Tafsiri ya Surat Al-Buruj
Tafsiri ya Surat Al-Buruj
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْبُرُوجِ (1) وَالْيَوْمِ الْمَوْعُودِ (2) وَشَاهِدٍ وَمَشْهُودٍ (3) قُتِلَ أَصْحَابُ الْأُخْدُودِ (4) النَّارِ ذَاتِ الْوَقُودِ (5) إِذْ هُمْ عَلَيْهَا قُعُودٌ (6) وَهُمْ عَلَى مَا يَفْعَلُونَ بِالْمُؤْمِنِينَ شُهُودٌ (7) وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَنْ يُؤْمِنُوا بِاللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ (8) الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ (9) إِنَّ الَّذِينَ فَتَنُوا الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ الْحَرِيقِ (10) إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ذَلِكَ الْفَوْزُ الْكَبِيرُ (11) إِنَّ بَطْشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ (12) إِنَّهُ هُوَ يُبْدِئُ وَيُعِيدُ (13) وَهُوَ الْغَفُورُ الْوَدُودُ (14) ذُو الْعَرْشِ الْمَجِيدُ (15) فَعَّالٌ لِمَا يُرِيدُ (16) هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْجُنُودِ (17) فِرْعَوْنَ وَثَمُودَ (18) بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي تَكْذِيبٍ (19) وَاللَّهُ مِنْ وَرَائِهِمْ مُحِيطٌ (20) بَلْ هُوَ قُرْآنٌ مَجِيدٌ (21) فِي لَوْحٍ مَحْفُوظٍ (22)}.
1. Ninaapa kwa mbingu yenye Buruji! 2. Na kwa siku iliyoahidiwa! 3. Na kwa shahidi na kinachoshuhudiwa! 4. Wameangamizwa watu wa makhandaki. 5. Yenye moto wenye kuni nyingi. 6. Walipokuwa wamekaa hapo. 7. Na wao ni mashahidi wa yale waliyokuwa wakiwafanyia Waumini. 8. Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa. 9. Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kila kitu. 10. Hakika waliowafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua. 11. Hakika walioamini na wakatenda mema watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa. 12. Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali. 13. Yeye ndiye anayeanzisha na ndiye anayerejeza tena. 14. Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi. 15. Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu. 16. Atendaye ayatakayo. 17. Je! Zimekuwasilia habari za majeshi? 18. Ya Firauni na Thamudi? 19. Lakini waliokufuru wamo katika kukadhibisha. 20. Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka. 21. Bali hii ni Qur-ani tukufu. 22. Katika Ubao Uliohifadhiwa.
#
{1 - 3} {والسماءِ ذات البُروج}؛ أي: ذات المنازل المشتملة على منازل الشمس والقمر والكواكب المنتظمة في سيرها على أكمل ترتيبٍ ونظامٍ دالٍّ على كمال قدرة الله [تعالى] ورحمته وسعة علمِه وحكمتِه. {واليوم الموعودِ}: وهو يومُ القيامةِ، الذي وَعَدَ اللهُ الخَلْقَ أن يجمَعَهم فيه ويضمَّ فيه أوَّلهم وآخرَهم وقاصيَهم ودانِيَهم، الذي لا يمكن أن يتغيَّر ولا يُخْلِفُ الله الميعاد. {وشاهدٍ ومشهودٍ}: وشمل هذا كلَّ من اتَّصف بهذا الوصف؛ أي: مبصِرٍ ومبصَرٍ وحاضرٍ ومحضورٍ وراءٍ ومرئيٍّ. والمقسَم عليه ما تضمَّنه هذا القسم من آيات الله الباهرة وحِكَمِهِ الظاهرة ورحمته الواسعة. وقيل: إنَّ المقسم عليه قوله:
{1 - 3} "Ninaapa kwa mbingu yenye Buruji!" Yaani, yenye mahali pa mashukio ya jua, mwezi, na sayari, ambazo zimepangika sawasawa katika mwendo wake utaratibu na nidhamu kamilifu kabisa, jambo linaloonyesha ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu, rehema zake, upana wa elimu yake na hekima yake. "Na kwa siku iliyoahidiwa!" Nayo ni Siku ya Kiyama ambayo Mwenyezi Mungu aliahidi viumbe kuwa atawakusanya ndani yake na atawajumuisha humo wa mwanzo wao na wa mwisho wao na wa mbali wao na wa karibu wao, siku ambayo Mwenyezi Mungu hawezi kubadilisha wala kuvunja ahadi yake. "Na kwa shahidi na kinachoshuhudiwa!" Haya yanajumuisha kila mwenye sifa hizi, yaani mwenye kuona, mwenye kuonwa, aliyepo, aliyeletwa. Na kinachokusudiwa na viapo hivi ni ishara zinazong'aa za Mwenyezi Mungu, hekima yake dhahiri, na rehema yake pana iliyoko katika viapo hivi.
