Nayo iliteremka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
{الم (1) غُلِبَتِ الرُّومُ (2) فِي أَدْنَى الْأَرْضِ وَهُمْ مِنْ بَعْدِ غَلَبِهِمْ سَيَغْلِبُونَ (3) فِي بِضْعِ سِنِينَ لِلَّهِ الْأَمْرُ مِنْ قَبْلُ وَمِنْ بَعْدُ وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ (4) بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ (5) وَعْدَ اللَّهِ لَا يُخْلِفُ اللَّهُ وَعْدَهُ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ (6) يَعْلَمُونَ ظَاهِرًا مِنَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ عَنِ الْآخِرَةِ هُمْ غَافِلُونَ (7)}.
1. Alif Lam Mim 2. Warumi wameshindwa. 3. Katika nchi iliyo karibu. Nao baada ya kushindwa kwao watashinda. 4. Katika miaka michache. Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi. 5. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu, humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu, Mwingi kurehemu. 6. Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake. Lakini wengi wa watu hawajui. 7. Wanajua hali ya dhahiri ya maisha ya dunia, na wameghafilika na Akhera.
#
{1 - 5} كانت الفرس والروم في ذلك الوقت من أقوى دول الأرض، وكان يكون بينهما من الحروب والقتال ما يكون بين الدول المتوازنة، وكانتِ الفرسُ مشركينَ يعبُدون النار، وكانت الرومُ أهلَ كتابٍ ينتسبون إلى التوراة والإنجيل، وهم أقربُ إلى المسلمين من الفرس، [فكان المؤمنون] يحبُّون غَلَبَتَهم وظهورَهم على الفرس، وكان المشركون لاشتراكِهِم والفرسُ في الشرك يحبُّون ظهورَ الفرس على الروم، فظهر الفرسُ على الروم وغلبوهم غُلباً لم يُحِطْ بِمُلْكِهِم بل بأدنى أرضهم، ففرح بذلك مشركو مكة وحزن المسلمون، فأخبرهم الله، ووعدَهم أنَّ الروم ستغلب الفرس {في بِضْعِ سنينَ}: تسع أو ثمان ونحو ذلك مما لا يزيدُ على العشر ولا ينقُصُ عن الثلاث، وأنَّ غلبةَ الفرس للروم ثم غلبةَ الروم للفرس كلُّ ذلك بمشيئتِهِ وقَدَرِهِ، ولهذا قال: {لله الأمرُ من قبلُ ومن بعدُ}: فليس الغلبةُ والنصر لمجرَّد وجود الأسباب، وإنَّما هي لا بدَّ أن يقترن بها القضاء والقدر.
{ويومئذٍ}؛ أي: يوم يغلب الرومُ الفرس ويقهرونهم، {يفرحُ المؤمنون. بنصر الله ينصُرُ مَنْ يشاءُ}؛ أي: يفرحون بانتصارهم على الفرس، وإنْ كان الجميع كفاراً، ولكنَّ بعضُ الشرِّ أهونُ من بعض، ويحزنُ يومئذٍ المشركون. {وهو العزيزُ}: الذي له العزَّةُ التي قهر بها الخلائق أجمعين، يؤتي المُلْكَ مَنْ يشاء، وينزِعُ الملك ممَّن يشاء، ويعزُّ من يشاء ويذلُّ من يشاء. {الرحيمُ}: بعباده المؤمنين؛ حيث قيَّضَ لهم من الأسباب التي تسعِدُهم وتنصُرُهم ما لا يدخُل في الحساب.
{1 - 5} Waajemi na Warumi wakati huo walikuwa miongoni mwa nchi zenye nguvu zaidi duniani, na kulikuwa na vita na mapigano kati yao ambayo huwa kati ya nchi zinazokaribiana kwa nguvu. Waajemi walikuwa washirikina walikuwa wakiabudu moto, nao Warumi walikuwa watu wa Kitabu ambacho kilikuwa Taurati na Injili, na walikuwa karibu na Waislamu kuliko Waajemi,
[kwa hivyo waumini] walikuwa wakitaka kwamba wao wawashinde Waajemi. Nao washirikina kwa sababu ya kushirikiana kwao na Waajemi katika ushirikina walikuwa wakipenda kwamba Waajemi wawashinde Warumi. Kwa hivyo Waajemi wakawashinda juu ya Warumi kwa ushindi ambao haukuumaliza ufalme wao, lakini ulifikia tu sehemu iliyokuwa karibu zaidi nao. kwa washirikina wa Makka wakafurahia hilo na Waislamu wakahuzunika. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawaambia, na kuwaahidi kwamba Warumi watashinda Waajemi, "Katika miaka michache" tisa au minane na mfano wake, kwa muda usiozidi miaka kumi wala haipungui chini ya miaka mitatu. "Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake." Kwa hivyo, ushindi na nusura hautokani tu kwa kuwepo kwa sababu zake. Bali ni lazima ufungamane na mapitisho ya Mwenyezi Mungu na kadari yake. "Na siku hiyo;" yaani, siku ambayo Warumi watawashinda Waajemi, "Waumini watafurahi." "Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu, humnusuru amtakaye." Yaani, watafurahia ushindi wao dhidi ya Waajemi, hata kama kila wote wawili ni makafiri, lakini baadhi ya uovu ni rahisi kuliko mwingine. Nao washirikina watahuzunika siku hiyo. "Naye ndiye Mwenye nguvu" ambaye ana nguvu ambayo kwayo aliwashinda viumbe wote; humpa ufalme amtakaye, na humwondolea ufalme amtakaye, na humtukuza amtakaye, na humuangusha umtakaye. "Mwingi wa kurehemu" waja wake waumini, ambapo amewawekea sababu zinazowafanya wafurahi na kuwasaidia zaidi ya namna ambayo hawakuwa wanatarajia.
#
{6} {وعدَ اللهِ لا يُخْلِفُ الله وعدَه}: فتيقَّنُوا ذلك، واجْزِمُوا به، واعْلَمُوا أنَّه لا بدَّ من وقوعه. فلمَّا نزلت هذه الآيات التي فيها هذا الوعدُ؛ صدَّق بها المسلمون، وكفر بها المشركون، حتى تراهن بعضُ المسلمين وبعضُ المشركين على مدَّة سنين عيَّنوها، فلما جاء الأجل الذي ضربه الله. انتصر الروم على الفرس، وأجْلَوْهم من بلادهم التي أخذوها منهم، وتحقَّق وعد الله. وهذا من الأمور الغيبيَّة التي أخبر بها الله قبل وقوعها ووجدت في زمان مَنْ أخبرهم الله بها من المسلمين والمشركين. {ولكنَّ أكثر الناس لا يعلمونَ}: أنَّ ما وَعَدَ اللهُ به حقٌّ؛ فلذلك يوجد فريقٌ منهم يكذِّبون بوعده، ويكذِّبون آياته.
{6} "Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake." Kwa hivyo kuweni na yakini na hilo, na uhakika, na jueni kwamba lazima litatokea. Wakati aya hizi, ambazo zina ahadi hii, zilipoteremka, Waislamu walizisadiki, lakini washirikina wakazikufuru, kiasi kwamba baadhi ya Waislamu na baadhi ya washirikina waliwekeana rehani kwa kipindi cha miaka fulani wakichopimiana. Na muda ambao Mwenyezi Mungu aliuweka ulipofika, Warumi wakawashinda Waajemi, na wakawahamisha kutoka katika nchi yao waliyokuwa wamechukua kutoka kwao, na ahadi ya Mwenyezi Mungu ikatimia. Na hili ni katika mambo ghaibu ambayo Mwenyezi Mungu alijulisha kutokea kwake kabla hayajatokea, na yakatokea katika zama za wale ambao Mwenyezi Mungu alijulisha kwamba yatatokea katika wakati wao. "Lakini wengi wa watu hawajui" ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Na ndiyo maana lipo kundi miongoni mwao wanaokadhibisha ahadi yake na Ishara zake.
#
{7} وهؤلاء الذين لا يعلمون؛ أي: لا يعلمون بواطن الأشياء وعواقِبَها، وإنَّما {يعلمونَ ظاهراً من الحياة الدُّنيا}: فينظرون إلى الأسباب، ويجزمون بوقوع الأمر الذي في رأيهم انعقدتْ أسباب وجودِهِ، ويتيقَّنون عدم الأمر الذي لم يشاهِدوا له من الأسباب المقتضية لوجودِهِ شيئاً؛ فهم واقفون مع الأسباب، غيرُ ناظرين إلى مسبِّبها المتصرف فيها. {وهم عن الآخرةِ هم غافلونَ}: قد توجَّهت قلوبُهم وأهواؤهم وإراداتهم إلى الدنيا وشهواتِها وحطامِها؛ فعملتْ لها وسعتْ وأقبلتْ بها وأدبرتْ، وغفلت عن الآخرة؛ فلا الجنة تشتاقُ إليها، ولا النار تخافها وتخشاها، ولا المقام بين يدي الله ولقائه يروِّعُها ويزعِجُها، وهذا علامة الشقاء، وعنوانه الغفلة عن الآخرة.
ومن العجبِ أنَّ هذا القسم من الناس قد بلغتْ بكثيرٍ منهم الفطنةُ والذكاءُ في ظاهر الدُّنيا إلى أمرٍ يحيِّر العقول ويدهش الألباب، وأظهروا من العجائِب الذَّرِّيَّةِ والكهربائيةِ والمراكب البريَّة والبحريَّة والهوائيَّة ما فاقوا به، وبرَّزوا وأعجبوا بعقولهم، ورأوا غيرهم عاجزاً عما أقدرهم اللهُ عليه، فنظروا إليهم بعين الاحتقار والازدراء، وهم مع ذلك أبلد الناس في أمرِ دينهم، وأشدُّهم غفلةً عن آخرتهم، وأقلُّهم معرفة بالعواقب. قد رآهم أهل البصائرِ النافذةِ في جهلهم يتخبَّطون، وفي ضلالهم يَعْمَهون، وفي باطِلِهم يتردَّدون، نسوا الله فأنساهم أنفسهم، أولئك هم الفاسقون، ثم نظروا إلى ما أعطاهم الله وأقدرهم عليه من الأفكار الدقيقة في الدنيا وظاهرها، وحرموا من العقل العالي، فعرفوا أنَّ الأمر لله والحكم له في عبادِهِ، إنْ هو إلا توفيقُه أو خذلانُه، فخافوا ربهم وسألوه أن يتمَّ لهم ما وهبهم من نور العقول والإيمان حتى يصلوا إليه ويحلُّوا بساحته. وهذه الأمور لو قارنها الإيمان وبُنِيَتْ عليه؛ لأثمرت الرقيَّ العالي والحياة الطيبة، ولكنها لما بُني كثيرٌ منها على الإلحاد؛ لم تثمر إلا هبوط الأخلاق وأسباب الفناء والتدمير.
{7} Na hawa ambao hawajui undani wa mambo na matokeo yake, lakini "Wanajua tu hali ya dhahiri ya maisha ya dunia" Wanaangalia tu sababu, na wanakuwa na uhakika kwamba litatokea jambo hilo ambalo kulingana na wao zimeshapatikana sababu za kutokea kwake, na wanakuwa na uhakika kwamba haliwezi kutokea jambo ambalo hawajaona sababu zake zozote zinazolazimu kutokea kwake. Wao wanasimamia kwenye sababu za mambo tu, na hawaangalii yule anayezisababisha na kuziendesha. "Na wameghafilika na Akhera." Nyoyo zao, matamanio yao na matashi yao yameielekea dunia na matamanio yake na pumbao zake. Kwa hivyo wakatenda kwa ajili ya hayo, na wakayfanyia juhudi, na wakaja nayo na wakaondoka nayo, na akaisahau Akhera; kwa hivyo akawa hata haitamani Pepo wala hahofu na kuuogpa moto, wala haimtishi na kumsumbua kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu na kukutana naye. Na hii ni alama ya kuwa mtu wa mashakani, na sababu yake kuu ni kughafilika na Akhera. Ni katika maajabu kwamba kundi hili la watu, ambao wengi wao wamefikia kiwango cha ufahamu na akili katika sura ya nje ya kiulimwengu kiwango ambacho kinachanganya akili za na kuzishangaza ufahamu mkubwa, na wakaovumbua maajabu ya kiatomiki na kiumeme na vipando vya juu ya ardhi, baharini, na ndege za angani, ambazo walishinda kwazo, na wakasimama wazi na wakajiona na akili zao, na wakaona wengine kwamba hawana uwezo wa kile ambacho Mwenyezi Mungu aliwawezesha wao, kwa hivyo wakawatazama kwa jicho la dharau, nao pamoja na hayo ndiyo wajinga zaidi ya watu wote katika mambo ya dini yao, na walioghafilika zaidi katika maisha yao ya baada ya kufa, na wasiojua zaidi matokeo yake. Watu wenye ufahamu wa kupenya waliwaona wakiyumbayumba katika ujinga wao, wakitangatanga katika upotovu wao, na wakasitasita katika batili yao, wakamsahau Mwenyezi Mungu, naye akawasahaulisha nafsi zao. Hao ndio waliotoka nje ya mipaka. Kisha wakatazama yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwapa, na kuwapa uwezo juu yake kama vile fikira za ndani mno za kidunia na mambo yake ya dhahiri, lakini wakanyimwa akili ya juu, kwa hivyo wakajua kuwa jambo hilo ni la Mwenyezi Mungu na kwamba hukumu ni yake katika waja wake; haikuwa isipokuwa ni kuwezesha kwake au kuwaachilia mbali. Kwa hivyo, wakamhofu Mola wao Mlezi na wakamuomba awatimizie yale aliyowatunuku ya nuru ya akili na imani ili waweze kumfikia na waingie katika medani yake. Mambo haya, lau kuwa yaliunganishwa na imani na yakajengwa juu yake; basi yangezaa ustaarabu wa hali ya juu na maisha mazuri. Lakini kwa vile mengi yake yalijengwa juu ya kutokuamini Mwenyezi Mungu; hayakuzaa isipokuwa kuzorota kwa maadili na sababu za kupotelea mbali kuangamia.
{أَوَلَمْ يَتَفَكَّرُوا فِي أَنْفُسِهِمْ مَا خَلَقَ اللَّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَأَجَلٍ مُسَمًّى وَإِنَّ كَثِيرًا مِنَ النَّاسِ بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ لَكَافِرُونَ (8) أَوَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنْظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ كَانُوا أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَأَثَارُوا الْأَرْضَ وَعَمَرُوهَا أَكْثَرَ مِمَّا عَمَرُوهَا وَجَاءَتْهُمْ رُسُلُهُمْ بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا كَانَ اللَّهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَكِنْ كَانُوا أَنْفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ (9) ثُمَّ كَانَ عَاقِبَةَ الَّذِينَ أَسَاءُوا السُّوأَى أَنْ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّهِ وَكَانُوا بِهَا يَسْتَهْزِئُونَ (10)}.
8. Je, hawajifikirii nafsi zao? Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na vilivyo ndani yake isipokuwa kwa Haki na kwa muda maalumu. Na hakika watu wengi bila ya shaka ni wenye kukufuru kuwa watakutana na Mola wao Mlezi. 9. Je, hawatembei katika ardhi wakaona ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Nao walikuwa na nguvu zaidi kuliko wao, na wakaitimbua ardhi na wakaistawisha zaidi kuliko walivyoistawisha wao. Na Mitume wao wakawajia na ushahidi wa wazi. Basi hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwadhulumu, lakini wenyewe walikuwa wakijidhulumu nafsi zao. 10. Kisha ulikuwa mwisho wa wale waliofanya ubaya ni mbaya zaidi kwa sababu walizikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakawa wanazifanyia stihizai.
#
{8} أي: أفلم يتفكَّر هؤلاء المكذِّبون لرسل الله ولقائه {في أنفسهم}؛ فإنَّ في أنفسهم آيات يَعْرِفُون بها أن الذي أوجدهم من العدم سيعيدُهم بعد ذلك، وأن الذي نقلهم أطواراً من نطفةٍ إلى علقةٍ إلى مضغةٍ إلى آدميٍّ قد نفخ فيه الروح إلى طفل إلى شاب إلى شيخ إلى هرم غيرُ لائقٍ أن يتركَهم سدى مهملين. لا يُنهون، ولا يُؤمرون، ولا يثابون، ولا يعاقبون. {ما خلق اللهُ السمواتِ والأرضَ وما بينهما إلاَّ بالحق}؛ أي: ليبلوكم أيكم أحسن عملاً، {وأجلٍ مسمًّى}؛ أي: مؤقَّت بقاؤهما إلى أجل تنقضي به الدنيا وتجيء القيامة، وتبدَّل الأرض غير الأرض والسماواتُ. {وإنَّ كثيراً من الناس بلقاءِ ربِّهم لكافرونَ}: فلذلك لم يستعدُّوا للقائه، ولم يصدِّقوا رسلَه التي أخبرت به.
