:
Tafsiri ya Surat At-Takwir
Tafsiri ya Surat At-Takwir
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
: 1 - 14 #
{إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ (1) وَإِذَا النُّجُومُ انْكَدَرَتْ (2) وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ (3) وَإِذَا الْعِشَارُ عُطِّلَتْ (4) وَإِذَا الْوُحُوشُ حُشِرَتْ (5) وَإِذَا الْبِحَارُ سُجِّرَتْ (6) وَإِذَا النُّفُوسُ زُوِّجَتْ (7) وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ (8) بِأَيِّ ذَنْبٍ قُتِلَتْ (9) وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ (10) وَإِذَا السَّمَاءُ كُشِطَتْ (11) وَإِذَا الْجَحِيمُ سُعِّرَتْ (12) وَإِذَا الْجَنَّةُ أُزْلِفَتْ (13) عَلِمَتْ نَفْسٌ مَا أَحْضَرَتْ (14)}.
1. Jua litakapokunjwa, 2. Na nyota zikazimwa, 3. Na milima ikaondolewa, 4. Na ngamia wenye mimba pevu watakapoachwa wasishughulikiwe, 5. Na wanyama wa mwituni wakakusanywa, 6. Na bahari zikawaka moto, 7. Na nafsi zikaunganishwa, 8. Na msichana aliyezikwa hai atakapoulizwa, 9. Kwa kosa gani aliuliwa? 10. Na madaftari yatakapoenezwa, 11. Na mbingu itakapotanduliwa, 12. Na Jahannamu itakapochochewa, 13. Na Pepo ikasogezwa, 14. Kila nafsi itajua ilichokihudhurisha.
#
{1 - 14} أي: إذا حصلتْ هذه الأمور الهائلةُ؛ تميَّز الخلقُ، وعلم كلٌّ ما قدَّمه لآخرته وما أحضره فيها من خيرٍ وشرٍّ، وذلك أنَّه إذا كان يومُ القيامةِ؛ تُكَوَّرُ الشمس؛ أي: تُجمع وتلفُّ ويُخسف القمر ويلقيان في النار، {وإذا النُّجوم انكدرتْ}؛ أي: تغيَّرت وتناثرت من أفلاكها، {وإذا الجبال سُيِّرَتْ}؛ أي: صارت كثيباً مهيلاً، ثم صارت كالعهن المنفوش، ثم تغيَّرت وصارت هباءً منبثًّا وأزيلت - عن أماكنها، {وإذا العِشارُ عُطِّلَتْ}؛ أي: عَطَّل الناس يومئذٍ نفائسَ أموالهم التي كانوا يهتمُّون لها، ويراعونها في جميع الأوقات، فجاءهم ما يُذْهِلُهم عنها، فنبَّه بالعشار - وهي النوق التي تتبعها أولادُها، وهي أنفس أموال العرب إذ ذاك عندهم - على ما هو في معناها من كل نفيس. {وإذا الوحوشُ حُشِرَتْ}؛ أي: جُمِعَتْ ليوم القيامةِ؛ ليقتصَّ الله من بعضها لبعض، ويري العبادَ كمالَ عدلِهِ، حتى إنَّه يقتصُّ للشاة الجمَّاء من الشاةِ القرناء ثم يقال لها: كوني تراباً ، {وإذا البحارُ سُجِّرَتْ}؛ أي: أوقدت فصارت على عظمها ناراً تتوقَّد، {وإذا النُّفوس زُوِّجَتْ}؛ أي: قُرِنَ كلُّ صاحب عمل مع نظيره، فجُمِعَ الأبرار مع الأبرار والفجَّار مع الفجَّار، وزوِّج المؤمنون بالحور العين والكافرون بالشياطين، وهذا كقوله تعالى: {وسيقَ الذين كَفَروا إلى جهنَّم زُمَراً}، {وسيق الذين اتَّقَوْا ربَّهم إلى الجنَّةِ زُمَراً}، {احْشُروا الذين ظَلَموا وأزواجَهم}. {وإذا الموؤُدةُ سُئِلَتْ}: وهي التي كانت الجاهليَّة الجهلاء تفعله من دفن البنات وهنَّ أحياء من غير سببٍ إلاَّ خشيةَ الفقر، فتسأل: {بأيِّ ذنبٍ قُتِلَتْ}، ومن المعلوم أنَّها ليس لها ذنبٌ، ولكن هذا فيه توبيخٌ وتقريعٌ لقاتليها، {وإذا الصُّحُفُ}: المشتملة على ما عمله العاملون من خيرٍ وشرٍّ، {نُشِرَتْ}: وفرِّقت على أهلها؛ فآخذٌ كتابه بيمينه وآخذٌ كتابه بشماله أو من وراء ظهره. {وإذا السماءُ كُشِطَتْ}؛ أي: أزيلت؛ كما قال تعالى: {يومَ تَشَقَّقُ السماءُ بالغمام}، {يومَ نَطْوي السماءَ كطَيِّ السِّجِلِّ للكُتُبِ}، {والأرضُ جميعاً قبضَتُه يوم القيامةِ والسموات مطوياتٌ بيمينه}، {وإذا الجحيمُ سُعِّرَتْ}؛ أي: أوقد عليها فاستعرتْ والتهبت التهاباً لم يكنْ لها قبل ذلك، {وإذا الجنَّةُ أزْلِفَتْ}؛ أي: