Juzuu ya saba ya Taysir Al-Karim Al-Mannan katika tafsiri ya aya za Qur-ani. Cha mwandishi wake Abdur-Rahman bin Nassir bin Abdullah As-Sa'adi, Mwenyezi Mungu amsamehe yeye, wazazi wake, na Waislamu wote kwa ujumla.
Nayo iliteremka Makka
{ص وَالْقُرْآنِ ذِي الذِّكْرِ (1) بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي عِزَّةٍ وَشِقَاقٍ (2) كَمْ أَهْلَكْنَا مِنْ قَبْلِهِمْ مِنْ قَرْنٍ فَنَادَوْا وَلَاتَ حِينَ مَنَاصٍ (3) وَعَجِبُوا أَنْ جَاءَهُمْ مُنْذِرٌ مِنْهُمْ وَقَالَ الْكَافِرُونَ هَذَا سَاحِرٌ كَذَّابٌ (4) أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَهًا وَاحِدًا إِنَّ هَذَا لَشَيْءٌ عُجَابٌ (5) وَانْطَلَقَ الْمَلَأُ مِنْهُمْ أَنِ امْشُوا وَاصْبِرُوا عَلَى آلِهَتِكُمْ إِنَّ هَذَا لَشَيْءٌ يُرَادُ (6) مَا سَمِعْنَا بِهَذَا فِي الْمِلَّةِ الْآخِرَةِ إِنْ هَذَا إِلَّا اخْتِلَاقٌ (7) أَأُنْزِلَ عَلَيْهِ الذِّكْرُ مِنْ بَيْنِنَا بَلْ هُمْ فِي شَكٍّ مِنْ ذِكْرِي بَلْ لَمَّا يَذُوقُوا عَذَابِ (8) أَمْ عِنْدَهُمْ خَزَائِنُ رَحْمَةِ رَبِّكَ الْعَزِيزِ الْوَهَّابِ (9) أَمْ لَهُمْ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَلْيَرْتَقُوا فِي الْأَسْبَابِ (10) جُنْدٌ مَا هُنَالِكَ مَهْزُومٌ مِنَ الْأَحْزَابِ (11)}.
1. Swad. Naapa kwa Qur-ani yenye mawaidha. 2. Lakini waliokufuru wamo katika majivuno na upinzani. 3. Mataifa mangapi tumeyaangamiza kabla yao, na wakapiga kelele, lakini wakati wa kuokoka ulikwisha pita. 4. Na walistaajabu kuwajia mwonyaji anayetokana nao wenyewe,
na makafiri wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo. 5. Amewafanya miungu wote kuwa ni mungu
mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu. 6.
Na wakaondoka wakubwa wao wakiwaambia: Nendeni zenu na dumuni na miungu yenu, kwani hili ni jambo lililopangwa. 7. Sisi hatukusikia haya katika mila hii ya mwisho. Haya si chochote ila ni uzushi tu. 8. Ati yeye tu ndiye aliye teremshiwa mawaidha peke yake katika sisi? Lakini hao wana shaka na mawaidha yangu, bali hawajaionja adhabu yangu. 9. Au wanazo wao hazina za rehema za Mola wako Mlezi, Mwenye nguvu, Mpaji? 10. Au wao wana ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yavyo? Basi na wazipande njia za kwendea huko! 11. Hao ni askari watakaoshindwa miongoni mwa makundi yatakayoshindwa.
#
{1} هذا بيانٌ من الله تعالى لحال القرآن وحال المكذِّبين به معه ومع من جاء به، فقال: {ص والقرآنِ ذي الذِّكْرِ}؛ أي: ذي القَدْر العظيم والشرف، المذكِّر للعباد كلَّ ما يحتاجون إليه من العلم بأسماء الله وصفاته وأفعاله، ومن العلم بأحكام الله الشرعية، ومن العلم بأحكام المعاد والجزاء؛ فهو مذكِّرٌ لهم في أصول دينهم وفروعه. وهنا لا يُحتاجُ إلى ذِكْرِ المقسَم عليه؛ فإنَّ حقيقة الأمر أنَّ المقسم به وعليه شيءٌ واحدٌ، وهو هذا القرآن الموصوف بهذا الوصف الجليل.
{1} Huku ni kubainisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu hali ya Qur-ani na hali ya wale wanaoikadhibisha, namna wanavyoamiliana nayo na pia namna wanavyoamiliana na yule aliyekuja nayo.
Akasema: "Swad. Ninaapa kwa Qur-ani yenye mawaidha," cheo kikuu na utukufu. Ambayo huwakumbusha waja kila wanachohitaji miongoni mwa elimu ya majina ya Mwenyezi Mungu, sifa zake, na vitendo vyake. Na pia elimu ya hukumu za Mwenyezi Mungu. Na pia elimu kuhusu akhera na hukumu za kimalipo. Inakumbusha mambo ya kimsingi na ya matawi ya dini yao. Hapa hakuna haja ya kumtaja yule ambaye imeapwa kwa ajili yake. Kwani uhakika wa hilo hapa ni kwamba kilichoapiwa na kilichoapwa kwa ajili yake ni kitu kimoja, nacho ni Qur-ani hii, yenye maelezo haya matukufu.
#
{2} فإذا كان القرآن بهذا الوصف؛ عُلِمَ ضرورةُ العبادِ إليه فوق كلِّ ضرورةٍ، وكان الواجبُ عليهم تلقِّيه بالإيمان والتَّصديق والإقبال على استخراج ما يُتَذَكَّرُ به منه، فهدى الله مَنْ هدى لهذا، وأبى الكافرون به وبمن أنزلَه، وصار معهم عِزَّةٌ وشقاقٌ، عزَّةٌ وامتناعٌ عن الإيمان به، واستكبارٌ وشقاقٌ له؛ أي: مشاقَّة ومخاصمة في ردِّه وإبطاله وفي القَدْح بمن جاء به.
{2} Ikiwa Qur-ani ni ya maelezo haya, basi ilijulikana kuwa waja wanaihitaji zaidi ya hitajio lolote. Na ilikuwa ni wajibu juu yao kuipokea kwa imani, kuisadiki na kuielekea njia ya kutoka humo yenye kukumbusha. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamuongoa aliyemuongoa. Akafanya hivyo, nao makafiri wakaikataa na wakamkataa yule aliyeiteremsha. Basi makafiri wakaingia katika majivuno na upinzani dhidi yake, kuikataa, kuibatilisha, kuikashifu na pia kumkashifu aliyekuja nayo.
#
{3} فتوعَّدهم بإهلاك القرون الماضية المكذِّبة بالرسل، وأنَّهم حين جاءهم الهلاكُ؛ نادَوْا واستغاثوا في صرف العذاب عنهم، ولكنْ {لاتَ حينَ مناص}؛ أي: وليس الوقت وقتَ خلاصٍ مما وقعوا فيه ولا فرج لما أصابهم، فليحذَرْ هؤلاء أن يَدوموا على عزَّتِهِم وشقاقِهِم؛ فيصيبُهم ما أصابهم.
{3} Basi Mwenyezi Mungu akawatishia na maangamizo ya karne zilizopita zilizowakadhibisha Mitume. Na kwamba yalipowafikia maangamizo, wakapiga kelele na kuomba msaada waondolewe adhabu hiyo, lakini "wakati wa kuokoka ulikwishapita" kutokana na yale yaliyowafikia. Basi na watahadhari hawa wasije dumu katika majivuno na upinzani wao, wakaja patwa na yaliyowapata wenzao.
#
{4} {وعَجِبوا أن جاءهم منذرٌ منهم}؛ أي: عجب هؤلاء المكذِّبون في أمرٍ ليس محلَّ عجبٍ أن جاءهم منذرٌ منهم ليتمكَّنوا من التلقِّي عنه وليعرفوه حقَّ المعرفة، ولأنَّه من قومهم؛ فلا تأخُذُهم النَّخوة القوميَّة عن اتِّباعِهِ؛ فهذا مما يوجبُ الشكر عليهم وتمامَ الانقيادِ له، ولكنَّهم عكسوا القضيَّة، فتعجَّبوا تعجُّب إنكار، وقالوا من كفرهم وظلمهم: {هذا ساحرٌ كذابٌ}!
{4} "Na walistaajabu kuwajia mwonyaji anayetokana nao wenyewe." Yaani, hao wanaokadhibisha walistaajabia jambo ambalo sio la kustaajabisha, kwamba aliwajia mwonyaji anayetokana nao wenyewe ili wapate kujifunza kutoka kwake na kumjua vyema zaidi; na kwa kuwa yeye ni miongoni mwa watu wao ili wasione ugumu wa kufuata mtu asiyekuwa wa kutokana nao. Kwani walipaswa kushukuru na kumtii kikamilifu kwa sababu ya hili, lakini wao walifanya kinyume cha jambo hili na wakastaajabia kwa njia ya kukanusha.
Na kwa sababu ya ukafiri wao na dhuluma yao wakasema: "Huyu ni mchawi, mwongo mno."
#
{5} وذنبُهُ عندَهم أنَّه {جعل الآلهة إلهاً واحداً}؛ أي: كيف ينهى عن اتِّخاذ الشركاء والأنداد ويأمُرُ بإخلاص العبادة لله وحده؟! {إنَّ هذا}: الذي جاء به {لشيءٌ عُجابٌ}؛ أي: يقضى منه العجب لبطلانِهِ وفسادِهِ عندهم.
{5} Dhambi yake kulingana nao ni kwamba "Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu" na kwamba anawezaje kuwakataza kujifanyia washirika, na wenza, na akawaamrisha kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika ibada zao? "Hakika hili" alilokuja nalo, "ni jambo la ajabu" na batili kulingana na wao.
#
{6} {وانطَلَقَ الملأ منهم}: المقبولُ قولُهم، محرِّضينَ قومَهم على التمسُّك بما هم عليه من الشرك. {أنِ امْشوا واصبِروا على آلِهَتِكُم}؛ أي: استمرَّوا عليها وجاهدوا نفوسَكم في الصبر عليها وعلى عبادتها، ولا يردُّكم عنها رادٌّ، ولا يصدَّنَّكم عن عبادتها صادٌّ. {إنَّ هذا}: الذي جاء به محمدٌ من النهي عن عبادتها {لشيءٌ يُرادُ}؛ أي: يُقْصَدُ؛ أي: له قصدٌ ونيةٌ غير صالحة في ذلك، وهذه شبهةٌ لا تَروج إلاَّ على السُّفهاء؛ فإنَّ مَنْ دعا إلى قول حقٍّ أو غير حقٍّ لا يُرَدُّ قولُه بالقدح في نيَّتِهِ؛ فنيَّتُهُ وعملُه له، وإنَّما يُرَدُّ بمقابلتِهِ بما يُبْطِلُهُ ويفسِدُهُ من الحُجج والبراهين، وهم قصدُهم أنَّ محمداً ما دعاكم إلى ما دعاكم إلاَّ ليرأس فيكم ويكونَ معظَّماً عندكم متبوعاً.
{6} "Na wakaondoka wakubwa wao wakiwaambia" watu wao kwa njia ya kuwahimiza kushikamana na ushirikina wao huo. "Nendeni zenu na dumuni na miungu yenu." Na pambaneni na nafsi zenu juu ya kuvumulia katika kuiabudu, wala kisikuzuieni chochote kufanya hivyo, wala chochote kisikuzuieni kuiabudu. "Kwani hili" alilokuja nalo Muhammad la kukataza kuiabudu miungu yetu, "ni jambo lililopangwa" na lina makusudio yasiyokuwa mazuri. Lakini hii ni fikira potofu ya utata isiyochanganya isipokuwa watu wapumbavu tu. Kwa maana mwenye kulingania kauli ya haki au isiyokuwa ya haki haikataliwi kauli yake hiyo kwa sababu ya kuikashifu niya yake, kwani nia yake na matendo yake ni vyake. Bali anapaswa kukataliwa kwa kumkabili na hoja na ushahidi unaoibatilisha na kuiharibu. Nao walikusudia kwamba Muhammad hakuwalingania kwake yale aliyowalingania isipokuwa ili awe mkuu wao anayefuatwa.
#
{7} {ما سمعنا بهذا}: القول الذي قاله والدين الذي دعا إليه {في الملَّةِ الآخرةِ}؛ أي: في الوقت الأخير، فلا أدْرَكْنا عليه آباءنا، ولا آباؤنا أدركوا آباءهم عليه؛ فامضوا على الذي مضى عليه آباؤكم؛ فإنَّه الحقُّ، وما هذا الذي دعا إليه محمدٌ إلاَّ اختلاقٌ اخْتَلَقَهُ وكذبٌ افتراه. وهذه أيضاً شبهةٌ من جنس شبهتهم الأولى؛ حيث ردُّوا الحقَّ بما ليس بحجَّة لردِّ أدنى قول، وهو أنَّه قولٌ مخالف لما عليه آباؤهم الضالُّون؛ فأين في هذا ما يدلُّ على بطلانه؟!
{7} "Sisi hatukusikia haya" maneno aliyoyasema na Dini hii aliyokuja nayo "katika mila hii ya mwisho." Yaani, zama za mwisho, na hata hatukuwapata baba zetu wakiifuata, wala baba zetu hawakuwapata baba zao wakiifuata. Basi endeleeni kufuata yale waliyoyafuata baba zenu, kwani hayo ndiyo haki, na haya anayoyalingania Muhammad si chochote isipokuwa uzushi aliouzua na uwongo tu. Hii pia ni fikira potofu ya utata ya aina sawa na ile ya kwanza. Ambapo waliikataa haki kwa kitu ambacho si hoja inayoweza kupinga kauli ya chini kabisa. Nayo ni kusema kwamba maneno yake yanapingana na yale wanayofuata baba zao wapotofu. Je, ni wapi katika hili panaashiria ubatili wake?
#
{8} {أأُنزِلَ عليه الذِّكْرُ من بيننا}؛ أي: ما الذي فضَّله علينا حتى ينزل الذِّكْر عليه من دوننا ويخصَّه الله به؟! وهذه أيضاً شبهةٌ، أين البرهانُ فيها على ردِّ ما قاله؟ وهل جميع الرسل إلاَّ بهذا الوصف؟! يمنُّ الله عليهم برسالته ويأمُرُهم بدعوة الخلق إلى الله. ولهذا؛ لما كانت هذه الأقوالُ الصادرةُ منهم لا يَصْلُحُ شيءٌ منها لردِّ ما جاء به الرسول؛ أخبر تعالى من أين صَدَرَتْ، وأنَّهم {في شكٍّ من ذِكْري}: ليس عندَهم علمٌ ولا بيِّنةٌ، فلما وقعوا في الشكِّ وارتَضَوا به وجاءهم الحقُّ الواضحُ وكانوا جازمين بإقامتهم على شكِّهم؛ قالوا ما قالوا من تلك الأقوال لدفع الحقِّ، لا عن بيِّنة من أمرهم، وإنَّما ذلك من باب الائتفاكِ منهم. ومن المعلوم أنَّ مَنْ هو بهذه الصفة يتكلَّم عن شكٍّ وعنادٍ؛ فإنَّ قولَه غيرُ مقبول ولا قادح أدنى قدحٍ في الحقِّ، وأنَّه يتوجَّه عليه الذمُّ واللوم بمجرَّد كلامه، ولهذا توعَّدهم بالعذاب، فقال: {بل لَمَّا يَذوقوا عذابِ}؛ أي: قالوا هذه الأقوالَ وتجرَّؤوا عليها؛ حيث كانوا ممتَّعين في الدُّنيا، لم يصبْهم من عذاب الله شيءٌ؛ فلو ذاقوا عذابَه؛ لم يتجرَّؤوا.
