Tafsiri ya Surat Ash-Shams
Tafsiri ya Surat Ash-Shams
Ilishuka Makka
{وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا (1) وَالْقَمَرِ إِذَا تَلَاهَا (2) وَالنَّهَارِ إِذَا جَلَّاهَا (3) وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَاهَا (4) وَالسَّمَاءِ وَمَا بَنَاهَا (5) وَالْأَرْضِ وَمَا طَحَاهَا (6) وَنَفْسٍ وَمَا سَوَّاهَا (7) فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَا (8) قَدْ أَفْلَحَ مَنْ زَكَّاهَا (9) وَقَدْ خَابَ مَنْ دَسَّاهَا (10) كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِطَغْوَاهَا (11) إِذِ انْبَعَثَ أَشْقَاهَا (12) فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّهِ نَاقَةَ اللَّهِ وَسُقْيَاهَا (13) فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمْدَمَ عَلَيْهِمْ رَبُّهُمْ بِذَنْبِهِمْ فَسَوَّاهَا (14) وَلَا يَخَافُ عُقْبَاهَا (15)}.
1. Ninaapa kwa jua na mwangaza wake! 2. Na kwa mwezi unapolifuatia! 3. Na kwa mchana unapolidhihirisha! 4. Na kwa usiku unapolifunika! 5. Na kwa mbingu na kwa aliyeijenga! 6. Na kwa ardhi na kwa aliyeitandaza! 7. Na kwa nafsi na kwa aliyeitengeneza! 8. Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake. 9. Hakika amefanikiwa aliyeitakasa. 10. Na hakika amehasiri aliyeiviza. 11. Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao. 12. Aliposimama mwovu wao mkubwa. 13.
Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipowaambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake. 14. Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa. 15. Wala Yeye haogopi matokeo yake.
#
{1 - 6} أقسم تعالى بهذه الآيات العظيمة على النفس المفلحة وغيرها من النفوس الفاجرة، فقال: {والشمس وضُحاها}؛ أي: نورها ونفعها الصادر منها، {والقمر إذا تلاها}؛ أي: تبعها في المنازل والنور، {والنَّهار إذا جلاَّها}؛ أي: جلَّى ما على وجه الأرض وأوضحه، {والليل إذا يغشاها}؛ أي: يغشى وجه الأرض، فيكون ما عليها مظلماً؛ فتعاقُبُ الظُّلمة والضياء والشمس والقمر على هذا العالم بانتظام وإتقانٍ وقيامٍ لمصالح العباد أكبر دليل على أن الله بكلِّ شيءٍ عليمٌ وعلى كلِّ شيءٍ قديرٌ، وأنَّه المعبود وحده، الذي كلُّ معبودٍ سواه باطل ، {والسَّماء وما بناها}: يحتمل أن {ما} موصولة، فيكون الإقسام بالسماء وبانيها، وهو الله تعالى ، ويحتمل أنها مصدريَّة، فيكون الإقسام بالسماء وبنيانها الذي هو غاية ما يقدَّر من الإحكام والإتقان والإحسان. ونحو هذا قوله: {والأرضِ وما طحاها}؛ أي: مدَّها ووسَّعها، فتمكَّن الخلق حينئذٍ من الانتفاع بها بجميع أوجه الانتفاع.
{1 - 6} Mwenyezi Mungu Mtukufu aliapa kwa ishara hizi kubwa juu ya nafsi iliyofanikiwa na nafsi nyinginezo ambazo ni ovu,
akasema: "Ninaapa kwa jua na mwangaza wake" na manufaa yake yatokayo humo. "Na kwa mwezi unapolifuatia" katika mashukio na nuru. "Na kwa mchana unapolidhihirisha!" Yaani unapodhihirisha na kuweka wazi vitu vilivyo juu ya uso wa ardhi. "Na kwa usiku unapolifunika." Yaani, unapofunika uso wa ardhi, kwa hivyo kila kilicho juu yake kinakuwa gizani. Basi mfuatano wa giza, nuru, jua na mwezi juu ya ulimwengu huu kwa mpangilio nzuri sana na kusimama sawaswa kwa masilahi ya waja ni ushahidi mkubwa zaidi kwamba Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi kila kitu, na ni Mwenye uwezo mno juu ya kila kitu, na kwamba Yeye pekee ndiye anayepasa kuabudiwa, ambaye kila kitu kingine kinachoabudiwa ni batili. "Na kwa mbingu na kwa aliyeijenga" Hapa inawezekana kwamba Mwenyezi Mungu aliapa kwa mbingu na aliyeijenga, ambaye ni Mwenyezi Mungu Mtukufu mwenyewe. Na inawezekana kwamba aliapa kwa mbingu na kujengwa kwake, ambako ndicho kipimo cha mwisho zaidi cha uundaji wa ustadi na uzuri.
Na mfano wa hili ni kauli yake: "Na kwa ardhi na kwa aliyeitandaza" ili viumbe viweze kunufaika kwayo katika nyanja zote za manufaa.
