:
Tafsir ya Surat Luqman
Tafsir ya Surat Luqman
Nayo iliteremka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
: 1 - 5 #
{الم (1) تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْحَكِيمِ (2) هُدًى وَرَحْمَةً لِلْمُحْسِنِينَ (3) الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ بِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ (4) أُولَئِكَ عَلَى هُدًى مِنْ رَبِّهِمْ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ (5)}
1. Alif Laam Miim 2. Hizi ni Aya za Kitabu chenye hekima. 3. Kuwa ni Uwongofu na rehema kwa wafanyao wema. 4. Wale wanaoshika Swala, na wanatoa Zaka, nao wana yakini na Akhera. 5. Hao ndio walio kwenye uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio waliofaulu.
#
{2} يشيرُ تعالى إشارةً دالَّةً على التعظيم إلى {آيات الكتاب الحكيم}؛ أي: آياتُهُ محكمةٌ صدرتْ من حكيم خبير. ومن إحكامها أنَّها جاءت بأجلِّ الألفاظ وأفصحها وأبينها، الدالَّة على أجلِّ المعاني وأحسنها. ومن إحكامها أنها محفوظةٌ من التغييرِ والتبديل والزيادة والنقص والتحريف. ومن إحكامها أنَّ جميعَ ما فيها من الأخبار السابقةِ واللاحقة والأمور الغيبيَّة كلِّها مطابقةٌ للواقع، مطابقٌ لها الواقع، لم يخالِفْها كتابٌ من الكتب الإلهية، ولم يخبر بخلافها نبيٌّ من الأنبياء، ولم يأتِ ولن يأتيَ علم محسوسٌ ولا معقولٌ صحيحٌ يناقِضُ ما دلَّتْ عليه. ومن إحكامها أنها ما أَمَرَتْ بشيء إلاَّ وهو خالصُ المصلحة أو راجِحُها، ولا نَهَتْ عن شيء إلاَّ وهو خالصُ المفسدة أو راجِحُها، وكثيراً ما يجمع بين الأمر بالشيء مع ذكر حكمتِهِ وفائدتِهِ، والنهي عن الشيء مع ذكرِ مضرَّتِهِ. ومن إحكامها أنَّها جمعت بين الترغيب والترهيب والوعظ البليغ الذي تعتدل به النفوس الخيِّرة، وتحتكمُ فتعملُ بالحزم. ومن إحكامها: أنَّك تَجِدُ آياتها المتكرِّرة كالقصص والأحكام ونحوها قد اتَّفقت كلُّها وتواطأت، فليس فيها تناقضٌ ولا اختلافٌ؛ فكلَّما ازدادَ بها البصير تدبُّراً وأعمل فيها العقل تفكُّراً؛ انبهر عقلُه وذهلَ لبُّه من التوافُق والتواطُؤ، وجزم جزماً لا يُمْتَرى فيه أنه تنزيلٌ من حكيم حميدٍ.
{2} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaashiria ishara ya kuonyesha taadhima ya "Aya za Kitabu chenye hekima." Yaani, aya zake ni madhubuti ambazo zilitoka kwa Mwenye hekima, Mwenye habari zote. Na katika umadhubuti wake ni kwamba zilikuja na maneno matukufu zaidi, na yenye ufasaha mkubwa zaidi katika kubainisha, zenye kuonyesha maana tukufu zaidi, na zilizo nzuri zaidi. Na katika umadhubuti wake ni kwamba zimehifadhiwa kutokana na kugeuzwa, kubadilishwa, kuongezewa kitu, kupunguzwa na kupotoshwa. Na miongoni mwa hukumu zake ni kwamba, habari zote zilizotangulia na zilizofuata na mambo ya ghaibu zilizo ndani yake, zinafanana na uhalisia, na uhalisia unafanana nayo. Hakuna kitabu chochote miongoni mwa vitabu vya Mwenyezi Mungu kilichokipinga, wala hakuna Mtume yeyote aliyesema kinyume chake, wala haijawahi kuja na wala haitakuja elimu yoyote inayohisiwa wala jambo la kiakili lililo sahihi ambalo linapingana na kile ambacho kinaonyesha. Na miongoni mwa uimara wake ni kwamba haikuamrisha chochote isipokuwa ni chenye manufaa matupu au chenye uwezekano mkubwa wa kuleta manufaa, wala haikukatazi chochote isipokuwa ni chenye madhara matupu au chenye uwezekano mkubwa wa kuleta madhara. Na mara nyingi hujumuisha kuamrisha kitu pamoja na kutaja hekima yake na faida yake, na kukataza kitu pamoja na kutaja madhara yake. Na miongoni mwa uimara wake ni kwamba kilijumuisha kati ya kutia moyo, kutishia, na kuaidhi kwa njia bora zaidi, ambako kwayo nafsi nzuri zinakuwa sawasawa. Na miongoni mwa uimara wake ni kwamba utazikuta Aya zake zinazorudiwarudiwa, kama vile za hadithi, hukumu mbalimbali na mfano wa hayo, zote zinaafikiana, na hakuna mgongano wowote ndani yake wala kutofautiana. Kwa hivyo, kila mwenye ufahamu anapozidi kwazo kuzingatia na akatumia akili yake katika kutafakari; akili yake na moyo wake vinastaajabu kwa sababu ya kuafikiana kwake, kwa hivyo anakuwa na uhakika mkubwa ambao hauna shaka yoyote kwamba ni ufunuo kutoka kwa Mwenye hekima, Msifiwa.
#
{3} ولكن مع أنه حكيمٌ يدعو إلى كلِّ خُلُق كريم وينهى عن كلِّ خُلُقٍ لئيم، أكثرُ الناس محرومون من الاهتداءِ به، معرِضون عن الإيمان والعمل به؛ إلاَّ مَنْ وفَّقَه الله تعالى وعَصَمَه، وهم المحسنون في عبادة ربِّهم، والمحسِنون إلى الخلق؛ فإنَّه {هدىً}: لهم يهديهم إلى الصراط المستقيم، ويحذِّرهم من طرق الجحيم. {ورحمةً}: لهم تحصُلُ لهم به السعادةُ في الدنيا والآخرة والخيرُ الكثيرُ والثوابُ الجزيلُ والفرح والسرور، ويندفِعُ عنهم الضَّلال والشقاءُ.
{3} Lakini pamoja na kwamba Yeye ni Mwenye hekima analingania kwenye kila tabia tukufu na anakataza kila tabia mbaya, watu wengi wamenyimwa kuongoka kwacho, wamejitenga na kukiamini na kukifanyia kazi. Isipokuwa wale ambao Mwenyezi Mungu amewawezesha na akamlinda, na hao ndio wale wanaomuabudu Mola wao Mlezi kwa uzuri sana, na wanaowafanyia wema viumbe. Kwani huo ndio "uwongofu" kwao unaowaongoa kwenye njia iliyonyooka, na kinawatahadharisha kutokana na njia za Jahannamu. "Na rehema" kwao, ambayo kwayo wanapata furaha katika dunia na Akhera, na heri nyingi, na malipo mengi, na furaha, raha, na wanazuilika kutokana na upotovu na mashaka.
#
{4} ثم وَصَفَ المحسنين بالعلم التامِّ، وهو اليقين الموجب للعمل والخوف من عقاب الله، فيتركون معاصيه، ووصَفَهم بالعمل، وخصَّ من العمل عملين فاضلينِ: {الصلاة} المشتمِلَة على الإخلاص، ومناجاة الله تعالى، والتعبُّد العامِّ للقلب واللسان والجوارح المعينة على سائر الأعمال. {والزَّكاة}: التي تُزَكِّي صاحبها من الصفات الرذيلة، وتنفعُ أخاه المسلمَ وتسدُّ حاجته، ويَبينُ بها أنَّ العبدَ يُؤْثِرُ محبَّةَ الله على محبَّتِهِ للمال، فيخرِجُ محبوبَه من المال لما هو أحبُّ إليه، وهو طلب مرضاة الله.
{4} Kisha akawaelezea wafanyao wema kwa elimu kamili, ambayo ni yakini inayowalazimu kutenda na kuhofu adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo wanaacha kumuasi. Na akawaelezea kuwa wanatenda matendo, na akataja hasa matendo mawili bora: "Swala " ambayo inajumuisha ikhlasi, na kunong'ona na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuabudu kwa ujumla kwa moyo, ulimi, na viungo vinavyosaidia juu ya kutekeleza matendo mengine yote. Na "Zaka," ambayo humtakasa mwenyewe kutokana na tabia mbaya, na humnufaisha nduguye Mwislamu na humkidhia haja zake, na kwayo inabainika kwamba mja anapendelea mapenzi ya Mwenyezi Mungu kuliko kupenda mali, kwa kutoa mali yake pendwa kwa ajili ya kile kilicho kipenzi zaidi kwake, ambacho ni kutafuta radhi ya Mwenyezi Mungu.
#
{5} فَـ {أولئك}: المحسنون الجامعون بين العلم التامِّ والعمل {على هدىً}؛ أي: عظيم كما يفيدُه التنكيرُ، وذلك الهدى حاصلٌ لهم وواصلٌ إليهم {من ربِّهم}: الذي لم يَزَلْ يربِّيهم بالنعم ويدفَعُ عنهم النِّقَمَ، وهذا الهدى الذي أوصله إليهم من تربيتِهِ الخاصَّة بأوليائه، وهو أفضلُ أنواع التربية. {وأولئك هم المفلحونَ}: الذين أدركوا رضا ربِّهم وثوابَه الدنيوي والأخروي، وسلموا من سَخَطِهِ وعقابه، وذلك لسلوكهم طريقَ الفلاح، الذي لا طريقَ له غيرها.
{5} Basi, "hao" wafanyao wema waliojumuisha kati ya elimu kamili na matendo "ndio walio kwenye uwongofu" mkubwa, kama inavyodhihirika katika ukawaida wa neno 'uwongofu'. Na uwongofu huo umeshapatikana ndani yao na umeshawafikia "kutoka kwa Mola wao Mlezi," ambaye hajaacha kuwalea kwa neema zake na kuwaepusha kutokana na adhabu. Na uwongofu huu aliowafikishia ni katika ulezi wake maalumu kwa vipenzi wake, nayo ndiyo malezi bora zaidi. "Na hao ndio waliofaulu," ambao walipata radhi za Mola wao Mlezi na malipo Yake ya dunia na ya kiakhera, na wakaepushwa na ghadhabu yake na adhabu yake, kwa sababu walifuata njia ya kufaulu ambako hakuna njia yake nyingine isipokuwa hiyo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alipowataja wale waliongoka kwa Qur-ani, wanaoifuata, akamtaja aliyejiepusha nayo na wala hakuijali, na kwamba aliadhibiwa kwa hilo kwa kuchukua badala yake kila batili ya kimaneno, kwa hivyo akaacha maneno ya juu kabisa na hadithi iliyo bora zaidi, na badala yake akachukua kauli ya chini kabisa na mbaya zaidi. Na ndiyo maana akasema:
: 6 - 9 #
{وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا أُولَئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُهِينٌ (6) وَإِذَا تُتْلَى عَلَيْهِ آيَاتُنَا وَلَّى مُسْتَكْبِرًا كَأَنْ لَمْ يَسْمَعْهَا كَأَنَّ فِي أُذُنَيْهِ وَقْرًا فَبَشِّرْهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ (7) إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ جَنَّاتُ النَّعِيمِ (8) خَالِدِينَ فِيهَا وَعْدَ اللَّهِ حَقًّا وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (9)}.
6. Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu mbali na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni masihara. Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha. 7. Na mtu kama huyo anaposomewa Aya zetu, huzipa mgongo kwa kujivuna, kana kwamba hakuzisikia, au masikioni mwake mna uziwi. Basi mbashirie kuwa atapata adhabu chungu. 8. Hakika walioamini na wakatenda mema watakuwa na Bustani za neema. 9. Watadumu humo, ni ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kweli. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
#
{6} أي: {ومن الناس من}: هو محرومٌ مخذولٌ {يشتري}؛ أي: يختارُ ويرغب رغبة من يبذُلُ الثمن في الشيء، {لهو الحديث}؛ أي: الأحاديث الملهية للقلوب، الصادَّة لها عن أجلِّ مطلوب، فدخل في هذا كلُّ كلام محرَّم وكلُّ لغوٍ وباطل وهَذَيان؛ من الأقوال المرغِّبة في الكفر والفسوق والعصيان، ومن أقوال الرادِّين على الحقِّ المجادلين بالباطل لِيُدْحِضوا به الحقَّ، ومن غيبةٍ ونميمةٍ وكذبٍ وشتم وسبٍّ، ومن غناء ومزامير شيطان. ومن الماجرياتِ الملهيةِ التي لا نفع فيها في دين ولا دُنيا؛ فهذا الصنف من الناس {يشتري لهو الحديث} عن هدي الحديث {ليضلَّ} الناس {بغير علم}؛ أي: بعد ما ضلَّ في فعله أضلَّ غيرَه؛ لأنَّ الإضلال ناشئٌ عن الضَّلال، وإضلالُه في هذا الحديث صدُّه عن الحديث النافع والعمل النافع والحقِّ المُبين والصراطِ المستقيم، ولا يتمُّ له هذا حتى يقدحَ في الهدى والحقِّ، ويتَّخذ آيات الله هُزواً، يَسْخَرُ بها وبِمَنْ جاء بها؛ فإذا جمع بين مدح الباطل والترغيب فيه والقدح في الحقِّ والاستهزاء به وبأهله؛ أضلَّ مَنْ لا علم عندَه، وخَدَعَه بما يوحيه إليه من القول الذي لا يميِّزه ذلك الضالُّ، ولا يعرف حقيقته، {أولئك لهم عذابٌ (مهينٌ)}: بما ضلُّوا، وأضلُّوا، واستهزؤوا بآيات الله، وكذَّبوا الحقَّ الواضح.
