:
Tafsiri ya Surat Sajda
Tafsiri ya Surat Sajda
Nayo iliteremka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
: 1 - 3 #
{الم (1) تَنْزِيلُ الْكِتَابِ لَا رَيْبَ فِيهِ مِنْ رَبِّ الْعَالَمِينَ (2) أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ بَلْ هُوَ الْحَقُّ مِنْ رَبِّكَ لِتُنْذِرَ قَوْمًا مَا أَتَاهُمْ مِنْ نَذِيرٍ مِنْ قَبْلِكَ لَعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ (3)}
1. Alif Laam Miim 2. Huu ni mteremsho wa Kitabu kisicho kuwa na shaka yoyote kinachotoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 3. Au wanasema: Amekizua? Bali hiki ni kweli iliyotoka kwa Mola wako Mlezi ili uwaonye watu wasiofikiwa na mwonyaji kabla yako; huenda wakaongoka.
#
{2} يخبر تعالى أنَّ هذا الكتاب الكريم تنزيلٌ نزل من ربِّ العالمين، الذي ربَّاهم بنعمتِهِ، ومن أعظم ما ربَّاهم به هذا الكتاب، الذي فيه كلُّ ما يُصْلِحُ أحوالَهم ويتمِّم أخلاقَهم، وأنَّه لا ريبَ فيه ولا شكَّ ولا امتراءَ.
{2} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuwa Kitabu hiki kitukufu ni uteremsho kutoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote, ambaye aliwalea kwa neema zake. Na miongoni mwa makubwa aliyowalea kwayo ni Kitabu hiki, ambacho kina kila kinachoboresha hali zao na hukamilisha maadili yao, na kwamba hakuna shaka yoyote ndani yake.
#
{3} ومع ذلك؛ قالَ المكذِّبون للرسول الظالمونَ في ذلك: افتراه محمدٌ واختلَقَه من عند نفسه! وهذا من أكبر الجراءة على إنكارِ كلام اللَّه، ورَمْي محمدٍ بأعظم الكذِبِ، وقدرة الخَلْق على كلام مثل كلام الخالق، وكلُّ واحد من هذه، من الأمور العظائم، قال الله رادًّا على من قال: افتراه: {بل هو الحقُّ}: الذي لا يأتيه الباطلُ من بين يديه ولا من خلفِهِ تنزيلٌ من حكيم حميدٍ {من ربِّكَ}: أنزله رحمةً للعباد، {لِتُنذِرَ قوماً ما أتاهم من نذيرٍ من قبلِكَ}؛ أي: هم في حال ضرورة وفاقةٍ لإرسال الرسول وإنزال الكتاب لعدم النذير، بل هم في جهلهم يَعْمَهون، وفي ظُلمة ضلالهم يتردَّدون، فأنزلنا الكتاب عليك، {لعلَّهم يهتدونَ}: من ضلالهم، فيعرفون الحقَّ ويؤثِرونَه. وهذه الأشياء التي ذَكَرها الله كلُّها مناقضةٌ لتكذيبهم له، وإنَّها تقتضي منهم الإيمان والتصديق التامَّ به، وهو كونُه من ربِّ العالَمين، وأنَّه حقٌّ، والحق مقبولٌ على كلِّ حال، وأنه لا ريبَ فيه بوجه من الوجوه؛ فليس فيه ما يوجب الريبة؛ لا بخبر غير مطابق للواقع ، ولا بخفاء واشتباه معانيه، وأنهم في ضرورة وحاجة إلى الرسالة، وأن فيه الهداية لكلِّ خير وإحسان.
{3} Na pamoja na hayo, watu madhalimu wanaomkadhibisha Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, walisema juu ya hilo kwamba: Muhammad aliizua na akaitunga mwenyewe! Huu ni miongoni mwa ujasiri mkubwa zaidi wa kukanusha maneno ya Mwenyezi Mungu, na kumtuhumu Muhammad kwa uongo mkubwa zaidi, na uwezo wa viumbe kusema maneno kama ya Muumba. Kila moja katika haya ni moja ya mambo makubwa. Mwenyezi Mungu akasema akawajibu waliosema kwamba ametunga, "Bali hiki ni Kweli" ambaye haifikiwi na batili mbele kwa yake wala kwa nyuma yake, ni uteremsho kutoka kwa Mwenye hekima, Msifiwa. "Iliyotoka kwa Mola wako Mlezi" aliyeiteremsha iwe rehema kwa waja, "ili uwaonye watu wasiofikiwa na mwonyaji kabla yako." Yaani, wako katika hali inayolazimu na kuhitaji watumiwe Mtume na kuteremshiwa Kitabu kwa sababu hawakuwahi kutumiwa mwonyaji. Bali bado wanatangatanga kwa upofu katika ujinga wao. Na bado wanasitasita katika giza la upotofu wao. Basi tukakiteremsha Kitabu juu yako "huenda wakaongoka," kutokana na upotofu wao, wakapata kuijua haki na kuipendelea. Haya aliyoyataja Mwenyezi Mungu yote yanapingana na kukadhibisha kwao huko, na kwamba yanawahitajia kuwa na imani kamili na kusadiki kamili, kwamba kinatoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote, na kwamba hicho ni haki, na haki inakubaliwa katika hali zote, na kwamba hakina shaka yoyote ndani yake kwa njia yoyote ile. Kwa hivyo, hakina chochote cha kusababisha shaka, si kwa habari zisizolingana na hali ya halisi ya mambo, wala kwa sababu ya kujificha na kuchanganya kwa maana zake, na kwamba wao ni wahitaji sana kutumia ujumbe, na kwamba kina uongofu kufikia kila heri na ihsani.
: 4 - 9 #
{اللَّهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ مَا لَكُمْ مِنْ دُونِهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا شَفِيعٍ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ (4) يُدَبِّرُ الْأَمْرَ مِنَ السَّمَاءِ إِلَى الْأَرْضِ ثُمَّ يَعْرُجُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ أَلْفَ سَنَةٍ مِمَّا تَعُدُّونَ (5) ذَلِكَ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ (6) الَّذِي أَحْسَنَ كُلَّ شَيْءٍ خَلَقَهُ وَبَدَأَ خَلْقَ الْإِنْسَانِ مِنْ طِينٍ (7) ثُمَّ جَعَلَ نَسْلَهُ مِنْ سُلَالَةٍ مِنْ مَاءٍ مَهِينٍ (8) ثُمَّ سَوَّاهُ وَنَفَخَ فِيهِ مِنْ رُوحِهِ وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ قَلِيلًا مَا تَشْكُرُونَ (9)}
4. Mwenyezi Mungu ndiye aliyeumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake kwa siku sita, na akatawala kwenye Kiti cha Enzi. Nyinyi hamna mlinzi wala mwombezi isipokuwa Yeye tu. Basi, je, hamkumbuki? 5. Anapitisha mambo yote yaliyo baina ya mbingu na ardhi, kisha yanapanda kwake kwa siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu kwa mnavyohesabu nyinyi. 6. Huyu ndiye Mwenye kuyajua yasiyoonekana na yanayoonekana. Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. 7. Ambaye ametengeneza vizuri umbo la kila kitu na akaanzisha kumuumba mtu kwa udongo. 8. Na kisha akajaalia uzao wake utokane na kizazi cha maji madhaifu. 9. Kisha akamtengeneza sawasawa, na akampulizia katika roho yake, na akawajalieni kusikia na kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyoshukuru.
#
{4} يخبر تعالى عن كمال قدرته بخلقه السماوات والأرض في ستة أيام، أولها يوم الأحد، وآخرها الجمعة، مع قدرته على خلقها بلحظة، ولكنَّه تعالى رفيقٌ حكيمٌ، {ثم استوى على العرش}: الذي هو سقفُ المخلوقات استواءً يليقُ بجلالِهِ، {ما لكم من دونِهِ من وليٍّ}: يتولاَّكم في أمورِكم فينفَعُكم {ولا شفيع}: يشفعُ لكم إنْ توجَّه عليكم العقاب. {أفلا تتذكَّرونَ}: فتعلمون أنَّ خالق الأرض والسماواتِ، المستوي على العرش العظيم، الذي انفرد بتدبيركم وتولِّيكم، وله الشفاعةُ كلُّها، هو المستحقُّ لجميع أنواع العبادة!
