:
Tafsiri ya Surat Ra'd
Tafsiri ya Surat Ra'd
Nayo iliteremka Madina, na pia inasemekana kuwa iliteremka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
: 1 #
{المر تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ وَالَّذِي أُنْزِلَ إِلَيْكَ مِنْ رَبِّكَ الْحَقُّ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ (1)}.
1. Alif Lam Mim Ra. Hizi ni Ishara za Kitabu. Na yale uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki. Lakini wengi wa watu hawaamini.
#
{1} يخبر تعالى أنَّ هذا القرآن هو آيات الكتاب الدالَّة على كلِّ ما يحتاج إليه العباد من أصول الدين وفروعه، وأن الذي أُنزلَ إلى الرسول من ربِّه هو الحقُّ المُبين؛ لأنَّ أخباره صدق وأوامره ونواهيه عدلٌ مؤيَّدة بالأدلَّة والبراهين القاطعة؛ فمن أقبل عليه وعلى علمه؛ كان من أهل العلم بالحقِّ الذي يوجب لهم علمهم العمل بما أحب الله. {ولكنَّ أكثر الناس [لا يؤمنون]}: بهذا القرآن: إمّا جهلاً وإعراضاً عنه وعدم اهتمام به، وإما عناداً وظلماً؛ فلذلك أكثر الناس غير منتفعين به؛ لعدم السبب الموجب للانتفاع.
{1} Yeye Mtukufu anajulisha kuwa Qur’ani hii ni ishara za Kitabu zinazoonyesha kila wanachokihitaji waja katika misingi na matawi ya Dini, na kwamba yale yaliyoteremshwa kwa Mtume kutoka kwa Mola wake Mlezi ndiyo haki iliyo wazi. Kwa sababu habari zake ni za ukweli na amri zake na makatazo yake ni ya uadilifu, yanayoungwa mkono na ushahidi na hoja za mkato. Kwa hivyo mwenye kukielekea kwa kukisoma, basi anakuwa miongoni mwa wenye elimu juu ya haki ambao elimu yao hiyo inawasababishia kufanya kile ambacho Mwenyezi Mungu anapenda. “Lakini wengi wa watu [hawaamini] katika Qur’ani hii: ima kwa sababu ya ujinga na kupeana tu mgongo na kutoijali, au kwa sababu ya ukaidi na dhuluma. Na ndiyo sababu hiyo, wengi wa watu hawafaidiki nayo, kwa sababu hawana sababu ya kuwafanya wafaidike.
: 2 - 4 #
{اللَّهُ الَّذِي رَفَعَ السَّمَاوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُسَمًّى يُدَبِّرُ الْأَمْرَ يُفَصِّلُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ بِلِقَاءِ رَبِّكُمْ تُوقِنُونَ (2) وَهُوَ الَّذِي مَدَّ الْأَرْضَ وَجَعَلَ فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنْهَارًا وَمِنْ كُلِّ الثَّمَرَاتِ جَعَلَ فِيهَا زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ (3) وَفِي الْأَرْضِ قِطَعٌ مُتَجَاوِرَاتٌ وَجَنَّاتٌ مِنْ أَعْنَابٍ وَزَرْعٌ وَنَخِيلٌ صِنْوَانٌ وَغَيْرُ صِنْوَانٍ يُسْقَى بِمَاءٍ وَاحِدٍ وَنُفَضِّلُ بَعْضَهَا عَلَى بَعْضٍ فِي الْأُكُلِ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَعْقِلُونَ (4)}
2. Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziinua mbingu bila ya nguzo mnazoziona, kisha akainuka juu ya Kiti cha Enzi, na akatiisha jua na mwezi, kila kimoja kinakwenda kwa muda maalumu. Anaendesha mambo, na anazipambanua Ishara kwa kina ili mpate kuwa na yakini ya kukutana na Mola wenu Mlezi. 3. Naye ndiye aliyeikunjua ardhi na akaweka humo milima mathubuti na mito. Na katika kila matunda akafanya jozi mbili la kiume na la kike. Huufunika usiku juu ya mchana. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa kaumu wanaotafakari. 4. Na katika ardhi vimo vipande vilivyokaribiana, na zipo bustani za mizabibu, na mimea mingine, na mitende yenye kuchipua kwenye shina moja na isiyochipua kwenye shina moja, nayo inanyweshwa katika maji yale yale. Na tunaifanya baadhi yao kuwa bora kuliko mengine katika kula. Hakika katika hayo zimo ishara kwa kaumu wanaotia mambo akilini.
#
{2} يخبر تعالى عن انفراده بالخلق والتدبير والعظمة والسلطان الدالِّ على أنه وحده المعبود الذي لا تنبغي العبادة إلاَّ له، فقال: {الله الذي رفعَ السموتِ}: على عظمها واتِّساعها بقدرته العظيمة، {بغير عَمَدٍ تَرَوْنها}؛ أي: ليس لها عَمَدٌ من تحتها؛ فإنَّه لو كان لها عَمَدٌ؛ لرأيتُموها، {ثم}: بعدما خلق السماواتِ والأرض، {استوى على العرش}: العظيم، الذي هو أعلى المخلوقات، استواءً يَليق بجلاله ويناسب كماله. {وسخَّر الشمس والقمر}: لمصالح العباد ومصالح مواشيهم وثمارهم. {كلٌّ}: من الشمس والقمر، {يَجْري}: بتدبير العزيز العليم {إلى أجل مسمّى}: بسير منتظم لا يفتُران ولا يَنِيان حتى يجيء الأجل المسمَّى، وهو طيُّ الله هذا العالم ونقلهم إلى الدار الآخرة التي هي دار القرار؛ فعند ذلك يطوي الله السماواتِ ويبدِّلها ويُغَيِّر الأرض ويبدِّلها، فتكوَّر الشمس والقمر و [يُجمع] بينهما فيلقيانِ في النار؛ ليرى من عبدهما أنَّهما غير أهل للعبادة، فيتحسَّر بذلك أشدَّ الحسرة، وليعلم الذين كفروا أنَّهم كانوا كاذبين. وقوله: {يدبِّر الأمر يفصِّلُ الآياتِ}: هذا جمعٌ بين الخلق والأمر؛ أي: قد استوى الله العظيم على سرير الملك؛ يدبِّر الأمور في العالم العلويِّ والسفليِّ، فيخلق ويرزق، ويغني ويُفْقِر، ويرفع أقواماً ويضع آخرين، ويعزُّ ويذلُّ، ويَخْفِضُ ويرفعُ، ويَقيلُ العثراتِ، ويفرِّجُ الكربات، وينفذُ الأقدار في أوقاتها التي سبق بها علمهُ وجرى بها قلمه، ويرسل ملائكته الكرام لتدبير ما جعلهم على تدبيرِهِ، وينزِّل الكتب الإلهية على رسله، ويبين ما يحتاجُ إليه العباد من الشرائع والأوامر والنواهي، ويفصِّلها غايةَ التفصيل ببيانها وإيضاحها وتمييزها. {لعلَّكم}: بسبب ما أخرج لكم من الآيات الأفقيَّة والآيات القرآنيَّة، {بلقاء ربِّكم توقنون}: فإنَّ كثرة الأدلَّة وبيانها ووضوحها من أسباب حصول اليقين في جميع الأمور الإلهيَّة، خصوصاً في العقائد الكبار؛ كالبعث والنشور والإخراج من القبور. وأيضاً؛ فقد عُلم أنَّ الله تعالى حكيمٌ؛ لا يخلُق الخلق سدىً، ولا يتركهم عبثاً؛ فكما أنَّه أرسل رسله وأنزل كتبه لأمر العباد ونهيهم؛ فلا بدَّ أن ينقلَهم إلى دار يحلُّ فيهم جزاؤه؛ فيجازي المحسنين بأحسن الجزاء، ويجازي المسيئين بإساءتهم.
{2} Yeye Mtukufu anajulisha juu ya upekee wake katika uumbaji, uendeshaji mambo, ukuu, na mamlaka, jambo ambalo linaashiria kwamba Yeye peke yake ndiye anayepaswa kuabudiwa, ambaye haifai kufanya ibada isipokuwa kwa ajili yake tu. Kwa hivyo akasema, “Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziinua mbingu” pamoja na ukubwa wake na upana wake, kwa uwezo wake mkubwa, "bila ya nguzo mnazoziona.” Yaani, hazina nguzo zozote kwa chini yake. Kwa maana zingekuwa zina nguzo, basi mngeliziona “kisha” baada ya kuziumba mbingu na ardhi, “akainuka juu ya Kiti cha Enzi” kikubwa, ambacho ndicho kiumbe cha juu zaidi. Aliinuka juu kuinuka kunakolingana na utukufu wake na ukamilifu wake, “na akatiisha jua na mwezi” kwa masilahi ya waja na masilahi ya mifugo yao na matunda yao. "Kila kimoja" yaani jua na mwezi, "kinakwenda" kwa uendeshaji wa Mwenye nguvu, Mwenye kujua yote “kwa muda maalumu,” kwa mwendo uliopangwa, havipumziki, wala havichoki mpaka utakapokuja muda uliowekwa. Ambayo ni muda ule Mwenyezi Mungu ataukunja ulimwengu huu na kuwahamisha hadi kwenye nyumba ya akhera, ambayo ndiyo nyumba ya makazi ya kudumu. Kisha Mwenyezi Mungu atazikunja mbingu na kuzibadilisha, na ataighairi ardhi na kuibadilisha. Nalo jua na mwezi atavikunjakunja, na [kuviunganisha] na vitatupwa ndani ya Moto. Ili wale wanaoviabudu waone kuwa hivyo havistahiki kuabudiwa, kwa hivyo watajuta majuto makubwa zaidi kwa sababu ya hilo, na ile wajue wale waliokufuru kwamba walikuwa waongo. Na kauli yake, “anaendesha mambo, na anazipambanua Ishara kwa kina.” Huku ni kujumuisha kati ya uumbaji na amri. Yaani, Mwenyezi Mungu Mkuu ameinuka juu ya kiti cha ufalme, anaendesha mambo yote ya ulimwengu wa juu na wa chini. Kwa hivyo anaumba na kuruzuku, anatajirisha na kufukarisha, anawanyanyua baadhi ya watu na kuwadunisha wengine, anatukuza na kudhalilisha, anateremsha na kuinua, anakinga kutokana na vikwazo, anaondoa misiba, anatekeleza majaliwa katika nyakati zake ambazo alikwisha jua na kalamu yake ikayaandika; na anawatuma Malaika wake watukufu kuyaendesha yale aliyowafanya kuendesha. Na anateremsha Vitabu vya kiungu kwa Mitume wake, na anabainisha yale wanayohitaji waja wake katika sheria mbalimbali, maamrisho na makatazo, na anayabainisha kwa kina zaidi na kuyapambanua. "ili" kwa sababu ya yale aliyowatolewa miongoni mwa ishara mbalimbali za kiupeo na ishara za kiqur-ani, "mpate kuwa na yakini ya kukutana na Mola wenu Mlezi.” Kwa maana, wingi wa ushahidi, na ubainifu wake na kuwa kwake wazi ni katika sababu za kupata yakini katika mambo yote ya kimungu, hasa katika itikadi kuu, kama vile ufufuo, na kupelekwa mahali pa hesabu, na kutolewa makaburini. Na pia, inajulikana kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye hekima. Yeye haumbi viumbe bure, wala haviachi bure. Kama vile alivyowatuma Mitume wake na akateremsha vitabu vyake kuamrisha na kuwakataza waja wake, basi ni lazima atawahamisha hadi katika nyumba ambayo kuna malipo yao, ili awalipe wafanyao mazuri kwa malipo mazuri zaidi, na awalipe wafanyao mabaya kwa ubaya wao.
#
{3} {وهو الذي مدَّ الأرض}؛ أي: خلقها للعباد ووسَّعها وبارك فيها ومهَّدَها للعباد وأودعَ فيها من مصالحهم ما أودع، {وجعل فيها رواسيَ}؛ أي: جبالاً عظاماً؛ لئلاَّ تميدَ بالخلق؛ فإنَّه لولا الجبال؛ لمادت بأهلها؛ لأنها على تيار ماء لا ثبوت لها ولا استقرار إلا بالجبال الرَّواسي التي جعلها الله أوتاداً لها. {و} جعل فيها {أنهاراً} تسقي الآدميين وبهائمهم وحروثهم؛ فأخرج بها من الأشجار والزروع والثمار خيراً كثيراً، ولهذا قال: {ومن كلِّ الثمرات جعل فيها زوجين اثنينِ}؛ أي: صنفين مما يحتاج إليه العباد. {يُغشي الليل النهار}: فتظلم الآفاق، فيسكن كلُّ حيوان إلى مأواه، ويستريحون من التعب والنصب في النهار، ثم إذا قَضَوْا مآربهم من النوم؛ غشي النهارُ الليلَ؛ فإذا هم مصبحون [منتشرون] في مصالحهم وأعمالهم في النهار، {ومن رحمتِهِ جعل لكم الليلَ والنَّهار لتسكُنوا فيه ولِتَبْتَغوا من فضلِهِ ولعلَّكم تشكُرون}. {إنَّ في ذلك لآياتٍ}: على المطالب الإلهيَّة {لقوم يتفكَّرون}: فيها وينظرون فيها نظر اعتبارٍ دالَّة على أن الذي خلقها ودبَّرها وصرَّفها هو الله الذي لا إله إلاَّ هو، ولا معبود سواه، وأنَّه عالم الغيب والشهادة الرحمن الرحيم، وأنَّه القادر على كل شيء، الحكيم في كلِّ شيء، المحمود على ما خَلَقَه وأمر به، تبارك وتعالى.
{3} "Naye ndiye aliyeikujua ardhi;” yaani, aliiumba kwa ajili ya waja, akaipanua, akabariki ndani yake, akaitandaza kwa ajili ya waja, na akaweka ndani yake yale yenye manufaa kwao, "akaweka humo milima mathubuti.” Yaani, milima mikubwa, ili isiyumbeyumbe na viumbe. Kwa maana lau kuwa si milima, basi ingeyumbayumba na wakazi wake, kwa sababu iko juu ya mkondo wa maji, ambao haina uthabiti wowote wala kukaa tulivu isipokuwa kwa milima imara ambayo Mwenyezi Mungu ameifanya kuwa vigingi vyake. Na akafanya humo “mito” yenye kuwanywesha wanadamu, mifugo yao na mimea yao. Basi akatoa kwayo heri nyingi katika miti, mimea na matunda, na ndiyo maana akasema: "Na katika kila matunda akafanya jozi mbili la kiume na la kike;” yaani, sampuli mbili katika wanavyovihitaji waja. "Huufunika usiku juu ya mchana” kwa hivyo peo za macho zinakuwa giza, na kila mnyama anarudi kwenye makazi yake, na kupumzika kutokana na taabu na uchovu wa mchana. Kisha wanapotimiza haja yao katika kulala, mchana unaufunika usiku; basi wanakuwa hivi wameingia asubuhi wakawa [wanaenea] katika kutafuta masilahi yao na matendo yao mchana. “Na katika rehema zake ni kwamba amewafanyia usiku na mchana ili mpate kutulia humo na ili mtafute katika fadhila zake, ili mshukuru.” “Hakika katika hayo zimo Ishara” juu ya matakwa ya kiungu “kwa kaumu wanaotafakari,” juu yake na wanaziangalia kwa mtazamo wa kuzingatia wenye kunyesha kwamba aliyeziumba na kuziendesha na kuzibadilishabadilisha ni Mwenyezi Mungu ambaye hakuna mungu isipokuwa Yeye. Na hakuna muabudiwa asiyekuwa Yeye, na kwamba Yeye ni Mwenye kujua ghaibu na yanayoshuhudiwa, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu, na kwamba Yeye ni Muweza wa kila kitu, Mwenye hekima katika kila kitu, Msifika kwa alichokiumba na alichoamrisha, Mwenye baraka na Mtukufu.
#
{4} {و} من الآيات على كمال قدرتِهِ وبديع صنعته أن جعل {في الأرض قِطَعٌ متجاوراتٌ وجناتٌ}: فيها أنواع الأشجار: من الأعنابٍ والنخل والزَرْع، وغير ذلك، والنخيل التي بعضها {صنوان}؛ أي: عدة أشجار في أصل واحدٍ. {وغيرُ صِنْوانٍ}: بأن كان كل شجرة على حدتها، والجميع {يُسْقى بماء واحدٍ}: وأرضُه واحدةٌ. {ونُفضِّل بعضَها على بعضٍ في الأُكُل}: لوناً وطعماً ونفعاً ولذَّةً؛ فهذه أرض طيِّبة تنبت الكلأ والعشب الكثير والأشجار والزروع، وهذه أرضٌ تلاصِقُها لا تنبتُ كلأً ولا تمسك ماءً، وهذه تمسك الماء ولا تنبت الكلأ، وهذه تنبِتُ [الزروع] والأشجار ولا تنبِتُ الكلأ، وهذه الثمرةُ حلوةٌ وهذه مرَّةٌ وهذه بين ذلك؛ فهل هذا التنوُّع في ذاتها وطبيعتها أم ذلك تقدير العزيز الرحيم؟ {إنَّ في ذلك لآياتٍ لقوم يعقلونَ}؛ أي: لقوم لهم عقولٌ تهديهم إلى ما ينفعُهم وتقودهم إلى ما يرشدون ويعقلون عن الله وصاياه وأوامره ونواهيه، وأما أهلُ الإعراض وأهل البلادة؛ فهم في ظُلُماتهم يعمَهون وفي غيِّهم يتردَّدون، لا يهتدون إلى ربِّهم سبيلاً ولا يعون له قيلاً.
