Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَى (1) وَالنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّى (2) وَمَا خَلَقَ الذَّكَرَ وَالْأُنْثَى (3) إِنَّ سَعْيَكُمْ لَشَتَّى (4) فَأَمَّا مَنْ أَعْطَى وَاتَّقَى (5) وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَى (6) فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَى (7) وَأَمَّا مَنْ بَخِلَ وَاسْتَغْنَى (8) وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَى (9) فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَى (10) وَمَا يُغْنِي عَنْهُ مَالُهُ إِذَا تَرَدَّى (11) إِنَّ عَلَيْنَا لَلْهُدَى (12) وَإِنَّ لَنَا لَلْآخِرَةَ وَالْأُولَى (13) فَأَنْذَرْتُكُمْ نَارًا تَلَظَّى (14) لَا يَصْلَاهَا إِلَّا الْأَشْقَى (15) الَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّى (16) وَسَيُجَنَّبُهَا الْأَتْقَى (17) الَّذِي يُؤْتِي مَالَهُ يَتَزَكَّى (18) وَمَا لِأَحَدٍ عِنْدَهُ مِنْ نِعْمَةٍ تُجْزَى (19) إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ رَبِّهِ الْأَعْلَى (20) وَلَسَوْفَ يَرْضَى (21)}.
1. Ninaapa kwa usiku unapofunika! 2. Na mchana unapodhihiri! 3. Na kwa Aliyeumba dume na jike! 4. Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali. 5. Ama mwenye kutoa na akamcha Mungu. 6. Na akaliwafiki lililo jema. 7. Tutamsahilishia yawe mepesi. 8. Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake. 9. Na akakanusha lililo jema. 10. Tutamsahilishia yawe mazito! 11. Na mali yake yatamfaa nini atapokuwa anadidimia? 12. Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu. 13. Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia. 14. Basi nakuonyeni na Moto unaowaka 15. Hatauingia ila mwovu kabisa! 16. Anayekadhibisha na kupa mgongo. 17. Na mcha Mungu ataepushwa nao. 18. Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa. 19. Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliyemfanyia hisani ndio anamlipa. 20. Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa. 21. Naye atakuja ridhika!
#
{1 - 2} هذا قسمٌ من الله بالزمان الذي تقع فيه أفعال العباد على تفاوت أحوالهم، فقال: {والليلِ إذا يغشى}؛ أي: يعمُّ الخلق بظلامه، فيسكنُ كلٌّ إلى مأواه ومسكنه، ويستريحُ العباد من الكدِّ والتعب، {والنَّهار إذا تجلَّى}: للخلق، فاستضاؤوا بنوره، وانتشروا في مصالحهم.
{1 - 2} Hiki ni kiapo kitokacho kwa Mwenyezi Mungu juu ya muda ambao ndani yake ndio vitendo vya waja wake hufanyika kulingana na hali zao tofauti tofauti.
Akasema: "Ninaapa kwa usiku unapofunika" viumbe na kuvigubika kwa giza lake, kwa hivyo kila kimoja kikatulia kwenye makazi yake, na waja wakapumzika kutokana na uchovu na taabu. "Na kwa mchana unapodhihiri wazi" kwa hivyo, viumbe vikaangazwa kwa nuru yake na vikaenea kwa ajili ya kutafuta masilahi yao.
#
{3} {وما خلقَ الذَّكَرَ والأنثى}: إن كانت {ما} موصولةً؛ كان إقساماً بنفسه الكريمة الموصوفة بكونه خالق الذُّكور والإناث، وإن كانت مصدريَّة؛ كان قسماً بخلقه للذَّكر والأنثى، وكمال حكمته في ذلك؛ أن خلق من كلِّ صنفٍ من الحيوانات التي يريد إبقاءها ذكراً وأنثى؛ ليبقى النوع ولا يضمحلَّ، وقاد كلًّا منهما إلى الآخر بسلسلة الشهوة، وجعل كلًّا منهما مناسباً للآخر؛ فتبارك الله أحسن الخالقين.
{3} "Na kwa aliyeumba dume na jike!" Hapa inawezekana kwamba Mwenyezi Mungu anaapa kwa nafsi yake tukufu, iliyoelezewa kuwa ni Yeye Muumba wa madume na majike. Na pia inawezekana kwamba aliapa tu kwa kuumba kwake madume na majike. Na ukamilifu wa hekima yake katika hilo ni kwamba aliumba katika kila aina ya mnyama ambaye alitaka kusalia kwake dume na jike; Ili viumbe vibaki na visiangamie. Kisha akakiongoza kila kimoja katika hivyo kwa mwenzake kwa msururu wa matamanio, na akafanya kila kimoja kikifae kingine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora zaidi wa waumbaji.