{4} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya ukamilifu wa uwezo wake kwa kuumba mbingu na ardhi kwa siku sita, na siku ya kwanza yake ikiwa ni Jumapili, na ya mwisho yake ikiwa ni Ijumaa, pamoja na kwamba ana uwezo wa kuumba mara moja, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mpole, Mwenye hekima "na akatawala kwenye Kiti cha Enzi," ambacho ndicho paa la viumbe vyote. Alitawala kutawala kunakoufailia utukufu wake. "Nyinyi hamna mlinzi yeyote atakayewasimamia katika mambo yenu, akawanufaisha, wala mwombezi atakayewafanyia uombezi ikiwa mtaelekewa na adhabu." "Je, hamkumbuki?" Basi mkajua kwamba Muumba wa ardhi na mbingu, ambaye ametawala juu ya kiti kikubwa cha enzi, ambaye ndiye Peke Yake katika kuwaendesha na kuwasimamia, na ambaye ana uombezi wote, ndiye anayestahiki kila aina ya ibada!
#
{5} {يدبِّرُ الأمرَ}: القدريَّ والأمر الشرعيَّ، الجميع هو المنفرد بتدبيره، نازلةٌ تلك التدابير من عند الملك القدير، {من السماء إلى الأرض}: فيُسْعِدُ بها ويشقي، ويُغني ويُفقر، ويعزُّ ويذلُّ ويكرِم ويُهين، ويرفع أقواماً ويضع آخرينَ، وينزِّل الأرزاق، {ثم يَعْرُجُ إليه}؛ أي: الأمر ينزِلُ من عنده، ويعرُجُ إليه {في يوم كان مقدارُهُ ألفَ سنةٍ ممَّا تعدُّونَ}: وهو يعرُجُ إليه، ويصِلُه في لحظة.
{5} "Anapitisha mambo yote" ya kimajaliwa na ya kisheria peke yake, na ikateremka mipangilio hiyo kutoka kwa Mfalme mwenye uwezo juu ya "yaliyo baina ya mbingu na ardhila" akawatia furaha na akatia mashakani, na akatajirisha na anafanya mtu kuwa masikini, na akatia nguvu na akadhalilisha, na akatukuza na akadunisha, na akawanyanyua baadhi ya watu na kuwaangusha wengine, na akateremsha riziki, "kisha yanapanda kwake." Yaani, amri inashuka kutoka kwake, na inapanda kwake "kwa siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu kwa mnavyohesabu nyinyi." Nayo yanapanda kwake na yanamfikia muda huo huo.
#
{6} {ذلك}: الذي خلق تلك المخلوقات العظيمة، الذي استوى على العرش العظيم، وانفرد بالتدابير في المملكة، {عالمُ الغيب والشهادة العزيزُ الرحيم}: فبسعة علمِهِ وكمال عزَّتِهِ وعموم رحمتِهِ أوجَدَها، وأوْدَعَ فيها من المنافع ما أوْدَعَ، ولم يعسُرْ عليه تدبيرُها.
{6} "Huyu," aliyeviumba viumbe hivyo vikubwa, ambaye ametawala kwenye Arshi kubwa, na akaendesha peke yake mamlaka yake, "ndiye Mwenye kuyajua yasiyoonekana na yanayoonekana. Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu." Kwa hivyo, kwa upana wa elimu yake, na ukamilifu wa nguvu zake, na ujumla wa rehema yake, akaviumba vyote, na akaweka ndani yake manufaa na wala haikumuwia vigumu kuvisimamia.
#
{7} {الذي أحسنَ كلَّ شيءٍ خَلَقَه}؛ أي: كلّ مخلوقٍ خلقَهُ الله؛ فإنَّ الله أحسن خلقَه، وخَلَقَهُ خلقاً يليقُ به ويوافِقُه؛ فهذا عامٌّ، ثم خصَّ الآدميَّ لشرفِهِ وفضلِهِ، فقال: {وبدأ خَلْقَ الإنسانِ من طينٍ}: وذلك بخلق آدم عليه السلام أبي البشر.
{7} "Ambaye ametengeneza vizuri umbo la kila kitu" na akakiumba kwa umbile linalikifailia. Na hayo ni kwa ujumla, kisha akamchagua mwanaadamu kwa sababu ya heshima yake na fadhila yake, akasema, "na akaanzisha kumuumba mtu kwa udongo" kwa kuumbwa Adam, amani iwe juu yake, baba wa watu.
#
{8} {ثم جعل نَسْلَه}؛ أي: ذريَّة آدم ناشئة {من ماء مَهين}: وهو النطفةُ المستقذرةُ الضعيفة.
{8} "Na kisha akajaalia uzao wake;" yaani, kizazi cha Adam utokane "na maji madhaifu." Ambayo ni manii yanayoonekana kwamba ni machafu na madhaifu.
#
{9} {ثم سوَّاه} بلحمِهِ وأعضائِهِ وأعصابه وعروقِهِ، وأحسن خِلْقَتَه، ووضع كلَّ عضو منه بالمحلِّ الذي لا يليقُ به غيره، {ونفخ فيه من روحِهِ}: بأن أرسل إليه المَلَكَ؛ فينفخ فيه الروحَ، فيعود بإذن الله حيواناً بعد أن كان جماداً، {وجَعَلَ لكم السمعَ والأبصارَ}؛ أي: ما زال يعطيكم من المنافع شيئاً فشيئاً حتى أعطاكم السمع والأبصار {والأفئدة قليلاً ما تشكُرون}: الذي خلقكم، وصوَّركم.
{9} "Kisha akamtengeneza sawasawa" kwa nyama yake, viungo vyake, mishipa yake, na akamtengeneza kwa sura nzuri, na akaweka kila kiungo mahali pasipokifailia kinginecho, "na akampulizia roho yake" kwa kumtuma malaika; naye akampulizia roho ndani yake, kwa hivyo akawa hai baada ya kwamba alikuwa kitu kisichokuwa na uhai. "Na akawajalia kusikia na kuona;" yaani, hakuacha kuwapa manufaa kidogo kidogo mpaka akawapa kusikia na kuona; "na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyoshukuru" yule ambaye aliwaumba na akawaunda.
: 10 - 11 #
{وَقَالُوا أَإِذَا ضَلَلْنَا فِي الْأَرْضِ أَإِنَّا لَفِي خَلْقٍ جَدِيدٍ بَلْ هُمْ بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ كَافِرُونَ (10) قُلْ يَتَوَفَّاكُمْ مَلَكُ الْمَوْتِ الَّذِي وُكِّلَ بِكُمْ ثُمَّ إِلَى رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ (11)}
10. Nao husema: Tutapokwisha potea chini ya ardhi, ni kweli tutarudishwa katika umbo jipya? Bali wao wanakanusha kwamba watakutana na Mola wao Mlezi. 11. Sema, "Atakufisheni Malaika wa mauti aliyewakilishwa juu yenu; kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu Mlezi."
#
{10} أي: قال المكذِّبون بالبعثِ على وجه الاستبعاد: {أإذا ضلَلْنا في الأرض}؛ أي: بَلينا وتمزَّقْنا وتفرَّقْنا في المواضع التي لا تعلم، {أإنَّا لَفي خلقٍ جديدٍ}؛ أي: لمبعوثون بعثاً جديداً؛ بزعمهم أن هذا من أبعد الأشياء! وذلك بقياسهم قدرة الخالق على قُدَرِهِم ، وكلامهم هذا ليس لطلب الحقيقة، وإنَّما هو ظلمٌ وعنادٌ وكفرٌ بلقاء ربهم وجحدٌ، ولهذا قال: {بل هم بلقاءِ ربِّهم كافرونَ}: فكلامُهم عُلِمَ مصدرُهُ وغايتُهُ، وإلاَّ؛ فلو كان قصدُهم بيان الحق لبُيِّنَ لهم من الأدلَّة القاطعة على ذلك ما يجعله مشاهداً للبصيرة بمنزلة الشمس للبصر، ويكفيهم أنهم عندهم علمٌ أنهم قد ابتُدِئوا من العدم؛ فالإعادةُ أسهلُ من الابتداء، وكذلك الأرضُ الميتة ينزِلُ الله عليها المطرَ فتحيا بعد موتها، وينبتُ به متفرِّقُ بذورها.