{8} Yaani, je, hawakutafakari hawa waliokanusha Mitume wa Mwenyezi Mungu na kukutana naye "nafsi zao?" Kwani katika nafsi zao, zimo ishara ambazo wanajua kwazo kwamba yule aliyewaumba baada ya kutokuwepo kwao, atawarudisha baada ya hayo, na kwamba yule aliyewahamisha kwa awamu kutoka kwenye manii hadi kwenye damu iliyoganda hadi kwenye pande la nyama hadi wakawa wanadamu aliyepuliziwa roho ndani yake, hadi akawa mtoto mdogo hadi akawa kijana hadi akawa mzee hadi akawa mkongwe haifai kuwaacha bure na kuwapuuza; hawakatazwi wala hawaamrishwi, wala hawalipwi mazuri wala hawaadhibiwi. "Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake isipokuwa kwa Haki." Yaani ili awajaribu ni nani miongoni mwenu ndiye mwenye vitendo vizuri zaidi "na kwa muda maalumu." Yaani, uliowekwa kubakia hadi muda ambao dunia itaisha na Kiyama kuja, na ardhi itabadilishwa iwe ardhi nyingine na hata mbingu. "Na hakika watu wengi bila ya shaka ni wenye kukataa kuwa watakutana na Mola wao Mlezi." Na ndiyo maana hawakujiandaa kwa ajili ya kukutana naye, wala hawakuwasadiki Mitume wake waliojulisha juu yake.
#
{9} وهذا الكفر عن غير دليل، بل الأدلَّة القاطعة دلَّت على البعث والجزاء، ولهذا نبَّههم على السير في الأرض والنظر في عاقبة الذين كذَّبوا رسلَهم وخالفوا أمرهم ممَّن هم أشدُّ من هؤلاء قوَّة وأكثر آثاراً في الأرض من بناء قصورٍ ومصانع ومن غرس أشجارٍ ومن زرع وإجراء أنهارٍ، فلم تُغْنِ عنهم قوَّتُهم، ولا نفعتْهم آثارُهم حين كذَّبوا رسلَهم الذين جاؤوهم بالبينات الدالات على الحقِّ وصحة ما جاؤوهم به؛ فإنَّهم حين ينظُرون في آثار أولئك؛ لم يجِدوا إلاَّ أمماً بائدةً، وخلقاً مهلَكين، ومنازل بعدهم موحشة. وذمٌّ من الخلق عليهم متتابعٌ، وهذا جزاءٌ معجَّل نموذج للجزاء الأخروي ومبتدأ له؛ وكلُّ هذه الأمم المهلَكة لم يظلِمْهُمُ الله بذلك الإهلاك، وإنما ظلموا أنفسهم وتسبَّبوا في هلاكها.
{9} Ukafiri huu hautokani na ushahidi wowote, bali ushahidi wa uhakika unaonyesha kuwepo ufufuo na malipo, na ndiyo maana akatanabahisha kwamba wasafiri katika ardhi na wazingatie matokeo ya wale waliokadhibisha Mitume wao na wakaasi amri yao, ambao walikuwa wana nguvu zaidi kuliko hawa, na wana athari kubwa zaidi juu ya ardhi, kama vile kujenga makasri na majengo ya kifahari, na ambao walipanda miti na mimea, na mitiririko ya mito. Lakini nguvu zao hazikuwafaa kitu, na athari zao hazikuwafaa wakati walipowakadhibisha Mitume wao waliowajia na hoja zilizo wazi zinazoonyesha haki na usahihi wa yale waliyowaletea. Kwani hawa wanapoangalia athari za wale, hawatapata chochote isipokuwa umma waliotoweka, na viumbe walioangamizwa, na nyumba zilizokuwa ukiwa baada yao, na utajo mbaya unaoendelea kutoka kwa viumbe. Na haya ndiyo malipo yaliyoharakishwa, na mfano tu wa adhabu ya Akhera na mwanzo wake. Na umma hawa wote walioangamizwa, Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu kwa maangamizo hayo, bali wao wenyewe walijidhulumu nafsi zao na wakajisababishia kuangamizwa.
#
{10} {ثم كان عاقبةُ الذين أساؤوا}؛ أي: المسيئين {السوأى}؛ أي: الحالة السيئة الشنيعة، وصار ذلك داعياً لهم لأن {كذَّبوا بآيات الله وكانوا بها يستهزئون}: فهذا عقوبةٌ لسوئهم وذنوبهم، ثم ذلك الاستهزاء والتكذيب يكونُ سبباً لأعظم العقوبات وأعضل المثلات.
{10} "Kisha ulikuwa mwisho wa wale waliofanya ubaya." Yaani, wale wabaya "ni mbaya zaidi" ya kutisha, "kwa sababu kuzikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakawa wanazifanyia stihizai." Hii ni adhabu ya ubaya wao na dhambi zao. Kisha kejeli hiyo na kukadhibisha huko kulikuwa ni sababu ya adhabu kubwa zaidi na mifano mibaya zaidi.
{اللَّهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ (11) وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يُبْلِسُ الْمُجْرِمُونَ (12) وَلَمْ يَكُنْ لَهُمْ مِنْ شُرَكَائِهِمْ شُفَعَاءُ وَكَانُوا بِشُرَكَائِهِمْ كَافِرِينَ (13) وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يَوْمَئِذٍ يَتَفَرَّقُونَ (14) فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَهُمْ فِي رَوْضَةٍ يُحْبَرُونَ (15) وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَلِقَاءِ الْآخِرَةِ فَأُولَئِكَ فِي الْعَذَابِ مُحْضَرُونَ (16)}.
11. Mwenyezi Mungu huanzisha uumbaji, tena akaurudisha mara ya pili, na kisha mtarejeshwa kwake. 12. Na siku itakaposimama Saa ya Kiama, wahalifu watakata tamaa. 13. Wala hawatakuwa na waombezi wowote miongoni mwa wale waliokuwa wakiwashirikisha na Mwenyezi Mungu; na wao wenyewe watawakataa hao washirikishwa wao. 14. Na siku itakaposimama Saa ya Kiyama, siku hiyo watatengana. 15. Ama wale walioamini na wakatenda mema, watafurahishwa katika Bustani. 16. Na ama wale waliokufuru na wakazikanusha Ishara zetu na mkutano wa Akhera, hao basi watahudhurishwa katika adhabu.
#
{11 - 13} يخبر تعالى أنَّه المتفرِّدُ بإبداء المخلوقات، ثم يعيدُهم. ثم إليه يُرجعون بعد إعادتهم ليجازيهم بأعمالهم. ولهذا ذكر جزاء أهل الشرِّ ثم جزاء أهل الخير، فقال: {ويوم تقومُ الساعةُ}: ويقوم الناس لربِّ العالمين، [ويرون] القيامة عياناً، يومئذٍ {يُبْلِسُ المجرمون}؛ أي: ييأسون من كلِّ خير، وذلك أنهم ما قَدَّمُوا لذلك اليوم إلاَّ الإجرام، وهي الذنوب من كفرٍ وشركٍ ومعاصٍ، فلما قدَّموا أسباب العقاب، ولم يخلِطوها بشيءٍ من أسباب الثواب؛ أيسوا، وأبلسوا، وأفلسوا، وضلَّ عنهم ما كانوا يفترونه من نفع شركائهم وأنهم يشفعون لهم، ولهذا قال: {ولم يكن لهم من شركائِهِم}: التي عَبَدوها مع الله {شفعاءُ وكانوا بشركائِهِم كافرينَ}: تبرَّأ المشركون ممَّن أشركوهم مع الله، وتبرَّأ المعبودون وقالوا: تبرَّأنا إليك، ما كانوا إيَّانا يعبدونَ، والتعنوا وابتعدوا.
{11 - 13} Mwenyezi Mungu anatujulisha kwamba Yeye ndiye pekee anayeanzisha uumbaji wa viumbe, kisha akavirudisha. Kisha kwake watarejeshwa baada ya kurudishwa kwao, ili awalipe kwa vitendo vyao. Ndiyo maana akataja malipo ya watu waovu, kisha malipo ya watu wema. Akasema, "Na siku itakaposimama Saa ya Kiyama," na watu wasimame mbele ya Mola Mlezi wa walimwengu wote
[na wakione] Kiyama kwa macho yao wenyewe, siku hiyo "wahalifu watakata tamaa" juu ya kila heri, na hilo ni kwa sababu hawakuitangulizia siku hiyo isipokuwa uhalifu, ambao ni madhambi kama vile ukafiri, ushirikina na maasi. Kwa hivyo, walipotanguliza sababu za adhabu, na hawakuzichanganya na chochote katika sababu za kulipwa mazuri, wakakata tamaa, wakafilisika, na yakawapotea yale waliyokuwa wakiyazua ya kunufaishwa na washirika wao, na kwamba watawafanyia uombezi. Ndiyo maana akasema, "Wala hawatakuwa na waombezi wowote miongoni mwa wale waliokuwa wakiwashirikisha na Mwenyezi Mungu; na wao wenyewe watawakataa hao washirikishwa wao." Hao washirikina watajitenga mbali na wale ambao wao wenyewe waliwashirikisha pamoja na Mwenyezi Mungu, na pia wale walioabudiwa watajitenga nao,
na watasema: Tunajitenga nao mbele yako. Hawakuwa wakituabudu sisi.
#
{14 - 16} وفي ذلك اليوم يفترق أهل الخير والشرِّ كما افترقتْ أعمالهم في الدنيا. {فأمَّا الذين آمنوا وعملوا الصالحاتِ}: آمنوا بقلوبِهِم وصدَّقوا ذلك بالأعمال الصالحة {فهم في روضةٍ}: فيها سائرُ أنواع النبات وأصنافِ المشتَهَياتِ {يُحْبَرونَ}؛ أي: يُسَرَّون، وينعَّمون بالمآكل اللذيذة والأشربة والحور الحسان والخدم والوِلْدان والأصوات المطربات والسماع المشجي والمناظر العجيبة والروائح الطيبة والفرح والسرور واللَّذَّة والحبور، مما لا يقدِرُ أحدٌ أن يصفه. {وأما الذين كفروا}: وجَحَدوا نعمه، وقابلوها بالكفر، {وكذَّبوا بآياتنا}: التي جاءتهم بها رسُلُنا {فأولئكَ في العذاب مُحْضَرونَ}: فيه، قد أحاطتْ بهم جهنَّم من جميع جهاتهم، واطَّلع العذابُ الأليمُ على أفئدتهم، وشوى الحميمُ وجوهَهم، وقطَّع أمعاءَهم؛ فأين الفرق بين الفريقين؟! وأين التساوي بين المنعمين والمعذبين؟!
{14 - 16} Na siku hiyo watu wema na wabaya watatengana, kama vile matendo yao yalivyotengana katika dunia hii. "Ama wale walioamini na wakatenda mema," waliamini kwa nyoyo zao na wakasadikisha hilo kwa vitendo vizuri "watafurahishwa katika Bustani," yenye kila aina ya mimea na kila aina ya vitu vinavyotamaniwa. Humo watafurahishwa kwa chakula kitamu, vinywaji, wanawali warembo, watumishi, watoto, sauti za kuimba, kusikia maneno mazuri, na mandhari ya ajabu, harufu za kupendeza, furaha na raha ambazo hakuna mtu anayeweza kuzielezea. "Na ama wale waliokufuru" na wakakadhibisha neema zake, na wakakabiliana nazo kwa kuzikufuru, "na wakazikadhibisha Ishara zetu" ambazo Mitume wetu waliwaletea, "hao basi watahudhurishwa katika adhabu." Jahannam itawazunguka kwa pande zao zote, na adhabu iumizayo itafika kwenye nyoyo zao, na Moto wa Jahannam utabambua nyuso zao, na kukata matumbo yao. Kwa hivyo tofauti kati ya makundi haya mawili iko wapi? Na uko wapi usawa kati ya wenye kufurahishwa na wenye kuadhibiwa?
{فَسُبْحَانَ اللَّهِ حِينَ تُمْسُونَ وَحِينَ تُصْبِحُونَ (17) وَلَهُ الْحَمْدُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَعَشِيًّا وَحِينَ تُظْهِرُونَ (18) يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَيُحْيِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَكَذَلِكَ تُخْرَجُونَ (19)}.
17. Basi Subhanallah
(Mtakaseni Mwenyezi Mungu) jioni na asubuhi. 18. Na sifa zote njema ni zake katika mbingu na ardhi, na alasiri na adhuhuri. 19. Hukitoa kilicho hai kutokana na kilichokufa, na hukitoa kilichokufa kutokana na kilicho hai. Na huihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Na kama hivyo ndivyo mtavyofufuliwa.
#
{17 - 18} هذا إخبارٌ عن تنزُّهه عن السوء والنقص وتقدُّسه عن أن يماثِلَه أحدٌ من الخلق، وأمرٌ للعباد أن يسبِّحوه حين يُمسون، وحين يُصبحون، ووقت العشي ووقت الظهيرة؛ فهذه الأوقات الخمسةُ أوقاتُ الصلوات الخمس، أمر الله عبادَه بالتسبيح فيها والحمدِ، ويدخُلُ في ذلك الواجب منه؛ كالمشتملة عليه الصلوات الخمس، والمستحبُّ؛ كأذكار الصباح والمساء وأدبار الصلوات وما يقترنُ بها من النوافل؛ لأنَّ هذه الأوقات التي اختارها الله لأوقات المفروضات هي أفضلُ الأوقات؛ فالتسبيحُ والتحميدُ فيها والعبادة فيها أفضلُ من غيرها، بل العبادةُ وإنْ لم تشتملْ على قول: سبحان الله؛ فإنَّ الإخلاص فيها تنزيهٌ لله بالفعل أنْ يكون له شريكٌ في العبادة، أو أن يستحقَّ أحدٌ من الخلق ما يستحقُّه من الإخلاص والإنابة.
{17 - 18} Huku ni kujulisha juu ya kutakasika kwake mbali na ubaya na upungufu, na utakatifu wake ambao hakuna yeyote anayefanana naye katika kiumbe wake, na kuwaamrisha waja wake wamtakase jioni na asubuhi, na alasiri na adhuhuri. Nyakati hizi tano ndizo nyakati za Swala tano, ambazo Mwenyezi Mungu aliwaamrisha waja wake kumtakasa ndani yake na kumsifu. Zinaingia ndani yake swala za wajibu kama vile hizo swala tano, na mambo ya kupendekezwa kama vile nyiradi za asubuhi na jioni, na baada ya swala, na pia swala za hiari zinazohusiana nazo. Kwa sababu nyakati hizi ambazo Mwenyezi Mungu alizichagua kwa ajili ya swala za faradhu ndizo nyakati bora zaidi. Kwa hivyo, kumtakasa, kumsifu ndani yake, na kuabudu ndani yake ni bora zaidi kuliko nyakati nyinginezo.
Na ikiwa ibada haijumuisha kusema: Ametakasika Mwenyezi Mungu, basi kuifanya iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu kunakuwa kwa kumtakasa Mwenyezi Mungu kwa vitendo vinavyoonyesha kwamba hana mshirika yeyote katika ibada, au yeyote katika kiumbe kustahiki kile anachostahiki Mwenyezi Mungu cha kukusudiwa Yeye tu na kutubia kwake.
#
{19} {يُخْرِجُ الحيَّ من الميِّتِ}: كما يُخرج النباتَ من الأرض الميتة، والسنبلة من الحبة، والشجرة من النواة، والفرخ من البيضة، والمؤمن من الكافر ... ونحو ذلك. {ويخرِجُ الميِّتَ من الحيِّ}: بعكس المذكور، {ويُحيي الأرضَ بعدَ موتِها}: فينزل عليها المطر وهي ميتة هامدةٌ؛ فإذا أنزل عليها الماء؛ اهتزَّتْ، ورَبَتْ، وأنبتَتْ من كلِّ زوج بهيج. {وكذلك تُخْرَجونَ}: من قبورِكم.
فهذا دليلٌ قاطعٌ وبرهانٌ ساطعٌ أنَّ الذي أحيا الأرض بعد موتها فإنه يحيي الأموات؛ فلا فرقَ في نظر العقل بين الأمرين، ولا موجب لاستبعاد أحدهما مع مشاهدة الآخر.
{19} "Hukitoa kilicho hai kutokana na kilichokufa" kama vile anavyotoa mche katika udongo uliokufa, na masuke kutoka katika punje, mti kutoka katika kokwa, na kifaranga kutoka katika yai, na Muumini kutoka kwa kafiri... na mifano ya hayo. "Na hukitoa kilichokufa kutokana na kilicho hai" kinyume na ilivyotajwa. "Na huihuisha ardhi baada ya kufa kwake" mvua inapoiyeshea hali ya kuwa imekufa na imetulia tuli. Hapo, inasisimka na kututumka, na kumea kila namna ya mimea mizuri. "Na kama hivyo ndivyo mtavyofufuliwa" kutoka makaburini mwenu. Huu ni ushahidi wa uhakika na uthibitisho wa wazi kwamba aliyeihuisha ardhi baada ya kufa kwake atawahuisha wafu. Hakuna tofauti yoyote katika kutazama kwa akili kati ya mambo haya mawili, na hakuna sababu yeoye ya kulikataa moja yake pamoja na kuona wazi wazi uwezekano wa linginelo.
{وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَكُمْ مِنْ تُرَابٍ ثُمَّ إِذَا أَنْتُمْ بَشَرٌ تَنْتَشِرُونَ (20) وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُمْ مِنْ أَنْفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُمْ مَوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ (21)}.
20. Na katika Ishara zake ni kuwa aliwaumba kwa udongo. Kisha mmekuwa watu mliotawanyika kote kote. 21. Na katika Ishara zake ni kuwa aliwaumbia wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye ameweka mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaotafakari.
#
{20} هذا شروعٌ في تعداد آياتِهِ الدَّالَّة على انفراده بالإلهيَّة وكمال عظمته ونفوذ مشيئتِهِ وقوَّة اقتدارِهِ وجميل صنعِهِ وسعة رحمتِهِ وإحسانه، فقال: {ومن آياتِهِ أنْ خَلَقَكُم من ترابٍ}: وذلك بخلق أصل النسل آدم عليه السلام، {ثم إذا أنتُم بشرٌ تنتَشِرون}؛ [أي: الذي خلقكم من أصلٍ وَاحدٍ وَمَادَّةٍ وَاحدةٍ]، وبثَّكم في أقطار الأرض وأرجائها.