{4} "Na" miongoni mwa ishara za ukamilifu wa uwezo wake na ufundi wake wa hali ya juu zaidi ni kwamba alifanya "katika ardhi vimo vipande vilivyokaribiana na zipo bustani;" ambayo ndani yake kuna kila aina ya miti ya mizabibu, na mitende, na mimea na visivyokuwa hivyo, na mitende, ambayo baadhi yake ni "yenye kuchipua kwenye shina moja na isiyochipua kwenye shina moja" kwa namna kwamba kila mti uko kivyake, na yote "inanyweshwa katika maji yale yale" na ardhi yake ni moja. "Na tunaifanya baadhi yao kuwa bora kuliko mengine katika kula" katika rangi, ladha, manufaa, na raha. Kwa hivyo, hii ardhi ni nzuri inaotesha malisho, nyasi nyingi, miti na mimea, na karibu yake kuna ardhi ambayo haioteshi malisho wala haishikilii maji, na hii nyingine inashikilia maji lakini haioti malisho. Na hii nyingine inaotesha [mimea na] miti lakini haioti malisho. Na haya matunda ni matamu na haya ni machungu na haya ni kati ya hayo. Basi je, utofauti huu ni yenyewe tu ndani yake na maumbile yake, au hilo ni kwa sababu ya majaliwa ya Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu? "Hakika katika hayo zimo ishara kwa kaumu wanaotia mambo akilini." Yaani, kaumu wenye akili zinazowaongoza kwenye yale yanayowafaa na kuwaongoza katika yale yanayowafanya kunyooka na kuyafahamu maamrisho ya Mwenyezi Mungu na makatazo yake. Na ama wale wanaopeana mgongo na wala hawatumii akili zao, wao wanatangatanga na ni vipofu katika giza mbalimbali, na wanasitasita katika upotovu wao. Hawawezi kuongoka kufikia njia ya kwenda kwa Mola wao Mlezi, wala hawawezi kuelewa neno lake lolote.
: 5 #
{وَإِنْ تَعْجَبْ فَعَجَبٌ قَوْلُهُمْ أَإِذَا كُنَّا تُرَابًا أَإِنَّا لَفِي خَلْقٍ جَدِيدٍ أُولَئِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ وَأُولَئِكَ الْأَغْلَالُ فِي أَعْنَاقِهِمْ وَأُولَئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ (5)}.
5. Na kama ukistaajabu, basi cha ajabu zaidi ni huo usemi wao: Je, tukishakuwa mchanga, kweli tutakuwa katika umbo jipya? Hao ndio waliomkufuru Mola wao Mlezi. Na hao ndio watakaokuwa na makongwa shingoni mwao, na hao ndio watu wa Motoni. Humo watadumu.
#
{5} يحتمل أنَّ معنى قوله: {وإن تَعْجَبْ}: من عظمة الله تعالى وكثرة أدلَّة التوحيد؛ فإنَّ العجب مع هذا إنكار المكذِّبين وتكذيبهم بالبعث وقولهم: {أإذا كُنَّا تراباً أإنّا لفي خلقٍ جديدٍ}؛ أي: هذا بعيدٌ في غاية الامتناع بزعمهم أنَّهم بعدما كانوا تراباً أن الله يُعيدهم؛ فإنَّهم من جهلهم قاسوا قدرة الخالق بقدرة المخلوق، فلما رأوا هذا ممتنعاً في قدرة المخلوق، ظنُّوا أنه ممتنعٌ على قدرة الخالق، ونسوا أنَّ الله خلقهم أول مرَّة ولم يكونوا شيئاً. ويُحتمل أنَّ معناه: وإنْ تعجَبْ من قولهم وتكذيبهم للبعث؛ فإنَّ ذلك من العجائب؛ فإنَّ الذي تُوَضَّح له الآيات ويرى منها الأدلة القاطعة على البعث ما لا يقبل الشكَّ والريبَ ثم ينكِرُ ذلك؛ فإنَّ قوله من العجائب، ولكن ذلك لا يُستغرب على {الذين كفروا بربهم}: وجَحَدوا وحدانيَّته، وهي أظهرُ الأشياء وأجلاها. {وأولئك الأغلالُ}: المانعة لهم من الهدى {في أعناقِهِم}: حيث دُعُوا إلى الإيمان فلم يؤمنوا، وعُرِضَ عليهم الهدى فلم يهتدوا، فقلِبَت قلوبهم وأفئدتهم عقوبةً على أنهم لم يؤمنوا به أول مرة. {وأولئك أصحابُ النار هم فيها خالدون}: لا يخرجون منها أبداً.
{5} Inawezekana kwamba maana ya kauli yake, "Na kama ukistaajabu;" yaani, ukistaajabu na ukuu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na wingi wa ushahidi wa tauhidi, basi hakika la kustaajabisha zaidi ya hilo ni kukanusha kwa hao wanaokadhibisha na kukadhibisha kwao kufufuliwa na kusema kwao. "Je, tukishakuwa mchanga, kweli tutakuwa katika umbo jipya?" Yaani, hili haliwezekani kabisa kulingana na madai yao kwamba baada ya kuwa kwao udongo, kwamba Mwenyezi Mungu atawarudisha. Kwa kuwa, kwa sababu ya ujinga wao, walilinganisha uwezo wa Muumba yote na uwezo wa kiumbe, na walipoona jambo hili haliwezekani kwa uwezo wa kiumbe huyo, wakafikiri kwamba haliwezekani kwa uwezo wa Muumba yote, na wakasahau kwamba mwenyezi Mungu aliwaumba mara ya kwanza na hawakuwa chochote. Na inawezekana kwamba maana yake ni, kuwa hata ukistaajabishwa na maneno yao na kukadhibisha kwao kufufuliwa, basi hilo ni katika maajabu. Kwa maana yule anayebainishiwa ishara mbalimbali na akaona ndani yake ushahidi wa kukata juu ya kufufuliwa usiokubali shaka yoyote wala kusitasita, kisha akakakunusha hilo, basi hakika kauli yake ni miongoni mwa maajabu, lakini hilo halishangazi kutoka kwa wale "waliomkufuru Mola wao Mlezi" na wakakanusha upweke wake ambao ndio kitu kilicho dhahiri zaidi na kilicho wazi zaidi. "Na hao ndio watakaokuwa na makongwa" zinazowazuilia kuongoka, "shingoni mwao" kwa kuwa waliitwa kwenye Imani lakini hawakuamini, na wakawekewa mbele uwongofu lakini hawakuongoka, basi nyoyo zao zikapinduliwa kama adhabu kwa kuwa hawakuiamini mara ya kwanza. "Na hao ndio watu wa Motoni. Humo watadumu" na hawatatoka humo abadan.
: 6 #
{وَيَسْتَعْجِلُونَكَ بِالسَّيِّئَةِ قَبْلَ الْحَسَنَةِ وَقَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلِهِمُ الْمَثُلَاتُ وَإِنَّ رَبَّكَ لَذُو مَغْفِرَةٍ لِلنَّاسِ عَلَى ظُلْمِهِمْ وَإِنَّ رَبَّكَ لَشَدِيدُ الْعِقَابِ (6)}.
6. Na wanakuhimiza ulete mabaya kabla ya mazuri, hali ya kuwa zimekwisha pita kabla yao adhabu za kupigiwa mfano. Na hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye msamaha kwa watu juu ya udhalimu wao. Na hakika Mola wako Mlezi ni Mkali wa kuadhibu.
#
{6} يخبر تعالى عن جهل المكذِّبين لرسوله، المشركين به، الذين وُعظوا فلم يتَّعظوا، وأُقيمت عليهم الأدلَّة فلم ينقادوا لها، بل جاهروا بالإنكار، واستدلُّوا بحِلْم الله الواحد القهار عنهم وعدم معاجلتهم بذنوبهم أنهم على حقٍّ، وجعلوا يستعجلون الرسول بالعذاب، ويقول قائلهم: {اللهمَّ إن كان هذا هو الحقَّ من عندِكَ فأمطِرْ علينا حجارةً من السماء أو ائتِنا بعذابٍ أليم}! {و} الحال أنَّه {قد خَلَتْ من قبلهم المَثُلاتُ}؛ أي: وقائع الله وأيامه في الأمم المكذبين، أفلا يتفكَّرون في حالهم ويتركون جهلهم؟! {وإنَّ ربَّك لذو مغفرةٍ للناس على ظلمِهِم}؛ أي: لا يزال خيره إليهم وإحسانُه وبرُّه وعفوه نازلاً إلى العباد، وهم لا يزال شِرْكهم وعصيانهم إليه صاعداً؛ يعصونه فيدعوهم إلى بابه، ويجرِمون فلا يحرِمُهم خيره وإحسانه؛ فإنْ تابوا إليه؛ فهو حبيبُهم؛ لأنَّه يحبُّ التوَّابين ويحبُّ المتطهِّرين، وإن لم يتوبوا؛ فهو طبيبُهم؛ يبتليهم بالمصائب ليطهِّرهم من المعايب: {قل يا عبادي الذين أسرفوا على أنفسهم لا تقنَطوا من رحمةِ الله إنَّ الله يغفرُ الذُّنوب جميعاً إنَّه هو الغفور الرحيم}. {وإنَّ ربَّك لشديدُ العقابِ}: على من لم يزلْ مصرًّا على الذُّنوب، قد أبى التوبة والاستغفار والالتجاء إلى العزيز الغفار؛ فليحذرِ العبادُ عقوباتِهِ بأهل الجرائم؛ فإنَّ أخذَه أليم شديدٌ.
{6} Yeye Mtukufu anajulisha juu ya ujinga wa wale waliomkadhibisha Mtume wake, wale wanaomshirikisha na wengine, ambao waliaidhiwa lakini hawakuaidhika, na ukasimamishwa ushahidi mbalimbali juu yao, lakini hawakufuata. Bali walikanusha hayo waziwazi na wakatumia kama ushahidi ustahamilivu wa Mwenyezi Mungu Mmoja, Mshindi juu yao na kwamba hakuwaharakishia adhabu kwa sababu ya dhambi zao, kwamba wao wako katika haki, kwa hivyo wakaanza kumharakisha Mtume kuwafikishia adhabu, na anasema msemaji wao: "Ewe Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ndiyo ya haki kutoka kwako, basi tunyeshee mawe kutoka mbinguni, au tuletee adhabu yoyote iliyo chungu." "Na" hali ni kwamba "zimekwisha pita kabla yao adhabu za kupigiwa mfano." Yaani, matukio ya Mwenyezi Mungu na siku zake katika umma waliokadhibisha. Je, hawatafakari katika hali zao na kuacha ujinga wao? "Na hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye msamaha kwa watu juu ya udhalimu wao." Yaani, haijaacha kuwateremkia waja wake heri yake na ihsani yake, na wema wake, na msamaha wake nao haujaacha kupanda kwake ushirikina wao na maasia yao. Wanamuasi, naye anawalingania kwenye mlango wake, na wanafanya uhalifu, lakini yeye hawanyimi heri yake na ihsani yake. Kwa hivyo, wakitubia kwake, basi Yeye ni kipenzi chao. Kwa sababu anawapenda wanaotubu na anawapenda wanaojitakasa. Na wasipotubia, basi yeye ndiye daktari wao. Anawajaribu kwa misiba ili awatakase kutokana na makosa yao. “Sema: Enyi waja wangu walijidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu." "Na hakika Mola wako Mlezi ni Mkali wa kuadhibu" kwa yule ambaye haachi kuendelea kufanya madhambi, ambaye amekataa kutubu na kuomba msamaha, na kukimbilia kwa Mwenye nguvu, Mwingi sana wa kusamehe. Basi na wajihadhari waja kutokana na adhabu zake kwa wafanyao uhalifu. Kwa maana hakika mshiko wake ni mchungu sana na mkali.
: 7 #
{وَيَقُولُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْلَا أُنْزِلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِنْ رَبِّهِ إِنَّمَا أَنْتَ مُنْذِرٌ وَلِكُلِّ قَوْمٍ هَادٍ (7)}.
7. Na wale waliokufuru wanasema: Mbona hakuteremshiwa ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi? Hakika wewe ni Mwonyaji tu, na kila kaumu ina wa kuwaongoza.
#
{7} أي: ويقترح الكفارُ عليك من الآيات التي يُعَيِّنُونَها ويقولون: {لولا أنزِلَ عليه آيةٌ من ربِّه}، ويجعلون هذا القول منهم عُذراً لهم في عدم الإجابة إلى الرسول، والحال أنَّه منذرٌ، ليس له من الأمر شيءٌ، والله هو الذي ينزِّل الآيات، وقد أيَّده بالأدلَّة البيِّنات التي لا تخفى على أولي الألباب، وبها يهتدي من قصدُهُ الحقُّ، وأما الكافر الذي مِنْ ظلمه وجهله يقترح على الله الآيات؛ فهذا اقتراحٌ منه باطلٌ وكذبٌ وافتراءٌ ؛ فإنَّه لو جاءته أيُّ آية كانت؛ لم يؤمن ولم ينقد؛ لأنَّه لم يمتنع من الإيمان لعدم ما يدلُّه على صحته، وإنَّما ذلك لهوى نفسه واتِّباع شهوته. {ولكلِّ قوم هادٍ}؛ أي: داعٍ يدعوهم إلى الهدى من الرسل وأتباعهم، ومعهم من الأدلَّة والبراهين ما يدلُّ على صحَّة ما معهم من الهدى.
{7} Yaani makafiri wanakupendekezea baadhi ya ishara wanazozitaka wao, na wanasema: “Mbona hakuteremshiwa ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi?" Na wanaifanya kauli yao hii kuwa ni udhuru wao wa kutomuitikia Mtume, na hali ni kuwa yeye ni mwonyaji tu, wala hana lolote katika jambo hilo, na Mwenyezi Mungu ndiye anayeteremsha ishara mbalimbali. Na alimuunga mkono kwa ushahidi mbalimbali ulio wazi ambao haufichikani kwa wenye akili, na kwayo anaongoka yule ambaye ameikusudia haki. Na ama kafiri, ambaye kwa sababu ya dhuluma yake na ujinga wake anampendekezea Mwenyezi Mungu kuleta ishara mbalimbali, basi pendekezo lake hili ni batili uwongo, na uzushi. Kwa maana lau kuwa itamjia ishara yoyote ile, hataamini wala kuifuata. Kwa sababu hakukataa kuamini kwa sababu ya kukosa cha kumuonyesha usahihi wake; bali hilo ni kwa sababu ya matamanio ya nafsi yake na kufuata tamaa zake. "Na kila kaumu ina wa kuwaongoza." Yaani, mlinganiaji anayewalingania kwenye uwongofu kama vile Mitume na wafuasi wao, nao huwa na ushahidi na hoja mbalimbali pamoja nao zenye kuwaonyesha usahihi wa uwongofu walio nao.
: 8 - 11 #
{اللَّهُ يَعْلَمُ مَا تَحْمِلُ كُلُّ أُنْثَى وَمَا تَغِيضُ الْأَرْحَامُ وَمَا تَزْدَادُ وَكُلُّ شَيْءٍ عِنْدَهُ بِمِقْدَارٍ (8) عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْكَبِيرُ الْمُتَعَالِ (9) سَوَاءٌ مِنْكُمْ مَنْ أَسَرَّ الْقَوْلَ وَمَنْ جَهَرَ بِهِ وَمَنْ هُوَ مُسْتَخْفٍ بِاللَّيْلِ وَسَارِبٌ بِالنَّهَارِ (10) لَهُ مُعَقِّبَاتٌ مِنْ بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ يَحْفَظُونَهُ مِنْ أَمْرِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُوا مَا بِأَنْفُسِهِمْ وَإِذَا أَرَادَ اللَّهُ بِقَوْمٍ سُوءًا فَلَا مَرَدَّ لَهُ وَمَا لَهُمْ مِنْ دُونِهِ مِنْ وَالٍ (11)}.
8. Mwenyezi Mungu anajua mimba abebayo kila cha kike, na kinachopunguka na kuzidi matumboni mwa uzazi. Na kila kitu kwake ni kwa kipimo. 9. Yeye ndiye Mwenye kujua ya ghaibu na yanayoonekana, Mkubwa, Mtukufu. 10. Ni sawa anayeficha kauli yake miongoni mwenu na anayeidhihirisha, na anayejibanza usiku na anayetembea jahara mchana. 11. Kila mtu analo kundi la malaika mbele yake na nyuma yake linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa kaumu mpaka wabadili wao yaliyomo katika nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu anapowatakia kaumu ubaya, basi hakuna cha kuyazuia wala hawana mlinzi yeyote asiyekuwa Yeye.
#
{8 - 9} يخبر تعالى بعموم علمه وسعة اطَّلاعه وإحاطته بكلِّ شيء، فقال: {الله يعلمُ ما تحمِلُ كلُّ أنثى}: من بني آدم وغيرهم، {وما تَغيضُ الأرحامُ}؛ أي: تَنْقُصُ مما فيها، إما أن يَهْلِكَ الحمل أو يتضاءل أو يضمحلَّ، {وما تزدادُ}: الأرحام وتكبر الأجنَّة التي فيها. {وكلُّ شيءٍ عنده بمقدارٍ}: لا يتقدَّم عليه ولا يتأخَّر ولا يزيد ولا يَنْقُص إلاَّ بما تقتضيه حكمته وعلمه؛ فإنَّه {عالمُ الغيب والشهادةِ الكبيرُ}: في ذاته وأسمائه وصفاته، {المتعالِ}: على جميع خلقه بذاتِهِ وقدرته وقهره.
{8 - 9} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu ujumla ya elimu yake, na upana wa kujua kwake, na kukizunguka kwake kila kitu, kwa hivyo akasema, "Mwenyezi Mungu anajua mimba abebayo kila cha kike" katika wanadamu na wengineo. "Na kinachopunguka matumboni mwa uzaz;i" yaani, ima kwa kuharibika kwa mimba au hupungua "na kuzidi" matumboni mwa uzazi na kuongezeka kwa ukubwa wa mimba. "Na kila kitu kwake ni kwa kipimo" hakitangulii kipimo hicho, wala hakichelewi, wala hakizidishi wala hakipungui isipokuwa kwa kile kinachohitajiwa na hekima na elimu yake. Kwa maana, hakika Yeye ndiye "Mwenye kujua ya ghaibu na yanayoonekana, Mkubwa" katika dhati Yake, majina yake, na sifa Zake, "Mtukufu" kwa viumbe vyake vyote kwa dhati Yake, na uwezo Wake, na ushindi Wake.
