Tafsiri ya Surat Al-Muuminun
Tafsiri ya Surat Al-Muuminun
Nayo iliteremka Makka
{قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ (1) الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ (2) وَالَّذِينَ هُمْ عَنِ اللَّغْوِ مُعْرِضُونَ (3) وَالَّذِينَ هُمْ لِلزَّكَاةِ فَاعِلُونَ (4) وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ (5) إِلَّا عَلَى أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ (6) فَمَنِ ابْتَغَى وَرَاءَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْعَادُونَ (7) وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ (8) وَالَّذِينَ هُمْ عَلَى صَلَوَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ (9) أُولَئِكَ هُمُ الْوَارِثُونَ (10) الَّذِينَ يَرِثُونَ الْفِرْدَوْسَ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ (11)}.
1. Hakika wamefaulu Waumini. 2. Ambao ni wanyenyekevu katika Swala zao. 3. Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi. 4. Na ambao wanatoa Zaka. 5. Na ambao wanazilinda tupu zao. 6. Isipokuwa kwa wake zao au kwa wale iliyowamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa. 7. Lakini anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio wavukao mipaka. 8. Na ambao wanazitunza amana zao na ahadi zao. 9. Na ambao Swala zao wanazihifadhi. 10. Hao ndio warithi. 11. Ambao watairithi Pepo ya Firdausi, nao watadumu humo.
Hii ni ishara kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwataja waja wake Waumini, kutaja kufaulu kwao na furaha yao, na ni kwa kitu gani walifikia hayo. Na katika hayo kuna himizo juu ya kusifika na sifa zao hizo na kutia moyo katika hilo. Basi mja na ajipime mwenyewe na wengineo juu ya ishara hizi, atajua alicho nacho na kile walicho nacho wengine cha imani yenye kuongezeka na kupunguka, na imani nyingi na chache.
#
{1} فقوله: {قد أفلح المؤمنونَ}؛ أي: قد فازوا وسَعِدوا ونجحوا، وأدركوا كلَّ ما يرام، المؤمنون الذين آمنوا بالله، وصدَّقوا المرسلين.
{1} Kwa hivyo kauli yake, "Hakika wamefaulu Waumini." Yaani, wamefuzu, wamefurahi, wamefanikiwa, na wamefikia yote yatafutwayo. Nao ni waumini ambao walimwamini Mwenyezi Mungu, na wakawasadiki Mitume.
#
{2} الذين من صفاتهم الكاملة أنهم {في صلاتهم خاشِعونَ}: والخشوع في الصلاة هو حضورُ القلب بين يدي الله تعالى، مستحضراً لقربه، فيسكن لذلك قلبه، وتطمئن نفسه، وتسكن حركاتُه، ويقلُّ التفاتُه، متأدِّباً بين يدي ربِّه، مستحضراً جميع ما يقوله ويفعله في صلاتِهِ من أول صلاته إلى آخرها، فتنتفي بذلك الوساوس والأفكار الرديَّة، وهذا روح الصلاة والمقصود منها، وهو الذي يُكْتَبُ للعبد؛ فالصلاةُ التي لا خشوع فيها ولا حضورَ قلبٍ، وإنْ كانت مُجْزِيَةً مثاباً عليها؛ فإنَّ الثواب على حسب ما يَعْقِلُ القلب منها.
{2} Wale ambao katika sifa zao kamilifu ni kwamba wao, "ni wanyenyekevu katika Swala zao." Na kunyenyekea katika Swala ni kuwepo kwa moyo mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ukawa unatilia maanani ukaribu wake Mwenyezi Mungu, kwa hivyo ukawa moyo wake unatulia kwa sababu ya hilo, na nafsi yake ikawa imetua, na harakati zake zikawa zimetulia, na kukapunguka kugeukageuka kwake, akawa na adabu nzuri mbele ya Mola wake Mlezi, akawa anayatilia maanani yote anayosema na kufanya katika Swala yake kuanzia mwanzo wake hadi mwisho wake. Kwa hivyo zinaondoka kwa hayo wasiwasi na mawazo mabaya. Na hii ndiyo roho ya swala na makusudio yake. Nayo ndiyo anayoandikwa mja. Kwa maana swala ambayo haina unyenyekevu ndani yake wala uwepo wa moyo, hata kama inatosheleza, na inalipwa thawabu, lakini thawabu hizo ni kulingana na kile ambacho moyo unaelewa kwayo.
#
{3} {والذين هم عن اللغو}: وهو الكلام الذي لا خير فيه ولا فائدة، {معرضون}: رغبةً عنه وتنزيهاً لأنفسهم وترفُّعاً عنه، وإذا مرُّوا باللغو مرُّوا كراماً، وإذا كانوا معرضين عن اللغو؛ فإعراضُهم عن المحرَّم من باب أولى وأحرى، وإذا مَلَكَ العبدُ لسانَه وخَزَنَه إلاَّ في الخير؛ كان مالكاً لأمرِهِ؛ كما قال النبيُّ - صلى الله عليه وسلم - لمعاذ بن جبل حين وصَّاه بوصايا؛ قال: «ألا أخبرك بملاك ذلك كله؟». قلت: بلى يا رسول الله! فأخذ بلسان نفسه وقال: «كفَّ عليك هذا». فالمؤمنون من صفاتهم الحميدة كفُّ ألسنتهم عن اللغو والمحرَّمات.
{3} "Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi." Nayo ni maneno yasiyokuwa na heri wala manufaa. Kwa hivyo wanajiepusha nayo kwa kutoyapenda, na kujitakasa nafsi zao kutokana nayo na kujiweka mbali sana nao, na pindi wapitapo penye upuuzi, hupita kwa heshima yao. Na kama wanajiepusha na upuuzi, basi inawafailia na inawastahiki zaidi kujiepusha na yaliyoharamishwa. Na pindi mja ataumiliki ulimi wake na akauhifadhi isipokuwa katika mambo ya heri, basi anakuwa amemiliki mambo yake. Kama alivyosema Nabii, rehema za amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - akimuambia Muadh bin Jabal alipomuusia wasia mbalimbali, akasema, “Je, nikwambie chenye kuyamiliki hayo yote? Nikasema, "Ndiyo, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu!" Akaushika ulimi wake na akasema, "Jizuie na huu." Basi katika sifa nzuri za Waumini ni kuzizuia ndimi zao kutokana na upuuzi na mambo yaliyoharamishwa.
#
{4} {والذين هم للزَّكاةِ فاعلون}؛ أي: مؤدُّون لزكاة أموالهم على اختلاف أجناس الأموال؛ مزكين لأنفسهم من أدناس الأخلاق ومساوئ الأعمال التي تزكو النفوس بتركِها وتجنُّبِها؛ فأحسنوا في عبادة الخالق في الخشوع في الصلاة، وأحسنوا إلى خلقه بأداء الزَّكاة.
{4} "Na ambao wanatoa Zaka" katika mali zao tofautitofauti huku wakijitakasa nafsi zao kutokana na tabia chafu na matendo mabaya ambayo nafsi zinasafika kwa kuyaacha na kujiepusha nayo. Kwa hivyo, wakawa wamefanya vizuri katika kumwabudu Muumba kwa kunyenyekea katika swala, na wakawafanyia uzuri viumbe wake kwa kuwapa Zaka.
#
{5} {والذين هم لفروجهم حافظون}: عن الزِّنا، ومن تمام حفظها تجنُّب ما يدعو إلى ذلك؛ كالنظر واللمس ونحوهما، فحفظوا فروجهم من كلِّ أحدٍ.
{5} "Na ambao wanazilinda tupu zao" kutokana na uzinzi. Na katika kuzihifadhi kukamilifu ni kujiepusha na yenye kuitia hilo, kama vile kuangalia, kugusa, na mfano wa hayo. Basi zihifadhini tupu zenu kutokana na kila moja.
#
{6} {إلاَّ على أزواجهم أو ما ملكت أيمانُهم}: من الإماء المملوكات؛ {فإنَّهم غيرُ ملومين}: بقربهما؛ لأن الله تعالى أحلهما.
{6} "Isipokuwa kwa wake zao au kwa wale iliyowamiliki mikono yao ya kulia," kama vile wajakazi; "kwani hao si wenye kulaumiwa" kwa kuwakaribia hao, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu amewahalalisha.
#
{7} {فمنِ ابتغى وراء ذلك}: غير الزوجة والسُّرِّيَّة؛ {فأولئك هم العادونَ}: الذين تعدَّوا ما أحلَّ الله إلى ما حرَّمه، المتجرِّئون على محارم الله. وعموم هذه الآية يدلُّ على تحريم [نكاح] المتعة؛ فإنَّها ليست زوجةً حقيقةً مقصوداً بقاؤها ولا مملوكةً، وتحريم نكاح المحلِّل لذلك. ويدل قوله: {أو ما مَلَكَتْ أيمانُهم}: أنَّه يُشترط في حلِّ المملوكة أن تكونَ كلُّها في ملكه؛ فلو كان له بعضُها؛ لم تحلَّ؛ لأنَّها ليست ممَّا ملكت يمينُه، بل هي ملكٌ له ولغيره؛ فكما أنَّه لا يجوز أن يَشْتَرِكَ في المرأة الحرَّة زوجان؛ فلا يجوزُ أن يشترِكَ في الأمة المملوكة سيدان.
{7} "Lakini anayetaka kinyume cha haya" miongoni mwa asiyekuwa mke na suria, "basi hao ndio wavukao mipaka," ambao walivuka yale aliyohalalisha Mwenyezi Mungu hadi kwa yale aliyoharamisha, wale ambao wanayafanyia ujasiri maharamisho ya Mwenyezi Mungu. Na kwa ujumla, aya hii inaonyesha uharamu wa
[nikah ya] Al-Mut'a. Kwa sababu mwanamke huyo siyo mke kihalisia anayekusudiwa kukaa wala kummiliki, na pia inaharamisha nikaha ya kumhalishia mke kuolewa na mke wake aliyekuwa amempa talaka zote tatu. Na inaashiria kauli yake, "wale iliyowamiliki mikono yao ya kulia" kwamba, ili kijakazi awe halali, ni sharti awe amemilikiwa kikamilifu na mtu mmoja. Na ikiwa atakuwa amemmiliki baadhi yake tu, basi hawi halali kwake. Kwa maana, mwanamke kama huyo si katika wale uliomiliki mkono wake wa kulia, bali yeye ni miliki yake na ya wengineo. Kwa hivyo, kama vile hairuhusiwi kwa wanaume wawili kushiriki katika mwanamke huru, basi hairuhusiwi kwa mabwana wawili kushiriki katika kijakazi mmoja.
#
{8} {والذين هم لأماناتِهِم وعَهْدِهِم راعونَ}؛ أي: مراعون لها، ضابطون، حافظون، حريصون على القيام بها وتنفيذها. وهذا عامٌّ في جميع الأمانات التي هي حقٌّ لله، والتي هي حقٌّ للعباد؛ قال تعالى: {إنَّا عَرَضْنا الأمانة على السمواتِ والأرضِ والجبال فأبَيْنَ أنْ يحمِلْنها وأشفَقْنَ منها وحملها الإنسانُ}: فجميع ما أوجبه الله على عبدِهِ أمانةٌ على العبد حفظُها بالقيام التامِّ بها. وكذلك يدخُلُ في ذلك أمانات الآدميِّين؛ كأمانات الأموال والأسرار ونحوهما؛ فعلى العبد مراعاة الأمرين وأداء الأمانتين؛ {إنَّ اللَّه يأمُرُكم أنْ تؤدُّوا الأماناتِ إلى أهلها}، وكذلك العهد يَشْمَلُ العهدَ الذي بينهم وبين ربهم والذي بينهم وبين العباد، وهي الالتزامات والعقود التي يعقدها العبد؛ فعليه مراعاتها والوفاء بها، ويحرُمُ عليه التفريطُ فيها وإهمالها.
{8} "Na ambao wanazitunza amana zao na ahadi zao;" na wanafanya bidii kubwa kuzitekeleza. Na hili ni jumla katika amana zote ambazo ni haki ya Mwenyezi Mungu, na ambazo ni haki za waja wake. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema, "Kwa hakika Sisi tulikadimisha amana kwa mbingu na ardhi na milima; na vyote hivyo vikakataa kuichukua na vikaogopa. Lakini mwanadamu akaichukua. "Kwa hivyo, yote ambayo Mwenyezi Mungu alimwajibishia mja wake ni amana, na ni lazima kwake kuihifadhi kwa kuitekeleza kikamilifu. Na vile vile inaingia katika hilo amana za wanadamu, kama vile amana za mali, siri na mfano wake. Kwa hivyo, ni lazima kwa mja kuzingatia mambo hayo mawili na kutekeleza amana hizo mbili. "Hakika Mwenyezi Mungu anawaamrisha kwamba mzirudishe amana kwa wenyewe." Vile vile agano linajumuisha agano iliyoko kati yao na Mola wao Mlezi, na ile iliyoko kati yao na waja wenzao. Nayo ni majukumu mbalimbali na mikataba ambayo mja anaifunga. Basi ni lazima juu yake kuyatunza na kuyatimiza, na ni haramu kwake kutoyatekeleza vyema na kuyapuuza.
#
{9} {والذين هم على صَلَواتهم يحافِظونَ}؛ أي: يداومون عليها في أوقاتها وحدودها وأشراطها وأركانها؛ فمدحهم بالخشوع بالصلاة وبالمحافظة عليها، لأنَّه لا يتمُّ أمرُهم إلاَّ بالأمرين؛ فمن يداوِمُ على الصلاة من غير خُشوع أو على الخُشوع من دون محافظةٍ عليها؛ فإنَّه مذمومٌ ناقصٌ.
{9} "Na ambao Swala zao wanazihifadhi;" yaani, wanadumu katika kuzitekeleza katika nyakati zake, mipaka yake, masharti yake, na nguzo zake. Kwa hivyo, akawasifu kwa kunyenyekea katika swala, na kuitunza, kwa sababu mambo yao hayatimii isipokuwa kwa mambo mawili haya. Kwa hivyo, mwenye kudumu katika swala bila ya unyenyekevu au akawa na unyenyekevu bila ya kuihifadhi swala, basi yeye kwa hakika analaumiwa na amefanya upungufu.
#
{10} {أولئك}: الموصوفون بتلك الصفات {هم الوارثونَ}.
{10} "Hao," wanaosifika kwa sifa hizo, "ndio warithi."
#
{11} {الذين يَرِثونَ الفِرْدَوْسَ}: الذي هو أعلى الجنَّة ووسطُها وأفضلُها؛ لأنَّهم حُلُّوا من صفات الخير أعلاها وذروتها، أو المراد بذلك جميع الجنة؛ ليدخلَ بذلك عموم المؤمنين على درجاتهم في مراتبهم كلٌّ بحسب حاله. {هم فيها خالدونَ}: لا يَظْعَنون عنها ولا يَبْغون عنها حِولاً؛ لاشتمالها على أكمل النعيم وأفضله وأتمِّه من غير مكدِّرٍ ولا منغصٍ.
{11} "Ambao watairithi Pepo ya Firdausi," ambayo ndiyo Pepo ya juu zaidi, ya katikati, na iliyo bora zaidi. Kwa sababu walivalishwa sifa za heri za juu zaidi na ambazo ndizo kilele cha sifa hizo. Au kilichomaanishwa ni kwamba watairithi Pepo yote, ili waingie katika hilo waumini wote kwa ujumla katika daraja zao kila mmoja kulingana na hali yake. "Nao watadumu humo," hawataondoka humo, wala hawatataka kwenda kwingine, kwa sababu ya furaha zake kamili na ubora wake, na hakutakuwemo na shida yoyote wala mapungufu yoyote.
{وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ مِنْ سُلَالَةٍ مِنْ طِينٍ (12) ثُمَّ جَعَلْنَاهُ نُطْفَةً فِي قَرَارٍ مَكِينٍ (13) ثُمَّ خَلَقْنَا النُّطْفَةَ عَلَقَةً فَخَلَقْنَا الْعَلَقَةَ مُضْغَةً فَخَلَقْنَا الْمُضْغَةَ عِظَامًا فَكَسَوْنَا الْعِظَامَ لَحْمًا ثُمَّ أَنْشَأْنَاهُ خَلْقًا آخَرَ فَتَبَارَكَ اللَّهُ أَحْسَنُ الْخَالِقِينَ (14) ثُمَّ إِنَّكُمْ بَعْدَ ذَلِكَ لَمَيِّتُونَ (15) ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ تُبْعَثُونَ (16)}.
12. Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asili ya udongo. 13. Kisha tukamfanya kuwa tone la mbegu ya uzazi katika mahali patulivu palipo madhubuti. 14. Kisha tukaliumba tone hilo kuwa damu iliyoganda, na tukaiumba damu hiyo kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande hilo la nyama kuwa mifupa, na mifupa hiyo tukaivisha nyama. Kisha tukamfanya kuwa kiumbe mwingine. Basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa baraka, Mbora zaidi wa waumbaji. 15. Kisha hakika nyinyi baada ya hayo mtakufa. 16. Kisha hakika nyinyi Siku ya Qiyama mtafufuliwa.
Katika aya hizi, Mwenyezi Mungu alitaja awamu za maisha ya mwanadamu na kubadilika kwake kuanzia kuumbwa kwake hadi atakavyoishia.
#
{12} فذكر ابتداء خلق أبي النوع البشري آدم عليه السلام، وأنه {من سُلالةٍ من طينٍ}؛ أي: قد سُلَّتْ وأُخِذَتْ من جميع الأرض، ولذلك جاء بنوه على قدر الأرض: منهم الطيب والخبيث وبين ذلك، والسهل والحزن وبين ذلك.
{12} Alitaja mwanzo wa kuumbwa kwa baba wa wanadamu, Adam, amani iwe juu yake, na kwamba, yeye ni "kutokana na asili ya udongo." Yaani, ilitolewa na kuchukuliwa kutoka katika ardhi yote. Na ndiyo maana, wakawa wanawe ni kulingana na ardhi waliyoumbiwa. Miongoni mwao kuna mzuri na muovu, na aliye kati ya hivyo, na rahisi na mgumu, na aliye kati ya hivyo.
#
{13} {ثم جعلناه}؛ أي: جنس الآدميين {نطفةً}: تخرُجُ من بين الصُّلب والترائب، فتستقر {في قَرارٍ مكينٍ}: وهو الرحم، محفوظةً من الفساد والريح وغير ذلك.
{13} "Kisha tukamfanya," yaani wanadamu "kuwa tone la mbegu ya uzazi" linalotoka kati ya uti wa mgongo na mbavu. Kisha linatulia, "katika mahali patulivu palipo madhubuti." Yaani, tumbo la uzazi, ambalo limehifadhiwa kutokana na uharibifu, upepo, na yasiyokuwa hayo.
#
{14} {ثم خلقنا النطفةَ}: التي قد استقرَّت قبل {علقةً}؛ أي: دماً أحمر بعد مضيِّ أربعين يوماً من النطفة، ثم {خلقنا العلقةَ}: بعد أربعين يوماً {مضغةً}؛ أي: قطعة لحم صغيرةٍ بقدر ما يُمْضَغ من صغرها، {فَخلْقنا المضغة}: اللينةَ {عظاماً}: صلبةً قد تخلَّلت اللحم بحسب حاجة البدن إليها، {فكَسَوْنا العظام لحماً}؛ أي: جعلنا اللحم كسوة للعظام؛ كما جعلنا العظام عماداً للحم، وذلك في الأربعين الثالثة، {ثم أنشأناه خَلْقاً آخر}: نفخ فيه الروح، فانتقل من كونه جماداً إلى أنْ صار حيواناً. {فتبارك الله}؛ أي: تعالى وتعاظم وكثر خيره، {أحسنُ الخالقينَ}: {الذي أحسنَ كلَّ شيءٍ خَلَقَهُ وبدأ خَلْقَ الإنسان من طين. ثم جعل نسله من سلالةٍ من ماءٍ مَهين. ثم سوَّاه ونَفَخَ فيه من روحِهِ وجعل لكم السمع والأبصار والأفئدةَ قليلاً ما تشكرون}؛ فخلقه كلُّه حسنٌ، والإنسان من أحسن مخلوقاته، بل هو أحسنها على الإطلاق؛ كما قال تعالى: {لقد خَلَقْنا الإنسان في أحسن تقويم}، ولهذا كان خواصُّه أفضل المخلوقات وأكملها.
{14} "Kisha tukaliumba tone hilo" ambalo lilitulia katika tumbo la uzazi "kuwa damu iliyoganda;" yaani, damu nyekundu siku arobaini baada ya kuwa tone la mbegu ya uzazi. Kisha "tukaiumba damu hiyo" baada ya siku arobaini, "kuwa pande la nyama" la kiasi kinachotosha kutafunwa kwa sababu ya udogo wake. "Kisha tukaliumba pande hilo la nyama" laini "kuwa mifupa" migumu iliyoingiliana na nyama kulingana na namna mwili unavyoihitajia. "Na mifupa hiyo tukaivisha nyama" kama tulivyoifanya mifupa kuwa nguzo ya nyama, na hilo ni baada ya siku arobaini za tatu. "Kisha tukamfanya kuwa kiumbe mwingine" aliyepuliziwa roho ndani yake, kwa hivyo akageuka kutoka kuwa kitu kisicho na uhai hadi akawa mnyama. "Basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa baraka, Mbora wa waumbaji," "ambaye ametengeneza vizuri kila kitu alichoumba, na akaanzisha kumuumba mtu kwa udongo, kisha akajaalia uzao wake utokane na asili ya maji dhaifu. Kisha akamtengeneza, na akampulizia roho yake, na akawajaalia kusikia na kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyoshukuru." Basi viumbe vyake vyote vizuri, na mtu ni katika bora zaidi wa viumbe vyake, bali yeye ndiye mbora wao kabisa. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio zuri zaidi." Na ndiyo maana wakawa wateule wake ndio viumbe wake bora zaidi na wakamilifu zaidi yao wote.
#
{15} {ثم إنكم بعد ذلك}: الخلق ونفخ الروح، {لَمَيِّتون}: في أحد أطواركم وتنقُّلاتكم.
{15} "Kisha hakika nyinyi baada ya hayo;" ya kuumbwa na kupuliziwa roho "mtakufa" katika moja ya awamu zenu na kubadilika kwenu.
#
{16} {ثم إنَّكم يوم القيامةِ تُبْعَثونَ}: فتجازَوْن بأعمالكم حسنها وسيئها؛ قال تعالى: {أيحسَبُ الإنسان أن يُتْرَكَ سدى. ألم يَكُ نطفةً من مَنِيٍّ يُمْنى. ثم كان علقةً فَخَلَقَ فسَوَّى. فَجَعَلَ منه الزوجينِ الذَّكَرَ والأنثى. أليس ذلك بقادرٍ على أن يُحيي الموتى}.
{16} "Kisha hakika nyinyi Siku ya Qiyama mtafufuliwa" kisha mtalipwa kwa matendo yenu, mazuri yake kwa mazuri, na mabaya yake kwa mabaya. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Ati anadhani mtu kwamba ataachwa bure? Kwani hakuwa ni tone la manii lililoshushwa? Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza sawasawa? Kisha akamfanya kwayo jozi, wa kiume na wa kike? Je, huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu?"
{وَلَقَدْ خَلَقْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعَ طَرَائِقَ وَمَا كُنَّا عَنِ الْخَلْقِ غَافِلِينَ (17) وَأَنْزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً بِقَدَرٍ فَأَسْكَنَّاهُ فِي الْأَرْضِ وَإِنَّا عَلَى ذَهَابٍ بِهِ لَقَادِرُونَ (18) فَأَنْشَأْنَا لَكُمْ بِهِ جَنَّاتٍ مِنْ نَخِيلٍ وَأَعْنَابٍ لَكُمْ فِيهَا فَوَاكِهُ كَثِيرَةٌ وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ (19) وَشَجَرَةً تَخْرُجُ مِنْ طُورِ سَيْنَاءَ تَنْبُتُ بِالدُّهْنِ وَصِبْغٍ لِلْآكِلِينَ (20)}.
17. Na kwa yakini tumeziumba juu yenu njia saba. Nasi hatukuwa wenye kughafilika na viumbe. 18. Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi na tukayatuliza katika ardhi. Na hakika Sisi tunaweza kuyaondoa. 19. Kwa maji hayo tukawafanyia bustani za mitende na mizabibu, mnapata humo matunda mengi, na katika hayo mnakula. 20. Na mti utokao katika mlima wa Sinai, unaotoa mafuta na kuwa kitoweo kwa walao.
#
{17} لما ذكر تعالى خلق الآدميِّ؛ ذكر مسكنه وتوفُّر النعم عليه من كل وجهٍ، فقال: {ولقد خَلَقْنا فوقَكُم}: سقفاً للبلاد ومصلحةً للعباد، {سبع طرائقَ}؛ أي: سبع سماواتٍ طباقاً، كلُّ طبقةٍ فوق الأخرى، قد زُيِّنَتْ بالنُّجوم والشمس والقمر، وأودِعَ فيها من مصالح الخلق ما أودع. {وما كُنَّا عن الخلق غافلين}؛ فكما أن خَلْقَنا عامٌّ لكل مخلوق؛ فعلمنا أيضاً محيطٌ بما خَلَقْنا؛ فلا نغفل مخلوقاً ولا ننساه، ولا نَخْلُقُ خلقاً فنضيِّعه، ولا نغفل عن السماء فتقع على الأرض، ولا ننسى ذرَّةً في لجج البحار وجوانب الفلوات ولا دابَّة إلاَّ سُقنا إليها رزقها، {وما من دابَّةٍ في الأرض إلاَّ على الله رِزْقُها ويعلم مُسْتَقَرَّها ومُسْتَوْدَعَها}: وكثيراً ما يقرِنُ تعالى بين خلقِهِ وعلمِهِ؛ كقوله: {ألا يعلمُ من خَلَقَ وهو اللطيفُ الخبير}، {بلى وهو الخلاقُ العليم}؛ لأنَّ خلق المخلوقات من أقوى الأدلَّة العقليَّة على علم خالقها وحكمته.
{17} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kuumbwa kwa mwanadamu, akataja makao yake na kumpa neema kwa njia zote. Akasema, "Kwa yakini tumeziumba juu yenu" dari kwa nchi na masilahi kwa waja, "njia saba." Yaani, mbingu saba katika matabaka, kila tabaka juu ya lingine, na zimepambwa kwa nyota, jua na mwezi, na akatia humo mambo yenye masilahi kwa waja. "Nasi hatukuwa wenye kughafilika na viumbe." Na kama vile uumbaji wetu ni wa jumla kwa kila kiumbe, basi elimu yetu pia imezunguka yote tuliyoumba. Hatughafiliki na kiumbe chochote wala hatukisahau, wala hatuumbi kiumbe kisha tukakipuuza. Wala hatughafiliki tukaiacha mbingu ikaiangukia ardhi. Wala hatuisahau chembe iliyoko ndani ya bahari na pande za majangwa, wala mnyama yeyote isipokuwa tunamfikishia riziki yake. "Naye anajua makao yake na mapitio yake." Na mara nyingi Mwenyezi Mungu Mtukufu huunganisha kati ya kuumba kwake na elimu yake. Kama vile kauli yake, "Asijue aliyeumba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye habari zote?" "Kwani! Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Ajuaye zaidi." Kwa sababu, kuwaumba viumbe ni katika ushahidi wenye nguvu wa kiakili juu ya elimu na hekima ya Muumba wao.