#
{4} وقوله: {إنَّ سعيَكُم لشتًّى}: هذا هو المقسم عليه؛ أي: إن سعيكم أيُّها المكلَّفون لمتفاوتٌ تفاوتاً كثيراً، وذلك بحسب تفاوت نفس الأعمال ومقدارها والنشاط فيها، وبحسب الغاية المقصودة بتلك الأعمال؛ هل هو وجه الله الأعلى الباقي، فيبقى العمل له ببقائه، وينتفع به صاحبه؟ أم هي غايةٌ مضمحلَّةٌ فانيةٌ؛ فيبطل السعي ببطلانها ويضمحلُّ باضمحلالها؟ وهذا كلُّ عملٍ يقصَد به غير وجه الله [تعالى] بهذا الوصف.
{4} Na kauli yake: "Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali." Hili ndilo ambalo Mwenyezi Mungu ameapa kwa ajili yake. Na jitihada hizi zinatofautiana sana kulingana na kutofautiana kwa matendo, kiasi chake, ukakamavu na kulingana na lengo lililokusudiwa la matendo hayo. Je, ni kuutafuta uso wa Mwenyezi Mungu, aliye juu, wa kubakia milele? Kwa hivyo matendo yakabakia kwa ajili yake kwa muda wa kubakia kwake, na mtendaji wake akanufaika nayo? Au ni kwa ajili ya lengo la kupotelea mbali na la muda mfupi? Kwa hivyo juhudi hizo zikabatilika kwa kubatilika kwake na kupotelea mbali kwa kupotelea mbali kwake? Hivi ndivyo huwa kila kitendo kilichokusudiwa kwa kitu kingine kisichokuwa uso wa Mwenyezi Mungu Mtukutu.
#
{5 - 7} ولهذا فصَّل الله العاملين ووصف أعمالهم، فقال: {فأمَّا من أعطى}؛ أي: ما أمر به من العبادات الماليَّة كالزَّكوات والنَّفقات والكفَّارات والصَّدقات والإنفاق في وجوه الخير، والعبادات البدنيَّة كالصَّلاة والصوم وغيرهما ، والمركَّبة من ذلك - كالحجِّ والعمرة ونحوهما، {واتَّقى}: ما نُهِي عنه من المحرَّمات والمعاصي على اختلاف أجناسها، {وصدَّق بالحُسنى}؛ أي: صدَّق بلا إله إلاَّ الله، وما دلَّت عليه من [جميع] العقائد الدينيَّة وما ترتَّب عليها من الجزاء [الأخروي]، {فسنيسِّره لليُسرى}؛ أي: نيسِّر له أمره ونجعله مسهَّلاً عليه كلُّ خيرٍ، ميسَّراً له ترك كلِّ شرٍّ؛ لأنَّه أتى بأسباب التيسير، فيسَّر الله له ذلك.
{5 - 7} Ndiyo maana Mwenyezi Mungu aliwapambanua watendaji matendo na akaelezea vitendo vyao,
akisema: "Ama mwenye kutoa" yale aliyoyaamrisha miongoni mwa ibaada za kimali, kama vile zaka, matumizi ya nyumbani, kafara, sadaka na kutoa sadaka kwa ajili ya mambo mengine ya heri, na vile vile ibada za kimwili, kama vile kuswali, kufunga saumu na mengineyo, na vile vile ibada zinazojumuisha hayo kama vile Hija, Umra, na zinginezo. "na akamcha Mungu" katika yale aliyokatazwa ya haramu na maasia ya aina mbalimbali. "Na akasadiki lililo jema" yaani hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, na yale inayoashiria imani hii ya itikadi zote za kidini, na yale yanayoambatana nayo ya malipo ya kiakhera. "Tutamsahilishia yawe mepesi." Yaani, tutamsahilishia mambo yake kwa kufikia yaliyo ya heri na kuacha maovu. Kwa sababu alifanya visababu vya kurahisishiwa, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akamfanyia rahisi.