Na ilisemekana kwamba kinachokusudiwa na viapo hivi ni kauli yake:
#
{4 - 9} {قُتِلَ أصحابُ الأخدود}: وهذا دعاءٌ عليهم بالهلاك، والأخدودُ الحُفَرُ التي تُحْفَرُ في الأرض، وكان أصحابُ الأخدود هؤلاء قوماً كافرين، ولديهم قومٌ مؤمنون، فراودوهم على الدُّخول في دينهم، فامتنع المؤمنون من ذلك، فشقَّ الكافرون أخدوداً في الأرض، وقذفوا فيها النار، وقعدوا حولَها، وفتنوا المؤمنين، وعرضوهم عليها؛ فمن استجاب لهم أطلقوه، ومن استمرَّ على الإيمان قذفوه في النار، وهذا غايةُ المحاربة لله ولحزبه المؤمنين، ولهذا لعنهم الله وأهلكهم وتوعَّدهم، فقال: {قُتِلَ أصحابُ الأخدودِ}، ثم فسَّر الأخدود بقوله: {النارِ ذاتِ الوَقود. إذ هم عليها قعودٌ. وهم على ما يفعلون بالمؤمنين شهودٌ}: وهذا من أعظم ما يكون من التجبُّر وقساوة القلب؛ لأنَّهم جمعوا بين الكفر بآيات الله ومعاندتها ومحاربة أهلها وتعذيبهم بهذا العذاب الذي تَنْفَطِرُ منه القلوب وحضورهم إيَّاهم عند إلقائهم فيها. والحالُ أنَّهم ما نقموا من المؤمنين إلاَّ حالةً - يُمْدَحون عليها وبها سعادتُهم، وهي أنَّهم كانوا يؤمنون {بالله العزيز الحميد}؛ أي: الذي له العزَّة، التي قَهَرَ بها كلَّ شيء، وهو حميدٌ في أقواله وأفعاله وأوصافه. {الذي له مُلْكُ السموات والأرض}: خلقاً وعبيداً يتصرَّف فيهم بما يشاء. {والله على كلِّ شيءٍ شهيدٌ}: علماً وسمعاً وبصراً؛ أفلا خاف هؤلاء المتمرِّدون عليه أن يأخُذَهم العزيز المقتدر، أوَ ما علموا كلُّهم أنَّهم مماليك لله، ليس لأحدٍ على أحدٍ سلطةٌ من دون إذن المالك؟! أوَ خَفِيَ عليهم أنَّ الله محيطٌ بأعمالهم مجازيهم عليها ؟! كلاَّ إنَّ الكافر في غرورٍ، والجاهل في عمىً وضلالٍ عن سواء السبيل.
{4 - 9} "Wameangamizwa watu wa makhandaki." Nazo ni zile handaki zilizochombwa na hao watu ambao walikuwa makafiri waliokuwa wakiishi pamoja na watu Waumini, wakawahimiza waingie katika dini yao, lakini Waumini wakakataa kufanya hivyo, kwa hivyo makafiri hao wakachimba mahandaki katika ardhi, wakawasha humo moto, wakakaa pembezoni mwake, wakatia Waumini mtihanini kwa kuwaleta mbele ya moto huo. Basi yeyote aliyewaitikia wakawa wanamwachilia. Na anayeendelea kuamini, wakawa wanamtupa katika moto huo. Hiki ndicho kiwango kikubwa mno cha kupigana vita Mwenyezi Mungu na kundi lake la waumini, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akawalaani, akawaangamiza na akawaahidi adhabu.