{6} "Na miongoni mwa watu wapo," wale walionyimwa na kuachwa "wanaonunua" yaani, wanachagua na kutamani kama kutamani kwa mwenye kutumia thamani katika ya kitu, "maneno ya upuuzi" yenye kusahaulisha nyoyo na kuziuia mambo makubwa zaidi yatafutwayo. Kwa hivyo yanaingia humo kila kauli iliyoharamishwa, na kila upuuzi batili na kuropokwa kama vile maneno yanayohimiza ukafiri na kuvuka mipaka na kuasi, na pia kauli za wale wanaoikataa haki na kubishana kwa batili ili waivunje haki kwa hayo, na pia kunaingia humo kusengenya, kufitinisha, kusema uongo, kutukana, na pia kuimba na miziki ya Shetani. na vile vile matukio yanayoghafilisha ambayo hayana faida yoyote katika dini wala dunia. Kwa hivyo watu wa aina hii "hununua maneno ya upuuzi" wakaacha maneno ya uongofu "ili wawapoteze" watu "mbali na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua." Yaani, baada ya yeye mwenye kupotea katika matendo yake, akawapoteza wengine. Kwa sababu kupoteza kwake huko kulitokana na kupotea kwake. Na kupoteza kwake katika Hadithi hii ni kuzuilia kwake wengine kufikia hadithi yenye manufaa, na matendo yenye manufaa, na haki iliyo wazi, na njia iliyonyooka. Na jambo hili haliwezi kutimia mpaka akosoe uongofu na haki, na akazichukua Aya za Mwenyezi Mungu kuwa ni mzaha, akawa anazikejeli na pia anamkejeli aliyekuja nazo. Basi anapokusanya kati ya kuisifu batili na kuhimiza juu yake, na kukosoa haki na kuifanyia mzaha na watu wake, anampoteza asiyekuwa na elimu, na anamdanganya kwa yale anayomwambia ambayo ni maneno asiyoweza kuyatambua huyo anayepotea na wala hata hajui uhakika wake. "Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha" kwa sababu walipotea na wakapoteza, na wakazifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu, na wakaikadhibisha haki iliyo wazi.
#
{7} ولهذا قال: {وإذا تُتلى عليه آياتُنا}: ليؤمنَ بها وينقادَ لها، {ولَّى مستكبراً}؛ أي: أدبر إدبار مستكبرٍ عنها رادٍّ لها ولم تدخُلْ قلبَه ولا أثَّرتْ فيه بل أدبر عنها {كأن لم يَسْمَعْها}، بل: {كأنَّ في أذُنَيْه وقراً}؛ أي: صمماً لا تصلُ إليها الأصوات؛ فهذا لا حيلة في هدايتِهِ. {فبشِّرْه}: بشارةً تؤثِّر في قلبه الحزنَ والغمَّ، وفي بشرتِهِ السوء والظُّلمة والغبرة، {بعذابٍ أليم}: مؤلم لقلبِهِ ولبدنِهِ، لا يقادَرُ قدرُهُ، ولا يُدرى بعظيم أمره؛ فهذه بشارةُ أهل الشرِّ؛ فلا نعمتِ البشارةُ.
{7} Na ndiyo maana akasema, "Na mtu kama huyo anaposomewa Aya zetu" ili aziamini na kuzinyenyekea, "huzipa mgongo kwa kujivuna" wala haziingii moyoni mwake wala hazikumuathiri, "kana kwamba hakuzisikia" bali "ni kana kwamba masikioni mwake mna uziwi," ambapo sauti haziwezi kuyafikia, basi huyu hakuna njia ya kumuongoza. "Basi mbashirie" bishara itakayoathiri moyo wake kwa huzuni na majonzi, na uovu, giza na mavumbi katika ngozi yake, "kuwa atapata adhabu chungu;" yenye kuumiza moyo wake na mwili wake, wala haiwezekani kupimwa kiasi chake wala haiwezekani kujua ukubwa wa jambo lake. Hii ndiyo bishara ya watu waovu. Na hii kweli si bishara njema hata kidogo.
#
{8 - 9} وأما بشارةُ أهل الخير؛ فقال: {إنَّ الذين آمنوا وعَمِلوا الصالحاتِ}: جمعوا بينَ عبادة الباطن بالإيمان والظاهر بالإسلام والعمل الصالح، {لهم جناتُ النعيم}: بشارةً لهم بما قدَّموه وقِرىً لهم بما أسلفوه {خالدين فيها}؛ أي: في جنات النعيم نعيم القلب والروح والبدن. {وعد الله حقًّا}: لا يمكن أن يُخْلَفَ ولا يغيَّر ولا يتبدَّل. {وهو العزيزُ الحكيم}: كامل العزَّة، كامل الحكمة، من عزَّته وحكمتِهِ، وَفَّق من وَفَّق، وخَذَل بحسب ما اقتضاه علمُه فيهم وحكمتُه.
{8 - 9} Na ama habari ya watu wema, akasema "Hakika walioamini na wakatenda mema," waliokusanya kati ya kuabudu kwa ndani kwa kuamini, na kwa nje, kwa Uislamu na matendo mema, "watakuwa na mabustani ya neema," iwe bishara kwao kwa yale waliyoyatanguliza na makaribisho mazuri kwao kwa yale waliyoyatanguliza. "Watadumu humo" huku wakifurahia kwa moyo, roho na mwili. "Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kweli," haiwezi kuvunjwa wala kugeuzwa wala kubadilishwa. "Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima," Mkamilifu wa nguvu, Mkamilifu wa hekima, na kutokana na nguvu yake na hekima yake, aliwawezesha wale aliowawezesha, na akawachilia mbali wengine kulingana na ilivyohitaji elimu yake juu yao na hekima yake.
: 10 - 11 #
{خَلَقَ السَّمَاوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا وَأَلْقَى فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَنْ تَمِيدَ بِكُمْ وَبَثَّ فِيهَا مِنْ كُلِّ دَابَّةٍ وَأَنْزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَنْبَتْنَا فِيهَا مِنْ كُلِّ زَوْجٍ كَرِيمٍ (10) هَذَا خَلْقُ اللَّهِ فَأَرُونِي مَاذَا خَلَقَ الَّذِينَ مِنْ دُونِهِ بَلِ الظَّالِمُونَ فِي ضَلَالٍ مُبِينٍ (11)}
10. Ameziumba mbingu bila ya nguzo mnazoziona, na ameweka katika ardhi milima ili ardhi isiwayumbishe, na ametawanya humo kila namna ya wanyama, na tumeteremsha maji kutoka mbinguni, na tukaotesha katika ardhi mimea mizuri ya kila namna. 11. Huu ni uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Basi nionyesheni wameumba nini hao wasiokuwa Yeye! Lakini madhalimu wamo katika upotovu ulio dhahiri.
#
{10} يتلو تعالى على عبادِهِ آثاراً من آثار قدرته وبدائعَ من بدائع حكمتِهِ ونعماً من آثار رحمتِهِ، فقال: {خلقَ السمواتِ}: السبع على عظمها وسَعَتها وكثافتها وارتفاعها الهائل {بغير عَمَدٍ تَرَوْنَها}؛ أي: ليس لها عمدٌ، ولو كان لها عَمَدٌ؛ لرؤيتْ، وإنَّما استقرَّتْ، واستمسَكَتْ بقدرة الله تعالى، {وألقى في الأرضِ رواسِيَ}؛ أي: جبالاً عظيمة ركزها في أرجائها وأنحائها لئلاَّ {تميدَ بكم}؛ فلولا الجبالُ الراسياتُ؛ لمادتِ الأرض ولما استقرَّتْ بساكنيها، {وبثَّ فيها من كلِّ دابَّةٍ}؛ أي: نشر في الأرض الواسعة من جميع أصناف الدوابِّ التي هي مسخَّرة لبني آدم ولمصالحهم ومنافعهم، ولمَّا بثَّها في الأرض؛ علم تعالى أنه لا بدَّ لها من رزقٍ تعيشُ به، فأنزل من السماء ماء مباركاً، {فأنبتْنا فيها من كلِّ زوج كريم}: المنظر، نافع، مبارك، فرتعت فيه الدوابُّ المنبثَّة، وسكن إليه كلُّ حيوان.
{10} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawasomea waja wake athari miongoni mwa athari za uweza wake, na maajabu miongoni mwa maajabu ya hekima yake, na neema miongoni mwa athari za rehema yake. "Ameziumba mbingu" saba pamoja na ukubwa wake, upana wake, uzito wake na kuinuka kwake juu kukubwa mno, "bila ya nguzo mnazoziona." Na kama zingekuwa na nguzo, zingeonekana, lakini zilitulia na zikashikamana kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Na ameweka katika ardhi milima" mikubwa aliyoiweka katika sehemu mbalimbali na pande zake ili “isiwayumbishe." Lau si milima iliyothibitika, basi ardhi ingenyumbayumba, na wala haingetulia kwa ajili ya wanaokaa humo, "na ametawanya humo kila namna ya wanyama" ambao wametiishwa kwa ajili ya wanadamu na kwa masilahi na manufaa yao. Na alipowatawanya katika ardhi, Mwenyezi Mungu Mtukufu alijua kwamba watahitaji riziki ya kuishi, basi akateremsha kutoka mbinguni maji yenye baraka. "Na tukaotesha katika ardhi mimea mizuri ya kila namna," kwa muonekano, yenye manufaa na yenye baraka. Kwa hivyo, wanyama hao waliotawanywa wakala humo, na wakakaa humo kwa utulivu.
#
{11} {هذا}؛ أي: خَلْقُ العالم العلويِّ والسفليِّ من جماد وحيوانٍ وسوق أرزاق الخلق إليهم، {خَلْقُ الله}: وحدَه لا شريكَ له، كلٌّ مقرٌّ بذلك، حتى أنتم يا معشر المشركين، {فأروني ماذا خَلَقَ الذين من دونِهِ}؛ أي: الذين جَعَلْتُموهم له شركاءَ تدعونهم وتعبدونهم، يلزم على هذا أن يكون لهم خَلْقٌ كخلقِهِ ورزقٌ كرزقِهِ؛ فإنْ كان لهم شيء من ذلك؛ فأرونيه؛ ليصحَّ ما ادَّعيتم فيهم من استحقاق العبادة. ومن المعلوم أنَّهم لا يقدرونَ أن يُروه شيئاً من الخلق لها؛ لأنَّ جميع المذكورات قد أقرُّوا أنَّها خلق الله وحده، ولا ثَمَّ شيءٌ يعلم غيرها، فثبت عجزُهم عن إثبات شيء لها تستحقُّ به أن تُعبد، ولكن عبادتُهم إيَّاها عن غير علم وبصيرةٍ، بل عن جهل وضلال، ولهذا قال: {بل الظالمون في ضلال مبينٍ}؛ أي: جليٍّ واضح؛ حيث عَبَدوا من لا يملكُ نفعاً ولا ضرًّا ولا موتاً ولا حياةً ولا نشوراً، وتركوا الإخلاص للخالقِ الرازق المالك لكلِّ الأمور.
{11} "Huu," yaani kuumba ulimwengu wa juu na wa chini na vilivyomo kama vile vitu visivyo na uhai na wanyama, na kuwafikishia viumbe riziki zao; "ni uumbaji wa Mwenyezi Mungu" peke yake, hana mshirika yeyote, jambo ambalo kila mtu anakiri, hata nyinyi washirikina. "Basi nionyesheni wameumba nini hao wasiokuwa Yeye," ambao mliwafanya kuwa washirika wake, mkawaomba na kuwaabudu, jambo linalolazimu kwamba wao pia wana uumbaji kama uumbaji wake, na riziki kama riziki yake. Basi ikiwa wanayo yoyote katika hayo, basi nionyesheni ili yawe sahihi hayo mliyodai kuhusiana nao ya kuwa wanastahiki kuabudiwa. Na inavyojulikana ni kuwa hawawezi kumuonyesha chochote ambacho hao waliumba; kwa sababu walishakiri kwamba mambo yote yaliyotajwa ni uumbaji wa Mwenyezi Mungu peke yake, na hakuna chochote kinachojulikana isipokuwa hivyo. Kwa hivyo, kukathibiti kutoweza kwao kuwathibitishia hao chochote ambacho kwacho wanastahiki kuabudiwa. Lakini kuwaabudu kwao huko ni bila ya elimu na ufahamu, bali ni kwa ujinga na upotofu, na ndiyo maana akasema, "Lakini madhalimu wamo katika upotovu ulio dhahiri," ambapo waliabudu yule ambaye hamiliki manufaa yoyote, wala madhara, wala kifo, wala uhai, wala ufufuo, na wakaacha kumfanyia ikhlas Muumba, Mwenye kuruzuku, Mmiliki wa mambo yote.