{10} Yaani, wale waliokadhibisha kufufuliwa walisema kwa kuona kwamba hilo haliwezekani, "Tutapokwisha potea chini ya ardhi," na tukachanika na kutawanyika katika sehemu zisizozijulikana, "ni kweli tutarudishwa katika umbo jipya?" Kwani, walidai kwamba hili ni katika mambo yasiyowezekana kabisa! Haya ni kwa sababu walilinganisha uwezo wa Muumba na uwezo wao, na maneno yao haya si kutafuta uhakika, bali ni dhuluma, ukaidi, kukufuru kukutana na Mola wao Mlezi, na ukanushaji. Na ndiyo maana akasema, "Bali wao wanakanusha kwamba watakutana na Mola wao Mlezi." Basi chanzo na makusudio ya maneno yao hayo vinajulikana, vinginevyo; Lau kama makusudio yao yangelikuwa ni kubainisha haki, wangelibainishiwa ushahidi wa kukata juu ya hayo ambao ungelifanya kuwa jambo la kuonyesha ufahamu kama vile jua lilivyo kwa mwenye kuona, na inawatosheleza kwamba wanajua kuwa walianzishwa baada ya wao kutokuwepo. Basi kuwarudisha ni rahisi zaidi kuliko kuwaanzisha. Hali kadhalika, ardhi iliyokufa, Mwenyezi Mungu huiteremshia mvua, na huhuisha baada ya kufa kwake, na anaotesha juu yake mbegu mbalimbali.
#
{11} {قل يتوفَّاكم مَلَكُ الموت الذي وُكِّلَ بكم}؛ أي: جعله الله وكيلاً على قبض الأرواح، وله أعوان، {ثمَّ إلى ربِّكُم تُرجعونَ}: فيجازيكم بأعمالكم، وقد أنكرتُم البعث؛ فانظُروا ماذا يفعلُ الله بكم.
{11} "Sema," Atawafisheni Malaika wa mauti aliyewakilishwa juu yenu" juu ya kuchukua roho zenu. Naye anao wale wanaomsaidia, "kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu Mlezi." Naye atawalipa kwa matendo yenu. Nanyi mlikuwa mmekanusha kufufuliwa; basi tazameni yale ambayo Mwenyezi Mungu atawafanyia.
: 12 - 14 #
{وَلَوْ تَرَى إِذِ الْمُجْرِمُونَ نَاكِسُو رُءُوسِهِمْ عِنْدَ رَبِّهِمْ رَبَّنَا أَبْصَرْنَا وَسَمِعْنَا فَارْجِعْنَا نَعْمَلْ صَالِحًا إِنَّا مُوقِنُونَ (12) وَلَوْ شِئْنَا لَآتَيْنَا كُلَّ نَفْسٍ هُدَاهَا وَلَكِنْ حَقَّ الْقَوْلُ مِنِّي لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ (13) فَذُوقُوا بِمَا نَسِيتُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَذَا إِنَّا نَسِينَاكُمْ وَذُوقُوا عَذَابَ الْخُلْدِ بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ (14)}
12. Na ungeliwaona wakosefu wanavyoinamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao Mlezi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Tumeshaona, na tumeshasikia. Turejeshe tukatende mema, kwani hakika sisi tumekwisha kuwa na yakini sasa. 13. Na lau tungelitaka, tungempa kila mtu uwongofu wake. Lakini imekwisha kuwa kauli iliyotoka kwangu: Kwa yakini nitaijaza Jahannamu kwa wote hawa, majini na watu. 14. Basi onjeni kwa vile mlivyousahau mkutano wa Siku yenu hii. Na Sisi hakika tunakusahauni. Basi onjeni adhabu ya milele kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
#
{12} لما ذكر تعالى رجوعَهم إليه يوم القيامةِ؛ ذكر حالَهم في مقامهم بين يديه، فقال: {ولو ترى إذِ المجرِمونَ}: الذين أصرُّوا على الذنوبِ العظيمة، {ناكِسوا رؤوسِهِم عند ربِّهم}: خاشعين خاضعين، أذلاَّء مقرِّين [بجرمهم] ، سائلين الرجعة قائلين: {ربَّنا أبْصَرْنا وسَمِعْنا}؛ أي: بان لنا الأمرُ ورأيناه عياناً، فصار عينَ يقينٍ، {فارْجِعْنا نعملْ صالحاً إنَّا موقِنونَ}؛ أي: صار عندَنا الآن يقينٌ بما كنا نكذِّب به؛ أي: لرأيت أمراً فظيعاً وحالاً مزعجة وأقواماً خاسرين وسؤالاً غير مجابٍ؛ لأنَّه قد مضى وقتُ الإمهال.
{12} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja marejeo yao kwake Siku ya Kiyama; akataja hali yao watakapokuwa wamesimama mbele yake, akasema, "Na ungeliwaona wakosefu," ambao waliendelea kufanya madhambi makubwa "wanavyoinamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao Mlezi" huku wamenyenyekea na kudhalilika na kukiri uhalifu wao, wakiomba warudishwe wakisema, "Mola wetu Mlezi, tumeshaona, na tumeshasikia." Yaani, mambo yametubainikia na tukayaona kwa macho yetu, basi yakawa jicho la yakini, "Turejeshe tukatende mema, kwani hakika sisi tumekwisha kuwa na yakini sasa" kwa yale tuliyokuwa tukiyakadhibisha. Basi ungeona jambo la kushangaza, na hali ya kusumbua, na watu waliohasirika, na maswali yasiyojibiwa; kwa sababu kipindi cha kupewa muhula kilikwisha pita.
#
{13} وكلُّ هذا بقضاءِ الله وقدرِهِ؛ حيث خلَّى بينَهم وبين الكفر والمعاصي؛ فلهذا قال: {ولو شِئْنا لآتَيْنا كلَّ نفس هُداها}؛ أي: لهدينا الناس كلَّهم وجَمَعْناهم على الهدى، فمشيئتُنا صالحةٌ لذلك، ولكنَّ الحكمة تأبى أن يكونوا كلُّهم على الهدى، ولهذا قال: {ولكنْ حقَّ القولُ مني}؛ أي: وجب وثبت ثبوتاً لا تغيُّر فيه، {لأملأنَّ جهنَّم من الجِنَّةِ والناس أجمعينَ}: فهذا الوعدُ لا بدَّ منه ولا محيدَ عنه؛ فلابدَّ من تقرير أسبابه من الكفرِ والمعاصي.
{13} Na yote haya ni kwa mipango ya Mwenyezi Mungu na kadari yake. Ambapo aliwaachilia huru kukufuru na kufanya maasia. Na ndiyo maana akasema, "Na lau tungelitaka, tungempa kila mtu uwongofu wake." Yaani, tungeliwaongoa watu wote na kuwakusanya pamoja kwenye uwongofu. Kwani utashi wetu unaweza kufanya hivyo, lakini hekima inakataa kwamba wote wawe katika uwongofu. Na ndiyo maana akasema, "Lakini imekwisha kuwa kauli iliyotoka kwangu" wala haiwezekani kuibadilisha kwamba, "Kwa yakini nitaijaza Jahannamu kwa wote hawa, majini na watu." Hivyo basi, ahadi hii ni lazima itokee, na wala haiwezi kuepukwa. Kwa hivyo, ni lazima iwekewe sababu zake kama vile kufuru na maasia.
