:
Tafsiri ya Surat Al-Fath
Tafsiri ya Surat Al-Fath
Ilishuka Madina
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
: 1 - 3 #
{إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُبِينًا (1 ضضض) لِيَغْفِرَ لَكَ اللَّهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ وَيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَيَهْدِيَكَ صِرَاطًا مُسْتَقِيمًا (ضضض 2) وَيَنْصُرَكَ اللَّهُ نَصْرًا عَزِيزًا (3)}
1. Hakika sisi tumekufungulia Ushindi wa dhahiri. 2. Ili Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yajayo, na akutimizie neema zake, na akuongoe katika njia iliyonyooka. 3. Na Mwenyezi Mungu akunusuru nusura yenye nguvu.
#
{1} هذا الفتحُ المذكور هو صلحُ الحديبيةِ، حين صدَّ المشركون رسولَ الله - صلى الله عليه وسلم - لمَّا جاء معتمراً في قصة طويلة ، صار آخر أمرها أن صالحهم رسولُ الله - صلى الله عليه وسلم - على وَضْع الحرب بينه وبينهم عشر سنين، وعلى أن يعتمرَ من العام المقبل، وعلى أنَّ مَن أراد أن يَدْخُلَ في عهد قريش وحلفهم؛ دَخَلَ، ومن أحبَّ أن يدخُلَ في عهد رسول الله - صلى الله عليه وسلم - وعقده؛ فعل. وسبب ذلك لما أمَّن الناس بعضهم بعضاً؛ اتَّسعت دائرة الدعوة لدين الله عزَّ وجلَّ، وصار كلُّ مؤمن بأيِّ محلٍّ كان من تلك الأقطار يتمكَّن من ذلك، وأمكن الحريص على الوقوف على حقيقة الإسلام، فدخل الناسُ في تلك المدَّة في دين الله أفواجاً؛ فلذلك سمَّاه الله فتحاً، ووصفه بأنَّه فتحٌ مبينٌ؛ أي: ظاهرٌ جليٌّ، وذلك لأنَّ المقصود في فتح بلدان المشركين إعزازُ دين الله وانتصار المسلمين، وهذا حصل بذلك الفتحُ.
{1} Ushindi huu uliotajwa hapa ni Mkataba wa amani wa Hudaybiyyah, pale washirikina walipomzuilia Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake – alipokuja kwa ajili ya kufanya Umra, katika kisa kirefu, ambacho mwisho wake ulikuwa kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - alifanya nao suluhu juu ya kumaliza vita kati yake na wao kwa muda wa miaka kumi, na kwamba atafanya Umra katika mwaka uliofuata, na kwamba anayetaka kuingia katika mkataba wa kusaidiana na Maquraishi, ana ruhusa ya kufanya hivyo, na anayetaka kuingia katika mkataba wa kusaidiana na Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake, basi anaweza kufanya hivyo. Na sababu ya hilo kwamba pindi watu walipopata amani kutokana na wao kwa wao, eneo la kulingania kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu likapanuka, na akawa kila Muumini katika sehemu yoyote iliyopo katika nchi hizo anaweza kufanya hivyo, na likamwezesha mwenye uchu wa kuujua ukweli wa Uislamu kuujua. Kwa hivyo watu wakaingia katika dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi wakati wa kipindi hicho. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akauita (mkataba huo) ushindi, na akauelezea kwamba ni ushindi ulio wazi. Kwa sababu makusudio ya kuziteka nchi za washirikina ni kuimarisha dini ya Mwenyezi Mungu na kuwapa ushindi Waislamu, na hili lilitokea kwa ushindi huo.
#
{2} ورتَّب الله على هذا الفتح عدة أمور، فقال: {ليغفر لك اللهُ ما تقدَّم من ذنبِكَ وما تأخَّر}: وذلك ـ والله أعلم ـ بسبب ما حَصَلَ بسببه من الطاعات الكثيرة والدُّخول في الدين بكثرة، وبما تحمل - صلى الله عليه وسلم - من تلك الشروط التي لا يصبِرُ عليها إلاَّ أولو العزم من المرسلين، وهذا من أعظم مناقبه وكراماته - صلى الله عليه وسلم -: أنْ غَفَرَ الله له ما تقدَّم من ذنبه وما تأخَّر، {ويتمَّ نعمته عليك}: بإعزاز دينك ونصرِك على أعدائك واتِّساع كلمتك، {ويهدِيَك صراطاً مستقيماً}: تنال به السعادةَ الأبديَّة والفلاح السرمديَّ.
{2} Mwenyezi Mungu alipanga mambo kadhaa kutokana na ushindi huu, akasema: "Ili Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yajayo." Na hili - na Mwenyezi Mungu ndiye anajua zaidi - ni kwa sababu ya utiifu mwingi uliotokea kwa sababu yake na watu wengi kuingia katika Dini, na kwa sababu ya yale aliyoyastahimili - rehema na amani ziwe juu yake, - miongoni mwa masharti hayo ambayo hawezi kuyavumilia isipokuwa wenye stahamala kubwa miongoni mwa Mitume, na hili ni katika fadhila zake kubwa na utukufu wake - rehema na amani ziwe juu yake, kwamba Mwenyezi Mungu alimghufiria madhambi yake yaliyopita na yajayo, ''na akutimizie neema zake" kwa kuitia nguvu dini yako, na ushindi wako dhidi ya maadui zako, na kupanuka kwa maneno yako ''na akuongoe katika njia iliyonyooka'' ambayo kwayo utapata furaha ya milele na kufaulu kwenye kudumu milele.
#
{3} {وينصُرَك الله نصراً عزيزاً}؛ أي: قويًّا لا يتضعضعُ فيه الإسلام، بل يحصُلُ الانتصار التامُّ وقمع الكافرين وذُلُّهم ونقصُهم، مع توفُّر قوى المسلمين ونموِّهم ونموِّ أموالهم؛ [ثم] ذكر آثار هذا الفتح على المؤمنين، فقال:
{3} ''Na Mwenyezi Mungu akunusuru nusura yenye nguvu." Yaani, yenye nguvu, ambayo ndani yake Uislamu hautadhoofika, bali ushindi kamili utatokea, na makafiri watakandamizwa, kudhalilishwa, na kupunguzwa, kwa kupatikana kwa nguvu za Waislamu, kukua kwao, na kukua kwa mali zao. [Kisha] akataja athari za ushindi huo kwa Waumini, na akasema:
: 4 - 6 #
{هُوَ الَّذِي أَنْزَلَ السَّكِينَةَ فِي قُلُوبِ الْمُؤْمِنِينَ لِيَزْدَادُوا إِيمَانًا مَعَ إِيمَانِهِمْ وَلِلَّهِ جُنُودُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَكَانَ اللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا (4) لِيُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَيُكَفِّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَكَانَ ذَلِكَ عِنْدَ اللَّهِ فَوْزًا عَظِيمًا (5) وَيُعَذِّبَ الْمُنَافِقِينَ وَالْمُنَافِقَاتِ وَالْمُشْرِكِينَ وَالْمُشْرِكَاتِ الظَّانِّينَ بِاللَّهِ ظَنَّ السَّوْءِ عَلَيْهِمْ دَائِرَةُ السَّوْءِ وَغَضِبَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ وَلَعَنَهُمْ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَهَنَّمَ وَسَاءَتْ مَصِيرًا (6)}
4. Yeye ndiye aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za Waumini ili wazidi Imani juu ya Imani yao. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye majeshi ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye elimu mno, Mwenye hekima. 5. Ili awaingize Waumini wanaume na Waumini wanawake katika Bustani za mbinguni zipitazo mito chini yake, wadumu humo, na awafutie makosa yao. Na huko ndiko kufuzu kukubwa mbele ya Mwenyezi Mungu. 6. Na awape adhabu wanafiki wanaume na wanafiki wanawake, na washirikina wanaume na washirikina wanawake, wanaomdhania Mwenyezi Mungu dhana mbaya. Utawafikia mgeuko mbaya, na Mwenyezi Mungu awakasirikie, na awalaani, na awaandalie Jahanamu. Na hayo ni marudio maovu kabisa.
#
{4} يخبر تعالى عن منَّته على المؤمنين بإنزال السكينة في قلوبهم، وهي السكونُ والطمأنينةُ والثباتُ عند نزول المحنِ المقلقةِ والأمور الصعبة التي تشوِّشُ القلوبَ وتزعجُ الألباب وتضعِفُ النفوس؛ فمن نعمة الله على عبده في هذه الحال أن يثبِّتَه ويربطَ على قلبه، وينزِلَ عليه السكينةَ، ليتلقَّى هذه المشقَّاتِ بقلبٍ ثابتٍ ونفس مطمئنةٍ، فيستعدَّ بذلك لإقامة أمر الله في هذه الحال، فيزداد بذلك إيمانُه، ويتمَّ إيقانُه. فالصحابةُ رضي الله عنهم لمَّا جرى ما جرى بينَ رسول اللهِ - صلى الله عليه وسلم - والمشركين من تلك الشروطِ التي ظاهرُها أنَّها غضاضةٌ عليهم وحطٌّ من أقدارِهم، وتلك لا تكادُ تصبِرُ عليها النفوس، فلما صبروا عليها ووطَّنوا أنفسَهم لها؛ ازدادوا بذلك إيماناً مع إيمانهم. وقوله: {ولله جنودُ السمواتِ والأرضِ}؛ أي: جميعها في ملكه وتحت تدبيره وقهره؛ فلا يظنُّ المشركون أنَّ الله لا ينصُرُ دينَه ونبيَّه، ولكنَّه تعالى عليمٌ حكيمٌ، فتقتضي حكمته المداولةَ بين الناس في الأيام وتأخيرَ نصر المؤمنين إلى وقتٍ آخر.
{4} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaeleza juu ya baraka zake juu ya waumini kwa kupeleka utulivu katika nyoyo zao, ambao ni utulivu, utulivu, na uthabiti pale yanaposhuka mitihani yenye kusumbua na mambo magumu ambayo yanachanganya nyoyo, yanasumbua akili na kudhoofisha roho. Miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu juu ya mja wake katika hali hii ni kumfanya kuwa na uthabiti, kuutia nguvu moyo wake, na kumpa utulivu, ili akabiliane na magumu hayo kwa moyo thabiti na nafsi iliyotulia, hivyo kumuweka tayari kutekeleza. Amri ya Mungu katika hali hii, hivyo kuongeza imani yake na kukamilisha uhakika wake. Yalipotokea Maswahabah, yaliyotokea baina ya Mtume wa Mwenyezi Mungu - Rehema na Amani zimshukie - na washirikina, miongoni mwa hali zinazoonekana kuwa ni dharau kwao na udhalilishaji wao. Na zile ambazo nafsi hazikuwa na subira nazo, basi zilipozivumilia na wakatulia humo. Waliongeza imani yao pamoja na imani yao. Na kauli yake: ''Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye majeshi ya mbingu na ardhi.'' Yaani, wote wako katika milki yake na chini ya udhibiti wake na ukandamizaji. Washirikina wasidhani kuwa Mwenyezi Mungu haungi mkono dini yake na Nabii wake, bali Yeye, Mwenye nguvu, ni Mjuzi, Mwenye hekima, hivyo hekima yake inahitaji mashauriano baina ya watu katika siku na kuchelewesha ushindi wa Waumini mpaka. wakati mwingine.
#
{5} {ليدخِلَ المؤمنين والمؤمناتِ جناتٍ تجري من تحتِها الأنهارُ خالدينَ فيها ويكفِّرَ عنهم سيئاتِهِم}: فهذا أعظمُ ما يحصُلُ للمؤمنين؛ أي: يحصُلُ لهم المرغوبُ المطلوبُ بدخول الجنات، ويزيل عنهم المحذور بتكفير السيئات، {وكان ذلك}: الجزاء المذكورُ للمؤمنينَ، {عند الله فوزاً عظيماً}: فهذا ما يفعلُ بالمؤمنين في ذلك الفتح المبين.
{5} ''Ili awaingize Waumini wanaume na Waumini wanawake katika Bustani za mbinguni zipitazo mito kati yake, wadumu humo, na awafutie makosa yao." Haya ndiyo makubwa zaidi yatakayowapata Waumini kwa kupata wanayoyatamani kwa kuingia katika Bustani za mbinguni, na kuwaondolea wanayohofiwa kwa kuwafutia mabaya yao. ''Na huko" ambako kumetajwa kuhusu malipo ya Waumini, ''ndiko kufuzu kukubwa mbele ya Mwenyezi Mungu." Hivi ndivyo watakavyofanyiwa Waumini katika ushindi huo wa wazi.
#
{6} وأمَّا المنافقون والمنافقاتُ والمشركون والمشركاتُ؛ فإنَّ الله يعذِّبُهم بذلك ويريهم ما يسوؤُهم؛ حيث كان مقصودُهم خِذلان المؤمنين، وظنُّوا بالله ظنَّ السَّوْءِ أنَّه لا ينصُرُ دينَه ولا يُعلي كلمته، وأنَّ أهل الباطل ستكونُ لهم الدائرةُ على أهل الحقِّ، فأدار الله عليهم ظَنَّهم، وكانت دائرةُ السوء عليهم في الدنيا، {وغضبَ الله عليهم}: بما اقترفوه من المحادَّة لله ولرسولِهِ، {ولَعَنَهم}؛ أي: أبعدهم وأقصاهم عن رحمتِهِ، {وأعدَّ لهم جهنَّم وساءت مصيراً}.