: 12 - 19 #
{وَلَقَدْ آتَيْنَا لُقْمَانَ الْحِكْمَةَ أَنِ اشْكُرْ لِلَّهِ وَمَنْ يَشْكُرْ فَإِنَّمَا يَشْكُرُ لِنَفْسِهِ وَمَنْ كَفَرَ فَإِنَّ اللَّهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ (12) وَإِذْ قَالَ لُقْمَانُ لِابْنِهِ وَهُوَ يَعِظُهُ يَابُنَيَّ لَا تُشْرِكْ بِاللَّهِ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ (13) وَوَصَّيْنَا الْإِنْسَانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْنًا عَلَى وَهْنٍ وَفِصَالُهُ فِي عَامَيْنِ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُ (14) وَإِنْ جَاهَدَاكَ عَلَى أَنْ تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا وَاتَّبِعْ سَبِيلَ مَنْ أَنَابَ إِلَيَّ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُمْ بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ (15) يَابُنَيَّ إِنَّهَا إِنْ تَكُ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِنْ خَرْدَلٍ فَتَكُنْ فِي صَخْرَةٍ أَوْ فِي السَّمَاوَاتِ أَوْ فِي الْأَرْضِ يَأْتِ بِهَا اللَّهُ إِنَّ اللَّهَ لَطِيفٌ خَبِيرٌ (16) يَابُنَيَّ أَقِمِ الصَّلَاةَ وَأْمُرْ بِالْمَعْرُوفِ وَانْهَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَاصْبِرْ عَلَى مَا أَصَابَكَ إِنَّ ذَلِكَ مِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ (17) وَلَا تُصَعِّرْ خَدَّكَ لِلنَّاسِ وَلَا تَمْشِ فِي الْأَرْضِ مَرَحًا إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ (18) وَاقْصِدْ فِي مَشْيِكَ وَاغْضُضْ مِنْ صَوْتِكَ إِنَّ أَنْكَرَ الْأَصْوَاتِ لَصَوْتُ الْحَمِيرِ (19)}.
12. Na tulimpa Luqman hekima, tukamwambia; "Mshukuru Mwenyezi Mungu." Na mwenye kushukuru, basi hakika anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake. Na aliyekufuru, basi Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Msifiwa. 13. Na Luqman alipomwambia mwanawe kwa kumpa mawaidha, "Ewe mwanangu, usimshirikishe Mwenyezi Mungu. Kwani, hakika ushirikina bila ya shaka ni dhuluma iliyo kubwa." 14. Na tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili. Tumemuusia, "Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni kwangu Mimi ndiyo marejeo yenu." 15. Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii. Lakini kaa nao kwa wema duniani, nawe ishike njia ya anayeelekea kwangu. Kisha marejeo yenu ni kwangu Mimi, na Mimi nitawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda. 16. "Ewe mwanangu, kikiwapo kitu cha uzito wa chembe ya khardali kikawa ndani ya jabali au ndani ya mbingu au ndani ya ardhi, basi Mwenyezi Mungu atakileta. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyofichika, Mwenye habari za yote. 17. Ewe mwanangu, shika Swala, na amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayokupata. Hayo ni katika mambo ya kuazimiwa. 18. Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika nchi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anayejivuna na kujifakhirisha. 19. Na ushike mwendo wa katikati, na teremsha sauti yako. Hakika katika sauti mbaya zote bila ya shaka iliyozidi ni sauti ya punda.
#
{12} يخبرُ تعالى عن امتنانِهِ على عبدِهِ الفاضل لقمان بالحكمة، وهي العلم بالحقِّ على وجهه وحكمته؛ فهي العلم بالأحكام، ومعرفةُ ما فيها من الأسرار والأحكام؛ فقد يكون الإنسانُ عالماً ولا يكون حكيماً، وأما الحكمة؛ فهي مستلزمةٌ للعلم، بل وللعمل، ولهذا فُسِّرت الحكمةُ بالعلم النافع والعمل الصالح. ولمَّا أعطاه اللَّه هذه المنَّة العظيمة؛ أمره أن يشكره على ما أعطاه؛ ليباركَ له فيه، وليزيدَه من فضله، وأخبره أنَّ شكر الشاكرين يعودُ نفعُه عليهم، وأنَّ من كفر فلم يشكُر اللَّه؛ عاد وبالُ ذلك عليه، والله غنيٌّ عنه حميدٌ فيما يقدِّره ويقضيه على مَنْ خالف أمره؛ فغناه تعالى من لوازم ذاته، وكونُه حميداً في صفات كماله حميداً في جميل صنعه من لوازم ذاته، وكلُّ واحد من الوصفين صفة كمال، واجتماع أحدهما إلى الآخر زيادة كمال إلى كمال. واختلف المفسرون هل كان لقمانُ نبيًّا أو عبداً صالحاً ، والله تعالى لم يذكُر عنه إلاَّ أنه آتاه الحكمة، وذكر بعضَ ما يدلُّ على حكمته في وعظه لابنه، فذكر أصول الحكمة وقواعدها الكبار، فقال:
{12} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu neema zake kwa mja wake mwema Luqman kwa kumpa hekima, ambayo ni kujua haki kama ilivyo na hekima yake, kwa kujua hukumu mbalimbali, na kujua siri zilizomo ndani yake. Kwani, mtu anaweza kuwa anajua kitu lakini hana hekima. Na ama hekima, hiyo hulazimu kwamba mtu huyo ana elimu, na hata pia matendo. Na ndiyo maana hekima imefasiriwa kuwa ni elimu yenye manufaa na matendo mema. Na Mwenyezi Mungu alipompa neema hii kuu; akamuamuru kwamba amshukuru kwa hayo aliyompa; ili ambariki ndani yake, na amzidishie katika fadhila zake, na akamwambia kuwa kushukuru kwa wenye kushukuru kunawafaa wao wenyewe, na kwamba mwenye kukufuru na asimshukuru Mwenyezi Mungu; msiba wa hayo unamrudia yeye mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Msifiwa kwa yale anayoyapanga na kuwapitishia wale wanaohalifu amri yake. Ukwasi wake Yeye Mtukufu ni katika mambo yasiyotengana na dhati yake, na kwamba Yeye ni Msifiwa katika sifa zaka za ukamilifu, na ni Msifiwa katika vitendo vyake vizuri. Na kila moja katika sifa zake hizi ni sifa ya ukamilifu, na kukutana kwamba mbili hizo kunaozidisha ukamilifu juu ya ukamilifu. Wafasiri wamehitalifiana kuhusu Luqman iwapo ni Nabii au mja mwema tu. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu hakutaja kumhusu isipokuwa tu kwamba alimpa hekima, na akataja baadhi ya mambo yanayoashiria hekima yake katika mawaidha yake kwa mwanawe. Kwa hivyo akataja misingi ya hekima na kanuni zake kuu. Akasema:
#
{13} {وإذ قال لقمانُ لابنِهِ وهو يَعِظُهُ}؛ أو: قال له قولاً به يعظه، والوعظُ: الأمرُ والنهيُ المقرون بالترغيب والترهيب؛ فأمَرَهُ بالإخلاص ونهاه عن الشرك وبيَّن له السبب في ذلك، فقال: {إنَّ الشركَ لظلمٌ عظيمٌ}: ووجه كونه عظيماً أنَّه لا أفظع وأبشع ممَّن سوَّى المخلوق من تراب بمالك الرقاب، وسوَّى الذي لا يملك من الأمر شيئاً بمالك الأمرِ كلِّه، وسوَّى الناقص الفقير من جميع الوجوه بالربِّ الكامل الغنيِّ من جميع الوجوه، وسوَّى مَن لم يُنْعِمْ بمثقال ذرَّةٍ من النعم، بالذي ما بالخلق من نعمةٍ في دينهم ودنياهم وأخراهم وقلوبهم وأبدانهم إلاَّ منه، ولا يصرف السوء إلاَّ هو؛ فهل أعظم من هذا الظلم شيءٌ؟! وهل أعظمُ ظلماً ممَّن خلقه الله لعبادته وتوحيدِهِ، فذهب بنفسه الشريفة، فجعلها في أخسِّ المراتب، جعلها عابدةً لمن لا يسوى شيئاً، فظلم نفسه ظلماً كبيراً؟!
{13} "Na Luqman alipomwambia mwanawe kwa kumpa mawaidha." Na mawaidha ni kuamrisha na kukataza kwa njia ya kuhimiza na kutishia. Basi akamwamrisha kuwa na ikhlas na akamkataza ushirikina, na akamueleza sababu ya hilo. Akasema: "Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhuluma iliyo kubwa." Na sababu ya kuwa kwake kubwa ni kwamba hakuna kitu kibaya zaidi wala kibovu zaidi, zaidi ya mwenye kutoshanisha kiumbe kilichoumbwa kwa udongo na Yule anayemiliki shingo zote, na akatoshanisha yule asiyemiliki jambo lolote na yule anayemiliki mambo yote, na akatoshanisha mwenye upungufu, masikini kwa namna zote na Mola Mlezi, Mkamilifu, Mkwasi kwa namna zote, na akatoshanisha yule ambaye hakuneemesha hata kwa chembe ya neema na Yule ambaye hakuna kiumbe yeyote aliye na neema yoyote katika dini yao, dunia yao, akhera yao, nyoyo zao na miili yao isipokuwa ni kutoka kwake, na wala hakuna anayeondoa ubaya isipokuwa yeye. Basi je, kuna kitu kikubwa zaidi kuliko dhuluma hii? Je, kuna mwenye dhuluma kubwa zaidi kuliko yule ambaye Mwenyezi Mungu alimuumba ili amuabudu na ampwekeshe, kisha akaichukua nafsi yake yenye heshima na akaiweka katika tabaka za chini kabisa, na akaifanya kuabudu kisicho na thamani yoyote, kwa hivyo akawa amejidhulumu dhuluma kubwa?
#
{14} ولما أمر بالقيام بحقِّه بترك الشرك الذي من لوازمه القيام بالتوحيد؛ أمر بالقيام بحقِّ الوالدين، فقال: {ووصَّيْنا الإنسان}؛ أي: عهدنا إليه وجعلناه وصيةً عنده سنسأله عن القيام بها وهل حَفِظَها أم لا؟ فوصيناه {بوالديه}، وقلنا له: {اشكُرْ لي}: بالقيام بعبوديَّتي وأداء حقوقي وأنْ لا تستعينَ بنعمي على معصيتي {ولوالديك}: بالإحسان إليهما بالقول الليِّن والكلام اللطيف والفعل الجميل والتواضع لهما وإكرامهما وإجلالهما والقيام بمؤونتهما واجتناب الإساءة إليهما من كلِّ وجه بالقول والفعل، فوصيناه بهذه الوصية وأخبرناه أنَّ {إليَّ المصيرُ}؛ أي: سترجع أيُّها الإنسان إلى من وصَّاك وكلَّفك بهذه الحقوق، فيسألك: هل قمتَ بها فيثيبك الثواب الجزيل، أم ضيَّعْتها فيعاقبك العقاب الوبيل؟! ثمَّ ذَكَرَ السببَ الموجبَ لبرِّ الوالدين في الأم، فقال: {حَمَلَتْه أمُّه وهناً على وهنٍ}؛ أي: مشقة على مشقة؛ فلا تزال تلاقي المشاقَّ من حين يكون نطفةً من الوحم والمرض والضعف والثقل وتغير الحال، ثم وجع الولادة ذلك الوجع الشديد، ثم {فصالُهُ في عامينِ}: وهو ملازمٌ لحضانة أمِّه وكفالتها ورضاعها. أفما يحسُنُ بمن تحمَّل على ولده هذه الشدائد مع شدة الحب أن يؤكِّد على ولده، ويوصي إليه بتمام الإحسان إليه؟
{14} Na alipoamrishwa kutekeleza haki yake kwa kuacha ushirikina, jambo ambalo la Iinazimu kumpwekesha; akaamrisha kuzitekeleza haki za wazazi wawili, akasema: "Na tumemuusia mtu," na tutakuja muuliza juu yake je aliitunza amri hii au hakuitunza? Basi tukamuusia "kwa wazazi wake wawili" na tukamwambia, "Nishukuru Mimi" kwa kuniabudu na kutekeleza haki zangu, na kwamba usitafute msaada kutoka kwa neema zangu kwa ajili ya kuniasi mimi "na wazazi wako" kwa kuwatendea wema kwa maneno laini, maneno ya upole, na matendo mazuri, kuwanyenyekea, kuwakirimu, kuwaheshimu, kuwapa matumizi yao, na kuepuka kuwaudhi kwa njia zote; kwa kauli na vitendo. Tulimuusia wasia huu na tukamwambia kwamba, "Ni kwangu Mimi ndiyo marejeo yenu." Na utarudi ewe mwanadamu kwa yule aliyekuusia na kukujukumisha haki hizi, naye atakuuliza: Je, ulizitimiza ili akulipe malipo mengi, au ulizipuuza ili akuadhibu kwa adhabu kali? Kisha akataja sababu inayolazimu kuwaheshimu wazazi wake, akasema kuhusiana na mama yake, "Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu" na akaendelea kupata matatizo kuanzia anapokuwa tone la manii akiugua homa, maradhi, udhaifu, uzito, na mabadiliko ya hali, kisha uchungu wa kuzaa ambao ni uchungu mkali mno, kisha "kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili;" huku yuko chini ya ulezi wa mama yake na utunzaji wake, na kunyonyeshwa. Je, si vizuri kwa mtu ambaye amevumilia magumu haya kwa ajili ya mwanawe, pamoja na ukubwa wa upendo wake juu yake, kumsisitizia mwanawe na kumuusia kumfanyia wema kamili?