قرِّبت للمتقين، {علمت نفسٌ}؛ أي: كلُّ نفس لإتيانها في سياق الشرط، {ما أحضرتْ}؛ أي: ما حضر لديها من الأعمال التي قدَّمتها؛ كما قال تعالى: {ووجدوا ما عملوا حاضراً}. وهذه الأوصافُ التي وصَفَ [اللَّهُ] بها يوم القيامة من الأوصاف التي تنزعج لها القلوب، وتشتدُّ من أجلها الكروب، وترتعد الفرائصُ، وتعمُّ المخاوف، وتحثُّ أولي الألباب للاستعداد لذلك اليوم، وتزجُرُهم عن كلِّ ما يوجب اللوم، ولهذا قال بعض السلف: من أراد أن يَنْظُرَ ليوم القيامة كأنه رأي عينٍ؛ فليتدبَّر سورة {إذا الشمسُ كُوِّرَتْ}.
{1 - 14} Yaani, mambo haya makubwa yatakapotokea, viumbe vitatofautishwa, na kila mmoja wao atajua yale yote aliyoyatanguliza kwa ajili ya Akhera yake na yale mema na mabaya aliyoyahudhurisha siku hiyo. Na hayo ni kwamba itakapofika Siku ya Kiyama, jua litakunjwakunjwa, nao mwezi utapatwa, kisha viwili hivyo vitatupwa Motoni. "Na nyota zikazimwa" na kuondoka katika njia zake. "Na milima ikaondolewa" iwe kama tifutifu la mchanga, kisha itakuwa kama sufi zilizochambuliwa, kisha itabadilika na kuwa mavumbi yanayopeperushwa, kisha itaondolewa - kutoka mahali pake. "Na ngamia wenye mimba pevu watakapoachwa wasishughulikiwe." Hii pia ina maana kwamba siku hiyo watu wataziacha mali zao za thamani, ambazo walikuwa wakizijali sana na kuzitunza kila wakati, lakini likawajia jambo ambalo liliwashangaza mbali nayo. Ndiyo akatumia 'ngamia wenye mimba pevu' au ngamia wa kike wanaofuatwa na wanao, - nao ndio mali ya thamani zaidi ya Waarabu siku hizo - kuashiria kila kitu cha thamani. "Na wanyama wa mwituni wakakusanywa" kwa ajili ya Siku ya Kiyama. Ili Mwenyezi Mungu awalipie kisasi wao kwa wao, na awaonyeshe waja wake ukamilifu wa uadilifu wake, kiasi kwamba atalipizia kisasi kondoo asiye na pembe kutoka kwa kondoo mwenye pembe, kisha wataambiwa: 'Kuweni udongo!' "Na bahari zikawaka moto" pamoja na ukubwa wake. "Na nafsi zikaunganishwa." Yaani, kila mtenda matendo pamoja na aliyetenda matendo sawa na yake. Wema wataunganishwa na wema, na waovu pamoja na waovu. Nao Waumini wataunganishwa na hurulaini, nao makafiri waunganishwe na mashetani. Na hayo ni kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Na waliokufuru wataongozwa kuendea Jahannamu kwa makundi." Na akasema, "Na walio mcha Mola wao Mlezi wataongozwa kuendea Peponi kwa makundi" na akasema, "Wakusanyeni waliodhulumu, na wake zao." "Na msichana aliyezikwa hai atakapoulizwa," haya ndiyo waliyokuwa wakiyafanya majahili wa zama za kabla ya Uislamu ya kuwazika wasichana wadogo wakiwa hai bila ya sababu yoyote isipokuwa kuogopa umasikini, basi ataulizwa: "Kwa kosa gani aliuliwa?" Na kama inavyojulikana ni kwamba yeye hakuwa na dhambi yoyote, lakini hili ni karipio na kemeo kwa wale waliomuua. "Na madaftari" yenye matendo waliyotenda watendaji ya heri na uovu "yatakapoenezwa" na yakapewa kwa wenyewe. Basi kutakuwa na yule atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia na kuna yule atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kushoto au kwa nyuma ya mgongo wake. "Na mbingu itapo tanduliwa" kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na siku zitakapofunguka mbingu kwa