{6} Ama wanaafiki wanaume na wanaafiki wanawake, na washirikina wanaume na washirikina wanawake, basi Mwenyezi Mungu atawaadhibu kwa hayo na atawaonyesha yatakayowawiya mabaya. Kwa vile nia yao ilikuwa ni kuwaangusha Waumini, na wakamdhania Mwenyezi Mungu dhana mbaya kwamba hatainusuru dini yake, wala hatalinyanyua neno lake, na kwamba wana batili watawashinda wana haki, lakini Mwenyezi Mungu akawageuzia dhana yao dhidi yao, kwa hivyo mgeuko mbaya ukawa ni wao katika dunia. ''Na Mwenyezi Mungu atawakasirikia" kwa sababu ya yale waliyoyazua ya kumpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake. ''Na akawalaani" kwa kuwaweka mbali na mno na rehema zake, ''na akawaandalia Jahanamu. Na hayo ni marudio maovu kabisa."
: 7 #
{وَلِلَّهِ جُنُودُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَكَانَ اللَّهُ عَزِيزًا حَكِيمًا (7)}.
7. Na Mwenyezi Mungu ana majeshi ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
#
{7} كرَّر الإخبار بأنَّ له ملك السماواتِ والأرض وما فيهما من الجنود؛ ليعلم العبادُ أنَّه تعالى هو المعزُّ المذلُّ، وأنَّه سينصر جنودَه المنسوبة إليه؛ كما قال تعالى: {وإنَّ جندَنا لهم الغالبونَ}، {وكان الله عزيزاً}؛ أي: قويًّا غالباً قاهراً لكلِّ شيءٍ، ومع عزَّته وقوَّته؛ فهو حكيمٌ في خلقه. وتدبيرُه يَجري على ما تقتضيه حكمتُه وإتْقانُه.
{7} Alirudia kujulisha kwamba yeye ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na majeshi yaliyomo; ili waja wajue kwamba Yeye, Mwenyezi ndiye Mwenye kutukuza na kudhalilisha na kwamba atawapa ushindi wanajeshi wake wanaonasibishwa naye. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: ''Na kwamba wanajeshi wetu ndio watakaoshinda." Kisha akasema: ''Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu" mwenye kushinda na kutiisha kila kitu. Na pamoja na utukufu wake na nguvu zake, Yeye ni Mwenye hekima katika kuumba kwake. Uendeshaji mambo wake unaenda kulingana inavyohitaji hekima yake na ustadi wake wa kutenda.
: 8 - 9 #
{إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا (8) لِتُؤْمِنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ وَتُعَزِّرُوهُ وَتُوَقِّرُوهُ وَتُسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا (9)}
8. Hakika tumekutuma wewe uwe Shahidi, na Mbashiri, na Mwonyaji. 9. Ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mumsaidie, na mumheshimu, na mumtakase asubuhi na jioni.
#
{8} أي: {إنَّا أرسلناكَ}: أيها الرسولُ الكريمُ، {شاهداً}: لأمتك بما فعلوه من خير وشرٍّ، وشاهداً على المقالات والمسائل حقِّها وباطِلِها، وشاهداً لله تعالى بالوحدانيَّة والانفراد بالكمال من كلِّ وجه، {ومبشراً}: من أطاعك وأطاع الله بالثواب الدنيويِّ والدينيِّ والأخرويِّ، ومنذراً من عصى الله بالعقاب العاجل والآجل، ومن تمام البشارةِ والنِّذارة بيان الأعمال والأخلاق التي يبشر بها وينذر؛ فهو المبيِّن للخير والشرِّ والسعادة والشقاوة والحقِّ من الباطل.
{8} Yaani, ''Hakika tumekutuma wewe'' ewe Mtume Mtukufu, ''uwe Shahidi'' kwa Umma wako kwa yale waliyoyafanya ya heri na maovu, na uwe shahidi juu ya maneno na masuala, ya haki na ya batili, na shahidi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya upweke wake na upekee wake katika ukamilifu kwa namna zote, ''na Mbashiri'' kwa anayekutii na akamtii Mwenyezi Mungu kwamba tapata malipo mazuri ya kidunia na ya kidini na ya kiakhera, na kuwaonya wanaomuasi Mwenyezi Mungu kwamba watapata adhabu ya sasa na ya baadaye. Na katika kubashiri na kuonya kikamilifu ni kubainisha matendo na maadili ambayo kwayo anabashiri na kuonya. Kwa hivyo, yeye anabainisha heri na shari, furaha na kuwa mashakani, na haki na batili.
#
{9} ولهذا رتَّب على ذلك قوله: {لتؤمِنوا باللهِ ورسولِهِ}؛ أي: بسبب دعوة الرسول لكم وتعليمه لكم ما ينفعكم أرسلناه؛ لتقوموا بالإيمان بالله ورسولِهِ، المستلزم ذلك لطاعتهما في جميع الأمور، {وتعزِّروهُ وتوقِّروهُ}؛ أي: تعزِّروا الرسول - صلى الله عليه وسلم - وتوقِّروه؛ أي: تعظِّموه، وتجلُّوه، وتقوموا بحقوقِهِ، كما كانت له المنَّة العظيمةُ برقابكم، {وتسبِّحوه}؛ أي: تسبِّحوا لله {بكرةً وأصيلاً}: أول النهار وآخره. فذكر الله في هذه الآية الحقَّ المشترك بين الله وبين رسوله، وهو الإيمان بهما، والمختصُّ بالرسول، وهو التعزير والتوقير، والمختصُّ بالله، وهو التسبيح له والتقديس بصلاةٍ أو غيرها.
{9} Ndiyo maana akasema, “Ili muamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake." Yaani, tulimtuma ili akulinganieni Mtume na akufundisheni yatakayokunufaisheni; ili mpate kumwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, jambo ambalo linalazimu kuwatii katika kila jambo, "na mumsaidie, na mumheshimu" na mumtekelezee haki zake, kama vile alivyo na neema kubwa juu ya shingo zenu. "Na mumtakase" Mwenyezi Mungu ''asubuhi na jioni." Basi Mwenyezi Mungu akataja katika Aya hii haki iliyo sawa baina ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, nayo ni kuwaamini, na ile iliyo mahususi kwa Mtume, ambayo ni kumsaidia na kumheshimu, na ile iliyo mahususi kwa Mwenyezi Mungu, ambayo ni kumtakasa kwa swala au kitu kingine chochote.
: 10 #
{إِنَّ الَّذِينَ يُبَايِعُونَكَ إِنَّمَا يُبَايِعُونَ اللَّهَ يَدُ اللَّهِ فَوْقَ أَيْدِيهِمْ فَمَنْ نَكَثَ فَإِنَّمَا يَنْكُثُ عَلَى نَفْسِهِ وَمَنْ أَوْفَى بِمَا عَاهَدَ عَلَيْهُ اللَّهَ فَسَيُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا (10)}
10. Bila ya shaka wale wanaokupa kiapo cha utii, kwa hakika wanampa Mwenyezi Mungu kiapo cha utii. Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao. Kwa hivyo, avunjaye ahadi hizi, basi anavunja kwa kuidhuru nafsi yake. Na anayetekeleza aliyomuahadi Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu atamlipa ujira mkubwa.
#
{10} هذه المبايعةُ التي أشار الله إليها هي بيعة الرضوان، التي بايع الصحابةُ رضي الله عنهم فيها رسولَ الله - صلى الله عليه وسلم - على أن لا يفرُّوا عنه؛ فهي عقدٌ خاصٌّ، من لوازمه أن لا يفرُّوا، ولو لم يبقَ منهم إلاَّ القليلُ، ولو كانوا في حال يجوزُ الفرارُ فيها. فأخبر تعالى: {إنَّ الذين يبايِعونَك}: حقيقةُ الأمرِ أنَّهم {يبايِعونَ الله}: ويعقِدونَ العقد معه، حتى إنه من شدَّة تأكُّده أنَّه قال: {يدُ الله فوق أيديهم}؛ أي: كأنهم بايعوا الله وصافحوه بتلك المبايعة، وكلُّ هذا لزيادة التأكيد والتقوية، وحملهم على الوفاء بها، ولهذا قال: {فمن نكث}: فلم يفِ بما عاهد الله عليه، {فإنَّما ينكُثُ على نفسه}؛ أي: لأنَّ وَبال ذلك راجعٌ إليه وعقوبتَه واصلةٌ له، {ومن أوفى بما عاهَدَ عليهُ اللهَ}؛ أي: أتى به كاملاً موفراً، {فسيؤتيه أجراً عظيماً}: لا يعلم عِظَمَه وقَدْرَه إلاَّ الذي آتاه إيَّاه.
{10} Ahadi hii ya utii aliyoiashiria Mwenyezi Mungu ni ile Ahadi ya utii ya Ridhwan, ambapo Maswahaba, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, walimpa ahadi zao za utii Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake – kwa sharti kwamba hawatakimbia wamwache. Hii ni ahadi ya utii mahususi, ambayo katika sharti yake ni kutokimbia katika vita, hata kama hakubakia miongoni mwao isipokuwa wachache tu, na hata kama watakuwa katika hali ambayo inaruhusika kukimbia. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kwamba: ''Bila ya shaka wale wanaokupa kiapo cha utii,'' uhakika wa jambo hilo ni kwamba wao ''wanampa Mwenyezi Mungu kiapo cha utii,'' na wanafunga ahadi hii naye ili kuonyesha msisitizo mkubwa ulio juu ya hilo. Akasema: ''Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao.'' Yaani, ni kana kwamba walimsalimia Mwenyezi Mungu mkononi kwa ahadi hiyo ya utii. Hayo yote ni kwa ajili ya kusisitiza na kuitia nguvu, na kuwafanya kuitekeleza, na ndiyo maana akasema: ''Kwa hivyo, avunjaye ahadi hizi'' na akakosa kutekeleza aliyomuahidi Mwenyezi Mungu, ''basi anavunja kwa kuidhuru nafsi yake." Yaani, kwa sababu ubaya wa hayo utamrudia mwenyewe, na adhabu yake itamfika mwenyewe. ''Na anayetekeleza aliyomuahadi Mwenyezi Mungu" kwa ukamilifu na kwa wingi, ''basi Mwenyezi Mungu atamlipa ujira mkubwa" ambao hakuna anayejua ukubwa wake kiasi chake isipokuwa yule aliyempa.
: 11 - 13 #
{سَيَقُولُ لَكَ الْمُخَلَّفُونَ مِنَ الْأَعْرَابِ شَغَلَتْنَا أَمْوَالُنَا وَأَهْلُونَا فَاسْتَغْفِرْ لَنَا يَقُولُونَ بِأَلْسِنَتِهِمْ مَا لَيْسَ فِي قُلُوبِهِمْ قُلْ فَمَنْ يَمْلِكُ لَكُمْ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا إِنْ أَرَادَ بِكُمْ ضَرًّا أَوْ أَرَادَ بِكُمْ نَفْعًا بَلْ كَانَ اللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا (11) بَلْ ظَنَنْتُمْ أَنْ لَنْ يَنْقَلِبَ الرَّسُولُ وَالْمُؤْمِنُونَ إِلَى أَهْلِيهِمْ أَبَدًا وَزُيِّنَ ذَلِكَ فِي قُلُوبِكُمْ وَظَنَنْتُمْ ظَنَّ السَّوْءِ وَكُنْتُمْ قَوْمًا بُورًا (12) وَمَنْ لَمْ يُؤْمِنْ بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ فَإِنَّا أَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ سَعِيرًا (13)}.
11. Watakuambia mabedui waliobaki nyuma: 'Zimetushughulisha mali zetu na ahali zetu, basi tuombee msamaha.' Wanasema kwa ndimi zao yasiyokuwamo katika nyoyo zao. Sema: 'Ni nani awezaye kukusaidieni chochote kwa Mwenyezi Mungu akitaka Yeye kuwadhuru au akitaka kuwanufaisha? Bali Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.' 12. Lakini mlidhani kwamba Mtume na Waumini hawatarudi kabisa kwa ahali zao, na mkapambiwa hayo katika nyoyo zenu, na mkadhania dhana mbaya, na mkawa watu wanaoangamia. 13. Na asiyemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi kwa hakika Sisi tumewaandalia makafiri Moto mkali.