ففي ذلك آيات على أنَّ الذي أنشأكم من هذا الأصل، وبثَّكم في أقطار الأرض هو الربُّ المعبود الملكُ المحمود والرحيمُ الودود، الذي سيعيدُكم بالبعث بعد الموت.
{20} Huu ndio mwanzo wa kuorodheshwa kwa ishara zake zinazoonyesha upekee wake katika uungu, ukamilifu wa ukuu wake, utekelezekaji wa mapenzi yake, na nguvu ya uweza wake, na uzuri wa matendo yake, na upana wa rehema yake na ihsani yake. Alisema, "Na katika Ishara zake ni kuwa aliwaumba kwa udongo" kwa kuumba asili ya dhuriya, Adam, amani iwe juu yake. "Kisha mmekuwa watu mliotawanyika kote kote."
[Yaani, Yeye ndiye aliyewaumba nyinyi kutokana na asili moja na kiini kimoja], na akawaeneza katika pande mbalimbali za ardhi na sehemu zake. Katika hayo zimo ishara kwamba aliyewaumba kutokana na asili hii na akawaeneza katika pande zote za ardhi ndiye Mola Mlezi anayeabudiwa, Mfalme anayehimidiwa, Mwingi wa kurehemu, Mwingi wa mapenzi, ambaye atawarudisha kwa kuwafufua baada ya kufa kwenu.
#
{21} {ومن آياتِهِ}: الدالَّة على رحمتِهِ وعنايتِهِ بعباده وحكمتِهِ العظيمة وعلمِهِ المحيط، {أنْ خَلَقَ لكم من أنفسِكم أزواجاً}: تناسِبُكم، وتناسبونهنَّ، وتشاكِلُكم، وتشاكلونهن؛ {لِتَسْكُنوا إليها وجعل بينكم مودَّةً ورحمةً}: بما رتَّب على الزواج من الأسباب الجالبة للمودَّة والرحمة، فحصل بالزوجة الاستمتاع واللَّذَّة والمنفعةُ بوجود الأولاد وتربيتهم والسكون إليها؛ فلا تجد بين أحد في الغالب مثل ما بين الزوجين من المودَّة والرحمة. {إنَّ في ذلك لآياتٍ لقومٍ يتفكَّرونَ}: يُعْمِلون أفكارَهم، ويتدبَّرون آياتِ الله، وينتَقِلون من شيء إلى شيء.
{21} "Na katika ishara zake" zinazoonyesha rehema yake na uangalizi wake kwa waja wake na hekima yake kubwa na elimu yake iliyozunguka kila kitu, "ni kuwa aliwaumbia wake zenu kutokana na nafsi zenu" wanaolingana nanyi, nanyi mnalingana nao, na wanafanana na nyinyi, nanyi mnafanana nao, "ili mpate utulivu kwao. Naye ameweka mapenzi na huruma baina yenu," kwa sababu ya kuwa ameweka katika ndoa mambo yenye kuleta mapenzi na rehema, kwa hivyo mtu akapata kutoka kwa mke wake starehe, raha, na manufaa, kwa kupatikana watoto, kuwalea, na kupata utulivu kwake; basi huwezi kupata mapenzi na rehema iliyopo kati ya wanandoa kwa mtu yeyote yule. "Hakika katika haya, bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaotafakari" ishara za Mwenyezi Mungu, na wanatoka kwa kitu kimoja hadi kingine.
{وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافُ أَلْسِنَتِكُمْ وَأَلْوَانِكُمْ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِلْعَالِمِينَ (22)}.
22. Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutofautiana ndimi zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wajuao.
#
{22} والعالمون: هم أهلُ العلم الذين يفهمون العِبَرَ ويتدبَّرون الآيات، والآياتُ في ذلك كثيرة: فمن آياتِ خَلْقِ {السمواتِ والأرضِ}: وما فيهما؛ أنَّ ذلك دالٌّ على عظمة سلطان الله وكمال اقتدارِهِ، الذي أوجد هذه المخلوقات العظيمة، وكمال حكمتِهِ؛ لما فيها من الإتقان، وسعة علمه؛ لأنَّ الخالق لا بدَّ أن يعلم ما خلقه؛ {ألا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ}، وعموم رحمته وفضله؛ لما في ذلك من المنافع الجليلة، وأنه المريد الذي يختارُ ما يشاءُ؛ لما فيها من التخصيصات والمزايا، وأنَّه وحده الذي يستحقُّ أن يُعبد ويوحَّد؛ لأنه المنفرد بالخلق؛ فيجب أن يُفْرَدَ بالعبادة.
فكل هذه أدلَّة عقليَّة نبَّه الله العقول إليها، وأمرها بالتفكُّر واستخراج العبرة منها، {و} كذلك في {اختلاف ألسنتكم وألوانكم}: على كَثْرَتِكُم وتبايُنِكُم مع أنَّ الأصل واحدٌ ومخارج الحروف واحدةٌ، ومع ذلك؛ لا تجدُ صوتين متَّفقين من كل وجه، ولا لونين متشابهين من كلِّ وجه؛ إلاَّ وتجد من الفرق بين ذلك ما به يحصُلُ التمييز.
وهذا دالٌّ على كمال قدرتِهِ ونفوذِ مشيئتِهِ وعنايته بعبادِهِ ورحمتِهِ بهم، أنْ قدَّرَ ذلك الاختلاف؛ لئلاَّ يقع التشابه، فيحصل الاضطراب، ويفوت كثير من المقاصد والمطالب.
{22} Na wajuao ni watu wenye elimu wanaofahamu mazingatio na wanazizingatia ishara mbalimbali, na ishara katika haya ni nyingi. Miongoni mwa ishara za "kuumba mbingu na ardhi" na vilivyomo ndani yake ni kwamba hilo linaonyesha ukuu wa mamlaka ya Mwenyezi Mungu na ukamilifu wa uwezo wake, ambaye aliumba viumbe hawa wakuu, na ukamilifu wa hekima yake. Kwa sababu ya ustadi wake mkubwa na upana wa elimu yake; kwa sababu Muumba lazima ajue alichokiumba. "Je, asijue yule aliyeumba" na pia linaonyesha ujumla wa rehema yake na fadhila zake; Kwa sababu ya manufaa makubwa ambayo yako ndani yake, na kwamba yeye ni mwenye utashi anayechagua chochote anachotaka; kwa sababu ya umaalumu ulio ndani yake, na kwamba Yeye pekee ndiye anayestahiki kuabudiwa na kupwekeshwa; kwa sababu yeye pekee ndiye muumbaji; kwa hivyo ni lazima aabudiwe peke yake. Yote haya ni ushahidi wa kimantiki ambao Mwenyezi Mungu amezitanabahisha akili juu yake, na akaziamrisha zitafakari na kutoa mazingatio ndani yake, "na" vile vile katika "kutofautiana ndimi zenu na rangi zenu" licha ya wingi wenu na tofauti zenu, licha ya kwamba asili yenu ni moja na sehemu za matamshi yenu ni zile zile, lakini pamoja na hayo, huwezi kupata sauti mbili zinazoafikiana kwa namna zote, wala rangi mbili zinazofanana kwa namna zote, walakini utapata tofauti kati yake, jambo ambalo kwalo wanatofautishwa. Hili linaonyesha ukamilifu wa uwezo wake, utekelezekaji wa mapenzi yake, utunzaji wake waja wake na rehema yake kwao, kwa kuweka utofauti huo; ili kufanana kusitokee, kwa hivyo machafuko yakatokea na kusababisha kukosekana malengo mengi na mahitaji.
{وَمِنْ آيَاتِهِ مَنَامُكُمْ بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَابْتِغَاؤُكُمْ مِنْ فَضْلِهِ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَسْمَعُونَ (23)}
23. Na katika Ishara zake ni kulala kwenu usiku na mchana, na kutafuta kwenu fadhila zake. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaosikia.
#
{23} أي: سماع تدبُّر وتعقُّل للمعاني والآيات في ذلك؛ إنَّ ذلك دليلٌ على رحمة الله تعالى؛ كما قال: {ومن رحمتِهِ جَعَلَ لكم الليلَ والنهارَ لِتَسْكُنوا فيه ولِتَبْتَغوا من فضلِهِ ولعلَّكم تشكرونَ}، وعلى تمام حكمتِهِ؛ إذْ حكمتُه اقتضتْ سكون الخلق في وقت ليستريحوا [به] ويجموا، وانتشارهم في وقت لمصالحهم الدينيَّة والدنيويَّة، ولا يتمُّ ذلك إلا بتعاقُب الليل والنهار عليهم، والمنفردُ بذلك هو المستحق للعبادة.
{23} Yaani, kusikiliza kwa kutafakari na kuelewa maana na ishara zilizo katika hilo. Hakika hayo ni ushahidi wa rehema za Mwenyezi Mungu, kama alivyosema, "Na ni katika rehema zake amekufanyieni usiku na mchana ili mpate kupumzika humo na ili mtafute katika fadhila zake, na ili mpate kushukuru." Na ni katika hekima yake kamili. Kwani hekima yake inahitaji kwamba viumbe vikae kwa utulivu muda fulani ili vipumzike na vijikusanye, na visambae katika wakati fulani kwa ajili ya masilahi yao ya kidini na ya kidunia, na hilo haliwezi kutimia isipokuwa kwa kufuatana mchana na usiku juu yao, na mwenye kutendesha hayo peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa.
{وَمِنْ آيَاتِهِ يُرِيكُمُ الْبَرْقَ خَوْفًا وَطَمَعًا وَيُنَزِّلُ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَيُحْيِي بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَعْقِلُونَ (24)}.
24. Na katika Ishara zake huwaonyesha umeme kwa kuwatia hofu na tamaa. Na huwateremshia maji kutoka mbinguni, na kwa hayo huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu watumiao akili.
#
{24} أي: ومن آياتِهِ أن يُنَزِّلَ عليكم المطر الذي تحيا به البلادُ والعباد، ويريكم قبلَ نزوله مقدِّماتِهِ من الرعد والبرق الذي يُخاف ويُطمع فيه. {إنَّ في ذلك لآياتٍ}: دالَّة على عموم إحسانِهِ وسَعةِ علمِهِ وكمال إتْقانِهِ وعظيم حكمتِهِ، وأنَّه يُحيي الموتى، كما أحيا الأرض بعد موتها، {لقوم يعقلونَ}؛ أي: لهم عقولٌ تعقِلُ بها ما تسمعُه وتراه وتحفظُه، وتستدلُّ به على ما جعل دليلاً عليه.
{24} Yaani, na katika Ishara zake ni kwamba Yeye huwateremshia mvua ambayo kwayo ardhi na waja vinakuwa hai, na huwaonyesha kabla ya kushuka kwake utangulizi wake kama vile ngurumo za radi na umeme, vinavyohofiwa na pia hutia matumaini. "Hakika katika hayo, zipo Ishara" zinazoonyesha ujumla ya ihsani yake, na upana wa elimu yake, na ukamilifu wa ustadi wake, na ukubwa wa hekima yake, na kwamba atawahuisha wafu kama alivyoihuisha ardhi baada ya kufa kwake, "kwa watu watumiao akili." Yaani, wana akili ambazo kwazo wanaelewa yale wanayoyasikia na kuyaona na kuyahifadhi, na huzitumia kuwa ni ushahidi wa yale ambayo ziliwekwa kwa ajili yake.
{وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ تَقُومَ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ بِأَمْرِهِ ثُمَّ إِذَا دَعَاكُمْ دَعْوَةً مِنَ الْأَرْضِ إِذَا أَنْتُمْ تَخْرُجُونَ (25) وَلَهُ مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ كُلٌّ لَهُ قَانِتُونَ (26) وَهُوَ الَّذِي يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ وَلَهُ الْمَثَلُ الْأَعْلَى فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (27)}.
25. Na katika Ishara zake ni kuwa mbingu na ardhi zimesimama kwa amri yake. Kisha atakapowaita mwito mmoja tu, hapo mtatoka kwenye ardhi. 26. Na ni vyake Yeye vilivyo mbinguni na katika ardhi. Vyote vinamtii Yeye. 27. Na Yeye ndiye anayeanzisha uumbaji, kisha ataurudisha mara nyingine. Na jambo hili ni jepesi zaidi kwake. Naye ndiye mwenye mfano bora zaidi katika mbingu na ardhi. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
#
{25} أي: ومن آياته العظيمة أنْ قامت السماواتُ والأرضُ واستقرَّتا وثبتتا لأمرِهِ، فلم يتزلزلا، ولم تسقطِ السماءُ على الأرض؛ فقدرتُه العظيمةُ التي بها أمسك السماواتِ والأرضَ أن تزولا؛ يقدِرُ بها على أنَّه إذا دعا الخلق دعوةً من الأرض؛ إذا هم يَخْرُجونَ. {لَخَلْقُ السمواتِ والأرض أكبرُ من خَلْق الناس}.
{25} Yaani, miongoni mwa ishara zake kubwa ni kuwa mbingu na ardhi zilisimama na zikatulia na kuimarika kwa amri yake, na wala hazikutetereka, na mbingu hazikuiangukia ardhi. Kwani kwa uweza wake mkuu ambao kwa huo alizishikilia mbingu na ardhi zisije kuondoka, basi pia anaweza kwa huo huo anapotaka kuwaita viumbe kwa wito mmoja kutoka katika ardhi, tazama, watatoka nje wote. "Bila ya shaka kuumba mbingu na ardhi ni kukubwa zaidi kuliko kuwaumba watu."
#
{26} {وله مَن في السمواتِ والأرض}: الكلُّ خلقُه ومماليكه والمتصرِّف فيهم من غير منازعٍ ولا معاونٍ ولا معارضٍ، وكلُّهم قانتون لجلالِهِ، خاضعون لكماله.
{26} "Na ni vyake Yeye vilivyo mbinguni na katika ardhi" vyote ni viumbe vyake na miliki yake, na anaendesha bila ya kizuizi chochote, wala msaidizi, wala mpinzani, na vyote vinatii kwa sababu ya utukufu wake na vinanyenyekea kwa sababu ya ukamilifu wake.
#
{27} {وهو الذي يبدأ الخَلْقَ ثم يعيدُه وهو}؛ أي: إعادةُ الخلق بعد موتهم، {أهونُ عليه}: من ابتداء خَلْقِهم، وهذا بالنسبة إلى الأذهان والعقول؛ فإذا كان قادراً على الابتداء الذي تقرُّون به؛ كان قدرتُه على الإعادة التي هي أهون أولى وأولى.
ولمَّا ذكر من الآيات العظيمةِ ما به يعتبر المعتبرونَ، ويتذكَّر المؤمنون، ويستبصِرُ المهتدون؛ ذكر الأمر العظيم والمطلب الكبير، فقال: {وله المَثَلُ الأعلى في السمواتِ والأرضِ}: وهو كلُّ صفةِ كمال، والكمال من تلك الصفة، والمحبة والإنابة التامة الكاملة في قلوب عباده المخلصين والذكر الجليل والعبادة منهم؛ فالمَثَلُ الأعلى هو وصفُه الأعلى وما ترتَّب عليه، ولهذا كان أهلُ العلم يستعمِلون في حقِّ الباري قياس الأولى، فيقولون: كلُّ صفة كمال في المخلوقاتِ؛ فخالِقُها أحق بالاتِّصاف بها على وجه لا يشارِكُه فيها أحدٌ، وكلُّ نقص في المخلوق يُنَزَّهُ عنه؛ فتنزيهُ الخالق عنه من باب أولى وأحرى. {وهو العزيزُ الحكيمُ}؛ أي: له العزَّة الكاملة والحكمة الواسعة، فعزَّتُه أوجدَ بها المخلوقاتِ وأظهرَ المأموراتِ، وحكمتُه أتقنَ بها ما صَنَعَه وأحسنَ فيها ما شَرَعَه.
{27} "Na Yeye ndiye anayeanzisha uumbaji, kisha ataurudisha mara nyingine." Yaani, kuumba viumbe upya baada ya kufa kwao, "ni jepesi zaidi kwake" kuliko kuanzisha kuwaumba. Na hili ni kulingana na bongo na akili. Kwani ikiwa Yeye ni muweza wa kuanzisha ambako nyinyi mnakiri hilo, basi ana uwezo wa kurudisha, ambako ni rahisi zaidi na kunakofailia zaidi kuaminiwa. Na alipotaja baadhi ya ishara zake kubwa ambazo kwazo wenye kuzingatia wanazingatia, na Waumini wanakumbuka, na wanapata ufahamu wale walioongoka, akataja amri kubwa na mahitaji makubwa, akasema, "Naye ndiye mwenye mfano bora zaidi katika mbingu na ardhi." Na huo
(mfano bora zaidi) ni kila sifa yenye ukamilifu, na ukamilifu unatokana na sifa hiyo, na mapenzi kamili na toba na kurudi kwake kikamilifu ambako kutoka katika nyoyo za waja wake wanaomkusudia yeye tu, na wanamtaja kwa wingi na wakamuabudu. Mfano bora zaidi ndio maelezo yake ya juu kabisa na yale yanayoambatana na hilo. Na ndiyo maana watu wenye elimu walikuwa wakitumia ulinganisho unaofailia zaidi kuhusiana na Muumba.
