Nayo iliteremka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{الر تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ وَقُرْآنٍ مُبِينٍ (1) رُبَمَا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ كَانُوا مُسْلِمِينَ (2) ذَرْهُمْ يَأْكُلُوا وَيَتَمَتَّعُوا وَيُلْهِهِمُ الْأَمَلُ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ (3) وَمَا أَهْلَكْنَا مِنْ قَرْيَةٍ إِلَّا وَلَهَا كِتَابٌ مَعْلُومٌ (4) مَا تَسْبِقُ مِنْ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسْتَأْخِرُونَ (5)}.
1. Alif Lam Ra. Hizi ni Aya za Kitabu na Qur-ani inayobainisha. 2. Huenda ikawa wale waliokufuru wakatamani kwamba wangekuwa Waislamu. 3. Waache wale, na wastarehe, na yawazuge matumaini. Watakuja jua. 4. Na hatukuuangamiza mji wowote ule isipokuwa ulikuwa na muda wake maalumu. 5. Hawawezi umma wowote kuutangulia muda wao, wala kuchelewa.
#
{1} يقول تعالى معظِّماً لكتابه مادحاً له: {تلك آياتُ الكتابِ}؛ أي: الآيات الدالَّة على أحسن المعاني وأفضل المطالب، {وقرآنٍ مُبينٍ}: للحقائق بأحسن لفظ وأوضحه وأدلِّه على المقصود.
{1} Yeye Mtukufu anasema akikitukuza na kukisifu Kitabu chake, "Hizi ni Aya za Kitabu." Yaani, ni Aya zinazoashiria maana nzuri zaidi na mahitaji bora zaidi, "na Qur-ani inayobainisha" hakika mbalimbali kwa maneno mazuri zaidi na yaliyo wazi zaidi, na yenye kuashiria zaidi kinachokusudiwa.
#
{2} وهذا مما يوجب على الخلق الانقياد إليه والتسليم لحكمه وتلقِّيه بالقَبول والفرح والسرور، فأما من قابل هذه النعمة العظيمة بردِّها والكفر بها؛ فإنَّه من المكذِّبين الضالِّين، الذين سيأتي عليهم وقتٌ يتمنَّوْن أنهم مسلمون؛ أي: منقادون لأحكامه، وذلك حين ينكشف الغطاء وتظهرُ أوائل الآخرة ومقدِّمات الموت؛ فإنهم في أحوال الآخرة كلِّها يتمنَّون أنهم مسلمون، وقد فات وقتُ الإمكان، ولكنَّهم في هذه الدُّنيا مغترُّون.
{2} Na hili ni katika yale yanayowahitaji viumbe kukifuata, na kujisalimisha kwa hukumu yake, na kukipokea kwa kukikubali, na kufurahi. Ama mwenye kuitikia neema hii kubwa anaikataa na kuikataa; kwani yeye ni miongoni mwa waongo wapotofu, na itafika wakati watatamani lau wangekuwa Waislamu. Yaani, wanatawaliwa na hukumu zake, na hapo ndipo kifuniko kinapofunuliwa na kudhihirika mwanzo wa maisha ya akhera na mwanzo wa kifo. Katika hali zote za maisha ya baada ya kifo, wanatamani wangekuwa Waislamu, na wakati wa uwezekano huu umepita, lakini katika ulimwengu huu wanadanganywa.
#
{3} فَـ {ذَرْهم يأكلوا ويتمتَّعوا}: بلذاتهم، {ويلههم الأمل}؛ أي: يؤمِّلون البقاء في الدنيا فيلهيهم عن الآخرة، {فسوف يعلمونَ}: أنَّ ما هم عليه باطلٌ، وأنَّ أعمالهم ذهبت خسراناً عليهم، ولا يغترُّوا بإمهال الله تعالى؛ فإنَّ هذه سنته في الأمم.
{3} Basi "waache wale, na wastarehe" kwa anasa zao, "na yawazuge matumaini." Yaani, wanataraji kubakia hapa duniani, kwa hivyo wanapumbazwa dhidi ya uhai wa Akhera. "Kwa hivyo watakuja jua," kwamba hayo wanayoyafanya ni batili, na kwamba matendo yao yamekuwa hasara kwao, wala wasidanganyike na Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwapa muhula. Kwa maana hii ndiyo desturi yake katika umma zilizotangulia.
#
{4} {وما أهلكْنا من قريةٍ}: كانت مستحقةً للعذاب، {إلاَّ ولها كتابٌ معلوم}: مقدَّر لإهلاكها.
{4} "Na hatukuuangamiza mji wowote ule" ambao ulikuwa unastahiki adhabu, "isipokuwa ulikuwa na muda wake maalumu" ulioandikwa wa wao kuangamizwa.
#
{5} {ما تسبِقُ من أمَّةٍ أجَلَها وما يستأخِرون}: وإلاَّ؛ فالذنوب لا بدَّ من وقوع أثرها وإن تأخَّر.
{5} "Hakuna umma unaotangulia muda wao, wala kuchelewesha." Nazo dhambi lazima ziwe na athari zake, hata zikichelewa.
{وَقَالُوا يَاأَيُّهَا الَّذِي نُزِّلَ عَلَيْهِ الذِّكْرُ إِنَّكَ لَمَجْنُونٌ (6) لَوْمَا تَأْتِينَا بِالْمَلَائِكَةِ إِنْ كُنْتَ مِنَ الصَّادِقِينَ (7) مَا نُنَزِّلُ الْمَلَائِكَةَ إِلَّا بِالْحَقِّ وَمَا كَانُوا إِذًا مُنْظَرِينَ (8) إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ (9)}.
6. Na walisema, "Ewe uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe ni mwendawazimu. 7. Mbona hutuletei Malaika ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli? 8. Sisi hatuwateremshi Malaika isipokuwa kwa sababu ya haki, na hapo hawatapewa muhula. 9. Hakika Sisi ndio tuliouteremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutakoulinda.
#
{6} أي: وقال المكذبون لمحمِّد - صلى الله عليه وسلم - استهزاءً وسخريةً: {يا أيها الذي نُزِّلَ عليه الذِّكر}: على زعمك، {إنَّك لمجنون}: إذ تظنُّ أنا سنتَّبعك ونترك ما وجدنا عليه آباءنا لمجرَّد قولك.
{6} Yaani, wale waliokadhibisha walimwambia Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie - kwa stihzai na masihara, "Ewe uliyeteremshiwa ukumbusho!" Kulingana na madai yako "hakika wewe ni wazimu" kwa maana unadhani kwamba sisi tutakufuata na kuyaacha yale tuliyowakuta nayo baba zetu kwa sababu ya kauli yako tu.
#
{7 - 8} {لو ما تأتينا بالملائكةِ}: يشهدون لك بصحَّة ما جئت به، {إن كنتَ من الصادقين}: فلما لم تأت بالملائكةِ؛ فلستَ بصادق. وهذا من أعظم الظُّلم والجهل: أما الظُّلم؛ فظاهر؛ فإنَّ هذا تجرؤ على الله وتعنُّت بتعيين الآيات التي لم يخترْها، وحَصَلَ المقصودُ والبرهان بدونها من الآيات الكثيرة الدالَّة على صحَّة ما جاء به. وأما الجهلُ؛ فإنَّهم جهلوا مصلحتهم من مضرَّتهم؛ فليس في إنزال الملائكة خيرٌ لهم، بل لا ينزل الله الملائكة إلاَّ بالحقِّ الذي لا إمهال على مَنْ لم يتَّبعه وينقد له. {وما كانوا إذاً}؛ أي: حين تنزل الملائكة إن لم يؤمنوا ولن يؤمنوا، {مُنْظَرين}؛ أي: بمُمْهَلينَ، فصار طلبهم لإنزال الملائكة تعجيلاً لأنفسهم بالهلاك والدمار؛ فإن الإيمان ليس في أيديهم، وإنما هو بيد الله، {ولو أنَّنا نزَّلنا إليهم الملائكة وكلَّمهم الموتى وحَشَرْنا عليهم كلَّ شيء قُبُلاً ما كانوا لِيؤمنوا إلاَّ أن يشاء الله، ولكنَّ أكثرَهم يجهلونَ}.
{7 - 8} "Kwa nini usituletee Malaika" ili wakushuhudilie juu ya usahihi wa yale uliyokuja nayo, "ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli?" Kwa hivyo, pindi hukuleta malaika, basi wewe si mkweli. Na hili ni katika dhuluma kubwa zaidi na ujinga. Ama kuhusu dhuluma yao, hilo liko dhahiri. Kwa maana, hili ni kuthubutu kumpendekezea Mwenyezi Mungu kuleta ishara ambazo hakuchagua Yeye, na kumfanyia ukaidi, na ilhali makusudio na uthibitisho tayari ulikwisha patikana kwa zisizokuwa hizo wazitakazo miongoni mwa ishara nyingi zinazoonyesha usahihi wa yale aliyokuja nayo. Na ama ujinga wao, hilo ni kwamba hawakujua yenye masilahi yao na madhara yao. Kwa maana hakuna heri yoyote kwao katika kuwateremsha Malaika. Bali Mwenyezi Mungu hawateremshi Malaika isipokuwa kwa haki, ambapo hawezi pewa muhula yeyote ambaye hakuifuata na kujisalimisha kwayo. "Na hapo hawatapewa muhula;" yaani, wakati malaika watakapoteremka ikiwa hawakuamini na wala hawataamini. Basi kukawa kuitisha kwao kwamba malaika wateremshwe ni kujiharakishia wenyewe maangamio na maharibifu. Kwani, kuamini hakuko mikononi mwao, bali kuko mikononi mwa Mwenyezi Mungu. "Na lau kuwa tungeliwateremshia Malaika, na maiti wakawazungumzisha, na tukawakusanyia kila kitu mbele yao, bado wasingeliamini, isipokuwa Mwenyezi Mungu atake. Lakini wengi wao wamo ujingani."
#
{9} ويكفيهم من الآيات إنْ كانوا صادقين هذا القرآن العظيم، ولهذا قال هنا: {إنَّا نحنُ نزَّلْنا الذِّكْرَ}؛ أي: القرآن الذي فيه ذكرى لكلِّ شيء من المسائل والدلائل الواضحة، وفيه يتذكَّر مَنْ أراد التذكُّر. {وإنَّا له لحافظونَ}؛ أي: في حال إنزاله وبعد إنزاله؛ ففي حال إنزاله حافظون له من استراق كلِّ شيطان رجيم، وبعد إنزاله أودعه الله في قلب رسولِهِ واستَوْدَعَهُ في قلوب أمَّته وحفظَ الله ألفاظَه من التغيير فيها والزيادة والنقص ومعانيه من التبديل؛ فلا يحرِّف محرِّفٌ معنى من معانيه إلاَّ وقيَّض الله له من يبيِّن الحقَّ المبين، وهذا من أعظم آيات الله ونعمه على عباده المؤمنين، ومن حفظه أنَّ الله يحفظُ أهله من أعدائهم، ولا يسلِّط عليهم عدوًّا يجتاحُهم.
{9} Na ikiwa wao ni wakweli, Qur-ani hii Tukufu inawatosha kuwa ni ishara, na ndiyo maana akasema hapa, "Hakika Sisi ndio tuliouteremsha Ukumbusho huu;" yaani, Qur' ani, ambayo ndani yake kuna ukumbusho wa kila kitu miongoni mwa masuala, na ushahidi mbalimbali ulio wazi, na ndani yake anakumbuka anayetaka kukumbuka. "Na hakika Sisi ndio tutakaoulinda;" yaani, katika hali ya kuiteremsha na hata baada ya kuiteremsha. Katika hali ya kuiteremsha, tuliihifadhi kutokana na kusikilizwa na kila shetani aliyelaaniwa, na baada ya kuiteremsha, Mwenyezi Mungu aliitia ndani ya moyo wa Mtume wake na akaitia ndani ya nyoyo za umma wake. Na Mwenyezi Mungu aliyahifadhi maneno yake kutokana na mabadiliko, sawa iwe kwa kuongezea au kupungua, na pia kimehifadhiwa kutokana na kubadilishwa maana zake. Kwa hivyo mpotoshaji yeyote hawezi kupotosha maana miongoni mwa maana zake isipokuwa Mwenyezi Mungu humwekea mwenye kumubainishia haki iliyo wazi. Na hili ni katika ishara kubwa zaidi za Mwenyezi Mungu na neema zake kwa waja wake Waumini. Na katika kukihifadhi ni kwamba Mwenyezi Mungu huwalinda watu wa Qur-ani kutokana na maadui zao, na wala hawapi nguvu adui yeyote wa kuwaangamiza.
{وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِنْ قَبْلِكَ فِي شِيَعِ الْأَوَّلِينَ (10) وَمَا يَأْتِيهِمْ مِنْ رَسُولٍ إِلَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ (11) كَذَلِكَ نَسْلُكُهُ فِي قُلُوبِ الْمُجْرِمِينَ (12) لَا يُؤْمِنُونَ بِهِ وَقَدْ خَلَتْ سُنَّةُ الْأَوَّلِينَ (13)}.