Akasema: “Wameangamizwa watu wa makhandaki." Kisha akaeleza maana ya mahandaki hayo kwa kauli yake. "Yenye moto wenye kuni nyingi, walipokuwa wamekaa hapo. Na wao ni mashahidi wa yale waliyokuwa wakiwafanyia Waumini." Hii ni miongoni mwa aina kubwa zaidi za kiburi na ugumu wa mioyo. Kwa sababu walichanganya kati ya kukufuru ishara za Mwenyezi Mungu, kuzifanyia ukaidi, kupigana vita na watu wake, na kuwatesa kwa adhabu hii ambayo nyoyo zinapasuka kwa sababu yake, na kuwepo kwao pamoja nao walipokuwa wanawatupa humo. Hali ni kuwa hawakuona baya lolote kwa Waumini ila kwa hali - wanayosifiwa kwa sababu yake na ambayo kwayo ndiyo wanaweza kuwa furahani, nayo ni kwamba walikuwa wamemuamini "Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa mno." Yaani, mwenye nguvu ambaye kwa hizo alishinda kila kitu, na anayesifiwa katika maneno yake, vitendo vyake na sifa zake. "Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi" kwa kuviumba viumbe, na kwamba wao ni waja wake ambao anawaendesha apendavyo. "Na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kila kitu" kwa elimu yake, kusikia kwake na kuona kwake. Basi je, wale waliomuasi hawahofu kwamba Mwenye Nguvu na Mwenye uwezo anaweza kuwachukua kwa adhabu? Au hawakujua wote kwamba wao ni wamilikiwa wa Mwenyezi Mungu, na kwamba hakuna mwenye mamlaka juu ya yeyote bila idhini ya Mmiliki wa kweli? Au imefichikana kwao kwamba Mwenyezi Mungu anayajua vyema matendo yao na atawalipa kwa hayo? Sivyo, hakika kafiri yuko katika udanganyifu, naye mjinga yuko katika upofu na upotevu mbali na njia iliyonyooka.
#
{10} ثم أوعدهم ووعدهم وعرض عليهم التوبة، فقال: {إنَّ الذين فتنوا المؤمنين والمؤمنات ثمَّ لم يَتوبوا فلهم عذابُ جهنَّم ولهم عذابُ الحريق}؛ أي: العذاب الشديد المحرِق. قال الحسن رحمه الله: انظُروا إلى هذا الكرم والجود؛ قتلوا أولياءه وأهل طاعته، وهو يدعوهم إلى التوبة.
{10} Kisha akawaonya, akawaahidi mazuri na akawafungulia mlango wa toba,
akasema: "Hakika waliowafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua." Al-Hasan, Mwenyezi Mungu amrehemu,
alisema: 'Tazama ukarimu huu na upaji kwa wingi huu. Waliwaua vipenzi wake na watu wanaomtii, kisha akawaita watubu.'
#
{11} ولما ذكر عقوبة الظالمين؛ ذكر ثواب المؤمنين، فقال: {إنَّ الذين آمنوا}: بقلوبهم، {وعمِلوا الصالحاتِ}: بجوارحهم، {لهم جناتٌ تجري من تحتِها الأنهارُ ذلك الفوزُ الكبيرُ}: الذي حَصَلَ لهم الفوزُ برضا الله ودار كرامته.
{11} Na alipotaja adhabu ya madhalimu, akataja malipo ya Waumini,
akasema: "Hakika wale walioamini" kwa nyoyo zao "na wakatenda mema" kwa viungo vyao "watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa" nako ni kuweza kufikia radhi za Mwenyezi Mungu na makazi ya utukufu wake.
#
{12} {إنَّ بطش ربِّكَ لشديدٌ}؛ أي: إن عقوبته لأهل الجرائم والذُّنوب العظام لقويَّةٌ شديدةٌ ، وهو للظالمين بالمرصاد ؛ قال الله تعالى: {وكذلك أخذُ ربِّك إذا أخَذَ القُرى وهي ظالمةٌ إنَّ أخذَه أليمٌ شديدٌ}.
{12} "Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali" kwa wahalifu wa watu wa madhambi makubwa, naye yuko macho kwa madhalimu.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na ndiyo kama hivyo ndivyo inavyokuwa Mola wako Mlezi anapoikamata miji inapokuwa imedhulumu. Hakika mkamato wake ni mchungu na mkali."
#
{13} {إنَّه هو يُبدِئُ ويعيدُ}؛ أي: هو المنفرد بإبداء الخلق وإعادته؛ فلا يشارِكهُ في ذلك مشارك.
{13} "Yeye ndiye anayeanzisha na ndiye anayerejeza tena" na hakuna mshiriki anayeshiriki naye katika haya.
#
{14} {وهو الغفورُ}: الذي يغفر الذُّنوب جميعها لمن تاب، ويعفو عن السيِّئات لمن استغفره وأناب. {الودودُ}: الذي يحبُّه أحبابه محبَّةً لا يشبهها شيءٌ؛ فكما أنَّه لا يشابهه شيءٌ في صفات الجلال والجمال والمعاني والأفعال؛ فمحبَّته في قلوب خواصِّ خلقه التابعة لذلك لا يشبِهُها شيءٌ من أنواع المحابِّ، ولهذا كانت محبَّتُه أصل العبوديَّة، وهي المحبَّة التي تتقدَّم جميع المحابِّ وتغلبها، وإن لم تكن غيرها تبعاً لها؛ كانت عذاباً على أهلها، وهو تعالى الودودُ الوادُّ لأحبابه؛ كما قال تعالى: {يُحِبُّهم ويحبُّونه}: والمودَّة هي المحبَّة الصافية.
