Juzuu ya tano ya "Taysir Al-Karim Ar-Rahman katika tafsiri ya maneno ya Al-Mannan" Cha mwanachuoni, Sheikh Abdur-Rahman An-Nasir bin Saadi, Mwenyezi Mungu amsamehe. Amin. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na ninamtakia rehema na amani Mtume Muhammad na familia yake na masahaba zake. Ama baada ya hayo, hakika elimu ya tafsiri ya Qur-ani ndiyo elimu tukufu zaidi ya elimu zote na iliyo muhimu zaidi, na yenye kustahiki zaidi kuhakikisha maana zake na kuelewa kanuni zake, kwa sababu ni uteremsho wa wahyi kutoka kwa Mwenye hekima, Msifika. Aliuteremsha uwe uwongofu na rehema kwa waja wake na ubainisho wa kila kitu na ufafanuzi wa kina wa kila wanachokihitaji katika dini yao, na katika dunia yao na akhera yao. Na katika elimu ya Qur-ani iliyo maalumu ni kwamba kufahamu baadhi yake husaidia kuielewa yote. Kwa sababu Qur-ani, kuanzia mwanzo wake hadi mwisho wake, inazunguka juu ya kueleza misingi yenye manufaa, hakika mbalimbali, sheria kubwa mbalimbali, hukumu nzuri mbalimbali, na itikadi sahihi mbalimbali, na inawaelekeza waja kwenye kila jambo la heri, na inawaonya dhidi ya kila uovu, na inakariri kusisitiza mambo haya na kuyadhihirisha, kwa mbinu mbalimbali na kubadilishabadilisha kufaako, kwa urahisi kabisa, wepesi, usahihi ambao hakuna kitu zaidi yake. Na nimekuwa nikiulizwa mara kwa mara na wenzangu wengi kuhusu kuchapisha tafsiri yetu hii yote, na walisisitiza sana kwa sababu kile walichoona kwamba ina faida kubwa, nami nikawa ninatoa udhuru kwamba hilo ni vigumu sana. Kwa sababu ni ndefu, na tena kwamba katika nyakati hizi utashi wa watu wa vitabu virefu ni kidogo sana. Kwa hivyo, nilipenda kwamba niwaitikie kuchapisha baadhi ya yale waliyoyaomba, nayo ni kuchapisha juzuu moja tu miongoni mwa juzuu za tafsiri hii. Na ikawa imechaguliwa juzuu ya katikati kuanzia Surat Al-Kahf mpaka mwisho wa Surat An-Naml. Na kisichoweza kupatwa chote, basi pia hakiwezi kuachwa chote. Nina matumaini kwa Mwenyezi Mungu na kumwomba aifanye kazi hii iwe imekusudiwa uso wake yeye tu, iwe ni yenye manufaa kwetu na kwa ndugu zetu, na kwamba atupe msaada wake, utunzaji wake, na atuwezeshe, kwani yeye hutoa kwa wingi, Mkarimu, Mpole, Mwingi wa kurehemu. Na niliifuatisha na kanuni za kijumla na misingi katika kanuni za jumla za tafsiri, ili kuwezesha kupata kile ambacho msomaji anaweza kukosa katika sehemu juzuu nyinginezo. Kwa maana misingi na kanuni za jumla ndizo hujengewa juu yake matawi na maelezo madogo madogo, na mtu hupata manufaa na faida kutoka kwayo pamoja na ufupi, jambo ambalo halipatikani katika meneno marefu. Basi Mwenyezi Mungu ndiye anayetutosheleza, naye ndiye mtegemewa bora zaidi. Mwandishi.
Nayo iliteremka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَنْزَلَ عَلَى عَبْدِهِ الْكِتَابَ وَلَمْ يَجْعَلْ لَهُ عِوَجًا (1) قَيِّمًا لِيُنْذِرَ بَأْسًا شَدِيدًا مِنْ لَدُنْهُ وَيُبَشِّرَ الْمُؤْمِنِينَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا حَسَنًا (2) مَاكِثِينَ فِيهِ أَبَدًا (3) وَيُنْذِرَ الَّذِينَ قَالُوا اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا (4) مَا لَهُمْ بِهِ مِنْ عِلْمٍ وَلَا لِآبَائِهِمْ كَبُرَتْ كَلِمَةً تَخْرُجُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ إِنْ يَقُولُونَ إِلَّا كَذِبًا (5) فَلَعَلَّكَ بَاخِعٌ نَفْسَكَ عَلَى آثَارِهِمْ إِنْ لَمْ يُؤْمِنُوا بِهَذَا الْحَدِيثِ أَسَفًا (6)}
1. Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye alimteremshia mja wake Kitabu, wala hakukifanya kuwa na upogo. 2. Kimenyooka sawa sawa, ili kionye adhabu kali kutoka kwake, na kiwabashirie Waumini watendao mema kwamba hakika wana ujira mzuri. 3. Wakae humo milele. 4. Na kiwaonye wasemao, "Mwenyezi Mungu amejifanyia mwana." 5. Wao hawana elimu yoyote ya jambo hili, wala baba zao. Ni neno kubwa hilo litokalo vinywani mwao. Hawasemi isipokuwa uongo tu. 6. Huenda ukajihiliki nafsi yako kwa ajili yao, kuwasikitikia kwa kuwa hawayaamini mazungumzo haya!
#
{1} {الحمد}: هو الثناء عليه بصفاته التي هي كلُّها صفات كمال، وبنعمه الظاهرة والباطنة، الدينيَّة والدنيويَّة، وأجلُّ نعمه على الإطلاق إنزالُه الكتاب العظيم على عبده ورسوله محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -، فحمد نفسه، وفي ضمنه إرشادُ العباد ليحمدوه على إرسال الرسول إليهم، وإنزال الكتاب عليهم. ثم وَصَفَ هذا الكتاب بوصفين مشتملين على أنَّه الكامل من جميع الوجوه، وهما: نفي العِوَج عنه، وإثباتُ أنَّه مقيمٌ مستقيمٌ: فنفي العِوَج يقتضي أنَّه ليس في أخباره كذبٌ، ولا في أوامره ونواهيه ظلمٌ ولا عَبَثٌ. وإثبات الاستقامة يقتضي أنَّه لا يخبر ولا يأمر إلاَّ بأجلِّ الإخبارات، وهي الأخبار التي تملأ القلوب معرفةً وإيماناً وعقلاً؛ كالإخبار بأسماء الله وصفاته وأفعاله، ومنها الغيوب المتقدِّمة والمتأخِّرة، وأنَّ أوامره ونواهيه تزكِّي النفوس وتطهِّرها وتنمِّيها وتكمِّلها؛ لاشتمالها على كمال العدل والقِسْط والإخلاص والعبوديَّة لله ربِّ العالمين وحده لا شريكَ له. وحقيقٌ بكتابٍ موصوفٍ بما ذُكِر أن يَحْمَدِ الله نفسَه على إنزالِهِ، وأن يتمدَّح إلى عباده به.
{1} "Kuhimidiwa" ni kwake Mwenyezi Mungu. Nako ni kumsifu kwa sifa zake, ambazo zote ni sifa za ukamilifu, na kwa neema zake za dhahiri na za ndani, za kidini na za kidunia. Na neema yake bora zaidi ni kuteremsha kwake Kitabu kitakatifu kwa mja wake na mtume wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Kwa hivyo alijihimidi mwenyewe, jambo ambalo ndani yake linajumuisha kuwaelekeza waja wake kumhimidi kwa kuwatumia mtume na kuwateremshia kitabu. Kisha akaelezea kitabu hiki kwa maelezo mawili ambayo yanajumuisha kwamba ndicho kitabu kikamilifu zaidi kwa njia zote. Yaani, kukanusha kuwepo na upogo wowote ndani yake, na kuthibitisha kwamba ni cha kunyoosha na chenyewe ni kinyoofu. Kwa hivyo, kukanusha upogo kunalazimu kwamba hakuna uongo wowote katika habari zake, wala hakuna dhuluma yoyote wala mambo bure katika amri zake na makatazo yake. Na kuthibitisha unyoofu wake unalazimu kwamba hakisemi wala hakiamuru isipokuwa habari bora zaidi. Nazo ni habari ambazo hujaza mioyo maarifa, imani, na akili, kama vile kupeana habari juu ya majina ya Mwenyezi Mungu, sifa zake, na matendo yake, ikiwa pia kuhusu mambo ya ghaibu yaliyotangulia na yajayo, na kwamba amri zake na makatazo yake hutakasa nafsi, na kuzisafisha, na kuzikuza, na kuzikamilisha. Kwa sababu zimejumuisha uadilifu kamili, na haki, na kumkusudia na kumuabudu Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu peke yake, ambaye hana mshirika yeyote. Basi kinastahili zaidi kitabu kilichoelezwa kwa hayo yaliyotajwa, kwamba Mwenyezi Mungu ajisifu mwenyewe kwa kwa sababu ya kukiteremsha, na kwamba asifiwe na waja wake kwacho.
#
{2} وقوله: {لينذِرَ بأساً شديداً من لَدُنْه}؛ أي: لينذر بهذا القرآن الكريم عقابَه الذي عنده؛ أي: قدره وقضاه على من خالف أمره، وهذا يشمَلُ عقاب الدُّنيا وعقاب الآخرة. وهذا أيضاً من نعمه أنْ خوَّف عباده وأنذرَهم ما يضرُّهم ويُهلكهم؛ كما قال تعالى لما ذَكَرَ في هذا القرآن وصف النار؛ قال: {ذلك يُخَوِّفُ الله به عبادَه يا عبادِ فاتَّقونِ}؛ فمن رحمته بعباده أن قيَّضَ العقوباتِ الغليظةَ على من خالف أمره وبيَّنها لهم وبيَّن لهم الأسباب الموصلة إليها. {ويبشِّر المؤمنين الذين يعملونَ الصَّالحاتِ أنَّ لهم أجراً حسناً}؛ أي: وأنزل الله على عبدِهِ الكتاب ليبشِّر المؤمنين به وبرسلِهِ وكتبِهِ الذين كمل إيمانهم، فأوجب لهم عمل الصالحات، وهي الأعمال الصالحة من واجبٍ ومستحبٍّ، التي جمعت الإخلاص والمتابعة: {أنَّ لهم أجراً حسناً}: وهو الثوابُ الذي رتَّبه الله على الإيمان والعمل الصالح، وأعظمُهُ وأجلُّه الفوز برضا الله ودخول الجنة التي فيها ما لا عينٌ رأت ولا أذنٌ سمعت ولا خَطَرَ على قلب بشر. وفي وصفه بالحُسْنِ دلالةٌ على أنَّه لا مكدِّر فيه ولا منغِّص بوجه من الوجوه؛ إذْ لو وُجِدَ فيه شيءٌ من ذلك؛ لم يكن حسنُهُ تامًّا.
{2} Na kauli yake, "ili kionye adhabu kali kutoka kwake." Yaani, ambayo alikwishaipitishia hukumu juu ya mwenye kuhalifu amri yake. Na hili linajumuisha adhabu ya duniani na ya Akhera. Hii pia ni katika neema zake kwamba aliwahofisha waja wake na kuwaonya juu ya kile chenye kuwadhuru na kuwaangamiza, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja katika Qur-ani hii maelezo ya Moto. Alisema, "Kwa hayo anawahofisha Mwenyezi Mungu waja wake. Enyi waja wangu nicheni mimi." Basi katika rehema yake kwa waja wake ni kwamba aliwawekea adhabu kali kwa wale ambao wanaasi amri yake na akawabainishia adhabu hio, na akawabainishia sababu zinazofikisha huko. "Na kiwabashirie Waumini watendao mema kwamba hakika wana ujira mzuri." Yaani, na Mwenyezi Mungu alimteremshia mja wake Kitabu ili awabashirie waumini kwacho, na kwa Mitume wake na Vitabu vyake wale ambao imani yao ilikamilika. Kwa hivyo hilo likawasababishia kufanya matendo mema, ya wajibu na yanayopendekezwa, yaliyokusudiwa kwayo Mwenyezi Mungu tu, na yanayomfuata Mtume, "kwamba hakika wana ujira mzuri." Nayo ni thawabu ambazo Mwenyezi Mungu ameyawekea imani na matendo mema, na makubwa na muhimu yake zaidi ni kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kuingia Peponi, ambayo ndani yake kuna yale ambayo jicho halijawahi kuyaona, wala hakuna sikio lililowahi kuyasikia, wala hayajawahi kupita katika moyo wa mtu yeyote. Na katika kuyaelezea malipo hayo kwamba ni mazuri kuna ishara kwamba hayana cha kuhuzunisha chochote wala kupunguzwa kitu kwa njia yoyote ile. Kwa maana, ikiwa kingekuwapo chochote katika hayo, basi uzuri wake haungekuwa kamili.
#
{3} ومع ذلك؛ فهذا الأجر الحسن {ماكثينَ فيه أبداً}: لا يزول عنهم ولا يزولون عنه، بل نعيمُهم في كلِّ وقت متزايدٌ. وفي ذكر التبشير ما يقتضي ذِكْر الأعمال الموجبة للمبشَّر به، وهو أنَّ هذا القرآن قد اشتمل على كل عمل صالح موصل لما تستبشرُ به النفوس، وتفرحُ به الأرواح.
{3} Na pamoja na hayo, ujira huu mzuri, "watakaa humo milele." Hautawaondokea wala wao hawataondoka wauache, bali furaha yao itakuwa inaongezeka kila wakati. Na katika kutaja bishara njema, kuna lenye kuhitaji yatajwe matendo hayo mazuri yenye kusababisha hicho kilichobashiriwa. Nayo ni kwamba Qur-ani hii imejumuisha kila tendo jema ambalo linafikisha katika hayo ambayo nafsi zinakuwa na bishara njema juu yake, na roho zinafurahia kwayo.
#
{4 - 5} {وينذرَ الذين قالوا اتَّخذ اللهُ ولداً}: من اليهود والنَّصارى والمشركين، الذين قالوا هذه المقالة الشنيعة؛ فإنَّهم لم يقولوها عن علم ولا يقين؛ لا علم منهم ولا علم من آبائهم الذين قلَّدوهم واتَّبعوهم، بل إن يتَّبعون إلاَّ الظنَّ وما تَهْوى الأنفُسُ. {كَبُرَتْ كلمةً تخرُجُ من أفواههم}؛ أي: عَظُمت شناعتُها واشتدَّت عقوبتُها، وأيُّ شناعة أعظم من وصفه بالاتِّخاذ للولد الذي يقتضي نقصه ومشاركة غيره له في خصائص الربوبيَّة والإلهيَّة والكذب عليه؟! {فمن أظلمُ ممَّن افترى على الله كذباً}؟! ولهذا قال هنا: {إن يقولون إلاَّ كَذِباً}؛ أي: كذباً محضاً ما فيه من الصدق شيء. وتأمَّل كيف أبطل هذا القول بالتدريج والانتقال من شيء إلى أبطل منه: فأخبر أولاً أنه {ما لهم به مِن علم ولا لآبائهم}: والقول على الله بلا علم لا شكَّ في منعه وبطلانه. ثم أخبر ثانياً أنَّه قولٌ قبيحٌ شنيعٌ، فقال: {كَبُرَتْ كلمةً تخرج من أفواههم}. ثم ذكر ثالثاً مرتبته من القُبح، وهو الكذب المنافي للصدق.
{4-5} "Na kiwaonye wasemao, "Mwenyezi Mungu amejifanyia mwana" kama vile Mayahudi, Wakristo, na washirikina, ambao walisema maneno haya mabaya mno. Kwa maana, hawakuyasema kutokana na elimu wala yakini. Wao wenyewe hawalijui hilo wala hawakulijua kutoka kwa baba zao ambao wao waliwaiga na kuwafuata. Bali hawafuati isipokuwa dhana tu na yale ambayo nafsi yanatamani. "Ni neno kubwa hilo litokalo vinywani mwao." Yaani, ubaya wake ni mkubwa mno na adhabu yake ni kali zaidi. Na ni ubaya gani ulio mkubwa zaidi kuliko ule wa kumuelezea kwamba alijifanyia mwana, jambo ambalo linalazimu kwamba Yeye ana upungufu na kuwepo ushirikiano kati yake na wengineo katika sifa maalumu za umola na uungu, na kumdanganyishia? "Basi ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu?" Na ndiyo maana akasema hapa, "Hawasemi isipokuwa uongo tu." Yaani, uongo mtupu ambao hauna ukweli wowote ndani yake. Na tafakari jinsi alivyobatilisha kauli hii hatua kwa hatua na kuhama kutoka katika kitu hadi kwenye kile kilicho batili zaidi yake. Kwanza, akasema, "Wao hawana elimu yoyote ya jambo hili, wala baba zao." Na kusema juu ya Mwenyezi Mungu bila elimu hakuna shaka yoyote kwamba hilo limekatazwa, na tena ni jambo batili. Kisha la pili akajulisha kwamba ni kauli mbaya na ovu, akasema, "Ni neno kubwa hilo litokalo vinywani mwao." Kisha la tatu akataja daraja lake katika ubaya, ambalo ni uongo ambao ni kinyume cha ukweli.
#
{6} ولما كان النبيُّ - صلى الله عليه وسلم - حريصاً على هداية الخلق، ساعياً في ذلك أعظم السعي، فكان - صلى الله عليه وسلم - يفرح ويسرُّ بهداية المهتدين، ويحزن ويأسفُ على المكذِّبين الضالِّين؛ شفقةً منه - صلى الله عليه وسلم - عليهم، ورحمةً بهم؛ أرشده الله أن لا يَشْغَلَ نفسه بالأسف على هؤلاء الذين لا يؤمنون بهذا القرآن؛ كما قال في [الآية] الأخرى: {لعلَّك باخعٌ نفسَكَ أن لا يكونوا مؤمنين}، وقال: {فلا تذهب نفسك عليهم حسراتٍ}، وهنا قال: {فلعلَّك باخعٌ نفسَك}؛ أي: مهلكها غمًّا وأسفاً عليهم، وذلك أنَّ أجرك قد وَجَبَ على الله، وهؤلاء لو عَلِمَ اللهُ فيهم خيراً لهداهم، ولكنَّه علم أنهم لا يَصْلُحون إلا للنار؛ فلذلك خَذَلَهم فلم يهتدوا؛ فإشغالك نفسك غمًّا وأسفاً عليهم ليس فيه فائدةٌ لك.
وفي هذه الآية ونحوها عبرةٌ؛ فإنَّ المأمور بدعاء الخلق إلى الله عليه التبليغ والسعي بكلِّ سبب يوصِلُ إلى الهداية، وسدِّ طرق الضَّلال والغواية، بغاية ما يمكِنُه، مع التوكُّل على الله في ذلك؛ فإن اهتدوا؛ فبها ونعمت، وإلاَّ؛ فلا يحزنْ ولا يأسفْ؛ فإنَّ ذلك مضعفٌ للنفس، هادمٌ للقُوى، ليس فيه فائدةٌ، بل يمضي على فعلِهِ الذي كُلِّف به وتوجَّه إليه، وما عدا ذلك؛ فهو خارجٌ عن قدرته. وإذا كان النبيُّ - صلى الله عليه وسلم - يقولُ الله له: {إنَّك لا تَهْدي مَنْ أحببتَ}، وموسى عليه السلام يقول: {ربِّ إني لا أملِكُ إلاَّ نَفْسي وأخي ... } الآية؛ فمن عداهم من باب أولى وأحرى؛ قال تعالى: {فذكِّرْ إنَّما أنتَ مُذَكِّرٌ لست عليهم بمصيطرٍ}.
{6} Kwa kuwa Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - alikuwa na hamu kubwa ya kuongoza viumbe, akifanya bidii kubwa katika hilo, alikuwa yeye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - akifurahi na kufurahishwa na kuongoka kwa wale wanaoongoka, na anahuzunika sana juu ya wakadhibishaji, wapotovu kwa sababu ya kuwa na huruma juu yao yeye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na kwa sababu ya kuwarehemu. Basi Mwenyezi Mungu akamuelekeza kwamba asiishughulishe nafsi yake katika kuwahuzunikia hawa ambao hawaiamini Qur-ani, kama alivyosema katika aya nyingine, "Huenda labda ukajikera nafsi yako kwa kuwa hawawi waumini" na akasema, "Basi nafsi yako isijihiliki kwa kuwasikitikia" na hapa akasema, "Huenda ukajihiliki nafsi yako" kwa sababu ya huzuni mkubwa juu yao. Na hilo ni kwa sababu ujira wako umeshafika kwa Mwenyezi Mungu. Na hawa, ikiwa Mwenyezi Mungu angejua kwamba kuna heri yoyote ndani yao, basi angewaongoa. Lakini alijua kwamba wao hawafailii isipokuwa Moto tu. Basi ndiyo sababu aliwaachilia mbali kwa hivyo hakuongoka. Kwa hivyo, kuishughulisha nafsi yako kwa huzuni kubwa na masikitiko juu yao hakuna faida yoyote kwako. Katika aya hii na mfano wake kuna mazingatio mbalimbali. Miongoni mwake ni kwamba aliyeamrishwa kuwalingania viumbe kwa Mwenyezi Mungu, kilicho juu yake ni kufikisha ujumbe na kujitahidi awezavyo kwa kutumia kila njia inayofikisha katika uwongofu, na azuie njia za upotovu na ukengeufu kwa kiasi awezavyo huku akimtegemea Mwenyezi Mungu katika hilo. Kwa hivyo, wakiongoka, basi ni sawa na ni neema. Vinginevyo, basi asihuzunike wala asisikitike. Kwani, hayo yanaidhoofisha nafsi, na kubomoa nguvu, na hayana faida yoyote. Bali aendelee na kitendo alichoamrishwa na akielekee. Na yoyote yasiyokuwa hayo, basi hayo yako nje ya uwezo wake. Na ikiwa Nabii -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - anaambiwa na Mwenyezi Mungu, “Kwa hakika wewe humwongoi umpendaye." Naye Musa amani iwe juu yake anasema, “Mola wangu Mlezi! Hakika mimi similiki isipokuwa nafsi yangu na kaka yangu..." hadi mwisho wa aya. Basi asiyekuwa wao anastahiki zaidi na anafailia zaidi. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Basi kumbusha, hakika wewe ni mkumbushaji tu, wala huna uwezo juu yao."
{إِنَّا جَعَلْنَا مَا عَلَى الْأَرْضِ زِينَةً لَهَا لِنَبْلُوَهُمْ أَيُّهُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا (7) وَإِنَّا لَجَاعِلُونَ مَا عَلَيْهَا صَعِيدًا جُرُزًا (8)}.
7. Kwa hakika tumevifanya vilivyoko juu ya ardhi kuwa ni pambo lake ili tuwafanyie mtihani, ni nani kati yao ndio wenye vitendo vizuri zaidi. 8. Na hakika Sisi tutavifanya vyote vilivyo juu ya ardhi kuwa kama nchi iliyopigwa na ukame.
#
{7} يخبر تعالى أنه جعل جميع ما على وجه الأرض من مآكل لذيذةٍ ومشاربَ وملابسَ طيبةٍ وأشجارٍ وأنهارٍ وزروع وثمارٍ ومناظرَ بهيجةٍ ورياضٍ أنيقةٍ وأصواتٍ شجيَّةٍ وصورٍ مليحةٍ وذهبٍ وفضةٍ وخيلٍ وإبلٍ ونحوها؛ الجميع جعله الله زينةً لهذه الدار فتنةً واختباراً؛ {لِنَبْلُوَهم أيُّهم أحسنُ عملاً}؛ أي: أخلصه وأصوبه.
{7} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba alivifanya vyote vilivyo juu ya uso wa ardhi kama vile vyakula vitamu, vinywaji, mavazi mazuri, miti, mito, mazao, matunda, mambo mazuri ya kutazamwa, bustani maridadi, sauti za kupendeza, picha za kupendeza, dhahabu, fedha, farasi, ngamia, na kadhalika. Mwenyezi Mungu amevifanya hivyo vyote kuwa pambo la nyumba hii, kama majaribio na mtihani, "ili tuwafanyie mtihani, ni nani kati yao ndio wenye vitendo vizuri zaidi." Yaani, yaliyokusudiwa zaidi Mwenyezi na yaliyo sahihi zaidi.
#
{8} ومع ذلك سيجعلُ الله جميع هذه المذكورات فانيةً مضمحلَّةً وزائلةً منقضيةً، وستعود الأرض {صعيداً جُرزاً}: قد ذهبت لذَّاتها وانقطعتْ أنهارُها واندرستْ آثارُها وزال نعيمُها.
هذه حقيقة الدُّنيا، قد جلاَّها الله لنا كأنَّها رأي عين، وحذَّرنا من الاغترار بها، ورغَّبنا في دارٍ يدوم نعيمها ويسعدُ مقيمها، كلُّ ذلك رحمةً بنا، فاغترَّ بزُخْرُفِ الدُّنيا وزينتها مَنْ نَظَرَ إلى ظاهر الدُّنيا دون باطنها، فصحبوا الدُّنيا صحبة البهائم، وتمتَّعوا بها تمتُّع السوائم، لا ينظُرون في حقِّ ربِّهم، ولا يهتمُّون لمعرفته، بل همُّهم تناول الشهوات من أيِّ وجهٍ حصلت وعلى أيِّ حالةٍ اتَّفقت؛ فهؤلاء إذا حضر أحدَهم الموتُ، قلق لخراب ذاتِهِ وفوات لذَّاتِهِ، لا لما قدَّمت يداه من التفريط والسيئات.
وأمَّا من نَظَرَ إلى باطن الدُّنيا وعلم المقصود منها ومنه؛ فإنَّه تناول منها ما يستعين به على ما خُلِقَ له، وانتهز الفرصة في عمره الشريف، فجعل الدُّنيا منزل عبورٍ لا محلَّ حبور، وشُقَّة سفرٍ لا منزل إقامةٍ، فبذل جهدَهُ في معرفة ربِّه وتنفيذ أوامره وإحسان العمل؛ فهذا بأحسن المنازل عند الله، وهو حقيقٌ منه بكلِّ كرامة ونعيم وسرورٍ وتكريم، فنظر إلى باطن الدُّنيا حين نظر المغترُّ إلى ظاهرها، وعمل لآخرتِهِ حين عملَ البطَّال لدُنياه، فشتَّان ما بين الفريقين! وما أبعد الفرقَ بين الطائفتين!
{8} Na pamoja na hayo Mwenyezi Mungu atayafanya haya yaliyotajwa yote kupotelea mbali, kuisha, kuondoka, na kutoweka, na ardhi itarudi iwe nchi "iliyopigwa na ukame." Anasa zake zitakwenda, na mito yake itakatika, na athari zake zitafutika, na furaha zake zitaisha. Huu ndio ukweli wa dunia. Mungu ametubainishia kana kwamba ni mtazamo wa macho. Ametuonya dhidi ya kudanganywa nayo.Tunatamani nyumba ambayo raha yake hudumu na mkazi wake ni mwenye furaha. Yote hayo ni kwa rehema kwetu. Basi anayetazama nje ya dunia badala ya ndani yake anadanganyika na mapambo ya dunia, basi fuateni dunia usuhuba wa wanyama na mfurahie kwayo. Walioghafilika hawazingatii haki za Mola wao Mlezi, wala hawajali kumjua, bali hamu yao ni kula matamanio kwa namna yoyote yanayotokea na katika hali yoyote inayotokea. Mauti yanapomkaribia mmoja wao, watu hawa huwa na wasiwasi juu ya kujiangamiza kwake mwenyewe na kupoteza nafsi yake, si kwa sababu ya uzembe na matendo mabaya aliyoyafanya. Ama mwenye kutazama ndani ya dunia na kujua nini maana yake na kutoka kwayo; alichukua kutoka humo kile ambacho angeweza kutumia kwa ajili ya kile kilichoumbwa kwa ajili yake, na akatumia fursa ya maisha yake ya heshima, hivyo akaifanya dunia hii kuwa mahali pa kupita, sio mahali pa kupumzika, na ghorofa kwa ajili ya safari, siyo mahali pa kuishi. Basi akafanya juhudi katika kumjua Mola wake Mlezi, kutekeleza amri zake, na kutenda mema. Hii ni moja ya nafasi nzuri zaidi mbele ya Mungu, na ni kweli kwake kwa hadhi, raha, furaha, na heshima. Alitazama ndani ya dunia hii wakati wadanganyifu walipotazama nje yake, na kufanya kazi kwa ajili yake. Alifanya kazi kwa ajili ya akhera yake wakati ubatili ulifanya kazi kwa ulimwengu wake. Kwa hiyo kuna tofauti kati ya makundi mawili! Tofauti kati ya madhehebu haya ni kubwa kiasi gani!
{أَمْ حَسِبْتَ أَنَّ أَصْحَابَ الْكَهْفِ وَالرَّقِيمِ كَانُوا مِنْ آيَاتِنَا عَجَبًا (9) إِذْ أَوَى الْفِتْيَةُ إِلَى الْكَهْفِ فَقَالُوا رَبَّنَا آتِنَا مِنْ لَدُنْكَ رَحْمَةً وَهَيِّئْ لَنَا مِنْ أَمْرِنَا رَشَدًا (10) فَضَرَبْنَا عَلَى آذَانِهِمْ فِي الْكَهْفِ سِنِينَ عَدَدًا (11) ثُمَّ بَعَثْنَاهُمْ لِنَعْلَمَ أَيُّ الْحِزْبَيْنِ أَحْصَى لِمَا لَبِثُوا أَمَدًا (12)}.
9. Kwani unadhani ya kwamba wale watu wa Pangoni na Maandishi walikuwa ni ajabu miongoni mwa ishara zetu? 10. Vijana hao walipokimbilia kwenye pango, na wakasema, "Mola wetu Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uwongofu katika jambo letu." 11. Basi tukayaziba masikio yao kuwalaza humo pangoni kwa muda wa miaka kadhaa. 12. Kisha tukawazindua ili tujue ni lipi katika makundi mawili yale ndilo lilihesabu sawa urefu wa muda waliokaa.
#
{9} وهذا الاستفهام بمعنى النفي والنهي؛ أي: لا تظنَّ أنَّ قصَّة أصحاب الكهف وما جرى لهم غريبةٌ على آيات الله وبديعةٌ في حكمته، وأنَّه لا نظير لها ولا مجانس لها، بل لله تعالى من الآيات العجيبة الغريبة ما هو كثيرٌ من جنس آياتِهِ في أصحاب الكهف وأعظم منها، فلم يزل الله يُري عباده من الآيات في الآفاق وفي أنفسهم ما يتبيَّن به الحقُّ من الباطل والهدى من الضلال. وليس المراد بهذا النفي عن أن تكون قصَّة أصحاب الكهف من العجائب، بل هي من آيات الله العجيبة، وإنَّما المرادُ أن جنسها كثيرٌ جدًّا؛ فالوقوف معها وحدها في مقام العَجَبِ والاستغراب نقصٌ في العلم والعقل، بل وظيفةُ المؤمن التفكُّر بجميع آيات الله التي دعا الله العبادَ إلى التفكُّر فيها؛ فإنَّها مفتاحُ الإيمان وطريقُ العلم والإيقان. وإضافتهم إلى الكهف الذي هو الغارُ في الجبل، {والرقيم}؛ أي: الكتاب الذي قد رُقِمَتْ فيه أسماؤهم وقصَّتُهم لملازمتهم له دهراً طويلاً.
