:
Tafsiri ya Surat Al-Dhuha
Tafsiri ya Surat Al-Dhuha
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
: 1 - 11 #
{وَالضُّحَى (1) وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَى (2) مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَى (3) وَلَلْآخِرَةُ خَيْرٌ لَكَ مِنَ الْأُولَى (4) وَلَسَوْفَ يُعْطِيكَ رَبُّكَ فَتَرْضَى (5) أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَآوَى (6) وَوَجَدَكَ ضَالًّا فَهَدَى (7) وَوَجَدَكَ عَائِلًا فَأَغْنَى (8) فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ (9) وَأَمَّا السَّائِلَ فَلَا تَنْهَرْ (10) وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ (11)}.
1. Ninaapa kwa mchana! 2. Na kwa usiku unapotanda! 3. Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe. 4. Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko uliotangulia. 5. Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike. 6. Kwani hakukukuta yatima akakupa makazi? 7. Na akakukuta umepotea akakuongoa? 8. Akakukuta mhitaji akakutosheleza? 9. Basi yatima usimwonee! 10. Na anayeomba au kuuliza usimkaripie! 11. Na neema za Mola wako Mlezi zisimulie.
#
{1 - 3} أقسم تعالى بالنهار إذا انتشر ضياؤه؛ بالضُّحى، وبالليل {إذا سجى} وادلهمَّت ظلمته؛ على اعتناء الله برسوله - صلى الله عليه وسلم -، فقال: {ما ودَّعك ربُّك}؛ أي: ما تركك منذ اعتنى بك، ولا أهملك منذ ربَّاك ورعاك، بل لم يزل يربِّيك أكمل تربيةٍ ويُعليك درجةً بعد درجةٍ، {وما}: قلاكَ الله؛ أي: ما أبغضك منذ أحبَّك؛ فإنَّ نفي الضِّدِّ دليلٌ على ثبوت ضدِّه، والنفي المحض لا يكون مدحاً إلاَّ إذا تضمَّن ثبوت كمال. فهذه حال الرسول - صلى الله عليه وسلم - الماضية والحاضرة، أكمل حال وأتمُّها، محبَّة الله له واستمرارها وترقيته في درجات الكمال ودوام اعتناء اللَّه به.
{1 - 3} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaapa kwa mchana unapotanda mwangaza wake wakati wa dhuha, na usiku "unapotanda" na giza lake likafunika sawasawa. Haya yanaonyesha kujali kwa Mwenyezi Mungu Mtume wake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie. Akasema: "Mola wako Mlezi hakukuacha" tangu alipokujali, wala hajakutelekeza tangu alipokulea na kukutunza. Bali anaendelea kukulea kwa malezi kamilifu zaidi na kukuinua daraja moja baada ya nyingine. "wala" Mwenyezi Mungu "hakukasirika nawea" tangu alipokupenda. Kwa maana kukanusha kinyume cha kitu ni ushahidi wa kuthibitika kwa kinyume chake, na ukanushaji mtupu tu hauonyeshi kusifika kwa kitu hicho isipokuwa ikiwa hilo linajumuisha kuthibitisha ukamilifu wake. Hii ndiyo hali ya Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – ya zamani na ya sasa, hali kamili zaidi ya upendo wa Mwenyezi Mungu kwake, kuendelea kwake, kumpandisha kwake hadi kwenye viwango vya ukamilifu, na Mwenyezi Mungu kuendelea kumtunza.
#
{4} وأمَّا حاله المستقبلة؛ فقال: {وللآخرةُ خيرٌ لك من الأولى}؛ أي: كلُّ حالةٍ متأخِّرةٍ من أحوالك؛ فإنَّ لها الفضل على الحالة السابقة، فلم يزل - صلى الله عليه وسلم - يصعد في درجات المعالي، ويمكِّن اللَّه له دينه، وينصره على أعدائِه، ويسدِّده في أحواله، حتَّى مات وقد وصل إلى حال ما وصل إليها الأوَّلون والآخرون؛ من الفضائل والنِّعم وقرَّة العين وسرور القلب.
{4} Na ama hali yake ya baadaye, akasema: "Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko uliotangulia" Kwa hivyo, yeye - rehema na amani ziwe juu yake - aliendelea kupanda katika daraja za utukufu, na Mwenyezi Mungu akamtilia nguvu katika dini yake, akampa ushindi dhidi ya maadui zake, na akamuweka sawasawa katika hali zake, mpaka akafa huku amefikia hali ambayo hawakuifikia watu wa kale na wa baadaye, kama vile fadhila, neema, kipendezacho macho na furaha ya moyo.
#
{5} ثمَّ بعد هذا لا تسأل عن حاله في الآخرةِ من تفاصيل الإكرام وأنواع الإنعام، ولهذا قال: {ولَسوف يعطيكَ ربُّك فترضى}: وهذا أمرٌ لا يمكن التعبير عنه إلاَّ بهذه العبارة الجامعة الشاملة.
{5} Kisha baada ya haya, hata usiulize kuhusu hali yake ya Akhera ya sifa za utukufu na aina mbalimbali za neema, na ndiyo maana akasema: "Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike." Hili ni jambo ambalo haliwezi kuelezewa isipokuwa kwa maneno haya yenye kujumuisha, ya kina.