{8} "Ati yeye tu ndiye aliyeteremshiwa mawaidha peke yake katika sisi?" Yaani, ni kitu gani kilichomfanya bora zaidi yetu hata Mwenyezi Mungu akamshukishia yeye tu ukumbusho badala yetu? Hii pia ni fikira potofu ya utata, lakini uko wapi ushahidi ndani yake wa kukanusha alichosema? Je, si kweli kwamba Mitume wote walikuwa hivi? Mwenyezi Mungu alikuwa akiwaneemesha kwa ujumbe wake na anawaamuru kuwalingania watu kwa Mwenyezi Mungu. Na kwa sababu maneno haya waliyosema hayakufailia hata kidogo kukanusha yale aliyokuja nayo Mtume,
Mwenyezi Mungu Mtukufu alitueleza ni wapi yalitoka: 'Na kwamba wao "wana shaka na mawaidha yangu," hawana elimu yoyote wala ushahidi ulio wazi.' Walipoingiwa na shaka na wakairidhia na ikawajia haki iliyo wazi, lakini walikuwa wameshaazimia kuendelea na shaka yao, wakasema yale waliyoyasema ili kuipinga haki hiyo si kwa msingi wa ushahidi ulio wazi kuhusiana na jambo lao hilo, bali ilikuwa ni kwa mbinu ya kuzua uongo. Inajulikana kwamba mtu aliye na tabia hii atazungumza kwa shaka na ukaidi. Basi maneno yake hayatakubalika na wala si kuikashifu haki hata kidogo. Na kwamba yeye ndiye anayefaa kukaripiwa na kulaumiwa pindi anapoanza kuzungumza. Ndiyo maana akawatishia kwa adhabu,
akasema: "Bali hawajaionja adhabu yangu." Yaani, walifanya ujasiri wa kusema haya maneno na wakaendelea kustareheshwa katika dunia hii bila ya kupatwa na adhabu yoyote ya Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa wangeliionja adhabu yake, basi hawangefanya ujasiri wa kufanya hivyo.
#
{9} {أم عِندَهُم خزائنُ رحمةِ ربِّك العزيز الوهَّاب}: فيعطون منها مَنْ شاؤوا ويمنعونَ منها مَن شاؤوا؛ حيث قالوا: {أأنزِلَ عليه الذِّكْرُ مِن بَيْنِنا}؛ أي: هذا فضلُه تعالى ورحمتُه، وليس ذلك بأيديهم حتى يتجرؤوا على الله.
{9} "Au wanazo wao hazina za rehema za Mola wako Mlezi, Mwenye nguvu, Mpaji?" Basi wakampa wamtakaye katika hizo na wakamnyima wamtakaye.
Ambapo walisema: "Ati yeye tu ndiye aliyeteremshiwa mawaidha peke yake katika sisi?" Yaani, hii ni fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema zake, na wala halimo mikononi mwao mpaka wakamfanyia Mwenyezi Mungu ujasiri huo.
#
{10} {أم لهم مُلْكُ السمواتِ والأرض وما بينَهما}: بحيثُ يكونون قادرين على ما يريدون، {فَلْيَرْتَقوا في الأسبابِ}: الموصلة لهم إلى السماء، فيقطعوا الرحمةَ عن رسول الله! فكيف يتكلَّمون وهم أعجزُ خلق الله وأضعفُهم بما تكلَّموا به؟!
{10} "Au wao wana ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake," kiasi kwamba wana uwezo wa kufanya watakalo? "Basi na wazipande njia za kwendea huko" zitakazowafikisha mbinguni, ili wamkatie Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema hiyo aliyopewa! Basi wanawezaje kusema hayo waliyosema ilhali wao ndio wasio na uwezo zaidi kati ya viumbe wa Mwenyezi Mungu na ndio madhaifu zaidi?
#
{11} أم قصدُهم التحزُّب والتجنُّد والتعاون على نصر الباطل وخذلان الحقِّ، وهو الواقعُ؛ فإنَّ هذا المقصودَ لا يتمُّ لهم، بل سعيُهم خائبٌ، وجندُهم مهزومٌ، ولهذا قال: {جندٌ ما هنالك مهزومٌ من الأحزابِ}.
{11} Au wanakusudia kufanya makundi na kushirikiana ili kuiunga mkono batili na kuiangusha chini haki. Na hii ndiyo hali yao halisi. Lakini hawawezi kufikia makusudio yao haya, na bidii yao hiyo itaambulia patupu, na jeshi lao hilo litashindwa.
Ndiyo maana akasema: "Hao ni askari watakaoshindwa miongoni mwa makundi yatakayoshindwa."
{كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَعَادٌ وَفِرْعَوْنُ ذُو الْأَوْتَادِ (12) وَثَمُودُ وَقَوْمُ لُوطٍ وَأَصْحَابُ الْأَيْكَةِ أُولَئِكَ الْأَحْزَابُ (13) إِنْ كُلٌّ إِلَّا كَذَّبَ الرُّسُلَ فَحَقَّ عِقَابِ (14) وَمَا يَنْظُرُ هَؤُلَاءِ إِلَّا صَيْحَةً وَاحِدَةً مَا لَهَا مِنْ فَوَاقٍ (15)}.
12. Walikanusha kabla yao kaumu ya Nuhu, na kina A'adi na Firauni mwenye majengo. 13. Na Thamud na kaumu Luti na watu wa Machakani. Hayo ndiyo makundi. 14. Hao wote waliwakadhibisha Mitume; basi wakastahiki adhabu yangu. 15. Na hawa hawangojei ila ukelele mmoja tu usio na muda.
#
{12 - 15} يحذِّرُهم تعالى أن يَفْعَلَ بهم ما فعل بالأمم من قبلهم، الذين كانوا أعظم قوَّةً منهم وتحزُّباً على الباطل. {قومُ نوح وعادٌ}: قوم هود وفرعونُ ذي الأوتادِ؛ أي: الجنود العظيمة والقوَّة الهائلة، {وثمودُ}: قوم صالح، {وقومُ لوطٍ وأصحابُ الأيْكَةِ}؛ أي: الأشجار والبساتين الملتفَّة، وهم قوم شعيب. {أولئك الأحزابُ}: الذين اجتمعوا بقوَّتهم وعَددِهِم وعُدَدِهِم على ردِّ الحقِّ، فلم تُغْنِ عنهم شيئاً {إن كُلٌّ}: من هؤلاء {إلاَّ كَذَّبَ الرُّسُلَ فحقَّ}: عليهم {عقاب}: الله، وهؤلاء ما الذي يطهِّرهم ويزكِّيهم أن لا يُصيبَهم ما أصاب أولئك؟! فلينتظروا {صيحة واحدة ما لها من فَواقٍ}؛ أي: من رجوع وردٍّ، تهلِكُهم، وتستأصِلُهم إن أقاموا على ما هم عليه.
{12 - 15} Mwenyezi Mungu anatahadharisha asijewafanyia yale aliyowafanyia mataifa ya kabla yao, ambao walikuwa na nguvu zaidi kuliko wao na wakali zaidi katika kushirikiana juu ya batili. "Kaumu ya Nuhu na kina A'adi" watu wa Hud, na Firauni mwenye askari wengi na nguvu kubwa zaidi, "na Thamud" watu wa Swalih, "na kaumu Lut'i na watu wa Machakani",nao ni watu wa nabii Shuaib. "Hayo ndiyo makundi" yaliyokusanyika kwa nguvu zao na idadi yao, na vifaa vyao ili kuipinga haki. Lakini hivyo havikuwafaa kitu; "Hao wote waliwakadhibisha Mitume, basi wakastahiki adhabu yangu." Basi hawa ni kitu gani kitawasafisha na kuwatakasa ili yasiwapate yaliyowapata wenzao hao? Basi na wangojee "ukelele mmoja tu usio na muda," ambao utawaangamiza na kuwafutilia mbali ikiwa wataendelea kuwa walivyo.
#
{16} أي: قال هؤلاءِ المكذِّبون من جَهْلِهِم ومعانَدَتِهِم الحقَّ مستعجلين للعذاب: {ربَّنا عَجِّلْ لنا قِطَّنا}؛ أي: قِسْطَنا وما قسم لنا من العذابِ عاجلاً {قبلَ يوم الحسابِ}: ولجُّوا في هذا القول، وزعموا أنَّك يا محمدُ إن كنتَ صادقاً؛ فعلامةُ صدقِكَ أن تأتينا بالعذاب.
{16} Yaani hao wanaokadhibisha walisema kwa sababu ya ujinga wao na ukaidi wao dhidi ya haki,
wakiiharakishia adhabu: "Mola wetu Mlezi! Tuletee upesi sehemu yetu ya adhabu kabla ya Siku ya Hesabu." Walikakamia kusema hivi, na wakadai kuwa wewe, ewe Muhammad, ikiwa wewe ni mkweli basi alama ya ukweli wako ni kwamba uwaletee adhabu.
#
{17} فقال لرسوله: {اصْبِرْ على ما يَقولونَ}: كما صبر مَنْ قَبْلَكَ من الرُّسل؛ فإنَّ قولَهم لا يضرُّ الحقَّ شيئاً، ولا يضرُّونك في شيءٍ، وإنَّما يضرُّون أنفسَهم.
{17} Basi Mwenyezi Mungu akamwambia Mtume wake: "Subiri kwa wanayoyasema" kama walivyosubiri Mitume kabla yako. Maneno yao hayadhuru haki kwa vyovyote vile, wala hawakudhuru chochote, bali wanajidhuru tu.
{وَاذْكُرْ عَبْدَنَا دَاوُودَ ذَا الْأَيْدِ إِنَّهُ أَوَّابٌ (17) إِنَّا سَخَّرْنَا الْجِبَالَ مَعَهُ يُسَبِّحْنَ بِالْعَشِيِّ وَالْإِشْرَاقِ (18) وَالطَّيْرَ مَحْشُورَةً كُلٌّ لَهُ أَوَّابٌ (19) وَشَدَدْنَا مُلْكَهُ وَآتَيْنَاهُ الْحِكْمَةَ وَفَصْلَ الْخِطَابِ (20)}.
17. Subiri kwa hayo wayasemayo, na umkumbuke mja wetu Daudi, mwenye nguvu. Hakika yeye alikuwa mwingi wa kutubia. 18. Hakika tuliidhalilisha milima pamoja naye ikisabihi jioni na asubuhi pamoja naye. 19. Na pia ndege waliokusanywa makundi kwa makundi; wote walikuwa wanyenyekevu kwake. 20. Na tukautia nguvu ufalme wake, na tukampa hekima, na kukata hukumu.
#
{17} لمَّا أمر الله رسولَه بالصبر على قومه؛ أمَرَه أن يستعينَ على الصبر بالعبادةِ لله وحدَه، ويتذكَّرَ حال العابدين؛ كما قال في الآية الأخرى: {فاصْبِرْ على ما يَقولونَ وسَبِّحْ بِحَمْدِ ربِّكَ قبلَ طُلوع الشمسِ وقبلَ غُروبها}. ومن أعظم العابدين نبيُّ الله داود عليه الصلاة والسلام، ذو {الأيْدِ}؛ أي: القوة العظيمة على عبادةِ الله تعالى في بدنِهِ وقلبِهِ. {إنَّه أوَّابٌ}؛ أي: رجاعٌ إلى الله في جميع الأمور بالإنابة إليه بالحبِّ والتألُّه والخوف والرجا وكثرَةِ التضرُّع والدُّعاء، رجاعٌ إليه عندما يقعُ منه بعض الخلل بالإقلاع والتوبة النَّصوح.
{17} Mwenyezi Mungu alipomwamrisha Mtume wake kuwa na subira juu ya kaumu yake, akamuamrisha atafute msaada wa kuwa na subira hiyo kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake. Na kwamba akumbuke hali ya watu waliokuwa wakimuabudu Mwenyezi Mungu sana.
Kama alivyosema katika aya nyingine: "Basi yavumilie haya wayasemayo, na umtakase Mola wako Mlezi kwa kumsifu kabla ya kuchomoza jua na kabla halijachwa." Miongoni mwa wale waliokuwa wakimuabudu Mwenyezi Mungu sana ni Nabii wa Mwenyezi Mungu, Daudi, rehema na amani ziwe juu yake. Ambaye alikuwa "mwenye nguvu" nyingi katika kumwabudu Mwenyezi Mungu katika mwili wake na moyo wake. "Hakika yeye alikuwa mwingi wa kutubia" kwa upendo, kumfanyia uungu, hofu, matumaini, kuomba dua nyingi kwa unyenyekevu na kurudi kwake pale anapokosea kwa kuachana na kosa hilo na kutubia toba ya kweli.
#
{18 - 19} ومن شدة إنابته لربِّه وعبادتِهِ أن سَخَّرَ الله الجبال معه تسبِّحُ معه بحمدِ ربِّها {بالعشيِّ والإشراقِ}: أول النهار وآخره، {و} سخَّر {الطيرَ محشورةً}: معه مجموعةً. {كلٌّ}: من الجبال والطير {له} تعالى {أوابٌ}: امتثالاً لقوله تعالى: {يا جبالُ أوِّبي معه والطير}: فهذه منَّةُ الله عليه بالعبادة.
{18 - 19} Na kwa sababu ya kutubia sana kwake kwa Mola wake Mlezi na kumuabudu zaidi, Mwenyezi Mungu akamtiishia milima ikisabihi "jioni na asubuhi pamoja naye. Na pia ndege waliokusanywa makundi kwa makundi." "Vyote;" yaani, milima na ndege,
"vilikuwa vinyenyekevu kwake" kwa kutekeleza kauli ya Mola Mtukufu: "Enyi milima! Karirini kumtakasa Mwenyezi Mungu pamoja naye! Na ndege pia." Hii ni neema ya Mwenyezi Mungu juu yake kwa kumuwezesha kumuabudu sawasawa.
#
{20} ثم ذكر منَّته عليه بالملك العظيم، فقال: {وشَدَدْنا مُلْكَه}؛ أي: قوَّيْناه بما أعطيناه من الأسباب وكثرة العَدَدِ والعُدَدِ التي بها قوَّى اللهُ ملكَه. ثم ذكر مِنَّتَه عليه بالعلم، فقال: {وآتَيْناه الحكمةَ}؛ أي: النبوَّة والعلم العظيم {وفصلَ الخطابِ}؛ أي: الخصومات بين الناس.
{20} Kisha akamtajia neema aliyompa, ufalme mkubwa.
Akasema: "Na tukautia nguvu ufalme wake" kwa njia mbalimbali alizompa, idadi kubwa na maandalizi makubwa mno ambayo kwayo Mwenyezi Mungu aliutia nguvu ufalme wake. Kisha akamtajia neema aliyompa ya elimu,
akasema: "na tukampa hekima." Yaani, unabii na elimu kubwa sana, "na kukata hukumu" katika migogoro ya baina ya watu.
{وَهَلْ أَتَاكَ نَبَأُ الْخَصْمِ إِذْ تَسَوَّرُوا الْمِحْرَابَ (21) إِذْ دَخَلُوا عَلَى دَاوُودَ فَفَزِعَ مِنْهُمْ قَالُوا لَا تَخَفْ خَصْمَانِ بَغَى بَعْضُنَا عَلَى بَعْضٍ فَاحْكُمْ بَيْنَنَا بِالْحَقِّ وَلَا تُشْطِطْ وَاهْدِنَا إِلَى سَوَاءِ الصِّرَاطِ (22) إِنَّ هَذَا أَخِي لَهُ تِسْعٌ وَتِسْعُونَ نَعْجَةً وَلِيَ نَعْجَةٌ وَاحِدَةٌ فَقَالَ أَكْفِلْنِيهَا وَعَزَّنِي فِي الْخِطَابِ (23) قَالَ لَقَدْ ظَلَمَكَ بِسُؤَالِ نَعْجَتِكَ إِلَى نِعَاجِهِ وَإِنَّ كَثِيرًا مِنَ الْخُلَطَاءِ لَيَبْغِي بَعْضُهُمْ عَلَى بَعْضٍ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَقَلِيلٌ مَا هُمْ وَظَنَّ دَاوُودُ أَنَّمَا فَتَنَّاهُ فَاسْتَغْفَرَ رَبَّهُ وَخَرَّ رَاكِعًا وَأَنَابَ (24) فَغَفَرْنَا لَهُ ذَلِكَ وَإِنَّ لَهُ عِنْدَنَا لَزُلْفَى وَحُسْنَ مَآبٍ (25) يَادَاوُودُ إِنَّا جَعَلْنَاكَ خَلِيفَةً فِي الْأَرْضِ فَاحْكُمْ بَيْنَ النَّاسِ بِالْحَقِّ وَلَا تَتَّبِعِ الْهَوَى فَيُضِلَّكَ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ إِنَّ الَّذِينَ يَضِلُّونَ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا نَسُوا يَوْمَ الْحِسَابِ (26)}.
21. Na je, imekufikia habari ya wagombanao walipopindukia ukuta kuingia chumbani? 22. Walipomuingilia Daudi, naye akawaogopa.