#
{18} {وأنزلنا من السماء ماءً}: يكون رزقاً لكُم ولأنعامكم بقدر ما يكفيكم؛ فلا ينقصه [بحيث لا يكفي الأرض والأشجار، فلا يحصل منه المقصود. ولا يزيده زيادة لا تحتمل]، بحيثُ يتلف المساكن، ولا تعيش منه النباتات والأشجار، بل أنزله وقتَ الحاجة لنزوله، ثم صرفه عند التضرُّر من دوامه، {فأسكنَّاه في الأرض}؛ أي: أنزلناه عليها، فسكن واستقرَّ وأخرج بقدرةِ منزلِهِ جميع الأزواج النباتيَّة، وأسكنه أيضاً معدًّا في خزائن الأرض؛ بحيث لم يذهبْ نازلاً حتى لا يوصل إليه ولا يُبلغَ قعره. {وإنَّا على ذَهابٍ به لَقادِرونَ}: إمَّا بأن لا نُنْزِلَه، أو نُنْزِلُه فيذهب نازلاً لا يوصَل إليه، أو لا يوجد منه المقصود منه، وهذا تنبيهٌ منه لعباده أن يشكروه على نعمته ويقدِّروا عدمها؛ ماذا يحصُلُ به من الضَّرر؛ كقوله تعالى: {قلْ أرأيتُم إنْ أصبحَ ماؤكم غَوْراً فمن يأتيكم بماءٍ معين}.
{18} "Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji," ili yawe riziki kwa yenu na ya wanyama wenu kwa kiasi kinachowatosha, na wala haipunguzi
[kwa namna ambayo haiwezi kuitosha ardhi na miti, kwa hivyo kikawa hakipatikani kile kilichokusudiwa nayo. Na tena haizidishi kwa kiasi ambacho haiwezi kustahimili], mpaka ikaharibu makazi, na wala mimea na miti ikawa haiwezi kumea humo. Bali anaishusha wakati inapohitajika kushuka, kisha akaiondoa wakati kunapokuwa kuendelea kwake ni madhara, "tukayatuliza katika ardhi" na akatoa jozi zote za mimea yule aliyeyashusha, tena akayafanya kukaa tayari ndani yake hazina ya ardhi, kwa namna ambayo hayakuendelea kushuka hadi yasifikiwe wala isifikiwe sehemu yake ya chini zaidi. "Na hakika Sisi tunaweza kuyaondoa. " Ima kwa kutoyateremsha, au huyateremsha kisha yakadidimia ndani kiwango cha kutofikiwa, au yasifikiwe makusudio yake. Na hii ni tanabahisho lake kwa waja wake kwamba wamshukuru kwa neema yake na wapime lau kuwa haingekuwa, ni madhara gani yangewapata. Kama vile kauli yake, "Sema, mwaonaje, ikiwa maji yenu yatadidimia chini, ni nani atakayewaletea maji yanayomiminika?"
#
{19} {فأنشأنا لكم به}؛ أي: بذلك الماء، {جناتٍ}؛ أي: بساتين {من نخيل وأعنابٍ}: خصَّ تعالى هذين النوعين، مع أنه ينشر منه غيرهما من الأشجار؛ لفضلهما ومنافعهما التي فاقت بها الأشجار، ولهذا ذكر العامَّ في قوله: {لكم}؛ أي: في تلك الجنات فواكه كثيرةٌ منها تأكُلون من تينٍ وأتْرُجٍّ ورمانٍ وتفاح وغيرها.
{19} "Kwa maji hayo tukawafanyia bustani za mitende na mizabibu." Mwenyezi Mungu alitaja aina mbili hizi pamoja na kwamba anatoa humo miti mingineyo kwa sababu ya ubora wake na manufaa yake ambayo kwayo ilizidi miti mingineyo. Na ndiyo maana akataja faida ya ujumla katika kauli yake, "mnapata humo." Yaani, katika bustani hizi kuna matunda mengi, na katika hayo mnakula kama vile tini, machungwa, makomamanga, tufaha, na mengineyo.
#
{20} {وشجرة تخرج من طور سَيْناءَ}: وهي شجرة الزيتون؛ أي: جنسها، خُصَّت بالذكر لأنَّ مكانها خاصٌّ في أرض الشام، ولمنافعها التي ذُكِرَ بعضُها في قوله: {تَنْبُتُ بالدُّهن وصِبْغٍ للآكلين}؛ أي: فيها الزيت الذي هو دهنٌ، يُسْتَعْمَلُ استعمالَه من الاستصباح به، واصطباغ للآكلين؛ أي: يجعل إداماً للآكلين وغير ذلك من المنافع.
{20} "Na mti utokao katika mlima wa Sinai" nao ni mzeituni. Na umetajwa haswa kwa jina sababu hadhi yake ni maalumu katika ardhi ya Shamu, na kwa sababu ya faida zake, ambazo baadhi yake zimetajwa katika kauli yake, "unaotoa mafuta na kuwa kitoweo kwa walao."
{وَإِنَّ لَكُمْ فِي الْأَنْعَامِ لَعِبْرَةً نُسْقِيكُمْ مِمَّا فِي بُطُونِهَا وَلَكُمْ فِيهَا مَنَافِعُ كَثِيرَةٌ وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ (21) وَعَلَيْهَا وَعَلَى الْفُلْكِ تُحْمَلُونَ (22)}.
21. Na hakika mnayo mazingatio makubwa katika wanyama hoa. Tunawanywesha nyinyi katika vile viliovymo matumboni mwao, na nyinyi mnapata katika hao manufaa mengi, na pia mnawala. 22. Na juu yao na juu ya marikebu mnabebwa.
#
{21} أي: ومن نعمه عليكم أن سَخَّرَ لكم الأنعام؛ الإبل والبقر والغنم، فيها عبرةٌ للمعتبرين ومنافع للمنتفعين، {نُسْقيكُم ممَّا في بُطونها}: من لبنٍ يخرُجُ من بين فَرْثٍ ودمٍ خالص سائغ للشاربين، {ولكم فيها منافعُ كثيرةٌ}: من أصوافها وأوبارها وأشعارِها، وجعل لكم من جلودِ الأنعام بيوتاً تستخفُّونها يوم ظَعْنِكُم ويومَ إقامتِكُم، {ومنها تأكُلون}: أفضل المآكل من لحم وشحم.
{21} Yaani,
katika neema zake juu yenu ni kwamba amewatiishia nyama hoa: ngamia, ng'ombe, kondoo na mbuzi. Ndani yao kuna mazingatio kwa wanaozingatia na manufaa kwa wanaonufaika. "Tunawanywesha nyinyi katika vile viliovymo matumboni mwao" kama vile maziwa safi mazuri kwa wanywao yanayotoka baina ya mavi na damu. "Na nyinyi mnapata katika hao manufaa mengi" kama vile sufu zao, manyoya yao, na nywele zao. Na akawafanyia kutoka kwa wanyama hoa hao, nyumba mnazoziona nyepesi wakati wa safari zenu na wakati wa kutua kwenu. "Na pia mnawala," chakula bora kama vile nyama na mafuta.
#
{22} {وعليها وعلى الفُلْكِ تُحْمَلونَ}؛ أي: جعلها سفناً لكم في البرِّ، تحملون عليها أثقالكم إلى بلدٍ لم تكونوا بالغيهِ إلاَّ بشِقِّ الأنفس؛ كما جعل لكم السفنَ في البحر تحملكم وتحمل متاعكم قليلاً كان أو كثيراً؛ فالذي أنعم بهذه النعم وصنَّف أنواع الإحسان وأدرَّ علينا من خيره المدرار هو الذي يستحقُّ كمالَ الشُّكْر وكمال الثناء والاجتهاد في عبوديَّته وأن لا يُستعان بنعمه على معاصيهِ.
{22} "Na juu yao na juu ya marikebu mnabebwa," Yaani aliwafanya kuwa safina zenu katika nchi kavu. Mnabebea juu yao mizigo yenu kupeleka kwenye miji msiyoweza kuifikia isipokuwa kwa mashaka ya nafsi, kama vile alivyowafanyia safina baharini zenye kuwabeba nyinyi na mizigo yenu hata kama ni michache au mingi. Basi yule ambaye alituneemesha kwa aina hizi za neema na wema mbalimbali na akatupa kwa wingi katika heri zake, ndiye anayestahili kushukuriwa kikamilifu na kusifiwa kikamilifu, na kujitahidi katika kumuabudu, na kwamba neema zake zisitumike katika kumuasi.
{وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَى قَوْمِهِ فَقَالَ يَاقَوْمِ اعْبُدُوا اللَّهَ مَا لَكُمْ مِنْ إِلَهٍ غَيْرُهُ أَفَلَا تَتَّقُونَ (23) فَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ قَوْمِهِ مَا هَذَا إِلَّا بَشَرٌ مِثْلُكُمْ يُرِيدُ أَنْ يَتَفَضَّلَ عَلَيْكُمْ وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ لَأَنْزَلَ مَلَائِكَةً مَا سَمِعْنَا بِهَذَا فِي آبَائِنَا الْأَوَّلِينَ (24) إِنْ هُوَ إِلَّا رَجُلٌ بِهِ جِنَّةٌ فَتَرَبَّصُوا بِهِ حَتَّى حِينٍ (25) قَالَ رَبِّ انْصُرْنِي بِمَا كَذَّبُونِ (26) فَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِ أَنِ اصْنَعِ الْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا وَوَحْيِنَا فَإِذَا جَاءَ أَمْرُنَا وَفَارَ التَّنُّورُ فَاسْلُكْ فِيهَا مِنْ كُلٍّ زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ وَأَهْلَكَ إِلَّا مَنْ سَبَقَ عَلَيْهِ الْقَوْلُ مِنْهُمْ وَلَا تُخَاطِبْنِي فِي الَّذِينَ ظَلَمُوا إِنَّهُمْ مُغْرَقُونَ (27) فَإِذَا اسْتَوَيْتَ أَنْتَ وَمَنْ مَعَكَ عَلَى الْفُلْكِ فَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي نَجَّانَا مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ (28) وَقُلْ رَبِّ أَنْزِلْنِي مُنْزَلًا مُبَارَكًا وَأَنْتَ خَيْرُ الْمُنْزِلِينَ (29) إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ وَإِنْ كُنَّا لَمُبْتَلِينَ (30)}.
23. Na hakika tulimtuma Nuhu kwa kaumu yake, akasema, "Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu yeyote asiyekuwa Yeye. Basi je, hamwogopi?" 24. Wakasema wale wakuu waliokufuru katika kaumu yake, "Huyu si chochote isipokuwa ni mtu tu kama nyinyi. Anataka kujipa ubora juu yenu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angetaka, basi kwa yakini angeliteremsha Malaika. Hatukusikia haya kwa baba zetu wa mwanzoni." 25. Huyu si lolote isipokuwa ni mwanamume mwenye wazimu. Basi mngojeeni tu kwa muda." 26. Akasema
(Nuhu), "Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa kuwa wamenikanusha." 27. Tukamfunulia wahyi kwamba, "Unda jahazi mbele ya macho yetu na ufunuo wetu! Na itakapofika amri yetu na ikafurika tanuri, hapo waingize ndani yake kutoka kwa kila jozi, dume na jike, na ahali zako, isipokuwa yule ambaye katika wao juu yake imekwisha tangulia kauli. Wala usiniongeleshe kuhusu hao waliodhulumu. Kwani hao bila ya shaka watazamishwa. 28. Basi utakapotulia sawasawa wewe na wale walio pamoja nawe humo merikebuni,
sema: Alhamdulillahi
(Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu), aliyetuokoa kutoka kwa kaumu madhalimu! 29.
Na sema: Mola wangu Mlezi! Niteremshe mteremsho wenye baraka, na Wewe ndiye Mbora wa wateremshaji. 30. Hakika katika hayo zipo ishara. Na kwa yakini Sisi ni wenye kuwajaribu.
#
{23} يذكر تعالى رسالة عبده ورسوله نوح عليه السلام أول رسول أرسله لأهل الأرض، فأرسله إلى قومه، وهم يعبدون الأصنام، فأمرهم بعبادة الله وحده، فقال: {يا قوم اعبُدوا الله}؛ أي: أخلصوا له العبادة؛ لأنَّ العبادة لا تصحُّ إلا بإخلاصها. {ما لكم من إلهٍ غيره}: فيه إبطال ألوهيَّة غير الله وإثباتُ الإلهيَّة لله تعالى؛ لأنَّه الخالق الرازق الذي له الكمالُ كلُّه، وغيرُه بخلاف ذلك. {أفلا تتَّقون}: ما أنتم عليه من عبادة الأوثان والأصنام التي صُوِّرت على صور قوم صالحين، فعبدوها مع الله؟
{23} Mwenyezi Mungu Mtukufu anataja ujumbe wa mja wake na mtume wake Nuhu, amani iwe juu yake, mtume wa kwanza aliyemtuma kwa watu wa ardhi, kwa hivyo akamtuma kwa kaumu yake. Nao walikuwa wakiabudu masanamu, na akawaamuru wamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na akasema, "Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu." Yaani, mfanyieni Yeye tu ibada, kwa sababu ibada haiwi sahihi isipokuwa tu kama amekusudiwa yeye tu kwayo. "Nyinyi hamna mungu yeyote asiyekuwa Yeye." Na hili ndani yake kuna kubatilisha uungu wa asiyekuwa Mwenyezi Mungu na kuthibitisha uungu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa maana, Yeye ndiye Muumba tu, Mwenye kuruzuku, ambaye ana ukamilifu wote, na wengine wote ni kinyume na hayo. "Basi je, hamwogopi," kuabudu kwenu sanamu na viabudiwavyo vingine ambavyo vilipewa sura za watu wema, na wakaviabudu pamoja na Mwenyezi Mungu?
#
{24} فاستمرَّ على ذلك يدعوهم سرًّا وجهاراً وليلاً ونهاراً ألف سنة إلاَّ خمسين عاماً، وهم لا يزدادون إلاَّ عتوًّا ونفوراً، {فقال الملأ}: من قومه الأشرافُ والسادة المتبوعون على وجه المعارضة لنبيِّهم نوح والتحذير من اتِّباعه: {ما هذا إلاَّ بشرٌ مثلُكم يريد أن يَتَفَضَّلَ عليكم}؛ أي: ما هذا إلاَّ بشرٌ مثلُكم، قصدُهُ حين ادَّعى النبوَّة أن يزيد عليكم فضيلة ليكون متبوعاً، وإلاَّ؛ فما الذي يفضِّله عليكم وهو من جنسكم؟! وهذه المعارضة لا زالت موجودة في مكذِّبي الرسل، وقد أجاب الله عنها بجوابٍ شافٍ على ألسنة رسله؛ كما في قوله: {قالوا}؛ أي: لرسلهم. {إنْ أنتُم إلاَّ بشرٌ مثلُنا تريدونَ أنْ تصدُّونا عمَّا كان يعبدُ آباؤنا فأتونا بسلطانٍ مبينٍ. قالَت لهم رسلُهم إن نحنُ إلاَّ بشرٌ مثلُكُم ولكنَّ الله يَمُنَّ على مَن يشاء من عبادِهِ}: فأخبروا أنَّ هذا فضلُ الله ومنَّته، فليس لكم أن تحجُروا على الله، وتمنَعوه من إيصال فضلِهِ علينا.
وقالوا أيضاً: {ولو شاء الله لأنزلَ ملائكةً}: وهذه أيضاً معارضةٌ بالمشيئة باطلةٌ؛ فإنَّه وإنْ كان لو شاء لأنزل ملائكة؛ فإنَّه حكيمٌ رحيمٌ، حكمتُه ورحمته تقتضي أن يكونَ الرسول من جنس الآدميِّين؛ لأنَّ الملائكة لا قدرة لهم على مخاطبتِهِ، ولا يمكن أن يكون إلاَّ بصورة رجل، ثم يعود اللبسُ عليهم كما كان. وقولهم: {ما سمعنا بهذا}؛ أي: بإرسال الرسول {في آبائنا الأوَّلينَ} وأيُّ حجَّة في عدم سماعِهم إرسالَ رسول في آبائهم الأولين؟! لأنَّهم لم يحيطوا علماً بما تقدَّم؛ فلا يجعلون جهلهم حجَّةً لهم! وعلى تقدير أنَّه لم يرسل منهم رسولاً: فإما أن يكونوا على الهدى؛ فلا حاجة لإرسال الرسول إذ ذاك، وإما أن يكونوا على غيره؛ فليحمدوا ربَّهم ويشكروه أن خصَّهم بنعمةٍ لم تأتِ آباءهم ولا شعروا بها، ولا يجعلوا عدم الإحسان على غيرهم سبباً لكفرِهم للإحسان إليهم.
{24} Basi akaendelea hivyo kuwalingania kwa siri, waziwazi, usiku na mchana kwa miaka elfu moja, isipokuwa miaka hamsini. Na wao wakawa hawazidishi isipokuwa kiburi na kujiweka mbali. "Wakasema wale wakuu" kutoka katika kaumu yake, waheshimiwa na mabwana wanaofuatwa, kwa njia ya kumpinga Nabii wao Nuhu na kutahadharisha dhidi ya kumfuata, "Huyu si chochote isipokuwa ni mtu tu kama nyinyi. Anataka kujipa ubora juu yenu;" ili ufuatwe. Vinginevyo, ni nini kinachomfanya kuwa bora zaidi yenu, naye ni wa aina yenu? Na upinzani huu haujaacha kuwapo katika wale wanaowakadhibisha Mitume. Na Mwenyezi Mungu alijibu hilo kwa jibu la kutosha, juu ya ndimi za Mitume wake. Kama katika kauli yake, "Wakasema;" yaani, wakiwaambia mitume wao, "Nyinyi si chochote isipokuwa watu kama sisi. Mnataka kutuzuilia na yale waliyokuwa wakiabudu baba zetu. Basi tuleteeni hoja iliyo wazi.
Mitume wao wakawaambia: Sisi kweli si chochote isipokuwa ni watu kama nyinyi. Lakini Mwenyezi Mungu humfanyia hisani amtakaye katika waja wake." Basi wakawajulisha kwamba hii ni fadhila ya Mwenyezi Mungu na neema yake. Nanyi hamuwezi kumkataza Mwenyezi Mungu, na kumzuia kutufikishia fadhila yake. Pia wakasema, "Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angetaka, basi kwa yakini angeliteremsha Malaika." Na hili pia ni pingamizi batili la kutumia majaliwa ya Mwenyezi Mungu kuwa ndiyo hoja. Kwani, hata kama angelitaka, angeliteremsha Malaika, yeye ni Mwenye hekima, Mwingi wa kurehemu. Hekima yake na rehema yake vinataka kwamba Mtume awe wa jamii ya binadamu, kwa sababu wao hawana uwezo wa kuwaongelesha Malaika, wala hawezi kuwa isipokuwa na umbo la mtu, kisha tena watachanganyikiwa tu kama ilivyokuwa. Na kauli yao, "Hatukuyasikia haya" ya kumtuma Mtume "kwa baba zetu wa mwanzoni." Lakini kuna hoja gani kwamba hawakusikia kutumwa kwa Mtume kwa baba zao wa mwanzoni? Kwa sababu wao hawakuzunguka kwa elimu hayo yaliyopita kitambo. Kwa hivyo hawafanyi kutumia ujinga wao kuwa ndiyo hoja yao! Na hata ikiwa itachukuliwa kwamba hakumtuma mtume kutoka kwao, basi ima wao walikuwa katika uwongofu, kwa hivyo hakuna haja ya kumtuma mtume wakati huo, au walikuwa vinginevyo, kwa hivyo hawa na wamsifu na kumshukuru Mola wao Mlezi kwa sababu aliwateua kwa neema ambayo haikuwahi kuwafikia baba zao wala hawakuwahi kuihisi, na tena hawafai kufanya kutoneemeshwa wengineo kuwa ndiyo sababu ya kukufuru kwao wema waliofanyiwa wao.
#
{25} {إنْ هو إلاَّ رجلٌ به جِنَّةٌ}؛ أي: مجنون، {فتربَّصوا به}؛ أي: انتظروا به {حتى حينٍ}: إلى أن يأتيه الموت.
وهذه الشبه [التي] أوردوها معارضةً لنبوَّة نبيِّهم دالةٌ على شدَّة كفرهم وعنادهم وعلى أنَّهم في غاية الجهل والضَّلال؛ فإنَّها لا تَصْلُحُ للمعارضة بوجهٍ من الوجوه؛ كما ذكرنا، بل هي في نفسها متناقضةٌ متعارضة؛ فقوله: {ما هذا إلاَّ بشرٌ مثلُكُم يريدُ أن يتفضَّلَ عليكُم}؛ أثبتوا أنَّ له عقلاً يكيدُهم به ليعلُوَهم ويسودَهم، ويحتاجُ مع هذا أن يُحْذَرَ منه لئلاَّ يُغترَّ به؛ فكيف يلتئم مع قولهم: {إنْ هو إلاَّ رجلٌ به جِنَّةٌ}؟! وهل هذا إلا من مشبِّهٍ ضالٍّ، منقلبٍ عليه الأمر، قصده الدفع بأيِّ طريق اتَّفق له، غير عالم بما يقول. ويأبى الله إلاَّ أنْ يُظْهِرَ خِزْيَ مَن عاداه وعادى رسله.
{25} "Huyu si lolote isipokuwa ni mwanamume mwenye wazimu. Basi mngojeeni tu kwa muda," mpaka kifo kitakapomfikia. Na hizi fikira potofu
[ambazo] walizitumia ili kupinga unabii wa nabii wao, zinaonyesha ukubwa wa ukafiri wao na ukaidi wao, na kwamba wao ni wajinga sana na wapotofu wa mwisho. Kwa maana, hizo hazifai kutumiwa kupinga kwa njia yoyote ile, kama tulivyotaja. Bali hizo zenyewe zinaangushana na kukinzana. Kwa hivyo, kauli yake, "Huyu si chochote isipokuwa ni mtu tu kama nyinyi. Anataka kujipa ubora juu yenu." Walithibitisha kwamba ana akili anayowadanganya kwayo ili awashinde na awe bwana juu yao, na anahitaji pamoja na hayo kutahadhariwa ili wasidanganyike naye. Basi inawezaje kauli hii kupatanishwa na kauli yao, "Huyu si lolote isipokuwa ni mwanamume mwenye wazimu?" Je, hili si isipokuwa kutoka kwa mfananishaji, mpotofu, aliyegeukiwa na mambo, ambaye nia yake ni kuzuia haki kwa njia yoyote ile anayokubaliana nayo, ambaye hajui anachosema? Naye Mwenyezi Mungu anakataa isipokuwa kudhihirisha hizaya ya mwenye kumfanyia uadui na kuwafanyia uadui Mitume wake.
#
{26} فلما رأى نوحٌ أنَّه لا يفيدُهم دعاؤه إلاَّ فراراً؛ {قال ربِّ انْصُرْني بما كذَّبونِ}: فاستنصر ربَّه عليهم غضباً لله حيث ضيَّعوا أمره وكذَّبوا رسله. وقال: {ربِّ لا تَذَرْ على الأرضِ من الكافرين دَيَّاراً. إنَّك إن تَذَرْهُم يُضِلُّوا عبادَكَ ولا يَلِدوا إلاَّ فاجراً كفَّاراً}. قال تعالى: {وَلَقَدْ نادانا نوحٌ فَلَنِعْمَ المجيبونَ}.
{26} Na Nuhu alipoona kwamba kulingania kwake hakuwafaidi isipokuwa kukimbia tu, "Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa kuwa wamenikanusha." Basi akamuomba msaada Mola wake Mlezi dhidi yao kwa sababu ya kukasirika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ambapo walipoteza amri yake, na wakawakadhibisha Mitume wake. Na akasema, "Mola wangu Mlezi! Usimwache juu ya ardhi mkaazi wake yeyote katika makafiri! Hakika ukiwaacha, watawapoteza waja wako, wala wao hawatazaa isipokuwa waovu, makafiri."Yeye Mtukufu alisema, "Na hakika Nuhu alituita, na Sisi ndio bora wa waitikiaji."
#
{27} {فأوحينا إليه}: عند استجابتنا له سبباً ووسيلةً للنجاة قبل وقوع أسبابِهِ: {أنِ اصْنَع الفُلْكَ}؛ أي: السفينة {بأعيننا ووحينا}؛ أي: بأمرِنا لك ومعونتنا، وأنت في حفظنا وكلاءتنا؛ بحيث نراك ونسمعك. {فإذا جاء أمرنا}: بإرسال الطوفان الذي عُذِّبوا به، {وفار التَّنُّورُ}؛ أي: فارت الأرض وتفجَّرت عيوناً حتى محلُّ النار الذي لم تجرِ العادة إلاَّ ببعدِهِ عن الماء. {فاسْلُكْ فيها من كلٍّ زوجينِ اثنينِ}؛ أي: أدخل في الفلك من كلِّ جنس من الحيوانات ذكراً وأنثى تبقى مادةَ النسل لسائر الحيوانات التي اقتضتِ الحكمةُ الربَّانيَّة إيجادها في الأرض. {وأهلك}؛ أي: أدخلهم {إلاَّ مَن سبقَ عليه القولُ}: كابنه، {ولا تخاطِبْني في الذين ظَلَموا}؛ أي: لا تَدْعُني أن أنجيهم؛ فإنَّ القضاء والقدَرَ قد حتم. {إنَّهُم مغرقون}.
{27} "Tukamfunulia wahyi" tunapomjibu, kufanya sababu na njia ya kuokoka kabla ya kutokea kwa sababu zake, "Unda jahazi mbele ya macho yetu na ufunuo wetu!" Nawe uko katika hifadhi yetu kwa kuwa tunakuona na kukusikia. "Na itakapofika amri yetu" kwa kutuma tufani ambayo waliadhibiwa kwayo, "na ikafurika tanuri." Yaani, ardhi ikafoka, na ikapasuka chemchemi mpaka mahali yenye moto ambapo kulingana na ada maji hayapatikani hapo. "Hapo waingize ndani yake kutoka kwa kila jozi, dume na jike." Yaani, ingiza ndani ya safina kutoka katika kila aina ya wanyama, dume na jike, ili ibakie asili ya uzao wa wanyama wote ambao hekima ya Mwenyezi Mungu ilihitaji waapatikane katika ardhi. "Na ahali zako," pia waingize humo "isipokuwa yule ambaye katika wao juu yake imekwisha tangulia kauli," kama vile mwanawe. "Wala usiniongeleshe kuhusu hao waliodhulumu." Yaani, usiniombe dua kwamba niwaokoe. Kwa maana, hukumu ya majaaliwa imekwisha pitishwa. "Kwani hao bila ya shaka watazamishwa."
#
{28} {فإذا استويتَ أنت ومن مَعَكَ على الفِلك}؛ أي: علوتُم عليها واستقلَّتْ بكم في تيارِ الأمواج ولُججِ اليمِّ؛ فاحْمَدوا الله على النجاة والسلامة. وقل: {الحمدُ لله الذي نجَّانا من القوم الظالمينَ}: وهذا تعليمٌ منه له ولمن معه أن يقولوا هذا شكراً له وحمداً على نَجاتِهِم من القوم الظالمين في عملهم وعذابهم.
{28} "Basi utakapotulia sawasawa wewe na wale walio pamoja nawe humo marikebuni," katika mikondo ya mawimbi na vilindi vya bahari, basi msifu Mwenyezi Mungu kwa kuwaokoa na kuwaweka salama. Na sema, "Alhamdulillahi
(Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu), aliyetuokoa kutoka kwa kaumu madhalimu!" Haya ni mafundisho kutoka kwake kwamba wayaseme haya ili kumshukuru na kumsifu kwa kuwaokoa kutoka kwa kaumu madhalimu katika matendo yao na pia kutokana na adhabu yao.