#
{10} {سواءٌ منكم}: في علمه وسمعه وبصره، {مَنْ أسرَّ القول ومن جَهَرَ به ومن هو مستخفٍ بالليل}؛ أي: مستقرٌّ بمكان خفي فيه، {وساربٌ بالنهار}؛ أي: داخل سربه في النهار، والسربُ هو ما يستخفي فيه الإنسان: إما جوف بيته، أو غار، أو مغارة، أو نحو ذلك.
{10} "Ni sawa" katika elimu yake, na kusikia kwake, na kuona kwake, "anayeficha kauli yake miongoni mwenu na anayeidhihirisha, na anayejibanza usiku." Yaani, mwenye kukaa mahali pa siri, "na anayetembea jahara mchana." Na ilisemwa kuwa maana yake ni mwenye kuingia katika maficho yake mchana, ima ndani ya nyumba yake, pango, au mfano wa hayo.
#
{11} {له}؛ أي: للإنسان {معقباتٌ}: من الملائكة يتعاقبون في الليل والنهار، {من بين يديهِ ومن خلفِهِ يحفظونَه من أمر الله}؛ أي: يحفظون بدنه وروحه من كلِّ مَن يريده بسوء، ويحفظون عليه أعماله، وهم ملازمون له دائماً؛ فكما أنَّ علم الله محيطٌ به؛ فالله قد أرسل هؤلاء الحفظة على العباد بحيث لا تَخْفى أحوالهم ولا أعمالهم ولا يُنسَى منها شيء. {إنَّ الله لا يغيِّر ما بقوم}: من النعمة والإحسان ورَغَدِ العيش، {حتَّى يغيِّروا ما بأنفسِهم}: بأن ينتقلوا من الإيمان إلى الكفر، ومن الطاعة إلى المعصية، أو من شكر نعم الله إلى البطر بها، فيسلُبُهم الله عند ذلك إياها، وكذلك إذا غير العباد ما بأنفسهم من المعصية، فانتقلوا إلى طاعة الله؛ غيَّر الله عليهم ما كانوا فيه من الشقاء إلى الخير والسرور والغبطة والرحمة. {وإذا أراد الله بقوم سوءاً}؛ أي: عذاباً وشدَّة وأمراً يكرهونه؛ فإنَّ إرادته لا بدَّ أن تنفذ فيهم، فإنه {لا مردَّ له}، ولا أحد يمنعهم منه، {وما لهم من دونِهِ من والٍ}: يتولَّى أمورهم، فيجلب لهم المحبوبَ، ويدفع عنهم المكروهَ. فَلْيَحْذروا من الإقامة على ما يكره الله؛ خشية أن يحلَّ بهم من العقاب ما لا يُرَدُّ عن القوم المجرمين.
{11} "Kila mtu analo kundi la malaika" wanaobadilishana zamu mchana na usiku, "mbele yake na nyuma yake linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu." Yaani, wanaulinda mwili wake na roho yake kutokana na kila anayemtakia mabaya, na wanamhifadhia matendo yake, nao huwa pamoja naye daima. Kama vile elimu ya Mwenyezi Mungu inavyomzunguka, Mwenyezi Mungu amewatuma walinzi hawa juu ya waja wake ili hali zao na matendo yao yasifiche, na kwamba kisisahaulike kitu chochote. "Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyo kwa kaumu" miongoni mwa neema, ihsani, na maisha ya starehe, "mpaka wabadili wao yaliyomo katika nafsi zao" kwa kutoka katika imani na kwenda kwenye ukafiri, na kutoka katika utiifu hadi katika uasi, au kutoka katika kushukuru neema za Mwenyezi Mungu hadi katika kujifahiri nazo, ambapo Mwenyezi Mungu hapo anawaondolea hayo. Na vivyo hivyo ikiwa waja watabadilisha yaliyo katika nafsi zao za ya uasi, kwenda katika kumtii Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atawabadilishia hali waliyokuwa nayo ya mashaka hadi kwenye heri, furaha, hali nzuri, na rehema. "Na Mwenyezi Mungu anapowatakia kaumu ubaya;" yaani, adhabu na ugumu, na jambo wanalolichukia, basi ni lazima mapenzi yake yatimie kwao, kwa maana yeye “hakuna cha kuyazuia" na hakuna wa kumzuia, “wala hawana mlinzi yeyote asiyekuwa Yeye," anayeweza kusimamia mambo yao na kuwaletea wanayoyapenda, na kuwazuia wanayoyachukia. Basi na watahadhari kudumu katika yale anayoyachukia Mwenyezi Mungu, kwa kuhofu kwamba itawapata adhabu ambayo hairudishwi dhidi ya kaumu wahalifu.
: 12 - 13 #
{هُوَ الَّذِي يُرِيكُمُ الْبَرْقَ خَوْفًا وَطَمَعًا وَيُنْشِئُ السَّحَابَ الثِّقَالَ (12) وَيُسَبِّحُ الرَّعْدُ بِحَمْدِهِ وَالْمَلَائِكَةُ مِنْ خِيفَتِهِ وَيُرْسِلُ الصَّوَاعِقَ فَيُصِيبُ بِهَا مَنْ يَشَاءُ وَهُمْ يُجَادِلُونَ فِي اللَّهِ وَهُوَ شَدِيدُ الْمِحَالِ (13)}
12. Yeye ndiye anayewaonyesha umeme kwa hofu na matumaini, na huyaanzisha mawingu mazito. 13. Na radi inamtakasa Mwenyezi Mungu kwa kumhimidi, na Malaika pia, kwa kumhofu. Naye hutuma mapigo ya radi na kumsibu kwayo amtakaye. Nao wanabishana kuhusiana na Mwenyezi Mungu, na Yeye ndiye Mwenye adhabu kali!
#
{12} يقول تعالى: {هو الذي يُريكم البرقَ خوفاً وطمعاً}؛ أي: يُخاف منه الصواعق والهدم وأنواع الضَّرر على بعض الثمار ونحوها، ويُطمع في خيره ونفعه، {ويُنشِئ السَّحاب الثِّقال}: بالمطر الغزير الذي به نفعُ العباد والبلاد.
{12} Yeye Mtukufu anasema, "Yeye ndiye anayewaonyesha umeme kwa hofu na matumaini." Yaani, inahofiwa kutoka kwake kupigwa na radi, kubomolewa, na aina nyengine za madhara juu ya baadhi ya matunda na mfano wake, na inatumainiwa heri yake na manufaa yake. "Na huyaanzisha mawingu mazito" yakija na mvua kubwa yenye manufaa kwa waja na ardhi.
#
{13} {ويسبِّح الرعدُ بحمده}: وهو الصوت الذي يُسمع من السحاب المزعج للعباد؛ فهو خاضعٌ لربِّه، مسبِّح بحمده، {و} تسبِّح {الملائكةُ من خِيفتِهِ}؛ أي: خُشَّعاً لربهم خائفين من سطوتِهِ، {ويرسل الصواعقَ}: وهي هذه النار التي تخرج من السحاب. {فيصيبُ بها مَن يشاءُ}: من عباده بحسب ما شاءه وأراده. {وهو شديدُ المحال}؛ أي: شديد الحَوْل والقوَّة؛ فلا يريد شيئاً إلاَّ فعله، ولا يتعاصى عليه شيءٌ، ولا يفوتُه هاربٌ. فإذا كان هو وحده الذي يسوق للعباد الأمطار والسحب التي فيها مادة أرزاقهم، وهو الذي يدبِّر الأمور وتخضع له المخلوقاتُ العظام التي يُخاف منها وتزعِجُ العباد، وهو شديد القوة؛ فهو الذي يستحقُّ أن يُعْبَدَ وحده لا شريك له، ولهذا قال:
{13} "Na radi inamtakasa Mwenyezi Mungu kwa kumhimidi." Nayo ni ile sauti inayosikika kutoka katika mawingu yenye kuwasumbua waja. Nayo huwa imemnyenyekea Mola wake Mlezi, ikimtakasa kwa kumhimidi "na" wanamtakasa "Malaika pia kwa kumhofu." Yaani, wao huwa wamemnyenyekea Mola wao Mlezi, wakiwa wamehofu mshiko wake. "Naye hutuma mapigo ya radi" nao ni moto unaotoka katika mawingu, "na kumsibu kwayo amtakaye" katika waja wake kulingana na apendavyo na atakavyo. "Na Yeye ndiye Mwenye adhabu kali!" Yaani, Yeye ndiye mwenye uwezo mkubwa na nguvu. Na hataki chochote isipokuwa hukifanya, wala hakuna chochote kinachomuwia kigumu, wala hampotei mwenye kukimbia. Na ikiwa Yeye pekee ndiye anayewafikishia waja mvua na mawingu ambayo ndani yake kuna asili ya riziki yao, na Yeye ndiye anayeendesha mambo, na viumbe vikubwa vinavyoogopewa na vinavyowasumbua waja vinamnyenyekea. Naye ni mwenye nguvu kubwa, basi Yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa peke yake, bila mshirika yeyote, na ndiyo maana akasema:
: 14 #
{لَهُ دَعْوَةُ الْحَقِّ وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِنْ دُونِهِ لَا يَسْتَجِيبُونَ لَهُمْ بِشَيْءٍ إِلَّا كَبَاسِطِ كَفَّيْهِ إِلَى الْمَاءِ لِيَبْلُغَ فَاهُ وَمَا هُوَ بِبَالِغِهِ وَمَا دُعَاءُ الْكَافِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَالٍ (14)}
14. Wa kuombwa kweli ni Yeye tu. Na hao wanaowaomba badala yake hawawajibu chochote; bali ni kama mwenye kunyoosha viganja vyake kwenye maji ili yafike kinywani mwake, lakini hayakifikii. Na maombi ya makafiri hayako isipokuwa katika upotovu.
#
{14} أي: لله وحده {دعوةُ الحقِّ}: وهي عبادته وحده لا شريك له، وإخلاص دعاء العبادة ودعاء المسألة له تعالى؛ أي: هو الذي ينبغي أن يُصرف له الدعاء والخوف والرجاء والحبُّ والرغبة والرهبة والإنابة؛ لأنَّ ألوهيَّته هي الحقُّ، وألوهيَّة غيره باطلة. فَـ {الذينَ يدعونَ من دونه}: من الأوثان والأنداد التي جعلوها شركاء لله، {لا يستجيبون لهم}؛ أي: لمن يَدْعوها ويعبُدها بشيء قليل ولا كثير، لا من أمور الدُّنيا ولا من أمور الآخرة. {إلاَّ كباسط كفَّيه إلى الماء}: الذي لا تناله كفَّاه لبعدِهِ؛ {ليبلغَ}: ببسط كفَّيه إلى الماء {فاه}؛ فإنَّه عطشان، ومن شدَّة عطشه يتناول بيده ويبسطها إلى الماء الممتنع وصولها إليه؛ فلا يصلُ إليه؛ كذلك الكفار الذين يدعون معه آلهةً لا يستجيبون لهم بشيء ولا ينفعونهم في أشدِّ الأوقات إليهم حاجةً؛ لأنَّهم فقراء؛ كما أنَّ من دعوهم فقراء {لا يملكون مثقال ذرَّة في السموات ولا في الأرض وما لهم فيهما من شِرْك وما له منهم من ظهير}، {وما دعاءُ الكافرين إلاَّ في ضلال}: لبطلان ما يَدْعون من دون الله، فبطلت عبادتُهم ودعاؤُهم؛ لأنَّ الوسيلة تَبْطُلُ ببطلان غايتها، ولما كان اللهُ تعالى هو الملك الحق المبين؛ كانت عبادتُه حقًّا متَّصلة النفع بصاحبها في الدنيا والآخرة. وتشبيه دعاء الكافرين لغير الله بالذي يبسط كفَّيه إلى الماء ليبلغ فاه من أحسن الأمثلة؛ فإنَّ ذلك تشبيهٌ بأمرٍ مُحال؛ فكما أن هذا محالٌ؛ فالمشبَّه به محالٌ، والتعليق على المحال من أبلغ ما يكون في نفي الشيء؛ كما قال تعالى: {إنَّ الذين كذَّبوا بآياتنا واستكبروا عنها لا تُفَتَّحُ لهم أبوابُ السماء ولا يدخلونَ الجنَّةَ حتى يَلِجَ الجَمَلُ في سَمِّ الخِياط}.
{14} Yaani, Mwenyezi Mungu peke yake ndiye "Wa kuombwa kweli ni Yeye tu" bila mshirika yeyote, na kumfanyia yeye tu Mtukufu dua ya kuomba kitu na dua ya ibada. Basi Yeye tu ndiye anayestahiki kuombwa dua, na hofu, matumaini, upendo, utashi, hofu kubwa, na kurudi kwake kwa sababu uungu wake ni wa haki, na uungu wa wengine ni wa batili. Basi "hao wanaowaomba badala yake" miongoni mwa masanamu na wenza ambao wao waliwafanya kuwa washirika wa Mwenyezi Mungu "hawawajibu chochote." Yaani, hawawaitikii wale wanaowaomba na kuwaabudu kwa kitu kidogo wala kikubwa, si katika mambo ya dunia wala ya Akhera. "Kama mwenye kunyoosha viganja vyake kwenye maji" ambaye mikono yake haiwezi kuyafikia kwa sababu ya umbali wake "ili yafike" kwa kunyoosha viganja vyake kwenye maji hayo "kinywani mwake," kwa maana ana kiu, na kutokana na kiu yake kali, anauchukua mkono wake na kuunyoosha kwenye maji ambayo hauwezi kuyafikia, kwa hivyo hawezi kuyafikia. Basi vile vile makafiri ambao wanawaomba waungu pamoja naye hawawaitikii kwa lolote wala hawawanufaishi katika nyakati zao za haja kubwa. Kwa sababu wao ni mafuqara, kama vile walivyo mafuqara wale waliowaomba. "Hawamiliki hata uzito wa chembe katika mbingu wala katika ardhi. Wala hawana ushirika wowote humo. Wala Yeye hana msaidizi yeyote miongoni mwao." "Na maombi ya makafiri hayako isipokuwa katika upotovu." Kwa sababu wale wanaowaomba kando na Mwenyezi Mungu ni batili, basi ibada zao na maombi yao yakabatilika. Kwa sababu njia inakuwa batili pale lengo lake linapobatilika. Na kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mfalme wa haki aliye wazi, ikawa kumuabudu yeye ndiyo haki inayomfungamanishia manufaa mwenye kufanya hivyo katika duniani na akhera. Na kufananisha kumuomba makafiri asiyekuwa Mwenyezi Mungu na mtu ambaye ananyoosha viganja vyake kwenye maji ili yafike kinywani mwake ni miongoni mwa mifano mizuri zaidi. Kwa maana, hilo ni kufananisha na jambo lisilowezekana. Kwa kuwa kilichofananishwa nacho hakiwezekani. Na kufungamanisha kitu na kile kisichowezekana ni katika njia bora zaidi za kukataa kitu. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Hakika wale wanaozikufuru Ishara zetu na wakazifanyia kiburi, hawatafunguliwa milango ya mbingu, wala hawataingia Peponi mpaka apite ngamia katika tundu ya sindano."
: 15 #
{وَلِلَّهِ يَسْجُدُ مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَظِلَالُهُمْ بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ (15)}.
15. Na vinamsujudia Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na katika ardhi kwa kutii na kwa lazima. Na pia vivuli vyao asubuhi na jioni.
#
{15} أي: جميع ما احتوت عليه السماوات والأرض كلُّها خاضعةٌ لربِّها، تسجد له {طوعاً وكرهاً}: فالطَّوْع لمن يأتي بالسجود والخضوع اختياراً كالمؤمنين، والكَرْهُ لمن يستكبر عن عبادة ربِّه، وحالُه وفطرتُه تكذِّبه في ذلك. {وظلالُهم بالغُدُوِّ والآصال}؛ أي: ويسجد له ظلال المخلوقات أوَّلَ النهار وآخره، وسجودُ كلِّ شيء بحسب حاله؛ كما قال تعالى: {وإن مِن شيءٍ إلاَّ يسبِّحُ بحمدِهِ ولكن لا تفقهونَ تسبيحَهم}؛ فإذا كانت المخلوقات كلُّها تسجد لربِّها طوعاً وكرهاً؛ كان هو الإله حقًّا، المعبود المحمود حقًّا، وإلهيَّة غيره باطلة، ولهذا ذكر بطلانها وبرهن عليه بقوله:
{15} Yaani, vyote vilivyo katika mbingu na ardhi, vyote vimemtii Mola wao Mlezi, vinamsujudia "kwa kutii na kwa lazima." Basi kwa kutii huwa ni yule anayesujudu na kunyenyekea kwa hiari kama vile waumini, nako kwa lazima ni kwa yule anayetakabari kufanya kumuabudu Mola wake Mlezi, lakini hali yake na maumbile yake ya asili vinamkadhibisha katika hilo. "Na pia vivuli vyao asubuhi na jioni;" yaani, vivuli vya viumbe vinamsujudia Yeye mwanzo wa mchana na mwisho wake. Na kila kitu kinasujudu kulingana na hali yake, kama alivyosema Yeye Mtukufu "Na hakuna kitu isipokuwa kinamtakasa kwa sifa zake. Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake." Kwa hivyo ikiwa viumbe vyote vinamsujudia Mola wao Mlezi kwa kupenda na kwa kutopenda, basi anakuwa yeye ndiye Mungu wa kweli, mwenye kuabudiwa na kusifiwa wa kweli. Na uungu wa wengine ni batili,na ndiyo maana akataja ubatili wake na akawekea hilo ushahidi kwa kauli yake:
: 16 #
{قُلْ مَنْ رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ قُلِ اللَّهُ قُلْ أَفَاتَّخَذْتُمْ مِنْ دُونِهِ أَوْلِيَاءَ لَا يَمْلِكُونَ لِأَنْفُسِهِمْ نَفْعًا وَلَا ضَرًّا قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الْأَعْمَى وَالْبَصِيرُ أَمْ هَلْ تَسْتَوِي الظُّلُمَاتُ وَالنُّورُ أَمْ جَعَلُوا لِلَّهِ شُرَكَاءَ خَلَقُوا كَخَلْقِهِ فَتَشَابَهَ الْخَلْقُ عَلَيْهِمْ قُلِ اللَّهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ (16)}.
16. Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu na ardhi? Sema: Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, mnawafanya wenginewe badala yake kuwa ni walinzi, nao hawajimilikii manufaa yoyote wala madhara? Sema: Je, kipofu na mwenye kuona huwa sawa? Au je, huwa sawa giza na mwangaza? Au wamemfanyia Mwenyezi Mungu washirika walioumba kama alivyoumba Yeye, na viumbe hivyo vikawachanganyikia? Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja, Mwenye kushinda!
#
{16} أي: قل لهؤلاء المشركين به أوثاناً وأنداداً؛ يحبُّونها كما يحبُّون الله، ويبذُلون لها أنواع التقرُّبات والعبادات: أفتاهتْ عقولكم حتى اتَّخذتم من دونه أولياء تتولَّوْنهم بالعبادة وليسوا بأهل لذلك؛ فإنَّهم {لا يملِكون لأنفسهم نفعاً ولا ضَرًّا}، وتتركون ولاية من هو كامل الأسماء والصفات، المالك للأحياء والأموات، الذي بيده الخَلْق والتدبير والنفع والضُّرُّ؛ فما تستوي عبادة الله وحده وعبادة المشركين به، كما لا يستوي الأعمى والبصير، وكما لا {تستوي الظلماتُ والنور}: فإنْ كان عندهم شكٌّ واشتباهٌ وجعلوا له شركاء، زعموا أنَّهم خلقوا كخَلْقه، وفعلوا كفعله؛ فأزِلْ عنهم هذا الاشتباه واللَّبس بالبرهان الدالِّ على تَوَحُّدِ الإله بالوحدانيَّة، فقل لهم: اللهُ خالقُ كلِّ شيء؛ فإنه من المحال أن يَخْلُقَ شيءٌ من الأشياء نفسَه، ومن المحال أيضاً أن يوجدَ مِن دون خالقٍ، فتعيَّن أنَّ لها إلهاً خالقاً لا شريك له في خلقه؛ لأنَّه الواحدُ القهَّارُ؛ فإنَّه لا توجد الوحدة والقهر إلاَّ لله وحده؛ فالمخلوقات كلُّ مخلوق فوقه مخلوقٌ يقهره، ثم فوق ذلك القاهر قاهرٌ أعلى منه، حتى ينتهي القهر للواحد القهار؛ فالقهر والتوحيد متلازمان متعيِّنان لله وحده، فتبيَّن بالدليل العقليِّ القاهر أنَّ ما يُدعى من دون الله ليس له شيء من خَلْق المخلوقات، وبذلك كانت عبادته باطلة.
{16} Yaani, waambie hao wanaomshirikisha na masanamu na wenza. Wanaowapenda kama wanavyompenda Mwenyezi Mungu, na wanawatolea aina mbalimbali za sadaka na ibada: Je, zimepotea akili zenu mpaka mkajifanyia walinzi wengine badala yake, mkawa mnawafanya marafiki kwa kuwaabudu, ilhali wao hawastahiki hayo? Kwani wao "hawajimilikii manufaa yoyote wala madhara?" Na mnaacha kumfanyia urafiki Yule aliyekamilika katika majina na sifa, Mmiliki wa walio hai na wafu, ambaye mkononi mwake umo uumbaji na uendeshaji mambo, na kunufaisha na kudhuru. Basi haiwi sawa kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na kumuabudu kwa wale wanaomshirikisha, kama vile hawi sawa kipofu na mwenye kuona, na kama vile haiwi "sawa giza na mwangaza." Na kama wana shaka na wamechanganyikiwa na wakamfanyia washirika, na wakadai kwamba hao wameumbwa kama kuumba kwake, na wakafanya kama kufanya kwake, basi waondolee mfanano huu na kuchanganyikiwa huku kwa ushahidi unaoashiria upweke wa Mungu katika umoja. Basi waambie: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu, kwa maana haiwezekani kwa kitu chochote kujiumba chenyewe, na pia haiwezekani kuwepo bila ya Muumba, kwa hivyo ikabakia tu kwamba wana Mungu, Muumba ambaye hana mshirika yeyote katika uumbaji wake. Kwa sababu Yeye ndiye Mmoja, Mshindi. Kwa maana Umoja na ushindi havipatikani isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Kwa maana viumbe, kila kiumbe kina kiumbe kilicho juu yake ambacho kinakishinda. Kisha juu ya mshindi huyo kuna mshindi aliye juu zaidi yake, mpaka ushindi huu umalizikie kwa Aliye Mmoja, Mshindi. Kwa hivyo, ushindi na upweke vinaambatana, na ni vya Mwenyezi Mungu tu peke yake. Kwa hivyo ikabainika kwa ushahidi wa kiakili wenye ushindi kwamba chenye kuombwa kando na Mwenyezi Mungu hakina chochote katika uumbaji wa viumbe, kwa hivyo kuabudiwa kwake ni batili.
: 17 #
{أَنْزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَسَالَتْ أَوْدِيَةٌ بِقَدَرِهَا فَاحْتَمَلَ السَّيْلُ زَبَدًا رَابِيًا وَمِمَّا يُوقِدُونَ عَلَيْهِ فِي النَّارِ ابْتِغَاءَ حِلْيَةٍ أَوْ مَتَاعٍ زَبَدٌ مِثْلُهُ كَذَلِكَ يَضْرِبُ اللَّهُ الْحَقَّ وَالْبَاطِلَ فَأَمَّا الزَّبَدُ فَيَذْهَبُ جُفَاءً وَأَمَّا مَا يَنْفَعُ النَّاسَ فَيَمْكُثُ فِي الْأَرْضِ كَذَلِكَ يَضْرِبُ اللَّهُ الْأَمْثَالَ (17)}.
17. Ameteremsha maji kutoka mbinguni. Na mabonde yakamiminika maji kwa kiasi chake. Na mafuriko yakabeba mapovu yaliyokusanyika juu yake. Na kutokana na wanavyoyeyusha katika moto kwa kutaka mapambo au vyombo hutokea povu vile vile. Namna hivyo Mwenyezi Mungu ndivyo anavyopiga mifano ya haki na batili. Basi lile povu linapita kama takataka tu. Na ama kinachowafaa watu hubakia kwenye ardhi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyopiga mifano.
#
{17} شبَّه تعالى الهدى الذي أنزل على رسوله لحياة القلوب والأرواح بالماء الذي أنزله لحياة الأشباح. وشبَّه ما في الهدى من النفع العام الكثير الذي يضطرُّ إليه العباد بما في المطر من النفع العامِّ الضروريِّ. وشبَّه القلوب الحاملة للهدى وتفاوتها بالأودية التي تسيل فيها السيول؛ فَوَادٍ كبيرٌ يَسَعُ ماءً كثيراً كقلبٍ كبيرٍ يسعُ علماً كثيراً، ووادٍ صغيرٌ يأخذ ماءً قليلاً كقلبٍ صغيرٍ يسعُ علماً قليلاً ... وهكذا. وشبَّه ما يكون في القلوب من الشهوات والشُّبهات عند وصول الحقِّ إليها بالزَّبد الذي يعلو الماءَ ويعلو ما يوقَدُ عليه النار من الحلية التي يُراد تخليصُها وسبكها، وأنها لا تزال فوق الماء طافيةً مكدِّرةً له حتى تذهب وتضمحلَّ، ويبقى ما ينفع الناس من الماء الصافي والحلية الخالصة، كذلك الشبهاتُ والشَّهوات لا يزال القلب يكرهها ويجاهدها بالبراهين الصادقة والإرادات الجازمة حتى تذهب وتضمحلَّ ويبقى القلبُ خالصاً صافياً ليس فيه إلاَّ ما ينفعُ الناس من العلم بالحقِّ وإيثاره والرغبة فيه؛ فالباطل يذهبُ ويَمْحَقُهُ الحقُّ؛ {إنَّ الباطل كان زهوقاً}، وقال هنا: {كذلك يضرِبُ الله الأمثال}: ليتَّضح الحقُّ من الباطل والهدى من الضلال.
{17} Mwenyezi Mungu akaufananisha uwongofu ulioteremshwa kwa Mtume wake kwa ajili ya uzima wa nyoyo na nafsi na maji aliyoyateremsha kwa ajili ya uhai wa mizimu. Alifananisha manufaa makubwa ya umma katika mwongozo ambao watu wanalazimishwa kupata na manufaa ya umma katika mvua. Alizifananisha nyoyo zinazobeba mwongozo na utofauti wake na mabonde ambamo mito inapita ndani yake. Bonde kubwa linalohifadhi maji mengi ni sawa na moyo mkubwa ulio na maarifa mengi, na bonde dogo linaloshika maji kidogo ni sawa na moyo mdogo unaoshika maarifa kidogo... na kadhalika. Amefananisha matamanio na mashaka yaliyomo ndani ya nyoyo pale ukweli unapowafikia na povu litokalo juu ya maji na juu ya vito vinavyowashwa moto vinavyokusudiwa kutakaswa na kutupwa, na kwamba vinabaki juu ya maji yanayoelea na kuyasumbua mpaka yanatoweka na kutoweka, na kilichobakia ni manufaa kwa watu wa maji safi na vito safi. Kadhalika, mashaka na matamanio, moyo huendelea kuwachukia na kujitahidi dhidi yao kwa hoja za kweli na madhubuti, mpaka yatoweke na kutoweka, na moyo ukabaki kuwa msafi na safi, usiokuwa na chochote ndani yake isipokuwa yale yanayowanufaisha watu kutokana na elimu ya haki, kuipendelea, na kuitamani. Uongo hutoweka na kuharibiwa na ukweli. "Hakika uongo umetoweka, na akasema hapa: "Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyopiga mifano" ili ukweli ubainike na uongo na uwongofu na upotofu.
: 18 #
{لِلَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِرَبِّهِمُ الْحُسْنَى وَالَّذِينَ لَمْ يَسْتَجِيبُوا لَهُ لَوْ أَنَّ لَهُمْ مَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا وَمِثْلَهُ مَعَهُ لَافْتَدَوْا بِهِ أُولَئِكَ لَهُمْ سُوءُ الْحِسَابِ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ وَبِئْسَ الْمِهَادُ (18)}.
18. Wale waliomuitikia Mola wao Mlezi watapata mazuri. Na wale ambao hawakumuitikia, hata wangelikuwa na vyote vilivyomo katika ardhi na mfano wa hivyo, bila ya shaka wangelivitoa kujikombolea! Hao wana hesabu mbaya kabisa, na makao yao ni Jahannamu. Na hapo ni pahali pabaya mno pa kupumzikia!
#
{18} لما بيَّن تعالى الحقَّ من الباطل؛ ذَكَرَ أنَّ الناس على قسمين: مستجيب لربِّه فذكر ثوابه، وغير مستجيب فذكر عقابه، فقال: {للذين استجابوا لربِّهم}؛ أي: انقادت قلوبُهم للعلم والإيمان، وجوارحُهم للأمر والنهي، وصاروا موافقين لربِّهم فيما يريده منهم؛ فلهم {الحسنى}؛ أي: الحالة الحسنة والثواب الحسن؛ فلهم من الصفات أجلُّها، ومن المناقب أفضلُها، ومن الثواب العاجل والآجل ما لا عينٌ رأت ولا أذنٌ سمعت ولا خطر على قلب بشر. {والذين لم يستجيبوا له}: بعدما ضَرَبَ لهم الأمثال وبيَّن لهم الحقَّ لهم الحالةُ غير الحسنة. فَـ {لو أنَّ لهم ما في الأرض جميعاً}: من ذهب وفضةٍ وغيرهما، {ومثلَه معه لافتَدَوْا به}: من عذاب يوم القيامة؛ ما تُقُبِّلَ منهم. وأنَّى لهم ذلك؟! {أولئك لهم سوء الحساب}: وهو الحساب الذي يأتي على كلِّ ما أسلفوه من عمل سيئ وما ضيعوه من حقوق الله وحقوق عباده، قد كُتِبَ ذلك وسُطِرَ عليهم: {وقالوا يا وَيْلَتَنا مالِ هذا الكتابِ لا يغادِرُ صغيرةً ولا كبيرةً إلا أحصاها ووَجَدوا ما عملوا حاضراً ولا يظلمُ ربُّك أحداً}. {و} بعد هذا الحساب السيئ، {مأواهم جهنَّم}: الجامعة لكلِّ عذابٍ من الجوع الشديد والعطش الوجيع والنار الحامية والزقُّوم والزمهرير والضَّريع، وجميع ما ذكره الله من أصناف العذاب. {وبئس المهادُ}؛ أي: المَقَرُّ والمسكن مسكنهم.
{18} Yeye Mtukufu alipobainisha haki kutokana na batili, akataja kuwa watu wamegawanyika makundi mawili: wale wanaomwitikia Mola wao Mlezi, basi akataja malipo ya hilo, na wale wasioitikia, basi akataja adhabu ya hilo pia, akasema: "Wale waliomuitikia Mola wao Mlezi." Yaani, wale ambao nyoyo zao zilifuata elimu na imani, na viungo vyao vikafuata amri na makatazo, na wakawa wameafikiana na Mola wao Mlezi katika yale anayoyataka kutoka kwao, basi hao wana "mazuri." Yaani, hali nzuri na malipo mazuri. Kwa hivyo wana sifa bora zaidi, matendo bora zaidi, na thawabu za haraka na za baadaye ambazo hakuna jicho limewahi kuziona, wala hakuna sikio lililowahi kusikia, wala hayakuwahi kupitia katika moyo wa mwanadamu yeyote. "Na wale ambao hawakumuitikia" baada ya kuwapigia mifano na kuwabainishia haki, wana hali isiyokuwa nzuri. Basi "lau wangelikuwa na vyote vilivyomo katika ardhi na mfano wa hivyo" vya dhahabu, fedha na vitu vingine, "bila ya shaka wangelivitoa kujikombolea!" Kutokana na adhabu ya Siku ya Kiyama, lakini havingekubaliwa kutoka kwao. Na hata wangewezaje kufanya hivyo? "Hao wana hesabu mbaya kabisa" ambayo ni hesabu itayajia mabaya waliyoyatanguliza na yale waliyoyapoteza katika haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake. Hayo yalikwisha andikwa juu yao. "Na watasema: Ole wetu! Kitabu hiki kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa isipokuwa hulidhibiti? Na watayakuta yote waliyoyatenda yamehudhuria hapo. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote." "Na" baada ya hesabu hii mbaya, "makao yao ni Jahannamu" ambayo imekusanya kila adhabu kama vile njaa kali, kiu kikali, Moto wenye mwako mkali, Zaqqum, Zamharir, na adh-Dhwarii', na yote ambayo Mwenyezi Mungu alitaja miongoni mwa aina mbalimbali za adhabu. "Na hapo ni pahali pabaya mno pa kupumzikia."
: 19 - 24 #
{أَفَمَنْ يَعْلَمُ أَنَّمَا أُنْزِلَ إِلَيْكَ مِنْ رَبِّكَ الْحَقُّ كَمَنْ هُوَ أَعْمَى إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ (19) الَّذِينَ يُوفُونَ بِعَهْدِ اللَّهِ وَلَا يَنْقُضُونَ الْمِيثَاقَ (20) وَالَّذِينَ يَصِلُونَ مَا أَمَرَ اللَّهُ بِهِ أَنْ يُوصَلَ وَيَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ وَيَخَافُونَ سُوءَ الْحِسَابِ (21) وَالَّذِينَ صَبَرُوا ابْتِغَاءَ وَجْهِ رَبِّهِمْ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنْفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً وَيَدْرَءُونَ بِالْحَسَنَةِ السَّيِّئَةَ أُولَئِكَ لَهُمْ عُقْبَى الدَّارِ (22) جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا وَمَنْ صَلَحَ مِنْ آبَائِهِمْ وَأَزْوَاجِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ وَالْمَلَائِكَةُ يَدْخُلُونَ عَلَيْهِمْ مِنْ كُلِّ بَابٍ (23) سَلَامٌ عَلَيْكُمْ بِمَا صَبَرْتُمْ فَنِعْمَ عُقْبَى الدَّارِ (24)}.
19. Je, anayejua ya kwamba yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki ni sawa na aliye kipofu? Hakika wenye akili tu ndio wanaokumbuka. 20. Wale ambao wanatimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu, wala hawavunji agano. 21. Na wale ambao huyaunga yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanamhofu Mola wao Mlezi, na wanaiogopa hesabu mbaya. 22. Na ambao husubiri kwa kuutaka uso wa Mola wao Mlezi, na wakasimamisha Swala, na wakatoa, kwa siri na kwa uwazi, katika vile tulivyowapa; na wakayaondoa mabaya kwa mazuri. Hao ndio wana malipo ya Nyumba ya Akhera. 23. Nayo ni Bustani za milele, wataziingia wao na wale waliotengenea miongoni mwa baba zao, na wake zao, na vizazi vyao. Na Malaika watawaingilia katika kila mlango. 24. (Wakiwaambia) Assalamu Alaikum (Amani iwe juu yenu), kwa sababu ya vile mlivyosubiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera.