Wakasema: Usiogope! Sisi ni wagombanao wawili, mmoja wetu amemdhulumu mwenziwe. Basi tuhukumu kwa haki, wala usipendelee. Na utuongoe kwenye njia iliyo sawa. 23. Hakika huyu ndugu yangu ana kondoo wa kike tisini na tisa; na mimi ninaye kondoo mke mmoja.
Akasema: Nipe huyo nikufugie! na amenishinda kwa maneno. 24.
Akasema: Kweli amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako mmoja kuongezea kwenye kondoo wake. Na hakika washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao, isipokuwa walioamini na wakatenda mema. Na hao ni wachache. Na Daudi akajua kuwa tumemfanyia mtihani. Basi akamwomba msamaha Mola wake Mlezi, na akaanguka kusujudu na kutubia. 25. Basi tukamsamehe kwa hayo. Naye kwa hakika anao mkaribisho mkubwa na marejeo mazuri kwetu. 26. Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi. Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika wanaoipotea Njia ya Mwenyezi Mungu wakaiacha, watapata adhabu kali kwa sababu ya kusahau kwao Siku ya Hisabu.
#
{21} لما ذكر تعالى أنَّه آتى نبيَّه داود الفصل في الخطاب بين الناس، وكان معروفاً بذلك مقصوداً؛ ذَكَرَ تعالى نبأ خصمينِ اختصما عنده في قضيَّةٍ جعلهما الله فتنةً لداود وموعظةً لخلل ارتَكَبَهُ، فتاب الله عليه وغَفَرَ له وقيَّضَ له هذه القضيَّة، فقال لنبيِّه محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -: {وهل أتاك نبأُ الخصم}: فإنَّه نبأ عجيبٌ، {إذ تَسَوَّروا}: على داود {المحرابَ}؛ أي: محلَّ عبادتِهِ من غير إذنٍ ولا استئذانٍ، ولم يدخُلوا عليه مع باب.
{21} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kwamba alimpa Nabii wake Daudi uwezo wa kukata hukumu sawasawa baina ya watu, na ilikuwa akijulikana kwa hilo na watu wakawa wanamjia kwa ajili yake. Mwenyezi Mungu akataja habari za wapinzani wawili waliogombana mbele yake kwa sababu ya jambo fulani, na Mwenyezi Mungu aliwafanya kuwa ni mtihani kwa Daudi na mawaidha kwa sababu ya kosa alilokuwa amelifanya. Basi Mwenyezi Mungu akamsamehe na akamuwekea tukio hili. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamwambia Nabii wake Muhammad -
rehema na amani zimshukie: "Na je, imekufikia habari ya wagombanao?" Kwani ni habari za ajabu "walipopindukia ukuta kuingia chumbani" mwa Daudi mwa kuabudia bila ya ruhusa yoyote, na wala hawakuingilia mlangoni.
#
{22} فلذلك لما دَخَلوا عليه بهذه الصورةِ؛ فَزِعَ منهم وخاف، فقالوا له: نحن خصمانِ؛ فلا تخفْ، {بغى بعضُنا على بعضٍ}: بالظلم، {فاحْكُم بينَنا بالحقِّ}؛ أي: بالعدل ولا تَمِلْ مع أحدِنا، {ولا تُشْطِطْ واهْدِنا إلى سواءِ الصِّراطِ}.
{22} Ndiyo maana, walipoingia alimokuwa kwa namna hii, akaingiwa na hofu na akaogopa.
Wakamwambia: Sisi ni mahasimu wawili, basi usihofu. "Mmoja wetu amemdhulumu mwenziwe, basi tuhukumu kwa haki" wala usimlalie mmoja wetu, "wala usipendelee. Na utuongoe kwenye njia iliyo sawa."
#
{23} والمقصود من هذا أن الخصمين قد عُرِفَ أنَّ قصدَهما الحقُّ الواضحُ الصرفُ، وإذا كان ذلك؛ فسيقصُّون عليه نبأهم بالحقِّ، فلم يشمئزَّ نبيُّ الله داود من وعِظِهما له ولم يؤنِّبْهما، فقال أحدُهما: {إنَّ هذا أخي}: نصَّ على الأخوَّة في الدين أو النسب أو الصداقة؛ لاقتضائِها عدم البغي، وأن بغيَه الصادرَ منه أعظمُ من غيره، {له تسعٌ وتسعون نعجةً}؛ أي: زوجة، وذلك خير كثيرٌ يوجِبُ عليه القناعة بما آتاه الله، {ولي نعجةٌ واحدةٌ}، فطمع فيها، {فقال أكْفِلْنيها}؛ أي: دعها لي وخَلِّها في كفالتي، {وعَزَّني في الخطاب}؛ أي: غلبني في القول، فلم يزلْ بي حتى أدركها أو كادَ.
{23} Maana yake ni kwamba, ilijulikana mahasimu wawili hao walikuwa wamekusudia kufanyiwa haki iliyo wazi. Na ikiwa ndivyo hivyo, basi watamwambia habari zao kwa haki. Kwa hivyo, Nabii wa Mwenyezi Mungu, Daudi, hakuchukizwa na mawaidha waliyompa wala hakuwakemea kwa hilo.
Mmoja wao akasema: "Hakika huyu ni ndugu yangu" katika dini, au ukoo, au urafiki kwa sababu hayo yanamzuia kunidhulumu, au kwa sababu udhalimu anaoweza kufanya ni mkubwa zaidi kuliko mtu mwingine, "ana kondoo wa kike tisini na tisa;" yaani, wa kike. Ambalo ni jambo linalomlazimu kuridhika na alichompa Mwenyezi Mungu. "Na mimi ninaye kondoo wa kike mmoja tu" lakini akamtamani.
"Akasema: 'Nipe huyo nikufugie!' Na amenishinda kwa maneno." Na akaendelea hivyo mpaka akamchukua au akawa karibu mno kumchukua.
#
{24} فقال داود لما سمع كلامَه، ومن المعلوم من السياق السابق من كلامِهِما أنَّ هذا هو الواقع؛ فلهذا لم يحتج أن يتكلَّم الآخرُ؛ فلا وجهَ للاعتراض بقول القائل: لِمَ حَكَمَ داودُ قبل أن يسمعَ كلام الخصم الآخر؟ {لقد ظَلَمَكَ بسؤال نعجتِكَ إلى نعاجِهِ}: وهذه عادةُ الخُلَطاء والقرناءِ الكثير منهم، فقال: {وإنَّ كثيراً من الخُلَطاءِ لَيَبْغي بعضُهم على بعضٍ}: لأنَّ الظُّلم من صفة النفوس {إلاَّ الذين آمنوا وعملوا الصالحاتِ}: فإنَّ ما مَعَهم من الإيمان والعمل الصالح يمنعُهم من الظُّلم، {وقليلٌ ما هم}؛ كما قال تعالى: {وقليلٌ من عِبادي الشَّكُورُ}. {وظنَّ داودُ}: حين حَكَمَ بينَهما {أنَّما فَتَنَّاهُ}؛ أي: اختبرناه ودبَّرْنا عليه هذه القضيةَ ليتنبَّهَ، {فاسْتَغْفَرَ ربَّه}: لما صدر منه، {وخَرَّ راكعاً}؛ أي: ساجداً، {وأناب}: لله تعالى بالتوبة النصوح والعبادة.
{24} Daudi aliposikia maneno yake, akasema - na ilijulikana kutokana na muktadha wa maneno yake aliyosema hapo awali kwamba hayo ndiyo yaliyotokea hasa - kwa hivyo, hakuhitaji huyo mwengine kusema kitu,
na hakuna msingi wowote kwa yule anayeweza kusema: 'Kwa nini Daudi alihukumu kabla ya kusikia maneno ya yule hasimu mwengine?' "Kweli amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako mmoja kuongezea kwenye kondoo wake." Hii ndiyo desturi ya wengi wanaochanganya vitu vyao.
Na akasema: "Na hakika washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao," kwa sababu dhuluma ni sifa ya nafsi zote "isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema." Hao kuamini kwao na kutenda kwao mema kunawazuia kufanya dhuluma. "Na hao ni wachache,
" kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Ni wachache katika waja wangu ndio wanaoshukuru." "Na Daudi akajua," alipohukumu kati yao, "kuwa tumemfanyia mtihani" kwa kumletea tukio hili ili apate kutanabahi. "Basi akamwomba msamaha Mola wake Mlezi" kwa yale aliyoyafanya, "na akaanguka kusujudu na kutubia" kwa Mwenyezi Mungu, toba ya kweli na kumuabudu sawasawa.
#
{25} {فغفرنا له ذلك}: الذي صَدَرَ منه، وأكرمه الله بأنواع الكراماتِ، فقال: {وإنَّ له عندَنا لَزُلْفى}؛ أي: منزلة عالية وقربة منَّا، {وحسنَ مآبٍ}؛ أي: مرجع. وهذا الذنبُ الذي صَدَرَ من داود عليه السلام لم يَذْكُرْهُ الله لعدم الحاجةِ إلى ذكرِهِ؛ فالتعرُّضُ له من باب التكلُّف، وإنَّما الفائدةُ ما قصَّه الله علينا من لطفِهِ به وتوبتِهِ وإنابتِهِ وأنَّه ارتفع محلُّه فكان بعد التوبةِ أحسنَ منه قبلَها.
{25} "Basi tukamsamehe kwa hayo" aliyoyafanya, na Mwenyezi Mungu akamtukuza kwa baraka za kila aina.
Akasema: "Naye kwa hakika anao mkaribisho mkubwa na marejeo mazuri kwetu." Mwenyezi Mungu hakuitaja dhambi hii aliyoifanya Daudi, amani iwe juu yake, kwa sababu hapakuwa na haja ya kuitaja. Kwa hivyo, kutafuta kuijua ni katika kujisumbua bure tu. Faida ya kweli iko katika yale aliyotuelezea Mwenyezi Mungu ya upole wake juu yake, kutubia kwake, kurejea kwake kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba hadhi yake iliinuliwa juu kwa hivyo akawa bora zaidi yake baada ya kutubia.
#
{26} {يا داود إنَّا جَعَلْناكَ خليفةً في الأرض}: تنفِّذُ فيها القضايا الدينيَّةَ والدنيويَّةَ، {فاحْكُم بين الناسِ بالحقِّ}؛ أي: العدل، وهذا لا يتمكَّن منه إلا بعلم بالواجب وعلم بالواقع وقدرةٍ على تنفيذ الحقِّ، {ولا تَتَّبِع الهوى}: فتميل مع أحدٍ لقرابةٍ أو صداقةٍ أو محبةٍ أو بغضٍ للآخر، {فيضلَّك}: الهوى {عن سبيل الله}: ويخرِجَك عن الصراط المستقيم. {إنَّ الذين يَضِلُّون عن سبيل الله}: خصوصاً المتعمِّدين منهم {لهم عذابٌ شديدٌ بما نسوا يومَ الحسابِ}؛ فلو ذَكَروه ووقع خوفُهُ في قلوبِهِم؛ لم يَميلوا مع الهوى الفاتن.
{26} "Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi" ili uweze kutekeleza humo mambo ya kidini na ya kidunia. "Basi wahukumu watu kwa haki." Na hili haliwezi kupatikana ila kwa kujua wajibu wake na kujua kilichotokea hasa na kuwa na uwezo wa kutekeleza haki. "Wala usifuate matamanio" ukamuegemea mtu mmoja kwa sababu ya undugu, urafiki, upendo, au kwa sababu ya kumchukia huyo mwengine, "yakakupoteza" matamanio hayo "kwenye Njia ya Mwenyezi Mungu" iliyonyoooka. "Hakika wale wanaoipotea Njia ya Mwenyezi Mungu wakaiacha," haswa wale wafanyao makusudi, "watapata adhabu kali kwa sababu ya kusahau kwao Siku ya Hesabu." Kwani ikiwa wangeikumbuka siku hiyo na wakaihofu mioyoni mwao, basi hawangeegemea upande wa matamanio yao hayo yanayofitinisha.
{وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاءَ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا بَاطِلًا ذَلِكَ ظَنُّ الَّذِينَ كَفَرُوا فَوَيْلٌ لِلَّذِينَ كَفَرُوا مِنَ النَّارِ (27) أَمْ نَجْعَلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَالْمُفْسِدِينَ فِي الْأَرْضِ أَمْ نَجْعَلُ الْمُتَّقِينَ كَالْفُجَّارِ (28) كِتَابٌ أَنْزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ (29)}
27. Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yavyo bure. Hiyo ni dhana ya waliokufuru. Ole wao waliokufuru kwa Moto utakaowapata. 28. Je, tuwafanye walioamini na wakatenda mema kama wafanyao uharibifu katika nchi? Au tuwafanye wacha Mungu kama waovu? 29. Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili.
#
{27} يخبر تعالى عن تمام حكمتِهِ في خلقه السماواتِ والأرضَ، وأنَّه لم يخلُقْهما {باطلاً}؛ أي: عبثاً ولعباً من غير فائدةٍ ولا مصلحةٍ. {ذلك ظنُّ الذين كفروا}: بربِّهم حيث ظنُّوا ما لا يَليقُ بجلالِهِ. {فويلٌ للذين كَفَروا من النارِ}: فإنَّها التي تأخُذُ الحقَّ منهم وتَبْلُغُ منهم كلَّ مبلغ. وإنَّما خلق الله السماواتِ والأرض بالحقِّ وللحقِّ، فخلقهما لِيَعْلَمَ العبادُ كمالَ علمِهِ وقدرتِهِ وسعةَ سلطانه، وأنه تعالى وحدَه المعبودُ دون من لم يَخْلُقْ مثقال ذَرَّةٍ من السماواتِ والأرض، وأنَّ البعث حقٌّ، وسيفصِلُ الله بين أهل الخير والشرِّ، ولا يظنُّ الجاهل بحكمة الله أن يُسَوِّيَ الله بينهما في حكمه.
{27} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya ukamilifu wa hekima yake katika kuumba mbingu na ardhi, na kwamba hakuziumba "bure" kwa mchezo bila faida wala faida. "Hiyo ni dhana ya wale waliokufuru" juu ya Mola wao Mlezi walipomdhania yasiyoufailia utukufu wake. "Ole wao waliokufuru kwa Moto utakaowapata." Huo ndio utakaochukua haki kutoka kwao na uwafikie kiwango kikubwa zaidi. Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa haki na kwa ajili ya haki tu. Hilo ni ili waja wake wajue ukamilifu wa elimu yake, uwezo wake na upana wa mamlaka yake. Na kwamba Yeye Mtukufu pekee ndiye anayepaswa kuabudiwa mbali na hao ambao hawakuumba uzito wa chembe katika mbingu na ardhi. Na kwamba ufufuo ni haki. Na Mwenyezi Mungu atahukumu kati ya watu wema na watu waovu. Na mjinga yule asiyeijua hekima ya Mwenyezi Mungu asifikirie kwamba Mwenyezi Mungu atasawazisha yao katika hukumu yake.
#
{28} ولهذا قال: {أم نجعلُ الذين آمنوا وعَمِلوا الصالحاتِ كالمفسدينَ في الأرض أم نَجْعَلُ المتَّقينَ كالفجَّارِ}: هذا غيرُ لائقٍ بحكمتِنا وحكمِنا.
{28} Ndiyo maana akasema: "Je, tuwafanye wale walioamini na wakatenda mema kama wafanyao uharibifu katika nchi? Au tuwafanye wacha Mungu kama waovu?" Haya hayaifailii hekima yetu na hukumu yetu.