{9} Na swali hili lina maana ya kukanusha na kukataza. Yaani, usidhani kuwa kisa cha wale watu wa Pangoni na yaliyowapata si mambo ya kawaida katika ishara za Mwenyezi Mungu na kwamba ni mageni katika hekima yake, na kwamba hakuna mfanano wake wala kwamba hakuna kinachofanana nayo. Bali Mwenyezi Mungu Mtukufu ana ishara za ajabu na zisizo za kawaida, ambazo nyingi kuliko tena za aina sawa na ishara zake za wale watu wa pangoni na tena ni kubwa zaidi kuliko hizo. Na Mwenyezi Mungu hajaacha kuendelea kuwaonyesha waja wake ishara mbalimbali katika upeo wa macho na katika nafsi zao ambazo kwazo inabainika haki kutoka kwa batili, na uwongofu kutoka kwa upotovu. Na kilichokusudiwa si kukanisha kwamba kisa cha watu wa Pangoni ni miongoni mwa maajabu, bali hicho ni miongoni mwa ishara za ajabu za Mwenyezi Mungu. Lakini kilichokusudiwa ni kwamba mfano wa hizo ni nyingi sana. Kwa hivyo, kukomea kwa hicho tu katika suala kushangaa na kustaajabu ni upungufu katika elimu na akili. Bali, wajibu wa muumini ni kutafakari ishara zote za Mwenyezi Mungu ambazo Mwenyezi Mungu aliwataka waja kuzitafakari. Kwa maana, hizo ni ufunguo wa imani na njia ya elimu na yakini. Na kuwafungamanisha na pango la mlimani. "Na Maandishi" ambayo ni maandishi yaliyojumuisha majina yao na kisa chao kwa sababu walikaa humo muda mrefu.
#
{10} ثم ذكر قصَّتهم مجملةً فصَّلها بعد ذلك فقال: {إذ أوى الفتيةُ}؛ أي: الشباب {إلى الكهف}: يريدون بذلك التحصُّن والتحرُّز من فتنة قومهم لهم، {فقالوا ربَّنا آتنا من لدُنك رحمةً}؛ أي: تُثَبِّتنا بها وتحفظُنا من الشرِّ وتوفِّقنا للخير، {وهيِّئ لنا من أمرِنا رَشَداً}؛ أي: يسِّر لنا كلَّ سببٍ موصل إلى الرشد، وأصلحْ لنا أمر ديننا ودُنيانا؛ فجمعوا بين السعي والفرار من الفتنة إلى محلٍّ يمكن الاستخفاء فيه، وبين تضرُّعهم وسؤالهم لله تيسير أمورهم وعدم اتِّكالهم على أنفسهم وعلى الخلق.
{10} Kisha akataja kisa chao kwa ujumla, kisha akakieleza baada ya hayo, akasema, "Vijana hao walipokimbilia kwenye pango" ili kujilinda na kujiweka mbali na majaribio ya kaumu yao kwao. "Na wakasema, "Mola wetu Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako." Yaani, tuimarishe kwayo na utuhifadhi kutokana na uovu na utuwezeshe ya heri. "Na tutengezee uwongofu katika jambo letu." Yaani, turahisishie kila njia ya yenye kufikisha katika uwongofu, na tutengenezee mambo ya dini yetu na dunia yetu. Basi wakakusanya kati ya kufanya bidii na kukimbia kutoka katika majaribio hadi katika mahali wanapoweza kujificha hapo, na kati ya kuomba kwao dua kwa unyenyekevu na kumuomba Mwenyezi Mungu kurahisisha mambo yao na tena hawakujitegemea tu wenyewe na kuwatengemea viumbe.
#
{11} فلذلك استجاب الله دعاءهم، وقيَّض لهم ما لم يكن في حسابهم؛ قال: {فضَرَبْنا على آذانهم في الكهف}؛ أي: أنمناهم {سنينَ عدداً}: وهي ثلاثمائة سنة وتسع سنين، وفي النوم المذكور حفظٌ لقلوبهم من الاضطراب والخوف وحفظٌ لهم من قومهم، [وليكون آية بينة].
{11} Na ndiyo maana, Mwenyezi Mungu akawaitikia dua yao, na akawawekea tayari yale ambayo hayakuwa katika mawazo yao. Akasema, "Basi tukayaziba masikio yao kuwalaza humo pangoni kwa muda wa miaka kadhaa," ambayo ilikuwa miaka mia tatu na tisa. Na katika kulala kwao huko kulikuwa na kuhifadhi nyoyo zao kutokana na kutotulia, hofu, na kuwalinda kutokana na kaumu yao,
[na ili iwe ni ishara iliyo wazi].
#
{12} {ثم بعثْناهم}؛ أي: من نومهم، {لنعلم أيُّ الحزبينِ أحصى لما لَبِثوا أمداً}؛ أي: لنعلم أيُّهم أحصى لمقدار مدَّتهم؛ كما قال تعالى: {وكذلك بَعَثْناهم ليتساءلوا بينهم ... } الآية، وفي العلم بمقدار لَبْثِهِم ضبطٌ للحساب، ومعرفةٌ لكمال قدرة الله تعالى وحكمتِهِ ورحمتِهِ؛ فلو استمرُّوا على نومهم؛ لم يحصُل الاطلاع على شيء من ذلك من قصتهم.
{12} "Kisha tukawazindua;" yaani, kutoka katika usingizi wao, "ili tujue ni lipi katika makundi mawili yale ndilo lilihesabu sawa urefu wa muda waliokaa." Kama alivyosema yeye Mtukufu, "Na kwa namna hiyo ndivyo tulivyowainua usingizini ili wapate kuulizana wao kwa wao..." hadi mwisho wa aya. Na katika kujua kwao kiwango cha wakati wa kukaa kwao kuna udhibiti mzuri wa hesabu, na kujua ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hekima yake, na rehema yake. Na ikiwa wangeendelea kulala, basi hakuna lolote katika hayo lingejulikana kuhusiana na kisa chao.
{نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ نَبَأَهُمْ بِالْحَقِّ إِنَّهُمْ فِتْيَةٌ آمَنُوا بِرَبِّهِمْ وَزِدْنَاهُمْ هُدًى (13) وَرَبَطْنَا عَلَى قُلُوبِهِمْ إِذْ قَامُوا فَقَالُوا رَبُّنَا رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَنْ نَدْعُوَ مِنْ دُونِهِ إِلَهًا لَقَدْ قُلْنَا إِذًا شَطَطًا (14)}.
13. Sisi tunakusimulia habari zao kwa haki. Hakika wao walikuwa ni vijana waliomuamini Mola wao Mlezi. Na Sisi tukawazidisha uwongofu. 14. Na tukazitia nguvu nyoyo zao waliposimama na wakasema, "Mola wetu Mlezi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi. Hatutamwita mwingine kabisa badala yake kuwa ni Mungu. Hivyo, itakuwa tumesema jambo la kuvuka mpaka.
#
{13} هذا شروعٌ في تفصيل قصَّتهم، وأنَّ الله يقصُّها على نبيِّه بالحقِّ والصدق الذي ما فيه شكٌّ ولا شبهةٌ بوجه من الوجوه. {إنَّهم فتيةٌ آمنوا بربِّهم}: وهذا من جموع القلَّة، يدلُّ ذلك على أنَّهم دون العشرة، آمنوا بالله وحدَه لا شريك له من دون قومهم، فشكر اللهُ لهم إيمانَهم، فزادهم هدىً؛ أي: بسبب أصل اهتدائهم إلى الإيمان زادهم الله من الهدى الذي هو العلم النافع والعمل الصالح؛ كما قال تعالى: {ويزيدُ الله الذين اهتَدَوْا هدىً}.
{13} Huu ndio mwanzo wa kubainisha kisa chao kwa kina, na kwamba Mwenyezi Mungu anambainishia Mtume wake kwa kina kisa hicho kwa haki na ukweli ambao hauna shaka yoyote ndani yake wala lolote la kuleta mchanganyiko kwa namna yoyote ile. "Hakika wao walikuwa ni vijana waliomuamini Mola wao Mlezi" kati ya kaumu yao, Yeye peke yake ambaye hana mshirika yeyote. Basi Mwenyezi Mungu akawashukuru kwa imani yao na akawazidishia uwongofu, ambao ni elimu yenye manufaa na matendo mema. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, “Na Mwenyezi Mungu huwazidishia uwongofu wale walioongoka."
#
{14} {وربطنا على قلوبهم}؛ أي: صبَّرناهم وثبَّتناهم وجعلنا قلوبهم مطمئنَّة في تلك الحالة المزعجة، وهذا من لطفِهِ تعالى بهم وبرِّه أنْ وفَّقهم للإيمان والهدى والصبر والثبات والطمأنينة. {إذْ قاموا فقالوا ربُّنا ربُّ السمواتِ والأرض}؛ أي: الذي خَلَقَنا ورَزَقَنا ودبَّرنا وربَّانا هو خالق السماواتِ والأرض، المنفرد بخلق هذه المخلوقات العظيمة، لا تلك الأوثان والأصنام، التي لا تَخْلُق ولا ترزُقُ ولا تملِكُ نفعاً ولا ضرًّا ولا موتاً ولا حياةً ولا نشوراً، فاستدلوا بتوحيد الربوبيَّة على توحيد الإلهيَّة. ولهذا قالوا: {لن نَدْعُوَ من دونِهِ إلهاً}؛ أي: من سائر المخلوقات، {لقد قُلْنا إذاً} ـ أي: إن دَعَوْنا معه آلهةً بعدما علمنا أنَّه الربُّ الإله الذي لا تجوز ولا تنبغي العبادة إلاَّ له ـ {شططاً}؛ أي: ميلاً عظيماً عن الحقِّ، وطريقاً بعيدة عن الصواب، فجمعوا بين الإقرار بتوحيد الربوبيَّة وتوحيد الإلهيَّة والتزام ذلك وبيان أنَّه الحقُّ وما سواه باطلٌ، وهذا دليلٌ على كمال معرفتهم بربِّهم وزيادة الهدى من الله لهم.
{14} "Na tukazitia nguvu nyoyo zao." Yaani, tuliwapa subira, na kuwaimarisha, na tukazifanya nyoyo zao kutulia katika hali hiyo ya kusumbua. Na haya ni katika upole wake Mwenyezi Mungu mtukufu kwao, na wema wake kwamba aliwawezesha kuamini, na uwongofu, na subira, na uimara, na utulivu. "Waliposimama na wakasema, Mola wetu Mlezi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi." Yaani, ambaye alituumba, na akaturuzuku, na akatuendesha, na akatulea. Yeye ndiye muumba wa mbingu na ardhi, ambaye ni wa Pekee katika kuumba viumbe hawa wakubwa. Siyo viabudiwavyo hivyo na masanamu, ambavyo haviumbi, wala haviruzuku, wala havimiliki manufaa wala madhara, wala kifo, wala uhai, wala kufufua. Kwa hivyo, wakatuumia tauhidi ya umola kama ushahidi wa tauhidi ya uungu. Na ndiyo maana wakasema, “Hatutamwita mwingine kabisa badala yake kuwa ni Mungu. Hivyo, itakuwa tumesema" ikiwa tutawaomba waungu wengine pamoja naye baada ya sisi kujua kwamba, Yeye ndiye Mola Mlezi ambaye hairuhusiki wala haifai kuabudiwa isipokuwa Yeye tu; "jambo la kuvuka mpaka" kutoka katika haki, na tutakuwa katika njia iliyo mbali na njia iliyo sawa. Kwa hivyo wakaunganisha kati ya kukiri tauhidi ya umola na tauhidi ya uungu, na kushikamana na hilo, na kubainisha kuwa hiyo ndiyo haki, na kila kitu kinginecho ni batili. Na huu ni ushahidi juu ya kumjua kwao kikamilifu Mola wao Mlezi na kuwaongezewa uwongofu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
{هَؤُلَاءِ قَوْمُنَا اتَّخَذُوا مِنْ دُونِهِ آلِهَةً لَوْلَا يَأْتُونَ عَلَيْهِمْ بِسُلْطَانٍ بَيِّنٍ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَى عَلَى اللَّهِ كَذِبًا (15)}.
15. Hawa kaumu yetu walijifanyia miungu mingine badala yake Yeye. Kwa nini basi hawawatolei uthibitisho ulio dhahiri? Na ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu?
#
{15} لما ذكروا ما مَنَّ الله به عليهم من الإيمان والهدى والتقوى؛ التفتوا إلى ما كان عليه قومُهم من اتِّخاذ الآلهة من دون الله، فمقتوهم، وبيَّنوا أنهم ليسوا على يقينٍ من أمرهم، بل هم في غاية الجهل والضلال، فقالوا: {لولا يأتونَ عليهم بسلطانٍ بيِّن}؛ أي: بحجَّة وبرهان على ما هُمْ عليه من الباطل، ولا يستطيعون سبيلاً إلى ذلك، وإنَّما ذلك افتراءٌ منهم على الله وكذبٌ عليه، وهذا أعظم الظُّلم، ولهذا قال: {فمن أظْلَمُ ممَّنِ افترى على الله كَذِباً}.
{15} Walipotaja yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwapa miongoni mwa imani, uwongofu, na uchamungu, wakageukia yale waliyokuwa wakiyafanya kaumu yao ya kujifanyia miungu badala ya Mwenyezi Mungu. Basi wakawachukia mno, na wakabainisha kuwa hawakuwa na yakini na mambo yao hayo. Bali wako katika ujinga mkubwa zaidi na wapotovu. Wakasema, "Kwa nini basi hawawatolei uthibitisho ulio dhahiri" juu ya hayo ya batili wayafanyayo? Na wala hawana njia yoyote ya kufanya hivyo. Kwa maana, hayo ni maneno yao tu waliyomzushia Mwenyezi Mungu na kumdanganyishia. Na hii ndiyo dhuluma kubwa zaidi. Na ndiyo maana akasema, “Na ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu?"
{وَإِذِ اعْتَزَلْتُمُوهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ إِلَّا اللَّهَ فَأْوُوا إِلَى الْكَهْفِ يَنْشُرْ لَكُمْ رَبُّكُمْ مِنْ رَحْمَتِهِ وَيُهَيِّئْ لَكُمْ مِنْ أَمْرِكُمْ مِرْفَقًا (16)}.
16. Na mkijitenga nao na vile wanavyoviabudu badala ya Mwenyezi Mungu, basi kimbilieni pangoni, awafungulie Mola wenu Mlezi katika rehema zake, na awatengenezee ya kuwafaa katika mambo yenu.
#
{16} أي: قال بعضهم لبعض: إذ حَصَلَ لكم اعتزالُ قومكم في أجسامكم وأديانكم؛ فلم يَبْقَ إلاَّ النجاء من شرِّهم والتسبُّب بالأسباب المفضية لذلك؛ لأنَّه لا سبيل لهم إلى قتالهم ولا بقائهم بين أظهرهم وهم على غير دينهم. {فأوُوا إلى الكهفِ}؛ أي: انضمُّوا إليه واختفوا فيه، {يَنْشُرْ لكم ربُّكم من رحمتِهِ ويهيِّئْ لكم من أمرِكُم مِرْفَقاً}: وفيما تقدَّم أخبر أنهم دَعَوْه بقولهم: {ربَّنا آتنا من لَدُنْكَ رحمةً وهَيِّئ لنا من أمرنا رَشَداً}؛ فجمعوا بين التبرِّي من حولهم وقوَّتهم والالتجاء إلى الله في صلاح أمرهم ودعائه بذلك، وبين الثقة بالله أنه سيفعل ذلك، لا جَرَمَ أنَّ الله نَشَرَ لهم من رحمتِهِ وهيَّأ لهم من أمرهم مِرْفَقاً؛ فحفظ أديانهم وأبدانهم، وجعلهم من آياته على خلقه، ونشر لهم من الثناء الحسن ما هو من رحمته بهم، ويسَّر لهم كلَّ سبب، حتَّى المحلَّ الذي ناموا فيه كان على غايةِ ما يمكنُ من الصيانة؛ ولهذا قال:
{16} Yaani wao kwa wao wakaambiana: Mkijitenga na kaumu yenu kwa miili yenu na dini zenu, basi haitabakia isipokuwa kuokoka kutokana na uovu wao na kufanya sababu zenye kusababisha hayo. Kwa sababu hawana njia yoyote ya kupigana nao wala kubakia miongoni mwao ilhali hawaifuati dini yao. "Basi kimbilieni pangoni" mjifiche humo "awafungulie Mola wenu Mlezi katika rehema zake, na awatengenezee ya kuwafaa katika mambo yenu." Na katika yaliyotangulia alijulisha kuwa wao walimuomba kwa kusema, "Mola wetu Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uwongofu katika jambo letu." Basi wakajumuisha kati ya kujitenga na uwezo wao na nguvu zao, na kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu ili awatengenezee mambo yao na wamuombe hayo, na kati ya kuwa na imani na Mwenyezi Mungu kwamba atafanya hivyo. Hakuna shaka kwamba Mwenyezi Mungu aliwafungulia katika rehema zake na akawatengenezea ya kuwafaa katika mambo yao. Basi akazihifadhi dini zao na miili yao, na akawafanya kuwa miongoni mwa ishara zake kwa viumbe vyake, na akawaeneza sifa nzuri jambo ambalo ni katika rehema yake kwao, na akawasahilishia kila njia, hata mahali walipokuwa wakilala palikuwa na kuhifadhiwa kwa hali ya juu zaidi iwezekanayo.
Na ndiyo maana akasema:
{وَتَرَى الشَّمْسَ إِذَا طَلَعَتْ تَزَاوَرُ عَنْ كَهْفِهِمْ ذَاتَ الْيَمِينِ وَإِذَا غَرَبَتْ تَقْرِضُهُمْ ذَاتَ الشِّمَالِ وَهُمْ فِي فَجْوَةٍ مِنْهُ ذَلِكَ مِنْ آيَاتِ اللَّهِ مَنْ يَهْدِ اللَّهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِ وَمَنْ يُضْلِلْ فَلَنْ تَجِدَ لَهُ وَلِيًّا مُرْشِدًا (17) وَتَحْسَبُهُمْ أَيْقَاظًا وَهُمْ رُقُودٌ وَنُقَلِّبُهُمْ ذَاتَ الْيَمِينِ وَذَاتَ الشِّمَالِ وَكَلْبُهُمْ بَاسِطٌ ذِرَاعَيْهِ بِالْوَصِيدِ لَوِ اطَّلَعْتَ عَلَيْهِمْ لَوَلَّيْتَ مِنْهُمْ فِرَارًا وَلَمُلِئْتَ مِنْهُمْ رُعْبًا (18)}.
17. Na unaliona jua linapochomoza, linainamia kuliani mwao kutoka hapo pangoni, na linapokuchwa, linawakwepa kushotoni, na wao wamo katika uwazi wa pango. Hizo ni katika ishara za Mwenyezi Mungu. Yule ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa, basi huyo ameongoka. Na yule ambaye anampoteza, basi hutampatia msimamizi wa kumwongoza. 18. Nawe utawadhania wa macho, na hali wamelala. Nasi tunawageuza kulia na kushoto. Na mbwa wao amenyoosha miguu yake ya mbele kizingitini. Kama ungeliwatokea, hapana shaka ungeligeuka kuwakimbia, huku umejaa hofu juu yao.
#
{17} أي: حفظهم الله من الشمس، فيسَّر لهم غاراً إذا طلعت الشمسُ؛ تميلُ عنه يميناً، وعند غروبها تميلُ عنه شمالاً؛ فلا ينالُهم حرُّها فتفسدُ أبدانُهم بها. {وهم في فجوةٍ منه}؛ أي: من الكهف؛ أي: مكان متَّسع، وذلك ليطرُقَهم الهواءُ والنسيمُ، ويزولُ عنهم الوخم والتأذِّي بالمكان الضيِّق، خصوصاً مع طول المكث، و {ذلك من آيات الله}: الدالَّة على قدرته ورحمته وإجابة دعائهم وهدايتهم حتى في هذه الأمور، ولهذا قال: {مَن يَهْدِ الله فهو المهتدِ}؛ أي: لا سبيل إلى نيل الهداية إلاَّ من الله؛ فهو الهادي المرشدُ لمصالح الدارين. {ومَن يُضْلِلْ فلن تَجِدَ له وليًّا مرشداً}؛ أي: لا تجد من يتولاَّه ويدبِّره على ما فيه صلاحُه، ولا يرشِدُه إلى الخير والفلاح؛ لأنَّ الله قد حَكَمَ عليه بالضَّلال، ولا رادَّ لحكمِهِ.
{17} Yaani, Mwenyezi Mungu aliwahifadhi kutokana na jua kwa kuwarahisishia kupata pango ambalo lilipokuwa jua linachomoza, linaliacha na kuelekea kulia wake, na linapotua, linaliacha na kuelekea kushoto kwake. Basi wakawa hawapatwi na joto lake ambalo lingeweza kuiharibu miili yao. "Na wao wamo katika uwazi wa pango" ili hewa na upepo mzuri viwaguse, na uwaondokee uvundo na kudhurika na mahali finyu, hasa ikiwa ni kukaa kwa muda mrefu. Na "hizo ni katika ishara za Mwenyezi Mungu" zinazoonyesha uwezo wake, rehema yake, kuitikia dua zao, na kuwaongoa hata katika mambo haya. Na ndiyo maana akasema, "Yule ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa, basi huyo ameongoka." Yaani, hakuna njia ya kupata uwongofu isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye mwenye kuongoa, kuelekeza masilahi ya nyumba hizi mbili. "Na yule ambaye anampoteza, basi hutampatia msimamizi wa kumwongoza." Yaani, hutampata mwenye kumsimamia na kumuendesha kwa namna ambayo ina manufaa kwake, wala kumuelekeza katika yale ambayo yana heri kwake na mafanikio. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alikwisha mhukumia upotovu, na hakuna wa kuzuia hukumu yake.
#
{18} {وتحسبهم أيقاظاً وهم رقودٌ}؛ أي: تحسبهم أيها الناظر إليهم كأنَّهم أيقاظٌ، والحالُ أنَّهم نيامٌ. قال المفسرون: وذلك لأنَّ أعينَهم منفتحةٌ لئلاَّ تفسدَ؛ فالناظرُ إليهم يحسبهم أيقاظاً وهم رقودٌ. {ونقلِّبُهم ذات اليمين وذات الشمال}: وهذا أيضاً من حفظه لأبدانهم؛ لأنَّ الأرض من طبيعتها أكلُ الأجسام المتَّصلة بها؛ فكان من قَدَرِ الله أن قلَّبهم على جنوبِهِم يميناً وشمالاً بقدر ما لا تُفْسِدُ الأرض أجسامهم، والله تعالى قادرٌ على حفظهم من الأرض من غير تقليبٍ، ولكنَّه تعالى حكيمٌ، أراد أن تجرِيَ سنَّته في الكون ويربُطَ الأسباب بمسبّباتها. {وكلبُهُم باسطٌ ذراعية بالوصيد}؛ أي: الكلب الذي كان مع أصحابِ الكهف أصابَهُ ما أصابَهم من النوم وقتَ حراستِهِ، فكان باسطاً ذراعيه بالوصيد؛ أي: الباب أو فنائه. هذا حفظُهم من الأرض، وأما حفظُهم من الآدميين؛ فأخبر أنَّه حماهم بالرُّعب الذي نَشَرَهُ الله عليه؛ فلو اطَّلع عليهم أحدٌ؛ لامتلأ قلبه رعباً وولَّى منهم فراراً، وهذا الذي أوجب أن يبقَوْا كلَّ هذه المدَّة الطويلة وهم لم يعثر عليهم أحدٌ مع قربهم من المدينة جدًّا، والدليل على قربهم أنَّهم لما استيقظوا؛ أرسلوا أحدَهم يشتري لهم طعاماً من المدينة، وبقوا في انتظاره، فدلَّ ذلك على شدَّة قربهم منها.
{18} "Nawe utawadhania wa macho, na hali wamelala." Yaani, ewe mwenye kuwatazama utawadhania kana kwamba wako macho, lakini hali ni kwamba wamelala.
Wafasiri walisema: Hayo ni kwa sababu macho yao yalikuwa wazi ili yasiharibike. Kwa hivyo, mwenye kuwatazama, atawadhania wako macho, ilhali wamelala. "Nasi tunawageuza kulia na kushoto." Haya pia ni katika kuihifadhi kwake miili yao. Kwa sababu kawaida ya ardhi ni kula vitu vinavyogusana nayo. Na ilikuwa ni katika majaliwa ya Mwenyezi Mungu kuwageuza ubavuni mwao, kulia na kushoto kwa kiasi ambacho ardhi haiwezi kuharibu miili yao. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye uwezo wa kuwahifadhi kutokana na ardhi hata bila ya kuwageuza, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye hekima. Alitaka kufanyisha sheria yake katika ulimwengu na kuunganisha visababishi na athari zake. "Na mbwa wao amenyoosha miguu yake ya mbele kizingitini." Yaani, mbwa yule aliyekuwa pamoja na hao watu wa pangoni alipatwa na usingizi ule ule uliowapata wakati alipokuwa anawachunga. Na akawa ameinyoosha miguu yake ya mbele kizingitini, au katika ua wake. Huku ni kuwalinda kutokana na ardhi. Na ama kuwalinda kutokana na wanadamu, basi alijulisha kwamba aliwalinda kutokana na hofu ambayo Mwenyezi Mungu aliieneza juu yake. Na ikiwa mtu angewaona, basi moyo wake ungejaa hofu kubwa na angegeuka akiwakimbia. Na hili ndilo liliwafanya wakae hapo kwa muda mrefu huo bila ya kupatwa na yeyote pamoja na kwamba walikuwa karibu sana na mji. Na ushahidi wa ukaribu wake ni kwamba walipoamka, walimtuma mmoja wao kwenda kuwanunulia chakula kutoka mjini, na wengineo wakabaki wakimngojea, basi hilo likaonyesha ukaribu wao mkubwa sana na mji huo.
{وَكَذَلِكَ بَعَثْنَاهُمْ لِيَتَسَاءَلُوا بَيْنَهُمْ قَالَ قَائِلٌ مِنْهُمْ كَمْ لَبِثْتُمْ قَالُوا لَبِثْنَا يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ قَالُوا رَبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَا لَبِثْتُمْ فَابْعَثُوا أَحَدَكُمْ بِوَرِقِكُمْ هَذِهِ إِلَى الْمَدِينَةِ فَلْيَنْظُرْ أَيُّهَا أَزْكَى طَعَامًا فَلْيَأْتِكُمْ بِرِزْقٍ مِنْهُ وَلْيَتَلَطَّفْ وَلَا يُشْعِرَنَّ بِكُمْ أَحَدًا (19) إِنَّهُمْ إِنْ يَظْهَرُوا عَلَيْكُمْ يَرْجُمُوكُمْ أَوْ يُعِيدُوكُمْ فِي مِلَّتِهِمْ وَلَنْ تُفْلِحُوا إِذًا أَبَدًا (20)}.
19. Na kwa namna hiyo tuliwainua usingizini ili wapate kuulizana wao kwa wao.
Alisema msemaji katika wao: Mmekaa muda gani? Wakasema: Tumekaa siku moja au sehemu ya siku.
Wakasema: Mola wenu Mlezi ndiye anayejua zaidi muda mliokaa. Hebu mtumeni mmoja wenu na hizi fedha zenu aende mjini, akatazame chakula chake kipi kilicho bora kabisa awaletee cha kula. Naye afanye mambo hayo kwa busara, wala asiwataje kabisa kwa yeyote. 20. Kwani wao wakiwatambua, watawapiga mawe, au watawarudisha katika dini yao, na hapo hamtafanikiwa kabisa!
#
{19} يقول تعالى: {وكذلك بَعَثْناهم}: من نومهم الطويل، {ليتساءلوا بينَهم}؛ أي: ليتباحثوا للوقوف على الحقيقة من مدَّة لبثهم. {قال قائلٌ منهم كم لبِثْتُم قالوا لَبِثنا يوماً أو بعض يوم}: وهذا مبنيٌّ على ظنِّ القائل، وكأنَّهم وقع عندهم اشتباهٌ في طول مدَّتهم؛ فلهذا {قالوا ربُّكم أعلمُ بما لَبِثْتُم}: فردُّوا العلم إلى المحيط علمُهُ بكلِّ شيءٍ جملةً وتفصيلاً، ولعلَّ الله تعالى بعد ذلك أطلعهم على مدَّة لبثهم؛ لأنَّه بَعَثَهم ليتساءلوا بينَهم، وأخبر أنَّهم تساءلوا وتكلَّموا بمبلغ ما عندَهم وصار آخر أمرهم الاشتباه؛ فلا بدَّ أن يكون قد أخبرهم يقيناً؛ عَلِمْنا ذلك من حكمته في بعثهم، وأنه لا يفعل ذلك عبثاً، ومن رحمته بمن طلبَ علم الحقيقة في الأمور المطلوب علمُها وسعى لذلك ما أمكنه؛ فإن الله يوضِّح له ذلك، وبما ذَكرَ فيما بعده من قوله: {وكذلك أعْثَرْنا عليهم ليَعْلَموا أنَّ وعد الله حقٌّ وأنَّ الساعةَ لا رَيْبَ فيها}؛ فلولا أنَّه حصل العلم بحالهم؛ لم يكونوا دليلاً على ما ذكر. ثم إنَّهم لما تساءلوا بينهم، وجرى منهم ما أخبر الله به؛ أرسلوا أحدَهم بوَرِقِهم؛ أي: بالدراهم التي كانت معهم؛ ليشتري لهم طعاماً يأكلونه من المدينة التي خرجوا منها، وأمروه أن يتخيَّر من الطعام أزكاه؛ أي: أطيبه وألذَّه، وأن يتلطَّف في ذهابه وشرائه وإيابه، وأن يختفي في ذلك، ويُخفي حال إخوانه، ولا يُشْعِرَنَّ بهم أحداً.
{19} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, "Na kwa namna hiyo tuliwainua usingizini" mwao mrefu, "ili wapate kuulizana wao kwa wao" na wapate kujua uhakika wa kipindi walichokaa hapo.