10. Na hakika tulikwisha watumia Mitume mataifa ya mwanzo. 11. Na hakuwajia Mtume isipokuwa walikuwa wakimfanyia stihizai. 12. Na kama hivi ndivyo tunavyoyaingiza katika nyoyo za wakosefu. 13. Hawayaamini haya, na ilhali imekwisha wapitia desturi ya wa mwanzo.
#
{10} يقول تعالى لنبيِّه إذ كذبه المشركون: لم يزلْ هذا دأب الأمم الخالية والقرون الماضية، فقد أرْسَلْنا {قبلك في شيع الأولين}؛ أي: فرقهم وجماعتهم رسلاً.
{10} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Nabii wake,
wakati washirikina walipomkadhibisha: Hii haijaacha kuwa ndiyo desturi ya umma zilizopita na vizazi vilivyopita, kwani hakika tulituma "kabla yako katika madhehebu ya watu wa kale;" yaani, mgawanyiko wao na kikundi chao kama wajumbe.
#
{11} {وما يأتيهم من رسول}: يدعوهم إلى الحقِّ والهدى، {إلاَّ كانوا به يستهزئون}.
{11} "Na hakuwajia Mtume yeyote" akiwalingania kwenye haki na uwongofu, "isipokuwa walikuwa wakimfanyia stihizai."
#
{12 - 13} {كذلك نَسْلُكُه}؛ أي: ندخل التكذيب {في قلوب المجرمين}؛ أي: الذين وصفهم الظلم والبَهْت، عاقبناهم لما تشابهت قلوبُهم بالكفر والتكذيب تشابهت معاملتهم لأنبيائهم ورسلهم بالاستهزاء والسخرية وعدم الإيمان، ولهذا قال: {لا يؤمنون بِهِ وقد خَلَتْ سنَّةُ الأولين}؛ أي: عادة الله فيهم بإهلاك مَنْ لم يؤمنْ بآيات الله.
{12 - 13} "Na kama hivi ndivyo tunavyoyaingiza;" yaani, ndivyo tunavyoingiza kukadhibisha "katika nyoyo za wahalifu." Yaani, wale ambao sifa yao ni udhalimu na uongo mkubwa, tuliwaadhibu kwa maana mioyo yao ilifanana na ukafiri na kukadhibisha, kuamiliana kwao na manabii na mitume kulifanana na stihizai na masihara na kutoamini. Na ndiyo sababu akasema, "Hawayaamini haya, na ilhali imekwisha wapitia desturi ya wa mwanzo" ya Mwenyezi Mungu kuwaangamiza wale ambao hawakuamini ishara za Mwenyezi Mungu.
{وَلَوْ فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَابًا مِنَ السَّمَاءِ فَظَلُّوا فِيهِ يَعْرُجُونَ (14) لَقَالُوا إِنَّمَا سُكِّرَتْ أَبْصَارُنَا بَلْ نَحْنُ قَوْمٌ مَسْحُورُونَ (15)}.
14. Na lau tungeliwafungulia mlango huko mbinguni, wakawa wanapanda kupitia humo, 15.
Basi wangelisema: Hakika macho yetu yameleweshwa tu. Bali sisi wenyewe ni kaumu tuliofanyiwa uchawi.
#
{14 - 15} أي: ولو جاءتهم كلُّ آية عظيمة؛ لم يؤمنوا وكابروها، فَـ {لَو فَتَحْنا عليهم باباً من السماء}: فصاروا يعرجون فيه ويشاهدونه عياناً بأنفسهم؛ لقالوا من ظلمهم وعنادهم منكِرين لهذه الآية: {إنَّما سُكِّرَتْ أبصارُنا}؛ أي: أصابها سكر وغشاوة حتى رأينا ما لم نَرَ. {بل نحنُ قومٌ مسحورون}؛ أي: ليس هذا بحقيقة، بل هذا سحرٌ. وقوم وصلت بهم الحال إلى هذا الإنكار؛ فإنَّهم لا مطمع فيهم ولا رجاء.
{14 - 15} Yaani, ikiwa kila ishara kubwa ingewajia, hawangeamini na wangeifanyia kiburi. Kwa hivyo "lau tungeliwafungulia mlango huko mbinguni," wakawa wanapandia humo na wanauona kwa macho wenyewe, wangesema kwa sababu ya udhalimu wao na ukaidi wao wakiikataa ishara hii. "Hakika macho yetu yameleweshwa tu" na yamefunikwa mpaka tukaona kile ambacho hatukuona. "Bali sisi wenyewe ni kaumu tuliofanyiwa uchawi." Yaani, huu si uhakika, lakini huu ni uchawi. Na ikiwa kaumu itafikia hali yao kukataa hivi, basi hao hakuna tamaa wala matumaini juu ya wao kuamini.
Kisha akataja ishara zinazoonyesha haki waliyokuja nayo mitume, akasema:
{وَلَقَدْ جَعَلْنَا فِي السَّمَاءِ بُرُوجًا وَزَيَّنَّاهَا لِلنَّاظِرِينَ (16) وَحَفِظْنَاهَا مِنْ كُلِّ شَيْطَانٍ رَجِيمٍ (17) إِلَّا مَنِ اسْتَرَقَ السَّمْعَ فَأَتْبَعَهُ شِهَابٌ مُبِينٌ (18) وَالْأَرْضَ مَدَدْنَاهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنْبَتْنَا فِيهَا مِنْ كُلِّ شَيْءٍ مَوْزُونٍ (19) وَجَعَلْنَا لَكُمْ فِيهَا مَعَايِشَ وَمَنْ لَسْتُمْ لَهُ بِرَازِقِينَ (20)}
16. Na hakika tumeweka katika mbingu vituo vya sayari, na tumezipamba kwa wenye kuangalia. 17. Na tumezilinda kutokana na kila shetani aliyelaaniwa. 18. Isipokuwa mwenye kusikiliza kwa kuibia, naye hufuatwa na kijinga cha moto kilicho dhahiri. 19. Na ardhi tumeitandaza, na humo tumeweka milima madhubuti, na tumeotesha katika kila kitu kwa kiasi chake. 20. Na tumewajaalia humo vitu vya maisha yenu, na ya hao ambao nyinyi sio wenye kuwaruzuku.
#
{16} يقول تعالى مبيناً كمال اقتداره ورحمته بخلقه: {ولقد جَعَلْنا في السماء بروجاً}؛ أي: نجوماً كالأبراج والأعلام العظام يُهتدى بها في ظُلمات البرِّ والبحر، {وزيَّنَّاها للناظرين}: فإنَّه لولا النجوم؛ لما كان للسماء هذا المنظر البهي والهيئة العجيبة، وهذا مما يدعو الناظرين إلى التأمُّل فيها والنظر في معانيها والاستدلال بها على باريها.
{16} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema akibainisha ukamilifu wa uwezo wake na rehema yake kwa waja wake, "Na hakika tumeweka katika mbingu vituo vya sayari" kama minara na alama kubwa zenye kuongoza katika giza la nchi kavu na baharini, "na tumezipamba kwa wenye kuangalia." Kwa maana kama zisingekuwa nyota, basi mbingu isingekuwa na mwonekano huu mzuri, na umbo la ajabu. Na hili ni katika yenye kuwafanya watazamaji kutafakari juu yake, na kuzingatia maana zake, na kuzitumia kama ushahidi juu ya Muumba wake.
#
{17} {وحَفِظناها من كلِّ شيطان رجيم}: إذا استرق السمع؛ اتَّبعته الشهبُ الثواقب، فبقيت السماء ظاهرها مجمّلٌ بالنجوم النيرات، وباطنها محروسٌ ممنوعٌ من الآفات.
{17} "Na tumezilinda kutokana na kila shetani aliyelaaniwa," anaposikiliza kwa kuiba, mara hufuatwa na kimondo kinachong'aa. Basi mbingu zikabakia kuwa na muonekano wa nje mzuri kwa nyota angavu, na zikawa zimelindwa kwa ndani yake dhidi ya majanga.
#
{18} {إلا من استرق السمع}؛ أي: [إلاّ] في بعض الأوقات قد يسترق بعضُ الشياطين السمع بخفية واختلاس. {فأتْبَعَهُ شهابٌ مبينٌ}؛ أي: بيِّن منير يقتله أو يخبله؛ فربما أدركه الشهاب قبل أن يوصِلَها الشيطان إلى وليِّه فينقطع خبر السماء عن الأرض، وربَّما ألقاها إلى وليِّه قبل أن يدرِكَه الشهاب، فيضمُّها، ويكذبُ معها مائة كذبة، ويستدلُّ بتلك الكلمة التي سُمعت من السماء.
{18} "Isipokuwa mwenye kusikiliza kwa kuibia;" yaani,
[isipokuwa] katika nyakati zingine, baadhi ya mashetani wanaweza kusikiliza kisiri na kuiba. "Naye hufuatwa na kijinga cha moto kilicho dhahiri" chenye kuangaza na kinachomuua au kumharibu. Na kimondo kinaweza kumkuta shetani kabla hajamfikishia rafiki yake, kwa hivyo habari za mbinguni zikawa hazikufika katika ardhi. Na huenda akamfikishia rafiki yake katika ardhi kabla hajapigwa na kimondo, kwa hivyo anaijumuisha habari hiyo na kusema uongo mia moja pamoja nayo na akatumia neno hilo lililosikiwa kutoka mbinguni kama ushahidi.
#
{19} {والأرض مددناها}؛ أي: وسعناها سعة يتمكَّن الآدميون والحيوانات كلُّها من الامتداد بأرجائها والتناول من أرزاقها والسكونِ في نواحيها. {وألقَيْنا فيها رواسيَ}؛ أي: جبالاً عظاماً تحفظ الأرض بإذن الله أن تميدَ وتثبِّتها أن تزول. {وأنبَتْنا فيها من كلِّ شيءٍ موزونٍ}؛ أي: نافع متقوَّم يضطرُّ إليه العباد والبلاد ما بين نخيل وأعناب وأصناف الأشجار وأنواع النبات والمعادن.
{19} "Na ardhi tumeitandaza;" yaani, tumeipanua kwa namna ambayo wanaweza wanadamu na wanyama wote kuenea katika pande zake na kula katika riziki zake na kutulia katika pande zake. "Na humo tumeweka milima madhubuti" mikubwa yenye kuhifadhi dunia kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, ili isiyumbe na ili kuiimarisha isiondoke. "Na tumeotesha katika kila kitu kwa kiasi chake," chenye kunufaisha kama chakula ambacho waja wanakihitaji zaidi na hata nchi kama vile mitende, zabibu, na aina mbalimbali za miti, aina mbalimbali za mimea, na madini.
#
{20} {وجعلنا لكم فيها معايش}: من الحرث ومن الماشية ومن أنواع المَكاسب والحِرَف، {ومَنْ لستم له برازقين}؛ أي: أنعمنا عليكم بعبيدٍ وإماءٍ وأنعامٍ لنفعكم ومصالحكم، وليس عليكم رزقُها، بل خوَّلكم الله إيَّاها، وتكفَّل بأرزاقها.
{20} "Na tumewajaalia humo vitu vya maisha yenu" kama vile ukulima, mifugo, na aina mbalimbali za kuchuma na kazi, "na ya hao ambao nyinyi sio wenye kuwaruzuku." Yaani, tumewaneemesha kwa kuwapa watumwa, wajakazi, wanyama hoa kwa ajili ya faida yenu na masilahi yenu, na wala si juu yenu kuwaruzuku. Lakini Mwenyezi Mungu amewapa hao na akadhamini kuwaruzuku.
{وَإِنْ مِنْ شَيْءٍ إِلَّا عِنْدَنَا خَزَائِنُهُ وَمَا نُنَزِّلُهُ إِلَّا بِقَدَرٍ مَعْلُومٍ (21)}
21. Na hakuna chochote ila asili yake inatokana na Sisi; wala hatukiteremshi isipokuwa kwa kipimo maalumu.
#
{21} أي: جميع الأرزاق وأصناف الأقدار لا يملِكُها أحدٌ إلاَّ الله؛ فخزائِنُها بيده، يعطي مَن يشاء ويمنع مَن يشاء بحسب حكمته ورحمته الواسعة. {وما ننزِّلُه}؛ أي: المقدَّر من كلِّ شيء من مطر وغيره، {إلاَّ بقدرٍ معلوم}: فلا يزيدُ على ما قدَّره الله، ولا ينقص منه.
{21} Yaani, riziki zote na aina zote za majaliwa hazimilikiwi isipokuwa na Mwenyezi Mungu tu. Hazina zake ziko mikononi Mwake, Yeye humpa amtakaye na humnyima amtakaye kulingana na hekima Yake na rehema yake pana. "Na hatukiteremshi;" yaani, kilichoandikwa nakupimwa katika mambo yote kama vile mvua na vinginevyo, "isipokuwa kwa kipimo maalumu." Kwa hivyo hawezi mja kuzidisha katika kile alichoandika Mwenyezi Mungu, wala hawezi kupunguza kwacho.