#
{29} {وقل ربِّ أنزِلْني منزلاً مباركاً وأنت خير المنزِلينَ}؛ أي: وبقيتْ عليكُم نعمةٌ أخرى؛ فادعوا الله فيها، وهي أن ييسِّرَ الله لكم منزلاً مباركاً، فاستجاب الله دعاءه؛ قال الله: {وقُضِيَ الأمرُ واستوتْ على الجوديِّ وقيل بُعداً للقوم الظَّالمين ... } إلى أن قال: {قيلَ يا نوحُ اهبِطْ بسلام منَّا وبركاتٍ عليك وعلى أمم ممَّن معكَ ... } الآية.
{29} "Na sema, Mola wangu Mlezi! Niteremshe mteremsho wenye baraka, na Wewe ndiye Mbora wa wateremshaji." Yaani, bado mna neema nyingine iliyobakia. Kwa hivyo mwombeni Mwenyezi Mungu awape hiyo pia. Nayo ni kwamba Mwenyezi Mungu awarahisishie mteremsho wenye baraka, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akaitikia dua yake. Na Mwenyezi Mungu akasema, "Na amri hiyo ikapitishwa, na
(jahazi) likasimama juu ya
(mlima) wa Al-Juudiy.
Na ikasemwa: Wapotelee mbali kaumu madhalimu!" Mpaka aliposema, "Ikasemwa, 'Ewe Nuhu! Shuka kwa salama itokayo kwetu, na baraka nyingi juu yako na juu ya wale walio pamoja nawe...'" hadi mwisho wa Aya.
#
{30} {إنَّ في ذلك}؛ أي: في هذه القصة {لآياتٍ}: تدلُّ على أنَّ الله وحدَه المعبود، وعلى أنَّ رسوله نوحاً صادقٌ، وأنَّ قومه كاذبون، وعلى رحمة الله بعباده؛ حيث حملهم في صُلْبِ أبيهم نوح في الفلك لما غَرِقَ أهلُ الأرض، والفلك أيضاً من آيات الله؛ قال تعالى: {ولقد تَرَكْناها آيةً فهل مِن مُدَّكِرٍ}. ولهذا جمعها هنا؛ لأنَّها تدلُّ على عدة آيات ومطالب. {وإن كنا لَمُبْتَلينَ}.
{30} "Hakika katika hayo" yaliyomo katika kisa hiki "zipo ishara" zinazoonyesha kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Muabudiwa, na kwamba Mtume wake Nuhu ni mkweli, na kwamba kaumu yake ni waongo, na rehema za Mwenyezi Mungu juu ya waja wake, ambapo aliwabeba katika katika mgongo wa baba yao Nuhu katika safina alipowazamisha wakazi wa ardhi, na pia safina hiyo ni katika ishara za Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anayekumbuka?" Na ndiyo maana akaikusanya hapa, kwa sababu zinaonyesha ishara mbalimbali na masuala kadhaa. "Na kwa yakini Sisi ni wenye kuwajaribu."
{ثُمَّ أَنْشَأْنَا مِنْ بَعْدِهِمْ قَرْنًا آخَرِينَ (31) فَأَرْسَلْنَا فِيهِمْ رَسُولًا مِنْهُمْ أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ مَا لَكُمْ مِنْ إِلَهٍ غَيْرُهُ أَفَلَا تَتَّقُونَ (32) وَقَالَ الْمَلَأُ مِنْ قَوْمِهِ الَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِلِقَاءِ الْآخِرَةِ وَأَتْرَفْنَاهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا مَا هَذَا إِلَّا بَشَرٌ مِثْلُكُمْ يَأْكُلُ مِمَّا تَأْكُلُونَ مِنْهُ وَيَشْرَبُ مِمَّا تَشْرَبُونَ (33) وَلَئِنْ أَطَعْتُمْ بَشَرًا مِثْلَكُمْ إِنَّكُمْ إِذًا لَخَاسِرُونَ (34) أَيَعِدُكُمْ أَنَّكُمْ إِذَا مِتُّمْ وَكُنْتُمْ تُرَابًا وَعِظَامًا أَنَّكُمْ مُخْرَجُونَ (35) هَيْهَاتَ هَيْهَاتَ لِمَا تُوعَدُونَ (36) إِنْ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ (37) إِنْ هُوَ إِلَّا رَجُلٌ افْتَرَى عَلَى اللَّهِ كَذِبًا وَمَا نَحْنُ لَهُ بِمُؤْمِنِينَ (38) قَالَ رَبِّ انْصُرْنِي بِمَا كَذَّبُونِ (39) قَالَ عَمَّا قَلِيلٍ لَيُصْبِحُنَّ نَادِمِينَ (40) فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ بِالْحَقِّ فَجَعَلْنَاهُمْ غُثَاءً فَبُعْدًا لِلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ (41)}.
31. Kisha baada yao tukaanzisha kizazi kingine. 32. Kisha tukawatumia Mtume miongoni mwao,
kuwaambia: Muabuduni Mwenyezi Mungu! Hamna mungu yeyote asiyekuwa Yeye. Je, hamchi? 33. Na wakubwa katika kaumu yake, wale waliokufuru na wakakadhibisha mkutano wa Akhera, na tukawastarehesha katika uhai wa dunia hii,
walisema: Huyu si chochote isipokuwa ni mtu kama nyinyi. Anakula katika mnavyokula, na anakunywa katika mnavyokunywa. 34. Kwa hivyo, nyinyi mkimtii mtu kama nyinyi, basi hakika mtakuwa hasarani. 35. Hivi anawaahidi ati mtakapokufa na mkawa udongo na mifupa, kuwa hakika mtatolewa? 36. Hayawi! Hayawi hayo mnayoahidiwa. 37. Hapana isipokuwa uhai wetu wa duniani tu, tunakufa na kuishi tu. Wala sisi hatutafufuliwa. 38. Huyu si lolote isipokuwa ni mwanamume anayemzulia Mwenyezi Mungu uongo, wala sisi sio wa kumuamini. 39.
Akasema: Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa sababu wananikanusha. 40.
(Mwenyezi Mungu) akasema: Baada ya muda mchache watakuwa wenye kujuta. 41. Basi ukawanyakua ukelele kwa haki, na tukawafanya kama takataka zinazoelea juu ya maji. Ikapotelea mbali kaumu ya madhalimu!
#
{31} لما ذكر نوحاً وقومه وكيف أهلكهم؛ قال: {ثم أنشأنا من بعْدِهم قرناً آخرينَ}: الظاهر أنَّهم ثمودُ قومُ صالح عليه السلام؛ لأنَّ هذه القصة تشبه قصتهم.
{31} Alipomtaja Nuhu na kaumu yake na jinsi alivyowaangamiza, akasema, "Kisha baada yao tukaanzisha kizazi kingine." Na dhahiri hapa ni kwamba hao walikuwa Thamud, kaumu ya Salih, amani iwe juu yake, kwa sababu kisa hiki kinafanana na kisa chao.
#
{32} {فأرسَلْنا فيهم رسولاً منهم}: من جنسِهِم يعرفون نسبه وحسبه وصدقَه؛ ليكونَ ذلك أسرعَ لانقيادِهم إذا كان منهم وأبعد عن اشمئزازِهم، فدعا إلى ما دعتْ إليه الرسلُ أممهم: {أنِ اعبدوا الله ما لكم من إلهٍ غيرُهُ}: فكلُّهم اتَّفقوا على هذه الدعوة، وهي أول دعوة يدعون بها أممهم؛ الأمر بعبادة الله، والإخبار أنَّه المستحقُّ لذلك، والنهي عن عبادة ما سواه، والإخبار ببطلان ذلك وفساده، ولهذا قال: {أفلا تتَّقونَ}: ربَّكم فتَجْتَنِبوا هذه الأوثان والأصنام.
{32} "Kisha tukawatumia Mtume miongoni mwao," ambaye walikuwa wanajua ukoo wake, hadhi yake, na ukweli wake, ili liwe hilo la kuwafanya kumfuata kwa wepesi ikiwa yeye ni miongoni mwao yuko mbali na wao kumchukia. Kwa hivyo akawalingania katika yale waliyolingania Mitume wengineo umma zao, kwamba, "Muabuduni Mwenyezi Mungu! Hamna mungu yeyote asiyekuwa Yeye." Wote walikubaliana juu ya mwito huu, ambao ndio mwito wa kwanza wanaowalingania umma wao, yaani, amri ya kumuabudu Mwenyezi Mungu, na kujulisha kwamba Yeye tu ndiye anayestahiki hilo, na kukataza kuabudu kitu kingine chochote kile, na kujulisha ubatili wake na uharibifu wake. Basi ndiyo maana akasema, "Je, hamchi," Mola wenu Mlezi, kwa hivyo mkayaepuka masanamu haya na vyote vinavyoabudiwa kando na Mwenyezi Mungu.
#
{33} فقال {الملأ من قومِهِ الذين كَفَروا وكذَّبوا بلقاءِ الآخرة وأتْرَفْناهم في الحياة الدنيا}؛ أي: قال الرؤساءُ الذين جَمَعوا بين الكفرِ والمعاندةِ وإنكار البعثِ والجزاء، وأطغاهم ترفُهم في الحياة الدُّنيا؛ معارضةً لنبيِّهم وتكذيباً وتحذيراً منه. {ما هذا إلاَّ بشرٌ مثلُكم}؛ أي: من جنسكم، {يأكُلُ ممَّا تأكُلونَ منه ويشربُ ممَّا تشرَبونَ}: فما الذي يُفَضِّلُه عليكم؟! فهلاَّ كان ملكاً لا يأكل الطعام ولا يشرب الشراب!
{33} Basi wakasema, "wakubwa katika kaumu yake, wale waliokufuru na wakakadhibisha mkutano wa Akhera, na tukawastarehesha katika uhai wa dunia hii." Nao walikuwa wamejumuisha kati ya ukafiri, ukaidi, kukanusha ufufuo na malipo, na wakavuka mipaka kwa sababu ya starehe zao katika uhai wa dunia hii. Kwa hivyo wakasema haya ili kumpinga nabii wao, na kumkadhibisha, na kuwatahadharisha watu kutokana naye. "Huyu si chochote isipokuwa ni mtu kama nyinyi. Anakula katika mnavyokula, na anakunywa katika mnavyokunywa." Basi ni kwa kitu gani anakuwa bora kuwaliko nyinyi?! Kwa nini hakuwa malaika ambaye hali chakula wala hanywi vinywaji!
#
{34} {ولئِنْ أطعتُم بشراً مثلَكم إنَّكم إذاً لخاسرونَ}؛ أي: إن تبعتُموه وجعلتُموه لكم رئيساً وهو مثلُكم؛ إنَّكم لمسلوبو العقل نادمون على ما فعلتم! وهذا من العجب؛ فإنَّ الخسارَ والندامةَ حقيقةً لمن لم يتابِعْه ولم يَنْقَدْ له، والجهلُ والسفهُ العظيم لِمَنْ تكبَّرَ عن الانقياد لبشرٍ خصَّه الله بوحيِهِ، وفضَّلَه برسالته وابتُلي بعبادة الشجر والحجر، وهذا نظيرُ قولهم: {قالوا أبشراً منَّا واحداً نتَّبِعُهُ إنَّا إذاً لفي ضلال وسُعُرٍ. أألْقِيَ الذِّكْرُ عليهِ من بَيْنِنا بل هو كذابٌ أشِرٌ}.
{34} "Kwa hivyo, nyinyi mkimtii mtu kama nyinyi, basi hakika mtakuwa hasarani." Na nyinyi mkimfuata na mkamfanya kuwa kiongozi wenu, basi hakika mtakuwa tena hamna akili, na mtajuta juu ya kile mlichofanya! Na hili ni katika maajabu. Kwa sababu hasara ya uhakika na majuto ni kwa yule ambaye hakumfuata na hakujisalimisha kwake, na ni ujinga na upumbavu mkubwa kwa yule ambaye alifanya kiburi kutomfuata mtu ambaye Mwenyezi Mungu alimteua kwa ufunuo wa wahyi, na akamboresha kwa ujumbe wake, naye mpinzani wake huyo akawa amejaribiwa kwa mtihani wa kuabudu miti na mawe. Na hii ni sawa na kauli yake,
"Wakasema: Ati tumfuate mtu mmoja katika sisi? Basi hakika hivyo sisi tutakuwa katika upotofu na kichaa! Ni yeye tu aliyeteremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote? Bali huyu ni mwongo mkubwa, mwenye kiburi!"
#
{35 - 36} فلما أنكروا رسالَتَه وَرَدُّوها؛ أنكروا ما جاء به من البعثِ بعد الموت والمجازاة على الأعمال، فقالوا: {أيَعِدُكُم أنَّكم إذا مِتُّم وكُنْتُم تُراباً وعظاماً أنَّكم مخرَجونَ. هيهاتَ هيهاتَ لما توعَدونَ}؛ أي: بعيدٌ بعيدٌ ما يعِدُكم به من البعث بعد أنْ تمزَّقتم وكنتم تراباً وعظاماً. فنظروا نظراً قاصراً، ورأوا هذا بالنسبة إلى قُدَرِهم غير ممكن، فقاسوا قدرة الخالق بقُدَرِهم، تعالى الله، فأنكروا قدرتَه على إحياء الموتى، وعجَّزوه غاية التَّعجيز، ونسوا خَلْقَهم أول مرة، وأنَّ الذي أنشأهم من العدم؛ فإعادته لهم بعد البلى أهون عليه، وكلاهما هيِّن لديه؛ فلمَ لا يُنِكْرون أول خَلْقهم ويكابرون المحسوسات ويقولون: إنَّنا لم نزل موجودين، حتى يَسْلَمَ لهم إنكارُهم البعث ويُنْتَقَل معهم إلى الاحتجاج على إثبات وجود الخالق العظيم؟! وهنا دليلٌ آخر، وهو أن الذي أحيا الأرض بعد موتها؛ إنَّ ذلك لمحيي الموتى؛ إنَّه على كل شيء قدير. وثَمَّ دليلٌ آخر، وهو ما أجاب به المنكرينَ للبعث في قوله: {بل عَجِبوا أن جاءهم مُنْذِرٌ منهم فقال الكافرونَ هذا شيءٌ عجيبٌ. أإذا مِتْنا وكُنَّا تُرابا ذلك رَجْعٌ بعيدٌ}. فقال في جوابهم: {قَدْ عَلِمْنا ما تَنْقُصُ الأرضُ منهم}؛ أي: في البِلى {وعندنا كتابٌ حفيظٌ}.
{35-36} Basi, walipoupinga ujumbe wake na kuukataa, wakakataa yale aliyokuja nayo kuhusu ufufuo baada ya kifo na malipo juu ya matendo, na wakasema, "Hivi anawaahidi ati mtakapokufa na mkawa udongo na mifupa, kuwa hakika mtatolewa?" "Hayawi! Hayawi hayo mnayoahidiwa," ya kufufuliwa baada ya kukatikakatika na kuwa udongo na mifupa. Kwa hivyo, wakawa wametazama kwa mtazamo mpungufu, na wakaliona hili kwa mujibu wa uwezo wao kwamba haliwezekani. Wakawa wamepima uwezo wa Muumba kwa uwezo wao. Ametukuka Mwenyezi Mungu na hilo. Kwa hivyo wakapinga uwezo wake wa kufufua wafu, na wakamfanya asiyeweza kabisa, na wakasahau kwamba yeye ndiye aliyewaumba mara ya kwanza, na kwamba yule aliyewaumba baada ya kutokuwepo, ni jepesi zaidi kwake kuwarudisha baada ya kuoza kwao. Na mawili hayo yote ni rahisi zaidi kwake. Kwa hivyo,
kwa nini wasikatae uumbaji wao wa kwanza na wakatae mambo ya kihisia na waseme kwamba: Sisi tutaendelea kuishi, ili kusalimike kukataa kwao ufufuo, na ili sasa iwe rahisi kuwasimamishia hoja hiyo hiyo juu ya kudhibitisha uwepo wa Muumba Mkuu? Na hapa kuna ushahidi mwingine, ambao ni kwamba yule aliyeifufua ardhi baada ya kufa kwake, basi hakika huyo anaweza kuwafufua wafu, kwani Yeye hakika ni Muweza wa kila kitu. Na tena kuna ushahidi mwingine, ambao ndio ule aliowajibu nao wale wanaokadhibisha ufufuo kwa kauli yake, "Bali wanastaajabu kwamba amewafikia mwonyaji kutoka miongoni mwao,
na wakasema makafiri: Hiki ni kitu cha ajabu." "Ati tutakapokufa na tukawa udongo...? Kurejea huko kuko mbali!" Basi akasema katika kuwajibu, "Hakika Sisi tunajua kiasi cha kila kinachopunguzwa na ardhi kutokana nao. Na kwetu kipo Kitabu kinachohifadhi vyema yote."
#
{37} {إنْ هي إلاَّ حياتُنا الدُّنيا نموتُ ونحيا}؛ أي: يموت أناس ويحيا أناس، {وما نحن بمبعوثينَ}.
{37} "Hapana isipokuwa uhai wetu wa duniani tu, tunakufa na kuishi tu. Wala sisi hatutafufuliwa."
#
{38} {إنْ هو إلا رجلٌ به جِنَّة}: فلهذا أتى بما أتى به من توحيد الله وإثبات المعادِ! {فتربَّصوا به حتى حين}؛ أي: ارفعوا عنه العقوبةَ بالقتل وغيره احتراماً له ولأنَّه مجنونٌ غيرُ مؤاخذ بما يتكلَّم به؛ أي: فلم يبقَ بزعمِهِم الباطل مجادلةٌ معه لصحَّة ما جاء به؛ فإنَّهم قد زعموا بُطلانه، وإنَّما بقي الكلام هل يوقِعون به أم لا؛ فبزعمهم أنَّ عقولَهم الرزينةَ اقتضتِ الإبقاءَ عليه وتركَ الإيقاع به مع قيام الموجب!! فهل فوق هذا العناد والكفر غاية؟!
{38} "Huyu si lolote ila ni mtu mwenye wazimu." Ndiyo sababu akaja na kile alichokuja nacho cha kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kuuthibitisha ufufuo! "Basi mngojeeni tu kwa muda." Yaani, muondoleeni adhabu ya kumuua na mengineyo kwa sababu ya kumheshimu na kwa sababu yeye ni mwendawazimu ambaye hachukuliwi kwa kile anachokizungumza. Kwa hivyo, - kulingana na madai yao batili, - hakukubakia kujadiliana naye kokote kwa sababu ya usahihi wa yale aliyokuja nayo. Kwa maana walidai kwamba yalikuwa batili, kwa hivyo mazungumzo yalibakia tu kwamba je wamuadhibu au la? Kwa hivyo kulingana na madai yao kwamba akili zao ndizo timamu zaidi, zilihitaji kumuacha na kutomuadhibu pamoja na kuwepo kwa sababu zake! Basi je, inawezekana kwenda mbali zaidi ya ukaidi huu na kufuru hii?
#
{39} ولهذا لما اشتدَّ كفرُهم ولم ينفعْ فيهم الإنذارُ؛ دعا عليهم نبيُّهم، فقال: {ربِّ انصُرْني بما كذَّبونِ}؛ أي: بإهلاكهم وخزيهم الدنيويِّ قبل الآخرة.
{39} Na ndiyo maana, ukafiri wao ulipozidi, na maonyo yakakosa kuwanufaisha. Nabii wao akawaapiza na akasema, "Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa sababu wananikanusha." Kwa hivyo waangamize na uwahizi katika dunia kabla ya Akhera.
#
{40 - 41} قال الله مجيباً لدعوته: {عمَّا قليل لَيُصْبِحُنَّ نادمينَ. فأخذتْهُمُ الصيحةُ بالحقِّ}: لا بالظلم والجَوْر، بل بالعدل وظلمهم أخذتْهُمُ الصيحةُ فأهلكَتْهم عن آخرهم. {فجعلناهم غُثاء}؛ أي: هشيماً يَبَساً بمنزلة غُثاء السيل الملقى في جَنَبات الوادي، وقال في الآية الأخرى: {إنَّا أرْسَلْنا عليهم صيحةً واحدةً فكانوا كَهَشيم المُحْتَظِر}. {فَبُعْداً للقوم الظالمين}؛ أي: أُتْبِعوا مع عذابهم البعدَ واللعنةَ والذمَّ من العالمين؛ {فما بَكَتْ عليهمُ السماءُ والأرضُ وما كانوا مُنْظَرين}.
{40-41} Mwenyzi Mungu Mtukufu alisema akimuitikia dua yake, "Baada ya muda mchache watakuwa wenye kujuta." "Basi ukawanyakua ukelele kwa haki" na si kwa dhuluma na ukandamizaji. Lakini ni kwa haki na udhalimu wao wenyewe, ndiyo ukelele ukawachukua kuwaangamiza hadi wa mwisho wao. "Tukawafanya kama takataka zinazoelea juu ya maji," kisha zikatupwa pembezoni mwa bonde. Na alisema katika aya nyingine, "Hakika Sisi tuliwatumia ukelele mmoja tu, basi wakawa kama mabua ya kujengea ua." "Ikapotelea mbali kaumu ya madhalimu!" Yaani, walifuatishwa pamoja na adhabu yao hiyo kuwekwa mbali, kulaaniwa, na kukashifiwa na walimwengu wote. "Basi mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula."
{ثُمَّ أَنْشَأْنَا مِنْ بَعْدِهِمْ قُرُونًا آخَرِينَ (42) مَا تَسْبِقُ مِنْ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسْتَأْخِرُونَ (43) ثُمَّ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا تَتْرَى كُلَّ مَا جَاءَ أُمَّةً رَسُولُهَا كَذَّبُوهُ فَأَتْبَعْنَا بَعْضَهُمْ بَعْضًا وَجَعَلْنَاهُمْ أَحَادِيثَ فَبُعْدًا لِقَوْمٍ لَا يُؤْمِنُونَ (44)}.
42. Kisha tukaleta baada yao vizazi vingine. 43. Hapana umma uwezao kutanguliza muda wake wala kuuchelewesha. 44. Kisha tukawatuma Mitume wetu, mmoja baada ya mmoja. Kila umma alipowafikia Mtume wao, walimkadhibisha. Tukawafuatanisha hawa baada ya hawa, na tukawafanya kuwa hadithi za kusimuliwa. Basi wakapotelea mbali kaumu wasioamini.
#
{42 - 43} أي: ثم أنشأنا من بعد هؤلاء المكذِّبين المعانِدين {قروناً آخرين}: كلُّ أمةٍ في وقت مسمًّى وأجل محدود، لا تتقدَّم عنه ولا تتأخَّر، وأرسَلْنا إليهم رُسُلاً متتابعةً لعلَّهم يؤمنون وينيبون، فلم يزلِ الكفرُ والتكذيب دأبَ الأمم العُصاة والكَفَرة البغاة، {كلَّ ما جاء أمَّةً رسولُها كذَّبوه}: مع أنَّ كلَّ رسول يأتي من الآيات ما يؤمن على مثلِهِ البشر، بل مجرَّد دعوةِ الرسل وشرعِهِم يدلُّ على حَقِّيَّة ما جاؤوا به.
{42-43} Yaani, baada ya hawa waliokadhibisha wakaidi tukaanzisha "vizazi vingine." Kila umma katika wakati wake maalumu uliopimwa, ambao hawawezi kuutangulia wala kuchelewa zaidi yake. Na tukatuma Mitume mfululizo huenda wakaamini na kutubu. Lakini kukufuru na kukadhibisha havikuacha kuendelea kuwa ndiyo ada ya umma waasi, makafiri, wavukao mipaka. "Kila umma alipowafikia Mtume wao, walimkadhibisha," pamoja na kwamba kila Mtume alikuwa akija na ishara ambazo mfano wake watu waliziamini. Bali hata kulingania tu kwa Mitume hao na sheria zao viliashiria uhaki wa yale waliyokuja nayo.
#
{44} {فأتْبَعْنا بعضَهم بعضاً}: بالهلاك، فلم يبقَ منهم باقيةٌ، وتعطَّلت مساكنُهم من بعدِهم، {وجَعَلْناهم أحاديثَ}: يتحدَّثُ بهم مَن بعدهم، ويكونون عبرةً للمتَّقين ونَكالاً للمكذِّبين وخزياً عليهم مقروناً بعذابهم. {فبعداً لقوم لا يؤمنونَ}: ما أشقاهم! وَتعْساً لهم! ما أخسر صفقتهم!
{44} "Tukawafuatanisha hawa baada ya hawa" kwa kuwaangamiza, na hakubakia na yeyote miongoni mwao, na makazi yao yakaharibika baada yao. "Na tukawafanya kuwa hadithi za kusimuliwa," ambazo wanazizungumzia wale walio baada yao, na wanakuwa mazingatio kwa wachamungu, na adhabu kwa wale wanaokadhibisha, na hizaya. "Basi wakapotelea mbali kaumu wasioamini," ni wa mashaka mengi namna gani! Na ni uovu mkubwa vipi ulio juu yao! Na ni mapatano yenye hasara kubwa yao haya!
{ثُمَّ أَرْسَلْنَا مُوسَى وَأَخَاهُ هَارُونَ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍ مُبِينٍ (45) إِلَى فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا عَالِينَ (46) فَقَالُوا أَنُؤْمِنُ لِبَشَرَيْنِ مِثْلِنَا وَقَوْمُهُمَا لَنَا عَابِدُونَ (47) فَكَذَّبُوهُمَا فَكَانُوا مِنَ الْمُهْلَكِينَ (48) وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ لَعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ (49)}.
45. Kisha tukamtuma Musa na kakaye, Haarun, pamoja na ishara zetu na hoja zilizo wazi. 46. Kumwendea Firauni na wakuu wake. Lakini wakatakabari, nao walikuwa kaumu majeuri. 47. Wakasema, "Je, tuwaamini watu wawili hawa kama sisi, na ambao kaumu yao ni watumwa wetu?" 48. Basi wakawakadhibisha, na wakawa miongoni mwa walioangamizwa. 49. Na hakika tulimpa Musa Kitabu ili wapate kuongoka.
Niliwahi kusoma kabla ya muda mrefu maneno ya baadhi ya wasomi, ambaye sasa siwezi kumkumbuka jina lake. Alisema kwamba baada ya Musa kutumwa na kuteremka Taurati, Mwenyezi Mungu aliondoa adhabu ya kuwaangamiza watu wote juu ya umma mbalimbali. Kwa hivyo, akaweka sheria ya kupigana jihadi na wanaokadhibisha, wafanyao ukaidi, lakini sikujua aliyatoa wapi haya. Na nilipoitafakari vyema aya hii pamoja na aya zilizoko katika Surat Al-Qasas, ikanibainikia kwa nini akasema hivyo: Ama aya hizi, Mwenyezi Mungu alitaja umma walioangamizwa kwa kufuatana namna walivyoangamizwa, kisha akajulisha kwamba alimtuma Musa baada yao na akamteremshia Taurati yenye uwongofu kwa watu, lakini kuangamia kwa Firauni hakuwezi kutatanisha. Kwa maana, hilo lilikuwa kabla ya kuteremka kwa Taurati. Ama Aya zile zilizoko katika Surat Al-Qasas, hizo ziko wazi sana. Alipotaja kuangamia kwa Firauni, akasema, "Na hakika bila ya shaka tulimpa Musa Kitabu baada ya kwisha viangamiza vizazi vya mwanzo, ili kiwafumbue macho watu, na kiwe uwongofu, na rehema, ili wapate kukumbuka." Basi hili liko wazi kwamba alimpa Kitabu baada ya kuwaangamiza umma waliovuka mipaka, na akajulisha kwamba alikiteremsha ili kuwafumbua macho watu, na kiwe uwongofu na rehema. Na huenda haya ndiyo aliyoyataja Mwenyezi Mungu katika Surat Yunus katika kauli yake, "Kisha baada yake," yaani, Nuhu "tukawatuma Mitume kwa kaumu zao. Nao wakawajia kwa Ishara zilizo wazi. Lakini hawakuwa wenye kuyaamini waliyoyakanusha kabla yake. Ndivyo kama hivyo tunavyoziba juu ya nyoyo za wavukao mipaka." "Kisha baada yao tukamtuma Musa na Haruni..." hadi mwisho wa aya. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.
