Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu
{قُلْ يَاأَيُّهَا الْكَافِرُونَ (1) لَا أَعْبُدُ مَا تَعْبُدُونَ (2) وَلَا أَنْتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ (3) وَلَا أَنَا عَابِدٌ مَا عَبَدْتُمْ (4) وَلَا أَنْتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ (5) لَكُمْ دِينُكُمْ وَلِيَ دِينِ (6)}.
1.
Sema: Enyi makafiri! 2. Siabudu mnachokiabudu; 3.Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu. 4.Wala sitaabudu mnachoabudu. 5. Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu. 6. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.
#
{1 - 6} أي: قلْ للكافرين معلناً ومصرِّحاً: {لا أعبُدُ ما تعبُدون}؛ أي: تبرَّأ مما كانوا يعبدون من دون الله ظاهراً وباطناً. {ولا أنتم عابدون ما أعبُدُ}: لعدم إخلاصكم في عبادتكم لله ؛ فعبادتُكم له المقترنةُ بالشِّرك لا تسمَّى عبادةً. وكرَّر ذلك ليدلَّ الأوَّل على عدم وجود الفعل، والثاني على أنَّ ذلك قد صار وصفاً لازماً، ولهذا ميَّز بين الفريقين، وفصل بين الطائفتين، فقال: {لكم دينُكُم وليَ دينٌ}؛ كما قال تعالى: {قلْ كلٌّ يَعْمَلُ على شاكِلَتِه}؛ أنتم بريئون ممَّا أعمل، وأنا بريءٌ ممَّا تعملون.
{1 - 6} Yaani: Sema uwaambie makafiri, ukiwatangazia wazi wazi "Siabudu mnachokiabudu." Yaani jiweke mbali na vile walivyokuwa wakiviabudu badala ya Mwenyezi Mungu, kwa nje na ndani. "Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu" kwa sababu ya kutomkusudia Yeye tu kwenu katika kumwabudu Mwenyezi Mungu. Kumuabudu kwenu kulikoungana na ushirikina hakuitwi ibada. Na alirudia kusema hivyo ili cha kwanza kionyeshe kutokuwepo kwa kitendo, na cha pili kionyeshe kuwa haya yameshakuwa sifa isiyowaacha, na kwa sababu hii akatofautisha baina ya makundi haya mawili na akayapambanua,
akasema: "Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.
" Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Sema: Kila mmoja anafanya kwa namna yake." Nyinyi mko mbali mno na ninachofanya, na mimi niko mbali mno na mnayofanya.
* * *