Tafsiri ya Surat Ash-Sharh
Tafsiri ya Surat Ash-Sharh
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{أَلَمْ نَشْرَحْ لَكَ صَدْرَكَ (1) وَوَضَعْنَا عَنْكَ وِزْرَكَ (2) الَّذِي أَنْقَضَ ظَهْرَكَ (3) وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ (4) فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا (5) إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا (6) فَإِذَا فَرَغْتَ فَانْصَبْ (7) وَإِلَى رَبِّكَ فَارْغَبْ (8)}.
1. Hatukukunjulia kifua chako? 2. Na tukakuondolea mzigo wako. 3. Uliovunja mgongo wako? 4. Na tukakunyanyulia utajo wako? 5. Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi. 6. Hakika pamoja na uzito upo wepesi. 7. Na ukipata faragha, fanya juhudi. 8. Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie.
#
{1 - 4} يقول تعالى ممتنًّا على رسوله: {ألم نشرحْ لك صدرَك}؛ أي: نوسِّعْه لشرائع الدِّين والدَّعوة إلى الله والاتِّصاف بمكارم الأخلاق والإقبال على الآخرة وتسهيل الخيرات، فلم يكن ضيِّقاً حرجاً لا يكاد ينقاد لخيرٍ ولا تكاد تجده منبسطاً، {ووضعْنا عنك وِزْرَك}؛ أي: ذنبك، {الذي أنقَضَ}؛ أي: أثقل {ظهركَ}؛ كما قال تعالى: {ليغفرَ لك اللهُ ما تقدَّم من ذنبِكَ وما تأخَّر}، {ورفَعْنا لكَ ذِكْرَك}؛ أي: أعليْنا قدرَك، وجعلنا لك الثَّناء الحسن العالي، الذي لم يصلْ إليه أحدٌ من الخلق؛ فلا يُذْكَرُ الله؛ إلاَّ ذُكِر معه رسوله - صلى الله عليه وسلم -؛ كما في الدُّخول في الإسلام، وفي الأذان، والإقامة، والخطب ... وغير ذلك من الأمور التي أعلى الله بها ذِكر رسوله محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -، وله في قلوب أمَّته من المحبَّة والإجلال والتَّعظيم ما ليس لأحدٍ غيره بعد الله تعالى؛ فجزاه الله عن أمَّته أفضل ما جزى نبيًّا عن أمَّته.
{1 - 4} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema akimkumbusha Mtume wake neema zake: "Hatukukunjulia kifua chako" Kwa kukuteremshia sheria za dini, wito kwa Mwenyezi Mungu, kuwa na maadili mema, kutafuta maisha ya akhera, na kusahihisha mambo ya heri. Kwani hakikuwa chenye dhiki kilichobanika kisichotaka kufuata heri. "Na tukakuondolea mzigo wako" yaani, dhambi zako.
"Uliovunja mgongo wako?" Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Ili Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yajayo" kisha akasema "Na tukakunyanyulia utajo wako?" Yaani, tumeitukuza hadhi yako, na tumekufanya kutajwa kwa sifa nzuri na za hali ya juu ambazo hakuna hata mmoja miongoni mwa viumbe aliyewahi kuzifikia. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu hatajwi, isipokuwa Mtume wake – rehema na amani zimshukie – atatajwa pamoja naye. Kama ilivyo katika kuingia katika Uislamu, katika adhana, kukimu swala, khutba mbalimbali... na mambo mengineyo miongoni mwa mambo ambayo Mwenyezi Mungu ameuinua utajo wa Mtume wake Muhammad -rehema na amani zimshukie - naye anao katika nyoyo za umma wake upendo, heshima na taadhima ambazo hakuna mtu mwingine yeyote anazo baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu amlipe kwa sababu ya umma wake bora zaidi ya anavyowezakumlipa Nabii kwa sababu ya umma wake.
#
{5 - 6} وقوله: {فإنَّ مع العُسْرِ يُسْراً. إنَّ مع العُسْرِ يُسْراً}: بشارةٌ عظيمةٌ أنَّه كلَّما وُجِدَ عسرٌ وصعوبةٌ؛ فإنَّ اليسر يقارنه ويصاحبه، حتى لو دخل العسر جحر ضبٍّ؛ لدخل عليه اليسر فأخرجه؛ كما قال تعالى: {سيجعل اللهُ بعدَ عُسْرٍ يُسْراً}، وكما قال النبيُّ - صلى الله عليه وسلم -: «وإنَّ الفرج مع الكرب، وإنَّ مع العسر يسراً ».