#
{11 - 13} يذمُّ تعالى المتخلِّفين عن رسول الله في الجهاد في سبيله من الأعراب، الذين ضَعُفَ إيمانُهم وكان في قلوبهم مرضٌ وسوء ظنٍّ بالله تعالى، وأنهم سيعتذرون؛ بأنَّ أموالهم وأهليهم شغلتهم عن الخروج في سبيله، وأنَّهم طلبوا من رسول اللهِ - صلى الله عليه وسلم - أن يستغفرَ لهم؛ قال الله تعالى: {يقولون بألسنَتِهِم ما ليس في قُلوبِهِم}: فإنَّ طلَبَهم الاستغفارَ من رسول الله - صلى الله عليه وسلم - يدلُّ على ندمهم وإقرارهم على أنفسهم بالذَّنب، وأنَّهم تخلَّفوا تخلُّفاً يحتاجُ إلى توبة واستغفار؛ فلو كان هذا الذي في قلوبهم؛ لكان استغفارُ الرسول نافعاً لهم؛ لأنَّهم قد تابوا وأنابوا، ولكنَّ الذي في قلوبهم أنَّهم إنَّما تخلَّفوا لأنَّهم ظنُّوا بالله ظنَّ السَّوْء، فظنُّوا {أن لن يَنقَلِبَ الرسولُ والمؤمنون إلى أهليهم أبداً}؛ أي: أنَّهم سيُقتلون ويُستأصلون، ولم يزلْ هذا الظنُّ يُزَيَّن في قلوبهم، ويطمئنُّون إليه حتى استحكَمَ، وسببُ ذلك أمران: أحدُهما: أنَّهم كانوا {قوماً بوراً}؛ أي: هلكى لا خير فيهم؛ فلو كان فيهم خيرٌ؛ لم يكن هذا في قلوبهم. الثاني: ضَعْفُ إيمانهم ويقينهم بوعد الله ونصرِ دينِهِ وإعلاءِ كلمتِهِ، ولهذا قال: {ومن لم يؤمن بالله ورسولِهِ}؛ أي: فإنَّه كافرٌ مستحقٌّ للعقاب، {فإنَّا أعْتَدْنا للكافرين سعيراً}.
{11 - 13} Mwenyezi Mungu anawakashifu wale Mabedui waliobaki nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu katika kupigana jihadi katika njia yake, ambao imani yao ilikuwa dhaifu na ambao nyoyoni mwao walikuwa na maradhi na kumdhania Mwenyezi Mungu Mtukufu dhana mbaya, na kwamba watatumia udhuru wa kwamba: mali zao na ahali zao viliwashughulisha mbali wakashindwa kutoka kwenda katika njia yake, na kwamba walimuomba Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani zimshukie - awaombee msamaha. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: ''Wanasema kwa ndimi zao yasiyokuwamo katika nyoyo zao." Kwani ombi lao la kutafuta msamaha kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani zimshukie - linaonyesha majuto yao na kujifikiria wenyewe kwamba wana dhambi, na kwamba walisalia nyuma kusalia ambako kunahitaji toba na kutafuta msamaha. Ikiwa hayo ndiyo yaliyokuwa katika nyoyo zao, basi kuomba msamaha kwa Mtume kungelikuwa na manufaa kwao. Kwa sababu wangekuwa wametubu na wakarudi kwa Mwenyezi Mungu. Lakini yaliyomo nyoyoni mwao ni kuwa walisalia nyuma kwa sababu ya kumdhania Mwenyezi Mungu dhana mbaya. Walidhania ''kwamba Mtume na Waumini hawatarudi kabisa kwa ahali zao." Yaani, watauawa na kung'olewa kabisa, na dhana hii iliendelea kupambwa katika nyoyo zao, na wakatulizana juu yake mpaka ikawa imara ndani yao. Na sababu ya hayo ni mambo mawili: la kwanza ni kwamba walikuwa ''watu wanaoangamia" na wasiokuwa na heri ndani yao. Na ikiwa kweli kulikuwa na heri ndani yao, hili halingekuwa mioyoni mwao. La pili ni udhaifu wa imani yao na kutokuwa na yakini katika ahadi ya Mwenyezi Mungu, kuinusuru dini yake, na kuliinua juu neno lake, na ndiyo maana akasema: ''Na asiyemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake" basi yeye ni kafiri anayestahiki adhabu ''basi kwa hakika Sisi tumewaandalia makafiri Moto mkali.''
: 14 #
{وَلِلَّهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ يَغْفِرُ لِمَنْ يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَنْ يَشَاءُ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَحِيمًا (14)}
14. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Humsamehe amtakaye, na humuadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe muno, Mwingi wa kurehemu.
#
{14} أي: هو تعالى المنفردُ بملك السماواتِ والأرضِ، يتصرَّف فيهما بما يشاء من الأحكام القدريَّة والأحكام الشرعيَّة والأحكام الجزائيَّة، ولهذا ذكر حكم الجزاء المرتَّب على الأحكام الشرعيَّة، فقال: {يَغْفِرُ لِمَن يشاءُ}: وهو مَنْ قام بما أمره الله به، {ويعذِّبُ مَن يشاءُ}: ممَّن تهاونَ بأمرِ الله، {وكان الله غفوراً رحيماً}؛ أي: وصفه اللازم الذي لا ينفكُّ عنه المغفرةُ والرحمةُ، فلا يزال في جميع الأوقات يغفِرُ للمذنبين، ويتجاوزُ عن الخطَّائين، ويتقبَّل توبة التائبين، ويُنزِلُ خيرَه المدرار آناء الليل والنهار.
{14} Yaani: Yeye peke yake ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na anaviendesha atakavyo kwa hukumu zake za kimipango na ya kisheria na za kimalipo, na ndiyo maana akataja hukumu ya kimalipo inayotokana na hukumu Yake ya kisheria, akasema: ''Humsamehe amtakaye.'' Naye ni yule aliyefanya aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu, ''Na humuadhibu amtakaye'' miongoni mwa wale waliozembea katika kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu. ''Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mno, Mwingi wa kurehemu." Yaani, sifa yake isiyoachana naye ni kusamahe na kurehemu. Kwa hivyo kila wakati huwasamehe wafanyao dhambi, kuwaachia wakosefu, na anawakubalia toba wale wanaotubu, na anateremsha wema wake mwingi usiku na mchana.
: 15 #
{سَيَقُولُ الْمُخَلَّفُونَ إِذَا انْطَلَقْتُمْ إِلَى مَغَانِمَ لِتَأْخُذُوهَا ذَرُونَا نَتَّبِعْكُمْ يُرِيدُونَ أَنْ يُبَدِّلُوا كَلَامَ اللَّهِ قُلْ لَنْ تَتَّبِعُونَا كَذَلِكُمْ قَالَ اللَّهُ مِنْ قَبْلُ فَسَيَقُولُونَ بَلْ تَحْسُدُونَنَا بَلْ كَانُوا لَا يَفْقَهُونَ إِلَّا قَلِيلًا (15)}
15. Wale waliobaki nyuma watasema: 'Mtakapokwenda kuchukua ngawira, tuacheni tukufuateni!' Wanataka kuyabadili maneno ya Mwenyezi Mungu. Sema: 'Hamtatufuata kabisa. Mwenyezi Mungu alikwisha sema hivi zamani.' Hapo watasema: 'Bali nyinyi mnatuhusudu.' Sivyo, bali walikuwa hawafahamu ila kidogo.
#
{15} لما ذكر تعالى المخلَّفين وذمَّهم؛ ذكر أنَّ من عقوبتهم الدنيويَّة أنَّ الرسول - صلى الله عليه وسلم - وأصحابه إذا انطلقوا إلى غنائم لا قتال فيها ليأخذوها؛ طلبوا منهم الصحبةَ والمشاركةَ، ويقولون: {ذَرونا نَتَّبِعْكم يريدونَ}: بذلك {أن يبدِّلوا كلامَ الله}؛ حيث حَكَمَ بعقوبتهم واختصاصِ الصحابةِ المؤمنين بتلك الغنائم شرعاً وقدراً، {قل}: لهم: {لن تَتَّبِعونا كذلِكُم قال اللهُ مِن قبلُ}: إنَّكم محرومون منها بما جنيتم على أنفسكم وبما تركتم القتال أول مرة؛ {فسيقولون}: مجيبين لهذا الكلام الذي مُنِعوا به عن الخروج: {بل تحسُدوننا}: على الغنائم! هذا منتهى علمهم في هذا الموضع، ولو فَهموا رُشدَهم؛ لعلموا أنَّ حرمانهم بسبب عصيانهم، وأنَّ المعاصي لها عقوباتٌ دنيويَّةٌ ودينيَّةٌ، ولهذا قال: {بل كانوا لا يفقهونَ إلاَّ قليلاً}.
{15} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipowataja wale walioachwa nyuma na akawakashifu, akataja kuwa miongoni mwa adhabu zao za kidunia ni kwamba Mtume – rehema na Amani zimshukie – na maswahaba wake wanapotoka kwenda kuchukua ngawira bila ya kupigana vita, hao wanawaomba kwamba waandamane nao na washiriki pamoja nao, na wanasema: "Tuacheni tukufuateni!'' Kwa kufanya hivyo, “wanataka kuyabadili maneno ya Mwenyezi Mungu” ambapo alikuwa amehukumu kwamba wataadhibiwa na kwamba ngawira hizo ni za Maswahaba Waumini tu, kisheria na kulingana na mipango ya Mwenyezi Mungu. ''Sema'' ukiwaambia wao: ''Hamtatufuata kabisa. Mwenyezi Mungu alikwisha sema hivi zamani,'' kwamba hamtapewa ngawira hizo kwa sababu ya yale mliyoyafanya wenyewe na kwa kuwa mlikataa kupigana vita mara ya kwanza. ''Hapo watasema" wakiyajibu maneno haya ambayo walizuiliwa kwayo kutoka: ''Bali nyinyi mnatuhusudu" juu ya ngawira! Huu ndio upeo wa elimu yao katika jambo hili, lakini lau kuwa wangelifahamu usawa wa jambo lao hili, wangejua kwamba kunyimwa kwao huku kulikuwa kwa sababu ya uasi wao, na kwamba maasia yana adhabu za kidunia na za kidini, na ndiyo maana akasema: ''Sivyo, bali walikuwa hawafahamu ila kidogo."
: 16 - 17 #
{قُلْ لِلْمُخَلَّفِينَ مِنَ الْأَعْرَابِ سَتُدْعَوْنَ إِلَى قَوْمٍ أُولِي بَأْسٍ شَدِيدٍ تُقَاتِلُونَهُمْ أَوْ يُسْلِمُونَ فَإِنْ تُطِيعُوا يُؤْتِكُمُ اللَّهُ أَجْرًا حَسَنًا وَإِنْ تَتَوَلَّوْا كَمَا تَوَلَّيْتُمْ مِنْ قَبْلُ يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا (16) لَيْسَ عَلَى الْأَعْمَى حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْأَعْرَجِ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْمَرِيضِ حَرَجٌ وَمَنْ يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَنْ يَتَوَلَّ يُعَذِّبْهُ عَذَابًا أَلِيمًا (17)}.
16. Waambie wale walioachwa nyuma katika mabedui: 'Mtakuja itwa kwenda kupigana na watu wakali kwa vita, mpigane nao au wasalimu amri. Basi mkimtii, Mwenyezi Mungu atawapa ujira mzuri. Na mkigeuka kama mlivyogeuka kwanza, atawaadhibu kwa adhabu iliyo chungu.' 17. Kipofu hana lawama, wala kiguru hana lawama, wala mgonjwa hana lawama. Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, atamuingiza katika Mabustani ya mbinguni yapitayo mito chini yake. Na atakayegeuka upande, atamuadhibu kwa adhabu chungu.
#
{16} لما ذكر تعالى أنَّ المخلَّفين من الأعراب يتخلَّفون عن الجهاد في سبيله، ويعتذِرون بغير عذرٍ، وأنَّهم يطلبون الخروج معهم إذا لم يكن شوكةٌ ولا قتالٌ، بل لمجرَّد الغنيمة؛ قال تعالى ممتحناً لهم: {قل للمخلَّفين من الأعراب سَتُدْعَوْنَ إلى قوم أولي بأس شديدٍ}؛ أي: سيدعوكم الرسولُ ومَنْ ناب منابَه من الخلفاء الراشدين والأئمة، وهؤلاء القوم فارسٌ والرومُ ومَنْ نحا نحوَهم وأشبههم، {تقاتِلونَهم أو يُسْلِمونَ}؛ أي: إمَّا هذا وإمَّا هذا، وهذا هو الأمر الواقع؛ فإنَّهم في حال قتالهم ومقاتلتهم لأولئك الأقوام إذا كانت شدتُهم وبأسُهم معهم؛ فإنَّهم في تلك الحال لا يقبلون أن يبذُلوا الجزيةَ، بل إمَّا أنْ يدخُلوا في الإسلام، وإمَّا أن يُقاتِلوا على ما هم عليه، فلما أثخنهم المسلمونَ وضَعُفوا وذلُّوا؛ ذهب بأسُهم، فصاروا إمَّا أنْ يسلِموا وإمَّا أن يبذُلوا الجزية، {فإن تُطيعوا}: الداعي لكم إلى قتال هؤلاء، {يؤتِكُمُ الله أجراً حسناً}: وهو الأجر الذي رتَّبه الله ورسولُهُ على الجهادِ في سبيل الله، {وإن تَتَوَلَّوْا كما تولَّيْتُم من قبلُ}: عن قتال مَنْ دعاكم الرسولُ إلى قتالِهِ، {يعذِّبْكم عذاباً أليماً}. ودلَّت هذه الآية على فضيلة الخلفاء الرَّاشدين الداعين لجهادِ أهل البأس من الناس، وأنَّه تجب طاعتُهم في ذلك.