Walikuwa wakisema: kila sifa ya ukamilifu iliyo katika viumbe; basi Muumba wake ndiye anayestahiki zaidi kusifika nayo kwa namna ambayo hakuna yeyote anayeshiriki naye ndani yake. Na kila upungufu ulio katika kiumbe ambao kinawekwa mbali, basi kumuweka Muumba mbali nao kunafailia na kustahili zaidi. "Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima." Yaani, ana nguvu kamili na hekima pana, na kwa nguvu zake, aliumba viumbe na akadhihirisha maamrisho, na kwa hekima yake, akaumba sawasawa vile alivyounda na akafanya vizuri aliyafanya kuwa katika sheria.
{ضَرَبَ لَكُمْ مَثَلًا مِنْ أَنْفُسِكُمْ هَلْ لَكُمْ مِنْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ مِنْ شُرَكَاءَ فِي مَا رَزَقْنَاكُمْ فَأَنْتُمْ فِيهِ سَوَاءٌ تَخَافُونَهُمْ كَخِيفَتِكُمْ أَنْفُسَكُمْ كَذَلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْقِلُونَ (28) بَلِ اتَّبَعَ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَهْوَاءَهُمْ بِغَيْرِ عِلْمٍ فَمَنْ يَهْدِي مَنْ أَضَلَّ اللَّهُ وَمَا لَهُمْ مِنْ نَاصِرِينَ (29)}.
28. Amewapigia mfano kutokana na nafsi zenu. Je, katika hao iliyowamiliki mikono yenu ya kulia mnao washirika katika hivyo tulivyowaruzuku, mkawa nyinyi katika hivyo ni sawasawa, mnawaogopa kama mnavyoogopana wenyewe kwa wenyewe? Namna hivyo tunazipambanua Aya zetu kwa watu watumiao akili. 29. Bali waliodhulumu wamefuata mapendo ya nafsi zao pasina kujua. Basi ni nani atamwongoa ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza? Wala hao hawatakuwa na wa kuwanusuru."
#
{28} هذا مثلٌ ضربَه الله لِقُبح الشرك وتهجينه، مثلاً من أنفسكم لا يحتاجُ إلى حلٍّ وترحال وإعمال الجِمال. {هل لكم ممَّا ملكتْ أيمانُكم من شُرَكاء فيما رَزَقْناكم}؛ أي: هل أحدٌ من عبيدكم وإمائِكم الأرقاءِ يشارِكُكم في رزقكم، وتَرَوْنَ أنَّكم وهم فيه على حدٍّ سواء. {تخافونَهم كخيفَتِكم أنفسَكُم}؛ أي: كالأحرار الشركاء في الحقيقة، الذين يُخاف من قسمه واختصاص كل شيء بحاله؟! ليس الأمر كذلك؛ فإنَّه ليس أحدٌ مما ملكت أيمانُكم شريكاً لكم فيما رَزَقَكم الله تعالى، هذا؛ ولستُم الذين خَلَقْتُموهم ورزَقْتُموهم، وهم أيضاً مماليكُ مثلُكم؛ فكيفَ تَرْضَوْنَ أن تجعلوا لله شريكاً من خلقه، وتجعلونَه بمنزلتِهِ وعديلاً له في العبادة، وأنتُم لا تَرْضَوْنَ مساواة مماليككم لكم؟! هذا من أعجب الأشياء، ومن أدلِّ شيءٍ على سَفَهِ من اتَّخذ شريكاً مع الله، وأنَّ ما اتَّخذه باطل مضمحلٌّ، ليس مساوياً لله ولا له من العبادة شيء. {كذلك نفصِّلُ الآيات}: بتوضيحها بأمثلتها {لقوم يَعْقِلونَ}: الحقائقَ ويعرِفون. وأمَّا مَنْ لا يعقِلُ؛ فلو فُصلت له الآياتُ وبينتْ له البيِّناتُ؛ لم يكن له عقلٌ يبصِرُ به ما تبيَّن، ولا لبٌّ يعقِل به ما توضَّح؛ فأهلُ العقول والألباب هم الذين يُساق إليهم الكلام، ويوجَّه الخطاب.
{28} Huu ni mfano uliopigwa na Mwenyezi Mungu ili kuonyesha ubaya wa ushirikina na uduni wake. Ni mfano kutoka kwa nafsi zenu wenyewe ambao hauhitaji kusafiri na kuondoka na kuwaandaa ngamia. "Je, katika hao iliyowamiliki mikono yenu ya kulia mnao washirika katika hivyo tulivyowaruzuku." Yaani, je, kuna yeyote katika watumwa wenu wa kiume na wa kike anayewashiriki katika riziki zenu, na mkaona kwamba nyinyi na wao ni sawa katika riziki hiyo? "Mnawaogopa kama mnavyoogopana wenyewe kwa wenyewe?" Yaani, kama watu huru ambao ni washirika katika uhalisia, ambao wanaogopewa kugawiwa, na kila mmoja wao akachukua mgao wake maalumu? Sivyo hivyo; kwani hakuna hata mmoja katika hao iliyomiliki mikono yenu ya kulia aliye mshirika wenu katika yale aliyowaruzuku Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hilo ni hivyo, hata ingawa si nyinyi mliowaumba na kuwaruzuku, na tena wao pia wanamilikiwa tu kama nyinyi. Basi vipi mnaridhia kumfanyia Mwenyezi Mungu mshirika miongoni mwa viumbe vyake, na kumfanya kuwa katika nafasi yake na kuwa sawa naye katika ibada, na hali nyinyi wenyewe hamridhii kuwa sawa na wale mnaowamiliki? Hili ni miongoni mwa mambo ya kustaajabisha sana, na moja ya mambo yaonyeshayo zaidi upumbavu wa mwenye kumfanyia Mwenyezi Mungu mshirika, na kwamba alichochukua kuwa ni mshirika nila batili na kitapotelea mbali, hakiwezi kuwa sawa na Mwenyezi Mungu, wala hakistahiki chochote katika ibada. "Namna hivyo tunazipambanua Aya zetu" kwa kuzibainisha kwa mifano yake "kwa watu watumiao akili." Na kuelewa uhakika wa mambo na kuujua. Ama yule asiyeelewa; lau angeelezewa Aya kwa undani na akabainishiwa hoja zilizo wazi; hangekuwa na akili ya kuona kile kilicho wazi, wala ufahamu wa kuelewa kile kilichobainishwa. Kwa hivyo, watu wenye akili na ufahamu ndio wanaoongeleshwa.
#
{29} وإذا عُلِمَ من هذا المثال أنَّ من اتَّخذ من دون الله شريكاً يعبُدُه ويتوكَّل عليه في أموره؛ فإنه ليس معه من الحقِّ شيءٌ؛ فما الذي أوجبَ لهم الإقدامَ على أمرٍ باطل توضَّح بطلانُه وظهر برهانُه؟ أوجب لهم ذلك اتِّباع الهوى، فلهذا قال: {بل اتَّبَعَ الذين ظَلَموا أهواءَهم بغيرِ علم}: هويت أنفسُهم الناقصةُ التي ظهر من نقصها ما تعلَّق به هواها أمراً يجزِمُ العقل بفسادِهِ والفِطَرُ بردِّه بغير علم دلَّهم عليه ولا برهان قادَهُم إليه، {فمن يهدي مَن أضلَّ الله}؛ أي: لا تعجبوا من عدم هدايتهم؛ فإنَّ الله تعالى أضلَّهم بظلمهم، ولا طريقَ لهداية من أضلَّ الله؛ لأنَّه ليس أحدٌ معارضاً لله أو منازعاً له في ملكه، {ومالهم من ناصِرينَ}: ينصُرونَهم حين تحقُّ عليهم كلمةُ العذاب، وتنقطِعُ بهم الوصل والأسباب.
{29} Ikishajulikana kutokana na mfano huu kwamba anayemfanyia Mwenyezi Mungu mshirika akamuabudu na kumtegemea katika mambo yake, huyo hana haki yoyote katika hayo, basi ni nini kilichomsukuma kufanya jambo hili batili, ambalo ubatili wake uko wazi na uthibitisho wake umedhihirika? Hili lilisababishwa na kufuata kwao matamanio yao, na ndiyo maana akasema, "Bali waliodhulumu wamefuata mapendo ya nafsi zao pasina kujua." Nafsi zao pungufu na ambao upungufu wake umedhihirika na ambazo matamanio yake yamefungamana na mambo ambayo akili ina uhakika kwamba ni mabovu, na pia maumbile ya asili yanayakataa, hayo wanayafanya bila ya elimu yoyote iliyowaelekeza kwayo wala hata hoja iliyowafikisha kwayo. "Basi ni nani atamwongoa ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza?" Yaani, msishangae kutoongoka kwao. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwapoteza kwa dhuluma yao, na hakuna njia yoyote ya kuwaongoa yule ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza. Kwa sababu hakuna yeyote anayeweza kumpinga Mwenyezi Mungu au kubishana naye katika ufalme wake, "Wala hao hawatakuwa na wa kuwanusuru;" neno la adhabu litakapowastahiki, na wakakatikiwa mafungamano yao na njia zao.
{فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا فِطْرَتَ اللَّهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّهِ ذَلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ (30) مُنِيبِينَ إِلَيْهِ وَاتَّقُوهُ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَلَا تَكُونُوا مِنَ الْمُشْرِكِينَ (31) مِنَ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ (32)}.
30. Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini kwa unyoofu, ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo Dini iliyonyooka sawa. Lakini watu wengi hawajui. 31. Muwe wenye kutubia kwake, na mcheni Yeye, na simamisheni Swala, na wala msiwe katika washirikina. 32. Katika wale ambao kwamba wameigawanya dini yao, na wakawa makundi makundi, kila kikundi kinafurahia kilicho nacho.
#
{30} يأمرُ تعالى بالإخلاص له في جميع الأحوال وإقامةِ دينِهِ، فقال: {فأقم وجهَكَ}؛ أي: انصبْه ووجِّهْه {للدين}: الذي هو الإسلامُ والإيمانُ والإحسان، بأن تتوجَّه بقلبك وقصدِك وبَدَنِكَ إلى إقامة شرائع الدين الظاهرة كالصلاة والزكاة والصوم والحج ونحوها، وشرائعه الباطنة كالمحبَّة والخوف والرجاء والإنابة، والإحسان في الشرائع الظاهرة والباطنة؛ بأن تعبدَ الله فيها كأنَّك تراه؛ فإنْ لم تكنْ تراه؛ فإنَّه يراك.
وخص الله إقامة الوجه؛ لأنَّ إقبال الوجه تَبَعٌ لإقبال القلب، ويترتَّب على الأمرين سعيُ البدن، ولهذا قال: {حَنيفاً}؛ أي: مقبلاً على الله في ذلك معرضاً عمَّا سواه، وهذا الأمر الذي أمرناك به هو {فطرةَ الله التي فَطَرَ الناس عليها}: ووضع في عقولهم حُسْنَها واستقباحَ غيرها؛ فإنَّ جميع أحكام الشرع الظاهرة والباطنة قد وَضَعَ اللهُ في قلوب الخلق كلِّهم الميلَ إليها، فوضع في قلوبهم محبَّة الحقِّ وإيثار الحقِّ، وهذا حقيقة الفطرة. ومَنْ خَرَجَ عن هذا الأصل؛ فلعارض عرض لفطرته أفسدها؛ كما قال النبيُّ - صلى الله عليه وسلم -: «كلُّ مولودٍ يولَدُ على الفطرةِ؛ فأبواه يهوِّدانِهِ أو ينصِّرانِهِ أو يمجِّسانِهِ». {لا تبديلَ لِخَلْقِ اللهِ}؛ أي: لا أحد يبدِّلُ خلق الله فيجعلُ المخلوقَ على غير الوضع الذي وَضَعَهُ الله. {ذلك}: الذي أمَرْناك به {الدِّينُ القيِّمُ}؛ أي: الطريق المستقيم الموصل إلى الله وإلى كرامتِهِ؛ فإنَّ مَن أقام وجهه للدين حنيفًا؛ فإنَّه سالك الصراط المستقيم في جميع شرائعِهِ وطرقِهِ، {ولكنَّ أكثرَ الناسِ لا يعلمون}: فلا يتعرَّفون الدِّين القيِّم، وإنْ عرفوه؛ لم يَسْلُكوه.
{30} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaamrisha kwamba akusudiwe Yeye tu katika kila hali na kuisimamisha Dini yake. Alisema, "Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini" ambayo ni Uislamu, Imani, na ihsani, kwa kuelekeza moyo wako, nia yako, na mwili wako katika kusimamisha sheria dhahiri za Dini, kama vile swala, zaka, saumu, Hijja, na mfano ya hayo, na sheria zake zilizofichika, kama vile upendo, hofu, matumaini, kurudi kwa Mwenyezi Mungu, na kufanya kwa uzuri sana sheria zilizo wazi na zilizofichikana; kwa kumwabudu Mwenyezi Mungu ndani yake kana kwamba unamwona. Na ikiwa hamuoni; basi hakika Yeye anakuona. Na hapa Mwenyezi Mungu aliamrisha kuusimamisha uso hasa; kwa sababu kuelekea kwa uso kunafuata kuelekea kwa moyo, na hao mawili yanasababisha mwili pia kufanya juhudi. Na ndiyo maana akasema, "kwa unyoofu;" yaani, kwa kumuelekea Mwenyezi Mungu katika hayo, na kukipa mgongo kila kitu kinginecho. Na jambo hili tulilokuamrisha ndilo "umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu" na akaweka katika akili zao uzuri wake, na akawafanya waone yasiyokuwa hilo kuwa ni mabaya. Kwa maana Mwenyezi Mungu ameweka ndani ya nyoyo za viumbe vyote kuzielekea hukumu zote za kisheria zilizo dhahiri na zilizofichikana, na pia akaweka ndani ya nyoyo zao kupenda haki na kuipendelea. Na huu ndio uhakika wa umbile la asili. Na mwenye kutoka katika msingi huu; basi ni kwa sababu ya jambo lililoingia katika umbile lake la asili na likaliharibu, kama alivyosema Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake,
“Kila mtoto huzaliwa katika umbile la asili. Kisha wazazi wake wanamfanya kuwa Myahudi, au Mkristo, au Majusi.” "Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu." Yaani, hakuna anayeweza kuwabadilisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu na akawafanya viumbe katika hali nyingine isipokuwa ile ambayo Mwenyezi Mungu aliwaumbia. "Hiyo" ambayo tulikuamrisha "ndiyo Dini iliyonyooka sawa." Yaani, njia iliyonyooka inayofikisha kwa Mwenyezi Mungu na utukufu wake. Kwani, mwenye kuuelekeza uso wake sawasawa kwenye Dini, basi yeye amefuata njia iliyonyooka katika sheria zake zote na njia zake zote, "Lakini watu wengi hawajui" Dini hii iliyonyooka sawa, na hata kama wataijua, hawataifuata.
#
{31} {منيبينَ إليه واتَّقوه}: وهذا تفسيرٌ لإقامة الوجه للدين؛ فإنَّ الإنابةَ إنابةُ القلب وانجذابُ دواعيه لمراضي الله تعالى، ويلزم من ذلك عملُ البدن بمقتضى ما في القلب، فشمل ذلك العبادات الظاهرة والباطنة، ولا يتمُّ ذلك إلا بترك المعاصي الظاهرة والباطنة؛ فلذلك قال: {واتَّقوه}؛ فهذا يشملُ فعلَ المأمورات وتركَ المنهيات، وخصَّ من المأمورات الصلاةَ لكونها تدعو إلى الإنابة والتقوى لقوله تعالى: {وأقم الصلاةَ إنَّ الصَّلاةَ تَنْهى عن الفحشاءِ والمنكرِ}: فهذا إعانتها على التقوى، ثم قال: {وَلَذِكْرُ الله أكبرُ}: فهذا حثُّها على الإنابةِ. وخصَّ من المنهيَّات أصلَها، والذي لا يُقبل معه عملٌ، وهو الشركُ، فقال: {ولا تكونوا من المشركين}: لكونِ الشرك مضادًّا للإنابة التي رُوحها الإخلاصُ من كلِّ وجه.
{31} "Muwe wenye kutubia kwake, na mcheni Yeye" na hii ndiyo tafsiri ya kusimamisha Dini. Kwani toba ina maana ya moyo kutubia na kuvutiwa kwenye yale yanayompendeza Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na hilo linalazimu kwamba mwili utende kulingana na yale yaliyo moyoni, kwa hilo likajumuisha ibada zoye za dhahiri na za ndani, na wala hayo hayatimii isipkuwa kwa kuacha maasi ya dhahiri na ya ndani. Na ndiyo maana akasema, "Na mcheni Yeye" Hilo linajumuisha kufanya maamrisho na kuacha makatazo. Na alitaja katika maamrisho swala hasa kwa sababu inaitia kwenye toba na uchamungu, kwa mujibu wa maneno yake Mola Mtukufu, "na ushike Swala. Hakika Swala inazuilia mambo machafu na maovu." Na huku ndiko kumsaidia kwake juu ya uchamungu. Kisha akasema, "Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa" Na huku ndiko kumhimiza kwake juu ya kutubu. Na alitaja katika makatazo, katazo la msingi kabisa, ambalo tendo lolote halikubaliki pamoja nalo, nalo ni ushirikina. Akasema, "Na wala msiwe katika washirikina," kwa sababu ushirikina ni kinyume cha toba ambayo roho yake ni kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake kwa namna zote.