#
{7 - 8} {ونفسٍ وما سوَّاها}: يحتمل أنَّ المراد: ونفس سائر المخلوقات الحيوانيَّة؛ كما يؤيِّد هذا العموم، ويُحتمل أنَّ الإقسام بنفس الإنسان المكلَّف؛ بدليل ما يأتي بعده. وعلى كل؛ فالنفس آيةٌ كبيرةٌ من آياته التي يحقُّ الإقسام بها ؛ فإنَّها في غاية اللُّطف والخفَّة، سريعة التنقُّل والحركة والتغيُّر والتأثُّر والانفعالات النفسيَّة من الهمِّ والإرادة والقصد والحبِّ والبغض، وهي التي لولاها؛ لكان البدن مجرَّد تمثال لا فائدة فيه، وتسويتها على ما هي عليه آيةٌ من آيات الله العظيمة.
{7 - 8} "Na kwa nafsi na kwa aliyeitengeneza sawasawa!" Inawezekana kwamba kinachokusudiwa hapa ni nafsi za wanyama wote. Hili linaungwa mkono na ujumla huu, na pia inawezekana kwamba kiapo hiki kinahusiana na mtu ambaye yeye ndiye aliyejukumishwa kisheria, kwa ushahidi wa yale yanayokuja baada yake. Kwa hivyo, nafsi ni ishara kubwa katika ishara zake zinazostahiki kuapa kwazo. Kwani imefichikana na ni nyepesi zaidi, ni yenye kusonga kwa harakati za wepesi mno, na kubadilika, kuathirika, na kuwa na mihemko ya kisaikolojia kama vile wasiwasi kubwa, utashi, nia, upendo na chuki. Na kama haingekuwa hiyo, basi mwili ungekuwa tu sanamu isiyo na maana, na kuitengeneza sawasawa kama ilivyo ni moja katika ishara kuu za Mwenyezi Mungu.
#
{9 - 10} وقوله: {قد أفلح من زكَّاها}؛ أي: طهَّر نفسه من الذُّنوب، ونقَّاها من العيوب، ورقَّاها بطاعة الله، وعلاَّها بالعلم النافع والعمل الصالح، {وقد خاب من دسَّاها}؛ أي: أخفى نفسه الكريمة التي ليست حقيقة بقمعها وإخفائها بالتدنُّس بالرَّذائل والدُّنوِّ من العيوب والذُّنوب ، وترك ما يكمِّلها وينمِّيها، واستعمال ما يشينها ويدسِّيها.
{9 - 10} Na kauli yake: "Hakika amefanikiwa aliyeitakasa" kutokana na madhambi, kasoro, na akaipandisha kwa kumtii Mwenyezi Mungu, na akaiinua juu kwa elimu yenye manufaa na matendo mema. "Na hakika amekhasiri aliyeiviza." Yaani, aliificha nafsi yake kwa kuichafua kwa machafu na kuwa karibia na kasoro na madhambi, kuacha yale yanayoikamilisha na kuikuza.
#
{11 - 15} {كذَّبت ثمود بطَغْواها}؛ أي: بسبب طغيانها وترفُّعها عن الحقِّ وعتوِّها على رسولهم ، {إذ انبعث أشقاها}؛ أي: أشقى القبيلة ، وهو قُدَار بن سالف؛ لعقرها؛ حين اتَّفقوا على ذلك وأمروه فائتمر لهم، {فقال لهم رسولُ اللهِ}: صالحٌ عليه السلام محذِّراً: {ناقة الله وسُقْياها}؛ أي: احذروا عقر ناقة الله التي جعلها لكم آيةً عظيمةً، ولا تقابلوا نعمة الله عليكم بسقي لبنها أن تعقروها، فكذَّبوا نبيَّهم صالحاً، {فعقروها فدمدم عليهم ربُّهم بذنبهم}؛ أي: دمَّر عليهم، وعمَّهم بعقابه، وأرسل عليهم الصَّيحة من فوقهم والرَّجفة من تحتهم، فأصبحوا جاثمين على ركبهم، لا تجد منهم داعياً ولا مجيباً، {فسوَّاها}: عليهم؛ أي: سوَّى بينهم في العقوبة ، {ولا يخافُ عُقْباها}؛ أي: تبعتها. وكيف يخاف من هو قاهر لا يخرج عن قهره وتصرُّفه مخلوقٌ. الحكيم في كلِّ ما قضاه وشرعه.
{11 - 15} "Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao" wakaacha haki na wakamuasi Mtume wao. "Aliposimama mwovu wao mkubwa" ambaye ni Qudar bin Salif ili amchinje walipokubaliana juu ya hilo na wakamuamuru awafanyie hivyo. "Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu" Salih, amani ziwe juu yake, "akawaambia" akionya "Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake." Yaani, jihadharini na kumuua ngamia wa Mwenyezi Mungu ambaye amekuwekeeni kuwa ni ishara kubwa, na wala msiipinge neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu ya kukunywesheni maziwa yake kwa kumuua, lakini wakamkadhibisha Mtume wao Salih "na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao" kwa kuwatumia ukelele kutokea juu yao na mtetemeko wa kutokea chini yao, basi kulipokucha wakawa majumbani mwao kifudifudi, wala hakukuta miongoni mwao mwenye kuita wala mwenye kuitikia. "Na akawafuta kabisa. Wala Yeye haogopi matokeo yake." Na je, anawezaje kuhofu Yule ambaye ni mshindi na wala hakuna kiumbe kinachoweza kutosha katika ushindi wake wala uendeshaji wake, ambaye ni Mwenye hekima katika kila anachopanga na kukiweka kama sheria?
[Imekamilika, sifa njema ni za Mwenyezi Mungu].
* * *