#
{45} فقوله: {ثم أرسلْنا موسى}: ابن عمرانَ كليمَ الرحمن، {وأخاه هارونَ}: حين سأل ربَّه أن يُشْرِكَه في أمره فأجاب سُؤْلَه، {بآياتنا}: الدالَّة على صدقهما وصحَّة ما جاءا به، {وسلطانٍ مُبينٍ}؛ أي: حجَّة بيَّنة من قوتها أن تَقْهَرَ القلوب وتتسلَّط عليها لقوَّتها فتنقادَ لها قلوبُ المؤمنين وتقومَ الحجَّة البيِّنة على المعاندين. وهذا كقوله: {ولقد آتَيْنا موسى تسعَ آياتٍ بيِّناتٍ}: ولهذا رئيسُ المعاندين عَرَفَ الحقَّ وعاند. {فاسأل بني إسرائيلَ إذْ جاءَهم}: بتلك الآياتِ البيِّناتِ، فقال له [فرعون]: {إنِّي لأظنُّك يا موسى مسحوراً}. فقال موسى: {لقدْ علمتَ ما أنزلَ هؤلاء إلا ربُّ السمواتِ والأرض بصائرَ وإنِّي لأظنُّك يا فرعونُ مَثْبوراً}. وقال تعالى: {وجَحَدوا بها واسْتَيْقَنَتْها أنفسُهم ظُلماً وعلوًّا}.
{45} Basi kauli yake, "Kisha tukamtuma Musa," Ibn Imran, aliyezungumza na Mwingi wa rehema moja kwa moja, "na kakaye, Haarun" alipomwomba Mola wake Mlezi amshirikishe katika jambo lake hili, naye akamuitikia ombi lake; "pamoja na ishara zetu" zenye kuonyesha ukweli wao, na usahihi halali wa yale waliyokuja nayo; "na hoja zilizo wazi" ambazo kwa sababu ya nguvu zake, zilishinda nyoyo na kuwa na mamlaka juu yake, kwa hivyo zinakuwa nyoyo za waumini ni zenye kuzifuata hoja hizi, na zinasimamisha hoja juu ya wapinzani. Na hili ni sawa na kauli yake, "Na kwa yakini, tulimpa Musa ishara tisa zilizo wazi." Na ndiyo maana mkuu wa wapinzani, Firauni alijua haki na akaifanyia ukaidi. "Basi waulize Wana wa Israili alipowajia" na ishara hizo zilizo wazi, naye Firauni akamwambia, "Hakika mimi ninakuona wewe Musa umerogwa!" Musa akasema, "Wewe unajua bila ya shaka kuwa haya hakuyateremsha isipokuwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ili kuwa ni ushahidi wa kuonekana. Na hakika mimi bila ya shaka ninakuona wewe, Firauni, kuwa umekwisha angamia." Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na wakazikataa kwa dhuluma na kujivuna."
#
{46} وقال هنا: {ثم أرسَلْنا موسى وأخاه هارونَ بآياتِنا وسلطانٍ مُبينٍ. إلى فرعونَ وملئِهِ}: كهامان وغيره من رؤسائهم، {فاستَكْبَروا}؛ أي: تكبَّروا عن الإيمان بالله واستكبروا على أنبيائِهِ، {وكانوا قوماً عالينَ}؛ أي: وصفهم العلوُّ والقهرُ والفسادُ في الأرض، فلهذا صدر منهم الاستكبار، ذلك غيرُ مستكثَرٍ منهم.
Na hapa akasema, "Kisha tukamtuma Musa na kakaye, Haaruni, pamoja na ishara zetu na hoja zilizo wazi." "Kumwendea Firauni na wakuu wake. Lakini wakatakabari," kumuamini Mwenyezi Mungu na manabii wake, "nao walikuwa kaumu majeuri." Ndiyo maana wakatakabari, na hilo halikuwa kitu kigeni kwao.
#
{47} {فقالوا} كِبْراً وتيهاً وتحذيراً لضُعفاء العقول وتمويهاً: {أنؤمنُ لِبَشَرَيْنِ مثلِنا}: كما قاله مَنْ قبلَهم سواءً بسواءٍ؛ تشابهتْ قلوبُهم في الكفر، فتشابهت أقوالُهم وأفعالُهم، وجحدوا منَّةَ الله عليهما بالرسالة. {وقومُهُما}؛ أي: بنو إسرائيل. {لنا عابدونَ}؛ أي: معبَّدونَ بالأعمال والأشغال الشاقَّة؛ كما قال تعالى: {وإذْ نَجَّيْناكم من آلِ فرعونَ يسومونَكم سوءَ العذابِ يذبِّحون أبناءَكم ويستَحْيون نساءَكم وفي ذلِكُم بلاءٌ من ربِّكم عظيمٌ}: فكيف نكون تابعين بعد أن كُنَّا متبوعينَ؟! وكيف يكون هؤلاءِ رؤساءَ علينا؟! ونظيرُ قولِهِم قولُ قوم نوح: {أنؤمنُ لك واتَّبَعَكَ الأرذَلونَ}، {وما نراك اتَّبَعَكَ إلاَّ الذين هم أراذلُنا بادِيَ الرأي}.
{47} "Walisema," kwa kiburi na kuwatahadharisha wenye akili dhaifu na kugeuza uhakika wa mambo, "Je, tuwaamini watu wawili hawa kama sisi," kama walivyosema hayo hayo wale wa kabla yao, nyoyo zao zilifanana katika ukafiri wake, kwa hivyo maneno yao na vitendo vyao vikafanana, na wakaikataa neema ya ujumbe wa Mwenyezi Mungu juu yao. "Na ambao kaumu yao," yaani Wana wa Israili, "ni watumwa wetu," wanaotufanyia kazi na shughuli ngumu? Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema, "Na vile tulipowaokoa kutoka kwa watu wa Firauni waliowapa adhabu mbaya, wakiwachinja wana wenu wa kiume na wakawaacha hai wanawake wenu, na katika hayo ulikuwa ni mtihani mkubwa uliotoka kwa Mola wenu Mlezi." Basi tutawafuatwaje baada ya kwamba sisi ndio tulikuwa tukifuatwa? Na hawa wanawezaje kuwa viongozi wetu? Na mfano wa kauli yao hii, ni kaumu ya Nuhu waliposema, "Je, tukuamini wewe, ilhali wanaokufuata ni watu duni?" Na kauli yao, "Hatukuoni wewe isipokuwa ni mtu tu kama sisi, wala hatukuoni, wamekufuata isipokuwa wale walio duni katika sisi, wasiokuwa hata na akili."
#
{48} من المعلوم أن هذا لا يَصْلُحُ لدفع الحقِّ، وأنه تكذيبٌ ومعاندةٌ، ولهذا قال: {فكذَّبوهما فكانوا من المُهْلَكينَ}: في الغرقِ في البحر وبنو إسرائيل ينظُرون.
{48} Na inavyojulikana ni kwamba haya hayawezi kutumiwa kama hoja ya kuikataa haki. Huku siyo isipokuwa kukadhibisha na kufanya ukaidi. Na ndiyo maana, akasema, "Basi wakawakadhibisha, na wakawa miongoni mwa walioangamizwa," katika kuzama baharini hali ya kuwa Wana wa Israili wanatazama.
#
{49} {ولقد آتَيْنا موسى}: بعدما أهلكَ الله فرعونَ وخلَّص الشعبَ الإسرائيليَّ مع موسى وتمكَّن حينئذٍ من إقامة أمرِ الله فيهم وإظهارِ شعائرِهِ؛ وعدَه اللهُ أن ينزِّل عليه التوراةَ أربعين ليلةً، فذهب لميقاتِ ربِّه؛ قال الله تعالى: {وكَتَبْنا له في الألواح من كلِّ شيءٍ موعظةً وتفصيلاً لكلِّ شيءٍ}. ولهذا قال هنا: {لعلَّهم يهتدونَ}؛ أي: بمعرفة تفاصيل الأمر والنهي والثوابِ والعقابِ ويعرفونَ ربَّهم بأسمائِهِ وصفاتِهِ.
{49} "Na hakika tulimpa Musa," baada ya Mwenyezi Mungu kumwangamiza Firauni na kuwaokoa Wana wa Israili pamoja na Musa, kwa hivyo akaweza kusimamisha amri ya Mwenyezi Mungu miongoni mwao na kudhihirisha alama zake, Mwenyezi Mungu akamuahidi kwamba atamteremshia Taurati kwa usiku arobaini. Kwa hivyo akaenda katika miadi ya Mola wake Mlezi. Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, "Na tukamuandikia katika mbao kila kitu, mawaidha na maelezo ya kina ya mambo yote." Na ndiyo maana akasema hapa, "ili wapate kuongoka," kwa kujua maelezo ya kina ya amri, makatazo, thawabu, na adhabu, na wamjue Mola wao Mlezi kwa majina yake na sifa zake.
{وَجَعَلْنَا ابْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُ آيَةً وَآوَيْنَاهُمَا إِلَى رَبْوَةٍ ذَاتِ قَرَارٍ وَمَعِينٍ (50)}.
50. Na tukamfanya mwana wa Mariamu na mama yake kuwa ni Ishara, na tukawapa makimbilio kwenda mahali palipoinuka penye utulivu na chemchemi za maji.
#
{50} أي: وامتَنَنَّا على عيسى ابن مريم وجَعَلْناه وأمَّه من آيات الله العجيبة؛ حيث حملتْه وولدتْه من غيرِ أبٍ، وتكلَّم في المهد صبيًّا، وأجرى الله على يديه من الآيات ما أجرى. {وآوَيْناهما إلى ربوةٍ}؛ أي: مكان مرتفع، وهذا والله أعلم وقتَ وضعِها، {ذاتِ قَرارٍ}؛ أي: مستقَرٍّ وراحةٍ، {ومَعين}؛ أي: ماء جارٍ؛ بدليلِ قوله: {قد جعل ربُّكِ تحتَكِ}؛ أي: تحت المكان الذي أنت فيه لارتفاعه {سَرِيًّا}؛ أي: نهراً، وهو المَعِيْن. {وهُزِّي إليكِ بجِذْعِ النخلةِ تُساقِطْ عليك رُطَباً جَنِيًّا. فكُلي واشْرَبي وقَرِّي عيناً}.
{50} Yaani, tulimneemesha Isa mwana wa Mariamu, na tukamfanya yeye na mama yake kuwa miongoni mwa ishara za ajabu za Mwenyezi Mungu, ambapo alimbeba tumboni, na akamzaa bila ya baba, na akazungumza hali ya kuwa bado yuko mtoto mdogo katika malezi, na Mwenyezi Mungu akatendesha mikononi mwake ishara mbalimbali alizotendesha. "Na tukawapa makimbilio kwenda mahali palipoinuka" na hilo lilikuwa, - na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi, - wakati wa kuzaliwa kwake. "Penye utulivu na chemchemi za maji;" kwa ushahidi wa kauli yake, "Hakika Mola wako Mlezi amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji!" Yaani, mahali pa chini kidogo kuliko mahali ulipo. "Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu." "Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako."
{يَاأَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ (51) وَإِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاتَّقُونِ (52) فَتَقَطَّعُوا أَمْرَهُمْ بَيْنَهُمْ زُبُرًا كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ (53) فَذَرْهُمْ فِي غَمْرَتِهِمْ حَتَّى حِينٍ (54) أَيَحْسَبُونَ أَنَّمَا نُمِدُّهُمْ بِهِ مِنْ مَالٍ وَبَنِينَ (55) نُسَارِعُ لَهُمْ فِي الْخَيْرَاتِ بَلْ لَا يَشْعُرُونَ (56)}.
51. Enyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na tendeni mema. Hakika Mimi ninajua vyema mnayoyatenda. 52. Na kwa yakini huu Umma wenu ni Umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi, basi nicheni Mimi. 53. Lakini walikatiana jambo lao mapande mbalimbali. Kila kundi likifurahia kwa waliyo nayo. 54. Basi waache katika ghafla yao kwa muda. 55. Je, wanadhani ya kuwa kwa vile tunavyowapa mali na watoto. 56. Ndiyo tunawahimizia kheri? Lakini wenyewe hawatambui.
#
{51} هذا أمرٌ منه تعالى لرسلِهِ بأكل الطيِّبات التي هي: الرزق والطيِّبُ الحلال، والشكر للَّه بالعمل الصالح الذي به يَصْلُحُ القلب والبدن والدنيا والآخرة، ويخبِرُهم أنَّه بما يعملون عليم؛ فكلُّ عمل عملوه وكلُّ سعي اكتسبوه؛ فإنَّ الله يعلمه، وسيجازيهم عليه أتمَّ الجزاء وأفضلَه، فدلَّ هذا على أنَّ الرسل كلَّهم متفقون على إباحة الطيبات من المآكل وتحريم الخبائثِ منها، وأنَّهم متَّفقون على كلِّ عمل صالح، وإنْ تنوَّعت بعضُ أجناس المأموراتِ واختلفتْ بها الشرائعُ؛ فإنَّها كلَّها عملٌ صالح، ولكنْ تتفاوت بتفاوتِ الأزمنة. ولهذا؛ الأعمال الصالحة التي هي صلاحٌ في جميع الأزمنة قد اتَّفقت عليها الأنبياء والشرائع؛ كالأمر بتوحيد الله وإخلاص الدِّين له ومحبَّته وخوفِهِ ورجائِهِ والبرِّ والصدقِ والوفاءِ بالعهد وصلةِ الأرحام وبرِّ الوالدين والإحسان إلى الضعفاء والمساكين واليتامى والحنوِّ والإحسان إلى الخلق ونحو ذلك من الأعمال الصالحة، ولهذا كان أهل العلم والكُتُب السابقة والعقل حين بَعَثَ الله محمداً - صلى الله عليه وسلم - يستدلُّون على نبوَّته بأجناس ما يأمر به وينهى عنه؛ كما جرى لِهرَقْل وغيره؛ فإنَّه إذا أمر بما أمر به الأنبياءُ الذين من قبلِهِ ونهى عما نَهَوْا عنه؛ دلَّ على أنَّه من جنسهم؛ بخلاف الكذَّاب؛ فلا بدَّ أن يأمرَ بالشرِّ وينهى عن الخير.
{51} Hii ni amri kutoka kwake Yeye Mtukufu kwa Mitume wake kwamba, wale vitu vizuri ambavyo ni riziki ya halali na nzuri, na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutenda matendo mema ambayo kwayo unatengenea moyo, mwili, dunia, na Akhera. Na anawajulisha kwamba kile wanachofanya anakijua vyema. Kwa hivyo, kila tendo walilolifanya, na bidii waliyoitia, basi hakika Mwenyezi Mungu anaijua, na atawalipa juu yake kwa malipo kamili na bora zaidi. Basi hilo likaonyesha kwamba Mitume wote wanakubaliana juu ya kuruhusika vitu vizuri miongoni mwa vyakula, na kuharamishwa kwa vitu viovu miongoni mwake, na kwamba pia wanakubaliana juu ya tendo jema, hata kama kuna aina mbalimbali za yale yaliyoamrishwa, na sheria zao zikawa zimetofautiana katika hayo. Basi hayo yote ni matendo mema, lakini yanatofautiana kulingana na kutofauti kwa nyakati mbalimbali. Na ndiyo maana, manabii na sheria zao walikubaliana juu ya matendo mema ambayo ni mazuri katika nyakati zote, kama vile amri ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu, kumfanyia yeye tu Dini, kumpenda, kumhofu, kumtumaini, wema, ukweli, kutimiza agano, kuunga jamaa, kuwafanyia wazazi wema, kuwafanyia ihsani maskini, mayatima, na kuwahurumia na kuwafanyia ihsani viumbe wote na mfano wa hayo miongoni mwa matendo mema. Ndiyo maana, wanachuoni na vitabu vya zamani, na akili wakati Mwenyezi Mungu alipomtuma Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - walikuwa wakitumia ushahidi wa yale anayoamrisha na kukataza kuwa ushahidi juu ya unabii wake, kama alivyofanya Hirakli na wengineo. Kwani, ikiwa anaamuru yale ambayo Manabii waliomtangulia waliamrisha na akakataza yale waliyokataza, hilo linaonyesha kwamba yeye ni wa aina yao, tofauti na mwongo. Yeye ni lazima aamuru maovu na akataze mema.
#
{52} ولهذا قال تعالى للرسل: {وإنَّ هذه أمَّتُكم أمَّةً}؛ أي: جماعتُكم يا معشرَ الرسل {واحدةً}: متفقةً على دينٍ واحدٍ وربُّكم واحدٌ. {فاتَّقونِ}: بامتثال أوامري واجتناب زواجري. وقد أمر الله المؤمنين بما أمر به المرسلين؛ لأنَّهم بهم يَقْتَدون وخلفَهم يسلُكون، فقال: {يا أيُّها الذين آمنوا كُلوا من طيِّبات ما رَزَقْناكم واشكُروا للهِ إنْ كنتُم إيَّاه تعبُدونَ}: فالواجب على كل المنتسبين إلى الأنبياء وغيرهم أن يَمْتَثِلوا هذا ويعملوا به.
{52} Na ndiyo sababu Mwenyezi Mungu mtukufu akawaambia Mitume, "Na kwa yakini huu Umma wenu ni Umma mmoja," enyi Mitume. Kwa maana mna Dini ile ile mmoja, na Mola wenu Mlezi ni mmoja. "Basi nicheni Mimi," kwa kutekeleza amri zangu na kuepuka makemeo yangu. Na Mwenyezi Mungu aliwaamrisha Waumini kama alivyowaamrisha Mitume, kwa kuwa wao Waumini wanawaiga Mitume hao, na wanatembelea nyuma yao. Na akasema, "Enyi mlioamini! Kuleni katika vizuri tulivyowaruzuku, na mumshukuru Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu." Kwa hivyo, la wajibu kwa wote wanaojinasibisha na Manabii na wengineo ni kutekeleza haya na wayatende.
#
{53} ولكنْ أبى الظالمون المُفْتَرقُون إلاَّ عصياناً، ولهذا قال: {فتقطَّعوا أمرَهم بينَهم زُبُراً}؛ أي: تقطَّع المنتسبون إلى أتباع الأنبياء {أمْرَهم}؛ أي: دينهم {بينَهم زُبُرا}؛ أي: قطعاً. {كلُّ حزبٍ بما لديهم}؛ أي: بما عندهم من العلم والدين {فرِحون}: يزعمون أنَّهم المحقُّون، وغيرُهم على غير الحقِّ، مع أن المحقَّ منهم مَنْ كان على طريق الرُّسل من أكل الطيبات والعمل الصالح، وما عداهم فإنَّهم مبطِلون.
{53} Lakini madhalimu wanaozua uongo walikataa isipokuwa kuasi tu. Na ndiyo maana akasema, "Lakini walikatiana jambo lao mapande mbalimbali." "Kila kundi likifurahia kwa waliyo nayo," miongoni mwa elimu na dini. Na kila mmoja wao wanadai kuwa, wao ndio walio kwenye haki, na kwamba wengineo wako makosani, ingawa walio kwenye haki miongoni mwao ni wale ambao wako katika njia ya Mitume kuhusiana na kula vitu vizuri na kufanya matendo mema, na wasio kuwa hao, wote wako katika batili.
#
{54} {فَذَرْهُم في غمرتهم}؛ أي: في وسط جهلهم بالحقِّ ودعواهم أنَّهم هم المحقون {حتى حينٍ}؛ أي: إلى أن ينزِلَ العذابُ بهم؛ فإنَّهم لا ينفعُ فيهم وعظٌ، ولا يفيدُهم زجرٌ؛ فكيفَ يفيدُ بمن يزعُمُ أنَّه على الحقِّ ويطمع في دعوة غيرِهِ إلى ما هو عليه؟
{54} "Basi waache katika ghafla yao;" yaani, wako katikati ya kutojua kwao haki na kudai kwao kwamba, wao ndio walio katika haki "kwa muda," mpaka itakapowateremkia adhabu. Kwa maana, hawafaidiki kitu mawaidha wala makemeo. Kwa hivyo itamnufaishaje yule anayedai kwamba yuko katika haki, na anatamani kuwaita wengineo katika anachokilingania?
#
{55 - 56} {أيحسبونَ أنَّما نُمِدُّهُم به من مالٍ وبنينَ. نسارِعُ لهم في الخيرات}؛ أي: أيظنُّونَ أنَّ زيادتنا إيَّاهم بالأموال والأولاد دليلٌ على أنَّهم من أهل الخير والسعادة، وأنَّ لهم خيرَ الدُّنيا والآخرة، وهذا مقدَّم لهم؟! ليس الأمر كذلك؛ {بل لا يشعرونَ}: أنَّما نُملي لهم ونُمْهِلُهم ونُمِدُّهم بالنعم ليزدادوا إثماً وليتوفَّر عقابهم في الآخرة، وليغتَبِطوا بما أوتوا، حتى إذا فَرِحوا بما أوتوا؛ أخَذْناهم بغتةً.
{55-56} "Je, wanadhani ya kuwa kwa vile tunavyowapa mali na watoto." "Ndiyo tunawahimizia heri?" Yaani, je, wanafikiri kwamba namna tunanavyowaongezea mali na watoto ni ushahidi kwamba, wao ni miongoni mwa watu wema na walio na furaha, na kwamba wana heri ya dunia na Akhera, na kwamba haya ni utangulizi tu kwao? Sivyo hivyo, "Lakini wenyewe hawatambui," kwamba muhula huo tunaowapa, na neema tunazowapa ni ili waongeze dhambi ili ipatikane adhabu yao huko Akhera, na ili wafurahi kwa yale waliyopewa, na pindi watakapofurahia hayo tuliyowapa, tutawachukua kwa ghafla.
{إِنَّ الَّذِينَ هُمْ مِنْ خَشْيَةِ رَبِّهِمْ مُشْفِقُونَ (57) وَالَّذِينَ هُمْ بِآيَاتِ رَبِّهِمْ يُؤْمِنُونَ (58) وَالَّذِينَ هُمْ بِرَبِّهِمْ لَا يُشْرِكُونَ (59) وَالَّذِينَ يُؤْتُونَ مَا آتَوْا وَقُلُوبُهُمْ وَجِلَةٌ أَنَّهُمْ إِلَى رَبِّهِمْ رَاجِعُونَ (60) أُولَئِكَ يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَهُمْ لَهَا سَابِقُونَ (61) وَلَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا وَلَدَيْنَا كِتَابٌ يَنْطِقُ بِالْحَقِّ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ (62)}.
57. Kwa hakika hao ambao kwa kumwogopa Mola wao Mlezi wananyenyekea. 58. Na wale ambao Ishara za Mola wao Mlezi wanaziamini. 59. Na wale ambao Mola wao Mlezi hawamshirikishi. 60. Na wale ambao wanatoa kile walichopewa, na hali nyoyo zao zinaogopa kwa kuwa watarejea kwa Mola wao Mlezi. 61. Basi wote hao ndio wanaokimbilia katika mambo ya heri, na ndio watakaotangulia kuyafikia. 62. Na hatuitwiki nafsi isipokuwa kwa kiasi cha uwezo wake. Na tunacho kitabu kisemacho kweli. Nao hawatadhulumiwa.
Mwenyezi Mungu Mtukufu alipowataja wale waliounganisha kati ya kufanya ubaya na kukaa katika amani, wale ambao wanadai kwamba, yale anayowapa Mwenyezi Mungu katika dunia hii ni ushahidi juu ya wema wao na fadhila yao, akawataja wale waliounganisha kati ya kufanya wema na kuwa na kuhofu, akasema:
#
{57} {إنَّ الذينَ هم من خَشْيَةِ ربِّهم مشفِقونَ}؛ أي: وجِلون، مشفقة قلوبُهم، كلُّ ذلك من خشية ربِّهم؛ خوفاً أن يَضَعَ عليهم عدلَه؛ فلا يُبقي لهم حسنةً، وسوءَ ظنٍّ بأنفسهم أنْ لا يكونوا قد قاموا بحقِّ الله تعالى، وخوفاً على إيمانِهِم من الزَّوال، ومعرفةً منهم بربِّهم وما يستحقُّه من الإجلال والإكرام. وخوفُهم وإشفاقُهم يوجِبُ لهم الكفَّ عما يوجِبُ الأمرُ المخوفُ من الذُّنوب والتقصير في الواجبات.
{57} "Kwa hakika, hao ambao kwa kumwogopa Mola wao Mlezi wananyenyekea." Yaani, nyoyo zao zinahofu kwa kumuogopa Mola wao Mlezi, kwa kuhofia aje wafanyia uadilifu wake; kwa hivyo wakawa hawajabakia na mazuri yoyote, na wakazidhania nafsi zao dhana mbaya kwamba, isije ikawa hawakutekeleza haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu vyema, na kwa kuhofia imani yao isije ikaondoka, na kwa kumjua kwao vyema Mola wao Mlezi kuhusiana na utukufu anaostahiki na heshima. Na hofu yao hiyo, ikawafanya kuachana na yale yanayosababisha jambo la kuhofisha kama vile madhambi na kutotekeleza wajibu vikamilifu.
#
{58} {والذين هم بآياتِ ربِّهم يؤمنونَ}؛ أي: إذا تُلِيَتْ عليهم آياتُه؛ زادتْهم إيماناً، ويتفكَّرون أيضاً في الآيات القرآنيَّة، ويتدبَّرونها، فَيَبِينُ لهم من معاني القرآن وجلالتِهِ واتِّفاقِهِ وعدم اختلافِهِ وتناقضِهِ وما يدعو إليه من معرفة الله وخوفِهِ ورجائِهِ وأحوال الجزاء، فيحدثُ لهم بذلك من تفاصيل الإيمان ما لا يُعَبِّرُ عنه اللسانُ، ويتفكَّرون أيضاً في الآيات الأفقيَّة؛ كما في قوله: {إنَّ في خَلْقِ السمواتِ والأرضِ واختلافِ الليل والنهارِ لآياتٍ لأولي الألباب ... } إلى آخر الآيات.
(58) "Na wale ambao Ishara za Mola wao Mlezi wanaziamini." Yaani, wanaposomewa Aya zake huwazidisha Imani, na wanatafakari vile vile katika Aya za Qur-ani, na wanazizingatia, kisha wanabainikiwa na maana za Qur-ani na utukufu wake na kuafikiana kwake na kutopingana kwake, na yale inayoyalingania ya kumjua Mwenyezi Mungu na kumhofu, na kumtumaini kwake na hali za malipo. Kwa hivyo, kutokana na hayo huweza kupata undani wa Imani ambao hauwezi kuelezewa kwa ulimi. Na hutafakari vile vile katika Aya zilizoko katika upeo wa macho, kama ilivyo katika kauli yake, "Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi na kuhitalifiana usiku na mchana, ziko Ishara kwa wenye akili." hadi mwisho wa aya.
