wajibu na yasiyowezekana na yanayowezekana. Na katika kutaja Majina haya mawili Matukufu baada ya kukataza kutanguliza mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kuamrisha kumcha Mungu, kuna kutia kuhimiza kufuata maamrisho hayo mazuri na adabu njema, na kutishia dhidi ya kinyume chake.
#
{2} ثم قال تعالى: {يا أيُّها الذين آمنوا لا ترفعوا أصواتَكُم فوقَ صوتِ النبيِّ ولا تَجْهَروا له بالقولِ}: وهذا أدب مع الرسول - صلى الله عليه وسلم - في خطابه؛ أي: لا يرفع المخاطِبُ له صوتَهُ معه فوق صوتِهِ، ولا يجهرْ له بالقول، بل يغضُّ الصوتَ ويخاطبُه بأدبٍ ولينٍ وتعظيم وتكريم وإجلال وإعظام، ولا يكون الرسول كأحدهم، بل يميِّزونه في خطابهم كما تميَّز عن غيرِه في وجوبِ حقِّه على الأمَّة، ووجوب الإيمان به، والحبِّ الذي لا يتمُّ الإيمانُ إلا به؛ فإن في عدم القيام بذلك محذوراً وخشية أن يحبط عملُ العبد وهو لا يشعر؛ كما أن الأدب معه من أسباب حصول الثواب وقبول الأعمال.
{2} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: ''Enyi mlioamini! Msinyanyue sauti zenu kuliko sauti ya Nabii, wala msiseme naye kwa kelele.'' Hii ni kufanya adabu nzuri mbele ya Mtume – rehema na amani ziwe juu yake - katika kuzungumza naye. Bali ateremshe sauti yake na aseme naye kwa adabu nzuri, upole, taadhima, heshima na kumtukuza, wala asimfanye Mtume kuwa kama mmoja wao. Bali wanapaswa kumfanya tofauti katika kusema naye kama alivyo tofauti na wengine katika uwajibu wa haki yake juu ya umma huu, na uwajibu wa kumwamini na kumpenda ambako imani haitimii isipokuwa kwa huo. Kwani katika kutofanya hivi, kunatahadhariwa jambo baya na kuhofiwa kwamba matendo ya mja yanaweza kuharibika hali ya kuwa hatambui. Pia, kuwa na adabu nzuri mbele yake ni katika sababu za kupata malipo mazuri na kukubaliwa matendo.
#
{3} ثم مدح من غضَّ صوته عند رسول الله - صلى الله عليه وسلم - بأنَّ الله امتحن قلوبَهم للتقوى؛ أي: ابتلاها واختبرها، فظهرت نتيجةُ ذلك بأن صَلَحَت قلوبهم للتقوى. ثم وَعَدَهم المغفرةَ لذنوبهم، المتضمِّنة لزوال الشرِّ والمكروه، وحصول الأجر العظيم، الذي لا يعلم وصفه إلاَّ الله تعالى، وفيه حصولُ كل محبوب. وفي هذا دليلٌ على أن الله يمتحنُ القلوبَ بالأمر والنهي والمحن؛ فمَن لازمَ أمر الله واتَّبع رضاه وسارعَ إلى ذلك وقدَّمه على هواه؛ تمحَّض وتمحَّص للتقوى، وصار قلبُه صالحاً لها، ومَن لم يكن كذلك؛ علم أنه لا يصلح للتقوى.
{3} Kisha akawasifu wale walioteremsha chini sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake – kwamba Mwenyezi Mungu amezisafisha nyoyo zao kwa ucha Mungu. Yaani, alizijaribu na kuzipa mtihani, na matokeo yake yakawa kwamba nyoyo zao zilitengenea kwa ajili ya ucha Mungu. Kisha akawaahidi msamaha wa dhambi zao, ambao unajumuisha kuondoka kwa uovu na kinachochukiwa, na kupatikana kwa malipo makubwa ambayo hakuna anayejua maelezo yake isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu tu, na pia ndani yake kuna kupata kila kinachopendwa. Katika haya kuna ushahidi kwamba Mwenyezi Mungu huijaribu mioyo kwa amri, makatazo na balaa. Basi mwenye kushikamana na amri ya Mwenyezi Mungu na akafuata radhi yake na akayakimbilia hayo na kuyatanguliza mbele ya matamanio yake, anasafika mno kwa ajili ya uchamungu, na moyo wake ukawa mahali pazuri kwa ajili yake. Na asiyekuwa hivyo, anajua kwamba haufailii ucha Mungu.
: 4 - 5 #
{إِنَّ الَّذِينَ يُنَادُونَكَ مِنْ وَرَاءِ الْحُجُرَاتِ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ (4) وَلَوْ أَنَّهُمْ صَبَرُوا حَتَّى تَخْرُجَ إِلَيْهِمْ لَكَانَ خَيْرًا لَهُمْ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ (5)}
4. Hakika hao wanaokuita nawe uko nyuma ya vyumba, wengi wao hawatumii akili. 5. Na lau wao wangelingojea mpaka uwatokee, ingelikuwa heri kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira, Mwingi wa kurehemu.
#
{4} نزلت هذه الآيات الكريمة في ناس من الأعراب، الذين وصفهم الله بالجفاء، وأنهم أجدرُ أن لا يعلموا حدودَ ما أنزل الله على رسوله؛ قدموا وافدين على رسول الله - صلى الله عليه وسلم -، فوجدوه في بيته وحجرات نسائِهِ، فلم يصبروا ويتأدَّبوا حتى يخرج، بل نادوه: يا محمد، يا محمد ؛ أي: اخرج إلينا. فذمَّهم الله بعدم العقل؛ حيث لم يعقلوا عن الله الأدب مع رسوله واحترامه؛ كما أن من العقل استعمال الأدب؛ فأدب العبد عنوان عقله، وأنَّ الله مريدٌ به الخير.
{4} Aya hizi tukufu ziliteremshwa kuhusu watu fulani kutoka kwa Mabedui ambao Mwenyezi Mungu amewaelezea kwamba wana ugumu, na kwamba wao wana uwezekano mkubwa zaidi wa kutojua mipaka ya yale aliyomteremshia Mwenyezi Mungu Mtume wake. Watu hao walimjia Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake – na wakamkuta ndani ya nyumba yake miongoni mwa vyumba vya wanawake wake, lakini hawakuwa na subira na adabu nzuri mpaka atoke nje. Bali walimwita: 'Ewe Muhammad, ewe Muhammad.' Yaani, toka utujie nje. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawakashifu kwamba hawana akili, ambapo hawakufahamu kutoka kwa Mwenyezi Mungu adabu ya kufanya mbele ya Mtume wake na heshima yake. Kama vile kuwa na akili, ni kuwa na adabu nzuri, basi adabu nzuri ya mja, ni ishara ya akili yake, na kwamba Mwenyezi Mungu anamtakia mema.
#
{5} ولهذا قال: {ولو أنَّهم صَبَروا حتى تخرُجَ إليهم لكان خيراً لهم والله غفورٌ رحيمٌ}؛ أي: غفورٌ لما صدر عن عباده من الذُّنوب والإخلال بالآداب، رحيمٌ بهم حيث لم يعاجلْهم بذنوبهم بالعقوبات والمَثُلات.