"Alisema msemaji katika wao: Mmekaa muda gani? Wakasema: Tumekaa siku moja au sehemu ya siku." Hili linatokana na dhana ya mzungumzaji huyo. Na ni kana kwamba walichanganyikiwa kuhusiana na urefu wa muda huo. Na ndiyo maana,
"wakasema: Mola wenu Mlezi ndiye anayejua zaidi muda mliokaa." Kwa hivyo, wakarudisha elimu kwa Yule aliyezunguka kwa elimu yake kila kitu kwa ujumla na undani. Na huenda Mwenyezi Mungu Mtukufu baada ya hayo aliwajulisha muda wa kukaa kwao hapo. Kwa sababu aliwainua usingizini ili waulizane wao kwa wao, naye akatoa taarifa kwamba waliuliza na kusema kulingana na waliyokuwa nayo, na jambo lao la mwisho likawa shaka. Lazima aliwaambia kwa uhakika. Tunayajua haya kutokana na hekima yake katika kuwatuma, na kwamba hafanyi hivyo bure, na kutoka kwa rehema yake kwa wale wanaotafuta elimu ya ukweli katika mambo yanayotakiwa kujulikana na kujitahidi kufanya hivyo kadiri inavyowezekana. Mwenyezi Mungu anambainishia hilo,
na katika yale aliyoyataja baadaye katika kauli yake: “Na namna hivi ndivyo tulivyowajulisha kwa watu wapate kujua ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, na kwamba Saa (Qiyama) haina shaka.” Lau asingepata elimu ya hali yao, isingekuwa ushahidi wa kile kilichotajwa.
#
{20} وذكروا المحذور من اطِّلاع غيرهم عليهم وظهورهم عليهم أنَّهم بين أمرين: إما الرَّجم بالحجارة فيقتلونهم أشنع قِتلة لِحِنْقهم عليهم وعلى دينهم، وإما أن يفتنوهم عن دينهم ويردُّوهم في ملَّتهم، وفي هذه الحال لا تفلحون أبداً، بل يخسرون في دينهم ودُنياهم وأخراهم.
وقد دلَّت هاتان الآيتان على عدة فوائد:
منها: الحثُّ على العلم وعلى المباحثة فيه؛ لكون الله بعثهم لأجل ذلك.
ومنها: الأدب فيمن اشتبه عليه العلم أن يردَّه إلى عالمه، وأن يَقِفَ عند حدِّه.
ومنها: صحة الوكالة في البيع والشراء وصحَّة الشركة في ذلك.
ومنها: جواز أكل الطيِّبات والمطاعم اللَّذيذة إذا لم تخرُجْ إلى حدِّ الإسراف المنهيِّ عنه؛ لقوله: {فَلْيَنظُرْ أيُّها أزكى طعاماً فليأتِكُم برزقٍ منه}: وخُصوصاً إذا كان الإنسان لا يلائمه إلا ذلك، ولعلَّ هذا عمدة كثير من المفسِّرين القائلين بأنَّ هؤلاء أولاد ملوك؛ لكونهم أمروه بأزكى الأطعمة التي جرت عادة الأغنياء الكبار بتناولها.
ومنها: الحثُّ على التحرُّز والاستخفاء والبعد عن مواقع الفتن في الدين واستعمال الكِتْمان في ذلك على الإنسان وعلى إخوانه في الدين.
ومنها: شدة رغبة هؤلاء الفتية في الدين وفرارهم من كلِّ فتنةٍ في دينهم وتركُهم أوطانَهم في الله.
ومنها: ذِكْر ما اشتمل عليه الشرُّ من المضارِّ والمفاسد الداعية لبغضِهِ وتركِهِ، وأنَّ هذه الطريقة هي طريقة المؤمنين المتقدِّمين والمتأخِّرين؛ لقولهم: {ولن تُفْلِحوا إذاً أبداً}.
{20} Na wakataja yale yanayotahadhariwa katika wengine kuwajua na wao kuwadhihirikia wengine nayo ni kuwa wao wako baina ya vitu viwili: ima kupigwa mawe na kuwaua mauaji mabaya zaidi kwa sababu ya kuwaghadhibikia wao na dini yao, au kuwatia katika majaribio ili waiache Dini yao na kuwarejesha katika mila zao. Na katika hali hii hawatafaulu kamwe, bali watapata hasara katika Dini yao, dunia yao na Akhera yao.
Na Aya hizi mbili ziliashiria manufaa kadhaa: Miongoni mwake ni kuhimiza kutafuta elimu na kuifanyia utafiti elimu hiyo, kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwainua kutoka usingizini kwa ajili ya hayo. Na miongoni mwake ni kwamba adabu njema kwa yule ambaye amechanganyikiwa katika elimu yake ni kuirejesha kwa anayeijua, na kwamba asimamie kwenye kikomo chake. Na miongoni mwake ni kwamba kuwakilisha wengine kunaruhusika katika kuuza na kununua na kwamba kufanya ushirika katika hayo kunaruhusika. Na miongoni mwake ni kwamba inaruhusika kula vitu vizuri na vyakula vitamu ikiwa havijafikia kiwango cha kupitiliza mipaka ambako kulikatazwa, kwa sababu ya kauli yake, "akatazame chakula chake kipi kilicho bora kabisa awaletee cha kula" hasa ikiwa mtu huyo haimfailii kitu kingine isipokuwa hicho. Na huenda huu ndio msingi wa wafasiri wengi wanaosema kuwa hawa ni watoto wa wafalme. Kwa sababu walimwamuru aje na vyakula bora zaidi ambavyo kwa kawaida watu matajiri huvila. Na miongoni mwake ni kuhimiza kutahadhari, kujificha, na kujiweka mbali na maeneo ya majaribio katika dini, na kutumia usiri katika kumficha mtu na ndugu zake katika dini. N miongoni mwake ni kwamba utashi mkubwa mno wa vijana hao juu ya dini, na kukimbia kwao kila majaribio katika dini yao, na kuziacha nchi zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na miongoni mwake ni kwamba kutaja madhara na uharibifu uliomo ndani ya uovu yanayomfanya mtu kuuchukia na kuuacha, na kwamba njia hii ndiyo njia ya Waumini wa mwanzo na wa baadaye, kama wanavyosema, “Na hapo hamtafaulu kamwe."
{وَكَذَلِكَ أَعْثَرْنَا عَلَيْهِمْ لِيَعْلَمُوا أَنَّ وَعْدَ اللَّهِ حَقٌّ وَأَنَّ السَّاعَةَ لَا رَيْبَ فِيهَا إِذْ يَتَنَازَعُونَ بَيْنَهُمْ أَمْرَهُمْ فَقَالُوا ابْنُوا عَلَيْهِمْ بُنْيَانًا رَبُّهُمْ أَعْلَمُ بِهِمْ قَالَ الَّذِينَ غَلَبُوا عَلَى أَمْرِهِمْ لَنَتَّخِذَنَّ عَلَيْهِمْ مَسْجِدًا (21)}.
21. Na namna hivo ndivyo tulivyowajulisha kwa watu ili wapate kujua ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, na kwamba Saa haina shaka. Walipokuwa wakigombania jambo lao wao kwa wao,
wakasema: Jengeni jengo juu yao. Mola wao Mlezi anawajua vyema.
Wakasema wale walioshinda katika shauri yao: Bila ya shaka tutajenga msikiti juu yao.
#
{21} يخبر تعالى أنَّه أطْلَعَ الناس على حال أهل الكهف، وذلك ـ والله أعلم ـ بعدما استيقظوا وبعثوا أحدهم يشتري لهم طعاماً وأمروه بالاستخفاء والإخفاء، فأراد الله أمراً فيه صلاحٌ للناس وزيادةُ أجرٍ لهم، وهو أنَّ الناس رأوا منهم آيةً من آيات الله المشاهَدَةِ بالعيان على أنَّ وعدَ الله حقٌّ لا شكَّ فيه ولا مِرْيةَ ولا بُعْدَ بعدما كانوا يتنازعون بينَهم أمرَهم؛ فمن مثبتٍ للوعد والجزاء ومن نافٍ لذلك، فجعل قصَّتَهم زيادةَ بصيرةٍ ويقينٍ للمؤمنين وحجَّةً على الجاحدين، وصار لهم أجرُ هذه القضيَّة، وشهَّر الله أمرهم، ورفع قدرهم، حتى عظَّمهم الذين اطَّلعوا عليهم؛ قالوا: {ابنوا عليهم بُنياناً}: الله أعلمُ بحالهم ومآلهم! وقال مَنْ غَلَبَ على أمرهم ـ وهم الذين لهم الأمرُ ـ:
{لَنَتَّخِذَنَّ عليهم مسجداً}؛ أي: نعبد الله تعالى فيه ونتذكَّر به أحوالهم وما جرى لهم. وهذه الحالة محظورةٌ نهى عنها النبيُّ - صلى الله عليه وسلم - وذمَّ فاعليها، ولا يدلُّ ذكرها هنا على عدم ذمِّها؛ فإنَّ السياق في شأن أهل الكهف والثناء عليهم، وأنَّ هؤلاء وصلت بهم الحالُ إلى أن قالوا ابنوا عليهم مسجداً بعد خوف أهل الكهف الشديد من قومهم وحَذَرِهم من الاطِّلاع عليهم، فوصلت الحال إلى ما ترى.
وفي هذه القصة دليلٌ على أنَّ من فرَّ بدينه من الفتن؛ سلَّمه الله منها، وأنَّ مَن حرص على العافية؛ عافاه الله، ومن أوى إلى الله؛ آواه الله وجعله هدايةً لغيره، ومن تحمل الذُّلَّ في سبيله وابتغاء مرضاته؛ كان آخرُ أمره وعاقبته العز العظيم من حيث لا يحتسب، وما عند الله خيرٌ للأبرار.
{21} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba aliwajulisha watu juu ya hali ya hao watu wa pangoni, na hilo ni kwa sababu - na Mwenyezi Mungu anajua zaidi - baada ya wao kuamka na kumtuma mmoja wao kuwanunulia chakula na wakamuamuru kujificha, na kuzificha habari zao, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akataka kitu ambacho ni kizuri kwa watu na kuwaongezea malipo. Nalo ni kwamba watu waliona kutoka kwao ishara miongoni mwa ishara za Mwenyezi Mungu zinazoonekana kwa macho, kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu bila shaka ni ya haki, wala haina kusitasita kokote juu yake. Wala si ati haliwezekani baada ya kwamba walikuwa wakibishana kati yao juu yao. Kukawa kuna anayeithibitisha ahadi hiyo na malipo, na yule anayelikataa hilo. Basi kisa chao hicho kikawazidisha Waumini ufahamu, yakini na hoja dhidi ya wale wanaolikataa. Nao wakapata malipo ya suala hili, na Mwenyezi Mungu akalifanya jambo lao kuwa mashuhuri, na akainua hadhi yao, mpaka wale waliowaona wakawatukuza. Wakasema, "Jengeni jengo juu yao.
" Mwenyezi Mungu ndiye anayajua hali zao na hatima yao! Akasema: Yeyote mwenye mamlaka juu ya mambo yao - hao ndio wenye mamlaka. "Bila ya shaka tutajenga msikiti juu yao." Yaani, ili tumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu humo na tukumbuke kwa huo msikiti hali zao na yaliyowatokea. Lakini hali hii imeharamishwa na Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - aliikataza na akawashutumu wanaoifanya. Na kutajwa kwake hapa hakuonyeshi kuwa haishutumiwi. Kwa maana, muktadha huu unahusu suala la watu wale wa pangoni na kuwasifu,
na kwamba watu hao waliowakuta humo walifikia hali ya kusema: Jengeni msikiti juu yao baada ya watu wa pangoni kuwaogopa sana kaumu yao na kujitahadhari kwao waje kujulikana, kwa hivyo hali ikafikia kile unachokiona. Katika kisa hiki kuna ushahidi kwamba yeyote anayekimbia majaribio katika dini yake, Mwenyezi Mungu humkinga kutokana nayo, na kwamba anayefanya bidii kubwa juu ya kuwa salama, Mwenyezi Mungu humpa salama. Na mwenye kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humpa kimbilio na anamfanya kuwa mwongozo kwa wengine. Na mwenye kuvumilia unyonge katika njia yake na kutafuta radhi zake, mwisho wake huwa ni utukufu mkubwa kutokea asipotarajia. Na kilicho kwa Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kwa walio wema.
{سَيَقُولُونَ ثَلَاثَةٌ رَابِعُهُمْ كَلْبُهُمْ وَيَقُولُونَ خَمْسَةٌ سَادِسُهُمْ كَلْبُهُمْ رَجْمًا بِالْغَيْبِ وَيَقُولُونَ سَبْعَةٌ وَثَامِنُهُمْ كَلْبُهُمْ قُلْ رَبِّي أَعْلَمُ بِعِدَّتِهِمْ مَا يَعْلَمُهُمْ إِلَّا قَلِيلٌ فَلَا تُمَارِ فِيهِمْ إِلَّا مِرَاءً ظَاهِرًا وَلَا تَسْتَفْتِ فِيهِمْ مِنْهُمْ أَحَدًا (22)}.
22.
Watasema: Walikuwa watatu, wa nne wao ni mbwa wao.
Na wanasema: Walikuwa watano, wa sita wao ni mbwa wao. Wanabahatisha ghaibu.
Na wanasema: Walikuwa saba, na wa nane wao ni mbwa wao.
Sema: Mola wangu Mlezi ndiye anayejua sawa sawa hesabu yao. Hawawajui isipokuwa wachache tu. Basi usibishane juu yao isipokuwa kwa mabishano ya juu juu tu hivi. Wala usiulize habari zao kwa yeyote yule.
#
{22} يخبر تعالى عن اختلاف أهل الكتاب في عدَّة أصحاب الكهف اختلافاً صادراً عن رجمهم بالغيب وتقوُّلهم بما لا يعلمون، وأنَّهم فيهم على ثلاثة أقوال: منهم من يقولُ: {ثلاثةٌ رابُعهم كلبهم}، ومنهم من يقول: {خمسةٌ سادسُهم كلبُهم}، وهذان القولان ذكر الله بعدهما أنَّ هذا رجمٌ منهم بالغيب، فدلَّ على بطلانهما، ومنهم من يقول: {سبعةٌ وثامِنُهم كلبُهم}، وهذا ـ والله أعلم ـ هو الصوابُ؛ لأنَّ الله أبطل الأوَّلَيْن ولم يبطِلْه، فدلَّ على صحَّته، وهذا من الاختلاف الذي لا فائدة تحته، ولا يحصُلُ بمعرفة عددهم مصلحةٌ للناس دينيَّة ولا دنيويَّة، ولهذا قال تعالى: {قل ربِّي أعلمُ بعِدَّتِهم ما يعلمُهُم إلاَّ قليلٌ}: وهم الذين أصابوا الصوابَ وعلموا إصابتهم. {فلا تمارِ}: تجادل وتُحاج {فيهم إلاَّ مراء ظاهرا}؛ أي: مبنياً على العلم واليقين، ويكون أيضاً فيه فائدةٌ، وأما المماراة المبنيَّة على الجهل والرجم بالغيب أو التي لا فائدةَ فيها: إما أنْ يكونَ الخصمُ معانداً، أو تكون المسألةُ لا أهميَّة فيها ولا تحصُلُ فائدةٌ دينيَّةٌ بمعرفتها؛ كعدد أصحاب الكهف ونحو ذلك؛ فإنَّ في كثرة المناقشات فيها والبحوث المتسلسلة تضييعاً للزَّمان وتأثيراً في مودَّة القلوب بغير فائدة. {ولا تَسْتَفْتِ فيهم}؛ أي: في شأن أهل الكهف {منهم}؛ أي: من أهل الكتاب، {أحداً}: وذلك لأنَّ مبنى كلامهم فيهم على الرجم بالغيب والظنِّ الذي لا يُغني من الحقِّ شيئاً؛ ففيها دليلٌ على المنع من استفتاء مَنْ لا يَصْلُحُ للفتوى: إما لقصوره في الأمر المستفتى فيه، أو لكونه لا يبالي بما تكلَّم به، وليس عنده ورعٌ يحجُزُه، وإذا نُهي عن استفتاءِ هذا الجنس؛ فنهيُهُ هو عن الفتوى من باب أولى وأحرى.
وفي الآية أيضاً دليلٌ على أن الشخص قد يكون منهيًّا عن استفتائه في شيء دون آخر، فيُسْتَفْتى فيما هو أهلٌ له بخلاف غيره؛ لأنَّ الله لم يَنْهَ عن استفتائهم مطلقاً، إنَّما نهى عن استفتائهم في قصَّةِ أصحاب الكهف وما أشبهها.
{22} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu kuhitalifiana kwa Watu wa Kitabu kuhusu idadi ya watu wa Pangoni, tofauti inayotokana na kubahatisha kwao ghaibu na kusema wasiyoyajua.
Na kwamba wao wana rai tatu juu yao: Miongoni mwao wapo wanaosema: "Walikuwa watatu, wa nne wao ni mbwa wao",
na miongoni mwao wapo wanaosema: "Walikuwa watano, wa sita wao ni mbwa wao." Na baada ya maneno haya mawili Mwenyezi Mungu akataja kuwa huku ni kubahatisha kwao tu ghaibu, kwa hivyo hilo likaashiria ubatili wake.
Na miongoni mwao wapo wanaosema: "Walikuwa saba na wa nane wao ni mbwa wao." Na idadi hii- na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi - ndiyo idadi sahihi. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alibatilisha zile mbili za mwanzo na hakubatilisha hii, kwa hivyo hilo likaashiria usahihi wake. Na huku ni katika kuhitilafiana ambako hakuna manufaa yoyote ndani yake, wala hakuna masilahi yoyote kwa watu ya kidini wala ya kidunia yanayopatikana katika kujua idadi yao. Na ndiyo maana Yeye Mtukufu akasema,
"Sema: Mola wangu Mlezi ndiye anayejua sawa sawa hesabu yao. Ni wachache tu wanaowajua.” Na hao ndio wale walioafikiana na usahihi, na wakajua kuwa wamepata usahihi. "Basi usibishane juu yao isipokuwa kwa mabishano ya juu juu tu hivi." Yaani bishana, tu kubishana kulikojengeka juu ya elimu na yakini, na ambako kuna manufaa. Ama kubishana kulikojengeka juu ya ujinga na kubahatisha tu ghaibu au ambako hakuna faida yoyote, ima kwa kuwa mpinzani ni mkaidi, na ima kwa kuwa suala lenyewe halina umuhimu wowote wala hakuna faida yoyote ya kidini inayopatikana kwa kulijua, kama vile idadi ya watu wa Pangoni na kadhalika. Kwa maana, kukithiri katika kuyajadili hayo na kuyafanyia utafiti wa mfululizo ni kupoteza tu muda na kuathiri kusikofaa katika mapenzi ya mioyo. "Wala usiulize habari zao yeyote yule miongoni mwao." Na hayo ni kwa sababu maneno yao juu yao yanatokana na kubahatisha tu ghaibu na kuwa na dhana ambayo haina faida yoyote mbele ya haki. Basi ndani yake kuna ushahidi wa kukataza kumuuliza uamuzi wa kidini yule asiyefaa kutoa uamuzi huo. Ima kwa sababu ya upungufu wake katika jambo hilo linalotafutiwa fatwa, au kwa sababu hajali anayoyasema, na hata hana uungwana wa kumzuia. Na ikiwa imekatazwa kuulizwa fatwa watu wa sampuli hii, basi yeye mwenyewe kukatazwa kutoa fatwa ni bora zaidi na ni jambo linalofaa zaidi. Aya hii pia ina ushahidi kwamba mtu anaweza kukatazwa kuulizwa fatwa katika jambo moja na si lingine. Kwa hivyo anaweza ulizwa fatwa kuhusu jambo ambalo anastahiki, tofauti na lingine asilostahiki. Kwa sababu Mwenyezi Mungu hakuwakataza kuwauliza kabisa kabisa, bali alikataza kuwauliza kuhusu kisa cha watu wa pangoni na mambo yanayofanana na hayo.
{وَلَا تَقُولَنَّ لِشَيْءٍ إِنِّي فَاعِلٌ ذَلِكَ غَدًا (23) إِلَّا أَنْ يَشَاءَ اللَّهُ وَاذْكُرْ رَبَّكَ إِذَا نَسِيتَ وَقُلْ عَسَى أَنْ يَهْدِيَنِ رَبِّي لِأَقْرَبَ مِنْ هَذَا رَشَدًا (24)}.
23.
Wala usiseme kamwe kwa jambo lolote lile: Hakika nitalifanya hilo kesho. 24. Isipokuwa Mwenyezi Mungu akipenda. Na mkumbuke Mola wako Mlezi pale unaposahau,
na sema: huenda Mola wangu Mlezi ataniongoa kwenye uwongozi ulio karibu zaidi kuliko huu.
#
{23} هذا النهيُ كغيرِهِ، وإنْ كان لسببٍ خاصٍّ وموجه للرسول - صلى الله عليه وسلم -؛ فإنَّ الخطاب عامٌّ للمكلَّفين؛ فنهى الله أن يقولَ العبدُ في الأمور المستقبلة: {إنِّي فاعلٌ ذلك}: من دون أن يقرِنَه بمشيئة الله، وذلك لما فيه من المحذورِ، وهو الكلامُ على الغيوب المستقبلة التي لا يَدْري هل يفعلُه أم لا؟ وهل تكون أم لا؟ وفيه ردُّ الفعل إلى مشيئة العبد استقلالاً، وذلك محذورٌ محظورٌ؛ لأنَّ المشيئة كلها لله، {وما تشاؤون إلاَّ أنْ يشاءَ اللهُ ربُّ العالمين}، ولما في ذكر مشيئة الله من تيسير الأمر وتسهيلِهِ وحصول البركةِ فيه والاستعانةِ من العبد لربِّه.
{23} Katazo hili ni kama mengineyo. Hata ingawa ni kwa sababu maalumu iliyoelekezwa kwa Mtume -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - mazungumzo haya ni ya jumla kwa watu wote wanaojukumishwa na sheria ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akakataza mja kusema kuhusu mambo yajayo, "Hakika nitalifanya hilo" bila ya kulifungamanisha na mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Na hilo ni kwa sababu ya katazo lililo katika hilo ambalo kuzungumza juu ya mambo ya baadaye yasiyoonekana ambayo hajui kama atayafanya au la? Na je, yatakuwa au la? Na ndani yake kuna kurudisha kutenda kwa kitendo kwa mja mwenyewe kivyake, jambo ambalo linatahadhariwa na limekatazwa. Kwa sababu mapenzi yote ni ya Mwenyezi Mungu, "Wala nyinyi hamtataka isipokuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote." Na katika kutaja mapenzi ya Mwenyezi Mungu kuna kufanya jambo kuwa jepesi, na kulirahisha, na kupata baraka ndani yake, na kutaka msaada kwa mja kutoka kwa Mola wake Mlezi.
#
{24} ولما كان العبد بشراً لا بدَّ أن يسهو عن ذكر المشيئة ؛ أمَرَه الله أن يستثني بعد ذلك إذا ذَكَرَ؛ ليحصُلَ المطلوب ويندفِعَ المحذورُ. ويؤخَذُ من عموم قوله: {واذكُرْ رَبَّك إذا نسيتَ}: الأمرُ بذِكْر الله عند النسيان؛ فإنَّه يزيله ويذكِّر العبدَ ما سها عنه. وكذلك يؤمَرُ الساهي الناسي لذِكْرِ الله أن يَذْكُرَ ربَّه ولا يكوننَّ من الغافلين. ولما كان العبدُ مفتقراً إلى الله في توفيقه للإصابة وعدم الخطأ في أقواله وأفعاله؛ أمره الله أن يقول: {عسى أن يَهْدِيَني ربِّي لأقربَ من هذا رَشَداً}: فأمره أن يدعو الله ويرجوه ويَثِقَ به أنْ يَهْدِيَه لأقرب الطرق الموصلة إلى الرشد، وحريٌّ بعبد تكون هذه حاله، ثم يبذل جهده، ويستفرغُ وسعه في طلب الهدى والرشد، أن يُوَفَّق لذلك، وأن تأتِيَه المعونةُ من ربِّه، وأن يسدِّدَه في جميع أموره.
{24} Na kwa vile mja ni mtu, na hana budi kusahau kutaja mapenzi ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu akamuamuru kulitaja anapokumbuka baada ya hilo, ili kinachotarajiwa kipatikane na kilichotahadhariwa kiondoke. Na imechukuliwa katika ujumla wa kauli yake, "Na mkumbuke Mola wako Mlezi pale unaposahau" amri ya kumdhukuru Mwenyezi Mungu unaposahau. Kwa maana, hilo humkumbusha mja yale aliyoyasahau. Vilevile yule aliyesahau kumkumbuka Mwenyezi Mungu ameamrishwa amdhukuru Mola wake Mlezi wala kamwe asiwe miongoni mwa walioghafilika. Na kwa vile mja humhitajia zaidi Mwenyezi Mungu ili awezeshwe kufikia usawa na asikosee katika maneno yake na vitendo vyake, Mwenyezi Mungu alimuamuru aseme,
“Huenda Mola wangu Mlezi ataniongoa kwenye uwongozi ulio karibu zaidi kuliko huu.” Basi akamuamuru kuomwomba Mwenyezi Mungu, na amtarajie, na awe na imani naye kwamba atamwongoa kwenye njia iliyo karibu zaidi ifikishayo kwenye uwongofu. Basi inamfailia zaidi mja ambaye hii ndiyo hali yake, kisha akafanya juhudi, na akafanya awezavyo katika kutafuta uwongofu na usawa, kwamba huwezeshwa kuyafikia hayo, na hujiwa na msaada kutoka kwa Mola wake Mlezi, na kwamba Mola wake Mlezi humuweka sawasawa katika mambo yake yote.
{وَلَبِثُوا فِي كَهْفِهِمْ ثَلَاثَ مِائَةٍ سِنِينَ وَازْدَادُوا تِسْعًا (25) قُلِ اللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا لَبِثُوا لَهُ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَبْصِرْ بِهِ وَأَسْمِعْ مَا لَهُمْ مِنْ دُونِهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا يُشْرِكُ فِي حُكْمِهِ أَحَدًا (26)}.
25. Na walikaa katika pango lao hilo miaka mia tatu, na wakazidisha tisa. 26.
Sema: Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi muda waliokaa. Ni zake tu siri za mbingu na ardhi. Kuona vyema kulikoje kwake na kusikia kuzuri kulikoje! Hawana mlinzi yeyote isipokuwa Yeye, wala hamshirikishi yeyote katika hukumu yake.
#
{25 - 26} لمَّا نهاه الله عن استفتاء أهل الكتاب في شأن أهل الكهف لعدم علمهم بذلك، وكان الله عالم الغيب والشهادة العالم بكلِّ شيء؛ أخبره الله بمدَّة لَبثهم، وأنَّ علم ذلك عنده وحدَه؛ فإنَّه من غيب السماواتِ والأرض، وغيبُها مختصٌّ به؛ فما أخبر به عنها على ألسنةِ رُسُلِهِ؛ فهو الحقُّ اليقين الذي لا يُشَكُّ فيه، وما لا يُطْلِعُ رسلَه عليه؛ فإنَّ أحداً من الخلق لا يعلمه. وقوله: {أبصِرْ به وأسمعْ}: تعجُّبٌ من كمال سمعه وبصره وإحاطتهما بالمسموعات والمبصَرات بعدما أخبر بإحاطة علمِهِ بالمعلومات، ثم أخبر عن انفراده بالولاية العامَّة والخاصَّة؛ فهو الوليُّ الذي يتولَّى تدبير جميع الكون، والوليُّ لعباده المؤمنين؛ يخرِجُهم من الظُّلمات إلى النور، وييسِّرهم لليسرى، ويجنِّبهم العسرى، ولهذا قال: {ما لهم من دونِهِ من وليٍّ}؛ أي: هو الذي تولَّى أصحاب الكهف بلطفِهِ وكرمِهِ، ولم يَكِلْهم إلى أحدٍ من الخلق. {ولا يُشْرِكُ في حكمِهِ أحداً}: وهذا يشمَلُ الحكمَ الكونيَّ القدريَّ والحكم الشرعيَّ الدينيَّ؛ فإنَّه الحاكم في خلقه قضاءً وقدراً وخلقاً وتدبيراً، والحاكم فيهم بأمرِهِ ونهيِهِ وثوابِهِ وعقابِهِ.
ولما أخبر أنه تعالى له غيب السماواتِ والأرض؛ فليس لمخلوقٍ إليها طرها طريقٌ إلاَّ عن الطريق التي يُخبر بها عبادَه، وكان هذا القرآن قد اشتمل على كثيرٍ من الغُيوب؛ أمر تعالى بالإقبال عليه، فقال:
{25 - 26} Pale Mwenyezi Mungu alipomkataza kuuliza fatwa Watu wa Kitabu juu ya watu wale wa Pangoni kwa sababu hawana elimu yoyote kuhusu hilo, na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi siri na dhahiri, Mwenye kujua kila kitu. Mwenyezi Mungu akamjulisha kuhusu muda waliokaa, na kwamba Yeye peke yake ndiye aliyejua hilo. Kwani hilo ni katika ghaibu ya mbingu na ardhi, na ghaibu yake hiyo ni mahsusi kwake tu. Kwa hivyo, yale aliyojulisha juu yake kupitia ndimi za Mitume wake, basi hayo ndiyo haki ya yakini ambayo haishukiwi. Na yale ambayo hakuwajulisha Mitume wake, basi hakuna yeyote miongoni mwa viumbe anayeyajua. Na kauli yake, "Kuona vyema kulikoje kwake na kusikia kuzuri kulikoje!" Ni mshangao juu ya ukamilifu wa kusikia kwake na kuona kwake, na kuzungukwa kwake yote yanayosikika na yanayoonekana, baada ya kujulisha juu ya kuzungukwa kwa elimu yake mambo yote. Kisha akajulisha kuhusu upekee wake katika ulinzi wa kiujumla na wa mahususi. Basi Yeye ndiye mlinzi ambaye anasimamia uendeshaji wa ulimwengu wote, na ni mlinzi wa waja wake waumini. Anawatoa katika giza mbalimbali hadi katika nuru, na anawasahilishia yawe mepesi, na anawaepusha ugumu. Na ndiyo maana akasema, “Hawana mlinzi yeyote isipokuwa Yeye." Yaani, Yeye ndiye aliyewasimamia wale watu wa pangoni kwa upole wake na ukarimu wake, na wala hakuwakabidhi kwa yeyote katika viumbe. "wala hamshirikishi yeyote katika hukumu yake." Na hii linajumusisha hukumu ya kimajaliwa na hukumu ya kisheria ya kidini. Yeye ndiye anayehukumu katika viumbe wake kwa kutoa hukumu juu ya hatima yao, kuumba na kuendesha, naye ndiye anayewahukumu kwa amri yake, makatazo yake, thawabu zake na adhabu yake. Na alipojulisha kwamba yeye Mtukufu ndiye ana ghaibu ya mbingu na ardhi, kwa hivyo hakuna njia kwa kiumbe yeyote kuifikia isipokuwa kwa njia ile ambayo kwayo anawajulisha waja wake, na pindi Qur-ani hii ilipokuwa ina mengi ya ghaibu, Yeye Mtukufu akawaamrisha watu waikusudie Qur-ani hii,
akasema:
{وَاتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنْ كِتَابِ رَبِّكَ لَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ وَلَنْ تَجِدَ مِنْ دُونِهِ مُلْتَحَدًا (27)}.