#
{14} {فذوقوا بما نَسيتُم لقاء يومِكُم هذا}؛ أي: يقال للمجرمين الذين ملكهم الذلُّ، وسألوا الرجعة إلى الدُّنيا؛ ليستدركوا ما فاتهم: قد فات وقت الرجوع، ولم يبق إلاَّ العذابُ، فذوقوا العذابَ الأليم بما نسيتُم لقاء يومِكُم هذا، وهذا النسيانُ نسيانُ ترك؛ أي: بما أعرضتُم عنه، وتركتُم العمل له، وكأنّكم غير قادمين عليه ولا ملاقيه. {إنَّا نَسيناكُم}؛ أي: تركناكم بالعذاب جزاءً من جنس عملِكُم؛ فكما نَسيتم نُسيتم، {وذوقوا عذابَ الخُلْدِ}؛ أي: العذاب غير المنقطع؛ فإنَّ العذاب إذا كان له أجلٌ وغايةٌ؛ كان فيه بعضُ التنفيس والتخفيف، وأمَّا عذابُ جهنَّم ـ أعاذنا الله منه ـ؛ فليس فيه روحُ راحةٍ ولا انقطاع لعذابهم فيها؛ {بما كنتُم تعملون}: من الكفر والفسوقِ والمعاصي.
{14} "Basi onjeni kwa vile mlivyousahau mkutano wa Siku yenu hii." Yaani, wataambiwa wahalifu waliojawa na unyonge na wakaomba kurejea katika dunia hii, ili waweze kufanya yale yaliyowapita: Tayari muda wa kurejea umeshapita, na hakuna kilichobakia isipokuwa adhabu tu, basi onjeni adhabu chungu kwa sababu mlisahau kukutana na siku yenu hii. Na kusahau huku ni kule kusahau kwa kuacha; yaani, kwa sababu ya yale mliyotapuuza na mkaacha kufanya matendo mema kwa ajili yake, na ni kana kwamba hamtaijia wala hamtakutana nayo, kwa yale mliyokuwa mkiyatenda."Na Sisi hakika tunakusahauni," na tunawaacha katika adhabu kuwa ni malipo ya aina sawa na vitendo vyenu. Kama vile mlivyosahau, ndivyo mlivyosahauliwa "Basi onjeni adhabu ya milele," isiyokatika. Kwani, adhabu inapokuwa na muda maalumu na mwisho, inakuwa na unafuu fulani ndani yake. Na ama adhabu ya Jahannamu - Mwenyezi Mungu atulinde kutokana nayo - humo hakuna kupumzika wala raha wala kukatika kuadhibiwa kwao, "kwa yale mliyokuwa mkiyatenda" ya ukafiri, kuvuka mipaka na maasia.
: 15 - 17 #
{إِنَّمَا يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا الَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا بِهَا خَرُّوا سُجَّدًا وَسَبَّحُوا بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ (15) تَتَجَافَى جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنْفِقُونَ (16) فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (17)}
15. Hakika wanaoziamini Aya zetu ni hao tu ambao wakikumbushwa hizo, basi wao huanguka kusujudu, na humsabihi Mola wao Mlezi kwa kumhimidi, nao hawajivuni. 16. Mbavu zao zinaachana na vitanda kwa kumwomba Mola wao Mlezi kwa khofu na kutumaini, na hutoa kutokana na tulivyowaruzuku. 17. Nafsi yoyote haijui waliyofichiwa katika hayo yanayofurahisha macho - ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyatenda.
#
{15} لما ذَكَرَ الكافرين بآياته وما أعدَّ لهم من العذاب؛ ذَكَرَ المؤمنين بها ووَصْفَهم وما أعدَّ لهم من الثواب، فقال: {إنَّما يؤمنُ بآياتنا}؛ أي: إيماناً حقيقيًّا مَنْ يوجد منه شواهدُ الإيمان، وهم {الذين إذا ذُكِّروا} بآياتِ ربِّهم، فتُلِيَتْ عليهم آيات القرآن، وأتتهم النصائحُ على أيدي رسل الله، ودُعوا إلى التذكُّر؛ سمعوها فقبلوها وانقادوا و {خرُّوا سُجَّداً}؛ أي: خاضعين لها خضوعَ ذِكْرٍ لله وفرح بمعرفتِهِ، {وسبَّحوا بحمدِ ربِّهم وهم لا يستكْبِرونَ}: لا بقلوبِهِم ولا بأبدانِهِم فيمتنعون من الانقيادِ لها، بل متواضعون لها، قد تَلَقَّوْها بالقَبول والتسليم وقابَلوها بالانشراح والتسليم، وتوصَّلوا بها إلى مرضاة الربِّ الرحيم، واهتَدَوا بها إلى الصراط المستقيم.
{15} Alipowakumbusha makafiri Ishara zake na adhabu aliyowaandalia, akawataja wale wanaoiamini na sifa zao, na malipo aliyowaandalia. Akasema, "Hakika wanaoziamini Aya zetu" imani ya kweli ni wale wambao kunapatikana ndani yao ushahidi wa Imani. Na hao ni "ambao wakikumbushwa" Aya za Mola wao Mlezi, na wakasomewa Aya za Qur'ani, na wakajiwa na nasaha juu ya mikono ya Mitume wa Mwenyezi Mungu, na wakaitwa kukumbuka; Wanazisikia, kuzikubali, kuzifuata, na "basi wao huanguka kusujudu" kwa kunyenyekea kwa njia ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na kufurahia kumjua, "na humsabihi Mola wao Mlezi kwa kumhimidi, nao hawajivuni." Si kwa nyoyo zao wala kwa miili yao, wakakataa kuzifuata, bali wao ni wanyenyekevu kwazo, na walizipokea kwa kuzikubali na kujisalimisha kwazo, na wakazifungukia nyoyo, na wakazitumia kufikia radhi za Mola Mlezi, Mwingi wa kurehemu, na wakaongoka kwazo kwenye njia iliyonyooka.
#
{16} {تتجافى جُنوبهم عن المضاجِع}؛ أي: ترتفع جنوبُهم وتنزعجُ عن مضاجِعِها اللذيذِة إلى ما هو ألذُّ عندهم منه وأحبُّ إليهم، وهو الصلاة في الليل ومناجاة الله تعالى، ولهذا قال: {يَدْعون ربَّهم}؛ أي: في جلب مصالِحِهم الدينيَّة والدنيويَّة ودفع مضارِّهما {خوفاً وطمعاً}؛ أي: جامعين بين الوصفينِ؛ خوفاً أن تُرَدَّ أعمالُهم، وطمعاً في قبولها؛ خوفاً من عذاب الله، وطمعاً في ثوابه، {وممَّا رزَقْناهم}: من الرزق قليلاً أو كثيراً، {يُنفِقونَ}: ولم يذكُر قيد النفقة، ولا المنفَق عليه؛ ليدلَّ على العموم؛ فإنَّه يدخُلُ فيه النفقة الواجبة؛ كالزكوات والكفارات ونفقة الزوجات والأقارب، والنفقة المستحبَّة في وجوه الخير، والنفقة والإحسان المالي خيرٌ مطلقاً؛ سواء وافق فقيراً أو غنيًّا ، قريباً أو بعيداً، ولكن الأجر يتفاوت بتفاوتِ النفع، فهذا عملهم.
{16} "Mbavu zao zinaachana na vitanda" na kuacha jambo tamu la kulala juu yake wakaenda kwenye kile ambacho ni kitamu zaidi kwao na kipendwa zaidi kwao, nacho ni kuswali usiku na kunong'ona na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ndiyo maana akasema, "Kwa kumwomba Mola wao Mlezi" ili awaletee masilahi yao ya kidini na ya kidunia na awaondoshee madhara yao "kwa khofu na kutumaini." Yaani, walikusanya kati ya sifa mbili; kuhofu kwamba matendo yao yanaweza kurudishwa na kutumaini kwamba yatakataliwa, na pia kuhofu adhabu ya Mwenyezi Mungu, na kutumaini malipo yake, "na hutoa kutokana na tulivyowaruzuku," sawa iwe riziki chache au nyingi. Na hapa hakutaja ukomo wa kutoa wala mwenye kupewa; ili iwe na maana ya jumla. Kwani, humo kunaingia kutoa kwa wajibu, kama vile zaka, kafara, na kutoa matumizi ya wake na jamaa, na pia kunaingia ndani yake kutoa kunakopendekezwa katika mambo yote ya heri. Na kutoa kwa ajili ya mambo ya heri na matumizi na kufanya wema kwa kutoa mali ni jambo la heri tupu, hata kama alipawa masikini au tajiri, jamaa wa karibu au wa mbali, lakini malipo yanatofautiana kulingana na faida yake, na haya ndiyo matendo yao.