#
{59} {والذين هم بربِّهم لا يُشْرِكونَ}؛ أي: لا شركاً جليًّا؛ كاتخاذ غير الله معبوداً يدعوه ويرجوه، ولا شركاً خفيًّا؛ كالرياء ونحوه، بل هم مخلصونَ لله في أقوالهم وأعمالهم وسائر أحوالهم.
{59} "Na wale ambao Mola wao Mlezi hawamshirikishi;" yaani, hawafanyi ushirikina ulio wazi. Kama vile, kuchukua mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu kuwa ndiye mwabudiwa wao wanayemuabudu na kumtumaini, na hawafanyi ushirikina uliofichwa, kama vile kujionyesha na mengineyo. Lakini, wao ni kumnyenyekea tu Mwenyezi Mungu kwa maneno yao, matendo yao, na katika hali zao nyinginezo zote.
#
{60} {والذين يؤتونَ ما آتوْا}؛ أي: يعطون من أنفسهم مما أُمِروا به ما آتوا من كلِّ ما يقدرون عليه من صلاةٍ وزكاةٍ وحجٍّ وصدقةٍ وغير ذلك، ومع هذا {قلوبُهُم وَجِلَةٌ}؛ أي: خائفة {أنَّهم إلى ربِّهم راجِعونَ}؛ أي: خائفةٌ عند عرض أعمالها عليه والوقوف بين يديه أن تكونَ أعمالُهم غيرَ منجِّيةٍ من عذاب الله؛ لعلمِهِم بربِّهم، وما يستحقُّه من أصناف العبادات.
{60} "Na wale ambao wanatoa walichopewa," katika yale waliyoamrishwa kutoka kwa kila wanachoweza kama vile swala, zaka, hija, sadaka na mengineyo. Na pamoja na hili, "na nyoyo zao zinaogopa kuwa watarejea kwa Mola wao Mlezi," kuhusiana na wakati yatawekwa mbele yao matendo yao na watakaposimama mbele Yake, kwamba huenda matendo yao yasiweze kuwaokoa kutokana na adhabu ya Mwenyezi; kwa sababu wanamjua Mola wao Mlezi, na aina mbalimbali za ibada ambazo anastahili.
#
{61} {أولئك يسارِعونَ في الخيراتِ}؛ أي: في مَيْدان التَّسارع في أفعال الخير؛ همُّهم ما يقرِّبُهم إلى الله، وإرادتُهم مصروفةٌ فيما يُنجي من عذابِهِ؛ فكلُّ خيرٍ سمعوا به أو سَنَحَتْ لهم الفرصةُ [إليه]؛ انتهزوه وبادَروه؛ قد نَظَروا إلى أولياءِ الله وأصفيائِهِ أمامهم، ويمنةً ويسرةً؛ يسارِعون في كلِّ خيرٍ، وينافِسون في الزُّلْفى عند ربِّهم؛ فنافَسوهُم، ولمَّا كان المسابِقُ لغيرِهِ المسارِعُ؛ قد يسبِقُ لجِدِّه وتشميره، وقد لا يسبِقُ لتقصيرِهِ؛ أخبر تعالى أنَّ هؤلاء من القسم السابقين، فقال: {وهم لها}؛ أي: للخيرات، {سابِقونَ}: قد بلغوا ذِرْوَتَها، وتبارَوْا هم والرعيل الأول، ومع هذا قد سبقت لهم من الله سابقةُ السعادةِ أنَّهم سابقونَ.
{61} "Basi wote hao ndio wanaokimbilia katika mambo ya heri," na hamu yao kubwa ni yale yatakayowaleta karibu na Mwenyezi Mungu, na utashi wao umeelekea tu kwenye yale yatayowaokoa kutokana na adhabu yake. Kwa hivyo, kila jema wanalolisikia au wakapata fursa
[kulifikia], wanaichukua fursa hiyo na kuharakisha kulitekeleza. Waliwatazama vipenzi wa Mwenyezi Mungu na wateule wake mbele yao, kulianini kwao na kushoto kwao; wanakimbilia kufanya kila jambo la heri, na wanashindana katika kutafuta kuwa karibu na Mola wao Mlezi. Kwa hivyo, wakashindana nao. Na kwa vile yule anayeshindana na mwenzake anayekwenda mbio, huenda akatangulia kwa bidii yake na kujiandaa kwake vyema, au huenda asitangulie kwa sababu ya kutofanya kwake hilo vyema, Yeye Mtukufu akajulisha kwamba, hawa pia ni miongoni mwa kundi la watakaotangulia. Akasema, "Na ndio," kwa ajili ya mema "watakaotangulia kuyafikia," na wamekwisha fika kilele chake, na wakashindana wao na kizazi cha kwanza. Na pamoja na haya, tayari walikwisha pata kutoka kwa Mwenyezi Mungu, utangulizi wa furaha kwamba wao ndio watakaotangulia.
#
{62} ولما ذَكَرَ مسارَعَتَهم إلى الخيرات وَسَبْقَهم إليها؛ ربَّما وَهِمَ واهمٌ أنَّ المطلوب منهم ومن غيرهم أمرٌ غير مقدورٍ أو متعسِّر؛ أخبر تعالى أنه {لا نكلِّفُ نفساً إلاَّ وُسْعَها}؛ أي: بقدر ما تسعه ويفضُلُ من قوتها عنه، ليس ممَّا يستوعبُ قوَّتها؛ رحمةً منه وحكمةً؛ لتيسير طريق الوصول إليه، ولتعمر جادةُ السالكين في كلِّ وقت إليه. {ولَدَيْنا كتابٌ ينطِقُ بالحقِّ}: وهو الكتابُ الأوَّل الذي فيه كل شيء، وهو يطابِقُ كلَّ واقع يكون؛ فلذلك كان حقًّا. {وهم لا يُظْلَمون}: ينقص من إحسانهم، أو يزداد في عقوبتِهم وعصيانِهِم.
{62} Na Mwenyezi Mungu alipotaja kukimbilia kwao katika mambo ya heri na kutangulia kwao kwayo; huenda akafikiri mwenye kufikiri kwamba, linalotakiwa kwao na kwa wengineo ni jambo lisilowezekana au jambo gumu. Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kuwa, "Hatuitwiki nafsi yoyote isipokuwa kwa kiasi cha uwezo wake," na inabaki ina uwezo hata baadaye, na siyo chenye kumaliza nguvu zake. Na hii rehema kutoka kwake na hekima yake; ili kurahisisha njia ya kumfikia, na ili kuimarisha juhudu za wenye kumuendea katika kila wakati. "Na tunacho kitabu kisemacho kweli." Nacho ni kitabu cha kwanza ambacho ndani yake kuna kila kitu, nacho kinaafikiana na kila tukio linalotokea kwa uhalisia. Na ndiyo maana, kikawa ni kitabu cha haki. "Nao hawatadhulumiwa," kwa kupunguzwa katika mema yao, au kuzidishwa katika adhabu yao na uasi wao.
{بَلْ قُلُوبُهُمْ فِي غَمْرَةٍ مِنْ هَذَا وَلَهُمْ أَعْمَالٌ مِنْ دُونِ ذَلِكَ هُمْ لَهَا عَامِلُونَ (63) حَتَّى إِذَا أَخَذْنَا مُتْرَفِيهِمْ بِالْعَذَابِ إِذَا هُمْ يَجْأَرُونَ (64) لَا تَجْأَرُوا الْيَوْمَ إِنَّكُمْ مِنَّا لَا تُنْصَرُونَ (65) قَدْ كَانَتْ آيَاتِي تُتْلَى عَلَيْكُمْ فَكُنْتُمْ عَلَى أَعْقَابِكُمْ تَنْكِصُونَ (66) مُسْتَكْبِرِينَ بِهِ سَامِرًا تَهْجُرُونَ (67) [أَفَلَمْ يَدَّبَّرُوا الْقَوْلَ أَمْ جَاءَهُمْ مَا لَمْ يَأْتِ آبَاءَهُمُ الْأَوَّلِينَ (68) أَمْ لَمْ يَعْرِفُوا رَسُولَهُمْ فَهُمْ لَهُ مُنْكِرُونَ (69) أَمْ يَقُولُونَ بِهِ جِنَّةٌ بَلْ جَاءَهُمْ بِالْحَقِّ وَأَكْثَرُهُمْ لِلْحَقِّ كَارِهُونَ (70) وَلَوِ اتَّبَعَ الْحَقُّ أَهْوَاءَهُمْ لَفَسَدَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ وَمَنْ فِيهِنَّ بَلْ أَتَيْنَاهُمْ بِذِكْرِهِمْ فَهُمْ عَنْ ذِكْرِهِمْ مُعْرِضُونَ (71)}].
63. Lakini nyoyo zao zimefunikwa hazitambui hayo, na wanavyo vitendo vingenvyo wanavyovifanya. 64. Hata tutakapowatia katika adhabu wale waliodekezwa kwa starehe kati yao, hapo ndipo watakapoyayatika. 65. Msiyayatike leo! Hakika nyinyi hamtanusurika nasi. 66. Hakika zilikuwa Aya zangu mkisomewa, nanyi mkirudi nyuma juu ya visigino vyenu. 67. Na huku mkiitakabari na usiku mkiizungumza
(Qur-ani) kwa dharau. 68. Je, hawakuifikiri kauli, au yamewajia ambayo hayakuwafikia baba zao wa zamani? 69. Au hawakumjua Mtume wao, ndiyo maana wanamkataa? 70.
Au wanasema: Ana wazimu? Bali amewajia kwa Haki, na wengi wao wanaichukia Haki. 71. Na lau kuwa Haki ingelifuata matamanio yao, basi zingeliharibika mbingu na ardhi na waliomo ndani yake. Bali tumewaletea ukumbusho wao, nao wanajitenga mbali na ukumbusho wao.
#
{63} يخبر تعالى أنَّ قلوبَ المكذِّبين في غمرةٍ من هذا؛ أي: وسط غمرةٍ من الجهل والظُّلم والغفلة والإعراض تمنَعُهم من الوصول إلى هذا القرآن؛ فلا يهتدونَ به، ولا يصل إلى قلوبهم منه شيءٌ، {وإذا قَرَأتَ القرآنَ جَعَلْنا بينَك وبين الذين لا يؤمنون بالآخرةِ حجاباً مستوراً، وجَعَلْنا على قلوبِهِم أكِنَّةً أنْ يَفْقَهوه وفي آذانِهِم وقراً}؛ فلمَّا كانت قلوبُهم في غمرةٍ منه؛ عملوا بحسب هذا الحال من الأعمال الكفريَّة والمعاندة للشَّرع ما هو موجبٌ لعقابهم، ولكنْ {لهم أعمالٌ من دونِ}: هذه الأعمال {هم لها عاملونَ}؛ أي: فلا يستغرِبوا عدم وقوع العذاب فيهم؛ فإنَّ الله يُمْهِلُهم ليعملوا هذه الأعمال التي بقيت عليهم مما كُتِبَ عليهم؛ فإذا عملوها، واستَوْفَوها؛ انتقلوا بشرِّ حالةٍ إلى غضب الله وعقابه.
{63} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema kwamba nyoyo za wakadhibishaji ziko katika hali ya kufunikwa, haziyatambui hayo. Yaani, ziko katikati ya kughafilika kutokana na ujinga, udhalimu, kughafilika na kupeana mgongo, mambo ambayo yanawazuia kuifikia Qur-ani hii; basi hawawezi kuongoka kwayo, wala hakifiki chochote kwayo katika nyoyo zao. "Na unaposoma Qur-ani, tunaweka baina yako na wale wasioiamini Akhera pazia linalowafunika, na tunaweka vizibo juu ya nyonyo zao wasije wakaifahamu, na tunaweka kwenye masikio yao uziwi." Na kwa kuwa mioyo yao iko katika hali ya kufunikwa; haziitambui, wakafanya kwa mujibu wa hii hali vitendo vya kikafiri na vya kupinga sheria mambo ambayo yanayolazimu waadhibiwe; lakini, "wanavyo vitendo vinginevyo," mbali na hivi vitendo "wanavyovifanya," lakani wasishangae kutotokea kwa adhabu juu yao. Kwa maana hakika Mwenyezi Mungu anawapa muhula ili wafanye vitendo hivi ambavyo vilibakia katika maisha yao miongoni mwa yale waliyoandikiwa. Na watakapovifanya na wakavitimiza; wataondoka na kwenda katika hali yao mbovu kwenda kwa hasira ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake.
#
{64 - 65} {حتى إذا أخَذْنا مُتْرَفيهم}؛ أي: متنعِّميهم الذين ما اعتادوا إلاَّ التَّرفَ والرَّفاهية والنعيم، ولم تحصُل لهم المكارهُ؛ فإذا أخذْناهم {بالعذابِ}، ووجدوا مسَّه؛ {إذا هم يجأرون}: يصرُخون ويتوجَّعون؛ لأنَّه أصابهم أمرٌ خالفَ ما هم عليه، ويستغيثونَ، فيقالُ لهم: {لا تجأروا اليومَ إنَّكم منَّا لا تُنصَرونَ}: وإذا لم تأتِهِم النُّصرةُ من الله، وانقطع عنهم الغوثُ من جانِبِه؛ لم يستطيعوا نصرَ أنفسِهِم، ولم ينصُرْهم أحدٌ.
{64-65} "Hata tutakapo watia waliodekezwa;" yaani; wale matajiri ambao hawajazoea chochote isipokuwa anasa, starehe na raha, na hakuna shida zinazowapata; basi tutakapowachukua "katika adhabu," na wakahisi mguso wake; "hapo ndipo watakapoyayatika." Wanapiga kelele na wana maumivu; kwa sababu yamewasibu yaliyo kinyume na waliyokuwa juu yake, na wanaomba msaada. Basi wataambiwa; "Msiyayatike leo! Hakika nyinyi hamtanusurika nasi." Ikiwa hauwafikii usaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na msamaha kutoka kwake umekatika; hawataweza kuzinusuru nafsi zao, na hakuna yeyote atakayewanusuru.
#
{66} فكأنَّه قيل: ما السببُ الذي أوصلَهم إلى هذه الحال؟ قال: {قد كانتْ آياتي تُتْلى عليكم}: لتؤمِنوا بها وتُقْبِلوا عليها، فلم تَفْعَلوا ذلك، بل {كنتُم على أعقابِكُم تنكِصونَ}؛ أي: راجعين القهقرى إلى الخلف، وذلك لأنَّ باتِّباعهم القرآن يتقدَّمون، وبالإعراض عنه يستأخِرون، وينزلون إلى أسفل سافلين.
{66} Ni kana kwamba ilisemwa: Ni sababu gani iliyowafikisha kwenye hali hii? Akasema: "Hakika zilikuwa Aya zangu mkisomewa," ili mziamini na mzikubali, na hamkufanya hivyo, bali "nanyi mlikuwa mkirudi nyuma juu ya visigino vyenu." Yaani, kurudi nyuma, kwa sababu kwa kufuata Qur-ani wanaendelea mbele, na kwa kujiwweka mbali nayo wanarudi nyuma, na kushuka chini kabisa.
#
{67} {مستكبِرينَ به سامراً تَهْجُرونَ}: قال المفسِّرون: معناه: مستكبرين به: الضمير يعود إلى البيت المعهود عند المخاطبين أو الحرم؛ أي: متكبِّرين على الناس بسببه، تقولون: نحنُ أهلُ الحرم؛ فنحنُ أفضلُ من غيرِنا وأعلا. {سامراً}؛ أي: جماعة يتحدثون بالليل حول البيت. {تَهْجُرونَ}؛ أي: تقولون الكلامَ الهُجْرَ الذي هو القبيح في هذا القرآن؛ فالمكذِّبون كانت طريقتُهم في القرآنِ الإعراضُ عنه، ويوصي بعضُهم بعضاً بذلك، {وقال الذين كَفَروا لا تَسْمَعوا لهذا القرآن والْغَوْا فيه لعلَّكم تغلِبونَ}، وقال الله عنهم: {أفَمِنْ هذا الحديثِ تَعْجَبونَ. وتَضْحَكونَ ولا تبكونَ. وأنتم سامِدون}، {أم يقولون تقوَّلَه} فلما كانوا جامعينَ لهذه الرذائل؛ لا جَرَمَ حقَّت عليهم العقوبةُ، ولَمَّا وقعوا فيها؛ لم يكن لهم ناصرٌ ينصُرُهم ولا مغيثٌ ينقِذُهم، ويوبَّخون عند ذلك بهذه الأعمال الساقطة.
{67} "Na huku mkiitakabari na usiku mkiizungumza
(Quran) kwa dharau." Walisema wafasiri, maana yake; wanatakabari ina kwenye nyumba ya kawaida ya wanaoongea au Al-haram
(mahali patakatifu). Yaani, wanatakabari kwa watu kwa sababu yake.
Wanasema: Sisi ni watu wa Al-haram; sisi ni bora kuliko wengine na wenye daraja ya juu. "Usiku mkiizungumza
(Qur-ani);" yaani, kundi la watu wanaoizungumza usiku karibu na nyumba, "kwa dharau." Yaani, mnasema maneno ya dharau ambayo ni ya kuchukiza katika Qur-ani hii; wakanushaji ilikuwa njia yao katika hii Qur-ani ni kuikataa na kujitenga nayo, na baadhi yao wakiwahusia wengine wao kwa hilo.
"Na walio kufuru walisema: Msiisikilize Qur-ani hii, na tumieni zogo, huenda mkashinda.
" Na akasema Mwenyezi Mungu juu yao:"Je, mnayastaajabia maneno haya? Na mnacheka,
wala hamlii? Nanyi mmeghafilika?" "Au ndio wanasema: Ameitunga hii!" Walipokuwa wanajikusanya katika kufanya uovu huu; hapana shaka ilistahiki juu yao adhabu, na ilipotokea juu yao adhabu; hawakuwa naye wa kuwanusuru wao, wala mwokozi wa kuwaokoa wao,na wanakemewa juu ya hilo kwa vitendo hivi viovu.
#
{68} {أفلم يَدَّبَّروا القولَ}؛ أي: أفلا يتفكَّرون في القرآن ويتأمَّلونه ويتدبَّرونه؛ أي: فإنَّهم لو تدبَّروه؛ لأوجبَ لهم الإيمانَ، ولَمَنَعَهم من الكفرِ، ولكن المصيبةَ التي أصابتهم بسبب إعراضهم عنه. ودل هذا على أنَّ تدبُّرَ القرآن يدعو إلى كلِّ خير ويعصِمُ من كلِّ شرٍّ، والذي منعهم من تدبُّرِهِ أنَّ على قلوبِهِم أقفالُها. {أم جاءهم ما لم يأتِ آباءَهُمُ الأوَّلينَ}؛ أي: أَوَ منعهم من الإيمان أنَّه جاءهم رسولٌ وكتابٌ ما جاء آباءَهم الأوَّلين، فرضوا بسلوك طريقِ آبائِهِم الضالِّين، وعارَضوا كلَّ ما خالفَ ذلك! ولهذا قالوا هم ومن أشبههم من الكفار ما أخبر الله عنهم: {وكذلك ما أرْسَلْنا من قبلِكَ في قريةٍ من نذيرٍ إلاَّ قال مُتْرَفوها إنَّا وَجَدْنا آباءَنا على أمَّةٍ وإنَّا على آثارِهِم مُقتدونَ}. فأجابهم بقوله: {قال أوَلَوْ جئتُكم بأهدى ممَّا وَجَدْتم عليه آباءَكم} فهل تَتَّبِعونِ: إنْ كان قصدُكم الحقَّ. فأجابوا بحقيقةِ أمرِهم: {قالوا إنا بما أرسِلْتم به كافرونَ}.
{68} "Je, hawakuifikiri kauli?" Yaani, je, hawaitafakari Qur-ani, na wakaizingatia na wakaifikiri; yaani, kama wao wangeliizingatia; ingeliwawajibishia imani , na ingeliwazuia wasikufuru, bali msiba uliowapata ni kwa sababu ya kukataa kwao kufanya hivyo. Hii ilionyesha kwamba, kutafakari kwa Qur-ani kunaita katika mema yote na kukataza dhidi ya maovu yote, na lilowazuia kuitafakari Qur-ani ni kwamba, mioyo yao ina kufuli. "Au yamewajia yasiyowafikia baba zao wa zamani?" Yaani, walizuiwa kuamini kwamba aliwajia mjumbe na kitabu ambacho hakikuwafikia baba zao wa zamani, walijifaridhishia kufuata njia ya baba zao waliopotea, na wakapinga kila kitu ambacho kilikuwa kinyume na hayo! Kwa sababu hiyo,
wao na makafiri wengine kama wao walisema juu ya aliyowaambia Mwenyezi Mungu: "Na kadhalika hatukumtuma kabla yako mwonyaji kwenye mji wowote ila watu wake waliodeka kwa starehe walisema: 'Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, na sisi tunafuata nyayo zao.' Na Mwenyezi Mungu aliwajibu kwa kauli yake,
"Akasema: Nikiwajieni na mwongozo bora kuliko yale mliyowapata baba zenu juu yake je, mtanifuata," ikiwa makusidio yenu ni haki? Walijibu kwa uhakika wa hali yao, "Walisema, Hakika sisi tunayakataa hayo mliyotumwa nayo."
#
{69} وقوله: {أمْ لم يعرِفوا رسولَهم فهم له منكرونَ}؛ أي: أَوَ منعهم من اتّباع الحقِّ أنَّ رسولَهم محمداً - صلى الله عليه وسلم - غير معروفٍ عندهم فهم منكرونَ له يقولونَ: لا نعرِفُه ولا نعرِفُ صدقَه، دعونا [حتى] نَنْظُر حالَه ونسألَ عنه مَنْ له به خبرةٌ؟ أي: لم يكنِ الأمرُ كذلك؛ فإنَّهم يعرفون الرسولَ - صلى الله عليه وسلم - معرفةً تامّةً، صغيرهم وكبيرهم، يعرفون منه كلَّ خُلُق جميل، ويعرِفون صدقَه وأمانَتَه، حتى كانوا يسمُّونه ـ قبل البعثة ـ: الأمين ؛ فَلِمَ لا يصدِّقونَه حين جاءهم بالحقِّ العظيم والصدق المبين؟!
{69} Na kauli yake Mwenyezi Mungu, "Au hawakumjua Mtume wao,ndiyo maana wanamkataa?" Yaani, au walizuilika kufuata haki kwa kuwa mtume wao Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - hakuwa maarufu kwao, basi wakawa wanamkanusha wakisema, 'Hatumjui yeye wala hatujui ukweli wake, ametulingania
[mpaka] tuitafiti hali yake na tuulize kumhusu yeye kwa yule aliye na habari juu yake?' Yaani, haikuwa hivyo; hakika wao walimjua kabisa Mtume - rehema na amani za Mungu ziwe juu yake, - mdogo kwa mkubwa, wanajua kutoka kwake kila tabia nzuri, na wanajua ukweli wake na uaminifu wake, mpaka wakawa wanamwita - kabla ya utume. - Al-Amin
(Mwaminifu); basi kwa nini hawakumsadikisha alipowajia na haki kubwa na ukweli ulio wazi?
#
{70} {أم يقولونَ به جِنَّةٌ}؛ أي: جنون؛ فلهذا قال ما قال! والمجنونُ غيرُ مسموع منه، ولا عبرة بكلامه؛ لأنَّه يهذي بالباطل والكلام السخيف! قال الله في الردِّ عليهم في هذه المقالة: {بل جاءهم بالحقِّ}؛ أي: بالأمر الثابت الذي هو صدقٌ وعدلٌ لا اختلافَ فيه ولا تناقُضَ؛ فكيفَ يكونُ مَنْ جاء به، به جِنَّةٌ؟! وهلاَّ يكون إلاَّ في أعلى درج الكمال من العلم والعقل ومكارم الأخلاق! وأيضاً؛ فإنَّ في هذا الانتقال مما تقدَّم؛ أي: بل الحقيقة التي منعتهم من الإيمان أنَّه {جاءَهُم بالحقِّ وأكثرُهم للحقِّ كارهون}، وأعظمُ الحقِّ الذي جاءهم به: إخلاصُ العبادة للَّه وحده، وترك ما يُعْبَد من دون اللَّه، وقد علم كراهتهم لهذا الأمر وتعجُّبهم منه؛ فكونُ الرسول أتى بالحقِّ، وكونُهم كارهين للحقِّ بالأصل، هو الذي أوجب لهم التكذيب بالحقِّ؛ لا شكًّا ولا تكذيباً للرسول؛ كما قال تعالى: {فإنَّهم لا يكذِّبونَك ولكنَّ الظالمينَ بآياتِ الله يَجْحَدون}.
{70} "Au wanasema,
ana wazimu?" Yaani: wazimu; ndiyo maana alisema aliyosema! Na mwendawazimu hasikilizwi, na maneno yake hayana funzo, kwa sababu anaropoka uongo na maneno ya kejeli! Katika kuwajibu, Mwenyezi Mungu alisema katika maneno haya, "Bali amewajia kwa Haki;" yaani, kwa amri thabiti ambayo ni ukweli na uadilifu , ambayo haina tofauti wala utata; basi itakuwaje kwamba, aliyekuja nayo ana wazimu? Inaweza tu kuwa katika kiwango cha juu cha ukamilifu kutokana na elimu, akili na maadili mazuri! Na vile vile; katika hii kuna mwendelezo wa yale yaliyotangulia. Yaani, uhakika uliowazuia wao kuamini ni kwamba, "Amewajia kwa Haki,na wengi wao wanaichukia Haki.
" Na Haki kubwa zaidi aliowajia nayo ni: Ikhlasi kwa kumuabudu Mola pekee, na kuacha walioabudu dhidi ya Mwenyezi Mungu, na hakika alijua chuki yao juu ya jambo hili na kustaajabia kwao kwalo; na kuwa kwake Mtume alikuja kwa Haki, na kuwa kwao ni wachukivu kwa Haki kwa asili, ndilo lililowawajibishia kukanusha Haki; siyo kwamba walikuwa na shaka wala kuwakanusha Mitume. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Basi hakika wao hawakukanushi wewe, lakini hao madhalimu wanazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu.
#
{71} فإنْ قيلَ: لِمَ لم يكنِ الحقُّ موافقاً لأهوائهم؛ لأجْل أن يؤمنوا أو يُسْرِعوا الانقيادَ؟ أجاب تعالى بقوله: {ولوِ اتَّبَعَ الحقُّ أهواءهم لَفَسَدَتِ السمواتُ والأرضُ}: ووجهُ ذلك أنَّ أهواءهم متعلِّقة بالظُّلم والكفر والفسادِ من الأخلاق والأعمال؛ فلو اتَّبع الحقُّ أهواءهم؛ لفسدتِ السماواتُ والأرضُ؛ لفساد التصرُّف والتدبير المبنيِّ على الظُّلم وعدم العدل؛ فالسماواتُ والأرض ما استقامتا إلاَّ بالحقِّ والعدل. {بل أَتيْناهم بذِكْرِهِم}؛ أي: بهذا القرآن المذكِّر لهم بكل خيرٍ، الذي به فخرُهُم وشرفُهم حين يقومون به ويكونون به سادةَ الناس. {فهم عن ذِكْرِهِم مُعْرِضون}: شقاوةً منهم وعدمَ توفيق؛ {نَسُوا الله فَنَسِيَهم}، {نَسُوا الله فأنساهم أنفُسَهم}؛ فالقرآن ومَنْ جاء به أعظمُ نعمةٍ ساقها الله إليهم، فلم يقابلوها إلا بالردِّ والإعراض؛ فهل بعد هذا الحرمان حرمانٌ؟! وهل يكون وراءَه إلاَّ نهايةُ الخسران؟!