#
{32} ثم ذَكَرَ حالة المشركين مهجِّناً لها ومقبِّحاً، فقال: {من الذين فَرَّقوا دينَهم}: مع أنَّ الدين واحدٌ، وهو إخلاصُ العبادة لله وحدَه، وهؤلاء المشركون فرَّقوه: منهم من يعبدُ الأوثان والأصنام، ومنهم من يعبدُ الشمس والقمر، ومنهم من يعبدُ الأولياء والصالحين، ومنهم يهودٌ، ومنهم نصارى، ولهذا قال: {وكانوا شِيَعاً}؛ أي: كلُّ فرقةٍ من فرق الشرك تاهتْ وتعصَّبتْ على نصرِ ما معها من الباطل ومنابذةِ غيرِهِم ومحاربتِهم. {كلُّ حزبٍ بما لديهم}: من العلوم المخالفة لعلوم الرسل {فرِحونَ}: به يحكُمون لأنفسِهم بأنَّه الحقُّ وأنَّ غيرهم على باطل.
وفي هذا تحذيرٌ للمسلمين من تشتُّتهم وتفرُّقهم فرقاً، كلُّ فريق يتعصَّبُ لما معه من حقٍّ وباطلٍ، فيكونون مشابهين بذلك للمشركين في التفرُّق، بل الدين واحدٌ، والرسول واحدٌ، والإله واحدٌ، وأكثر الأمور الدينيَّة وقع فيها الإجماع بين العلماء والأئمَّة، والأخوَّة الإيمانيَّة قد عقدها الله وربَطَها أتمَّ ربط؛ فما بالُ ذلك كلِّه يُلغى ويُبنى التفرُّقُ والشقاقُ بين المسلمين على مسائل خفيَّةٍ أو فروع خلافيَّةٍ يضلِّلُ بها بعضُهم بعضاً ويتميَّز بها بعضُهم عن بعضٍ؟! فهل هذا إلاَّ من أكبر نزغات الشيطانِ وأعظم مقاصدِهِ التي كاد بها المسلمين؟! وهل السعي في جمع كلمتهم وإزالةِ ما بينَهم من الشقاق المبنيِّ على ذلك الأصل الباطل إلاَّ من أفضل الجهادِ في سبيل الله وأفضلِ الأعمال المقرِّبة إلى الله؟!
ولما أمر تعالى بالإنابة إليه، وكان المأمور بها هي الإنابة الاختيارية، التي تكون في حالِ العسر واليسر والسَّعة والضيق؛ ذكر الإنابة الاضطراريَّة التي لا تكون مع الإنسان إلاَّ عند ضيقِهِ وكربِهِ؛ فإذا زال عنه الضيق؛ نَبَذَها وراء ظهرِهِ، وهذه غيرُ نافعةٍ، فقال:
{32} Kisha akataja hali ya washirikina na kuonyesha uduni wake na ubaya wake. Akasema, "Katika wale ambao kwamba wameigawanya dini yao," ijapokuwa Dini ni moja, ambayo ni kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika ibada.
Na washirikina hawa waliigawanya: miongoni mwao wapo wanaoabudu masanamu, na miongoni mwao wapo wanaoabudu jua na mwezi, na miongoni mwao wapo wanaoabudu mawalii
(watu walio karibu na Mwenyezi Mungu) na watu wema, na miongoni mwao wapo Mayahudi, na miongoni mwao wapo Wakristo. Na ndiyo maana akasema, "Na wakawa makundi makundi." Yaani, kila kundi miongoni mwa washirikina wakapotea na wakawa washabiki katika kuunga mkono batili waliyo nayo, na kuwapinga wengineo na kuwapiga vita. "Kila kikundi kinafurahia kilicho nacho" cha elimu mbalimbali iliyo kinyume na elimu ya Mitume na kwayo wanajihukumu wenyewe kuwa hiyo ndiyo haki na kwamba wengineo wako katika batili. Na katika hilo kuna hatadharisho kwa Waislamu dhidi ya kutawanyika na kutengana makundi makundi, kila kundi likawa linatetea yale waliyo nayo ya haki na batili, kwa hivyo wakawa wamefanana na washirikina katika kugawanyika kwao. Bali Dini ni moja, Mtume ni mmoja, na Mwenyezi Mungu ni mmoja, na katika mambo mengi ya kidini kuna maafikiano baina ya wanachuoni na maimamu, na udugu wa kiimani ulikwisha wekwa na Mwenyezi Mungu na akaufunga vyema kabisa. Basi kwa nini yote haya yanafutwa na unajengwa mgawanyiko na fitina baina ya Waislamu juu ya mambo yaliyofichikana au masuala ya kimatawi yenye utata ambayo kwayo wao kwa wao wanaonana kwamba kila mmoja wao amepotea, na wanajitofautisha baadi yao kutoka kwa wengineo? Je, huu si isipokuwa uchochezi mkubwa wa Shetani na malengo yake makubwa zaidi ambayo kwayo anawapangia njama Waislamu? Je, kujitahidi kuunganisha neno lao na kuondoa tofauti hizi zilizo baina yao zilizojengeka juu ya msingi huo batili, si isipokuwa ndiyo jihadi bora zaidi katika njia ya Mwenyezi Mungu na matendo bora zaidi yanayomuweka mtu karibu na Mwenyezi Mungu? Na pale Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoamuru kutubia kwake, na kukawa kutubia huko ni kule kwa hiari, ambako kunakuwa katika hali ya shida, na urahisi, na wingi na dhiki, akataja kutubia kwa kulazimishwa ambako hutokea mtu isipokuwa wakati anapokuwa katika shida na dhiki. Na pindi dhiki hiyo inapomuondokea, anaitupa nyuma ya mgongo wake, lakini toba hii hainufaishi kitu.
Akasema:
{وَإِذَا مَسَّ النَّاسَ ضُرٌّ دَعَوْا رَبَّهُمْ مُنِيبِينَ إِلَيْهِ ثُمَّ إِذَا أَذَاقَهُمْ مِنْهُ رَحْمَةً إِذَا فَرِيقٌ مِنْهُمْ بِرَبِّهِمْ يُشْرِكُونَ (33) لِيَكْفُرُوا بِمَا آتَيْنَاهُمْ فَتَمَتَّعُوا فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ (34) أَمْ أَنْزَلْنَا عَلَيْهِمْ سُلْطَانًا فَهُوَ يَتَكَلَّمُ بِمَا كَانُوا بِهِ يُشْرِكُونَ (35)}.
33. Na watu wanapoguswa na madhara, humwomba Mola wao Mlezi huku wanatubu kwake. Kisha akiwaonjesha rehema itokayo kwake, mara kikundi miongoni mwao humshirikisha Mola wao Mlezi. 34. Kwa kuyakufuru yale tuliyowapa. Basi stareheni. Mtakuja jua! Au tumewateremshia hoja ambayo inazungumza juu ya kile walichokuwa wakishirikisha nacho?
#
{33 - 34} {وإذا مَسَّ الناسَ ضُرٌّ}: مرضٌ أو خوفٌ من هلاك ونحوه، {دَعَوْا ربَّهم منيبين إليه}: ونسوا ما كانوا به يشرِكون في تلك الحال؛ لعلمِهم أنَّه لا يكشفُ الضُّرَّ إلاَّ الله، فَـ {إذَا أذاقَهُم منه رحمةً}: شفاهم من مرضهم وآمَنَهم من خوفهم، {إذا فريقٌ منهم}: ينقُضون تلك الإنابةَ التي صدرت منهم، ويشرِكون به مَنْ لا دَفَعَ عنهم ولا أغنى ولا أفقر ولا أغنى، وكلُّ هذا كفرٌ بما آتاهم اللَّه ومنَّ به عليهم حيثُ أنجاهم وأنقَذَهم من الشدَّة وأزال عنهم المشقَّة؛ فهلاَّ قابلوا هذه النعمة الجليلة بالشُّكر والدوام على الإخلاص له في جميع الأحوال؟!
{33 - 34} "Na watu wanapoguswa na madhara," kama vile maradhi au hofu ya kuangamia na mengineyo, "humwomba Mola wao Mlezi huku wanatubu kwake." Na husahau yale waliyokuwa wakimshirikisha nayo katika hali hiyo, kwa sababu wanajua kwao hakuna anayeweza kuondoa madhara isipokuwa Mwenyezi Mungu. Basi "akiwaonjesha rehema itokayo kwake" kama vile kuwaponya maradhi yao na huwapa amani kutokana na hofu yao, "mara kikundi miongoni mwao" huivunjilia mbali toba hiyo waliyofanya, wakaanza tena kumshirikisha na wale wasio na hifadhi kwao, wala tajiri, masikini, wala tajiri, na yote haya ni kuyakufuru aliyowapa Mwenyezi Mungu na aliyowapa kwa kuwaokoa na kuwaepusha na dhiki na kuwaondolea taabu. Je, hawataitikia baraka hii kubwa kwa shukrani na kuendelea kuwa waaminifu kwake katika hali zote?
#
{35} {أم أنزَلْنا عليهم سلطاناً}؛ أي: حجَّة ظاهرةً، {فهو}؛ أي: ذلك السلطان {يتكلَّمُ بما كانوا به يشرِكون}: ويقول لهم: اثْبُتوا على شِرْكِكُم واستمرُّوا على شكِّكُم؛ فإنَّ ما أنتم عليه هو الحقُّ، وما دعتكم الرسلُ إليه باطل؛ فهل ذلك السلطان موجودٌ عندهم حتى يوجِبَ لهم شدَّة التمسُّك بالشرك؟ أم البراهين العقليَّة والسمعيَّة والكتب السماويَّة والرسل الكرام وسادات الأنام قد نَهَوْا أشدَّ النهي عن ذلك، وحذَّروا من سلوك طرقه الموصلة إليه، وحكموا بفساد عقل ودين من ارتكبه؟! فشركُ هؤلاء بغير حجَّة ولا برهانٍ، وإنَّما هو أهواء النُّفوس ونَزَغات الشيطانِ.
{35} "Au tumewateremshia hoja" iliyo dhahiri.
Basi hiyo" hoja "inazungumza juu ya kile walichokuwa wakishirikisha nacho?" Na inawaambia: Kuweni imara juu ya ushirikina wenu na endeleeni kuwa na shaka; kwani mliyo juu yake ndiyo Haki, na yale waliyowaitia Mitume ni batili. Basi je, wanayo hoja hiyo ambayo inawafanya kushikamana sawasawa na ushirikina? Ama ushahidi wa kiakili wote na wa kusikia, na vitabu vya mbinguni, na Mitume watukufu, na mabwana wa wanadamu, walikataza kabisa jambo hili, na wakatahadharisha juu ya kufuata njia zake zinazofikisha huko, na wakahukumu kuwa akili na dini ya mwenye kufanya hivyo ni mbovu? Basi ushirikina wa watu hawa hauna hoja yoyote wala uthibitisho, bali ni matamanio tu ya nafsi na uchochezi wa Shetani.
{وَإِذَا أَذَقْنَا النَّاسَ رَحْمَةً فَرِحُوا بِهَا وَإِنْ تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ إِذَا هُمْ يَقْنَطُونَ (36) أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّهَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَنْ يَشَاءُ وَيَقْدِرُ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ (37)}.
36. Na tunapowaonjesha watu rehema, huifurahia. Na ukiwasibu ubaya kwa iliyoyatanguliza mikono yao wenyewe, mara wanakata tamaa. 37. Kwani hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na humkunjia amtakaye? Hakika katika hayo, zipo Ishara kwa watu wanaoamini.
#
{36 - 37} يخبر تعالى عن طبيعة أكثر الناس في حال الرخاء والشدَّة أنَّهم إذا أذاقهم الله منه رحمةً من صحَّةٍ وغنى ونصرٍ ونحو ذلك؛ فرحوا بذلك فرحَ بَطَرٍ لا فرح شُكْرٍ وتبجُّح بنعمة الله. {وإنْ تُصِبْهم سيئةٌ}؛ أي: حالٌ تسوؤهم، وذلك {بما قدَّمت أيديهم}: من المعاصي، {إذا هم يَقْنَطون}: ييأسون من زوال ذلك الفقر والمرض ونحوه، وهذا جهلٌ منهم وعدم معرفة. {أوَلَمْ يرَوْا أنَّ الله يبسطُ الرزقَ لمن يشاء وَيَقْدِرُ}: فالقنوط بعدما علم أن الخير والشرَّ من الله والرزق سعته وضيقه من تقديره ضائعٌ ليس له محلٌّ؛ فلا تنظر أيُّها العاقل لمجرَّد الأسباب، بل اجعلْ نَظَرَكَ لمسبِّبها، ولهذا قال: {إنَّ في ذلك لآياتٍ لقوم يؤمنون}: فهم الذين يعتبِرونَ ببسطِ الله لِمَنْ يشاءُ وقَبْضِهِ، ويعرفون بذلك حكمة الله ورحْمته وجوده وجذب القلوب لسؤالِهِ في جميع مطالب الرزق.
{36 - 37} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu maumbile asili ya watu wengi katika nyakati za mafanikio na shida, kwamba Mwenyezi Mungu anapowaonjesha rehema kutoka kwake, kama vile afya njema, mali, ushindi, na mfano wake; wanayafurahia hayo kwa furaha ya kiburi, si furaha ya shukrani na kujivunia neema ya Mwenyezi Mungu. "Na ukiwasibu ubaya kwa iliyoyatanguliza mikono yao wenyewe," kama vile maasi, "mara wanakata tamaa" ya kuondoka kwa ufukara huo, maradhi na mengineyo. Na huu ndio ujinga wao, na kutojua. "Kwani hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na humkunjia amtakaye?" Kwa hivyo, halina mahali popote jambo la kukata tamaa baada ya kujua kwamba heri na shari zinatoka kwa Mwenyezi Mungu na kwamba riziki nyingi na chache ni katika mipango yake. Basi ewe mwenye akili usiangalie sababu za mambo tu, bali yaelekeze macho yako kwa aliyeyasababisha mambo hayo, na ndiyo maana akasema, "Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanaoamini." Hao ndio wanaozingatia kwamba Mwenyezi Mungu humkujulia amtakaye na kumkunjia amtakaye, na kwa hayo wanapata kujua hekima ya Mwenyezi Mungu, rehema yake, uwepo wake, na kuivutia mioyo kumwomba Yeye katika mahitaji yote ya riziki.
{فَآتِ ذَا الْقُرْبَى حَقَّهُ وَالْمِسْكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ ذَلِكَ خَيْرٌ لِلَّذِينَ يُرِيدُونَ وَجْهَ اللَّهِ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ (38) وَمَا آتَيْتُمْ مِنْ رِبًا لِيَرْبُوَ فِي أَمْوَالِ النَّاسِ فَلَا يَرْبُو عِنْدَ اللَّهِ وَمَا آتَيْتُمْ مِنْ زَكَاةٍ تُرِيدُونَ وَجْهَ اللَّهِ فَأُولَئِكَ هُمُ الْمُضْعِفُونَ (39)}.
38. Basi mpe jamaa haki yake, na masikini, na msafiri. Hayo ni heri kwa wanaotaka uso wa Mwenyezi Mungu. Na hao ndio waliofaulu. 39. Na mnachokitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Mwenyezi Mungu. Lakini mnachokitoa kwa Zaka kwa kutaka uso wa Mwenyezi Mungu, basi hao ndio watakaozidishiwa.
#
{38} أي: فأعطِ القريب منك ـ على حسب قربِهِ وحاجتِهِ ـ حقَّه الذي أوجبه الشارع أو حضَّ عليه من النفقةِ الواجبة والصدقةِ والهديَّة والبرِّ والسلام والإكرام والعفوِ عن زلَّته والمسامحة عن هفوتِهِ، وكذلك آتِ المسكين الذي أسْكَنَهُ الفقرُ والحاجةُ ما تُزيل به حاجَتَه وتدفعُ به ضرورتَه من إطعامه وسقيه وكسوتِهِ. {وابنَ السبيل}: الغريب المنقطع به في غير بلدِهِ، الذي في مظنَّة شدَّة الحاجة، وأنَّه لا مال معه ولا كسب قد دَبّر نفسَه به في سفره؛ بخلاف الذي في بلده؛ فإنَّه وإن لم يكن له مالٌ، لكن لا بدَّ في الغالب أن يكونَ في حرفةٍ أو صناعةٍ ونحوها تسدُّ حاجته، ولهذا جعل الله في الزَّكاة حصةً للمسكين وابن السبيل.
{ذلك}؛ أي: إيتاء ذي القربى والمسكين وابن السبيل: {خيرٌ للذين يريدون}: بذلك العمل {وَجْهَ الله}؛ أي: خير غزيرٌ وثوابٌ كثيرٌ؛ لأنَّه من أفضل الأعمال الصالحة، والنفعُ المتعدِّي الذي وافق محلَّه المَقْرونُ به الإخلاص؛ فإن لم يُرَدْ به وجهُ الله؛ لم يكن خيراً للمعطي، وإن كان خيراً ونفعاً للمعطى؛ كما قال تعالى: {لا خيرَ في كثير مِن نَجْواهم إلاَّ مَنْ أمر بصدقةٍ أو معروفٍ أو إصلاح بينَ الناس}: مفهومُها أنَّ هذه المستثنيات خيرٌ؛ لنفعها المتعدِّي، ولكن مَنْ يفعلُ ذلك ابتغاء مرضاة الله؛ فسوف نؤتيه أجراً عظيماً، وقوله: {وأولئك}: الذين عملوا هذه الأعمالَ وغيرَها لوجه الله، {هم المفلحون}: الفائزونَ بثواب الله الناجون من عقابه.