{وَأَرْسَلْنَا الرِّيَاحَ لَوَاقِحَ فَأَنْزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَسْقَيْنَاكُمُوهُ وَمَا أَنْتُمْ لَهُ بِخَازِنِينَ (22)}
22. Na tunazipeleka pepo za kupandishia, na tunateremsha kutoka mbinguni maji, kisha tukakunywesheni maji hayo. Wala si nyinyi mnayoyaweka.
#
{22} أي: وسخَّرنا الرياح رياح الرحمة تُلْقِحُ السحاب كما يُلْقِحُ الذكر الأنثى، فينشأ عن ذلك الماء بإذن الله، فيسقيه الله العبادَ ومواشيَهم وأرضَهم، ويُبقي في الأرض مدَّخراً لحاجاتهم وضروراتهم ما هو مقتضى قدرته ورحمته. {وما أنتم له بخازِنينَ}؛ أي: لا قدرة لكم على خزنِهِ وادِّخاره، ولكن الله يخزِنُه لكم ويَسْلُكُه ينابيع في الأرض رحمةً بكم وإحساناً إليكم.
{22} Yaani, tumezitiisha pepo, pepo za rehema ambazo ni za kupandishia mawingu kama vile mwanamume anavyomtungisha mwanamke mimba ili maji yatokane na hilo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawanywesha maji hayo waja wake, mifugo yao, na ardhi yao, na anayaacha katika ardhi yakiwa yamehifadhika humo kwa ajili ya mahitaji na mahitaji yao ya kawaida na ya lazima. Haya yote yanaashiria uwezo wake na rehema zake. "Wala si nyinyi mnayoyaweka." Yaani, hamna uwezo wa kuyaweka na kuyahifadhi. Lakini Mwenyezi Mungu anawawekea hayo kisha akayapitisha kwenye chemchemi katika ardhi kama rehema na hisani juu yenu.
{وَإِنَّا لَنَحْنُ نُحْيِي وَنُمِيتُ وَنَحْنُ الْوَارِثُونَ (23) وَلَقَدْ عَلِمْنَا الْمُسْتَقْدِمِينَ مِنْكُمْ وَلَقَدْ عَلِمْنَا الْمُسْتَأْخِرِينَ (24) وَإِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَحْشُرُهُمْ إِنَّهُ حَكِيمٌ عَلِيمٌ (25)}
23. Na hakika Sisi ndio tunaohuisha na tunaofisha. Na Sisi ndio Warithi. 24. Na hakika tunawajua waliotangulia katika nyinyi, na tunawajua waliobaki nyuma. 25. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye atakayewakusanya. Hakika Yeye ni Mwenye hekima, Mjuzi.
#
{23 - 25} أي: هو وحده لا شريك له الذي يحيي الخلق من العدم بعد أن لم يكونوا شيئاً مذكوراً، ويميتهم لآجالهم التي قدرها، {ونحن الوارثون}؛ كقوله: {إنا نحنُ نَرِثُ الأرضَ ومَنْ عليها وإلينا يُرْجَعون}: وليس ذلك بعزيز ولا ممتنع على الله؛ فإنه تعالى يعلم المستقدِمين من الخلق والمستأخِرين منهم، ويعلم ما تَنْقُصُ الأرض منهم وما تفرِّقُ من أجزائهم، وهو الذي قدرتُهُ لا يعجِزُها معجِزٌ، فيعيد عباده خلقاً جديداً، ويحشُرُهم إليه. {إنَّه حكيمٌ}: يضع الأشياء مواضعها، وينزِلُها منازِلَها، ويجازي كلَّ عامل بعمله: إن خيراً؛ فخير، وإن شرًّا؛ فشر.
{23 - 25} Yaani, yeye Mwenyezi Mungu ni mmoja, hana mshirika yeyote. Yeye ndiye huhuisha viumbe baada ya kwamba hawakuwepo na kwamba havikuwa chochote cha kutajwa. Naye ndiye huvifisha kwa muda wao ambao aliwaandikia, "na sisi ndio Warithi" kama anavyosema, "Hakika Sisi ndio tutakaoirithi ardhi na walio juu yake. Na kwetu watarejeshwa." Na hilo si gumu wala lisilowezekana kwa Mwenyezi Mungu. Kwa maana, Yeye Mtukufu, anajua waliotangulia katika viumbe na anajua waliobakia nyuma katika wao. Na Yeye anajua kila kinachopunguzwa na ardhi miongoni mwao, na kile kilichotengana katika viungo vyao. Naye ndiye hakuna mwenye kushinda uwezo wake, na atawarudisha viumbe wake katika umbile jipya, na atawakusanya kwake. "Hakika Yeye ni Mwenye hekima" Yeye huweka vitu mahali panapovistahiki, na huviteremsha katika daraja zake, na humlipa kila mtendaji kwa matendo yake, kama ni heri, basi kwa heri, na kama ni maovu, basi kwa maovu.
{وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ مِنْ صَلْصَالٍ مِنْ حَمَإٍ مَسْنُونٍ (26) وَالْجَانَّ خَلَقْنَاهُ مِنْ قَبْلُ مِنْ نَارِ السَّمُومِ (27) وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِنْ صَلْصَالٍ مِنْ حَمَإٍ مَسْنُونٍ (28) فَإِذَا سَوَّيْتُهُ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِنْ رُوحِي فَقَعُوا لَهُ سَاجِدِينَ (29) فَسَجَدَ الْمَلَائِكَةُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ (30) إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَى أَنْ يَكُونَ مَعَ السَّاجِدِينَ (31) قَالَ يَاإِبْلِيسُ مَا لَكَ أَلَّا تَكُونَ مَعَ السَّاجِدِينَ (32) قَالَ لَمْ أَكُنْ لِأَسْجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقْتَهُ مِنْ صَلْصَالٍ مِنْ حَمَإٍ مَسْنُونٍ (33) قَالَ فَاخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ (34) وَإِنَّ عَلَيْكَ اللَّعْنَةَ إِلَى يَوْمِ الدِّينِ (35) قَالَ رَبِّ فَأَنْظِرْنِي إِلَى يَوْمِ يُبْعَثُونَ (36) قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ الْمُنْظَرِينَ (37) إِلَى يَوْمِ الْوَقْتِ الْمَعْلُومِ (38) قَالَ رَبِّ بِمَا أَغْوَيْتَنِي لَأُزَيِّنَنَّ لَهُمْ فِي الْأَرْضِ وَلَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ (39) إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ الْمُخْلَصِينَ (40) قَالَ هَذَا صِرَاطٌ عَلَيَّ مُسْتَقِيمٌ (41) إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ إِلَّا مَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْغَاوِينَ (42) وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوْعِدُهُمْ أَجْمَعِينَ (43) لَهَا سَبْعَةُ أَبْوَابٍ لِكُلِّ بَابٍ مِنْهُمْ جُزْءٌ مَقْسُومٌ (44)}
26. Na hakika tulimuumba Mtu kwa udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura. 27. Naye Jini tulimuumba hapo kabla kutokana na moto wa upepo moto. 28.
Na Mola wako Mlezi alipowaambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura. 29. Basi nitakapomtengeneza sawasawa, na nikampulizia roho yangu, basi mmwangukie kumsujudia. 30. Basi Malaika wote pamoja walimsujudia. 31. Isipokuwa Iblisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na waliosujudu. 32.
(Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Iblisi! Una nini hata hukuwa pamoja na waliosujudu? 33.
Akasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliyemuumba kutokana na udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura. 34.
(Mwenyezi Mungu) akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umefukuziliwa mbali! 35. Na hakika juu yako ipo laana mpaka Siku ya Malipo. 36. Akasema
(Iblisi): Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watakapofufuliwa. 37.
(Mwenyezi Mungu) akasema: Hakika wewe ni katika waliopewa muhula. 38. Mpaka siku ya wakati maalumu. 39.
Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyokuwa umenitia makosani, basi hakika nitawapambia katika dunia na hakika nitawapoteza wote. 40. Isipokuwa waja wako walioteuliwa miongoni mwao. 41.
Akasema: Hii ni njia ya kujia kwangu iliyonyooka. 42. Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipokuwa wale wapotofu waliokufuata. 43. Na hakika Jahannamu ndipo mahali pao walipoahidiwa wote. 44. Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu waliotengewa.
Yeye Mtukufu anataja neema yake na wema wake kwa baba yetu Adam - amani iwe juu yake - na kile kilichotokea kutoka kwa adui yake, Iblisi. Na ndani yake kuna kututahadharisha kutokana na uovu wake na majaribu yake. Kwa hivyo, Yeye Mtukufu akasema:
#
{26} {ولقد خلقنا الإنسان}؛ أي: آدم عليه السلام {من صَلْصال من حَمَإٍ مسنونٍ}؛ أي: من طين قد يبس بعدما خُمِّرَ حتى صار له صَلْصَلَةٌ وصوتٌ كصوت الفخار. والحمأ المسنون: الطينُ المتغيِّر لونه وريحه من طول مكثه.
{26} "Na hakika tulimuumba mtu;" yaani, Adam - amani iwe juu yake - "kutokana na udongo unaotoa sauti" yaani, kutokana na udongo uliokauka baada ya kufunikwa hadi ukawa mkavu na wenye kutoa sauti kama ya kinamo. Na matope yaliyotiwa sura ni matope yaliyobadilika rangi na harufu yake kutokana na kukaa kwa muda mrefu.
#
{27} {والجانَّ}: وهو أبو الجنِّ؛ أي: إبليس، {خَلَقْناه من قبل}: خَلْقِ آدم، {من نار السَّموم}؛ أي: من النار الشديدة الحرارة.
{27} "Naye Jini" ambaye ndiye baba wa majini; yaani, Iblisi. "tulimuumba hapo kabla ya kumuumba Adam, "kutokana na moto wa upepo moto." Yaani, kutoka kwa moto mkali mno.
#
{28 - 29} فلما أراد الله خَلْقَ آدم؛ قال للملائكة: {إنِّي خالقٌ بشراً من صَلْصال من حمإٍ مَسْنونٍ. فإذا سوَّيْتُه}: جسداً تامًّا، {ونفختُ فيه من روحي فَقَعُوا له ساجدينَ}.
{28-29} Na Mwenyezi Mungu alipotaka kumuumba Adam, aliwaambia Malaika, "Mimi nitamuumba mtu kutokana na udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura. Basi nitakapomtengeneza sawasawa" katika kiwiliwili kikamilifu "na nikampulizia roho yangu, basi mmwangukie kumsujudia."
#
{30 - 31} فامتثلوا أمرَ ربِّهم، {فسجد الملائكةُ كلُّهم أجمعون}: تأكيدٌ بعد تأكيدٍ؛ ليدلَّ على أنه لم يتخلَّف منهم أحدٌ، وذلك تعظيماً لأمر الله وإكراماً لآدم حيث عَلِمَ ما لم يعلموا. {إلاَّ إبليسَ أبى أن يكونَ مع الساجدين}: وهذه أول عداوته لآدم وذرِّيَّته.
{30-31} Kwa hivyo, wakaitii amri ya Mola wao Mlezi "basi Malaika wote pamoja walimsujudia." Na huku ni kusisitiza baada ya kusisitiza ili kuonyesha kwamba hakuna hata mmoja wao aliyesalia nyuma. Na hilo lilikuwa kwa ajili ya kuitukuza na kuitii amri ya Mwenyezi Mungu na kumheshimu Adamu - amani iwe juu yake. Kwa maana alijua yale ambayo hawayakujua wao. "Isipokuwa Iblisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na waliosujudu." Na huu ndio mwanzo wa uadui wake kwa Adam na kizazi chake.
#
{32 - 33} {قال}: الله: {يا إبليسُ ما لك ألا تكون مع الساجدين. قال لم أكنْ لأسجدَ لبشرٍ خلقتَه من صلصال من حمإٍ مسنونٍ}: فاستكبر على أمر الله، وأبدى العداوة لآدم وذرِّيَّته، وأعجِبَ بعنصره، وقال: أنا خيرٌ من آدم.
{32 - 33} (Mwenyezi Mungu) "akasema: Ewe Iblisi! Una nini hata hukuwa pamoja na waliosujudu? Akasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliyemuumba kwa udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura." Basi akawa amefanya kiburi juu ya amri ya Mwenyezi Mungu, na akadhihirisha uadui kwa Adam na kizazi chake, na akajivuna na asili yake aliyotokana nayo, na akasema, "Mimi ni bora kuliko Adam."
#
{34 - 35} {قال} الله معاقباً له على كفره واستكباره: {فاخْرُجْ منها فإنَّك رجيمٌ}؛ أي: مطرود ومبعدٌ من كل خير، {وإنَّ عليك اللعنةَ}؛ أي: الذمَّ والعيب والبعد عن رحمة الله {إلى يوم الدين}. ففيها وما أشبهها دليلٌ على أنَّه سيستمرُّ على كفره وبعده من الخير.
