Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ (1) وَطُورِ سِينِينَ (2) وَهَذَا الْبَلَدِ الْأَمِينِ (3) لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ (4) ثُمَّ رَدَدْنَاهُ أَسْفَلَ سَافِلِينَ (5) إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَلَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ (6) فَمَا يُكَذِّبُكَ بَعْدُ بِالدِّينِ (7) أَلَيْسَ اللَّهُ بِأَحْكَمِ الْحَاكِمِينَ (8)}.
1. Ninaapa kwa tini na zaituni! 2. Na kwa Mlima wa Sinai! 3. Na kwa mji huu wenye amani! 4. Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa. 5. Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini! 6. Lakini wale walioamini na wakatenda mema, hao watapata ujira usiokwisha. 7. Basi ni kipi baadaye kitakachokukukadhibishia malipo? 8. Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?
#
{1 - 3} {التين}: هو التين المعروف، وكذلك {الزَّيتون}؛ أقسم بهاتين الشجرتين؛ لكثرة منافع شجرهما وثمرهما، ولأنَّ سلطانهما في أرض الشام محلِّ نبوَّة عيسى ابن مريم عليه السلام، {وطورِ سينينَ}؛ أي: طور سيناء محلِّ نبوَّة
موسى عليه السلام ، {وهذا البلدِ الأمينِ}: وهو مكَّة المكرَّمة محلُّ نبوَّة محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -. فأقسم تعالى بهذه المواضع المقدَّسة التي اختارها وابتعث منها أفضل الأنبياء وأشرفهم.
{1 - 3} Mwenyezi Mungu aliapa kwa miti hii miwili; kwa sababu ya manufaa mengi ya miti hii na matunda yake, na kwa sababu mamlaka yake katika ardhi ya Sham ndiyo yalikuwa mahala pa unabii wa Isa bin Maryam, amani iwe juu yake "Na kwa Mlima wa Sinai" ambapo palikuwa mahali pa unabii wa Musa, amani iwe juu yake. "Na kwa mji huu wenye amani!" Nao ni Makka Tukufu, mahala pa unabii pa Muhammad - rehema na amani zimshukie. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akaapa kwa sehemu hizi takatifu ambazo alizichagua na akatuma kutoka hapo manabii bora na watukufu zaidi.
#
{4} والمقسم عليه قوله: {لقد خَلَقْنا الإنسان في أحسنِ تقويمٍ}؛ أي: تامَّ الخلق، متناسب الأعضاء، منتصب القامة، لم يفقد ممَّا يحتاج إليه ظاهراً وباطناً شيئاً.
{4} Kinachoapwa kwa ajili yake hapa ni kauli yake: "Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lililo bora kabisa" na hakukosa chochote anachohitaji, kwa nje na ndani.
#
{5 - 6} ومع هذه النعم العظيمة، التي ينبغي منه القيام بشكرها؛ فأكثر الخلق منحرفون عن شكر المنعم، مشتغلون باللَّهو واللَّعب، قد رضوا لأنفسهم بأسافل الأمور وسفساف الأخلاق، فردَّهم الله {في أسفل سافلين}؛ أي: أسفل النَّار موضع العصاة المتمرِّدين على ربِّهم؛ إلاَّ مَن منَّ الله عليه بالإيمان والعمل الصَّالح والأخلاق الفاضلة العالية، {فلهم}: بذلك المنازل العالية، و {أجرٌ غيرُ ممنونٍ}؛ أي: غير مقطوع، بل لَذَّاتٌ متوافرةٌ وأفراحٌ متواترةٌ ونعمٌ متكاثرةٌ؛ في أبدٍ لا يزول، ونعيمٍ لا يحول، أكُلُها دائمٌ وظلُّها.
{5 - 6} Na licha ya neema hizi kuu, ambazo anapaswa kushukuru kwa sababu yake; viumbe wengi wamepotoka mbali na kutoa shukurani kwa neema hizi, kwa sababu ya wamejishughulisha pumbao na michezo, na wamejiridhisha na mambo duni kabisa na tabia chafu, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawarudisha "kuwa chini kuliko walio chini" Motoni, ambapo ni mahali pa watu maasi wanaomuasi Mola wao Mlezi. Isipokuwa wale ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha kwa imani, vitendo vyema na maadili mema ya juu. "Hao watapata" kwa sababu ya hayo vyeo vya juu na "ujira usiokwisha" Bali ni raha zinazopatikana, furaha za kuwajia mara kwa mara, na neema nyingi za kudumu umilele bila ya kuondoka, matunda yake ni ya daima na pia kivuli chake.
#
{7 - 8} {فما يكذِّبك بعدُ بالدِّينِ}؛ أي: أيُّ شيءٍ يكذِّبك أيُّها الإنسان بيوم الجزاء على الأعمال؟ وقد رأيت من آيات الله الكثيرة ما يحصل لك به اليقين ، ومن نعمه ما يوجب عليك أن لا تكفر بشيءٍ منها. {أليس الله بأحكم الحاكمينَ}: فهل تقتضي حكمته أن يترك الخلق سدىً لا يُؤمرون ولا يُنْهَوْن ولا يُثابون ولا يُعاقبون؟ أم الذي خلق الإنسان أطواراً بعد أطوارٍ، وأوصل إليهم من النعم والخير والبرِّ ما لا يحصونه، وربَّاهم التربية الحسنة؛ لا بدَّ أن يعيدهم إلى دارٍ هي مستقرُّهم وغايتهم التي إليها يقصدون ونحوها يؤمُّون.
{7 - 8} "Basi ni kipi baadaye kitakachokukukadhibishia malipo?" Yaani, ni nini kinachokufanya kukanusha ewe mwanadamu Siku ya Malipo juu ya matendo? Umeshaziona ishara nyingi za Mwenyezi Mungu zinazokupa yakini, na neema zake ambazo zinaweza kukufanya kutokufuru hata kimoja katika hizo. "Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?" Je, hekima yake inaweza kutaka aache viumbe bure, wasiamrishwe wala wasikatazwe, wala wasilipwe mazuri wala wasiadhibiwe? Au yule aliyemuumba mwanadamu hatua baada ya hatua, na akawafikisha neema mbalimbali, heri na wema visivyo na kipimo, na akawalea kwa malezi mazuri ni lazima awarudishe kwenye nyumba ambayo ndiyo makazi yao na marudio yao wanayokwenda na wanayoamini.
Imekamilika, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.
* * *