mawingu" na akasema "Siku tutakapozikunja mbingu kama mkunjo wa karatasi za vitabu." Na akasema, "Na Siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa mkononi mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kuume" na akasema, "Na Jahannamu itakapochochewa" na iwake kwa moto ambao haukuwahi kuwaka kabla ya hapo. "Na Pepo ikasogezwa" karibu na wacha Mungu. "Kila nafsi itajua ilichokihudhurisha" miongoni mwa matendo ambayo zilitanguliza, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na watayakuta yote waliyoyatenda yamehudhuria hapo." Na maelezo haya ambayo Mwenyezi Mungu aliieleza Siku ya Kiyama kwayo ni miongoni mwa maelezo ambayo kwa sababu yake nyoyo zinafadhaika, dhiki inakuwa nyingi kwa sababu yake, misuli inatetemeka, na hofu zinazidi kuwatawala, na zinawahimiza wenye akili nzuri kujiandaa kwa ajili ya siku hiyo, na kuwakomesha dhidi ya kila linalolazimu kulaumiwa. Na ndiyo maana wakasema baadhi ya watangulizi wema kwamba anayetaka kutazama Siku ya Kiyama kama kwamba anaitazama kwa macho yake, basi na aizingatie Sura ya "Jua litakapokunjwa."
: 15 - 29 #
{فَلَا أُقْسِمُ بِالْخُنَّسِ (15) الْجَوَارِ الْكُنَّسِ (16) وَاللَّيْلِ إِذَا عَسْعَسَ (17) وَالصُّبْحِ إِذَا تَنَفَّسَ (18) إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ (19) ذِي قُوَّةٍ عِنْدَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ (20) مُطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ (21) وَمَا صَاحِبُكُمْ بِمَجْنُونٍ (22) وَلَقَدْ رَآهُ بِالْأُفُقِ الْمُبِينِ (23) وَمَا هُوَ عَلَى الْغَيْبِ بِضَنِينٍ (24) وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَيْطَانٍ رَجِيمٍ (25) فَأَيْنَ تَذْهَبُونَ (26) إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِلْعَالَمِينَ (27) لِمَنْ شَاءَ مِنْكُمْ أَنْ يَسْتَقِيمَ (28) وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَنْ يَشَاءَ اللَّهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ (29)}.
15. Ninaapa kwa nyota zinaporejea nyuma. 16. Zinazokwenda, kisha zikajificha. 17. Na kwa usiku unapopungua. 18. Na kwa asubuhi inapopambazuka. 19. Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu. 20. Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi. 21. Anayetiiwa, tena muaminifu. 22. Na wala huyu mwenzenu hana wazimu. 23. Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi. 24. Wala yeye si bahili kwa mambo ya ghaibu. 25. Wala hii si kauli ya Shetani aliyelaaniwa. 26. Basi mnakwenda wapi? 27. Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote. 28. Kwa yule miongoni mwenu anayetaka kwenda sawa. 29. Wala nyinyi hamtataka isipokuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.
#
{15 - 16} أقسم تعالى {بالخُنَّسِ}: وهي الكواكب التي تخنس؛ أي: تتأخَّر عن سير الكواكب المعتاد إلى جهة المشرق، وهي النجوم السبعة السيَّارة؛ الشمس والقمر والزُّهرة والمشتري والمريخ وزُحل وعطارد؛ فهذه السبعة لها سيران: سيرٌ إلى جهة المغرب مع سائر الكواكب والفلك. وسير معاكسٌ لهذا من جهة المشرق تختصُّ به هذه السبعة دون غيرها، فأقسم الله بها في حال خنوسها؛ أي: تأخُّرها، وفي حال جريانها، وفي حال كُنوسها؛ أي: استتارها بالنهار. ويُحتمل أنَّ المراد بها جميع الكواكب السيَّارة وغيرها.