{71} Na ikisemwa: Kwa nini ukweli haukuambatana na matamanio, ili waamini au watiii kwa upesi? Mwenyezi alijibu kwa kauli yake, "Na lau kuwa haki ingelifuata matamanio yao, basi zingeliharibika mbingu na ardhi." Sababu ya hayo ni kwamba matamanio yao yanahusiana na dhuluma, ukafiri, na ufisadi wa maadili na matendo. Ikiwa haki ingelifuata matamanio yao, mbingu na ardhi zingeliharibika; kwa sababu ya ufisadi wa tabia na usimamizi unaotokana na dhuluma na ukosefu wa haki; basi mbingu na ardhi hazijakuwa ila kwa haki na uadilifu. "Bali tumewaletea ukumbusho wao." Yaani, kwa hii Qur-ani ambayo inawakumbusha wema wote, ambamo ndani yake kuna fahari yao na heshima yao wanapoitekeleza na huwa mabwana wa watu. "Nao wanajitenga mbali na ukumbusho wao" ni shaka kutoka kwao na kukosekana taufiki; "Wamemsahau Mwenyezi Mungu, basi na Yeye pia amewasahau." "Walimsahau Mwenyezi Mungu, na Yeye akawasahaulisha nafsi zao." Kwa hivyo Qur-ani na aliyekuja nayo ni neema kubwa zaidi aliyowaneemsha Mola kwao, na hawakuikabili ila kwa kuikataa na kujitenga mbali. Je, kuna kunyimwa zaidi baada ya kunyimwa huku? Na je, kutakuwa chochote nyuma yake isipokuwa mwisho wa hasara?
{أَمْ تَسْأَلُهُمْ خَرْجًا فَخَرَاجُ رَبِّكَ خَيْرٌ وَهُوَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ (72)}.
72. Au unawaomba ujira? Lakini ujira wa Mola wako Mlezi ni bora ,na Yeye ndiye Mbora wa wanaoruzuku.
#
{72} أي: أَوَ مَنَعَهم من اتِّباعك يا محمد أنَّك تسألُهم على الإجابة أجراً؛ {فهم من مَغْرَم مُثْقَلون}: يتكلَّفون من اتِّباعك بسبب ما تأخُذُ منهم من الأجرِ والخراج، ليس الأمر كذلك. {فخراجُ ربِّك خيرٌ وهو خير الرازقينَ}: وهذا كما قال الأنبياءُ لأممهم: {يا قوم لا أسألُكُم عليه أجراً إنْ أجرِيَ إلاَّ على الله}؛ أي: ليسوا يدعون الخلق طمعاً فيما يُصيبهم منهم من الأموال، وإنَّما يدعونَهم نُصحاً لهم وتحصيلاً لمصالحهم، بل كان الرسلُ أنصحَ للخلق من أنفسهم، فجزاهُم اللهُ عن أممهم خيرَ الجزاءِ، ورزَقَنا الاقتداء بهم في جميع الأحوال.
{72} Yaani, au walizuilika kukufuata ewe Muhammad kwa wewe uliwaitisha malipo; "Na kwa hivyo ndio wanaelemewa na uzito wa gharama." Walikataa kukufuata kwa sababu ya kile unachochukua kutoka kwao kutokana na malipo na kodi, sivyo hivyo. "Lakini ujira wa Mola wako Mlezi ni bora, na Yeye ndiye Mbora wa wanao ruzuku." Na hivi ndivyo walivyosema manabii kwa watu wao, "Na enyi watu wangu! Mimi sikuombeni ujira kwa ajili ya haya. Mimi sina ujira ila kwa Mwenyezi Mungu." Yaani, hawakuwalingania watu kwa tamaa eti watapata mali kutoka kwao, lakini wanawalingania wao ikiwa ni nasaha kwao na kwa ajili ya maslahi yao, bali walikuwa Mitume wanajinasihi zaidi kuliko watu wao, basi awalipe Mwenyezi Mungu kwa ajili ya watu wao malipo yaliyo mema,na atujaalie kuwaiga wao katika hali zote.
{وَإِنَّكَ لَتَدْعُوهُمْ إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ (73) وَإِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ عَنِ الصِّرَاطِ لَنَاكِبُونَ (74)}.
73. Na kwa yakini, wewe unawaita kwenye Njia iliyonyooka. 74. Na hakika wale wasioiamini Akhera wanajitenga na Njia hiyo.
#
{73 - 74} ذكر الله تعالى في هذه الآيات الكريمات كلَّ سببٍ موجبٍ للإيمان، وذَكَرَ الموانع، وبيَّن فسادها واحداً بعد واحدٍ، فذكر من الموانع: أنَّ قلوبَهم في غَمْرةٍ، وأنهم لم يَدَّبَّروا القول، وأنَّهم اقتدَوْا بآبائهم، وأنَّهم قالوا: برسولهم جِنَّةٌ؛ كما تقدم الكلام عليها.
وذكر من الأمور الموجبة لإيمانهم: تدبُّرُ القرآن، وتلقِّي نعمة الله بالقَبول، ومعرفة حال الرسول محمدٍ - صلى الله عليه وسلم - وكمال صدقِهِ وأمانتِهِ، وأنَّه لا يسألُهم عليه أجراً، وإنَّما سعيُهُ لنفعهم ومصلحتهم، وأنَّ الذي يَدْعوهم إليه صراطٌ مستقيمٌ، سهلٌ على العاملين لاستقامتِهِ، موصلٌ إلى المقصودِ من قرب، حنيفيَّةٌ سمحةٌ؛ حنيفيَّةٌ في التوحيد، سمحةٌ في العمل؛ فدعوتُك إيَّاهم إلى الصراط المستقيم موجب لمن يريد الحقَّ أن يَتَّبِعَك؛ لأنَّه مما تشهدُ العقول والفطر بحسنِهِ وموافقتِهِ للمصالح؛ فأين يذهبونَ إنْ لم يتابِعوك؟ فإنَّهم ليس عندهم ما يُغنيهم ويكفيهم عن متابعتِكَ؛ لأنَّهم {عن الصراط}: ناكِبون، متجنِّبون، منحرِفون عن الطريق الموصل إلى الله وإلى دار كرامته، ليس في أيديهم إلاَّ ضلالاتٌ وجهالاتٌ، وهكذا كلُّ من خالَفَ الحقَّ؛ لا بدَّ أن يكونَ منحرفاً في جميع أمورِهِ؛ قال تعالى: {فإن لم يَسْتَجيبوا لك فاعْلَمْ أنَّما يَتَّبِعون أهواءهم ومَنْ أضَلُّ مِمَّنِ اتَّبع هواه بغير هدىً من الله}.
{73-74} Katika aya hizi tukufu, Mwenyezi Mungu alitaja kila sababu inayopatisha imani, akataja vizuizi, na akabainisha yanayofisadi imani moja baada ya nyingine, na akataja katika vizuizi, kwamba mioyo yao iko katika hofu, na kwamba hawakuzingatia neno, na kwamba waliwafuata baba zao,
na kwamba walisema: Mjumbe wao ana wazimu; kama yalivyotangulia maelezo yao.
Na alitaja Mola miongoni mwa mambo ya muhimu katika imani yao: Ni kuizingatia Qur-ani, na kupokea neema za Mwenyezi Mungu kwa kuzikubali, na ufahamu wa hali ya Mtume Muhammad- rehema na amani za Mwenyezi Mungu iwe juu yake, - na ukamilifu wa ukweli wake na uaminifu wake, na kwamba yeye hawaombi ujira kwa hayo, na kwamba hakika vitendo vyake ni kwa ajili ya manufaa yao na maslahi yao, na kwamba hayo anayowalingania juu yake ndiyo njia nyoofu, iliyo sahali kwa wafanyao kwa unyoofu wake, inayowasilisha kwa makusudio kwa ukaribu zaidi, iliyo safi na nyepesi; iliyo safi katika tauhidi, nyepesi katika kuitenda; ulinganizi wako kwao katika njia iliyonyooka ni wajibu kwa anayetaka haki kukufuata; kwa sababu ni katika yale yanayoshuhudika kwa akili na maumbile kwa uzuri wake na kuwafikika kwake kwa maslahi; basi wanaenda wapi wasipokufuata wewe? Hakika wao hawana yatayowatajirisha na kuwatosheleza dhidi ya kukufuata wewe Mtume, kwa kuwa wao "katika njia." Wamejitenga, wamejiepusha, wamepotoka katika njia inayofikisha kwa Mwenyezi Mungu na katika nyumba ya karama zake. Hawana katika mikono yao ila upotefu na ujinga, na hivi hivi ndivyo alivyo kila aliyekhalifu haki. Hapana budi ila atakuwa mpotefu katika mambo yake yote. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na ikiwa hawakuitikii, basi jua kuwa wanafuata pumbao lao tu. Na nani aliyepotea zaidi kumshinda anayefuata pumbao lake bila ya uwongofu utokao kwa Mwenyezi Mungu."
{وَلَوْ رَحِمْنَاهُمْ وَكَشَفْنَا مَا بِهِمْ مِنْ ضُرٍّ لَلَجُّوا فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ (75) وَلَقَدْ أَخَذْنَاهُمْ بِالْعَذَابِ فَمَا اسْتَكَانُوا لِرَبِّهِمْ وَمَا يَتَضَرَّعُونَ (76) حَتَّى إِذَا فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَابًا ذَا عَذَابٍ شَدِيدٍ إِذَا هُمْ فِيهِ مُبْلِسُونَ (77)}.
75. Na lau tungeliwarehemu na tukawaondolea shida waliyo nayo, bila ya shaka wangeliendelea katika upotofu wao, vile vile wakitangatanga. 76. Na hakika tuliwatia adhabu kali; lakini hawakuelekea kwa Mola wao Mlezi wala hawakunyenyekea. 77. Mpaka tulipowafungulia mlango wa adhabu, hapo ndipo wakawa wenye kukata tamaa.
#
{75} هذا بيانٌ لشدَّة تمرُّدهم وعنادهم، وأنَّهم إذا أصابهم الضُّرُّ؛ دَعَوُا الله أن يكشف عنهم ليؤمنوا، أو ابتلاهم بذلك ليرجعوا إليه؛ أنَّ الله إذا كشف الضُّرَّ عنهم؛ {لَجُّوا}؛ أي: استمرُّوا {في طُغيانهم يَعْمَهون}؛ أي: يجولون في كفرهم حائرينَ متردِّدين؛ كما ذكر الله حالهم عند ركوب الفُلك، وأنَّهم يدعون مخلصين له الدينَ، وينسَوْن ما يشركُون به، فلما أنجاهم؛ إذا هم يَبْغونَ في الأرض بالشِّرْك وغيره.
75} Hii ni taarifa ya ukali wa uasi wao na ukaidi wao, na kwamba ikiwa madhara yatawapata, wanamwomba Mungu awaondolee ili waweze kuamini, au awatahini kwa hilo ili waweze kurudi kwake. Kwamba anapowaondolea Mwenyezi Mungu shida juu yao, "wanaendelea." Yaani, wanaendelea "katika upotofu wao, vile vile wakitangatanga." Yaani, wanatangatanga katika ukafiri wao wakiwa wamechanganyikiwa wakisitasita; kama alivyotaja Mwenyezi Mungu hali zao wanapopanda safina, na kwamba wao humwomba kwa dhati muda huo, na husahau ushirikina wao juu yake, na anapowaokoa; hufanya dhuluma katika ardhi kwa kufanya shirki na mengine.
#
{76} {ولقد أخَذْناهم بالعذابِ}: قال المفسِّرونَ: المرادُ بذلك الجوع الذي أصابهم سبع سنين، وأنَّ الله ابتلاهم بذلك ليرجِعوا إليه بالذُّلِّ والاستسلام، فلم ينجَعْ فيهم، ولا نَجَحَ منهم أحدٌ. {فما استَكانوا لربِّهم}؛ أي: خضعوا وذلُّوا، {وما يتضرَّعون}: إليه ويفتقرون، بل مرَّ عليهم ذلك ثم زال كأنه لم يُصِبْهم، لم يزالوا في غيِّهم وكفرهم.
{76} "Na hakika tuliwatia adhabu kali." Walisema wafasiri, maana ya njaa ile iliyowasibu kwa miaka saba, na kwamba Mwenyezi Mungu aliwatahini kwa hayo ili wamrudie Yeye kwa kunyenyekea na kujisalimisha, haikufanya kazi kwao, wala hakufaulu yeyote miongoni mwao. "Lakini hawakuelekea kwa Mola wao Mlezi;" yaani, kunyenyekea na kujisalimisha, "wala hawakunyenyekea" kwake Yeye Mola na wakawa mafukara, bali yaliwapitia hayo kisha yakatoweka kana kwamba hayakuwasibu, nao hawakuondoka katika upotovu wao na ukafiri wao.
#
{77} ولكن وراءهم العذاب الذي لا يردُّ، وهو قوله: {حتى إذا فَتَحْنا عليهم بابًا ذا عذابٍ شديدٍ}: كالقتل يومَ بدرٍ وغيره؛ {إذا هم فيه مُبْلِسونَ}: آيِسون من كلِّ خيرٍ، قد حَضَرَهم الشرُّ وأسبابُه؛ فليحْذَروا قبل نزول عذاب الله الشديد، الذي لا يردُّ؛ بخلاف مجرَّد العذاب؛ فإنَّه ربما أقلع عنهم؛ كالعقوبات الدنيويَّة التي يؤدِّب الله بها عبادَه؛ قال تعالى فيها: {ظَهَرَ الفسادُ في البرِّ والبحر بما كَسَبَتْ أيدي الناسِ لِيذُيقَهم بعضَ الذي عَمِلوا لعلَّهم يرجِعونَ}.
{77} Lakini nyuma yao kuna adhabu isiyoweza kuzuilika,
ambayo ni kauli yake: "Mpaka tulipowafungulia mlango wa adhabu kali," kama vifo vya siku ya Badr na nyinginezo. "Hapo ndipo wakawa wenye kukata tamaa," wamekata tamaa kutokana na kila heri, imeshawajia shari na sababu zake; basi wajihadhari kabla kushuka adhabu ya Mwenyezi Mungu kali, ambayo haiepukiki; kwa kuhalifu inapaswa adhabu. Na hakika Yeye Mola huenda anawaondolea wao; kama adhabu za kidunia ambazo kwamba huwatia adabu kwazo waje wake. Amesema Mwenyezi Mtukufu kuzihusu, "Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyoyafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonjeshe baadhi ya waliyoyatenda. Huenda wakerejea kwa kutubu."
{وَهُوَ الَّذِي أَنْشَأَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ قَلِيلًا مَا تَشْكُرُونَ (78) وَهُوَ الَّذِي ذَرَأَكُمْ فِي الْأَرْضِ وَإِلَيْهِ تُحْشَرُونَ (79) وَهُوَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ وَلَهُ اخْتِلَافُ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ أَفَلَا تَعْقِلُونَ (80)}.
78. Na Yeye ndiye aliyewaumbia kusikia na kuona na nyoyo za kufahamu. Ni kuchache mno kushukuru kwenu. 79. Na Yeye ndiye aliye aliyewaeneza katika ardhi, na kwake Yeye mtakusanywa. 80. Na Yeye ndiye anayehuisha na kufisha, na ni yake Yeye mabadiliko ya usiku na mchana. Basi je, hamfahamu?
#
{78} يخبرُ تعالى بِمِنَنِه على عباده الدّاعي لهم إلى شكرِهِ والقيام بحقِّه، فقال: {وهو الذي أنشأ لكم السمعَ}: لِتُدْرِكوا به المسموعاتِ فَتَنْتَفِعوا في دينِكم ودُنْياكم، {والأبصارَ}: لِتُدْرِكوا بها المُبْصَراتِ فتنتفِعوا بها في مصالِحِكم، {والأفئدةَ}؛ أي: العقول التي تدرِكون بها الأشياءَ وتتميَّزون بها عن البهائم؛ فلو عدِمْتُم السمعَ والأبصارَ والعقولَ بأن كنتم صمًّا عمياً بكماً؛ ماذا تكونُ حالكم؟ وماذا تفقِدون من ضروريَّاتِكم وكمالكم؟ أفلا تشكُرون الذي منَّ عليكُم بهذه النِّعم؛ فتقومون بتوحيدِهِ وطاعتِهِ؟ ولكنَّكم قليلاً شكركم مع توالي النعم عليكم.
{78} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaeleza yale aliyowapa waja wake, akiwalingania kumshukuru na kutekeleza haki zake.
Akasema: “Na ndiye aliyewaumbia kusikio” ili kwa hayo mpate kuyajua yanayosikika na kunufaika katika nafsi zenu, dini yenu na maisha yenu ya kidunia.
“Na macho;” ili mpate kuyaona yanayoonekana na mpate kufaidika nayo kwa maslahi yenu, “na nyoyo.” Yaani, akili ambayo kwamba mnapata kujua nayo vitu na mnatofautika kwayo kutoka kwa wanyama. Basi lau mngelikosa masikio na macho na akili kwamba mngelikuwa viziwi na vipofu na bubu; ingelikuwaje hali yenu? Je, mnapoteza nini katika mahitaji yenu na ukamilifu wenu? Basi je, hamumshukuru yule aliyekufanyieni hisani kwa neema hizi; basi mkasimama katika kumpwekesha na kumtii? Lakini kushukuru kwenu ni kudogo, pamoja na mfululizo wa neema juu yenu.
#
{79} {وهو}: تعالى {الذي ذَرَأَكم في الأرض}؛ أي: بثَّكم في أقطارها وجهاتها، وسلَّطكم على استخراج مصالحها ومنافعها، وجعلها كافيةً لمعايِشِكُم ومساكِنِكم. {وإليه تُحْشَرون}: بعد موتِكُم فيجازيكم بما عَمِلْتُم في الأرض من خيرٍ وشرٍّ، وتُحدِّث الأرضُ التي كنتُم فيها بأخبارها.
{79} "Na Yeye," Mtukufu "ndiye aliyewaenezeni katika ardhi." Yaani, aliwaenezeni katika pande zake na maeneo yake, na akawapa uwezo wa kuchukua kwayo yaliyo mazuri na yenye manufaa, na akaijalia ni yenye kutosheleza kwa maisha yenu na makazi yenu. "Na kwake Yeye mtakusanywa," baada ya kufa kwenu na atawalipeni kwa yale mliyoyafanya mema na mabaya, na itasimulia ardhi mliyokuwa ndani yake habari zake.
#
{80} {وهو}: تعالى وحدَه {الذي يُحيي ويُميتُ}؛ أي: المتصرِّف في الحياة والموت هو الله وحده. {وله اختلافُ الليل والنهار}؛ أي: تعاقُبُهما وتناوُبُهما؛ فلو شاء أنْ يجعلَ النهار سرمداً، مَن إلهٌ غيرُ الله يأتيكم بليل تسكنون فيه؟ ولو شاء أن يجعل الليل سرمداً من إلهٌ غيرُ الله يأتيكم بضياءٍ أفلا تُبْصِرونَ؟ ومن رحمتِهِ جَعَلَ لكُم الليلَ والنهار لِتَسْكُنوا فيه ولِتَبْتَغوا من فضلِهِ ولعلَّكم تشكُرون. ولهذا قال هنا: {أفلا تعقلون}؛ فتعرِفون أنَّ الذي وَهَبَ لكم من النِّعم السمعَ والأبصارَ والأفئدةَ، والذي نَشَرَكم في الأرض وحدَه، والذي يُحيي ويُميت وحدَه، والذي يتصرَّف بالليل والنهار وحدَه؛ إنَّ ذلك موجبٌ لكم أن تُخْلِصوا له العبادة وحدَه لا شريك له، وتترُكوا عبادةَ مَنْ لا ينفَعُ ولا يضرُّ ولا يتصرَّف بشيء، بل هو عاجزٌ من كلِّ وجهٍ؛ فلو كان لكم عقلٌ؛ لم تَفْعَلوا ذلك.
{80}"Na Yeye," Mtukufu aliye pekee "anayehuisha na kufisha;" yaani, yule anayebadilisha katika uhai na umauti ni Mwenyezi Mungu pekee yake. "Na ni yake Yeye mabadiliko ya usiku na mchana." Yaani, kufuatana kwake na kupishana kwake; basi lau angelipenda kufanya mchana kuwa ni wa kudumu, basi ni nani mungu asiyekuwa Mwenyezi Mungu ambaye angeliwaleteeni usiku mpate kutulia humo? Na lau angeliufanya usiku ukawa wa kudumu ni mungu yupi asiyekuwa Mwenyezi Mungu, angeliwaleteeni mwangaza, hamuoni? Na kwa rehema zake amewafanyieni usiku na mchana mpate kutulia kwayo, na ili mpate kutafuta kutokamana na fadhila zake, na ili mpate kushukuru. Na kwa ajili ya hili alisema Mwenyezi Mungu hapa; "Je, hamfahamu," mkapata kujua kwamba aliyewapeni kutokana na neema ya kusikia na kuona na nyoyo, na ambaye amewaenezeni ardhini peke yake, na anayehuisha na kufisha peke yake, na anayebadilisha usiku na mchana peke yake. Hakika hayo yana wawajibisheni kupwekesha ibada kwake Yeye peke, asiye na mshirika naye, na kuacha kuabudu asiyenufaisha wala kudhuru wala habadilishi chochote,bali ni ajizi katika nyanja zote. Basi mngelikuwa wenye akili; msingelifanya hivyo.
{بَلْ قَالُوا مِثْلَ مَا قَالَ الْأَوَّلُونَ (81) قَالُوا أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ (82) لَقَدْ وُعِدْنَا نَحْنُ وَآبَاؤُنَا هَذَا مِنْ قَبْلُ إِنْ هَذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ (83)}.
81. Bali wanasema kama walivyosema watu wa kwanza. 82.
Walisema: Je, tukisha kufa tukawa udongo na mifupa, ndio tutafufuliwa? 83. Tuliahidiwa haya sisi na baba zetu wa zamani. Hayakuwa haya ila ni visa vya uwongo vya watu wa zamani.
#
{81 - 83} أي: بل سَلَكَ هؤلاء المكذِّبون مَسْلَكَ الأوَّلين من المكذِّبين بالبعث، واستَبْعَدوه غايةَ الاستبعاد، وقالوا: {أإذا مِتْنا وكُنَّا تراباً وعظاماً أإنا لَمَبْعوثونَ}؛ أي: هذا لا يُتَصَوَّرُ ولا يدخلُ العقل بزعمهم. {لقد وُعِدْنا نحنُ وآباؤُنا هذا من قبلُ}؛ أي: ما زلنا نوعد بأنَّ البعث كائنٌ نحن وآباؤنا، ولم نره، ولم يأت بعدُ. {إنْ هذا إلا أساطيرُ الأولينَ}؛ أي: قَصَصُهم وأسمارُهم التي يُتَحَدَّثُ بها وتُلهي، وإلاَّ؛ فليس لها حقيقةٌ، وكَذَبوا قبَّحهم الله؛ فإنَّ الله أراهم من آياتِهِ أكبرَ من البعث، ومثله: {لَخَلْقُ السمواتِ والأرضِ أكبرُ من خلق الناس}، {وضرب لنا مثلاً ونَسِيَ خَلْقَه قال مَن يُحيي العظام وهي رميمٌ ... } الآيات، {وترى الأرضَ هامدةً فإذا أنزلنا عليها الماء اهتزَّتْ ورَبَتْ ... } الآيات.
{81-83} Yaani, bali makafiri hawa waliifuata njia ya watu wa mwanzo waliokanusha kufufuliwa, na wakaitenga kwa mbali kabisa,
na wakasema: “Je, tukisha kufa tukawa udongo na mifupa ndio tutafufuliwa?" Yaani, hili haliwezekani na haliingii akilini kwa mujibu wa madai yao. "Tuliahidiwa haya sisi na baba zetu zamani." Yaani, hatujaacha kuahidiwa kwamba ufufuo utakuwapo sisi na baba zetu, wala hatuuoni, wala haujafika bado. "Hayakuwa haya ila ni visa vya uwongo vya watu wa zamani." Yaani, hadithi zao na tani zao ambazo huzungumza kuzihusu na hukengeuka, vinginevyo; basi hazina ukweli, na walikanusha akawefedhehesha Mwenyezi Mungu; kwani hakika Mwenyezi Mungu aliwaonesha kutokana na ishara zake kubwa kuliko ufufuo.
Na mfano wake: "Bila shaka kuumba mbingu na ardhi ni kukubwa zaidi kuliko kuwaumba watu," "Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake,
akasema: Ni nani huyo atakayeihuisha mifupa nayo imekwisha mung'unyika... hadi mwisho wa aya. "Na unaiona ardhi imetulia kimya, lakini tunapoyateremsha maji juu yake husisimka na kututumka... hadi mwisho wa Aya hizi.
{قُلْ لِمَنِ الْأَرْضُ وَمَنْ فِيهَا إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ (84) سَيَقُولُونَ لِلَّهِ قُلْ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ (85) قُلْ مَنْ رَبُّ السَّمَاوَاتِ السَّبْعِ وَرَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ (86) سَيَقُولُونَ لِلَّهِ قُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ (87) قُلْ مَنْ بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ يُجِيرُ وَلَا يُجَارُ عَلَيْهِ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ (88) سَيَقُولُونَ لِلَّهِ قُلْ فَأَنَّى تُسْحَرُونَ (89)}.
84.
Sema: Ni ya nani ardhi na vilivyomo ndani yake, kama nyinyi mnajua? 85.
Watasema: Ni vya Mwenyezi Mungu! Sema: Basi, je, hamkumbuki? 86.
Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu saba na Mola Mlezi wa A'rshi kuu. 87.
Watasema: Ni vya Mwenyezi Mungu. Sema, Basi, je, hamwogopi? 88.
Sema: Ni nani mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu, naye ndiye anayelinda, wala hakilindwi asichotaka, kama mnajua? 89. Watasema, "Ufalme huo" ni wa Mwenyezi Mungu.
Sema: Basi vipi mnadanganyika?"
#
{84 - 85} أي: قُلْ لهؤلاء المكذِّبين بالبعث، العادلين بالله غيرَهُ؛ محتجًّا عليهم بما أثبتوه وأقرُّوا به من توحيد الرُّبوبيَّة وانفرادِ اللهّ بها على ما أنكروه من توحيد الإلهيَّة والعبادة، وبما أثبتوه من خَلْق المخلوقات العظيمة على ما أنكروه من إعادةِ الموتى الذي هو أسهل من ذلك: {لِمَنِ الأرضُ ومَن فيها}؛ أي: مَنْ هو الخالقُ للأرض ومَنْ عليها من حيوان ونباتٍ وجمادٍ وبحارٍ وأنهارٍ وجبال، المالك لذلك، المدبِّر له؛ فإنَّك إذا سألتَهم عن ذلك؛ لا بدَّ أن يقولوا: اللهُ وحدَه. فقل لهم إذا أقرُّوا بذلك: {أفلا تَذَكَّرونَ}؛ أي: أفلا ترجعون إلى ما ذكَّركم الله به مما هو معلومٌ عندكم مستقرٌّ في فِطَرِكُم قد يُغيبه الإعراضُ في بعض الأوقات، والحقيقة أنَّكم إن رجعتم إلى ذاكِرَتِكُم بمجرَّد التأمُّل؛ علمتُم أنَّ مالك ذلك هو المعبود وحده، وأن إلهيَّة من هو مملوكٌ أبطلُ الباطل.