{34 - 35} Mwenyezi Mungu "Akasema" akimwadhibu juu ya ukafiri wake na kiburi chake: "Basi toka humo, kwani hakika wewe umefukuziliwa mbali." Yaani, umefukuzwa na kuwekwa mbali na kila heri, "Na hakika juu yako ipo laana;" yaani, kukashifiwa, na kutokuwa na heshima, na kuwekwa mbali na rehema za Mwenyezi Mungu "mpaka Siku ya malipo." Na katika hili na mfano wake kuna ushahidi kwamba Iblisi ataendelea kukufuru na kuwa kwake mbali na heri.
#
{36 - 38} {قال ربِّ فأنْظِرْني}؛ أي: أمهِلْني {إلى يوم يُبْعَثونَ. قال فإنَّك من المُنْظَرينَ. إلى يوم الوقتِ المعلوم}: وليس إجابةُ الله لدعائِهِ كرامةً في حقِّه، وإنما ذلك امتحانٌ وابتلاءٌ من الله له وللعباد؛ ليتبيَّن الصادق الذي يطيع مولاه دون عدوه ممن ليس كذلك، ولذلك حذَّرنا منه غاية التحذير، وشرح لنا ما يريده منَّا.
{36-38} "Akasema
(Iblisi): Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watakapofufuliwa.
(Mwenyezi Mungu) akasema: Hakika wewe ni katika waliopewa muhula. Mpaka siku ya wakati maalumu." Na Mwenyezi Mungu kuitikia dua yake siyo heshima aliyompa, lakini huo ni mtihani na majaribio kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwake na kwa waja wake, ili apambanuke mkweli ambaye anamtii Mola wake na hamtii adui yake ambaye siyo hivyo. Na ndio maana akatutahadharisha kutokana naye kwa tahadharisho kubwa zaidi, na akatuelezea kile anachotaka kutoka kwetu.
#
{39} {قال ربِّ بما أغويتني لأزيِّنَنَّ لهم في الأرض}؛ أي: أزيِّن لهم الدنيا، وأدعوهم إلى إيثارها على الأخرى، حتى يكونوا منقادين لكلِّ معصيةٍ، {ولأغوِيَنَّهم أجمعين}؛ أي: أصدُّهم كلَّهم عن الصراط المستقيم، {إلاَّ عبادَك منهم المخلَصين}؛ أي: الذين أخلصتهم، واجتبيتهم لإخلاصهم وإيمانهم وتوكلهم.
{39} "Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyokuwa umenitia makosani, basi hakika nitawapambia katika dunia." Yaani, ninawapamba dunia na kuwaita kuipendelea zaidi ya akhera ili wawe wa kufuata kila maasia "na hakika nitawapoteza wote." Yaani, nitawazuia wote kutokana na njia iliyonyooka, "Isipokuwa waja wako walioteuliwa miongoni mwao;" yaani, wale ambao amewateua, na kuwachagua kwa sababu ya unyoofu wao, imani yao, na kutegemea kwao.
#
{40} قال الله: {هذا صراطٌ عليَّ مستقيمٌ}؛ أي: معتدلٌ موصلٌ إليَّ وإلى دار كرامتي.
{40} Mwenyezi Mungu akasema, "Hii ni njia ya kujia kwangu iliyonyooka;" yenye kufikisha kwangu na kwa nyumba ya utukufu wangu.
#
{41} {إنَّ عبادي ليس لك عليهم سلطانٌ}: تميلهم به إلى ما تشاء من أنواع الضَّلالات بسبب عبوديَّتهم لربِّهم وانقيادهم لأوامره، أعانهم الله وعصمهم من الشيطان.
{41} "Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao" ya kuwaelekeza utakavyo miongoni mwa aina za upotovu kwa maana wao humfanyia tu Bwana wao Mlezi na Mola wao ibada na kufuata maamrisho Yake. Mwenyezi Mungu aliwasaidia na kuwalinda kutokana na Shetani.
#
{42} {إلاَّ من اتَّبعك}: فرضي بولايتك وطاعتك بدلاً من طاعة الرحمن، {من الغاوينَ}: والغاوي ضدُّ الراشد؛ فهو الذي عرف الحقَّ وتركه، والضالُّ الذي تركه من غير علم منه به.
{42} "Isipokuwa wale wenye kukufuata" na akaridhia kukufanya rafiki na kukutii badala ya kumtii Mwingi wa rehema, "miongoni mwa wapotofu." Naye ni mwenye kujua haki lakini akaiacha.
#
{43} {وإنَّ جهنَّم لَمَوْعِدُهم أجمعين}؛ أي: إبليس وجنوده.
{43} " Na hakika Jahannamu ndipo mahali pao walipoahidiwa wote;" yaani, Iblisi na majeshi wake.
#
{44} {لها سبعةُ أبوابٍ}: كل باب أسفل من الآخر. {لكلِّ باب منهم}؛ أي: من أتباع إبليس {جزءٌ مقسومٌ}: بحسب أعمالهم؛ قال تعالى: {فَكُبْكِبوا فيها هم والغاوونَ وجنودُ إبليسَ أجمعونَ}.
{44} "Ina milango saba," kila mlango uko chini ye mwingine. "Na kwa kila mlango iko sehemu waliyotengewa" wafuasi wa Iblis kulingana na matendo yao. Yeye Mtukufu alisema, "Basi watavurumizwa humo wao na hao wakosefu na majeshi ya Ibilisi yote."
Na Yeye Mtukufu alipotaja yale aliyowaandalia maadui zake, wafuasi wa Iblisi ya mateso na adhabu kali, akataja yale aliyowaandalia marafiki zake miongoni mwa fadhila kubwa na neema ya kudumu, akasema:
{إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ (45) ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ آمِنِينَ (46) وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِمْ مِنْ غِلٍّ إِخْوَانًا عَلَى سُرُرٍ مُتَقَابِلِينَ (47) لَا يَمَسُّهُمْ فِيهَا نَصَبٌ وَمَا هُمْ مِنْهَا بِمُخْرَجِينَ (48) نَبِّئْ عِبَادِي أَنِّي أَنَا الْغَفُورُ الرَّحِيمُ (49) وَأَنَّ عَذَابِي هُوَ الْعَذَابُ الْأَلِيمُ (50)}.
45. Hakika wachamungu watakuwa katika Mabustani na chemchemi. 46.
(Wataambiwa:) Ingieni humo kwa salama na amani. 47. Na tutaondoa chuki iliyokuwa vifuani mwao, wawe ndugu, juu ya viti vya enzi huku wameelekeana. 48. Humo hayatawagusa machovu, wala hawatatolewa humo. 49. Wape habari waja wangu ya kwamba Mimi ndiye Mwenye kusamehe zaidi, Mwingi wa kurehemu. 50. Na kwamba adhabu yangu ndiyo adhabu iliyo chungu!
#
{45} يقول تعالى: {إنَّ المتَّقين}: الذين اتَّقوا طاعة الشيطان وما يدعوهم إليه من جميع الذنوب والعصيان، {في جنَّاتٍ وعيون}: قد احتوت على جميع الأشجار، وأينعت فيها جميعُ الثمار اللذيذة في جميع الأوقات.
{45} Yeye Mtukufu anasema, "Hakika wachamungu" ambao walijiepusha na kumtii Shetani na yale anayowaitia miongoni mwa madhambi yote na maasia, "watakuwa katika Mabustani na chemchemi" yenye miti yote, na matunda yote matamu yaliyoning'inia chini katika kila wakati.
#
{46} ويقال لهم حال دخولها: {ادخُلوها بسلام آمنينَ}: من الموت والنوم والنَّصَب واللُّغوب وانقطاع شيء من النعيم الذي هم فيه أو نقصانه ومن المرض والحزن والهمِّ وسائر المكدرات.
{46} Na wataambiwa watakapokuwa wanaingia humo, "Ingieni humo kwa salama na amani" kutokana na kifo, usingizi, taabu, machovu, na kukatika kwa chochote katika neema waliyomo, au kupunguka kwake kwa sababu ya ugonjwa, huzuni, wasiwasi na shida zinginezo zote.
#
{47} {ونزعنا ما في صدورهم من غِلٍّ}: فتبقى قلوبُهم سالمةً من كلِّ غلٍّ وحسدٍ متصافية متحابَّة، {إخواناً على سُرُر متقابلين}: دلَّ ذلك على تزاورهم واجتماعهم وحسن أدبهم فيما بينهم في كون كلٍّ منهم مقابلاً للآخر لا مستدبراً له، متكئين على تلك السُّرر المزيَّنة بالفرش واللؤلؤ وأنواع الجواهر.
{47} "Na tutaondoa chuki iliyokuwa vifuani mwao" na mioyo yao itabakia kuwa salama kutokana na kila chuki, husuda iwe safi, yenye kupendana, "wawe ndugu, juu ya viti vya enzi huku wameelekeana." Hili linaonyesha kuwa watatembeleana na kukusanyika, na adabu zao nzuri kati yao kwa kuwa kila mmoja wao atakuwa anakabiliana na mwenzake bila ya kumpa mgongo, huku wameegemea kwenye vitanda hivyo vilivyopambwa kwa matandiko, lulu, na aina mbalimbali za johari.
#
{48} {لا يَمَسُّهم فيها نصبٌ}: لا ظاهرٌ ولا باطنٌ، وذلك لأنَّ الله يُنشئهم نشأةً وحياةً كاملةً لا تقبل شيئاً من الآفات. {وما هم منها بمُخْرَجين}: على سائر الأوقات.
{48} "Humo hayatawagusa machovu yoyote" si kwa dhahiri wala kwa ndani, kwa sababu Mwenyezi Mungu anawaumba kuumbwa kwingine na uhai kamili ambao haukubali majanga yoyote. " Wala hawatatolewa humo" katika nyakati zote.
#
{49} ولما ذكر ما يوجب الرغبة والرهبة من مفعولات الله من الجنة والنار؛ ذكر ما يوجب ذلك من أوصافه تعالى، فقال: {نبِّئ عبادي}؛ أي: أخبرهم خبراً جازماً مؤيداً بالأدلَّة، {أني أنا الغفورُ الرحيم}: فإنَّهم إذا عرفوا كمال رحمته ومغفرته؛ سعوا بالأسباب الموصلة لهم إلى رحمته، وأقلعوا عن الذُّنوب وتابوا منها؛ لينالوا مغفرتَهُ.
{49} Na alipotaja mambo yenye kusababisha kutamani na kuhofu ya matendo ya Mwenyezi Mungu ya Pepo na Moto, akataja yenye kusababisha hayo miongoni mwa sifa zake yeye Mtukufu, "Wape habari waja wangu" habari ya uhakika inayounga mkono ushahidi mbalimbali, "kwamba Mimi ndiye Mwenye kusamehe zaidi, Mwingi wa kurehemu." Kwa maana, wakijua ukamilifu wa rehema yake na msamaha Wake, watazifanyia bidii sababu za kuwafikisha katika rehema Yake, na wataacha dhambi na kutubu kutokana nazo ili wapate msamaha Wake.
#
{50} ومع هذا؛ فلا ينبغي أن يتمادى بهم الرجاءُ إلى حال الأمن والإدلال؛ فنبئهم {أنَّ عذابي هو العذابُ الأليمُ}؛ أي: لا عذاب في الحقيقة إلاَّ عذابُ الله الذي لا يقادَرُ قَدْره ولا يُبْلَغ كُنْهه، نعوذ به من عذابه؛ فإنهم إذا عرفوا أن لا يعذِّبَ عذابَه أحدٌ ولا يوثِقُ وَثاقَهُ أحدٌ؛ حذروا وأبعدوا عن كلِّ سبب يوجب لهم العقاب.
فالعبد ينبغي أن يكون قلبه دائماً بين الخوف والرجاء والرغبة والرهبة؛ فإذا نظر إلى رحمة ربِّه ومغفرته وجوده وإحسانه؛ أحدث له ذلك الرجاءَ والرغبةَ، وإذا نظر إلى ذنوبه وتقصيره في حقوق ربِّه؛ أحدث له الخوفَ والرهبة والإقلاع عنها.
{50} Lakini pamoja na hayo, haifai waendelee kutumaini sana kwao mpaka wakawa katika hali ya usalama na kulegea, kwa hivyo waambie, "kwamba adhabu yangu ndiyo adhabu iliyo chungu!" Yaani, hakuna adhabu kwa uhakika isipokuwa adhabu ya Mwenyezi Mungu, ambayo haiwezi kupimwa kiasi chake wala kufikia kujua uhalisi wake. Tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na adhabu yake. Kwa maana, wakijua kwamba hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake. Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake, wanajitahadharisha na kuwa mbali sana na kila njia ya kuwasababishia adhabu. Kwa hivyo, moyo wa mja unapaswa daima kuwa kati ya hofu na matumaini. Anapoangalia rehema ya Mola wake Mlezi, msamaha wake, ukarimu wake mkubwa, na wema wake, hayo yanamfanya kuwa na matumaini na kutaka yaliyo kwa Mwenyezi Mungu. Na akiangalia dhambi zake na kutotekeleza vyema yampasayo katika haki za Mola wako Mlezi, hayo yanamfanya kuhofu na kuogopa, na kuachana nayo.