#
{19 - 20} يقول تعالى: مفرقاً بين أهل العلم والعمل وبين ضدِّهم: {أفَمَن يعلمُ أنَّما أنزِلَ إليك من ربِّك الحقُّ}: ففهم ذلك وعمل به. {كَمَنْ هو أعمى}: لا يعلم الحقَّ ولا يعمل به؛ فبينهما من الفرق كما بين السماء والأرض؛ فحقيقٌ بالعبد أن يتذكَّر ويتفكَّر، أيُّ الفريقين أحسن حالاً وخير مآلاً، فيؤثر طريقها، ويسلك خلف فريقها، ولكن ما كلُّ أحدٍ يتذكَّر ما ينفعه ويضره. {إنَّما يتذكَّر أولو الألباب}؛ أي: أولو العقول الرزينة والآراء الكاملة، الذين هم لبُّ العالم وصفوةُ بني آدم. فإن سألتَ عن وصفِهم؛ فلا تجدُ أحسن من وصف الله لهم بقوله: {الذين يُوفونَ بعهدِ اللهِ}: الذي عَهِدَهُ إليهم والذي عاهدهم عليه من القيام بحقوقه كاملة موفرة؛ فالوفاء بها توفيتها حقَّها من التتميم لها والنصح فيها، ومن تمام الوفاء بها أنَّهم {لا ينقُضون الميثاقَ}؛ أي: العهد الذي عاهدوا الله عليه، فدخل في ذلك جميع المواثيق والعهود والأيمان والنُّذور التي يعقِدُها العباد، فلا يكون العبد من أولي الألباب الذين لهم الثواب العظيم إلا بأدائها كاملةً وعدم نقضها وبخسها.
{19 - 20} Yeye Mtukufu Anasema akipambanua baina ya watu wa elimu na vitendo na kinyume chao: "Anayejua ya kwamba yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki." Basi akalifahamu hilo na akalifanyia kazi, "ni sawa na aliye kipofu?" Ambaye hajui haki wala haitendei kazi? Kuna tofauti kubwa kati yao kama ilivyo kati ya mbingu na ardhi. Basi mja anafaa zaidi kukumbuka na kutafakari ni lipi kati ya makundi mawili hayo ndiyo yenye hali nzuri zaidi na maishio bora zaidi, kwa hivyo akapendelea njia yake na akafuata nyuma ya kikundi chake, lakini sio kila mtu anakumbuka kile chenye kumnufaisha na kinachomdhuru. "Hakika wenye akili tu ndio wanaokumbuka;" yaani, wenye akili timamu na maoni kamili, ambao ndio kiini cha ulimwengu na walio bora zaidi katika wanadamu. Na ukiuliza kuhusu maelezo yao, basi hutapata bora zaidi kuliko maelezo aliyotoa Mwenyezi Mungu juu yao aliposema: "Wale ambao wanatimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu" ambayo aliwakabidhi na akaahidiana nao kama vile kutekeleza haki zake kwa ukamilifu na kwa wingi. Kwa hivyo, kuzitimiza ni kutimizia haki zake ya kuzitimiza na kuwa na ikhlasi ndani yake. Na katika utimilifu wa kuzitekeleza ni kwamba “hawavunji agano." Yaani, agano ambalo walifunga na Mwenyezi Mungu juu yake, kwa hivyo yanaingia humo maagano yote, ahadi, viapo, na nadhiri ambazo waja wanazifunga, kwa hivyo mja hawezi kuwa miongoni mwa watu wenye akili ambao wana malipo makubwa isipokuwa kwa kuyatekeleza kwa ukamilifu na siyo kuzivunja au kuzipunja.
#
{21} {والذين يصِلونَ ما أمرَ اللهُ به أن يوصَلَ}: وهذا عامٌّ في كلِّ ما أمر الله بوصله من الإيمان به وبرسوله ومحبَّته ومحبَّة رسوله والانقياد لعبادته وحده لا شريك له ولطاعة رسوله، ويصلون آباءهم وأمهاتهم ببرِّهم بالقول والفعل وعدم عقوقهم، ويصلون الأقارب والأرحام بالإحسان إليهم قولاً وفعلاً، ويصلون ما بينَهم وبين الأزواج والأصحاب والمماليك بأداء حقِّهم كاملاً موفَّراً من الحقوق الدينيَّة والدنيويَّة. والسبب الذي يجعل العبد واصلاً ما أمر الله به أن يوصَلَ خشيةُ الله وخوفُ يوم الحساب، ولهذا قال: {ويَخْشَوْنَ ربَّهم}؛ أي: يخافونه، فيمنعهم خوفُهم منه ومن القدوم عليه يوم الحساب أن يتجرَّؤوا على معاصي الله أو يقصروا في شيء ممَّا أمر الله به؛ خوفاً من العقاب ورجاءً للثواب.
{21} "Na wale ambao huyaunga yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu yaungwe." Na hili ni jambo la jumla katika kila aliloamrisha Mwenyezi Mungu liungwe, kama vile kumuamini Yeye na Mtume wake, kumpenda Yeye, kumpenda Mtume wake, kunyenyekea, kumuabudu Yeye peke yake bila mshirika, na kumtii Mtume wake, na kuwaunga baba zao na mama zao kwa kuwafanyia wema kwa kauli na vitendo na kutowaasi, na kuwaunga jamaa wa karibu na watu wa ukoo kwa kuwafanyia ihsani kwa kauli na vitendo, na wanaunga mafungamano yaliyopo baina yao na bibi na bwana zao, marafiki zao, na wale waliowamiliki, kwa kutekeleza haki zao kikamilifu, miongoni mwa haki za kidini na za kidunia. Na sababu inayomfanya mja kuunga yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu kwamba yaungwe ni kumhofu Mwenyezi Mungu na kuiogopa Siku ya Kiyama, na ndiyo maana akasema: "Na wanamhofu Mola wao Mlezi." Yaani, wanamuogopa, kwa hivyo kumhofu huko na jambo la kumjia Siku ya hesabu vinawazuia kuthubutu kumuasi Mwenyezi Mungu au kutotekeleza kikamilifu katika yale ambayo Mwenyezi Mungu aliamrisha, wanahofu adhabu na wanatumaini malipo.
#
{22} {والذين صبروا}: على المأمورات بالامتثال، وعن المنهيَّات بالانكفاف عنها والبعد منها، وعلى أقدار الله المؤلمة بعدم تسخُّطها، ولكن بشرط أن يكون ذلك الصبر {ابتغاءَ وجهِ ربِّهم}: لا لغير ذلك من المقاصد والأغراض الفاسدة؛ فإنَّ هذا الصبر النافع، الذي يَحْبِسُ به العبد نفسه طلباً لمرضاة ربِّه ورجاءً للقرب منه والحظوة بثوابه، وهو الصبر الذي من خصائص أهل الإيمان، وأما الصبر المشترك الذي غايتُهُ التجلُّد ومنتهاه الفخر؛ فهذا يصدُرُ من البَرِّ والفاجر والمؤمن والكافر؛ فليس هو الممدوح على الحقيقة. {وأقاموا الصَّلاة}: بأركانها وشروطها ومكمِّلاتها ظاهراً وباطناً. {وأنفقوا مما رزقْناهم سرًّا وعلانية}: دخل في ذلك النفقات الواجبة كالزكوات والكفارات والنفقات المستحبَّة، وأنهم ينفقون حيث دعت الحاجةُ إلى النفقة سرًّا وعلانيةً. {ويدرؤونَ بالحسنةِ السيئةَ}؛ أي: مَن أساء إليهم بقول أو فعل؛ لم يقابلوه بفعله، بل قابلوه بالإحسان إليه، فيعطون من حَرَمَهم، ويعفون عمَّن ظَلَمهم، ويصِلون من قَطَعهم، ويحسِنون إلى مَن أساء إليهم، وإذا كانوا يقابلون المسيء بالإحسان؛ فما ظنُّك بغير المسيء. {أولئك}: الذين وُصِفَتْ صفاتهم الجليلة ومناقبهم الجميلة؛ {لهم عُقبى الدار}.
{22} "Na ambao husubiri" juu ya maamrisho kwa kuyatekeleza. Na kujizuia na makatazo na kuwa mbali nayo. Na kusubiri juu ya majaliwa machungu ya Mwenyezi Mungu kwa kutokasirika kwa sababu yake, lakini kwa sharti kwamba subira hiyo iwe "kuutaka uso wa Mola wao Mlezi" si kwa ajili ya mengineyo miongoni mwa malengo mabovu. Kwa maana hii ndiyo subira yenye manufaa, ambayo mja hujizuia nafsi yake kwayo akitafuta radhi za Mola wake Mlezi na kwa kutaraji kuwa karibu Naye na kupata malipo yake; nayo ni subira ambayo ni miongoni mwa sifa za watu wa imani. Na ama subira ambayo lengo lake ni uvumilivu na mwisho wake ni kiburi, basi hilo linatoka kwa watu wema na waovu, Muumini na kafiri, na subira hiyo siyo yenye kusifiwa kwa uhakika. "Na wakasimamisha Swala" pamoja na nguzo zake, masharti yake, na vikamilishi vyake, kwa nje na ndani. "Na wakatoa, kwa siri na kwa uwazi, katika vile tulivyowapa" Na kunaingia katika hili kutoa matumizi kwa wajibu kama vile zaka, kafara na kutoa matumizi yaliyopendekezwa, na wanatoa kwa siri na hadhara popote panapohitajika. "Na wakayaondoa mabaya kwa mazuri;" yaani, mwenye kuwafanyia ubaya kwa maneno au kwa kitendo, wao hawakabiliani naye kwa kitendo chake, bali wanakabiliana naye kwa kumfanyia wema, kwa hivyo wanampa mwenye kuwanyima, na wanamsamehe aliyewadhulumu, na wanamuunga aliyewakata, na wanatendea mazuri aliyewafanyia mabaya. Kwa hivyo, ikiwa wanamkabili anayewafanyia mabaya kwa wema, basi unafikiri wanamkabili vipi yule ambaye hakuwafanyia mabaya? "Hao" ambao wameelezwa kwa sifa hizi tukufu na matendo haya mazuri, "wana malipo ya Nyumba ya Akhera."
#
{23 - 24} فسَّرها بقوله: {جناتُ عدنٍ}؛ أي: إقامةٍ لا يزولون عنها ولا يبغون عنها حِوَلاً؛ لأنَّهم لا يرون فوقها غايةً؛ لما اشتملت عليه من النعيم والسرور، الذي تنتهي إليه المطالب والغايات، ومن تمام نعيمهم وقرَّة أعينهم أنَّهم {يدخُلونها وَمَن صَلَحَ من آبائهم وأزواجهم وذرِّيَّاتهم}: من الذكور والإناث وأزواجهم؛ أي: الزوج أو الزوجة، وكذلك النظراء والأشباه والأصحاب والأحباب؛ فإنَّهم من أزواجهم وذُرِّيَّاتهم. {والملائكةُ يدخُلون عليهم من كلِّ بابٍ}: يهنونهم بالسلامة وكرامة الله لهم، ويقولون: {سلامٌ عليكم}؛ أي: حلَّت عليكم السلامة والتحيَّة من الله وحَصَلَت لكم، وذلك متضمِّنٌ لزوال كلِّ مكروه ومستلزمٌ لحصول كل محبوب {بما صبرتُم}؛ أي: صبركم هو الذي أوصلكم إلى هذه المنازل العالية والجنان الغالية. {فنعم عُقبى الدار}: فحقيقٌ بمن نصح نفسه، وكان لها عنده قيمة أن يجاهِدَها لعلَّها تأخُذُ من أوصاف أولي الألباب بنصيب، ولعلها تحظى بهذه الدار التي هي مُنْيَةُ النفوسِ وسرورُ الأرواحِ الجامعة لجميع اللَّذَّات والأفراح؛ فلمِثْلها فليعمل العاملون، وفيها فليتنافس المتنافسون.
{23 - 24} Akayafafanua malipo hayo kwa kauli yake: "Bustani za milele;" yaani, mabusatani ya kudumu ambayo hawatatoka humo, wala hawatatafuta kwenda kwingine, kwa maana hawaoni lengo lolote zaidi yake; kwa sababu ya neema iliyomo humo na furaha, ambayo kwayo mahitaji na malengo yanaisha. Na katika ukamilifu wa neema yake na furaha ya macho yao ni kwamba "wataziingia wao na wale waliotengenea miongoni mwa baba zao, na wake zao, na vizazi vyao." Wanaume, wanawake, na wake na wanaume zao, na vile vile wale ambao wako katika hali sawa na wao, marafiki, na wapendwa. Kwa sababu hawa pia ni katika waume au wake za na dhuria zao. "Na Malaika watawaingilia katika kila mlango" watawapongeza kwa usalama wao na utukufu wa Mwenyezi Mungu juu yao, na watasema: "Assalamu Alaikum (Amani iwe juu yenu)." Yaani, salamu na maamkizi yawe juu yenu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na hilo linajumuisha kutoweka kwa kila machukizo na linalazimu kupatikana kwa kila kipendwacho "kwa sababu ya vile mlivyosubiri!" Yaani, subira yenu ndiyo iliyowafikisha pahali hapa pa juu na mabustani ya thamani kubwa. "Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera." Kwa hivyo, anafaa zaidi yule ambaye amejinasihi nafsi yake, nayo ikawa ina thamani kwake kupigana nayo ili huenda ikapata fungu katika sifa za watu wenye akili, na pengine ikapata nyumba hii ambayo ni matamanio ya nafsi na furaha ya roho ambayo inakusanya raha zote na furaha zote. Basi kwa mfano wake na wafanye wafanyaji, na katika hayo na washindane washindani.
: 25 #
{وَالَّذِينَ يَنْقُضُونَ عَهْدَ اللَّهِ مِنْ بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّهُ بِهِ أَنْ يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ أُولَئِكَ لَهُمُ اللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوءُ الدَّارِ (25)}.
25. Na wale wanaovunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kuzifunga, na wanakata yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanafanya uharibifu katika ardhi, hao wana laana, na wana Nyumba mbaya.
#
{25} لما ذكر حال أهل الجنة؛ ذكر أنَّ أهل النار بعكس ما وصفهم به، فقال عنهم: {والذين ينقُضون عهد الله من بعد ميثاقِهِ}؛ أي: من بعدما أكَّده عليهم على أيدي رسله وغلَّظ عليهم، فلم يقابلوه بالانقياد والتسليم، بل قابلوه بالإعراض والنقض. {ويقطَعون ما أمر الله به أن يوصَلَ}: فلم يَصِلوا ما بينهم وبين ربِّهم بالإيمان والعمل الصالح، ولا وصلوا الأرحام، ولا أدَّوا الحقوق، بل أفسدوا في الأرض بالكفر والمعاصي والصدِّ عن سبيل الله وابتغائها عوجاً. {أولئك لهم اللعنةُ}؛ أي: البعد والذمُّ من الله وملائكته وعباده المؤمنين. {ولهم سوء الدار}: وهي الجحيم بما فيها من العذاب الأليم.
{25} Alipotaja hali ya watu wa Peponi, akataja kuwa watu wa Motoni ni kinyume cha yale aliyowaeleza nayo watu wa Peponi. Kwa hivyo akasema juu yao, "Na wale wanaovunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kuzifunga." Yaani, baada ya kuwasisitizia ahadi hizo juu ya mikono ya Mitume wake na akazifanya kuwa kali zaidi, lakini wao hawakumkabili kwa kufuata na kujisalimisha; bali walimkabili kwa kumpa mgongo na kuvunja ahadi. "Na wanakata yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu yaungwe" kwa hivyo hawakuunga yale yaliyo baina yao na Mola wao Mlezi kwa Imani na vitendo vyema, wala hawakuwaunga jamaa, wala hawakutimiza haki, bali walieneza uharibifu katika ardhi kwa ukafiri na maasia na kuzuia njia ya Mwenyezi Mungu na kutaka kuipotosha. "Hao wana laana;" yaani, kuwekwa mbali na kushutumiwa na Mwenyezi Mungu, Malaika wake na waja wake waumini. "Na wana Nyumba mbaya" ambayo ni Jahiim pamoja na yaliyomo miongoni mwa adhabu chungu.
: 26 #
{اللَّهُ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَنْ يَشَاءُ وَيَقْدِرُ وَفَرِحُوا بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا مَتَاعٌ (26)}.
26. Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye, na humkunjia kwa kipimo. Na waliufurahia uhai wa dunia. Na uhai wa dunia kwa kulinganisha na Akhera si kitu isipokuwa ni starehe ndogo.
#
{26} أي: هو وحده يوسِّع الرزق ويبسُطُه على من يشاء ويَقْدِره ويضيِّقه على مَن يشاء. {وفرحوا}؛ أي: الكفار {بالحياة الدنيا}: فرحاً أوجب لهم أن يطمئنُّوا بها ويغفلوا عن الآخرة، وذلك لنقصان عقولهم. {وما الحياة الدُّنيا في الآخرة إلاَّ متاعٌ}؛ أي: شيء حقيرٌ يُتَمَتَّع به قليلاً ويفارق أهله وأصحابه ويُعْقِبُهم وَيلاً طويلاً.
{26} Yaani Yeye pekee ndiye humpanulia na kumkunjulia riziki amtakaye, na kuikunja na kuifanya kuwa finyu kwa amtakaye. "Na waliufurahia;" yaani, makafiri "uhai wa dunia" furaha iliyowasababishia kutulia nao na kuisahau akhera, kwa sababu ya upungufu wa akili zao. "Na uhai wa dunia kwa kulinganisha na Akhera si kitu isipokuwa ni starehe ndogo." Yaani, ni kitu duni cha kujistarehesha kwacho kidogo, kisha kinamuacha mwenyewe na baadaye kinafuatwa na taabu ndefu.