{16} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kwamba Mabedui wanajikalisha na kusalia nyuma wakakosa kwenda kufanya jihadi katika njia yake, na kwamba wanatumia udhuru usio wa kweli, na kwamba wanaomba kutoka pamoja nao ikiwa hakuna ugumu wala vita, bali kwa ajili ya ngawira tu, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu akiwajaribu: ''Waambie wale walioachwa nyuma katika mabedui: 'Mtakuja itwa kwenda kupigana na watu wakali kwa vita.'" Yaani, Mtume na wale watakaochukua nafasi yake miongoni mwa Makhalifa waongofu na Maimamu watawaita. Na watu hawa ni Mafursi na Warumi na wote wenye kufanya sawa na wao na wanaofanana nao, ''mpigane nao au wasalimu amri." Yaani, ima hili au lile. Huu ndio uhalisia wa mambo. Kwani wao katika hali ya kupigana vita na watu hao, ikiwa watakuwa ni wenye nguvu sana, basi katika hali hiyo, hawatakubali kulipa kodi (jizya). Bali ima watasilimu au watapigana vita kama walivyo. Lakini wakati Waislamu walipowadhoofisha na kuwadhalilisha, nguvu zao hizo zikaisha na ikawa ni ima wasilimu au watoe kodi. ''Basi mkimtii'' mwenye kuwaita kupigana vita dhidi ya watu hawa, ''Mwenyezi Mungu atawapa ujira mzuri'' malipo ambayo Mwenyezi Mungu na Mtume wake wameyaandika kwa sababu ya kufanya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. "Na mkigeuka kama mlivyogeuka kwanza'' mkaacha kufanya jihadi dhidi ya wale ambao Mtume aliwaita kupigana nao, ''atawaadhibu kwa adhabu iliyo chungu." Aya hii inaashiria fadhila za Makhalifa waongofu ambao wanalingania kufanya jihadi dhidi ya watu wakali mno katika vita, na kwamba ni lazima kuwatii katika hilo.
#
{17} ثم ذكر الأعذار التي يُعْذَرُ بها العبد عن الخروج إلى الجهاد، فقال: {ليس على الأعمى حَرَجٌ ولا على الأعرج حَرَجٌ ولا على المريض حَرَجٌ}؛ أي: في التخلُّف عن الجهاد لعذرِهم المانع، {ومن يطع اللهَ ورسولَه}: في امتثال أمرهما واجتناب نهيهما، {يُدْخِلْه جناتٍ تجري من تحتها الأنهار}: فيها ما تشتهيه الأنفس، وتلذُّ الأعينُ، {ومن يَتَوَلَّ}: عن طاعة الله ورسوله، {يعذِّبْه عذاباً أليماً}: فالسعادةُ كلُّها في طاعة الله، والشقاوة في معصيته ومخالفته.
{17} Kisha akataja udhuru ambao mja anaweza kukubaliwa akaacha kutoka kwenda katika jihadi, akasema: ''Kipofu hana lawama, wala kiguru hana lawama, wala mgonjwa hana lawama" ya kusalia nyuma wakaacha kufanya jihadi kwa sababu ya udhuru wao unaowazuilia. ''Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake'' katika kutii amri zao na kujiepusha na makatazo yao, ''atamuingiza katika Mabustani ya mbinguni yapitayo mito kati yake.'' Ndani yake kuna yanayotamaniwa na nafsi na kufurahisha macho. ''Na atakayegeuka upande" akaacha kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, ''atamuadhibu kwa adhabu chungu." Kwa hivyo, furaha yote iko katika kumtii Mwenyezi Mungu, na mashaka yote yako katika kumuasi na kumhalifu.
: 18 - 21 #
{لَقَدْ رَضِيَ اللَّهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَنْزَلَ السَّكِينَةَ عَلَيْهِمْ وَأَثَابَهُمْ فَتْحًا قَرِيبًا (18) وَمَغَانِمَ كَثِيرَةً يَأْخُذُونَهَا وَكَانَ اللَّهُ عَزِيزًا حَكِيمًا (19) وَعَدَكُمُ اللَّهُ مَغَانِمَ كَثِيرَةً تَأْخُذُونَهَا فَعَجَّلَ لَكُمْ هَذِهِ وَكَفَّ أَيْدِيَ النَّاسِ عَنْكُمْ وَلِتَكُونَ آيَةً لِلْمُؤْمِنِينَ وَيَهْدِيَكُمْ صِرَاطًا مُسْتَقِيمًا (20) وَأُخْرَى لَمْ تَقْدِرُوا عَلَيْهَا قَدْ أَحَاطَ اللَّهُ بِهَا وَكَانَ اللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرًا (21)}
18. Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewapa radhi Waumini walipokupa ahadi ya utii chini ya mti, na alijua yaliyomo nyoyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa kwa Ushindi wa karibu. 19. Na ngawira nyingi watakazozichukua. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima. 20. Mwenyezi Mungu anawaahidi ngawira nyingi mtakazozichukua, basi amewatangulizia hizi kwanza, na akaizuia mikono ya watu isiwafikie, na ili hayo yawe ni Ishara kwa Waumini, na akawaongoza njia iliyonyooka. 21. Na yale mengine hamwezi kuyapata bado, Mwenyezi Mungu amekwisha yazingira. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza mno wa kila kitu.
#
{18 - 19} يخبر تعالى بفضله ورحمته برضاه عن المؤمنين إذ يبايعون الرسول - صلى الله عليه وسلم - تلك المبايعة التي بيَّضت وجوههم واكتسبوا بها سعادة الدُّنيا والآخرة. وكان سبب هذه البيعة - التي يقال لها: بيعةُ الرضوان؛ لرضا الله عن المؤمنين فيها. ويقال لها: بيعةُ أهل الشجرة - أنَّ رسول الله - صلى الله عليه وسلم - لما دارَ الكلامُ بينه وبين المشركين يوم الحديبيةِ في شأن مجيئه، وأنَّه لم يجئ لقتال أحدٍ، وإنَّما جاء زائراً هذا البيت معظِّماً له، فبعث رسولُ الله - صلى الله عليه وسلم - عثمان بن عفان لمكَّة في ذلك، فجاء خبر غير صادق أنَّ عثمان قتله المشركون، فجمع رسولُ الله - صلى الله عليه وسلم - مَنْ معه مِنَ المؤمنين، وكانوا نحواً من ألف وخمسمائة، فبايعوه تحت شجرةٍ على قتال المشركين وأنْ لا يفرُّوا حتى يموتوا، فأخبر تعالى أنَّه رضيَ عن المؤمنين في تلك الحال التي هي من أكبر الطاعات وأجلِّ القُرُبات. {فعلم ما في قُلوبِهم}: من الإيمان، {فأنزلَ السكينةَ عليهم}: شكراً لهم على ما في قلوبهم، زادهم هدىً، وعلم ما في قلوبهم من الجزع من تلك الشروط التي شَرَطَها المشركون على رسولِهِ، فأنزل عليهم السكينة تثبِّتُهم، وتطمئنُّ بها قلوبهم، {وأثابهم فتحاً قريباً}: وهو فتح خيبر، لم يحضُرْه سوى أهل الحديبية، فاختصُّوا بخيبر وغنائمها جزاءً لهم وشكراً على ما فعلوه من طاعة الله تعالى والقيام بمرضاته، {ومغانم كثيرةً يأخُذونها وكانَ الله عزيزاً حكيماً}؛ أي: له العزَّة والقدرة، التي قهر بها الأشياء؛ فلو شاء؛ لانتصر من الكفَّار في كلِّ وقعة تكون بينهم وبين المؤمنين، ولكنَّه حكيمٌ يَبْتلي بعضَهم ببعض ويمتحنُ المؤمنَ بالكافر.
{18 - 19} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu fadhila na rehema zake za kuwaridhia Waumini walipokuwa wanafunga ahadi ya utii kwa Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kiapo kile cha utii kilichong'arisha nyuso zao na kwacho wakapata furaha katika dunia hii na akhera. Na ilikuwa sababu ya kiapo hiki cha utii, kilichoitwa Ahadi ya Ridhwan (ahadi ya utii ya maridhiano) kwa sababu ya Mwenyezi Mungu kuwaridhia Waumini katika hilo. Pia inaitwa Ahadi ya utii ya watu wa Mti - ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - yalipotokea mazungumzo kati yake na washirikina siku ya Hudaybiyyah kuhusu kuja kwake, na kwamba hakuja kwa ajili ya kupigana vita na mtu yeyote, bali alikuja kwa ajili ya kuizuru Nyumba hii ili kuitukuza. Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani zimshukie – akamtuma Uthman bin Affan Makka kwa ajili ya hilo, kisha ikaja habari isiyo za kweli kwamba Uthman ameuawa na washirikina. Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani zimshukie – akawakusanya pamoja wale waliokuwa pamoja naye miongoni mwa Waumini, nao walikuwa wapatao elfu moja na mia tano, na wakampa ahadi zao na utii chini ya Mti juu ya kuwapiga vita washirikina na kutokimbia mpaka wafe. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kwamba amewaridhia Waumini katika hali hiyo, ambayo ni miongoni mwa matendo makubwa zaidi ya utiifu, na matendo makubwa zaidi ya kumweka mtu karibu na Mwenyezi Mungu. ''Na alijua yaliyomo nyoyoni mwao'' kama vile imani, ''Basi akateremsha utulivu juu yao'' na kuwashukuru kwa yale yaliyokuwa nyoyoni mwao, na akawazidishia uwongofu, na alijua yaliyomo nyoyoni mwao juu ya yale masharti yale ambayo washirikina walikuwa wameweka juu ya Mtume wake, basi akateremsha utulivu juu yao ili kuwafanya imara na ili kuzituliza nyoyo zao kwa hayo, ''na akawalipa kwa Ushindi wa karibu." Nao ni ushindi wa Khaybar, ambao hawakuuhudhuria isipokuwa watu wa Hudaybiyya, basi Khaybar ikawa maalumu kwa wao tu pamoja na ngawira zake ili yawe ni malipo yao kwao na shukrani kwa yale waliyoyafanya katika kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu na kutekeleza anayoridhia. ''Na ngawira nyingi watakazozichukua. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima." Yaani, anazo nguvu na uwezo, ambavyo kwa hivyo alishinda vitu vyote. Na ikiwa alitaka, angewashinda makafiri katika kila pambano linalokuwa baina yao na Waumini. Lakini Yeye ni Mwenye hekima, na huwajaribu wao kwa wao na humpa mtihani Muumini kwa kafiri.
#
{20} {وعدكم اللهُ مغانمَ كثيرةً تأخُذونها}: وهذا يشمل كلَّ غنيمة غَنَّمها المسلمين إلى يوم القيامة، {فعجَّلَ لكم هذهِ}؛ أي: غنيمة خيبر؛ أي: فلا تحسَبوها وحدَها، بل ثمَّ شيءٌ كثيرٌ من الغنائم سيتبعها، {و} احمدوا الله إذْ {كفَّ أيدِيَ الناسِ}: القادرين على قتالكم الحريصين عليه {عنكم}: فهي نعمةٌ وتخفيفٌ عنكم، {ولتكونَ}: هذه الغنيمة {آيةً للمؤمنينَ}: يستدلُّون بها على خبر الله الصادق ووعده الحقِّ وثوابه للمؤمنين، وأنَّ الذي قدَّرها سيقدِّر غيرها، {ويهدِيَكم}: يما يُقَيِّضُ لكم من الأسباب {صراطاً مستقيماً}: من العلم والإيمان والعمل.
{20} ''Mwenyezi Mungu anakuahidini ngawira nyingi mtakazozichukua.'' Hili linajumuisha kila ngawira watakayoichukua Waislamu mpaka Siku ya Kiyama, ''basi amewatangulizia hizi kwanza.'' Yaani, ngawira za Khaybar. Kwa hivyo, msiidhanie kuwa ndiyo hiyo peke yake, bali kutakuwa na ngawira nyingi zitakazoifuata, ''na'' msifuni Mwenyezi Mungu "alipoizuia mikono ya watu" waliokuwa na uwezo wa kuwapiga vita na ambao wana hamu kubwa ya kufanya hivyo 'isikufikieni." Hiyo ilikuwa neema na kukuhafifishia "na ili hayo" ya kupata ngawira "yawe ni Ishara kwa Waumini," ili waitumie kuwa ni ushahidi juu ya habari za Mwenyezi Mungu Mkweli, ambaye ahadi yake ni ya kweli na ujira wake kwa Waumini, na kwamba Yule aliyepanga hilo atapanga mengine. ''Na akakuongozeni'' kwa atakayopitisha miongoni mwa visababu ''njia iliyonyooka'' ya elimu, Imani na matendo.
#
{21} {وأخرى}؛ أي: وعدكم أيضاً غنيمة أخرى، {لم تقدِروا عليها}: وقت هذا الخطاب، {قد أحاطَ اللهُ بها}؛ أي: هو قادر عليها وتحت تدبيره وملكه، وقد وعَدَكُموها؛ فلا بدَّ من وقوع ما وَعَدَ به؛ لكمال اقتدار الله تعالى، ولهذا قال: {وكان الله على كلِّ شيءٍ قديراً}.
{21} ''Na yale mengine;'' yaani, tena aliwaahidi ngawira nyingine, ''hamwezi kuyapata bado'' wakati walipokuwa wanaambiwa maneno haya, ''Mwenyezi Mungu amekwisha yazingira.'' Yaani, Yeye ni muweza juu yake na yako chini ya uendeshaji wake na umiliki wake, na tayari aliwaahidi hayo. Basi hakuna budi kwamba alichoahidi kitatokea; kwa sababu ya ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ndiyo maana akasema: ''Na Mwenyezi Mungu ni Muweza mno wa kila kitu."