27. Na soma yale uliyofunuliwa katika Kitabu cha Mola wako Mlezi. Hakuna yeyote awezaye kubadilisha maneno yake. Wala nawe hutapata makimbilio yoyote isipokuwa kwake.
#
{27} التلاوة: هي الاتِّباع؛ أي: اتَّبع ما أوحى الله إليك بمعرفة معانيه وفهمها وتصديق أخباره وامتثال أوامره ونواهيه؛ فإنَّه الكتاب الجليل، الذي لا مبدِّل لكلماته؛ أي: لا تُغَيَّر ولا تُبَدَّل لصدقها وعدلها وبلوغها من الحسن فوق كلِّ غاية، {وَتَمَّتْ كلمةُ ربِّك صدقاً وعدلاً}؛ فلكمالها استحال عليها التغييرُ والتبديل، فلو كانت ناقصةً؛ لَعَرَضَ لها ذلك أو شيءٌ منه. وفي هذا تعظيم للقرآن في ضمنه الترغيبُ على الإقبال عليه. {وَلَن تَجِدَ من دونه مُلْتَحَداً}؛ أي: لن تجد من دون ربِّك ملجأ تلجأ إليه ولا مَعاذًا تعوذ به؛ فإذا تعيَّن أنَّه وحده الملجأ في كلِّ الأمور؛ تعيَّن أن يكون هو المألوه المرغوب إليه في السرَّاء والضرَّاء، المفتَقر إليه في جميع الأحوال، المسؤول في جميع المطالب.
{27} Na maana yake ni fuata yale aliyokufunulia wahyi Mwenyezi Mungu kwa kuzijua maana zake, kuzifahamu, kuzisadikisha habari zake, na kutekeleza amri zake na makatazo yake. Kwa maana, hicho ni Kitabu kitukufu, ambacho hakuna awezaye kuyabadilisha maneno yake. Yaani hayawezi kubadilishwa wala kugeuzwa kwa sababu ya ukweli wake, uadilifu wake, na kufikia kwake uzuri wa hali ya juu zaidi, "na neno la Mola wako Mlezi limekamilika katika ukweli na haki." Na kwa sababu ya ukamilifu wake, haiwezekani kugeuzwa na kubadilishwa. Na lau yangekuwa mapungufu, basi huenda yangetokea hayo au kitu kama hayo. Na hakika hilo kuna kuitukuza Qur-ani, ikiwa ni pamoja na kutia moyo kwa kuikumbatia. "Wala nawe hutapata makimbilio yoyote isipokuwa kwake." Na ikishadhihirika kuwa yeye peke yake ndiye kimbilio katika mambo yote, basi inapasa kuwa Yeye pekee ndiye anayepasa kufanyiwa uungu, anayetafutwa katika nyakati nzuri na nyakati mbaya, anayehitajika katika hali zote, na anayeombwa katika kila ombi.
{وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ عَنْهُمْ تُرِيدُ زِينَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُ عَنْ ذِكْرِنَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ وَكَانَ أَمْرُهُ فُرُطًا (28)}.
28. Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni, hali ya kuwa wanataka uso wake. Wala macho yako yasiwaruke kwa kutaka pambo la uhai wa dunia. Wala usimtii tuliyemghafilisha moyo wake asitukumbuke, na akafuata matamanio yake, na mambo yake yakawa ni kupita mpaka tu.
#
{28} يأمر تعالى نبيَّه محمداً - صلى الله عليه وسلم -، وغيره أسوته في الأوامر والنواهي أن يصبر نفسه مع المؤمنين العُبَّاد المنيبين. {الذين يَدْعونَ ربَّهم بالغداة والعشيِّ}؛ أي: أول النهار وآخره؛ يريدون بذلك وجه الله، فوصفهم بالعبادة والإخلاص فيها؛ ففيها الأمر بصحبة الأخيار ومجاهدة النفس على صحبتهم ومخالطتهم، وإنْ كانوا فقراء؛ فإنَّ في صحبتهم من الفوائد ما لا يُحصى. {ولا تَعْدُ عيناك عنهم}؛ أي: لا تجاوزهم بصرك وترفع عنهم نظرك؛ {تريد زينةَ الحياةِ الدُّنيا}؛ فإنَّ هذا ضارٌّ غير نافع، قاطعٌ عن المصالح الدينيَّة؛ فإنَّ ذلك يوجب تعلُّق القلب بالدُّنيا، فتصير الأفكار والهواجس فيها، وتزول من القلب الرغبةُ في الآخرة؛ فإنَّ زينة الدُّنيا تروق للناظر وتَسْحَر القلب ، فيغفل القلب عن ذكر الله، ويُقْبِلُ على اللَّذَّات والشهوات، فيضيع وقته، وينفرط أمره، فيخسر الخسارة الأبديَّة والندامة السرمديَّة، ولهذا قال: {ولا تُطِعْ من أغْفَلْنا قلبه عن ذكرنا}: غَفَلَ عن الله فعاقبه بأن أغْفَلَه عن ذكره، {واتَّبَع هواه}؛ أي: صار تبعاً لهواه؛ حيث ما اشتهتْ نفسُه فعله، وسعى في إدراكه، ولو كان فيه هلاكه وخُسرانه؛ فهو قد اتَّخذ إلهه هواه؛ كما قال تعالى: {أفرأيتَ مَنِ اتَّخذ إلهه هواه وأضلَّه الله على علم ... } الآية. {وكان أمرُهُ}؛ أي: مصالح دينه ودنياه {فُرُطاً}؛ أي: ضائعة معطَّلة؛ فهذا قد نهى الله عن طاعته؛ لأن طاعته تدعو إلى الاقتداء به، ولأنَّه لا يدعو إلاَّ لما هو متَّصف به.
ودلَّت الآية على أنَّ الذي ينبغي أن يُطاع، ويكون إماماً للناس مَن امتلأ قلبُه بمحبَّة الله، وفاض ذلك على لسانه، فلهج بذكر الله، واتَّبع مراضي ربِّه، فقدَّمها على هواه، فحفظ بذلك ما حَفِظَ من وقته، وصلحت أحوالُه، واستقامت أفعاله، ودعا الناس إلى ما منَّ الله به عليه؛ فحقيقٌ بذلك أن يُتَّبع، ويُجعل إماماً.
والصبر المذكور في هذه الآية هو الصبر على طاعة الله، الذي هو أعلى أنواع الصبر، وبتمامه يتمُّ باقي الأقسام.
وفي الآية استحبابُ الذِّكر والدُّعاء والعبادة طرفي النهار؛ لأنَّ الله مدحهم بفعله، وكلُّ فعل مَدَحَ الله فاعله؛ دلَّ ذلك على أن الله يحبُّه؛ وإذا كان يحبه فإنَّه يأمر به ويرغِّب فيه.
{28} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwamrisha Mtume wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - na wengineo wana kiigizo bora kwake katika maamrisho na makatazo kwamba awe na subira pamoja na waumini, waja wanarudi kwa Mwenyezi Mungu. "Na wanaomuomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni." Yaani, mwanzo wa mchana na mwisho. Kwa kufanya hivyo, wanatafuta uso wa Mwenyezi Mungu, kwa hivyo akawasifia kwa ibada na kumkusudia Mwenyezi Mungu tu ndani yake. Basi ndani ya hili kuna amri ya kuwafanyia usuhuba na watu wema na kujitahidi kuwa pamoja nao na kuchanganyika nao, hata kama ni maskini. Kwa maana kuna manufaa mengi yasiyohesabika katika kufuatana nao. "Wala macho yako yasiwaruke." Yaani, usiwaondolee jicho lako ukaacha kuwatazama, "kwa kutaka pambo la uhai wa dunia." Hili linadhuru na si la manufaa, na linataka mtu kutoka katika masilahi ya kidini. Na hilo linalazimu moyo kufungamana na dunia hii, kwa hivyo mawazo na matamanio huwa hapo tu, na hamu ya akhera hupotea kutoka moyoni. Kwa maana, mapambo ya dunia yanamfurahisha mwenye kuyatazama na kuutia uchawi moyo, hivyo moyo unaghafilika na kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kugeukia anasa na matamanio, kwa hivyo anapoteza muda wake na kutofanya vyema amri yake, hivyo anapata hasara ya milele na majuto ya milele. Ndiyo maana akasema, "Wala usimtii tuliyemghafilisha moyo wake asitukumbuke." Alimsahau Mwenyezi Mungu, naye akamuadhibu kwa kughafilisha na kumkumbuka. "Na akafuata matamanio yake." Yaani, akawa mwenye kufuata matamanio yake. Ambapo nafsi yake inapotamani kitu, yeye anakifanya, na anajitahidi kukifikia, hata kama ndani yake kuna maangamivu kwake na hasara kwake. Kwa maana, yeye alikwisha yafanya matamanio yake kuwa ndiyo mungu wake. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema, "Je, umemwona aliyefanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akamwacha apotee pamoja na kuwa ana elimu..." hadi mwisho wa Aya. "Na mambo yake;" yaani, masilahi ya dini yake na dunia yake, "yakawa ni kupita mpaka tu." Basi huyu ndiye Mwenyezi Mungu amekataza kumtii, kwa sababu kumtii kunaitia kumuiga, na kwa sababu yeye halinganii isipokuwa kile ambacho anasifika kwacho. Na Aya hii iliashiria kuwa yule anayepaswa kutiiwa na kuwa imamu wa watu ni yule ambaye moyo wake umejaa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, na yakaenea hayo katika ulimi wake. Kwa hivyo akadumu katika kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na kufuata yale yanayomridhisha Mola wake Mlezi, na kuyatanguliza hayo mbele ya matamanio yake, basi akahifadhi kwa hayo yale aliyohifadhi katika wakati wake, na hali zake zikatengenea, na vitendo vyake vikanyooka, na anawalingania watu kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu aliyomneemesha nayo. Basi huyu anastahili zaidi kufuatwa na kufanywa imamu. Na subira iliyotajwa katika aya hii ni kuwa na subira katika kumtii Mwenyezi Mungu, ambayo ndiyo aina ya juu zaidi ya subira, na kwa kukamilika kwake, aina nyinginezo zilizobakia hutimia. Na katika Aya hii kuna pendekezo la kumtaja Mwenyezi Mungu na kumuomba dua, na kufanya ibada katika ncha mbili za mchana. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwasifu kwa kufanya hivyo. Na kila kitendo ambacho Mwenyezi Mungu alimsifu mtendaji wake, hili lilionyesha kwamba Mwenyezi Mungu anakipenda. Na ikiwa anakipenda, basi anakiamuru na kutia moyo katika kukifanya.
{وَقُلِ الْحَقُّ مِنْ رَبِّكُمْ فَمَنْ شَاءَ فَلْيُؤْمِنْ وَمَنْ شَاءَ فَلْيَكْفُرْ إِنَّا أَعْتَدْنَا لِلظَّالِمِينَ نَارًا أَحَاطَ بِهِمْ سُرَادِقُهَا وَإِنْ يَسْتَغِيثُوا يُغَاثُوا بِمَاءٍ كَالْمُهْلِ يَشْوِي الْوُجُوهَ بِئْسَ الشَّرَابُ وَسَاءَتْ مُرْتَفَقًا (29) إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ مَنْ أَحْسَنَ عَمَلًا (30) أُولَئِكَ لَهُمْ جَنَّاتُ عَدْنٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِنْ ذَهَبٍ وَيَلْبَسُونَ ثِيَابًا خُضْرًا مِنْ سُنْدُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُتَّكِئِينَ فِيهَا عَلَى الْأَرَائِكِ نِعْمَ الثَّوَابُ وَحَسُنَتْ مُرْتَفَقًا (31)}.
29.
Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae. Hakika Sisi tumewaandalia wenye kudhulumu Moto ambao utawazunguka kama hema. Na wakiomba msaada, watasaidiwa kwa kupewa maji kama mafuta yaliyotibuka. Yatakayowababua nyuso zao. Ni kinywaji kiovu mno kilioje hicho! Ni matandiko mabaya mno ya kupumzikia yaliyoje hayo! 30. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, hakika Sisi hatupotezi ujira wa anayetenda mazuri. 31. Hao watapata Bustani za milele, zinazopita mito kwa chini yao. Humo watapambwa kwa mavazi ya mikononi ya dhahabu, na watavaa nguo za kijani za hariri na atilasi, huku wakiegemea humo juu ya makochi. Hayo ndiyo malipo bora zaidi! Na ndiyo matandiko mazuri mno ya kupumzikia!
#
{29} أي: {قل} للناس يا محمدُ: هو {الحقُّ من ربِّكم}؛ أي: قد تبيَّن الهدى من الضلال، والرُّشد من الغيِّ، وصفات أهل السعادة وصفات أهل الشقاوة، وذلك بما بيَّنه الله على لسان رسوله؛ فإذا بان واتَّضح ولم يبقَ فيه شبهةٌ؛ {فمن شاء فليؤمن ومن شاء فليكفر}؛ أي: لم يبق إلاَّ سلوكُ أحد الطريقين بحسب توفيق العبد وعدم توفيقه، وقد أعطاه الله مشيئةً بها يقدِرُ على الإيمان والكفر والخير والشرِّ؛ فمن آمن؛ فقد وُفِّق للصواب، ومن كَفَرَ؛ فقد قامت عليه الحجَّة، وليس بمكرهٍ على الإيمان؛ كما قال تعالى: {لا إكْراهَ في الدِّينِ قد تَبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الغَيِّ}، [وليس في قوله: {فمن شاء فليؤمن ومن شاء فليكفر} الإذن في كلا الأمرين وإنما ذلك تهديد ووعيد لمن اختار الكفر بعد البيان التام كما ليس فيها تركه قتال الكافرين]. ثم ذكر تعالى مآل الفريقين، فقال: {إنَّا أعْتَدْنا للظالمين}: بالكفر والفسوق والعصيان، {ناراً أحاطَ بهم سُرادِقُها}؛ أي: سورها المحيط بها؛ فليس لهم منفذٌ ولا طريقٌ ولا مخلصٌ منها، تصلاهم النار الحامية. {وإن يَسْتغيثوا}؛ أي: يطلبوا الشراب ليطفئ ما نزل بهم من العطش الشديد؛ {يُغاثوا بماءٍ كالمهل}؛ أي: كالرصاص المذاب أو كعكر الزيت من شدَّة حرارته. {يَشْوي الوجوهَ}؛ أي: فكيف بالأمعاء والبطون؟! كما قال تعالى: {يُصْهَرُ به ما في بطونِهِم والجلودُ. ولهم مَقامِعُ من حديدٍ}. {بئس الشرابُ}: الذي يُراد ليطفئ العطش ويدفع بعض العذابِ فيكون زيادةً في عذابهم وشدَّة عقابهم، {وساءت}: النار {مرتفقاً}: وهذا ذمٌّ لحالة النار؛ أنَّها ساءت المحلَّ الذي يرتفق به؛ فإنَّها ليس فيها ارتفاقٌ؛ وإنَّما فيها العذاب العظيم الشاقُّ الذي لا يُفَتَّر عنهم ساعةً، وهم فيه مُبْلِسونَ، قد أيسوا من كلِّ خيرٍ، ونسيهم الرحيم في العذاب كما نسوه.
{29} Yaani, "Sema" uwaambie watu, ewe Muhammad, "Hii ni haki itokayo kwa Mola wenu Mlezi." Yaani, tayari uwongofu umeshabainika kutokana na upotovu, na usawa kutokana na ukengeufu, na sifa za watu wa furaha na sifa za watu wa mashaka, na hayo ni kupitia yale ambayo Mwenyezi Mungu aliyabainisha juu ya ulimi wa mtume wake. Na ikishabainika na ikawa wazi, na isibakie na shaka yoyote, "Basi anayetaka, na aamini, na anayetaka, na akufuru." Yaani, haikubakia isipokuwa kufuata moja kati ya njia mbili hizo kulingana na mja kuwezeshwa au kutowezeshwa. Na Mwenyezi Mungu alimpa utashi ambao kwa huo anaweza kuamini na kukufuru, na kufanya heri na maovu. Kwa hivyo, mwenye kuamini, basi atakuwa amewezeshwa kufikia usahihi. Na mwenye kukufuru, basi tayari imekwisha msimamia hoja, wala hawezi kulazimishwa kuamini, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema, "Hapana kulazimisha kokote katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka kutokana na upotovu."
[Na hakuna katika kauli yake, "Basi anayetaka, na aamini, na anayetaka," idhini yoyote ya kufanya mawili hayo. Lakini hilo ni tishio na onyo kali kwa anayechagua ukafiri baada ya ubainisho kamili, kama vile hakuna katika hilo kuacha kwake kupigana na makafiri]. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja mwisho wa makundi hayo mawili, akasema,
“Hakika Sisi tumewaandalia wenye kudhulumu” kwa kukufuru, kuvuka mipaka, na kuasi.
“Moto ambao utawazunguka kama hema” na hawana sehemu ya kutokea wala njia, wala kuokoka na hayo. Watachomwa na moto mkali. "Na wakiomba msaada;" yaani, wanapoomba kinywaji ili kutuliza kiu kikali kilichowapata, "watasaidiwa kwa kupewa maji kama mafuta yaliyotibuka." Kwa sababu ya joto lake kali, "yatakayowabambua nyuso zao." Basi yatakuwa vipi matumbo na tumbo zao? Kama alivyosema Mwenyezi Mungu, "Kwa maji hayo vitayeyushwa vilivyomo matumboni mwao, na ngozi zao pia. Na wana marungu ya chuma." "Ni kinywaji kiovu mno kilioje hicho" ambacho kinakusudiwa kuzima kiu na kuwaepusha baadhi ya adhabu hiyo! Basi itakuwa ni ongezeko la adhabu yao na ukali wa adhabu yao. "Na matandiko mabaya mno ya kupumzikia yaliyoje hayo!" Na huku ni kushutumu hali ya Moto huo. Kwamba ndipo mahali pabaya zaidi pa kupumzikia. Kwa maana, hapo hakuna kupumzika kokote, bali humo kuna adhabu kubwa na ngumu hawapumzishwi kutokana nayo hata kwa saa moja, nao humo watakata tamaa ya heri yoyote, na Mwingi wa rehema atawasahau katika adhabu hiyo kama walivyomsahau.
#
{30} ثم ذكر الفريق الثاني، فقال: {إنَّ الذين آمنوا وعملوا الصالحاتِ}؛ أي: جمعوا بين الإيمان بالله وملائكته وكتبه ورسله واليوم الآخر والقَدَر خيره وشرِّه وعمل الصالحات من الواجبات والمستحبات. {إنَّا لا نُضيعُ أجْرَ مَنْ أحسنَ عملاً}: وإحسانُ العمل أن يريدَ العبدُ العمل لوجه الله متبعاً في ذلك شرع الله؛ فهذا العمل لا يضيِّعه الله ولا شيئاً منه، بل يحفظُه للعاملين، ويوفِّيهم من الأجر بحسب عملهم وفضله وإحسانه.
{30} Kisha akalitaja kundi la pili, akasema, "Hakika wale walioamini na wakatenda mema." Yaani, wale waliojumuisha kati ya kumuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, na majaaliwa ya Mwenyezi Mungu, ya heri yake na ya shari yake, na kutenda mema miongoni mwa mambo ya wajibu na yale yanayopendekezwa. "Hakika Sisi hatupotezi ujira wa anayetenda mazuri." Na kufanya uzuri katika matendo ni kuyafanya matendo hayo kwa kutaka uso wa Mwenyezi Mungu na kufuata sheria ya Mwenyezi Mungu katika hayo. Basi matendo haya ndiyo ambayo Mwenyezi Mungu hayapotezi wala hata chochote katika hayo. Bali huyahifadhi kwa ajili ya walioyatenda, na huwaweza kupata malipo kulingana na matendo yao, na fadhila yake na ukarimu wake.
#
{31} وذكر أجرهم بقوله: {أولئك لهم جناتُ عَدْنٍ تجري من تحتها الأنهار يُحَلَّوْن فيها من أساورَ من ذهبٍ ويلبسون ثياباً خضراً من سُنْدُسٍ وإسْتَبْرَقٍ متَّكئين فيها على الأرائك}؛ [أولئك] أي: أولئك الموصوفون بالإيمان والعمل الصالح، لهم الجناتُ العالياتُ التي قد كَثُرَتْ أشجارُها فأجَنَّتْ مَنْ فيها، وكثرت أنهارُها، فصارت تجري من تحت تلك الأشجار الأنيقة والمنازل الرفيعة، وحليتُهم فيها الذهب، ولباسُهم فيها الحرير الأخضر من السُّندس، وهو الغليظُ من الدِّيباج، والإستبرق وهو ما رَقَّ منه، متَّكئين فيها على الأرائك، وهي السرر المزيَّنة المجمَّلة بالثياب الفاخرة؛ فإنَّها لا تسمَّى أريكة حتى تكون كذلك، وفي اتِّكائهم على الأرائك ما يدلُّ على كمال الراحة وزوال النَّصب والتعب وكون الخدم يسعَوْن عليهم بما يشتهون، وتمام ذلك الخلود الدائم والإقامة الأبديَّة؛ فهذه الدار الجليلة، {نعم الثوابُ}: للعاملين، {وحَسُنَتْ مرتَفَقاً}: يرتَفِقون بها، ويتمتَّعون بما فيها مما تشتهيه الأنفسُ، وتلذُّ الأعينُ من الحبرة والسرور والفرح الدائم واللَّذَّات المتواترة والنعم المتوافرة، وأيُّ مرتَفَقٍ أحسنُ من دارٍ، أدنى أهلها يسير في مُلكِهِ ونعيمه وقصورِهِ وبساتينه ألفي سنة؟ ولا يرى فوقَ ما هو فيه من النعيم، قد أعْطِيَ جميعَ أمانيه ومطالبِهِ، وزيد من المطالب ما قَصَّرَتْ عنه الأماني، ومع ذلك؛ فنعيمُهم على الدوام، متزايدٌ في أوصافه وحسنه، فنسأل الله الكريم أنْ لا يحرِمَنا خيرَ ما عنده من الإحسان بشرِّ ما عندنا من التقصير والعصيان. ودلت الآية الكريمة وما أشبهها على أن الحِلْيَةَ عامَّةٌ للذكور والإناث؛ كما ورد في الأخبار الصحيحة؛ لأنَّه أطلقها في قوله: {يُحَلَّوْنَ}، وكذلك الحرير ونحوه.
{31} Na akataja malipo yao kwa kauli yake, "Hao watapata Bustani za milele, zinazopita mito kwa chini yao. Humo watapambwa kwa mavazi ya mikononi ya dhahabu, na watavaa nguo za kijani za hariri na atilasi, huku wakiegemea humo juu ya makochi."
[Hao] yaani, wale waliosifiwa kwa Imani na matendo mema, wana bustani za juu ambazo miti yake ni mingi, kwa hivyo ikawasitiri waliomo humo, na mito yake ikawa mingi, kwa hivyo ikawa inapita kwa chini yake miti hiyo ya maridadi, na majumba ya kifahari. Na mapambo yao humo ni dhahabu, na mavazi yao humo ni hariri ya kijani kibichi kutoka kwa hariri nzito. Watakuwa wameegemea humo juu ya makochi. Navyo ni vitanda vilivyopambwa na kurembeshwa kwa nguo za kifahari. Na kuegemea kwao kwenye makochi hayo kunaonyesha kupumzika kwao kamili, na kutokuwa kwao na uchovu na tabu, na pia kuhudumiwa kwao na watumishi kwa chochote wanachotamani, na utimilifu wa hayo yote ni kudumu na kukaa humo milele. Na nyumba hii tukufu ndiyo, "malipo bora zaidi!" kwa watendao matendo. "Na ndiyo matandiko mazuri mno ya kupumzikia." Watapumzikia hapo na kujistarehesha kwa yaliyomo ndani yake miongoni mwa yale yanayotamaniwa na nafsi, na kupendeza macho miongoni mwa furaha na raha ya daima, na matamu ya mara kwa mara, na neema na baraka nyingi. Na ni mapumzikio gani ambapo ni pazuri zaidi kuliko nyumba ambayo wa chini zaidi kati ya wakazi wake anatembea katika ufalme wake, na neema zake, na makasri yake, na bustani zake kwa muda wa miaka elfu mbili? Naye haoni kwamba kuna neema yoyote zaidi ya ile aliyo ndani yake. Amepewa matamanio yake na matakwa yake yote, na hata akazidishiwa katika matakwa yake yale ambayo matamanio yake hayakuweza kuyafikia. Na licha ya hayo, furaha yao hiyo ni ya kudumu na kuzidi katika sifa zake na uzuri wake. Basi tunamuomba Mwenyezi Mungu Mkarimu asitunyime heri aliyo nayo kwa sababu ya uovu tulio nao unaotokana na kutotekeleza kwetu mambo vyema na uasi wake. Na Aya hii tukufu na Aya zinazofanana nayo ziliashiria kuwa mapambo hayo yanawajumuisha wanaume na wanawake, kama ilivyokuja katika riwaya zilizo sahihi, kwa sababu aliliwacha katika hali ya ujumla katika kauli yake, "watapambwa", na kadhalika hariri na mengineyo.
{وَاضْرِبْ لَهُمْ مَثَلًا رَجُلَيْنِ جَعَلْنَا لِأَحَدِهِمَا جَنَّتَيْنِ مِنْ أَعْنَابٍ وَحَفَفْنَاهُمَا بِنَخْلٍ وَجَعَلْنَا بَيْنَهُمَا زَرْعًا (32) كِلْتَا الْجَنَّتَيْنِ آتَتْ أُكُلَهَا وَلَمْ تَظْلِمْ مِنْهُ شَيْئًا وَفَجَّرْنَا خِلَالَهُمَا نَهَرًا (33) وَكَانَ لَهُ ثَمَرٌ}.
32.
Na wapigie mfano wa wanaume wawili: mmoja wao tulimpa vitalu viwili vya mizabibu, na tukavizungushia mitende, na kati yake tukatia mimea ya nafaka. 33. Na hivyo vitalu viwili vikatoa mazao yake, wala hapana kitu katika hayo kilichotindikia. Na ndani yake tukapasua mito.
#
{32} يقول تعالى لنبيه - صلى الله عليه وسلم -: اضرِبْ للناس مَثَلَ هذين الرجلين: الشاكر لنعمة الله، والكافر لها، وما صدر من كلٍّ منهما من الأقوال والأفعال، وما حصل بسبب ذلك من العقاب العاجل والآجل والثواب؛ ليعتبروا بحالهما، ويتَّعظوا بما حصل عليهما، وليس معرفة أعيان الرجلين وفي أيِّ زمان أو مكانٍ هما فيه فائدة أو نتيجة؛ فالنتيجة تحصُلُ من قصتهما فقط، والتعرُّض لما سوى ذلك من التكلُّف. فأحدُ هذين الرجلين الكافر لنعمة الله الجليلة جعل الله له جنتين؛ أي: بستانَيْنِ حسنَيْنِ {من أعناب وحفَفْناهما بنخل}؛ أي: في هاتين الجنتين من كل الثمرات، وخصوصاً أشرف الأشجار العنب والنخل؛ فالعنب وسطها، والنخل قد حفَّ بذلك ودار به، فحصل فيه من حسن المنظر وبهائه وبروز الشجر والنخل للشمس والرياح التي تكمُلُ بها الثمار وتنضج وتتجوهر، ومع ذلك جعل بين تلك الأشجار زَرْعاً.
{32} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake-
rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: -
Wapigie watu mfano wa wanaume hawa wawili: mwenye kushukuru neema ya Mwenyezi Mungu, na mwenye kuikufuru, na maneno na matendo ambayo kila mmoja wao alifanya, na adhabu na thawabu za haraka na za baadaye zilizotokea kwa sababu ya hayo, ili wazingatie kutokana na hali zao hizo, na waaidhike kutokana na yaliyowapata. Na hakuna faida yoyote wala matokeo yenye manufaa katika kujua wanaume hao wawili walikuwa ni akina nani na walikuwa katika wakati gani au mahali gani. Matokeo mazuri yanapatikana tu kutoka katika kisa chao, na kutafuta yasiyokuwa hayo, ni katika kujisumbua bure. Basi mmoja wa wanaume hawa wawili aliyekufuru neema kubwa ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu alimfanyia vitalu viwili vizuri "vya mizabibu, na tukavizungushia mitende." Nayo mizabibu ikawa iko katikati yake, kwa hivyo vikawa na sura nzuri ya kuvutia, na miti na mitende yake ikainuka juu kiwango cha kuangazwa na jua na kufikiwa na upepo, mambo ambayo kwayo matunda hukomaa na kuiva. Licha ya hayo, aliweka mazao kati ya miti hiyo.
#
{33} فلم يبق عليهما إلا أن يقالَ: كيف ثمارُ هاتين الجنتين؟ وهل لهما ماءٌ يكفيهما؟ فأخبر تعالى أنَّ كلًّا من {الجنتين آتت أكُلَها}؛ أي: ثمرها وزرعها ضعفين؛ أي: متضاعفاً، وأنها {لم تظلم منه شيئاً}؛ أي: لم تنقص من أُكُلِها أدنى شيء، ومع ذلك فالأنهار في جوانبها سارحة كثيرة غزيرة.
{33} Basi hakukubakia juu ya hayo mawili ila kusemwa: Yakoje matunda ya bustani hizi mbili? Je, yana maji ya kutosha? Kwa hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kwamba "Na kila moja ya vitalu viwili hivyo ikatoa mazao yake." Yaani, matunda yake na mazao yake kwa wingi, "wala hapana kitu katika hayo kilichotindikia." Yaani, haikupungua hata kidogo katika mazao yake, pamoja na kwamba mito ilikuwa pembezoni mwake ikikwenda kwa maji mengi.
#
{34} {وكان له}؛ أي: لذلك الرجل {ثمرٌ}؛ أي: عظيم؛ كما يفيده التنكير؛ أي: قد استكملت جنتاه ثمارهما، وارجحنَّت أشجارهما ولم تعرض لهما آفةٌ أو نقصٌ، فهذا غاية منتهى زينة الدُّنيا في الحرث، ولهذا اغترَّ هذا الرجل وتبجَّح وافتخر، ونسي آخرته.
{34} "Naye alikuwa na;" yaani, mwanamume huyo "matunda" mengi, na bustani zake zilikuwa zimekamilika matunda yake, na miti yake ilikuwa na nguvu, na wala hivyo vyote havikuwa vimepatwa na janga wala dosari yoyote. Basi huu ndio mwisho wa pambo la dunia hii katika kilimo, na ndiyo maana mwanamume huyu akadanganyika, akajivuna, akajifahiri, na akasahau Akhera yake.
