:
Tafsiri ya Surat At-Tariq
Tafsiri ya Surat At-Tariq
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
: 1 - 17 #
{وَالسَّمَاءِ وَالطَّارِقِ (1) وَمَا أَدْرَاكَ مَا الطَّارِقُ (2) النَّجْمُ الثَّاقِبُ (3) إِنْ كُلُّ نَفْسٍ لَمَّا عَلَيْهَا حَافِظٌ (4) فَلْيَنْظُرِ الْإِنْسَانُ مِمَّ خُلِقَ (5) خُلِقَ مِنْ مَاءٍ دَافِقٍ (6) يَخْرُجُ مِنْ بَيْنِ الصُّلْبِ وَالتَّرَائِبِ (7) إِنَّهُ عَلَى رَجْعِهِ لَقَادِرٌ (8) يَوْمَ تُبْلَى السَّرَائِرُ (9) فَمَا لَهُ مِنْ قُوَّةٍ وَلَا نَاصِرٍ (10) وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الرَّجْعِ (11) وَالْأَرْضِ ذَاتِ الصَّدْعِ (12) إِنَّهُ لَقَوْلٌ فَصْلٌ (13) وَمَا هُوَ بِالْهَزْلِ (14) إِنَّهُمْ يَكِيدُونَ كَيْدًا (15) وَأَكِيدُ كَيْدًا (16) فَمَهِّلِ الْكَافِرِينَ أَمْهِلْهُمْ رُوَيْدًا (17)}.
1. Ninaapa kwa mbingu na Kinachokuja usiku! 2. Na nini kitakachokujulisha ni nini hicho Kinachokuja usiku? 3. Ni Nyota yenye mwanga mkali. 4. Hapana nafsi ila inayo mwangalizi. 5. Hebu na ajitazame mwanadamu ameumbwa kwa kitu gani? 6. Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa. 7. Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu. 8. Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha. 9. Siku zitakapodhihirishwa siri. 10. Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi. 11. Ninaapa kwa mbingu yenye marejeo! 12. Na kwa ardhi inayopasuka! 13. Hakika hii ni kauli ya kupambanua. 14. Wala si mzaha. 15. Hakika wao wanapanga mpango. 16. Na Mimi napanga mpango. 17. Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole.
#
{1 - 4} يقول الله تعالى: {والسماءِ والطارقِ}: ثم فسَّر الطارقَ بقوله: {النَّجمُ الثاقبُ}؛ أي: المضيء الذي يثقب نورُه فيخرِقُ السماوات فينفذ حتى يُرى في الأرض. والصحيح أنَّه اسم جنس يشمل سائر النجوم الثواقب. وقد قيل: إنَّه زحل، الذي يخرق السماوات السبع وينفذها فيُرى منها، وسُمِّيَ طارقاً لأنَّه يطرق ليلاً. والمقسَم عليه قوله: {إن كلُّ نفسٍ لَمَّا عليها حافظ}: يحفظ عليها أعمالها الصالحة والسيئة، وستُجازى بعملها المحفوظ عليها.
{1 - 4} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Ninaapa kwa mbingu na Kinachokuja usiku!" Kisha akakifafanua hicho kinachokuja usiku kwa kauli yake: "Ni Nyota yenye mwanga mkali" ambayo hupenya mbingu mpaka ikaonekana katika ardhi. Lakini maana sahihi hapa ni kwamba ni jina la jenasi linalojumuisha nyota zote zinazoonekana usiku. Na imesemwa kwamba ni Zohali inayopenya mbingu saba hadi mtu akaweza kuiona. Na kilichokusudiwa na kiapo hapa ni kauli yake "Hapana nafsi ila inayo mwangalizi." Yeye huihifadhia matendo yake nzuri na mbaya, na italipwa kwa vitendo vyake alivyohifadhiwa.