{وَنَبِّئْهُمْ عَنْ ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ (51) إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا قَالَ إِنَّا مِنْكُمْ وَجِلُونَ (52) قَالُوا لَا تَوْجَلْ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ (53) قَالَ أَبَشَّرْتُمُونِي عَلَى أَنْ مَسَّنِيَ الْكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ (54) قَالُوا بَشَّرْنَاكَ بِالْحَقِّ فَلَا تَكُنْ مِنَ الْقَانِطِينَ (55) قَالَ وَمَنْ يَقْنَطُ مِنْ رَحْمَةِ رَبِّهِ إِلَّا الضَّالُّونَ (56)}.
51. Na wape habari za wageni wa Ibrahim. 52.
Walipoingia kwake na wakasema: Salama! Yeye akasema: Hakika sisi tunawaogopa. 53.
Wakasema: Usiogope. Hakika, Sisi tunakubashiria kijana mwenye elimu mno. 54.
Akasema: Mnanibashiria nami uzee umenishika! Basi kwa njia gani mnanibashiria? 55.
Wakasema: Tunakubashiria kwa haki, basi usiwe miongoni mwa wanaokata tamaa. 56.
Akasema: Na ni nani anayekata tamaa na rehema ya Mola wake Mlezi isipokuwa wapotovu?
#
{51} يقول تعالى لنبيِّه محمد - صلى الله عليه وسلم -: {ونبِّئْهم عن ضيفِ إبراهيم}؛ أي: عن تلك القصَّة العجيبة؛ فإنَّ في قصِّك عليهم أنباء الرسل وما جرى لهم ما يوجب لهم العبرةَ والاقتداء بهم، خصوصاً إبراهيم الخليل، الذي أمرنا اللهُ أن نتَّبِعَ ملَّته، وضيفه هم الملائكة الكرام، أكْرَمَهُ الله بأنْ جَعَلَهم أضيافه.
{51} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake - "Na wape habari za wageni wa Ibrahim;" yaani, juu ya kisa hiki cha ajabu. Kwa sababu katika kuwasimulia habari za Mitume na yaliyowapata, ambayo yanawafanya kuzingatia na kuwaiga, hasa Ibrahim Al-Khalil, ambaye Mwenyezi Mungu alituamrisha kufuata mila yake, na wageni wake ambao walikuwa malaika watukufu ambao Mwenyezi Mungu alimtukuza kwa kuwafanya kuwa wageni wake.
#
{52} {إذ دخلوا عليه فقالوا سلاماً}؛ أي: سلَّموا عليه فردَّ عليهم، {قال إنَّا منكم وَجِلونَ}؛ أي: خائفون؛ لأنَّه لما دخلوا عليه، وحسبهم ضيوفاً؛ ذهب مسرعاً إلى بيته، فأحضر لهم ضيافتهم عجلاً حنيذاً، فقدَّمه إليهم، فلما رأى أيدِيَهم لا تصِلُ إليه؛ خاف منهم أن يكونوا لصوصاً أو نحوهم فقالوا له:
{52} "Walipoingia kwake na wakasema: Salama!" yaani, walimsalimia naye akawajibu salamu yao,
"akasema: Hakika sisi tunawaogopa." Kwa sababu walipoingia kwake na akadhani kwamba ni wageni, akaenda haraka nyumbani kwake na akawaletea ndama wa kuchomwa na akamweka mbele yao. Kwa hivyo alipoona mikono yao haimfikii, akawaogopa akidhani huenda ni wezi au mfano wao,
basi wakamwambia:
#
{53} {لا تَوْجَلْ إنَّا نبشِّرك بغلام عليم}: وهو إسحاق عليه الصلاة والسلام. تضمنت هذه البشارة بأنَّه ذكرٌ لا أنثى. {عليم}؛ أي: كثير العلم. وفي الآية الأخرى: {وبشَّرْناه بإسحاقَ نبيًّا من الصَّالحينَ}.
{53} "Usiogope. Hakika, Sisi tunakubashiria kijana mwenye elimu mno." Yaani, Is-haq rehema na amani ziwe juu yake. Bishara hii ilijumuisha kwamba atakuwa wa kiume, si wa kike. Katika aya nyingine, alisema, "Na tukambashiria kuzaliwa Is-haq, naye ni Nabii miongoni mwa walio wema."
#
{54} {قال} لهم متعجِّباً من هذه البشارة: {أبشَّرْتُموني}: بالولد {على أن مَسَّنِيَ الكِبَرُ}: وصار نوع إياس منه. {فبم تبشِّرونِ}؛ أي: على أيِّ وجهٍ تبشِّرون وقد عدمت الأسباب؟!
{54} "Akasema" akiwaambia kwa kushangazwa na bishara hii, "Mnanibashiria" mwana "nami uzee umenishika!" Hata ikawa aina ya kukata tamaa ya kuzaa. "Basi kwa njia gani mnanibashiria?" Yaani, ni kwa njia gani mnanibashiria wakati hakuna sababu za hilo?
#
{55} {قالوا بشَّرْناك بالحقِّ}: الذي لا شكَّ فيه؛ لأنَّ الله على كلِّ شيءٍ قديرٌ، وأنتم بالخصوص يا أهل هذا البيت، رحمة الله وبركاته عليكم؛ فلا يُسْتَغْرَبُ فضل الله وإحسانُه إليكم. {فلا تَكُنْ من القانطينَ}: الذين يستبعدون وجودَ الخير، بل لا تزال راجياً لفضل الله وإحسانِهِ وبرِّه وامتنانه.
{55} "Wakasema: Tunakubashiria kwa haki" isiyokuwa na shaka yoyote. Kwa sababu Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu, na hasa nyinyi, enyi watu wa nyumba hii - rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yenu - haiwezi ikawa fadhila ya Mwenyezi Mungu na wema wake juu yenu kuwa kitu cha ajabu. "Basi usiwe miongoni mwa wanaokata tamaa," ambao huona kwamba heri haiwezi kupatikana. Bali usiache kuendelea kutumaini fadhila ya Mwenyezi Mungu, hisani yake, wema wake, na neema yake.
#
{56} فأجابهم إبراهيمُ بقوله: {ومَن يَقْنَطُ من رحمةِ ربِّه إلاَّ الضَّالُّون}: الذين لا علم لهم بربِّهم وكمال اقتداره، وأما مَنْ أنعم الله عليه بالهداية والعلم العظيم؛ فلا سبيل إلى القنوط إليه؛ لأنَّه يعرف من كَثْرة الأسباب والوسائل والطرق لرحمة الله شيئاً كثيراً.
ثم لما بشَّروه بهذه البشارة؛ عَرَفَ أنَّهم مرسلون لأمرٍ مهمٍّ.
{56} Kwa hivyo, Ibrahim akawajibu akisema, "Na ni nani anayekata tamaa na rehema ya Mola wake Mlezi isipokuwa wapotovu," ambao hawamjui Mola wao Mlezi na ukamilifu wa uwezo wake? Na ama yule ambaye Mwenyezi Mungu amemneemesha na uwongofu na elimu kubwa, basi hakuna njia ya kukata tamaa naye, kwa sababu anajua kutokana na wingi wa sababu, mbinu, na njia za rehema za Mwenyezi Mungu nyingi. Kisha, walipombashiria bishara hii, akajua kwamba wao ni wajumbe kwa ajili ya jambo muhimu.
{قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ (57) قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَى قَوْمٍ مُجْرِمِينَ (58) إِلَّا آلَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمْ أَجْمَعِينَ (59) إِلَّا امْرَأَتَهُ قَدَّرْنَا إِنَّهَا لَمِنَ الْغَابِرِينَ (60) فَلَمَّا جَاءَ آلَ لُوطٍ الْمُرْسَلُونَ (61) قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ مُنْكَرُونَ (62) قَالُوا بَلْ جِئْنَاكَ بِمَا كَانُوا فِيهِ يَمْتَرُونَ (63) وَأَتَيْنَاكَ بِالْحَقِّ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ (64) فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِنَ اللَّيْلِ وَاتَّبِعْ أَدْبَارَهُمْ وَلَا يَلْتَفِتْ مِنْكُمْ أَحَدٌ وَامْضُوا حَيْثُ تُؤْمَرُونَ (65) وَقَضَيْنَا إِلَيْهِ ذَلِكَ الْأَمْرَ أَنَّ دَابِرَ هَؤُلَاءِ مَقْطُوعٌ مُصْبِحِينَ (66) وَجَاءَ أَهْلُ الْمَدِينَةِ يَسْتَبْشِرُونَ (67) قَالَ إِنَّ هَؤُلَاءِ ضَيْفِي فَلَا تَفْضَحُونِ (68) وَاتَّقُوا اللَّهَ وَلَا تُخْزُونِ (69) قَالُوا أَوَلَمْ نَنْهَكَ عَنِ الْعَالَمِينَ (70) قَالَ هَؤُلَاءِ بَنَاتِي إِنْ كُنْتُمْ فَاعِلِينَ (71) لَعَمْرُكَ إِنَّهُمْ لَفِي سَكْرَتِهِمْ يَعْمَهُونَ (72) فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ مُشْرِقِينَ (73) فَجَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِنْ سِجِّيلٍ (74) إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِلْمُتَوَسِّمِينَ (75) وَإِنَّهَا لَبِسَبِيلٍ مُقِيمٍ (76) إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَةً لِلْمُؤْمِنِينَ (77)}.
57.
Akasema: Hebu mna jambo gani, enyi wajumbe? 58.
Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya wahalifu! 59. Isipokuwa watu wa familia ya Lut'. Bila ya shaka sisi tutawaokoa hao wote. 60. Isipokuwa mkewe. Tumekwisha pitisha kwamba huyo hakika atakuwa miongoni mwa watakaobakia nyuma. 61. Basi wale wajumbe walipowajia watu wa familia ya Lut'. 62.
(Lut') Alisema: Hakika nyinyi ni kaumu msiojulikana. 63.
Wakasema: Bali sisi tumekuletea yale waliyokuwa wakiyafanyia shaka. 64. Na tumefika kwako kwa Haki, na hakika sisi ni wakweli. 65. Basi ondoka na ahali zako usiku ungalipo, nawe ufuate nyuma yao, wala yeyote kati yenu asigeuke nyuma. Na mwende huko mnakoamrishwa. 66. Na tukamfunulia hukumu hiyo, ya kwamba hata wa mwisho wao hao ikifika asubuhi atakuwa amekwisha katiliwa mbali. 67. Na wakaja watu wa mji ule huku wamefurahi. 68.
Akasema: Hakika hawa ni wageni wangu. Basi msinifedheheshe. 69. Na mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi. 70.
Wakasema: Kwani hatukukukataza
(kuwakaribisha) walimwengu hawa? 71. Akasema, "Hawa binti zangu, ikiwa nyinyi ni watendaji." 72. Ninaapa kwa umri wako! Hakika hao walikuwa katika ulevi wao, wakihangaika ovyo. 73. Basi ukelele ukawatwaa wakipambaukiwa. 74. Kwa hivyo, tukaugeuza mji huo juu chini, na tukawanyeshea mvua ya mawe ya udongo wa kutoka Motoni. 75. Hakika katika hayo zipo ishara kwa wanaotafakari na kuzingatia. 76. Na hakika miji hii ipo kwenye njia inayopitiwa. 77. Hakika katika hayo ipo ishara kwa Waumini.
#
{57} أي: {قال} الخليلُ عليه السلام للملائكة: {فما خطبكُم أيُّها المرسلون}؛ أي: ما شأنكم؟ ولأيِّ شيءٍ أرسِلْتُم؟!
{57} Yaani, Ibrahim Al-Khalil - amani iwe juu yake - "aliwaambia" malaika, "Hebu mna jambo gani, enyi wajumbe?"
#
{58} {قالوا إنَّا أرسِلْنا إلى قوم مجرِمين}؛ أي: كثر فسادُهم وعَظُم شرُّهم لنعذِّبَهم ونعاقبهم.
{58} "Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya wahalifu!" Yaani, wale ambao uharibifu wao umekithiri, na uovu wao ni mkubwa sana, ili tuwatese na kuwaadhibu.