{5} Ndiyo maana akasema: ''Na lau wao wangelingojea mpaka uwatokee, ingelikuwa heri kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira, Mwingi wa kurehemu." Yaani: Kusamehe mno madhambi na uvunjaji wa maadili yaliyotendwa na waja wake, Mwingi wa kuwarehemu, kwani hakuwaharakishia dhambi zao kwa mateso na adhabu za mifano.
: 6 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَنْ تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَى مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ (6)}.
6. Enyi mlioamini! Akikujieni mpotovu na habari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kutojua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyoyatenda.
#
{6} وهذا أيضاً من الآداب التي على أولي الألباب التأدُّبُ بها واستعمالها، وهو أنه إذا أخبرهم فاسقٌ بنبأ؛ أي: خبرٍ: أن يتثبَّتوا في خبره، ولا يأخذوه مجرداً؛ فإن في ذلك خطراً كبيراً ووقوعاً في الإثم؛ فإنَّ خبره إذا جُعل بمنزلة خبر الصادق العدل؛ حكم بموجب ذلك ومقتضاه، فحصل من تلف النفوس والأموال بغير حقٍّ بسبب ذلك الخبر ما يكون سبباً للندامة، بل الواجبُ عند خبر الفاسق التثبُّت والتبيُّن؛ فإن دلَّت الدلائل والقرائن على صدقه؛ عُمِلَ به وصُدِّق، وإن دلت على كذبه؛ كذِّب ولم يعمل به؛ ففيه دليل على أن خبر الصادق مقبول، وخبر الكاذب مردود، وخبر الفاسق متوقَّف فيه ، ولهذا كان السلف يقبلون روايات كثير من الخوارج المعروفين بالصدق، ولو كانوا فساقاً.
{6} Hii pia ni moja ya adabu ambazo watu wenye ufahamu mkubwa wanapaswa kuzingatia na kuzitumia, ambayo ni kwamba ikiwa mpotofu atawaambia habari kwamba wathibitishe habari zake, wala wasizichukulie kwa udhahiri wake. Kwani kuna hatari kubwa katika kufanya hivyo na kuanguka katika dhambi. Kwa maana, ikiwa habari zake zimepewa hadhi ya habari za mkweli na muadilifu, basi itahukumiwa kwa mujibu wake na inavyohitaji, basi watu na mali vikaharibika bila ya haki kwa sababu ya habari hiyo, ambayo ni sababu ya majuto. Bali la wajibu inapokuja habari ya mpotofu ni kuithibitisha na kubainisha uhakika wake. Ikiwa ushahidi na viashiria vitaonyesha ukweli wake, basi itafanyiwa kazi na kuaminiwa. Lakini kama vitaonyesha uwongo wake, basi haitakadhibishwa na haitafanyiwa kazi. Katika hili kuna ushahidi kwamba habari ya mtu mkweli inakubaliwa, nayo habari ya mwongo inakataliwa, na habari ya mtu mpotofu haihukumiwi papo hapo, bali inangojewa kwanza. Ndiyo maana watangulizi wema walikuwa wakikubali riwaya za wengi katika Makhawarij ambao wanajulikana kwamba ni wakweli, hata kama ni watu wanaovuka mipaka.
: 7 - 8 #
{وَاعْلَمُوا أَنَّ فِيكُمْ رَسُولَ اللَّهِ لَوْ يُطِيعُكُمْ فِي كَثِيرٍ مِنَ الْأَمْرِ لَعَنِتُّمْ وَلَكِنَّ اللَّهَ حَبَّبَ إِلَيْكُمُ الْإِيمَانَ وَزَيَّنَهُ فِي قُلُوبِكُمْ وَكَرَّهَ إِلَيْكُمُ الْكُفْرَ وَالْفُسُوقَ وَالْعِصْيَانَ أُولَئِكَ هُمُ الرَّاشِدُونَ (7) فَضْلًا مِنَ اللَّهِ وَنِعْمَةً وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ (8)}
7. Na jueni kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko nanyi. Lau angeliwatii katika mambo mengi, bila ya shaka mngelitaabika. Lakini Mwenyezi Mungu amewapendezea Imani, na akaipamba katika nyoyo zenu, na amewafanya muuchukie ukafiri, na upotovu, na uasi. Hao ndio walioongoka. 8. Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na neema zake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua mno, Mwenye hekima.
#
{7} أي: وليكن لديكم معلومًا أنَّ {رسول الله} - صلى الله عليه وسلم - بين أظهُرِكم، وهو الرسولُ الكريم البارُّ الراشدُ، الذي يريد بكم الخير، وينصح لكم، وتريدون لأنفسكم من الشرِّ والمضرَّة ما لا يوافقكم الرسولُ عليه، و {لو يطيعكم في كثيرٍ من الأمر} لشقَّ عليكم وأعنتكم، ولكن الرسول يرشدكُم، والله تعالى يحبِّب إليكم {الإيمان} ويزيِّنه {في قلوبكم} بما أودع في قلوبكم من محبة الحقِّ وإيثاره، وبما نصب على الحقِّ من الشواهد والأدلَّة الدالَّة على صحَّته وقبول القلوب والفِطَر له، وبما يفعله تعالى بكم من توفيقه للإنابة إليه، ويكرِّه {إليكم الكفر والفسوق}؛ أي: الذنوبَ الكبار. {والعصيان}؛ أي: الذنوبَ الصغار؛ بما أودع في قلوبكم من كراهة الشرِّ وعدم إرادة فعله، وبما نَصَبَه من الأدلَّة والشواهد على فسادِه ومضرَّته وعدم قبول الفطر له، وبما يجعل الله في القلوب من الكراهة له. {أولئك}؛ أي: الذين زيَّن الله الإيمان في قلوبهم وحبَّبه إليهم، وكرَّه إليهم الكفر والفسوق والعصيان {هم الراشدونَ}؛ أي: الذين صلحت علومُهم وأعمالُهم، واستقاموا على الدين القويم والصراط المستقيم، وضدُّهم الغاوون الذين حُبِّب إليهم الكفر والفسوق والعصيان، وكُرِّه إليهم الإيمان، والذنب ذنبُهم؛ فإنهم لما فسقوا؛ طبعَ اللهُ على قلوبهم، ولما زاغوا؛ أزاغ اللهُ قلوبهم، ولما لم يؤمنوا بالحق لمَّا جاءهم أولَ مرة؛ قلب الله أفئدتهم.