#
{29} {كتابٌ أنزلناه إليك مبارَكٌ}: فيه خيرٌ كثيرٌ وعلمٌ غزيرٌ، فيه كلُّ هدى من ضلالة وشفاء من داء ونور يُسْتَضاء به في الظُّلمات، وكلُّ حكم يحتاج إليه المكلَّفون، وفيه من الأدلَّة القطعيَّة على كلِّ مطلوب ما كان به أجَلَّ كتاب طَرَقَ العالَمَ منذ أنشأه الله، {لِيَدَّبَّروا آياتِهِ}؛ أي: هذه الحكمة من إنزاله؛ ليتدبَّر الناسُ آياتِهِ، فيستخرِجوا علمَها، ويتأمَّلوا أسرارها وحِكَمَها؛ فإنَّه بالتدبُّر فيه والتأمُّل لمعانيه وإعادة الفكر فيها مرةً بعد مرةٍ تُدْرَكُ بركتُهُ وخيرُهُ، وهذا يدلُّ على الحثِّ على تدبُّرِ القرآن، وأنَّه من أفضل الأعمال، وأنَّ القراءة المشتملة على التدبُّرِ أفضل من سرعةِ التلاوةِ التي لا يحصُلُ بها هذا المقصودُ، {ولِيَتَذَكَّرَ أولو الألبابِ}؛ أي: أولو العقول الصحيحة، يتذكَّرون بتدبُّرهم لها كلَّ علم ومطلوب. فدَّل هذا على أنه بحسب لُبِّ الإنسان وعقله يحصُلُ له التذكُّر والانتفاعُ بهذا الكتاب.
{29} "Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa." Ndani yake mna heri nyingi na elimu nyingi, na ndani yake mna kila uwongofu kutokana na upotofu na ponya kutokana na maradhi, na nuru inayotumika kuangazia gizani. Na kina kila hukumu wanayohitaji watu waliojukumishwa na sheria. Pia umo ushahidi mbalimbali wa kukata juu ya kila kinachotafutwa. Mambo ambayo yalikifanya kuwa Kitabu kitukufu zaidi kilichowahi kuja ulimwenguni tangu Mwenyezi Mungu alipouumba, "ili wazizingatie Aya zake." Na hii ndiyo hekima ya kuteremshwa kwake, ili watu waweze kutoa humo elimu zake na wazitafakari siri zake na hekima zake. Kwa kuizingatia na kutafakari maana zake mara kwa mara, zinadhihirika baraka zake na heri zake. Hili linaashiria suala la kutafakari Qur-ani na kwamba ni katika matendo bora zaidi, na kwamba kusoma kunakojumuisha kuitafakari ni bora kuliko kuisoma upesi bila ya kuizingatia, ambako hayapatikani makusudio haya. "Na wawaidhike wenye akili" sahihi. Hilo linaonyesha kwamba kulingana na werevu na akili ya mtu, atakumbuka na kufaidika na Kitabu hiki.
{وَوَهَبْنَا لِدَاوُودَ سُلَيْمَانَ نِعْمَ الْعَبْدُ إِنَّهُ أَوَّابٌ (30) إِذْ عُرِضَ عَلَيْهِ بِالْعَشِيِّ الصَّافِنَاتُ الْجِيَادُ (31) فَقَالَ إِنِّي أَحْبَبْتُ حُبَّ الْخَيْرِ عَنْ ذِكْرِ رَبِّي حَتَّى تَوَارَتْ بِالْحِجَابِ (32) رُدُّوهَا عَلَيَّ فَطَفِقَ مَسْحًا بِالسُّوقِ وَالْأَعْنَاقِ (33) وَلَقَدْ فَتَنَّا سُلَيْمَانَ وَأَلْقَيْنَا عَلَى كُرْسِيِّهِ جَسَدًا ثُمَّ أَنَابَ (34) قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي وَهَبْ لِي مُلْكًا لَا يَنْبَغِي لِأَحَدٍ مِنْ بَعْدِي إِنَّكَ أَنْتَ الْوَهَّابُ (35) فَسَخَّرْنَا لَهُ الرِّيحَ تَجْرِي بِأَمْرِهِ رُخَاءً حَيْثُ أَصَابَ (36) وَالشَّيَاطِينَ كُلَّ بَنَّاءٍ وَغَوَّاصٍ (37) وَآخَرِينَ مُقَرَّنِينَ فِي الْأَصْفَادِ (38) هَذَا عَطَاؤُنَا فَامْنُنْ أَوْ أَمْسِكْ بِغَيْرِ حِسَابٍ (39) وَإِنَّ لَهُ عِنْدَنَا لَزُلْفَى وَحُسْنَ مَآبٍ (40)}.
30. Na Daudi tukamtunukia Suleiman. Alikuwa mja mwema. Na hakika alikuwa mwingi wa kutubia. 31. Alipopelekewa jioni farasi wasimamao kidete, tayari kutoka shoti. 32.
Basi akasema: Navipenda vitu vizuri kwa kumkumbuka Mola wangu Mlezi. Kisha wakafichikana nyuma ya boma. 33.
(Akasema:) Nirudishieni! Akaanza kuwapapasa miguu na shingo. 34. Na tulimtia mtihanini Suleiman, na tukauweka mwili juu ya kiti chake, kisha akarejea kwa kutubu. 35.
Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usiomwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji. 36. Basi tukaufanya upepo umtumikie, ukenda kwa amri yake, popote alipotaka kufika. 37. Na tukayafanya mashetani yamtumikie, wote wajenzi na wapiga mbizi. 38. Na wengine wafungwao kwa minyororo. 39. Hichi ndicho kipawa chetu. Basi toa au zuia, bila ya hisabu. 40. Na hakika yeye kwetu Sisi ana cheo cha kukaribishwa kwetu, na pahala pazuri pa kurejea.
#
{30} لما أثنى الله تعالى على داودَ وذَكَرَ ما جرى له ومنه؛ أثنى على ابنِهِ سليمانَ عليهما السلام، فقال: {ووَهَبْنا لداودَ سليمانَ}؛ أي: أنْعَمْنا به عليه وأقررْنا به عينَه. {نعم العبدُ}: سليمانُ عليه السلام، فإنَّه اتَّصف بما يوجب المدح، وهو {إنَّه أوابٌ}؛ أي: رجاعٌ إلى الله في جميع أحوالِهِ بالتألُّه والإنابة والمحبَّة والذِّكر والدُّعاء والتضرُّع والاجتهاد في مرضاة الله وتقديمها على كل شيءٍ.
{30} Mwenyezi Mungu alipomsifu Daudi na kutaja yaliyompata kutoka kwake; akamsifu mwanawe Suleiman, amani iwe juu yao wawili,
akasema: "Na Daudi tukamtunukia Suleiman," na tukalifanya jicho lake kutua kwa ajili yake. Suleiman, amani ziwe juu yake, "alikuwa mja mwema" kwa sababu ya sifa nzuri alizokuwa nazo. "Na hakika alikuwa mwingi wa kutubia" na kurudi kwa Mungu katika hali zake zote kwa kumfanyia Yeye tu uungu, kumpenda, kumtaja, kumuomba dua, kumnyenyekea na kujitahidi katika mambo yanayomridhisha Mwenyezi Mungu na kuyatanguliza mbele ya kila kitu kingine.
#
{31 - 33} ولهذا؛ لما عُرِضَتِ [عليه] الخيل الجياد السبق {الصافناتُ}؛ أي: التي من وصفها الصُّفونُ، وهو رفع إحدى قوائِمِها عند الوقوف، وكان لها منظرٌ رائقٌ وجمالٌ معجبٌ، خصوصاً للمحتاج إليها؛ كالملوك؛ فما زالتْ تُعْرَضُ عليه حتى غابتِ الشمس في الحجاب، فألهتْه عن صلاة المساءِ وذِكْرِهِ، فقال ندماً على ما مضى منه، وتقرُّباً إلى الله بما ألهاه عن ذكرِهِ، وتقديماً لحبِّ الله على حبِّ غيره: {إنِّي أحببتُ حُبَّ الخيرِ}: وضمَّنَ أحببتُ معنى آثرتُ؛ أي: آثرتُ حبَّ الخير الذي هو المالُ عموماً وفي الموضع المرادُ الخيل {عن ذِكْرِ ربِّي حتى تَوارَتْ بالحجابِ. ردُّوها عليَّ}: فردُّوها، {فطَفِقَ}: فيها {مسحاً بالسُّوقِ والأعناقِ}؛ أي: جعل يعقِرُها بسيفِهِ في سوقِها وأعناقها.
{31 - 33} Ndiyo maana walipoletwa mbele yake farasi hao waendao shoti, "wasimamao kidete" na wakaonekana kwa mwonekano mzuri wa kupendeza, hasa kwa wale wanaowahitaji, kama vile wafalme, na wakaendelea kuletwa mbele yake mpaka jua lilipozama kwenye upeo wa macho, kwa hivyo wakamshughulisha asiswali swala ya jioni na kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Akasema akijutia hayo aliyoyafanya na akitaka kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa hayo yaliyomzuilia mbali kumkumbuka Mwenyezi Mungu.
Na akautanguliza upendo wa Mwenyezi Mungu mbele ya upendo wa wengineo: "Hakika mimi nimevipenda vitu vizuri" ambavyo ni mali kwa ujumla, na mahali hapa kilichokusudiwa ni farasi hao, "kuliko kumkumbuka Mola wangu Mlezi mpaka jua likapotelea kwenye upeo wa macho." "Warudisheni kwangu!" Basi wakawarudisha na "akaanza kuwapapasa miguu na shingo." Yaani, akaanza kuwachinja kwa kuwapiga kwa upanga wake kwenye miguu na shingo zao.
#
{34} {ولقد فتنَّا سليمانَ}؛ أي: ابتليْناه واختبرْناه بذَهابِ ملكِهِ وانفصالِهِ عنه بسبب خلل اقتضتْه الطبيعةُ البشريةُ، {وألقَيْنا على كرسيِّه جسداً}؛ أي: شيطاناً قضى الله وقَدَّر أن يجلسَ على كرسيِّ ملكِهِ ويتصرَّفَ في الملك في مدَّةِ فتنة سليمان، {ثم أنابَ}: سليمانُ إلى الله تعالى، وتابَ.
{34} "Na tulimtia katika mtihani Suleiman" kwa kumuondolea ufalme wake na kumuweka mbali nao, kwa sababu ya kosa alilofanya kulingana na maumbile ya asili ya kibinadamu. "Na tukauweka mwili juu ya kiti chake." Yaani shetani, ambaye Mwenyezi Mungu alipitisha na akamuweka kuketi juu ya kiti cha enzi cha ufalme wake na akawa anauendesha ufalme wake katika kipindi alichokuwa Suleiman ametiwa katika mtihani. "Kisha" Suleiman "akarejea" kwa Mwenyezi Mungu, na kutubu.
#
{35 - 39} فَـ {قَالَ ربِّ اغْفِرْ لي وَهَبْ لي مُلْكاً لا ينبغي لأحدٍ من بعدي إنَّك أنت الوهابُ}: فاستجاب الله له، وغفر له، وردَّ عليه مُلْكَه، وزادَه ملكاً لم يحصُلْ لأحدٍ من بعده، وهو تسخيرُ الشياطين له يبنونَ ما يريدُ ويغوصون له في البحر يستخرِجون الدُّرَّ والحُلِيَّ، ومَنْ عصاه منهم؛ قَرَّنَه في الأصفاد وأوثقه، وقلنا له: {هذا عطاؤنا}: فَقُرَّ به عيناً، {فامنُنْ}: على من شئتَ، {أو أمْسِكْ}: مَنْ شئتَ {بغير حسابٍ}؛ أي: لا حرج عليك في ذلك ولا حسابَ؛ لعلمه تعالى بكمال عدلِهِ وحسن أحكامِهِ.
{35 - 39} Kwa hivyo
(Suleiman) Akasema: "Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usiomwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji." Basi Mwenyezi Mungu akamuitikia, akamsamehe na akamrudishia ufalme wake, na akauzidishia ufalme wake ambao hakuwahi kumpa mtu yeyote baada yake. Na hilo lilikuwa kwa kumtiishia mashetani wakawa wanamjengea vitu apendavyo, na wanampigia mbizi baharini na kumtolea lulu na vito. Na anayemuasi miongoni mwao, anamfunga pamoja katika pingu.
Basi tulimwambia Suleiman: "Hiki ndicho kipawa chetu. Basi toa au zuia, bila ya hesabu." Hili ni kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu alijua ukamilifu wa uadilifu wake na uzuri wa hukumu zake.
#
{40} ولا تحسبنَّ هذا لسليمانَ في الدُّنيا دون الآخرة، بل له في الآخرة خيرٌ عظيمٌ، ولهذا قال: {وإنَّ له عندَنا لَزُلْفى وحسنَ مآبٍ}؛ أي: هو من المقرَّبين عند اللهِ المكرَمين بأنواع الكراماتِ لله.
{40} Wala kamwe usidhani kwamba Suleiman atapata haya katika dunia peke yake na si Akhera, bali anayo heri kubwa zaidi akhera.
Ndiyo maana akasema: "Na hakika yeye kwetu Sisi ana cheo cha kukaribishwa kwetu, na pahala pazuri pa kurejea." Kwani atakuwa miongoni mwa wale walio karibu mno na Mwenyezi Mungu, ambao atawatukuza aina mbalimbali za kutukuzwa.