#
{59 - 60} {إلاَّ آلَ لوطٍ}؛ أي: إلاَّ لوطاً وأهله، {إلاَّ امرأتَهُ قدَّرْنا أنَّها لَمِنَ الغابرين}؛ أي: الباقين بالعذاب، وأما لوطٌ؛ فَسَنُخْرِجَنَّه وأهله وننجِّيهم منها. فجعل إبراهيم يجادل الرسل في إهلاكهم ويراجعهم، فقيل له: {يا إبراهيمُ أعْرِضْ عن هذا إنَّه قد جاء أمُر ربِّك وإنَّهم آتيهم عذابٌ غير مردودٍ}. فذهبوا منه.
{59 - 60} "Isipokuwa watu wa familia ya Lut';" yaani, isipokuwa Lut' na watu wa familia yake, Isipokuwa mkewe. Tumekwisha pitisha kwamba huyo hakika atakuwa miongoni watakaobakia nyuma" katika adhabu. Na ama Lut', hakika yeye na familia yake tutawatoa na kuwaokoa kutoka humo. Basi Ibrahim akawa anajadiliana na wajumbe hao juu ya kuwaangamiza na kuwarai, lakini akaambiwa, "Ewe Ibrahim! Wachilia mbali haya! Hakika amri ya Mola wako Mlezi imekwisha kuja, na hakika hao itawafikia adhabu isiyorudi nyuma." Basi wakaondoka hapo kwake.
#
{61 - 62} {فلما جاء آلَ لوطٍ المرسلونَ قال} لهم لوط: {إنَّكم قوم مُنْكَرونَ}؛ أي: لا أعرفكم، ولا أدري من أنتم.
{61 - 62} "Basi wale wajumbe walipowajia watu wa familia ya Lut'.
(Lut') akasema: "Hakika nyinyi ni kaumu msiojulikana." Yaani, siwajui, sijui nyinyi ni akina nani.
#
{63} فَـ {قالوا بل جِئْناك بما كانوا فيه يَمْتَرون}؛ أي: جئناك بعذابهم الذي كانوا يشكُّون فيه ويكذِّبونك حين تَعِدُهم به.
{63} Kwa hivyo,
"Wakasema: Bali sisi tumekuletea yale waliyokuwa wakiyafanyia shaka." Yaani, tumekujia na adhabu yao, ambayo walikuwa wakiishuku, na wanakukadhibisha unapowaahidi kuja kwake.
#
{64} {وأتيناك بالحقِّ}: الذي ليس بالهزل. {وإنَّا لصادقونَ}: فيما قلنا لك.
{64} "Na tumefika kwako kwa Haki" ambayo siyo mzaha. "Na hakika sisi ni wakweli," katika haya tuliyokuambia.
#
{65} {فأسْرِ بأهلك بقِطْع من الليل}؛ أي: في أثنائه حين تنام العيون ولا يدري أحدٌ عن مَسْراك. {ولا يَلْتَفِتْ منكم أحدٌ}؛ أي: بل بادروا وأسرعوا، {وامْضوا حيثُ تُؤْمَرون}: كأنَّ معهم دليلاً يدلُّهم على أين يتوجَّهون.
{65} "Basi ondoka na ahali zako usiku ungalipo;" yaani, wakati watakapokuwa watu wanalala na hakuna yeyote anayejua kuhusu kuondoka kwako. "Wala yeyote kati yenu asigeuke nyuma;" yaani, fanyeni halahala na harakisheni, "Na mwende huko mnakoamrishwa," kana kwamba walikuwa na mwelekezi aliyekuwa anawaelekeza pa kuelekea.
#
{66} {وقضَيْنا إليه ذلك}؛ أي: أخبرناه خبراً لا مَثْنَوِيَّة فيه، {أنَّ دابرَ هؤلاء مقطوعٌ مصبحينَ}؛ أي: سيصبِّحهم العذابُ الذي يجتاحهم، ويستأصلهم.
{66} "Na tukamfunulia hukumu hiyo" kwa habari isiyo na shaka yoyote, "ya kwamba hata wa mwisho wao hao ikifika asubuhi atakuwa amekwisha katiliwa mbali." Yaani, itawafikia asubuhi adhabu itakayowafagilia mbali na kuwaondoa kabisa.
#
{67 - 69} {وجاء أهلُ المدينة}؛ أي: المدينة التي فيها لوطٌ، {يستبشرونَ}؛ أي: يبشِّر بعضُهم بعضاً بأضياف لوطٍ وصباحةِ وجوههم واقتدارهم عليهم، وذلك لقصدِهِم فعلَ الفاحشة فيهم، فجاؤوا حتى وصلوا إلى بيت لوطٍ، فجعلوا يعالجون لوطاً على أضيافه، ولوطٌ يستعيذُ منهم ويقولُ: {إنَّ هؤلاء ضَيْفي فلا تَفْضَحونِ. واتَّقوا الله ولا تُخْزُونِ}؛ أي: راقبوا الله أول ذلك، وإن كان ليس فيكم خوفٌ من الله؛ فلا تفضحوني في أضيافي، وتنتَهكِوا منهم الأمر الشنيع.
{67 - 69} "Na wakaja watu wa mji ule" alimokuwa Lut' "huku wamefurahi" na wakawa wanapeana bishara wao kwa wao juu ya wageni wale wa Lut' na uzuri wa nyuso zao na kwamba wana uwezo dhidi yao. Na hilo ni kwa sababu walikuwa wanataka kufanya uchafu na wao. Kwa hivyo wakaja hadi walipofika kwenye nyumba ya Lut', na wakaanza kumsihi Lut' juu ya wageni wake hao, ilhali Lut' anajilinda kutokana nao na kusema, "Hakika hawa ni wageni wangu. Basi msinifedheheshe. Na mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi." Yaani, mchungeni Mwenyezi Mungu kwa sababu ya haya, hata kama nyinyi hamna hofu kwa Mwenyezi Mungu, basi msinifedheheshe katika wageni wangu, na mkawafanyia jambo hilo ovu.
#
{70} فَـ {قَالوا} له جواباً عن قوله: {ولا تخزونِ} فقط: {أولم نَنْهَكَ عن العالمين}: أن تضيِّفهم، فنحن قد أنذرناك، ومن أنذر؛ فقد أعذر.
{70} Lakini "wakasema" wakimjibu kauli yake "wala msinihizi" tu: "Kwani hatukukukataza
(kuwakaribisha) walimwengu hawa?" kwamba hufai kuwakaribisha. Basi sisi tulikwisha kuonya. Na mwenye kuonya, basi atakuwa ameshakubaliwa udhuru wake.
#
{71 - 72} فَـ {قَال} لهم لوطٌ من شدَّة الأمر الذي أصابه: {هؤلاء بناتي إن كنتُم فاعلينَ}: فلم يبالوا بقوله، ولهذا قال الله لرسوله محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -: {لَعَمْرُك إنَّهم لفي سكرتِهِم يعمهونَ}: وهذه السكرة هي سكرة محبَّة الفاحشة التي لا يُبالون معها بعذل ولا لوم.
{71 - 72} Kwa hivyo Lut' "akasema" kwa sababu ya ugumu wa jambo hilo lililompata: "Hawa binti zangu, ikiwa nyinyi ni watendaji." Lakini hawakuijali kauli yake, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akamwambia Mtume wake Muhammad -
rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: - "Ninaapa kwa umri wako! Hakika hao walikuwa katika ulevi wao, wakihangaika ovyo." Na ulevi huu ni ulevi wa kupenda mchafu ambayo hawajali kulaumiwa na kushutumiwa juu yake.
#
{73} فلما بينت له الرسل حالَهم؛ زال عن لوطٍ ما كان يَجِدُه من الضيق والكرب، فامتثل أمر ربِّه، وسرى بأهله ليلاً، فنجوا. وأما أهل القرية؛ {فأخذتْهُمُ الصيحةُ مشرقينَ}؛ أي: وقت شروق الشمس؛ حين كانت العقوبة عليهم أشدّ.
{73} Wajumbe hao walipomuelezea hali yao, yakamuondoka Lut'
yale aliyokuwa anapata ya dhiki na taabu, kwa hivyo akatii amri ya Mola wake Mlezi, na akaondoka pamoja na familia yake usiku, kwa hivyo wakaokoka. Na ama watu wa kijiji hicho, "ukelele ukawatwaa wakipambaukiwa" wakati adhabu ilipokuwa kali zaidi kwao.
#
{74} {فجعَلْنا عالِيَها سافِلَها}؛ أي: قلبنا عليهم مدينتهم، {وأمطَرْنا عليهم حجارةً من سجِّيل}: تتبع فيها من شذَّ من البلد منهم.
{74} "Kwa hivyo, tukaugeuza mji huo juu chini, na tukawanyeshea mvua ya mawe ya udongo wa kutoka Motoni," ukawa unamfuata mwenye kutoroka kutoka miongoni mwao kutoka mji huo.
#
{75} {إن في ذلك لآيات للمتوسِّمين}؛ أي: المتأمِّلين المتفكِّرين الذين لهم فكرٌ ورويَّة وفراسةٌ يفهمون بها ما أريد بذلك مِن أنَّ من تجرّأ على معاصي الله، خصوصاً هذه الفاحشة العظيمة، وأنَّ الله سيعاقِبُهم بأشنع العقوباتِ؛ كما تجرؤوا على أشنع السيئات.
{75} "Hakika katika hayo zipo ishara kwa wanaotafakari na kuzingatia," ambao wana werevu wa maono wanayofahamu kwayo yaliyokusudiwa katika hilo kwamba mwenye kuthubutu kumuasi Mwenyezi Mungu, hasa aina hii mbaya ya uchafu mkubwa, na kwamba Mwenyezi Mungu atawaadhibu kwa adhabu mbaya zaidi, kama walivyothubutu kufanya dhambi mbaya zaidi.
#
{76} {وإنَّها}؛ أي: مدينة قوم لوط {لَبسبيل مُقيم}: للسالكين، يعرفه كلُّ مَنْ تردَّد في تلك الدِّيار.
{76} "Na hakika miji hii" yaani, miji wa watu wa Lut' "ipo kwenye njia inayopitiwa." Anaijua kila mwenye kufika katika makazi hayo.
#
{77} {إنَّ في ذلك لآيةً للمؤمنين}: وفي هذه القصة من العبر: عنايتُه تعالى بخليله إبراهيم؛ فإنَّ لوطاً عليه السلام من أتباعه وممَّن آمن به، فكأنه تلميذٌ له؛ فحين أراد الله إهلاك قوم لوطٍ حين استحقُّوا ذلك؛ أمر رسله أن يمرُّوا على إبراهيم عليه السلام كي يبشِّروه بالولد ويخبروه بما بعثوا له، حتى إنَّه جادلهم عليه السلام في إهلاكهم، حتى أقنعوه، فطابت نفسُه، وكذلك لوط عليه السلام، لما كانوا أهل وطَنِهِ؛ فربما أخذتْه الرقة عليهم والرأفة بهم؛ قدَّر الله من الأسباب ما به يشتدُّ غيظُه وحِنْقُهُ عليهم، حتَّى استبطأ إهلاكَهم لمَّا قيل له: {إنَّ موعِدَهم الصبحُ أليس الصبحُ بقريبٍ}.
ومنها: أن الله تعالى إذا أراد أن يُهْلِكَ قرية ازداد شرُّهم وطغيانهم؛ فإذا انتهى؛ أوقع بهم من العقوبات ما يستحقُّونه.
{77} "Hakika katika hayo ipo ishara kwa Waumini." Basi katika kisa hiki kuna mazingatio mbalimbali. Kujali kukubwa kwake Yeye Mtukufu juu ya mwandani wake, Ibrahim. Kwa maana, Lut' - amani iwe juu yake - alikuwa katika wafuasi wake na wale waliomwamini, na ni kana kwamba alikuwa mwanafunzi wake. Kwa hivyo, wakati Mwenyezi Mungu alitaka kuwaangamiza kaumu ya Lut' walipostahiki hilo, aliwaamuru wajumbe wake kwamba wapitie kwa Ibrahim - amani iwe juu yake - ili wambashirie kupata mwana, na kile walichomtuma kufanya, kiasi kwamba yeye amani iwe juu yake akaanza kujadiliana nao kuhusu kuwaangamiza watu wa Lut', hadi walipomshawishi, kwa hivyo nafsi yake ikatulia. Na vile vile Lut' - amani iwe juu yake - walipokuwa ni watu wa mji wake, huenda ikamchukua huruma juu yao, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akaweka sababu za kuipandisha juu hasira yake dhidi yao, hadi akaona kuko mbali kuangamizwa kwao alipoambiwa, "Hakika miadi yao ni asubuhi. Je, asubuhi si karibu?" Na miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anapotaka kuuangamiza mji, huongeza uovu wao na upotovu wao. Basi anapomaliza, anawafikishia adhabu wanayostahiki.
{وَإِنْ كَانَ أَصْحَابُ الْأَيْكَةِ لَظَالِمِينَ (78) فَانْتَقَمْنَا مِنْهُمْ وَإِنَّهُمَا لَبِإِمَامٍ مُبِينٍ (79)}.
