Tafsiri ya Surat Ibrahim - rehema na amani ziwe juu yake
Tafsiri ya Surat Ibrahim - rehema na amani ziwe juu yake
Nayo iliteremka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{الر كِتَابٌ أَنْزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَى صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ (1) اللَّهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَوَيْلٌ لِلْكَافِرِينَ مِنْ عَذَابٍ شَدِيدٍ (2) الَّذِينَ يَسْتَحِبُّونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَيَصُدُّونَ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا أُولَئِكَ فِي ضَلَالٍ بَعِيدٍ (3)}
1. Alif Lam Ra. Hiki ni Kitabu tulichokiteremsha kwako ili uwatoe watu kwenye giza mbalimbali uwapeleke kwenye mwangaza, kwa idhini ya Mola wao Mlezi, uwafikishe kwenye Njia ya Mwenye nguvu, Msifika, 2. Naye ni Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake Yeye vyote vilivyo katika mbingu zote na ardhi. Na ole wao makafiri kwa adhabu kali! 3. Wale wanaofadhilisha uhai wa dunia kuliko Akhera, na wanawazuilia watu Njia ya Mwenyezi Mungu, na wanataka kuipotosha. Hao wako katika upotofu wa mbali.
#
{1 - 2} يخبر تعالى أنه أنزل كتابه على رسوله محمد - صلى الله عليه وسلم -؛ لنفع الخلق؛ ليخرج الناس من ظلمات الجهل والكفر والأخلاق السيِّئة وأنواع المعاصي إلى نور العلم والإيمان والأخلاق الحسنة. وقوله: {بإذن ربِّهم}؛ أي: لا يحصل منهم المراد المحبوب لله إلا بإرادةٍ من الله ومعونة؛ ففيه حثٌّ للعباد على الاستعانة بربهم. ثم فسَّر النور الذي يهديهم إليه هذا الكتاب، فقال: {إلى صراط العزيز الحميد}؛ أي: الموصل إليه وإلى دار كرامته، المشتمل على العلم بالحقِّ والعمل به. وفي ذكر العزيز الحميد بعد ذكر الصراط الموصل إليه إشارة إلى أنَّ مَنْ سَلَكه؛ فهو عزيزٌ بعزِّ الله، قويٌّ ولو لم يكن له أنصار إلاَّ الله، محمودٌ في أموره، حسن العاقبة، وليدلَّ ذلك على أنَّ صراطَ الله من أكبر الأدلَّة على ما لله من صفات الكمال ونعوت الجلال، وأنَّ الذي نصبه لعباده عزيزُ السلطان حميدٌ في أقواله وأفعاله وأحكامه، وأنه مألوهٌ معبودٌ بالعبادات التي هي منازل الصراط المستقيم، وأنه كما أن له ملك السماوات والأرض خلقاً ورزقاً وتدبيراً؛ فله الحكم على عباده بأحكامه الدينيَّة؛ لأنَّهم ملكه، ولا يَليق به أن يترُكَهم سدىً. فلما بيَّن الدليل والبرهان؛ توعَّد مَن لم يَنْقَدْ لذلك، فقال: {وويلٌ للكافرين من عذابٍ شديدٍ}: لا يقدَّر قَدْره، ولا يوصَفُ أمره.
{1 - 2} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba aliteremsha Kitabu Chake kwa Mtume Wake Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwa manufaa ya viumbe, nayo ni kuwatoa watu katika giza la ujinga, ukafiri, tabia mbaya, na aina mbalimbali za maasia hadi kwenye nuru ya elimu, imani na tabia nzuri. Na kauli yake, "kwa idhini ya Mola wao Mlezi;" yaani, hawawezi kufanya kunachohitajika, kinachopendwa na Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa idhini na msaada wa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo ndani yake kuna himizo kwa waja juu kuomba msaada kwa Mola wao Mlezi. Kisha akaibainisha nuru ambayo kitabu hiki kinawaongoza kuiendea,
akasema: "Kwenye Njia ya Mwenye Nguvu, Msifika." Yaani, kuifikia na kufikia nyumba ya utukufu wake, ambacho kinajumuisha kuijua haki na kuifanyia kazi. Na katika kumtaja Mwenye nguvu, Msifika baada ya kutaja njia inayoelekea huko kuna ishara kwamba mwenye kuifuata, basi yeye ni mtukufu kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu, mwenye nguvu hata kama hana wasaidizi isipokuwa Mwenyezi Mungu, mwenye kusifiwa katika mambo yake, mwenye mwisho mwema, na hii inaashiria kuwa njia ya Mwenyezi Mungu ni moja ya ushahidi mkubwa zaidi juu ya kile alicho nacho Mwenyezi Mungu cha sifa kamilifu na utukufu. Na kwamba yule aliyewawekea waja wake ni mwenye mamlaka ya utukufu, Msifika katika kauli zake, vitendo vyake, na hukumu zake. Na kwamba Yeye ndiye afanyiwaye uungu, muabudiwa kwa ibada ambazo ndizo vituo vya njia hiyo iliyonyooka, na kwamba namna alivyo ina ufalme wa mbingu na ardhi kwa kuviumba, kuruzuku, na kuviendesha, basi anayo haki ya kuwahukumu waja Wake kwa mujibu wa hukumu zake za kidini. Kwa sababu hao ni milki yake, na haimfailii kuwaacha bure hivyo. Kwa hivyo, alipobainisha ushahidi na hoja, akawaahidi adhabu wale ambao hawakuyafuata hayo. Basi akasema, "Na ole wao makafiri kutokana na adhabu kali!" ambayo haiwezekani kupima kiasi chake, wala haiwezi kuelezwa jambo lake.
#
{3} ثم وصفهم بأنهم الذين استحبوا {الحياة الدُّنيا على الآخرة}: فرضوا بها واطمأنوا وغفلوا عن الدار الآخرة. {ويصدُّون} الناس {عن سبيل الله}: التي نَصَبها لعباده وبيَّنها في كتبه وعلى ألسنة رسله؛ فهؤلاء قد نابَذوا مولاهم بالمعاداة والمحاربة. {ويَبْغونها}؛ أي: سبيل الله {عوجاً}؛ أي: يحرصون على تهجينها وتقبيحها للتنفير عنها، ولكن يأبى الله إلا أن يُتِمَّ نوره ولو كره الكافرون. {أولئك}: الذين ذُكِر وصفهم {في ضلال بعيد}: لأنهم ضلُّوا وأضلُّوا وشاقُّوا اللهَ ورسولَهُ وحاربوهما؛ فأيُّ ضلال أبعدُ من هذا؟! وأما أهل الإيمان؛ فبعكس هؤلاء؛ يؤمنون بالله وآياته، ويستحبُّون الآخرة على الدنيا، ويدعون إلى سبيل الله، ويحسِّنونها مهما أمكنهم، ويبينون استقامتها.
{3} Kisha akawaeleza kuwa wao ndio wale wanaopendelea "uhai wa dunia hii kuliko Akhera" wakauridhia, na wakatulia, na wakaisahau nyumba ya Akhera. "Na wanawazuilia watu wasifuate Njia ya Mwenyezi Mungu" aliyowawekea waja wake, na akaibainisha katika Vitabu vyake na juu ya ndimi za Mitume wake. Basi watu hawa walimkataa Mola wao kwa ukaidi na vita. "Na wanaitakia" Njia hiyo ya mwenyezi Mungu "ijipinde;" yaani, wanafanya bidii katika kuichanganya na kuifanya kuwa mbovu ili kuwatenga watu nayo, lakini Mwenyezi Mungu anakataa isipokuwa kuikamilisha nuru yake, hata kama makafiri wataichukia. "Hao' waliotajwa maelezo yao
“wako katika upotevu wa mbali” kwa sababu wao wenyewe walipotea, na wakawapoteza wengine, na wakampinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakapigana vita nao. Basi ni upotofu gani ulio mbali zaidi kuliko huu? Na ama watu wa imani, wao wako kinyume na hawa. Wao wanamuamini Mwenyezi Mungu na ishara zake, na wanapendelea akhera kuliko dunia, na wanalingania katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wanaifanya kuwa nzuri namna wawezavyo, na wanabainisha unyoofu wake.
{وَمَا أَرْسَلْنَا مِنْ رَسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوْمِهِ لِيُبَيِّنَ لَهُمْ فَيُضِلُّ اللَّهُ مَنْ يَشَاءُ وَيَهْدِي مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (4)}.
4. Na hatukumtuma Mtume yeyote isipokuwa kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi Mwenyezi Mungu anampoteza amtakaye, na anamwongoa amtakaye. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
#
{4} وهذا من لطفه بعباده أنَّه ما أرسل رسولاً إلا بلسان قومه؛ ليبيِّن لهم ما يحتاجون إليه، ويتمكَّنون من تعلُّم ما أتى به، بخلاف ما لو أتى على غير لسانهم؛ فإنهم يحتاجون إلى تعلُّم تلك اللغة التي يتكلَّم بها، ثم يفهمون عنه. فإذا بيَّن [لهم] الرسول ما أمروا به ونُهوا عنه وقامت عليهم حجَّة الله؛ {فيضلُّ الله مَن يشاء}: ممَّن لم ينقدْ للهدى، {ويَهْدي من يشاء}: ممَّن اختصَّه برحمته. {وهو العزيز الحكيم}: الذي من عزته أنه انفرد بالهداية والإضلال وتقليب القلوب إلى ما شاء، ومن حكمته أنه لا يضع هدايته ولا إضلاله إلا بالمحل اللائق به.
ويستدل بهذه الآية الكريمة على أن علوم العربية الموصلة إلى تبيُّن كلامه وكلام رسوله أمورٌ مطلوبةٌ محبوبةٌ لله؛ لأنَّه لا يتمُّ معرفة ما أنزل على رسوله إلا بها، إلا إذا كان الناس في حالة لا يحتاجون إليها، وذلك إذا تمرَّنوا على العربية، ونشأ عليها صغيرهم، وصار طبيعةً لهم؛ فحينئذٍ قد اكتفوا المؤنة، وصلحوا على أن يَتَلَقَّوْا عن الله وعن رسوله ابتداءً، كما تلقَّى عنهم الصحابة رضي الله عنهم.
{4} Na hili ni katika upole wake kwa waja wake, kwamba hakumtuma Mtume yeyote isipokuwa kwa ulimi wa kaumu yake. Ili awabainishie kile wanachohitaji, ili wao pia waweze kujifunza katika yale aliyokuja nayo, tofauti na ikiwa angekuja na usiokuwa ulimi wao; basi wangehitaji kujifunza lugha ile anayozungumza, kisha ndiyo wamuelewe. Na Mtume anapowabainishia yale waliyoamrishwa na kukatazwa, na ikawasimamia hoja ya Mwenyezi Mungu juu yao. "Basi Mwenyezi Mungu humpoteza amtakaye" miongoni mwa wale ambao hawakufuata uwongofu huo "na anamwongoa amtakaye" katika wale aliowateua kuwapa rehema zake. "Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima" ambaye katika utukufu wake ni kwamba Yeye ndiye wa pekee wa kuongoa na kupoteza, na kuzigeuza nyoyo apendavyo. Na katika hekima yake ni kwamba haweki uwongofu wake wala kupoteza kwake isipokuwa mahali panapostahiki hayo. Na Aya hii tukufu inatumika kama ushahidi kwamba elimu za Kiarabu zinazofikisha katika kubainishwa maneno Yake na maneno ya Mtume Wake ni mambo yanayotakiwa na yanayopendwa na Mwenyezi Mungu. Kwa sababu haitimii kujua yale yaliyoteremshwa kwa Mtume wake bila ya hayo, isipokuwa ikiwa watu wamo katika hali ambayo hawahitaji hayo, na hilo ni kama wakifanyia Kiarabu mazoezi, na watoto wao wakakuwa nacho, na kikawa ni asili yao, basi hapo wakakuwa wametoshelezwa juhudi hiyo, na watakuwa wako tayari kupokea kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake mwanzoni, kama Maswahaba - Mwenyezi Mungu awawie radhi - walivyopokea kutoka kwao.
{وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَى بِآيَاتِنَا أَنْ أَخْرِجْ قَوْمَكَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَذَكِّرْهُمْ بِأَيَّامِ اللَّهِ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ (5) وَإِذْ قَالَ مُوسَى لِقَوْمِهِ اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ أَنْجَاكُمْ مِنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ وَيُذَبِّحُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ وَفِي ذَلِكُمْ بَلَاءٌ مِنْ رَبِّكُمْ عَظِيمٌ (6) وَإِذْ تَأَذَّنَ رَبُّكُمْ لَئِنْ شَكَرْتُمْ لَأَزِيدَنَّكُمْ وَلَئِنْ كَفَرْتُمْ إِنَّ عَذَابِي لَشَدِيدٌ (7) وَقَالَ مُوسَى إِنْ تَكْفُرُوا أَنْتُمْ وَمَنْ فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا فَإِنَّ اللَّهَ لَغَنِيٌّ حَمِيدٌ (8)}.
5. Na tulimtuma Musa na miujiza yetu,
tukamwambia: Watoe kaumu yako kwenye giza mbalimbali uwapeleke kwenye nuru. Na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu. Hakika katika hayo zipo ishara kwa kila mwenye kusubiri sawasawa, mwenye kushukuru sana. 6. Na Musa alipowaambia kaumu yake, "Kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu pale alipowaokoa kutokana na watu wa Firauni waliokuwa wakiwatia adhabu mbaya kabisa, wakiwachinja wana wenu wanaume, na wakiwaacha hai wanawake wenu. Na katika hayo ulikuwa mtihani mkubwa unaotoka kwa Mola wenu Mlezi." 7.
Na alipotangaza Mola wenu Mlezi: Mkishukuru, nitawazidishia; na mkikufuru, basi adhabu yangu ni kali. 8.
Na Musa alisema: Mkikufuru nyinyi na wote walio katika dunia, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifika.
#
{5} يخبر تعالى أنه أرسل موسى بآياته العظيمة الدالَّة على صدق ما جاء به وصحَّته، وأمره بما أمر الله به رسوله محمداً - صلى الله عليه وسلم -، بل وبما أمر به جميع الرسل قومهم: {أن أخْرِجْ قومك من الظُّلمات إلى النور}؛ أي: ظلمات الجهل والكفر وفروعه إلى نور العلم والإيمان وتوابعه. {وذكِّرْهم بأيام الله}؛ أي: بنعمه عليهم وإحسانه إليهم، وبأيَّامه في الأمم المكذِّبين ووقائعه بالكافرين؛ ليشكروا نعمه وليحذروا عقابه. {إنَّ في ذلك}؛ أي: في أيام الله على العباد، {لآياتٍ لكلِّ صبَّارٍ شكور}؛ أي: صبار في الضرَّاء والعسر والضيق، شكور على السراء والنعمة؛ فإنَّه يستدلُّ بأيامه على كمال قدرته وعميم إحسانه وتمام عدله وحكمته.
{5} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba alimtuma Musa na ishara zake kubwa zinazoonyesha ukweli na usahihi wa yale aliyokuja nayo, na akamuamrisha yale aliyomuamrisha Mwenyezi Mungu Mtume wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake; - bali yale Mitume wote waliwaamrisha kaumu zao. "Watoe kaumu yako kwenye giza mbalimbali hadi kwenye nuru;" yaani, giza la ujinga, ukafiri na matawi yake hadi katika nuru ya elimu, imani na matawi yake. "Na wakumbushe siku za Mwenyezi Mungu;" yaani, neema zake juu yao na wema wake kwao. Na siku zake pia katika umma waliokadhibisha na matukio yake dhidi ya makafiri, ili washukuru neema zake na watahadhari adhabu yake. "Hakika katika hayo;" yaani, katika siku za Mwenyezi Mungu juu ya waja wake, "zipo ishara kwa kila mwenye kusubiri sawasawa, mwenye kushukuru sana." Yaani, mwenye kusubiri katika dhiki, ugumu, taabu, mwenye kushukuru sana juu ya nyakati nzuri na neema. Kwa maana siku zake zinatumika kama ushahidi juu ya ukamilifu wa uwezo wake, na ujumla wa wema wake, na ukamilifu wa uadilifu wake na hekima yake.
#
{6} ولهذا امتثل موسى عليه السلام أمر ربِّه، فذكَّرهم نعم الله، فقال: {اذكروا نعمة الله عليكم}؛ أي: بقلوبكم وألسنتكم، {إذ أنجاكم من آل فرعونَ يسومونكم}؛ أي: يُولُونكم، {سوء العذاب}؛ أي: أشده. وفسَّر ذلك بقوله: {ويذبِّحون أبناءكم ويَسْتَحْيون نساءكم}؛ أي: يبقونهنَّ فلا يقتلونهنَّ. {وفي ذلكم}: الانجاء {بلاءٌ من ربِّكم عظيمٌ}؛ أي: نعمة عظيمة، أو وفي ذلكم العذاب الذي ابتُليتم به من فرعون وملئه ابتلاءٌ من الله عظيمٌ لكم لينظر هل تصبرون أم لا.