Masuala mbalimbali Katika yale ambayo yametubainikia miongoni mwa faida na hekima katika kisa cha Daudi na Suleiman, amani iwe juu yao, ni kama ifuatavyo: Miongoni mwake ni kwamba, Mwenyezi Mungu Mtukufu anamhadithia Nabii wake Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, habari za wale waliokuwa kabla yake ili kuutia nguvu moyo wake na kuituliza nafsi yake. Na anamtajia katika ibada zao na ukubwa wa subira yao na kutubia kwao; jambo litakalomfanya kuwa na hamu ya kushindana nao na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu ambaye walijikurubisha kwake, na kuwa na subira juu ya maudhi ya kaumu yake. Ndipo Mwenyezi Mungu alipotaja mahali hapa yale aliyotaja kuhusu jinsi kaumu yake walivyomuudhi, na wakasema kumhusu yeye na yale aliyokuja nayo, akamuamrisha kuwa na subira, na kwamba amkumbuke mja wake Daudi ili ajiliwaze naye. Na miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anasifu na anapenda mtu kuwa na nguvu ya moyo na mwili katika kumtii. Kwani kutokana na hayo zinapatikana athari za utiifu, uzuri wake na wingi wake kiasi ambacho hakipatikani katika kuwa dhaifu. Na kwamba mja anapaswa kutafuta visababu vya kuwa na nguvu na wala asitegemee uvivu ambao unaweza kuidhoofisha nguvu yake na nafsi yake. Na miongoni mwake ni kwamba kurejea kwa Mwenyezi Mungu katika mambo yote, ni moja ya sifa za Mitume wa Mungu na sifa za viumbe wake maalumu, kama vile Mwenyezi Mungu alivyomsifu Daudi na Suleiman kwa hili. Basi na wawaige wale wanaoiga, na waongoke kwa uwongofu wao wale wanaofuata njia yao. Kwani "hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewaongoa, basi fuata uwongofu wao." Na miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu alimtukuza Nabii wake Daudi, amani ziwe juu yake, kwamba alikuwa na sauti nzuri na kubwa. Ambayo kwa sababu yake Mwenyezi Mungu aliifanya milima isiyosikia, na ndege mabubu wasiozungumza kumuitikia anapoirudia sauti yake kwa kumtukuza Mwenyezi Mungu, na wakawa wanamtukuza Mwenyezi Mungu pamoja naye jioni na asubuhi. Na miongoni mwake ni kwamba, miongoni mwa neema kubwa za Mwenyezi Mungu juu ya mja wake ni kumpa elimu yenye manufaa na kujua jinsi ya kuhukumu vyema na baina ya watu. Kama vile Mwenyezi Mungu alivyompa hayo mja wake Daudi, amani iwe juu yake. Na miongoni mwake ni utunzaji wa Mwenyezi Mungu kwa Mitume wake na watu wake walio safi, wanapofanya makosa kwa kuwapa majaribio na mitihani kwa kitu ambacho kitawaondolea kosa lao hilo, kisha wanarudi kwenye hali kamilifu zaidi kuliko hali yao ya kwanza. Kama ilivyomtokea Daudi na Suleiman, amani iwe juu yao. Na miongoni mwake ni kwamba Mitume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, wamehifadhiwa kutokana na kukosea katika yale wanayoyafikisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa sababu madhumuni ya ujumbe hayawezi kufikiwa bila hilo, lakini kwa mujibu wa maumbile yao ya kibinadamu wanaweza kufanya baadhi ya maasia, lakini Mwenyezi Mungu baadaye anawaweka mbali na hilo kwa upole wake. Na miongoni mwake ni kwamba Daudi, amani ziwe juu yake, katika hali zake nyingi alikuwa akikaa mahali pake pa kuswalia kwa ajili ya kumtumikia Mola wake Mlezi. Na ndiyo maana mahasimu wale wawili wakaipindukia mihrab yake na kuiangia humo. Kwa sababu alikuwa anapokuwa peke yake katika mihrab yake, haingii humo mtu yeyote. Kwa hivyo hakuwapa watu muda wake wote, licha ya hukumu nyingi zilizokuwa zikimjia. Bali alitenga muda wa kuwa peke yake na Mola wake Mlezi, ili jicho lake lifurahie kwa kumuabudu Yeye na kumsaidia kumkusudia Yeye tu katika mambo yake yote. Miongoni mwake ni kwamba mtu anapaswa kuwa na adabu anapoingia kwa watawala na wengineo. Kwa sababu mahasimu wale wawili walipoingia kwa Daudi katika hali isiyo ya kawaida na si kwa kupitia mlango wa kawaida; akawahofu sana kwa sababu yao, na akaona kwamba hilo halifai katika hali hiyo. Miongoni mwake ni kwamba hakimu hafai kuzuiliwa kuhukumu kwa haki, kwa sababu ya tabia mbaya za mahasimu na kufanya kwao yasiyofaa. Miongoni mwake ni ukailifu wa ustahamilivu wa Daudi, amani iwe juu yake. Kwani hakuwakasirikia walipomjia bila ruhusa, ilhali yeye ndiye mfalme, wala hakuwakemea wala kuwakaripia. Miongoni mwake ni kwamba aliyedhulumiwa anaruhusiwa kumwambia aliyemdhulumu: 'Umenidhulumu' au 'Ewe dhalimu!' Na kitu kama hicho au 'ewe uliyenivukia mipaka!' Hii ni kwa sababu walisema: "Sisi ni wagombanao wawili, mmoja wetu amemdhulumu mwenziwe." Miongoni mwake ni kwamba mtu akiwaidhiwa au akinasihiwa hata kama ana cheo kikubwa na elimu nyingi, hafai kukasirika au kuchukia, bali aharakishe kuikubali na kumshukuru. Kwa maana mahasimu wale wawili walimshauri Daudi, naye hakuchukizwa wala kukasirika. Na hilo halikumzuia kutenda haki, bali alihukumu kwa haki safi. Miongoni mwake ni kuchanganyika baina ya jamaa wa karibu na marafiki. Na wingi wa mafungamano yao ya kidunia na ya kimali husababisha uadui baina yao, na baadhi yao kuvukiana mipaka. Na kwamba jambo hilo haliepukiki isipokuwa kwa kumcha Mwenyezi Mungu na kuwa na subira juu ya mambo kwa kuwa na imani na kutenda matendo mema. Na hayo ndiyo matendo ambayo watu huyafanya kwa uchache zaidi. Miongoni mwake ni kuomba msamaha na ́kufanya ibaada, hasa swala. Ni katika mambo yanayofuta madhambi, kwa sababu Mwenyezi Mungu alimsamehe Daudi dhambi yake baada ya Daudi kumuomba msamaha na kusujudu. Miongoni mwake ni Mwenyezi Mungu kumtukuza mja wake Daudi na Suleiman kwa kuwaweka karibu naye na kuwalipa kwa uzuri, kwamba isidhaniwe kuwa kile walichofanya kiliwapunguzia hadhi yao mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hili ni kutokana na upole wake kamili kwa waja wake wanaomuelekea Yeye tu. Na kwamba anapowasamehe na kuwaondolea madhambi yao, pia zinaondoka athari zake zote zinazotokana nayo, hata yale yanayoingia katika nyoyo za viumbe. Kwa maana wanaposikia baadhi ya dhambi zao, inaingia kwenye nyoyo zao kwamba walishuka kutoka katika daraja lao la kwanza. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akaondoa athari hizi. Na hilo si jambo kubwa kwa Mkarimu wa wote, Mwingi wa kusamehe. Miongoni mwake ni kwamba kuhukumu baina ya watu ni daraja ya kidini waliyoichukua Mitume wa Mwenyezi Mungu na viumbe wake maalumu. Na kwamba kazi ya mtu anayesimamia hilo ni kuhukumu kwa haki na kujiepusha na matamanio. Kuhukumu kwa haki kunahitaji mtu kuwa na elimu ya mambo ya kisheria na kujua vyema namna lilivyo suala hilo analotaka kulitolea hukumu, na namna ya kuliingiza katika hukumu za kisheria. Kwa yule asiyejua lolote kati ya mambo mawili haya hafai kuhukumu wala haruhusiwi kukaribia kazi ya kutoa hukumu. Miongoni mwake ni kwamba hakimu anapaswa kujihadhari na matamanio yake na ayaweke maanani, kwani hakuna nafsi isiyokuwa na matamanio. Anapaswa kupambana na nafsi yake kwa kuifanya haki kuwa ndiyo makusudio yake. Na kwamba ajiondolee wakati wa kuhukumu kila upendo au chuki kwa yeyote miongoni mwa mahasimu walio mbele yake. Miongoni mwake ni kwamba Suleiman, amani iwe juu yake, alikuwa ni miongoni mwa fadhila alizopewa Daudi na mojawapo ya neema za Mwenyezi Mungu juu yake, ambapo alimtunukia mwana huyu. Na kwamba katika neema kubwa zaidi za Mwenyezi Mungu juu ya mja wake ni kumpa mtoto mwema. Ikiwa atakuwa mwenye elimu, hali hiyo itakuwa ni nuru juu ya nuru. Miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu alimsifu na kumtaja Suleiman kwa uzuri katika kauli yake: "Alikuwa mja mwema kabisa. Na hakika alikuwa mwingi wa kutubia." Miongoni mwake ni kwamba heri nyingi na wema kutoka kwa Mwenyezi Mungu, huwa kwa kuwaneemeshea matendo mema na maadili mema, kisha kuwasifu kwa hayo. Kwani Yeye ndiye Mwingi wa fadhila, Mpaji. Miongoni mwake ni Suleimani kuutanguliza upendo wa Mwenyezi Mungu mbele ya upendo wa kila kitu. Miongoni mwake ni kwamba kila kitu kinachomshughulisha mja akamsahau Mwenyezi Mungu, basi hicho ni kibaya na ni cha kulaumiwa. Basi mja anapaswa kuachana nacho na aelekee kwa kilicho na manufaa zaidi kwake. Miongoni mwake ni kanuni hii mashuhuri: 'Yeyote anayeacha kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamlipa jambo jema zaidi ya hicho.' Suleiman, amani iwe juu yake, aliwachinja farasi wale waendao shoti, wasimamao kidete, wapendezao nafsi, kwa sababu ya kuutanguliza upendo wa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akamlipa kitu bora zaidi kuliko hao; kwa kumtiishia upepo mwanana, laini. Ukawa unakwenda kwa amri yake popote anapotaka na anapokusudia. Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja, na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. Na akamtiishia mashetani waliokuwa na uwezo wa kufanya yale ambayo wanadamu hawawezi. Miongoni mwake ni kwamba hakuna mwengine atakayetiishiwa mashetani baada ya Suleiman, amani iwe juu yake. Miongoni mwake ni kwamba Suleimani, amani iwe juu yake, alikuwa Nabii na mfalme aliyekuwa akifanya anachotaka. Lakini hakuwa akitaka isipokuwa uadilifu, tofauti na Nabii mja. Huyo utashi wake huwa chini ya amri ya Mwenyezi Mungu; hafanyi kitu wala haachi isipokuwa kwa amri. Kama hali ya Nabii wetu, Muhammad, rehema na amani ziwe juu yake. Hii ndiyo hali kamili zaidi.
{وَاذْكُرْ عَبْدَنَا أَيُّوبَ إِذْ نَادَى رَبَّهُ أَنِّي مَسَّنِيَ الشَّيْطَانُ بِنُصْبٍ وَعَذَابٍ (41) ارْكُضْ بِرِجْلِكَ هَذَا مُغْتَسَلٌ بَارِدٌ وَشَرَابٌ (42) وَوَهَبْنَا لَهُ أَهْلَهُ وَمِثْلَهُمْ مَعَهُمْ رَحْمَةً مِنَّا وَذِكْرَى لِأُولِي الْأَلْبَابِ (43) وَخُذْ بِيَدِكَ ضِغْثًا فَاضْرِبْ بِهِ وَلَا تَحْنَثْ إِنَّا وَجَدْنَاهُ صَابِرًا نِعْمَ الْعَبْدُ إِنَّهُ أَوَّابٌ (44)}.
41.
Na mkumbuke mja wetu Ayubu alipomwita Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika Shetani amenifikishia udhia na adhabu. 42.
(Akaambiwa:) Piga-piga ardhi kwa mguu wako! Basi haya maji baridi ya kuogea na ya kunywa. 43. Na tukampa ahali zake na wengine kama wao pamoja nao, kuwa ni rehema itokayo kwetu, na iwe kumbusho kwa watu wenye akili. 44. Na shika kicha cha vijiti tu mkononi mwako, kisha ndio upigie nacho, wala usivunje kiapo. Hakika tulimkuta mwenye subira, mbora wa waja, kwa hakika alikuwa mwingi wa kutubu.
#
{41} أي: {واذكر}: في هذا الكتاب ذي الذكر {عبدَنا أيُّوبَ}: بأحسن الذِّكْر، وأثْنِ عليه بأحسن الثناء؛ حين أصابه الضُّرُّ فصبر على ضُرِّه، فلم يشتكِ لغير ربِّه، ولا لجأ إلاَّ إليه. فـ {نادى ربَّه}: داعياً، وإليه لا إلى غيره شاكياً، فقال: ربِّ {إنِّي مَسَّنِيَ الشيطانُ بِنُصْبٍ وعذابٍ}؛ أي: بأمر مُشِقٍّ متعبٍ معذبٍ، وكان سُلِّطَ على جسدِهِ فنفخ فيه حتى تقرَّحَ ثم تقيَّحَ بعد ذلك، واشتدَّ به الأمر، وكذلك هلك أهلُه ومالُه.
{41} Yaani, "na mkumbuke" katika Kitabu hiki chenye Ukumbusho "mja wetu Ayubu" kwa ukumbusho bora kabisa, na msifu kwa sifa njema kabisa; yalipomfika madhara, lakini akayavumilia madhara hayo, na wala hakumlalamikia asiyekuwa Mola wake Mlezi, na wala hakukimbilia isipokuwa kwake tu. "Alipomwita Mola wake Mlezi" akimwomba na kumlalamikia Yeye tu,
akasema: "Kwa hakika Shetani amenifikishia udhia na adhabu." Na alikuwa amepewa ugonjwa kwenye mwili wake ambapo ulikuwa ukivimba vidonda na kupasuka. Na jambo hilo likawa gumu zaidi kwake, na pia familia yake na mali yake vikaangamia.
#
{42} فقيل له: {اركُضْ برِجْلِكَ}؛ أي: اضربِ الأرض بها؛ لينبعَ لك منها عينٌ تغتسلُ منها وتشربُ، فيذهب عنك الضرُّ والأذى، ففعل ذلك، فذهب عنه الضرُّ وشفاه الله تعالى.
{42} Kisha akaambiwa: "Piga-piga ardhi kwa mguu wako!" Ili itokee chemchemi ambamo utaweza kuoga na kunywa, ili udhia na madhara hayo yakuondoke.
#
{43} {ووهَبْنا له أهلَه}: قيل: إنَّ الله تعالى أحياهم له {ومثلَهُم معهم}: في الدنيا، وأغناه الله وأعطاه مالاً عظيماً، {رحمةً منَّا}: بعبدنا أيوبَ حيث صَبَرَ فأثبناه من رحمتنا ثواباً عاجلاً وآجلاً. {وذِكرى لأولي الألبابِ}؛ أي: وليتذكَّر أولو العقول بحالةِ أيُّوب ويعتبِروا فيعلموا أنَّ مَنْ صَبَرَ على الضُّرِّ؛ فإنَّ الله تعالى يُثيبه ثواباً عاجلاً وآجلاً ويستجيبُ دعاءه إذا دعاه.
{43} "Na tukampa ahali zake." Ilisemwa kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alimhuishia ahali zake wa kitambo "na wengine kama wao pamoja nao" hapa duniani. Na Mwenyezi Mungu akamtajirisha na kumpa mali nyingi sana; "Kuwa ni rehema itokayo kwetu," kwa mja wetu Ayubu ambapo alisubiri, basi tukamlipa kutokana na rehema yetu malipo ya hivi sasa na ya baadaye. "Na iwe ukumbusho kwa watu wenye akili" kutokana na hali hii ya Ayubu na waizingatie na wajue kwamba yeyote mwenye subira juu ya udhia na madhara, basi Mwenyezi Mungu atamlipa malipo ya sasa na ya baadaye, na atamuitikia dua zake anapomwomba.
#
{44} {وخُذْ بيدِكَ ضِغْثاً}؛ أي: حزمة شماريخ، {فاضْرِبْ به ولا تَحْنَثْ}: قال المفسِّرون: وكان في مرضه وضُرِّه قد غضب على زوجتِهِ في بعض الأمور، فحلف لئن شفاهُ الله ليضرِبَنَّها مائةَ جلدةٍ، فلمَّا شفاه الله، وكانت امرأتُه صالحةً محسنةً إليه؛ رحمها الله ورحمه، فأفْتاه أن يضرِبَها بِضِغْثٍ فيه مائةُ شمراخ ضربةً واحدةً فيبَرَّ في يمينه. {إنا وجَدْناه}؛ أي: أيوب {صابراً}؛ أي: ابتليناه بالضُّرِّ العظيم فصبر لوجه الله تعالى. {نعم العبدُ}: الذي كَمَّلَ مراتبَ العبوديَّة في حال السرَّاءِ والضرَّاءِ والشدَّة والرَّخاء، {إنَّه أوابٌ}؛ أي: كثير الرجوع إلى الله في مطالبه الدينيَّة والدنيويَّة، كثير الذِّكْرِ لربِّه والدعاء والمحبة والتألُّه.
{44} "Na shika kicha cha vijiti tu mkononi mwako, kisha ndio upigie nacho, wala usivunje kiapo.
" Wafasiri walisema: Wakati wa maradhi yake na dhiki yake hii, alikuwa amemkasirikia mkewe katika baadhi ya mambo, kwa hivyo akaapa kwamba Mwenyezi Mungu akimponya, lazima atampiga mijeledi mia moja. Basi Mwenyezi Mungu alipomponya, na mkewe huyo alikuwa mwema na alikuwa akimfanyia uzuri. Mwenyezi Mungu akamrehemu mkewe huyu na pia akamrehemu Ayubu. Kwa hivyo akamtolea hukumu kwamba ampige kwa kicha cha vijiti mpigo mmoja tu, na kwa hilo atakuwa ameshatimiza kiapo chake. "Hakika tulimkuta ni mwenye subira." Ambapo tulimpa mtihani wa balaa kubwa, lakini akavumilia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. "Mbora wa waja," kwani alikamilisha viwango vya kumuabudu Mwenyezi Mungu katika nyakati nzuri na nyakati mbaya, katika dhiki na wepesi. "Kwa hakika alikuwa mwingi wa kutubu," na kumrudia Mwenyezi Mungu katika matakwa yake ya kidini na ya kidunia. Na alikuwa mwingi wa kumtaja Mola wake Mlezi, mwingi wa kumuomba dua, mwenye upendo mkubwa kwake, na mwingi wa kumfanyia Yeye tu uungu.
{وَاذْكُرْ عِبَادَنَا إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ أُولِي الْأَيْدِي وَالْأَبْصَارِ (45) إِنَّا أَخْلَصْنَاهُمْ بِخَالِصَةٍ ذِكْرَى الدَّارِ (46) وَإِنَّهُمْ عِنْدَنَا لَمِنَ الْمُصْطَفَيْنَ الْأَخْيَارِ (47)}.
45. Na wakumbuke waja wetu, Ibrahim na Is-haqa na Yaa'qubu waliokuwa na nguvu na busara. 46. Sisi tumewahusisha wao kwa sifa ya ukumbusho wa Akhera. 47. Na hakika wao kwetu sisi ni wateuliwa walio bora.