#
{17} وأمَّا جزاؤهم؛ فقال: {فلا تعلمُ نفسٌ}: يدخل فيه جميعُ نفوس الخلق؛ لكونه نكرةً في سياق النفي؛ أي: فلا يعلمُ أحدٌ {ما أُخْفِيَ لهم من قُرَّةِ أعينٍ}: من الخير الكثير والنعيم الغزير والفرح والسرور واللَّذَّة والحبور؛ كما قال تعالى على لسان رسوله: «أعددتُ لِعبادي الصالحين ما لا عينٌ رأت، ولا أذنٌ سمعت، ولا خَطَرَ على قلب بشر »؛ فكما صلُّوا في الليل ودعوا وأخفوا العمل؛ جازاهم من جنس عملهم، فأخفى أجرهم، ولهذا قال: {جزاءً بما كانوا يَعْمَلونَ}.
{17} Ama malipo yao, akasema, "Nafsi yoyote haijui." Na hili zinaingia ndani yake nafsi za viumbe wote, kwa sababu imetumika nomino ya kawaida katika muktadha wa kukanusha. Yaani, hakuna yeyote ajuaye "waliyofichiwa katika hayo yanayofurahisha macho" ya heri nyingi na neema tele, na furaha tele na raha. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema kwa ulimi wa Mtume Wake, “Nimewaandalia waja wangu wema kile ambacho jicho halijapata kuona, wala sikio halijapata kusikia, wala halijapata kupita katika moyo wa mwanadamu yeyote.” Basi kama vile walivyoswali usiku na wakaomba na wakaficha matendo yao; akawalipa kwa aina sawa na matendo yao. Na ndiyo maana akasema "ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyatenda."
: 18 - 20 #
{أَفَمَنْ كَانَ مُؤْمِنًا كَمَنْ كَانَ فَاسِقًا لَا يَسْتَوُونَ (18) أَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَلَهُمْ جَنَّاتُ الْمَأْوَى نُزُلًا بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (19) وَأَمَّا الَّذِينَ فَسَقُوا فَمَأْوَاهُمُ النَّارُ كُلَّمَا أَرَادُوا أَنْ يَخْرُجُوا مِنْهَا أُعِيدُوا فِيهَا وَقِيلَ لَهُمْ ذُوقُوا عَذَابَ النَّارِ الَّذِي كُنْتُمْ بِهِ تُكَذِّبُونَ (20)}
18. Ati aliye Muumini atakuwa sawa na aliye mpotovu? Hawawi sawa. 19. Ama walioamini na wakatenda mema, watakuwa nazo Bustani za makazi mazuri. Ndio pa kufikia kwa waliyokuwa wakiyatenda. 20. Na ama wale waliotenda uovu, basi makazi yao ni Motoni. Kila wakitaka kutoka humo, watarudishwa humo humo. Na wataambiwa: Onjeni adhabu ya Moto ambayo mlikuwa mkiikanusha.
#
{18} ينبِّه تعالى العقول على ما تقرَّرَ فيها من عدم تساوي المتفاوتَيْنِ المتبايِنَيْن، وأن حكمته تقتضي عدم تساويهما، فقال: {أفمن كان مؤمناً}: قد عَمَرَ قلبَه بالإيمان، وانقادتْ جوارِحُه لشرائعه، واقتضى إيمانُه آثاره وموجباتِه من ترك مساخِطِ الله التي يضرُّ وجودها بالإيمان، {كمن كان فاسقاً}: قد خرب قلبُه وتعطَّل من الإيمان، فلم يكن فيه وازعٌ دينيٌّ، فأسرعتْ جوارحُه بموجبات الجهل والظلم في كلِّ إثم ومعصيةٍ، وخرج بفسقِهِ عن طاعة ربِّه، أفيستوي هذان الشخصان؟! {لا يستوونَ}: عقلاً وشرعاً؛ كما لا يستوي الليل والنهار والضياء والظلمة، وكذلك لا يستوي ثوابُهما في الآخرة.
{18} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatanabahisha akili uu ya yale ambayo yamethibiti ndani yake ya kwamba haviwezi kutoshana vitu viwili tofauti, na kwamba hekima yake inahitaji kwamba visiwe sawa. Akasema: "Ati aliye Muumini" ambaye amejaza imani katika moyo wake, na viungo vyake vikafuata sheria zake, na imani yake hiyo ikahitaji zitekelezwe athhri zake na wajibu zake kama vile kuacha yanye kumghadhabisha Mwenyezi Mungu, ambayo yanapokuwepo yanadhuru imani, "atakuwa sawa na aliye mpotovu," ambaye moyo wake uliharibika na ukakosa imani, na ukawa hauna shinikizo la kidini ndani yake, kwa hivyo viungo vyake vikakimbilia mambo ya ujinga na dhuluma katika kila dhambi na maasia, na akatoka kwa kuvuka kwake mipaka katika kumtii Mola wake Mlezi, basi je wanatoshana watu hawa wawili? "Hawawi sawa" katika akili na katika sheria; kama vile usiku na mchana, nuru na giza haviwi sawa, basi vile vile malipo yao katika Akhera hayatakuwa sawa.
#
{19} {أمَّا الذين آمنوا وعَمِلوا الصالحاتِ}: من فروض ونوافلَ، {فلهم جناتُ} {المأوى}؛ أي: الجنات التي هي مأوى اللذَّات، ومعدنُ الخيرات، ومحلُّ الأفراح، ونعيمُ القلوب والنفوس والأرواح، ومحلُّ الخلود، وجوار الملك المعبود، والتمتُّع بقربه والنظر إلى وجهه وسماع خطابه، {نُزُلاً}: لهم؛ أي: ضيافةً وقِرىً؛ {بما كانوا يعملونَ}: فأعمالُهم التي تَفَضَّلَ الله بها عليهم هي التي أوصلَتْهم لتلك المنازل الغالية العالية، التي لا يمكن التوصُّل إليها ببذل الأموال، ولا بالجنود والخدم، ولا بالأولاد، بل ولا بالنفوس والأرواح، ولا يتقرَّب إليها بشيء أصلاً سوى الإيمان والعمل الصالح.
{19} "Ama walioamini na wakatenda mema" ya wajibu na ya hiari "watakuwa nazo Bustani za makazi mazuri" penye heri nyingi, na mahali pa furaha, na neema kwa nyoyo, nafsi na roho, na ni mahali pa milele, palipo karibu wa Mfalme anayeabudiwa, na kufurahi kwa karibu naye, na kuutazama uso wake, na kuyasikia maneno yake "Ndiyo pa kufikia" makaribisho "kwa waliyokuwa wakiyatenda." Kwa sababu matendo yao aliyowapa Mwenyezi Mungu ndiyo yaliyowafikisha kwenye vyeo hivyo vya thamani na vya juu, ambavyo haviwezi kufikiwa kwa kutoa mali, wala kwa askari na watumishi, wala kwa watoto, wala kwa nafsi na roho, na wala haiwezekani kuyafikia kwa chochote isipokuwa imani tu na matendo mema.
#
{20} {وأمَّا الذين فَسَقوا فمأواهُمُ النارُ}؛ أي: مقرُّهم ومحلُّ خلودهم النارُ، التي جمعت كلَّ عذابٍ وشقاءٍ، ولا يُفَتَّرُ عنهم العقابُ ساعة، {كلَّما أرادوا أن يَخْرُجوا منها أُعيدوا فيها}: فكلَّما حدَّثتهم إرادتُهم بالخروج لبلوغ العذابِ منهم كلَّ مبلغ؛ رُدُّوا إليها، فذهب عنهم روح ذلك الفرج، واشتدَّ عليهم الكرب، {وقيل لهم ذوقوا عذابَ النارِ الذي كنتُم به تكذِّبون}.