{فَقَالَ لِصَاحِبِهِ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ أَنَا أَكْثَرُ مِنْكَ مَالًا وَأَعَزُّ نَفَرًا (34) وَدَخَلَ جَنَّتَهُ وَهُوَ ظَالِمٌ لِنَفْسِهِ قَالَ مَا أَظُنُّ أَنْ تَبِيدَ هَذِهِ أَبَدًا (35) وَمَا أَظُنُّ السَّاعَةَ قَائِمَةً وَلَئِنْ رُدِدْتُ إِلَى رَبِّي لَأَجِدَنَّ خَيْرًا مِنْهَا مُنْقَلَبًا (36)}.
34. Naye alikuwa na mazao mengi.
Basi akamwambia mwenzake naye akibishana naye: Mimi nimekushinda wewe kwa mali na nguvu za watu! 35. Na akaingia kitaluni kwake, huku anajidhulumu nafsi yake.
Akasema: Sidhani kabisa kuwa haya yatawahi haribika milele. 36. Wala sidhani kuwa hiyo Saa
(ya Qiyama) itatokea. Na ikiwa nitarudishwa kwa Mola wangu Mlezi, bila ya shaka nitapata marejeo bora zaidi kuliko haya.
#
{34} أي: فقال صاحب الجنتين لصاحبه المؤمن وهما يتحاوران؛ أي: يتراجعان بينهما في بعض الماجريات المعتادة مفتخراً عليه: {أنا أكثرُ منك مالاً وأعزُّ نفراً}: فَخَرَ بكثرة مالِهِ وعزَّةِ أنصاره من عبيدٍ وخدمٍ وأقارب، وهذا جهلٌ منه، وإلاَّ؛ فأيُّ افتخار بأمر خارجيٍّ ليس فيه فضيلةٌ نفسيَّة ولا صفةٌ معنويَّة، وإنَّما هو بمنزلة فخر الصبيِّ بالأماني التي لا حقائق تحتها؟!
{34} Yaani, yule mwenye vitalu vile viwili alimwambia mwenzake Muumini walipokuwa wanabishana, katika baadhi ya mambo ya kawaida akijifakhirisha juu yake, "Mimi nimekushinda wewe kwa mali na nguvu za watu" miongoni mwa watumwa, watumishi na jamaa zake. Na huu ni ujinga kwa upande wake. Vinginevyo, ni fahari gani iliyopo katika jambo la nje ambalo halina fadhila ya kibinafsi wala sifa isiyokuwa ya kihisia. Bali ni kama kujifahiri afanyako mtoto juu ya matamanio ambayo hayana uhakika wowote?
#
{35 - 36} ثم لم يكفِهِ هذا الافتخار على صاحبه، حتى حَكَمَ بجهله وظلمه، وظنَّ لما دخل جنته، {فقال ما أظنُّ أن تبيدَ}؛ أي: تنقطعَ وتضمحلَّ {هذه أبداً}: فاطمأنَّ إلى هذه الدنيا، ورضي بها، وأنكر البعث، فقال: {وما أظنُّ الساعة قائمةً ولئن رُدِدتُّ إلى ربِّي}: على ضرب المثل؛ {لأجِدَنَّ خيراً منها مُنْقَلَباً}؛ أي: ليعطيني خيراً من هاتين الجنتين! وهذا لا يخلو من أمرين: إمَّا أن يكون عالماً بحقيقة الحال، فيكون كلامُهُ هذا على وجه التهكُّم والاستهزاء، فيكون زيادةَ كفرٍ إلى كفرِهِ. وإما أن يكون هذا ظنَّه في الحقيقة، فيكون من أجهل الناس وأبخسهم حظًّا من العقل؛ فأيُّ تلازم بين عطاء الدُّنيا وعطاء الآخرة حتى يظنَّ بجهله أنَّ من أُعْطِي في الدنيا أُعْطِيَ في الآخرة؟! بل الغالب أنَّ الله تعالى يَزْوي الدُّنيا عن أوليائِهِ وأصفيائِهِ، ويوسِّعها على أعدائه، الذين ليس لهم في الآخرة نصيبٌ. والظاهر أنَّه يعلم حقيقة الحال، ولكنَّه قال هذا الكلام على وجه التهكُّم والاستهزاء؛ بدليل قوله: {وَدَخَلَ جنَّته وهو ظالمٌ لنفسِهِ}: فإثْبات أنَّ وصفه الظلم في حال دخوله الذي جرى منه من القول ما جرى، يدلُّ على تمرُّده وعناده.
{35 - 36} Kisha hakukumtosha kujifahiri kwake huku mbele ya mwenzake mpaka akahukumu kwa ujinga wake na dhuluma yake, na akafikiri alipoingia kitaluni mwake,
"Akasema: Sidhani kabisa kuwa haya yatawahi haribika milele.” Basi akawa na utulivu juu ya dunia hii na akairidhia, na akakanusha kufufuliwa, na akasema, “Wala sidhani kuwa hiyo Saa
(ya Qiyama) itatokea. Na ikiwa" kwa mfano "nitarudishwa kwa Mola wangu Mlezi, bila ya shaka nitapata marejeo bora zaidi kuliko haya." Yaani,
atanipa kilicho bora zaidi kuliko vitalu hivi viwili! Na hili halikosi kuwa na mambo mawili: Ima yeye anajua uhakika wa hali yake ya akhera, kwa hivyo yakawa maneno yake hayo ni kwa njia ya kejeli na masihara, kwa hivyo hilo likawa ni kuongeza ukafiri juu ya ukafiri wake. Au awe anadhani tu kuhusu uhakika huo, kwa hivyo akawa ni katika watu wajinga zaidi wasiokuwa na akili hata kidogo. Kwa maana, kuna uwiano gani baina ya kipawa cha duniani na kipawa cha akhera, mpaka anafikiri kwa ujinga wake kwamba anayepewa duniani atapewa akhera? Bali, uwezekano mkubwa zaidi ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu huwakunjia dunia vipenzi wake na wateule wake, na awakunjulia dunia maadui wake, ambao hawana fungu lolote katika Akhera. Na la dhahiri ni kuwa anajua uhakika wa hali hiyo, lakini akasema maneno haya kwa kejeli na masihara, kwa ushahidi wa kauli yake, "huku anajidhulumu nafsi yake" kwa maana, kuthibitisha kuwa yeye anasifika kwa sifa ya dhuluma katika kuingia kwake, kama alivyosema alichosema, inaonyesha uasi wake na ukaidi wake.
{قَالَ لَهُ صَاحِبُهُ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ أَكَفَرْتَ بِالَّذِي خَلَقَكَ مِنْ تُرَابٍ ثُمَّ مِنْ نُطْفَةٍ ثُمَّ سَوَّاكَ رَجُلًا (37) لَكِنَّا هُوَ اللَّهُ رَبِّي وَلَا أُشْرِكُ بِرَبِّي أَحَدًا (38) وَلَوْلَا إِذْ دَخَلْتَ جَنَّتَكَ قُلْتَ مَا شَاءَ اللَّهُ لَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ}.
37.
Mwenzake akamwambia kwa kubishana naye: Je, unamkufuru aliyekuumba kutokana na udongo, tena kutokana na tone la manii, kisha akakufanya mwanamume aliye sawasawa? 38. Lakini Yeye Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi. Wala simshirikishi Mola wangu Mlezi na yeyote.
#
{37} أي: قال له صاحبُهُ المؤمنُ ناصحاً له ومذكِّراً له حاله الأولى التي أوجده الله فيها في الدُّنيا {من ترابٍ ثم من نطفةٍ ثم سوَّاك رَجُلاً}؛ فهو الذي أنعم عليك بنعمة الإيجاد والإمداد، وواصَلَ عليك النعم، ونقلك من طَوْرٍ إلى طَوْرٍ، حتى سوَّاك رجلاً كامل الأعضاء والجوارح المحسوسة والمعقولة، وبذلك يسَّر لك الأسباب وهيَّأ لك ما هيَّأ من نعم الدنيا، فلم تحصُل لك الدُّنيا بحولك وقوَّتك، بل بفضل الله تعالى عليك؛ فكيف يَليقُ بك أن تكفُرَ بالله الذي خلقك من ترابٍ ثم من نطفةٍ ثم سوَّاك رجلاً، وتجهل نعمته، وتزعم أنَّه لا يبعثك، وإن بعثك أنَّه يعطيك خيراً من جنتك؟! هذا ممَّا لا ينبغي ولا يليقُ.
{37} Yaani, huyo mwenzake Muumini akamwambia, akimnasihi na kumkumbusha hali yake ya mwanzo ambayo Mwenyezi Mungu alimuumba kwayo katika dunia hii "kutokana na udongo, tena kutokana na tone la manii, kisha akakufanya mwanamume aliye sawasawa." Basi, Yeye ndiye aliyekuneemesha kwa neema ya kukufanya uwepo na riziki, na akaendelea kukuneemesha, na akakupitisha kutoka hatua moja hadi nyingine, mpaka akakufanya mwanamume aliye sawasawa, mkamilifu wa viungo vya kihisia na visivyo vya kihisia. Na kwa hayo akakurahisishia njia na kukuandalia yale aliyokuandalia miongoni mwa neema za kidunia, kwa hivyo, dunia hii haukuipata kwa uwezo wako na nguvu zako, bali kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu yako. Basi imekufailiaje kumkufuru Mwenyezi Mungu ambaye alikuumba kwa udongo, kisha kwa manii, kisha akakufanya mwanamume sawasawa, hivi unasahau na kutojua fadhila zake, na kudai kuwa hatakufufua, na ikiwa atakufufua, kwamba atakupa kilicho bora kuliko kitalu chako? Hili ni katika yale yasiyopasa wala halifai kabisa.
#
{38} ولهذا لما رأى صاحبُهُ المؤمن حاله واستمراره على كفرِهِ وطغيانه؛ قال مخبراً عن نفسه على وجه الشُّكر لربِّه والإعلان بدينِهِ عند ورود المجادلات والشُّبه: {لكنَّاْ هو الله ربِّي ولا أشرِكُ بربِّي أحداً}: فأقرَّ بربوبيَّة ربِّه وانفراده فيها والتزام طاعته وعبادته، وأنَّه لا يشرك به أحداً من المخلوقين.
{38} Na ndiyo sababu huyo sahibu yake Muumini alipoiona hali yake na kuendelea kwake kufuru na kuvuka mipaka, akasema kujihusu kwa njia ya kumshukuru Mola wake Mlezi na kuitangaza dini yake pindi kunapotokea mabishano na shaka, "Lakini Yeye Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi. Wala simshirikishi Mola wangu Mlezi na yeyote." Basi akakiri umola wa Mola wake Mlezi na upekee wake katika hilo, na kushikamana na kumtii Yeye na kumuabudu. Na kwamba yeye hamshirikishi na yeyote katika viumbe wake.
Kisha akajulisha kwamba neema za Mwenyezi Mungu juu yake miongoni mwa imani na Uislamu, hata kama yeye ana uchache wa mali na watoto, hayo ndiyo neema ya uhakika, na kwamba chochote kisichokuwa hayo vinaweza kutoweka, na kumsababishia mtu adhabu na mateso. Akasema:
{إِنْ تَرَنِ أَنَا أَقَلَّ مِنْكَ مَالًا وَوَلَدًا (39) فَعَسَى رَبِّي أَنْ يُؤْتِيَنِ خَيْرًا مِنْ جَنَّتِكَ وَيُرْسِلَ عَلَيْهَا حُسْبَانًا مِنَ السَّمَاءِ فَتُصْبِحَ صَعِيدًا زَلَقًا (40) أَوْ يُصْبِحَ مَاؤُهَا غَوْرًا فَلَنْ تَسْتَطِيعَ لَهُ طَلَبًا (41) وَأُحِيطَ بِثَمَرِهِ فَأَصْبَحَ يُقَلِّبُ كَفَّيْهِ عَلَى مَا أَنْفَقَ فِيهَا وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَى عُرُوشِهَا وَيَقُولُ يَالَيْتَنِي لَمْ أُشْرِكْ بِرَبِّي أَحَدًا (42) وَلَمْ تَكُنْ لَهُ فِئَةٌ يَنْصُرُونَهُ مِنْ دُونِ اللَّهِ وَمَا كَانَ مُنْتَصِرًا (43) هُنَالِكَ الْوَلَايَةُ لِلَّهِ الْحَقِّ هُوَ خَيْرٌ ثَوَابًا وَخَيْرٌ عُقْبًا (44)}.
39. Na lau kuwa ulipoingia kitaluni kwako,
ungelisema: Mashaallah
(alitakalo Mwenyezi Mungu huwa)! Hakuna nguvu yoyote isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Ikiwa unaniona mimi nina mali kidogo na watoto kuliko wewe. 40. Basi huenda Mola wangu Mlezi akanipa kilicho bora kuliko kitalu chako, na akakitumia balaa kutoka mbinguni kwa hivyo kikageuka kuwa ardhi tupu inayoteleza. 41. Au maji yake yakazama
[katika ardhi], basi usiweze kuyatafuta ukayapata. 42. Basi, yakateketezwa matunda yake, akabaki akipinduapindua viganja vyake, kwa vile alivyoyagharamia, huku miti yake imebwagika juu ya chanja zake.
Akawa anasema: Laiti nisingelimshirikisha Mola wangu Mlezi na yeyote! 43. Wala hakuwa na kikundi cha kumnusuru badala ya Mwenyezi Mungu, wala mwenyewe hakuweza kujinusuru. 44. Huko ulinzi ni wa Mwenyezi Mungu wa Haki tu. Yeye ndiye mbora zaidi wa malipo, na wa mwisho ulio bora zaidi.
#
{39} أي: قال للكافر صاحبُهُ المؤمنُ: أنت وإن فخرتَ عليَّ بكثرة مالك وولدك، ورأيتني {أقلَّ منك مالاً وولداً}؛ فإنَّ ما عند الله خيرٌ وأبقى، وما يُرجى من خيره وإحسانه أفضلُ من جميع الدُّنيا التي يتنافس فيها المتنافسون.
{39} Yaani,
yule sahibu yake Muumini alimwambia yule rafiki yake kafiri: Hata kama unajifakhari mbele yangu kwa sababu ya wingi wa mali yako na watoto wako, na ukaniona mimi "nina mali kidogo na watoto kuliko wewe," basi hakika yaliyo kwa Mwenyezi Mungu ndiyo bora na ya kubakia zaidi, na heri na wema unaotarajiwa kutoka kwake ni bora kuliko dunia yote ambayo wanashindana juu yake washindani.
#
{40} {فعسى ربِّي أن يُؤْتِيَني خيراً من جنَّتك ويرسلَ عليها}؛ أي: على جنَّتك التي طغيتَ بها وغَرَّتْك، {حُسباناً من السماء}؛ أي: عذاباً بمطر عظيم أو غيره. {فتصبحَ}: بسبب ذلك {صعيداً زَلَقاً}؛ أي: قد اقتلعت أشجارها، وتلفت ثمارها وغرق زرعُها، وزال نفعُها.
{40} "Basi huenda Mola wangu Mlezi akanipa kilicho bora kuliko kitalu chako, na akakitumia" kitalu chako hicho ambacho ulivuka mipaka kwa sababu yake na kikakudanganya, "balaa kutoka mbinguni." Yaani, adhabu ya mvua kubwa au mengineyo. "Kwa hivyo kikageuka kuwa" kwa sababu ya hayo ikawa "ardhi tupu inayoteleza" kwa miti yake ikang'olewa, na matunda yake yakaharibiwa, na mazao yake yakazama, na manufaa yake yakatoweka.
#
{41} {أو يصبحَ ماؤها} الذي مادتُها منه {غوراً}؛ أي: غائراً في الأرض. {فلنْ تستطيعَ له طَلَباً}؛ أي: غائراً لا يُستطاع الوصول إليه بالمعاول ولا بغيرها، وإنَّما دعا على جنته المؤمن غضباً لربِّه؛ لكونها غرَّته وأطغتْه واطمأنَّ إليها؛ لعلَّه ينيبُ، ويراجع رُشده، ويبصر في أمره.
{41} "Au maji yake" ambayo hayo yote yanataokana nayo "yakazama" katika ardhi, "basi usiweze kuyatafuta ukayapata." Si kwa kutumia jembe wala vifaa vinginevyo. Na Muumini huyo alikiapiza kitalu chake kwa sababu ya hasira kwa ajili ya Mola wake Mlezi. Kwa sababu kitalu hicho kilimdanganya na kumzidisha kuvuka mipaka na akawa na utulivu juu ya kitalu hicho, ili huenda akatubu, akarudi akawa sawasawa, na akapata ufahamu katika jambo lake hilo.
#
{42} فاستجاب الله دعاءه، {وأحيطَ بثمرِهِ}؛ أي: أصابه عذابٌ أحاط به واستهلكه فلم يبقَ منه شيءٌ، والإحاطة بالثمر يستلزمُ تَلَفَ جميع أشجارِهِ وثمارِهِ وزرعِهِ، فندم كلَّ الندامة، واشتدَّ لذلك أسفه. {فأصبحَ يقلِّبُ كفَّيْه على ما أنفق فيها}؛ أي: على كثرة نفقاته الدنيويَّة عليها، حيث اضمحلَّت وتلاشت، فلم يبق لها عوضٌ، وندم أيضاً على شِرْكِه وشرِّه، ولهذا قال: {ويقولُ يا ليتني لم أشرِكْ بربِّي أحداً}.
{42} Basi Mwenyezi Mungu akamuitikia dua yake, na "Yakateketezwa matunda yake" kwa adhabu iliyomzunguka na kumteketeza, na hakuna kitu hata kimoja chake kilichosalia katika miti yake, matunda yake, na mazao yake yote. Kwa hivyo akajuta majuto yote na akawa na huzuni mkubwa mno kwa sababu ya hilo. "Akabaki akipinduapindua viganja vyake kwa vile alivyoyagharamia." Yaani, kutokana na gharama zake kubwa za kidunia, zilipopotea na kutoweka, na wala hayakubakia malipo yoyote juu yake. Na pia akajuta juu ya ushirikina wake na uovu wake, na ndiyo maana akasema,
“Akawa anasema: Laiti nisingelimshirikisha Mola wangu Mlezi na yeyote."
#
{43} قال الله تعالى: {ولم تكُن له فئةٌ ينصُرونَه من دونِ الله وما كان منتصراً}؛ أي: لما نزل العذاب بجنَّته؛ ذهب عنه ما كان يفتخرُ به من قوله لصاحبه: {أنا أكثرُ منك مالاً وأعزُّ نفراً}، فلم يدفعوا عنه من العذاب شيئاً أشدَّ ما كان إليهم حاجةً، وما كان بنفسه منتصراً، وكيف ينتصر أو يكون له انتصارٌ على قضاء الّله وقدرِهِ الذي إذا أمضاه وقدَّره لو اجتمع أهلُ السماء والأرض على إزالة شيءٍ منه لم يقدروا؟! ولا يُستبعد من رحمة الله ولطفِهِ أنَّ صاحب هذه الجنَّة التي أحيط بها تحسَّنت حاله، ورزقه الله الإنابة إليه وراجع رشدَه، وذهب تمرُّدُه وطغيانه؛ بدليل أنَّه أظهر النَّدم على شركه بربِّه، وأنَّ الله أذهب عنه ما يُطغيه وعاقبه في الدُّنيا، وإذا أراد الله بعبدٍ خيراً عجَّل له العقوبة في الدُّنيا، وفضلُ الله لا تحيطُ به الأوهام والعقول، ولا ينكِرُه إلاَّ ظالمٌ جهولٌ.
{43} Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, "Wala hakuwa na kikundi cha kumnusuru badala ya Mwenyezi Mungu, wala mwenyewe hakuweza kujinusuru." Yaani, adhabu ilipokishukia kitalu chake, yalimwondokea na kupotea yale aliyokuwa akijifahari nayo alipokuwa anamwambia mwenziwe, "Mimi nimekushinda wewe kwa mali na nguvu za watu." Na hawakumzuilia chochote kutokana na adhabu alipokuwa inawahitaji zaidi, na hata yeye mwenyewe hakuweza kujinusuru. Na vipi atajinusuru au apate wa kumnusuru dhidi ya hukumu na majaliwa ya Mwenyezi Mungu, ambayo anapoyapitisha na kuyajaalia, hata kama wakazi wa mbinguni na ardhini watakusanyika ili kuiondoa sehemu yake yoyote, basi wasingeweza? Na si kwamba haiwezekani kwa rehema na fadhila za Mwenyezi Mungu kwamba hali ya mmiliki wa kitalu hiki kilichoteketezwa ilitengenea hali yake, na Mwenyezi Mungu akamjaalia kurejea kwake, na akairudia hali yake ya sawasawa, na ukaondoka uasi wake na kuvuka kwake mipaka. Haya ni kwa ushahidi wa kwamba alionyesha kujuta kwake juu ya kumshirikisha kwake Mola wake Mlezi, na kwamba Mwenyezi Mungu alimuondolea yale yaliyokuwa yakimfanya kuvuka mipaka na akamuadhibu katika dunia hii, na Mwenyezi Mungu anapomtakia heri mja, humharakishia adhabu hapa duniani. Na fadhila za Mwenyezi Mungu hazizungukwi na fikira na akili, na hakuna anayezikanusha isipokuwa dhalimu mjinga mno.
#
{44} {هنالك الوَلايةُ لله الحقِّ هو خيرٌ ثواباً وخيرٌ عقباً}؛ أي: في تلك الحال التي أجرى الله فيها العقوبة على من طغى وآثر الحياة الدُّنيا، والكرامة لمن آمن وعمل صالحاً وشكر الله ودعا غيره لذلك؛ تبيَّن وتوضَّح أن الولاية الحق لله وحده ؛ فمن كان مؤمناً به تقيًّا؛ كان له وليًّا، فأكرمه بأنواع الكرامات، ودَفَعَ عنه الشرور والمَثُلات ـ ومن لم يؤمنْ بربِّه ويتولاَّه؛ خَسِرَ دينه ودُنياه ـ فثوابُهُ الدنيويُّ والأخرويُّ خيرُ ثواب يُرجى ويؤمَّل.
ففي هذه القصة العظيمة اعتبارٌ بحال الذي أنعم الله عليه نعماً دنيويَّة، فألهتْه عن آخرته، وأطغتْه، وعصى الله فيها، أنَّ مآلها الانقطاع والاضمحلال، وأنَّه وإنْ تمتَّع بها قليلاً؛ فإنَّه يحرمها طويلاً، وأنَّ العبد ينبغي له إذا أعجبه شيءٌ من مالِهِ أو ولدِهِ أن يضيفَ النعمة إلى موليها ومُسْديها، وأن يقولَ: ما شاء اللهُ، لا قوَّة إلاَّ بالله؛ ليكون شاكراً [لله] متسبِّباً لبقاء نعمته عليه؛ لقوله: {ولولا إذْ دخلتَ جنَّتَك قلتَ ما شاء اللهُ لا قوَّةَ إلاَّ بالله}.
وفيها: الإرشاد إلى التسلِّي عن لذَّات الدُّنيا وشهواتها بما عند الله من الخير؛ لقوله: {إنْ تَرَنِ أنا أقلَّ منك مالاً وولَداً فعسى ربِّي أن يُؤْتِيَني خيراً من جنَّتك}.
وفيها: أنَّ المال والولد لا ينفعانِ إنْ لم يُعينا على طاعة الله؛ كما قال تعالى: {وما أموالكم ولا أولادُكم بالتي تُقَرِّبُكم عندنا زُلفى إلاَّ مَنْ آمنَ وعملَ صالحاً}.
وفيه: الدُّعاء بِتَلَفِ مال مَنْ كان مالُهُ سببَ طغيانِهِ وكفره وخسرانِهِ، خصوصاً إنْ فضَّل نفسه بسببهِ على المؤمنين، وفَخَرَ عليهم.
وفيها: أنَّ ولاية الله وعدمها إنما تتَّضح نتيجتها إذا انجلى الغبار وحقَّ الجزاء، ووجد العاملونَ أجرهم؛ فـ {هنالِكَ الوَلاية لله الحقِّ هو خيرٌ ثواباً وخيرٌ عُقْباً}؛ أي: عاقبةً ومآلاً.
{44} "Huko ulinzi ni wa Mwenyezi Mungu wa Haki tu. Yeye ndiye mbora zaidi wa malipo, na wa mwisho ulio bora zaidi." Yaani, katika hali ile ambayo Mwenyezi Mungu alimuadhibu yule aliyeasi na akapendelea uhai wa dunia hii, na akamkirimu yule aliyeamini na akatenda mema na akamshukuru Mwenyezi Mungu na akawalingia wengine kufanya hivyo, ilibainika na ikawa wazi kwamba ulinzi wa kweli ni wa Mwenyezi Mungu pekee. Kwa hivyo, Mwenye kumuamini na akawa mchamungu, basi Yeye atakuwa mlinzi wake, na atamtukuza kwa kila aina za kutukuza, na atamwondolea maovu na adhabu za kupigiwa mifano. Na yule asiyemuamini Mola wake Mlezi na kumfanyia urafiki, atahasiri dini yake na dunia yake. Basi thawabu zake za kidunia na kiakhera ndizo thawabu bora zinazotarajiwa na kutumainiwa. Basi katika kisa hiki kikubwa kuna mazingatio ya hali ya yule ambaye Mwenyezi Mungu alimneemesha neema za kidunia, lakini zikamsahaulisha akhera, na zikamfanya kuvuka mipaka na akamuasi Mwenyezi Mungu katika neema hizo, kwamba mwisho wake ni kuisha na kutoweka. Na kwamba hata ikiwa anafurahia kwazo kidogo, basi atanyimwa hizo kwa muda mrefu, na kwamba mja anafaa anapopenda kitu katika mali yake au mtoto wake, basi na azifungamanishe neema hizo kwa Yule aliyempa, na aseme, atakacho Mwenyezi Mungu huwa, hakuna nguvu yoyote isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu ili awe mwenye kumshukuru
[Mwenyezi Mungu] na kufanya neema zake hizo ziendelee kubaki. Kwa kauli yake, "Na lau kuwa ulipoingia kitaluni kwako,
ungelisema: MashaAllah
(Alitakalo Mwenyezi Mungu huwa). Hapana nguvu isipokuwa kwa Mungu.” Na ndani yake kuna mwongozo wa kujiliwaza dhidi ya starehe za dunia na matamanio yake kwa heri iliyoko kwa Mwenyezi Mungu. Kwa kauli yake, "Ikiwa unaniona mimi nina mali kidogo na watoto kuliko wewe. Basi huenda Mola wangu Mlezi akanipa kilicho bora kuliko kitalu chako." Na ndani yake kuna kwamba mali na watoto havifai kitu ikiwa havisaidii katika kumtii Mwenyezi Mungu, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema,
“Na si mali zenu wala watoto wenu watakaowaweka karibu nasi mkawa karibu, isipokuwa mwenye kuamini na akatenda mema.” Na ndani yake kuna kuomba dua ili iangamizwe mali ya yule ambaye mali yake ni sababu ya kuvuka kwake mipaka, kukufuru, na kuhasiri, hasa ikiwa atajifadhilisha kwa sababu yake juu ya waumini na anajifahirisha kwao. Na ndani yake kuna kwamba natija ya ulinzi wa Mwenyezi Mungu na kutokuwepo kwake huwa wazi pale tu vumbi inapotoweka na malipo yakaja, na watendao wakapata malipo yao. Basi
“huko ulinzi ni wa Mwenyezi Mungu wa Haki tu. Yeye ndiye mbora zaidi wa malipo, na wa mwisho ulio bora zaidi.”
{وَاضْرِبْ لَهُمْ مَثَلَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنْزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ فَأَصْبَحَ هَشِيمًا تَذْرُوهُ الرِّيَاحُ وَكَانَ اللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ مُقْتَدِرًا (45) الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِنْدَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا (46)}.
45. Na wapigie mfano wa uhai wa dunia ambao ni kama maji tunayoyateremsha kutoka mbinguni, yakachanganyika na mimea ya ardhi, kisha mimea hiyo ikawa vibuwa vinavyopeperushwa na upepo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. 46. Mali na wana ni pambo la uhai wa dunia. Na mema yanayobakia ni bora mbele ya Mola wako Mlezi kwa malipo, na bora kwa matumaini.
#
{45} يقول تعالى لنبيِّه - صلى الله عليه وسلم - أصلاً ولمن قام بوراثته بعده تبعاً: اضرب للناس {مَثَلَ الحياة الدنيا}؛ ليتصوَّروها حقَّ التصوُّر ويعرِفوا ظاهرها وباطنها، فيقيسوا بينها وبين الدار الباقية، ويؤثروا أيَّهما أولى بالإيثار. وإنَّ مَثَلَ هذه الحياة الدُّنيا كمثل المطر؛ ينزِلُ على الأرض، فيختلط نباتها، تُنْبِتُ من كلِّ زوج بهيج، فبينا زهرتُها وزُخرفها تسرُّ الناظرين، وتفرِحُ المتفرِّجين، وتأخذُ بعيون الغافلين؛ إذ أصبحتْ {هشيماً تذروه الرياح}: فذهب ذلك النبات الناضر والزهر الزاهر والمنظر البهيُّ، فأصبحت الأرض غبراء تراباً قد انحرف عنها النظرُ، وصرف عنها البصرُ، وأوحشت القلبَ؛ كذلك هذه الدُّنيا؛ بينما صاحبها قد أعْجِبَ بشبابِهِ، وفاق فيها على أقرانِهِ وأترابِهِ، وحصَّل درهمَها ودينارَها، واقتطف من لذَّتِهِ أزهارها، وخاض في الشهوات في جميع أوقاته، وظنَّ أنَّه لا يزال فيها سائر أيامه؛ إذْ أصابه الموتُ أو التلفُ لماله، فذهب عنه سرورُهُ، وزالت لذَّتُه وحبوره، واستوحش قلبُه من الآلام، وفارق شبابَه وقوتَه ومالَه، وانفرد بصالح أو سيئ أعماله، هنالك يعضُّ الظالم على يديه حين يعلم حقيقةَ ما هو عليه ويتمنَّى العَوْدَ إلى الدُّنيا، لا ليستكمل الشهوات، بل ليستدركَ ما فرط منه من الغفلات؛ بالتوبة والأعمال الصالحات، فالعاقل الحازمُ الموفَّق يعرِضُ على نفسِهِ هذه الحالة، ويقول لنفسه: قدِّري أنَّك قد متِّ، ولا بدَّ أن تموتي؛ فأيُّ الحالتين تختارين: الاغترار بزخرِف هذه الدار، والتمتُّع بها كتمتُّع الأنعام السارحة، أم العمل لدارٍ أكُلُها دائمٌ وظلُّها، وفيها ما تشتهيه الأنفسُ وتلذُّ الأعين؛ فبهذا يُعْرَفُ توفيقُ العبد من خذلانِهِ، وربحُهُ من خسرانِهِ.