#
{15} {وإن جاهداك}؛ أي: اجتهد والداك {على أن تشرِكَ بي ما ليس لك به علمٌ فلا تُطِعْهُما}: ولا تظنَّ أنَّ هذا داخل في الإحسان إليهما؛ لأنَّ حق الله مقدَّم على حقِّ كل أحدٍ، ولا طاعة لمخلوقٍ في معصية الخالق، ولم يقلْ: وإنْ جاهداك على أن تُشْرِكَ بي ما ليس لك به علمٌ؛ فعقَّهما، بل قال: {فلا تُطِعْهُما}؛ أي: في الشرك ، وأمَّا برُّهما؛ فاستمرَّ عليه، ولهذا قال: {وصاحِبْهُما في الدُّنيا معروفاً}؛ أي: صحبة إحسان إليهما بالمعروف، وأما اتِّباعُهما وهما بحالة الكفر والمعاصي؛ فلا تتَّبِعْهما، {واتَّبِعْ سبيلَ مَنْ أناب إليَّ}: وهم المؤمنون بالله وملائكته وكتبه ورسله، المستسلمون لربِّهم، المنيبون إليه، واتِّباع سبيلهم أن يَسْلُكَ مسلَكَهم في الإنابة إلى الله، التي هي انجذابُ دواعي القلب وإراداته إلى الله، ثم يتبَعُها سعي البدن فيما يرضي الله ويقرِّبُ منه، {ثمَّ إليَّ مرجِعُكم}: الطائع والعاصي والمنيب وغيره، {فأنِبِّئُكُم بما كنتُم تعملونَ}: فلا يخفى على اللَّه من أعمالهم خافيةٌ.
{15} "Na pindi wakikushikilia" na wakafanya juhudi ili "kunishirikisha na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii." Wala usidhani kuwa hilo linaingia katika kuwafanyia wema. Kwa sababu haki ya Mwenyezi Mungu imetangulizwa mbele ya haki ya kila mtu, na hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba. Na wala hakusema, "Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna elimu nayo, basi wafanyie kiburi" bali alisema, "basi usiwatii." Yaani, katika kunishirikisha, na ama suala la kuwafanyia wema, hilo andelea nalo. Na ndiyo maana akasema, "Lakini kaa nao kwa wema duniani." Na ama kuwafuata katika hali waliyomo ya ukafiri na maasi, wewe usiwafuate katika hayo "nawe ishike njia ya anayeelekea kwangu." Ambao ni wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, wanaojisilimisha kwa Mola wao Mlezi, na wanaotubia kwake. Na kufuata njia yao ni kufuata njia yao katika kurejea kwa Mwenyezi Mungu, ambayo ni mvuto yale ambayo moyo unataka kwa Mwenyezi Mungu, kisha yakafuatiwa na harakati ya mwili katika yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu na yenye kumfanya mtu kuwa karibu naye. "Kisha marejeo yenu ni kwangu Mimi" watiifu, na waasi, na mwenye kutubia na wengineo "na Mimi nitawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda." Na hakuna hata kitu kidogo katika matendo yao kitakachofichikana kwa Mwenyezi Mungu.
#
{16} {يا بنيَّ إنَّها إن تَكُ مثقالَ حبةٍ من خردلٍ}: التي هي أصغرُ الأشياء وأحقرُها {فتكن في صخرةٍ}؛ أي: في وسطها، {أو في السمواتِ أو في الأرض}: في أيِّ جهة من جهاتهما؛ {يأتِ بها اللهُ}: لسعةِ علمِهِ وتمامِ خبرتِهِ وكمال قدرتِهِ، ولهذا قال: {إنَّ الله لطيفٌ خبيرٌ}؛ أي: لطف في علمه وخبرته، حتى اطَّلع على البواطن والأسرار وخفايا القفار والبحار. والمقصودُ من هذا الحثُّ على مراقبة الله والعمل بطاعته مهما أمكن، والترهيبُ من عمل القبيح قلَّ أو كَثُرَ.
{16} "Ewe mwanangu, kikiwapo kitu cha uzito wa chembe ya khardali" ambayo ndiyo kitu kidogo zaidi na kilicho duni zaidi, "kikawa ndani ya jabali au ndani ya mbingu au ndani ya ardhi" katika upande wake wowote, "basi Mwenyezi Mungu atakileta." Kwa sababu ya upana wa elimu yake, na utimilifu wa kuwa kwake na habari, na ukamilifu wa uwezo wake, na ndiyo maana akasema, "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyofichika, Mwenye habari za yote," katika elimu yake na kuwa kwake na habari za mambo yote, mpaka anajua mambo ya ndani, na ya siri, na yote yaliyofichikana katika nyika na bahari. Kinachokusudiwa hapa ni kuwatia moyo watu kumchunga Mwenyezi Mungu na kumtii kiasi iwezekanavyo, na kuwatishia dhidi ya kutenda matendo maovu, yawe machache au mengi.
#
{17} {يا بنيَّ أقِمِ الصَّلاة}: حثَّه عليها وخصَّها لأنَّها أكبرُ العبادات البدنيَّة، {وأمُرْ بالمعروفِ وانْهَ عن المنكرِ}: وذلك يستلزم العلم بالمعروف؛ ليأمر به، والعلم بالمنكر؛ لينهى عنه، والأمر بما لا يتمُّ الأمر بالمعروف، والنهي عن المنكر إلاَّ به، من الرفق والصبر، وقد صرَّح به في قوله: {واصْبِرْ على ما أصابك}: ومن كونه فاعلاً لما يأمر به، كافًّا لما يُنهى عنه، فتضمَّن هذا تكميلَ نفسه بفعل الخير وترك الشر، وتكميلَ غيره بذلك بأمره ونهيه. ولمَّا عُلِمَ أنَّه لا بدَّ أن يُبتلى إذا أمر ونهى وأنَّ في الأمر والنهي مشقَّة على النفوس؛ أمره بالصبر على ذلك، فقال: {واصبِرْ على ما أصابَكَ إنَّ ذلك}: الذي وَعَظَ به لقمانُ ابنَه {من عزم الأمورِ}؛ أي: من الأمور التي يُعْزَمُ عليها، ويهتمُّ بها، ولا يوفَّق لها إلا أهلُ العزائم.
{17} "Ewe mwanangu, shika Swala." Alimhimiza kuitekeleza hii hasa kwa sababu hiyo ndiyo ibada kubwa kabisa ya kimwili, "na amrisha mema, na kataza maovu." Na hili linahitaji mtu kuyajua kwanza mambo mema, ili ayaamirishe, na kuyajua maovu ili ayakataze. Na pia kuamrisha yale ambayo kuamrisha mema na kukataza maovu hakutimii isipokuwa kwa hayo, kama vile upole na subira. Na aliyataja hayo wazi wazi katika kauli yake, "na subiri kwa yanayokupata." Naye mwenyewe pia anapaswa kufanya hayo anayoyaamrisha, na kujizuia na yale anayokataza. Kwa hivyo, hilo likajumuisha kujikamilisha yeye mwenyewe kwa kufanya heri, na kuacha maovu, na kuwakamilisha wengine kwa hayo kupitia maamrisho yake na makatazo yake. Na ilipojulikana kuwa ni lazima ajaribiwe anapoamrisha, na kwamba kuna ugumu kwa nafsi katika kuamrisha na kukataza, akamuamrisha kuwa na subira katika hilo. Akasema, "na subiri kwa yanayokupata" miongoni mwa mambo ambayo mtu amedhamiria kufanya, na anayajali, na hawawezeshwi kulifikia hilo isipokuwa watu wenye azimio kubwa.
#
{18} {ولا تُصَعِّرْ خدَّك للناس}؛ أي: لا تُمِلْهُ وتعبسْ بوجهك للناس تكبُّراً عليهم وتعاظماً، {ولا تَمْشِ في الأرض مَرَحاً}؛ أي: بَطِراً فخراً بالنعم ناسياً المنعِم معجباً بنفسك. {إنَّ الله لا يحبُّ كلَّ مختالٍ}: في نفسه وهيئته وتعاظُمه {فخورٍ}: بقوله.
{18} "Wala usiwabeuwe watu" kwa kuwakunjia watu uso wako kwa kiburi na kujiinua juu yao "wala usitembee katika nchi kwa maringo." Yaani, kwa kiburi, kujivuna juu ya neema za Mwenyezi Mungu, huku amesahau yule aliyemneemesha, na kujiona. "Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anayejivuna" juu ya nafsi yake na sura yake na kiburi chake "na kujifakhirisha" katika kauli zake.
#
{19} {واقصِدْ في مشيِكَ}؛ أي: امش متواضعاً مستكيناً لا مشي البطر والتكبُّر ولا مشي التماوت، {واغْضُضْ من صوتِكَ}: أدباً مع الناس ومع الله، {إنَّ أنكر الأصواتِ}؛ أي: أفظعها وأبشعها {لصوتُ الحميرِ}: فلو كان في رفع الصوت البليغ فائدةٌ ومصلحةٌ؛ لما اختصَّ بذلك الحمار الذي قد عُلِمْتَ خسَّتَه وبلادَتَه.
{19} "Na ushike mwendo wa katikati" na utembee kwa unyenyekevu na utulivu, wala si kutembea kwa kiburi, wala mwendo wa kunyamaza, "na teremsha sauti yako." Iwe ndiyo adabu yako kwa watu na mbele ya Mwenyezi Mungu. "Hakika katika sauti mbaya zote bila ya shaka iliyozidi ni sauti ya punda." Na iwapo palikuwa na manufaa yoyote na masilahi katika kuinua sauti juu mno, basi asingemtaja punda hasa na hilo pamoja na kwamba ulishajulikana ubaya wake.
Hizi amri ambazo Luqman alimuusia mwanawe zinajumuisha mama ya hekima, na zinahitaji utekelezaji wa yale ambayo hayajatajwa. Na kila amri inaambatanishwa na kitu kinachohitaji ifanywe ikiwa ni amri na kuiacha ikiwa ni katazo. Na hili linaashiria yale tuliyoyataja katika tafsiri ya hekima: kuwa ni kujua hukumu mbalimbali, hekima zake, na kunasibiana kwake. Basi akamuamrisha msingi wa dini, ambayo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na akamkataza ushirikina, na akamuelezea sababu ya kuiacha. Na akamuamrisha kuwafanyia wema wazazi wake, na akamueleza sababu inayolazimu kuwaheshimu, na akamuamrisha kumshukuru yeye na wao kisha akabainisha kwamba inapasa kuwaheshimu na kutii amri zao maadamu hawakuamrisha uasi. Lakini pamoja na hayo, asiwafanyie kiburi, bali awafanyie wema, ingawa hafai kuwatii ikiwa watapambana naye ili amshirikishe Mwenyezi Mungu. Na alimuamuru kumchunga Mwenyezi Mungu na kuogopa kumjia, na kwamba haachi jambo dogo wala kubwa la heri au ovu isipokuwa atalileta, na akamkataza kufanya kiburi. Na alimuamuru kuwa mnyenyekevu na akamkataza kujivuna, kuwa muovu na kijifahiri. Na alimuamuru kuwa na utulivu katika harakati na sauti, na akamkataza kufanya kinyume cha hayo. Na akamuamrisha kuamrisha mema na akamkataza maovu, na kusimamisha Swala, na kuwa na subira ambayo kwayo kila jambo hurahisishwa, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kusali." Ni kweli kwamba aliyependekeza maamrisho haya ni lazima apambanuliwe kwa hekima yake na mashuhuri kwa hayo, na kwa ajili hiyo ni neema ya Mwenyezi Mungu,kwake na kwa waja wake wote, kwamba aliwasimulia hekima yake ili iwe mfano mzuri kwao.