{7} Yaani: Ifahamike kwenu kwamba ''Mtume wa Mwenyezi Mungu'' - rehema na Amani zimshukie - yumo miongoni mwenu, naye ni Mtume mtukufu, mwema na mwongofu, ambaye anawatakia heri na anawanasihi mazuri, nanyi mnajitakia maovu na madhara asiyowakubalieni Mtume. ''Lau angeliwatii katika mambo mengi," basi ingeliwawiya vigumu na mngetaabika, lakini Mtume anawaelekezeni sawasawa, naye Mwenyezi Mungu anawafanya kuipenda ''imani'' na kuipamba ''katika nyoyo zenu'' kwa yale aliyoyaweka ndani ya nyoyo zenu ya kuipenda haki na kuipendelea, na kwa yale aliyoiwekea haki miongoni mwa ushahidi na hoja zenye kuonyesha usahihi wake na kukubaliwa na nyoyo na maumbile ya asili, na pia yale ambayo Yeye Mtukufu anawafanyieni ya kuwapa mafanikio na kurejea kwake. Na akawafanya kuchukia "ukafiri, na kutoka nje ya mipaka;" yaani, madhambi makubwa "na uasi" yaani, madhambi madogo. Hayo ni kwa sababu ya kuchukia uovu na kutoutaka ambako Mwenyezi Mungu aliweka katika nyoyo zenu, na kwa sababu ya ushahidi na hoja alizoweka zenye kuonyesha ubovu wake, madhara yake na kutokubaliwa kwake na maumbile ya asili, na kwa sababu ya kuyachukia ambako Mwenyezi Mungu aliweka katika mioyo. "Hao;" yaani, wale ambao Mwenyezi Mungu amewapambia imani katika nyoyo zao na akawafanya kuipenda, na akawafanya kuchukia ukafiri, kutoka nje ya mipaka na uasi "ndio walioongoka." Yaani, wale ambao elimu zao na vitendo vyao vilitengenea, na wakashikamana na Dini iliyo madhubuti na njia iliyonyooka. Na kinyume chao ni wapotofu ambao walifanywa kupenda ukafiri, kuvuka mipaka na uasi, na wakafanywa kuchukia imani, kwani dhambi na sababu ya hayo ilikuwa ni yao. Kwa sababu walipovuka mipaka, Mwenyezi Mungu akaziba ya nyoyo zao, na walipokengeuka, Mwenyezi Mungu akazipotosha nyoyo zao, na pindi hawakuamini Haki ilipowajia mara ya kwanza, Mwenyezi Mungu akageuza mioyo yao.
#
{8} وقوله: {فضلاً من اللهِ ونعمةً}؛ أي: ذلك الخير الذي حصل لهم هو بفضل الله عليهم وإحسانِهِ، لا بحولهم وقوَّتهم. {واللهُ عليمٌ حكيمٌ}؛ أي: عليمٌ بمن يشكر النعمة فيوفِّقه لها ممَّن لا يشكرها ولا تليقُ به، فيضع فضلَه حيث تقتضيه حكمتُه.
{8} Na kauli yake, "Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na neema zake." Yaani, heri hiyo iliyowapata ni kwa sababu ya fadhila za Mwenyezi Mungu na wema wake, siyo uwezo na nguvu zao. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua mno, Mwenye hekima." Yaani, Yeye anajua vyema mwenye kushukuru neema zake, kwa hivyo anamuwezesha kuifikia. Na yule asiyeishukuru wala hata hafailii hilo, kwa hivyo anaiweka fadhila yake pale inapohitaji hekima yake.
: 9 - 10 #
{وَإِنْ طَائِفَتَانِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ اقْتَتَلُوا فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا فَإِنْ بَغَتْ إِحْدَاهُمَا عَلَى الْأُخْرَى فَقَاتِلُوا الَّتِي تَبْغِي حَتَّى تَفِيءَ إِلَى أَمْرِ اللَّهِ فَإِنْ فَاءَتْ فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا بِالْعَدْلِ وَأَقْسِطُوا إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ (9) إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ (10)}
9. Na ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana, basi yapatanisheni. Na likiwa moja la hao linamdhulumu mwenziwe, basi lipigeni linalodhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu. Na likirudi, basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaohukumu kwa haki. 10. Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe.
#
{9} هذا متضمِّنٌ لنهي المؤمنين عن أن يبغيَ بعضُهم على بعض ويقتلَ بعضُهم بعضاً، وأنه إذا اقتتلتْ طائفتان من المؤمنين؛ فإن على غيرهم من المؤمنين أن يتلافَوْا هذا الشرَّ الكبير بالإصلاح بينهم والتوسُّط على أكمل وجه يقع به الصلحُ ويسلكوا الطرق الموصلة إلى ذلك؛ فإن صلحتا؛ فبها ونعمت. {فإن بغتْ إحداهُما على الأخْرى فقاتِلوا التى تبغي حتى تفيءَ إلى أمرِ اللهِ}؛ أي: ترجع إلى ما حدَّ الله ورسولُه من فعل الخير وترك الشرِّ الذي من أعظمه الاقتتال. وقولُه: {فإن فاءتْ فأصْلِحوا بينَهما بالعَدْلِ}: هذا أمرٌ بالصُّلح وبالعدل في الصلح؛ فإنَّ الصُّلح قد يوجد، ولكن لا يكون بالعدل، بل بالظُّلم والحيف على أحد الخصمين؛ فهذا ليس هو الصُّلح المأمورُ به، فيجب أن لا يراعَى أحدهما لقرابةٍ أو وطنٍ أو غير ذلك من المقاصد والأغراض، التي توجب العدول عن العدل. {إنَّ اللهَ يحبُّ المُقْسِطينَ}؛ أي: العادلين في حكمهم بين الناس، وفي جميع الولايات التي تولوها، حتى إنه قد يدخل في ذلك عدلُ الرجل في أهله وعيالِه في أداء حقوقهم، وفي الحديث الصحيح: «المقسِطون عند الله على منابرَ من نورٍ؛ الذين يعدِلون في حكمِهم وأهليهم وما ولوا».
{9} Hili linajumuisha kuwakataza Waumini kushambuliana wao kwa wao na kuuana wao kwa wao, na kwamba ikiwa makundi mawili ya Waumini yatapigana, basi ni wajibu kwa Waumini wengineo kuuondoa uovu huu mkubwa kwa kusuluhisha baina yao na kufanya mapatano kati yao kwa njia iliyo bora zaidi ambayo kwayo maridhiano yanaweza kupatikana, na wafuate njia zinazofikisha kwa hilo. Ikiwa watasuluhishwa, basi hilo ni bora mno. "Na likiwa moja la hao linamdhulumu mwenzie, basi lipigeni linalodhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu." Yaani, mpaka lirejee katika yale aliyoyawekea mipaka Mwenyezi Mungu na Mtume wake miongoni mwa kutenda heri na kuacha maovu, ambayo kubwa yake zaidi ni kupigana vita. Na kauli yake: "Na likirudi, basi yapatanisheni kwa uadilifu" ni amri ya kufanya suluhu na kuwa waadilifu katika suluhu hiyo. Kwani suluhu inaweza kuwepo, lakini kwa njia isiyokuwa ya haki, bali kwa dhuluma na kutotendea haki mmoja wa mahasimu hao. Basi hii sio suluhu iliyoamrishwa. Ni lazima kwamba asipendelewe mmoja wao kwa sababu ya undugu, nchi, au malengo na madhumuni mengineyo ambayo yanasababisha kuiacha haki. "Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaohukumu kwa haki." Yaani: wale ambao ni waadilifu katika kuhukumu kwao baina ya watu, na katika majukumu yote wanayoyasimamia, kiasi kwamba inaingia humo uadilifu wa mwanamume kwa familia yake na wategemezi wake katika kutimiza haki zao. Ilisimuliwa katika hadithi sahihi kwamba, “Wale wanaofanya uadilifu mbele ya Mwenyezi Mungu watakuwa kwenye majukwaa ya nuru, wale ambao hufanya uadilifu katika kuhukumu kwao, familia zao, na wale ambao wao wanawasimamia.”