{38} Yaani, basi mpe jamaa yako wa karibu - kulingana na ukaribu wake na haja yake, - haki yake ambayo Mtunga sheria aliiwajibisha au alihimiza juu yake kama vile kutoa matumizi ya lazima, sadaka, zawadi, wema, salamu, ukarimu, kumsamehe dhambi zake, na kuachilia mbali kuteleza kwake. Na vile vile, mpe masikini aliyetulizwa na umasikini na mahitaji kitu ambacho utamuondolea mahitaji yake hayo na kumzuia kutokana na kuhitaji kwake huko. "Na msafiri" mgeni ambaye amekatikiwa hali ya kuwa yuko mbali na nchi yake, ambaye yuko katika hali inayodhaniwa sana kwamba yuko katika ugumu mkubwa, na kwamba hana mali wala mapato yenye kumkimu katika safari yake. Huyu ni tofauti na yule ambaye yuko katika nchi yake. Huyu hata kama hana mali, katika hali nyingi ni lazima anajishughulisha na kazi ya ufundi au sekta kama hiyo inayoweza kumkidhia mahitaji yake. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akaweka fungu maalumu la masikini na msafiri katika Zaka. "Hayo" ya kuwapa jamaa, masikini, na msafiri "ni heri kwa wanaotaka" kwa kitendo hicho "uso wa Mwenyezi Mungu." Yaani, heri nyingi na malipo mengi. Kwa sababu hayo ni miongoni mwa bora ya matendo mema, na yana manufaa yanayowafikia wengine ambayo yaliingia sawasawa mahali pake na ambayo yalifungamana na ikhlasi. Na ikiwa hakuutaka kwayo uso wa Mwenyezi Mungu; basi hayawezi kuwa ni heri kwa mtoaji, hata kama ni heri kwa anayepewa na yenye kumnufaisha, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Hakuna kheri katika mengi ya wanayoshauriana kwa siri, isipokuwa kwa yule anayeamrisha kutoa sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu." Na maana yake ya kinyume ni kuwa haya yaliyotolewa katika hukumu hii ni mema; kwa sababu ya manufaa yake yanayowafikia wengine, bali mtu afanyaye hayo kwa kutafuta uso wa Mwenyezi Mungu; basi tutakuja mpa ujira mkubwa. Na maneno yake, "Na hao" ambao walifanya vitendo hivi na mengineyo kwa ajili ya uso wa Mwenyezi Mungu, "ndio waliofaulu" watakaopata malipo mazuri ya Mwenyezi Mungu na wataokoka kutokana na adhabu yake.
#
{39} ولمَّا ذكر العمل الذي يُقْصَدُ به وجهُه من النفقات؛ ذكر العمل الذي يُقْصَدُ به مَقْصِدٌ دنيويٌّ، فقال: {وما آتيتُم من ربا لِيَرْبُوا في أموال الناس}؛ أي: ما أعطيتم من أموالكم الزائدة عن حوائجكم، وقصدُكم بذلك أن يَرْبُوَ؛ أي: يزيد في أموالكم؛ بأن تُعطوها لمن تطمعون أن يعاوِضكم عنها بأكثر منها؛ فهذا العمل لا يربو أجرُهُ عند الله؛ لكونه معدومُ الشرط الذي هو الإخلاص.
ومثل ذلك العملُ الذي يُراد به الزيادة في الجاه والرياء عند الناس؛ فهذا كلُّه لا يربو عند الله. {وما آتيتُم من زكاةٍ}؛ أي: مال يطهِّرِكم من الأخلاق الرَّذيلة، ويطهِّر أموالكم من البُخل بها، ويزيدُ في دفع حاجة المعطى؛ {تريدونَ}: بذلك {وجهَ الله فأولئك هم المُضْعِفونَ}؛ أي: المضاعَف لهم الأجر، الذين تربو نفقاتُهم عند الله، ويُربيها اللهُ لهم، حتى تكونَ شيئاً كثيراً، ودلَّ قولُه: {وما آتَيْتُم من زكاةٍ}: أنَّ الصدقة مع اضطرارِ من يَتَعَلَّق بالمنفق أو مع دَيْنٍ عليه لم يَقْضِهِ ويقدِّمُ عليه الصدقَة؛ أنَّ ذلك ليس بزكاةٍ يؤجَر عليه العبد، ويُرَدُّ تصرُّفُه شرعاً؛ كما قال تعالى في الذي يُمْدَحُ: {الذي يؤتي ماله يتزكَّى}؛ فليس مجردُ إيتاءِ المال خيراً، حتى يكون بهذه الصفة، وهو أن يكونَ على وجهٍ يَتَزَكَّى به المؤتي.
{39} Na alipotaja matendo yanayokusudiwa uso wake, kama vile kutoa kwa ajili ya matumizi; akataja matendo yanayokusudiwa mambo ya kidunia. Akasema, "Na mnachokitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu." Yaani, mlichotoa kutoka katika mali zenu zilizozidi mahitaji yenu, kwa nia ya kuifanya iongezeke, kwa njia ya kumpa mtu ili naye awarudishie kwa zaidi yake; basi malipo ya matendo haya hayaongezeki kwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu hayana sharti la hilo, ambalo ni ikhlasi. Na mfano wa hilo pia ni matendo yanayokusudiwa kuongeza hadhi ya mtu na kujionyesha kwa watu. Yote haya hayaongezeki kwa Mwenyezi Mungu. "Lakini mnachokitoa kwa Zaka" Yaani, mali itakayokutakaseni kutokana na tabia mbaya, itakayosafisha mali zenu kutokana na ubahili, na inaongeza kuzuia mahitaji ya anayepewa. "kwa kutaka" kwa hayo "uso wa Mwenyezi Mungu, basi hao ndio watakaozidishiwa" malipo, ambao walichotoa kwa ajili ya matumizi kitazidi kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu atakikuza mpaka kiwe kitu kikubwa. Na iliashiria kauli yake, "Lakini mnachokitoa kwa Zaka" kwamba kutoa sadaka pamoja na kuwepo na mwenye mahitaji makubwa katika wale walio chini ya yule anayetoa, au ikiwa mtoaji ana deni ambalo bado hajalilipa, naye akatanguliza sadaka mbele ya hayo; basi hiyo sio Zaka ambayo mja atalipwa juu yake. Kitendo chake hiki kinapaswa kuvunjiliwa mbali kwa mujibu wa sheria,
kama alivyosema Mwenyezi Mungu kuhusu mwenye kusifiwa: "Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa." Kwa hivyo, kutoa mali tu siyo heri, hadi kuwe kwa njia hii, ambayo ni kwa njia ambayo mtoaji anajitakasa.
{اللَّهُ الَّذِي خَلَقَكُمْ ثُمَّ رَزَقَكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ هَلْ مِنْ شُرَكَائِكُمْ مَنْ يَفْعَلُ مِنْ ذَلِكُمْ مِنْ شَيْءٍ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَى عَمَّا يُشْرِكُونَ (40)}.
40. Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaumba, kisha akawaruzuku, kisha atawafisha, na kisha atawafufua. Je, yupo yeyote katika hao mnaowashirikisha na Mwenyezi Mungu afanyae lolote katika hayo? Yeye ametakasika, na ametukuka mbali na hayo mnayomshirikisha naye.
#
{40} يخبر تعالى أنَّه وحده المنفرد بخلقكم ورزقكم وإماتتكم وإحيائكم، وأنه ليس أحدٌ من الشركاء التي يدعوها المشركون مَنْ يشارِكُ الله في شيءٍ من هذه الأشياء؛ فكيف يشرِكون بِمَنِ انفردَ بهذه الأمور من ليس له تصرُّفٌ فيها بوجهٍ من الوجوه؟ فسبحانَه وتعالى، وتقدَّس، وتنزَّه، وعلا عن شِرْكِهِم؛ فلا يضرُّه ذلك، وإنَّما وبالُه عليهم.
{40} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba Yeye peke yake ndiye aliyewaumba, naye ndiye anayewaruzuku, naye ndiye atakayewafisha na kuwahuisha, na kwamba hakuna yeyote katika washirika ambao washirikina wanawaomba anayeshirikiana na Mwenyezi Mungu katika chochote miongoni mwa mambo haya. Basi vipi wanaweza kumshirikiana yule ambaye yuko peke yake katika mambo haya na yule ambaye hana utendaji wowote kwa namna yoyote ile katika hayo? Ametakasika, ametukuka, na yuko juu zaidi ya ushirikina wao huu. Kwa hivyo, hilo halimdhuru kitu, bali msiba wake uko juu yao.
{ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُمْ بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ (41)}
41. Uharibifu umedhihiri barani na baharini kwa yale iliyoyafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonjeshe baadhi ya yale waliyoyatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu.
#
{41} أي: استعلن {الفسادُ في البرِّ والبحرِ}؛ أي: فساد معايشهم ونقصها وحلول الآفات بها وفي أنفسهم من الأمراض والوباء وغير ذلك، وذلك بسبب ما قدَّمَتْ أيديهم من الأعمال الفاسدةِ المفسدةِ بطبعها. هذه المذكورة، {لِيُذيقَهم بعضَ الذي عملوا}؛ أي: ليعلموا أنَّه المجازي على الأعمال، فعجَّل لهم نموذجاً من جزاء أعمالهم في الدنيا؛ {لعلَّهم يرجِعونَ}: عن أعمالهم التي أثَّرت لهم من الفساد ما أثَّرت، فتَصْلُحُ أحوالُهم، ويستقيمُ أمرُهم؛ فسبحان من أنعم ببلائِهِ، وتفضَّلَ بعقوبتِهِ، وإلاَّ؛ فلو أذاقهم جميعَ ما كسبوا؛ ما ترك على ظهرِها من دابَّةٍ.
{41} Yaani, umekuwa wazi wazi "Uharibifu barani na baharini" katika maisha yao, na kuna upungufu ndani yake, na umeingiwa na balaa mbalimbali, na kuna magonjwa na mlipuko wa majanga na mambo mengineyo katika nafsi zao. Hayo ni kutokana na yale yaliyotangulizwa na mikono yao ya matendo mabovu yenye kuharibu maumbile yao. Hayo yaliyotajwa "ili Mwenyezi Mungu awaonjeshe baadhi ya yale waliyoyatenda." Yaani, ili wajue kwamba Yeye ndiye mlipaji wa matendo, basi akawafanyia haraka mfano wa malipo ya matendo yao hapa duniani. "Huenda wakarejea kwa kutubu" kutokana na vitendo vyao vilivyowasababishia uharibifu mwingi namna vilivyosababisha, basi hali zao zikaboreshwa, na mambo yao yakanyooka. Ametakasika yule aliyetia neema katika dhiki yake, na akaweka fadhila katika adhabu yake. Sivyo, ikiwa angewaonjesha yote waliyoyachuma, basi hangeacha mnyama yeyote juu ya mgongo wake.
{قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانْظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِنْ قَبْلُ كَانَ أَكْثَرُهُمْ مُشْرِكِينَ (42)}
42.
Sema: Safirini duniani na muangalie ulikuwaje mwisho wa wale waliotangulia. Wengi wao walikuwa washirikina.
#
{42} والأمر بالسير في الأرض يدخُلُ فيه السير بالأبدان والسيرُ في القلوب للنظر والتأمُّل بعواقب المتقدِّمين، {كان أكثرُهُم مشركينَ}: تجِدون عاقِبَتَهم شرَّ العواقب، ومآلهم شرَّ مآلٍ: عذابٌ استأصلهم، وذمٌّ، ولعنٌ من خَلْق الله يتبعهم، وخزيٌ متواصلٌ؛ فاحذروا أن تفعلوا أفعالهم؛ يُحذى بكم حَذْوَهم؛ فإنَّ عدل الله وحكمته في كل زمان ومكان.
{42} Na amri ya kutembea katika ardhi inajumuisha kutembea kwa miili na kutembea katika nyoyo ili kuangalia na kutafakari mwisho wa wale waliotangulia, "Wengi wao walikuwa washirikina" na utapata kwamba mwisho wao ulikuwa mwisho mbaya zaidi, ambayo yalikuwa adhabu ambayo iliwaangamiza, na kufuatwa na shutuma na laana kutoka kwa viumbe vya Mwenyezi Mungu, na fedheha inayoendelea. Kwa hivyo jitahadharini msifanye matendo yao; mkaja fanyiwa mfano wa walivyofanyiwa; kwani, uadilifu wa Mwenyezi Mungu na hekima yake iko katika kila wakati na mahali.
{فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ الْقَيِّمِ مِنْ قَبْلِ أَنْ يَأْتِيَ يَوْمٌ لَا مَرَدَّ لَهُ مِنَ اللَّهِ يَوْمَئِذٍ يَصَّدَّعُونَ (43) مَنْ كَفَرَ فَعَلَيْهِ كُفْرُهُ وَمَنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِأَنْفُسِهِمْ يَمْهَدُونَ (44) لِيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْ فَضْلِهِ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْكَافِرِينَ (45)}
43. Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini iliyonyooka kabla ya kufika Siku hiyo isiyozuilika, inayotoka kwa Mwenyezi Mungu. Siku hiyo watu watatengana. 44. Anayekufuru, basi ukafiri wake utakuwa juu yake mwenyewe. Na anayetenda mema, basi wanazitengezea nafsi zao. 45. Ili awalipe wale walioamini na wakatenda mema kutokana na fadhila yake. Hakika Yeye hawapendi makafiri.
#
{43} أي: أقبل بقلبك وتوجَّه بوجهِك، واسْعَ ببدنِك لإقامة الدين القيِّم المستقيم، فنفِّذْ أوامره ونواهيه بجدٍّ واجتهاد، وقمْ بوظائفِهِ الظاهرة والباطنة، وبادِرْ زمانك وحياتك وشبابك، {من قبلِ أن يأتيَ يومٌ لا مردَّ له من الله}: وهو يوم القيامةِ، الذي إذا جاء؛ لا يمكنُ ردُّه، ولا يُرجأ العاملون ليستأنفوا العمل، بل فُرِغَ من الأعمال، ولم يبقَ إلاَّ جزاءُ العمال. {يومئذٍ يَصَّدَّعون}؛ أي: يتفرَّقون عن ذلك اليوم، ويصدُرون أشتاتاً متفاوتين؛ لِيُرَوْا أعمالهم.
{43} Yaani, njoo kwa moyo wako na uelekeze uso wako, na jitahidi kwa mwili wako kusimamisha Dini iliyo sawasawa, iliyonyooka, kwa kutekeleza maamrisho yake na makatazo yake kwa bidii na jitihada, na tekeleza mambo yake ya dhahiri na ya siri, na uharakishe kutumia vyema wakati wako, maisha yako, na ujana wako, "kabla ya kufika Siku hiyo isiyozuilika, inayotoka kwa Mwenyezi Mungu," ambayo ni Siku ya Kiyama, ambayo inapokuja, haiwezekani kuirejesha, na wala watendaji hawawezi kuahirishwa ili waendelee kutenda matendo, bali matendo yalishaisha, na hakikubakia isipokuwa kuwalipa watendaji. "Siku hiyo watu watatengana," na watakuja wakiwa mbalimbali huku wametofautiana ili waonyeshwe matendo yao.
#
{44 - 45} فَـ {مَنْ كفر}: منهم، {فعليه كفرُهُ}: ويعاقَب هو بنفسِهِ، لا تزِرُ وازرةٌ وزرَ أخرى، {ومن عَمِلَ صالحاً}: من الحقوق التي لله والتي للعباد الواجبة والمستحبَّة {فلأنفسِهِم}: لا لغيرهم؛ {يَمْهَدونَ}؛ أي: يهيِّئون، ولأنفسهم يعمرون آخرتهم، ويستعدُّون للفوز بمنازلها وغرفاتها، ومع ذلك جزاؤهم ليس مقصوراً على أعمالهم، بل يجزيهم الله من فضلِهِ الممدود وكرمِهِ غير المحدود ما لا تبلغُهُ أعمالُهم، وذلك لأنَّه أحبَّهم، وإذا أحبَّ الله عبداً؛ صبَّ عليه الإحسان صبًّا، وأجزل له العطايا الفاخرةَ، وأنعم عليه بالنعم الظاهرة والباطنة، وهذا بخلاف الكافرين؛ فإنَّ الله لمَّا أبغضَهم ومقَتَهم؛ عاقَبَهم وعذَّبهم، ولم يَزِدْهم كما زاد من قبلهم؛ فلهذا قال: {إنَّه لا يحبُّ الكافرين}.
{44 - 45} Basi "anayekufuru" miongoni mwao, "basi ukafiri wake utakuwa juu yake mwenyewe," naye mwenyewe ndiye atakayeadhibiwa, na wala hatabeba mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe. "Na anayetenda mema" miongoni mwa haki za Mwenyezi Mungu, na za waja ambazo ni za wajibu, na zinazopendekezwa, "basi wanazitengezea nafsi zao." Si kwa ajili ya mwingine, na ni akhera yao ambayo wanaiimarisha, na wanajitayarishia kufikia nyumba zake na vyumba vyake, na pamoja na hayo, malipo yao hayatakomea tu kwenye matendo yao, bali Mwenyezi Mungu atawalipa kutokana na fadhila zake kunjufu, na ukarimu wake usio na mipaka malipo ambayo matendo yao hayawezi kufikia. Hayo ni kwa sababu Yeye aliwapenda, na Mwenyezi Mungu anapompenda mja, hummiminia wema wake kwa wingi, na humpa vipawa vya kifahari, na anamneemesha kwa neema za dhahiri na zilizofichika. Na hili ni kinyume na makafiri, hao Mwenyezi alipowachukia mno, akawaadhibu na kuwatesa, lakini hakuwazidishia kama alivyowazidishia wale wa kabla yao. Ndiyo maana akasema, "Hakika Yeye hawapendi makafiri."
{وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ يُرْسِلَ الرِّيَاحَ مُبَشِّرَاتٍ وَلِيُذِيقَكُمْ مِنْ رَحْمَتِهِ وَلِتَجْرِيَ الْفُلْكُ بِأَمْرِهِ وَلِتَبْتَغُوا مِنْ فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ (46)}
46. Na katika Ishara zake ni kuzituma pepo ziletazo bishara njema, na ili kuwaonjesha baadhi ya rehema zake, na ili majahazi yaende kwa amri yake; na mtafute kutokana na fadhila yake, na ili mumshukuru.
#
{46} أي: ومن الأدلَّة الدالَّة على رحمته وبعثِهِ الموتى وأنَّه الإله المعبود والملك المحمود، أن أرسل {الرياحَ}: أمام المطر {مبشراتٍ}: بإثارتها للسحاب ثم جمعِها، فتبشر بذلك النفوس قبل نزوله، {ولِيذيقَكم من رحمتِهِ}: فَيُنْزِلَ عليكم مطراً تحيا به البلادُ والعبادُ وتذوقون من رحمتِهِ ما تعرِفون أنَّ رحمته هي المنقذة للعباد الجالبة لأرزاقهم، فتشتاقون إلى الإكثار من الأعمال الصالحة الفاتحة لخزائن الرحمة، {ولِتَجْرِيَ الفلكُ}: في البحر {بأمرِهِ}: القدريِّ، {ولِتَبْتَغوا من فضلِهِ}: بالتصرُّفِ في معايشكم ومصالحكم. {ولعلَّكُم تشكُرونَ}: مَنْ سخَّر لكم الأسباب، ويَسَّرَ لكم الأمور؛ فهذا المقصود من النعم أنْ تقابَلَ بشكر الله تعالى؛ ليزيدَكم الله منها، ويبقيَها عليكم، وأمَّا مقابلة النعم بالكفرِ والمعاصي؛ فهذه حالُ من بدَّل نعمة الله كفراً، ونعمته محنةً، وهو معرَّضٌ لها للزوال والانتقال منه إلى غيره.
{46} Yaani, miongoni mwa ishara zinazoonyesha rehema yake na kuwafufuwa kwake wafu, na kwamba Yeye ndiye Mola Mlezi anayeabudiwa na Mfalme Msifiwa, ni kuzituma pepo mbele ya mvua "ziletazo bishara njema" kwa kuyatimua mawingu na kuyakusanya, kwa hivyo zikazibashiria nafsi kwa hilo kabla ya kunyesha kwake "na ili kuwaonjesha baadhi ya rehema zake" Basi akawateremshia mvua ambayo kwayo nchi na waja vinakuwa hai, na mnaonja katika rehema yake kile mnachojua kwacho kwamba rehema yake ndiyo inayowaokoa waja na kuwaletea riziki, basi mkawa na shauku kubwa ya kuzidisha matendo mema yenye kufungua hazina za rehema. "na ili majahazi yaende" baharini "kwa amri yake" ya kimajaliwa, "na mtafute kutokana na fadhila yake" kwa kujishughulisha na maisha yenu na mambo yenye masilahi kwenu. "na ili mumshukuru" aliyewatiishia njia za hayo na akawarahisishia mambo. Na hilo ndilo linalokusudiwa katika neema, kwamba mtu amshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, ili awazidishie katika hizo neema, na azidumishe. Ama kuzikabili neema za Mwenyezi Mungu kwa kukufuru na kufanya maasi, hii ndiyo hali ya mwenye kubadilisha neema za Mwenyezi Mungu kwa ukafiri, na mtihani, na huyo anataka kusababisha neema hiyo kuondoka na kuhama kutoka kwake kwenda kwa mtu mwingine.
{وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِنْ قَبْلِكَ رُسُلًا إِلَى قَوْمِهِمْ فَجَاءُوهُمْ بِالْبَيِّنَاتِ فَانْتَقَمْنَا مِنَ الَّذِينَ أَجْرَمُوا وَكَانَ حَقًّا عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ (47)}.
47. Na hakika tulikwisha watuma Mitume kabla yako kwa kaumu zao, na wakawajia kwa hoja zilizo wazi. Tukawaadhibu wale waliofanya uhalifu. Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini.
#
{47} أي: {ولقد أرْسَلْنا من قبلِكَ}: في الأمم السالفين {رسلاً إلى قومهم}: حين جَحَدوا توحيدَ الله وكذَّبوا بالحقِّ، فجاءتهم رسلُهم يدعونَهم إلى التوحيد والإخلاص والتصديق بالحقِّ وبطلان ما هم عليه من الكفر والضَّلال، وجاؤوهم بالبينات والأدلَّة على ذلك، فلم يؤمِنوا ولم يزولوا عن غيهم، {فانتَقَمْنا من الذين أجْرَموا}: ونصرنا المؤمنينَ أتباع الرسل، {وكان حقًّا علينا نصرُ المؤمنين}؛ أي: أوجَبْنا ذلك على أنفسنا، وجعلْناه من جملةِ الحقوقِ المتعيِّنة، ووعدناهم به؛ فلا بدَّ من وقوعِهِ، فأنتُم أيُّها المكذِّبون لمحمدٍ - صلى الله عليه وسلم - إنْ بقيتُم على تكذيبكم؛ حلَّتْ بكم العقوبةُ، ونصرناه عليكم.
{47} Yaani, "Na hakika tulikwisha watuma Mitume kabla yako" miongoni mwa mataifa yaliyotangulia "kwa kaumu zao." Walipokataa kumpwekesha Mwenyezi Mungu na wakaikadhibisha haki, kwa hivyo Mitume wao wakawajia wakiwalingania kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na kumkusudia Yeye tu, na kuisadiki haki na kubatilisha yale wanayoyaamini na kutenda ya ukafiri na upotovu, na waliwajia na hoja za wazi na ushahidi wa hayo, lakini hawakuamini na hawakuachana na upotofu wao, "kwa hivyo, tukawaadhibu wale waliofanya uhalifu" na tukawanusuru waumini, wafuasi wa Mitume, "Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini." Yaani, tulijiwajibishia hilo juu yetu wenyewe, na tukalifanya kuwa moja ya haki zinazopasa kuzitekeleza, na tukawaahidi hilo; na lazima litokee. Basi enyi mnaomkadhibisha Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ikiwa mtaendelea kukadhibisha; mtapatwa na adhabu, na tutamnusuru yeye juu yenu.
{اللَّهُ الَّذِي يُرْسِلُ الرِّيَاحَ فَتُثِيرُ سَحَابًا فَيَبْسُطُهُ فِي السَّمَاءِ كَيْفَ يَشَاءُ وَيَجْعَلُهُ كِسَفًا فَتَرَى الْوَدْقَ يَخْرُجُ مِنْ خِلَالِهِ فَإِذَا أَصَابَ بِهِ مَنْ يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ إِذَا هُمْ يَسْتَبْشِرُونَ (48) وَإِنْ كَانُوا مِنْ قَبْلِ أَنْ يُنَزَّلَ عَلَيْهِمْ مِنْ قَبْلِهِ لَمُبْلِسِينَ (49) فَانْظُرْ إِلَى آثَارِ رَحْمَتِ اللَّهِ كَيْفَ يُحْيِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا إِنَّ ذَلِكَ لَمُحْيِ الْمَوْتَى وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (50)}.
48. Mwenyezi Mungu ndiye anayezituma pepo zikayatimua mawingu, kisha akayatandaza mbinguni kama apendavyo. Na akayafanya mapande mapande, basi ukaiona mvua inatoka ndani yake. Anapowafikishia awatakao katika waja wake, mara hao huwa na furaha. 49. Na ingawa kabla ya kuteremshiwa walikuwa wenye kukata tamaa. 50. Basi ziangalie athari za rehema ya Mwenyezi Mungu, jinsi anavyoihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Basi hakika huyo ndiye bila ya shaka mwenye kuhuisha wafu. Na Yeye ni Muweza wa kila kitu.
#
{48 - 49} يخبر تعالى عن كمال قدرته وتمام نعمته أنَّه {يرسلُ الرياح فتثير سحاباً}: من الأرض، {فيَبْسُطُه في السماء}؛ أي: يمدُّه ويوسِّعه {كيف يشاءُ}؛ أي: على أيِّ حالة أرادها من ذلك، {ثم يجعلُه}؛ أي: ذلك السحاب الواسع {كِسَفاً}؛ أي: سحاباً ثخيناً قد طبَّق بعضَه فوق بعض. {فترى الوَدْقَ يخرُجُ من خلالِهِ}؛ أي: السحاب؛ نقطاً صغاراً متفرِّقة، لا تنزل جميعاً فتُفْسِدُ ما أتت عليه، {فإذا أصابَ}؛ أي: بذلك المطر مَنْ {يشاءُ من عبادِهِ إذا هم يستبشرون}: يبشِّر بعضهم بعضاً بنزوله، وذلك لشدَّة حاجتهم وضرورتهم إليه؛ فلهذا قال: {وإن كانوا مِن قبلِ أن يُنَزَّلَ عليهم من قبلِهِ لَمُبْلِسينَ}؛ أي: آيِسين قانطين لتأخُّر وقت مجيئه؛ أي: فلما نزل في تلك الحال؛ صار له موقعٌ عظيم عندهم وفرحٌ واستبشارٌ.
{48 - 49} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu ukamilifu wa uwezo wake na utimilifu wa neema yake kwamba, "huzituma pepo zikayatimua mawingu" kutoka ardhini, "kisha akayatandaza mbinguni kama apendavyo. Na akayafanya mapande mapande" yaliyopandana juu kwa juu. "Basi ukaiona mvua inatoka ndani yake," kwa namna ya matone madogo yaliyotawanyika, na hayateremki maji hayo yote pamoja yakaharibu chochote yanachokifikia. "Anapowafikishia awatakao katika waja wake, mara hao huwa na furaha," wakibashiriana wao kwa wao juu ya kunyesha kwake. Na hilo ni kwa sababu ya mahitaji yao na haja yao kubwa juu yake. Ndiyo maana akasema, "Na ingawa kabla ya kuteremshiwa walikuwa wenye kukata tamaa," kwa sababu ya kuchelewa kwa wakati wa kuja kwake. Na iliponyesha katika hali hiyo, ikawa ina nafasi kubwa sana kwao, na furaha na kuwa na bishara nzuri kwao.
#
{50} {فانظر إلى آثارِ رحمةِ الله كيف يُحيي الأرضَ بعد موتها}: فاهتزَّتْ ورَبَتْ وأنبتتْ من كلِّ زوج كريم. {إنَّ ذلك}: الذي أحيا الأرض بعد موتها {لَمُحْيي الموتى وهو على كلِّ شيءٍ قديرٌ}: فقدرتُه تعالى لا يتعاصى عليها شيءٌ، وإن تعاصى على قَدْرِ خَلْقِهِ، ودقَّ عن أفهامهم، وحارت فيه عقولهم.
{50} "Basi ziangalie athari za rehema ya Mwenyezi Mungu, jinsi anavyoihuisha ardhi baada ya kufa kwake," ikasisimka na kututumka, na kuotesha kila namna ya mimea mizuri. "Basi hakika huyo" ambaye aliihuisha ardhi baada ya kufa kwake, "ndiye bila ya shaka mwenye kuhuisha wafu. Na Yeye ni Muweza wa kila kitu." Uwezo wake, Mola Mtukufu, haupingwi na kitu chochote, hata kama ni vigumu mno kwa viumbe wake, na ikawashinda kabisa kuingia katika ufahamu wao, na akili zao zikachanganyikiwa juu yake.
{وَلَئِنْ أَرْسَلْنَا رِيحًا فَرَأَوْهُ مُصْفَرًّا لَظَلُّوا مِنْ بَعْدِهِ يَكْفُرُونَ (51) فَإِنَّكَ لَا تُسْمِعُ الْمَوْتَى وَلَا تُسْمِعُ الصُّمَّ الدُّعَاءَ إِذَا وَلَّوْا مُدْبِرِينَ (52) وَمَا أَنْتَ بِهَادِ الْعُمْيِ عَنْ ضَلَالَتِهِمْ إِنْ تُسْمِعُ إِلَّا مَنْ يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا فَهُمْ مُسْلِمُونَ (53)}
51. Na tungeutuma upepo na wakauona umekuwa rangi ya manjano, juu ya hayo wangeendelea kukufuru. 52. Kwani wewe hakika huwafanyi maiti wakasikia, wala viziwi wakasikia wito wakishageuka kukupa mgongo. 53. Wala wewe huwaongoi vipofu kutoka katika upotovu wao. Huwasikilizishi isipokuwa wale wanaoziamini Aya zetu. Hao ndio Waislamu, walionyenyekea.
#
{51} يخبر تعالى عن حالة الخَلْق وأنَّهم مع هذه النعم عليهم بإحياء الأرض بعد موتها ونشرِ رحمةِ الله تعالى: لو أرسَلْنا على هذا النبات الناشئ عن المطرِ وعلى زُروعهم ريحاً مضرَّةً متلفةً أو منقصةً، {فرأوْهُ مُصفرًّا}: قد تداعى إلى التلف، {لَظَلُّوا من بعدِهِ يكفُرون}: فينسَوْن النعم الماضية، ويبادِرون إلى الكفر! وهؤلاء لا ينفع فيهم وعظٌ ولا زجرٌ.
{51} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu hali ya viumbe na kwamba pamoja na kupewa neema hizi kama vile; kuifufua ardhi baada ya kufa kwake na kueneza rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: kama tungeliuteremshia mmea huu unaotokana na mvua na juu ya mimea yao upepo wenye madhara, wenye kuharibu au kupunguza, "wakauona umekuwa rangi ya manjano" tayari umekaribia kuharibika, "juu ya hayo wangeendelea kukufuru" na wakasahau neema zilizopita na wakakimbilia kufuru! Hawa hayawafai mawaidha wala kukemewa.
#
{52} {فإنَّك لا تُسْمِعُ الموتى ولا تُسْمِعُ الصُّمَّ الدُّعاء}: وبالأولى: {إذا وَلَّوْا مُدْبِرينَ}: فإنَّ الموانع قد توفَّرت فيهم عن الانقياد والسماع النافع كتوفُّر هذه الموانع المذكورة عن سماع الصوتِ الحسيِّ.
{52} "Kwani wewe hakika huwafanyi maiti wakasikia, wala viziwi wakasikia wito" na katika hali inayofailia zaidi "wakishageuka kukupa mgongo." Kwani vizuizi vimeshapatikana kwao vinavyowazuia kufuata na kusikia kwenye manufaa, kama vile kuwepo kwa vizuizi hivi vilivyotajwa hapo juu vinavyozuia kusikia sauti ya kihisia.
#
{53} {وما أنت بهادِ العُمْيِ عن ضلالَتِهِم}: لأنَّهم لا يقبلون الإبصارَ بسبب عَماهم؛ فليس فيهم قابليَّةٌ له. {إن تُسْمِعُ إلاَّ مَن يؤمنُ بآياتنا فهم مسلمونَ}: فهؤلاء الذين ينفعُ فيهم إسماعُ الهدى، المؤمنون بآياتنا بقلوبهم، المنقادون لأوامرنا، المسلمون لنا؛ لأنَّ معهم الداعي القويَّ لقَبول النصائح والمواعظ، وهو استعدادُهم للإيمان بكلِّ آيةٍ من آيات الله، واستعدادُهم لتنفيذ ما يقدِرون عليه من أوامرِ الله ونواهيه.
{53} "Wala wewe huwaongoi vipofu kutoka katika upotovu wao" kwa sababu hawakubali kuonyeshwa kwa sababu ya upofu wao. Hawana uwezo wowote wa kufanya hilo. "Huwasikilizishi isipokuwa wale wanaoziamini Aya zetu. Hao ndio Waislamu, walionyenyekea." Hao ndio wanaonufaika na kusikiliza uwongofu, ndio wanaoziamini Ishara zetu kwa nyoyo zao, na wanaofuata amri zetu, na wanaojisalimisha kwetu; Kwa sababu wana sababu kubwa sana inayowafanya kukubali nasaha na mawaidha, nayo ni utayari wao wa kuamini kila ishara ya Mwenyezi Mungu, na utayari wao wa kutekeleza amri na makatazo yoyote ya Mwenyezi Mungu wanayoweza kuyafanya.
{اللَّهُ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ ضَعْفٍ ثُمَّ جَعَلَ مِنْ بَعْدِ ضَعْفٍ قُوَّةً ثُمَّ جَعَلَ مِنْ بَعْدِ قُوَّةٍ ضَعْفًا وَشَيْبَةً يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ وَهُوَ الْعَلِيمُ الْقَدِيرُ (54)}
54. Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaumba kutokana na udhaifu, kisha akajaalia nguvu baada ya unyonge, kisha akajaalia baada ya nguvu unyonge tena na ukongwe. Anaumba atakavyo. Naye ndiye ajuaye zaidi, Mwenye uweza wote.