{6} Na ndiyo maana Musa - amani ziwe juu yake - akatekeleza amri ya Mola wake Mlezi, akawakumbusha neema za Mwenyezi Mungu,
akasema: "Kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu" kwa nyoyo zenu na ndimi zenu, "pale alipowaokoa kutoka kwa watu wa Firauni waliowatia adhabu mbaya kabisa" na akaeleza hayo kwa kauli yake "na wakiwachinja wana wenu wanaume, na wakiwaacha hai wanawake wenu. Na katika hayo" yaani kuwaokoa "ulikuwa mtihani mkubwa kutoka kwa Mola wenu Mlezi;" yaani, neema kubwa. Ama katika hayo kulikuwa na adhabu ambayo Firaun na waheshimiwa wake waliwajaribu kwayo; mtihani mkubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili aone ikiwa mtasubiri au la.
#
{7} وقال لهم حاثًّا على شكر نعم الله: {وإذْ تأذَّن ربُّكم}؛ أي: أعلم ووعد، {لئن شكرتُم لأزيدنَّكم}: من نعمي، {ولئن كفرتُم إن عذابي لشديدٌ}: ومن ذلك أنْ يزيل عنهم النعمة التي أنعم بها عليهم. والشكرُ: هو اعتراف القلب بنعم الله، والثناء على الله بها، وصرفها في مرضاة الله تعالى. وكفر النعمة ضدُّ ذلك.
{7} Na akawaambia akiwahimiza wazishukuru neema za Mwenyezi Mungu "Na alipotangaza Mola wenu Mlezi: Mkishukuru, hakika nitawazidishia" neema zangu "na mkikufuru, basi hakika adhabu yangu ni kali." Na katika hayo ni kwamba atawaondolea neema hizo alizowaneemesha kwazo. Na kushukuru ni moyo kukiri neema za Mwenyezi Mungu, kumsifu Mwenyezi Mungu juu yake, na kuzitumia katika ayapendayo Mwenyezi Mungu Mtukufu. Nako kufuru neema ni kinyume cha hayo.
#
{8} {وقال موسى إن تكفُروا أنتم ومن في الأرض جميعاً}: فلن تضرُّوا الله شيئاً، فإنَّ الله غنيٌ حميدٌ، فالطاعات لا تزيد في ملكه، والمعاصي لا تنقصه، وهو كامل الغنى، حميدٌ في ذاته وأسمائه وصفاته وأفعاله، ليس له من الصفات إلا كل صفة حمدٍ وكمال، ولا من الأسماء إلا كل اسم حسن، ولا من الأفعال إلاَّ كل فعل جميل.
{8} "Na Musa alisema: Mkikufuru nyinyi na wote walio katika dunia" basi hamtamdhuru Mwenyezi Mungu hata kidogo. Kwa maana, hakika Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Msifika. Basi utiifu haumzidishii chochote katika ufalme wake, na uasi haumpunguzii. Naye ndiye Mkwasi kamili, Msifika katika dhati yake, na majina yake na sifa zake, na vitendo vyake, hana sifa isipokuwa kila sifa ya kusifika na ukamilifu, wala hana jina isipokuwa kila jina zuri, wala vitendo isipokuwa kila kitendo kizuri.
{أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَبَأُ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ وَالَّذِينَ مِنْ بَعْدِهِمْ لَا يَعْلَمُهُمْ إِلَّا اللَّهُ جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُمْ بِالْبَيِّنَاتِ فَرَدُّوا أَيْدِيَهُمْ فِي أَفْوَاهِهِمْ وَقَالُوا إِنَّا كَفَرْنَا بِمَا أُرْسِلْتُمْ بِهِ وَإِنَّا لَفِي شَكٍّ مِمَّا تَدْعُونَنَا إِلَيْهِ مُرِيبٍ (9) قَالَتْ رُسُلُهُمْ أَفِي اللَّهِ شَكٌّ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ يَدْعُوكُمْ لِيَغْفِرَ لَكُمْ مِنْ ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرَكُمْ إِلَى أَجَلٍ مُسَمًّى قَالُوا إِنْ أَنْتُمْ إِلَّا بَشَرٌ مِثْلُنَا تُرِيدُونَ أَنْ تَصُدُّونَا عَمَّا كَانَ يَعْبُدُ آبَاؤُنَا فَأْتُونَا بِسُلْطَانٍ مُبِينٍ (10) قَالَتْ لَهُمْ رُسُلُهُمْ إِنْ نَحْنُ إِلَّا بَشَرٌ مِثْلُكُمْ وَلَكِنَّ اللَّهَ يَمُنُّ عَلَى مَنْ يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَمَا كَانَ لَنَا أَنْ نَأْتِيَكُمْ بِسُلْطَانٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّهِ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ (11) وَمَا لَنَا أَلَّا نَتَوَكَّلَ عَلَى اللَّهِ وَقَدْ هَدَانَا سُبُلَنَا وَلَنَصْبِرَنَّ عَلَى مَا آذَيْتُمُونَا وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُتَوَكِّلُونَ (12)}.
9. Je, hazikuwafikia habari za wale waliokuwa kabla yenu? Kaumu ya Nuhu, na 'Aadi, na Thamud, na wale waliokuwa baada yao, ambao hakuna awajuaye isipokuwa Mwenyezi Mungu? Mitume wao waliwajia kwa hoja zilizo wazi, na wao wakarudisha mikono yao kwenye vinywa vyao,
wakasema: Hakika sisi tumeyakufuru hayo mliyotumwa nayo, na hakika sisi tuko katika shaka kubwa na hayo mnayotuitia. 10.
Mitume wao wakasema: Ati kuna shaka kuhusiana na Mwenyezi Mungu, Muumba mbingu na ardhi? Yeye anawaita ili awafutie madhambi yenu, na awape muhula mpaka muda uliowekwa.
Wakasema: Nyinyi si chochote isipokuwa ni wanadamu tu kama sisi. Mnataka kutuzuilia na yale waliyokuwa wakiabudu baba zetu. Basi tujieni na hoja iliyo wazi. 11.
Mitume wao wakawaambia: Sisi kweli si chochote isipokuwa ni wanadamu kama nyinyi. Lakini Mwenyezi Mungu humneemesha amtakaye katika waja wake. Wala sisi hatuwezi kuwaletea uthibitisho isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na juu ya Mwenyezi Mungu basi na wategemee Waumini. 12. Na tuna nini hata tusimtegemee Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ametuongoa kwenye Njia zetu. Na hakuna hakika tutayavumilia hayo maudhi mnayotuudhi nayo. Na juu ya Mwenyezi Mungu na wategemee wanaotegemea.
#
{9} يقول تعالى مخوِّفاً عباده ما أحلَّه بالأمم المكذِّبة حين جاءتهم الرسل فكذَّبوهم، فعاقبهم بالعقاب العاجل الذي رآه الناس وسمعوه، فقال: {ألم يأتِكُم نبأ الذين من قبلكم قومُ نوح وعادٍ وثمودَ}: وقد ذكر الله قصصهم في كتابه وبسطها. {والذين من بعدِهم لا يعلمُهم إلاَّ الله}: من كثرتهم وكون أخبارهم اندرست؛ فهؤلاء كلُّهم {جاءتهم رسلُهم بالبيناتِ}؛ أي: بالأدلة الدالَّة على صدق ما جاؤوا به، فلم يرسل الله رسولاً إلا آتاه من الآيات ما يؤمِنُ على مثلِهِ البشرُ؛ فحين أتتهم رسلُهم بالبينات؛ لم ينقادوا لها، بل استكبروا عنها، {فردُّوا أيدِيَهم في أفواههم}؛ أي: لم يؤمنوا بما جاؤوا به، ولم يتفوَّهوا بشيء مما يدلُّ على الإيمان؛ كقوله: {جعلوا أصابِعَهم في آذانهم من الصواعِقِ حَذَرَ الموت}. {وقالوا} صريحاً لرسلهم: {إنَّا كَفَرْنا بما أرسِلْتم به وإنا لفي شكٍّ مما تدعوننا إليه مريبٍ}؛ أي: موقع في الريبة.
{9} Yeye Mtukufu anasema akiwahofisha waja wake kwa yale aliyowatia umma waliokadhibisha walipojiwa na Mitume lakini wa wakawakadhibisha, basi akawaadhibu kwa adhabu ya haraka ambayo watu waliiona na kuisikia,
kwa hivyo akasema: "Je, hazikuwajia habari za wale walio kabla yenu? Kaumu ya Nuhu, na 'Aadi, na Thamud" Na Mwenyezi Mungu alivitaja visa vyao katika Kitabu chake na akavipanua; "Na wale waliokuwa baada yao, ambao hakuna awajuaye isipokuwa Mwenyezi Mungu?" Kwa sababu ya wingi wao na habari zao zilipotelea mbali. Basi hao wote "Mitume wao waliwajia kwa hoja zilizo wazi" zenye kuonyesha ukweli wa yale waliyokuja nayo, kwani Mwenyezi Mungu hakumtuma Mtume yeyote isipokuwa alimpa ishara ambazo mfano wake wanadamu wanaziamini. Lakini hawa walipojiwa na Mitume wao na hoja zilizo wazi, hawakuzifuata, bali walizifanyia kiburi, "wakarudisha mikono yao kwenye vinywa vyao." Yaani, hawakuamini yale waliyowajia nayo, na wala hawakutamka lolote linaloashiria kuwa wameamini, kama kauli yake, "wakawa wanatia vidole vyao katika masikio yao kwa sababu ya mingurumo, kwa kuogopa kufa." "Na wakawaambia" waziwazi Mitume wao, "Hakika sisi tumeyakataa hayo mliyotumwa nayo, na hakika sisi tuna shaka kubwa na hayo mnayotuitia."
#
{10} وقد كذبوا في ذلك وظلموا، ولهذا {قالتْ} لهم {رسُلُهم أفي الله شكٌّ}؛ أي: فإنه أظهر الأشياء وأجلاها؛ فمن شَكَّ في الله {فاطرِ السمواتِ والأرضِ}: الذي وجود الأشياء مستندٌ إلى وجوده؛ لم يكن عنده ثقةٌ بشيء من المعلومات، حتى الأمور المحسوسة. ولهذا خاطبتهم الرسل خطابَ من لا يشكُّ فيه، ولا يصلح الريب فيه. {يدعوكم}: إلى منافعكم ومصالحكم، {ليغفرَ لكم من ذنوبكم ويؤخِّرَكم إلى أجل مسمًّى}؛ أي: ليثيبكم على الاستجابة لدعوته بالثواب العاجل والآجل، فلم يدعُكم لينتفع بعبادتكم، بل النفع عائد إليكم. فردُّوا على رسلهم ردَّ السفهاء الجاهلين، {وقالوا} لهم: {إنْ أنتم إلاَّ بشرٌ مثلُنا}؛ أي: فكيف تَفْضُلوننا بالنبوة والرسالة؟ {تريدون أن تصدُّونا عما كان يعبد آباؤنا}: فكيف نترُكُ رأي الآباء وسيرتهم لرأيكم؟! وكيف نطيعكم وأنتم بشرٌ مثلنا؟! {فأتونا بسلطانٍ مبينٍ}؛ أي: بحجَّة وبيِّنة ظاهرة، ومرادهم بيِّنة يقترحونها هم، وإلاَّ؛ فقد تقدَّم أنَّ رسلهم جاءتهم بالبينات.
10. Lakini walidanganya katika hayo, na wakadhulumu,
na ndiyo maana "wakawaambia Mitume wao: Je, kuna shaka kuhusiana na Mwenyezi Mungu" kwa sababu yeye ndiye wa dhahiri zaidi ya vitu vyote na wa wazi zaidi. Kwa hivyo mwenye kuwa na shaka juu ya Mwenyezi Mungu "Muumba wa mbingu na ardhi" ambaye uwepo wa vitu vyote unategemea juu ya uwepo wake, basi huyo hana imani yoyote katika habari zozote, hata mambo yanayohisika. Na ndiyo maana Mitume hao wakawazungumzisha kwa mazungumzo ya mtu ambaye hana shaka naye, na wala haipasi kuwepo na shaka kuhusiana naye. "Yeye anawaita" katika manufaa yenu na masilahi yenu, "ili awafutie katika madhambi yenu, na awaache mpaka muda uliowekwa." Yaani, ili awalipe kwa sababu ya kuitikia wito wake kwa malipo ya haraka na ya baadaye. Na wala hakuwaita ili anufaike na ibada yenu, bali manufaa yake yatarudi kwenu. Lakini wao wakawajibu Mitume wao kama wanavyofanya wapumbavu wajinga,
"na wakasema" wakiwaambia: "Nyinyi si chochote isipokuwa ni wanaadamu mfano wetu." Yaani, basi vipi mnakuwa bora zaidi yetu kwa unabii na utume? "Mnataka kutuzuia yale waliyokuwa wakiabudu baba zetu?" Basi vipi tuache rai na mwenendo wa baba zetu kwa rai yenu? Na vipi tuwatii nyinyi ilhali nyinyi ni binadamu mfano wetu? "Basi tuleteeni hoja iliyo wazi;" yaani, hoja na ushahidi ulio wazi. Na kwa hili walikuwa wanakusudia ushahidi ambao wanaupendekeza wao. Vinginevyo, hakika ilikwisha tangulia kwamba Mitume wao waliwajia na hoja zilizo wazi.
#
{11} {قالت لهم رسلهم} مجيبين لاقتراحهم واعتراضهم: {إن نحن إلاَّ بشرٌ مثلُكم}؛ أي: صحيح وحقيقة أنَّا بشرٌ مثلكم. {ولكن} ليس في ذلك ما يدفعُ ما جئنا به من الحقِّ؛ فإنَّ {الله يَمُنُّ على مَن يشاء من عبادِهِ}؛ فإذا منَّ الله علينا بوحيه ورسالته؛ فذلك فضله وإحسانه، وليس لأحدٍ أن يَحْجُرَ على الله فضله ويمنعه من تفضله؛ فانظروا ما جئناكم به؛ فإنْ كان حقًّا؛ فاقبلوه، وإن كان غير ذلك؛ فردُّوه، ولا تجعلوا حالنا حجَّة لكم على ردِّ ما جئناكم به، وقولكم: {فائتونا بسلطانٍ مبين}، فإنَّ هذا ليس بأيدينا وليس لنا من الأمر شيء. {وما كان لنا أن نأتِيَكم بسلطانٍ إلاَّ بإذن الله}: فهو الذي إن شاء جاءكم به وإن شاء لم يأتِكُم به، وهو لا يفعل إلاَّ ما هو مقتضى حكمته ورحمته. {وعلى الله}: لا على غيره، {فليتوكَّل المؤمنون}: فيعتمدون عليه في جلب مصالحهم ودفع مضارِّهم؛ لعلمهم بتمام كفايته وكمال قدرتِهِ وعميم إحسانه، ويثقون به في تيسير ذلك، وبحسب ما معهم من الإيمان يكونُ توكُّلهم. فعُلم بهذا وجوب التوكُّل وأنَّه من لوازم الإيمان ومن العبادات الكبار التي يحبُّها الله ويرضاها لتوقُّف سائر العبادات عليه.
{11} "Mitume wao wakawaambia" kwa kuwajibu pendekezo lao na upinzani wao: "Sisi kweli si chochote isispokuwa ni wanadamu kama nyinyi," na hilo ni sahihi na ndio uhakika wa mambo kwamba sisi ni wanadamu kama nyinyi. "Lakini" hakuna katika hilo cha kuzuia yale tuliyokuja nayo ya haki. Kwani "Mwenyezi Mungu humneemesha amtakaye katika waja wake." Kwa hivyo Mwenyezi Mungu anapotuneemesha kwa ufunuo na ujumbe wake, basi hilo ni fadhila zake na ukarimu wake. Na hakuna yeyote mwenye haki ya kumwekea kipimo Mwenyezi Mungu katika kupeana fadhila zake na kumzuia kutoa fadhila zake hizo. Kwa hivyo, tazameni yale tuliyowajia nayo, kama ni haki, basi ikubalini. Na kama si hivyo, basi ikataeni, wala msiifanye hali yetu kuwa ndiyo hoja yenu ya kuyakataa yale tuliyowajia nayo. Na kauli yenu "Basi tuleteeni hoja iliyo wazi" hili halimo mikononi mwetu, na sisi hatuna chochote katika jambo hilo. "Wala sisi hatuwezi kuwaletea uthibitisho isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu" kwani Yeye ndiye akitaka, anawaletea, na akitaka, hawaletei. Naye hafanyi isipokuwa kile kinachotakiwa tu na hekima yake na rehema yake. "Na juu ya Mwenyezi Mungu" na si kwa mwengine yeyote "basi na wategemee Waumini," katika kuwaletea yenye kuwanufaisha na kuwaepusha na yenye kuwadhuru. Kwa sababu wanajua utoshelevu wake kamili, na ukamilifu wa uwezo wake, na ujumla wa wema wake, na wanamuamini Yeye katika kuendesha hayo. Na kulingana na imani waliyo nayo, ndiyo kunakuwa kutegemea kwao. Basi ikajulikana kwa hilo ulazima wa kutegemea kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba ni katika matakwa ya imani na ni mojawapo ya ibada kubwa ambazo Mwenyezi Mungu anazipenda na kuziridhia kwa maana ibada zote zinaitegemea hii.