{45} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Nabii wake – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake -
awali na kwa atakayemrithi baada yake pili: Wapigieni watu "mfano wa uhai wa dunia" ili waifikirie ipasavyo na waijue nje na ndani yake, ili wapate kupima kati yake na nyumba inayobakia, na wapendelee ile kati yake inayofailia zaidi kupendelewa. Na kwamba mfano wa uhai wa dunia ni kama mvua inayonyesha juu ya ardhi na ikachanganyika na mimea yake, kisha ikaotesha kila jozi la kupendeza. Na wakati uzuri wake na mapambo yake vilikuwa vinawapendeza watazamaji, na kuwafurahisha wanaofurahia, na kuyavutia macho ya walioghafilika, tazama vikawa "vibuwa vinavyopeperushwa na upepo" kwa hivyo ndipo ikatoweka mimea hiyo ya kupendeza, na uzuri huo mkubwa, na mandhari hayo mazuri. Basi ardhi ikawa vumbi na mchanga ambayo haingaliwi tena, na moyo ukawa mpweke. Vivyo hivyo ndivyo ilivyo dunia hii, wakati mwenye kuipenda anapokuwa amependezwa na ujana wake, na akawashinda wenzake na rika zake, na akachuma dirhamu na dinari zake, akapata starehe katika mazuri yake, akajiingiza katika matamanio katika wakati wake wote, na akadhani kwamba ataendelea kuwa katika hali hiyo kwa muda siku zake zote zilizobakia, ghafla mauti yakamfika au kuharibika kwa mali yake, kwa hivyo furaha yake hiyo ikatoweka, na raha zake hizo na starehe zikaisha, na moyo wake ukahisi upweke kutokana na maumivu, na ujana wake na nguvu zake na utajiri wake vikaisha, basi akabakia peke yake na matendo yake mema au mabaya. Hapo dhalimu ataing'ata mikono yake atakapojua uhakika wa hali yake na atamani kurejea duniani, si ili akamilishe matamanio yake, bali ili arekebishe yale ambayo aliyapuuza, kwa toba na matendo mema. Basi mwenye akili, mwenye azimio aliyefanikiwa anaiweka hali hii mbele ya nafsi yake,
kisha aiambie nafsi yake: Chukulia kwamba umekufa, nawe lazima utakufa.
Ni ipi kati ya hali mbili hizi utaichagua: kuhadaika na mapambo ya nyumba hii, ambayo mwenye kujistarehesha kwayo ni kama wanyama walio katika malisho wanavyostarehe. Au aifanyie matendo nyumba ambayo matunda yake ni ya daima, na pia kivuli chake, na ndani yake kuna yale ambayo nafsi zinayatamani na macho yanayafurahia? Basi kwa haya ndiyo inajulikana kuwezeshwa kwa mja au kauchiliwa mbali, na kupata kwake faida au hasara.
#
{46} ولهذا أخبر تعالى أنَّ المال والبنين {زينةُ الحياة الدُّنيا}؛ أي: ليس وراء ذلك شيءٌ، وأنَّ الذي يبقى للإنسان وينفعُهُ ويسرُّه الباقيات الصالحات، وهذا يَشْمَلُ جميع الطاعات الواجبات والمستحبَّة من حقوق الله وحقوق عبادِهِ من صلاةٍ وزكاةٍ وصدقةٍ وحجٍّ وعمرةٍ وتسبيح وتحميدٍ وتهليل [وتكبير] وقراءةٍ وطلب علم نافع وأمرٍ بمعروفٍ ونهي عن منكرٍ وصلة رحم وبرِّ والدين وقيام بحقِّ الزوجات والمماليك والبهائم وجميع وجوه الإحسان إلى الخلق، كلُّ هذا من الباقيات الصالحات؛ فهذه خيرٌ عند الله ثواباً وخيرٌ أملاً؛ فثوابُها يبقى ويتضاعفُ على الآباد، ويؤمَّل أجرُها وبرُّها ونفعها عند الحاجة؛ فهذه التي ينبغي أن يَتَنافَس بها المتنافسون، ويستبقَ إليها العاملون، ويجدَّ في تحصيلها المجتهدون. وتأمَّل كيف لما ضَرَبَ الله مثل الدُّنيا وحالها واضمحلالها؛ ذَكَرَ أنَّ الذي فيها نوعان: نوعٌ من زينتها يُتمتَّع به قليلاً ثم يزول بلا فائدةٍ تعود لصاحبه، بل ربَّما لحقته مضرَّته، وهو المال والبنون. ونوعٌ يبقى لصاحبِهِ على الدَّوام، وهي الباقياتُ الصالحاتُ.
{46} Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kuwa fedha mali na watoto ni "pambo la uhai ya dunia" na kwamba hakuna chochote zaidi ya hilo. Na kwamba kile kinachombakia mtu na kumnufaisha na kumfurahisha ni mema yanayobakia. Na hili linajumuisha utiifu wote wa faradhi na ule unaopendekezwa miongoni mwa haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake, kama vile swala, zaka, na sadaka na Hajj na Umra, na kumtakasa Mwenyezi Mungu na kumsifu, na kusema hakuna mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kutoa takbira, na kusoma, na kutafuta elimu yenye manufaa, na kuamrisha mema na kukataza maovu, kuwaunga jamaa, kuwafanyia wema wazazi wawili, na kutekeleza haki za mke, watumwa, na mifugo, na mambo yote ya ihsani kwa viumbe. Yote hayo ni miongoni mwa mambo mema yenye kubakia. Haya ndiyo yaliyo bora mbele ya Mwenyezi Mungu kwa malipo, na bora kwa matumaini. Kwa maana, thawabu zake zinabakia na kuongezeka milele, na yanatarajiwa malipo yake, wema wake, manufaa yake yanapohitajika. Basi haya ndiyo washindani wanapaswa kushindania, na watendaji wayakimbilie, na wayafanyie bidii kubwa wafanyao bidii. Na tazama vipi, Mwenyezi Mungu alipopiga mfano wa dunia, hali yake, na kutoweka kwake,
akataja kwamba vilivyomo ndani yake ni vya aina mbili: Aina moja ni mapambo yake ambayo watu hujistarehesha kwayo muda kidogo, kisha yanatoweka bila ya manufaa yoyote kumrudia mwenyewe. Na hata labda anaweza kudhuriwa nayo. Haya ni mali na watoto. Na aina ile nyingine ni ya kumbakia mwenyewe milele, ambayo ndiyo mema yenye kubakia.
{وَيَوْمَ نُسَيِّرُ الْجِبَالَ وَتَرَى الْأَرْضَ بَارِزَةً وَحَشَرْنَاهُمْ فَلَمْ نُغَادِرْ مِنْهُمْ أَحَدًا (47) وَعُرِضُوا عَلَى رَبِّكَ صَفًّا لَقَدْ جِئْتُمُونَا كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ بَلْ زَعَمْتُمْ أَلَّنْ نَجْعَلَ لَكُمْ مَوْعِدًا (48) وَوُضِعَ الْكِتَابُ فَتَرَى الْمُجْرِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا فِيهِ وَيَقُولُونَ يَاوَيْلَتَنَا مَالِ هَذَا الْكِتَابِ لَا يُغَادِرُ صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً إِلَّا أَحْصَاهَا وَوَجَدُوا مَا عَمِلُوا حَاضِرًا وَلَا يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا (49)}.
47. Na siku tutakapoiondoa milima na ukaiona ardhi iwazi, na tukawafufua, wala hatutamwacha hata mmoja miongoni mwao. 48. Na wakahudhurishwa mbele ya Mola wako Mlezi kwa safu
(wakaambiwa): Mmetujia kama tulivyowaumba mara ya kwanza! Bali mlidai kwamba hatutawawekea miadi. 49. Na kitawekwa kitabu. Basi utawaona wakosefu wanavyoogopa kwa yale yaliyomo.
Na watasema: Ole wetu! Kitabu hiki kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa isipokuwa hulidhibiti vyema? Na watayakuta yote waliyoyatenda yapo hadharani. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote.
#
{47 - 48} يخبر تعالى عن حال يوم القيامة وما فيه من الأهوال المقلقة والشَّدائد المزعجة، فقال: {ويومَ نُسَيِّرُ الجبالَ}؛ أي: يزيلها عن أماكنها؛ يجعلها كثيباً، ثم يجعلها كالعهن المنفوش، ثم تضمحلُّ وتتلاشى وتكون هباءً منبثًّا، وتبرز الأرض فتصير قاعاً صفصفاً لا عوج فيه ولا أمتاً، ويحشُرُ الله جميع الخَلْق على تلك الأرض؛ فلا يغادِرُ منهم أحداً، بل يجمع الأولين والآخرين من بطون الفلوات وقعور البحار، ويجمعهم بعدما تفرَّقوا، ويعيدهم بعدما تمزَّقوا خلقاً جديداً، فَيُعْرَضونَ عليه صفًّا ليستعرِضَهم وينظرَ في أعمالهم ويحكم فيهم بحكمه العدل الذي لا جَوْر فيه ولا ظُلْم، ويقول لهم: {لقد جِئْتُمونا كما خَلَقْناكم أولَ مرةٍ}؛ أي: بلا مال ولا أهل ولا عشيرة، ما معهم إلا الأعمال التي عملوها والمكاسب في الخير والشرِّ التي كسبوها؛ كما قال تعالى: {ولقد جِئْتمونا فُرادى كما خَلَقْناكم أولَ مرَّة وتركتُم ما خوَّلْناكم وراءَ ظهورِكُم وما نَرى معكم شفعاءَكم الذين زعمتُم أنَّهم فيكم شركاءُ}، وقال هنا مخاطباً للمنكرين للبعث وقد شاهدوه عياناً: {بل زعمتُم أن لن نجعلَ لكم موعداً}؛ أي: أنكرتُم الجزاء على الأعمال ووعدَ الله ووعيده؛ فها قد رأيتُموه وذقتموه.
Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu hali ya Siku ya Qiyama na hofu iliyomo ndani yake ya kutia wasiwasi na mambo magumu ya kusumbua. Akasema, "Na siku tutakapoiondoa milima" na kuifanya kuwa matifutifu ya mchanga, kisha ataifanya milima hiyo kuwa kama sufi zilizochambuliwa, kisha milima hiyo itatoweka na kuondoka iwe mavumbi yanayopeperushwa. Nayo ardhi itainuka na iwe uwanja tambarare, bila ya mdidimio wowote wala mwinuko. Na Mwenyezi Mungu atakusanya viumbe vyote katika ardhi hiyo, na wala hatamwacha hata mmoja miongoni mwao. Bali atawakusanya wa mwanzo na wa mwisho kutoka katika vilindi vya majangwa na chini ya bahari. Na atawakusanya baada ya kutawanyika kwao, na awarudishe katika umbo jipya baada ya kuchanika. Kisha wataletwa mbele yake safu ili awaangalie na ayaangalie matendo yao na awahukumu kwa hukumu yake ya uadilifu ambayo ukandamizaji wowote ndani yake wala dhuluma. Na atawaambia, "Mmetujia kama tulivyowaumba mara ya kwanza." Yaani, bila mali yoyote, na jamaa, wala ukoo, na hawana chochote pamoja nao isipokuwa matendo waliyoyafanya na heri au maovu waliyochuma. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema, "Na hakika mlitujia wapweke kama tulivyowaumba mara ya kwanza na mkayaacha nyuma yenu yote tuliyowapa, na wala hatuwaoni hao waombezi wenu ambao mlidai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwenu." Na akasema hapa, akiwaongelesha wale waliokadhibisha ufufuo na huku wamekwishauona kwa macho yao wenyewe, "Bali mlidai kwamba hatutawawekea miadi." Yaani, mlipinga malipo juu ya matendo yenu na ahadi na tishio kali la Mwenyezi Mungu. Basi ndio huu ufufuo mmeshauona na kuuonja.
#
{49} فحينئذٍ تُحْضَرُ كتب الأعمال التي كتبها الملائكة الأبرار ، فتطير لها القلوبُ، وتَعْظُم من وقعها الكروبُ، وتكاد لها الصمُّ الصلاب تذوبُ، ويشفق منها المجرمون؛ فإذا رأوها مسطرةً عليهم أعمالهم محصى عليهم أقوالهم وأفعالهم؛ قالوا: {يا وَيْلَتَنا مالِ هذا الكتابِ لا يغادِرُ صغيرةً ولا كبيرةً إلاَّ أحصاها}؛ أي: لا يترك خطيئة صغيرة ولا كبيرة إلاَّ وهي مكتوبةٌ فيه محفوظة لم ينس منها عملُ سرٍّ ولا علانية ولا ليل ولا نهار. {ووجدوا ما عَمِلوا حاضراً}: لا يقدرون على إنكارِهِ، {ولا يظلم ربُّك أحداً}: فحينئذٍ يجازَوْن بها ويُقَرَّرون بها ويُخْزَون ويحقُّ عليهم العذاب، {ذلك بما قدَّمتْ أيديهم وأنَّ الله ليس بظلاَّم للعبيدٍ}: بل هم غيرُ خارجين عن عدلِهِ وفضلِهِ.
{49} Kisha wakati huo vitaletwa vitabu vya matendo vilivyoandikwa na Malaika wema. Na mioyo itawaruka kwa sababu yake, na dhiki itakuwa kubwa mno kwa sababu yake, na utakaribia uziwi mgumu kuyeyuka, na wahalifu wataviogopa mno. Na wanapoona kwamba yameandikwa humo matendo yao, yemedhibitiwa maneno yao na vitendo vyao, watasema,
“Ole wetu! Kitabu hiki kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa isipokuwa hulidhibiti.” Yaani, hakiachi dhambi, dogo wala kubwa, isipokuwa liliandikwa humo na kuhifadhiwa, hakuna siri wala tendo lolote la hadharani wala la usiku wala mchana lililosahaulika. "Na watayakuta yote waliyoyatenda yapo hadharani," hawataweza kuyakanusha. "Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote." Basi wakati huo watalipwa kwayo na watafanywa kuyakubali, na watafedheheshwa na itawadhibitikia adhabu. "Hayo ni kwa yale iliyotanguliza mikono yao, na kwamba Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja wake." Bali hawakutoka katika uadilifu wake na fadhila zake.
{وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ كَانَ مِنَ الْجِنِّ فَفَسَقَ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِ أَفَتَتَّخِذُونَهُ وَذُرِّيَّتَهُ أَوْلِيَاءَ مِنْ دُونِي وَهُمْ لَكُمْ عَدُوٌّ بِئْسَ لِلظَّالِمِينَ بَدَلًا (50)}.
50.
Na tulipowaambia Malaika: Msujudieni Adam! Walimsjudia isipokuwa Iblisi. Yeye alikuwa miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake Mlezi. Je, mnamchukua yeye na dhuria yake kuwa vipenzi badala yangu, hali wao ni adui zenu? Ni ovu mno badala hii ya madhalimu.
#
{50} يخبر تعالى عن عداوة إبليس لآدم وذُرِّيَّته، وأنَّ الله أمر الملائكة بالسجودِ لآدم إكراماً وتعظيماً وامتثالاً لأمر الله، فامتثلوا ذلك؛ {إلاَّ إبليس كان من الجِنِّ فَفَسَقَ عن أمرِ ربِّه}، وقال: {أأسجدُ لمن خَلَقْتَه طيناً}. وقال: {أنا خيرٌ منه}،، فتبيَّن بهذا عداوته لله ولأبيكم؛ فكيف تتَّخذونه {وذُرِّيَّته}؛ أي: الشياطين {أولياء من دوني وهم لكم عدُوٌّ بئس للظالمينَ بدلاً}؛ أي: بئس ما اختاروا لأنفسهم من ولاية الشيطان الذي لا يأمرهم إلاَّ بالفحشاء والمنكر عن ولاية الرحمن الذي كلُّ السعادة والفلاح والسرور في ولايته. وفي هذه الآية الحثُّ على اتِّخاذ الشيطان عدوًّا والإغراء بذلك وذِكْرُ السبب الموجب لذلك، وأنَّه لا يفعل ذلك إلاَّ ظالمٌ، وأيُّ ظلم أعظم من ظلم من اتَّخذ عدوَّه الحقيقي وليًّا وترك الوليَّ الحميد؟! قال تعالى: {اللهُ وليُّ الذين آمنوا يُخْرِجُهُم من الظُّلماتِ إلى النُّورِ والذين كَفَروا أولياؤُهُم الطَّاغوتُ يُخْرِجونَهم من النُّورِ إلى الظُّلُماتِ}، وقال تعالى: {إنَّهم اتَّخذوا الشياطين أولياءَ مِنْ دونِ الله}.
{50} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu uadui wa Iblisi kwa Adam na kizazi chake. Na kwamba Mwenyezi Mungu aliwaamuru Malaika wamsujudie Adam kwa heshima, kumtukuza, na kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu, basi wakatekeleza hayo, "Isipokuwa Iblisi, yeye alikuwa miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake Mlezi" na akasema, "Je, nimsujudie uliyemuumba kwa udongo?" Naye akasema,
“Mimi ni bora kuliko yeye.” Kwa hivyo kwa hayo ukabainika uadui wake kwa Mwenyezi Mungu na baba yenu Adam. Basi vipi mnamchukua yeye "na dhuria yake;" yaani, mashetani "kuwa vipenzi badala yangu mimi, na wao ni maadui zenu? Ni ovu mno badala hii ya madhalimu." Yaani, ni ovu mno walilojichagulia wenyewe la kufanya Shetani kuwa kipenzi, ambaye hawaamrishi isipokuwa kufanya mambo machafu na maovu badala ya kumfanya Mwingi wa kurehemu kuwa ndiye kipenzi, ambaye furaha zote na mafanikio yako katika kumfanya yeye kuwa kipenzi. Katika aya hii, kuna himizo la kumfanya Shetani kuwa ni adui na kuwashawishi watu kufanya hivyo, na kutaja sababu ya kulazimu hilo, na kwamba hafanyi yeye kuwa kipenzi isipokuwa dhalimu. Na ni dhuluma gani iliyo kubwa zaidi kuliko dhuluma ya mwenye kumchukua adui yake wa kweli kuwa ndiye kipenzi na kumwacha yule aliye Mlinzi, Msifika? Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, “Mwenyezi Mungu ndiye mlinzi wa wale walioamini. Huwatoa gizani na kuwapeleka kwenye nuru. Lakini wale waliokufuru, walinzi wao ni Mashetani. Huwatoa kwenye nuru na kuwaingiza gizani." Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, “Hakika wamewafanya mashetani kuwa marafiki walinzi badala ya Mwenyezi Mungu."
{مَا أَشْهَدْتُهُمْ خَلْقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَا خَلْقَ أَنْفُسِهِمْ وَمَا كُنْتُ مُتَّخِذَ الْمُضِلِّينَ عَضُدًا (51) وَيَوْمَ يَقُولُ نَادُوا شُرَكَائِيَ الَّذِينَ زَعَمْتُمْ فَدَعَوْهُمْ فَلَمْ يَسْتَجِيبُوا لَهُمْ وَجَعَلْنَا بَيْنَهُمْ مَوْبِقًا (52)}.
51. Sikuwashuhudisha kuumbwa kwa mbingu na ardhi, wala kuumbwa kwa nafsi zao. Wala sikuwafanya wapotezao kuwa ni wasaidizi. 52. Na siku atakaposema
(Mwenyezi Mungu): Waiteni hao mliodai kuwa ni washirika wangu. Basi watawaita, na wao hawatawaitikia. Nasi tutaweka baina yao maangamio.
#
{51} يقول تعالى: ما أشهدتُ الشياطين وهؤلاء المضلِّين خَلْقَ السماواتِ والأرض ولا خَلْقَ أنفسِهِم؛ أي: ما أحضرتهم ذلك ولا شاورتهم عليه؛ فكيف يكونون خالقين لشيء من ذلك، بل المتفرِّد بالخلق والتدبير والحكمة والتقدير هو الله، خالقُ الأشياء كلِّها، المتصرِّف فيها بحكمته؛ فكيف يُجعلُ له شركاءُ من الشياطين يوالَوْن ويُطاعون كما يُطاع الله وهم لم يخلُقوا ولم يشهدوا خلقاً ولم يعاونوا الله تعالى، ولهذا قال: {وما كُنْتُ مُتَّخِذَ المُضِلِّين عَضُداً}؛ أي: معاونين مظاهرين لله على شأن من الشؤون؛ أي: ما ينبغي ولا يليق بالله أن يجعل لهم قسطاً من التَّدبير؛ لأنهم ساعون في إضلال الخلق والعداوة لربهم؛ فاللائقُ أن يُقْصِيَهم ولا يُدنيهم.
{51} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Sikuwafanya mashetani na hawa wapotezao washuhudie uumbaji wa mbingu na ardhi, wala uumbaji wao wenyewe, wala sikutafuta ushauri wao kuhusu hilo. Basi wanawezaje kuwa wao ndio waumbaji wa lolote katika hayo? Bali, aliye wa pekee katika uumbaji, uendeshaji, hekima, kuweka majaliwa ni Mwenyezi Mungu, Muumba wa vitu vyote, aendeshaye mambo yao kwa hekima yake. Basi vipi atafanyiwa washirika miongoni mwa mashetani ili wafanywe vipenzi na kutiiwa jinsi Mwenyezi Mungu anavyotiiwa, na hali hawakuumba, hawakushuhudia uumbaji wowote, na hawakumsaidia Mwenyezi Mungu Mtukufu? Na ndiyo maana akasema,
“Wala sikuwafanya wapotoshaji kuwa ni wasaidizi” katika jambo lolote, na wala haimfailii wala haiendani na Mwenyezi Mungu kuwapa sehemu katika uendeshaji. Kwa maana, wanawania kuwapoteza viumbe na kumfanyia uadui Mola wao Mlezi. Basi kinachofaa ziadi ni kuwaweka mbali na wala asiwaweke karibu naye.
#
{52} ولما ذكر حال من أشرك به في الدُّنيا، وأبطل هذا الشرك غاية الإبطال، وحكم بجهل صاحبه وسفَّهه؛ أخبر عن حالهم مع شركائهم يوم القيامة، وأنَّ الله يقول لهم: نادوا شُرَكائِيَ بزعمكم؛ أي: على موجب زعمكم الفاسد، وإلاَّ؛ فبالحقيقة ليس لله شريكٌ في الأرض ولا في السماء؛ أي: نادوهم لينفعوكم ويخلِّصوكم من الشدائد. {فَدَعَوْهم فلم يستجيبوا لهم}: لأنَّ الحكم والملك يومئذٍ لّله، لا أحد يملِكُ مثقال ذرَّة من النفع لنفسه ولا لغيره. {وجعلنا بينهم}؛ أي: بين المشركين وشركائهم {موبقاً}؛ أي: مهلكاً يفرِّق بينهم وبينهم، ويبعِدُ بعضهم من بعض، ويتبيَّن حينئذٍ عداوة الشركاء لشركائهم، وكفرهم بهم، وتبرِّيهم منهم؛ كما قال تعالى: {وإذا حُشِرَ الناسُ كانوا لهم أعداءً وكانوا بعبادتِهم كافرينَ}.
{52} Na alipotaja hali ya wanaomshirikisha duniani, na akaibatilisha kabisa shirki hii, na akahukumu kwamba mwenye hayo ni mjinga na mpumbavu, akajulisha kuhusu hali yao kwa washirika wao Siku ya Qiyama,
na kwamba Mwenyezi Mungu atawaambia: Waiteni washirika wangu - kulingana na madai yenu mabovu, Vinginevyo, ukweli ni kwamba Mwenyezi Mungu hana mshirika yeyote katika ardhi wala mbinguni. Yaani, waiteni ili wawanufaishe na wawaepushe na magumu. "Basi watawaita, na wao hawatawaitikia." Kwa sababu hukumu na ufalme siku hiyo ni wa Mwenyezi Mungu, na hakuna yeyote atakayemiliki manufaa uzito wa chembe kwa ajili yake mwenyewe wala kwa ajili ya mwingine. "Na tutaweka baina yao;" yaani, baina ya washirikina na washirika wao "maangamio", yatakayowatenganisha wao kwa wao, na kuwaweka mbali wao kwa wao, na wakati huo utabainika uadui wa washirika kwa washirika wao, na kuwakufuru kwao, na kuijitenga kwao nao. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na watakapokusanywa watu, watakuwa maadui zao wataikufuru ibada yao."
{وَرَأَى الْمُجْرِمُونَ النَّارَ فَظَنُّوا أَنَّهُمْ مُوَاقِعُوهَا وَلَمْ يَجِدُوا عَنْهَا مَصْرِفًا (53)}.
53. Na wahalifu watauona Moto na watajua ya kwamba wao lazima wataingia humo; wala hawatapata pa kuuepukia.
#
{53} أي: لما كان يوم القيامة، وحصل من الحساب ما حصل، وتميَّز كلُّ فريق من الخلق بأعمالهم، وحقَّت كلمة العذاب على المجرمين، فرأوا جهنَّم قبل دخولها، فانزعجوا، واشتدَّ قلقهم لظنِّهم أنهم مواقعوها، وهذا الظنُّ قال المفسرون: إنَّه بمعنى اليقين، فأيقنوا أنَّهم داخلوها، {ولم يجدوا عنها مصرِفاً}؛ أي: معدلاً يعدلون إليه، ولا شافع لهم من دون إذنه. وفي هذا من التخويف والترهيب ما ترعد له الأفئدة والقلوب.
{53} Yaani, ilipofika Siku ya Qiyama, na mambo ya hesabu yakafanyika namna yatakavyofanyika, na kila kundi la viumbe likapambanuka kwa matendo yao, na likadhibitika neno la adhabu kwa wahalifu, basi wakaiona Jahannamu kabla ya kuingia humo, kwa hivyo wakafadhaika, na wasiwasi wao ukawa mkubwa basi wakajua kwa uhakika kwamba wataingia humo, "wala hawatapata pa kuuepukia" si mahali pa kukimbilia wala mwombezi wa kuwaombea bila ya idhini ya Mwenyezi Mungu. Katika hili kuna kuhofisha na kuogofya ambako kunatetemesha vifua na mioyo.
{وَلَقَدْ صَرَّفْنَا فِي هَذَا الْقُرْآنِ لِلنَّاسِ مِنْ كُلِّ مَثَلٍ وَكَانَ الْإِنْسَانُ أَكْثَرَ شَيْءٍ جَدَلًا (54)}.
54. Na bila ya shaka tumewaelezea watu katika Qur-ani hii kila namna ya mfano. Lakini mwanaadamu amezidi kuliko kila kitu kwa ubishi.
#
{54} يخبر تعالى عن عظمة القرآن وجلالته وعُمومه، وأنَّه صرَّف فيه {من كلِّ مَثَل}؛ أي: من كلِّ طريق موصل إلى العلوم النافعة والسعادة الأبديَّة وكل طريق يعصِمُ من الشرِّ والهلاك؛ ففيه أمثالُ الحلال والحرام، وجزاء الأعمال، والترغيب والترهيب، والأخبار الصادقة النافعة للقلوب؛ اعتقاداً وطمأنينةً ونوراً، وهذا مما يوجب التسليم لهذا القرآن وتلقِّيه بالانقياد والطَّاعة وعدم المنازعة له في أمر من الأمور، ومع ذلك؛ كان كثير من الناس يجادلونَ في الحقِّ بعدما تبيَّن، ويجادلون بالباطل ليُدْحِضوا به الحقَّ، ولهذا قال: {وكانَ الإنسانُ أكثر شيءٍ جَدَلاً}؛ أي: مجادلةً ومنازعةً فيه، مع أنَّ ذلك غير لائقٍ بهم، ولا عدل منهم، والذي أوجب له ذلك، وعدم الإيمان بالله، إنَّما هو الظلم والعناد، لا لقصور في بيانِهِ وحجَّته وبرهانه، وإلاَّ؛ فلو جاءهم العذاب وجاءهم ما جاء قبلهم؛ لم تكن هذه حالهم، ولهذا قال:
{54} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya ukuu wa Qur-ani, na utukufu wake, na ujumla wake, na kwamba ameeleza ndani yake "kila namna ya mfano." Yaani, kila njia zenye kufikisha kwenye elimu zenye manufaa na furaha ya milele na kila njia inayokinga kutokana na uovu na maangamivu. Basi ndani yake kuna mifano ya halali na haramu, malipo ya matendo, kutia moyo na kutishia, na habari za ukweli zenye kunufaisha nyoyo kiitikadi na utulivu na nuru. Na haya ni katika yale yanayolazimu kujisalimu kwa Qur-ani hii na kuipokea kwa kuifuata na kuitii na kutobishana nayo katika jambo lolote lile. Lakini pamoja na hayo, wengi wamekuwa wakibishana juu ya haki baada ya kudhihirika kwake, na hubishana kwa batili ili waivunje haki kwayo. Na ndio maana akasema, “Lakini mwanaadamu amezidi kuliko kila kitu kwa ubishi." Yaani, kujadili na kubishana juu yake, pamoja na hayo hayawafailii, wala sio waadilifu katika hayo. Na kilichomsababishia hayo na kutomuamini Mwenyezi Mungu, ni dhuluma tu na ukaidi, si kwa sababu ya kuwepo upungufu wowote katika kubainisha kwake, na hoja zake, na uthibitisho wake. Vinginevyo, lau kuwa ingewajia adhabu na yakawafikia yale yaliyowafikia wa kabla yao, basi hii isingekuwa hali yao.
Na ndiyo maana akasema:
{وَمَا مَنَعَ النَّاسَ أَنْ يُؤْمِنُوا إِذْ جَاءَهُمُ الْهُدَى وَيَسْتَغْفِرُوا رَبَّهُمْ إِلَّا أَنْ تَأْتِيَهُمْ سُنَّةُ الْأَوَّلِينَ أَوْ يَأْتِيَهُمُ الْعَذَابُ قُبُلًا (55)}.
55. Na hakikuwazuia watu kuamini ulipowajia uwongofu, na kuomba maghfira kwa Mola wao Mlezi, isipokuwa iwafikie desturi ya wale wa mwanzo, au iwafikie adhabu jahara.
#
{55} أي: ما منع الناس من الإيمان ـ والحالُ أنَّ الهدى الذي يحصُلُ به الفرق بين الهدى والضلال والحقِّ والباطل قد وَصَلَ إليهم وقامت عليهم حُجَّة الله، فلم يمنعهم عدم البيان، بل منعهم الظُّلم والعدوان عن الإيمان، فلم يبقَ إلاَّ أن تأتيهم سنَّة الله وعادتُه في الأولين، من أنَّهم إذا لم يؤمنوا؛ عوجلوا بالعذاب، أو يرونَ العذاب قد أقبل عليهم، ورأوه مقابلةً ومعاينةً؛ أي: فَلْيخافوا من ذلك، ولْيتوبوا من كفرهم؛ قبل أن يكون العذاب الذي لا مردَّ له.
{55} Yaani, hakuna kilichowazuia watu kuamini na hali ni kwamba uwongofu unaoleta tofauti baina ya uwongofu na upotovu, na haki na batili umekwisha wafikia na hoja ya Mwenyezi Mungu ikawasimamia juu yao. Kwa hivyo, hawakuzuiwa na kutokuwepo ubainisho, bali walizuiwa na dhuluma na kuvuka mipaka. Basi hakuna kinachobakia isipokuwa kuwajia desturi ya Mwenyezi Mungu na ada yake katika wa mwanzo, kwamba ikiwa hawataamini, wataharakishiwa adhabu, au wataona adhabu ikiwajia, waione imewaelekea moja kwa moja. Basi na walihofu hilo, na watubie kutoka kwa ukafiri wao kabla ya kuja kwa adhabu hiyo isiyoweza kuzuiliwa.