#
{45} يقول تعالى: {واذْكُرْ عِبَادَنا}: الذين أخلصوا لنا العبادةَ ذكراً حسناً {إبراهيم}: الخليل {و} ابنه {إسحاقَ} وابن ابنه {يعقوب أولي الأيدي}؛ أي: القوَّة على عبادة اللَّه تعالى، {والأبصار}؛ أي: البصيرة في دين اللَّه. فوصَفَهم بالعلم النافع والعمل الصالح الكثير.
{45} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na wakumbuke waja wetu" waliokuwa wakitufanyia Sisi tu ibada. Na uwataje kwa utajo mzuri "Ibrahim," mwandani wa Mwenyezi Mungu, na mwanawe "Is-haqa" na mwana wa mwanawe, "Yaa'qubu, waliokuwa na nguvu" za kumwabudu Mwenyezi Mungu, "na busara" katika mambo ya dini ya Mwenyezi Mungu. Hapa, Mwenyezi Mungu amewaelezea kwamba wana elimu yenye manufaa na matendo mema mengi.
#
{46} {إنَّا أخْلَصْنَاهم بخالصةٍ}: عظيمة وخصيصةٍ جسيمةٍ، وهي: {ذِكْرى الدارِ}: جعلنا ذكرى الدارِ الآخرةِ في قلوبهم والعملَ لها صفوةَ وقتِهِم. والإخلاصُ والمراقبةُ لله وَصْفُهُمُ الدائمُ، وجَعَلْناهم ذكرى الدار، يتذكَّر بأحوالِهِم المتذكِّرُ ويعتبرُ بهم المعتبِرُ، ويُذْكَرونَ بأحسن الذِّكر.
{46} "Sisi tumewafanya kuwa maalumu kwa sifa" kubwa, ambayo ni "kuikumbuka Akhera" katika nyoyo zao na kuifanyia kazi katika nyakati zao bora. Hii sifa ya kumkusudia Mwenyezi Mungu tu na kumchinga katika mambo yao ndiyo ilikuwa sifa yao ya kudumu. Pia tumewafanya kuwa ni kukumbusha wengine nyumba ya Akhera kwa kukumbuka hali zao wenye kukumbuka, na pia wenye kuzingatia kuzizingatia hali zao, na kuwataja kwa utajo mzuri zaidi.
#
{47} {وإنَّهم عندنا لَمِنَ المُصْطَفَيْنَ}: الذين اصطفاهم الله من صفوة خلقه {الأخيار}: الذين لهم كلُّ خُلُق كريم وعمل مستقيم.
{47} "Na hakika wao kwetu sisi ni wateuliwa" ambao Mwenyezi Mungu aliwateuwa na ambao ni katika viumbe wake watukufu zaidi, "waliobora." Ambao wana kila tabia njema na matendo yaliyonyooka.
#
{48} أي: واذكر هؤلاء الأنبياء بأحسن الذِّكْر، وأثنِ عليهم أحسن الثناء؛ فإنَّ كلاًّ منهم من الأخيار، الذين اختارهم الله من الخلق، واختار لهم أكمل الأحوال من الأعمال والأخلاق والصفاتِ الحميدةِ والخصال السديدةِ.
{48} Yaani, wakumbuke Manabii hawa kwa ukumbusho bora kabisa, na uwasifu kwa sifa njema kabisa. Kwa maana kila mmoja wao ni katika walio bora, ambao Mwenyezi Mungu aliwachagua katika viumbe wake na akawachagulia hali kamilifu kabisa za matendo, maadili mema, sifa nzuri na mambo yaliyonyooka sawasawa.
#
{49} هذا؛ أي: ذِكْرُ هؤلاء الأنبياء الصفوة، وذِكْر أوصافهم {ذِكْرٌ}: في هذا القرآن ذي الذكر، يَتَذَكَّرُ بأحوالهم المتذكِّرون، ويشتاقُ إلى الاقتداء بأوصافهم الحميدةِ المقتدونَ، ويُعَرفُ ما منَّ الله عليهم به من الأوصاف الزكيَّة، وما نَشَرَ لهم من الثناء بين البريَّة. فهذا نوعٌ من أنواع الذكر، وهو ذكر أهل الخير.
{49} Hili la kuwakumbuka Manabii hawa wakubwa, na kutaja sifa zao "ni ukumbusho" ulioko katika Qur-ani hii yenye ukumbusho. Wenye kukumbuka wanakumbuka kwa hali zao, na wenye kuiga wana hamu kubwa sana ya kuiga sifa zao za kusifika. Na zinajulikana neema alizowapa Mwenyezi Mungu za safi takatifu, ambazo ziliwafanya kusifiwa mbele ya viumbe wote. Hii ni aina moja miongoni mwa aina mbalimbali za ukumbusho, ambayo ni kuwakumbuka watu wema.
Na miongoni mwa aina za kukumbuka, ni kukumbuka malipo ya watu wema na watu waovu. Na ndiyo maana akasema:
{وَإِنَّ لِلْمُتَّقِينَ لَحُسْنَ مَآبٍ (49) جَنَّاتِ عَدْنٍ مُفَتَّحَةً لَهُمُ الْأَبْوَابُ (50) مُتَّكِئِينَ فِيهَا يَدْعُونَ فِيهَا بِفَاكِهَةٍ كَثِيرَةٍ وَشَرَابٍ (51) وَعِنْدَهُمْ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ أَتْرَابٌ (52) هَذَا مَا تُوعَدُونَ لِيَوْمِ الْحِسَابِ (53) إِنَّ هَذَا لَرِزْقُنَا مَا لَهُ مِنْ نَفَادٍ (54)}
49. Huu ni ukumbusho. Na hakika wacha Mungu wana marudio mazuri. 50. Bustani za milele zitakazofunguliwa milango yao kwa ajili yao. 51. Humo wataegemea matakia, wawe wanaagiza humo matunda mengi na vinywaji. 52. Na pamoja nao wake zao wenye kutuliza macho, hirimu zao. 53. Haya ndiyo mliyoahidiwa kwa Siku ya Hisabu. 54. Hakika hii ndiyo riziki yetu isiyomalizika.
#
{49} أي: {وإنَّ للمتقين}: ربَّهم؛ بامتثال الأوامر واجتناب النواهي من كلِّ مؤمن ومؤمنة {لَحُسْنَ مآبٍ}؛ أي: لمآباً حسناً ومرجعاً مستحسناً.
{49} Yaani, "Na hakika wanaomcha Mungu," Mola wao Mlezi, kwa kutii amri zake na kujiepusha na makatazo yake miongoni mwa Muumini wa kiume na wa kike, "wana marudio mazuri."
#
{50} ثم فسَّره وفصَّله فقال: {جناتِ عدنٍ}؛ أي: جنات إقامةٍ لا يبغي صاحبها بدلاً منها من كمالها وتمام نعيمها، وليسوا بخارجين منها ولا بمُخْرَجينَ، {مفتَّحةً لهم الأبوابُ}؛ أي: مفتحة لأجلهم أبوابُ منازِلِها ومساكِنِها، لا يحتاجونَ أن يَفْتَحوها هم، بل هم مخدومونَ، وهذا دليلٌ أيضاً على الأمان التامِّ، وأنَّه ليس في جناتِ عدنٍ ما يوجِبُ أن تُغَلَّقَ لأجلِهِ أبوابُها.
{50} Kisha akayafafanua akisema: "Bustani za milele" ambazo aliyemo hawezi kutaka kubadilishiwa apewe zingine kwa sababu ya ukamilifu wake na neema yake kamili, wala hawatatoka humo wala hawatatolewa. "Zitazofunguliwa milango yao kwa ajili yao." Wao wenyewe hawataifungua, bali watakuwa wanahudumiwa tu. Huu pia ni ushahidi kwamba watakuwa na usalama kamili, na kwamba hakuna kitu katika Bustani hizo za milele kitakachohitaji milango yake ifungwe.
#
{51} {متكئين فيها}: على الأرائك المزيَّنات والمجالس المزخرفات. {يَدْعون فيها}؛ أي: يأمرون خدَّامهم أن يأتوا {بفاكهةٍ كثيرةٍ وشرابٍ}: من كلِّ ما تشتهيه نفوسُهم وتلذُّه أعينُهم، وهذا يدلُّ على كمال النعيم وكمال الراحة والطُّمأنينة وتمام اللَّذَّة.
{51} "Humo wataegemea" juu ya makochi yaliyopambwa na mabaraza yaliyorembeshwa. "Wawe wanaagiza humo" watumishi wao kuwaletea "matunda mengi na vinywaji," miongoni mwa kila kitu ambacho nafsi zao zinakitamani na macho yao yanafurahia. Hili linaashiria furaha yao kamili, raha kamili, utulivu na ladha kamili.
#
{52} {وعندَهم}: من أزواجهم الحور العين {قاصراتُ} طرفهن على أزواجهنَّ، وطَرْفِ أزواجهنَّ عليهنَّ لجمالهم كلِّهم ومحبَّة كلٍّ منهما للآخر وعدم طموحِهِ لغيره، وأنَّه لا يبغي بصاحبه بدلاً ولا عنه عِوَضاً، {أترابٌ}؛ أي: على سنٍّ واحدٍ، أعدل سنِّ الشباب وأحسنُه وألذُّه.
{52} "Na pamoja nao wake zao wenye kutuliza macho" wakiwaangalia waume wao tu, nao waume wao wakiwaangalia wao tu kwa sababu ya uzuri wao wote na upendo wa kila mmoja wao kwa mwenzake, bila ya kumtaka mwengine na bila ya kutaka kupewa yeyote badala ya mwenza wake huyo. "Hirimu zao," walio katika umri mzuri zaidi, umri wa ujana wenye kufurahisha zaidi.
#
{53} {هذا ما توعَدونَ}: أيُّها المتَّقونَ {ليوم الحسابِ}: جزاء على أعمالِكُم الصالحة.
{53} "Haya ndiyo mliyoahidiwa" enyi wacha Mungu, "kwa Siku ya Hesabu," yawe malipo kwa matendo yenu mema.
#
{54} {إنَّ هذا لرِزْقُنا}: الذين أوردناه على أهل دار النعيم {ما له من نفادٍ}؛ أي: انقطاع، بل هو دائمٌ مستقرٌّ في جميع الأوقات، متزايدٌ في جميع الآنات، وليس هذا بعظيم على الربِّ الكريم، الرءوف الرحيم، البَرِّ الجواد، الواسع الغني، الحميد اللطيف، الرحمن، الملك الديان، الجليل الجميل المنان، ذي الفضل الباهر والكرم المتواتر، الذي لا تُحصى نعمُه ولا يُحاط ببعض بِرِّه.
{54} "Hakika hii ndiyo riziki yetu" tuliyowapa wakazi wa maskani ya neema "isiyomalizika," bali itadumu wakati wote na kuongezeka kila wakati. Hii si kubwa kwa Mola Mlezi, Mkarimu, Mpole, Mwingi wa kurehemu, Mwema, atoaye kwa wingi, Mwenye wasaa, Mkwasi, Msifiwa, Mjua siri, Mwingi wa rehema, Mfalme, Mlipaji, Mtukufu, Mzuri, Mwenye fadhila ya kushangaza, Mwenye ukarimu wa kuendelea, ambaye neema zake hazihesabiki wala hata baadhi ya wema wake hauwezi kudhibitiwa na yeyote.
{هَذَا وَإِنَّ لِلطَّاغِينَ لَشَرَّ مَآبٍ (55) جَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا فَبِئْسَ الْمِهَادُ (56) هَذَا فَلْيَذُوقُوهُ حَمِيمٌ وَغَسَّاقٌ (57) وَآخَرُ مِنْ شَكْلِهِ أَزْوَاجٌ (58) هَذَا فَوْجٌ مُقْتَحِمٌ مَعَكُمْ لَا مَرْحَبًا بِهِمْ إِنَّهُمْ صَالُو النَّارِ (59) قَالُوا بَلْ أَنْتُمْ لَا مَرْحَبًا بِكُمْ أَنْتُمْ قَدَّمْتُمُوهُ لَنَا فَبِئْسَ الْقَرَارُ (60) قَالُوا رَبَّنَا مَنْ قَدَّمَ لَنَا هَذَا فَزِدْهُ عَذَابًا ضِعْفًا فِي النَّارِ (61) وَقَالُوا مَا لَنَا لَا نَرَى رِجَالًا كُنَّا نَعُدُّهُمْ مِنَ الْأَشْرَارِ (62) أَتَّخَذْنَاهُمْ سِخْرِيًّا أَمْ زَاغَتْ عَنْهُمُ الْأَبْصَارُ (63) إِنَّ ذَلِكَ لَحَقٌّ تَخَاصُمُ أَهْلِ النَّارِ (64)}.
55. Ndiyo hivi! Na hakika wenye kuasi bila ya shaka watapata marudio maovu kabisa; 56. Nayo ni Jahannamu! Wataingia humo. Nacho hicho ni kitanda kiovu mno cha kulalia. 57. Ndiyo hivi! Basi na wayaonje maji ya moto na ya usaha! 58. Na adhabu nyenginezo za namna hii. 59. Hili ndilo kundi litakalo ingia pamoja nanyi. Hapana makaribisho mema kwao. Hakika hao wanaingia Motoni. 60.
Waseme: Lakini nyinyi! Hamna mapokezi mazuri! Nyinyi ndio mliotusabibisha haya, napo ni pahala paovu kabisa! 61.
Waseme: Mola wetu Mlezi aliyetusabibisha haya, mzidishie adhabu mara mbili Motoni. 62.
Watasema: Tuna nini hata hatuwaoni wale watu ambao tukiwahisabu ndio katika waovu? 63. Tulikosea tulipowafanyia masihara, au macho yetu tu hayawaoni? 64. Hakika hayo bila ya shaka ndiyo mahasimiano ya watu wa Motoni.
#
{55} {هذا} الجزاء للمتَّقين ما وصفناه، {وإنَّ للطَّاغين}؛ أي: للمتجاوزين للحدِّ في الكفر والمعاصي {لَشَرَّ مآبٍ}؛ أي: لشرَّ مرجع ومُنْقَلَبٍ.
{55} "Ndivyo hivi," yatakavyokuwa malipo ya wacha Mungu kama tulivyowaelezea. "Na hakika wenye kuasi" kwa ukafiri na maasia, "bila ya shaka watapata marudio maovu kabisa."
#
{56} ثم فَصَّلَه فقال: {جَهَنَّم}: التي جمع فيها كلَّ عذاب واشتدَّ حرُّها وانتهى قرُّها {يَصْلَوْنها}؛ أي: يعذَّبون فيها عذاباً يحيطُ بهم من كل وجهٍ، لهم من فوقهم ظلل من النار ومن تحتهم ظلل. {فبئس المِهادُ}: المعدُّ لهم مسكناً ومستقرًّا.
{56} Kisha akayafafanua akisema: "Jahannamu," ambayo humo zimekusanywa adhabu zote na ambayo joto lake ni kali mno, "wataingia humo" ili waadhibiwe kwa adhabu itakayowazunguka kutokea kila upande. Yatawekwa matabaka ya moto juu yao na chini yao. "Basi ndipo mahali pabaya mno pa kupumzikia" ambapo wameandaliwa yawe makao yao na mahali pa kukaa.
#
{57} {هذا}: المهاد، هذا العذاب الشديد والخزي والفضيحة والنَّكالُ. {فَلْيَذوقوهُ حميمٌ}: ماءٌ حارٌّ قد اشتدَّ حرُّه، يشربونه فيقطِّع أمعاءهم، {وغَسَّاقٌ}: وهو أكرهُ ما يكون من الشرابِ من قيح وصديدٍ، مرِّ المذاق، كريه الرائحة.
{57} "Ndivyo hivi," Itawapata adhabu kali, hizaya, fedheha na mateso. "Basi na wayaonje maji ya moto!" Watakapoyanywa maji hayo, yatayakata matumbo yao," na ya usaha" wenye harufu mbaya mno.
#
{58} {وآخرُ من شكلِهِ}؛ أي: من نوعه {أزواجٌ}؛ أي: عدَّة أصناف من أصناف العذاب، يعذَّبون بها ويُخْزَوْنَ بها.
{58} "Na adhabu nyinginezo za namna hii," ambazo wataadhibiwa na kuhiziwa kwazo.