#
{12} {وما لنا أن لا نتوكَّل على الله وقد هدانا سُبُلَنا}؛ أي: أيُّ شيء يمنعنا من التوكُّل على الله والحال أننا على الحقِّ والهدى، ومن كان على الحقِّ والهدى؛ فإنَّ هداه يوجب له تمام التوكُّل، وكذلك ما يُعْلَمُ من أنَّ الله متكفِّل بمعونة المهتدي وكفايته، يدعو إلى ذلك؛ بخلاف من لم يكن على الحقِّ والهدى؛ فإنَّه ليس ضامناً على الله؛ فإنَّ حاله مناقضةٌ لحال المتوكِّل؟! وفي هذا كالإشارة من الرسل عليهم الصلاة والسلام لقومهم بآيةٍ عظيمةٍ، وهو أنَّ قومهم في الغالب أنَّ لهم القهر والغلبة عليهم، فتحدَّتهم رسلُهم بأنَّهم متوكِّلون على الله في دفع كيدهم ومكرهم، وجازمون بكفايته إيَّاهم، وقد كفاهم الله شرَّهم مع حرصهم على إتلافهم وإطفاء ما معهم من الحقِّ، فيكون هذا كقول نوح لقومِهِ: {يا قوم إن كان كَبُرَ عليكم مقامي وتذكيري بآيات الله فعلى الله توكَّلْتُ فأجمِعوا أمرَكم وشُركاءَكم ثمَّ لا يكنْ أمرُكم عليكم غُمَّة ثم اقضوا إليَّ ولا تُنظِرونِ ... } الآيات، وقول هود عليه السلام: {قالَ إنِّي أُشْهِدُ الله واشْهَدوا أني بريءٌ مما تشرِكونَ من دونِهِ فكيدوني جميعاً ثم لا تُنظِرونِ}. {ولَنَصْبِرَنَّ على ما آذَيْتُمونا}: ولنستمرنَّ على دعوتِكم ووعظِكم وتذكيركم، ولا نبالي بما يأتينا منكم من الأذى؛ فإنَّا سنوطِّن أنفسنا على ما ينالنا منكم من الأذى؛ احتساباً للأجر ونصحاً لكم، لعلَّ الله أن يهدِيَكم مع كثرة التذكير. {وعلى الله}: وحدَه لا على غيره، {فليتوكَّل المتوكِّلون}: فإنَّ التوكُّل عليه مفتاح لكل خير.
واعلم أن الرسل عليهم الصلاة والسلام توكُّلهم في أعلى المطالب وأشرف المراتب، وهي التوكُّل على الله في إقامة دينه ونصره وهداية عبيده وإزالة الضَّلال عنهم. وهذا أكمل ما يكون من التوكُّل.
"Na tuna nini hata tusimtegemee Mwenyezi Mungu, na ilhali Yeye ametuongoa kwenye Njia zetu?" Yaani, ni kitu gani kinatuzuia kumtegemea Mwenyezi Mungu ilhali tuko katika haki na uongofu. Na yule aliye katika haki na uwongofu, basi uwongofu wake unalazimu kumtegemea Mwenyezi Mungu kiukamilifu. Na vile vile kile kinachojulikana kwamba Mwenyezi Mungu anamdhamini kwa msaada na kumtosheleza mwongofu, hilo linaitia katika hayo. Na hilo ni Tofauti na yule ambaye hayuko katika haki na uwongofu, yeye hana udhamini wowote wa Mwenyezi Mungu. Hali yake ni kinyume na hali ya wale wanaomtegemea Mwenyezi Mungu? Huku ni kama kuashiria kutoka kwa Mitume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwashukie - kwa kaumu zao juu ya ishara kubwa, ambayo ni kwamba kaumu yao katika hali nyingi wana nguvu na ushindi dhihi yao. Kwa hivyo Mitume wao wakawapa changamoto ya kwamba wao wanamtegemea Mwenyezi Mungu katika kuwaondolea njama zao na vitimbi vyao, na wana yakini kuwa Yeye atawatosha dhidi yao. Na hakika Mwenyezi Mungu aliwatosheleza uovu wao pamoja na pupa yao ya kuwaangamiza na kuzima haki waliyo nayo. Haya ni kama Nuh alivyowaambia kaumu yake, "Enyi kaumu yangu! Ikiwa ni kukubwa kwenu kukaa kwangu nanyi na kukumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungu, basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, nyinyi likusanyeni jambo lenu pamoja na washirika wenu, kisha jambo lenu hilo lisiwe la kufichikana kwenu, kisha nihukumuni, wala msinipe muhula..." hadi mwisho wa Aya. Na kauli ya Hud - amani iwe juu yake, - "Akasema, "Hakika, mimi ninamshuhudisha Mwenyezi Mungu, na nyinyi shuhudieni, ya kwamba mimi niko mbali na hao mnaowafanya washirika." Badala ya Yeye. Basi nyote nyinyi nipangieni njama, na kisha msinipe muhula!" "Na hakuna shaka sisi tutayavumilia hayo maudhi mnayotuudhi." Na hakika tutaendelea kuwalingania, na kuwaaishi, na kuwakumbusha, wala hatutajali udhia utakaotupata kutoka kwenu, tukitarajia malipo na kuwanasihi nyinyi. Huenda Mwenyezi Mungu akawaongoa pamoja na kuwakumbusha kwa wingi. "Na juu ya Mwenyezi Mungu" peke yake na si kwa mwingine yeyote "na wategemee wanaotegemea." Kwa maana, kumtegemea ndiyo ufunguo wa heri yote. Na jua kwamba kutegemea kwa Mitume - rehema ana amani ziwe juu yao - huwa katika matakwa ya juu kabisa na vyeo vitukufu zaidi, ambako ni kumtegemea Mwenyezi Mungu katika kuisimamisha Dini yake, na nusura yake na kuwaongoza waja wake, na kuwaondolea upotofu. Hii ndiyo aina kamili zaidi ya kutegemea.
{وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِرُسُلِهِمْ لَنُخْرِجَنَّكُمْ مِنْ أَرْضِنَا أَوْ لَتَعُودُنَّ فِي مِلَّتِنَا فَأَوْحَى إِلَيْهِمْ رَبُّهُمْ لَنُهْلِكَنَّ الظَّالِمِينَ (13) وَلَنُسْكِنَنَّكُمُ الْأَرْضَ مِنْ بَعْدِهِمْ ذَلِكَ لِمَنْ خَافَ مَقَامِي وَخَافَ وَعِيدِ (14) وَاسْتَفْتَحُوا وَخَابَ كُلُّ جَبَّارٍ عَنِيدٍ (15) مِنْ وَرَائِهِ جَهَنَّمُ وَيُسْقَى مِنْ مَاءٍ صَدِيدٍ (16) يَتَجَرَّعُهُ وَلَا يَكَادُ يُسِيغُهُ وَيَأْتِيهِ الْمَوْتُ مِنْ كُلِّ مَكَانٍ وَمَا هُوَ بِمَيِّتٍ وَمِنْ وَرَائِهِ عَذَابٌ غَلِيظٌ (17)}.
13.
Na wale waliokufuru wakawaambia Mitume wao: Hakika, tutawatoa katika nchi yetu, au lazima mtarudi katika mila yetu.
Basi Mola wao Mlezi aliwafunulia wahyi: Hakika tutawaangamiza madhalimu! 14. Na tutawaweka katika ardhi baada yao. Haya ni kwa anayehofu kusimamishwa mbele yangu, na akahofu ahadi yangu ya adhabu. 15. Na wakaomba ushindi, na akashindwa kila jabari mkaidi. 16. Ambaye nyuma yake ipo Jahannamu, na atanyweshwa katika maji ya usaha. 17. Awe anayagugumia, wala hawezi kuyameza. Na mauti yatamjia kutokea kila upande, naye wala hafi. Na zaidi ya hayo ipo adhabu nyengine kali vile vile.
#
{13} لما ذكر دعوة الرسل لقومهم ودوامهم على ذلك وعدم مللهم؛ ذكر منتهى ما وصلت بهم الحال مع قومهم، فقال: {وقال الذين كفروا لرسلهم}: متوعِّدين لهم: {لَنُخْرِجَنَّكم من أرضِنا أو لَتعودُنَّ في مِلَّتنا}: وهذا أبلغ ما يكون من الردِّ، وليس بعد هذا فيهم مطمع؛ لأنَّه ما كفاهم أن أعرضوا عن الهدى، بل توعَّدوهم بالإخراج من ديارهم، ونسبوها إلى أنفسهم، وزعموا أنَّ الرسل لا حقَّ لهم فيها، وهذا من أعظم الظُّلم؛ فإنَّ الله أخرج عباده إلى الأرض، وأمرهم بعبادته، وسخَّر لهم الأرض وما عليها يستعينون بها على عبادته؛ فمن استعان بذلك على عبادة الله؛ حلَّ له ذلك وخرج من التَّبِعة، ومن استعان بذلك على الكفر وأنواع المعاصي؛ لم يكن ذلك خالصاً له ولم يحلَّ له، فعلم أن أعداء الرسل في الحقيقة ليس لهم شيء من الأرض التي تَوَعَّدوا الرسل بإخراجهم منها. وإن رجَعْنا إلى مجرَّد العادة؛ فإنَّ الرسل من جملة أهل بلادهم وأفراد منهم؛ فلأيِّ شيء يمنعونهم حقًّا لهم صريحاً واضحاً؟! هل هذا إلا من عدم الدين والمروءة بالكلية؟! ولهذا لما انتهى مكرهم بالرسل إلى هذه الحال؛ ما بقي حينئذٍ إلاَّ أن يُمضي الله أمره وينصر أولياءه. {فأوحى إليهم ربُّهم لَنُهْلِكَنَّ الظالمين}: بأنواع العقوبات.
{13} Alipotaja ulinganiaji wa Mitume kwa kaumu zao na kudumu kwao katika hilo bila ya kuchoka, akataja hali ya mwisho zaidi waliyofika na kaumu yao,
akasema: "Na wale waliokufuru wakawaambia Mitume wao" huku wakiwatishia, "Hakika tutawatoa katika nchi yetu, au lazima mrudi katika mila yetu" Na hili ndilo jibu kubwa zaidi, ambalo baada ya hili hakuna matumaini yoyote juu yao. Kwa sababu haikutosha tu kuupa mgongo uwongofu, bali waliwatishia kuwatoa katika makazi yao, na wakayaita makazi hayo kwamba ni yao, na wakadai kuwa Mitume hawana haki yoyote humo. Na hii ndiyo dhuluma kubwa kabisa. Kwani Mwenyezi Mungu aliwatoa waja wake wakaja kwenye ardhi, na akawaamrisha kwamba wamwabudu, na akaitiisha ardhi na vyote vilivyomo kwa ajili yao, ili watafute msaada wa hayo katika kumwabudu. Kwa hivyo, Yeyote anayetumia hayo kumsaidia kumwabudu Mwenyezi Mungu, basi ni hivyo vinakuwa halali kwake na hawi wa kulaumiwa. Na mwenye kutafua msaada wa hivyo katika kukufuru na aina mbalimbali za madhambi, hivyo haviwezi kuwa vyake tu wala haviwi halali kwake. Kwa hivyo akajulikana kwamba maadui wa Mitume kwa hakika hawakuwa na chochote katika ardhi ambayo waliwatishia Mitume kwamba watawatoa humo. Na hata kama tutarudi katika desturi, Mitume ni miongoni mwa wakazi wa nchi zao na watu miongoni mwao. Basi ni kwa kitu gani wanawazuia kuwa na haki ya moja kwa moja na iliyo wazi? Je, haya si chochote isipokuwa ukosefu kamili wa dini na uungwana? Na ndiyo maana njama zao dhidi ya Mitume zilipoishia katika hali hii, haikubakia isipokuwa Mwenyezi Mungu kupitisha amri yake na kuwanusuru marafiki wake.
"Basi Mola wao Mlezi aliwafunulia wahyi: Hakika tutawaangamiza madhalimu" kwa aina mbalimbali za adhabu.
#
{14} {ولَنُسْكِنَنَّكُمُ الأرض من بعدهم ذلك}؛ أي: العاقبة الحسنة التي جعلها الله للرسل ومَنْ تَبِعَهم جزاء، {لِمَنْ خاف مقامي}: عليه في الدنيا، وراقب الله مراقبة من يعلم أنه يراه، {وخاف وعيدِ}؛ أي: ما توعَّدت به مَنْ عصاني؛ فأوجب له ذلك الانكفاف عمَّا يكرهُهُ الله والمبادرة إلى ما يحبُّه الله.
{14} "Na hakika tutawapa maskani katika ardhi baada yao. Hayo;" yaani, mwisho mwema aliowajaalia Mwenyezi Mungu Mitume wake na wale waliowafuata ni malipo "kwa yule anayehofu kusimamishwa mbele yangu" katika dunia, na akamchunga Mwenyezi Mungu kuchunga kwa yule anayejua kwamba anamuona. "Na akahofu maonyo yangu" niliyowaahidi kuwaadhibu wale walioniasi. Kwa hivyo, hilo likamfanya kujiepusha na yale ambayo Mwenyezi Mungu anachukia, na kuyaharakishia yale ambayo Mwenyezi Mungu anapenda.
#
{15} {واستفتحوا}؛ أي: الكفار؛ أي: هم الذين طلبوا واستعجلوا فَتْحَ الله وفرقانَهُ بين أوليائه وأعدائه، فجاءهم ما استفتحوا به، وإلاَّ؛ فالله حليمٌ، لا يعاجِل من عصاه بالعقوبة. {وخاب كلُّ جبارٍ عنيدٍ}؛ أي: خسر في الدنيا والآخرة من تجبَّر على الله وعلى الحقِّ وعلى عباد الله، [واستكبر] في الأرض، وعاند الرسل، وشاقَّهم.
{15} "Na wakaomba ushindi." Nao ni wale makafiri walioomba na kutaka ushindi wa Mwenyezi Mungu kuja haraka na upambanuzi wake baina ya marafiki zake na maadui zake, kisha ule ushindi waliokuwa wakitafuta ukawajia. Vinginevyo, Mwenyezi Mungu ni Mstahamilivu, na hamharakishii adhabu mwenye kumuasi; "na akashindwa kila jabari mkaidi." Yaani, alihasirika katika dunia na akhera kila mwenye kumfanyia kiburi Mwenyezi Mungu, na juu ya haki, na juu ya waja wa Mwenyezi Mungu
[na akatakabari] katika ardhi, na akawafanyia Mitume ukaidi, na akawapinga.
#
{16} {من ورائه جهنَّمُ}؛ أي: جهنَّم لهذا الجبار العنيد بالمرصاد؛ فلا بدَّ له من ورودها، فيذاق حينئذٍ العذاب الشديد. {ويُسْقى من ماءٍ صديدٍ}: في لونه وطعمه ورائحته الخبيثة، وهو في غاية الحرارة.
{16} "Ambaye nyuma yake ipo Jahannamu;" yaani, Jahannamu inamngoja dhalimu huyu mkaidi. Na ni lazima itaiingia, na ndipo ataonja adhabu kali; "na atanyweshwa katika maji ya usaha" katika rangi yake, ladha yake, na harufu yake mbaya. Nayo yatakuwa ya moto zaidi.
#
{17} {يَتَجَرَّعُه}: من العطش الشديد، {ولا يكادُ يُسيغُهُ}: فإنه إذا قرب إلى وجهه؛ شواه، وإذا وصل إلى بطنه؛ قطع ما أتى عليه من الأمعاء، {ويأتيه الموتُ من كلِّ مكان وما هو بميِّتٍ}؛ أي: يأتيه العذاب الشديد من كلِّ نوع من أنواع العذاب، وكلُّ نوع منه من شدَّته يبلغ إلى الموت، ولكنَّ الله قضى أن لا يموتوا؛ كما قال تعالى: {لا يُقْضى عليهم فيموتوا ولا يُخَفَّفُ عنهم من عذابها كذلك نَجْزي كلَّ كفورٍ}. وهم يصطرخون فيها، {ومن ورائِه}؛ أي: الجبار العنيد {عذابٌ غليظٌ}؛ أي: قويٌّ شديدٌ لا يعلم بوصفه وشدَّته إلا الله تعالى.
