Tafsiri ya Surat Al-Kawthar
Tafsiri ya Surat Al-Kawthar
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu
{إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ (1) فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ (2) إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الْأَبْتَرُ (3)}
1. Hakika tumekupa kheri nyingi. 2. Basi sali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi. 3. Hakika anayekuchukia ndiye aliye mpungufu.
#
{1} يقول الله تعالى لنبيِّه محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -[ممتنًّا عليه]: {إنَّا أعطيناكَ الكَوْثَرَ}؛ أي: الخير الكثير والفضل الغزير، الذي من جملته ما يعطيه اللهُ لنبيِّه - صلى الله عليه وسلم -[يوم القيامة] من النهر الذي يقال له: الكوثر ، ومن الحوض ؛ طولُه شهرٌ وعرضُه شهرٌ، ماؤه أشدُّ بياضاً من اللبن، وأحلى من العسل، آنيته عدد نجوم السماء في كثرتها واستنارتها، من شرب منه شربةً؛ لم يظمأ بعدها أبداً.
{1} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Mtume wake Muhammad - rehema na amani zimshukie -
[akimkumbusha neema zake juu yake]: "Hakika tumekupa heri nyingi" ambazo miongoni mwake ni yale ambayo Mwenyezi Mungu atampa Nabii wake – rehema na amani ziwe juu yake –
[Siku ya Kiyama] kutoka kwenye mto uitwao: Al-Kawthar, na kutoka katika hodhi yake ambalo urefu wake ni mwendo wa mwezi mmoja, na upana wake ni mwendo wa mwezi mmoja. Maji yake ni meupe kuliko maziwa na ni matamu kuliko asali. Vyombo vyake katika wingi wake na kung'aa kwake ni kama idadi ya nyota za mbinguni. Mwenye kunywa humo, hakuwa na kiu kamwe baada ya hapo.
#
{2} ولمَّا ذكر مِنَّتَه عليه؛ أمَرَهُ بشكرها، فقال: {فصلِّ لربِّك وانْحَر}: خصَّ هاتين العبادتين بالذِّكر؛ لأنَّهما أفضل العبادات وأجلُّ القربات، ولأنَّ الصلاة تتضمَّن الخضوع في القلب والجوارح لله، وتنقله في أنواع العبوديَّة، وفي النحر تقرُّبٌ إلى الله بأفضل ما عند العبد من النحائر، وإخراجٌ للمال الذي جُبِلَت النُّفوس على محبَّته والشُّحِّ به.
{2} Na alipomtajia wema wake juu yake; akamuamrisha kumshukuru,
akasema: "Basi sali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi." Amezitaja ibada hizi mbili hasa kwa sababu hizo ndizo ibada bora kabisa na mambo matukufu zaidi ya kujiweka kwayo karibu na Mwenyezi Mungu, na kwa sababu swala inajumuisha kunyenyekea moyoni na kwa viungo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na humhamisha kupitia aina mbali mbali za uja. Na katika kuchinja kuna kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu kwa bora zaidi alicho nacho mja miongoni mwa dhabihu, na kutoa mali ambazo roho zimefanywa kuzipenda na kuzifanyia ubahili.
#
{3} {إنَّ شانِئَكَ}؛ أي: مبغضك وذامَّك ومتنقصك، {هو الأبتر}؛ أي: المقطوع من كلِّ خيرٍ؛ مقطوعُ العمل، مقطوعُ الذِّكر، وأمَّا محمدٌ - صلى الله عليه وسلم -؛ فهو الكامل حقًّا، الذي له الكمال الممكن للمخلوق من رفع الذكر وكثرة الأنصار والأتباع - صلى الله عليه وسلم -.
{3} "Hakika anayekuchukia" na kukukashifu na kukupunguzia heshima, "ndiye aliye mpungufu zaidi" naye ndiye atakayekatikiwa matendo yake na utajo wake. Na ama Muhammad – rehema na amani ziwe juu yake, yeye hakika ndiye mkamilifu wa kweli, ambaye ana ukamilifu unaowezekana kwa kiumbe; kwa kuinuliwa utajo wake na wingi wa wasaidizi na wafuasi - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
* * *