:
Tafsiri ya Surat Al-Balad
Tafsiri ya Surat Al-Balad
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
: 1 - 20 #
{لَا أُقْسِمُ بِهَذَا الْبَلَدِ (1) وَأَنْتَ حِلٌّ بِهَذَا الْبَلَدِ (2) وَوَالِدٍ وَمَا وَلَدَ (3) لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ فِي كَبَدٍ (4) أَيَحْسَبُ أَنْ لَنْ يَقْدِرَ عَلَيْهِ أَحَدٌ (5) يَقُولُ أَهْلَكْتُ مَالًا لُبَدًا (6) أَيَحْسَبُ أَنْ لَمْ يَرَهُ أَحَدٌ (7) أَلَمْ نَجْعَلْ لَهُ عَيْنَيْنِ (8) وَلِسَانًا وَشَفَتَيْنِ (9) وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ (10) فَلَا اقْتَحَمَ الْعَقَبَةَ (11) وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْعَقَبَةُ (12) فَكُّ رَقَبَةٍ (13) أَوْ إِطْعَامٌ فِي يَوْمٍ ذِي مَسْغَبَةٍ (14) يَتِيمًا ذَا مَقْرَبَةٍ (15) أَوْ مِسْكِينًا ذَا مَتْرَبَةٍ (16) ثُمَّ كَانَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ وَتَوَاصَوْا بِالْمَرْحَمَةِ (17) أُولَئِكَ أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ (18) وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا هُمْ أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ (19) عَلَيْهِمْ نَارٌ مُؤْصَدَةٌ (20)}.
1. Ninaapa kwa Mji huu! 2. Nawe unaukaa Mji huu. 3. Na ninaapa kwa mzazi na alichokizaa. 4. Hakika tumemuumba mtu katika taabu. 5. Ati anadhani hapana yeyote atayemuweza? 6. Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali. 7. Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona? 8. Kwani hatukumpa macho mawili? 9. Na ulimi, na midomo miwili? 10. Na tukambainishia zote njia mbili? 11. Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. 12. Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani? 13. Kumkomboa mtumwa. 14. Au kumlisha siku ya njaa. 15. Yatima aliye jamaa. 16. Au masikini aliye vumbini. 17. Tena awe miongoni mwa walioamini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana. 18. Hao ndio watu wa kheri wa kuliani. 19. Lakini waliozikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni. 20. Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande.
#
{1 - 3} يقسم تعالى {بهذا البلدِ} الأمين، وهو مكَّة المكرَّمة، أفضل البلدان على الإطلاق، خصوصاً وقت حلول الرسول - صلى الله عليه وسلم - فيها، {ووالدٍ وما وَلَدَ}؛ أي: آدم وذرِّيَّته.
{1 - 3} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaapa "kwa Mji huu," ambayo ni Makka Tukufu, iliyo bora zaidi kuliko miji yote, hasa wakati wa kuwepo huko kwa Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie. "Na kwa mzazi na alichokizaa." Yaani, Adam na kizazi chake.
#
{4 - 7} والمقسَم عليه قولُه: {لقد خَلَقْنا الإنسانَ في كَبَدٍ}: يُحتمل أنَّ المراد بذلك ما يكابده ويقاسيه من الشَّدائد في الدُّنيا وفي البرزخ ويوم يقوم الأشهاد، وأنَّه ينبغي له أن يسعى في عملٍ يُريحُهُ من هذه الشَّدائد ويوجب له الفرح والسرور الدَّائم، وإن لم يفعلْ؛ فإنَّه لا يزال يكابد العذاب الشديد أبد الآباد، ويحتمل أن المعنى لقد خلقنا الإنسان في أحسن تقويم وأقوم خِلْقة يقدر على التصرف والأعمال الشديدة ومع ذلك فإنه لم يشكر الله على هذه النِّعمة العظيمة، بل بطر بالعافية، وتجبَّر على خالقه، فَحَسِبَ بجهله وظلمه أنَّ هذه الحال ستدوم له، وأنَّ سلطان تصرُّفه لا ينعزل، ولهذا قال [تعالى]: {أيحسبُ أن لن يقدِر عليه أحدٌ}: ويطغى ويفتخر بما أنفق من الأموال على شهوات نفسه؛ فيقول {أهلكتُ مالاً لُبَداً}؛ أي: كثيراً بعضه فوق بعض. وسمى الله [تعالى] الإنفاق في الشَّهوات والمعاصي إهلاكاً؛ لأنَّه لا ينتفع المنفق بما أنفق، ولا يعود إليه من إنفاقه إلاَّ النَّدم والخسار والتَّعب والقلَّة، لا كمن أنفق في مرضاة الله في سبيل الخير؛ فإنَّ هذا قد تاجر مع الله وربح أضعاف أضعاف ما أنفق، قال الله متوعِّداً هذا الذي افتخر بما أنفق في الشهوات: {أيحسبُ أن لم يَرَهُ أحدٌ}؛ أي: أيظنُّ في فعله هذا أنَّ الله لا يراه ويحاسبه على الصغير والكبير؟! بل قد رآه الله وحفظ عليه أعماله ووكل به الكرام الكاتبين لكل ما عمله من خيرٍ وشرٍّ.