{17} "Awe anayagugumiza" kutokana na kiu kali, "wala hawezi kuyameza;" kwa maana, yanapoukaribia uso wake, yanambambua ngozi. Na yakifika tumboni mwake, yanayakata matumbo yote ambayo yanayafikia. "Na mauti yawe yanamjia kutokea kila upande, naye wala hafi." Yaani, atajiwa adhabu kali kwa kila aina yake. Na kila aina yake kwa sababu ya ukali wake inafikia mauti, lakini Mwenyezi Mungu alipitisha kwamba wasife, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "hawahukumiwi wakafa, wala hawatapunguziwa adhabu yake. Hivyo ndivyo tunavyomlipa kila mwenye kuzidi ukafiri." Na humo watapiga makelele, "Na zaidi ya hayo, ipo adhabu nyingine kali vile vile" kwa huyu jabari mkaidi. Atapata adhabu ya nguvu na mkali, ambayo hakuna ajuaye maelezo yake na ukali wake isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
{مَثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ أَعْمَالُهُمْ كَرَمَادٍ اشْتَدَّتْ بِهِ الرِّيحُ فِي يَوْمٍ عَاصِفٍ لَا يَقْدِرُونَ مِمَّا كَسَبُوا عَلَى شَيْءٍ ذَلِكَ هُوَ الضَّلَالُ الْبَعِيدُ (18)}
18. Mfano wa wale waliomkufuru Mola wao Mlezi, vitendo vyao ni kama jivu linalopeperushwa kwa nguvu za upepo katika siku ya upepo mkali. Hawawezi kupata chochote katika yale waliyoyachuma. Huko ndiko kupotea kwa mbali!
#
{18} يخبِّر تعالى عن أعمال الكفار التي عملوها: إما أن المراد بها الأعمال التي عملوها لله بأنَّها في ذَهابها وبطلانها واضمحلالها كاضمحلال الرماد الذي هو أدقُّ الأشياء وأخفها إذا اشتدَّت به الريح في يوم عاصف شديد الهبوب؛ فإنَّه لا يُبقي منه شيئاً ولا يُقْدَرُ منه على شيء يذهب ويضمحلُّ؛ فكذلك أعمال الكفار، {لا يقدِرونَ ممَّا كسبوا على شيء}، ولا على مثقال ذرَّة منه؛ لأنَّه مبنيٌّ على الكفر والتكذيب. {ذلك هو الضلال البعيد}: حيث بَطَلَ سعيُهم واضمحلَّ عملُهم. وإمَّا أنَّ المراد بذلك أعمال الكفار التي عملوها لِيَكيدوا بها الحقَّ؛ فإنَّهم يسعون ويكدحون في ذلك، ومكرهم عائدٌ عليهم، ولن يضرُّوا الله ورسله وجنده وما معهم من الحقِّ شيئاً.
{18} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu matendo ya makafiri ambayo waliyafanya. Ima kinachokusudiwa hapa ni yale matendo waliyoyafanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwamba katika kupotea kwake na kubatilika kwake na kufifia kwake ni kama vile kufifia kwa jivu ambalo ndicho kitu kidogo zaidi na chepesi zaidi, linalopeperushwa kwa nguvu za upepo katika siku ya pepo kali. Hapo hautabakisha kwalo kitu kati yake kinachobaki, na hakuna chochote kwalo kinaweza kuhifadhiwa katika kile kitakachoondoka na kutoweka. Basi hivyo ndivyo yalivyo matendo ya makafiri, "Hawawezi kupata chochote katika yale waliyoyafanya" wala hata uzito wa chembe yake. Kwa sababu yamejengeka juu ya msingi wa ukafiri na ukadhibishaji. "Huko ndiko kupotea kwa mbali!" kwa maana zilibatilika juhudi zao, na matendo yao yakapotea. Na ima kinachokusudiwa hapa ni matendo ya makafiri waliyoyafanya ili kuyafanyia njama haki. Kwani wao wanajitahidi na kutaabika katika hayo, lakini njama zao hizo zinawarudia wao wenyewe, wala hawatamdhuru Mwenyezi Mungu, na Mitume wake, na majeshi yake, na wala hawana chochote katika haki pamoja nao.
{أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ إِنْ يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَأْتِ بِخَلْقٍ جَدِيدٍ (19) وَمَا ذَلِكَ عَلَى اللَّهِ بِعَزِيزٍ (20) وَبَرَزُوا لِلَّهِ جَمِيعًا فَقَالَ الضُّعَفَاءُ لِلَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا كُنَّا لَكُمْ تَبَعًا فَهَلْ أَنْتُمْ مُغْنُونَ عَنَّا مِنْ عَذَابِ اللَّهِ مِنْ شَيْءٍ قَالُوا لَوْ هَدَانَا اللَّهُ لَهَدَيْنَاكُمْ سَوَاءٌ عَلَيْنَا أَجَزِعْنَا أَمْ صَبَرْنَا مَا لَنَا مِنْ مَحِيصٍ (21)}
19. Je, huoni kuwa Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa Haki? Akitaka, anawaondoa na alete viumbe wapya! 20. Na hilo kwa Mwenyezi Mungu si jambo gumu. 21. Na wote watajitokeza mbele ya Mwenyezi Mungu.
Wanyonge watawaambia wale waliotakabari: Hakika sisi tulikuwa wafwasi wenu; basi hebu hamtuondolei kidogo hivi katika adhabu ya Mwenyezi Mungu? Watasema: Lau Mwenyezi Mungu angelituongoa, basi hakuna shaka nasi tungeliwaongoa. Ni mamoja kwetu tukipapatika au tukisubiri; hatuna popote pa kukimbilia.
#
{19} ينبِّه تعالى عباده بأنّه {خَلَقَ السمواتِ والأرض بالحقِّ}؛ أي: ليعبده الخلق ويعرفوه ويأمرهم وينهاهم، وليستدلوا بهما وما فيهما على ما له من صفات الكمال، وليعلموا أنَّ الذي خَلَقَ السماوات والأرض ـ على عظمهما وسعتهما ـ قادرٌ على أن يعيدَهم خلقاً جديداً؛ ليجازِيَهم بإحسانهم وإساءتهم، وأنَّ قدرته ومشيئته لا تَقْصُرُ عن ذلك.
ولهذا قال: {إنْ يَشَأ يُذْهِبْكم ويأتِ بخَلْقٍ جديدٍ}: يُحتمل أنَّ المعنى: إنْ يشأ يُذهبكم ويأت بقوم غيركم يكونون أطوعَ لله منكم. ويُحتمل أنَّ المراد: إنْ يشأ يُفْنيكم ثم يعيدهم بالبعث خلقاً جديداً. ويدلُّ على هذا الاحتمال ما ذكره بعده من أحوال القيامة.
{19} Yeye Mtukufu anawatanabahisha waja wake kwamba "aliziumba mbingu na ardhi kwa Haki." Yaani, ili viumbe vimuabudu Yeye, vimjue, aviamrishe na avikataze, na ili vitumie hayo yaliyomo ndani yake kuwa ni ushahidi juu ya sifa zake kamilifu, na ili wajue kwamba yule aliyeziumba mbingu na ardhi - pamoja na ukubwa wake na upana wake - ana uwezo wa kuwarejesha katika uumbaji mpya, ili awalipe kwa uzuri wao na ubaya wao, na kwamba uwezo wake na utashi wake hauwezi kushindwa hayo.
Na ndiyo maana akasema: "Akitaka, anawaondoa na alete viumbe wapya!" Inawezekana kwamba maana yake ni kuwa akitaka anawaondoa na alete kaumu wengine wasiokuwa nyinyi, ambao watakuwa watiifu zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko nyinyi. Na inawezekana kwamba kinachokusudiwa ni kuwa akitaka, anawaangamiza kisha awarudishe kama viumbe wapya kwa kuwafufua. Na uwezekano huu unaashiriwa na yale aliyotaja baada yake kuhusu hali za Qiyama.
#
{20} {وما ذلك على الله بعزيزٍ}؛ أي: بممتنع، بل هو سهلٌ عليه جدًّا، {ما خَلْقُكُم ولا بَعْثُكم إلا كنفس واحدةٍ}، {وهو الذي يبدأ الخَلْق ثم يعيدُه وهو أهونُ عليه}.
{20} "Na hilo kwa Mwenyezi Mungu si jambo gumu;" yaani, si lenye kushindikana; bali ni rahisi sana kwake. "Hakukuwa kuumbwa kwenu, wala kufufuliwa kwenu isipokuwa ni kama nafsi moja tu." "Na Yeye ndiye anayeanzisha uumbaji, kisha ataurudisha mara nyengine. Na jambo hili ni jepesi zaidi kwake."
#
{21} {وبرزوا}؛ أي: الخلائق {لله جميعاً}: حين يُنفخُ في الصور فيخرجون من الأجداث إلى ربِّهم، فيقفون في أرض مستوية، قاعٍ صفصفٍ، لا ترى فيها عوجاً ولا أمتاً، ويبرُزون له لايخفى عليه منهم خافيةٌ؛ فإذا برزوا؛ صاروا يتحاجُّون، وكلٌّ يدفع عن نفسه ويدافع ما يقدر عليه، ولكن أنَّى لهم ذلك؟! فيقول {الضعفاء}؛ أي: التابعون والمقلِّدون، {للذين استكبروا}: وهم المتبوعون الذين هم قادة في الضَّلال: {إنَّا كنَّا لكم تَبَعاً}؛ أي: في الدنيا أمرتمونا بالضلال وزيَّنتموه لنا فأغويتمونا. {فهل أنتم} اليوم {مُغنون عنَّا من عذاب الله من شيء}؛ أي: ولو مثقال ذرَّة {قالوا}؛ أي: المتبوعون والرؤساء: أغويناكم كما غوينا، فَـ {لو هدانا الله لهديناكم}؛ فلا يُغني أحدٌ أحداً. {سواءٌ علينا أجَزِعْنا}: من العذاب، {أم صَبَرْنا}: عليه. {ما لنا من مَحيصٍ}؛ أي: [من] ملجأ نلجأ إليه، ولا مَهْرَبَ لنا من عذاب الله.
{21} "Na wote;" yaani, viumbe "mbele ya Mwenyezi Mungu" itakapopulizwa katika barugumu, kisha wakatoka makaburini kwenda kwa Mola wao Mlezi, na watasimama katika ardhi iliyotandazwa, tambarare, uwanda. Hutaona humo mdidimio wala muinuko. Na watajitokeza mbele yake wala hakitafichika kwake chochote cha kufichika kutoka kwao. Kisha wataanza kubishana huku kila mmoja akijitetea nafsi yake kiasi awezavyo, lakini watawezaje kufanya hivyo? Basi watasema "wanyonge;" yaani, wafuasi waliokuwa wakiiga "watawaambia wale waliotakabari" yaani wale waliofuata ambao wao ndio viongozi katika upotovu; "Hakika sisi tulikuwa wafwasi wenu." Yaani, katika dunia mlipotuamrisha upotevu, na mkatupambia upotevu huo basi mkatupoteza. "Basi hebu hamtuondolei kidogo hivi katika adhabu ya Mwenyezi Mungu?" Hata kama ni cha uzito wa chembe "watasema" hao waliofuatwa, na viongozi, "Tuliwapoteza kama tulivyopotea, basi "Lau Mwenyezi Mungu angelituongoa, basi hapana shaka nasi tungeliwaongoza" kwa hivyo hakuna mtu yeyote atakayemfaa mwingine.
"Ni mamoja kwetu tukipapatika" kutokana na adhabu "au tukisubiri: juu yake. "Hatuna pa kukimbilia popote" kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu.
{وَقَالَ الشَّيْطَانُ لَمَّا قُضِيَ الْأَمْرُ إِنَّ اللَّهَ وَعَدَكُمْ وَعْدَ الْحَقِّ وَوَعَدْتُكُمْ فَأَخْلَفْتُكُمْ وَمَا كَانَ لِيَ عَلَيْكُمْ مِنْ سُلْطَانٍ إِلَّا أَنْ دَعَوْتُكُمْ فَاسْتَجَبْتُمْ لِي فَلَا تَلُومُونِي وَلُومُوا أَنْفُسَكُمْ مَا أَنَا بِمُصْرِخِكُمْ وَمَا أَنْتُمْ بِمُصْرِخِيَّ إِنِّي كَفَرْتُ بِمَا أَشْرَكْتُمُونِ مِنْ قَبْلُ إِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ (22) وَأُدْخِلَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِمْ تَحِيَّتُهُمْ فِيهَا سَلَامٌ (23)}.
22.
Na shetani atasema itakapokatwa hukumu: Hakika Mwenyezi Mungu aliwaahidi ahadi ya kweli. Nami niliwaahidi; lakini sikuwatimizia ahadi yangu. Na sikuwa na mamlaka yoyote juu yenu, isipokuwa niliwaita, nanyi mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe. Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu, wala nyinyi hamuwezi kuwa watetezi wangu. Hakika mimi niliyakufuru tangu zamani huko kunishirikisha kwenu na Mwenyezi Mungu. Hakika madhalimu wana adhabu chungu. 23. Na wale walioamini na wakatenda mema wataingizwa katika Mabustani yapitayo mito kwa chini yake, wadumu humo kwa idhini ya Mola wao Mlezi.
Maamkizi yao humo yatakuwa: Salaam!
#
{22} أي: {وقال الشيطان}: الذي هو سببٌ لكلِّ شرٍّ يقع ووقع في العالم مخاطباً لأهل النار ومتبرئاً منهم، {لمَّا قُضِيَ الأمر}: ودخل أهلُ الجنةِ الجنةَ وأهلُ النارِ النارَ: {إنَّ الله وَعَدَكم وعدَ الحقِّ}: على ألسنة رسله فلم تطيعوه؛ فلو أطعتموه؛ لأدركتم الفوز العظيم. {ووعدتُكم}: الخير، {فأخلفتُكم}؛ أي: لم يحصُلْ ولن يحصُلَ لكم ما منَّيتكم به من الأماني الباطلة. {وما كان لي عليكُم من سلطانٍ}؛ أي: من حجة على تأييد قولي، {إلاَّ أن دعوتُكم فاستجبتُم لي}؛ أي: هذه نهاية ما عندي أني دعوتُكم إلى مُرادي وزيَّنته لكم فاستجبتُم لي اتِّباعاً لأهوائكم وشهواتكم؛ فإذا كانت الحال بهذه الصورة؛ {فلا تلوموني ولوموا أنفسكم}: فأنتم السبب وعليكم المدار في موجب العقاب. {ما أنا بمصرِخِكُم}؛ أي: بمغيثكم من الشدَّة التي أنتم بها، {وما أنتم بمصرخيَّ}: كلٌّ له قسطٌ من العذاب. {إنِّي كفرتُ بما أشركتمونِ من قبلُ}؛ أي: تبرأت من جعلكم لي شريكاً مع الله، فلست شريكاً لله، ولا تجب طاعتي. {إنَّ الظالمين}: لأنفسهم بطاعة الشيطان {لهم عذابٌ أليمٌ}: خالدين فيه أبداً. وهذا من لطف الله بعباده أن حذَّرهم من طاعة الشيطان، وأخبر بمداخلِهِ التي يدخل منها على الإنسان ومقاصدِهِ فيه، وأنه يقصدُ أن يدخله النيران.
وهنا بيَّن لنا أنَّه إذا دخل النار وجندُه ؛ أنَّه يتبرَّأ منهم هذه البراءة، ويكفُر بشركِهِم، ولا ينبِّئك مثل خبيرٍ. واعلم أن الله ذكر في هذه الآية أنه ليس له سلطانٌ، وقال في آية أخرى: {إنَّما سُلْطانُهُ على الذين يَتَوَلَّوْنَهُ والذين هم به مشركونَ}؛ فالسلطان الذي نفاه عنه هو سلطان الحجَّة والدليل، فليس له حجَّة أصلاً على ما يدعو إليه، وإنما نهاية ذلك أن يُقيم لهم من الشُبَه والتزيينات ما به يتجرؤون على المعاصي، وأما السلطان الذي أثبته؛ فهو التسلُّط بالإغراء على المعاصي لأوليائه يؤزُّهم إلى المعاصي أزًّا، وهم الذين سلَّطوه على أنفسهم بموالاته والالتحاق بحزبه، ولهذا ليس له سلطان على الذين آمنوا وعلى ربِّهم يتوكَّلون.
