:
Tafsiri ya Surat Al-Ma'un
Tafsiri ya Surat Al-Ma'un
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu
: 1 - 7 #
{أَرَأَيْتَ الَّذِي يُكَذِّبُ بِالدِّينِ (1) فَذَلِكَ الَّذِي يَدُعُّ الْيَتِيمَ (2) وَلَا يَحُضُّ عَلَى طَعَامِ الْمِسْكِينِ (3) فَوَيْلٌ لِلْمُصَلِّينَ (4) الَّذِينَ هُمْ عَنْ صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ (5) الَّذِينَ هُمْ يُرَاءُونَ (6) وَيَمْنَعُونَ الْمَاعُونَ (7)}
1. Je! Umemwona anayekadhibisha Malipo? 2. Huyo ndiye anayemsukuma yatima. 3. Wala hahimizi kumlisha masikini. 4. Basi, ole wao wanaosali. 5. Ambao wanapuuza Sala zao. 6. Ambao wanajionyesha. 7. Nao huku wanazuia msaada.
#
{1} يقول تعالى ذامًّا لمن ترك حقوقه وحقوق عباده: {أرأيتَ الذي يُكَذِّبُ بالدِّين}؛ أي: بالبعث والجزاء؛ فلا يؤمن بما جاءت به الرُّسل.
{1} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema akiwakashifu wale wanaoziacha haki zake na haki za waja wake: "Je! Umemwona anayekadhibisha Malipo" baada ya kufufuliwa, akaacha kuyaamini yale yaliyoletwa na Mitume.
#
{2} {فذلك الذي يَدُعُّ اليتيمَ}؛ أي: يدفعه بعنفٍ وشدَّةٍ، ولا يرحمه؛ لقساوة قلبه، ولأنَّه لا يرجو ثواباً ولا يخاف عقاباً.
{2} "Huyo ndiye anayemsukuma yatima" kwa nguvu na kwa ukali, wala hana huruma naye. Kwa sababu ya ugumu wa moyo wake, na kwa sababu hatarajii malipo wala haogopi adhabu.
#
{3} {ولا يحضُّ}: غيره {على طعام المسكينِ}: ومن باب أولى أنَّه بنفسه لا يطعم المسكين.
{3} "Wala hahimizi" wengine "kumlisha masikini" naye mwenyewe basi ndiyo hata hawalishi masikini.
#
{4 - 5} {فويلٌ للمصلِّينَ}؛ أي: الملتزمين لإقامة الصلاة، ولكنهم {عن صلاتهم ساهونَ}؛ أي: مضيِّعون لها، تاركون لوقتها، مُخِلُّون بأركانها، وهذا لعدم اهتمامهم بأمر الله؛ حيث ضيَّعوا الصلاة التي هي أهمُّ الطاعات، والسَّهو عن الصَّلاة هو الذي يستحقُّ صاحبه الذمَّ واللوم ، وأمَّا السَّهو في الصَّلاة؛ فهذا يقع من كلِّ أحدٍ، حتَّى من النبيِّ - صلى الله عليه وسلم -.
{4 - 5} "Basi, ole wao wanaoswali" lakini “ambao wanapuuza Sala zao." Yaani, wanaipoteza, wanapuuza wakati wake, na wanaharibu nguzo zake, na hili ni kwa sababu hawajali amri ya Mwenyezi Mungu. Pale ambapo walipuuza swala, ambayo ndiyo tendo muhimu zaidi la utiifu. Na mwenye kusahau swala ndiye anayestahiki kukashifiwa na kulaumiwa. Ama kusahau tu katika swala, hilo analifanya kila mtu, hata Nabii – rehema na amani ziwe juu yake.
#
{6 - 7} ولهذا وصف الله هؤلاء بالرِّياء والقسوة وعدم الرحمة، فقال: {الذين هم يراؤون}؛ أي: يعملون الأعمال لأجل رئاء الناس، {ويمنعون الماعون}؛ أي: يمنعون إعطاء الشيء الذي لا يضرُّ إعطاؤه على وجه العارية أو الهبة؛ كالإناء والدَّلو والفأس ونحو ذلك ممَّا جرت العادة ببذله والسَّماح به ، فهؤلاء لشدَّة حرصهم يمنعون الماعون؛ فكيف بما هو أكثر منه؟! وفي هذه السورة الحثُّ على إطعام اليتيم والمساكين، والتَّحضيض على ذلك، ومراعاة الصَّلاة، والمحافظة عليها، وعلى الإخلاص فيها، وفي سائر الأعمال ، والحثُّ على فعل المعروف، وبذل الأمور الخفيفة كعارية الإناء والدَّلو والكتاب ونحو ذلك؛ لأنَّ الله ذمَّ من لم يفعل ذلك. والله سبحانه أعلم.
{6 - 7} Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akawaelezea watu hawa kwamba wanajionyesha, na kwamba ni wagumu na hawana huruma, akasema: "Ambao wanajionyesha." Yaani: wanafanya vitendo kwa ajili ya kujionyesha kwa watu. "Nao huku wanazuia msaada." Yaani, wanazuia kutoa kitu ambacho hakina madhara kwao kukitoa kama vile kuazima au zawadi; kama vile kuazima chombo, ndoo, shoka, na mambo mengine ambayo ni desturi kuyatoa bure. Lakini watu hawa kutokana na hamu yao kubwa juu ya vitu vyao, wanazuia msaada. Basi vipi wakiambiwa kutoa vilivyo vikubwa zaidi ya hayo? Katika Sura hii kuna kuhimizwa kulisha yatima na masikini, na kuchunga na kuihifadhi swala, na kuifanya kwa kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake, na kuhimiza kutenda mema, na kupeana bure mambo mepesi kama vile kuazima chombo, ndoo, kitabu, na mfano wa hivyo. Kwa sababu Mwenyezi Mungu amewakashifu wale wasiofanya hivyo. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi.
* * *