#
{8 - 10} {وأمَّا مَن بَخِلَ}: بما أمِرَ به، فترك الإنفاق الواجب والمستحبَّ، ولم تسمح نفسه بأداء ما وجب لله، {واستغنى}: عن الله، فترك عبوديَّته جانباً، ولم ير نفسه مفتقرةً غاية الافتقار إلى ربِّها، الذي لا نجاة لها ولا فوز ولا فلاح إلاَّ بأن يكون هو محبوبها ومعبودها الذي تقصده وتتوجَّه إليه، {وكذَّب بالحُسنى}؛ أي: بما أوجب الله على العباد التصديق به من العقائد الحسنة، {فسنيسِّرهُ للعُسْرى}؛ أي: للحالة العسرة والخصال الذَّميمة؛ بأن يكون ميسَّراً للشرِّ أينما كان ومقيَّضاً له أفعالُ المعاصي. نسأل الله العافية.
{8 - 10} "Na ama mwenye kufanya ubakhili" katika yale aliyoamrishwa, basi akaacha kutoa mali kwa ajili ya matumizi ya faradhi na yasiyo ya faradhi. "Na akajiona kajitosheleza" mbali na Mwenyezi Mungu, basi akaacha kumuabudu, ambaye hakuna wokovu wala kufaulu isipokuwa hadi Yeye awe ndiye kipenzi chake na muabudiwa wake ambaye anamkusudia na kuelekea kwake tu. "Na akakanusha lililo jema." Yaani, yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwajibisha juu ya waja wake kuyasadiki ya itikadi mbalimbali nzuri. "Tutamsahilishia yawe mazito" kwa kurahisishiwa kufanya maovu popote alipo. Tunamuomba Mwenyezi Mungu salama.
#
{11} {وما يُغني عنه مالُه}: الذي أطغاه واستغنى به وبخل به إذا هلك ومات؛ فإنَّه لا يصحب الإنسان إلاَّ عمله الصالح. وأمَّا ماله الذي لم يخرج منه الواجب؛ فإنَّه يكون وبالاً عليه؛ إذ لم يقدِّم منه لآخرته شيئاً.
{11} "Na mali yake yatamfaa nini" mali ambayo ilimfanya kuvuka mipaka, na akajiona kajitosheleza, na akaifanyia ubahili, atakapoangamia na kufa. Kwa maana mtu hataenda akhera isipokuwa na matendo yake mazuri. Ama mali yake, ambayo hakutoa humo kilicho cha wajibu, basi hiyo itakuwa balaa kwake. Kwa sababu hakutanguliza chochote kutoka kwayo kwa ajili ya Akhera.
#
{12} {إنَّ علينا لَلهُدى}؛ أي: إنَّ الهدى المستقيم طريقه يوصل إلى الله ويدني من رضاه، وأمَّا الضَّلال؛ فطرقه مسدودةٌ عن الله، لا توصل صاحبها إلاَّ للعذاب الشديد.
{12} "Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu" unaofikisha kwa Mwenyezi Mungu na dini yake na radhi zake. Na ama upotofu, njia zake zimezuiliwa kufika kwa Mwenyezi Mungu, na hazimfikishi mwenye kuzifuata isipokuwa katika adhabu kali.
#
{13} {وإنَّ لنا للآخرةَ والأولى}: ملكاً وتصرُّفاً، ليس له فيهما مشاركٌ، فليرغب الراغبون إليه في الطلب، ولينقطع رجاؤهم عن المخلوقين.
{13} "Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia" kwa kuvimiliki na kuviendesha, na wala hana mshirika yeyote katika hivyo. Basi wenye kumtafuta na wamtafute Yeye, na wakate matumaini yao kwa viumbe.
#
{14 - 16} {فأنذرتُكم ناراً تلظَّى}؛ أي: تستعر وتتوقَّد، {لا يصْلاها إلاَّ الأشقى. الذي كذَّب}: بالخبر، {وتولَّى}: عن الأمر.
{14 - 16} "Basi nakuonyeni na Moto unaowaka" sana "Hatauingia ila mwovu kabisa! Anayekadhibisha" habari za Mwenyezi Mungu "na kupa mgongo" amri yake.