{22} Yaani, "Na Shetani atasema" - naye ndiye alikuwa sababu ya kila uovu unaotokea na uliotokea duniani - akiwaongelesha wale walio Motoni na akijiweka mbali nao "itapokatwa hukumu" na wale wa Peponi wakaingia Peponi na wale wa Motoni wakaingia Motoni. "Hakika Mwenyezi Mungu aliwaahidi ahadi ya kweli" juu ya ndimi za Mitume wake, lakini hamkumtii. Na kama mngemtii mngepata kufaulu kukubwa. "Nami niliwaahidi" heri "lakini sikuwatimizia ahadi yangu." Yaani, hamkupata wala hamtapata yale niliyowapa matumaini juu yake miongoni mwa matumaini batili. "Na sikuwa na mamlaka yoyote juu yenu." Yaani, sikuwa na hoja yoyote ya kuunga mkono kauli yangu, “isipokuwa tu kwamba niliwaita, nanyi mkaniitikia." Yaani, huu ndio mwisho wa yale niliyo nayo, kwamba niliwaita tu kwenye yale niliyoyataka na nikawapambia hayo, basi mkaniitikia kwa kufuata hawaa zenu na matamanio yenu. Kwa hivyo ikiwa hali iko hivi; "Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe" kwa maana nyinyi ndiyo sababu na adhabu hiyo. "Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu;" yaani, kwa kuwasaidia kutokana na ugumu ambao mko ndani yake, "wala nyinyi hamwezi kuwa watetezi wangu;" kila mmoja atapata fungu lake la adhabu. "Hakika mimi niliyakataa tangu zamani hayo mliyonishirikisha na Mwenyezi Mungu." Kwa hivyo, mimi si mshirika na Mwenyezi Mungu, na wala si wajibu kunitii. "Hakika madhalimu" waliojidhulumu kwa kumtii Shetani "wana adhabu chungu;" watadumu humo milele. Na hili ni katika upole wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake kwamba aliwaonya dhidi ya kumtii Shetani, na akawajulisha njia zake anazomuingia kwazo mwanadamu na makusudio yake kwake, na kwamba anakusudia kumuingiza Motoni. Hapa alitubainishia kuwa atakapoingia Motoni na majeshi wake, yeye atajiweka mbali nao huku kujiweka mbali, na atakufuru kumshirikisha kwao. Na wala hawezi kukupa habari vilivyo kama Yeye Mwenye habari zote. Basi jua kwamba Mwenyezi Mungu alitaja katika Aya hii kwamba Shetani hana mamlaka. Na akasema katika Aya nyingine, "Hakika mamlaka yake ni juu ya wale wanaomfanya rafiki yao, na wale wanaomfanya mshirika (wa Mwenyezi Mungu." Kwa hivyo, mamlaka aliyoyakanusha ni mamlaka ya hoja na ushahidi. Kwa hivyo yeye hana hoja hata kidogo kwa anachokiitia, lakini mwisho wa hayo ni yeye kuwawekea fikira potofu na mapambo ambayo kwayo wanathubutu kufanya maasia. Na ama mamlaka ambayo aliyathibitisha, basi ni kule kuwa na nguvu dhidi ya marafiki zake na kuwadanganya kufanya maasia na kuwachochea mchocheo mkubwa juu ya kufanya maasia. Nao wenyewe ndio waliompa mamlaka juu yao kwa kumfanya rafiki na kujiunga na kikundi chake, na kwa sababu ya hili yeye hana mamlaka juu ya wale walioamini na wanamtegemea Mola wao Mlezi.
#
{23} ولما ذكر عقاب الظالمين؛ ذكر ثواب الطائعين، فقال: {وأُدْخِلَ الذين آمنوا وعملوا الصالحات}؛ أي: قاموا بالدين قولاً وعملاً واعتقاداً، {جناتٍ تجري من تحتها الأنهارُ}: فيها من اللَّذَّات والشَّهَوات ما لا عينٌ رأتْ ولا أذنٌ سمعتْ ولا خطر على قلب بشرٍ. {خالدين فيها بإذنِ ربِّهم}؛ أي: لا بحولهم وقوَّتهم، بل بحول الله وقوته. {تحيَّتُهم فيها سلامٌ}؛ أي: يحيّي بعضُهم بعضاً بالسلام والتحية والكلام الطيب.
{23} Na alipotaja adhabu ya madhalimu, akataja malipo ya watiifu,
akasema: "Na wale walioamini na wakatenda mema wataingizwa." Yaani, wale walioisimamisha Dini kwa kauli na vitendo na imani "katika Mabustani yapitayo mito kwa chini yake;" ambayo ndani yake zimo starehe na matamanio ambayo hakuna jicho lililowahi kuona, wala hakuna sikio lililowahi kusikia, wala hayakuwahi pitia katika moyo wa mwanadamu yeyote. "Wadumu humo kwa idhini ya Mola wao Mlezi," na si kwa uwezo wao na nguvu zao; bali kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na nguvu zake.
"Maamkizi yao humo yatakuwa: Salaam!" Yaani, wataamkiana wao kwa wao kwa salamu, maamkizi, na maneno mazuri.
{أَلَمْ تَرَ كَيْفَ ضَرَبَ اللَّهُ مَثَلًا كَلِمَةً طَيِّبَةً كَشَجَرَةٍ طَيِّبَةٍ أَصْلُهَا ثَابِتٌ وَفَرْعُهَا فِي السَّمَاءِ (24) تُؤْتِي أُكُلَهَا كُلَّ حِينٍ بِإِذْنِ رَبِّهَا وَيَضْرِبُ اللَّهُ الْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ (25) وَمَثَلُ كَلِمَةٍ خَبِيثَةٍ كَشَجَرَةٍ خَبِيثَةٍ اجْتُثَّتْ مِنْ فَوْقِ الْأَرْضِ مَا لَهَا مِنْ قَرَارٍ (26)}
24. Je, hukuona vipi Mwenyezi Mungu alivyopiga mfano wa neno zuri? Ni kama mti mzuri, mizizi yake ni imara, na matawi yake yako mbinguni. 25. Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano ili wapate kukumbuka. 26. Na mfano wa neno ovu ni kama mti muovu, uliong'olewa juu ya ardhi. Hauna uimara wowote.
#
{24} يقول تعالى: {ألم تَرَ كيف ضَرَبَ الله مثلاً كلمةً طيبةً}: وهي شهادة أن لا إله إلا الله وفروعها {كشجرةٍ طيبةٍ}: وهي النخلة {أصلُها ثابتٌ}: في الأرض. {وفرعُها}: منتشرٌ {في السماء}: وهي كثيرة النفع دائماً.
{24} Yeye Mtukufu anasema, "Je, hukuona vipi Mwenyezi Mungu alivyopiga mfano wa neno zuri," ambalo kushuhudia kwamba hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu na matawi yake? "Ni kama mti mzuri" ambao ni mtende, "mizizi yake ni imara" katika ardhi "na matawi yake" yemeenea "mbinguni" nayo daima yana manufaa mengi.
#
{25} {تؤتي أكُلَها}؛ أي: ثمرتها، {كلَّ حين بإذن ربِّها}: فكذلك شجرة الإيمان أصلُها ثابتٌ في قلب المؤمن علماً واعتقاداً، وفرعُها من الكلم الطيِّب والعمل الصالح والأخلاق المرضيَّة والآداب الحسنة في السماء دائماً، يصعَدُ إلى الله منه من الأعمال والأقوال التي تخرِجُها شجرة الإيمان، ما ينتفعُ به المؤمن وينتفع غيره، {ويضرِبُ الله الأمثالَ للناس لعلَّهم يتذكَّرون}: ما أمرهم به ونهاهم عنه؛ فإنَّ في ضرب الأمثال تقريباً للمعاني المعقولة من الأمثال المحسوسة، ويتبيَّن المعنى الذي أراده الله غاية البيان ويتَّضح غاية الوضوح، وهذا من رحمته وحسن تعليمه؛ فللَّه أتمُّ الحمد وأكمله وأعمُّه. فهذه صفة كلمة التوحيد، وثباتُها في قلب المؤمن.
{25} "Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake Mlezi." Na vile vile mti wa Imani, mizizi yake imeimarika katika moyo wa Muumini kwa elimu na itikadi, na matawi yake ya maneno mazuri, na matendo mema na tabia zinazopendeza, na maadili daima yako mbinguni. Hupanda kwa Mwenyezi Mungu kutoka kwake matendo na maneno mti huo wa imani unayatoa, ambayo ananufaika kwayo Muumini na pia wengineo wananufaika kwayo. "Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano ili wapate kuyakumbuka" yale aliyowaamrisha na aliyowakataza. Kwa maana katika kupiga mifano kuna kuzileta karibu maana zisizohisika kwa mifano ya vitu vinavyohisika, kwa hivyo maana ile ambayo Mwenyezi Mungu alikusudia inabainika kwa kubainika kukubwa zaidi na inakuwa wazi kwa uwazi mkubwa zaidi. Na haya ni katika rehema yake na kufundisha kwake kuzuri. Basi sifa njema zote kamili na timilifu na za jumla zaidi ni zake Mwenyezi Mungu. Na hii ndiyo sifa ya neno tauhidi, na uthabiti wake katika moyo wa Muumini.
#
{26} ثم ذكر ضدَّها، وهي كلمة الكفر وفروعها، فقال: {ومَثَلُ كلمةٍ خبيثة كشجرةٍ خبيثةٍ}: المأكل والمطعم، وهي شجرة الحنظل ونحوها. {اجتُثَّت}: هذه الشجرة {من فوق الأرض ما لها من قرارٍ}؛ أي: [من] ثبوت؛ فلا عروق تمسكها، ولا ثمرة صالحة تنتِجُها، بل إنْ وُجِدَ فيها ثمرةٌ؛ فهي ثمرةٌ خبيثة، كذلك كلمة الكفر والمعاصي، ليس لها ثبوتٌ نافعٌ في القلب، ولا تثمِرُ إلا كلَّ قولٍ خبيثٍ وعملٍ خبيثٍ يستضر به صاحبه، ولا ينتفعُ، ولا يصعدُ إلى الله منه عملٌ صالح، ولا ينفع نفسه، ولا ينتفع به غيره.
{26} Kisha akataja kinyume chake, nacho ni neno la kufuru na matawi yake,
akasema: "Na mfano wa neno ovu ni kama mti muovu" wa kula na hata ladha yake. Nao ni mti wa handhali na mfano wake "uliong'olewa juu ya ardhi. Hauko imara hata kidogo" kwa maana hauna mizizi ya kuushikilia, wala hautoi matunda mazuri. Bali ikiwa utaleta matunda, basi matunda hayo ni maovu. Na vile vile maneno ya ukafiri na maasia, hayana uthabiti wowote moyoni, wala hauzai isipokuwa kila neno ovu na matendo maovu yenye kumdhuru mwenyewe, wala hanufaiki nayo, wala hayapandi kwa Mwenyezi Mungu matendo yoyote mazuri kutoka kwake, tena hajinufaishi yeye mwenyewe, wala wengine hafaidiki naye.
{يُثَبِّتُ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ وَيُضِلُّ اللَّهُ الظَّالِمِينَ وَيَفْعَلُ اللَّهُ مَا يَشَاءُ (27)}
27. Mwenyezi Mungu huwaimarisha wale walioamini kwa kauli ya imara katika uhai wa dunia na katika Akhera. Na Mwenyezi Mungu huwapoteza madhalimu. Na Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo.
#
{27} يخبر تعالى أنَّه يثبِّت عباده المؤمنين؛ أي: الذين قاموا بما عليهم من الإيمان القلبيِّ التامِّ، الذي يستلزم أعمال الجوارح ويثمِّرها، فيثبتهم الله: في الحياة الدنيا عند ورود الشبهات بالهداية إلى اليقين، وعند عروض الشهوات بالإرادة الجازمة على تقديم ما يحبُّه الله على هوى النفس ومرادها، وفي الآخرة عند الموت بالثبات على الدين الإسلاميِّ والخاتمة الحسنة، وفي القبر عند سؤال الملكين للجواب الصحيح إذا قيل للميت: من ربُّك؟ وما دينُك؟ ومن نبيُّك؟ هداهم للجواب الصحيح بأن يقولَ المؤمن: اللهُ ربِّي، والإسلامُ ديني، ومحمدٌ نبيِّي. {ويضِلُّ الله الظالمين}: عن الصواب في الدنيا والآخرة، وما ظلمهم الله ولكنَّهم ظلموا أنفسهم.
وفي هذه الآية دلالة على فتنة القبر وعذابه ونعيمه؛ كما تواترت بذلك النصوص عن النبيِّ - صلى الله عليه وسلم - في الفتنة وصفتها ونعيم القبر وعذابه.
{27} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba Yeye huwaimarisha waja wake waumini ambao walifanya wajibu wa kuamini kimoyo kikamilifu ulio juu yao, ambako kunalazimu kuwepo kwa matendo ya viungo nako kweli kuvizalisha. Na Mwenyezi Mungu huwaimarisha katika uhai wa dunia wanapotokewa na fikira potofu kwa kuwaongoa kufikia yakini, na wanapotokewa na matamanio kwa kuwapa utashi thabiti wa kuupendelea kile anachokipenda Mwenyezi Mungu juu ya matamanio ya nafsi na utashi wake. Na katika akhera wakati wa kufa kwa kuwaimarisha juu ya dini ya Kiislamu na mwisho mwema. Na kaburini wakati Malaika wale wawili watakapowauliza kwa kuwapa jibu sahihi,
maiti atakapoambiwa: Ni nani Mola wako Mlezi? Na Dini yako ni ipi? Na Nabii wako ni nani? Yeye Mwenyezi Mungu atawaongoa kufikia jawabu sahihi kwa kusema: Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi, na Uislamu ndiyo dini yangu, na Muhammad ndiye Nabii wangu. "Na Mwenyezi Mungu huwapoteza madhalimu" wasifikie usahihi katika dunia na Akhera, na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, bali walizidhulumu wenyewe nafsi zao. Aya hii inaashiria majaribio, adhabu, na raha ya kaburini, kama ilivyokuja kuhusiana na hayo katika maandiko mengi matakatifu kutoka kwa Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kuhusu majaribio ya kaburini, na maelezo yake, na starehe zake na adhabu yake.
{أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ بَدَّلُوا نِعْمَتَ اللَّهِ كُفْرًا وَأَحَلُّوا قَوْمَهُمْ دَارَ الْبَوَارِ (28) جَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا وَبِئْسَ الْقَرَارُ (29) وَجَعَلُوا لِلَّهِ أَنْدَادًا لِيُضِلُّوا عَنْ سَبِيلِهِ قُلْ تَمَتَّعُوا فَإِنَّ مَصِيرَكُمْ إِلَى النَّارِ (30)}
28. Je, hukuwaona wale waliobadilisha neema ya Mwenyezi Mungu kwa kufuru, na wakawafikisha kaumu yao kwenye nyumba ya maangamizo? 29. Nayo ni Jahannamu wataiingia! Na ni mabaya mno makazi hayo!" 30. Na walimfanyia Mwenyezi Mungu wenza ili wapoteze watu kutoka kwenye Njia yake.
Sema: Stareheni! Kwani maishio yenu ni Motoni!
#
{28} يقول تعالى مبينِّاً حال المكذِّبين لرسوله من كفار قريش وما آلَ إليه أمرُهم: {ألم تَرَ إلى الذين بدَّلوا نعمة الله كفراً}: ونعمة الله هي إرسال محمد - صلى الله عليه وسلم - إليهم يدعوهم إلى إدراك الخيرات في الدُّنيا والآخرة وإلى النجاة من شرور الدُّنيا والآخرة، فبدَّلوا هذه النعمة بردِّها والكفر بها والصدِّ عنها بأنفسهم وصدِّهم غيرهم حتى {أحلُّوا قومَهم دار البوارِ}: وهي النار؛ حيث تسبَّبوا لإضلالهم، فصاروا وبالاً على قومهم من حيث يُظَنُّ نفعهم، ومن ذلك أنهم زيَّنوا لهم الخروج يوم بدر ليحاربوا الله ورسوله، فجرى عليهم ما جرى، وقُتِلَ كثيرٌ من كبرائهم وصناديدهم في تلك الوقعة.
{28} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu,
akieleza hali ya wale waliomkadhibisha Mtume wake miongoni mwa makafiri wa Kiquraishi na namna hali yao ilivyoisha: "Je hukuwaona wale waliobadilisha neema ya Mwenyezi Mungu kwa kufuru." Na neema ya Mwenyezi Mungu ni kumtuma Muhammad - Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - kwao akiwalingania kufikia heri katika dunia na akhera na kuokoka na maovu ya dunia na Akhera. Basi wakaibadilisha neema hii kwa kuikataa na kuikufuru, na kuzuia dhidi yake wao wenyewe, na kuwazuia wengine dhidi yake, mpaka "wakawafikisha kaumu yao kwenye nyumba ya maangamizo?" Yaani, Moto. Kwa maana walikuwa ndiyo sababu ya kupotea kwao, na wakawa ni balaa kwa kaumu yao kwa kuwa ilidhaniwa kuwa ni wenye manufaa. Na katika hayo ni kwamba waliwapambia kwamba watoke katika siku ya Badr kupigana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kwa hivyo yakawapata yaliyowapata. Na wengi katika wakuu wao na viongozi wao wakauawa katika tukio hilo.