{4 - 7} Kinachokusudiwa na kiapo hapa ni kauli yake: "Hakika tumemuumba mtu katika taabu." Inawezekana kwamba kinachokusudiwa kwa hilo ni dhiki anazostahimili duniani, katika kaburi na Siku watakaposimama mashahidi, na kwamba ajitahidi kufanya matendo yatakayomwondolea matatizo haya na kumletea furaha na raha ya kudumu. Na kama hatafanya hivyo, basi ataendelea kupata mateso makali milele na milele. Na inawezekana kwamba maana yake ni kwamba tumemuumba mwanadamu katika umbo lililo bora kabisa na umbile lililonyooka kabisa, mwenye uwezo wa kutenda na kufanya vitendo vigumu, lakini pamoja na hayo, hakumshukuru Mwenyezi Mungu juu ya neema hizi kuu. Bali alifanyia majigambo salama aliyopewa, na kumfanyia kiburi Muumba wake, kwa hivyo akafikiri, kwa ujinga wake na udhalimu wake, kwamba ataendelea kuwa katika hali hii, na mamlaka ya vitendo vyake hayataondolewa, na ndiyo maana [Mwenyezi Mungu] akasema: "Ati anadhani hapana yeyote atakayemuweza?" Anafanya kiburi na fahari juu ya mali anazozitumia kwa ajili ya matamanio yake. Anasema: “Nimeteketeza chungu ya mali." Hapa Mwenyezi Mungu aliita kutumia mali katika matamanio na maasia kuwa ni kuteketeza. Kwa sababu mtoaji wake hanufaiki na alichotoa, na hakuna kinachomrudia katika kutoa kake isipokuwa majuto, hasara, uchovu na uhaba. Si kama mtu aliyetoa kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu katika njia za heri. Kwa maana mtu huyu amefanya biashara na Mwenyezi Mungu na amepata faida mara nyingi zaidi kuliko alivyotoa. Mwenyezi Mungu amesema akimtishia kwa adhabu mtu huyu ambaye alijivunia kile alichokitumia katika matamanio: "Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anayemwona?" Na kwamba Mwenyezi Mungu hamuoni na atamuuliza kuwajibika juu ya mambo madogo na makubwa? Bali Mwenyezi Mungu alimwona, akamhifadhia matendo yake, na akamuwekea hapo waandishi wa heshima kwa yote aliyoyafanya, yawe mema au maovu.
#
{8 - 10} ثم قرَّره بنعمه، فقال: {ألم نجعل له عينين. ولساناً وشفتين}: للجمال والبصر والنُّطق وغير ذلك من المنافع الضروريَّة فيها؛ فهذه نعم الدُّنيا. ثم قال في نعم الدين: {وَهَدَيْناهُ النَّجْدَيْنِ}؛ أي: طريقي الخير والشرِّ؛ بيَّنَّا له الهدى من الضَّلال، والرُّشد من الغيِّ. فهذه المنن الجزيلة تقتضي من العبد أن يقوم بحقوق الله ويشكره على نعمه، وأن لا يستعين بها على معاصي الله.
{8 - 10} Kisha akamfanya kutambua neema zake, akasema: "Kwani hatukumpa macho mawili? Na ulimi, na midomo miwili" ili awe na mwonekano mzuri, na kwa ajili ya kuona kutamka na manufaa mengineyo anayoyahitaji? Hizi ni neema za duniani. Kisha akasema kuhusu neema za kidini: "Na tukambainishia zote njia mbili?" Yaani, njia ya heri na njia ya uovu. Na tukambainishia uwongofu na upotofu. Basi neema hizi nyingi zinamtaka mja kutimiza haki za Mwenyezi Mungu na kumshukuru kwa neema zake, na wala asizitumie kumuasi Mwenyezi Mungu.
#
{11} ولكن هذا الإنسان لم يفعل ذلك؛ {فلا اقتحم العقبة}؛ أي: لم يقتحمْها ويعبُرْ عليها؛ لأنه متَّبع لهواه ، وهذه العقبة شديدةٌ عليه.
{11} Lakini mtu huyu hakufanya hivyo; "lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani." Kwa sababu anafuata matamanio yake tu, na vikwazo hivi ni vigumu kwake.