#
{54} يخبر تعالى عن سعةِ علمِهِ وعظيم اقتدارِهِ وكمال حكمتِهِ؛ أنَّه ابتدأ خَلْقَ الآدميين من ضَعْفٍ، وهو الأطوارُ الأولى من خلقِهِ من نطفةٍ إلى علقةٍ إلى مضغةٍ إلى أنْ صار حيواناً في الأرحام إلى أن وُلِدَ وهو في سنِّ الطُّفولية، وهو إذْ ذاك في غاية الضعفِ وعدم القوَّة والقدرة، ثمَّ ما زال الله يزيدُ في قوَّته شيئاً فشيئاً، حتى بلغ سنَّ الشبابَ، واستوتْ قوَّتُه، وكملتْ قواه الظاهرةُ والباطنةُ، ثم انتقل من هذا الطورِ ورجع إلى الضعف والشيبةِ والهرم. {يَخْلُقُ ما يشاءُ}: بحسب حكمتِهِ، ومن حكمتِهِ أن يُريَ العبدَ ضعفَه، وأنَّ قوَّتَه محفوفةٌ بضعفين، وأنَّه ليس له من نفسه إلا النقصُ، ولولا تقويةُ الله له؛ لما وصل إلى قوَّة وقدرة، ولو استمرَّتْ قوتُه في الزيادة؛ لطغى وبغى وعتا، وليعلم العبادُ كمالَ قدرةِ الله، التي لا تزال مستمرَّةً؛ يخلق بها الأشياء، ويدبِّر بها الأمورَ، ولا يلحقُها إعياءٌ ولا ضعفٌ ولا نقصٌ بوجه من الوجوه.
{54} Mungu Mwenyezi anajulisha juu ya upana wa elimu yake, ukuu wa uwezo wake, na ukamilifu wa hekima yake, kwamba alianzisha uumbaji wa wanadamu kutokana na udhaifu, ambao ni awamu za kwanza za kuumbwa kwake kutokana na manii hadi kwenya pande la damu hadi kwenye pande la nyama hadi akawa mnyama ndani ya matumbo ya uzazi hadi akazaliwa katika umri wa utoto, na wakati huo alikuwa dhaifu sana bila ya kuwa na nguvu na uwezo. Kisha Mwenyezi Mungu akaendelea kuongeza nguvu zake kidogo kidogo, hadi akafikia umri wa ujana, na nguvu zake zikawa sawasawa, basi nguvu zake za dhahiri na zilizofichwa zikakamilika. Kisha akatoka katika awamu hii na akarudi kuwa dhaifu, akawa mzee mkongwe. "Anaumba atakavyo" kulingana na hekima yake. Na katika hekima yake ni kwamba anamuonyesha mja udhaifu wake, na kwamba nguvu zake zimezungukwa na madhaifu mawili, na kwamba hana chochote kutokana na nafsi yake isipokuwa upungufu, na lau si kwa sababu ya Mwenyezi Mungu kumtia nguvu, asingepata nguvu na uwezo, na kama nguvu zake zingeendelea kuongezeka, basi angevuka mipaka na akaasi sana, na ili mja ajue ukamilifu wa nguvu za Mwenyezi Mungu, ambazo bado zinaendelea. Anaumba kwazo vitu, na anaendesha kwazo mambo, na wala haziathiriwi na uchovu, wala udhaifu, wala upungufu kwa njia yoyote ile.
{وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يُقْسِمُ الْمُجْرِمُونَ مَا لَبِثُوا غَيْرَ سَاعَةٍ كَذَلِكَ كَانُوا يُؤْفَكُونَ (55) وَقَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ وَالْإِيمَانَ لَقَدْ لَبِثْتُمْ فِي كِتَابِ اللَّهِ إِلَى يَوْمِ الْبَعْثِ فَهَذَا يَوْمُ الْبَعْثِ وَلَكِنَّكُمْ كُنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ (56) فَيَوْمَئِذٍ لَا يَنْفَعُ الَّذِينَ ظَلَمُوا مَعْذِرَتُهُمْ وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ (57)}
55. Na siku itakaposimama Saa ya Kiyama, wahalifu wataapa kwamba hawakukaa duniani isipokuwa saa moja tu. Hivyo ndivyo walivyokuwa wakipotoshwa. 56.
Na wale waliopewa elimu na Imani watasema: Hakika nyinyi mlikwisha kaa katika hukumu ya Mwenyezi Mungu mpaka Siku ya kufufuliwa. Basi hii ndiyo Siku ya kufufuliwa! Lakini nyinyi mlikuwa hamuijui. 57. Basi Siku hiyo hautawafaa wale waliodhulumu udhuru wao, wala haitatakiwa toba yao.
#
{55} يخبر تعالى عن يوم القيامةِ وسرعةِ مجيئه، وأنَّه إذا قامت الساعةُ؛ أقسم {المجرمونَ}: بالله أنهم {ما لَبِثوا}: في الدُّنيا {إلاَّ ساعةً}، وذلك اعتذارٌ منهم؛ لعلَّه ينفعُهم العذر، واستقصارٌ لمدَّة الدنيا. ولمَّا كان قولُهم كذباً لا حقيقةَ له؛ قال تعالى: {كذلك كانوا يُؤْفَكون}؛ أي: ما زالوا وهم في الدنيا يؤفَكون عن الحقائق ويأتَفِكون الكذبَ؛ ففي الدُّنيا كذَّبوا الحقَّ الذي جاءت به المرسلون، وفي الآخرة أنكَروا الأمرَ المحسوس، وهو اللبثُ الطويلُ في الدنيا؛ فهذا خُلُقهم القبيح، والعبدُ يُبْعَثُ على ما مات عليه.
{55} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu Siku ya Kiyama na upesi wa kuja kwake, na kwamba itakapofika Saa, "wahalifu" wataapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba "hawakukaa duniani isipokuwa saa moja tu." Watafanya hivyo, ili wakubaliwe udhuru labda udhuru huo uwafae, na kwamba muda wa maisha ya dunia ulikuwa mfupi. Na kwa vile kauli yao hiyo ni uongo na haina uhakika wowote. Yeye Mtukufu akasema, "Hivyo ndivyo walivyokuwa wakipotoshwa" walipokuwa duniani, wakaiacha haki waliyokuja nayo Mitume. Na katika Akhera walikataa jambo linalohisiwa ambalo ni kukaa kwa muda mrefu katika dunia hii. Hii ndiyo tabia yao mbaya, na mja atafufuliwa katika hali aliyofia.
#
{56} {وقال الذين أوتوا العلم والإيمانَ}؛ أي: منَّ اللهُ عليهم بهما، وصارا وصفاً لهم، العلم بالحق والإيمان المستلزمُ إيثار الحقِّ، وإذا كانوا عالمينَ بالحقِّ، مؤثرين له؛ لزمَ أن يكونَ قولُهم مطابقاً للواقع مناسباً لأحوالهم؛ فلهذا قالوا الحقَّ: {لقدْ لَبِثْتُم في كتاب الله}؛ أي: في قضائِهِ وقدرِهِ الذي كتبه الله عليكم وفي حكمه {إلى يوم البعثِ}؛ أي: عُمرتم عمراً يتذكَّر فيه المتذكِّر، ويتدبَّر فيه المتدبِّر ويعتبر فيه المعتبر، حتى صار البعثُ، ووصلتُم إلى هذه الحال. {فهذا يوم البعثِ ولكنَّكم كنتُم لا تعلمون}: فلذلك أنكرتُموه في الدُّنيا، وأنكرتُم إقامتكم في الدُّنيا وقتاً تتمكَّنون فيه من الإنابةِ والتوبةِ، فلم يزل الجهلُ شعاركم، وآثاره من التكذيبِ والخسارِ دِثاركم.
{56} "Na wale waliopewa elimu na Imani watasema;" yaani,
Mwenyezi Mungu aliwaneemesha mawili hayo na yakawa ndiyo sifa yao: kujua haki na kuwa na imani inayolazimu kuipendelea haki. Na ikiwa wanaijua haki na kuipendelea, basi maneno yao lazima yalingane na hali halisi ya mambo, na inayofailia hali zao. Ndiyo maana wakasema kweli, "Hakika nyinyi mlikwisha kaa katika hukumu ya Mwenyezi Mungu" aliyowaandikia "mpaka Siku ya Kiyama." Yaani, mliishi maisha umri ambao mwenye kukumbuka anakumbuka, na mwenye kuzingatia anazingatia juu yake mpaka ufufuo ulipotokea, na mkafikia hali hii. "Basi hii ndiyo Siku ya kufufuliwa! Lakini nyinyi mlikuwa hamuijui." Ndiyo maana mliikataa duniani, na mkakataa kukaa kwenu duniani kwa muda ambao mngeweza kurudi kwa Mwenyezi Mungu na kutubu. Basi haukuacha ujinga kuwa ndio kauli mbiu yenu, na athari zake kama vile kukadhibisha na hasara vikawa ndiyo nguo yenu ya juu ya mwili.
#
{57} {فيومئذٍ لا ينفعُ الذين ظَلَموا معذِرَتُهم}: فإن كذَّبوا، وزعموا أنَّهم ما قامت عليهم الحجَّة، أو ما تمكَّنوا من الإيمان؛ ظهر كَذِبُهم بشهادة أهل العلم والإيمان وشهادة جلودِهِم وأيديهم وأرجلهم، وإنْ طلبوا الإعذارَ، وأنَّهم يردُّون، ولا يعودون لِما نُهوا عنه؛ لم يمكَّنوا؛ فإنَّه فات وقتُ الإعذار، فلا تُقبل معذرتُهم. {ولا هم يُسْتَعْتَبونَ}؛ أي: يُزَالُ عتبُهم والعتابُ عنهم.
{57} "Basi Siku hiyo hautawafaa wale waliodhulumu udhuru wao," wakikadhibisha na wakadai kuwa hakuna ushahidi wowote uliothibiti juu yao, au hawakuweza kuamini, uongo wao huo utadhihirika kwa ushahidi wa watu wenye elimu na imani, na ushahidi wa ngozi zao, mikono yao na miguu yao. Na wakiomba kukubaliwa udhuru, na kwamba warudhishwe na kwamba hawatarejea katika yale waliyokatazwa, hawatawezeshwa kufikia hilo; kwani wakati wa visingizio ulikwisha pita, kwa hivyo udhuru wao hautakubaliwa. "wala haitatakiwa toba yao."
{وَلَقَدْ ضَرَبْنَا لِلنَّاسِ فِي هَذَا الْقُرْآنِ مِنْ كُلِّ مَثَلٍ وَلَئِنْ جِئْتَهُمْ بِآيَةٍ لَيَقُولَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ أَنْتُمْ إِلَّا مُبْطِلُونَ (58) كَذَلِكَ يَطْبَعُ اللَّهُ عَلَى قُلُوبِ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ (59) فَاصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ اللَّهِ حَقٌّ وَلَا يَسْتَخِفَّنَّكَ الَّذِينَ لَا يُوقِنُونَ (60)}
58. Na hakika tulikwisha wapigia watu kila mfano katika hii Qur-ani. Na ukiwaletea Ishara yoyote, hapana shaka wale waliokufuru watasema, "Nyinyi si chochote isipokuwa ni wana batili." 59. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyoziba kwenye nyoyo za wale wasiojua. 60. Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki. Wala wasikupaparishe hao wasiokuwa na yakini.
#
{58 - 59} أي: {ولقد ضَرَبْنا}: لأجل عنايتنا ورحْمَتِنا ولطفنا وحسنِ تعليمنا {للناس في هذا القرآنِ من كلِّ مثلٍ}: تتَّضِح به الحقائقُ وتُعرف به الأمور وتنقطعُ به الحجَّةُ، وهذا عامٌّ في الأمثال التي يضرِبُها الله في تقريب الأمور المعقولة بالمحسوسة، وفي الإخبار بما سيكون وجلاءِ حقيقتِهِ حتى كأنَّه وَقَعَ، ومنه في هذا الموضع ذكرُ الله تعالى ما يكون يوم القيامةِ، وحالةَ المجرمين فيه، وشدَّةَ أسَفِهم، وأنَّه لا يقبلُ منهم عذرٌ ولا عتابٌ، ولكن أبى الظالمون الكافرون إلاَّ معاندة الحقِّ الواضح، ولهذا قال: {ولئن جِئْتَهم بآيةٍ}؛ أي: أيَّ آية تدلُّ على صحة ما جئتَ به، {لَيقولَنَّ الذين كَفَروا إنْ أنتُم إلاَّ مبطلونَ}؛ أي: قالوا للحقِّ: إنَّه باطل! وهذا من كفرهم وجراءتهم وطَبْعِ الله على قلوبهم وجَهْلهم المفرطِ، ولهذا قال: {كذلك يَطْبَعُ الله على قلوبِ الذين لا يعلمونَ}: فلا يَدْخُلُها خيرٌ، ولا تدركُ الأشياءَ على حقيقتها، بل ترى الحقَّ باطلاً والباطل حقًّا.
{58 - 59} Yaani, "Na hakika tulikwisha wapigia watu kila mfano" kwa sababu ya ulezi wetu mzuri, rehema yetu, wema wetu, na mafunzo yetu mema "katika hii Qur-ani," ambayo inayafanya uhakika kuwa wazi, na mambo yanapata kujulikana, na hoja inakatwa kwa hiyo mifano. Nayo ni ya jumla katika mifano ambayo Mwenyezi Mungu hupiga katika kuleta mambo yasiyoonekana kwa yale yanayoshikika, na katika kupeana habari kuhusu yale yatakayotokea na kuweka wazi uhakika wake hadi yakawa ni kana kwamba yametokea. Na miongoni mwake, ni kwamba mahali hapa, Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaja yatakayotokea Siku ya Kiyama, na hali ya wahalifu ndani yake, na ukubwa wa majuto yao, na kwamba hatakubali udhuru wowote wala hata kutubia kutoka kwao, lakini madhalimu na makafiri walikataa isipokuwa kuipinga haki iliyo wazi, na ndiyo maana akasema, "Na ukiwaletea Ishara yoyote" inayoonyesha usahihi wa yale uliyoyaleta, "hapana shaka wale waliokufuru watasema, "Nyinyi si chochote isipokuwa ni wana batili," wakimaanisha kwamba haki ni batili! Hili ni kwa sababu ya ukafiri wao na ujasiri wao, na Mwenyezi Mungu kuziziba nyoyo zao, na ujinga wao uliopitiliza. Na ndiyo maana akasema, "Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyoziba kwenye nyoyo za wale wasiojua." Basi haiingii heri yoyote ndani yake, wala hazifahamu mambo kama yalivyo kihakika, bali zinaona kwamba haki ndiyo batili, nayo batili ndiyo haki.
#
{60} {فاصبرْ}: على ما أمرتَ به وعلى دعوتِهِم إلى اللَّه ولو رأيتَ منهم إعراضاً؛ فلا يصدَّنَّك ذلك. {إنَّ وعدَ الله حقٌّ}؛ أي: لا شكَّ فيه، وهذا مما يُعين على الصبر؛ فإنَّ العبد إذا علم أنَّ عمله غير ضائع، بل سيجدُه كاملاً؛ هانَ عليه ما يلقاه من المكاره، وتيسَّر عليه كلُّ عسيرٍ، واستقلَّ من عملِهِ كلَّ كثير. {ولا يَسْتَخِفَّنَّكَ الذين لا يوقنونَ}؛ أي: قد ضعف إيمانُهم وقلَّ يقينُهم فخفَّت لذلك أحلامُهم، وقلَّ صبرُهم؛ فإيَّاكَ أن يستخِفَّكَ هؤلاء؛ فإنَّك إنْ لم تجعلْهم منكَ على بالٍ، وتحذَرْ منهم، وإلاَّ؛ استخُّفوك وحملوك على عدم الثبات على الأوامر والنواهي، والنفسُ تساعِدُهم على هذا، وتطلُبُ التشبُّه والموافقة ، وهذا مما يدلُّ على أنَّ كلَّ مؤمن موقن رزين العقل؛ يَسْهُلُ عليه الصبر، وكلّ ضعيف اليقين؛ ضعيف العقل خفيفُه؛ فالأول بمنزلة اللُّبِّ، والآخر بمنزلة القشور. فالله المستعان.
{60} "Basi subiri," juu ya yale uliyoamrishwa kuyafanya na juu ya kuwalingania kwa Mwenyezi Mungu, hata ukiwaona wanakugeuzia mgongo, kamwe hayo yasikuzuie. "Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki" na haina shaka yoyote juu yake. Na haya ni katika yale yanayomsaidia mtu kuwa na subira. Kwani, mja anapojua kwamba matendo yake hayawezi kupotea, bali atayapata yakiwa kamili; machukizo yoyote anayokutana nayo yanakuwa rahisi kwake, na kila jambo gumu linakuwa rahisi kwake kiasi kwamba anaona matendo yailiyo mengi kwamba ni machache sana. "Wala wasikupaparishe hao wasiokuwa na yakini." Yaani, wale ambao imani yao ni dhaifu, na yakini yao ni chache, na kwa sababu ya hayo maono yao yakawa hafifu, na subira yao ikapunguka. Kwa hivyo jihadhari na watu hawa wasije kukupaparisha. Kwani, ikiwa hutawaweka akilini na ukajihadhari nao, vinginevyo; watakupaparisha na kukufanya usiwe imara katika kufuata maamrisho na kuacha makatazo, nayo nafsi yako itawasaidia katika hili, na itataka ufanane nao na uafikiane nao. Na hili ni katika mambo yanayoonyesha kwamba kila Muumini mwenye yakini na ana akili timamu; ni rahisi sana kwake kuwa na subira. Lakini kila mwenye yakini dhaifu, mwenye akili dhaifu na nyepesi haliwezi hilo. Kwa hivyo, huyo wa kwanza yuko katika nafasi ya kiini cha kitu, naye wa pili ni kama gamba la mbegu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayeombwa msaada juu ya hayo.
* * *