{15 - 16} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaapa kwa "nyota zinaporejea nyuma" zikasalia nyuma ya harakati za kawaida za sayari kuelekea mashariki, ambazo ni zile nyota saba zinazozunguka: Jua, Mwezi, Zuhura, Mshtarii, Mirihi, Zohali na Utaridi. Hizi saba zina safari mbili: safari ya kuelekea magharibi pamoja na sayari zingine na vyote vinavyozunguka angani, na safari iliyo kinyume na hili kutoka Mashariki, ambayo hizi husalia nyuma ya zingine. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akaapa kwa hizo katika hali ya kusalia kwake nyuma, na katika hali ya kuzunguka kwake, na katika hali ya zikajificha kwake mchana. Na inawezekana kwamba kinachomaanishwa hapa ni sayari zote zinazozunguka na zinginezo.
#
{17 - 18} {والليل إذا عسعس}؛ أي: أقبل، وقيل أَدبر ، والنهار {إذا تَنَفَّسَ}؛ أي: بدت علائم الصبح، وانشقَّ النور شيئاً فشيئاً حتى يستكمل وتطلع الشمس.
{17 - 18} "Na kwa usiku unapopungua" na pia ilisemekana inamaanisha siku unapoingia. "Na kwa asubuhi inapopambazuka" na nuru ya asubuhi ikaanza kuenea kidogo kidogo mpaka ikakamilika na jua likachomoza.
#
{19} وهذه آياتٌ عظامٌ أقسم الله عليها لقوَّة سند القرآن وجلالته وحفظه من كلِّ شيطانٍ رجيم، فقال: {إنَّه لَقولُ رسولٍ كريم}: وهو جبريل عليه السلام، نزل به من الله تعالى؛ كما قال تعالى: {وإنَّه لَتنزيل ربِّ العالمين. نَزَلَ به الرُّوحُ الأمينُ. على قلبكَ لتكونَ من المُنذِرينَ}. ووصفه الله بالكريم لكرم أخلاقِهِ و [كثرة] خصالِهِ الحميدة؛ فإنَّه أفضل الملائكة وأعظمهم رتبةً عند ربِّه.
{19} Na hizi ni ishara kubwa alizoapa Mwenyezi Mungu kwazo kwa sababu ya nguvu ya msingi wa Qur-ani, utukufu wake na kulindwa kwake kutokana na kila shetani aliyelaaniwa. Akasema, "Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu" Naye ni Jibril, amani iwe juu yake, aliteremka nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote. Ameuteremsha Roho muaminifu. Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji." Mwenyezi Mungu alimuelezea kwa sifa ya utukufu kwa sababu ya utukufu wa maadili yake na wingi wa sifa zake za kusifiwa. Kwani yeye ndiye mbora wa Malaika wote na ndiye aliye juu wao kabisa wa daraja mbele ya Mola wake Mlezi.
#
{20} {ذي قوَّةٍ}: على ما أمره الله به، ومن قوَّته أنَّه قَلَبَ ديار قوم لوطٍ بهم فأهلكهم، {عند ذي العرش}؛ أي: جبريل مقرَّبٌ عند الله، له منزلةٌ رفيعةٌ وخصيصةٌ من الله اختصَّه بها، {مكينٌ}؛ أي: له مكانةٌ ومنزلةٌ فوق منازل الملائكة كلِّهم.
{20} "Mwenye nguvu" kwa yale aliyomuamrisha Mwenyezi Mungu. Na katika nguvu zake ni kwamba alizipindua juu chini nyumba za watu wa Luti na akawaangamiza. "Kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi." Yaani, Jibril yuko karibu na Mwenyezi Mungu, ana hadhi ya juu na sifa maalumu ambazo Mwenyezi Mungu alimpa yeye tu. "Mwenye cheo" cha juu zaidi ya malaika wote.
#
{21} {مطاع ثَمَّ}؛ أي: جبريل مطاعٌ في الملأ الأعلى؛ لأنَّه من الملائكة المقرَّبين، نافذ فيهم أمرُه، مطاعٌ رأيه، {أمينٍ}؛ أي: ذو أمانة وقيام بما أُمِرَ به، لا يزيد ولا ينقص ولا يتعدَّى ما حُدَّ له، وهذا كلُّه يدلُّ على شرف القرآن عند الله تعالى: فإنَّه بعث به هذا الملك الكريم الموصوف بتلك الصفات الكاملة، والعادةُ أنَّ الملوك لا ترسل الكريم عليها إلاَّ في أهمِّ المهمَّات وأشرف الرسائل.