#
{10} {إنَّما المؤمنونَ إخوةٌ}: هذا عقدٌ عقدَه الله بين المؤمنين؛ أنَّه إذا وجد من أيِّ شخصٍ كان في مشرق الأرض ومغربها الإيمانُ بالله وملائكته وكتبه ورسله واليوم الآخر؛ فإنَّه أخٌ للمؤمنين أخوَّةً توجبُ أن يحبَّ له المؤمنون ما يحبُّون لأنفسهم، ويكرهوا له ما يكرهون لأنفسهم، ولهذا قال النبيُّ - صلى الله عليه وسلم - آمراً بالأخوَّة الإيمانيَّة: «لا تَحاسدوا ولا تَناجشوا ولا تَباغضوا ولا تَدابروا، وكونوا عبادَ اللهِ إخواناً. المسلمُ أخو المسلم؛ لا يظلمُه ولا يخذُلُه ولا يكذبه». متفقٌ عليه. وفيهما عن النبيِّ - صلى الله عليه وسلم -: «المؤمنُ للمؤمن كالبنيان يشدُّ بعضُه بعضاً، وشبك - صلى الله عليه وسلم - بين أصابعه». ولقد أمر اللهُ ورسولُه بالقيام بحقوق المؤمنين بعضهم لبعض وبما يحصُلُ به التآلفُ والتوادُدُ والتواصُلُ بينهم، كل هذا تأييدٌ لحقوق بعضهم على بعض؛ فمن ذلك إذا وقع الاقتتال بينهم الموجب لتفرُّق القلوب وتباغُضها وتدابُرها؛ فَلْيُصْلِح المؤمنون بين إخوانهم، ولْيَسْعَوا فيما به يزول شَنَآنهم. ثم أمر بالتقوى عموماً، ورتب على القيام بالتقوى وبحقوق المؤمنين الرحمةَ، فقال: {لعلَّكم تُرْحَمونَ}، وإذا حصلت الرحمةُ؛ حصل خيرُ الدنيا والآخرة. ودلَّ ذلك على أنَّ عدم القيام بحقوق المؤمنين من أعظم حواجب الرحمة. وفي هاتين الآيتين من الفوائد غير ما تقدم: أنَّ الاقتتال بين المؤمنين منافٍ للأخوَّة الإيمانيَّة، ولهذا كان من أكبر الكبائر. وأنَّ الإيمان والأخوَّة الإيمانيَّة لا يزولان مع وجود الاقتتال؛ كغيره من الذنوب الكبائر، التي دون الشرك، وعلى ذلك مذهب أهل السنة والجماعة. وعلى وجوب الإصلاح بين المؤمنين بالعدل. وعلى وجوب قتال البُغاة حتى يرجِعوا إلى أمر الله، وعلى أنهم لو رجعوا لغير أمرِ الله؛ بأن رجعوا على وجهٍ لا يجوز الإقرار عليه والتزامه؛ أنَّه لايجوز ذلك. وأنَّ أموالهم معصومةٌ؛ لأنَّ الله أباح دماءهم وقت استمرارهم على بَغْيِهم خاصةً دون أموالهم.
{10} "Hakika Waumini ni ndugu." Huu ni mkataba alioufunga Mwenyezi Mungu baina ya Waumini. Kwamba anayemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho hata kama atakuwa mashariki na magharibi ya ardhi, basi yeye ni ndugu kwa Waumini, udugu unaowalazimu Waumini wampendee kile wanachojipendea wao wenyewe, na wamchukie kile wanachojichukia wao wenyewe, na ndiyo maana Mtume - rehema na amani ziwe juu yake - alisema, akiamuru udugu wa kiimani, "Msihusudiane, msidanganyane katika biashara, msichukiane, wala msigeuziane migongo, na kuweni ndugu enyi waja wa Mwenyezi Mungu. Mwislamu ni ndugu wa Mwislamu. Hamdhulumu, hamwachi peke yake, wala hamdanganyi.” Imesimuliwa na Bukhari na Muslim. Na katika Bukhari na Muslim pia ilisimuliwa kutoka kwa Nabii - rehema na amani zimshukie - kwamba, "Muumini kwa Muumini mwenzake ni kama jengo linalotiana nguvu lenyewe kwa lenyewe - naye rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - akafungamanisha vidole vyake.” Mwenyezi Mungu na Mtume wake waliamrisha kwamba haki za Waumini zitekelezwe wao kwa wao, na wakaamrisha mambo yanayosababisha kuwepo maelewano kati yao, upendo na mawasiliano. Hayo yote ni kwa ajili ya kuimarisha haki za wenzao juu ya wenzao. Na katika hayo ni kwamba ikiwa kutatokea vita kati yao vinavyosababisha nyoyo zao kugawanyika, kuchukiana, na kupeana migongo, basi Waumini wanapaswa kusuluhisha kati ya ndugu zao, na wajitahidi kufanya yenye kutatua chuki zao. Kisha akaamrisha uchamungu kwa ujumla, na akaamrisha uchamungu na akaweka malipo ya rehema kwa mwenye kutekeleza haki za Waumini, kwa hivyo akasema, "ili mrehemewe." Na ikitokea rehema, mtu anakuwa amepata heri ya dunia na akhera. Hilo linaashiria kwamba kutotimiza haki za Waumini ni mojawapo ya vizuizi vikubwa vya rehema. Katika aya mbili hizi kuna manufaa zaidi ya yale yaliyotajwa hapo juu: kama vile kupigana baina ya Waumini kunapingana na udugu wa kiimani, na ndiyo maana kukawa ni katika madhambi makubwa zaidi. Pia imani hiyo na udugu wa kiimani havipotei hata kama watapigana vita, kama madhambi mengineyo makubwa, ambayo ni madogo kuliko ushirikina, na hilo ndilo dhehebu la wana Sunna na Jamaa. Pia kuna ulazima wa kupatanisha baina ya wale Waumini kwa uadilifu. Na pia kuna kwamba ni lazima kupigana vita na kundi linalopindukia mpaka warejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu, na kwamba ikiwa watarejea kwenye kitu kisichokuwa amri ya Mwenyezi Mungu, kwa namna kwamba walirudi kwa njia ambayo hairuhusiki kuikiri na kushikamana nayo, basi hilo haliruhusiki. Na pia kuna kwamba mali zao hazifai kuchukuliwa; kwa sababu Mwenyezi Mungu aliruhusu damu zao wakati walipokuwa wanaendelea kupindukia kwao mipaka, na hakuruhusu mali zao.
: 11 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِنْ قَوْمٍ عَسَى أَنْ يَكُونُوا خَيْرًا مِنْهُمْ وَلَا نِسَاءٌ مِنْ نِسَاءٍ عَسَى أَنْ يَكُنَّ خَيْرًا مِنْهُنَّ وَلَا تَلْمِزُوا أَنْفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ بِئْسَ الِاسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الْإِيمَانِ وَمَنْ لَمْ يَتُبْ فَأُولَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ (11)}
11. Enyi mlioamini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao, wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao. Huenda hao wakawa bora kuliko wao. Wala msivunjiane heshima, wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kwisha amini. Na wasiotubu, hao ndio wenye kudhulumu.