: 20 - 21 #
{أَلَمْ تَرَوْا أَنَّ اللَّهَ سَخَّرَ لَكُمْ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَأَسْبَغَ عَلَيْكُمْ نِعَمَهُ ظَاهِرَةً وَبَاطِنَةً وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يُجَادِلُ فِي اللَّهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَلَا هُدًى وَلَا كِتَابٍ مُنِيرٍ (20) وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّبِعُوا مَا أَنْزَلَ اللَّهُ قَالُوا بَلْ نَتَّبِعُ مَا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا أَوَلَوْ كَانَ الشَّيْطَانُ يَدْعُوهُمْ إِلَى عَذَابِ السَّعِيرِ (21)}
20. Kwani hamwoni ya kwamba Mwenyezi Mungu amevifanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na kwenye ardhi, na akakujalizieni neema zake, za dhahiri na za siri? Na miongoni mwa watu wapo wanaobishana juu ya Mwenyezi Mungu pasipo elimu, wala uwongofu, wala Kitabu chenye nuru. 21. Na wanapoambiwa, "Fuateni aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu," husema: "Bali tunafuata tuliyowakuta nayo baba zetu". Je! Shetani anawaita kwenye adhabu ya Moto uwakao?
#
{20 - 21} يمتنُّ تعالى على عباده بنعمِهِ، ويدعوهم إلى شكرها ورؤيتها وعدم الغفلة عنها، فقال: {ألم تروا}؛ أي: تشاهدوا وتُبصروا بأبصاركم وقلوبكم، {أنَّ الله سخَّر لكم ما في السمواتِ}: من الشمس والقمر والنُّجوم كلِّها مسخرات لنفع العباد، {وما في الأرض}: من الحيوانات والأشجار والزُّروع والأنهار والمعادن ونحوها؛ كما قال تعالى: {هو الذي خَلَقَ لكم ما في الأرض جميعاً}، {وأسبغَ عليكم}؛ أي: عمَّكم وغمركم نعمَه الظاهرةَ والباطنةَ؛ التي نعلم بها والتي تخفى علينا؛ نعم الدنيا ونعم الدين، حصول المنافع ودفع المضار؛ فوظيفتُكم أن تقوموا بشكرِ هذه النعم بمحبَّة المنعم والخضوع له وصرفها في الاستعانة على طاعتِهِ وأنْ لا يُستعان بشيء منها على معصيته. {و} لكن مع توالي هذه النعم {مِنَ الناس مَن}: لم يَشْكُرْها، بل كَفَرها، وكفر بمنْ أنعم بها، وجحدَ الحقَّ الذي أنزل به كتبه، وأرسل به رسله، فجعل {يجادِلُ في الله}؛ أي: يجادل عن الباطل ليدحضَ به الحقَّ، ويدفع به ما جاء به الرسول من الأمر بعبادةِ الله وحده، وهذا المجادلُ على غير بصيرة؛ فليس جدالُه عن علم؛ فيترك وشأنه، ويسمح له في الكلام. {ولا هدىً}: يقتدي به بالمهتدين {ولا كتابٍ منيرٍ}؛ أي: نيِّر مبين للحق؛ فلا معقول ولا منقول ولا اقتداء بالمهتدين، وإنما جداله في الله مبنيٌّ على تقليد آباءٍ غير مهتدين، بل ضالِّين مضلِّين، ولهذا قال: {وإذا قيلَ لهم اتَّبِعوا ما أنزلَ الله}: على أيدي رسله؛ فإنَّه الحقُّ، وبُيِّنَتْ لهم أدلتُه الظاهرة، {قالوا} معارضينَ ذلك: {بل نتَّبِعُ ما وَجَدْنا عليه آباءنا}: فلا نترك ما وجدنا عليه آباءنا لقول أحدٍ كائناً مَن كان. قال تعالى في الردِّ عليهم وعلى آبائهم: {أوَلَوْ كان الشيطانُ يدعوهم إلى عذابِ السعير}؛ أي: فاستجاب له آباؤهم، ومشوا خلفه، وصاروا من تلاميذ الشيطان، واستولت عليهم الحيرة؛ فهل هذا موجب لاتِّباعهم لهم ومشيهم على طريقتهم؟! أم ذلك يرهِبُهم من سلوك سبيلهم، وينادي على ضلالهم وضلال من تبعهم؟! وليس دعوة الشيطان لآبائهم ولهم محبة لهم ومودة، وإنَّما ذلك عداوةٌ لهم ومكرٌ لهم، وبالحقيقة أتباعه من أعدائِهِ الذين تمكَّن منهم، وظَفِرَ بهم، وقرَّتْ عينُه باستحقاقهم عذابَ السعير بقَبول دعوته.
{20 - 21} Mwenyezi Mungu anawashukuru waja wake kwa neema zake, na anawaita washukuru kwa ajili yao, kuwaona, na wasiwe wenye kughafilika nao, basi akasema: "Je, hukuwaona?" Yaani, nyinyi mnatazama na mnaona kwa macho yenu na nyoyo zenu. Hakika Mwenyezi Mungu amevitiisha kwenu vilivyomo mbinguni; jua, mwezi na nyota, vyote vinatiishwa kwa manufaa ya waja wake. Na vilivyomo katika ardhi; kutoka kwa wanyama, miti, mimea, mito, madini, na mfano wa hayo. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu,Yeye ndiye aliyewaumbieni vyote vilivyomo katika ardhi, na akakupeni.Yaani,aliwasitiri na akawatia neema zake zilizo dhahiri na zilizofichika. Ambayo tunayajua na yamefichwa kwetu; Baraka za dunia na neema za dini, kupata manufaa na kuepuka madhara. Kazi yako ni kutoa shukurani kwa baraka hizi kwa upendo kwa yule anayezineemesha, kunyenyekea kwake, na kuzitumia katika kutafuta msaada katika kumtii, na kutomtumia hata mmoja wao kumuasi. Na katika mfululizo wa neema hizo, miongoni mwa watu,wapo ambao hawakushukuru kwa ajili yao, bali walizikataa, na wakawakataa waliopewa, na wakakanusha haki aliyoituma. Akateremsha Vitabu vyake na aliowatuma navyo Mitume wake, wakaanza kubishana juu ya Mwenyezi Mungu. Yaani anabishana juu ya uwongo ili kuikanusha haki, na kukanusha kwayo aliyokuja nayo Mtume kuhusu amri ya kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na mjadili huyu hana akili,hoja yake haitokani na maarifa. Anaachwa peke yake na kuruhusiwa kuzungumza. Wala hakuna uwongofu, wafuatwe na walioongoka. Wala Kitabu chenye nuru; yaani, nuru inayoonyesha ukweli. Hakuna sababu, uhamisho, na mfano wa wenye kuongoka. Bali hoja yake juu ya Mwenyezi Mungu inatokana na kuwaiga mababa ambao hawakuongoka, bali ni wapotovu na waliopotea kwao. Fuateni aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, kwa mikono ya Mitume wake. Kwani hiyo ni haki, na ushahidi wake uliodhahiri ulibainishwa kwao. Wakasema wakipinga kuwa: "Bali sisi tunafuata tuliyowakuta nayo baba zetu," maoni ya mtu yeyote yule. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuwajibu wao na baba zao: "Je, shetani alikuwa akiwaita kwenye adhabu ya Moto mkali?" Yaani, baba zao walimwitikia, wakamfuata, wakawa wanafunzi wa Shetani, na machafuko yakawashika. Je, hii ni sababu ya wao kuwafuata na kufuata njia yao? Au je, hilo linawatia khofu wasiifuate njia yao, na linaita upotofu wao na upotofu wa wanaowafuata? Mwito wa Shetani kwa baba zao na kwao sio kwa mapenzi kwao, bali huo ni uadui kwao na hadaa juu yao, na hakika wafuasi wake ni miongoni mwa maadui zake aliowatawala, na amewaridhisha macho kwa kustahiki adhabu ya Moto mkali kwa kuukubali wito wake.
: 22 - 24 #
{وَمَنْ يُسْلِمْ وَجْهَهُ إِلَى اللَّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَى وَإِلَى اللَّهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ (22) وَمَنْ كَفَرَ فَلَا يَحْزُنْكَ كُفْرُهُ إِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ فَنُنَبِّئُهُمْ بِمَا عَمِلُوا إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ (23) نُمَتِّعُهُمْ قَلِيلًا ثُمَّ نَضْطَرُّهُمْ إِلَى عَذَابٍ غَلِيظٍ (24)}
22. Na mwenye kuuelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu, naye akawa anafanya wema, basi huyo hakika amekwisha kamata fundo liliomadhubuti. Na mwisho wa mambo yote ni kwa Mwenyezi Mungu. 23. Na anayekufuru, isikuhuzunishe kufuru yake. Kwetu ndio marudio yao, na hapo tutawaambia waliyoyatenda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani. 24. Unawastarehesha kwa uchache, kisha tutawasukuma kwenye adhabu ngumu.
#
{22} {ومَن يسلمْ وجهَه إلى الله}؛ أي: يخضعُ له وينقادُ له بفعل الشرائع مخلصاً له دينَه، {وهو محسنٌ}: في ذلك الإسلام؛ بأن كان عملُه مشروعاً، قد اتَّبع فيه الرسولَ صلّى الله عليه وسلّم، أو: ومن يسلمْ وجهَه إلى الله بفعل جميع العباداتِ وهو محسنٌ فيها؛ بأن يعبدَ الله كأنَّه يراه؛ فإنْ لم يكنْ يراه؛ فإنَّه يراه. أو: ومَنْ يسلمْ وجهَه إلى الله بالقيام بحقوقه، وهو محسن إلى عباد الله، قائم بحقوقهم، والمعاني متلازمةٌ، لا فرق بينها إلاَّ من جهة اختلاف مورد اللفظتين، وإلاَّ؛ فكلُّها متفقة على القيام بجميع شرائع الدين على وجه تُقبل به وتَكْمل؛ فمن فعل ذلك؛ {فقد استمسكَ بالعروةِ الوُثقى}؛ أي: بالعروة التي مَنْ تمسَّكَ بها؛ توثَّق ونجا وسلم من الهلاك وفاز بكلِّ خير، ومَنْ لم يُسلم وجهه لله، أو: لم يحسِنْ؛ لم يستمسك بالعروة الوثقى، وإذا لم يستمسكْ [بالعروة الوثقى]؛ لم يكنْ ثَمَّ إلاَّ الهلاك والبوار. {وإلى الله عاقبةُ الأمور}؛ أي: رجوعُها وموئلُها ومنتهاها، فيحكم في عباده ويجازيهم بما آلتْ إليه أعمالُهم، ووصلت إليه عواقِبُهم، فليستعدُّوا لذلك الأمر.
{22} Na anayeelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu,yaani kumnyenyekea na kumnyenyekea kwa sheria, kwa ikhlasi, dini yake, na ni mtenda wema katika Uislamu huo. Kwamba kazi yake ilikuwa halali, ambayo alimfuata Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - au na mwenye kuusalimisha uso wake kwa Mwenyezi Mungu kwa kufanya ibada na akawafanyia wema, kumwabudu Mungu kana kwamba anamwona ikiwa haoni. Au na mwenye kuusalimisha uso wake kwa Mwenyezi Mungu kwa kutimiza haki zake, naye ni mkarimu kwa waja wa Mwenyezi Mungu, akisimamia haki zao, hakuna tofauti baina yao isipokuwa kwa tofauti ya asili ya maneno mawili, vinginevyo; Wote wanakubaliwa kutekeleza sheria zote za dini kwa njia inayokubalika na kukamilishwa. Yeyote anayefanya hivyo ameshikilia kishiko kilicho imara zaidi.Yaani, kwa mshiko wa mkono anaoushikilia, alitiwa nguvu, akanusurika, na akasalimika na uharibifu, na akashinda kila kitu kizuri. Hakushikamana na mshiko wa kutegemewa zaidi, na ikiwa hakushikamana na mshiko wa kutegemewa zaidi, basi hapakuwa na chochote ila uharibifu. Na mwisho wa mambo ni kwa Mwenyezi Mungu. Yaani, marejeo yake na mahali pake pa kuishi. Basi atawahukumu waja wake na kuwalipa sawasawa na yale yaliyopelekea amali zao, na matokeo yao, basi wajiandae kwa jambo hilo.
#
{23} {ومَن كَفَرَ فلا يَحْزُنكَ كفرُه}: لأنَّك أدَّيت ما عليك من الدَّعوة والبلاغ؛ فإذا لم يهتدِ ؛ فقد وجب أجرُك على الله، ولم يبقَ للحزن موضعٌ على عدم اهتدائِهِ؛ لأنَّه لو كان فيه خيرٌ؛ لهداه الله، ولا تحزنْ أيضاً على كونهم تجرؤوا عليك بالعداوة، ونابذوك المحاربة، واستمرُّوا على غيِّهم وكفرِهم، ولا تتحرَّقْ عليهم بسبب أنَّهم ما بودروا بالعذاب، إنَّ {إلينا مرجِعُهم فننبِّئُهم بما عملوا}: من كفرِهم وعداوتِهم وسعيِهم في إطفاءِ نورِ الله وأذى رسله. إنه {عليمٌ بذات الصُّدور}: التي ما نطق بها الناطقون؛ فكيف بما ظهر وكان شهادة؟!