#
{5 - 7} {فلينظُرِ الإنسانُ ممَّ خُلِقَ}؛ أي: فليتدبَّر خلقته ومبدأه؛ فإنَّه مخلوق {من ماءٍ دافقٍ}: وهو المنيُّ، الذي {يخرُجُ من بين الصُّلْبِ والترائبِ}: يُحتمل أنَّه من بين صلبِ الرجل وترائب المرأة، وهي ثدياها، ويُحتمل أنَّ المراد المنيُّ الدافق، وهو منيُّ الرجل، وأنَّ محلَّه الذي يخرج منه ما بين صلبه وترائبه، ولعلَّ هذا أولى؛ فإنَّه إنَّما وصف به الماء الدافق الذي يُحَسُّ به ويشاهَدُ دفْقُه ، وهو منيُّ الرجل، وكذلك لفظ الترائب؛ فإنَّها تستعمل للرجل؛ فإنَّ الترائب للرجل بمنزلة الثديين للأنثى؛ فلو أريدت الأنثى؛ لقيل من الصُّلب والثديين ونحو ذلك. والله أعلم.
{5 - 7} "Hebu na ajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani?" Yaani, na atafakari uumbaji wake na chanzo chake. Kwa maana ameumbwa "kwa maji yatokayo kwa kuchupa" ambayo ni manii, ambayo "Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu." Inawezekana kwamba maana yake ni kuwa hutoka kati ya mgongo wa mwanamume na mbavu za mwanamke. Na inawezekana kwamba maana yake ni manii ya mwanamume yanayotoka kwa kuchupa, na kwamba yanatoka katikati ya mgongo na mbavu zake, na labda hii ni maana sahihi zaidi. Kwa maana alimwelezea kwamba anatokana na maji yanayotoka kwa mpingo unaohisiwa, ambayo ni manii ya mwanamume, na vile neno "taraib" hutumika kwa wanaume. Kwani taraib za mwanamume ni kama matiti yalivyo kwa mwanamke. Na kama maana hii ingekusudiwa mwanamke, basi ingesemwa: 'kutoka mgongoni na matiti mawili', au mfano wa hivyo. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.
#
{8 - 10} فالذي أوجد الإنسان من ماءٍ دافقٍ يخرج من هذا الموضع الصعب قادرٌ على رجعه في الآخرة وإعادته للبعث والنُّشور والجزاء. وقد قيل: إنَّ معناه أنَّ الله على رجع الماءِ المدفوق في الصُّلب لَقادرٌ، وهذا وإن كان المعنى صحيحاً؛ فليس هو المرادُ من الآية، ولهذا قال بعده: {يومَ تُبلى السرائر}؛ أي: تختبر سرائر الصدور ويظهر ما كان في القلوب من خيرٍ وشرٍّ على صفحات الوجوه؛ كما قال تعالى: {يوم تبيضُّ وجوهٌ وتسودُّ وجوهٌ}؛ ففي الدُّنيا تنكتم كثيرٌ من الأشياء ولا يظهر عياناً للناس، وأمَّا يوم القيامة ؛ فيظهر بِرُّ الأبرار وفجورُ الفجار، وتصير الأمور علانيةً. وقوله: {فما له من قوَّةٍ}؛ أي: من نفسه يدفع بها ، {ولا ناصرٍ}: من خارجٍ - ينتصر به، فهذا القسمُ على العاملين وقت عملهم وعند جزائهم.