وفي هذا سرٌّ لطيفٌ؛ حيث قرن الودود بالغفور؛ ليدلَّ ذلك على أنَّ أهل الذُّنوب إذا تابوا إلى الله، وأنابوا غفر لهم ذنوبهم، وأحبهم فلا يقال تغفر ذنوبهم، ولا يرجع إليهم الود كما قاله بعض الغالطين، بل الله أفرح بتوبة عبده حين يتوب من رجلٍ على راحلته عليها طعامُهُ وشرابه وما يصلحه، فأضلَّها في أرضِ فلاةٍ مهلكةٍ، فأيس منها، فاضطجع في ظلِّ شجرةٍ ينتظر الموت، فبينما هو على تلك الحال؛ إذا راحلته على رأسه، فأخذ بخطامها. فالله أعظم فرحاً بتوبة العبد من هذا براحلته، وهذا أعظم فرح يقدَّر؛ فلله الحمد والثناء وصفو الوداد ما أعظمَ برَّه وأكثر خيرَه وأغزرَ إحسانَه وأوسع امتنانَه!
{14} "Naye ni Mwenye kusamehe" anayesamehe madhambi yote kwa anayetubia. "Mwenye mapenzi" anayependwa na vipenzi vyake kwa mapenzi tofauti na kitu kingine chochote. Na kama vile hakuna kitu kinachofanana naye katika sifa za utukufu wake, uzuri, maana na vitendo, basi pia upendo wake ndani ya mioyo ya viumbe wake maalumu unaofuatana na hilo, haufanani na aina yoyote ya upendo, na ndiyo maana kumpenda ndiyo msingi wa uja, nao ni upendo unaotangulia na kushinda upendo wote. Na kama upendo mwingine haufuatani nao, basi huo utakuwa ni adhabu kwa watu wake, na Yeye Mtukufu ndiye Mwenye mapenzi kwa vipenzi vyake,
kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: "Anawapenda na wao wanampenda." Kuna siri nzuri sana katika hili; ambapo aliunganisha kati ya Mwenye mapenzi na Mwenye kusamehe mno; ili hili liashirie kuwa wenye madhambi wakitubu kwa Mwenyezi Mungu na kurudi kwake, atawasamehe madhambi yao na kuwapenda, kwa hivyo haisemwi kuwa watasamehewa dhambi zao, wala hatawapenda kama walivyosema baadhi ya watu waliokosea katika hili. Bali Mwenyezi Mungu hufurahishwa na toba ya mja wake anapotubia kuliko mtu anavyofurahia juu ya ngamia wake ambaye ana chakula chake na kinywaji chake juu yake na vyote vyenye kumfaa, kisha akampoteza katika nchi iliyo kame yenye maangamizo, na akakata tamaa naye. Kisha akajilaza chini ya kivuli cha mti, akingojea kifo. Na alipokuwa katika hali hii, tazama, ngamia wake huyo wa kusafiria akaja akasimama karibu na kichwa chake, basi akashika kamba zake za kumwendeshea. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu ana furaha kubwa zaidi kwa toba ya mja wake kuliko huyu anavyofurahia juu ya ngamia wake huyu. Na hii ndiyo furaha kubwa zaidi ambayo inaweza kukadiriwa. Basi sifa njema ni za Mwenyezi Mungu na kutajwa kwa uzuri, na upendo safi zaidi. Ni wema mkubwa wa jinsi gani huu kutoka kwake, na ni heri nyingi ya jinsi gani hii kutoka kwake, na ni ukarimu gani mwingi huu kutoka kwake, na ni neema pana jinsi gani hii kutoka kwake.
#
{15} {ذو العرش المجيدُ}؛ أي: صاحب العرش العظيم، الذي من عظمته أنه وسع السماواتِ والأرض والكرسيَّ؛ فهي بالنسبة إلى العرش كحلقة ملقاةٍ في فلاةٍ بالنسبة لسائر الأرض ، وخصَّ الله العرش بالذِّكر لعظمته، ولأنَّه أخصُّ المخلوقات بالقرب منه [تعالى]. وهذا على قراءة الجرِّ يكون {المجيد} نعتاً للعرش، وأما على قراءة الرفع؛ فإنَّه يكون نعتاً لله ، والمجدُ سعة الأوصاف وعظمتها.