: 22 - 23 #
{وَلَوْ قَاتَلَكُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوَلَّوُا الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يَجِدُونَ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا (22) سُنَّةَ اللَّهِ الَّتِي قَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلُ وَلَنْ تَجِدَ لِسُنَّةِ اللَّهِ تَبْدِيلًا (23)}.
22. Na lau makafiri wangelipigana nanyi, basi bila ya shaka wangeligeuza migongo, kisha wasingelipata mlinzi wala msaidizi. 23. Huo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu uliokwisha pita zamani, wala hutapata mabadiliko katika mwendo wa Mwenyezi Mungu.
#
{22} هذه بشارةٌ من الله لعباده المؤمنين بنصرهم على أعدائهم الكافرين، وأنَّهم لو قابَلوهم وقاتلوهم؛ {لَوَلَّوا الأدبار ثمَّ لا يجدونَ وليًّا}: يتولَّى أمرَهم، {ولا نصيراً}: ينصُرُهم ويعينُهم على قتالكم، بل هم مخذولونَ مغلوبونَ.
{22} Hii ni bishara itokayo kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake walioamini kwamba atawanusuru dhidi ya maadui zao makafiri, na kwamba ikiwa wangekutana nao na kupigana nao ''wangelipigana nanyi, basi bila ya shaka wangeligeuza migongo, kisha wasingelipata mlinzi'' ambaye anasimamia mambo yao, ''wala msaidizi'' ambaye atawanusuru na kuwasaidia kupigana nanyi. Bali wao ndio watakaoachwa bila kusaidiwa na washindwe kabisa.
#
{23} وهذه سنةُ اللهِ في الأمم السابقة أنَّ جندَ الله هم الغالبونَ، {ولن تَجِدَ لِسُنَّة الله تبديلاً}.
{23} Na huu ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu katika umma zilizotangulia, kwamba wanajeshi wa Mwenyezi Mungu ndio washindi, ''wala hutapata mabadiliko katika mwendo wa Mwenyezi Mungu."
: 24 - 25 #
{وَهُوَ الَّذِي كَفَّ أَيْدِيَهُمْ عَنْكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ عَنْهُمْ بِبَطْنِ مَكَّةَ مِنْ بَعْدِ أَنْ أَظْفَرَكُمْ عَلَيْهِمْ وَكَانَ اللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرًا (24) هُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوكُمْ عَنِ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَالْهَدْيَ مَعْكُوفًا أَنْ يَبْلُغَ مَحِلَّهُ وَلَوْلَا رِجَالٌ مُؤْمِنُونَ وَنِسَاءٌ مُؤْمِنَاتٌ لَمْ تَعْلَمُوهُمْ أَنْ تَطَئُوهُمْ فَتُصِيبَكُمْ مِنْهُمْ مَعَرَّةٌ بِغَيْرِ عِلْمٍ لِيُدْخِلَ اللَّهُ فِي رَحْمَتِهِ مَنْ يَشَاءُ لَوْ تَزَيَّلُوا لَعَذَّبْنَا الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا (25)}
24. Na Yeye ndiye aliyeizuia mikono yao kwenu, na mikono yenu kwao, katika bonde la Makka baada ya kuwapeni Ushindi juu yao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mno myatendayo. 25. Hao ndio waliokufuru na wakawazuia msiingie Msikiti Mtakatifu, na wakawazuilia dhabihu kufika mahala pao. Na lau si wanaume Waumini na wanawake Waumini msiowajua mkawasaga na mkaingia makosani kutokana nao bila ya kujua... Mwenyezi Mungu (amefanya haya) ili amuingize amtakaye katika rehema yake. Lau wangelitengana, bila ya shaka tungeliwaadhibu wale waliokufuru kwa adhabu chungu.
#
{24} يقول تعالى ممتنًّا على عباده بالعافية من شرِّ الكفار ومن قتالهم، فقال: {وهو الذي كَفَّ أيْدِيَهم}؛ أي: أهل مكة {عنكم وأيدِيَكُم عنهم ببطنِ مكَّة من بعدِ أن أظْفَرَكُم عليهم}؛ أي: من بعد ما قدرتُم عليهم وصاروا تحت ولايتكم بلا عقدٍ ولا عهدٍ، وهم نحو ثمانين رجلاً، انحدروا على المسلمين ليصيبوا منهم غِرَّةً، فوجدوا المسلمين منتبهين، فأمسكوهم، فتركوهم ولم يقتُلوهم؛ رحمةً من الله بالمؤمنين إذْ لم يقتُلوهم، {وكان الله بما تعملون بصيراً}: فيجازي كلَّ عامل بعملِهِ، ويدبِّركم أيها المؤمنون بتدبيره الحسن.
{24} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, akiwajulisha waja wake neema zake za kuwaweka salama kutokana na shari ya makafiri na kupigana vita nao, akasema: ''Na Yeye ndiye aliyeizuia mikono yao kwenu.'' Yaani, watu wa Makka ''na mikono yenu kwao, katika bonde la Makka baada ya kukupeni Ushindi juu yao" wakawa chini ya mamlaka yenu bila ya mkataba wala agano, nao walikuwa wanaume wapatao themanini, ambao waliwashukia Waislamu ili wawashambulie bila ya wao kujua, lakini wakawakuta Waislamu tayari wako macho, na wakawakamata sawasawa. Kwa hivyo, wakawaacha na hawakuwaua kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu juu ya Waumini, ambapo hawakuwaua, ''Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mno myatendayo.'' Basi atamlipa kila mtendaji matendo kwa matendo yake, na anawaendesha enyi Waumini kwa uendeshaji wake mzuri.
#
{25} ثم ذكر تعالى الأمور المهيِّجة على قتال المشركين، وهي كفرُهم بالله ورسولِهِ، وصدُّهم رسولَ الله ومَنْ معه من المؤمنين أنْ يأتوا للبيت الحرام زائرين معظِّمين له بالحجِّ والعمرة، وهم الذين أيضاً صدُّوا {الهديَ معكوفاً}؛ أي: محبوساً، {أن يبلغَ مَحِلَّه}: وهو مَحِلُّ ذبحِهِ في مكة ، حيث تذبح هدايا العمرة، فمنعوه من الوصول إليه ظلماً وعدواناً. وكلُّ هذه أمورٌ موجبةٌ وداعيةٌ إلى قتالهم، ولكن ثمَّ مانعٌ، وهو وجودُ رجال ونساء من أهل الإيمان بين أظهر المشركين، وليسوا بمتميِّزين بمحلةٍ أو مكانٍ يمكن أن لا ينالَهم أذى؛ فلولا هؤلاء الرجال المؤمنون والنساء المؤمنات الذين لا يعلمهم المسلمون {أن تطؤوهم}؛ أي: خشية أن تطؤوهم، {فتصيبَكم منهم مَعَرَّةٌ بغير علم}: والمعرَّةُ ما يدخل تحت قتالهم من نيلِهِم بالأذى والمكروه، وفائدةٌ أخريَّةٌ، وهو أنه لِيُدْخِلَ {في رحمته مَن يشاءُ}: فَيَمُنَّ عليهم بالإيمان بعد الكفر، وبالهدى بعد الضلال، فيمنعكم من قتالهم لهذا السبب، {لو تَزَيَّلوا}؛ أي: لو زالوا من بين أظهرهم، {لعذَّبْنا الذين كَفَروا منهم عذاباً أليماً}: بأن نبيحَ لكم قتالَهم، ونأذنَ فيه، وننصرَكم عليهم.
{25} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja mambo yanayochochea kupigana dhidi ya washirikina, ambayo ni kumkufuru kwao Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kumzuilia kwao Mtume wa Mwenyezi Mungu na Waumini walio pamoja naye kuingia kwenye Nyumba tukufu wakiwa ni wageni na kwa ajili ya kuipa taadhima kwa kuhiji na kufanya Umra, na hao hao pia ndio waliowazuilia ''dhabihu kufika mahala pao" pa kuchinjiwa huko Makka, kwa njia ya dhuluma na uadui. Yote hayo ni mambo ambayo yanasababisha na kuwahimiza watu kupigana vita nao, lakini kuna kikwazo, ambacho ni kuwepo wanaume na wanawake waumini miongoni mwa washirikina, na wao hawakujitenga mbali nao katika sehemu ambayo hawawezi kutowadhuru. Lau si hawa Waumini wanaume na Waumini wanawake ambao Waislamu hawawajui kwa kuwa ilihofiwa huenda ''mkawasaga na mkaingia makosani kutokana nao bila ya kujua." Na pia katika hilo kuna faida ya kiakhera, ambayo amuingize "amtakaye katika rehema yake.'' Ili awatajie neema yake ya kuwapa imani baada ya kuwa kwao makafiri, na uwongofu baada ya upotofu, na hivyo akawazuilia kupigana vita nao kwa sababu hizo. ''Lau wangelitengana'' wakawa mbali na washirikina hao ''bila ya shaka tungeliwaadhibu wale waliokufuru miongoni mwao kwa adhabu chungu," kwa kuwaruhusu kupigana vita nao, na kuwanusuru dhidi yao.
: 26 #
{إِذْ جَعَلَ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي قُلُوبِهِمُ الْحَمِيَّةَ حَمِيَّةَ الْجَاهِلِيَّةِ فَأَنْزَلَ اللَّهُ سَكِينَتَهُ عَلَى رَسُولِهِ وَعَلَى الْمُؤْمِنِينَ وَأَلْزَمَهُمْ كَلِمَةَ التَّقْوَى وَكَانُوا أَحَقَّ بِهَا وَأَهْلَهَا وَكَانَ اللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا (26)}
26. Pale wale waliokufuru walipotia katika nyoyo zao hasira, hasira za kijinga, Mwenyezi Mungu aliteremsha utulivu juu ya Mtume wake na juu ya Waumini, na akawalazimisha neno la kumcha Mungu. Na wao walikuwa ndio wenye haki nalo na wenye kustahili. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua mno kila kitu.
#
{26} يقول تعالى: {إذْ جعلَ الذين كفروا في قلوبِهِمْ الحميَّةَ حميَّةَ الجاهليَّةِ}: حيث أنفوا من كتابة «بسم الله الرحمن الرحيم»، وأنفوا من دخول رسول الله - صلى الله عليه وسلم - والمؤمنين إليهم في تلك السنة ؛ لئلاَّ يقولَ الناس: دَخَلوا مكَّة قاهرين لقريش! وهذه الأمور ونحوها من أمور الجاهلية لم تزلْ في قلوبِهِم حتَّى أوجبتْ لهم ما أوجبتْ من كثيرٍ من المعاصي، {فأنزل الله سكينَتَه على رسوله وعلى المؤمنين}: فلم يحمِلْهم الغضب على مقابلة المشركين بما قابلوهم به بل صبروا لحكم الله والتزموا الشروط التي فيها تعظيم حرمات الله، ولو كانت ما كانت، ولم يبالوا بقول القائلين ولا لوم اللائمين، {وألزَمَهم كلمةَ التَّقوى}، وهي لا إله إلاَّ الله وحقوقها، ألزمهم القيام بها، فالتزموها وقاموا بها، {وكانوا أحقَّ بها}: من غيرهم، {و} كانوا {أهلَها}: الذين استأهلوها؛ لما يعلمُ الله عندَهم وفي قلوبهم من الخير، ولهذا قال: {وكان الله بكلِّ شيءٍ عليماً}.
{26} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: ''Pale wale waliokufuru walipotia katika nyoyo zao hasira, hasira za kijinga'' ambapo walipinga kuandika “Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu” katika makataba, na wakamkataza Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na Waumini kuingia Makka katika mwaka huo; ili watu wasije wakasema: 'Waliingia Makka huku wamewashinda Maquraishi!' Lakini mambo haya na mambo yanayofanana na hayo ni mambo ya zama za Ujinga (za kabla ya Uislamu), yaliyosalia katika nyoyo zao mpaka yakawasababishia kufanya yale yaliyoyafanya katika miongoni mwa madhambi mengi. ''Basi Mwenyezi Mungu akateremsha utulivu juu ya Mtume wake na juu ya Waumini,'' kwa hivyo hawakuchochewa na ghadhabu ili wakabiliane na washirikina kwa yale waliyowafanyia, bali walikuwa na subira juu ya hukumu ya Mwenyezi Mungu na wakashikamana na masharti hayo ambayo ndani yake kulikuwa na kuyatukuza matakatifu ya Mwenyezi Mungu, hata kama nini kingetokea, na wala hawakujali maneno ya wasemao wala lawama za wale wanaolaumu, ''na akawalazimisha neno la kumcha Mungu." Yaani, hapana mungu ila Mwenyezi Mungu na haki zake. Nao walikuwa wamestahiki zaidi kuliko wengine. "Na wao walikuwa ndio wenye haki nalo na wenye kustahili." Kwa sababu ya yale ambayo Mwenyezi Mungu alijua kwamba wanayo, na heri iliyo katika nyoyo zao, na ndiyo maana akasema: ''Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua mno kila kitu."