{84-85} Yaani: Waambie hawa wanaokanusha ufufuo, waadilifu kwa wengine asiye Mwenyezi Mungu; hoja dhidi yao kwa yale tuliowathibitishia na kukiri juu yake kutokana na umoja wa uungu na upekee wa Mungu ndani yake, pamoja na yale tuliyowakataza juu ya upweke wa uungu na ibada,
na kwa yale tuliyowathibitishia juu ya uumbaji wa viumbe ni kubwa zaidi kuliko walilolikanusha la kuwarejesha wafu hai ambalo ni jepesi kuliko hilo: "Ni ya nani ardhi na vilivyomo ndani yake." Yaani, nani ndiye muumbaji wa ardhi na vilivyomo ndani yake kutokana na wanyama na mimea na vitu visivyo hai na bahari na mito na majabali, Mmiliki wa hayo, anayezisimamia. Basi hakika ukiwauliza kuhusu hilo,
hapana budi watasema: Ni Mwenyezi Mungu peke yake.
Basi waambie watapokiri hilo: "Basi,je hamkumbuki?" Yaani, je, hamtarejea katika yale aliyowakumbusheni Mwenyezi Mungu, ambayo yanajulikana kwenu na yamekaa katika maumbile yenu, ambayo dalili zinaweza kuifanya kutoweka wakati fulani, na ukweli ni kwamba ikiwa mnarudi kwenye kumbukumbu zenu kwa kutafakari tu. Mnajua kwamba mmiliki wa hayo ni Mwenyezi Mungu peke yake, na kwamba uungu wa mwenye kumilikiwa ni ubatili wa hali ya juu.
#
{86 - 87} ثم انتقل إلى ما هو أعظم من ذلك، فقال: {قلْ مَن ربُّ السمواتِ السبع}: وما فيها من النيِّرات والكواكب السيَّارات والثوابت، {وربُّ العرش العظيم}: الذي هو أعلى المخلوقات وأوسُعها وأعظمُها؛ فمن الذي خَلَقَ ذلك ودبَّره وصرَّفه بأنواع التدبير؟ {سيقولون لله}؛ أي: سيقرُّون بأنَّ الله ربُّ ذلك كله، قل لهم حين يُقِرُّون بذلك: {أفلا تتَّقونَ}: عبادةَ المخلوقاتِ العاجزةِ وتتَّقون الربَّ العظيم كامل القدرة عظيم السلطان؟! وفي هذا من لطف الخطاب من قوله: {أفلا تذكرون}، {أفلا تتَّقونَ}؛ والوعظ بأداة العرض الجاذبة للقلوب ما لا يخفى.
{86-87} Kisha akaelekea kwenye jambo kubwa kuliko hilo,
na akasema: “Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu saba?" Na mianga na nyota zinazotembea na vilivyomo ndani yake, ‘Na Mola Mlezi wa A’rshi Kuu," ambaye ndiye aliye juu zaidi, aliyeenea zaidi, na mkuu kuliko viumbe vyote? Ni nani aliyeumba hivyo na akavipanga na akavisarifisha katika aina mbalimbali za viwango? "Watasema; ni vya Mwenyezi Mungu;" yaani, watakiri kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mola wa hivyo vyote,
waambie watakapokiri hilo:"Basi Je, hamwogopi" kuwaabudu viumbe visivyo na msaada na mkamcha Mwenyezi Mungu Mkuu, Mkamilifu wa uweza Mkuu wa Ufalme? Na katika haya,
umo wema wa kauli katika kusema kwake: "Basi, je, hamkumbuki?" "Basi je, hamwogopi?" Na kuhubiri ni kwa chombo cha uwasilishaji kinachovutia mioyo kwa yale ambayo yako wazi.
#
{88 - 89} ثم انتقل إلى إقرارهم بما هو أعمُّ من ذلك كلِّه، فقال: {قل من بيدِهِ ملكوتُ كلِّ شيءٍ}؛ أي: ملك كل شيء من العالم العلويِّ والعالم السفليِّ، ما نبصِرُه وما لا نبصِرُه، والملكوتُ صيغةُ مبالغةٍ؛ بمعنى الملك. {وهو يُجيرُ}: عباده من الشرِّ ويدفعُ عنهم المكارِهَ ويحفَظُهم مما يضرُّهم، {ولا يُجارُ عليه}؛ أي: لا يقدر أحدٌ أن يجيرَ على الله ولا يدفَعَ الشرَّ الذي قدَّره الله، بل ولا يشفَعُ أحدٌ عنده إلاَّ بإذنه. {سيقولون لله}؛ أي: سيقرُّون أنَّ الله المالك لكل شيءٍ، المجيرُ الذي لا يُجار عليه، {قل} لهم حين يقرُّون بذلك ملزِماً لهم: {فأنَّى تُسْحَرونَ}؛ أي: فأين تذهبُ عقولُكم حيث عبدتم مَنْ علمتم أنَّهم لا مُلك لهم ولا قِسْطَ من الملك، وأنَّهم عاجزون من جميع الوجوه، وتركتُم الإخلاص للمالِكِ العظيم القادرِ المدبِّر لجميع الأمور؟ فالعقول التي دلَّتكم على هذا لا تكون إلاَّ مسحورةً، وهي بلا شكٍّ قد سَحَرَها الشيطانُ بما زيَّنَ لهم، وحسَّنَ لهم وقَلَبَ الحقائق لهم فَسَحَرَ عقولَهم، كما سَحَرَت السحرةُ أعينَ الناس.
{88-89} Kisha akaendelea na kukiri kwao kile kilicho cha jumla zaidi kuliko yote hayo,
na akasema: "Sema: ni nani mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu?" Yaani, Ufalme wa kila kitu kutoka ulimwengu wa juu na ulimwengu wa chini, kile tunachokiona na kile tusichokiona, na ufalme ni hali iliyozidishwa kwa maana ya mfalme. "Naye ndiye anayewalinda" waja wake kutokana na shari na huwaondolea yanayowaudhi, na anawahifadhi kutokamana na yanayowadhuru, "wala hakilindwi asichotaka." Yaani, hawezi mtu yeyote kulinda juu ya Mwenyezi Mungu na wala hazui shari ambayo amekadiria Mola, bali pia haponyi yeyote mbele yake ila kwa idhini yake. "Watasema
(Ufalme huo) ni wa Mwenyezi Mungu." Yaani, watakiri kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mmiliki wa kila kitu,anayelinda ambaye hakilindwi asichotaka." "Sema" kwao wanapokiri kwa jambo hilo la lazima kwao, "Basi vipi mnadanganyika;" yaani, basi akili zenu zinakwenda wapi mlipowaabudu wale mliowajua kuwa hawana ufalme wala sehemu ya utawala, na kwamba hawakuwa na uwezo kwa kila jambo, na mkaacha uaminifu kwa Mmiliki Mkuu na Mwenye Nguvu anayesimamia kila kitu? Basi akili zilizowaongaza kwenye haya si chochote ila ni kurogwa, na bila ya shaka, Shetani aliziroga kwa yale aliyowapambia, akawarembeshea na akapotosha ukweli kwao, na akaziroga akili zao, kama wachawi walivyoroga macho ya watu.
{بَلْ أَتَيْنَاهُمْ بِالْحَقِّ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ (90) مَا اتَّخَذَ اللَّهُ مِنْ وَلَدٍ وَمَا كَانَ مَعَهُ مِنْ إِلَهٍ إِذًا لَذَهَبَ كُلُّ إِلَهٍ بِمَا خَلَقَ وَلَعَلَا بَعْضُهُمْ عَلَى بَعْضٍ سُبْحَانَ اللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ (91) عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَتَعَالَى عَمَّا يُشْرِكُونَ (92)}.
90. Bali tumewaletea Haki, na kwa yakini hao ni waongo. 91. Mwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hanaye mungu mwingine. Ingekuwa hivyo basi kila mungu angelichukua alivyoumba, na baadhi yao wangeliwashinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazomsifu. 92. Mjuzi wa siri na dhahiri, na ametukuka juu ya hayo wanayomshirikisha nayo.
#
{90 - 92} يقولُ تعالى: بل أتينا هؤلاء المكذِّبين بالحقِّ؛ المتضمِّن للصدق في الأخبار، العدل في الأمر والنهي؛ فما بالُهم لا يعترِفون به، وهو أحقُّ أن يُتَّبَع، وليس عندَهم ما يعوِّضُهم عنه إلاَّ الكذبُ والظلمُ؟! ولهذا قال: {وإنَّهم لَكاذبون. ما اتَّخَذَ الله من ولدٍ وما كان معه من إلهٍ}: كذبٌ يُعْرَفُ بخبرِ الله وخبرِ رسلِهِ، ويُعْرَفُ بالعقل الصحيح، ولهذا نَبَّهَ تعالى على الدليل العقليِّ على امتناع إلهين فقال: {إذاً}؛ أي: لو كان معه آلهةٌ كما يقولون؛ {لَذَهَبَ كلُّ إلهٍ بما خَلَقَ}؛ أي: لانفرد كلُّ واحدٍ من الإلهين بمخلوقاتِهِ واستقلَّ بها، ولحرص على ممانعة الآخر ومغالبته، {ولَعَلا بعضُهم على بعضٍ}؛ فالغالب يكون هو الإله؛ فمع التمانُع لا يمكِنُ وجودُ العالَم ولا يُتَصَوَّرُ أن يَنْتَظِمَ هذا الانتظامَ المدهشَ للعقول، واعتبر ذلك بالشمس والقمر والكواكب الثابتة والسيَّارة؛ فإنَّها منذ خُلِقَتْ وهي تجري على نظام واحدٍ وترتيبٍ واحدٍ، كلُّها مسخرةٌ بالقدرةِ، مدبَّرةٌ بالحكمة لمصالح الخَلْق كلِّهم، ليست مقصورةً على مصلحةِ أحدٍ دون أحدٍ، ولن ترى فيها خللاً ولا تناقضاً ولا معارضةً في أدنى تصرُّف؛ فهل يُتَصَوَّرُ أن يكون ذلك تقدير إلهيْنِ ربَّيْنِ. {سبحان اللهِ عمَّا يصفِون}: قد نطقتْ بلسانِ حالِها، وأفهمتْ ببديع أشكالها: أنَّ المدبِّر لها إلهٌ واحدٌ؛ كامل الأسماء والصفات، قد افتقرتْ إليه جميعُ المخلوقات في ربوبيَّتِهِ لها وفي إلهيَّتِهِ لها؛ فكما لا وجود لها ولا دوام إلاَّ بربوبيَّتِهِ؛ كذلك لا صلاح لها ولا قِوامَ إلاَّ بعبادته وإفراده بالطاعة. ولهذا نبَّه على عظمةِ صفاتِهِ بأنموذج من ذلك، وهو علمُهُ المحيطُ، فقال: {عالم الغيب}؛ أي: الذي غاب عن أبصارِنا وعلمنا من الواجبات والمستحيلات والممكنات {والشهادةِ}: وهو ما نشاهِدُ من ذلك. {فتعالى}؛ أي: ارتفع وعظم {عما يُشْرِكون}: به، ولا علم عندَهم إلاَّ ما علَّمه الله.
{90-92} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Tumewajia hawa wanaokanusha haki, inayojumulisha ukweli katika habari, iliyo na uadilifu katika maamrisho na makatazo; kwa hivyo ni kitu gani ambacho hazitambui akili zao, na ni sahihi zaidi kufuatwa,
na hawana cha isipokuwa uongo na dhuluma? Na kwa sababu ya hili akasema Mwenyezi Mungu: "Na kwa yakini hao ni waongo." "Mwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hanaye mungu mwengine." Uongo unaojulikana kwa habari ya Mwenyezi Mungu na habari za Mitume wake, na unajulikana kwa hoja nzuri. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akabainisha ushahidi wa kimantiki wa kujiepusha na waungu wawili,
na akasema: "Basi"; Yaani, lau kuwa wangelikuwa pamoja naye miungu wengine kama wasemavyo; "Kila mungu angelichukua alivyoumba." Yaani, kwa sababu kila mmoja katika hao miungu wawili, ni wa kipekee katika kuumbwa kwake na hajitegemei nao, na kwa sababu ana shauku ya kumpinga na kumshinda mwingine. "Na baadhi yao wangeliwashinda wengine;" basi mwenye kushinda ndiye atakuwa mungu; kwa kupingana, ulimwengu hauwezi kuwako, na haifikiriki kwamba utaratibu huu wa kustaajabisha wa akili ungeweza kupangwa, na utafakari kwa jua, mwezi, na sayari zisizobadilika na zinazosonga; tangu ziumbwe, zimekuwa zikiendeshwa kwa mfumo mmoja na mpangilio mmoja, zote zimeamrishwa kwa uwezo na kusimamiwa kwa hekima kwa ajili ya maslahi ya viumbe vyote, haijapungua katika masilahi ya mtu yeyote dhidi ya mwingine, hutaona dosari yoyote, ukinzani, au upinzani ndani yake katika tabia hata kidogo. Je, inafikirika kwamba hii ni uwezo wa miungu walezi wawili? "Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazomsifu." Ilinena kwa lugha yake yenyewe, na ilifahamika kwa umbo lake zuri zaidi. Kwamba, ina Mungu mmoja katika usimamizi wake; mkamilifu wa majina na sifa, viumbe vyote vinamtegemea katika ubwana wake juu yao na katika uungu wake juu yao; kama vile hakuna kuwepo au kudumu isipokuwa kwa ubwana Wake. Vile vile kutakasika wala kunyooka ila kwa kumuabudu Yeye na kumpwekesha kwa utiifu. Kwa sababu hii akajulisha ukubwa wa sifa zake kwa mfano wa hayo,
nayo ni elimu yake iliyoenea na akasema: "Mjuzi wa siri," yaani, ni yule ambaye ametoweka mbele ya macho yetu na akatufundisha mambo ya wajibu na ya muhali na yanayowezekana, "na dhahiri." Nayo ni yale tunayoyashudia katika hayo. "Na ametukuta;" yaani, ametakasika na ametukuka "juu ya hayo wanayomshirikisha nayo." Na hawana elimu ila yale aliyowafundisha Mola.
{قُلْ رَبِّ إِمَّا تُرِيَنِّي مَا يُوعَدُونَ (93) رَبِّ فَلَا تَجْعَلْنِي فِي الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ (94) وَإِنَّا عَلَى أَنْ نُرِيَكَ مَا نَعِدُهُمْ لَقَادِرُونَ (95)}.
93.
Sema: Mola wangu Mlezi! Ukinionyesha adhabu waliyoahidiwa. 94. Mola wangu Mlezi! Usinijalie katika watu madhalimu hao. 95. Na hakika Sisi ni waweza wa kukuonyesha tuliyowaahidi.
#
{93 - 95} لمَّا أقام تعالى على المكذِّبين أدلَّتَه العظيمةَ، فلم يلتَفِتوا لها، ولم يُذْعِنوا لها؛ حقَّ عليهم العذابُ، ووُعِدوا بنزوله، وأرشد اللهُ رسولَه أن يقول: {قُلْ ربِّ إمَّا تُرِيَنِّي ما يوعَدونَ}؛ أي: أيَّ وقتٍ أريتني عذابَهم وأحضرتَني ذلك، {ربِّ فلا تَجْعَلْني في القوم الظالمين}؛ أي: اعصِمْني وارْحَمْني مما ابتلَيْتَهم به من الذُّنوب الموجبة للنقم، واحْمِني أيضاً من العذاب الذي ينزِلُ بهم؛ لأنَّ العقوبة العامَّة تَعُمُّ عند نزولها العاصي وغيره. قال الله في تقريب عذابهم: {وإنَّا على أن نُرِيَكَ ما نَعِدُهُم لَقادِرونَ}: ولكنْ إنْ أخَّرْناه؛ فلحكمةٍ، وإلاَّ؛ فقُدْرَتنا صالحةٌ لإيقاعِهِ [فيهم].
{93-95} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoweka ushahidi wake mkubwa dhidi ya wakanushaji, hawakuizingatia, wala hawakuinyenyekea, adhabu ilistahiki juu yao, na wakaahidiwa kuwa itashuka,
na Mwenyezi Mungu akamwongoza Mwenyezi Mungu mtume wake aseme: "Sema: Mola wangu Mlezi! Ukinionyesha adhabu waliyo ahidiwa;" yaani, wakati wowote utakaponionyesha adhabu yao na unitahadharishe mimi juu ya hilo, "Mola wangu Mlezi! Usinijalie katika watu madhalimu hao;" yaani, nikinge mimi na unirehemu kutokana na utakayowapa shida kwayo kutokana na dhambi zinazowajibisha kisasi, na unilinde vile vile kutokana na adhabu itakayowashukia ; kwa sababu adhabu huenea wakati wa kushuka kwake kwa aliyeasi na mwenginewe.
Amesema Mwenyezi Mungu katika kukaribia kwa adhabu yao: "Na hakika Sisi ni waweza wa kukuonyesha tuliyowaahidi," na lakini tukichelewesha;ni kwa hekima; la sivyo; uweza wetu unaswihisha kutokea adhabu hii "juu yao."
{ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ السَّيِّئَةَ نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَصِفُونَ (96) وَقُلْ رَبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ (97) وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَنْ يَحْضُرُونِ (98)}.
96. Kinga maovu kwa kutenda yaliyo mema zaidi. Sisi tunayajua wayasemayo. 97.
Na sema: Mola wangu Mlezi! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashetani. 98. Na najikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie.
#
{96} هذا من مكارم الأخلاق التي أمر اللهُ رسولَه بها، فقال: {ادفَعْ بالتي هي أحسنُ السيئةَ}؛ أي: إذا أساء إليك أعداؤك بالقول والفعل؛ فلا تقابِلْهم بالإساءة؛ مع أنَّه يجوزُ معاقبة المسيء بمثل إساءته، ولكن ادْفَعْ إساءتهم إليك بالإحسان منك إليهم؛ فإنَّ ذلك فضلٌ منك على المسيء، ومن مصالح ذلك أنَّه تخفُّ الإساءة عنك في الحال وفي المستقبل، وأنَّه أدعى لجلب المسيء إلى الحقِّ، وأقرب إلى ندمه وأسفه ورجوعِهِ بالتوبة عمَّا فَعَلَ، ويتَّصِفُ العافي بصفة الإحسان، ويقهرُ بذلك عدوَّه الشيطان، ويستوجبُ الثواب من الربِّ؛ قال تعالى: {فَمَنْ عفا وأصلحَ فأجرُهُ على الله}، وقال تعالى: {ادفَعْ بالتي هي أحسنُ السيئةَ فإذا الذي بينَكَ وبينَهُ عداوةٌ كأنَّه وليٌّ حميمٌ. وما يُلَقَّاها}؛ أي: ما يوفَّق لهذا الخُلُق الجميل {إلاَّ الذين صَبَروا وما يُلَقَّاها إلاَّ ذو حظٍّ عظيم}.
وقوله: {نحن أعلم بما يَصِفون}؛ أي: بما يقولون من الأقوال المتضمِّنة للكفر والتكذيب بالحق، قد أحاط علمُنا بذلك، وقد حَلِمْنا عنهم وأمهَلْناهم وصبَرْنا عليهم، والحقُّ لنا، وتكذيبُهم لنا؛ فأنت يا محمد ينبغي لك أن تصبِرَ على ما يقولون، وتقابِلَهم بالإحسان. هذه وظيفة العبد في مقابلة المسيء من البشر.
{96} Hii ni moja ya maadili matukufu ambayo Mwenyezi Mungu alimwamuru Mtume wake kutekeleza.
Akasema: "Kinga maovu kwa kutenda yaliyo mema zaidi." Yaani, ikiwa maadui zako wanakuudhi kwa maneno na vitendo, usiwakabili kwa uovu, pamoja na kwamba inafaa kumuadhibu muovu kwa mfano wa maovu yake, lakini kinga maovu yao kwako kwa wema kutoka kwako juu yao. Hii ni fadhila kutoka kwako kwa muovu, na uzuri wa kufanya hivo ni kwamba muovu atapunguza maovu yake kwako kwa muda huu na muda ujao, na kwamba unaita katika kumleta muovu kwenye haki,na humkurubisha zaidi katika kujutia,na kuhuzunika na kutaka toba kwa aliyofanya, na anasifika msamehevu kwa sifa ya ihsani, na kwa hilo humshinda adui yake shetani, na anastahiki thawabu kutoka kwa Mola Mlezi.
Amesema Mtukufu: "Lakini mwenye kusamehe,na akasuluhisha, basi malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu.
" Na Akasema Mtukufu: "Pinga uovu kwa lililo jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu." "Lakini hawapewi wema huu." Yaani, haafikiwa kwa tabia nzuri, "ila wanaosubiri, wala hawapewi ila wenye bahati.
Na kauli yake: "Sisi tunajua wayasemayo;" yaani, wanayoyasema kutokana na maneno yanayojumuisha ukafiri na kukanusha ukweli, hakika imeizunguka elimu yetu kwa hayo, na tumewastahimili, na tumewapa muda na tumekuwa wenye subira kwao, na ukweli ni wetu, na kukanusha kwao kwetu. Ewe, Muhammad, inapaswa uwe na subira kwa yale wanayoyasema, na uwakabili kwa Ihsani. Huu ndio wadhifa wa mja katika kukabili maovu kutoka kwa wanadamu.
#
{97 - 98} وأما المسيء من الشياطين؛ فإنَّه لا يُفيد فيه الإحسانُ، ولا يدعو حِزْبَهُ إلاَّ لِيكونوا من أصحاب السعير؛ فالوظيفةُ في مقابلته أن يسترشِدَ بما أرشد الله إليه رسوله، فقال: {وقُل ربِّ أعوذُ بك}؛ [أي: أعتصم بحولك وقوَّتك متبرئًا من حولي وقوَّتي]، {من هَمَزات الشياطين. وأعوذُ بكَ ربِّ أن يحضُرونِ}؛ أي: أعوذُ بك من الشرِّ الذي يصيبُني بسبب مباشرتِهِم وهَمْزِهِم ومسِّهم، ومن الشرِّ الذي بسبب حضورِهِم ووسوستِهِم، وهذه استعاذةٌ من مادَّة الشرِّ كلِّه وأصله، ويدخُلُ فيه الاستعاذةُ من جميع نَزَغات الشيطان ومن مسِّه ووسوستِهِ؛ فإذا أعاذ اللهُ عبدَه من هذا الشرِّ، وأجاب دعاءَه؛ سَلِمَ من كلِّ شرٍّ، ووفِّقَ لكلِّ خير.
{97-98} Ama yule ambaye kwamba ni muovu kutokamana na mashetani; hufaidika na wema, wala halinganii kundi lake isipokuwa wawe miongoni mwa watu wa motoni; basi katika jambo la muhimu katika kukabiliana naye, ajiongoze katika uongozi ambao alimwongoza Mwenyezi Mungu mtume wake.
Na akasema "Na sema: Mola wangu Mlezi! Najikinga kwako;"
(yaani, najilinda kwa hila zako na nguvu zako na kujieka mbali na hila zangu na nguvu)," na wasiwasi wa mashetani. "Na najikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie;" yaani, najilinda kwako kutokana na shari itakayonipata kwa sababu ya kutangamana nao na wasiwasi wao na mguso wao, na kutokana na shari ambayo ni kwa sababu ya kuhudhuria kwao na wasiwasi wao, na dua hii ya kujilinda ni kutokana na kila lenye shari na asili yake, na yaingia katika kila kujikinga na kila mvutano wa shetani na mguso wake na wasiwasi wake. Basi pindi akimkinga Mwenyezi Mungu mja wake kutokana na shari hii, na akajibu dua yake; atasalimika kutokana na kila shari, na atawafikika katika kila heri.
{حَتَّى إِذَا جَاءَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ رَبِّ ارْجِعُونِ (99) لَعَلِّي أَعْمَلُ صَالِحًا فِيمَا تَرَكْتُ كَلَّا إِنَّهَا كَلِمَةٌ هُوَ قَائِلُهَا وَمِنْ وَرَائِهِمْ بَرْزَخٌ إِلَى يَوْمِ يُبْعَثُونَ (100)}.
99. Mpaka yanapomfikia mmoja wao mauti,
husema: Mola wangu Mlezi! Nirudishe. 100. Ili nitende mema sasa badala ya yale niliyoyaacha. Wapi! Hii ni kauli aisemayo Yeye tu. Na nyuma yao kipo kizuizi mpaka siku watakapofufuliwa.
#
{99 - 100} يخبرُ تعالى عن حال مَنْ حَضَرَهُ الموت من المفرِّطين الظَّالمين: أنَّه يندمُ في تلك الحال إذا رأى مآله، وشاهَدَ قُبْحَ أعماله، فيطلبُ الرجعة إلى الدنيا، لا للتمتُّع بلذَّاتها واقتطاف شَهَواتها، وإنَّما ذلك يقول: {لعلِّي أعملُ صالحاً فيما تركتُ}: من العمل وفرَّطْتُ في جَنْب الله. {كلاَّ}؛ أي: لا رجعةَ له ولا إمهالَ، قد قضى اللهُ أنَّهم إليها لا يُرْجَعون، {إنَّها}؛ أي: مقالتُه التي تمنَّى فيها الرجوعَ إلى الدُّنيا {كلمةٌ هو قائلُها}؛ أي: مجرد قول باللسانِ، لا يفيدُ صاحبَه إلاَّ الحسرةَ والندم، وهو أيضاً غير صادقٍ في ذلك؛ فإنَّه لَوْ رُدَّ لَعادَ لما نُهِيَ عنه. {ومن ورائِهِم برزخٌ إلى يوم يُبْعَثونَ}؛ أي: من أمامهم وبين أيديهم برزخٌ، وهو الحاجز بين الشيئين؛ فهو هنا الحاجزُ بين الدُّنيا والآخرة، وفي هذا البرزخ يتنعَّم المطيعونَ، ويعذَّبُ العاصونَ من موتِهِم إلى يوم يبعثونَ؛ أي: فَلْيَعُدُّوا له عُدَّتَهُ، وليأخذوا له أُهْبَتَهُ.
{99-100} Mwenyezi Mungu anaelezea juu ya hali ya yule ambaye amejiwa na mauti kutokana na waliovuka mipaka, madhalimu. Kuwa yeye atajuta katika hali hiyo atakapoona hatima yake, na akashuhudia uovu wa matendo yake, akataka kurejea katika dunia, siyo kwa ajili ya kustarehe kwa ladha zake na kumaliza shahawa zake. Hakika siyo lingine alisemalo kwamba "ili nipate mimi kufanya mema, niliyoacha" kutokana na matendo na katika yale niliyovuka mipaka katika maamrisho ya Mwenyezi Mungu. "Wapi!"; yaani, hakuna kurejea wala kupewa muhula, na ameshahukumu Mwenyezi Mungu kwamba wao hawatarejea duniani. "Hii ni;" yaani, maneno yake aliyosema ya kutamani kurejea duniani; "kauli aisemayo yeye tu." Yaani, kwa kutamka tuu kwa ulimi, haimfaidishi msemaji isipokuwa ni hasara na majuto, na yeye vilevile si mkweli katika maneno haya; kwani hakika yeye lau atarejeshwa duniani atafanya yale yale aliyokatazwa juu yake. "Na nyuma yao, kipo kizuizi mpaka siku watakapofufuliwa." Yaani, kutoka mbele yao na kutoka mikononi mwao kuna kizuizi, ambacho ni kizuizi kati ya vitu viwili; na hapa ni kizuizi kati ya ulimwengu na Akhera, na katika hapa Barzakh wataneemeka watiifu, na wataadhibiwa wenye kuasi tangu kufa kwao mpaka watakapofufuliwa. Yaani, basi wajiandalie maandilizi yake, na wachukue zawadi zake.