#
{11} وهذا أيضاً من حقوق المؤمنين بعضهم على بعض؛ أن: {لا يَسْخَرْ قومٌ من قومٍ}: بكلِّ كلامٍ وقولٍ وفعلٍ دالٍّ على تحقير الأخ المسلم؛ فإنَّ ذلك حرامٌ لا يجوز، وهو دالٌّ على إعجاب الساخر بنفسه، وعسى أن يكون المسخورُ به خيراً من الساخر، وهو الغالبُ والواقعُ؛ فإنَّ السخرية لا تقع إلاَّ من قلب ممتلئٍ من مساوئ الأخلاق، متحلٍّ بكل خلقٍ ذميمٍ، متخلٍّ من كلِّ خلقٍ كريم، ولهذا قال النبي - صلى الله عليه وسلم -: «بحسب امرئٍ من الشرِّ أن يحقر أخاه المسلمَ». ثم قال: {ولا تَلْمِزوا أنفُسَكُم}؛ أي: لا يعب بعضكم على بعض، واللَّمزُ بالقول، والهمز بالفعل، وكلاهما منهيٌّ عنه حرامٌ متوعَّدٌ عليه بالنار؛ كما قال تعالى: {ويلٌ لكلِّ هُمَزَةٍ لُمَزَةٍ ... } الآية، وسمَّى الأخ المسلم نفساً لأخيهِ؛ لأن المؤمنين ينبغي أن يكون هكذا حالُهم؛ كالجسد الواحد، ولأنَّه إذا همزَ غيرَه؛ أوجبَ للغير أن يهمزه، فيكون هو المتسبِّب لذلك، {ولا تنابَزوا بِالألقابِ}؛ أي: لا يعيِّر أحدُكم أخاه ويلقِّبه بلقبٍ يكره أن يقالَ فيه، وهذا هو التنابز، وأما الألقاب غير المذمومة؛ فلا تدخل في هذا. {بئسَ الاسمُ الفُسوقُ بعدَ الإيمانِ}؛ أي: بئسما تبدَّلتم عن الإيمان والعمل بشرائعِهِ وما يقتضيه بالإعراضِ عن أوامرِهِ ونواهيه باسم الفسوق والعصيان الذي هو التنابُزُ بالألقاب، {ومَن لم يَتُبْ فأولئك هم الظَّالمونَ}: وهذا هو الواجب على العبد: أن يتوبَ إلى الله تعالى، ويخرجَ من حقِّ أخيه المسلم باستحلالِهِ والاستغفار والمدح له مقابلةً على ذمِّه. {ومَن لمْ يَتُبْ فأولئكَ هم الظالمونَ}؛ فالناس قسمان: ظالمٌ لنفسه غيرُ تائبٍ، وتائبٌ مفلحٌ، ولا ثَمَّ غيرهما.
{11} Hili pia ni katika haki za Waumini wao kwa wao. Kwamba: "Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao" kwa kila neno, kauli na kitendo kinachoashiria kumdharau ndugu yake Muislamu. Kwani hilo ni haramu na haliruhusiwi, na ni linaonyesha kwamba mwenye kudharau anajiona tu yeye kuwa bora, ilhali pengine anayedharauliwa ni bora kuliko mwenye kumdharau, na hivyo ndivyo huwa uhalisia wa mambo mara nyingi. Kwa maana kukejeli hakutokei isipokuwa kutoka kwenye moyo uliojaa maadili mabaya, uliojaa kila tabia yenye kukashifiwa, ambayo haina hata tabia yoyote ya heshima, na ndiyo maana Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - akasema, "Inatosha mtu kwamba ni uovu kumdharau ndugu yake Mwislamu." Kisha akasema: "Wala msivunjiane heshima" Yaani, msitiane dosari nyinyi kwa nyinyi. Na hili huwa kwa kauli, na kwa vitendo, na hayo yote yamekatazwa, ni haramu na Mwenyezi Mungu ameahidi adhabu ya moto wa Jahannamu juu yake. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: "Ole wake kila mwenye kudhihaki kwa kauli na kwa vitendo..." hadi mwisho wa Aya. Na alisema kwamba ndugu Mwislamu nafsi moja na mwenzake; kwa sababu hali ya Waumini inapaswa kuwa hivi; Kama vile mwili mmoja, na kwa sababu ikimdhihaki mwingine, inamsababisha huyo mwengine pia kumdhihaki, nasi anakuwa yeye ndiye aliyesababisha hayo "wala msiitane kwa majina ya kejeli" ambayo anachukia kuitwa kwayo. Ama majina ya utani yasiyokashifiwa, hayo hayaingii katika hili. "Jina ovu mno ni kupindukia mipaka baada ya kwisha amini" kwani ni ubaya ulioje mlibadilisha mkaacha imani na kuacha kutenda kwa mujibu wa sheria zake na yale inalazimu, mkaacha maamrisho yake na kufanya makatazo yake mkawa mmepindukia mipaka na kuasi kwa kudhihaki wengine kwa kuitana kwa majina ya kejeli. "Na wasiotubu, hao ndio wenye kudhulumu." Basi ni wajibu wa mja, kutubia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutoka katika haki ya ndugu yake Muislamu kwa kukiri makosa yake na kuomba msamaha, na kumsifu kwa sababu ya kumkashifu alikomkashifu. "Na wasiotubu, hao ndio wenye kudhulumu." Kwa hivyo, watu wamegawanyika katika makundi mawili: mwenye kujidhulumu nafsi yake na ambaye hakutubia, na mwenye kutubia na akafanikiwa, na wala hakuna kikundi kingine.
: 12 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ وَلَا تَجَسَّسُوا وَلَا يَغْتَبْ بَعْضُكُمْ بَعْضًا أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَنْ يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ تَوَّابٌ رَحِيمٌ (12)}.
12. Enyi mlioamini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je, yupo katika nyinyi anayependa kuila nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba mno, Mwingi wa kurehemu.
#
{12} نهى تعالى عن كثيرٍ من الظَّنِّ السيِّئِ بالمؤمنين، {إنَّ بعضَ الظَّنِّ إثمٌ}: وذلك كالظَّنِّ الخالي من الحقيقة والقرينة، وكظنِّ السَّوْءِ الذي يقترن به كثيرٌ من الأقوال والأفعال المحرَّمة؛ فإنَّ بقاءَ ظنِّ السَّوْءِ بالقلب لا يقتصر صاحبه على مجرَّد ذلك، بل لا يزال به حتى يقول ما لا ينبغي ويفعل ما لا ينبغي، وفي ذلك أيضاً إساءةُ الظنِّ بالمسلم وبغضُهُ وعداوتُهُ المأمور بخلافها منه، {ولا تَجَسَّسوا}؛ أي: لا تفتِّشوا عن عورات المسلمين، ولا تَتَّبعوها، ودَعُوا المسلم على حاله، واستعملوا التغافُل عن زلاَّته، التي إذا فُتِّشَتْ؛ ظهرَ منها ما لا ينبغي، {ولا يَغْتَب بعضُكُم بعضاً}: والغيبة كما قال النبي - صلى الله عليه وسلم -: «ذِكْرُكَ أخاك بما يكرَهُ، ولو كان فيه». ثم ذَكَرَ مثلاً منفراً عن الغيبة، فقال: {أيحبُّ أحدُكُم أن يأكُلَ لحمَ أخيه مَيْتاً فكَرِهْتُموه}: شبَّه أكلَ لحمِهِ ميتاً المكروه للنفوس غايةَ الكراهةِ باغتيابه؛ فكما أنَّكم تكرهون أكل لحمه، خصوصاً إذا كان ميتاً فاقد الروح؛ فكذلك فَلْتَكْرهوا غيبته وأكل لحمه حيًّا، {واتَّقوا اللهَ إنَّ اللهَ توابٌ رحيمٌ}: والتوَّابُ: الذي يأذن بتوبة عبده، فيوفِّقه لها، ثم يتوبُ عليه بقبول توبته، رحيمٌ بعباده؛ حيث دعاهم إلى ما ينفعهم، وقبل منهم التوبة. وفي هذه الآية دليلٌ على التَّحذير الشديد من الغِيبة، وأنَّها من الكبائر؛ لأنَّ الله شبَّهها بأكل لحم الميت، وذلك من الكبائر.