#
{59 - 60} وعند توارُدِهِم على النار يشتُمُ بعضُهم بعضاً ويقول بعضُهم لبعضٍ: {هذا فوجٌ مقتحمٌ معكم}: النار {لا مرحباً بهم إنَّهم صالوا النار. قالوا}؛ أي: الفوج المقبِلُ المقتحم: {بل أنتُم لا مرحباً بكم أنتم قدَّمْتُموه}؛ أي: العذاب {لنا}: بدعوتِكُم لنا وفِتْنَتِكم وإضْلالِكُم وتسبُّبكم. {فبئس القرارُ}: قرار الجميع قرار السَّوْء والشرِّ.
{59 - 60} Na wanapofika kwenye Moto,
watatukanana na wataambiana: "Hili ndilo kundi litakaloingia pamoja nanyi" Motoni. "Hapana makaribisho mema kwao. Hakika hao wanaingia Motoni.
" "Waseme: Lakini nyinyi! Hamna mapokezi mazuri! Nyinyi ndio mliotusababishia haya." Kwani mlitulingania, mkatutia katika majaribu, mkatupoteza. "Napo ni pahala paovu kabisa pa kukaa!"
#
{61} ثم دعوا على المغوين لهم: {قالوا ربَّنا مَن قَدَّمَ لنا هذا فَزِدْهُ عذاباً ضِعْفاً في النارِ}. وقال في الآية الأخرى: {قال لِكُلٍّ ضعفٌ ولكن لا تعلمون}.
{61} Kisha wakawaapiza wale waliowahadaa,
"Waseme: Mola wetu Mlezi aliyetusababishia haya, mzidishie adhabu mara mbili Motoni." Na alisema katika aya nyingine,
"Akasema: Itakuwa kwenu nyote maradufu, lakini nyinyi hamjui tu."
#
{62} {وقالوا}: وهم في النار: {ما لَنا لا نرى رِجالاً كُنَّا نعدُّهم من الأشرارِ}؛ أي: كنَّا نزعُمُ أنَّهم من الأشرارِ المستحقِّين لعذاب النار، وهم المؤمنون، تَفَقَّدَهُم أهلُ النار قبَّحَهم الله؛ هل يَرَوْنَهم في النار؟
{62} "Na watasema" ilhali wako Motoni: "Tuna nini hata hatuwaoni wale watu ambao tukiwahesabu ndio katika waovu?" Ambao walistahiki adhabu ya Motoni, yaani waumini. Wakazi wa Motoni watawatafuta ili waone ikiwa wao pia ni watu wa Motoni.
#
{63} {أتَّخَذْناهُم سِخْرِيًّا أم زاغَتْ عنهُمُ الأبصارُ}؛ أي: عدم رؤيتنا لهم دائرٌ بين أمرينِ: إمَّا أنَّنا غالِطونَ في عدِّنا إيَّاهم من الأشرارِ، بل هم من الأخيارِ، وإنَّما كلامُنا لهم من باب السُّخرية والاستهزاء بهم، وهذا هو الواقع؛ كما قال تعالى لأهل النار: {إنَّه كان فريقٌ من عِبادي يقولون رَبَّنا آمَنَّا فاغْفِرْ لنا، وارْحَمْنا وأنت خيرُ الراحمين. فاتَّخَذْتُموهم سِخْريًّا حتى أنْسَوْكُم ذِكْري وكنتُم منهم تضحكونَ}.
والأمرُ الثاني: أنَّهم لعلَّهم زاغتْ أبصارُنا عن رؤيتهم معنا في العذاب، وإلاَّ؛ فهم معنا معذَّبون، ولكن تجاوزَتْهُم أبصارُنا! فيُحتمل أنَّ هذا الذي في قلوبهم، فتكون العقائدُ التي اعتقدوها في الدُّنيا وكثرة ما حكموا لأهل الإيمان بالنار تمكَّنتْ من قلوبِهم وصارتْ صبغةً لها، فدخلوا النار وهم بهذه الحالة، فقالوا ما قالوا.
ويُحتمل أنَّ كلامَهم هذا كلامُ تمويهٍ؛ كما موَّهوا في الدُّنيا موَّهوا حتى في النار، ولهذا يقول أهلُ الأعراف لأهل النار: {أهؤلاء الذين أقْسَمْتُم لا ينالُهُمُ الله برحمةٍ، ادْخُلوا الجنةَ لا خوفٌ عليكم ولا أنتم تحزنونَ}.
{63} "Tulikosea tulipowafanyia masihara,
au macho yetu tu hayawaoni?" Yaani kutowaona kwetu kunatokana na mambo mawili: ima tulikosea katika kuwazingatia kwamba ni waovu, ilhali kwa hakika wao ni miongoni mwa wema, lakini tukawaita hivyo tu kwa njia ya kuwakejeli. Na huu ndio ukweli,
kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema kuhusu watu wa Motoni: "Bila ya shaka lilikuwepo kundi katika waja wangu likisema: Mola wetu Mlezi! Tumeamini, basi tusamehe na uturehemu, nawe ndiwe Mbora wa wanaorehemu. Lakini nyinyi mliwakejeli hata wakakusahaulisheni kunikumbuka, na mlikuwa mkiwacheka." Jambo la pili ni kwamba pengine macho yetu yamekengeuka na hatuwezi kuwaona pamoja nasi Motoni. Vinginevyo, wanapaswa kuwa pamoja nasi wakiadhibiwa, lakini ni macho yetu ambayo hayawaoni. Inawezekana kwamba hayo ndiyo yaliyomo katika nyoyo zao. Kwa hivyo itikadi hiyo waliyoiitakidi duniani na wakawahukumu waumini kwamba wataingia Motoni, ilibakia madhubuti katika mioyo yao na ikawa ndiyo rangi yake. Basi wakaingia Motoni wakiwa katika hali hii, ndiyo maana wakasema hayo waliyosema. Na inawezekana kwamba maneno yao haya ni ya kuficha haki, kama walivyoificha duniani. Na ndiyo maana watu wa Al-
A`raf wakawaambia watu wa Motoni: "Je, hawa sio wale mliokuwa mkiwaapia kuwa Mwenyezi Mungu hatawafikishia rehema? Ingieni Peponi, hapana khofu kwenu, wala hamtahuzunika!"
#
{64} قال تعالى مؤكِّداً ما أخبر به، وهو أصدقُ القائلين: {إنَّ ذلك}: الذي ذكرتُ لكم {لَحَقٌّ}: ما فيه شكٌّ ولا مِرْيةٌ {تخاصُمُ أهل النارِ}.
{64} Amesema Mwenyezi Mungu, akisisitiza yale aliyojulisha,
naye ndiye mkweli zaidi wa wasemao: "Hakika hayo" niliyokutajieni "bila ya shaka ndiyo mahasimiano ya watu wa Motoni," yasiyokuwa na shaka yoyote.
{قُلْ إِنَّمَا أَنَا مُنْذِرٌ وَمَا مِنْ إِلَهٍ إِلَّا اللَّهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ (65) رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا الْعَزِيزُ الْغَفَّارُ (66) قُلْ هُوَ نَبَأٌ عَظِيمٌ (67) أَنْتُمْ عَنْهُ مُعْرِضُونَ (68) مَا كَانَ لِيَ مِنْ عِلْمٍ بِالْمَلَإِ الْأَعْلَى إِذْ يَخْتَصِمُونَ (69) إِنْ يُوحَى إِلَيَّ إِلَّا أَنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُبِينٌ (70) إِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِنْ طِينٍ (71) فَإِذَا سَوَّيْتُهُ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِنْ رُوحِي فَقَعُوا لَهُ سَاجِدِينَ (72) فَسَجَدَ الْمَلَائِكَةُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ (73) إِلَّا إِبْلِيسَ اسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ (74) قَالَ يَاإِبْلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَنْ تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ أَسْتَكْبَرْتَ أَمْ كُنْتَ مِنَ الْعَالِينَ (75) قَالَ أَنَا خَيْرٌ مِنْهُ خَلَقْتَنِي مِنْ نَارٍ وَخَلَقْتَهُ مِنْ طِينٍ (76) قَالَ فَاخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ (77) وَإِنَّ عَلَيْكَ لَعْنَتِي إِلَى يَوْمِ الدِّينِ (78) قَالَ رَبِّ فَأَنْظِرْنِي إِلَى يَوْمِ يُبْعَثُونَ (79) قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ الْمُنْظَرِينَ (80) إِلَى يَوْمِ الْوَقْتِ الْمَعْلُومِ (81) قَالَ فَبِعِزَّتِكَ لَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ (82) إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ الْمُخْلَصِينَ (83) قَالَ فَالْحَقُّ وَالْحَقَّ أَقُولُ (84) لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنْكَ وَمِمَّنْ تَبِعَكَ مِنْهُمْ أَجْمَعِينَ (85) قُلْ مَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُتَكَلِّفِينَ (86) إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِلْعَالَمِينَ (87) وَلَتَعْلَمُنَّ نَبَأَهُ بَعْدَ حِينٍ (88)}.
65.
Sema: Hakika mimi ni mwonyaji tu; na hapana mungu ila Mwenyezi Mungu Mmoja, Mtenda nguvu. 66. Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na viliomo baina yake, Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe. 67.
Sema: Hii ni habari kubwa kabisa. 68. Ambayo nyinyi mnaipuuza. 69. Sikuwa na elimu ya mambo ya viumbe wakuu watukufu walipokuwa wakishindana. 70. Haikufunuliwa kwangu isipokuwa ya kwamba hakika mimi ni mwonyaji dhahiri. 71.
Mola wako Mlezi alipowaambia Malaika: Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na udongo. 72. Na nitakapomkamilisha na kumpulizia roho inayotokana nami, basi muangukieni kwa kumtii. 73. Basi wakasujudu Malaika wote pamoja. 74. Isipokuwa Iblisi; alijivuna na akawa katika makafiri. 75.
Mwenyezi Mungu akamwambia: Ewe Iblisi! Kipi kilicho kuzuia kumtii yule niliyemuumba kwa mikono yangu? Je, umejiona mkubwa, au umekuwa katika wakuu kweli? 76.
Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo. 77.
Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaanika. 78. Na hakika laana yangu itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo. 79.
Akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watakayofufuliwa viumbe. 80.
Mwenyezi Mungu akasema: Basi umekwisha kuwa miongoni mwa waliopewa muhula. 81. Mpaka siku ya wakati maalumu. 82. Akasema
(Iblisi): Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote. 83. Isipokuwa wale waja wako miongoni mwao waliohitariwa. 84.
Akasema: Haki! Na haki ninaisema. 85. Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wewe na kwa hao wote wenye kukufuata miongoni mwao. 86. Sema
(Ewe Mtume): Sikuombeni ujira juu ya haya, wala mimi si katika wadanganyifu. 87. Hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu wote. 88. Na bila ya shaka mtajua habari zake baada ya muda.
#
{65} {قل}: يا أيُّها الرسولُ لهؤلاء المكذِّبين إنْ طَلَبوا منك ما ليس لك ولا بيدِكَ: {إنَّما أنا منذرٌ}: هذا نهايةُ ما عندي، وأمَّا الأمرُ؛ فلله تعالى، ولكني آمرُكُم وأنهاكُم وأحثُّكم على الخير وأزجُرُكم عن الشرِّ؛ فمنِ اهتدى فلنفسِهِ، ومن ضلَّ فعليها. {وما مِنْ إلهٍ إلاَّ الله}؛ أي: ما أحدٌ يؤلَّه ويُعبدُ بحقِّ إلاَّ الله، {الواحدُ القهارُ}: هذا تقريرٌ لألوهيَّته بهذا البرهان القاطع، وهو وحدتُه تعالى وقهرُه لكلِّ شيء؛ فإنَّ القهر ملازمٌ للوحدة؛ فلا يكون قهّارَيْنِ متساوِيَيْنِ في قهرهما أبداً، فالذي يقهر جميع الأشياءِ هو الواحدُ الذي لا نظير له، وهو الذي يستحقُّ أن يُعْبَدَ وحدَه كما كان قاهراً وحدَه.
{65} "Sema" ewe Mtume, ukiwaambia hawa wanaokadihibisha,
ikiwa watakuomba kisichokuwa chako wala kisichokuwa mkononi mwako: "Hakika mimi ni mwonyaji tu." Huu ndio mwisho wa niliyo nayo, na amri ni ya Mwenyezi Mungu tu. Lakini mimi ninawaamrisha na kuwakataza, na ninawahimiza kutenda mema na kuwakemea dhidi ya maovu. Kwa hivyo, mwenye kuongoka, basi ni kwa faida yake na mwenye kupotea, basi ni hasara ya nafsi yake. "Na hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu;" yaani, hakuna yule aliye na haki ya kufanyiwa ibada ila Mwenyezi Mungu "Mmoja, Mwenye nguvu zote." Huu ni uthibitisho wa uungu wake kwa ushahidi huu wa kukata, ambao ni upweke wake, Yeye Mtukufu na ushindi wake juu ya kila kitu. Kwani ushindi unalazimu kwamba Yeye ni Mmoja tu. Kwa sababu kamwe haiwezekani kuwepo washindi wawili walio sawa katika ushindi wao. Kwa hivyo, mwenye kushinda kila kitu ndiye wa pekee ambaye,hana aliye sawa naye. Na ndiye anayestahiki kuabudiwa peke yake, kama vile alivyoshinda peke yake.
#
{66} وقرَّر ذلك أيضاً بتوحيد الربوبيَّة، فقال: {ربُّ السمواتِ والأرضِ وما بينَهما}؛ أي: خالقُهما ومربِّيهما ومدبِّرُهما بجميع أنواع التدابير، {العزيزُ}: الذي له القوة التي بها خَلَقَ المخلوقاتِ العظيمة. {الغفَّارُ}: لجميع الذنوب؛ صغيرها وكبيرها، لمن تاب إليه وأقلع منها. فهذا الذي يحبُّ، ويستحقُّ أن يُعْبَدَ دونَ مَنْ لا يخلُق، ولا يرزُق ولا يضرُّ، ولا ينفعُ، ولا يملِكُ من الأمر شيئاً، وليس له قوَّةُ الاقتدار، ولا بيدِهِ مغفرةُ الذُّنوب والأوزار.
{66} Vile vile umethibitishwa upweke wake katika umola wake,
akisema: "Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake." Yaani, Yeye ndiye Muumba wao, mlezi wao, anayewaendesha kwa kila namna. "Mwenye nguvu," ambaye kwa nguvu zake hizo aliviumba viumbe vikubwa. "Mwenye kusamehe mno" dhambi zote, ndogo na kubwa, kwa wale wanaotubia kwake na kuachana na dhambi. Huyu ndiye ambaye ni wajibu na anayestahiki kuabudiwa. Na si yeye ambaye haumbi wala haruzuku wala hadhuru wala hakufaishi wala hamiliki jambo lolote, hana nguvu za kumpa uwezo wala suala la kusamehe dhambi na makosa haliko mkononi mwake.
#
{67 - 68} {قل}: لهم مخوفاً ومحذِّراً ومنهضاً لهم ومنذراً: {هو نبأٌ عظيمٌ}؛ أي: ما أنبأتُكم به من البعث والنشور والجزاء على الأعمال خبرٌ عظيم ينبغي الاهتمام الشديد بشأنه، ولا ينبغي إغفالُه. ولكنْ {أنتُم عنه معرِضونَ}: كأنَّه ليس أمامكم حسابٌ ولا عقابٌ ولا ثوابٌ.
{67 - 68} "Sema" kwa njia ya kuwahofisha, kuwatahadharisha,
kuwaonya na kuwafanya wanyanyuke: "Hii ni habari kubwa kabisa" niliyokuambieni kuhusu ufufuo, kuwatawanya watu, malipo juu ya matendo, ambayo inafaa kuzingatiwa sana na wala haifai kughafilika na kuisahau. Lakini "ambayo nyinyi mnaipuuza," kana kwamba hakuna hesabu wala adhabu wala malipo mbele yenu.
#
{69 - 70} فإنْ شَكَكْتُم في قولي وامْتَرَيْتُم في خبري؛ فإني أخبركم بأخبارٍ لا علم لي بها ولا دَرَسْتُها في كتاب؛ فإخباري بها على وجهها من غير زيادةٍ ولا نقصٍ أكبرُ شاهدٍ لصدقي وأدلُّ دليل على حقِّ ما جئتُكم به، ولهذا قال: {ما كان لي من علم بالملأ الأعلى}؛ أي: الملائكة؛ {إذْ يَخْتَصِمونَ}؛ لولا تعليم الله إيَّاي وإيحاؤه إليَّ، ولهذا قال: {إن يوحى إليَّ إلاَّ أنَّما أنا نذيرٌ مبينٌ}؛ أي: ظاهر النذارة جليُّها؛ فلا نذير أبلغ من نذارتِهِ - صلى الله عليه وسلم -.