: 27 - 29 #
{وَيَقُولُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْلَا أُنْزِلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِنْ رَبِّهِ قُلْ إِنَّ اللَّهَ يُضِلُّ مَنْ يَشَاءُ وَيَهْدِي إِلَيْهِ مَنْ أَنَابَ (27) الَّذِينَ آمَنُوا وَتَطْمَئِنُّ قُلُوبُهُمْ بِذِكْرِ اللَّهِ أَلَا بِذِكْرِ اللَّهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ (28) الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ طُوبَى لَهُمْ وَحُسْنُ مَآبٍ (29)}.
27. Na wanasema wale waliokufuru: Kwa nini hakuteremshiwa ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema: Hakika Mwenyezi Mungu humpoteza amtakaye, na humwongoa anayerudi kwake. 28. Wale walioamini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Sikilizeni! Kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndiyo nyoyo hutua! 29. Wale walioamini na wakatenda mema watakuwa na raha na marejeo mazuri.
#
{27} يخبر تعالى أنَّ الذين كفروا بآيات الله يتعنَّتون على رسول الله ويقترحون ويقولون: {لولا أنزِلَ عليه آيةٌ من ربِّه}: وبزعمهم أنها لو جاءت لآمنوا، فأجابهم الله بقوله: {قل إنَّ الله يُضِلُّ مَن يشاء ويهدي إليه من أنابَ}؛ أي: طلب رضوانه، فليست الهداية والضلال بأيديهم حتى يجعلوا ذلك متوقِّفاً على الآيات، ومع ذلك؛ فهم كاذبون فـ {لو أننا نزَّلنا إليهم الملائكة وكلَّمهم الموتى وحَشَرْنا عليهم كلَّ شيءٍ قُبُلاً ما كانوا لِيُؤمنوا إلاَّ أنْ يشاء الله ولكنَّ أكثرهم يجهلونَ}. ولا يلزمُ أن يأتي الرسولُ بالآية التي يعيِّنونها ويقترحونها، بل إذا جاءهم بآيةٍ تبيِّنُ ما جاء به من الحقِّ؛ كفى ذلك وحصل المقصودُ وكان أنفع لهم من طلبهم الآيات التي يعيِّنونها؛ فإنَّها لو جاءتهم طِبْقَ ما اقترحوا، فلم يؤمنوا بها؛ لعاجلهم العذاب.
{27} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba wale waliokufuru ishara za Mwenyezi Mungu ni wanamfanyia ukaidi Mtume wa Mwenyezi Mungu, na wanapendekeza wakisema, "Kwa nini hakuteremshiwa ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi?" Na kwa wanadai kuwa lau kuwa zingewajia, basi wangeamini, lakini Mwenyezi Mungu akawajibu kwa kauli yake, "Sema: Hakika Mwenyezi Mungu humpoteza amtakaye, na humwongoa anayerudi kwake." Yaani, mwenye kutafuta radhi zake kwa maana, uwongofu na upotofu haumo mikononi mwao mpaka wayafanye hayo kutegemea ishara mbalimbali. Na pamoja na hayo, wao ni waongo, kwani "lau kuwa tungeliwateremshia Malaika, na maiti wakazungumza nao, na tukawakusanyia kila kitu mbele yao, bado wasingeliamini, isipokuwa Mwenyezi Mungu atake. Lakini wengi wao wanafanya tu ujinga." Na si lazima kwa Mtume kuja na ishara ambazo wanazitaka wao na kuzipendekeza, bali akiwajia na Ishara inayobainisha yale aliyokuja nayo ya haki, hilo linatosha, na kusudi likapatikana, na linakuwa la kuwafaa zaidi kuliko kuuliza kwao ishara wanazozitaka wao. Kwa maana, lau kuwa zingewajia kulingana na walivyopendekeza, kisha wasiziamini, basi angewaharakishia adhabu.
#
{28} ثم ذكر تعالى علامة المؤمنين، فقال: {الذين آمنوا وتطمئنُّ قلوبُهم بذكر الله}؛ أي: يزول قلقها واضطرابها، وتحضُرُها أفراحها ولذَّاتها. {ألا بذكرِ الله تطمئنُّ القلوب}؛ أي: حقيق بها وحريٌّ أن لا تطمئنَّ لشيءٍ سوى ذكره؛ فإنَّه لا شيء ألذُّ للقلوب ولا أشهى ولا أحلى من محبة خالقها والأنس به ومعرفته، وعلى قَدْرِ معرفتها بالله ومحبَّتها له يكون ذِكْرُها له، هذا على القول بأنَّ ذكرَ الله ذِكْرُ العبد لربِّه من تسبيح وتهليل وتكبير وغير ذلك، وقيل: إن المراد بذِكْر الله كتابُه الذي أنزله ذكرى للمؤمنين؛ فعلى هذا معنى طمأنينة القلب بذكر الله أنها حين تَعْرِفُ معاني القرآن وأحكامه تطمئنُّ لها؛ فإنَّها تدل على الحقِّ المبين المؤيَّد بالأدلة والبراهين، وبذلك تطمئنُّ القلوب؛ فإنَّها لا تطمئنُّ إلا باليقين والعلم، وذلك في كتاب الله مضمونٌ على أتمِّ الوجوه وأكملها، وأما ما سواه من الكتب التي لا ترجِعُ إليه؛ فلا تطمئنُّ بها، بل لا تزال قلقةً من تعارض الأدلَّة وتضادِّ الأحكام، {ولو كان من عندِ غيرِ الله لَوَجَدوا فيه اختلافاً كثيراً}، وهذا إنما يعرفه من خَبَرَ كتابَ الله، وتدبَّره، وتدبَّر غيره من أنواع العلوم؛ فإنَّه يجد بينها وبينه فرقاً عظيماً.
{28} Kisha Yeye Mtukufu akataja alama za Waumini, akasema: "Wale walioamini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu;" yaani, unaondoka wasiwasi wake na msukosuko wake, na hujiwa na furaha zake na raha zake. "Sikilizeni! Kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua!" Yaani, zinastahiki na zinafaa zaidi kutotulia kwa chochote kisichokuwa kumkumbuka. Kwani hakuna kitu kitamu zaidi mioyoni, wala cha kutamaniwa zaidi, wala kitamu zaidi kuliko kumpenda Muumba wake, kutulia kwa sababu yake, na kumjua Yeye, na kulingana na kiasi cha kumjua kwake, na kumpenda kwake, ndiyo kunakuwa kumkumbuka Yeye. Haya ni kama itasemwa kwamba kumkumbuka Mwenyezi Mungu ni mja kumkumbuka Mola wake Mlezi kwa kumtakasa, na kusema hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kutoa takbira na mambo mengine. Na imesemwa kuwa kinachokusudiwa na kumkumbuka Mwenyezi Mungu ni Kitabu chake alichokiteremsha kiwe ukumbusho kwa Waumini. Kwa hivyo, kwa mujibu wa maana unakuwa utulivu wa moyo kwa kujua maana za Qur’an na hukumu zake, na kutulia kwa sababu ya hayo. Kwa maana hizo zinaonyesha haki iliyo wazi inayoungwa mkono na ushahidi na hoja, na kwa hayo mioyo hutulia. Kwani haitulii isipokuwa kwa yakini na elimu, na hilo limehakikishwa ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa njia iliyo timilifu na kamili zaidi. Na ama vitabu vinginevyo ambavyo havikirejelei, hivyo mioyo havitulii kwa sababu yake; bali haiachi kuwa na wasiwasi kwa sababu ya kupingana kwa ushahidi na kugongana kwa hukumu. "Na lau kuwa ingekuwa inatoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, basi bila ya shaka wangelikuta ndani yake hitilafu nyingi." Na haya yanajulikana kutoka katika habari za Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na kukitafakari, na kutafakari aina nyinginezo za elimu, kwani atapata tofauti kubwa kati yake na hizo.
#
{29} ثم قال تعالى: {الذين آمنوا وعملوا الصالحات}؛ أي: آمنوا بقلوبهم بالله وملائكته وكتبه ورسله واليوم الآخر، وصدَّقوا هذا الإيمان بالأعمال الصالحة؛ أعمال القلوب كمحبة الله وخشيته ورجائه، وأعمال الجوارح كالصلاة ونحوها. {طوبى لهم وحسنُ مآب}؛ أي: لهم حالةٌ طيبةٌ ومرجع حسنٌ، وذلك بما ينالون من رضوان الله وكرامته في الدنيا والآخرة، وإنَّ لهم كمال الراحة وتمام الطمأنينة، ومن جملة ذلك شجرةُ طوبى التي في الجنة، التي يسير الراكب في ظلِّها مائة عام ما يقطعُها؛ كما وردت بها الأحاديث الصحيحة.
{29} Kisha akasema yeye Mtukufu, "Wale walioamini na wakatenda mema." Yaani, walimuamini Mwenyezi Mungu kwa nyoyo zao, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, na wakaisadikisha imani hiyo kwa matendo mema. Matendo ya mioyo, kama vile upendo, hofu, na kumtumaini Mwenyezi Mungu. Na matendo ya viungo, kama vile swala na mfano wake. "Watakuwa na raha na marejeo mazuri;" yaani, wana hali nzuri na marejeo mazuri, na hayo ni kwa sababu watapata radhi ya Mwenyezi Mungu kuwatukuza katika dunia na akhera, na wana raha kamili na utulivu kamili, na miongoni mwao ni mti wa Tuuba uliomo ndani ya Pepo ambao mpanda farasi anaweza kwenda katika kivuli chake kwa muda wa miaka mia bila ya kukimaliza, kama ilivyokuja katika Hadithi sahihi.
: 30 #
{كَذَلِكَ أَرْسَلْنَاكَ فِي أُمَّةٍ قَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلِهَا أُمَمٌ لِتَتْلُوَ عَلَيْهِمُ الَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَهُمْ يَكْفُرُونَ بِالرَّحْمَنِ قُلْ هُوَ رَبِّي لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ مَتَابِ (30)}.
30. Ndivyo hivyo tulivyokutuma kwa umma ambao wamekwsiha pita kabla yao umma nyingine, ili uwasomee yale tuliyokufunulia, na wao wanamkufuru Rahmani (Mwingi wa Rehema)! Sema: Yeye ndiye Mola wangu Mlezi. Hakuna mungu isipokuwa Yeye. Juu yake nimetegemea, na kwake ndiyo marejeo!
#
{30} يقول تعالى لنبيِّه محمد - صلى الله عليه وسلم -: {كذلك أرسلناك}: إلى قومك تدعوهم إلى الهدى، {قد خَلَتْ من قبلها أممٌ}: أرسلنا فيهم رسلنا، فلستَ ببدع من الرسل حتى يستنكروا رسالتك، ولستَ تقول من تلقاءِ نفسك، بل تتلو عليهم آياتِ الله، التي أوْحاها الله إليك، التي تطهِّر القلوب وتزكِّي النفوس، والحال أنَّ قومك يكفرون بالرحمن، فلم يقابلوا رحمته وإحسانه ـ التي أعظمها أنْ أرسلناك إليهم رسولاً وأنزلنا عليك كتاباً ـ بالقبول والشكر، بل قابلوها بالإنكار والردِّ؛ أفلا يعتبرون بمَنْ خلا من قبلهم من القرون المكذِّبة كيف أخذهم الله بذنوبهم؟ {قل هو ربِّي لا إله إلاَّ هو}: وهذا متضمِّن [للتوحيدين]: توحيد الألوهيَّة وتوحيد الربوبيَّة؛ فهو ربي الذي رَبَّاني بنعمِهِ منذ أوجدني، وهو إلهي الذي {عليه توكلتُ} في جميع أموري وإليه أنيب ؛ أي: أرجع في جميع عباداتي وفي حاجاتي.
{30} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. - "Ndivyo hivyo tulivyokutuma" kwa kaumu yako ili uwalinganie kwenye uwongofu. "Wamekwsiha pita kabla yao umma nyingine" ambao tuliwatumia Mitume wetu. Basi wewe si kitu kigeni miongoni mwa Mitume mpaka wakaukanusha utume wako, na wala husemi kwa kupenda kwako, bali unawasomea aya za Mwenyezi Mungu ambazo Mwenyezi Mungu alikufunulia, ambazo na zinazisafisha nyoyo, kuzitakasa nafsi, na hali ni kuwa kaumu yako wanamkufuru Mwingi wa Rehema, na hawakuikabili rehema yake na wema wake - ambazo kubwa zake zaidi ni kuwa tulikutuma kwao kama Mtume na tukakuteremshia kitabu - kwa kuzikubali na kushukuru. Lakini badala yake walizikabili kwa kuzipinga na kuzikataa. "Sema: Yeye ndiye Mola wangu Mlezi. Hakuna mungu isipokuwa Yeye." Na hili linajumuisha zile aina mbili za tauhid: Tauhidi ya uungu na tauhidi ya umola. Basi yeye ndiye mola wangu mlezi ambaye amenilea kwa neema zake tangu aliponiumba, naye ndiye Mungu wangu ambaye "Juu yake nimetegemea" katika mambo yangu yote na kwake Yeye ninarejea katika ibada zangu zote na mahitaji yangu.
: 31 #
{وَلَوْ أَنَّ قُرْآنًا سُيِّرَتْ بِهِ الْجِبَالُ أَوْ قُطِّعَتْ بِهِ الْأَرْضُ أَوْ كُلِّمَ بِهِ الْمَوْتَى بَلْ لِلَّهِ الْأَمْرُ جَمِيعًا أَفَلَمْ يَيْأَسِ الَّذِينَ آمَنُوا أَنْ لَوْ يَشَاءُ اللَّهُ لَهَدَى النَّاسَ جَمِيعًا وَلَا يَزَالُ الَّذِينَ كَفَرُوا تُصِيبُهُمْ بِمَا صَنَعُوا قَارِعَةٌ أَوْ تَحُلُّ قَرِيبًا مِنْ دَارِهِمْ حَتَّى يَأْتِيَ وَعْدُ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ لَا يُخْلِفُ الْمِيعَادَ (31)}.
31. Na kama ingelikuwako Qur-ani inayoendeshewa milima, na kupasuliwa kwayo ardhi, na kusemeshwa kwayo wafu, (basi ingelikuwa Qur-ani hii). Bali mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Je, hawajajua wale walioamini kwamba lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa bila ya shaka angeliwaongoa watu wote? Na wale waliokufuru hawaachi kusibiwa na balaa kwa yale waliyoyatenda, au ikawateremkia karibu na nyumbani kwao, mpaka ije ahadi ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake.
#
{31} يقول تعالى مبيِّناً فضل القرآن الكريم على سائر الكتب المنزَّلة: {ولو أنَّ قرآناً}: من الكتب الإلهيَّة، {سُيِّرتْ به الجبال}: عن أماكنها، و {قُطِّعت به الأرضُ}: جناناً وأنهاراً، و {كُلِّم به الموتى}: لكان هذا القرآن. {بل لله الأمرُ جميعاً}: فيأتي بالآيات التي تقتضيها حكمته؛ فما بال المكذبين يقترحون من الآيات ما يقترحون؟! فهل لهم ولغيرهم من الأمر شيء؟! {أفلم ييأسِ الذين آمنوا أن لو يشاءُ الله لهدى الناسَ جميعاً}: فليعلموا أنَّه قادرٌ على هدايتهم جميعاً، ولكنه لا يشاء ذلك، بل يهدي مَنْ يشاء ويُضِلُّ من يشاء. {ولا يزالُ الذين كفروا}: على كفرهم لا يعتبرون ولا يتَّعظون، والله تعالى يوالي عليهم القوارعَ التي تصيبُهم في ديارهم أو تَحُلُّ قريباً منها وهم مصرُّون على كفرهم. {حتى يأتي وعدُ الله}: الذي وَعَدَهم به لنزول العذاب المتَّصل الذي لا يمكن رفعُه. {إنَّ الله لا يخلِفُ الميعاد}: وهذا تهديدٌ لهم وتخويفٌ من نزول ما وعدهم الله به على كفرهم وعنادهم وظلمهم.
{31} Yeye Mtukufu Anasema akibainisha ubora wa Qur-ani hii Tukufu juu ya vitabu vingine vyote vilivyoteremshwa: "Na kama ingelikuwako Qur-ani" katika Vitabu vya kiungu "itaendeshewa milima" kutoka mahali pake, "na kupasuliwa kwayo ardhi" mabustani na mito, "na kusemeshwa kwayo wafu" basi ingekuwa Qur'ani hii. "Bali mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu" yeye analeta ishara ambazo inazihitaji hekima yake. Basi wana nini hao wanaokadhibisha wanapendekeza ishara wanazozipendekeza wao? Je, wao na wengine wana chochote katika jambo hili? "Je, hawajajua wale walioamini kwamba lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa bila ya shaka angeliwaongoa watu wote?" Basi na wajue kwamba Yeye ni Muweza wa kuwaongoa wote, lakini hataki hilo, bali humwongoa amtakaye na humpoteza amtakaye. "Na wale waliokufuru hawaachi" wanaendelea na ukafiri wao, wala hawazingatii wala hawaaidhiki. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anawafikishia maangamizi yanayowasibu katika makazi yao, au yanafika karibu nayo, ilhali wao wanaendelea tu na ukafiri wao. "Mpaka ije ahadi ya Mwenyezi Mungu" ambayo aliwaahidi ya kushuka kwa adhabu ya kuendelea isiyoweza kuondolewa. "Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake." Na hili ni tishio kwao na kuhofisha juu ya kuteremshwa kwa kile ambacho Mwenyezi Mungu aliahidi kwa sababu ya ukafiri wao, ukaidi wao na dhulma yao.
: 32 #
{وَلَقَدِ اسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِنْ قَبْلِكَ فَأَمْلَيْتُ لِلَّذِينَ كَفَرُوا ثُمَّ أَخَذْتُهُمْ فَكَيْفَ كَانَ عِقَابِ (32)}.
32. Na hakika walifanyiwa kejeli Mitume waliokuwa kabla yako. Na nikawapururia wale waliokufuru, kisha nikawashika! Basi ilikuwaje adhabu yangu!