{12} Mwenyezi Mungu amekataza dhana nyingi mbaya juu ya Waumini, "kwani baadhi ya dhana ni dhambi." Hii ni kama vile dhana isiyo na uhakika wala ushahidi, na kama dhana mbaya inayohusishwa na maneno na vitendo vingi vilivyoharamishwa. Kwani kusalia kwa dhana mbaya moyoni hakubakii hivyo tu kwa mwenye dhana hiyo, bali inaendelea dhana hiyo kuwa pamoja naye mpaka aseme yasiyofaa na kufanya yasiyofaa, na katika hili pia kuna kumdhania vibaya Muislamu, kumchukia na kumfanyia uadui, mambo ambayo imeamrishwa kufanya kinyume nayo. "Wala msipelelezane." Yaani, msipekue dosari za Waislamu, wala msiyafuate, na muwacheni Muislamu jinsi alivyo, na puuzeni dosari zake, ambazo zikipekuliwa, yatadhihirika kutoka kwazo yasiyofaa. "Wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi," kama alivyosema Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Ni wewe kumtaja ndugu yako kwa asiyoyapenda, hata kama yako ndani yake.” Kisha akataja mfano wa kuchukiza wa kusengenya, akasema: "Je, yupo katika nyinyi anayependa kuila nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo!" Amefananisha kula nyama ya maiti yake ambayo ni chukizo kubwa kwa nafsi na suala la kumsengenya. Basi kama vile unavyochukia kula nyama yake, haswa ikiwa amekufa na amepoteza roho yake, kadhalika chukieni kumsengenya na kula nyama yake hali ya kuwa yu hai. "Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba mno, Mwingi wa kurehemu" kwa sababu alikubali toba ya waja wake, na akawarehemu wake kwani aliwaita kwenye yale yatakayowanufaisha. Katika aya hii kuna ushahidi wa onyo kali dhidi ya kusengenya, na kwamba ni miongoni mwa madhambi makubwa. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alifananisha hilo na kula nyama ya mtu aliyekufa, na hilo ni katika madhambi makubwa.
: 13 #
{يَاأَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ ذَكَرٍ وَأُنْثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ (13)}
13. Enyi watu! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua mno, Mwenye habari.
#
{13} يخبرُ تعالى أنَّه خلقَ بني آدم من أصل واحدٍ وجنسٍ واحدٍ، وكلُّهم من ذكر وأنثى، ويرجعون جميعُهم إلى آدم وحواء، ولكنَّ الله تعالى بثَّ منهما رجالاً كثيراً ونساءً، وفرَّقهم، وجعلهم {شعوباً وقبائلَ}؛ أي: قبائل صغاراً وكباراً، وذلك لأجل أن يتعارَفوا؛ فإنَّه لو استقلَّ كلُّ واحد منهم بنفسه؛ لم يحصُلْ بذلك التعارف الذي يترتَّب عليه التَّناصر والتَّعاون والتَّوارث والقيام بحقوق الأقارب، ولكنَّ الله جعلهم شعوباً وقبائل؛ لأجل أن تحصُلَ هذه الأمور وغيرها ممَّا يتوقَّف على التعارف ولحوق الأنساب، ولكن الكرمَ بالتَّقوى؛ فأكرمُهم عند الله أتقاهم، وهو أكثرُهم طاعةً وانكفافاً عن المعاصي، لا أكثرُهم قرابةً وقوماً، ولا أشرفُهم نسباً، ولكن اللهَ تعالى {عليمٌ خبيرٌ}، يعلمُ منهم مَن يقوم بتقوى الله ظاهراً وباطناً ممَّن لا يقوم بذلك ظاهراً ولا باطناً، فيجازي كلًّا بما يستحقُّ. وفي هذه الآية دليلٌ على أنَّ معرفة الأنساب مطلوبةٌ مشروعةٌ؛ لأنَّ الله جعلهم شعوباً وقبائلَ لأجل ذلك.
{13} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kuwa aliwaumba wanadamu kutoka katika asili moja na jinsia moja, wote kwamba wote wametokana na mwanamume mmoja na mwanamke mmoja, na wote wanarudi kwa Adam na Hawa, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu akaeneza kutoka kwao wanaume wengi na wanawake, akawatenganisha na akawafanya kuwa "mataifa na makabila" na hilo ni ili wajuane. Kwani ikiwa kila mmoja wao angekuwa kivyake, basi hakungepatikana kujuana ambako kunasababisha kusaidiana, kushirikiana, kurithiana, na kutekeleza haki za jamaa, lakini Mwenyezi Mungu akawafanya kuwa mataifa na makabila, ili yapatikane mambo haya na mengineyo yanayotegemea kujuana na nasaba, lakini utukufu kunatokana na uchamungu. Kwa hivyo, Mtukufu zaidi miongoni mwao mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule aliye mcha Mungu zaidi miongoni mwao, naye ni yule ambaye ni mtiifu zaidi na mwenye kujiepusha na maasia, si wa karibu wao zaidi kijamaa na kwa watu, wala si mtukufu wao zaidi wa nasaba, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu "ni Mwenye kujua mno, Mwenye habari." Anawajua miongoni mwao mwenye kumcha Mwenyezi Mungu kwa nje na kwa ndani na anajua asiyefanya hivyo kwa nje au kwa ndani, na atamlipa kila mmoja wao anachostahiki. Katika aya hii kuna ushahidi kwamba kujua nasaba ni jambo linalohitajika kisheria. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwafanya watu kuwa mataifa na makabila kwa sababu ya hilo.