{20} "Na ama wale waliotenda uovu, basi makazi yao ni Motoni" ndipo mahali pao pa kudumu milele, katika Moto uliokusanya adhabu na mashaka yote, na wala adhabu yao haipungui hata saa moja. "Kila wakitaka kutoka humo, watarudishwa humo humo." Kila wanapotaka kutoka humo kwa sababu ya kufikiwa na adhabu hiyo kila mahali, wanarudishwa humo, na kuzidishiwa dhiki. "Na wataambiwa: Onjeni adhabu ya Moto ambayo mlikuwa mkiikanusha."
Hii ndiyo adhabu ya Moto ambayo ndani yake kutakuwa na makazi yao. Na ama adhabu iliyo kabla ya hii na utangulizi wake, nayo ni adhabu ya kaburini; hiyo ilitajwa katika kauli yake:
: 21 #
{وَلَنُذِيقَنَّهُمْ مِنَ الْعَذَابِ الْأَدْنَى دُونَ الْعَذَابِ الْأَكْبَرِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ (21)}
21. Na hakika tutawaonjesha katika adhabu hafifu kabla ya adhabu kubwa, huenda labda watarejea.
#
{21} أي: ولنذيقنَّ الفاسقين المكذِّبين نموذجاً من العذاب الأدنى، وهو عذاب البرزخ، فنذيقهم طرفاً منه قبل أن يموتوا: إما بعذابٍ بالقتل ونحوه كما جرى لأهل بدر من المشركين، وإمَّا عند الموت؛ كما في قوله تعالى: {ولو ترى إذِ الظالمونَ في غَمَراتِ الموتِ والملائكةُ باسطوا أيديهم أخرِجوا أنفُسَكُم اليومَ تُجْزَوْنَ عذابَ الهُونِ}، ثم يكمل لهم العذابُ الأدنى في برزَخِهم. وهذه الآيةُ من الأدلة على إثبات عذاب القبر، ودلالتُها ظاهرةٌ؛ فإنَّه قال: {وَلَنُذيقَنَّهم من العذاب الأدنى}؛ أي: بعض وجزء منه، فدلَّ على أن ثَمَّ عذاباً أدنى قبل العذاب الأكبر، وهو عذاب النار، ولما كانت الإذاقة من العذابِ الأدنى في الدنيا قد لا يَتَّصلُ بها الموت، فأخبر تعالى أنَّه يذيقُهم ذلك؛ لعلَّهم يرجِعون إليه، ويتوبون من ذنوبهم؛ كما قال تعالى: {ظَهَرَ الفسادُ في البرِّ والبحرِ بما كَسَبَتْ أيدي الناس لِيُذيقَهم بعضَ الذي عَمِلوا لعلَّهم يرجِعونَ}.
{21} Yaani, hakika tutawaonjesha wale waliovuka mipaka waliokadhibisha mfano wa adhabu ya chini zaidi, nayo ni adhabu ya kaburini. Tutawaonjesha kiasi kidogo tu katika hiyo kabla ya kufa kwao; ima kwa adhabu ya kuuawa, na mfano wake, kama ilivyokuwa kwa washirikina wa watu wa Badr, au katika wakati wa kufa; kama ilivyo katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na lau ungeliwaona madhalimu wanavyokuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea mikono wakiwambia: Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ya fedheha," kisha watakamilishiwa hiyo adhabu ya chini zaidi katika makaburi yao. Aya hii ni katika ushahidi unaothibitisha adhabu ya kaburini, nayo inaonyesha hilo wa uwazi. Kwani alisema, "Na hakika tutawaonjesha katika adhabu hafifu," basi ikaashiria kuwa kuna adhabu ndogo kabla ya adhabu kubwa zaidi, ambayo ni adhabu ya Motoni. Na kwa kuwa kuonja adhabu hii ndogo katika dunia huenda kusiunganishwee na kifo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kuwa atawaonjesha haiyo. Labda watarejea kwake na kutubia dhambi zao, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Ufisadi umedhihiri barani na baharini kwa iliyoyafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyoyatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu."
: 22 #
{وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنْ ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ ثُمَّ أَعْرَضَ عَنْهَا إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِينَ مُنْتَقِمُونَ (22)}
22. Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anayekumbushwa kwa Ishara za Mola wake Mlezi, kisha akazikataa? Hakika Sisi tutajilipiza kwa wakosefu.
#
{22} أي: لا أحد أظلمُ وأزيدُ تعدِّياً ممَّنْ ذُكِّرَ بآيات ربِّه، التي أوصلها إليه ربُّه، الذي يريد تربيتَه وتكميلَ نعمتِهِ عليه على يدِ رسلِهِ، تأمره وتذكِّره مصالحه الدينيَّة والدنيويَّة، وتنهاه عن مضارِّه الدينيَّة والدنيويَّة، التي تقتضي أنْ يقابِلَها بالإيمان والتسليم والانقياد والشكر، فقابلها هذا الظالمُ بضدِّ ما ينبغي، فلم يؤمنْ بها ولا اتَّبَعها، بل أعرض عنها وتركها وراء ظهرِهِ؛ فهذا من أكبر المجرمين، الذين يستحقُّون شديد النقمة، ولهذا قال: {إنَّا من المجرِمين منتَقِمون}.
{22} Yaani, hakuna dhalimu zaidi na avukae zaidi mipaka kuliko yule anayekumbushwa Ishara za Mola wake Mlezi alizomfikishia Mola wake Mlezi, ambaye anataka kumlea na kumtimizia neema zake kwa mikono ya Mitume wake, zikimuamrisha na kumkumbusha masilahi yake ya kidini na ya kidunia, na kumkataza madhara yake ya kidini na ya kidunia, ambazo zinamtaka kuzipokea kwa kuziamini na kujisalimisha na kuzifuata na kushukuru. Huyu dhalimu alizikabali kwa kinyume cha inavyopasa, akaacha kuziamini wala kuzifuata. Bali alizipa mgongo, na akaziacha nyuma ya mgongo wake. Basi huyu ni miongoni mwa wahalifu wakubwa zaidi wanaostahiki adhabu kali zaidi, na ndiyo maana akasema, "Hakika Sisi tutajilipiza kwa wakosefu."
: 23 - 25 #
{وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَلَا تَكُنْ فِي مِرْيَةٍ مِنْ لِقَائِهِ وَجَعَلْنَاهُ هُدًى لِبَنِي إِسْرَائِيلَ (23) وَجَعَلْنَا مِنْهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا لَمَّا صَبَرُوا وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يُوقِنُونَ (24) إِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَفْصِلُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ (25)}
23. Hakika Sisi tulikwisha mpa Musa Kitabu. Basi usiwe na shaka kuwa kakipokea. Na tukakifanya kuwa ni uwongofu kwa Wana wa Israili. 24. Na tukawafanya miongoni mwa waongozi wanaoongoa watu kwa amri yetu, waliposubiri na wakawa na yakini na Ishara zetu. 25. Hakika Mola wako Mlezi ndiye atakayefafanua baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakihitalifiana ndani yake.
#
{23} لما ذكر تعالى آياتِهِ التي ذَكَّرَ بها عباده، وهو القرآن الذي أنزله على محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -، ذكر أنه ليس ببدع من الكتب، ولا من جاء به بغريب من الرسل، فقد آتى اللَّه {موسى الكتابَ}: الذي هو التوراة المصدِّقَةُ للقرآن، التي قد صَدَّقَها القرآنُ، فتطابق حقُّهما، وثبت برهانُهما. {فلا تكن في مريةٍ من لقائِهِ}: لأنَّه قد تواردتْ أدلَّة الحق وبيناتُه، فلم يبق للشكِّ والمريةِ محلٌّ، {وجعلناه}؛ أي: الكتاب الذي آتيناه موسى {هدىً لبني إسرائيلَ}: يهتدونَ به في أصول دينهم، وفروعهم، وشرائعه موافقةٌ لذلك الزمان في بني إسرائيل، وأما هذا القرآن الكريم؛ فجعله الله هدايةً للناس كلِّهم؛ لأنَّه هدايةٌ للخلق في أمر دينهم ودُنياهم إلى يوم القيامة، وذلك لكمالِهِ وعلوِّه، {وإنَّه في أمِّ الكتاب لَدَيْنا لَعَلِيٌّ حكيمٌ}.