وتعريف العسر في الآيتين يدلُّ على أنَّه واحدٌ، وتنكير اليسرِ يدلُّ على تكراره؛ فلن يغلب عسرٌ يسرين.
وفي تعريفه بالألف واللاَّم الدالِّ - على الاستغراق والعموم يدل على أنَّ كلَّ عسرٍ وإنْ بلغ من الصعوبة ما بلغ؛ فإنَّه في آخره التيسير ملازمٌ له.
{5 - 6} Na kauli yake: "Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi. Hakika pamoja na uzito upo wepesi." Hii ni bishara kubwa kwamba kila inapopatikana dhiki na shida, basi urahisi unaambatana nayo na kuwa pamoja nayo, kiasi kwamba hata ikiwa uzito utaingia kwenye shimo la mjusi, basi wepesi ungeuingilia humo na kuutoa nje.
Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mwenyezi Mungu atajaalia baada ya dhiki faraja," na kama Nabii - rehema na amani zimshukie -
alivyosema: "Hakika pamoja na dhiki kuna faraja, na hakika pamoja na dhiki kuna wepesi." Neno uzito katika Aya hizi mbili limekuja kama nomino maalumu ili kuashiria kwamba ni mmoja, nalo neno wepesi limetumika katika hali ya nomino ya kawaida ili kuashiria kwamba wepesi hujirudiarudia. Kwa hivyo, uzito mmoja hauwezi kushinda wepesi mbili. Na pia matumizi ya herufi alif na lam katika neno uzito kwa Kiarabu, yenye maana ya ujumla, yanaashiria kwamba kila uzito hata ukiwa mgumu kiasi gani, lazima mwishoni mwake kuna wepesi.
#
{7 - 8} ثم أمر [اللَّهُ] رسوله أصلاً والمؤمنين تبعاً بشكره والقيام بواجب نعمه، فقال: {فإذا فرَغْتَ فانصَبْ}؛ أي: إذا تفرَّغْتَ من أشغالِك، ولم يبقَ في قلبكَ ما يعوقه؛ فاجتهدْ في العبادة والدُّعاء، {وإلى ربِّك}: وحده {فارغَبْ}؛ أي: أعظم الرغبة في إجابة دعائك وقبول دعواتك ، ولا تكنْ ممَّن إذا فرغوا ؛ لعبوا وأعرضوا عن ربِّهم وعن ذِكْرِه، فتكون من الخاسرين.
وقد قيل: إنَّ معنى هذا: فإذا فرغتَ من الصَّلاة وأكملتها؛ فانصب في الدُّعاء، وإلى ربِّك فارغبْ في سؤال مطالبك.
واستدلَّ من قال هذا القول على مشروعيَّة الدُّعاء والذِّكر عقب الصلوات المكتوبات. والله أعلم [وبذالك].
{7 - 8} Kisha
[Mwenyezi Mungu] akamwamrisha Mtume wake kwanza, na Waumini kwa kumfuata, kumshukuru na kutimiza wajibu wa neema zake,
akasema: "Na ukipata faragha, fanya juhudi" yaani unapomaliza shughuli zako, na kukawa hakuna kitu kinachobaki moyoni mwako cha kuuzuia, basi jitahidini katika ibada na dua, "Na Mola wako Mlezi" peke yake "ndio mshughulikie." Yaani, kuwa na shauku kubwa ya kutaka kuitikiwa dua zako, na usiwe miongoni mwa wale ambao wanapomaliza, wanafanya mchezo na wakampa mgongo Mola wao Mlezi na pia utajo wake, basi ukawa miongoni mwa waliohasirika. Na imesemwa kwamba maana yake ni kwamba unapomaliza swala na ukaikamilisha, basi jitahidi katika kuomba dua, na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie kwa kuomba unayoyataka. Aliyeisema kauli hii iliitumia kama ushahidi wa uhalali wa kuomba dua na kumtaja Mwenyezi Mungu baada ya swala za lazima. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye hilo zaidi.
Imekamilika, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.
* * *