{8-10} Kwa hivyo yule ambaye aliunda mtu kutoka kwa maji yanayotoka kwa kuchupa, ambayo hutoka mahali hapa pagumu, ana uwezo wa kumrudisha katika Akhera kwa ajili ya ufufuo na malipo. Na imesemwa kwamba inamaanisha kuwa Mwenyezi Mungu anaweza kurudisha maji hayo yanayotoka kwa kuchupa katika mgongo. Kulingana na kauli hii, hata kama maana hii ni sahihi lakini si hiyo iliyokusudiwa katika aya hii. Na ndiyo sababu akasema baada yake: "Siku zitakapodhihirishwa siri" za vifuani, na yadhihirike yale yaliyokuwa ndani ya mioyo ya wema na uovu mbele ya nyuso zote, kama alivyosema Mwenyezi Mungu pia: "Siku zitakapokuwa nyuso nyeupe, na nyuso zingine zikawa nyeusi." Kwa sababu, duniani mambo mengi hujificha wala hayaonekani mbele ya macho ya watu. Ama siku ya Kiyama, utadhihirika wema wa wema na uovu wa waovu, na mambo yote yataonekana hadharani. Na kauli yake: "Basi hatakuwa na nguvu" yeye mwenyewe akajisaidia "wala msaidizi" atakayemsaidia. Kwa hivyo, kiapo hiki ni juu ya watendaji matendo wakati wa kutenda kwao na wakati wa malipo yao.
#
{11 - 14} ثم أقسم قسماً ثانياً على صحة القرآن، فقال: {والسماءِ ذات الرَّجْع. والأرضِ ذاتِ الصَّدْع}؛ أي: ترجع السماء بالمطر كلَّ عام، وتنصدِعُ الأرض للنبات، فيعيش بذلك الآدميُّون والبهائم، وترجع السماء أيضاً بالأقدار والشؤون الإلهيَّة كلَّ وقتٍ، وتنصدع الأرض عن الأموات، {إنَّه}؛ أي: القرآن، {لقولٌ فصلٌ}؛ أي: حقٌّ وصدقٌ بيِّنٌ واضحٌ، {وما هو بالهَزْل}؛ أي: جدٌّ ليس بالهزل، وهو القول الذي يفصل بين الطوائف والمقالات، وتنفصل به الخصومات.
{11-14} Kisha akaapa kiapo cha pili juu ya usahihi wa Qur-ani, akasema: "Ninaapa kwa mbingu yenye marejeo! Na kwa ardhi inayopasuka!" Yaani, mbingu yenye kurejea na mvua kila mwaka, nayo ardhi inapasuka kwa mmea, kwa hivyo wanadamu na wanyama wakawa wanaishi kwa hayo. Na mbingu pia hurejea na mipango ya Mwenyezi Mungu kila wakati, nayo ardhi itapasuka iwatowe nje wafu. "Hakika hii" Qur-ani "ni kauli ya kupambanua. Wala si mzaha." Nayo ni kauli ambayo inapambanua kati ya makundi na maneno mbalimbali, na mizozo inapambanuka kwa hiyo.
#
{15 - 17} {إنَّهم}؛ أي: المكذِّبين للرسول - صلى الله عليه وسلم - وللقرآن، {يكيدون كيداً}: ليدفعوا بكيدِهِم الحقَّ ويؤيِّدوا الباطل، {وأكيدُ كيداً}: لإظهار الحقِّ، ولو كره الكافرون، ولدفع ما جاؤوا به من الباطل، ويُعلم بهذا مَنْ الغالب؛ فإنَّ الآدميَّ أضعفُ وأحقرُ من أن يغالب القويَّ العليم في كيدِهِ. {فمهِّلِ الكافرين أمْهِلْهم رويداً}؛ أي: قليلاً، فسيعلمون عاقبة أمرهم حين ينزل بهم العقاب.
{15 - 17} "Hakika wao" yaani wale wanaokadhibisha Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na Qur-ani, "wanapanga mpango" ili waipinge kwayo haki na kuiunga mkono batili. "Na Mimi napanga mpango" ili kuidhihirisha haki, hata kama makafiri watachukia, na ili kuzuia batili waliyokuja nayo, na ili kwa hayo ijulikane ni nani mshindi. Kwa maana, mwanadamu ni dhaifu sana kumshinda Mwenye Nguvu, ajuaye zaidi katika mipango yake. "Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole," kwa maana watakuja jua mwisho wa jambo lao hilo wakati itawaremkia adhabu.
Imekamilika tafsiri yake, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.