{69 - 70} Na mkishuku maneno yangu na habari niliyowapa, basi mimi ninawaambia habari nisizozijua wala sikuzisoma kwenye kitabu. Kwa hivyo kuwaelezea kwangu habari hizo kama zilivyo bila ya kuongeza wala kupunguza, ni ushahidi mkubwa wa ukweli wangu na tena ushahidi wa wazi kabisa kwamba niliyowajia nayo ni ya haki.
Ndiyo maana akasema: "Sikuwa na elimu ya mambo ya viumbe wakuu watukufu;" yaani, malaika "walipokuwa wakishindana." Lau si kwa kufundishwa na Mwenyezi Mungu na kunifunulia wahyi, basi nisingeyajua.
Ndiyo maana akasema: "Haikufunuliwa kwangu isipokuwa ya kwamba hakika mimi ni mwonyaji dhahiri."
#
{71 - 72} ثم ذَكَرَ اختصام الملأ الأعلى، فقال: {إذ قال ربُّك للملائكة}: على وجه الإخبارِ، {إنِّي خالقٌ بشراً من طينٍ}؛ أي: مادَّتُه من طين، {فإذا سَوَّيْتُهُ}؛ أي: سويت جسمه وتمَّ، {ونفختُ فيه من روحي فَقَعوا له ساجدينَ}.
{71 - 72} Kisha akataja ushindani huo wa viumbe wakuu watukufu.
Akasema: "Mola wako Mlezi alipowaambia Malaika" kwa njia ya kuwajulisha: "Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na udongo. Na nitakapomkamilisha na kumpulizia roho inayotokana nami, basi muangukieni kwa kumsujudia."
#
{73 - 74} فوطَّن الملائكةُ الكرامُ أنفسَهم على ذلك حين يتمُّ خلقُهُ ونفخُ الروح فيه امتثالاً لربِّهم وإكراماً لآدم عليه السلام، فلما تمَّ خلقُه في بدنِهِ وروحِهِ، وامتحنَ الله آدمَ والملائكةَ في العلم، وظهر فضلُه عليهم؛ أمرهم الله بالسجودِ، فسجدوا {كلُّهم أجمعون، إلاَّ إبليسَ}: لم يسجد، {استَكْبَرَ}: عن أمر ربِّه، واستكبر على آدم، {وكان من الكافرينَ}: في علم الله تعالى.
{73 - 74} Basi Malaika watukufu wakawa wamejizoesha hilo alipokuwa bado anaumbwa na kupuliziwa roho. Walifanya hivyo kwa njia ya kutekeleza amri ya Mola wao Mlezi na kwa njia ya kumheshimu Adam, amani iwe juu yake. Basi ulipokamilika uumbaji wake katika mwili wake na roho yake, kisha Mwenyezi Mungu akamjaribu Adam na Malaika katika elimu, na ubora wake ukadhihiri juu ya Malaika, Mwenyezi Mungu akawaamrisha kusujudu. Basi wakasujudu. "Wakasujudu wote pamoja, isipokuwa Iblisi." Yeye hakusujudu, "alijivuna" na akakaidi amri ya Mola wake Mlezi, na akajivuna mbele ya Adam. "Na akawa katika makafiri."
#
{75} فقال اللهُ له موبِّخاً ومعاتباً: {ما مَنَعَكَ أن تسجدَ لما خلقتُ بيديَّ}؛ أي: شرَّفْتُه وكرَّمْتُه واختصصتُه بهذه الخصيصة التي اختصَّ بها عن سائر الخلق، وذلك يقتضي عدم التكبُّر عليه. {أستكبرتَ}: في امتناعِك {أم كنتَ من العالينَ}.
{75} Mwenyezi Mungu akamwambia akimkemea na kumlaumu: "Kipi kilichokuzuia kuwa katika waliomsujudia yule niliyemuumba kwa mikono yangu?" Yaani, niliyemtukuza, nikamkirimu na nikamteua kwa sifa hii inayomtofautisha na viumbe vingine vyote, ambayo inahitaji kutomfanyia jeuri. "Je, umejiona mkubwa" katika kukataa kwako kusujudu "au umekuwa katika wakuu kweli?"
#
{76} {قال} إبليسُ معارضاً لربِّه مناقضاً: {أنا خيرٌ منه خَلَقْتَني من نارٍ وخَلَقْتَهُ من طين}: وبزعمِهِ أنَّ عنصر النار خيرٌ من عنصر الطين، وهذا من القياس الفاسدِ؛ فإنَّ عنصرَ النار مادَّةُ الشرِّ والفساد والعلوِّ والطيش والخفَّة، وعنصرُ الطِّين مادَّةُ الرزانة والتواضُع وإخراج أنواع الأشجارِ والنباتات، وهو يغلِبُ النار ويطفِئُها، والنارُ تحتاج إلى مادَّةٍ تقومُ بها والطينُ قائمٌ بنفسِهِ. فهذا قياسُ شيخ القوم، الذي عارض به الأمر الشفاهيَّ من الله، قد تبيَّن غايةُ بطلانِهِ وفسادِهِ؛ فما بالُك بأقيسةِ التلاميذ الذين عارضوا الحقَّ بأقْيِسَتِهِم؛ فإنَّها كلَّها أعظمُ بطلاناً وفساداً من هذا القياس.
{76} Iblisi "Akasema" akipingana na Mola wake Mlezi: "Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo." Hapo, akadai kwamba moto ni bora kuliko udongo, na hili ni katika kulinganisha kubovu. Kwani moto ndio kiini cha maovu, uharibifu, kiburi, kuvuka mipaka na wepesi. Ama udongo, huo ndio kiini cha utimamu, unyenyekevu, na uzalishaji wa aina mbalimbali za miti na mimea, nao unaushinda moto kwa kuuzima. Pia, moto unahitaji kitu ili kujitegemeza, ilhali udongo unaweza kujisimamia wenyewe. Huku ndiko kulinganisha kwa shekhe wa watu waovu. Kulinganisha ambako alikutumia kuipinga amri aliyoambiwa kwa mdomo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kulinganisha ambako ubatili wake mkubwa na ubovu wake tayari ulikwisha bainika wazi. Basi atasema vipi kuhusu kulinganisha wanakolinganisha wanafunzi wake ambao waliipinga haki kwa milinganisho yao? Hiyo yote ni batili na mbovu zaidi kuliko mlinganisho huu wa Iblisi.
#
{77 - 78} فقال الله له: اخرج {منها}؛ أي: من السماء والمحلِّ الكريم، {فإنَّك رجيمٌ}؛ أي: مبعد مدحور، {وإنَّ عليك لعنتي} أي: طردي وإبعادي {إلى يوم الدين}: دائماً أبداً.
{77 - 78} Basi Mwenyezi Mungu akamwambia: Toka "humo" mbinguni na mahali patukufu, "kwani hakika wewe umelaanika. Na hakika laana yangu itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo."
#
{79} {قال ربِّ فأنظِرْني إلى يوم يبعثون}: لشدَّة عداوتِهِ لآدمَ وذرَّيَّته؛ ليتمكَّن من إغواء مَنْ قَدَّرَ الله أن يُغْوِيَه.
{79} "Akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watakayofufuliwa viumbe," kwa sababu ya ukubwa wa uadui wake kwa Adam na kizazi chake. Hili ni ili aweze kumpoteza yule ambaye Mwenyezi Mungu alipitisha ampoteze.
#
{80 - 81} فـ {قال} الله مجيباً لدعوتِهِ حيث اقتضتْ حكمتُهُ ذلك: {إنَّكَ من المُنْظَرين. إلى يوم الوقتِ المعلوم}: حين تُسْتَكْمَلُ الذريَّةُ، ويتمُّ الامتحان.
{80 - 81} Kisha Mwenyezi Mungu "akasema" akimuitikia ombi lake kama ilivyohitajika katika hekima yake: "Basi umekwisha kuwa miongoni mwa waliopewa muhula. Mpaka siku ya wakati maalumu." Wakati uzao wa Adam utakamilika, na mtihani watakaopewa ukamilike.
#
{82 - 83} فلما علم أنه مُنْظَرٌ؛ بادى ربَّه من خبثه بشدَّة العداوةِ لربِّه ولآدم وذُرِّيَّتِهِ، فقال: {فبعزَّتِك لأغْوِيَنَّهُم أجمعينَ}:
يُحتمل أنَّ الباء للقسم، وأنَّه أقسم بعزَّةِ الله ليغوينَّهم كلَّهم أجمعين {إلاَّ عبادك منهم المخلَصين}: علم أنَّ الله سيحفظُهم من كيدِهِ. ويُحتمل أنَّ الباء للاستعانة، وأنَّه لما علم أنه عاجزٌ من كل وجهٍ، وأنه لا يضلُّ أحداً إلاَّ بمشيئة الله تعالى، فاستعانَ بعزَّةِ الله على إغواءِ ذُرِّيَّةِ آدمَ. هذا وهو عدوُّ الله حقًّا، ونحن يا ربَّنا العاجزونَ المقصرونَ، المقرُّونَ لك بكل نعمةٍ، ذُرِّيَّةُ من شَرَّفْتَه وكرَّمْتَه؛ فنستعين بعزَّتك العظيمة، وقدرتك، ورحمتك الواسعة لكلِّ مخلوق، ورحمتك التي أوصلتَ إلينا بها ما أوصلتَ من النعم الدينيَّة والدنيويَّة، وصرفتَ بها ما عنَّا صرفتَ من النِّقم، أن تعينَنا على محاربتِهِ وعداوتِهِ والسلامة من شرِّه وشركِهِ، ونحسنُ الظَّنَّ بك أن تجيبَ دعاءنا، ونؤمنُ بوعدِك الذي قلت لنا: {وقال ربُّكم ادْعوني أسْتَجِبْ لكُم}؛ فقد دَعَوْناك كما أمَرْتَنا، فاستجِبْ لنا كما وَعَدْتَنا. {إنَّك لا تُخْلِفُ الميعاد}.
{82 - 83} Alipojua kwamba amepewa muhula, akamuonyesha Mola wake Mlezi ukubwa wa uadui wake kwake na kwa Adam na kizazi chake.
Akasema: "Ninaapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote." Inawezekana kwamba “ba” iliyotumika hapa ni ile ya kuapia. Na kwamba aliapa kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu kwamba atawapoteza wote; "Isipokuwa wale waja wako miongoni mwao waliosafishwa." Hao alijua kwamba Mwenyezi Mungu atawalinda kutokana na vitimbi vyake. Na inawezekana kwamba "ba" hii ni ile inayotumiwa katika kutafuta msaada wa kitu fulani. Na kwamba alipojua kuwa hana uwezo kwa namna zote, na kwamba hataweza kumpoteza yeyote isipokuwa kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, akatafuta msaada kutoka kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu ili kukipoteza kizazi cha Adam. Huyu kwa hakika ndiye adui wa Mwenyezi Mungu. Nasi, ewe Mola wetu Mlezi, ni wanyonge na wasioweza kutekeleza mambo vilivyo, ambao tunakiri kila neema yako; kizazi cha yule uliyemtukuza na kumkirimu. Basi tunaomba msaada kutoka kwa utukufu wako mkubwa, uwezo wako na rehema yako iliyoenea kila kiumbe. Rehema ambayo kwayo umetufikishia neema mbalimbali za kidini na za kidunia, na ambayo kwayo ulituepusha adhabu mbalimbali kwamba utusaidie kupigana naye na utusaidie dhidi ya uadui wake. Na utuweke salama kutokana na uovu wake na shirki yake.
Na tuna imani na Wewe kwamba utatuitikia dua zetu na tunaamini ahadi yako uliyotuambia: "Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni." Basi, tumeshakuomba kama ulivyotuamrisha, kwa hivyo tuitikie kama ulivyotuahidi. "Hakika Wewe huvunji miadi yako."
#
{84 - 85} {قال} الله تعالى: {فالحقُّ والحقَّ أقولُ}؛ أي: الحقُّ وصفي والحقُّ قولي، {لأملأنَّ جهنَّم منك ومِمَّن تَبِعَكَ منهم أجمعينَ}.
{84 - 85} Mwenyezi Mungu Mtukufu "Akasema: Haki" ndiyo sifa yangu "na haki ninaisema. Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wewe na kwa hao wote wenye kukufuata miongoni mwao."
#
{86} فلما بيَّنَ الرسول للناس الدليلَ، ووضَّح لهم السبيلَ؛ قال الله له: {قل ما أسألُكُم عليه}؛ أي: على دعائي إياكم {من أجرٍ وما أنا من المتكلِّفين}: أدَّعي أمراً ليس لي، وأقفو ما ليس لي به علمٌ، لا أتَّبِعُ إلاَّ ما يُوحى إليَّ.
{86} Mtume alipowabainishia watu ushahidi na akawawekea njia wazi,
Mwenyezi Mungu akamwambia: "Sema
(ewe Mtume): Sikuombeni ujira juu ya haya" ninayowalingania, "wala mimi si katika wadanganyifu." Na sifuati isipokuwa yale ninayoteremshiwa.
#
{87} {إنْ هو}؛ أي: هذا الوحي والقرآن {إلاَّ ذِكْرٌ للعالَمين}: يتذكَّرون به كلَّ ما ينفعُهم من مصالح دينهم ودُنياهم، فيكون شرفاً ورفعةً للعالمين به وإقامةَ حجَّة على المعاندين.
فهذه السورة العظيمة مشتملةٌ على الذِّكْر الحكيم، والنبأ العظيم، وإقامةِ الحُجَج والبراهين على مَنْ كذَّب بالقرآن، وعارَضَه، وكذَّب مَنْ جاء به، والإخبار عن عباد الله المخلَصين، وجزاء المتَّقين والطاغين؛ فلهذا أقسم في أولها بأنَّه ذو الذِّكْر، ووصفه في آخرها بأنَّه ذِكْرٌ للعالمين، وأكثَرَ التَّذْكيرَ بها فيما بين ذلك؛ كقوله: {واذْكُرْ عَبْدَنا}، {واذْكُرْ عِبَادَنا}، {رحمةً منّا وذِكْرى}، {هذا ذكرٌ}. اللهمَّ علِّمْنا منه ما جهلنا، وذكِّرْنا منه ما نَسينا نِسيانَ غفلةٍ ونسيان تركٍ.
{87} "Hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu wote." Ambayo kwayo wanakumbuka kila yenye kuwanufaisha miongoni mwa masilahi ya dini yao na dunia yao. Kwa hivyo ni utukufu na kunyanyuliwa kwa walimwengu, na pia ni hoja dhidi ya wakaidi. Sura hii kubwa inajumuisha ukumbusho wenye hekima, habari kuu, kusimamisha hoja na ushahidi juu ya wale wanaoikadhibisha Qur-ani, wanaoipinga na kumkadhibisha yule aliyekuja nayo. Na inapeana habari juu ya waja wa Mwenyezi Mungu waliosafishwa, na malipo ambayo Mwenyezi Mungu atawalipa wacha Mungu na madhalimu. Ndiyo maana aliapa mwanzoni mwake kwamba Qur-ani hii ni yenye ukumbusho.
Kama alivyosema: "Na umkumbuke mja wetu,
" na kauli yake: "Na wakumbuke waja wetu,
" na kauli yake: "kuwa ni rehema itokayo kwetu, na iwe kumbusho,
" na kauli yake: "Huu ni ukumbusho." Ewe Mwenyezi Mungu tufundishe katika Qur-ani hii yale ambayo hatuyajui, na utukumbushe yale tuliyoyasahau kwa njia ya kughafilika na kuwa katika njia ya kuyaacha.
#
{88} {ولَتَعْلَمُنَّ نبأه}؛ أي: خبره {بعد حينٍ}: وذلك حين يقع عليهم العذابُ، وتتقطَّع عنهم الأسبابُ.
{88} "Na bila ya shaka mtajua habari zake baada ya muda." Yaani, hapo ndipo adhabu itakapowafikia na kukatikiwa njia zote.
Imekamilika tafsiri ya Surat Swad kwa neema na msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
* * *