: 14 - 18 #
{قَالَتِ الْأَعْرَابُ آمَنَّا قُلْ لَمْ تُؤْمِنُوا وَلَكِنْ قُولُوا أَسْلَمْنَا وَلَمَّا يَدْخُلِ الْإِيمَانُ فِي قُلُوبِكُمْ وَإِنْ تُطِيعُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ لَا يَلِتْكُمْ مِنْ أَعْمَالِكُمْ شَيْئًا إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ (14) إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنْفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ أُولَئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ (15) قُلْ أَتُعَلِّمُونَ اللَّهَ بِدِينِكُمْ وَاللَّهُ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَاللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ (16) يَمُنُّونَ عَلَيْكَ أَنْ أَسْلَمُوا قُلْ لَا تَمُنُّوا عَلَيَّ إِسْلَامَكُمْ بَلِ اللَّهُ يَمُنُّ عَلَيْكُمْ أَنْ هَدَاكُمْ لِلْإِيمَانِ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (17) إِنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ غَيْبَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاللَّهُ بَصِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ (18)}
14. Mabedui walisema: 'Tumeamini.' Sema: 'Hamjaamini, lakini semeni: 'Tumesilimu.' Kwani Imani haijaingia katika nyoyo zenu. Na mkimtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hatakupunguzieni chochote katika vitendo vyenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mno, Mwingi wa kurehemu.' 15. Hakika Waumini ni wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake tena wasitie shaka kabisa, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio wakweli. 16. Sema: 'Ati ndio mnamfundisha Mwenyezi Mungu Dini yenu, na hali Mwenyezi Mungu anayajua ya katika mbingu na ardhi, na Mwenyezi Mungu anajua vyema kila kitu?' 17. Wanakusimbulia kuwa wamesilimu! Sema: 'Msinisimbulie kwa kusilimu kwenu. Bali Mwenyezi Mungu ndiye aliyewafanyia hisani kwa kukuongoeni kwenye Imani, ikiwa nyinyi ni wakweli.' 18. Hakika Mwenyezi Mungu anajua siri za mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu anayaona mno myatendayo.
#
{14} يخبرُ تعالى عن مقالةِ الأعراب، الذين دخلوا في الإسلام على عهد رسول الله - صلى الله عليه وسلم - دخولاً من غير بصيرةٍ ولا قيامٍ بما يجبُ ويقتضيه الإيمان؛ أنَّهم مع هذا ادَّعوا وقالوا {آمنَّا}؛ أي: إيماناً كاملاً مستوفياً لجميع أموره. هذا موجب هذا الكلام، فأمر الله رسوله أن يردَّ عليهم، فقال: {قل لمْ تؤمِنوا}؛ أي: لا تدَّعوا لأنفسِكُم مقامَ الإيمان ظاهراً وباطناً كاملاً، {ولكن قولوا أسْلَمْنا}؛ أي: دخلْنا في الإسلام، واقْتَصِروا على ذلك، {و} السبب في ذلك أنه {لَمَّا يدخلِ الإيمانُ في قلوبِكُم}: وإنَّما أسلمتم خوفاً أو رجاءً أو نحو ذلك مما هو السبب في إيمانكم؛ فلذلك لم تدخل بشاشة الإيمان في قلوبكم. وفي قوله: {ولمَّا يدخلِ الإيمانُ في قلوبِكُم}؛ أي: وقتَ هذا الكلام الذي صدر منكم، فكان فيه إشارةٌ إلى أحوالهم بعد ذلك؛ فإنَّ كثيراً منهم منَّ الله عليهم بالإيمان الحقيقيِّ والجهاد في سبيل الله، {وإن تُطيعوا اللهَ ورسولَه}: بفعل خير أو ترك شرٍّ {لا يَلِتْكُم من أعمالِكُمْ شيئاً}؛ أي: لا يَنْقُصْكم منها مثقال ذرَّةٍ، بل يوفيكم إيَّاها أكمل ما تكون، لا تفقدون منها صغيراً ولا كبيراً. {إنَّ الله غفورٌ رحيمٌ}؛ أي: غفورٌ لمَن تابَ إليه وأناب، رحيمٌ به؛ حيث قبل توبته.
{14} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasimulia kisa cha Mabedui walioingia katika Uislamu wakati wa maisha ya Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani ziwe juu yake - bila ya ufahamu wa sawasawa wala kufanya yanayotakiwa na imani yao. Pamoja na hayo, walidai na kusema, "Tumeamini," wakimaanisha imani kamili inayotimiza mambo yake yote. Hii ndiyo sababu ya maneno haya, basi Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake awajibu, akasema: "Sema: 'Hamjaamini" wala msijidai kwamba mna imani kamili, kwa nje na kwa ndani, "lakini semeni: 'Tumesilimu.' Yaani, Tumeingia katika Uislamu, na mkomekee hapo. "Na" sababu yake ni kuwa "Imani haijaingia katika nyoyo zenu" kwani mlisilimu kwa sababu ya hofu au matarajio au mambo mengine ya aina hiyo ambayo ndiyo sababu ya imani yenu; kwa hivyo, furaha ya imani haikuingia mioyoni mwenu. Na katika kauli yake "Imani haijaingia katika nyoyo zenu;" yaani wakati walipoyasema hayo, na ndani yake kuna ishara ya hali yao baada ya hayo. Kwani wengi wao Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwa imani ya kweli na kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. "Na mkimtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake" kwa kufanya heri au kuacha maovu "hatawapunguzia chochote katika vitendo vyenu" hata kama ni kiasi uzito wa chembe, bali atakupeni kwa ukamilifu wake, wala hamtapoteza katika hayo kidogo au kikubwa. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mno, Mwingi wa kurehemu." Yaani, humsamehe mwenye kutubia kwake na akarejea kwake, na ni Mwingi wa kurehemu, ambapo alikubali toba yake.
#
{15} {إنَّما المؤمنون}؛ أي: على الحقيقة، {الذين آمنوا بالله ورسولِهِ وجاهدوا في سبيلِ اللهِ}؛ أي: من جمعوا بينَ الإيمان بالله ورسولِهِ والجهادِ في سبيله؛ فإنَّ مَن جاهدَ الكفارَ؛ دلَّ ذلك على الإيمان التامِّ في قلبِهِ؛ لأنَّ من جاهد غيره على الإسلام والإيمان والقيام بشرائعه؛ فجهاده لنفسه على ذلك من باب أولى وأحرى، ولأنَّ من لم يقوَ على الجهاد؛ فإنَّ ذلك دليلٌ على ضعف إيمانه. وشرط تعالى في الإيمان عدم الريب؛ أي: الشكِّ؛ لأنَّ الإيمان النافع هو الجزم اليقينيُّ بما أمر الله بالإيمان به، الذي لا يعتريه شكٌّ بوجه من الوجوه. وقوله: {أولئك هم الصادقون}؛ أي: الذين صدَّقوا إيمانهم بأعمالهم الجميلة؛ فإنَّ الصدقَ دعوى عظيمةٌ في كل شيء يُدَّعى، يحتاج صاحبه إلى حجة وبرهانٍ، وأعظم ذلك دعوى الإيمان، الذي هو مدار السعادة والفوز الأبديِّ والفلاح السرمديِّ؛ فمن ادَّعاه وقام بواجباته ولوازمه؛ فهو الصادق المؤمن حقًّا، ومن لم يكن كذلك؛ عُلِم أنه ليس بصادق في دعواه، وليس لدعواه فائدة؛ فإنَّ الإيمان في القلب، لا يطلع عليه إلا الله تعالى؛ فإثباتُه ونفيُه من باب تعليم الله بما في القلب وهو سوء أدبٍ وظنٍّ بالله.