{23} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipozitaja Aya zake alizowakumbusha nazo waja wake, nazo ni Qur-ani aliyomteremshia Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – akataja kuwa hiki si katika Vitabu vya kwanza, na wala yule aliyekileta pia ni mgeni miongoni mwa Mitume. Kwani, Mwenyezi Mungu "alimpa Musa Kitabu" ambacho ni Taurati, ambacho kimeisadikisha Qur-ani, na ambacho Qur'ani imekisadikisha, kwa hivyo haki iliyo katika viwili hivyo ikafanana, na ikathibiti hoja ya viwili hivyo. "Basi usiwe na shaka kuwa kakipokea." Kwa sababu zimekwisha dhihiri hoja za haki na ushahidi wake wa wazi, basi siyo kitu cha kuwa na shaka nacho. "Na tukakifanya;" yaani, Kitabu tulichompa Musa "kuwa ni uwongofu kwa Wana wa Israili," ili waongoke kwacho katika misingi ya dini yao, na matawi yake na sheria zake ni kwa mujibu wa zama hizo katika Wana wa Israili. Na ama Qur-ani hii Tukufu, Mwenyezi Mungu aliifanya kuwa uwongofu kwa viumbe vyote katika mambo ya Dini yao na mambo yao ya dunia yao mpaka Siku ya Kiyama. Na hilo ni kwa sababu ya ukamilifu wake na kutukuka kwake. "Na hakika, hiyo imo katika Asili ya Maandiko yaliyoko kwetu, ni tukufu na yenye hekima."
#
{24} {وجَعَلْنا منهم}؛ أي: من بني إسرائيل، {أئمة يهدونَ بأمرِنا}؛ أي: علماء بالشرع وطرق الهداية مهتدين في أنفسهم يهدون غيرهم بذلك الهدى؛ فالكتاب الذي أُنْزِل إليهم هدى، والمؤمنون به منهم على قسمين: أئمَّة يهدون بأمرِ الله، وأتباعٌ مهتدون بهم، والقسمُ الأول أرفع الدرجات بعد درجة النبوَّة والرسالة، وهي درجة الصديقين، وإنما نالوا هذه الدرجة العالية، {لما صبروا}: على التعلُّم والتعليم والدَّعوة إلى الله والأذى في سبيله، وكفُّوا نفوسَهم عن جِماحها في المعاصي واسترسالِها في الشهوات. {وكانوا بآياتِنا يوقِنونَ}؛ أي: وصلوا في الإيمان بآيات الله إلى درجة اليقين، وهو العلم التامُّ الموجب للعمل، وإنَّما وصلوا إلى درجة اليقين؛ لأنَّهم تعلَّموا تعلُّما صحيحاً، وأخذوا المسائل عن أدلتها المفيدة لليقين، فما زالوا يتعلَّمون المسائل، ويستدلُّون عليها بكثرة الدَّلائل، حتى وصلوا لذاك؛ فبالصبر واليقين تُنال الإمامة في الدين.
{24} "Na tukawafanya miongoni mwao;" yaani, Wana wa Israili, "waongozi wanaoongoa watu kwa amri yetu." Yaani, wanachuoni wa sheria na njia za uwongofu, ambao wao wenyewe wameongoka na wanaowaongoza wengine kwa uwongofu huo. Kitabu kilichoteremshwa kwao ni uwongofu, na walioamini miongoni mwao wamegawanyika katika makundi mawili: waongozi wanaoongoa kwa amri ya Mwenyezi Mungu, na wafuasi wanaoongozwa nao. Na kundi hili la kwanza lina daraja za juu baada ya kiwango cha unabii na utume. Nacho ni kiwango cha wakweli tu. Nao walifikia kiwango hiki cha juu "waliposubiri" juu ya kujifunza, kufundisha, na kulingania kwa Mwenyezi Mungu na kuudhiwa katika njia yake, na wakazizuia nafsi zao dhidi ya kuziingiza katika maasia, na kuziachilia kuendelea katika matamanio. "Na wakawa na yakini na Ishara zetu." Yaani, walifikia kiwango cha yakini katika kumuamini Mwenyezi Mungu na ishara zake, nacho ni kuwa na elimu kamili yenye kulazimu matendo mema. Na walifikia kiwango hiki cha yakini, kwa sababu walijifunza kujifunza sahihi, na wakachukua masuala kutoka katika ushahidi wake wenye yakini, kwa hivyo wakaendelea kujifunza masuala, na kuyatumia kama ushahidi kwa kwa ushahidi mwingi, mpaka wakafikia kiwango hicho. Kwa hivyo, kwa kusubiri na kuwa na yakini mtu anapata kuwa muongozi katika dini.
#
{25} وثمَّ مسائلُ اختلف فيها بنو إسرائيل، منهم من أصاب فيها الحقَّ، ومنهم من أخطأه خطأ أو عمداً، والله تعالى {يَفْصِلُ بينَهم يوم القيامةِ فيما كانوا فيه يختلفونَ}: وهذا القرآن يقصُّ على بني إسرائيل بعض الذي يختلفون فيه؛ فكلُّ خلاف وقع بينهم، ووُجِدَ في القرآن تصديقٌ لأحد القولين؛ فهو الحقُّ، وما عداه مما خالفه باطلٌ.
{25} Na yapo masuala ambayo Wana wa Israili walihitilafiana ndani yake. Baadhi yao waliifikia haki ndani yake na baadhi yao waliokosea si kwa makusudi, au hata kwa kukusudia. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu "atafafanua baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakihitalifiana ndani yake." Na Qur-ani hii inawasimulia Wana wa Israili baadhi ya yale wanayohitalifiana ndani yake. Kwa hivyo, kila tofauti iliyotokea baina yao kulipatikana ndani ya Qur-ani chenye kusadikisha mojawapo ya kauli hizo mbili. Na hiyo ndiyo haki. Na chochote kisichokuwa hiyo miongoni mwa yanayopingana nayo ni batili.
: 26 - 27 #
{أَوَلَمْ يَهْدِ لَهُمْ كَمْ أَهْلَكْنَا مِنْ قَبْلِهِمْ مِنَ الْقُرُونِ يَمْشُونَ فِي مَسَاكِنِهِمْ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ أَفَلَا يَسْمَعُونَ (26) أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا نَسُوقُ الْمَاءَ إِلَى الْأَرْضِ الْجُرُزِ فَنُخْرِجُ بِهِ زَرْعًا تَأْكُلُ مِنْهُ أَنْعَامُهُمْ وَأَنْفُسُهُمْ أَفَلَا يُبْصِرُونَ (27)}
26. Ee! Haijawabainikia kwamba kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao, nao wanapita katika maskani zao hizo? Hakika katika hayo zipo Ishara. Basi, je, hawasikii? 27. Je, hawaoni ya kwamba tunayapeleka maji kwenye ardhi kavu, kisha kwayo tunaitoa mimea wanayokula wanyama wao na wao wenyewe? Je, hawaoni?
#
{26} يعني: أولم يتبيَّن لهؤلاء المكذِّبين للرسول ويهديهم إلى الصواب كم أهْلَكْنا قبلهم من القرون الذين سَلَكوا مسلَكَهم، {يمشون في مساكنهم}: فيشاهِدونها عياناً؛ كقوم هود وصالح وقوم لوط. {إنَّ في ذلك لآياتٍ}: يستدلُّ بها على صدق الرسل التي جاءتهم، وبطلان ما هم عليه من الشرك والشرِّ، وعلى أنَّ مَنْ فعل مثل فعلهم؛ فُعِلَ بهم كما فُعِلَ بأشياعه من قبل، وعلى أنَّ الله تعالى مجازي العباد وباعثهم للحشر والتناد. {أفلا يسمعونَ}: آيات الله، فيعونَها، فينتفِعون بها؛ فلو كان لهم سمعٌ صحيحٌ وعقلٌ رجيحٌ؛ لم يقيموا على حالةٍ يجزم بها بالهلاك.