{15} "Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu." Yaani, mwenye Kiti cha Enzi kikubwa, ambacho katika ukubwa wake ni kwamba kimeenea mbingu, ardhi na mahali pa inapokanyaga miguu yake
(Kursii). Kwani mahali hapo kwa kulinganisha na Kiti cha Enzi ni kama pete iliyotupwa katika jangwa kwa kulinganisha na ardhi iliyobaki. Na hapa Mwenyezi Mungu amekitaja Kiti cha Enzi kwa njia maalumu kwa sababu ya utukufu wake, na kwa sababu ndicho kiumbe maalumu zaidi kilicho karibu zaidi naye. Maana hii inatokea neno "Al-Majiid" likisomwa na kasra
(herufi i) ili liwe sifa ya Kiti cha Enzi. Ama likisomwa na dhwamma
(herufi u) basi linakuwa ni sifa ya Mwenyezi Mungu kwamba ni Mtukufu.
#
{16} {فعَّالٌ لما يريد}؛ أي: مهما أراد شيئاً؛ فعله، إذا أراد شيئاً؛ قال له: كن، فيكون، وليس أحدٌ فعالاً لما يريد إلاَّ الله؛ فإنَّ المخلوقات ولو أرادت شيئاً؛ فإنَّه لا بدَّ لإرادتها من معاونٍ وممانع، والله لا معاون لإرادته ولا ممانع له ممَّا أراد.
{16} "Atendaye ayatakayo" Kwani akitaka kitu,
Yeye husema tu: Kuwa, na kinakuwa, na hakuna awezaye kufanya mno anachotaka isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. Kwa maana, kama viumbe watataka kitu, basi lazima utashi wao huo uwe chini ya na wasaidizi au vizuizi, lakini Mwenyezi Mungu hana wasaidizi au vizuizi kwa utashi wake kwa kile anachotaka.
#
{17 - 18} ثم ذكر من أفعاله الدالَّة على صدق ما جاءت به رسله، فقال: {هل أتاك حديث الجُنود. فرعونَ وثمودَ}: وكيف كذَّبوا المرسلين فجعلهم الله من المهلكين.
{17 - 18} Kisha akataja baadhi ya vitendo vyake vinavyoashiria ukweli wa yale waliyoyaleta Mitume wake,
akasema: "Je, zimekufikia habari za majeshi? Ya Firauni na Thamudi?" Na vipi waliwakadhibisha Mitume, basi Mwenyezi Mungu akawafanya kuwa miongoni mwa walioangamizwa?
#
{19} {بل الذين كَفَروا في تكذيبٍ}؛ أي: لا يزالون مستمرِّين على التكذيب والعناد، لا تنفع فيهم الآياتُ، ولا تُجدي لديهم العظات.
{19} "Lakini waliokufuru wamo katika kukadhibisha" na kukaidi, na wala ishara za Mwenyezi Mungu haziwaingii kitu, na mawaidha hayawafai kitu.
#
{20} {والله من ورائهم محيطٌ}: قد أحاط بهم علماً وقدرةً؛ كقوله: {إنَّ ربَّك لبالمرصاد}؛ ففيه الوعيد الشديد للكافرين من عقوبة مَنْ هم في قبضته وتحت تدبيره.
{20} "Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka" kwa elimu yake na uwezo wake.
Ni kama kauli yake: "Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia." Hili lina tishio kali kwa makafiri kuhusu adhabu ya Yule ambaye wako katika mshiko wake na chini ya uendeshaji wake.
#
{21 - 22} {بل هو قرآنٌ مجيدٌ}؛ أي: وسيع المعاني عظيمها كثير الخير والعلم. {في لوح محفوظٍ}: من التغيير والزيادة والنقص، ومحفوظ من الشياطين، وهو اللوح المحفوظ، الذي قد أثبت الله فيه كلَّ شيء، وهذا يدلُّ على جلالة القرآن وجزالته ورفعة قدره عند الله تعالى. والله أعلم.
{21 - 22} "Bali hii ni Qur-ani tukufu." Yaani, ina maana pana, heri na elimu nyingi. "Katika Ubao Ulio Hifadhiwa" kutokana na mabadiliko, kuongezewa na kupunguzwa, na umehifadhiwa kutokana na mashetani. Humo Mwenyezi Mungu ameweka kila kitu. Na hili linaashiria utukufu wa Qur-ani na kuinuliwa kwake cheo mbele ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.
Imekamilika tafsiri yake
* * *