#
{32} يقول تعالى لرسوله مثبِّتاً له ومسلياً: {ولقد استُهْزِئ برسل من قبلِكَ}: فلستَ أوَّلَ رسول كُذِّب وأوذِيَ. {فأمليتُ للذين كفروا}: برسلهم؛ أي: أمهلتهم مدة حتى ظنُّوا أنَّهم غيرُ معذَّبين، {ثم أخذتُهم}: بأنواع العذاب. {فكيف كان عقابِ}: كان عقاباً شديداً وعذاباً أليماً؛ فلا يغترَّ هؤلاء الذين كذَّبوك واستهزؤوا بك بإمهالنا؛ فلهم أسوةٌ فيمن قبلهم من الأمم، فليحذَروا أن يُفْعَلَ بهم كما فُعِلَ بأولئك.
{32} Yeye Mtukufu anamwambia Mtume wake, akimuimarisha na kumfariji, "Na hakika walifanyiwa kejeli Mitume waliokuwa kabla yako" Wewe si Mtume wa kwanza kukadhibishwa na kuudhiwa. "Na nikawapururia wale waliokufuru" Mitume wao mpaka wakadhani kuwa hawataadhibiwa, "kisha nikawashika" kwa aina mbalimbali za adhabu. "Basi ilikuwaje adhabu yangu!" Ilikuwa adhabu kali na adhabu chungu. Basi wasidanganyike hao waliokukadhibisha na kukufanyia stihizai na kutupa kwetu muhula. Wao wana mfano kutoka kwa wale waliokuwa kabla ya miongoni mwa umma. Basi na wajihadhari waje kufanyiwa kama walivyofanyiwa hao.
: 33 - 34 #
{أَفَمَنْ هُوَ قَائِمٌ عَلَى كُلِّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ وَجَعَلُوا لِلَّهِ شُرَكَاءَ قُلْ سَمُّوهُمْ أَمْ تُنَبِّئُونَهُ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِي الْأَرْضِ أَمْ بِظَاهِرٍ مِنَ الْقَوْلِ بَلْ زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا مَكْرُهُمْ وَصُدُّوا عَنِ السَّبِيلِ وَمَنْ يُضْلِلِ اللَّهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ (33) لَهُمْ عَذَابٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَشَقُّ وَمَا لَهُمْ مِنَ اللَّهِ مِنْ وَاقٍ (34)}.
33. Je, anayeisimamia kila nafsi kwa yale iliyoyachuma...? Na wamemfanyia Mwenyezi Mungu kuwa na washirika! Sema watajeni. Au ndiyo mnampa habari ya yale asiyoyajua katika ardhi, au ni maneno matupu tu? Bali wale waliokufuru wamepambiwa njama zao na wamezuiliwa njia ya sawasawa. Na yule ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza, basi hana wa kumwongoa yeyote. 34. Wana adhabu katika uhai wa dunia, na adhabu ya Akhera hakuna shaka ndiyo ngumu zaidi. Na wala hawatakuwa na wa kuwalinda kutokana na Mwenyezi Mungu.
#
{33} يقول تعالى: {أفمن هو قائمٌ على كلِّ نفس بما كسبتْ}: بالجزاء العاجل والآجل، بالعدل والقسط، وهو الله تبارك وتعالى؛ كمن ليس كذلك. ولهذا قال: {وجعلوا للهِ شركاءَ}: وهو اللهُ الأحدُ الفردُ الصمدُ الذي لا شريك له ولا ندَّ ولا نظير. {قل}: لهم إن كانوا صادقين: {سموهم}: لِتَعْلَمَ حالَهم. {أم تنبِّئونَه بما لا يعلم في الأرض}: فإنَّه إذا كان عالم الغيب والشهادة، وهو لا يعلم له شريكاً؛ عُلِمَ بذلك بطلان دعوى الشريك له، وأنَّكم بمنزلة الذي يُعْلِمُ الله أنَّ له شريكاً وهو لا يعلمه، وهذا أبطل ما يكون! ولهذا قال: {أم بظاهرٍ من القول}؛ أي: غاية ما يمكن من دعوى الشريك له تعالى أنه بظاهر أقوالكم، وأما في الحقيقة؛ فلا إله إلا الله، وليس أحدٌ من الخلق يستحقُّ شيئاً من العبادة. ولكن {زُيِّنَ للذين كفروا مكرُهم}: الذي مكروه، وهو كفرهم وشركهم وتكذيبهم لآيات الله. {وصدُّوا عن السبيل}؛ أي: عن الطريق المستقيمة الموصلة إلى الله وإلى دار كرامته. {ومن يُضْلِل الله فما له من هادٍ}: لأنه ليس لأحدٍ من الأمر شيءٌ.
{33} Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: "Je, anayeisimamia kila nafsi kwa yale iliyoyachuma...?" Kwa malipo ya haraka na ya baadaye, kwa uadilifu na haki. Naye ni Mungu, Mwenye baraka, Mtukufu, ni kama yule asiyekuwa hivyo. Na ndiyo maana akasema: "Na wamemfanyia Mwenyezi Mungu kuwa na washirika!" Ilhali Yeye ndiye Mwenyezi Mungu Mmoja, wa kipekee, Mkusudiwa ambaye hana mshirika yeyote wala mwenza, wala aliye sawa naye. "Sema" uwaambie ikiwa ni wakweli. "Watajeni" ili mjue hali zao. "Au ndio mnampa habari ya yale asiyoyajua katika ardhi" kwa maana ikiwa Yeye ndiye anayeyajua ya ghaibu na yanayoshuhudiwa, naye anajua kwamba hana mshirika yeyote, itajulikana kwa hayo ubatili wa madai ya kwamba ana mshirika, na kwamba mko katika nafasi ya mwenye kumjulisha Mwenyezi Mungu kwamba ana mshirika ilhali hamjui, na hii ndiyo batili kuliko zote! Na ndiyo maana akasema: "Au ni maneno matupu tu?'' Yaani, mwisho kabisa wa madai ya kwamba Yeye Mtukufu ana mshirika ni kwamba hilo linategemea maneno matupu tu yao. Na ama kiuhakika, hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, na hakuna yeyote miongoni mwa viumbe anayestahiki kuabudiwa. Lakini "wale waliokufuru wamepambiwa njama zao" ambazo walizipanga. Nazo ni kufuru yao, na ushirikina wao na kukadhibisha kwao Aya za Mwenyezi Mungu "wamezuiliwa njia ya sawasawa" yenye kufikisha kwa Mwenyezi Mungu na makazi ya utukufu wake. "Na yule ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza, basi hana wa kumwongoa yeyote." Kwa sababu hakuna yeyote mwenye mamlaka katika jambo hili isipokuwa Mwenyezi Mungu.
#
{34} {لهم عذابٌ في الحياة الدنيا ولعذابُ الآخرة أشقُّ}: من عذاب الدُّنيا؛ لشدَّته ودوامه. {وما لهم من الله من واقٍ}: يقيهم من عذابِ [اللهِ]؛ فعذابُهُ إذا وجَّهه إليهم لا مانع منه.
{34} "Wana adhabu katika uhai wa dunia, na adhabu ya Akhera hakuna shaka ndiyo ngumu zaidi" kuliko adhabu ya dunia, kwa sababu ya ukali wake na kudumu kwake. "Na wala hawatakuwa na wa kuwalinda kutokana na Mwenyezi Mungu," anayeweza kuwalinda kutokana na adhabu ya [Mwenyezi Mungu]. Kwa kuwa adhabu yake anapoielekeza kwao, hakuna kinachoweza kuizuia.
: 35 #
{مَثَلُ الْجَنَّةِ الَّتِي وُعِدَ الْمُتَّقُونَ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ أُكُلُهَا دَائِمٌ وَظِلُّهَا تِلْكَ عُقْبَى الَّذِينَ اتَّقَوْا وَعُقْبَى الْكَافِرِينَ النَّارُ (35)}
35. Mfano wa Bustani waliyoahidiwa wachamungu, kwa chini yake inapita mito, chakula chake ni cha daima, na pia kivuli chake. Huu ndio mwisho wa wale waliomcha Mungu. Na mwisho wa makafiri ni Moto.
#
{35} يقول تعالى: {مَثَلُ الجنة التي وُعِدَ المتَّقون}: الذين تركوا ما نهاهم الله عنه، ولم يقصِّروا فيما أمرهم به؛ أي: صفتها وحقيقتها، {تجري من تحتها الأنهار}: أنهار العسل وأنهار الخمر وأنهار اللبن وأنهار الماء التي تجري في غير أخدودٍ، فتسقي تلك البساتين والأشجار، فتحمل جميع أنواع الثمار. {أكُلُها دائمٌ وظلُّها}: دائمٌ أيضاً. {تلك عُقبى الذين اتَّقوا}؛ أي: عاقبتهم ومآلهم التي إليها يصيرون. {وعُقبى الكافرين النار}: فكم بين الفريقين من الفرق المبين؟
{35} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Mfano wa Bustani waliyoahidiwa wachamungu" wale walioacha yale aliyowakataza Mwenyezi Mungu, na wala hawapunguza katika yale aliyowaamrisha kuyafanya. Yaani, maelezo yake na uhalisia wake, ni kwamba "kwa chini yake inapita mito" mito ya asali, mito ya mvinyo, mito ya maziwa, na mito ya maji yapitayo si ndani ya sehemu iliyodidimia kwa kina ndani ya ardhi, nayo yananywesha bustani hizo na miti hiyo, na inazaa kila aina ya matunda. "Chakula chake ni cha daima na pia kivuli chake. Huu ndio mwisho wa wale waliomcha Mungu. Na mwisho wa makafiri ni Moto," basi ni tofauti ngapi zilizo wazi baina ya makundi haya mawili?
: 36 #
{وَالَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَفْرَحُونَ بِمَا أُنْزِلَ إِلَيْكَ وَمِنَ الْأَحْزَابِ مَنْ يُنْكِرُ بَعْضَهُ قُلْ إِنَّمَا أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ اللَّهَ وَلَا أُشْرِكَ بِهِ إِلَيْهِ أَدْعُو وَإِلَيْهِ مَآبِ (36)}.
36. Na wale tuliowapa Kitabu wanayafurahia yale yaliyoteremshwa kwako. Na katika makundi mengine wapo wanaoyakataa baadhi yake. Sema: Hakika nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu tu, na wala nisimshirikishe. Kwake Yeye ndiko ninaitia na kwake Yeye ndiko marejeo.
#
{36} يقول تعالى: {والذين آتَيْناهم الكتابَ}؛ أي: مننَّا عليهم به وبمعرفته، {يفرحون بما أنزل إليك}: فيؤمنون به ويصدِّقونه ويفرحون بموافقة الكتب بعضها لبعض وتصديق بعضها بعضاً، وهذه حال مَنْ آمن مِنْ أهل الكتابين. {ومن الأحزاب مَن ينكِرُ بعضه}؛ أي: ومن طوائف الكفار المتحزبين على الحقِّ من ينكر بعض هذا القرآن ولا يصدقه؛ فمن اهتدى فلنفسه، ومن ضلَّ؛ فإنما يضلُّ عليها، إنما أنت يا محمد منذرٌ تدعو إلى الله. {قل إنَّما أمِرْتُ أن أعبدَ الله ولا أشرك به}؛ أي: بإخلاص الدين لله وحده. {إليه أدعو وإليه مآبِ}؛ أي: مرجعي الذي أرجع به إليه، فيجازيني بما قمتُ به من الدعوة إلى دينه والقيام بما أمرت به.
{36} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Na wale tuliowapa Kitabu;" yaani, tuliwaneemesha kwacho, na tukawaneemesha kukijua "wanayafurahia yale yaliyoteremshwa kwako" kwa hivyo wanayaamini na kuyasadiki, na wanafurahia kuafikiana Vitabu vyenyewe kwa vyenyewe, na kusadikishana vyenyewe kwa vyenyewe. Na hii ndiyo hali ya wale walioamini miongoni mwa Watu wa Vitabu vile viwili. "Na katika makundi mengine wapo wanaoyakataa baadhi yake." Yaani, katika makundi ya makafiri waliofanya vikundi dhidi ya haki kuna wale wanaokataa baadhi ya Qur-ani hii na hawayaamini. Kwa hivyo mwenye kuongoka, basi ni kwa ajili yake mwenyewe, na mwenye kupotea, basi hakika anapotea kwa hasara yake, wewe hakika ewe Muhammad, ni muonyaji tu mwenye kulingania kwa Mwenyezi Mungu. "Sema: Hakika nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu tu, na wala nisimshirikishe." Yaani, nimeamrishwa nimuabudu kwa kumfanyia yeye peke yake tu dini. "Kwake Yeye ndiko ninaitia na kwake Yeye ndiko marejeo" yangu ambayo nitarejea, kisha atanilipa kwa yale niliyoyafanya ya kuilingania dini yake na kutekeleza yale niliyoamrishwa.
: 37 #
{وَكَذَلِكَ أَنْزَلْنَاهُ حُكْمًا عَرَبِيًّا وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُمْ بَعْدَ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ اللَّهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا وَاقٍ (37)}
37. Na ndivyo hivyo tumeiteremsha (Qur-ani hii kuwa ni) hukumu kwa lugha ya Kiarabu. Na ukifuata matamanio yao baada ya elimu hii iliyokujia, hutakuwa na rafiki yeyote wala mlinzi kando na Mwenyezi Mungu.
#
{37} أي: ولقد أنزلنا هذا القرآن والكتاب {حُكْماً عربيًّا}؛ أي: محكماً متقناً بأوضح الألسنة وأفصح اللغات؛ لئلاَّ يقع فيه شكٌّ واشتباهٌ، وليوجب أن يُتَّبع وحدَه ولا يُداهن فيه ولا يتَّبع ما يضادُّه ويناقضه من أهواء الذين لا يعلمون، ولهذا توعَّد رسوله ـ مع أنه معصومٌ ـ ليمتنَّ عليه بعصمته، ولتكون أمَّتُه أسوتَه في الأحكام، فقال: {ولئن اتَّبعتَ أهواءهم بعدما جاءك من العلم}: البيِّن، الذي ينهاك عن اتِّباع أهوائهم. {ما لك من الله من وليٍّ}: يتولاَّك فيحصل لك الأمر المحبوب. {ولا واقٍ}: يقيك من الأمر المكروه.
{37} Yaani, hakika tuliiteremsha Qur-ani hii na Kitabu hiki, "hukumu kwa lugha ya Kiarabu." Yaani, hukumu iliyo madhubuti kwa lugha iliyo wazi zaidi na yenye ufasaha zaidi ili asiingie shaka yoyote ndani yake wala mchanganyiko, na ili iwe sababu ya kukifuata hicho peke yake wala asibembelezwe yeyote kukifuata, wala kisifuatwe kilicho kinyume yake na yenye kukipinga miongoni mwa matamanio ya wale wasiojua. Na ndiyo maana akamtishia Mtume wake - pamoja na kwamba yeye amehifadhiwa hafanyi dhambi - ili iwe neema yake juu yake kwamba kumhifadhi, na ili umma wake uchukue kiigizo kutoka kwake katika hukumu mbalimbali, basi akasema: "Na ukifuata matamanio yao baada ya elimu hii iliyokujia" iliyo wazi, ambayo inakukataza kufuata matamanio yao. "Hutakuwa na rafiki yeyote kando na Mwenyezi Mungu" atakayekusimamia na kukuletea mambo uyapendayo "wala mlinzi" atakayekukinga kutokana na mambo yachukizayo.
: 38 - 39 #
{وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِنْ قَبْلِكَ وَجَعَلْنَا لَهُمْ أَزْوَاجًا وَذُرِّيَّةً وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَنْ يَأْتِيَ بِآيَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّهِ لِكُلِّ أَجَلٍ كِتَابٌ (38) يَمْحُو اللَّهُ مَا يَشَاءُ وَيُثْبِتُ وَعِنْدَهُ أُمُّ الْكِتَابِ (39)}.
38. Na hakika Sisi tulikwisha watuma Mitume kabla yako, na tukawafanya wawe na wake na dhuria. Na haikuwa kwa Mtume yeyote kuleta ishara isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kila kipindi kina hukumu yake iliyoandikwa. 39. Mwenyezi Mungu hufuta na huthibitisha ayatakayo. Na asili ya hukumu zote zilizoandikwa iko kwake.
#
{38} أي: لست أول رسول أرسل إلى الناس حتى يستغربوا رسالتك. فقد {أرسَلْنا رسلاً من قبلِكَ وجَعَلْنا لهم أزواجاً وذُرِّيَّةً}: فلا يعيبك أعداؤك بأن يكون لك أزواجٌ وذُرِّيَّة كما كان لإخوانك المرسلين؛ فلأيِّ شيء يقدحون فيك بذلك وهم يعلمون أن الرسل قبلك كذلك إلاَّ لأجل أغراضهم الفاسدة وأهوائهم، وإن طلبوا منك آيةً اقترحوها؛ فليس لك من الأمر شيء. فما {كان لرسول أن يأتي بآيةٍ إلاَّ بإذنِ الله}: والله لا يأذن فيها إلاَّ في وقتها الذي قدَّره وقضاه. {لكلِّ أجل كتابٌ}: لا يتقدم عليه ولا يتأخَّر عنه، فليس استعجالهم بالآيات أو بالعذاب موجباً لأنْ يقدِّم الله ما كتب أنه يؤخَّر، مع أنَّه تعالى فعَّالٌ لما يريد.