{15} "Hakika Waumini" wa kweli "ni wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake tena wasitie shaka kabisa, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu." Yaani, wale waliojumuisha kati ya kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kufanya jihadi katika njia yake. Kwani mwenye pigana na makafiri, hilo linaonyesha kwamba kuna imani kamili moyoni mwake. Kwa sababu yeyote anayepigana dhidi ya wengine kwa ajili ya Uislamu, imani, na kushikamana na sheria zake, basi jihadi yake dhidi ya nafsi yake juu ya hilo inafailia zaidi, na kwa sababu asiyekuwa na nguvu ya jihadi, hilo kwa hakika ni ishara ya udhaifu wa imani yake. Na Mwenyezi Mungu aliweka sharti la mtu kuwa na imani kwamba asiwe na shaka. Kwa sababu imani yenye manufaa ni ile yenye uhakika na yakini kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu aliamrisha kuyaamini, ambayo haiingiwi na shaka kwa namna yoyote ile. Na kauli yake: "Hao ndio wakweli." Yaani: wale waliosadikisha imani yao kwa matendo yao mazuri. Kwa maana ukweli ni madai makubwa katika kila jambo ambayo yanahitaji mwenye kuyadai kuwa hoja na uthibitisho, na kubwa zaidi kati ya hayo ni mtu kudai kwamba ana imani, ambayo ndiyo kiini cha furaha, kufuzu na kushinda milele. Kwa hivyo, mwenye kudai kwamba ana imani, kisha akatekeleza wajibu zake na mambo yanayofungamana nayo, basi yeye ndiye mkweli na Muumini wa kweli. Na asiyekuwa hivyo, inajulikana kwamba yeye si mkweli katika madai yake, na kwamba madai yake hayo hayana manufaa yoyote. Kwani imani iko moyoni, na hakuna anayeijua isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee. Kuithibitisha na kuikanusha ni katika suala la kumfundisha Mwenyezi Mungu yale yaliyo moyoni, na hilo ni kuwa na tabia mbaya na dhana mbaya kwa Mwenyezi Mungu.
#
{16} ولهذا قال: {قل أتُعَلِّمون اللهَ بِدينِكم واللهُ يعلمُ ما في السمواتِ وما في الأرضِ واللهُ بكلِّ شيءٍ عليمٌ}: وهذا شاملٌ للأشياء كلِّها، التي من جملتِها ما في القلوب من الإيمان والكفران والبرِّ والفجور؛ فإنَّه تعالى يعلمُ ذلك كلَّه، ويجازي عليه، إن خيراً فخيرٌ، وإن شرًّا فشرٌّ.
{16} Ndiyo maana akasema: "Sema: 'Ati ndio mnamfundisha Mwenyezi Mungu Dini yenu, na hali Mwenyezi Mungu anayajua ya katika mbingu na ardhi, na Mwenyezi Mungu anajua vyema kila kitu?" Na hili linajumuisha mambo yote yaliyo moyoni kama vile imani, ukafiri, wema na uovu. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu anayajua yote haya, na atayalipa juu yake, ikiwa ni nzuri, basi kwa nzuri, na ikiwa ni ubaya, basi kwa ubaya.
#
{17} هذه حالةٌ من أحوال من ادَّعى لنفسه الإيمان وليس به؛ فإنَّه إمَّا أن يكون ذلك تعليماً لله، وقد علم أنه عالمٌ بكلِّ شيء، وإمَّا أن يكون قصدُهم بهذا الكلام المنة على رسولِه، وأنَّهم قد بذلوا وتبرَّعوا بما ليس من مصالحهم بل هو من حظوظه الدنيويَّة، وهذا تجمُّلٌ بما لا يجمل، وفخرٌ بما لا ينبغي لهم الفخر به على رسوله؛ فإنَّ المنَّة لله تعالى عليهم؛ فكما أنه تعالى هو المانُّ عليهم بالخلق والرزق والنعم الظاهرة والباطنة؛ فمنَّتُه عليهم بهدايتهم إلى الإسلام ومنَّتُه عليهم بالإيمان أفضلُ من كلِّ شيء، ولهذا قال: {يَمُنُّونَ عليك أنْ أسلَموا قل لا تَمُنُّوا عليَّ إسلامكم بلِ اللهُ يمنُّ عليكم أنْ هداكُم للإيمانِ إن كنتُم صادقينَ}.
{17} Hii ni hali mojawapo ya hali za mtu anayedai kuwa ana imani lakini hana. Hilo ima ni kumfundisha Mwenyezi Mungu, na tayari anajulikana kwamba Yeye anajua kila kitu, na ima makusudio yao kwa maneno haya ni kumsimbulia Mtume wake, na kwamba wametoa sana visivyokuwa kwa masilahi yao, bali ni katika mambo ya kumfaidisha yeye katika dunia. Lakini huku ni kujipamba kwa yale ambayo si ya kujipamba kwayo, na kujifahiri kwa yale wasiyopaswa kujifahiri kwayo juu ya Mtume wake. Kwani Mwenyezi Mungu ndiye anayefaa kuwasimbulia. Kwa kuwa namna Yeye ndiye aliyewafanyia hisani kwa uumbaji, kuwaruzuku, na kuwaneemesha neema za dhahiri na zilizofichika, basi hisani yake juu yao kwa kuwaongoa kwenye Uislamu na neema yake juu yao kwa imani ni bora kuliko kila kitu, na ndiyo maana akasema: "Wanakusimbulia kuwa wamesilimu! Sema: 'Msinisimbulie kwa kusilimu kwenu. Bali Mwenyezi Mungu ndiye aliyewafanyia hisani kwa kuwaongoa kwenye Imani, ikiwa nyinyi ni wakweli."
#
{18} {إنَّ اللهَ يعلمُ غَيْبَ السَّمواتِ والأرضِ}؛ أي: الأمور الخفية فيهما، التي تخفى على الخلق؛ كالذي في لُجَج البحار، ومَهامِهِ القِفار، وما جنَّهُ الليلُ أو واراهُ النهارُ؛ يعلمُ قطرات الأمطار، وحبات الرمال، ومكنونات الصدور، وخبايا الأمور، {وما تَسْقُطُ مِن ورقةٍ إلاَّ يَعْلَمُها ولا حبَّةٍ في ظُلُماتِ الأرضِ ولا رَطْبٍ ولا يابس إلاَّ في كتابٍ مبينٍ}. {واللهُ بصيرٌ بما تعملون}: يُحصي عليكم أعمالَكم ويُوَفيكُم إيَّاها، ويجازيكم عليها بما تقتضيه رحمته الواسعة وحكمته البالغة.
{18} "Hakika Mwenyezi Mungu anajua siri za mbingu na ardhi." Yaani, mambo yaliyofichika ndani yake kwa viumbe kama yale yaliyo katika vilindi vya bahari, na sehemu za ndani mno katika jangwa, na yale yaliyofichwa na usiku au kusitiriwa na mchana. Anayajua matone ya mvua, na chembe za mchanga, na yaliyofichika ndani ya vifua, na siri za mambo. "Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinachobainisha." "Na Mwenyezi Mungu anayaona mno myatendayo." Anawahesabia vitendo vyenu na atawapa hayo kikamilifu, na atawalipa kwa hayo kulingana na inavyotaka rehema yake pana na hekima yake kubwa mno.
Imekamilika tafsiri ya Surat Al-Hujurat kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, kupeana kwake kwa wingi na ukarimu wake, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu.
* * *