#
{29} {جهنم يَصْلَوْنها}؛ أي: يحيط بهم حرُّها من جميع جوانبهم. {وبئس القرارُ}.
{29} "Nayo ni Jahannamu! Wataiingia." Yaani, litawazunguka joto lake kutokea pande za zote. "Na ni mabaya mno makazi hayo!"
#
{30} {وجعلوا لله أنداداً}؛ أي: نظراء وشركاء، {ليُضِلُّوا عن سبيله}؛ أي: ليضلُّوا العباد عن سبيل الله بسبب ما جعلوا لله من الأنداد ودَعَوْهم إلى عبادتها. {قل} لهم متوعِّداً: {تمتَّعوا} بكفركم وضلالكم قليلاً؛ فليس ذلك بنافعكم، {فإنَّ مصيركم إلى النار}؛ أي: مآلكم ومأواكم فيها وبئس المصير.
{30} "Na walimfanyia Mwenyezi Mungu wenza ili wawapoteze watu kwenye Njia yake." Yaani, ili wawapoteze waja kwenye njia ya Mwenyezi Mungu kwa sababu ya wenza waliomfanyia Mwenyezi Mungu na wakawalingania kuwaabudu. "Sema" uwaambie kwa njia ya kuwaahidi maovu, "Stareheni" kwa ukafiri wenu na upotofu wenu kwa muda kidogo. Na hayo hayatawafaa, "Kwani maishio yenu ni Motoni!" Nayo ndiyo maishio mabaya zaidi.
{قُلْ لِعِبَادِيَ الَّذِينَ آمَنُوا يُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُنْفِقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً مِنْ قَبْلِ أَنْ يَأْتِيَ يَوْمٌ لَا بَيْعٌ فِيهِ وَلَا خِلَالٌ (31)}.
31. Waambie waja wangu walioamini, wasimamishe Swala, na watoe katika tulivyowaruzuku, kwa siri na dhahiri, kabla ya kufika kwa Siku isiyokuwa na biashara yoyote wala urafiki wa dhati.
#
{31} أي: قل لعبادي المؤمنين آمراً لهم بما فيه غايةُ صلاحهم وأن ينتهزوا الفرصةَ قبل أن لا يمكنهم ذلك، {يُقيموا الصلاة}: ظاهراً وباطناً، {وينفِقوا مما رَزَقْناهم}؛ أي: من النعم التي أنعمنا بها عليهم قليلاً أو كثيراً، {سرًّا وعلانيةً}: وهذا يشمل النفقة الواجبة كالزكاة ونفقة من تجب عليه نفقته، والمستحبَّة كالصدقات ونحوها. {مِنْ قبل أن يأتي يومٌ لا بيعٌ فيه ولا خِلالٌ}؛ أي: لا ينفع فيه شيء، ولا سبيل إلى استدراك ما فات؛ لا بمعاوضة بيع وشراءٍ، ولا بهبة خليل وصديق؛ فكل امرئٍ له شأنٌ يغنيه؛ فليقدِّم العبد لنفسه، ولينظرْ ما قدَّمه لغدٍ، وليتفقدْ أعماله، ويحاسب نفسه قبل الحساب الأكبر.
{31} Yaani, waambie waja wangu waumini ukiwaamrisha kufanya yale yanayowafaa zaidi na kwamba waichukue fursa kabla ya wao kushindwa kufanya hivyo kwamba "washike Swala" kwa nje na kwa ndani; "na watoe katika vile tulivyowaruzuku." Yaani, kutoka katika neema tulizowaneemesha kwazo, kidogo au kingi, "kwa siri na dhahiri". Na hili linajumuisha kutoa kwa ajili ya matumizi ya wajibu kama vile zaka na matumizi ya wale inaomlazimu yeye kuwapa masurufu. Na pia kunaingia hapa kutoa kunakopendekezwa kama vile sadaka na mfano wake. "Kabla haijafika Siku isiyokuwa na biashara yoyote wala urafiki;" yaani, hakuna kitu kitakachofaa siku hiyo, wala hakutakuwa na njia ya kufanya yaliyopita. Si kwa kununua na kuuza, wala kwa zawadi ya mwandani na rafiki. Kila mtu atakuwa na jambo lake la kumtosha. Basi mja na aitangulizie nafsi yake, na aangalie alichotanguliza kwa ajili ya Kesho, na ayakague matendo yake, na ajifanyie hesabu kabla ya ile hesabu kubwa zaidi.
{اللَّهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَأَنْزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَكُمْ وَسَخَّرَ لَكُمُ الْفُلْكَ لِتَجْرِيَ فِي الْبَحْرِ بِأَمْرِهِ وَسَخَّرَ لَكُمُ الْأَنْهَارَ (32) وَسَخَّرَ لَكُمُ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ دَائِبَيْنِ وَسَخَّرَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ (33) وَآتَاكُمْ مِنْ كُلِّ مَا سَأَلْتُمُوهُ وَإِنْ تَعُدُّوا نِعْمَتَ اللَّهِ لَا تُحْصُوهَا إِنَّ الْإِنْسَانَ لَظَلُومٌ كَفَّارٌ (34)}.
32. Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi, na akateremsha maji kutoka mbinguni. Na kwa hayo akatoa matunda kuwa ni riziki yenu. Na akawatiishia majahazi yanayokwenda baharini kwa amri yake, na akawatiishia mito. 33. Na akawatiishia jua na mwezi vinavyokwenda daima dawamu, na akawatiishia usiku na mchana. 34. Na akawapa katika kila mlichomuomba. Na mkihesabu neema za Mwenyezi Mungu, hamwezi kuzidhibiti. Hakika mwanadamu ni dhalimu mkubwa, mwenye kuzikufuru neema.
#
{32} يخبر تعالى أنَّه وحده {الذي خلق السمواتِ والأرضَ}: على اتِّساعهما وعظمهما، {وأنزل من السماء ماءً}: وهو المطر الذي ينزله الله من السحاب، فأخرج بذلك الماء {من الثمراتِ}: المختلفة الأنواع، {رزقاً لكم}: ورزقاً لأنعامكم. {وسخَّر لكم الفُلْكَ}؛ أي: السفن والمراكب، {لتجرِيَ في البحر بأمرِهِ}: فهو الذي يسَّر لكم صنعتها وأقْدَرَكم عليها وحَفِظَها على تيار الماء لتحمِلَكم وتحمل تجاراتكم وأمتعتكم إلى بلدٍ تقصدونه. {وسخَّرَ لكم الأنهارَ}: لتسقي حروثكم وأشجاركم، وتشربوا منها.
{32} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba Yeye Pekee ndiye "aliyeziumba mbingu na ardhi" pamoja na upana wake na ukubwa wake, "na akateremsha maji kutoka mbinguni" nayo ni ile mvua anayoiteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mawinguni, kisha kwa maji hayo akatoa "matunda" ya aina mbalimbali "kuwa ni riziki yenu" na riziki kwa mifugo wenu. "Na akawatiishia majahazi yanayokwenda baharini kwa amri yake." Yeye ndiye aliyewarahisishia kuyaunda na akawawezesha kufanya hivyo na akayahifadhi juu ya mkondo wa maji ili yawabebe, na yabebe biashara zenu, na mizigo yenu hadi katika nchi mnayoenda. "Na akawatiishia mito" ili munyweshe mimea yenu, na miti yenu, nanyi mnywe kwayo.
#
{33} {وسخَّر لكم الشمسَ والقمر دائِبَيْنِ}: لا يفتران ولا يَنيان، يسعَيان لمصالحكم من حساب أزمنتكم ومصالح أبدانكم وحيواناتكم وزروعكم وثماركم. {وسخَّر لكم الليل}: لتسكُنوا فيه، {والنهار} مبصراً لتبتغوا من فضله.
{33} "Na akawatiishia jua na mwezi vinavyokwenda daima dawamu" havipumziki wala havichoki. Vinakwenda kwa ajili ya masilahi yenu kama vile kuhesabu nyakati zenu na masilahi ya miili yenu na wanyama wenu na mazao yenu, na matunda yenu. "Na akawatiishia usiku" ili mpate kutulia humo, "na mchana" wa kuonea ili mtafute katika fadhila zake.
#
{34} {وآتاكم من كلِّ ما سألتُموه}؛ أي: أعطاكم من كلِّ ما تعلَّقت به أمانيكم وحاجتكم مما تسألونه إيَّاه بلسان الحال أو بلسان المقال من أنعام وآلاتٍ وصناعاتٍ وغير ذلك. {وإن تَعُدُّوا نعمة الله لا تُحْصوها}: فضلاً عن قيامكم بشكرها. {إنَّ الإنسان لظلومٌ كفَّارٌ}؛ أي: هذه طبيعة الإنسان من حيثُ هو ظالمٌ متجرِّئٌ على المعاصي مقصِّرٌ في حقوق ربِّه، كفَّار لنعم الله لا يشكرها ولا يعترفُ بها؛ إلاَّ مَن هداه الله فشَكَرَ نِعَمَهُ، وعَرَفَ حقَّ ربِّه وقام به.
ففي هذه الآيات من أصناف نعم الله على العباد شيءٌ عظيمٌ مجملٌ ومفصَّلٌ يدعو الله به العباد إلى القيام بشكره وذكره، ويحثُّهم على ذلك، ويرغِّبهم في سؤاله ودعائه آناء الليل والنهار؛ كما أنَّ نعمته تتكرَّر عليهم في جميع الأوقات.
{34} "Na akawapa katika kila mlichomuomba;" yaani, aliwapa katika kila kitu ambacho matamanio yenu na mahitaji yenu yanafungamana nayo na miongoni mwa yale mliyomuomba kwa hali zenu na kwa maneno, kama vile mifugo, ala mbalimbali, vitu vinyotengenezwa na mambo mengineyo. "Na mkihesabu neema za Mwenyezi Mungu, hamwezi kuzidhibiti" zaidi ya kushukuru kwenu. "Hakika mwanadamu ni dhalimu mkubwa, mwenye kuzikufuru neema." Yaani, hii ndiyo tabia ya mwanadamu namna alivyoumbwa dhalimu, mwenye kuthubutu kutenda dhambi, asiyetimiza haki za Mola wake Mlezi, mwenye kukufuru sana neema za Mwenyezi Mungu, hazishukuru wala hazikubali. Isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu amewaongoa na akashukuru neema zake, na akazitambua haki za Mola wake Mlezi na akazitimiza. Katika aya hizi kuna aina nyingi mbalimbali za neema za Mwenyezi Mungu juu ya waja wake, za jumla na za kina, ambazo Mwenyezi Mungu anawaita waja kwa ajili yake ili wamshukuru na wamkumbuke, na anawahimiza kufanya hivyo, na anawatia moyo kumuuliza na kumuomba dua nyakati za usiku na mchana, kama vile neema yake inarudia kuwajia katika nyakati zote.
{وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ اجْعَلْ هَذَا الْبَلَدَ آمِنًا [وَاجْنُبْنِي وَبَنِيَّ أَنْ نَعْبُدَ الْأَصْنَامَ (35) رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيرًا مِنَ النَّاسِ فَمَنْ تَبِعَنِي فَإِنَّهُ مِنِّي وَمَنْ عَصَانِي فَإِنَّكَ غَفُورٌ رَحِيمٌ (36) رَبَّنَا إِنِّي أَسْكَنْتُ مِنْ ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيْرِ ذِي زَرْعٍ عِنْدَ بَيْتِكَ الْمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُوا الصَّلَاةَ فَاجْعَلْ أَفْئِدَةً مِنَ النَّاسِ تَهْوِي إِلَيْهِمْ وَارْزُقْهُمْ مِنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَشْكُرُونَ (37) رَبَّنَا إِنَّكَ تَعْلَمُ مَا نُخْفِي وَمَا نُعْلِنُ وَمَا يَخْفَى عَلَى اللَّهِ مِنْ شَيْءٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ (38) الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي وَهَبَ لِي عَلَى الْكِبَرِ إِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ إِنَّ رَبِّي لَسَمِيعُ الدُّعَاءِ (39) رَبِّ اجْعَلْنِي مُقِيمَ الصَّلَاةِ وَمِنْ ذُرِّيَّتِي رَبَّنَا وَتَقَبَّلْ دُعَاءِ (40) رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَابُ] (41)}.
35.
Na Ibrahim aliposema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ujaalie mji huu uwe wa amani, na uniepushe mimi na wanangu na kuabudu masanamu. 36. Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hayo yamewapoteza wengi wa watu. Basi aliyenifuata mimi, huyo ni wangu, na aliyeniasi, hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu. 37. Mola wetu Mlezi! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuria yangu katika bonde lisilokuwa na mimea, kwenye Nyumba yako Takatifu, ewe Mola wetu Mlezi, ili wasimamishe Swala. Basi zijaalie nyoyo za watu zielekee kwao, na waruzuku matunda, ili wapate kushukuru. 38. Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe unajua tunayoyaweka hadharani na tunayoyaficha. Na hakuna kitu kinachofichikana kwa Mwenyezi Mungu katika ardhi wala katika mbingu. 39. Alhamdulillahi
(Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu) aliyenitunuku pamoja na uzee wangu Ismail na Is-haq. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusikia sana maombi. 40. Mola wangu Mlezi! Nijaalie niwe mwenye kusimamisha Swala, na katika dhuria yangu pia. Ewe Mola wetu Mlezi, na ipokee dua yangu. 41. Mola wetu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku itakaposimama hesabu.
#
{35} أي: {و} اذكُرْ إبراهيم عليه الصلاة والسلام في هذه الحالة الجميلة. {إذ قال إبراهيم ربِّ اجعل هذا البلد}؛ أي: الحرم {آمناً}: فاستجاب الله دعاءه شرعاً وقدراً، فحرمه الله في الشرع، ويسَّر من أسباب حرمته قَدَراً ما هو معلوم، حتى إنه لم يردْه ظالمٌ بسوءٍ إلاَّ قصمه الله؛ كما فعل بأصحاب الفيل وغيرهم. ولما دعا له بالأمن؛ دعا له ولبنيه بالأمن، فقال: {واجْنُبْني وبَنِيَّ أن نعبُدَ الأصنام}؛ أي: اجعلني وإيَّاهم جانباً بعيداً عن عبادتها والإلمام بها.
{35} Yaani, "na" mtaje Ibrahim -rehema na amani ziwe juu yake - katika hali hii nzuri.
"Na Ibrahim aliposema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ujaalie mji huu" mtakatifu "uwe wa amani." Basi Mwenyezi Mungu akamuitikia dua yake kisheria na kimajaliwa. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akauharamisha katika sheria, na akaweka sababu za kuuharamisha kimajaliwa kama inavyojulikana, kiasi kwamba hakuna hata dhalimu mmoja aliyeutakia ubaya isipokuwa Mwenyezi Mungu alimuangamiza. Kama alivyowafanyia watu wa tembo na wengineo. Na alipouombea amani, aliuombea huo na watoto wake amani. Akasema "uniepushe mimi na wanangu na kuabudu masanamu." Yaani, niweke kando mimi na wao na kuiabudu na kuifahamu.
#
{36} ثم ذكر الموجب لخوفه عليه وعلى بنيه بكثرة مَن افتتن وابتُلِيَ بعبادتها. فقال: {ربِّ إنهنَّ أضْلَلْنَ كثيراً من الناس}؛ أي: ضلوا بسببها، {فمن تَبِعَنِي}: على ما جئتُ به من التوحيد والإخلاص لله ربِّ العالمين {فإنَّه منِّي}: لتمام الموافقة، ومن أحبَّ قوماً وتبعهم؛ التحق بهم. {ومَنْ عصاني فإنَّك غفورٌ رحيم}: وهذا من شفقة الخليل عليه الصلاة والسلام؛ حيث دعا للعاصين بالمغفرة والرحمة من الله، والله تبارك وتعالى أرحمُ منه بعباده، لا يعذِّب إلاَّ من تمرَّد عليه.
{36} Kisha akataja sababu ya hofu yake juu ya nafsi yake na juu ya wanawe kwa sababu ya wingi wa wale waliojaribiwa na kupewa mtihani wa kuyaabudu.
Akasema: "Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hayo yamewapoteza wengi wa watu. Basi aliyenifuata mimi" katika yale niliyokuja nayo ya tauhidi na kumkusudia Mwenyezi Mungu tu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, "huyo ni miongoni mwangu" kwa sababu ya ukamilifu wa kuafikiana kwake. Na mwenye kuwapenda kaumu fulani na akawafuata, atajiunga nao. "Mwenye kurehemu mno" Haya ni katika huruma yake Al-Khalil, rehema na amani ziwe juu yake. Ambapo aliwaombea waasi msamaha na rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka ni Mwenye huruma zaidi kumliko kwa waja wake. Hamuadhibu isipokuwa mwenye kumuasi.