{21} "Anayetiiwa," yaani; Jibril anatiiwa katika viumbe watukufu wa juu zaidi, kwa sababu yeye ni miongoni mwa Malaika walio karibu na Mwenyezi Mungu, na amri yake inatekelezeka kati yao, inatiiwa katika maoni yake. "Tena muaminifu mno;" yaani ni mwaminifu na anafanya yale aliyoamrishwa, hayazidishi wala hayapungui wala hapiti kiwango alichowekewa. Haya yote yanaonyesha utukufu wa Qur-ani mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwani aliituma nayo Malaika huyu mtukufu ambaye ameelezewa kwa sifa hizi kamilifu. Na desturi ni kwamba wafalme hawamtumi mtukufu wao isipokuwa katika mambo muhimu sana na ujumbe wa heshima zaidi.
#
{22} ولما ذكر فضل الرسول الملكيِّ الذي جاء بالقرآن؛ ذكر فضل الرسول البشريِّ الذي نزل عليه القرآنُ، ودعا إليه الناس، فقال: {وما صاحِبُكم}: وهو محمدٌ - صلى الله عليه وسلم - {بمجنونٍ}؛ كما يقوله أعداؤه المكذِّبون برسالته، المتقوِّلون عليه [من] الأقوال التي يريدون أن يطفِئوا بها ما جاء به ، بل هو أكملُ الناس عقلاً، وأجزلُهم رأياً، وأصدقُهم لهجةً.
{22} Na alipotaja fadhila za Mtume huyu wa kimalaika aliyeleta Qur-ani, akataja fadhila za Mtume wa kibinadamu aliyeteremshiwa Qur-ani, na akawalingania watu kuiendea, akasema: "Na wala huyu mwenzenu" Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - "hana wazimu" kama wanavyosema maadui zake waliokadhibisha ujumbe wake, na wale wanaomzulia maneno ambayo wanataka kuzima kwayo yale aliyoyaleta. Bali yeye ndiye mkamilifu zaidi wa watu wote katika akili, mwenye maoni bora zaidi na mkweli wao zaidi katika kuzungumza.
#
{23} {ولقد رآه بالأفُقِ المُبين}؛ أي: رأى محمدٌ - صلى الله عليه وسلم - جبريل عليه السلام بالأفُقِ البيِّن الذي هو أعلى ما يلوح للبصر.
{23} "Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi" Yaani, Muhammad – rehema na amani ziwe juu yake – alimuona Jibril, amani iwe juu yake, kwenye upeo wa macho ulio wazi.
#
{24} {وما هو على الغيب بضَنينٍ}؛ أي: وما هو على ما أوحاه الله إليه بِمُتَّهَم يزيد فيه أو ينقص أو يكتم بعضه، بل هو - صلى الله عليه وسلم - أمينُ أهل السماء وأهل الأرض، الذي بلَّغ رسالات ربِّه البلاغَ المبين، فلم يَشُحَّ بشيءٍ منه عن غنيٍّ ولا فقيرٍ ولا رئيسٍ ولا مرؤوسٍ ولا ذكرٍ ولا أنثى ولا حضريٍّ ولا بدويٍّ، ولذلك بعثه الله في أمَّةٍ أميَّةٍ جاهلةٍ جهلاء، فلم يمت - صلى الله عليه وسلم - حتى كانوا علماء ربَّانيِّين وأحباراً متفرِّسين، إليهم الغاية في العلوم، وإليهم المنتهى في استخراج الدقائق والمفهوم ، وهم الأساتذة، وغيرهم قصاراه أن يكون من تلاميذهم.
{24} "Wala yeye si bahili kwa mambo ya ghaibu." Yaani, yeye si mwenye kutuhumiwa katika yale ambayo Mwenyezi Mungu alimfunulia. Haongeza humo wala hapunguzi wala hafichi baadhi yake. Bali yeye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ni mdhamini wa wakazi wa mbinguni na wakazi wa ardhi, aliyefikisha jumbe za Mola wake Mlezi kwa kufikisha kwa wazi, wala hakufanya ubahili juu ya chochote katika jumbe hizo kwa tajiri wala masikini, wala mtawala, wala mtawaliwa wala mtu wa kiume wala wa kike wala wa mjini wala wa jangwani. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akamtuma kwa umma usiojua kusoma na kuandika, la kijinga na wajinga kweli kweli, na hakufa yeye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - mpaka walipokuwa wanachuoni wa kimungu ambao kwao ndiko kunakusudiwa vikuu katika kutafuta elimu, na wao ndio wenye uwezo wa mwisho zaidi katika kutoa mambo ya ndani kabisa na hata yasiyokuwa ya moja kwa moja hila na dhana. Hao ndio maprofesa, nao wengine walikuwa wanafunzi wao.