{23} "Na anayekufuru, isikuhuzunishe ukafiri wake," kwa sababu umetimiza wajibu wako wa kulingania na kufikisha ujumbe. Ikiwa hakuongoka, malipo yenu yanastahiki kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na hakuna mahali pa kuhuzunika kwa kukosa kwake mwongozo. Kwa sababu kama kulikuwa na nzuri ndani yake, Mwenyezi Mungu amuongoze, wala usihuzunike kwa sababu ya wao kuthubutu kukufanyia uadui, wakakukanusha, na wakaendelea na makosa yao na ukafiri wao, wala usiwaonee huruma kwa sababu hawakutishika na adhabu, "na hakika marejeo yao ni kwetu na tutawaambia waliyoyatenda;" ukafiri wao, uadui wao na juhudi zao za kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu na kuwadhuru Mitume wake. "Yeye Anajua dhati ya vifua," ambayo wasemaji hawakuzungumza. Basi vipi kuhusu kile kilichoonekana na kilikuwa ni ushuhuda?
#
{24} {نمتِّعُهم قليلاً}: في الدنيا؛ ليزداد إثمهُم ويتوفَّر عذابُهم. {ثم نضطرُّهم}؛ أي: نلجِئُهم {إلى عذابٍ غليظٍ}؛ أي: انتهى في عظمِهِ وكبرِهِ وفظاعتِهِ وألمه وشدَّته.
{24} "Tunawastarehesha kidogo" katika dunia hii, ili dhambi zao zizidi na adhabu yao izidi kuwa nyingi. "Kisha tutawalazimisha;" yaani, tutawapeleka "kwenye adhabu kali." Yaani, iliishia katika utukufu, kiburi, ukatili, maumivu na ukali wake.
: 25 - 28 #
{وَلَئِنْ سَأَلْتَهُمْ مَنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّهُ قُلِ الْحَمْدُ لِلَّهِ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ (25) لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ إِنَّ اللَّهَ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ (26) وَلَوْ أَنَّمَا فِي الْأَرْضِ مِنْ شَجَرَةٍ أَقْلَامٌ وَالْبَحْرُ يَمُدُّهُ مِنْ بَعْدِهِ سَبْعَةُ أَبْحُرٍ مَا نَفِدَتْ كَلِمَاتُ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ (27) مَا خَلْقُكُمْ وَلَا بَعْثُكُمْ إِلَّا كَنَفْسٍ وَاحِدَةٍ إِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ (28)}
25. Na ukiwauliza nani aliyeziumba mbingu na ardhi? Bila shaka watasema, Mwenyezi Mungu. Wewe sema Alhamdulillahi! Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu. Lakini wengi wao hawajui. 26. Ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyomo mbinguni na katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mkwasi, Mwenye kusifiwa. 27. Na lau kuwa miti yote iliyomo duniani ikawa ni kalamu, na bahari ikawa wino, na ikaongezewa juu yake bahari nyengine saba, maneno ya Mwenyezi Mungu yasingelikwisha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima. 28. Hakukuwa kuumbwa kwenu, wala kufufuliwa kwenu ila ni kama nafsi moja tu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.
#
{25} أي: {ولئن} سألتَ هؤلاء المشركين المكذِّبين بالحقِّ: {مَنْ خَلَقَ السمواتِ والأرضَ}: لعلموا أنَّ أصنامهم ما خلقتْ شيئاً من ذلك، ولبادروا بقولهم: {اللهُ}: الذي خلقهما وحدَه، فَـ {قُلْ} لهم ملزماً لهم ومحتجًّا عليهم بما أقرُّوا به على ما أنكروا: {الحمدُ لله}: الذي بيَّن النور وأظهر الاستدلال عليكم من أنفسكم؛ فلو كانوا يعلمون؛ لجزموا أنَّ المنفرد بالخَلْق والتدبير هو الذي يُفْرَدُ بالعبادة والتوحيد، ولكن {أكثرَهم لا يعلمونَ}: فلذلك أشركوا به غيره، ورَضُوا بتناقُض ما ذهبوا إليه على وجه الحيرة والشكِّ لا على وجهِ البصيرةِ.
{25} Yaani, "Na ikiwa" ungewauliza hawa washirikina wanaoikadhibisha haki, "Ni nani aliyeziumba mbingu na ardhi." Wanajua kwamba masanamu yao hayakuumba chochote katika hivyo na kwa hivyo wangeharakisha kusema, "Ni Mwenyezi Mungu," ambaye ameviumba peke yake. Basi, sema kuwaambia kwa kuwafunga na kuwathibitishia waliyokuwa wakiyachukia licha ya yale waliyoyakataa: "Alhamdulillah! (Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu)," ambaye ameibainisha Nuru na akawabainishieni kutoka kwa nafsi zenu. Laiti wangejua wangedai kuwa aliye peke yake katika uumbaji na usimamizi ni yule aliye peke yake katika ibada na tauhidi, lakini wengi wao hawajui, kwa hiyo wakamshirikisha na wakatosheka na kupingana kwa yale waliyoyaendea kwa msingi wa kuchanganyikiwa na shaka, si kwa msingi wa utambuzi.
#
{26} ثم ذكر في هاتين الآيتين نموذجاً من سعة أوصافه؛ ليدعو عباده إلى معرفته ومحبَّته وإخلاص الدين له، فذكر عموم ملكه، وأنَّ جميع ما في السماواتِ والأرض، وهذا شاملٌ لجميع العالم العلويِّ والسفليِّ؛ أنَّه ملكه، يتصرَّف فيهم بأحكام المُلك القدريَّة وأحكامه الأمريَّة وأحكامه الجزائيَّة؛ فكلُّهم عبيدٌ مماليكُ مدبَّرون مسخَّرون، ليس لهم من الملك شيءٌ، وأنَّه واسع الغنى؛ فلا يحتاجُ إلى ما يحتاجُ إليه أحدٌ من الخلق، {ما أريدُ منهم من رزقٍ وما أريد أن يُطْعِمونِ}، وأنَّ أعمال النبيِّين والصدِّيقين والشهداء والصالحين لا تنفعُ اللهَ شيئاً، وإنما تنفع عامليها، والله غنيٌّ عنهم وعن أعمالهم، ومن غناه أنْ أغناهم وأقناهم في دنياهم وأخراهم. ثم أخبر تعالى عن سَعَةِ حمدِهِ، وأنَّ حمدَه من لوازم ذاتِهِ؛ فلا يكون إلاَّ حميداً من جميع الوجوه؛ فهو حميدٌ في ذاته، وهو حميدٌ في صفاته؛ فكلُّ صفة من صفاته يستحقُّ عليها أكملَ حمدٍ وأتمَّه؛ لكونها صفاتِ عظمةٍ وكمال، وجميع ما فَعَلَه وخَلَقَه يُحمد عليه، وجميع ما أمر به ونهى عنه يُحمد عليه، وجميع ما حكم به في العباد وبين العباد في الدُّنيا والآخرة يُحمد عليه.
{26} Kisha akataja katika Aya hizi mbili mfano wa upana wa maelezo yake; ili kuwalingania waja wake wamjue, na kumpenda, na kumkusudia yeye tu katika dini yao. Akataja ujumla wa umiliki wake na kwamba unajumuisha yote yaliyomo mbinguni na ardhini, na hili linajumuisha kwamba ulimwengu wa juu wote na ulimwengu wa chini. Naye anaviendesha kwa hukumu za ufalme za kimajaliwa na amri zake za kimaamrisho na hukumu zake za adhabu. Wote ni waja wanaomilikiwa, wanaendeshwa, waliotiishwa. Hawana chochote katika ufalme wake, na kwamba yeye ni tajiri sana. Hahitaji chochote ambacho wanakihitaji viumbe: "Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe." Na kwamba hayamfai Mwenyezi Mungu kitu matendo ya Manabii, wakweli, mashahidi na watu wema, bali yanawanufaisha wale wanaoyafanya, na Mwenyezi Mungu ni mkwasi hawahitaji na hata hawahitaji. Na miongoni mwa kutohitaji kwake ni kwamba aliwatosheleza na kuwatosheleza katika dunia yao na akhera yao. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kuhusu upana wa sifa zake, na kwamba sifa zake ni katika mambo yasiyotengana na dhati yake. Kwa hivyo, hawi isipokuwa msifiwa kwa namna zote. Anasifiwa katika dhati Yake, naye ni msifiwa katika sifa zake. Kila moja ya sifa zake anastahiki kusifiwa kwayo sifa kamili zaidi. Kwa sababu hizo ni sifa za ukubwa na ukamilifu. Na kila alichofanya na kuumba anasifiwa juu yake. Na kila alichoamrisha na kukikataza anasifiwa juu yake. Na kila alilohukumu kuhusiana na waja wake na kati ya waja katika duniani na akhera anasifiwa juu yake.
#
{27} ثم أخبر عن سعة كلامِهِ وعظمةِ قوله بشرح يبلغُ من القلوبِ كلَّ مبلغ، وتنبهِرُ له العقول وتحير فيه الأفئدة وتسيح في معرفتِهِ أولو الألباب والبصائر، فقال: {ولو أنَّ ما في الأرض من شجرةٍ أقلامٌ}: يُكتب بها، {والبحرُ يَمُدُّه من بعدِهِ سبعةُ أبحرٍ}: مداداً يستمدُّ بها؛ لتكسَّرت تلك الأقلام، ولفني ذلك المداد، ولم تنفد {كلماتُ الله}: وهذا ليس مبالغةً لا حقيقةَ له، بل لمَّا علم تبارك وتعالى أنَّ العقول تتقاصر عن الإحاطة ببعض صفاته، وعلم تعالى أنَّ معرفته لعباده أفضل نعمةٍ أنعم بها عليهم وأجلُّ منقبةٍ حصَّلوها، وهي لا تمكِنُ على وجهها، ولكن ما لا يُدْرَكُ كلُّه لا يُتْرَكُ كلُّه، فنبَّههم تعالى على بعضها تنبيهاً تستنير به قلوبُهم، وتنشرحُ له صدورُهم، ويستدلُّون بما وصلوا إليه إلى ما لم يصلوا إليه، ويقولون كما قال أفضلُهم، وأعلمُهم بربِّه: «لا نُحْصي ثناءً عليك، أنت كما أثْنَيْتَ على نفسِك »، وإلاَّ؛ فالأمر أجلُّ من ذلك وأعظم. وهذا التمثيلُ من باب تقريب المعنى الذي لا يُطاق الوصول إليه إلى الأفهام والأذهان، وإلاَّ؛ فالأشجار وإنْ تضاعَفَتْ على ما ذُكِرَ أضعافاً كثيرةً، والبحور لو امتدَّت بأضعاف مضاعفةٍ؛ فإنَّه يُتَصَوَّر نفادها وانقضاؤها؛ لكونها مخلوقةً، وأمَّا كلام الله تعالى؛ فلا يُتَصَوَّرُ نفادُه، بل دلَّنا الدليلُ الشرعيُّ والعقليُّ على أنَّه لا نفاد له ولا منتهى؛ فكل شيء ينتهي إلاَّ الباري وصفاته، {وأنَّ إلى ربِّك المنتهى}، وإذا تصوَّر العقلُ حقيقة أوَّليَّته تعالى وآخريَّته، وأنَّ كلَّ ما فرضه الذهنُ من الأزمان السابقة مهما تسلسل الفرضُ والتقدير؛ فهو تعالى قبل ذلك إلى غير نهاية، وأنَّه مهما فرض الذهنُ والعقل من الأزمان المتأخرة وتسلسلَ الفرضُ والتقديرُ وساعد على ذلك مَنْ ساعد بقلبِهِ ولسانِهِ؛ فالله تعالى بعد ذلك إلى غير غايةٍ ولا نهاية، والله في جميع الأوقات يحكُم ويتكلَّم ويقولُ ويفعل كيف أرادَ، وإذا أراد، لا مانعَ له من شيء من أقواله وأفعاله؛ فإذا تصوَّر العقلُ ذلك؛ عرف أن المثل الذي ضربه الله لكلامه لِيُدْرِكَ العبادُ شيئاً منه، وإلاَّ؛ فالأمرُ أعظم وأجلُّ. ثم ذكر جلالة عزَّته وكمال حكمتِهِ، فقال: {إنَّ الله عزيزٌ حكيمٌ}؛ أي: له العزَّة جميعاً الذي ما في العالم العلويِّ والسفليِّ من القوَّة إلاَّ منه، هو الذي أعطاها للخلق؛ فلا حول ولا قوَّةَ إلاَّ به، وبعزَّته قهر الخلق كلَّهم، وتصرَّف فيهم ودبَّرهم، وبحكمته خَلَقَ الخلق، وابتدأه بالحكمة، وجعل غايتَه والمقصودَ منه الحكمة، وكذلك الأمرُ والنهي وُجِدَ بالحكمة، وكانت غايتُه المقصودةُ الحكمةَ؛ فهو الحكيم في خلقه وأمره.