{فَإِذَا نُفِخَ فِي الصُّورِ فَلَا أَنْسَابَ بَيْنَهُمْ يَوْمَئِذٍ وَلَا يَتَسَاءَلُونَ (101) فَمَنْ ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ (102) وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنْفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ (103) تَلْفَحُ وُجُوهَهُمُ النَّارُ وَهُمْ فِيهَا كَالِحُونَ (104) أَلَمْ تَكُنْ آيَاتِي تُتْلَى عَلَيْكُمْ فَكُنْتُمْ بِهَا تُكَذِّبُونَ (105) قَالُوا رَبَّنَا غَلَبَتْ عَلَيْنَا شِقْوَتُنَا وَكُنَّا قَوْمًا ضَالِّينَ (106) رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْهَا فَإِنْ عُدْنَا فَإِنَّا ظَالِمُونَ (107) قَالَ اخْسَئُوا فِيهَا وَلَا تُكَلِّمُونِ (108) إِنَّهُ كَانَ فَرِيقٌ مِنْ عِبَادِي يَقُولُونَ رَبَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا وَأَنْتَ خَيْرُ الرَّاحِمِينَ (109) فَاتَّخَذْتُمُوهُمْ سِخْرِيًّا حَتَّى أَنْسَوْكُمْ ذِكْرِي وَكُنْتُمْ مِنْهُمْ تَضْحَكُونَ (110) إِنِّي جَزَيْتُهُمُ الْيَوْمَ بِمَا صَبَرُوا أَنَّهُمْ هُمُ الْفَائِزُونَ (111) قَالَ كَمْ لَبِثْتُمْ فِي الْأَرْضِ عَدَدَ سِنِينَ (112) قَالُوا لَبِثْنَا يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ فَاسْأَلِ الْعَادِّينَ (113) قَالَ إِنْ لَبِثْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا لَوْ أَنَّكُمْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ (114)}.
101. Basi litakapopulizwa baragamu, hapo hautakuwapo ujamaa baina yao siku hiyo, wala hawataulizana. 102. Ama wale ambao mizani zao zitakuwa nzito, hao ndio wenye kufanikiwa. 103. Na wale ambao mizani zao zitakuwa nyepesi, hao ndio waliozitia hasarani nafsi zao, na katika Jahannamu watadumu. 104. Moto utababua nyuso zao, nao watakuwa na nyuso zilizo kunjana. 105. Je, hazikuwa Aya zangu mkisomewa, na nyinyi mkizikanusha? 106.
Watasema: Mola wetu Mlezi! Tulizidiwa na uovu wetu na tukawa watu tuliopotea. 107. Mola wetu Mlezi! Tutoe humu Motoni. Na tufanyapo tena basi kweli sisi ni wenye kudhulumu. 108.
Atasema Mwenyezi Mungu: Tokomeeni humo, wala msinisemeze. 109.
Bila ya shaka lilikuwapo kundi katika waja wangu likisema: Mola wetu Mlezi! Tumeamini; basi tusamehe na uturehemu, nawe ndiwe Mbora wa wanaorehemu. 110. Lakini nyinyi mliwakejeli hata wakawasahaulisheni kunikumbuka, na mlikuwa mkiwacheka. 111. Hakika Mimi leo nimewalipa kwa vile walivyosubiri. Bila ya shaka hao ndio wenye kufuzu. 112.
Atasema: Mlikaa muda gani katika ardhi kwa hisabu ya miaka? 113.
Watasema: Tulikaa siku moja au sehemu ya siku. Basi waulize wanaoweka hisabu.
(114) Atasema: Nyinyi hamkukaa huko duniani ila kidogo, laiti ingelikuwa mnajua.
#
{101} يخبر تعالى عن هول يوم القيامةِ، وما في ذلك [اليوم] من المزعجاتِ والمقلقاتِ، وأنَّه إذا نُفِخَ في الصور نفخةُ البعث، فحُشِرَ الناس أجمعون، لميقاتِ يوم معلوم؛ أنَّه يُصيبهم من الهول ما يُنسيهم أنسابَهم التي هي أقوى الأسباب، فغير الأنساب من باب أولى، وأنَّه لا يسألُ أحدٌ أحداً عن حالِهِ؛ لاشتغالِهِ بنفسه؛ فلا يدري هل يَنْجو نجاةً لا شقاوةَ بعدَها أو يشقى شقاوةً لا سعادةَ بعدها؛ قال تعالى: {فإذا جاءتِ الصَّاخَّة. يوم يَفِرُّ المرءُ من أخيه وأمّه وأبيه. وصاحبتِهِ وبنيه. لكلِّ امرئٍ منهم يومئذٍ شأنٌ يُغنيه}.
{101} Anatoa habari Mwenyezi Mungu kutokana na vitisho vya siku ya Qiyama, na ambayo yatapatikana katika hiyo
[siku] kutokana na vitisho na wasiwasi, pindi likipulizwa parapanda pulizo la kufufua, wakakusanywa watu wote, katika wakati uliopangwa; kuwa litawapata hilo tishio litakalowasahaulisha nasaba zao ambalo ndiyo sababu kubwa zaidi, na isiyokuwa nasaba ni katika mlango ulio bora zaidi, kwa sababu hatauliza yeyote mwingine kuhusu hali yake, kwa kushughulika kwake na nafsi yake.
Basi hajui je ataokoka uokozi ambao hauna uovu baada yake au atapata uovu ambao hakuna wema baada yake; Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Basi utakapokuja ukelele Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye, na mamaye, na babaye, na mkewe na wanawe. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha."
#
{102} وفي القيامة مواضعُ يشتدُّ كربُها ويعظُمُ وقْعُها؛ كالميزان الذي يُمَيَّزُ به أعمالُ العبدِ، ويُنْظَرُ فيه بالعدل ما له وما عليه، وتَبين فيه مثاقيلُ الذَّرِّ من الخيرِ والشر. {فَمَنْ ثَقُلَتْ موازينُهُ}: بأن رَجَحَتْ حسناتُه على سيئاته؛ {فأولئك هم المفلحونَ}: لنجاتِهِم من النار، واستحقاقِهِم الجنَّة، وفوزِهم بالثناء الجميل.
{102} Na siku ya Qiyama sehemu yatakuwa kali zaidi mateso yake na yatakuwa makubwa matukio yake, kama mizani ambayo kwamba itapambanua matendo ya mja, na yataangaliwa kwa uadilifu aliyofanya yeye na aliyowafanyia wengine, na itabainisha ndani yake uzito wa tembe wa kheri na shari. "Ama wale ambao mizani zao zitakuwa nzito" kwamba matendo yake mema yameshinda matendo yake mabaya; "hao ndio wenye kufanikiwa," kwa kuokolewa kwao na moto, na kustahiki kwao Pepo, na kushinda kwao kwa sifa nzuri.
#
{103} {ومَنْ خَفَّتْ موازينُهُ}: بأن رَجَحَتْ سيئاتُه على حسناتِهِ وأحاطتْ بها خطيئاتُهُ؛ {فأولئك الذين خَسِروا أنْفُسَهم}: كلُّ خسارةٍ غير هذه الخسارةِ؛ فإنَّها بالنسبة إليها سهلةٌ، ولكن هذه خسارةٌ صعبةٌ؛ لا يُجْبَرُ مُصابها، ولا يُسْتَدْرَكُ فائِتُها؛ خسارةٌ أبديَّة وشقاوةٌ سرمديَّة، قد خسر نفسَه الشريفة التي يتمكَّن بها من السعادة الأبديَّة، ففوَّتها هذا النعيم المقيم في جوار الربِّ الكريم. {في جهنَّمَ خالدونَ}: لا يخرُجون منها أبدَ الآبدينَ، وهذا الوعيد إنَّما هو ـ كما ذكرنا ـ لمن أحاطَتْ خطيئاتُهُ بحسناتِهِ، ولا يكون ذلك إلاَّ كافراً؛ فعلى هذا لا يُحاسَبُ محاسبةَ من توزَنُ حسناتُه وسيئاتُه؛ فإنَّهم لا حسنات لهم، ولكن تعدُّ أعمالُهم وتُحصى، فيوقَفون عليها، ويقرَّرون بها، ويُخْزَوْن بها.
وأمَّا مَنْ مَعَهُ أصلُ الإيمان، ولكنْ عَظُمَتْ سيئاتُه، فرجَحَتْ على حسناتِهِ؛ فإنَّه وإن دَخَلَ النار؛ لا يَخْلُدُ فيها كما دلَّت على ذلك نصوص الكتاب والسنة.
{103} "Na wale ambao mizani zao zitakuwa nyepesi" kwamba matendo yake maovu yamepita mema yake na yamezungukwa na madhambi yake; "hao ndio waliozitia hasarani nafsi zao." Kila hasara isipokuwa hii; kwa ajili ukilinganisha ni rahisi, lakini hii ni hasara ngumu; adhabu yake haiwezi kurekebishwa, wala hasara yake haiwezi kurukwa; hasara ya milele na taabu ya milele, alipoteza nafsi yake tukufu, ambayo kwayo angeweza kufurahia furaha ya milele, na akakosa neema hii iliyokuwa ya kuwa karibu na Mola Mtukufu. "Na katika jahannamu watadumu." Hawatatoka humo milele na milele, na hili kemeo ni - kama tulivyotaja kwa wale ambao dhambi zao zimezunguka matendo yao mema, na hawi hivi ila kafiri. Kwa ajili ya hili hatahesabiwa kutokana na kupimiwa mema yake na maovu yake; kwa kuwa wao hawana mema, lakini matendo yao huhesabiwa na huthibitiwa, watasimamishwa kwa hayo, na watakiri kwayo, na watafedheheka kwayo. Ama yule aliye na asili ya imani, lakini matendo yake mabaya ni makubwa, yanashinda amali zake njema. Kwani hata akiingia Motoni; hataishi humo milele, kama inavyoonyeshwa na maandiko na Sunnah.
#
{104} ثم ذَكَرَ تعالى سوءَ مصير الكافرين، فقال: {تَلْفَحُ وجوهَهُم النارُ}؛ أي: تغشاهم من جميع جوانِبِهم، حتى تصيبَ أعضاءهم الشريفةَ، ويتقطَّع لهبُها عن وجوههم، {وهم فيها كالِحونَ}: قد عَبَسَتْ وجوهُهم وقَلَصَتْ شفاهُهم، من شدَّة ما هم فيه، وعظيم ما يَلْقَوْنَه.
{104} Kisha akataja Mwenyezi Mungu hatima mbaya ya makafiri, na akasema; "Moto utabambua nyuso zao;" yaani, itawafunika pande zote, mpaka ivipige viungo vyao vya heshima, na mwali wake utakatika usoni mwao. "Nao watakuwa na nyuso zilizokunjana;" nyuso zao zimekunjamana na midomo yao imebana, kwa sababu ya ukali wa waliyomo ndani yake na ukubwa wa yale yanayowakabili.
#
{105} فيُقالُ لهم توبيخاً ولوماً: {ألم تَكُنْ آياتي تُتْلى عليكم}: تُدْعَون بها لِتؤمنوا وتُعْرَضُ عليكم لِتَنْظُروا؛ {فكنتم بها تكذِّبونَ}: ظلماً منكم وعناداً، وهي آياتٌ بيناتٌ، دالاَّتٌ على الحقِّ والباطل، مبيِّناتٌ للمحقِّ والمبطل؟!
{105} Na wataambiwa kwa kejeli na lawama: "Je, hazikuwa Aya zangu mkisomewa," mlilinganiwa kwazo ili mpate kuamini na kuhudhurishwa kwenu ili mpate kuzizingatia; "na nyinyi mkizikanusha" dhuluma na inadi kutoka kwenu, na hali zilikuwa ni ishara zilizo wazi, zinazobainisha ukweli na uwongo, zinazobainisha yule wa haki na wa batili?
#
{106} فحينئذٍ أقرُّوا بظلمهم حيث لا ينفع الإقرار: {قالوا ربَّنا غَلَبَتْ عَلَيْنا شِقْوَتُنا}؛ أي: غلبت علينا الشَّقاوة الناشئةُ عن الظُّلم والإعراض عن الحقِّ والإقبال على ما يضرُّ وتركِ ما ينفعُ، {وكنَّا قوماً ضالِّين}: في عملهم، وإن كانوا يَدْرون أنَّهم ظالمون؛ أي: فعلنا في الدُّنيا فعلَ التائِهِ الضالِّ السفيهِ؛ كما قالوا في الآية الأخرى: {وقالوا لو كُنَّا نَسْمَعُ أو نَعْقِلُ ما كُنَّا في أصحابِ السَّعير}.
{106} Wakati huo watakiri udhalimu wao ambapo kukiri hakutafaa,
"Watasema: Mola wetu Mlezi, tulizidiwa na uovu wetu." Yaani, tulizidiwa na uovu wetu uliotupelekea kufanya kutokana na udhalimu na kuipinga haki na kukubali yale yanayodhuru na kuacha ya manufaa. "Na tukawa watu tuliopotea" katika matendo yao, na hata kama wangelijua kwamba walikuwa madhalimu; yaani,
tulifanya duniani matendo maovu mabaya machafu; kama walivyosema katika aya nyingine: "Na watasema: Lau kuwa tungelisikia, au tungelikuwa na akili, tusingelikuwa katika watu wa Motoni!
#
{107} {ربَّنا أخْرِجْنا منها فإنْ عُدْنا فإنَّا ظالِمونَ}: وهم كاذِبون في وعدِهم هذا؛ فإنَّهم كما قال تعالى: {لو رُدُّوا لَعادوا لما نُهوا عنه}، ولم يُبْقِ الله لهم حجَّة، بل قطع أعذارَهم، وعَمَّرَهم في الدُّنيا ما يتذكَّر فيه من تذكَّر ، ويرتدِعُ فيه المجرمُ.
{107} "Mola wetu Mlezi, tutoe humu Motoni. Na tufanyapo tena basi kweli sisi ni wenye kudhulumu.
" Na wao ni waongo katika ahadi yao hii; na wao ni kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: "Na kama wangelirudishwa, bila ya shaka wangeyarejea yale yale waliyokatazwa," na Mwenyezi Mungu hakuwaachia hoja, bali alikata nyudhuru zao, na akawarefushia umri katika dunia ambayo ndani yake atakumbuka yule atayekumbuka, na atayapinga kwayo muovu.
#
{108} فقال الله جواباً لسؤالهم: {اخسؤوا فيها ولا تُكَلِّمونِ}: وهذا القول ـ نسألُه تعالى العافيةَ ـ أعظمُ قول على الإطلاق يسمعهُ المجرِمون في التخييبِ والتوبيخ والذُّلِّ والخسارِ والتأييس من كلِّ خيرٍ والبُشرى بكل شرٍّ، وهذا الكلام والغضب من الربِّ الرحيم أشدُّ عليهم، وأبلغُ في نِكايتهم من عذاب الجحيم.
{108} Mungu alisema katika kujibu swali lao: "Tokomeeni humo" kauli hii - tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atujalie kheri, - ni kauli kubwa kuliko zote zilizowahi kusikiwa na wapotefu kuhusiana na kukatishwa tamaa, kukemewa, kufedheheshwa, kuhasirika na kukata tamaa kwa kila kheri na na bishara ya shari yote. Maneno haya na ghadhabu kutoka kwa Mola mwingi wa Rehema, ni kali zaidi kwao na yenye ufanisi zaidi katika kukemea zaidi kuliko adhabu ya Jahannamu.
#
{109} ثم ذكر الحال التي أوصلَتْهم إلى العذاب وقَطَعَتْ عنهم الرحمةَ، فقال: {إنَّه كان فريقٌ من عبادي يقولونَ ربَّنا آمنَّا فاغْفِرْ لنا وارْحَمْنا وأنتَ خيرُ الراحمينَ}: فجمعوا بين الإيمان المقتضي لأعمالِهِ الصالحة، والدُّعاء لربِّهم بالمغفرة والرحمة، والتوسُّل إليه بربوبيَّته ومنَّته عليهم بالإيمان، والإخبار بسعةِ رحمتِهِ وعموم إحسانِهِ، وفي ضمنِهِ ما يدلُّ على خضوعهم وخشوعهم وانكسارِهم لربِّهم وخوفهم ورجائهم؛ فهؤلاءِ ساداتُ الناس وفضلاؤهم.
{109} Kisha akataja
(Mola) hali iliyowapelekea kuwaadhibu na kuwakatilia mbali na rehema,
na akasema: "Bila ya shaka lilikuwapo kundi katika waja wangu likisema: Mola wetu Mlezi, tumeamini; basi tusamehe na uturehemu, nawe ndiwe Mbora wa wanaorehemu." Walijumuisha imani inayotakiwa kwa matendo yake mema, na dua kwa Mola wao ya kutaka msamaha na rehema, na wakamtegemea kwake Yeye kwa Uungu wake na neema yake kwao kwa imani, na wakajulisha upana wa rehema yake na wingi wa hisani yake, na pamoja nayo ni yale yanayoashiria juu ya kunyenyekea kwao na uchaji wao na kujisalimisha kwao kwa Mola wao na hofu yao na matumaini yao; basi hawa ndio mabwana wa watu na wabora wao.
#
{110} {فاتَّخَذْتُموهم}: أيُّها الكفرةُ الأنذالُ ناقصو العقول والأحلام، {سِخْرِيًّا}: تهزؤون بهم وتحتقرونهم حتى اشتغلتُم بذكر السَّفه، {حتى أنْسَوْكُم ذِكْري وكنتم منهم تَضْحَكونَ}: وهذا الذي أوجبَ لهم نسيان الذِّكر اشتغالُهم بالاستهزاء بهم؛ كما أنَّ نسيانهم للذِّكر يحثُّهم على الاستهزاء؛ فكلٌّ من الأمرين يمدُّ الآخر؛ فهل فوق هذه الجرأة جرأة؟!
{110} "Lakini nyinyi," enyi makafiri wapumbavu, wapungufu wa akili na ndoto, "mliwakejeli" mnawafanyia mzaha na kuwadharau mpaka mnashughulika na ukumbusho ulio muovu. "Hata wakawasahaulisheni kunikumbuka, na mlikuwa mkiwacheka;" na haya ndiyo yaliyowapatisha wao kusahau kujishughulisha kwao kwa kuwakejeli; kama vile kusahau kwao ukumbusho pia kunawahimiza kufanya mzaha. Kila moja katika mambo haya mawili linavutia juu ya. Je, kuna ujasiri zaidi ya huu?
#
{111} {إنِّي جزيتُهُمُ اليومَ بما صَبَروا}: على طاعتي وعلى أذاكم حتى وصلوا إليَّ {أنَّهم هُمُ الفائزونَ}: بالنعيم المقيم والنَّجاة من الجحيم؛ كما قال في الآية الأخرى: {فاليومَ الذين آمنوا من الكُفَّارِ يَضْحَكونَ ... } الآيات.
{111} "Hakika Mimi leo nimewalipa kwa vile walivyosubiri," kwa kunitii na kuvumilia maudhi mpaka mkanifikia Mimi. "Bila ya shaka, hao ndio wenye kufuzu," kwa neema ya kudumu na wokovu dhidi ya moto. Kama alivyosema katika aya nyingine, "Basi leo walioamini ndio watawacheka makafiri..." hadi mwisho wa Aya hizi.
#
{112 - 114} {قال} لهم على وجهِ اللَّوم وأنَّهم سفهاءُ الأحلام حيث اكْتَسَبوا في هذه المدَّة اليسيرةِ كلَّ شرٍّ أوصَلَهم إلى غضبِهِ وعقوبتِهِ، ولم يكتَسِبوا ما اكْتَسَبَه المؤمنون من الخير الذي يوصِلُهم إلى السعادة الدائمة ورضوان ربِّهم: {كم لَبِثْتُم في الأرضِ عددَ سنينَ. قالوا لَبِثْنا يوماً أو بعضَ يوم}: كلامُهم هذا مبنيٌّ على استقصارِهم جدًّا لمدَّة مُكْثِهِم في الدُّنيا، وأفاد ذلك، لكنَّه لا يفيدُ مقدارَه ولا يُعَيِّنُه؛ فلهذا قالوا: {فاسألِ العادِّينَ}؛ أي: الضابطين لعددِهِ، وأمَّا هم؛ ففي شغل شاغل وعذاب مذهل عن معرفةِ عددِهِ. فقال لهم: {إن لبثتم إلاَّ قليلاً}: سواء عيَّنْتُم عدَدَه أم لا، {لو أنكم كنتُم تعلمونَ}.
{112-114} "Alisema," wanapaswa kulaumiwa na kwamba walikuwa katika ndoto za kipumbavu, kwani walipata katika kipindi hiki kifupi kila uovu uliowapeleka kwenye ghadhabu na adhabu yake, na hawakupata yale waliyoyapata Waumini katika wema ambao unawapeleka kwenye furaha ya milele na radhi ya Mola wao. "Mlikaa muda gani katika ardhi kwa hisabu ya miaka?" Watasema, tulikaa siku moja au sehemu ya siku." Kauli yao hii inatokana na makadirio yao mafupi sana ya muda wa kukaa kwao katika dunia hii, na hilo ni la manufaa, lakini halionyeshi kiasi chake au kubainisha. Ndiyo maana wakasema, "Basi waulize wanaoweka hisabu;" yaani, wanaodhibiti idadi yake, na ama wao; kuna wasiwasi mkubwa na adhabu ya kushangaza linapokuja suala la kujua idadi yake. Akawaambia Mola, "Nyinyi hamkukaa huko duniani ila kidogo" sawia mkiwa mumebaini idadi ya muda huo au la, "laiti ingelikuwa mnajua."
{أَفَحَسِبْتُمْ أَنَّمَا خَلَقْنَاكُمْ عَبَثًا وَأَنَّكُمْ إِلَيْنَا لَا تُرْجَعُونَ (115) فَتَعَالَى اللَّهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ (116)}.
(115) Je, mlidhani ya kwamba tuliwaumba bure, na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa? 116. Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki, hapana mungu yeyote isipokuwa Yeye, Mola Mlezi wa 'Arshi Tukufu.
#
{115 - 116} أي: {أفحَسِبْتُم} أيُّها الخلقُ، {أنَّما خَلَقْناكم عَبَثاً}؛ أي: سدىً وباطلاً تأكلون وتشربون وتمرَحون وتتمتَّعون بَلذَّات الدُّنيا ونتركُكم لا نأمُرُكم ولا ننهاكم ولا نُثيبكم ونعاقبكم، ولهذا قال: {وأنَّكم إلينا لا تُرْجَعونَ}؟ لا يَخْطُر هذا ببالكم. {فتعالى اللهُ}؛ أي: تعاظمَ وارتفعَ عن هذا الظنِّ الباطل الذي يرجِع إلى القدح في حكمته، {المَلكُ الحقُّ لا إله إلاَّ هو ربُّ العرش الكريم}: فكونُهُ ملكاً للخلق كلِّهم حقًّا في صدقِهِ ووعدِهِ [و] وعيدِهِ مألوهاً معبوداً لما له من الكمال ربَّ العرش العظيم فما دونه من باب أولى يمنَعُ أن يَخْلُقَكم عَبَثاً.
{116-115} Yaani, "je, mlidhani," enyi waumbwa; "ya kwamba tuliwaumba bure." Yaani, bure bila ya sababu na batili; mle na mnywe na mfurahi na mpumbae kwa mapambo ya dunia, na tuwaache na tusiwaamrishe na wala tusiwakataze na wala tusiwapeni thawabu na tusiwapeni dhambi. Na kwa sababu hii akasema, "na ya kwamba nyinyi, kwetu hamtarudishwa?" Hili haliingii akilini mwenu hata kidogo. "Ametukuka Mwenyezi Mungu;" yaani, ametukuka na amenyanyuka dhidi ya dhana hii batili, ambayo inarudi kwenye kashfa kwa hekima yake. "Mfalme wa Haki, hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A'rshi Tukufu." Na kuwa kwake Mmiliki wa viumbe wote ni haki katika ukweli wake na ahadi yake, "na" na furaha yake ni mwabudiwa kwa yale aliyo nayo kutokana na ukamilifu wa Mola wa A'rshi kuu, na vilivyo duni yake kutoka kwa mlango wa kwanza inapinga kuwaumba bure bila ya sababu.
{وَمَنْ يَدْعُ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِنْدَ رَبِّهِ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ (117) وَقُلْ رَبِّ اغْفِرْ وَارْحَمْ وَأَنْتَ خَيْرُ الرَّاحِمِينَ (118)}.
(117) Na anayemuomba - pamoja na Mwenyezi Mungu - mungu mwenginewe, hana ushahidi wa hili; basi bila ya shaka hisabu yake iko kwa Mola wake Mlezi. Kwa hakika makafiri hawafanikiwi. 118. Nawe sema, "Mola wangu Mlezi, Samehe na urehemu nawe ni Mbora wa wanaorehemu."
#
{117} أي: ومن دعا مع الله آلهةً غيره بلا بيِّنة من أمرِهِ ولا برهانٍ على ذلك يدلُّ على ما ذهب إليه، وهذا قيدٌ ملازمٌ؛ فكلُّ مَن دعا غير الله؛ فليس له برهانٌ على ذلك، بل دلَّت البراهينُ على بطلانِ ما ذهبَ إليه، فأعرض عنها ظلماً وعناداً؛ فهذا سيقدُمُ على ربِّه فيجازيه بأعمالِهِ ولا ينيلُه من الفلاح شيئاً؛ لأنه كافر، {إنَّه لا يفلحُ الكافرونَ}: فكفرُهم منعهم من الفلاح.
{117} Yaani, anayeomba miungu isiyokuwa yeye pamoja na Mwenyezi Mungu bila ya ushahidi wowote juu ya jambo lake hilo, na hakuna uthibitisho wowote unaoonyesha alichokifanya. Na hili ni sharti linalifungamana la suala hili wala haliachani nalo kamwe. Kwa hivyo, kila aombaye asiyekuwa Mwenyezi Mungu, basi hana uthibitisho wowote wa hilo. Bali uthibitisho wote uliashiria ubatili wa yale aliyoyafanya, lakini akayapa mgongo kwa dhuluma na ukaidi. Basi mtu huyu atakuja mbele ya Mola wake Mlezi, na atamlipa kwa matendo yake, wala hatamfanikisha kamwe, kwa sababu yeye ni kafiri. "Kwa hakika makafiri hawatafanikiwa" kwa kuwa ukafiri wao uliwazuia kufaulu.
#
{118} {وقل}: داعياً لربِّك مخلصاً له الدين: {ربِّ اغْفِرْ}: لنا حتى تُنْجِيَنا من المكروه، وارحَمْنا لتوصِلَنا برحمتك إلى كلِّ خير. {وأنت خيرُ الراحمين}: فكلُّ راحم للعبدِ؛ فالله خيرٌ له منه، أرحمُ بعبدِهِ من الوالدة بولدِها، وأرحمُ به من نفسه.
{118} "Nawe sema," ukimuomba Mola wako Mlezi huku ukimkusudia Yeye tu katika dini, "Mola wangu Mlezi, samehe," dhambi zetu ili utuepushe na machukizo, na uturehemu ili utufikishe kwa rehema zako kwenye kila la heri. "Nawe ni Mbora wa wanaorehemu." Kwa maana, kila anayemrehemu mja, Mwenyezi Mungu ni Mbora zaidi kwake kumliko, na ni Mwenye kumrehemu zaidi mja wake kuliko mama kwa mtoto wake, na ni Mwenye kumrehemu zaidi kuliko yeye mwenyewe anavyojirehemu.
Imekamilika tafsiri ya Surat Al-Muuminun, kwa fadhila zake na wema wake.
* * *