78. Na hakika watu wa Kichakani walikuwa wenye kudhulumu. 79. Kwa hivyo tukawaadhibu. Na hakika miji miwili hii iko kwenye njia iliyo wazi.
#
{78} وهؤلاء قوم شعيبٍ، نَعَتَهُم الله وأضافهم إلى الأيكَة، وهو البستان كثير الأشجار؛ ليذكر نعمته عليهم، وأنهم ما قاموا بها، بل جاءهم نبيُّهم شعيب، فدعاهم إلى التوحيد، وتَرْك ظُلْم الناس في المكاييل والموازين، وعالَجَهم على ذلك أشدَّ المعالجة، فاستمروا على ظلمهم في حقِّ الخالق وفي حقِّ الخلق، ولهذا وصفهم هنا بالظُّلم.
{78} Na hawa ni kaumu ya Shu'aib, ambao Mwenyezi Mungu aliwaelezea na kuwanasibisha na kichaka. Nacho ni bustani lenye miti mingi, ili akumbushe neema yake juu yao, na kwamba hawakuifanyia kazi. Bali Nabii wao Shu'aib aliwajia na akawalingania katika kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na kuacha kuwadhulumu watu katika vipimo na mizani, na akawarai sana juu ya hayo, lakini wakaendelea na kumdhulumu Muumba na viumbe, na ndiyo maana akawaelezea hapa kwamba walikuwa madhalimu.
#
{79} {فانْتَقَمْنا منهم}: فأخذهم عذابُ يومِ الظُّلَّةِ؛ إنه كان عذاب يوم عظيم. {وإنَّهما}؛ أي: ديار قوم لوطٍ وأصحاب الأيكة، {لبإمام مُبينٍ}؛ أي: لبطريق واضح يمرُّ بهم المسافرون كلَّ وقت، فيبين من آثارهم ما هو مشاهَدٌ بالأبصار، فيعتبر بذلك أولو الألباب.
{79} "Kwa hivyo tukawaadhibu" kwa hivyo ikawashika adhabu ya siku ya kivuli. Hakika ilikuwa adhabu ya siku kubwa. "Na hakika miji miwili hii;" yaani, ya kaumu ya Lut' na watu wa Vichakani, "iko kwenye njia iliyo wazi," ambayo wasafiri hupitia kila wakati, ili mabaki zao zibainike na kuonekana kwa macho, ili wenye ufahamu wapate kuzingatia kwa hayo.
{وَلَقَدْ كَذَّبَ أَصْحَابُ الْحِجْرِ الْمُرْسَلِينَ (80) وَآتَيْنَاهُمْ آيَاتِنَا فَكَانُوا عَنْهَا مُعْرِضِينَ (81) وَكَانُوا يَنْحِتُونَ مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا آمِنِينَ (82) فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ مُصْبِحِينَ (83) فَمَا أَغْنَى عَنْهُمْ مَا كَانُوا يَكْسِبُونَ (84)}
80. Na bila ya shaka wakaazi wa Hijr waliwakadhibisha Mitume. 81. Na tuliwaletea ishara zetu, nao wakawa wanazipa migongo. 82. Nao walikuwa wakichonga majumba katika milima kwa amani. 83. Basi ukelele ukawatwaa asubuhi. 84. Na hayakuwafaa yale waliyokuwa wakiyachuma.
#
{80} يخبر تعالى عن أهل الحجر، وهم قوم صالح، الذين يسكنون الحجرَ المعروف في أرض الحجاز: أنَّهم كذَّبوا المرسلين؛ أي: كذَّبوا صالحاً، ومن كذَّب رسولاً؛ فقد كذَّب سائر الرسل لاتفاق دعوتهم، وليس تكذيب بعضهم لشخصِهِ، بل لما جاء به من الحقِّ، الذي اشترك جميع الرسل بالإتيان به.
{80} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya watu wa Al-Hijr, ambao ni watu wa Saleh, ambao walikaa katika mji wa Al-Hijr unaojulikana katika maeneo ya Hijazi, kwamba waliwakadhibisha Mitume, yaani, Saleh. Na mwenye kumkadhibisha Mtume mmoja, basi atakuwa amewakadhibisha Mitume wengine wote kwa sababu wito wao ni mmoja. Na tena wao wanapowakadhibisha baadhi yao si kwamba wanamkadhibisha yeye mwenyewe, bali wanakadhibisha yale aliyokuja nayo ya haki, ambayo mitume wote walishirikiana katika kuja nayo.
#
{81} {وآتيناهم آياتنا}: الدالَّة على صحَّة ما جاءهم به صالح من الحق التي من جملتها تلك الناقة التي هي من آيات الله العظيمة. {فكانوا عنها معرضين}: كِبْراً وتجبُّراً على الله.
{81} "Na tuliwaletea ishara zetu" zenye kuonyesha usahihi wa yale aliyowajia nayo Saleh ya haki, ambayo miongoni mwake ni ngamia jike yule ambaye alikuwa ni katika Ishara kubwa za Mwenyezi Mungu. "Nao wakawa wanazipa migongo," kwa kiburi na kutakabari mbele ya Mwenyezi Mungu.
#
{82} {وكانوا}: من كثرة إنعام الله عليهم، {يَنْحِتون من الجبال بيوتاً آمنينَ}: من المخاوف، مطمئنين في ديارهم؛ فلو شكروا النعمة وصدَّقوا نبيَّهم صالحاً عليه السلام؛ لأدرَّ الله عليهم الأرزاق، ولأكرمهم بأنواع من الثواب العاجل والآجل، ولكنَّهم لما كذَّبوا وعقروا الناقة وعتوا عن أمرِ ربِّهم وقالوا: {يا صالحُ ائتِنا بما تَعِدُنا إن كنتَ من الصَّادقين}.
{82} "Nao walikuwa" kwa sababu ya wingi wa neema za Mwenyezi Mungu ju yao, "wakichonga majumba katika milima kwa amani," kutokana na hofu, wakiwa wametulia katika makazi yao. Na ikiwa wangeshukuru neema hizo na kumwamini nabii wao, Saleh - amani iwe juu yake - basi Mwenyezi Mungu angewaruzuku kwa wingi, na angewakirimu kwa aina mbalimbali za malipo ya haraka na ya baadaye, lakini wao walipokadhibisha na kumchinja ngamia jike yule na wakaasi amri ya Mola wao Mlezi, na wakasema, "Ewe Saleh! Tuletee hayo unayotuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa Mitume."
#
{83} {فَأخَذَتْهُمُ الصَيْحَةُ مُصْبِحِينَ}: فتقطعت قلوبهم في أجوافهم وأصبحوا في دارهم جاثمين هلكى، مع ما يتبع ذلك من الخزي واللعنة المستمرة.
{83} "Basi ukelele ukawatwaa asubuhi." Kwa hivyo, mioyo yao ikakatikia ndani ya miili yao, na wakaishia wameanguka kifudifudi katika makazi yao wamekwisha angamia, pamoja na kwamba hilo litafuatwa na hizaya na laana yenye kuendelea.
#
{84} {فما أغنى عنهم ما كانوا يَكْسبونَ}: لأنَّ أمر الله إذا جاء لا يردُّه كَثْرة جنودٍ ولا قوَّة أنصار ولا غزارة أموال.
{84} "Na hayakuwafaa yale waliyokuwa wakiyachuma." Kwa sababu amri ya Mwenyezi Mungu inapokuja, haizuiliwi na wingi wa idadi ya majeshi, wala nguvu za wasaidizi, wala wingi wa mali.
{وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَإِنَّ السَّاعَةَ لَآتِيَةٌ فَاصْفَحِ الصَّفْحَ الْجَمِيلَ (85) إِنَّ رَبَّكَ هُوَ الْخَلَّاقُ الْعَلِيمُ (86)}.
85. Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake isipokuwa kwa haki. Na hakika Saa ya Qiyama itafika. Basi samehe msamaha mzuri. 86. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Muumbaji, Mwenye kujua zaidi.
#
{85} أي: ما خلقناهما عَبَثاً باطلاً كما يظنُّ ذلك أعداء الله، بل ما خلقناهما {إلاَّ بالحقِّ}: الذي منه أن يكونا بما فيهما دالَّتين على كمال خالقهما واقتداره وسعة رحمتِهِ وحكمتِهِ وعلمِهِ المحيط، وأنَّه الذي لا تنبغي العبادةُ إلا له وحدَه لا شريك له. {وإنَّ الساعة لآتيةٌ}: لا ريبَ فيها؛ لَخَلْقُ السماوات والأرض أكبرُ من خَلْق الناس. {فاصفَح الصَّفْح الجميلَ}: وهو الصفح الذي لا أذيَّة فيه، بل يقابل إساءة المسيء بالإحسان وذنبَه بالغفران؛ لتنال من ربِّك جزيل الأجر والثواب؛ فإنَّ كلَّ ما هو آتٍ فهو قريبٌ.
وقد ظهر لي معنى أحسن مما ذكرتُ هنا، وهو أنَّ المأمور به هو الصفح الجميل؛ أي: الحسن الذي قد سَلِمَ من الحقد والأذيَّة القوليَّة والفعليَّة، دون الصفح الذي ليس بجميل، وهو الصفح في غير محلِّه؛ فلا يُصْفَح حيث اقتضى المقام العقوبة؛ كعقوبة المعتدين الظالمين الذين لا ينفعُ فيهم إلا العقوبة، وهذا هو المعنى.
{85} Yaani, hatukuziumba bure, kama maadui wa Mwenyezi Mungu wanavyofikiria, lakini hatukuziumba "isipokuwa kwa haki" ambayo zinafaa mbili hizo ziwe pamoja na vile vilivyomo vinaonyesha ukamilifu wa Muumba wake, uwezo wake, rehema yake pana, na hekima yake, na elimu yake yenye kuzunguka; na kwamba Yeye tu ndiye anayepasa kufanyiwa ibada, peke yake bila mshirika yeyote. "Na hakika Saa ya Qiyama itafika." Hapana shaka yoyote juu yake kwani, kuumbwa kwa mbingu na ardhi ni kukubwa zaidi kuliko kuumbwa kwa watu. "Basi samehe msamaha mzuri." Nao ni msamaha ambao hauna udhia wowote, bali ubaya wa mfanya mabaya unafaa kukabiliwa na wema, na dhambi yake kwa msamaha, ili upate malipo mengi kutoka kwa Mola wako Mlezi. Kwa maana kila kijacho, kiko karibu. Na nimedhihirikiwa na maana bora zaidi kuliko ile niliyotaja hapa, ambayo ni kwamba kilichoamrishwa ni msamaha mzuri, ambao umesalimika kutokana na chuki, udhia wa kimaneno na wa kivitendo, na si msamaha ambao siyo mzuri, ambao ni msamaha usiokuwa mahali pake. Kwa hivyo haisamehewi hali ambayo inalazimu adhabu, kama vile kuwaadhibu wavukao mipaka, madhalimu ambao haiwafaidi isipokuwa adhabu pekee. Na hii ndiyo maana sahihi.
#
{86} {إنَّ ربَّك هو الخلاَّق}: لكل مخلوق، {العليمُ}: بكل شيءٍ؛ فلا يعجِزُه أحدٌ من جميع ما أحاط به علمُه، وجرى عليه خلقُه، وذلك سائر الموجودات.
{86} "Hakika Mola wako Mlezi ndiye Muumbaji" wa kila kiumbe, "Mwenye kujua zaidi" kila kitu. Kwa hivyo hakuna yeyote anayeweza kumshinda katika kila kitu alichozunguka kwa elimu yake, na akakiumba, na hilo ni kuhusiana na vilivyopo vyote.
{وَلَقَدْ آتَيْنَاكَ سَبْعًا مِنَ الْمَثَانِي وَالْقُرْآنَ الْعَظِيمَ (87) لَا تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَى مَا مَتَّعْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِنْهُمْ وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِلْمُؤْمِنِينَ (88) وَقُلْ إِنِّي أَنَا النَّذِيرُ الْمُبِينُ (89) كَمَا أَنْزَلْنَا عَلَى الْمُقْتَسِمِينَ (90) الَّذِينَ جَعَلُوا الْقُرْآنَ عِضِينَ (91) فَوَرَبِّكَ لَنَسْأَلَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ (92) عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ (93) [فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ (94) إِنَّا كَفَيْنَاكَ الْمُسْتَهْزِئِينَ (95) الَّذِينَ يَجْعَلُونَ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ (96) وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّكَ يَضِيقُ صَدْرُكَ بِمَا يَقُولُونَ (97) فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَكُنْ مِنَ السَّاجِدِينَ (98) وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّى يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ (99)] }.