#
{25} {وما هو بقول شيطانٍ رجيمٍ}: لما ذكر جلالة كتابه وفضلَه بذكر الرسولين الكريمين اللذين وَصَلَ إلى الناس على أيديهما، وأثنى الله عليهما بما أثنى؛ دَفَعَ عنه كلَّ آفةٍ ونقصٍ مما يقدحُ في صدقه، فقال: {وما هو بقول شيطانٍ رجيمٍ}؛ أي: في غاية البعد عن الله وعن قربه.
{25} "Wala hii si kauli ya Shetani aliyelaaniwa." Alipotaja utukufu wa kitabu chake na fadhila yake kwa kuwataja Mitume wawili watukufu ambao kupitia kwao kiliwafikia watu, na Mwenyezi Mungu akawasifu kama alivyowasifu, akakiondolea kila dosari na upungufu unaoweza kukitia doa katika ukweli wake, akasema: "Wala hii si kauli ya Shetani aliyelaaniwa" na akafukuziliwa mbali na Mwenyezi Mungu
#
{26} {فأين تذهبون}؛ أي: كيف يخطر هذا ببالكم؟! وأين عَزَبَتْ عنكم أذهانكم حتى جعلتم الحقَّ الذي هو في أعلى درجات الصدق بمنزلة الكذب الذي هو أنزلُ ما يكون وأرذلُ وأسفلُ الباطل؟! هل هذا إلاَّ من انقلاب الحقائق؟!
{26} "Basi mnakwenda wapi?" Yaani, je, hili lilifikaje katika fikira zenu? Na akili zenu ziligeukia wapi kiasi kwamba mkaifanya haki iliyo katika viwango vya juu kabisa vya ukweli kuwa katika kiwango cha uwongo, ambao huwa katika kiwango cha chini kabisa, kibaya zaidi na batili ya chini kabisa? Je, hii si chochote ila ni kugeuza ukweli?
#
{27} {إنْ هو إلاَّ ذكرٌ للعالمين}: يتذكَّرون به ربَّهم وماله من صفات الكمال وما ينزَّه عنه من النقائص والرذائل والأمثال، ويتذكَّرون به الأوامر والنواهي وحكمها؛ ويتذكَّرون به الأحكام القدريَّة والشرعيَّة والجزائيَّة، وبالجملة يتذكَّرون به مصالح الدارين، وينالون بالعمل به السعادتين.
{27} "Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote." Kwa hayo watamkumbuka Mola wao Mlezi na sifa zake kamili na sifa za mapungufu na machafu na mifano ambayo ametakasika mbali nazo. Na kwa hayo watakumbuka maamrisho na makatazo yake na hukumu zake. Na kwa hayo pia watakumbuka hukumu zinazohusiana na mipango ya kimungu, kisheria, na za kimalipo. Na kwa ujumla watakumbuka masilahi ya nyumba hizi mbili, na kwa kuyafanyia kazi, watapata furaha mbili.
#
{28} {لمن شاء منكم أن يَسْتَقيمَ}: بعد ما تبيَّن الرشد من الغيِّ والهدى من الضَّلال.
{28} "Kwa yule miongoni mwenu anayetaka kwenda sawa" baada ya njia ya sawasawa kubainika kutoka na ukengeufu, na uwongofu kutokana na upotofu.
#
{29} {وما تشاؤون إلاَّ أن يشاء الله ربُّ العالمين}؛ أي: فمشيئتُه نافذةٌ لا يمكن أن تعارضَ أو تمانع. وفي هذه الآية وأمثالها ردٌّ على فرقتي القدريَّة النُّفاة والقدريَّة المجبرة؛ كما تقدَّم مثالها. والله أعلم والحمد لله.
{29} "Wala nyinyi hamtataka isipokuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote." Kwa maana utashi wake unatekelezeka, na hauwezi kupingwa wala kuzuiwa. Katika Aya hii na nyinginezo kama hizo, kuna jibu kwa madhehebu mawili: Al-Qadariya linalokanusha (majina na sifa za Mwenyezi Mungu) na Al-Qadariya Al-Jabriyya linalosema kwamba mwanadamu hatendi kihakika, bali hulazimishwa kutenda, kama ilivyotangulia kuelezea, na Mwenyezi Mungu ndiye anajua zaidi, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu.
* * *