{26} Maana yake ni kwamba, je haikuwabainikia wale waliomkadhibisha Mtume na kuwaongoa kufikia usahihi kwamba ni kaumu gani tuliziangamiza kabla yao, ambao walichukua njia waliyoichukua wao? "Nao wanapita katika maskani zao hizo?" Na wakayaona kwa macho, kama vile kaumu ya Hud na Salih na watu wa Luti. "Hakika katika hayo zipo Ishara." zinazotumika kuwa ushahidi juu ya ukweli wa Mitume waliowajia, na ubatili wa ushirikina na uovu wanaoufuata, na kwamba anayefanya kama walivyofanya wao, wao pia watafanyiwa kama walivyofanyiwa wenzao zamani, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu atawalipa waja wake na atawafufua kwa ajili ya kuwakusanya na wakawa wanapiga mayowe. "Basi, je, hawasikii?" Aya za Mwenyezi Mungu, na kuzielewa, na wakanufaika nazo? Na lau kuwa wangekuwa na kusikia sahihi na akili timamu, hawangedumu katika hali ambayo ni wazi kwamba wataangamia.
#
{27} {أولم يَرَوْا}: بأبصارهم نعمتنا وكمال حكمتنا، {أنَّا نسوقُ الماء إلى الأرض الجرز}: التي لا نبات فيها، فيسوق الله المطر الذي لم يكنْ قبلُ موجوداً فيها، فيفرِغُه فيها من السحاب أو من الأنهار؛ {فنخرِجُ به زرعاً}؛ أي: نباتاً مختلف الأنواع، {تأكُلُ منه أنعامُهم}: وهو نباتُ البهائم {وأنفسُهُم}: وهو طعام الآدميين. {أفلا يبصِرونَ}: تلك المنَّة التي أحيا الله بها البلاد والعباد، فيستبصِرون فيهتدون بذلك البصر وتلك البصيرة إلى الصراط المستقيم؟ ولكن غلب عليهم العمى، واستولتْ عليهم الغفلة، فلم يبصِروا في ذلك بصر الرجال، وإنَّما نظروا إلى ذلك نظر الغفلة ومجرَّد العادة، فلم يوفَّقوا للخير.
{27} "Je, hawaoni" kwa macho yao neema zetu na ukamilifu wa hekima yetu? "Ya kwamba tunayapeleka maji kwenye ardhi kavu" ambayo haina mimea. Basi Mwenyezi Mungu akaipelekea mvua ambayo haikuwepo hapo kabla, kisha anaimimina humo kutoka mawinguni au mitoni. "Kisha kwayo tunaitoa mimea" ya aina mbalimbali, "wanayokula wanyama wao" katika mimea wanayoila mifugo, "na wao wenyewe" katika chakula cha wanadamu. "Je, hawaoni" neema hii ambayo Mwenyezi Mungu aliihuisha kwayo ardhi na waja, basi wakaiona na wakaongoka kwa uoni huo na ufahamu huo kwenye njia iliyonyooka? Lakini upofu ulikuwa mwingi sana kwao na wakashindwa na kughafilika, kwa hivyo hawakuiona kwa macho ya watu, bali waliitazama kwa mtazamo wa kughafilika na mazoea tu, na hawakuwezeshwa kufikia heri.
: 28 - 30 #
{وَيَقُولُونَ مَتَى هَذَا الْفَتْحُ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (28) قُلْ يَوْمَ الْفَتْحِ لَا يَنْفَعُ الَّذِينَ كَفَرُوا إِيمَانُهُمْ وَلَا هُمْ يُنْظَرُونَ (29) فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَانْتَظِرْ إِنَّهُمْ مُنْتَظِرُونَ (30)}
28. Wanasema: Ushindi huu ni lini, kama nyinyi ni wakweli? 29. Sema: Siku ya Ushindi, wale waliokufuru imani yao haitawafaa kitu, wala wao hawatapewa muhula. 30. Basi wapuuze, nawe ngonja; hakika wao wanangoja.
#
{28} أي: يستعجلُ المجرمون بالعذاب الذي وُعِدوا به على التكذيب جهلاً منهم ومعاندةً، {ويقولونَ متى هذا الفتحُ}: الذي يفتحُ بيننا وبينكم بتعذيبنا على زعمكم {إن كنتُم} [أيها الرسلُ] {صادقينَ}: في دعواكم.
{28} Yaani, wahalifu wanaiharakisha adhabu waliyoahidiwa kwa sababu ya kukadhibisha kwao, kwa ujinga tu na ukaidi. "Na wanasema: Ushindi huu ni lini," ili ipambanulie baina yetu na nyinyi kwa kutuadhibu kulingana na madai yenu, "kama nyinyi" -enyi Mitume - "ni wakweli" katika madai yenu?
#
{29} {قُلْ يومَ الفتح}: الذي يحصُلُ به عقابُكم لا تستفيدون به شيئاً؛ فلو كان إذا حَصَلَ؛ حَصَلَ إمهالُكم لتستدركوا ما فاتكم حين صار الأمر عندكم يقيناً؛ لكان لذلك وجه، ولكن إذا جاء يومُ الفتح؛ انقضى الأمرُ، ولم يبق للمحنةِ والابتلاء محلٌّ، فلا {ينفعُ الذين كفروا إيمانُهم}: لأنَّه صار إيمانَ ضرورةٍ، {ولا هم يُنظَرون}؛ أي: يُمْهَلون، فيؤخَّرُ عنهم العذاب، فيستدركون أمرهم.
{29} "Sema: Siku ya Ushindi" ambayo siku hiyo ndipo mtaadhibiwa, wala hamtafaidika nayo kwa chochote. Na ikiwa ingekuwa kwamba ikitokea, mtapewa muhula ili myafanye yale ambayo yaliwapita wakati jambo hilo lilikuwa ni la yakini kwenu, basi hilo lingekuwa jambo bora. Lakini ikiwa siku ya ushindi itafika; jambo hilo litapita, na hakuna nafasi itakayobakia kwa ajili ya kupeana mtihani na majaribio, basi "wale waliokufuru imani yao haitawafaa kitu" kwa sababu hiyo sasa itakuwa ni imani ya lazima, "wala wao hawatapewa muhula," kwa kucheleweshewa adhabu ili watekeleze yale ambayo hawakutekeleza.
#
{30} {فأعرض عنهم}: لما وصل خطابهم لك وظلمهم إلى حالة الجَهْل واستعجال العذاب. {وانتظر}: الأمر الذي يَحِلُّ بهم؛ فإنَّه لا بدَّ منه، ولكن له أجلٌ إذا جاء لا يتقدَّم ولا يتأخَّر، {إنَّهم منتظرونَ}: بك رَيْبَ المنون، ومتربِّصون بكم دوائرَ السوء، والعاقبة للتقوى.
{30} "Basi wapuuze" pindi maneno yao hayo na dhuluma yao ilipofikia hali ya ujinga na kujiharakishia adhabu. "Nawe ngonja" jambo ambalo litawapata. Kwani, ni jambo ambalo halina budi litokee, lakini lina muda maalumu. Likifika, halitasonga mbele wala halitachelewa. "Hakika wao wanangoja" kupatilizwa na dahari, na wanawangojeleeni mambo yakugeukieni, lakini mwisho mwema ni wa uchamungu.
Imekamilika tafsiri ya Surat Sajda kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na neema yake. Na ni zake Mtukufu sifa zote kamili, na kutajwa kwa uzuri na utukufu. Na ni zake Mtukufu sifa zote kamili, na kutajwa kwa uzuri na utukufu.
* * *