{27} Kisha akajulisha kuhusu upana wa maneno yake na ukubwa wa kauli yake kwa kueleza kwa namna ambayo inafikia kila sehemu ya nyoyo, na akili zikastaajabishwa naye, na nyoyo zinachanganyika juu yake, na wenye akili na ufahamu wanatembea huku wakiwa wanayaelewa. Alisema, "Na lau kuwa miti yote iliyomo duniani ikawa ni kalamu" inayotumika kuandika, na bahari ikawa wino, na ikaongezewa juu yake bahari nyengine saba" ziwe ni wino, basi kalamu hizo zingevunjika, na wino huo ungeisha, lakini "maneno ya Mwenyezi Mungu" yasingalikwisha. Na huku si kutia chumvi kusikokuwa na uhakika. Bali kwa sababu Yeye, Mwingi wa baraka, Mtukufu alipojua kwamba akili zinapungukiwa kufahamu baadhi ya sifa zake, na yeye Mtukufu akajua kwamba waja wake kumjua ndiyo neema bora zaidi aliyowaneemesha kwayo na fadhila kubwa zaidi waliyoyapata, na kwamba haiwezekani kumjua namna alivyo hasa, bali kisichofaa kukiwacha chote, haifai kukiwacha chote, basi akawatanabahisha juu ya baadhi yake kwa tanabahisho yenye kutia mwangaza katika nyoyo zao na kuvifungua vifua vyao kufunguka, na wanatumia kama ushahidi yale ambayo wameweza kuyafikia juu ya yale ambayo hawakuweza kuyafikia, na wanasema kama alivyosema mbora wao, na mwenye kumjua zaidi Mola wao Mlezi, “Hatuwezi kukusifu vyema kama ulivyojisifu wewe mwenyewe." Kwa hivyo, jambo hili ni tukufu zaidi kuliko hilo na kubwa zaidi. Mfano huu ni mbinu ya kuleta karibu maana isiyoweza kufikiwa na ufahamu na akili. Vinginevyo, hata kama miti itazidishwa mizidisho mingi zaidi ya ilivyotajwa, na bahari zikaongezwa mara nyingi; bado inafikiriwa kuwa zitaisha na kumalizika; kwa sababu vimeumbwa. Na ama maneno la Mwenyezi Mungu Mtukufu, hayawezekani kufikiriwa kuwa yataisha, bali ushahidi wa kisheria na wa kiakili umetuonyesha kuwa hayawezi kuisha na wala hayana mwisho. Kwani kila kitu kina mwisho isipokuwa Muumba na sifa zake, "Na kwamba kwao Mola wako Mlezi ndio mwisho." Na ikiwa akili itafikiria uhakika wa kwamba yeye ndiye wa kwanza na wa mwisho, na kwamba kila kitu ambacho akili itafikiria tangu zamani, hata kama vitarudi nyuma vipi, Yeye Mtukufu alikuwa kabla yake bila kuwa na kikomo. Na kwamba hata kama akili itafikiria vipi nyakati za baadaye na kuendelea kwake kwenda mbele hivyo, na hata akasaidi juu ya hilo mwenye kusaidia kwa moyo wake na ulimi wake, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu yuko baada yake na hana kikomo wala mwisho. Na Mwenyezi Mungu wakati wote huhukumu na kuzungumza na anafanya anavyotaka. Na akitaka, hakuna kinachoweza kumpinga kutekeleza maneno yake na matendo yake. Kwa hivyo, ikiwa akili itafikiria hivyo; itajua kwamba mfano ambao Mwenyezi Mungu alipiga juu ya maneno yake ni ili waja wake watambue kitu kidogo kumhusu, vinginevyo; jambo hili ni kubwa zaidi na tukufu zaidi. Kisha akataja utukufu wake na ukamilifu wa hekima yake, akasema, "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima." Yaani, ana nguvu yote ambayo hakuna nguvu iliyo katika ulimwengu wa juu na wa chini isipokuwa ni kutoka kwake, na yeye ndiye aliyewapa viumbe nguvu hizo, na hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwake. Na kwa nguvu yake alivishinda viumbe vyote, na akaviendesha na kuvipanga, na akaumba viumbe kwa hekima yake. Na alivianzisha kwa hekima na akafanya mwisho wake na makusudio yake kuwa ni hekima. Na vile vile maamrisho na makatazo vilipatikana kwa hekima, na pia malengo yake na makusudio yake yalikuwa ni hekima. Basi Yeye ndiye Mwenye hekima katika uumbaji wake na maamrisho yake.
#
{28} ثم ذكر عظمةَ قدرتِهِ وكمالها، وأنَّه لا يمكن أن يتصوَّرها العقلُ، فقال: {ما خَلْقُكم ولا بعْثُكم إلاَّ كنفسٍ واحدةٍ}: وهذا شيءٌ يحير العقول: أنَّ خَلْقَ جميع الخَلْق على كثرتِهِم وبعثهم بعد موتِهِم بعد تفرُّقهم في لمحة واحدةٍ كخلقِهِ نفساً واحدةً؛ فلا وجه لاستبعادِ البعث والنُّشور والجزاء على الأعمال؛ إلاَّ الجهل بعظمة الله وقوَّة قدرتِهِ. ثم ذَكَرَ عموم سمعِهِ لجميع المسموعات وبصرِهِ لجميع المبصَرات، فقال: {إنَّ الله سميعٌ بصيرٌ}.
{28} Kisha akataja ukubwa na ukamilifu wa uweza wake, na kwamba hauwezi kufikiriwa na akili, akasema, "Hakukuwa kuumbwa kwenu, wala kufufuliwa kwenu ila ni kama nafsi moja tu." Na hili ni jambo linalochanganya akili, kwamba kuumba viumbe vyote pamoja na wingi wao na kuwafufua baada ya kufa kwao, baada ya kutawanyika kwao ni kitu kinachoweza kufanyika kwa muda mmoja mfupi kama vile anavyoweza kuumba nafsi moja. Kwa hivyo, hakuna sababu ya kuona kwamba ufufuo hauwezekani na pia malipo kwa matendo, isipokuwa yule asiyeujua ukuu wa Mwenyezi Mungu na nguvu ya uwezo wake. Kisha akataja ujumla wa kusikia kwake kila kinachosikika na kuona kwake kila kinachoonekana, akasema, "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kuona."
: 29 - 30 #
{أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِي إِلَى أَجَلٍ مُسَمًّى وَأَنَّ اللَّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ (29) ذَلِكَ بِأَنَّ اللَّهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِنْ دُونِهِ الْبَاطِلُ وَأَنَّ اللَّهَ هُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ (30)}.
29. Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu huuingiza usiku katika mchana, na huuingiza mchana katika usiku, na amedhalilisha jua na mwezi? Vyote hivyo vinakwenda mpaka wakati uliowekwa. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayoyatenda. 30. Hivi ni kwa sababu, Mwenyezi Mungu ndiye wa kweli, na hakika wanachokiomba ni cha uwongo. Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mtukufu na ndiye Mkubwa.
#
{29} وهذا فيه أيضاً انفرادُه بالتصرُّف والتدبير، وسعةِ تصرُّفه بإيلاج الليل في النهار وإيلاج النهارِ في الليل؛ أي: إدخال أحدِهِما على الآخر؛ فإذا دخل أحدُهما؛ ذهب الآخر، وتسخيره للشمس والقمر يجريان بتدبيرٍ ونظامٍ لم يختلَّ منذ خَلَقَهما؛ ليقيم بذلك من مصالح العباد ومنافِعِهم في دينهم ودُنياهم ما به يعتبِرون وينتَفِعون، و {كلٌّ} منهما {يجري إلى أجل مسمّى}: إذا جاء ذلك الأجل؛ انقطعَ جريانُهُما وتعطَّل سلطانُهما، وذلك في يوم القيامةِ حين تكوَّرُ الشمس، ويُخْسَفُ القمر، وتنتهي دار الدُّنيا، وتبتدئ الدار الآخرة. {وأنَّ الله بما تعملونَ}: من خيرٍ وشرٍّ. {خبيرٌ}: لا يخفى عليه شيء من ذلك، وسيجازيكم على تلك الأعمال بالثواب للمطيعين والعقاب للعاصين.
{29} Hii pia linajumuisha upekee wake katika kuendesha na kusimamia mambo, na upana wa uendeshaji wake kwa kuingiza usiku ndani ya mchana na kuingiza mchana katika usiku. Yaani, kuingiza moja katika nyingine. Na kinapoingia kimoja katika kingine, hicho kingine kinapotea. Na pia kulitiisha jua na mwezi vikaenda kama vilivyopangiwa kwa kipimo na utaratibu ambao haujawahi kutatizwa tangu kuumbwa kwake. Ili yafikiwe kwa hayo masilahi ya waja na manufaa yao katika Dini yao na maisha yao ya kidunia na ambayo kwayo watazingatia na kunufaika, na "kila moja" katika viwili hivyo, "vinakwenda mpaka wakati uliowekwa." Na utakapofika muda huo, basi kwenda kwake huko kutakatika na mamlaka yake yatasitishwa, na hilo litatokea Siku ya Kiyama ambapo jua litakunjwa na mwezi utapatwa, na nyumba ya dunia hii itaisha na Akhera itaanza. "Na hakika Mwenyezi Mungu kwa mnayoyatenda," ya heri na ya shari "anazo khabari." Halifichikani kwake chochote katika hayo, na atawalipa kwa matendo hayo malipo mazuri kwa watiifu na adhabu kwa wanaoasi.
#
{30} {ذلك}: الذي بيَّن لكم من عظمتِهِ وصفاتِهِ ما بيَّن {بأنَّ الله هو الحقُّ}: في ذاته وفي صفاته، ودينُهُ حقٌّ، ورسله حقٌّ، ووعدُه حقٌّ، ووعيده حقٌّ، وعبادتُه هي الحق. {وأنَّ ما يدعونَ من دونِهِ الباطلُ}: في ذاته وصفاته؛ فلولا إيجادُ الله له؛ لما وُجِدَ، ولولا إمدادُه؛ لما بقي؛ فإذا كان باطلاً؛ كانت عبادتُه أبطل وأبطل. {وأنَّ الله هو العليُّ}: بذاته فوق جميع مخلوقاته الذي علت صفاته أن يقاس بها صفات [أحدٍ من الخلق]، وعلا على الخلق؛ فقهرهم {الكبير}: الذي له الكبرياءُ في ذاته وصفاته، وله الكبرياءُ في قلوب أهل السماء والأرض.
{30} "Hivi," namna alivyowabainishia juu ya ukuu wake na sifa zake alizozibainisha, "kwamba Mwenyezi Mungu ndiye wa kweli" katika dhati yake na sifa zake. Na dini yake ndiyo ya haki, na Mitume wake ndio wa haki, na ahadi yake ndiyo ya haki, na ahadi yake ya adhabu ndiyo ya haki, na ibada yake ndiyo ya haki. "Na hakika wanachokiomba ni cha uongo" katika dhati yake na katika sifa zake. Na kama Mwenyezi Mungu asingekiumba, basi kisingekuwepo. Na kama asingekipa ya kukikimu, basi hakingebakia. Na kama ni cha batili, basi kukiabudu pia ni batili ya batili zote. "Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mtukufu" kwa dhati yake juu ya viumbe vyake vyote, ambaye sifa zake ni za juu kiasi kwamba hawezi kulinganishwa na sifa za yeyote katika viumbe vyake, na ametukuka zaidi juu ya viumbe na akavishinda. "Aliye Mkubwa," ambaye ana ukubwa katika dhati yake na sifa zake, na anao ukubwa katika mioyo ya wakazi wa mbinguni na duniani.
: 31 - 32 #
{أَلَمْ تَرَ أَنَّ الْفُلْكَ تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِنِعْمَتِ اللَّهِ لِيُرِيَكُمْ مِنْ آيَاتِهِ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ (31) وَإِذَا غَشِيَهُمْ مَوْجٌ كَالظُّلَلِ دَعَوُا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ فَلَمَّا نَجَّاهُمْ إِلَى الْبَرِّ فَمِنْهُمْ مُقْتَصِدٌ وَمَا يَجْحَدُ بِآيَاتِنَا إِلَّا كُلُّ خَتَّارٍ كَفُورٍ (32)}.
31. Kwani huoni kwamba merikebu hupita baharini zikichukua neema za Mwenyezi Mungu, ili kuwaonyesha baadhi ya Ishara zake? Hakika katika haya zipo Ishara kwa kila mwenye kusubiri na mwenye kushukuru. 32. Na wimbi linapowafunika kama wingu, wao humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafia dini. Lakini anapowaokoa wakafika nchi kavu, wapo baadhi yao huenda mwendo wa sawa. Wala hazikanushi Ishara zetu ila aliyekhaini kafiri mkubwa.
#
{31} أي: ألم تَرَ من آثار قدرتِهِ ورحمتِهِ وعنايتِهِ بعباده أنْ سَخَّرَ البحر تجري فيه الفُلْك بأمره القدريِّ ولطفِهِ وإحسانِهِ؛ {لِيُرِيَكُم من آياتِهِ}: ففيها الانتفاعُ والاعتبار. {إنَّ في ذلك لآياتٍ لكلِّ صبارٍ شكورٍ} فهم المنتفعون بالآيات {صبَّارٍ} على الضراء. {شكورٍ} على السَّراء، صبَّارٍ على طاعة الله وعن معصيته وعلى أقدارِهِ، شكورٍ لله على نِعَمِهِ الدينيَّة والدنيويَّة.