{وَمَا نُرْسِلُ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنْذِرِينَ وَيُجَادِلُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِالْبَاطِلِ لِيُدْحِضُوا بِهِ الْحَقَّ وَاتَّخَذُوا آيَاتِي وَمَا أُنْذِرُوا هُزُوًا (56)}.
56. Na hatuwatumi Mitume isipokuwa wawe wabashiri na waonyaji. Na wale waliokufuru wanabishana kwa batili, ili kwayo waivunje haki. Na walizifanya Ishara zangu na yale waliyoonywa kuwa ni mzaha.
#
{56} أي: لم نرسل الرُّسُلَ عَبَثاً، ولا ليتَّخذهم الناس أرباباً، ولا ليدعوا إلى أنفسهم، بل أرسلناهم يدعون الناس إلى كلِّ خير، وينهَوْن عن كلِّ شرٍّ، ويبشرونهم على امتثال ذلك بالثواب العاجل والآجل، وينذرونهم على معصية ذلك بالعقاب العاجل والآجل، فقامت بذلك حجة الله على العباد، ومع ذلك يأبى الظالمون الكافرون إلاَّ المجادلة بالباطل لِيُدْحِضوا به الحقَّ، فسَعَوا في نصر الباطل مهما أمكنهم، وفي دحض الحقِّ وإبطاله، واستهزؤوا برسل الله وآياته، وفرحوا بما عندهم من العلم، {ويأبى اللهُ إلاَّ أن يُتِمَّ نورَه ولو كره الكافرون}، ويظهر الحق على الباطل، {بل نقذف بالحقِّ على الباطل فيدمَغُه فإذا هو زاهِقٌ}، ومن حكمة الله ورحمته أنَّ تقييضه المبطِلين المجادلين الحقَّ بالباطل من أعظم الأسباب إلى وضوح الحقِّ وتبيُّن شواهده وأدلَّته وتبيُّن الباطل وفساده؛ فبضدِّها تتبيَّن الأشياء.
{56} Yaani, hatukuwatuma Mitume bure, wala ili watu wawafanye wao kuwa mola walezi, wala wajilinganie wao wenyewe. Bali tuliwatuma ili wawalinganie watu kwenye heri, na wawakataze maovu na wawape bishara ya malipo mema ya haraka juu ya kuyatekeleza hayo na ya baadaye, na wawaonye juu ya adhabu ya haraka na ya baadaye kwa sababu ya kuyaasi hayo. Kwa hivyo, hoja ya Mwenyezi Mungu akasimama juu ya waja wake kutokana na hayo. Lakini pamoja na hayo madhalimu makafiri walikataa isipokuwa kubishana kwa batili ili waivunje haki kwa hilo. Basi wakajitahidi katika kuinusuru batili wawezavyo, na katika kuivunja haki na kuibatilisha. Na wakawafanyia masihara Mitume wa Mwenyezi Mungu na ishara zake, na wakafurahia elimu waliyo nayo. "Na Mwenyezi Mungu amekataa isipokuwa kuikamilisha nuru yake, ijapokuwa makafiri wanaichukia." Na haki huibuka na kushinda batili, "Bali tunaitupa haki juu ya batili na inaivunja, na mara inatoweka." Na katika hekima ya Mwenyezi Mungu na rehema yake ni kwamba kuwaweka wana batili kuijadili haki kwa batili ni katika sababu kubwa mno zinazoifanya haki kuwa wazi na kubainika kwa hoja zake na ushahidi wake, na kubainika kwa batili na ubovu wake. Kwa maana kitu hubainika kwa kinyume chake.
{وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنْ ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ فَأَعْرَضَ عَنْهَا وَنَسِيَ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ إِنَّا جَعَلْنَا عَلَى قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَنْ يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا وَإِنْ تَدْعُهُمْ إِلَى الْهُدَى فَلَنْ يَهْتَدُوا إِذًا أَبَدًا (57) وَرَبُّكَ الْغَفُورُ ذُو الرَّحْمَةِ لَوْ يُؤَاخِذُهُمْ بِمَا كَسَبُوا لَعَجَّلَ لَهُمُ الْعَذَابَ بَلْ لَهُمْ مَوْعِدٌ لَنْ يَجِدُوا مِنْ دُونِهِ مَوْئِلًا (58) وَتِلْكَ الْقُرَى أَهْلَكْنَاهُمْ لَمَّا ظَلَمُوا وَجَعَلْنَا لِمَهْلِكِهِمْ مَوْعِدًا (59)}.
57. Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayekumbushwa Ishara za Mola wake Mlezi, naye akazipuuza na akasahau yaliyotangulizwa na mikono yake? Hakika Sisi tumeziba juu ya nyoyo zao ili wasifahamu, na uziwi kwenye masikio yao. Na ukiwaita kwenye uwongofu, hawataweza kabisa kuongoka. 58. Na Mola wako Mlezi ni Msamehevu Mwenye rehema. Lau angeliwachukulia kwa mujibu wa yale waliyoyachuma, bila ya shaka angeliwafanyia haraka kuwaadhibu. Lakini wanayo miadi ambayo hawatapata makimbilio yoyote ya kuepukana nayo. 59. Na miji hiyo tuliwaangamiza watu wake walipodhulumu. Na tukawawekea miadi ya maangamizo yao.
#
{57} يخبر تعالى أنَّه لا أعظم ظلماً ولا أكبر جرماً من عبدٍ ذُكِّر بآيات الله وبُيِّن له الحقُّ من الباطل والهدى من الضلال، وخُوِّف ورُهِّب ورُغِّب، فأعرض عنها، فلم يتذكَّر بما ذُكِّر به، ولم يرجِعْ عما كان عليه، {ونسي ما قدَّمت يداه} من الذُّنوب، ولم يراقب علاَّم الغيوب؛ فهذا أعظم ظلماً من المعرض الذي لم تأتِهِ آياتُ الله ولم يُذَكَّرْ بها، ـ وإن كان ظالماً ـ؛ فإنَّه أشدُّ ظلماً من هذا؛ لكون العاصي على بصيرةٍ وعلم أعظم ممَّن ليس كذلك، ولكنَّ الله تعالى عاقبه بسبب إعراضِهِ عن آياته ونسيانِهِ لذنوبه ورضاه لنفسه حالة الشرِّ مع علمه بها، أن سدَّ عليه أبواب الهداية بأنْ جَعَلَ على قلبِهِ أكنَّةً؛ أي: أغطية محكمةً تمنعه أن يفقه الآيات وإن سمعها؛ فليس في إمكانه الفقهُ الذي يصل إلى القلب. {وفي آذانهم وقراً}؛ أي: صمماً يمنعهم من وصول الآيات ومن سماعها على وجه الانتفاع، وإنْ كانوا بهذه الحالة؛ فليس لهدايتهم سبيلٌ. {وإن تَدْعُهُم إلى الهدى فلن يَهْتَدوا إذاً أبداً}: لأنَّ الذي يُرجى أن يجيبَ الداعي للهدى من ليس عالماً، وأما هؤلاء الذين أبصروا ثم عَموا، ورأوا طريق الحقِّ فتركوه، وطريق الضلال فسلكوه، وعاقبهم الّله بإقفال القلوب والطَّبْع عليها؛ فليس في هدايتهم حيلةٌ ولا طريقٌ. وفي هذه الآية من التخويف لمن ترك الحقَّ بعد علمه أن يُحالَ بينه وبينه، ولا يتمكَّن منه بعد ذلك ما هو أعظم مرهبٍ وزاجرٍ عن ذلك.
{57} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba hakuna dhalimu mkubwa zaidi au mhalifu mkubwa zaidi kuliko mja ambaye alikumbushwa ishara za Mwenyezi Mungu na akabainishiwa haki kutoka kwa batili, na uwongofu kutoka kwa upotovu, na akahofishwa, na akatiwa woga, na tena akatiwa moyo, lakini akayapuuza hayo, wala hakukumbuka yale aliyokumbushwa, na wala hakurejea akaacha yale aliyokuwa nayo. "Na akasahau yaliyotangulizwa na mikono yake" miongoni mwa madhambi, wala hakumchunga ajuaye zaidi wa ghaibu. Basi huyu ndiye dhalimu mkubwa zaidi kuliko yule anayezipuuza ambaye hakujiwa na ishara za Mwenyezi Mungu na wala hakukumbushwa kwazo, hata kama ni dhalimu, lakini yule wa kwanza ni dhalimu mno kumliko huyu. Kwa sababu mtenda dhambi huku ana ufahamu na elimu anafanya jambo kubwa zaidi kuliko asiyekuwa hivyo. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu alimuadhibu kwa sababu ya kupuuza kwake ishara zake, na kusahau kwake madhambi yake, na kuiridhika kwake nafsi yake hali ya uovu licha ya yeye kuijua, kwa kumfungia milango ya uwongofu kwa kumwekea vizuizi madhubuti juu ya moyo wake vyenye kumzuia kuzifahamu ishara, hata kama atazisikia, hawezi kuzifahamu ambako kunafika katika moyo. "Na uziwi kwenye masikio yao." Yaani, uziwi unaowazuia ishara kuwafikia na kuzisikia kwa njia ya kunufaika nazo. Na kama hali yao ni hii, basi hakuna njia yoyote ya kuwaongoa. "Na ukiwaita kwenye uwongofu, hawataweza kabisa kuongoka." Kwa sababu anayetarajiwa kumuitikia mwitaji kwenye uwongofu ni yule asiyekuwa na elimu. Ama hawa ambao waliona kisha wakawa vipofu, na wakaiona njia ya haki, na wakaiacha, na njia ya upotofu na wakaifuata, na Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa kuzifunga nyoyo zao na kuziziba, basi hakuna hila yoyote wala njia ya kuwaongoa. Na katika Aya hii, kuna kumhofisha mwenye kuacha haki baada ya kuijua kwamba itazuiliwa kati yake nayo, wala hataliweza baada ya hilo. Na huku ni kutishia na kukomesha kukubwa zaidi dhidi ya hilo.
#
{58} ثم أخبر تعالى عن سعة مغفرته ورحمته، وأنَّه يغفر الذنوب ويتوب الله على من يتوب فيتغمده برحمته ويشمله بإحسانه، وأنه لو آخذ العباد على ما قدَّمت أيديهم من الذُّنوب؛ لعجَّل لهم العذاب، ولكنَّه تعالى حليمٌ لا يَعْجَلُ بالعقوبة، بل يُمْهِلُ ولا يُهْمِلُ، والذُّنوب لا بدَّ من وقوع آثارها، وإنْ تأخَّرت عنها مدة طويلة، ولهذا قال: {بل لهم موعدٌ لن يَجِدوا من دونِهِ موئلاً}؛ أي: لهم موعد يجازون فيه بأعمالهم، لا بدَّ لهم منه، ولا مندوحة لهم عنه، ولا ملجأ ولا محيد عنه.
{58} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kuhusu upana wa msamaha wake na rehema zake, na kwamba Yeye husamehe dhambi, na anakubali toba ya anayetubia, na kumfunika kwa rehema yake na wema wake. Na kwamba ikiwa angewaadhibu waja kwa sababu ya dhambi ambazo mikono yao ilitanguliza, basi angewaharakishia adhabu. Lakini Yeye Mtukufu ni Mstahamilivu, wala haharakishi kuadhibu, bali hupeana muhula wala hapuuzi. Na madhambi lazima athari zake zipatikane, hata kama zitachelewa baada yake kwa muda mrefu. Na ndiyo maana akasema,
“Lakini wanayo miadi ambayo hawatapata makimbilio yoyote ya kuepukana nayo.” Na hapo watalipwa kwa matendo yao.
#
{59} وهذه سنَّته في الأولين والآخرين، أن لا يعاجِلَهم بالعقاب، بل يستدعيهم إلى التوبة والإنابة؛ فإنْ تابوا وأنابوا؛ غَفَرَ لهم ورحمهم وأزال عنهم العقاب، وإلاَّ؛ فإن استمرُّوا على ظلمهم وعنادهم، وجاء الوقتُ الذي جعله موعداً لهم؛ أنزل بهم بأسه، ولهذا قال: {وتلك القرى أهلكناهم لما ظلموا}؛ أي: بظلمهم، لا بُظلم منَّا. {وجعلنا لمهلكهم موعداً}؛ أي: وقتاً مقدَّراً لا يتقدَّمون عنه ولا يتأخَّرون.
{59} Na hii ndiyo desturi yake katika wa mwanzo na wa mwisho, ya kwamba hawaharakishii adhabu, bali anawaita kwenye toba na kurudi kwake. Kwa hivyo, wakitubu na wakarudi kwake, anawasamehe na anawarehemu, na anawaondolea adhabu. Vinginevyo, wakiendelea na dhuluma yao na ukaidi wao huo, na ukafika wakati aliouweka kuwa ndio miadi yao, anawateremshia adhabu yake. Na ndiyo maana akasema,
“Na miji hiyo tuliwaangamiza watu wake walipodhulumu” wao wenyewe, na si kwamba tuliwadhulumu. “Na tukawawekea miadi ya maangamizo yao." Yaani muda uliopangwa ambao hawawezi kuutangulia wala kukawia zaidi yake.
{وَإِذْ قَالَ مُوسَى لِفَتَاهُ لَا أَبْرَحُ حَتَّى أَبْلُغَ مَجْمَعَ الْبَحْرَيْنِ أَوْ أَمْضِيَ حُقُبًا (60) فَلَمَّا بَلَغَا مَجْمَعَ بَيْنِهِمَا نَسِيَا حُوتَهُمَا فَاتَّخَذَ سَبِيلَهُ فِي الْبَحْرِ سَرَبًا (61) فَلَمَّا جَاوَزَا قَالَ لِفَتَاهُ آتِنَا غَدَاءَنَا لَقَدْ لَقِينَا مِنْ سَفَرِنَا هَذَا نَصَبًا (62) قَالَ أَرَأَيْتَ إِذْ أَوَيْنَا إِلَى الصَّخْرَةِ فَإِنِّي نَسِيتُ الْحُوتَ وَمَا أَنْسَانِيهُ إِلَّا الشَّيْطَانُ أَنْ أَذْكُرَهُ وَاتَّخَذَ سَبِيلَهُ فِي الْبَحْرِ عَجَبًا (63) قَالَ ذَلِكَ مَا كُنَّا نَبْغِ فَارْتَدَّا عَلَى آثَارِهِمَا قَصَصًا (64) فَوَجَدَا عَبْدًا مِنْ عِبَادِنَا آتَيْنَاهُ رَحْمَةً مِنْ عِنْدِنَا وَعَلَّمْنَاهُ مِنْ لَدُنَّا عِلْمًا (65) قَالَ لَهُ مُوسَى هَلْ أَتَّبِعُكَ عَلَى أَنْ تُعَلِّمَنِ مِمَّا عُلِّمْتَ رُشْدًا (66) قَالَ إِنَّكَ لَنْ تَسْتَطِيعَ مَعِيَ صَبْرًا (67) وَكَيْفَ تَصْبِرُ عَلَى مَا لَمْ تُحِطْ بِهِ خُبْرًا (68) قَالَ سَتَجِدُنِي إِنْ شَاءَ اللَّهُ صَابِرًا وَلَا أَعْصِي لَكَ أَمْرًا (69) قَالَ فَإِنِ اتَّبَعْتَنِي فَلَا تَسْأَلْنِي عَنْ شَيْءٍ حَتَّى أُحْدِثَ لَكَ مِنْهُ ذِكْرًا (70) فَانْطَلَقَا حَتَّى إِذَا رَكِبَا فِي السَّفِينَةِ خَرَقَهَا قَالَ أَخَرَقْتَهَا لِتُغْرِقَ أَهْلَهَا لَقَدْ جِئْتَ شَيْئًا إِمْرًا (71) قَالَ أَلَمْ أَقُلْ إِنَّكَ لَنْ تَسْتَطِيعَ مَعِيَ صَبْرًا (72) قَالَ لَا تُؤَاخِذْنِي بِمَا نَسِيتُ وَلَا تُرْهِقْنِي مِنْ أَمْرِي عُسْرًا (73) فَانْطَلَقَا حَتَّى إِذَا لَقِيَا غُلَامًا فَقَتَلَهُ قَالَ أَقَتَلْتَ نَفْسًا زَكِيَّةً بِغَيْرِ نَفْسٍ لَقَدْ جِئْتَ شَيْئًا نُكْرًا (74) قَالَ أَلَمْ أَقُلْ لَكَ إِنَّكَ لَنْ تَسْتَطِيعَ مَعِيَ صَبْرًا (75) قَالَ إِنْ سَأَلْتُكَ عَنْ شَيْءٍ بَعْدَهَا فَلَا تُصَاحِبْنِي قَدْ بَلَغْتَ مِنْ لَدُنِّي عُذْرًا (76) فَانْطَلَقَا حَتَّى إِذَا أَتَيَا أَهْلَ قَرْيَةٍ اسْتَطْعَمَا أَهْلَهَا فَأَبَوْا أَنْ يُضَيِّفُوهُمَا فَوَجَدَا فِيهَا جِدَارًا يُرِيدُ أَنْ يَنْقَضَّ فَأَقَامَهُ قَالَ لَوْ شِئْتَ لَاتَّخَذْتَ عَلَيْهِ أَجْرًا (77) قَالَ هَذَا فِرَاقُ بَيْنِي وَبَيْنِكَ سَأُنَبِّئُكَ بِتَأْوِيلِ مَا لَمْ تَسْتَطِعْ عَلَيْهِ صَبْرًا (78) أَمَّا السَّفِينَةُ فَكَانَتْ لِمَسَاكِينَ يَعْمَلُونَ فِي الْبَحْرِ فَأَرَدْتُ أَنْ أَعِيبَهَا وَكَانَ وَرَاءَهُمْ مَلِكٌ يَأْخُذُ كُلَّ سَفِينَةٍ غَصْبًا (79) وَأَمَّا الْغُلَامُ فَكَانَ أَبَوَاهُ مُؤْمِنَيْنِ فَخَشِينَا أَنْ يُرْهِقَهُمَا طُغْيَانًا وَكُفْرًا (80) فَأَرَدْنَا أَنْ يُبْدِلَهُمَا رَبُّهُمَا خَيْرًا مِنْهُ زَكَاةً وَأَقْرَبَ رُحْمًا (81) وَأَمَّا الْجِدَارُ فَكَانَ لِغُلَامَيْنِ يَتِيمَيْنِ فِي الْمَدِينَةِ وَكَانَ تَحْتَهُ كَنْزٌ لَهُمَا وَكَانَ أَبُوهُمَا صَالِحًا فَأَرَادَ رَبُّكَ أَنْ يَبْلُغَا أَشُدَّهُمَا وَيَسْتَخْرِجَا كَنْزَهُمَا رَحْمَةً مِنْ رَبِّكَ وَمَا فَعَلْتُهُ عَنْ أَمْرِي ذَلِكَ تَأْوِيلُ مَا لَمْ تَسْطِعْ عَلَيْهِ صَبْرًا (82)}.
60. Na pale Musa alipomwambia kijana wake, "Sitaacha kuendelea mpaka nifike zinapokutana bahari mbili, au nitaendelea kwa muda mrefu." 61. Basi wawili hao walipofika zinapokutana hizo bahari mbili, walimsahau samaki wao, naye akashika njia yake akaponyokea baharini. 62. Walipokwisha pita,
alimwambia kijana wake: Tupe chakula chetu cha mchana. Kwa hakika tumepata machovu kweli kwa hii safari yetu. 63. Akasema
(kijana): Waona! Pale tulipopumzika penye jabali, basi mimi nilimsahau yule samaki. Na hakuna aliyenisahaulisha kumkumbuka isipokuwa Shetani tu. Naye akashika njia yake baharini kwa ajabu. 64.
(Musa) akasema: Hayo ndiyo tuliyokuwa tunayataka. Basi wakarudi nyuma kwa kufuata njia waliyojia. 65. Basi wakamkuta mja katika waja wetu tuliyempa rehema kutoka kwetu, na tukamfunza mafunzo yaliyotoka kwetu. 66.
Musa akamwambia: Nikufuate ili unifunze katika ule uwongofu uliofunzwa wewe? 67.
Akasema: Hakika wewe hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami. 68. Na utawezaje kuvumilia yale usiyoyajua vilivyo undani wake? 69.
Akasema: Inshaallah
(Mwenyezi Mungu akipenda), utanikuta mvumilivu, wala sitaasi amri yako yoyote. 70.
Akasema: Basi ukinifuata, usiniulize kitu mpaka mimi nianze kukutajia. 71. Basi wawili hao wakatoka, hata walipopanda jahazi
(yule mtu), akalitoboa.
(Musa) akasema: Unalitoboa ili uwazamishe watu wake? Hakika umefanya jambo baya mno. 72.
Akasema: Je, sikusema kwamba wewe hakika hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami? 73.
(Musa) akasema: Usinichukulie makosa kwa niliyosahau, wala usinipe uzito kwa jambo langu. 74. Basi wakatoka wawili hao mpaka wakamkuta kijana, akamuua.
(Musa) akasema: Ala! Umemuua mtu asiye na kosa, na wala hakuua nafsi yoyote! Ama hakika umefanya jambo baya kabisa! 75.
(Yule mtu) Akasema, "Je, sikukwambia kwamba hakika wewe hutaweza kusubiri kuwa pamoja nami?" 76.
(Musa) Akasema, "Nikikuuliza kuhusu kitu chochote baada ya haya, basi usifuatane nami. Kwani hakika umekwisha pata udhuru kutoka kwangu." 77. Basi wakaondoka mpaka wakawafikia watu wa mji mmoja. Wakawaomba watu wake wawape chakula, nao wakakataa kuwakaribisha. Hapo wakakuta ukuta unataka kuanguka,
(yule mja mwema) akausimamisha.
(Musa) akasema, "Ungelitaka, ungelichukua ujira kwa haya." 78.
(Yule mtu) akasema: Huku ndiko kufarikiana baina yangu na wewe. Sasa nitakueleza maana ya yale ambayo hukuweza kuyastahamili. 79. Ama lile jahazi, hilo lilikuwa la masikini fulani wafanyao kazi baharini. Kwa hivyo, nilitaka kulitia dosari, kwani nyuma yao alikuwako mfalme aliyekuwa akichukua kwa nguvu majahazi yote. 80. Na ama yule kijana, wazazi wake walikuwa ni Waumini. Tukahofu aje kuwatia mashakani kwa kupindukia mipaka na ukafiri. 81. Basi tulitaka Mola wao Mlezi awabadilishie aliye bora zaidi kuliko huyo kwa kutakasika, na aliye karibu zaidi kwa huruma. 82. Na ama ukuta ule, huo ulikuwa ni wa vijana wawili mayatima kule mjini. Na chini yake ilikuwako hazina yao; na baba yao alikuwa ni mtu mwema. Basi Mola wako Mlezi alitaka wafikie utu uzima wao na wajitolee hazina yao wenyewe, hii ikiwa ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Wala mimi sikutenda hayo kwa amri yangu. Hiyo ndiyo tafsiri ya hayo ambayo wewe hukuweza kuyasubiria.
#
{60} يخبر تعالى عن نبيِّه موسى عليه السلام وشدَّة رغبته في الخير وطلب العلم أنَّه قال لفتاه؛ أي: خادمه الذي يلازمه في حضره وسفره، وهو يُوشَعُ بن نون، الذي نبَّأه الّله بعد ذلك: {لا أبْرَحُ حتى أبْلُغَ مجمع البحرين}؛ أي: لا أزال مسافراً وإن طالت عليَّ الشُّقة ولحقتني المشقَّة حتى أصل إلى مجمع البحرين، وهو المكان الذي أوحي إليه أنَّك سَتَجِد فيه عبداً من عباد الله العالمين، عنده من العلم ما ليس عندك، {أو أمضيَ حُقُباً}؛ أي: مسافة طويلة. المعنى أنَّ الشوق والرغبة حَمَلَ موسى أن قال لفتاه هذه المقالة.
{60} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu Nabii wake Musa, amani iwe juu yake, na utashi wake mkubwa kwa kufanya heri na kutafuta elimu, kwamba alimwambia mtumishi wake ambaye alikuwa akiandamana naye safarini na nyumbani. Naye ni Yusha bin Nun, ambaye Mwenyezi Mungu alipeana habari zake baada ya hapo, "Sitaacha kuendelea mpaka nifike zinapokutana bahari mbili." Yaani, sitaacha kuendelea kusafiri, hata kama magumu ya safari yataniwiya marefu na kupatwa na dhiki, mpaka nifike zinapokutana bahari mbili. Napo ni pale mahali ambapo alifunuliwa kuwa utamkuta hapo mja katika waja wa Mwenyezi Mungu, mwenye elimu. Ambaye ana elimu usiyokuwa nayo wewe "au nitaendelea kwa muda mrefu." Na maana yake ni kwamba shuaku na utashi wake mkubwa ulimfanya Musa kumwambia kijana wake maneno hayo.
#
{61} وهذا عزمٌ منه جازم، فلذلك أمضاه، {فلما بلغا}؛ أي: هو وفتاه {مَجْمَعَ بينهما نسيا حوتَهما}: وكان معهما حوتٌ يتزوَّدان منه ويأكلان، وقد وُعِدَ أنَّه متى فقد الحوت؛ فثمَّ ذلك العبد الذي قصدته. {فاتَّخذ}: ذلك الحوت {سبيلَه}؛ أي: طريقه {في البحر سَرَباً}. وهذا من الآيات، قال المفسرون: إنَّ ذلك الحوت الذي كانا يتزوَّدان منه لما وصلا إلى ذلك المكان أصابه بللُ البحر، فانسرب بإذن الله في البحر، وصار مع حيواناته حيًّا.
{61} Na hii ilikuwa azimio madhubuti kutoka kwake, na ndiyo maana akaitimiza, "Basi wawili hao" yeye na kijana wake "walipofika zinapokutana hizo bahari mbili, walimsahau samaki wao." Naye alikuwa yule samaki ambaye walikuwa wakimla, na alikuwa ameahidiwa kwamba wakati atakapomteza samaki huyo, basi hapo ndipo kuna yule mja uliyemkusudia. "Naye" samaki yule "akashika njia yake akaponyokea baharini". Hii ni katika ishara.
Wamesema wafasiri: Samaki huyo ambaye walikuwa wakimla, walipofika mahali hapo, aliendewa na unyevu wa bahari, basi akaponyoka kwa idhini ya Mwenyezi Mungu akaingia baharini akawa hai pamoja na wanyama wake.
#
{62} فلما جاوز موسى وفتاه مجمعَ البحرين؛ قال موسى لفتاه: {آتِنا غداءنا لقد لَقينا مِنْ سَفَرِنا هذا نَصَباً}؛ أي: لقد تعبنا من هذا السفر المجاوز فقط، وإلاَّ؛ فالسفر الطويل الذي وصلا به إلى مجمع البحرين لم يجدا من التعب فيه، وهذا من الآيات والعلامات الدالَّة لموسى على وجود مطلبِهِ، وأيضاً؛ فإنَّ الشوق المتعلِّق بالوصول إلى ذلك المكان سهَّل لهما الطريق، فلمَّا تجاوزا غايتهما؛ وجدا مسَّ التعب.
{62} Musa na kijana wake walipopita makutano ya bahari mbili hizo, Musa akamwambia kijana wake, "Tupe chakula chetu cha mchana. Kwa hakika tumepata machovu kweli kwa hii safari yetu," iliyozidi tu pale tunapokusudia. Vinginevyo, safari ile ndefu waliyoichukua hadi kwenye makutano ya bahari mbili hizo, hawakupata uchovu wowote ndani yake. Na hili ni katika ishara na alama zilizomwonyesha Musa kwamba alikuwa amekwisha pata alichokuwa anakitafuta. Tena, hamu kubwa waliyokuwa nayo ya kufika mahali hapo iliwarahisishia njia, na walipovuka hapo walipokuwa wanakwenda, wakahisi mguso wa uchovu.
#
{63} فلما قال موسى لفتاه هذه المقالة؛ قال له فتاه: {أرأيتَ إذْ أوَيْنا إلى الصخرة فإنِّي نسيتُ الحوتَ} [أي: ألم تعلم حين آوانا الليل إلى تلك الصخرة المعروفة بينهما فإني نسيت الحوت]، {وما أنسانيهُ إلاَّ الشيطانُ}: لأنَّه السببُ في ذلك، {واتَّخذ سبيلَه في البحر عَجَباً}؛ أي: لما انسرب في البحر ودخل فيه؛ كان ذلك من العجائب. قال المفسرون: كان ذلك المسلك للحوت سرباً ولموسى وفتاه عجباً.
{63} Musa alipomwambia kijana wake maneno haya, kijana wake huyo akamwambia, "Waona! Pale tulipopumzika penye jabali, basi mimi nilimsahau yule samaki"
[Yaani hukujua kwamba usiku ulipotufanya kwenda katika jabali lile linalojulikana baina yetu, nilimsahau yule samaki?] "Na hapana aliyenisahaulisha kukumbuka isipokuwa Shetani tu. Naye akashika njia yake baharini kwa ajabu" alipoponyoka na kuingia baharini.
Wafasiri walisema: Njia hiyo ilikuwa ni ya kuponyokea kwa samaki huyo, na ilikuwa ni ya ajabu kwa Musa na kijana wake.
#
{64} فلما قال له الفتى هذا القول، وكان عند موسى وعدٌ من الله أنَّه إذا فَقَدَ الحوت؛ وَجَدَ الخَضِرَ، فقال موسى: {ذلك ما كُنَّا نَبْغ}؛ أي: نطلب. {فارْتَدَّا}؛ أي: رجعا {على آثارِهما قصصاً}؛ أي: رجعا يَقُصَّان أثرهما [إلى المكان] الذي نسيا فيه الحوت.
{64} Na kijana wake alipomwambia maneno haya, na Musa alikuwa ameahidiwa na Mwenyezi Mungu kwamba atakapompoteza samaki huyo, basi atamkuta Al-Khidhr. Basi Musa akasema, “Hayo ndiyo tuliyokuwa tunayataka" na kuyatafuta. "Basi wakarudi nyuma kwa kufuata njia waliyojia" wakifuata nyayo zao
[hadi mahali] ambapo walimsahaulia samaki huyo.
#
{65} فلما وصلا إليه؛ {وجدا عبداً من عبادنا}: وهو الخضر، وكان عبداً صالحاً لا نبيًّا على الصحيح. {آتيْناه رحمةً من عندنا}؛ أي: أعطاه الله رحمةً خاصَّة، بها زاد علمه وحسن عمله، {وعلَّمناه من لَدُنَّا}؛ أي: من عندنا {عِلْماً}: وكان قد أُعطي من العلم ما لم يعطَ موسى، وإنْ كان موسى عليه السلام أعلمَ منه بأكثر الأشياء وخصوصاً في العلوم الإيمانيَّة والأصوليَّة؛ لأنَّه من أولي العزم من المرسلين، الذين فضَّلهم الله على سائر الخلق بالعلم والعمل وغير ذلك.