#
{12 - 16} ثم فسَّر هذه العقبة بقوله: {فكُّ رقبةٍ}؛ أي: فكُّها من الرقِّ بعتقها أو مساعدتها على أداء كتابتها، ومن باب أولى فكاك الأسير المسلم عند الكفار، {أو إطعامٌ في يوم ذي مَسْغَبَةٍ}؛ أي: مجاعةٍ شديدةٍ؛ بأن يطعم وقت الحاجة أشدَّ الناس حاجةً، {يتيماً ذا مَقْرَبَةٍ}؛ أي: جامعاً بين كونه يتيماً وفقيراً ذا قرابة، {أو مسكيناً ذا مَتْرَبَةٍ}؛ أي: قد لزق بالتراب من الحاجة والضَّرورة.
{12 - 16} Kisha akaelezea vikwazo hivi kwa kauli yake: "Kumkomboa mtumwa" kutoka katika utumwa kwa kumwachilia huru au kumsaidia kulipa alichoandikiana na mmiliki wake, na tena lililo muhimu zaidi ni kumkomboa mateka Mwislamu anayeshikiliwa na makafiri. "Au kumlisha siku ya njaa" kali, kwa kuwalisha masikini wahitaji zaidi. "Yatima aliye jamaa." Naye huyu ameunganisha kati ya kuwa yatima na kuwa jamaa masikini. "Au masikini aliye vumbini" kutokana na mahataji yake mazito.
#
{17} {ثم كان من الذين آمنوا}: وعملوا الصالحات ؛ أي: آمنوا بقلوبهم بما يجب الإيمان به، وعملوا الصالحات بجوارحهم، فدخل في هذا كلُّ قول وفعل واجبٍ أو مستحبٍّ، {وتواصَوْا بالصَّبْرِ}: على طاعة الله وعن معصيته وعلى أقداره المؤلمة؛ بأن يحثَّ بعضهم بعضاً على الانقياد لذلك والإتيان به كاملاً منشرحاً به الصَّدر مطمئنَّةً به النفس، {وتواصَوْا بالمَرْحَمَةِ}: للخلق؛ من إعطاء محتاجهم، وتعليم جاهلهم، والقيام بما يحتاجون إليه من جميع الوجوه، ومساعدتهم على المصالح الدينيَّة والدنيويَّة، وأن يحبَّ لهم ما يحبُّ لنفسه، ويكره لهم ما يكره لنفسه.
{17} "Tena awe miongoni mwa walioamini" kwa mioyo yao yale yanayopasa kuamini, na wakatenda mema kwa viungo vyao. Basi kikaingia katika hilo kila neno na kitendo cha lazima na kisichokuwa cha lazima. "Wakausiana kusubiri" juu ya kumtii Mwenyezi Mungu, katika kujiepusha kumuasi, na juu ya mipango yake michungu; kwa kuhimizana wao kwa wao juu ya kufanya hivyo kwa ukamilifu, na kwa kifua kilichopanuka na nafsi iliyotulia "na wakausiana kuhurumiana" na kuhurumia viumbe; kwa kuwapa wahitaji wao, na kuwaelimisha wasiojua wao, na kuwafanyia wanayohitaji katika nyanja zote, na kuwasaidia katika masilahi ya kidini na ya kidunia, na kuwapendea yale anayopendea nafsi yake, na kuwachukia yale anayoichukia nafsi yake.
#
{18} {أولئك}: الذين قاموا بهذه الأوصاف، الذين وفقهم الله لاقتحام [هذه] العقبة، {أولئك أصحاب الميمنة}: لأنَّهم أدَّوا ما أمر الله به من حقوقه وحقوق عباده، وتركوا ما نُهوا عنه، وهذا عنوان السعادة وعلامتها.
{18} "Hao" waliotekeleza sifa hizi, ambao Mwenyezi Mungu aliwawezesha kuingia katika vikwazo hivi, "ndio watu wa kheri wa kuliani" kwa sababu walitimiza yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu miongoni mwa haki zake na haki za waja wake, na wakaacha yale waliyokatazwa, na hiki ndicho kichwa na alama ya furaha.
#
{19 - 20} {والذين كفروا بآياتنا}: بأن نبذوا هذه الأمور وراء ظُهورهم فلم يصدِّقوا بالله ولا آمنوا به ولا عملوا صالحاً ولا رحموا عباد الله. أولئك {أصحاب المشأمة. عليهم نارٌ مؤصدةٌ}؛ أي: مغلقةٌ، في عَمَدٍ ممدَّدةٍ، قد مدَّت من ورائها؛ لئلاَّ تنفتح أبوابها، حتى يكونوا في ضيقٍ وهمٍّ وشدَّةٍ.
{19 - 20} "Lakini waliozikataa Ishara zetu" kwa sababu waliyatupa mambo hayo nyuma ya migongo yao, na hawakumsadiki Mwenyezi Mungu, wala hawakumuamini, wala hawakutenda mema, wala hawakuwahurumia waja wa Mwenyezi Mungu. Hao "ndio watu wa shari wa kushotoni. Juu yao utakuwa Moto uliofungiwa kila upande" kwenye nguzo zilizonyooshwa; ili milango yake isifunguke, ili wawe katika dhiki, wasiwasi kubwa na ugumu.
Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu.
* * *