#
{37} {ربَّنا إني أسكنتُ من ذُرِّيَّتي بوادٍ غير ذي زرع عند بيتِكَ المحرَّم}: وذلك أنَّه أتى بهاجر أم إسماعيل وبابنها إسماعيل عليه الصلاة والسلام وهو في الرَّضاع من الشام حتى وضعهما في مكة، وهي إذ ذاك ليس فيها سكنٌ ولا داعٍ ولا مجيب، فلما وضعهما؛ دعا ربَّه بهذا الدعاء، فقال متضرِّعاً متوكِّلاً على ربِّه: رب {إني أسكنتُ من ذُرِّيَّتي}؛ أي: لا كل ذُرِّيَّتي؛ لأنَّ إسحاق في الشام وباقي بنيه كذلك، وإنما أسكن في مكة إسماعيل وذريته. وقوله: {بواد غير ذي زَرْع}؛ أي: لأن أرض مكة لا تصلح للزراعة. {ربَّنا لِيقيموا الصلاةَ}؛ أي: اجعلهم موحِّدين مقيمين الصلاة؛ لأنَّ إقامة الصلاة من أخصِّ وأفضل العبادات الدينيَّة؛ فمنْ أقامها كان مقيماً لدينه. {فاجْعَلْ أفئدةً من الناس تَهْوي إليهم}؛ أي: تحبُّهم وتحبُّ الموضع الذي هم ساكنون فيه. فأجاب الله دعاءه، فأخرج من ذريَّة إسماعيل محمداً - صلى الله عليه وسلم -، حتى دعا ذرِّيَّته إلى الدين الإسلاميِّ وإلى ملَّة أبيهم إبراهيم، فاستجابوا له وصاروا مقيمي الصلاة. وافترض الله حجَّ هذا البيت الذي أسكن به ذريَّته إبراهيم، وجعل فيه سرًّا عجيباً جاذباً للقلوب؛ فهي تحجُّه ولا تقضي منه وطراً على الدوام، بل كلَّما أكثر العبدُ التردُّد إليه؛ ازداد شوقُه وعظُم وَلَعُه وتَوْقُه، وهذا سرُّ إضافته تعالى إلى نفسه المقدسة. {وارزُقْهم من الثمرات لعلَّهم يشكرون}: فأجاب الله دعاءه، فصار يُجبى إليه ثمرات كل شيء؛ فإنك ترى مكة المشرفة كلَّ وقت، والثمارُ فيها متوفِّرة، والأرزاق تتوالى إليها من كل جانب.
{37} "Mola wetu Mlezi! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuria zangu katika bonde lisilokuwa na mimea, kwenye Nyumba yako Takatifu." Na hilo ni kwa sababu alimletea Hajar mama yake Ismail na mwanawe, Ismail, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake huku ananyonya baso, kutoka Sham mpaka akamuweka huko Makka. Nayo wakati huo ilikuwa hapakuwa na mahali pa kuishi wala mwitaji, wala mwitikiaji. Alipomuweka hapo, akamuomba Mola wake Mlezi kwa dua hii, akasema, akiomba dua kwa unyenyekevu na kumtegemea Mola wake Mlezi, "Mola wetu Mlezi! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuria zangu;" yaani, si dhuria yangu yote. Kwa sababu Is-haq alikuwa amebaki huko Sham na wanawe wengine pia. Lakini Ismaili tu na dhuria yake ndio aliwapa maskani huko Makka.
Na kauli yake: "katika bonde lisilokuwa na mimea" ni kwa sababu ardhi ya Makka si nzuri kwa kilimo. "ili wasimamishe Swala;" yaani, wafanyeni wenye kukupwekesha, wenye kusimamisha Swala. Kwa sababu kusimamisha swala ni miongoni mwa ibada mahususi na bora zaidi za kidini. Kwa hivyo, Mwenye kuisimamisha, anakuwa ameisimamisha dini yake. "Basi zijaalie nyoyo za watu zielekee kwao." Yaani, ziwapende na kupenda mahali ambapo wanaishi. Basi Mwenyezi Mungu akaitikia dua yake, na akatoa katika kizazi cha Ismail Muhammad -rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - mpaka akawalingania kizazi chake kwenye dini ya Kiislamu na mila ya baba yao Ibrahim, nao wakamwitikia na wakawa wanasimamisha Swala. Na Mwenyezi Mungu amefaradhisha kufanya hijja kwenye nyumba hii ambayo Ibrahimu aliwaweka kuishi baadhi ya dhuria yake, na akaweka ndani yake siri ya ajabu ambayo iliivutia mioyo. Basi mioyo inaupenda na wala haikatiki haja yake juu yake daima dawamu; bali kila mja anapouendea kwa wingi, inazidi shauku yake, na hamu yake na utashi mkubwa. Na hii ndiyo siri ya Mwenyezi Mungu kuifungamanisha na nafsi yake takatifu. "Na waruzuku katika matunda, ili wapate kushukuru." Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akaitikia dua yake, na ikawa yanaletwa hapo matunda ya kila kitu. Na utaiona Makka tukufu kila wakati hali ya kuwa matunda ni mengi humo, na riziki zinaijia kutoka pande zote.
#
{38} {ربَّنا إنك تعلم ما نُخفي وما نُعْلِنُ}؛ أي: أنت أعلم بنا منا، فنسألك من تدبيرك وتربيتك لنا أن تيسِّر لنا من الأمور التي نعلمها والتي لا نعلمها ما هو مُقتضى علمك ورحمتك. {وما يخفى على اللهِ من شيءٍ في الأرض ولا في السماء}: ومن ذلك هذا الدعاء الذي لم يَقْصِدْ به الخليل إلا الخير وكثرة الشكر لله ربِّ العالمين.
{38} "Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe unajua tunayoyaficha na tunayoyadhihirisha." Yaani, wewe unatujua vyema hata kujiliko sisi wenyewe. kwa hivyo tunakuomba kupitia uendeshaji wako na malezi yako kwamba uturahisishie katika mambo tunayoyajua na tusiyoyajua, ambayo yanatakiwa na elimu yako na rehema yako. "Na hakuna kitu kinachofichikana kwa Mwenyezi Mungu katika ardhi wala katika mbingu." Na katika hayo ni dua hii ambayo yeye Al-Khalil hakukusudia kwayo isipokuwa heri na wingi wa shukrani kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
#
{39} {الحمد لله الذي وَهَبَ لي على الكِبَرِ إسماعيل وإسحاقَ}: فَهِبَتُهم من أكبر النعم، وكونهم على الكبر في حال الإياس من الأولاد نعمةٌ أخرى، وكونهم أنبياء صالحين أجلُّ وأفضل. {إنَّ ربِّي لسميع الدعاء}؛ أي: لقريب الإجابة ممن دعاه، وقد دعوتُه فلم يخيِّبْ رجائي.
{39} "Alhamdulillahi
(Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu) aliyenitunuku pamoja na uzee wangu Ismail na Is-haq" kwani tunu hii ni katika neema kubwa zaidi, na kuja kwao katika uzee katika hali ya kukata tamaa ya watoto, ni neema nyingine tena. Na kwamba wao ni manabii wema ni kubwa zaidi na bora zaidi. "Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusikia sana maombi." Yaani, hujibu kwa karibu yule anayemuomba. Na nimemuomba, kwa hivyo matumaini yangu hayakupotelea mbali.
#
{40 - 41} ثم دعا لنفسه ولذرِّيَّته، فقال: {ربِّ اجعلني مقيم الصَّلاة ومن ذُرِّيَّتي ربَّنا وتقبَّل دُعاء. ربَّنا اغفِرْ لي ولوالديَّ وللمؤمنين يومَ يقومُ الحساب}: فاستجاب الله له في ذلك كلِّه؛ إلاَّ أنَّ دعاءه لأبيه إنما كان عن موعدةٍ وعدها إيَّاه، فلما تبيَّن له أنه عدوٌّ لله؛ تبرَّأ منه.
{40 - 41} Kisha akajiombea mwenyewe na dhuria yake,
akasema: "Mola wangu Mlezi! Nijaalie niwe mwenye kusimamisha Swala, na katika dhuria zangu pia. Ewe Mola wetu Mlezi, na ipokee dua yangu. Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku ya kusimama hesabu." Basi Mwenyezi Mungu akamuitikia katika hayo yote. Hata hivyo, dua yake kwa ajili ya baba yake iliegemezwa juu ya ahadi aliyomuahidi, kwa hivyo ilipomdhihirikia kwamba yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu, akajiweka mbali naye.
Kisha yeye Mtukufu akasema:
{وَلَا تَحْسَبَنَّ اللَّهَ غَافِلًا عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الْأَبْصَارُ (42) مُهْطِعِينَ مُقْنِعِي رُءُوسِهِمْ لَا يَرْتَدُّ إِلَيْهِمْ طَرْفُهُمْ وَأَفْئِدَتُهُمْ هَوَاءٌ (43)}.
42. Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayoyafanya madhalimu. Hakika Yeye anawaahirisha tu mpaka siku yatakapokodoka macho yao. 43. Natakuwa mbioni, vichwa juu, huku macho yao hayapepesi, na nyoyo zao tupu.
#
{42} هذا وعيدٌ شديد للظالمين وتسلية للمظلومين؛ يقول تعالى: {ولا تحسبنَّ الله غافلاً عما يعملُ الظالمون}: حيث أمهلهم وأدرَّ عليهم الأرزاق وتَرَكَهم يتقلَّبون في البلاد آمنين مطمئنِّين؛ فليس في هذا ما يدلُّ على حسن حالهم؛ فإنَّ الله يُملي للظالم ويُمْهِلُه ليزداد إثماً، حتى إذا أخذه؛ لم يُفْلِتْه، {وكذلك أخْذُ ربِّك إذا أخَذَ القُرى وهي ظالمةٌ إنَّ أخذَهُ أليمٌ شديدٌ}. والظلم ها هنا يشمل الظلم فيما بين العبد وربِّه وظلمه لعباد الله. {إنما يؤخِّرُهم ليوم تَشْخَصُ فيه الأبصارُ}؛ أي: لا تطرف من شدَّة ما ترى من الأهوال وما أزعجها من القلاقل.
{42} Hili ni tishio kali kwa madhalimu na ni liwazo kwa wanaodhulumiwa. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na hayo wanayoyafanya madhalimu" ambapo aliwapa muhula na akawaruzuku kwa wingi, na akawaacha watembee katika nchi kwa amani na utulivu. Lakini hakuna chochote katika haya kinachoonyesha kwamba wako katika hali nzuri. Kwa maana Mwenyezi Mungu humpururia dhalimu na kumpa muhula ili azidishe dhambi zake, mpaka anapomchukua, hawezi kumkwepa. “Na ndiyo kama hivyo ndivyo inavyokuwa Mola wako Mlezi anapoikamata miji inapokuwa imedhulumu. Hakika mkamato wake ni mchungu na mkali." Na dhuluma hapa inajumuisha dhuluma ya baina ya mja na Mola wake Mlezi, na dhuluma yake kwa waja wa Mwenyezi Mungu. "Hakika Yeye anawaahirisha tu mpaka siku yatakapokodoka macho yao;" kwa sababu ya ukubwa wa yale ambayo mambo yanayaona ya mahangaiko na ile wasiwasi inayoyasumbua.
#
{43} {مُهْطِعينَ}؛ أي: مسرعين إلى إجابة الداعي حين يدعوهم إلى الحضور بين يدي الله للحساب، لا امتناعَ لهم ولا محيص ولا ملجأ، {مُقنعي رؤوسهم}؛ أي: رافعيها، قد غُلَّتْ أيديهم إلى الأذقان، فارتفعت لذلك رؤوسهم، {لا يرتدُّ إليهم طرفُهم وأفئِدَتُهم هواء}؛ أي: أفئدتهم فارغةٌ من قلوبهم، قد صعدت إلى الحناجر، لكنَّها مملوءةٌ من كل همٍّ وغمٍّ وحزن وقلق.
{43} "Nao wako mbioni;" yaani, wanaharakisha kumuitikia mwitaji alipowaita waje mbele ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuhesabiwa matendo yao. Hawawezi kukataa, wala hawana pa kuokokea, wala pa kukimbilia. "Vichwa juu" huku mikono yao imefungwa kwenye videvu vyao, kwa hivyo vikainuka vichwa vyao kwa sababu ya hilo, "na macho hayapepesi, na nyoyo zao tupu." Yaani, vifua vyao ni tupu havina nyoyo zao kwa kuwa zimetoka zimefika kooni, lakini zimejaa wasiwasi kubwa, na huzuni kubwa.
{وَأَنْذِرِ النَّاسَ يَوْمَ يَأْتِيهِمُ الْعَذَابُ فَيَقُولُ الَّذِينَ ظَلَمُوا رَبَّنَا أَخِّرْنَا إِلَى أَجَلٍ قَرِيبٍ نُجِبْ دَعْوَتَكَ وَنَتَّبِعِ الرُّسُلَ أَوَلَمْ تَكُونُوا أَقْسَمْتُمْ مِنْ قَبْلُ مَا لَكُمْ مِنْ زَوَالٍ (44) وَسَكَنْتُمْ فِي مَسَاكِنِ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ وَتَبَيَّنَ لَكُمْ كَيْفَ فَعَلْنَا بِهِمْ وَضَرَبْنَا لَكُمُ الْأَمْثَالَ (45) وَقَدْ مَكَرُوا مَكْرَهُمْ وَعِنْدَ اللَّهِ مَكْرُهُمْ وَإِنْ كَانَ مَكْرُهُمْ لِتَزُولَ مِنْهُ الْجِبَالُ (46)}.
44. Na waonye watu siku itakapowajia adhabu, na wale waliodhulumu waseme, "Ewe Mola wetu Mlezi! Tuahirishe muda kidogo tuitikie wito wako na tuwafuate Mitume." Kwani nyinyi hamkuapa zamani kwamba hamuwezi kuondoka? 45. Na mkakaa katika maskani zile zile za wale waliozidhulumu nafsi zao. Na ikawabainikia jinsi tulivyowatendea. Nasi tukawapigia mifano mingi. 46. Na hakika walifanya vitimbi vyao, na vitimbi vyao anavijua Mwenyezi Mungu. Wala vitimbi vyao si vya kuondosha milima.
#
{44} يقول تعالى لنبيِّه محمد - صلى الله عليه وسلم -: {وأنذِرِ الناس يوم يأتيهم العذابُ}؛ أي: صف لهم صفة تلك الحال، وحذِّرهم من الأعمال الموجبة للعذاب، الذي حين يأتي في شدائده وقلاقله، فيقول الذين ظلموا بالكفر والتكذيب وأنواع المعاصي، نادمين على ما فعلوا، سائلين للرجعة في غير وقتها: {ربَّنا أخِّرْنا إلى أجل قريبٍ}؛ أي: رُدَّنا إلى الدُّنيا؛ فإنَّا قد أبصرنا؛ {نُجِبْ دعوتَكَ}: والله يدعو إلى دار السلام، {ونتَّبع الرُّسل}: وهذا كلُّه لأجل التخلُّص من العذاب الأليم، وإلاَّ؛ فهم كَذَبَةٌ في هذا الوعد؛ فلو رُدُّوا لعادوا لما نهوا عنه، ولهذا يوبَّخون ويُقال لهم: {أولم تكونوا أقسمتُمْ من قبلُ ما لكم من زوالٍ}: عن الدُّنيا وانتقال إلى الآخرة؛ فها قد تبيَّن لكم حنثكم في إقسامكم وكذبكم فيما تدَّعون.
{44} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad-
rehema na amani za mwenyezi mungu zimshukie: "Na waonye watu siku itakapowajia adhabu" Yaani, waelezee maelezo ya hali hiyo, na watahadharishe matendo yanavyosababisha adhabu, adhabu ambayo inapokuja katika dhiki yake na wasiwasi wake, basi watasema wale waliodhulumu kwa ukafiri, ukadhibishaji na aina mbalimbali za maasia wakijutia yale waliyoyafanya, wakiomba kurejea katika wakati usiokuwa wakati wake,
"Ewe Mola wetu Mlezi! Tuahirishe muda kidogo" Yaani: turudishe duniani. Kwa maana tumeshaona "tuitikie wito wako;" na Mwenyezi Mungu analingania kwenye nyumba ya salama, "na tuwafuate Mitume." Na haya yote ni kwa ajili ya kuokoka na adhabu chungu. Vinginevyo, wao ni waongo katika ahadi hii kwa maana lau watarudishwa, wangerejea katika yale waliyokatazwa,
na ndiyo maana wanakemewa na kuambiwa: "Kwani nyinyi hamkuapa zamani kwamba hamtaondoka kamwe" katika dunia na kuhamia Akhera? Sasa anaglieni, imeshawabainikia kwamba mmevivunja viapo vyenu na mmedanganya katika hayo mliyodai.