87. Na hakika tumekupa saba zinazosomwa mara kwa mara, na Qur-ani Tukufu. 88. Kamwe usivinyoshee macho yako vitu tulivyowastarehesha kwavyo makundi fulani kati yao, wala usiwahuzunikie. Na wainamishie bawa lako
(la huruma) Waumini. 89. Na sema, "Hakika mimi ni mwonyaji mwenye kubainisha." 90. Kama hivyo tuliwateremshia waliogawa. 91. Ambao wakaifanya Qur-ani vipande vipande. 92. Basi ninaapa kwa Mola wako Mlezi! Tutawauliza wote. 93. Kuhusu yale waliyokuwa wakiyatenda. 94. Basi wewe yadhihirishe yale uliyoamrishwa, na jitenge na washirikina. 95. Hakika Sisi tunatosha kukukinga na wanaofanya stihizai. 96. Ambao wanafanya mungu mwingine kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi, watakuja jua! 97. Na Sisi tunajua kwa hakika kuwa wewe kifua chako kinaona dhiki kwa hayo wayasemayo. 98. Basi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi, na uwe miongoni mwa wanaomsujudia. 99. Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini.
#
{87} يقول تعالى ممتنًّا على رسوله: {ولقد آتيناك سبعاً من المثاني}: وهنَّ على الصحيح السور السبع الطوال: البقرة وآل عمران والنساء والمائدة والأنعام والأعراف والأنفال مع التوبة. أو أنَّها فاتحة الكتاب؛ لأنها سبع آيات. فيكون عطف {القرآن العظيم} على ذلك من باب عطف العامِّ على الخاصِّ؛ لكثرة ما في المثاني من التوحيد وعلوم الغيب والأحكام الجليلة وتثنيتها فيها. وعلى القول بأن الفاتحة هي السبع المثاني معناها أنَّها سبعُ آياتٍ تُثنى في كلِّ ركعة.
{87} Mwenyezi Mungu anasema akitaja neema yake kwa Mtume wake: "Na hakika tumekupa saba zinazosomwa mara kwa mara.
" Nazo kulingana na kauli sahihi ni suras zile saba ndefu: Al-Baqara, Al-Imran, Nisaa, Maida, An'am, A'raf, na Anfal pamoja na Tawba. Au ni Surat Fatiha, kwa sababu ina aya saba. Kwa hivyo inakuwa kuunganisha huku "na Qur-ani tukufu" kulingana na maana hii ni katika mbinu ya kuunganisha cha jumla juu ya kilicho mahususi; kwa sababu ya upwekeshaji mwingi ulio ndani yake hizi saba zinazorudiwarudiwa, na elimu za ghaibu, na hukumu kubwa na kurudiwarudiwa kwake ndani yake. Na kwa mujibu wa kauli kwamba hizo saba za kurudiwarudiwa ni Surat Al-Fatiha inakuwa maana yake kwamba ni aya saba zinarorudiwa katika kila rakaa ya swala..
#
{88} وإذ كان اللهُ قد أعطاه القرآن العظيم مع السبع المثاني؛ كان قد أعطاه أفضلَ ما يتنافسُ فيه المتنافسون وأعظمَ ما فرح به المؤمنون، {قُلْ بفضل اللهِ وبرحمتِهِ فبذلك فَلْيَفْرحوا هو خيرٌ مما يجمعونَ}، ولذلك قال بعده: {لا تمدَّنَّ عينيك إلى ما متَّعنا به أزواجاً منهم}؛ أي: لا تعجب إعجاباً يحمِلُك على إشغال فكرك بشهوات الدُّنيا التي تمتَّع بها المترفون واغترَّ بها الجاهلون، واستغْنِ بما آتاك الله من المثاني والقرآن العظيم. {ولا تحزَنْ عليهم}: فإنَّهم لا خير فيهم يُرجى، ولا نفع يُرتَقَب؛ فلك في المؤمنين عنهم أحسنُ البدل وأفضل العوض. {واخفِضْ جناحك للمؤمنين}؛ أي: ألِنْ لهم جانبك وحسِّنْ لهم خُلُقَك محبةً وإكراماً وتودُّداً.
{88} Na kama Mwenyezi Mungu alimpa Qur'ani tukufu pamoja na saba hizo, basi alimpa kilicho bora zaidi wanachokishindania washindani na kikubwa zaidi wanachokifurahia Waumini.
"Sema: Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi na wafurahi kwa hayo. Haya ni bora kuliko hayo wanayoyakusanya." Na ndiyo maana akasema baada yake, "Kamwe usivinyoshee macho yako vitu tulivyowastarehesha kwavyo makundi fulani kati yao." Yaani, usipendezwe kupendezwa ambako kutakufanya kuishughulisha fikira yako na matamanio ya dunia ambayo wanastarehe kwayo, na wajinga wamedanganyika kwayo. Na tosheka na yale aliyokupa Mwenyezi Mungu miongoni mwa yale yanayorudiwarudiwa na Qur-ani Tukufu. "Wala usiwahuzunikie," kwa kuwa hakuna heri yoyote inayotarajiwa kwao, wala hakuna manufaa yanayongojewa. Nawe una kibadala kizuri zaidi miongoni mwa waumini kuliko wao. "Na wainamishie bawa lako
(la huruma) Waumini." Yaani, walainishie ubawa wako na waonyeshe tabia nzuri kwa kuwapenda, kuwakirimu, na kuwapenda.
#
{89} {وقل إني أنا النذير المبين}؛ أي: قم بما عليك من النذارة وأداء الرسالة والتبليغ للقريب والبعيد والعدوِّ والصديق؛ فإنَّك إذا فعلت ذلك؛ فليس عليك من حسابهم من شيء، وما من حسابك عليهم من شيء.
{89} "Na sema, "Hakika mimi ni mwonyaji mwenye kubainisha." Yaani, tekeleza yaliyo juu yako ya kuonya, kufikisha ujumbe kwa aliye karibu na aliye mbali, adui na rafiki. Kwa maana, ukifanya hivyo, basi hakuna chochote juu yako katika hesabu yao, nao hakuna chochote kilicho juu yao katika hesabu yako.
#
{90} وقوله: {كما أنزلنا على المقتسمين}؛ أي: كما أنزلنا العقوبة على المقتسمين على بطلان ما جئتَ به، الساعين لصدِّ الناس عن سبيل الله.
{90} Na kauli yake, "Kama hivyo tuliwateremshia waliogawa." Yaani, kama tulivyowateremshia adhabu wale waliogawa kwa sababu walibatilisha yale uliyokuja nayo, wale wanaofanya bidii kuzuia watu na njia ya Mwenyezi Mungu.
#
{91} {الذين جَعلوا القرآنَ عِضِين}؛ أي: أصنافاً وأعضاءً وأجزاءً يصرِّفونه بحسب ما يهوونه؛ فمنهم من يقولُ: سحرٌ، ومنهم من يقول: كهانةٌ، ومنهم من يقول: مفترىً ... إلى غير ذلك من أقوال الكفرة المكذِّبين به، الذين جعلوا قدحَهم فيه؛ ليصدُّوا الناس عن الهدى.
{91} "Ambao wakaifanya Qur-ani vipande vipande." Yaani, sampuli na sehemu mbalimbali wanazozivuruga kulingana na watakavyo. Miongoni mwao kuna anayesema, 'uchawi' na miongoni mwao kuna anayesema 'kuhani' na miongoni mwao kuna anayesema, 'uzushi' na maneno mengineyo ya makafiri wanaoikadhibisha, ambao waliitilia doa ili wawazuie watu kuongoka.
#
{92 - 93} {فوربِّك لنسألنَّهم أجمعين}؛ أي: جميع من قدح فيه وعابه وحرَّفه وبدله، {عمَّا كانوا يعملون}: وفي هذا أعظم ترهيب وزجر لهم عن الإقامة على ما كانوا يعملون.
{92-93} "Basi ninaapa kwa Mola wako Mlezi! Tutawauliza wote." Yaani, wote waliotia doa ndani yake, akaikashifu, akaipotosha, na kuibadilisha, "Kuhusu yale waliyokuwa wakiyatenda." Na katika hili kuna tishio kubwa zaidi na kemeo kwao dhidi ya kubakia katika yale waliyokuwa wakiyatenda.
#
{94} ثم أمر الله رسوله أن لا يبالي بهم ولا بغيرهم، وأن يَصْدَعَ بما أمر الله ويعلنَ بذلك لكلِّ أحدٍ ولا يعوقنَّه عن أمره عائقٌ ولا تصدُّه أقوال المتهوِّكين. {وأعرض عن المشركينَ}: أي؛ لا تبال بهم، واتركْ مشاتَمَتَهم ومسابَّتهم مقبلاً على شأنك.
{94} Kisha Mwenyezi Mungu akamwamuru Mtume wake kwamba asiwajali wao wala wengineo, na kwamba ayadhihirishe yale aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu na ayatangaze kwa kila mtu, wala kisimzuie kizuizi chochote dhidi ya jambo lake wala yasimzuie maneno ya wale waliochanganyikiwa. "Na jitenge na washirikina." Yaani, usiwajali, na achana na kuwatusi na ulielekee jambo lako sawasawa.
#
{95} {إنَّا كفيناك المستهزئين}: بك وبما جئت به. وهذا وعدٌ من الله لرسوله أن لا يضرُّه المستهزئون، وأن يكفيه الله إيَّاهم بما شاء من أنواع العقوبة، وقد فعل تعالى: فإنَّه ما تظاهر أحدٌ بالاستهزاء برسول الله - صلى الله عليه وسلم - وبما جاء به؛ إلا أهلَكَه الله وقَتَلَهُ شرَّ قِتْلَةٍ.
{95} "Hakika Sisi tunatosha kukukinga na wanaofanya stihizai." Na pia tumeyatosheleza yale uliyokuja nayo. Na hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kwamba hawatamdhuru wale wafanyao stihizai, na kwamba Mwenyezi Mungu atamtosheleza dhidi yao kwa apendacho miongoni mwa aina mbalimbali za adhabu. Na tayari yeye Mtukufu alikwisha fanya hivyo. Kwa maana hakuna yeyote aliyeyapinga yale aliyokuja nayo kwa kumfanyia stihizai Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - isipokuwa Mwenyezi Mungu alimwangamiza na kumuua mauaji maovu zaidi.
#
{96} ثم ذكر وصفهم، وأنهم كما يؤذونك يا رسول الله؛ فإنَّهم أيضاً يؤذون الله، {الذين يجعلون مع الله إلهاً آخر}: وهو ربُّهم وخالقهم ومدبرهم. {فسوف يعلمون}: غِبَّ أفعالهم إذا وردوا القيامة.
Kisha akataja maelezo yao, na kwamba kama vile wanavyokuudhi, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, pia wanamuudhi Mwenyezi Mungu. "Ambao wanafanya mungu mwingine kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu" ilhali Yeye ndiye Mola wao Mlezi, Muumba wao, na Muendeshaji wa mambo yao "Basi, watakuja jua" mwisho wa vitendo vyao watakapofika Siku ya Qiyama!
#
{97} {ولقد نعلمُ أنك يضيقُ صدرُكَ بما يقولون}: لك من التكذيب والاستهزاء؛ فنحن قادرون على استئصالهم بالعذاب والتَّعجيل لهم بما يستحقُّونه، ولكنَّ الله يمهِلُهم، ولا يهملُهم.
{97} "Na Sisi tunajua kwa hakika kuwa wewe kifua chako kinaona dhiki kwa hayo wayasemayo" ya kukukadhibisha na kukufanyia stihizai. Kwa maana Sisi tuna uwezo wa kuwaangamiza kabisa kwa adhabu na kuwaharakisha yale wanayostahili, lakini Mwenyezi Mungu huwapa muhula, na hawapuuzi.
#
{98} فأنت يا محمدُ، {سبِّحْ بحمد ربِّك وكن من الساجدين}؛ أي: أكثر من ذكر الله وتسبيحه وتحميده والصلاة؛ فإنَّ ذلك يوسع الصدر ويشرَحُه ويُعينك على أمورك.
{98} Kwa hivyo, ewe Muhammad "mtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi, na uwe miongoni mwa wanaomsujudia." Yaani, kithiri kumtaja Mwenyezi Mungu, kumtakasa, kumsifu, na kuswali. Kwani, hayo hukipanua kifua, kukituliza, na yanakusaidia katika mambo yako.
#
{99} {واعبُدْ ربَّك حتى يأتِيَكَ اليقينُ}؛ أي: الموت؛ أي: استمرَّ في جميع الأوقات على التقرُّب إلى الله بأنواع العبادات. فامتثل - صلى الله عليه وسلم - أمر ربِّه، فلم يزل دائباً في العبادة حتى أتاه اليقين من ربِّه، - صلى الله عليه وسلم - تسليماً كثيراً.
{99} "Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini." Yaani, mauti. Yaani, endelea kila wakati kumkaribia Mwenyezi Mungu kwa kila aina ya ibada. Kwa hivyo Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - akatekeleza amri ya Mola wake Mlezi, na hakuacha kuendelea kumuabudu mpaka alipojiwa na yakini kutoka kwa Mola wake Mlezi. Rehema na amani nyingi za Mwenyezi Mungu ziwe juu.
Imekamilika Tafsiri ya Surat Al-Hijr. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote. Amin.
* * *