{38} Yaani, wewe si mtume wa kwanza kutumwa kwa watu hadi waushangae utume wako. Hakika "tulikwisha watuma Mitume kabla yako, na tukawafanya wawe na wake na dhuria." Basi wasikutie doa adui zako ikiwa una wake na dhuria kama walivyokuwa ndugu zako miongoni mwa Mitume. Basi ni kwa kitu gani wanakukashifu kwa hayo, ilhali wanajua kwamba Mitume waliokuwa kabla yako walikuwa hivyo, isipokuwa tu kwa ajili ya kuepeana kwao mgongo kuovu na matamanio yao. Na wakikuomba ishara wanayoipendekeza wao, basi wewe huna chochote katika jambo hilo. Kwa maana, "haikuwa kwa Mtume yeyote kuleta ishara isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu" Na Mwenyezi Mungu haliruhusu hilo isipokuwa kwa wakati wake alioupitisha na kuuandika. "Kila kipindi kina hukumu yake iliyoandikwa" hakiitangulii hukumu hiyo iliyoandikwa wala hakichelewi zaidi yake. Kwa hivyo kuziharakisha kwao ishara au adhabu hakufanyi Mwenyezi Mungu kutanguliza au kuchelewesha alichoandika, pamoja na kwamba Yeye Mtukufu hufanya atakavyo.
#
{39} {يمحو الله ما يشاءُ}: من الأقدار، {ويُثْبِتُ}: ما يشاء منها، وهذا المحو والتغيير في غير ما سبق به علمُه وكَتَبَه قلمُه؛ فإنَّ هذا لا يقع فيه تبديلٌ ولا تغييرٌ؛ لأنَّ ذلك محالٌ على الله أن يقع في علمِهِ نقصٌ أو خللٌ، ولهذا قال: {وعنده أمُّ الكتاب}؛ أي: اللوح المحفوظ الذي ترجِعُ إليه سائر الأشياء؛ فهو أصلها، وهي فروعٌ [له] وشعبٌ؛ فالتغيير والتبديل يقع في الفروع والشعب؛ كأعمال اليوم والليلة التي تكتبها الملائكة ويجعل الله لثبوتها أسباباً ولمحوها أسباباً، لا تتعدَّى تلك الأسباب ما رُسِم في اللوح المحفوظ؛ كما جعل الله البرَّ والصلة والإحسان من أسباب طول العمر وسعة الرزق، وكما جعل المعاصي سبباً لمحق بركة الرزق والعمر، وكما جعل أسباب النجاة من المهالك والمعاطب سبباً للسلامة، وجعل التعرُّض لذلك سبباً للعطب؛ فهو الذي يدبِّر الأمور بحسب قدرته وإرادته، وما يدبِّره منها لا يخالف ما قد علمه وكتبه في اللوح المحفوظ.
{39} "Mwenyezi Mungu hufuta ayatakayo" katika hukumu na majaliwa, "na huthibitisha" atakayo katika hayo. Na kufuta huku na kubadilisha huku si katika yale aliyotangulia kuyajua na ikayaandika kalamu yake. Hayo hayaingiwi na mabadiliko wala mageuzi, kwa sababu hilo haliwezekani kwa Mwenyezi Mungu kutokea upungufu wowote wala dosari katika elimu yake. Na ndiyo maana akasema: "Na asili ya hukumu zote zilizoandikwa iko kwake." Yaani, ubao uliohifadhiwa ambao vitu vyote vinaurudia kwa maana huo ndio asili yake, nayo ni matawi yake na vipengele. Kwa hivyo, mageuzi na mabadiliko hutokea katika matawi na vipengele, kama vile matendo ya mchana na usiku ambayo Malaika huyaandika na Mwenyezi Mungu anawekea kuthibiti kwake sababu mbalimbali, na kufutwa kwake pia anakuwekea sababu mbalimbali pia, na sababu hizi hazizidi yale yaliyoandikwa katika Ubao Uliohifadhiwa. Kama vile Mwenyezi Mungu alivyofanya wema, kuunga jamaa, na ukarimu kuwa miongoni mwa njia za kurefusha umri na upana wa riziki, kama vile pia alivyofanya maasia kuwa sababu ya kuondoa baraka ya riziki na umri, na kama vile alivyofanya njia za kuokoka kutokana na maangamivu na maafa kuwa ndizo sababu za usalama; na akafanya kujitia katika hayo ndiyo sababu ya maafa. Basi Yeye ndiye anayeendesha mambo kulingana na uwezo wake na utashi wake. Na kile anachokiendesha miongoni mwa mambo hayahalifu yale aliyokwisha yajua na kuyaandika katika Ubao Uliohifadhiwa.
: 40 - 41 #
{وَإِنْ مَا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ الَّذِي نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ وَعَلَيْنَا الْحِسَابُ (40) أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا نَأْتِي الْأَرْضَ نَنْقُصُهَا مِنْ أَطْرَافِهَا وَاللَّهُ يَحْكُمُ لَا مُعَقِّبَ لِحُكْمِهِ وَهُوَ سَرِيعُ الْحِسَابِ (41)}.
40. Na ikiwa tutakuonyesha baadhi ya yale tuliyowaahidi au tukakufisha kabla yake, juu yako wewe ni kufikisha ujumbe tu na juu yetu ni hesabu. 41. Je, hawakuona kwamba tunaijia ardhi tukiipunguza kutokea nchani mwake? Na Mwenyezi Mungu huhukumu, na hakuna wa kurekebisha hukumu yake, naye ni Mwepesi wa kuhesabu.
#
{40} يقول تعالى لنبيِّه محمد - صلى الله عليه وسلم -: لا تعجل عليهم بإصابة ما يوعَدون [به] من العذاب؛ فهم إن استمرُّوا على طغيانهم وكفرهم؛ فلا بدَّ أن يصيبَهم ما وُعِدوا به: إما أنْ نرينَّك إيَّاه في الدنيا فَتَقَرَّ بذلك عينك، أو نتوفَّيَنَّكَ قبل إصابتهم؛ فليس ذلك شغلاً لك. {فإنما عليك البلاغ}: والتبيين للخلق، {وعلينا الحسابُ}: فنحاسب الخلق على ما قاموا به مما عليهم وضيَّعوه، ونثيبهم أو نعاقبهم.
{40} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie: - Usiwaharakishie kufikiwa na adhabu waliyoahidiwa. Kwa maana hata wakiendelea na upindukiaji wao na ukafiri wao, basi ni lazima yatawafika yale waliyoahidiwa. Ima tutakuonyesha adhabu hiyo katika dunia, kwa hivyo yafurahie hayo macho yako, au tukufishe kabla kuwafikishia adhabu hiyo. Na hiyo si kazi yako; "juu yako wewe ni kufikisha ujumbe tu" na kuwabainishia viumbe, "na juu yetu ni hesabu." Basi tutawahesabu viumbe kwa yale waliyoyafanya katika yale yaliyo juu yao na yale waliyokosa kufanya vyema, na tutawalipa thawabu au kuwaadhibu.
#
{41} ثم قال متوعِّداً للمكذبين: {أو لم يروا أنا نأتي الأرضَ ننقُصُها من أطرافها}: قيل: بإهلاك المكذبين واستئصال الظالمين، وقيل: بفتح بلدان المشركين ونقصهم في أموالهم وأبدانهم، وقيل غير ذلك من الأقوال. والظاهر ـ والله أعلم ـ أنَّ المراد بذلك أنَّ أراضي هؤلاء المكذِّبين جعل الله يفتحها ويجتاحها ويُحِلُّ القوارع بأطرافها تنبيهاً لهم قبل أن يجتاحهم النقص ويوقع الله بهم من القوارع ما لا يردُّه أحدٌ، ولهذا قال: {والله يحكم لا مُعَقِّبَ لحكمِهِ}: ويدخل في هذا حكمه الشرعيُّ والقدريُّ والجزائيُّ؛ فهذه الأحكام التي يحكم الله فيها توجد في غاية الحكمة والإتقان، لا خلل فيها ولا نقص، بل هي مبنيَّة على القسط والعدل والحمد؛ فلا يتعقَّبها أحدٌ، ولا سبيل إلى القدح فيها؛ بخلاف حكم غيره؛ فإنَّه قد يوافق الصواب وقد لا يوافقه. {وهو سريع الحساب}؛ أي: فلا يستعجلوا بالعذاب؛ فإنَّ كل ما هو آتٍ فهو قريبٌ.
{41} Kisha akasema akiwaahidi adhabu wale wanaokadhibisha, "Je, hawakuona kwamba tunaijia ardhi tukiipunguza kutokea nchani mwake?" Hapa ilisemwa maana yake ni kuwaangamiza wale wanaokadhibisha na kuwafutilia mbali madhalimu. Na ilisemwa pia kwamba hilo ni kwa kuziteka nchi za washirikina na kuwapunguza katika mali zao na miili yao, na kauli zinginezo pia zilisemwa. Na kauli iliyo dhahiri - na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi - ni kwamba maana yake ni kwamba Mwenyezi Mungu anaziteka ardhi za wale wanaokadhibisha hawa na kuzifutilia mbali, na anazifikishia misiba kwenye ncha zake ili liwe onyo kwao kabla ya kufutilia mbali na upungufu, na tena Mwenyezi Mungu huwafikishia misiba ambayo hakuna yeyote anayeweza kuizuia. Na ndiyo maana akasema: "Na Mwenyezi Mungu huhukumu, na hakuna wa kupinga hukumu yake," na inaingia katika hili hukumu yake ya kisheria na ya kimajaliwa, na ya kimalipo. Kwa hivyo, hukumu hizi ambazo Mwenyezi Mungu anazihukumu zinapatikana kwa sababu ya hekima ya hali ya juu zaidi na ubora mkubwa zaidi, hazina dosari yoyote wala upungufu; bali zimejengeka juu ya haki na uadilifu, na sifa njema. Kwa hivyo hawezi kuzirekebisha, na wala hakuna njia yoyote ya kuzitia dosari. Kinyume na hukumu ya asiyekuwa yeye, hiyo huenda ikaafikiana na usahihi au huenda isiafikiane nao. "Naye ni Mwepesi wa kuhesabu" kwa hivyo, wasiiharakishe adhabu, kwa maana kila kijacho, basi ki karibu.
: 42 - 43 #
{وَقَدْ مَكَرَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ فَلِلَّهِ الْمَكْرُ جَمِيعًا يَعْلَمُ مَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ وَسَيَعْلَمُ الْكُفَّارُ لِمَنْ عُقْبَى الدَّارِ (42) وَيَقُولُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَسْتَ مُرْسَلًا قُلْ كَفَى بِاللَّهِ شَهِيدًا بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ وَمَنْ عِنْدَهُ عِلْمُ الْكِتَابِ (43)}.
42. Na walipanga njama wale waliokuwa kabla yao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye njama zote. Yeye anajua kile inachochuma kila nafsi. Na makafiri watakuja jua ni ya nani nyumba ya mwisho Akhera! 43. Na wale waliokufuru wanasema: Wewe hukutumwa. Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi, na pia yule mwenye elimu ya Kitabu.
#
{42} يقول تعالى: {وقد مكر الذين من قبلهم}: برسلهم وبالحقِّ الذي جاءت به الرسل، فلم يُغْنِ عنهم مكرهم، ولم يصنعوا شيئاً؛ فإنَّهم يحاربون الله ويبارزونه. {فلله المكرُ جميعاً}؛ أي: لا يقدر أحدٌ أن يمكر مكراً إلاَّ بإذنه وتحت قضائه وقدره؛ فإذا كانوا يمكرون بدينه؛ فإنَّ مكرهم سيعود عليهم بالخيبة والندم؛ فإنَّ الله {يعلم ما تكسِبُ كلُّ نفسٍ}؛ أي: همومها وإراداتها وأعمالها الظاهرة والباطنة، والمكر لا بدَّ أن يكون من كسبها؛ فلا يخفى على الله مكرهم، فيمتنع أن يمكروا مكراً يضرُّ الحقَّ وأهله ويفيدهم شيئاً. {وسيعلم الكفَّار لمن عُقبى الدار}؛ أي: أَلَهُمْ أَوْ لِرُسُلِه؟ ومن المعلوم أنَّ العاقبةَ للمتَّقِينَ لِلْكُفْرِ، وَأَعْمَالِه.
{42} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na walipanga njama wale waliokuwa kabla yao" dhidi ya Mitume wao na haki waliyokuja nayo Mitume, lakini njama hizo hazikuwafaa kitu, wala hawakufanya lolote. Kwa maana hapo walikuwa wanapigana na Mwenyezi Mungu na kujitokeza dhidi yake, "lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye njama zote." Yaani, hakuna yeyote awezaye kupanga njama isipokuwa kwa idhini yake na chini ya hukumu yake na majaliwa yake. Kwa hivyo, ikiwa wanapanga njama dhidi ya dini yake, basi njama yao hiyo itawarudia kwa kuambulia patupu na majuto. Kwa maana Mwenyezi Mungu "anajua kile inachochuma kila nafsi" wasiwasi wake, utashi wake, na vitendo vyake vya dhahiri na vilivyofichika. Na njama lazima ni katika kuchuma kwake, kwa hivyo njama zao hizo hazifichikani kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo haiwezekani kwao kufanya njama zenye kuidhuru haki na watu wake na ikawanufaisha kitu. "Na makafiri watakuja jua ni ya nani nyumba ya mwisho Akhera!" Yaani, je, itakuwa yao au ya Mitume wake? Na inajulikana vyema kwamba mwisho mwema ni wa wachamungu, si wa ukafiri na matendo yake.
#
{43} {ويقول الذين كفروا لستَ مرسلاً}؛ أي: يكذِّبونك ويكذِّبون ما أرسلت به. {قل} لهم إن طلبوا على ذلك شهيداً: {كفى بالله شهيداً بيني وبينَكم}: وشهادته بقوله وبفعله وإقراره: أما قوله؛ فبما أوحاه الله إلى أصدق خلقه مما يُثْبِتُ به رسالته. وأما فعله؛ فلأنَّ الله تعالى أيَّد رسوله ونصره نصراً خارجاً عن قدرته وقدرة أصحابه وأتباعه، وهذا شهادةٌ منه له بالفعل والتأييد، وأما إقراره؛ فإنَّه أخبر الرسول عنه أنه رسول ، وأنه أمر الناس باتباعه؛ فمن اتَّبعه؛ فله رضوانُ الله وكرامته، ومن لم يتَّبعه؛ فله النار والسخط، وحلَّ له مالُه ودمه، والله يقرُّه على ذلك؛ فلو تقوَّل عليه بعض الأقاويل؛ لعاجله بالعقوبة. {ومَنْ عندَه علمُ الكتاب}: وهذا شاملٌ لكلِّ علماء أهل الكتابين؛ فإنَّهم يشهدون للرسول، من آمن واتَّبع الحقَّ، صرَّح بتلك الشهادة التي عليه، ومن كتم ذلك؛ فإخبار الله عنه أنَّ عنده شهادةً أبلغ من خبره، ولو لم يكن عنده شهادةٌ؛ لردَّ استشهاده بالبرهان؛ فسكوته يدلُّ على أن عنده شهادةً مكتومةً، وإنَّما أمر الله باستشهاد أهل الكتاب لأنَّهم أهل هذا الشأن، وكلُّ أمر إنما يُستشهد فيه أهله ومن هم أعلم به من غيرهم؛ بخلاف مَنْ هو أجنبيٌّ عنه؛ كالأميِّين من مشركي العرب وغيرهم؛ فلا فائدة في استشهادهم؛ لعدم خبرتهم ومعرفتهم. والله أعلم.
{43} "Na wale waliokufuru wanasema: Wewe hukutumwa;" yaani, wanakukadhibisha wewe na yale uliyotumwa nayo. "Sema" uwaambie ikiwa watataka shahidi juu ya hilo, "Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi." Na ushahidi wake ni kwa maneno yake, na vitendo vyake, na kukiri kwake. Ama kauli yake, basi ni kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu aliyafunua kwa yule wa kweli zaidi katika viumbe vyake miongoni mwa yale anayothibitisha kwayo ujumbe wake. Na ama kitendo chake, basi ni kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu alimuunga mkono Mtume wake na akamnusuru nusura iliyokuwa nje ya uwezo wake na uwezo wa masahaba wake na wafuasi wake. Na huu ni ushahidi kutoka Kwake kwa vitendo na uungaji mkono. Na ama kukiri kwake, basi ni kwamba alimjulisha Mtume kuhusu yeye kuwa ni Mtume, na kwamba aliwaamrisha watu wamfuate. Kwa hivyo, mwenye kumfuata, basi huyo ana radhi za Mwenyezi Mungu na utukufu wake. Na asiyemfuata, basi huyo ana Moto na ghadhabu, na mali yake na damu yake ni halali kwa Mtume huyu, na Mwenyezi Mungu amemkubalia hilo. Kwa hivyo, angemdanganyishia uongo hata kidogo, basi angemharakishia adhabu. "Na pia yule mwenye elimu ya Kitabu" na hili linajumuisha wazuoni wote wa Watu wa Vitabu hivi viwili. Kwani wao wanamshuhudia Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - katika wale walioamini na wakaifuata haki, wanatangaza ushahidi huo ulio juu yake. Na mwenye kuficha hilo, basi kujulisha kwa Mwenyezi Mungu juu yake kwamba ana ushahidi kunatosha zaidi hata kuliko habari yake mwenyewe. Na hata kama hangekuwa na ushahidi, basi angekataa kumfanya yeye kuwa shahidi kwa hijja. Kwa hivyo, kunyamaza kwake kunaonyesha kuwa ana ushahidi uliofichwa. Na Mwenyezi Mungu aliamrisha kutafuta ushahidi wa Watu wa Kitabu kwa sababu wao ni watu wa jambo hili, na katika kila jambo ni watu wake tu ndio wanaotafuta ushahidi wao, na wale ambao wajua zaidi katika wale wasiokuwa wao. Tofauti na yule ambaye ni mgeni katika hilo, kama vile wasiojua kusoma na kuandika katika washirikina wa Kiarabu na wengineo. Basi hakuna faida yoyote katika kutafuta ushahidi wao kwa sababu ya ukosefu wao wa uzoefu wao na maarifa yao. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi.
Imekamilika tafsiri ya Surat Ra'd. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.