#
{45} {و} ليس عليكم قاصر في الدنيا من أجل الآيات البينات، بل {سكنتُم في مساكن الذين ظلموا أنفُسَهم وتبيَّن لكم كيف فعلنا بهم}: من أنواع العقوبات، وكيف أحلَّ الله بهم العقوبات حين كذَّبوا بالآيات البينات، {وضَرَبْنا لكم الأمثالَ}: الواضحة التي لا تَدَعُ أدنى شكٍّ في القلب إلا أزالته، فلم تنفعْ فيكم تلك الآيات، بل أعرضتُم ودمتُم على باطلكم، حتى صار ما صار، ووصلتُم إلى هذا اليوم الذي لا ينفع فيه اعتذارُ مَنِ اعتذر بباطل.
{45} "Na" zaidi ya hayo, sababu ya kutofanya kwenu matendo mema katika uhai wa dunia haikuwa kwa sababu hakukuwa na ishara zilizo wazi; bali "mlikaa katika maskani zile zile za wale waliozidhulumu nafsi zao. Na ikawabainikia jinsi tulivyowatendea" kupitia aina mbalimbali za adhabu, na jinsi Mwenyezi Mungu alivyowapa adhabu walipozikadhibisha Ishara zilizo wazi, "Nasi tukawapigia mifano mingi" iliyo wazi ambayo haziachi shaka hata ya chini zaidi moyoni isipokuwa zinaiondoa. Lakini ishara hizo hazikuwafaa, bali mlizipa mgongo na mkadumu katika batili yenu mpaka yakatokea yaliyotokea, na mkafika katika siku hii ambayo haumfai udhuru mwenye kutoa udhuru batili.
#
{46} {وقد مكروا}؛ أي: المكذِّبون للرسل {مكرَهم}: الذي وصلت إراداتهم وقدرهم عليه، {وعند الله مكرُهُم}؛ أي: هو محيطٌ به علماً وقدرةً، فإنه عاد مكرُهم عليهم، ولا يَحيق المكر السيئ إلاَّ بأهله. {وإنْ كان مكرُهُم لِتَزولَ منه الجبالُ}؛ أي: ولقد كان مكرُ الكفار المكذِّبين للرسل بالحقِّ وبمن جاء به من عظمه لِتَزولَ الجبالُ الراسيات بسببه عن أماكنها؛ أي: مكروا مكراً كُبَّاراً لا يُقادَرُ قَدْرُه، ولكن الله ردَّ كيدهم في نحورهم. ويدخل في هذا كلُّ مَنْ مكر من المخالفين للرسل لينصر باطلاً أو يبطل حقًّا، والقصد أنَّ مكرهم لم يغنِ عنهم شيئاً ولم يضرَّوا الله شيئاً، وإنَّما ضروا أنفسهم.
{46} "Na kwa hakika walifanya vitimbi vyao;" yaani, wale waliowakadhibisha Mitume kwa vitimbi vyote vilivyofikiwa na utashi wao na uwezo wao. "Na vitimbi vyao anavijua Mwenyezi Mungu." Yaani, amevizunguka kwa elimu na uwezo. Kwani vitimbi vyao viliwarudia wenyewe, Na vitimbi viovu havimsibu isipokuwa mwenyewe aliyevifanya. "Wala vitimbi vyao si vya kuondosha milima." Na ilisemwa kwamba maana yake ni kuwa vitimbi vya makafiri waliowakadhibisha Mitume na haki na hata yule aliyeileta vilikaribia kuifanya milima madhubuti kuondoka katika mahali pake. Yaani, walipanga vitimbi vikubwa sana ambavyo haviwezi kupimwa kiasi chake. Lakini Mwenyezi Mungu akawarudishia kooni mwao vitimbi vyao hivyo. Na pia anaingia hapa kila anayepanga vitimbi vya batili au vya kubatilisha haki miongoni mwa wale wanaowahalifu Mitume. Na makusudio ya aya hii ni kwamba vitimbi vyao hivyo havikuwafaa kitu wala hawakumdhuru Mwenyezi Mungu kitu, bali walijidhuru wenyewe.
{فَلَا تَحْسَبَنَّ اللَّهَ مُخْلِفَ وَعْدِهِ رُسُلَهُ إِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ ذُو انْتِقَامٍ (47) يَوْمَ تُبَدَّلُ الْأَرْضُ غَيْرَ الْأَرْضِ وَالسَّمَاوَاتُ وَبَرَزُوا لِلَّهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّارِ (48) وَتَرَى الْمُجْرِمِينَ يَوْمَئِذٍ مُقَرَّنِينَ فِي الْأَصْفَادِ (49) سَرَابِيلُهُمْ مِنْ قَطِرَانٍ وَتَغْشَى وُجُوهَهُمُ النَّارُ (50) لِيَجْزِيَ اللَّهُ كُلَّ نَفْسٍ مَا كَسَبَتْ إِنَّ اللَّهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ (51) هَذَا بَلَاغٌ لِلنَّاسِ وَلِيُنْذَرُوا بِهِ وَلِيَعْلَمُوا أَنَّمَا هُوَ إِلَهٌ وَاحِدٌ وَلِيَذَّكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ (52)}
47. Basi kamwe usimdhanie Mwenyezi Mungu kuwa ni mwenye kuwavunjia ahadi yake Mitume wake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu, Mwenye kulipiza. 48. Siku itakapogeuzwa ardhi iwe ardhi nyingine, na mbingu zote pia. Nao watahudhuria mbele ya Mwenyezi Mungu Mmoja, Mshindi. 49. Na utaona wahalifu siku hiyo wamefungwa katika minyororo. 50. Nguo zao zitakuwa za lami, na Moto utazigubika nyuso zao. 51. Ili Mwenyezi Mungu ailipe kila nafsi kwa yale iliyoyachuma. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu. 52. Huu ni ufikishaji kwa watu, ili waonywe kwao, na wapate kujua kuwa hakika Yeye ni Mungu Mmoja, na wapate kukumbuka wenye akili.
#
{47} يقول تعالى: {فلا تحسبنَّ الله مُخْلِفَ وعدِهِ رسلَه}: بنجاتهم ونجاة أتباعهم وسعادتهم، وإهلاك أعدائهم وخذلانهم في الدنيا وعقابهم في الآخرة؛ فهذا لا بدَّ من وقوعه؛ لأنَّه وعد به الصادقُ قولاً على ألسنة أصدق خلقه، وهم الرسل، وهذا أعلى ما يكون من الأخبار، خصوصاً وهو مطابقٌ للحكمة الإلهيَّة والسنن الربانيَّة وللعقول الصحيحة، والله تعالى لا يعجزه شيءٌ؛ فإنَّه {عزيزٌ ذو انتقام}؛ أي: إذا أراد أن ينتقم من أحدٍ؛ فإنه لا يفوته ولا يعجزه، وذلك في يوم القيامة.
{47} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Basi kamwe usimdhanie Mwenyezi Mungu kuwa ni mwenye kuwavunjia ahadi yake Mitume wake" ya kuwaokoa wao na wafuasi wao, na kuwapa furaha, na kuwaangamiza maadui zao na kuwaangusha katika dunia na kuwaadhibu katika Akhera. Haya lazima yatokee. Kwa sababu ni ahadi ya Yule ambaye ndiye Mkweli wa kauli, juu ya ndimi za viumbe wake wa kweli zaidi, ambao ni Mitume. Na hii ndiyo habari ya hali ya juu kabisa, hasa kwa vile inaafikiana na hekima ya Mwenyezi Mungu, na desturi za kiungu, na akili timamu, na hakuna chochote kinachoweza kumshinda Mwenyezi Mungu. Kwani Yeye ni "Mwenye Nguvu, na ni Mwenye kulipiza." Yaani, anapotaka kumlipiza yeyote, basi hawezi kumkwepa wala kumshinda. Na hilo litatokea Siku ya Qiyama.
#
{48} {يوم تُبَدَّلُ الأرضُ غير الأرض والسمواتُ}: تُبَدَّلُ غيرَ السماوات، وهذا التبديل تبديل صفات لا تبديل ذات؛ فإنَّ الأرض يوم القيامة تُسَوَّى وتُمَدُّ كمدِّ الأديم، ويُلقى ما على ظهرها من جبل ومَعْلَم، فتصير قاعاً صفصفاً، لا ترى فيها عوجاً ولا أمتاً، وتكونُ السماء كالمهل من شدَّة أهوال ذلك اليوم، ثم يطويها الله تعالى بيمينه. {وبرزوا}؛ أي: الخلائق من قبورهم إلى يوم بعثهم ونشورهم في محلٍّ لا يخفى منهم على الله شيء، {لله الواحد القهار}؛ أي: المنفرد بعظمته وأسمائه وصفاته وأفعاله العظيمة وقهره لكلِّ العوالم؛ فكلُّها تحت تصرُّفه وتدبيره؛ فلا يتحرَّك منها متحرِّك، ولا يسكنُ ساكنٌ إلاَّ بإذنِهِ.
{48} "Siku itakapogeuzwa ardhi iwe ardhi nyingine, na mbingu pia" ibadilishwe isiwe mbingu tena. Na kubadilisha huku ni kubadilisha sifa, siyo uhalisia wake. Kwa maana Siku ya Qiyama ardhi itasawazishwa na kutandazwa kama kutandazwa kwa ngozi, na vitaangushwa vilivyo juu yake kama vile milima na alama mbalimbali, kisha itakuwa tambarare, uwanda. Hutaona humo mdidimio wala mwinuko. Nayo mbingu itakuwa kama maadeni iliyoyeyushwa kwa sababu ya ugumu wa mahangaiko ya siku hiyo. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu ataikunja kwa mkono wake wa kulia. "Nao;" yaani, viumbe "watajitokeza" kutoka makaburini mwao katika mahali ambapo hapana kitakachofichikana kwa Mwenyezi Mungu. "Mbele ya Mwenyezi Mungu Mmoja, Mshindi;" Yaani, wa Pekee katika ukuu wake, majina yake na sifa zake, na matendo yake makuu, na ushindi wake juu ya walimwengu wote. Wote watakuwa chini ya udhibiti wake na uendeshaji wake. Na hakuna atakayefanya harakati zozote wala kutulia miongoni mwao isipokuwa kwa idhini yake.
#
{49} {وترى المجرمين}؛ أي: الذين وصفُهم الإجرامُ وكثرة الذنوب في ذلك اليوم، {مقرَّنين في الأصفادِ}؛ أي: يُسَلْسَلُ كلُّ أهل عمل من المجرمين بسلاسل من نارٍ، فيُقادون إلى العذاب في أذلِّ صورة وأشنعها وأبشعها.
{49} 'Na utawaona wahalifu;" yaani, wale ambao wanasifika na uhalifu na madhambi mengi, katika siku hiyo, "wamefungwa katika minyororo" ya kutoka motoni, kisha watapelekwa kwenye adhabu katika sura ya kufedhehesha zaidi, na mbaya zaidi, na ya kutisha zaidi.
#
{50} {سرابيلُهم}؛ أي: ثيابهم {من قَطِرانٍ}: وذلك لشدَّة اشتعال النار فيهم وحرارتها ونتن ريحها، {وتَغْشى وجوهَهم}: التي هي أشرف ما في أبدانهم {النارُ}؛ أي: تحيط بها، وتَصلاها من كل جانب، وغير الوجوه من باب أولى وأحرى.
{50} "Nguo zao;" yaani nguo zao "zitakuwa za lami" na hayo ni kwa sababu ya kuwaka kwa moto mkali ndani yao na joto lake na uvundo wa harufu yake, "na utazigubika nyuso zao" ambazo ndicho kitu chenye heshima zaidi katika miili yao; "Moto" utakaozizunguka na kuziingia kutokea pande zote; yaani, kuizunguka. Basi viungo visivyokuwa nyuso vinalistahiki na kulifailia zaidi hilo.
#
{51} وليس هذا ظلماً من الله [لهم]، وإنما هو جزاءٌ لما قدَّموا وكسبوا، ولهذا قال تعالى: {لِيَجْزِيَ الله كلَّ نفس ما كَسَبَتْ}: من خير وشرٍّ بالعدل والقِسْط الذي لا جَوْر فيه بوجه من الوجوه. {إنَّ الله سريعُ الحساب}؛ كقوله تعالى: {اقتربَ للناس حسابُهم وهم في غفلةٍ معرضونَ}، ويُحتمل أن معناه سريع المحاسبة؛ فيحاسِبُ الخلق في ساعة واحدةٍ كما يرزقهم ويدبِّرهم بأنواع التدابير في لحظة واحدةٍ، لا يشغَلُه شأنٌ عن شأنٌ، وليس ذلك بعسير عليه.
{51} Na hii si dhuluma kutoka kwa Mwenyezi Mungu
[kwao], bali ni malipo ya yale waliyoyatanguliza na waliyoyachuma. Na ndiyo maana Yeye Mtukufu akasema, "Ili Mwenyezi Mungu ailipe kila nafsi kwa yale iliyoyachuma" ya heri na shari, kwa uadilifu na haki ambayo kukandamiza kokote ndani yake kwa namna yoyote ile. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu." Kama vile kauli yake Yeye Mtukufu, "Imewakaribia watu hesabu yao, nao wamo katika kughafilika wamepuuza." Na inawezekana kwamba maana yake ni ya kwamba Yeye ni wa haraka wa kuhesabu, kwa hivyo atavihesabu viumbe katika muda mmoja, kama vile anavyowaruzuku na kuwaendesha kwa aina mbalimbali za uendeshaji katika muda mmoja. Halimshughulishi jambo moja kutoka kwa jingine, na wala hilo si gumu kwake.
#
{52} فلما بيَّن البيان المبين في هذا القرآن؛ قال في مدحه: {هذا بلاغٌ للناس}؛ أي: يتبلَّغون به ويتزوَّدون إلى الوصول إلى أعلى المقامات وأفضل الكرامات؛ لما اشتمل عليه من الأصول والفروع وجميع العلوم التي يحتاجها العباد، {ولِيُنْذَروا به}: لما فيه من الترهيب من أعمال الشرِّ وما أعدَّ الله لأهلها من العقاب، {ولِيَعْلموا أنَّما هو إلهٌ واحدٌ}: حيث صرف فيه من الأدلَّة والبراهين على ألوهيَّته ووحدانيَّته ما صار ذلك حق اليقين، {ولِيَذَّكَّرَ أولو الألباب}؛ أي: العقول الكاملة ما ينفعهم فيفعلونه وما يضرُّهم فيتركونه، وبذلك صاروا أولي الألباب والبصائر؛ إذ بالقرآن ازدادت معارفهم وآراؤهم، وتنوَّرت أفكارهم لَمَّا أخذوه غضًّا طريًّا؛ فإنَّه لا يدعو إلاَّ إلى أعلى الأخلاق والأعمال وأفضلها، ولا يستدلُّ على ذلك إلا بأقوى الأدلة وأبينها، وهذه القاعدة إذا تدرَّب بها العبد الذكيُّ؛ لم يزل في صعود ورقيٍّ على الدوام في كلِّ خصلة حميدة. والحمد لله رب العالمين.
{52} Alipobainisha ubainisho ulio wazi katika Qur-ani hii, akasema katika kuisifu, "Huu ni ufikishaji kwa watu." Yaani, ili wafike kwayo, na ili wachukue masurufu ya kuwafikisha katika nafasi za juu zaidi na matukufu yaliyo bora zaidi. Kwa sababu ya kile ilichojumuisha cha misingi, matawi na elimu zote wanazozihitaji waja,
“Na ili waonywe kwao” kwa sababu ya vitishio vilivyomo ndani yake dhidi ya kutenda matendo maovu na yale ambayo Mwenyezi Mungu amewaandalia watu wake ya adhabu. “Na wapate kujua kuwa hakika Yeye ni Mungu Mmoja" ambapo ameweka humo ushahidi na hoja mbalimbali juu ya uungu wake na upweke wake, basi yakawa hayo ni haki ya yakini. "Na wapate kukumbuka wenye akili." Yaani, waweze kukumbuka wenye akili kamili yale yenye kuwafaa kwa hivyo wakayafanya, na yenye kuwadhuru, kwa hivyo wakayaacha. Na kwa hayo ndiyo wakawa wenye akili na ufahamu. Kwa sababu kupitia katika Qur-ani, yalizidi maarifa yao na rai zao na fikira zao yakatiwa nuru walipoichukua katika hali yake ya upya na laini. Kwa maana hiyo hailinganii isipokuwa kwa maadili na matendo ya hali ya juu na bora zaidi, na haya hayaonyeshwi isipokuwa kwa ushahidi wenye nguvu zaidi na wa wazi zaidi. Na kanuni hii, ikiwa mja mwerevu atajifunza, daima hataacha kuendelea kuinuka juu na kupanda katika kila sifa njema. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Imekamilika tafsiri ya Surat Ibrahim, mwandani wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake.
* * *