#
{6 - 8} ثم امتنَّ عليه بما يعلمه من أحواله الخاصَّة ، فقال: {ألمْ يجدْكَ يتيماً فآوى}؛ أي: وجدك لا أمَّ لك ولا أبَ، بل قد مات أبوه وأمُّه وهو لا يدبِّر نفسه، فآواه الله، وكفَّله جدَّه عبد المطلب، ثم لمَّا مات جدُّه؛ كفَّله الله عمَّه أبا طالب، حتى أيَّده [اللَّه] بنصره وبالمؤمنين، {ووجدك ضالًّا فهدى}؛ أي: وجدك لا تدري ما الكتابُ ولا الإيمانُ، فعلَّمك ما لم تكن تعلمُ، ووفَّقك لأحسن الأعمال والأخلاق. {ووجدك عائلاً}؛ أي: فقيراً، فأغناكَ الله بما فتح عليك من البلدان، التي جُبيت لك أموالها وخراجها، فالذي أزال عنك هذه النقائص سيزيل عنك كلَّ نقصٍ، والذي أوصلك إلى الغنى وآواك ونصرك وهداك، قابلْ نعمته بالشُّكران.
{6 - 8} Kisha akamwambia juu ya neema aliyompa na ambayo anaijua iliyokuwa katika hali zake zilizopita kitambo, akasema: "Kwani hakukukuta yatima akakupa makazi?" Kwani baba yake na mama yake walikuwa wameshakufa na hakuwa anaweza kujisimamia mwenyewe, basi Mwenyezi Mungu akampa hifadhi kwa kumfanya babu yake, Abdul-Muttalib kumlea. Kisha babu yake alipokufa, Mwenyezi Mungu akamfanya ami yake, Abu Talib kumlea mpaka [Mwenyezi Mungu] alipomuunga mkono kwa ushindi na kwa Waumini. "Na akakukuta umepotea akakuongoa?" Yaani: Alikukuta hujui Kitabu ni nini wala Imani, kwa hivyo akakufundisha yale ambayo hukuwa unayajua, na akakuwezesha kufanya matendo na maadili mema. "Akakukuta mhitaji" kwa hivyo, akakutosheleza kwa nchi alizokufungulia, ambazo mali zake na hazina zake zililetwa kwako. Kwa hivyo, yule aliyekuondolea mapungufu haya, atakuondolea kila mapungufu. na yule aliyekufikishia utajiri huu, akakupa hifadhi, akakunusuru na akakuongoza, basi zikabili neema zake hizi kwa kushukuru.
#
{9 - 11} ولهذا قال: {فأمَّا اليتيمَ فلا تَقْهَرْ}؛ أي: لا تُسِئْ معاملة اليتيم، ولا يَضِقْ صدرُك عليه، ولا تنهره، بل أكرمه، وأعطه ما تيسَّر، واصنع به كما تحبُّ أن يُصْنَعَ بولدك من بعدك، {وأمَّا السائلَ فلا تنهر}؛ أي: لا يصدر منك كلامٌ للسائل يقتضي ردَّه عن مطلوبه بنَهْرٍ وشراسةِ خلقٍ، بل أعطه ما تيسَّر عندك، أو ردَّه بمعروفٍ وإحسانٍ. ويدخل في هذا السائل للمال والسائل للعلم، ولهذا كان المعلِّم مأموراً بحسن الخلق مع المتعلِّم ومباشرته بالإكرام والتحنُّن عليه؛ فإنَّ في ذلك معونةً له على مقصده وإكراماً لمن كان يسعى في نفع العباد والبلاد، {وأمَّا بنعمة ربِّك فَحَدِّثْ}: وهذا يشمل النِّعم الدينيَّة والدنيويَّة ؛ أي: أثْنِ على الله بها، وخُصَّها بالذِّكر إن كان هناك مصلحةٌ، وإلاَّ؛ فحدِّث بنعم الله على الإطلاق؛ فإنَّ التحدُّث بنعمة الله داعٍ لشكرها وموجبٌ لتحبيب القلوب إلى من أنعم بها؛ فإنَّ القلوب مجبولةٌ على محبَّة المحسن.
{9 - 11} Ndiyo maana akasema: "Basi yatima usimwonee" kwa kuamiliana naye kwa ubaya, wala usiwe na kifua kifunyu mbele yake, wala usimkaripie, bali mheshimu, mpe uwezavyo, na mfanyie vile unavyotaka afanyiwe mtoto wako baada yako. "Na anaye omba au kuuliza usimkaripie" na kumwonyesha tabia mbaya, bali mpe kile kinachopatikana kwako kwa wepesi, au umjibu kwa wema na uzuri. Hili linajumuisha yule anayeomba mali na yule anayeomba elimu, na ndiyo maana mwalimu aliamrishwa kuwa na tabia njema mbele ya mwanafunzi na kumwonyesha heshima na huruma. Hayo ni msaada kwake katika kufikia lengo lake na ni kumtukuza yule anayefanya bidii ya kuwanufaisha waja na nchi. "Na neema za Mola wako Mlezi zisimulie." Hili linajumuisha neema za kidini na za kidunia. Yaani, msifu Mwenyezi Mungu kwa sababu yake, na zitaje hizo hasa ikiwa kuna masilahi, vinginevyo; zitaje tu neema za Mwenyezi Mungu kwa ujumla. Kwani kuzitaja neema za Mwenyezi Mungu ni sababu ya kumfanya mtu kumshukuru na husababisha mioyo kumpenda yule aliyezineemesha. Kwa sababu mioyo imeumbwa kumpenda aliyezifanyia wema.
* * *