: 27 - 28 #
{لَقَدْ صَدَقَ اللَّهُ رَسُولَهُ الرُّؤْيَا بِالْحَقِّ لَتَدْخُلُنَّ الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ إِنْ شَاءَ اللَّهُ آمِنِينَ مُحَلِّقِينَ رُءُوسَكُمْ وَمُقَصِّرِينَ لَا تَخَافُونَ فَعَلِمَ مَا لَمْ تَعْلَمُوا فَجَعَلَ مِنْ دُونِ ذَلِكَ فَتْحًا قَرِيبًا (27) هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَكَفَى بِاللَّهِ شَهِيدًا (28)}
27. Hakika Mwenyezi Mungu amemtimizia Mtume wake ndoto ya haki. Bila ya shaka nyinyi mtauingia Msikiti Mtakatifu, Inshallah (Mwenyezi Mungu akipenda), kwa amani, na hali mmenyoa vichwa vyenu na mmepunguza nywele. Hamtakuwa na hofu. Yeye anajua msiyoyajua. Basi atawapea kabla ya haya Ushindi karibuni. 28. Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki, ili aipe ushindi juu ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi.
#
{27} يقول تعالى: {لقد صدق اللهُ رسولَه الرُّؤيا بالحقِّ}: وذلك أنَّ رسول الله - صلى الله عليه وسلم - رأى في المدينة رؤيا أخبر بها أصحابه؛ أنَّهم سيدخلون مكَّة ويطوفون بالبيت، فلما جرى يوم الحديبية ما جرى، ورجعوا من غير دخول لمكَّة؛ كَثُرَ في ذلك الكلام منهم، حتى إنهم قالوا ذلك لرسول الله - صلى الله عليه وسلم -: ألم تُخْبِرْنا أنَّا سنأتي البيت ونطوف به؟! فقال: «أخبرتكم أنَّه العام؟!»، قالوا: لا، قال: «فإنَّكم ستأتونَه وتطوفونَ به». قال الله تعالى هنا: {لقد صَدَقَ الله رسولَه الرؤيا بالحقِّ}؛ أي: لا بدَّ من وقوعها وصِدْقها، ولا يقدُح في ذلك تأخُّر تأويلها، {لَتَدْخُلُنَّ المسجدَ الحرام إن شاء اللهُ آمنينَ محلِّقينَ رؤوسَكم ومقصِّرين}؛ أي: في هذه الحال المقتضية لتعظيم هذا البيت الحرام وأدائكم للنُّسك وتكميلِهِ بالحلق والتَّقصير وعدم الخوفِ. {فعلم}: من المصلحة والمنافع {ما لم تَعْلَموا فجَعَلَ من دونِ ذلك}: الدخول بتلك الصفة {فتحاً قريباً}.
{27} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: ''Hakika Mwenyezi Mungu amemtimizia Mtume wake ndoto ya haki.'' Haya ni kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani zimshukie - aliona njozi huko Madina akawaambia maswahaba zake kwamba wataingia Makka na kuizunguka Al-Kaaba, na yalipotokea yaliyotokea siku ya Hudaybiyya, na wakarudi bila ya kuingia Makka, wengi wao walisema maneno kuhusu jambo hili, hadi wakamwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na Amanza Mwenyezi Mungu zimshukie: "Je, hukutuambia kwamba tutakuja kwenye Nyumba na kuizunguka?" Akasema: “Niliwaambia ni mwaka huo?” Wakasema: "Hapana." Akasema: "Hakika mtaiingia na mtaizunguka." Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema hapa: ''Hakika Mwenyezi Mungu amemtimizia Mtume wake ndoto ya haki.'' Yaani, lazima itatokea na iwe ya kweli, na wala kuchelewa kwake kufika hakuwezi kuitia dosari. ''Bila ya shaka nyinyi mtauingia Msikiti Mtakatifu, Inshallah (Mwenyezi Mungu akipenda), kwa amani, na hali mmenyoa vichwa vyenu na mmepunguza nywele." Yaani, katika hali hii ambayo inawahitaji kuiheshimu Nyumba hii Takatifu na kufanyia kwenu hapo ibada mbalimbali na kuzikamilisha kwa kunyoa, kupunguza nywele zenu, na kutokuwa na hofu. ''Yeye anajua" masilahi na manufaa ''msiyoyajua. Basi atawapa kabla ya hayo'' ya kuingia kwa namna hiyo “Ushindi karibuni.”
#
{28} ولما كانت هذه الواقعة مما تشوَّشت بها قلوبُ بعض المؤمنين، وخفيتْ عليهم حكمتُها، فبيَّن تعالى حكمتَها ومنفعتَها، وهكذا سائر أحكامه الشرعيَّة؛ فإنَّها كلَّها هدى ورحمةٌ، أخبر بحكم عام، فقال: {هو الذي أرسل رسولَه بالهُدى}: الذي هو العلمُ النافعُ، الذي يهدي من الضلالة، ويبيِّن طرقَ الخير والشرِّ، {ودين الحقِّ}؛ أي: الدين الموصوف بالحقِّ، وهو العدل والإحسان والرحمة، وهو كلُّ عمل صالح مزكٍّ للقلوب مطهِّرٍ للنفوس مربٍّ للأخلاق معلٍ للأقدار، {ليظهِرَه}: بما بعثَه الله به {على الدِّين كلِّه}: بالحجَّة والبرهان، ويكون داعياً لإخضاعهم بالسيف والسنان.
{28} Na kwa kuwa tukio hili lilikuwa ni katika mambo ya yaliyoleta mkanganyiko katika nyoyo za baadhi ya Waumini, na hekima yake ikafichikana kwao, Mwenyezi Mungu Mtukufu akaeleza hekima yake na manufaa yake, na kadhalika hukumu zake zote za kisheria. Kwani zote ni uwongofu na rehema, akajulisha hayo kwa hukumu ya jumla, akisema: ''Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uwongofu'' ambayo ni elimu yenye manufaa, yenye kuongoa kutoka kwenye upotofu na kubainisha njia za heri na shari. ''Na Dini ya Haki'' ambayo ni uadilifu, ihsani, na rehema, na ni kila tendo jema linalotakasa nyoyo, linalosafisha nafsi, linalolea maadili mazuri, linalonyanyua vyeo, ''ili aipe ushindi'' kwa yale aliyomtuma nayo Mwenyezi Mungu "juu ya dini zote" kwa hoja na ushahidi, na iwe sababu ya kutii kwao kwa upanga na mkuki.
: 29 #
{مُحَمَّدٌ رَسُولُ اللَّهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِنَ اللَّهِ وَرِضْوَانًا سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِمْ مِنْ أَثَرِ السُّجُودِ ذَلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنْجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَى عَلَى سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْهُمْ مَغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا (29)}
29. Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na wale walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kutokana na athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea uliotoa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa.
#
{29} يخبر تعالى عن رسوله محمد - صلى الله عليه وسلم - وأصحابه من المهاجرين والأنصار؛ أنَّهم بأكمل الصفات وأجلِّ الأحوال، وأنَّهم {أشداءُ على الكفَّارِ}؛ أي: جادِّين ومجتهدين في عداوتهم، وساعين في ذلك بغاية جهدهم، فلم يروا منهم إلاَّ الغلظةَ والشدَّةَ؛ فلذلك ذلَّ أعداؤُهم لهم وانكسروا وقهرهم المسلمون، {رحماءُ بينَهم}؛ أي: متحابُّون متراحمون متعاطفون كالجسد الواحد، يحبُّ أحدُهم لأخيه ما يحبُّ لنفسه، هذه معاملتُهم مع الخلق، وأمَّا معاملتُهم مع الخالق؛ فتراهم {رُكَّعاً سجداً}؛ أي: وصفهم كثرة الصلاة التي أجلُّ أركانها الركوع والسجود، {يبتغونَ}: بتلك العبادة {فضلاً من الله ورضواناً}؛ أي: هذا مقصودهم، بلوغُ رضا ربِّهم والوصول إلى ثوابِهِ {سيماهم في وجوهِهِم من أثرِ السُّجودِ}؛ أي: قد أثَّرت العبادة مِنْ كثرتِها وحسنِها في وجوههم حتى استنارتْ، لمَّا استنارت بالصلاة بواطنهم؛ استنارتْ ظواهِرُهم. {ذلك}: المذكور {مَثَلُهُم في التَّوراةِ}؛ أي: هذا وصفُهم الذي وصَفَهم الله به مذكورٌ بالتوراة هكذا. وأما {مثلهم في الإنجيل}؛ فإنَّهم موصوفون بوصف آخر، وأنَّهم في كمالهم وتعاونهم {كزرع أخْرَجَ شطأه فآزره}؛ أي: أخرج فراخه فوازرتْه فراخُهُ في الشباب والاستواء، {فاستغلظَ}: ذلك الزرع؛ أي: قوي وغلظ، {فاستوى على سوقِهِ}: جمع ساق، {يعجِبُ الزُّرَّاعَ}: من كماله واستوائه وحسنه واعتداله، كذلك الصحابة رضي الله عنهم هم كالزرع في نفعهم للخلق واحتياج الناس إليهم، فقوَّة إيمانهم وأعمالهم بمنزلة قوَّة عروق الزرع وسوقِهِ، وكون الصغير والمتأخِّر إسلامه قد لَحِقَ الكبير السابق، ووازره وعاونه على ما هو عليه من إقامة دينِ الله والدعوةِ إليه، كالزرع الذي أخْرَجَ شَطأه فآزره فاستغلظ، ولهذا قال: {لِيَغيظَ بهم الكفارَ}: حين يَرَوْنَ اجتماعهم وشدَّتهم على دينهم، وحين يتصادمون هم وهم في معارك النِّزال ومعامع القتال، {وَعَدَ الله الذين آمنوا وعَمِلوا الصالحات منهم مغفرةً وأجراً عظيماً}: فالصحابة رضي الله عنهم، الذين جمعوا بين الإيمان والعمل الصالح، قد جمع الله لهم بين المغفرةِ التي من لوازمها وقايةُ شرور الدُّنيا والآخرة والأجر العظيم في الدنيا والآخرة.
{29} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu Mtume Wake Muhammad- rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na maswahaba zake Wahajiri na Ansari, kwamba wana sifa kamilifu zaidi na hali tukufu zaidi, na kwamba wao “wana nguvu mbele ya makafiri” na walijaribu kufanya hivyo kwa juhudi zao kubwa zaidi, na hawakuona chochote kutoka kwao isipokuwa ugumu na ukali. Basi ndiyo maana maadui zao wakadhalilika, wakavunjika, na Waislamu wakawashinda vikali. ''Na wanahurumiana wao kwa wao.'' Yaani, wanapendana, wanahurumiana, na wanafanyiana kama mwili mmoja. Kila mmoja wao anamtakia mwenzake anachojitakia. Na hivi ndivyo wanavyoamiliana na viumbe. Ama kuamiliana kwao na Muumba, basi utawaona ''wakiinama mno na kusujudu zaidi.'' Yaani, wanasifika kwa sifa ya kuswali kwa wingi ambayo nguzo zake kubwa zaidi ni kurukuu na kusujudu. ''Wakitafuta'' kwa ibada hizo, ''fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu'' na kupata ujira wake. ''Alama zao zi katika nyuso zao, kutokana na athari ya kusujudu.'' Yaani, wingi na uzuri wa ibada zao uliathiri katika nyuso zao mpaka zikang'aa. Na pale ndani yao ilipong'aa kwa sababu ya swala, nje yao pia ikang'aa. ''Huu'' uliotajwa ''ndio mfano wao katika Taurati'' na ndizo sifa zao ambazo Mwenyezi Mungu aliwaelezea kwazo humo. Na ama "mfano wao katika Injili" humo wameelezewa kwa sifa zingine, na kwamba katika ukamilifu wao na ushirikiano wao ni “kama mmea uliotoa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima" kwa sababu ya ukamilifu wake, ukomavu wake, uzuri wake, na kunyooka kwake. Basi vivyo hivyo ndivyo walivyokuwa maswahaba - radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao - kama mmea katika manufaa yao kwa viumbe na haja ya watu juu yao. Kwa hivyo nguvu ya imani yao na matendo yao ni kama nguvu ya mizizi ya mmea na shina lake, na kwamba kijana mdogo na yule aliyechelewa kusilimu aliwafikia aliyetangulia, akamsaidia katika yale ayafanyayo katika kusimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu na kuilingania kama mmea uliotoa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu na ukawa mnene. Ndiyo maana akasema: "ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri" pindi waonapoona kuwa kwao pamoja na bidii yao kubwa juu ya Dini yao, na wakati wanapogongana nao katika vita vikali mno. "Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa." Kwa hivyo, maswahaba - Mwenyezi Mungu awawie radhi - waliokusanya imani na vitendo vizuri, Mwenyezi Mungu aliwakusanyia maghufira, ambayo katika mambo yanayofungamana nayo ni kukingwa mbali na shari za duniani na Akhera, na malipo makubwa katika dunia na akhera.