{31} Je, hukuona katika athari za uwezo wake, rehema, zake na utunzaji wake waja wake, kwamba aliitiisha bahari ambayo merikebu zinapita humo kwa amri yake ya kimajaliwa, na upole wake na ukarimu wake -"ili kuwaonyesha baadhi ya Ishara zake?" Ndani yake mna manufaa na mazingatio. "Hakika katika haya, zipo Ishara kwa kila mwenye kusubiri na mwenye kushukuru," kwani hao ndio wenye kunufaika na Ishara, na wenye kuwa na subira juu ya dhiki. "Mwenye kushukuru" katika nyakati nzuri, mwenye subira katika kumtii Mwenyezi Mungu na katika kujizuia kumuasi, na juu ya kadari zake. Yeye humshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema zake za kidini na za dunia.
#
{32} وذكر تعالى حال الناس عند ركوبِهِم البحر وغشيان الأمواج كالظُّلل فوقهم أنَّهم يخلِصون الدُّعاء لله والعبادة، {فلما نجَّاهم إلى البرِّ}: انقسموا فريقينِ: فرقة مقتصدة؛ أي: لم تقم بشكر الله على وجه الكمال، بل هم مذنبون ظالمون لأنفسهم، وفرقة كافرة لنعمة الله جاحدة لها، ولهذا قال: {وما يَجْحَدُ بآياتِنا إلاَّ كلُّ خَتَّارٍ}؛ أي: غدَّار، ومن غدرِهِ أنَّه عاهد ربَّه لئن أنجيتَنا من البحرِ وشدَّتِهِ لنكوننَّ من الشاكرين. فغدر، ولم يفِ بذلك. {كفورٍ}: لنعم الله؛ فهل يَليقُ بِمَنْ نجَّاهم الله من هذه الشدَّة إلاَّ القيام التامُّ بشكر نعم الله؟!
{32} Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaja hali za watu wanapokuwa wamepanda baharini, na mawimbi yakawafunika kama vivuli juu yao, kwamba wao humuomba Mwenyezi Mungu dua na kumuabudu kwa kumkusudia yeye tu. "Lakini anapowaokoa wakafika nchi kavu" wanagawanyika katika makundi mawili: kundi la wale ambao hawakumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ukamilifu, bali walifanya madhambi na wakadhulumu nafsi zao, na kundi lilikokufuru neema ya Mwenyezi Mungu, lililozipinga. Na ndiyo maana akasema, "Wala hazikanushi Ishara zetu ila aliyekhaini." Na katika hiana yake ni kwamba alimuahidi Mola wake Mlezi kuwa: Ukituokoa kutoka katika bahari na dhiki yake, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye kushukuru. Lakini akafanya hiana, wala hakutimiza hayo "kafiri mkubwa." mwenye kukufuru neema za Mwenyezi Mungu. Basi je, inafaa kwa wale ambao Mwenyezi Mungu aliwaokoa kutokana na ugumu huu isipokuwa kufanya kushukuru kikamilifu neema neema za Mwenyezi Mungu?
: 33 #
{يَاأَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ وَاخْشَوْا يَوْمًا لَا يَجْزِي وَالِدٌ عَنْ وَلَدِهِ وَلَا مَوْلُودٌ هُوَ جَازٍ عَنْ وَالِدِهِ شَيْئًا إِنَّ وَعْدَ اللَّهِ حَقٌّ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَلَا يَغُرَّنَّكُمْ بِاللَّهِ الْغَرُورُ (33)}.
33. Enyi watu, mcheni Mola wenu Mlezi, na iogopeni siku ambayo mzazi hatamfaa mwana, wala mwana hatamfaa mzazi kwa lolote. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Basi yasiwadanganyeni maisha ya dunia, wala asiwadanganyeni na Mwenyezi Mungu mdanganyifu.
#
{33} يأمر تعالى الناس بتقواه، التي هي امتثال أوامرِهِ وتركُ زواجرِهِ، ويستلِفتُهم لخشية يوم القيامة، اليوم الشديدِ الذي فيه كلُّ أحدٍ لا يهمُّه إلاَّ نفسُهُ. و {لا يجزي والدٌ عن ولدِهِ ولا مولودٌ} عن والدِهِ شيئاً: لا يزيدُ في حسناتِهِ ولا ينقصُ من سيئاتِهِ، قد تمَّ على كلِّ عبدٍ عملُه، وتحقَّق عليه جزاؤه. فلفْتُ النظرِ لهذا اليوم المَهيل مما يقوِّي العبدَ ويسهِّل عليه تقوى الله، وهذا من رحمة الله بالعباد؛ يأمُرُهم بتقواه التي فيها سعادتُهم، ويَعِدُهم عليها الثواب، ويحذِّرُهم من العقاب، ويزعجهُم إليه بالمواعظِ والمخوفات، فلك الحمدُ يا ربَّ العالمين. {إنَّ وعدَ الله حقٌّ}: فلا تمتروا فيه، ولا تعملوا عملَ غير المصدِّقِ؛ فلهذا قال: {فلا تغرَّنَّكُمُ الحياةُ الدُّنيا}: بزينتها وزخارفها وما فيها من الفتنِ والمحنِ. {ولا يَغُرَّنَّكُم بالله الغَرورُ}: الذي هو الشيطان، الذي ما زال يخدعُ الإنسان، ولا يغفل عنه في جميع الأوقات؛ فإنَّ لله على عباده حقًّا، وقد وعدهم موعداً يجازيهم فيه بأعمالهم وهل وَفوا حقَّه أم قصَّروا فيه؟ وهذا أمرٌ يجب الاهتمامُ به، وأنْ يجعَلَه العبدُ نُصبَ عينيه ورأسَ مال تجارتِهِ التي يسعى إليه، ومن أعظم العوائق عنه والقواطع دونَه الدُّنيا الفتَّانةُ والشيطانُ الموسْوِسُ المسوِّلُ، فنهى تعالى عبادَه أن تَغُرَّهم الدُّنيا أو يَغُرَّهم بالله الغَرور، {يَعِدُهُم ويُمَنِّيهم وما يَعِدُهُم الشيطانُ إلاَّ غُروراً}.
{33} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha watu wamche Yeye, yaani kutekeleza amri zake na kuacha makemeo yake, na anawaelekeza kwenye suala la kuogopa Siku ya Kiyama, siku kali ambayo kila mtu siku hiyo hajali isipokuwa nafsi yake tu. Na "mzazi hatamfaa mwana, wala mwana" hatamfaa mzazi kwa lolote. Hataongeza kitu katika mazuri yake wala hatapunguza kitu katika mabaya yake. Matendo ya kila mja yatakuwa yameshatimia na atafikia malipo yake. Kwa hivyo kuelekeza fikira kwenye siku hii yenye kutisha, ni katika mambo ambayo humtia nguvu mja huyo na kumrahisishia kumcha Mwenyezi Mungu, na hii ni kutokana na rehema ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake. Anawaamrisha uchamungu, ambao ndani yake kuna furaha yao, na anawaahidi malipo kwa hilo. Na anawaonya juu ya adhabu, na anawaepusha nayo kwa mawaidha na mambo ya kuhofiha. Basi ni zako sifa njema ewe Mola Mlezi wa walimwengu wote. "Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli." Basi msiwe na shaka juu yake, wala msifanye matendo ya asiyesadiki. Na ndiyo maana akasema, "Basi yasiwadanganyeni maisha ya dunia" kwa mapambo yake na marembesho yake, na majaribio na mitihani iliyo ndani yake. "Wala asiwadanganyeni na Mwenyezi Mungu mdanganyifu." Ambaye ni Shetani, anayeendelea kumdanganya mwanadamu, wala haghafiliki akamuacha, katika nyakati zote. Kwani, Mwenyezi Mungu anayo haki juu ya waja wake, na amewaahidi miadi atakayowalipa ndani yake kwa matendo yao? Na je walitimiza haki yake au waliipuuza? Hili ni jambo ambalo ni lazima kulizingatia, na kwamba mja anapaswa kulifanya kuwa mbele ya macho yake na mtaji wa biashara yake anayotafuta. Na miongoni mwa vikwazo vyake vikubwa zaidi na vizuizi vilivyo mbele yake ni dunia yenye kufitini, na shetani mwenye kutia wasiwasi na kuchochea. Kwa hivyo, Yeye Mtukufu akawakataza waja wake wasidanganywe na dunia au kudanganywa na mdanganyifu. "Anawaahidi na anawatia tamaa. Na Shetani hawaahidi ila udanganyifu."
: 34 #
{إِنَّ اللَّهَ عِنْدَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَيُنَزِّلُ الْغَيْثَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْأَرْحَامِ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَاذَا تَكْسِبُ غَدًا وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ (34)}.
34. Hakika kuijua Saa ya Kiyama kuko kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ndiye anayeiteremsha mvua. Na anavijua vilivyo ndani ya matumbo ya uzazi. Na haijui nafsi yoyote itachuma nini kesho. Wala nafsi yoyote haijui itafia nchi gani. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua, Mwenye habari.
#
{34} قد تقرَّر أنَّ الله تعالى أحاطَ علمُه بالغيب والشهادة والظواهِرِ والبواطِن، وقد يُطْلِعُ الله عبادَه على كثيرٍ من الأمور الغيبيَّة، وهذه الأمور الخمسة من الأمور التي طَوَى علمها عن جميع الخَلْق؛ فلا يعلمُها نبيٌّ مرسلٌ ولا ملكٌ مقرَّبٌ، فضلاً عن غيرهما، فقال: {إنَّ الله عندَه علم الساعةِ}؛ أي: يعلم متى مُرساها؛ كما قال تعالى: {يَسْألونَكَ عن الساعةِ أيَّانَ مُرساها. قُل إنَّما علمُها عند ربِّي لا يُجَلِّيها لوقتِها إلاَّ هو ثقلت في السموات والأرض لا تأتيكم إلاَّ بَغْتَةً ... } الآية، {ويُنَزِّلُ الغيثَ}؛ أي: هو المنفرد بإنزاله، وعلمِ وقتِ نزولِهِ، {ويعلمُ ما في الأرحام}: فهو الذي أنشأ ما فيها، وعلم ما هو؛ هل هو ذكرٌ أم أنثى؟ ولهذا يسأل الملك الموكل بالأرحام ربَّه: هل هو ذَكَرٌ أم أنثى؟ فيقضي الله ما يشاء. {وما تَدْري نفسٌ ماذا تكسِبُ غداً}: من كَسْبِ دينها ودُنياها، {وما تدري نفسٌ بأيِّ أرضٍ تموتُ}: بل الله تعالى هو المختصُّ بعلم ذلك جميعه. ولمَّا خصَّص [اللَّه] هذه الأشياء؛ عمَّم علمَه بجميع الأشياء، فقال: {إنَّ الله عليمٌ خبيرٌ}: محيطٌ بالظواهر والبواطن والخفايا والخبايا والسرائر، ومن حكمتِهِ التامَّة أنْ أخفى علمَ هذه الخمسة عن العبادِ؛ لأنَّ في ذلك من المصالح ما لا يخفى على من تدبر ذلك.
{34} Imethibiti kwamba elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu imezunguka mambo ya ghaibu na yanayoshuhudiwa, na yaliyodhahiri na ya siri, na Mwenyezi Mungu anaweza kuwajulisha waja wake mambo mengi ya ghaibu. Na mambo matano haya ni miongoni mwa mambo ambayo elimu yake imeyaficha wasiyajue viumbe wote; Kwa hivyo, hakuna Nabii aliyetumwa anayeyajua, wala Malaika wa karibu, mbali zaidi na wasiokuwa wao. Akasema, "Hakika kuijua Saa ya Kiyama kuko kwa Mwenyezi Mungu." Ni lini itafika, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini? Sema: Kuijua kwake kuko kwa Mola Mlezi wangu. Haidhihirishi hiyo kwa wakati wake ila Yeye. Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haikujiini ila kwa ghafla tu..." hadi mwisho wa aya. "Na Yeye ndiye anayeiteremsha mvua" peke yake, naye peke yake ndiye ajuaye wakati wa kuteremka kwake. "Na anavijua vilivyo ndani ya matumbo ya uzazi." Kwani, Yeye ndiye aliyeumba vilivyomo ndani yake, na anajua ni akina nani; je ni wa kiume au wa kike? Na ndiyo maana malaika aliyepewa kusimamia matumbo ya uzazi humwuliza Mola wake Mlezi: Je, yeye ni wa kiume au wa kike? Kwa hiyo Mwenyezi Mungu kaamua chochote anachotaka. "Na haijui nafsi yoyote itachuma nini kesho" kuhusiana na dini yake na dunia yake. "Wala nafsi yoyote haijui itafia nchi gani." Bali Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye ajuaye tu hayo yote. Na Mwenyezi Mungu alipovitaja vitu hivyo hasa, akabainisha kwamba elimu yake inajumuisha kila kitu, akasema, "Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua, Mwenye habari." Ameyazunguka yaliyodhahiri, yaliyofichikana na siri zote. Na katika hekima yake kamili ni kwamba ameificha elimu ya matano haya wasiyajue waja. Kwa sababu kuna masilahi katika hili ambayo hayafichikani kwa mwenye kuyatafakari.
Imekamilika tafsiri ya Surat Luqman kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na kwa msaada wake, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.
* * *