#
{17 - 21} {وسيجنبها الأتقى. الذي يؤتي مالَه يتزكَّى}: بأن يكون قصده به تزكية نفسه وتطهيرها من الذُّنوب والأدناس ، قاصداً به وجه الله تعالى. فدلَّ هذا على أنَّه إذا تضمَّن الإنفاق المستحبُّ ترك واجبٍ كدينٍ ونفقةٍ ونحوهما؛ فإنَّه غير مشروع، بل تكون عطيَّتُه مردودةً عند كثيرٍ من العلماء؛ لأنَّه لا يتزكَّى بفعلٍ مستحبٍّ يفوِّتُ عليه الواجبَ، {وما لأحدٍ عنده من نعمةٍ تُجْزى}؛ أي: ليس لأحدٍ من الخلق على هذا الأتقى نعمةٌ تُجزى؛ إلاَّ وقد كافأه عليها ، وربَّما بقي له الفضل والمنَّة على الناس، فتمحَّض عبداً للَّه؛ لأنه رقيق إحسانه وحده، وأما من بقيت - عليه نعمةُ الناس فلم يجزِها ويكافئْها؛ فإنَّه لا بدَّ أن يترك للناس ويفعل لهم ما ينقص إخلاصه.
وهذه الآية وإن كانت متناولةً لأبي بكر الصديق رضي الله عنه، بل قد قيل: إنها نزلت بسببه ؛ فإنَّه رضي الله عنه ما لأحدٍ عنده من نعمةٍ تُجْزى، حتى ولا رسول الله - صلى الله عليه وسلم -؛ إلاَّ نعمة الرسول، التي لا يمكن جزاؤها، وهي نعمة الدعوة إلى دين الإسلام وتعليم الهدى ودين الحقِّ؛ فإنَّ لله ورسولهِ المنَّة على كلِّ أحدٍ، منةً لا يمكنُ لها جزاء ولا مقابلة؛ فإنَّها متناولةٌ لكلِّ من اتَّصف بهذا الوصف الفاضل، فلم يبقَ لأحدٍ عليه من الخلق نعمةٌ تُجْزى، فبقيت أعمالُه خالصةً لوجه الله تعالى، ولهذا قال: {إلاَّ ابتغاءَ وجهِ ربِّه الأعلى. ولَسوفَ يرضى}: هذا الأتقى بما يعطيه الله من أنواع الكرامات والمثوبات.
{17 - 21} "Na mcha Mungu ataepushwa nao. Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa." Naye ni yule ambaye huifanya nia yake kwa hilo ni kujitakasa na kutokana na madhambi na uchafu, tena kwa kuukusudia uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hili linaonyesha kwamba ikiwa kutoa matumizi yaliyopendekezwa kunajumuisha kuacha wajibu kama vile deni, kutoa matumizi ya wajibu na mfano wake; basi hilo haliruhusiwi. Bali kutoa kwake huko kunakataliwa kulingana na na wanachuoni wengi. Kwa sababu hawezi kujitakasa kwa kufanya jambo linalopendekezwa ambalo litamfanya akose jambo la faradhi. "Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliyemfanyia hisani ndio anamlipa." Pia na inaweza kuwa na maana ya kwamba hakuna yeyote aliye na cha kumdai huyu mcha Mungu isipokuwa tayari ashamlipa juu yake, na hata huenda fadhila zake fulani zilibakia juu ya watu, kwa hivyo akawa ni mja aliyesafika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu. Na ama yule ambaye anapaswa kuwalipa watu kitu fulani, na bado hajawalipa, basi ni lazima awaachie watu na awafanyie mambo ambayo yatapunguza uaminifu wake kwa Mwenyezi Mungu. Ingawa Aya hii inamjumuisha Abu Bakr As-Siddiq, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, bali hata imesemwa kwamba iliteremka kwa sababu yake. Kwani, yeye Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, hakuwa na neema ya mtu juu yake aliyopaswa kuilipa, hata Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- isipokuwa neema ya Mtume ambayo haiwezi kulipwa, nayo ni neema ya kumlingania kwenye dini ya Kiislamu na kumfundisha uongofu na dini ya haki. Kwani Mwenyezi Mungu na Mtume wake wana neema juu ya kila mtu, neema isiyoweza kulipwa wala kulinganishwa. Kwani inajumuisha kila mwenye kusifika kwa sifa hizi adhimu. Kwa hivyo, hakuna hata mmoja katika viumbe aliyebakisha neema yake juu yake inayopasa kulipwa, basi matendo yake yakabakia kuwa safi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu,
na ndiyo maana akasema: "Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa. Naye atakuja ridhika" huyu mcha Mungu zaidi kwa aina za neema na mambo matukufu ambayo Mwenyezi Mungu anampa.
Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
* * *