Hebu tusimulie kisa cha Al-Hudaybiyya kwa ukamilifu wake, kama alivyosimulia Imam Shams Ad-Din Ibn al-Qayyim katika “Al-Hadyu An-Nabawi (Mwongozo wa Mtume).” Kisa hiki kinasaidia katika kuifahamu Sura hii, na alizungumza kuhusu maana zake na siri zake. Yeye - Mwenyezi Mungu amrehemu - alisema: Sura ya kisa cha Al-Hudaybiyyah: Nafi' ilisema: Kisa hiki kilitokea mwaka wa sita katika mwezi wa Dhul-Qa’dah. Hii ndiyo kauli sahihi, na ndiyo kauli ya Az-Zuhri, Qatada, Musa bin Uqba, Muhammad bin Ishaq na wengineo. Naye Hisham bin Urwa alisema kutoka kwa baba yake: 'Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani zimshukie - alitoka kwenda Al-Hudaybiyya katika mwezi wa Ramadhani, na tukio lenyewe lilikuwa katika mwezi wa Shawwal.' Lakini huu ni mtazamo na dhana isiyokuwa sahihi. Vita vya Al-Fath (Utekaji wa Makka) ndivyo vilikuwa katika mwezi wa Ramadhani. Abu Al-Aswad alisema kutoka kwa Urwa: 'Kilikuwa kisa hiki katika mwezi wa Dhul-Qa’dah kulingana na maoni sahihi.' Na katika Sahih mbili, imesimuliwa kutoka kwa Anas kwamba Nabii - rehema na amani zimshukie - alifanya Umra nne katika maisha yake, na zote hizo zilikuwa katika mwezi wa Dhul-Qa’dah.' na akataja Umra hii ya Al-Hudaybiyya miongoni mwake. Alikuwa pamoja na watu elfu moja mia tano. Hivi ndivyo ilivyo katika Sahih mbili kutoka kwa Jabir (bin Abdillah). Na pia imesimuliwa kutoka kwake katika Sahih hizi kwamba walikuwa elfu moja na mia nne. Na katika Sahih zote mbili imesimuliwa kutoka kwa Abdullah bin Abi Awfa kuwa: 'Tulikuwa elfu moja na mia tatu.' Qatada alisema: 'Nilimwambia Said bin Al-Musayyab: Je, watu walioshuhudia Kiapo cha Utii kwa Ar-Ridhwan walikuwa wangapi?' Akasema: Elfu moja na mia tano.' Alisema: Nikasema: 'Hakika Jabir bin Abdullah kuwa alisema kwamba walikuwa elfu moja na mia nne?' Akasema: 'Mwenyezi Mungu amrehemu. Yeye hakulielewa hilo vyema. Yeye mwenyewe alinisimulia kwamba walikuwa elfu moja na mia tano.' Nikasema: Kauli zote mbili zilisimuliwa kisahihi kutoka kwa Jabir, na ikathibiti kutoka kwake pia kwamba walichinja ngamia sabini mwaka wa Hudaybiyyah, ngamia mmoja kwa niaba ya watu saba.' Akaambiwa: 'Mlikuwa wangapi?' Akasema: 'Elfu moja na mia nne pamoja na wapanda farasi wetu na wenye kwenda kwa miguu.' Na moyo wangu unaelekea zaidi kwenye kauli hii. Na hii ni kauli ya Al-Baraa bin Azib, Maqil bin Yasaar, na Salamah bin Al-Akwa’ katika riwaya sahihi zaidi kati ya hizo mbili, na ni kauli ya Al-Musayyab bin Hazn. Shu'bah alisema kutoka kwa Qatada kutoka kwa Said bin Al-Musayyab kutoka kwa baba yake: Tulikuwa pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani ziwe juu yake - chini ya Mti ilhali tuko watu elfu moja na mia nne, na atakayesema: 'Walikuwa mia saba' atakuwa amekosea waziwazi! Na hoja yake ni kwamba walichinja ngamia sabini siku hiyo, na ngamia mmoja alikuwa akichinjwa kwa niaba ya watu saba na kumi! Lakini hili halionyeshi alichosema mzungumzaji huyu. Kwani imethibiti kwamba katika vita hivi, ngamia mmoja walikuwa akichinjwa kwa niaba ya watu saba. Basi kama ngamia sabini hao walikuwa kwa niaba yao wote, basi wangekuwa watu mia nne na tisini. Na akasema mwisho wa hadithi yake hii kwamba walikuwa elfu moja na mia nne. Mlango: Walipokuwa Dhul-Hulaifah, Mtume wa Mwenyezi - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – akamvalisha makoja mnyama wake anayempeleka kama zawadi ya Al-Kaba, akawatia alama na akaweka nia (Ihram) ya kufanya 'Umra, kisha akamtuma jesusi wake kutoka kwa kabila la Khuza’a ili amletee habari kuhusu Maquraishi, mpaka alipokuwa karibu na mji wa 'Asfan, jesusi wake huyo akamjia. Akasema: 'Hakika nimemuacha Ka'b bin Luayy hali ya kuwa wamekukusanyia Wahabeshi na makundi mengi ya watu, na wako tayari kupigana nawe vita na kukuzuia kuifikia Nyumba.' Basi Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – akashauriana na maswahaba wake [na akasema]: "Je, mnaona kwamba tuelekee kwa dhuria za hawa waliowasaidia ili tuwashambulie? Ikiwa watakaa, basi hawatakaa isipokuwa wakiwa na wasiwasi na huzuni. Na ikiwa wataokoka, basi hilo litakuwa shingo alilolikata Mwenyezi Mungu. Au mnaona kwamba tuelekee kwenye Nyumba, na atakayetuzuia kuifikia, tutapigana naye?" Abu Bakr akasema: 'Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanajua zaidi. Hakika hatukuja kufanya Umra tu, wala hatukuja kupigana vita na yeyote. Lakini, mwenye kutuzuilia kuifikia Nyumba, tutampiga vita.' Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – akasema: “Basi nendeni!” Kwa hivyo, wakaenda, mpaka walipokuwa mahali fulani njiani, Nabii -rehema na amani zimshukie - akasema: “Hakika Khalid bin Al-Walid yuko huko Al-Ghumaim pamoja na kikosi cha mbele cha wapanda farasi wa Maquraishi. Kwa hivyo shika mkono wa kulia." Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, Khalid hakuhisi uwepo wao mpaka alipojikuta katikati ya jeshi la Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwa hivyo akaanza kukimbia kama akienda kuwaonya Maquraishi. Nabii – rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – aliendelea kwenda mpaka akafikia kwenye njia ya milimani ambayo anaweza kuwashukia kutokea hapo, ngamia wake akapiga magoti, kwa hivyo watu wakasema: 'Endelea kwenda! Endelea kwenda!' Lakini yeye akasisitiza kuendelea kupiga magoti. Kwa hivyo, watu wakasema: 'Al-Qaswa’a amekataa kuendelea na mwendo. Al-Qaswa’a amekataa kuendelea na mwendo.' Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – akasema: “Al-Qaswa’a hajakataa kuendelea na mwendo, na wala hiyo si tabia yake. Lakini amezuiliwa na Yule aliyemzuia tembo." Kisha akasema: “Ninaapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mkononi mwake. Hawataniomba mpango wowote ambao kwa huo wanatukuza matakatifu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa nitawapa." Kisha akamtikisa ili asimame, kwa hivyo akanyanyuka juu pamoja naye, kisha akaenda moja kwa moja, mpaka akashukia sehemu ya mwisho zaidi ya Al-Hudaybiyya yenye maji kidogo tu, na wakawa wanasaidia kuyanywa, mpaka hawakukaa muda isipokuwa walikuwa tayari wameshayamaliza yote. Kwa hivyo, wakamlalamikia Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwamba walikuwa na kiu. Basi akachukua mshale kutoka kwenye podo lake, kisha akawaamuru kuuweka ndani yake. Akasema: "Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu! Yaliendelea kuwabubujikia wakikata kiu mpaka wakaondoka hapo." Maquraishi waliingiwa na hofu kubwa kwa sababu ya kumuona amewafikia, basi Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – akapenda kwamba awatumie mwanamume kutoka kwa maswahaba zake, kwa hivyo akamwita 'Umar bin Al-Khattab ili amtume huko. Akasema: 'Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Sina mtu yeyote kutoka kwa Banu Ka'b huko Makka ambaye atanighadhibikia ikiwa nitadhuriwa. Basi mtume 'Uthman bin Affan. Kwani watu wa ukoo wake wako huko, naye atafikisha vizuri sana hayo unayoyataka." Kwa hivyo, Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani zimshukie – akamwita Uthman bin Affan, na akamtuma kwa Maquraishi. Akasema: “Waambie kwamba sisi hatukuja kwa ajili ya kupigana. [Lakini] tumekuja kwa ajili ya Umra, na waite kwenye Uislamu.’” Alimuamuru pia kwamba awaendee wanaume Waumini na wanaume Waumini huko Makka, na aingie waliko na awape bishara ya ushindi wa Waislamu juu ya Makka, na awaambie kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ataidhihirisha Dini yake huko Makka ili imani isifiche humo. Basi Uthman akaondoka na akawapita Maquraishi huko Baldah, wakasema: Unakwenda wapi? Akasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu – Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – amenituma nikulinganieni kwa Mwenyezi Mungu na kwenye Uislamu, na niwaambie kwamba hatukuja kupigana vita bali tumekuja kufanya Umra. Wakasema: Tumesikia unayoyasema. Basi nenda utimize haja yako. Basi Aban bin Said bin Al-Aas akasimama karibu naye, akamkaribisha, na akamtandikia farasi wake. Kisha akambeba Uthman juu ya farasi wake na akampa ulinzi mpaka alipofika naye Makka. Waislamu wakasema kabla ya Uthman kurudi: Uthman alifika kwenye Nyumba kabla yetu na akaizunguka. Mtume wa Mwenyezi Mungu - Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - akasema: “Sidhani kwamba aliizunguka Al-Kaaba na sisi tumezingirwa.” Wakasema: Ni nini kitakachomzuia, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, na hali ameifikia? Akasema: “Ni imani yangu kwamba hataizunguka Al-Kaaba mpaka tuizunguke pamoja naye.” Basi Waislamu wakachanganyikana na washirikina katika suala la suluhu ya amani, na mwanamume mmoja wa kundi moja katika makundi hayo akampiga mshale mwanamume mmoja kutoka katika kundi hilo jingine, kwa hivyo vita vikatokea, wakarushiana mishale na mawe, na makundi yote mawili yakapiga kelele, na kila moja ya makundi hayo yakapiga kelele, na kila kundi katika makundi hayo mawili likachukua watu wa kutoka katika kikundi kile kingine kama mateka, na Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – akafikiwa na habari kwamba Uthman ameuawa. Kwa hivyo akaitisha kwamba kiapo cha utii kifanywe kwa ajili yake. Basi Waislamu wakainuka haraka haraka wakamwendea Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – hali ya kuwa yuko chini ya Mti, kwa hivyo wakampa kiapo cha utii kwamba hawatakimbia vita. Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake – akashika mkono wake mwenyewe na akasema: “Huu ni kwa niaba ya Uthman.” Ahadi hiyo ya utii ilipokamilika, Uthman akarudi, na Waislamu wakamwambia: 'Je, umepata raha ewe Abu Abdullah kuizunguka Al-Kaaba?' Akasema: 'Ni ovu mno mlilonidhania. Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mkononi mwake, lau ningelikaa huko kwa muda wa mwaka mmoja ilhali Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – bado yuko Al-Hudaybiyyah, nisingeliizunguka mpaka Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake aizunguke kwanza. Hakika Maquraishi waliniita kuzunguka Al-Kaaba, lakini nikakataa.' Waislamu wakasema: 'Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – alikuwa ndiye mwenye kujua zaidi kati yetu kuhusu Mwenyezi Mungu na mwenye dhana nzuri zaidi kutuliko sisi sote.' Naye Umar alikuwa ameushika mkono wa Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie- ili ampe kiapo cha utii chini ya Mti, basi Waislamu wote wakampa kiapo cha utii isipokuwa Al-Jadd bin Qays, naye Maqil bin Yasaar alikuwa ameshikilia tawi lake ameliinua juu liwe mbali na Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake. Na alikuwa wa kwanza kumpa kiapo cha utii ni Abu Sinaan Al-Asadi, naye Salama bin Al-Akwa akampa kiapo cha utii mara tatu: kabla ya watu wote, na katikati yao, na wa mwisho wao. Huku wakiwa hivyo, tazama, akawajia Budail bin Warqa' Al-Khuza'i na kundi la watu kutoka kwa kabila la Khuza'a, nao walikuwa miongoni mwa watu wa Tihamah, waliokuwa wakimpa ushauri mzuri Mtume wa Mwenyezi Mungu-– rehema na amani ziwe juu yake. Akasema: 'Hakika nilimuacha Ka'b bin Luay na Aamir bin Luay huku wameshukia kwenye maji ya Al-Hudaybiyya pamoja na ngamia wa kike waliyozaa hivi karibuni na ambao wanawatunza watoto wao nao bila ya shaka wameazimia kupigana vita dhidi yako na kukuzuia kuifikia na Nyumba.' Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – akasema: “Hakika, sisi hatukuja kwa ajili ya kupigana na mtu yeyote, bali tulikuja kufanya Umra, na hakika Maquraishi walishachoshwa na vita na kuwadhuru sana. Wakitaka nitawarefushia muda wa amani na wasizuilie baina yangu na watu. Na wakipenda kuingia katika yale waliyoyaingia watu, basi na waifanye, vinginevyo, wameshapumzika. Na wakikataa ila kupigana vita, basi ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mkononi mwake, nitapigana nao kwa jambo langu hili mpaka nifikie matokeo mwenyewe au hadi Mungu atimize mapenzi yake." Budail akasema: 'Nitawafikishia ulichokisema.' Basi akaenda mpaka akafika kwa Maquraishi, na akasema: 'Hakika nimewajia kutoka kwa mwanamume huyu, na nilimsikia akisema kitu. Basi, mkipenda, nitawaambia alichosema.' Watu wao wapumbavu miongoni mwao wakasema: 'Hatuhitaji utuambie lolote juu yake.' Na wakasema wenye maono mazuri miongoni mwao: 'Leta ulichomsikia akisema!' Akasema: 'Nimemsikia akisema hivi na hivi.' [Kisha akawaambia aliyoyasema Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie], kwa hivyo Urwa bin Masud Ath-Thaqafi akasema: 'Hakika mtu huyu amewapa mpango wenye uwongofu. Kwa hivyo ukubalini kama mpango wa uwongofu kwenu, mniache nimwendee.' Wakasema: 'Mwendee!' Basi akamjia na akawa anazungumza naye, na Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – akasema kauli kama ile aliyomwambia Buadail. Basi Urwa akamwambia: 'Ewe Muhammad! Unaonaje ikiwa utaangamiza watu wako? Je, umewahi kumsikia Mwarabu yeyote aliyewahi kuangamiza familia yake kabla yako? Na ikiwa ni lingine hilo (la kupigana vita), basi ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, ninaona nyuso na ninaona matapeli miongoni mwa watu ambao wana uwezekano mkubwa mno wa kukukimbia na kukuacha peke yako.' Abu Bakr akamwambia: 'Nyonya sehemu za siri za al-Lat! Je, tumkimbie na kumuacha peke yake?' Akasema: 'Ni nani huyo?' Wakasema: 'Abu Bakr.' Akasema: 'Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mkononi mwake, lau haungekuwa ule wema wako ulionifanyia na bado sijakulipa, basi ningekujibu.' Kwa hivyo, akaendelea kuzungumza na Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – na kila alipozungumza naye, anashika ndevu zake, naye Al-Mughirah bin Shu'ba alikuwa amesimama karibu na kichwa cha Nabii - Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - huku amekamata upanga na amevalia helmeti. Basi kila Urwa alipogusa ndevu za Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, – anaupiga mkono wake kwa sehemu ya chini mno ya mpini wa upanga wake na anasema: 'Weka mkono wako mbali na ndevu za Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake!' Kwa hivyo, Urwa akainua juu kichwa chake na akasema: 'Ni nani huyu?' Akasema: 'Al-Mughira bin Shu’bah.' Akasema: 'Ewe msaliti mkubwa! Je, sifanyi juhudi kukabiliana na usaliti wako?" Hilo ni kwamba, Al-Mughirah alikuwa ameandamana na watu fulani na akawaua kisha akachukua mali zao kisha akaja na akasilimu, basi Nabii – Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – akasema: "Ama Uislamu, huo mimi ninaukubali. Na ama mali (alizozichukua), mimi sina uhusiano wowote nazo." Kisha Urwa akaanza kuwatazama maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kwa macho yake makali, na ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, Nabii – Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – hakutoa makohozi yoyote isipokuwa yalianguka kwenye kiganja cha mwanamume miongoni mwao, kisha anajipaka kwayo kwenye ngozi yake na usoni mwake. Na alipowaamuru kitu, waliharakisha kuitekeleza amri yake hiyo. Na akitawadha, wanakuwa karibu kupigania maji yake ya wudhuu. Na akizungumza, wanashusha chini sauti zao mbele yake, na wala hawamtazami moja kwa moja usoni; kwa sababu ya kumheshimu. Kwa hivyo, Urwa akarudi kwa wenzake na akasema: 'Enyi watu wangu! Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, niliwatembelea wafalme: Kisra, Kaisari na An-Najashi, lakini ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, sijawahi kuona mfalme anayeheshimiwa na watu wake kama vile masahaba wa Muhammad wanavyomheshimu Muhammad. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, hatoi kohozi ila linaanguka kwenye kiganja cha mwanamume mmoja miongoni mwao na analipaka usoni mwake na kwenye ngozi yake. Na akiwaamrisha jambo, wanaharakisha kuitekeleza amri yake hiyo. Na akitawadha, wanakuwa karibu kupigania maji yake ya wudhuu. Na akizungumza, wanashusha chini sauti zao mbele yake, na wala hawamtazami moja kwa moja usoni; kwa sababu ya kumheshimu, naye kwa hakika ameweka mbele yenu mpango wenye uwongofu, kwa hivyo ukubalini. Basi mwanamume mmoja kutoka kabila la Banu Kinana akasema: 'Niacheni nimwendee!' Wakasema: 'Mwendee!' Alipomkaribia Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – na maswahaba wake, Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – akasema: "Huyu ni fulani, na anatoka kwa watu wanaoheshimu wanyama wa dhabihu, basi mleteeni wanyama hao." Kwa hivyo, wakawaleta wanyama hao wa dhabihu mbele yao, kisha watu katika kundi la Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – wakakutana naye ilhali wanafanya Talbiya ya Umra, (yaani Labbaika Allahumma labbaika (tumekuitikia ewe Mwenyezi Mungu tumekuitikia). Na alipoona hivyo, akasema: 'Subhanallah (Mwenyezi Mungu ametakasika)! Hawa hawafai kuzuiliwa kuingia katika Nyumba Takatifu.' Basi akarudi kwa wenzake na akasema: 'Nimeona wanyama wa dhabihu wamevishwa makoja na wametiwa alama, na sioni kuwa wazuiliwe kuingia katika Nyumba Takatifu.' Basi Mikraz bin Hafs akainuka, [na] akasema: 'Hebu nimwendee!' Wakasema: 'Mwendee!' Basi alipowakaribia, Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - akasema: "Huyu ni Mikraz bin Hafs, naye ni mtu mwovu." Basi akaanza kuongea na Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – na alipokuwa bado anazungumza naye, akaja Suhail bin Amr, Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie -akasema: “Jambo lenu limewawiya jepesi." Akasema: 'Leteni niandike andiko baina yetu na wewe.' Basi akamwita mwandishi na akasema: “Andika: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwingi wa kurehemu." Suhail akasema: 'Ama Mwingi wa Rehema, ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, huyo hatumjui ni nini? Lakini andika: Kwa jina lako, ewe Mwenyezi Mungu' kama ulivyokuwa ukiandika. Waislamu wakasema: 'Tunaapa kwa Mwenyezi Mungu. Hatuliandiki isipokuwa kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwingi wa kurehemu.' Nabii -rehema na amani zimshukie - akasema: “Andika kwa jina lako ewe Mwenyezi Mungu.' Kisha akasema: “Andika: Hivi ndivyo alivyokubaliana Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu." Suhail akasema: Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, lau tungelijua kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, tusingelikuzuia kuingia katika Nyumba takatifu wala hata hatungepigana vita nawe. Lakini andika: Muhammad bin Abdullah.' Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - akasema: "Mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, hata mkinikadhibisha. Andika: Muhammad bin Abdullah." Mtume -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - akasema: "Kwa sharti kwamba mtuache tuingie katika Nyumba na tuizunguke." Suhail akasema: 'Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu. Waarabu hawatakujazungumza kwamba tulichukuliwa chini ya shinikizo. Lakini hilo ni katika mwaka ujao.' Kwa hivyo akaandika. Suhail akasema: Kwa sharti kwamba mtu yeyote miongoni mwetu asiwajie, hata kama atakuwa katika dini yenu, isipokuwa utamrudisha kwetu.' Waislamu wakasema: 'Ametakasika Mwenyezi Mungu! Vipi atarudishwa kwa washirikina ilhali ametujia akiwa Muislamu?' Basi walipokuwa katika hali hiyo, akaja Abu Jandal bin Suhail [bin Amr] huku anajikokota katika minyororo yake, na alikuwa ametokea upande wa chini wa Makka, mpaka alipojitupa katikati ya Waislamu, kwa hivyo Suhail akasema: 'Huyu ndiye wa kwanza ninayeandikana chini nawe ewe Muhammad kwamba umrudishe kwangu.' Basi Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – akasema: “Bado hatujamaliza kuandika makubaliano.” Akasema: 'Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, basi sitafanya suluhu nawe kwa chochote.' Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - akasema: "Basi niruhusu huyu tu." Akasema: 'Siwezi kukuhuru huyu.' Akasema: “Ndiyo, fanya hivyo.” Akasema: 'Siwezi kufanya.' Mikraz akasema: '[Ndiyo], tumemkubalia huyu.' Abu Jandal akasema: 'Enyi kundi la Waislamu! Nitarudishwaje kwa washirikina ilhali nimekujieni nikiwa Muislamu? Hamuoni nilichokipata?' Na alikuwa ameteswa sana kwa sababu ya Mwenyezi Mungu. Umar bin Al-Khattab akasema: 'Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu; Sikuwahi kuwa na shaka tangu niliposilimu isipokuwa siku hiyo. Basi nikamjia Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - na nikasema: 'Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Je, si kweli wewe ni Nabii wa Mungu?' Akasema: “Ndiyo.” Nikasema: 'Je, si kweli sisi tuko katika haki na adui zetu wako katika batili?' Akasema: “Ndiyo.” Nikasema: 'Kwa nini tuipe dini yetu thamani duni. Kama ni hivi tutarejea na hali Mwenyezi Mungu hajahukumu baina yetu na maadui zetu?' Akasema: “Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, naye ataninusuru, wala simuasi.” Nikasema: 'Je, hukuwa ukituambia kwamba tutakuja katika Nyumba takatifu na tuizunguke?' Akasema: "Ndiyo, lakini nikakuambia kwamba utaijia mwaka huu?" Nikasema: 'Hapana.' Akasema: "Basi hakika utaijia na utaizunguka." Akasema: 'Basi nikamjia Abu Bakr, na nikamwambia kama nilivyomwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu – Rehema na Amani zimshukie – naye Abu Bakr akamjibu kama vile Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - alivyomjibu kwa namna ile ile,' na akaongeza: 'Basi mshike vyema mshono wake mpaka ufe. Kwani ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, hakika yeye yuko kwenye haki.' Umar akasema: 'Kwa hivyo nikafanya matendo kwa ajili ya hilo.' Alipomaliza suala la kuandika mkataba huo, Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - akasema: “Simameni na mchinje wanyama wa dhabihu, kisha mtoke katika nia ya Umra.” Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, hakuna mtu aliyesimama miongoni mwao mpaka akayasema mara tatu. Basi pindi hakusimama hata mmoja wao, akainuka mwenyewe na kwenda kwa Ummu Salama na akamwambia aliyopata kutoka kwa watu. [Ummu Salama] akasema: Je, ungependa hilo, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Toka nje, kisha usiseme neno na yeyote katika [wao] mpaka uchinje mnyama wako wa dhabihu na umwite kinyozi wako naye akunyoe.' Kwa hivyo akainuka na akatoka nje, na wala hakuzungumza na yeyote miongoni mwao mpaka alipofanya hivyo: alimchinja mnyama wake wa dhabihu na akamwita kinyozi wake naye akamnyoa. Basi watu walipoona hivyo, wakanyanyuka, wakachinja wanyama wao wa dhabihu, kisha wakanyoana wao kwa wao mpaka baadhi yao wakawa karibu mno kuuana kwa sababu ya huzuni. Kisha wakaja wanawake Waumini, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha: ''Enyi mlioamini! Wakikujilieni wanawake Waumini waliohama, basi wafanyieni mtihani...'' mpaka ikafika ''wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa zenu'' basi Umar akawataliki siku hiyo wanawake wawili waliokuwa wake katika ushirikina, kwa hivyo Muawiya akamuoa mmoja wao na mwingine akaolewa na Safwan bin Umayya. Kisha akarejea Madina. Na katika marejeo yake, Mwenyezi Mungu akamteremshia: ''Hakika tumekufungulia Ushindi wa dhahiri. Ili Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yajayo, na akutimizie neema zake, na akuongoe katika njia iliyonyooka. Na Mwenyezi Mungu akunusuru nusura yenye nguvu...'' hadi mwisho wake, kwa hivyo, Umar akasema: 'Je, ni ushindi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?' Akasema: “Ndiyo.” Maswahaba wakasema: "Hongera sana ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Nasi tuna nini?" Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha: "Yeye ndiye aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za Waumini..." hadi mwisho wa Aya. Mwisho wa kisa.
Huu ndio mwisho wa tafsiri ya Surat Al-Fath, na sifa njema zote [na neema] ni za Mwenyezi Mungu. Na rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad na familia yake na maswahaba zake. Niliyatoa haya kutoka katika maandishi ya mfasiri, Mwenyezi Mungu amrehemu na amsamehe, na tamati ya kuiandika ilikuwa tarehe 13 Dhul-Hijja mwaka 1345, na rehema na amani ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad, ahali zake, na maswahaba zake mpaka Siku ya Malipo. Ewe Mwenyezi Mungu tukubalie. Kimeandikwa kwa kalamu ya masikini kwa Mola wake Mlezi, Sulaiman bin Hamad Al-Abdullah Al-Bassam, Mwenyezi Mungu amghufirie yeye na wazazi wake na Waislamu wote. Ewe Mwenyezi Mungu tukubalie. Na rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie Muhammad na ahali zake na maswahaba zake wote mpaka siku ya Malipo. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye kwa neema yake yanatimia mambo mema.
* * *