{65} Walipofika hapo, "wakamkuta mja katika waja wetu" ambaye ni Al-Khidhr. Naye alikuwa mja mwema, na hakuwa nabii, kulingana na kauli sahihi. "Tuliyempa rehema kutoka kwetu." Yaani, Mwenyezi Mungu alimpa rehema maalumu, ambayo kwayo alizidi elimu yake na matendo yake yakawa mazuri. "Na tukamfunza mafunzo yaliyotoka kwetu." Na alikuwa kapewa elimu ambayo hakupewa Musa hata ingawa Musa, amani iwe juu yake, alikuwa na elimu zaidi kumliko katika mambo mengi, hasa katika elimu za kiimani na kimisingi. Kwa sababu yeye ni katika Mitume wenye stahamala kubwa mno, ambao Mwenyezi Mungu aliwafadhilisha juu ya viumbe wengine wote kwa elimu, matendo na mambo mengineyo.
#
{66} فلما اجتمع به موسى؛ قال له على وجه الأدب والمشاورة والإخبار عن مطلبه: {هل أتَّبعُك على أن تُعَلِّمنَي مما عُلِّمْتَ رُشداً}؛ أي: هل أتَّبِعك على أن تُعَلِّمني مما علَّمك الله ما به أسترشدُ وأهتدي وأعرف به الحقَّ في تلك القضايا، وكان الخضر قد أعطاه الله من الإلهام والكرامة ما به يحصُلُ له الاطلاع على بواطن كثيرٍ من الأشياء التي خَفِيَتْ حتى على موسى عليه السلام.
{66} Musa alipokutana naye, akamwambia kwa njia ya adabu, na mashauriano, na kujulisha juu ya kile anachotafuta, "Je, nikufuate ili unifunze katika ule uwongofu uliofunzwa wewe," ili niweze kujua haki katika masuala hayo? Na Al-Khidri alikuwa Mwenyezi Mungu amempa ufahamu na utukufu ambayo aliweza kwayo kujua undani wa mambo mengi yaliyokuwa yamefichikana hata kwa Musa, amani iwe juu yake.
#
{67} فقال الخضر لموسى: لا أمتنع من ذلك، ولكنَّك {لَنْ تَسْتطيعَ معيَ صبراً}؛ أي: لا تقدر على اتِّباعي وملازمتي؛ لأنَّك ترى ما لا تقدر على الصبر عليه من الأمور، التي ظاهرها المنكَر وباطنها غيرُ ذلك.
{67} Al-
Khidhr akamwambia Musa: Silikatai hilo, lakini, "Hakika wewe hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami." Kwa sababu utaona mambo ambayo hutaweza kuyavumilia, ambayo dhahiri yake ni maovu, lakini ndani yake si hivyo.
#
{68} ولهذا قال: {وكيفَ تصبر على ما لم تُحِطْ به خُبْراً}؛ أي: كيف تصبر على أمرٍ ما أحطتَ بباطنه وظاهره وعلمتَ المقصودَ منه ومآله.
{68} Na ndiyo sababu akasema, "Na utawezaje kuvumilia yale usiyoyajua vilivyo undani wake" ambayo hujazunguka undani wake na nje yake, na ukajua makusudio yake na matokeo yake?
#
{69} فقال موسى: {سَتَجِدُني إن شاء اللهُ صابراً ولا أعصي لك أمراً}: وهذا عزمٌ منه قبل أن يوجد الشيء الممتَحَن به، والعزمُ شيء ووجودُ الصبر شيء آخر؛ فلذلك ما صَبَرَ موسى عليه السلام حين وقع الأمر.
{69} Basi Musa akasema, "Mwenyezi Mungu akipenda, utanikuta mvumilivu, wala sitaasi amri yako yoyote." Na hili ilikuwa azimio lake kabla ya kupatikana kwa jambo hilo analopewa mtihani wake. Na azimio ni kitu, na kusubiri pia ni kitu kingine. Na ndiyo maana Musa, amani iwe juu yake, hakuwa na subira wakati jambo hilo lilipotokea.
#
{70} فحينئذٍ قال له الخضر: {فإنِ اتَّبَعْتَني فلا تَسْألْني عن شيءٍ حتَّى أحدِثَ لك منه ذِكْراً}؛ أي: لا تبتدئني بسؤال منك وإنكارٍ حتى أكون أنا الذي أخبرك بحالِهِ في الوقت الذي ينبغي إخبارُك به، فنهاه عن سؤالِهِ، ووعَدَه أن يوقفه على حقيقة الأمر.
{70} Kisha Al-Khidhr akasema, "Basi ukinifuata, usiniulize kitu mpaka mimi nianze kukutajia." Yaani, usianze kuniuliza swali lolote wala kupinga kitu mpaka niwe ndiye ninayekujulisha hali yake wakati unaofaa kukujulisha juu yake. Basi akamkataza kumuuliza, na akamuahidi kwamba atamuambia uhakika wa mambo hayo.
#
{71} {فانطلقا حتى إذا رَكِبا في السفينةِ خَرَقَها}؛ أي: اقتلع الخضِرُ منها لوحاً، وكان له مقصودٌ في ذلك سيبيِّنه، فلم يصبرْ موسى عليه السلام؛ لأنَّ ظاهره أنه منكرٌ؛ لأنَّه عَيْبٌ للسفينة وسببٌ لغرق أهلها، ولهذا قال موسى: {أخَرَقْتَها لِتُغْرِقَ أهلها لقد جئتَ شيئاً إمْراً}؛ أي: عظيماً شنيعاً، وهذا من عدم صبره عليه السلام.
{71} "Basi wawili hao wakatoka, hata walipopanda jahazi
(yule mtu) akalitoboa." Yaani, Al-Khidhr akang'oa ubao mmoja, na alikuwa na lengo katika hayo, ambalo atakuja libainisha. Lakini Musa, amani iwe juu yake, hakuwa na subira juu ya hilo. Kwa sababu lilionekana kwa nje kuwa jambo ovu. Kwa sababu ni kutia dosari katika jahazi, na ni sababu ya kuzama kwa watu wake. Na ndiyo maana Musa akasema, “Unalitoboa ili uwazamishe watu wake? Hakika umefanya jambo baya mno." Na hili ni kutokana na kutokuwa na subira kwake, yeye amani iwe juu yake.
#
{72} فقال له الخضر: {ألم أقُلْ إنَّك لن تستطيعَ معي صبراً}؛ أي: فوقع كما أخبرتك.
{72} Al-Khidhr akamwambia, "Je sikusema kwamba wewe hakika hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami?" Yaani, yakawa kama nilivyokwambia.
#
{73} وكان هذا من موسى نسياناً، فقال: {لا تؤاخِذْني بما نسيتُ ولا تُرْهِقْني من أمري عُسراً}؛ أي: لا تُعَسِّرْ عليَّ الأمر، واسمح لي؛ فإنَّ ذلك وقع على وجه النسيان، فلا تؤاخِذْني في أول مرة، فجمع بين الإقرار به والعذر منه، وأنَّه ما ينبغي لك أيُّها الخضر الشدَّة على صاحبك، فسمح عنه الخضر.
{73} Na haya Musa aliyafanya kwa kusahau, na ndiyo akasema, "Usinichukulie makosa kwa niliyosahau, wala usinipe uzito kwa jambo langu;" na uniruhusu kuendelea kuwa pamoja nawe. Kwa maana, hili lilitokea kwa kusahau. Basi usinilaumu mara ya kwanza. Kwa hivyo, akawa amejumuisha kati ya kukiri na kumpa udhuru kwa hilo, basi Al-Khidhr akamruhusu kuendelea kuwa pamoja naye.
#
{74} {فانطلقا حتَّى إذا لقيا غُلاماً}؛ أي: صغيراً، {فقَتَلَه}: الخضر، فاشتدَّ بموسى الغضب، وأخذتْه الحميَّة الدينيَّة حين قتل غلاماً صغيراً لم يُذْنِبْ. {قال أقتلتَ نفساً زكِيَّةً بغير نفسٍ لقد جئتَ شيئاً نُكْراً}: وأيُّ نُكْرٍ مثل قتل الصغير الذي ليس عليه ذنبٌ ولم يقتلْ أحدا؟! وكان الأول من موسى نسياناً، وهذه غير نسيانٍ، ولكن عدم صبرٍ.
{74} "Basi wakatoka wawili hao mpaka wakamkuta kijana" mdogo, Al-Khidhr "akamuua" kijana huyo mdogo, kwa hivyo Musa akawa na hasira kubwa zaidi, na hamasa ya kidini ikamshika alipomuua kijana huyo mdogo ambaye hakuwa ametenda dhambi yoyote. "
(Musa) akasema: Ala! Umemuua mtu asiye na kosa, na wala hakuua nafsi yoyote! Ama hakika umefanya jambo baya kabisa!" Na ni kitendo gani kiovu kama kumuua mtoto mdogo ambaye hana dhambi wala hakumuua yeyote? Na kitendo kile cha kwanza cha Musa kilikuwa kwa kusahau, lakini hiki siyo kwa kusahau, lakini ni kwa sababu ya kutokuwa na subira.
#
{75} فقال له الخضرُ معاتباً ومذكِّراً: {ألم أقُلْ لكَ إنكَ لن تستطيعَ معيَ صبراً}؟
{75} Kwa hivyo, Al-Khidhir akamwambia
(Musa), akimlaumu na akimkumbusha, "Je, sikukwambia kwamba hakika wewe huwezi kusubiri kuwa pamoja nami?"
#
{76} فَـ {قال} له موسى: {إن سألتُكَ عن شيءٍ} بعد هذه المرة؛ {فلا تصاحِبْني}؛ أي: فأنت معذور بذلك وبترك صحبتي، {قد بَلَغْتَ من لَدُنِّي عُذْراً}؛ أي: أعذرت مني، ولم تقصر.
{76} Basi Musa "akamwambia: "Nikikuuliza kuhusu kitu chochote" baada ya mara hii, "basi usifuatane nami." Yaani, umesamehewa kwa hilo na kwa kuacha kampuni yangu. "Umepata udhuru kutoka kwangu." Yaani, hakika umekwisha pata udhuru kutoka kwangu na haikupungua.
#
{77} {فانطلقا حتى إذا أتيا أهل قريةٍ استطعما أهلها}؛ أي: استضافاهم فلم يُضَيِّفوهُما، {فوجدا فيها جداراً يريدُ أن ينقضَّ}؛ أي: [قد] عاب واستهدم، {فأقامَهُ}: الخضرُ؛ أي بناه وأعاده جديداً، فَـ {قال} له موسى: {لو شئتَ لاتَّخَذْتَ عليه أجراً}؛ أي: أهل هذه القرية لم يضيفونا مع وجوب ذلك عليهم، وأنت تبنيه من دون أجرةٍ، وأنت تقدِرُ عليها؟!
{77} "Basi wakaondoka mpaka wakawafikia watu wa mji mmoja. Wakawaomba watu wake wawape chakula" baada ya kwamba waliwaomba wawakaribishe, lakini wakakataa kuwakaribisha. "Hapo wakakuta ukuta unataka kuanguka." Yaani, ulikuwa
[tayari] umezeeka na unaanguka unabomoka, ''akausimamisha." Yaani, Al-Khidhr akaujenga na kuurudisha upya. Musa "akasema" akimwambia, "Ungelitaka, ungelichukua ujira kwa haya." Yaani, watu wa kijiji hiki hawakutukaribisha pamoja na kwamba hilo lilikuwa wajibu juu yao, nawe unaujenga bila malipo ilhali unaweza kuyaitisha kutoka kwao?
#
{78} فحينئذٍ لم يفِ موسى عليه السلام بما قال، واستعذر الخضرُ منه، فَـ {قال} له: {هذا فراقُ بيني وبينكَ}: فإنَّك شرطتَ ذلك على نفسك، فلم يبقَ الآن عذرٌ ولا موضعٌ للصُّحبة. {سأنبِّئك بتأويل ما لم تستطِعْ عليه صبراً}؛ أي: سأخبرك بما أنكرتَ عليَّ وأنبِّئك بأنَّ لي في ذلك من المآرب وما يؤول إليه الأمر.
(78) Basi hapo, Musa, amani iwe juu yake, hakutimiza kile alichosema hapo awali, kwa hivyo Al-Khidhr akaomba ampe udhuru. Kwa hivyo ''akasema'' akimwambia, ''Huku ndiko kufarikiana baina yangu na wewe." Kwa maana wewe mwenyewe ndiye ulijiwekea sharti hilo, kwa hivyo hauna udhuru wowote wala nafasi kuendelea kuandama naye. ''Sasa nitakueleza maana ya yale uliyokuwa huwezi kuyastahamilia." Yaani, nitakujulisha yale uliyonipinga na kukuambia kwamba nilikuwa na lengo katika hayo na nilijua namna utakavyokuwa mwisho wa mambo hayo.
#
{79} {أما السفينة}: التي خرقتها، {فكانتْ لمساكينَ يعملون في البحر}: يقتضي ذلك الرِّقَّة عليهم والرأفة بهم، {فأردتُ أن أَعِيبها وكان وراءَهُم مَلِكٌ يأخذ كلَّ سفينة غَصْباً}؛ أي: كان مرورهم على ذلك الملك الظالم؛ فكلُّ سفينة صالحةٍ تمرُّ عليه ما فيها عيبٌ غَصَبها وأخَذَها ظلماً، فأردتُ أن أخْرِقها ليكونَ فيها عيبٌ فتسلم من ذلك الظالم.
{79} ''Ama ile jahazi" ambayo niliitoboa, "hiyo ilikuwa ya masikini fulani wafanyao kazi baharini" jambo linalohitaji kuwafanyia upole na huruma. ''Kwa hivyo, nilitaka kuitoa dosari, kwani nyuma yao alikuwako mfalme anachukua kwa nguvu majahazi yote." Yaani, walikuwa wakipita karibu na mfalme huyo dhalimu, ambaye kila jahazi salama isiyokuwa na dosari ilipokuwa inapita karibu naye, alikuwa akiichukua kwa dhuluma. Kwa hivyo nilitaka kuitoboa ili iwe na dosari kwa hivyo isalimike kutokana na dhalimu huyo.
#
{80} {وأما الغلامُ}: الذي قتلتُه؛ {فكان أبواه مؤمِنَيْنِ فخشينا أن يُرهِقَهما طغياناً وكفراً}: وكان ذلك الغلام قد قُدِّر عليه أنَّه لو بَلَغَ لأرهق أبويه طغياناً وكفراً؛ أي: لحملهما على الطغيان والكفر: إمَّا لأجل محبَّتهما إيَّاه، أو للحاجة إليه؛ أو يحملهما على ذلك؛ أي: فقتلته؛ لاطِّلاعي على ذلك؛ سلامةً لدين أبويه المؤمِنَيْنِ، وأيُّ فائدة أعظمُ من هذه الفائدة الجليلة؟!
{80} "Na ama yule kijana" ambaye Al-Khidhr alimua, "wazazi wake walikuwa ni Waumini. Tukahofu aje kuwatia mashakani kwa uasi na ukafiri." Na kijana huyo alikuwa ameandikiwa kwamba ikiwa atabeleghe, basi atawatia wazazi wake mashakani kwa uasi na ukafiri, ima kwa sababu ya upendo wao kwake, au kwa sababu ya wao kumhitajia ,au yeye mwenyewe awatie katika hayo. Kwa hivyo nikamuua, kwa sababu nilijua hili, kwa ajili ya usalama kwa dini ya wazazi wake waumini. Basi ni faida gani iliyo kubwa zaidi kuliko faida hii kubwa mno?
#
{81} وهو وإن كان فيه إساءةٌ إليهما وقطعٌ لذُرِّيَّتهما؛ فإنَّ الله تعالى سيعطيهما من الذُّرِّيَّة ما هو خيرٌ منه، ولهذا قال: {فأرَدْنا أن يُبْدِلهَما ربُّهما خيراً منه زكاةً وأقربَ رُحْماً}؛ أي: ولداً صالحاً زكيًّا واصلاً لرحِمِهِ؛ فإنَّ الغلام الذي قُتِلَ لو بلغ لَعَقَّهما أشدَّ العقوق بحملهما على الكفر والطغيان.
{81} Na hili hata kama kuna kuwafanyia ubaya ndani yake na kukikata kizazi chao, Mwenyezi Mungu Mtukufu atawapa dhuria iliyo bora zaidi kuliko hiyo. Na ndiyo maana akasema, ''Basi tulitaka Mola wao Mlezi awabadilishie aliye bora zaidi kuliko huyo kwa kutakasika, na aliye karibu zaidi kwa huruma." Yaani, mwana mwema, aliyetakasika, mwenye kuunga jamaa zake. Kwa maana mvulana yule aliyeuawa ikiwa angebaleghe, basi angewaasi uasi mkubwa mno kwa kuwafanya wawe makafiri na kupindukia mipaka.
#
{82} {وأمَّا الجدارُ}: الذي أقمته؛ {فكان لِغُلامين يتيمينِ في المدينةِ وكان تحتهَ كنزٌ لهما وكان أبوهما صالحاً}؛ أي: حالهما تقتضي الرأفة بهما ورحمتهما؛ لكونِهِما صغيرين، عدما أباهما، وحفظهما الله أيضاً بصلاح والدهما. {فأراد ربُّك أن يَبْلُغا أشدَّهما ويستخْرِجا كَنْزَهُما}؛ أي: فلهذا هدمتُ الجدار واستخرجتُ ما تحتَهُ من كنزِهِما ورددتُهُ وأعدتُه مجاناً؛ {رحمةً من ربِّك}؛ أي: هذا الذي فعلتُه رحمةٌ من الله آتاها الله عبدَه الخضر. {وما فعلتُهُ عن أمري}؛ أي: ما أتيت شيئاً من قِبَلِ نفسي ومجرَّد إرادتي، وإنَّما ذلك من رحمةِ الله وأمره. {ذلك}: الذي فسَّرتُه لك {تأويلُ ما لم تَسْطِعْ عليه صبراً}.
وفي هذه القصة العجيبة الجليلة من الفوائد والأحكام والقواعد شيءٌ كثيرٌ ننبِّه على بعضه بعون الله:
فمنها: فضيلة العلم والرِّحلة في طلبه، وأنَّه أهمُّ الأمورِ؛ فإنَّ موسى عليه السلام رحل مسافةً طويلةً، ولقي النَّصب في طلبه، وترك القعود عند بني إسرائيل لتعليمهم وإرشادهم، واختار السفر لزيادة العلم على ذلك.
ومنها: البداءةُ بالأهمِّ فالأهمِّ؛ فإنَّ زيادة العلم وعلم الإنسان أهمُّ من تَرْكِ ذلك والاشتغال بالتعليم من دون تزوُّد من العلم، والجمعُ بين الأمرين أكمل.
ومنها: جواز أخذِ الخادم في الحضَرِ والسفر؛ لكفاية المؤن وطلب الراحة؛ كما فعل موسى.
ومنها: أنَّ المسافر لطلب علم أو جهادٍ أو نحوه، إذا اقتضتِ المصلحةُ الإخبار بمطلبه وأين يريدُه؛ فإنَّه أكمل من كتمه؛ فإنَّ في إظهاره فوائدَ من الاستعداد له عدَّته وإتيان الأمر على بصيرةٍ وإظهار الشوق لهذه العبادة الجليلة؛ كما قال موسى: {لا أبرحُ حتى أبلغَ مجمع البحرين أو أمضيَ حُقُباً}، وكما أخبر النبيُّ - صلى الله عليه وسلم - أصحابه حين غزا تبوك بوجهه مع أنَّ عادته التَّورية، وذلك تَبَعٌ للمصلحة.
ومنها: إضافةُ الشرِّ وأسبابه إلى الشيطان على وجه التسويل والتزيين، وإنْ كان الكلُّ بقضاء الله وقدره؛ لقول فتى موسى: {وما أنسانيهُ إلاَّ الشيطانُ أنْ أذْكُرَهُ}.
ومنها: جواز إخبار الإنسان عمَّا هو من مقتضى طبيعة النفس من نَصَبٍ أو جوع أو عطش إذا لم يكنْ على وجه التسخُّط وكان صدقاً؛ لقول موسى: {لقد لقينا من سَفَرِنا هذا نَصَباً}.
ومنها: استحبابُ كون خادم الإنسان ذكيًّا فطناً كيِّساً؛ ليتمَّ له أمره الذي يريده.
ومنها: استحباب إطعام الإنسان خادمه من مأكله وأكلهما جميعاً؛ لأنَّ ظاهر قوله: {آتنا غداءنا}: إضافة إلى الجميع: أنَّه أكل هو وهو جميعاً.
ومنها: أنَّ المعونة تنزل على العبد على حسب قيامه بالمأمور به، وأنَّ الموافق لأمر الله يُعان ما لا يُعان غيره؛ لقوله: {لقد لَقينا من سَفَرِنا هذا نَصَباً}، والإشارة إلى السفر المجاوز لمجمع البحرين، وأما الأول؛ فلم يَشْتكِ منه التعب مع طولِهِ؛ لأنَّه هو السفر على الحقيقة، وأما الأخير؛ فالظاهر أنه بعض يوم؛ لأنَّهم فقدوا الحوتَ حين أووا إلى الصخرة؛ فالظاهر أنَّهم باتوا عندها، ثم ساروا من الغد، حتى إذا جاء وقتُ الغداء؛ قال موسى لفتاه: آتنا غداءنا؛ فحينئذٍ تذكَّرَ أنَّه نَسِيَهُ في الموضع الذي إليه منتهى قصده.
ومنها: أنَّ ذلك العبد الذي لقياه ليس نبيًّا، بل عبداً صالحاً؛ لأنَّه وصفه بالعبوديَّة، وذكر منَّة الله عليه بالرحمة والعلم، ولم يَذْكُر رسالته ولا نبوَّته، ولو كان نبيًّا؛ لذكر ذلك كما ذكر غيره. وأما قوله في آخر القصة: {وما فعلتُهُ عن أمري}؛ فإنَّه لا يدلُّ على أنَّه نبيٌّ، وإنَّما يدلُّ على الإلهام والتحديث؛ كما يكون لغير الأنبياء؛ كما قال تعالى: {وأوْحَيْنا إلى أمِّ موسى أنْ أرْضِعيه}، {وأوْحى ربُّك إلى النَّحْل أنِ اتَّخِذي من الجبال بيوتاً}.
ومنها: أنَّ العلم الذي يعلِّمه الله لعبادِهِ نوعان: علمٌ مكتسبٌ يدرِكُه العبد بجدِّه واجتهاده، ونوعٌ: علمٌ لَدُنِّيٌّ يهبُه الله لمن يمنُّ عليه من عباده؛ لقوله: {وعلَّمْناه من لَدُنَّا علماً}.
ومنها: التأدب مع المعلِّم وخطاب المتعلِّم إيَّاه ألطف خطاب؛ لقول موسى عليه السلام: {هل أتَّبِعُك على أن تُعَلِّمني مما عُلِّمْتَ رُشْداً}: فأخرج الكلام بصورة الملاطفة والمشاورة، وأنَّك هل تأذنُ لي في ذلك أم لا؟ وإقرارُهُ بأنَّه يتعلَّم منه؛ بخلاف ما عليه أهل الجفاء أو الكِبْر، الذي لا يُظْهِر للمعلِّم افتقاره إلى علمه، بل يدَّعي أنَّه يتعاون هو وإيَّاه، بل ربَّما ظنَّ أنه يعلِّم معلِّمه وهو جاهلٌ جدًّا؛ فالذُّلُّ للمعلم وإظهارُ الحاجة إلى تعليمه من أنفع شيء للمتعلم.
ومنها: تواضع الفاضل للتعلُّم ممَّن دونه؛ فإنَّ موسى بلا شكٍّ أفضل من الخضر.
ومنها: تعلُّم العالم الفاضل للعلم الذي لم يتمهَّر فيه ممَّن مَهَرَ فيه، وإنْ كان دونَه في العلم بدرجاتٍ كثيرةٍ؛ فإنَّ موسى عليه السلام من أولي العزم من المرسلين، الذين منحهم الله وأعطاهم من العلم ما لم يعطِ سواهم، ولكن في هذا العلم الخاصِّ كان عند الخضر ما ليس عنده؛ فلهذا حرص على التعلُّم منه؛ فعلى هذا لا ينبغي للفقيه المحدِّث إذا كان قاصراً في علم النحو أو الصرف أو نحوه من العلوم أن لا يتعلَّمه ممَّن مَهَرَ فيه، وإنْ لم يكنْ محدِّثاً ولا فقيهاً.
ومنها: إضافة العلم وغيره من الفضائل لله تعالى، والإقرار بذلك، وشكر الله عليها؛ لقوله: {تُعَلِّمَني مما عُلِّمْتَ}؛ أي: مما علمك الله تعالى.
ومنها: أن العلم النافع هو العلم المرشد إلى الخير، فكلُّ علم يكون فيه رشد وهداية لطريق الخير وتحذيرٌ عن طريق الشرِّ أو وسيلة لذلك؛ فإنَّه من العلم النافع، وما سوى ذلك؛ فإمَّا أن يكون ضارًّا أو ليس فيه فائدةٌ؛ لقوله: {أن تُعَلِّمَني مما عُلِّمْتَ رُشْداً}.
ومنها: أن من ليس له قوَّة الصبر على صحبة العالم والعلم وحسن الثَّبات على ذلك؛ أنَّه [يفوته بحسب عدم صبره كثير من] العلم؛ فمن لا صبر له؛ لا يدرِكُ العلم، ومن استعمل الصبر ولازمه؛ أدرك به كل أمرٍ سعى فيه؛ لقول الخضر يتعذر من موسى بذكر المانع لموسى من الأخذ عنه: إنَّه لا يصبر معه.
ومنها: أن السبب الكبير لحصول الصبر إحاطةُ الإنسان علماً وخبرةً بذلك الأمر الذي أمِرَ بالصبر عليه، وإلاَّ؛ فالذي لا يدريه أو لا يدري غايته ولا نتيجته ولا فائدته وثمرته ليس عنده سببُ الصبر؛ لقوله: {وكيف تصبِرُ على ما لم تُحِطْ به خُبْراً}؛ فجعل الموجب لعدم صبرِهِ عدم إحاطته خُبراً بالأمر.
ومنها: الأمر بالتأنِّي والتثبُّت وعدم المبادرة إلى الحكم على الشيء حتى يعرفَ ما يُراد منه وما هو المقصود.
ومنها: تعليقُ الأمور المستقبلة التي من أفعال العباد بالمشيئة، وأن لا يقولَ الإنسان للشيء: إني فاعل ذلك في المستقبل إلاَّ أن يقول إن شاء الله.
ومنها: أن العزم على فعل الشيء ليس بمنزلة فعله؛ فإنَّ موسى قال: {سَتَجِدُني إن شاء الله صابراً}: فوطَّن نفسه على الصبر ولم يفعل.
ومنها: أنَّ المعلِّم إذا رأى المصلحة في إيزاعه للمتعلِّم أن يترك الابتداء في السؤال عن بعض الأشياء حتى يكون المعلِّم هو الذي يوقفه عليها؛ فإنَّ المصلحة تتَّبع؛ كما إذا كان فهمه قاصراً، أو نهاه عن الدقيق في سؤال الأشياء التي غيرها أهمُّ منها أو لا يدرِكُها ذهنُه، أو يسأل سؤالاً لا يتعلَّق في موضع البحث.
ومنها: جواز ركوب البحر في غير الحالة التي يخاف منها.
ومنها: أنَّ الناسي غير مؤاخذٍ بنسيانه؛ لا في حقِّ الله، ولا في حقوق العبادِ؛ لقوله: {لا تؤاخِذْني بما نسيتُ}.
ومنها: أنَّه ينبغي للإنسان أن يأخُذَ من أخلاق الناس ومعاملاتهم العفوَ منها وما سمحتْ به أنفسُهم، ولا ينبغي له أن يكلِّفَهم ما لا يطيقون أو يشقَّ عليهم ويرهِقَهم؛ فإنَّ هذا مدعاةٌ إلى النفور منه والسآمة، بل يأخذ المتيسِّر ليتيسر له الأمر.
ومنها: أنَّ الأمور تجري أحكامها على ظاهرها، وتُعَلَّقُ بها الأحكام الدنيويَّة في الأموال والدماء وغيرها؛ فإنَّ موسى عليه السلام أنكر على الخضِرِ خرقَه السفينة وقتلَ الغلام، وأنَّ هذه الأمور ظاهرها أنَّها من المنكر، وموسى عليه السلام لا يَسَعُهُ السكوتُ عنها في غير هذه الحال التي صَحِبَ عليها الخضر، فاستعجل عليه السلام، وبادَرَ إلى الحكم في حالتها العامَّة، ولم يلتفتْ إلى هذا العارض الذي يوجب عليه الصبر وعدم المبادرةِ إلى الإنكار.
ومنها: القاعدة الكبيرة الجليلة، وهو أنَّه يُدْفَعُ الشرُّ الكبير بارتكاب الشرِّ الصغير، ويُراعى أكبر المصلحتين بتفويت أدناهما؛ فإنَّ قتل الغلام شرٌّ، ولكنَّ بقاءه حتى يفتن أبويه عن دينهما أعظمُ شرًّا منه، وبقاء الغلام من دون قتل وعصمته وإن كان يظنُّ أنه خيرٌ؛ فالخير ببقاء دين أبويه وإيمانهما خيرٌ من ذلك؛ فلذلك قَتَلَهُ الخضر. وتحت هذه القاعدة من الفروع والفوائد ما لا يدخُلُ تحت الحصر، فتزاحُمُ المصالح والمفاسدِ كلِّها داخلٌ في هذا.
ومنها: القاعدة الكبيرة أيضاً، وهي أنَّ عمل الإنسان في مال غيره إذا كان على وجه المصلحة وإزالةِ المفسدةِ أنَّه يجوزُ، ولو بلا إذنٍ، حتى ولو ترتَّب على عمله إتلافُ بعض مال الغير؛ كما خَرَقَ الخضر السفينةَ لتعيبَ فتسلمَ من غَصْب الملك الظالم؛ فعلى هذا: لو وقع حرقٌ أو غرق أو نحوهما في دار إنسانٍ أو ماله، وكان إتلافُ بعض المال أو هدمُ بعض الدار فيه سلامةٌ للباقي؛ جاز للإنسان، بل شُرِعَ له ذلك؛ حفظاً لمال الغير. وكذلك لو أراد ظالمٌ أخذَ مال الغير، ودفع إليه إنسانٌ بعض المال افتداءً للباقي؛ جاز، ولو من غير إذن.
ومنها: أن العمل يجوز في البحر كما يجوز في البرِّ؛ لقوله: {يعملون في البحر}، ولم ينكر عليهم عملهم.
ومنها: أنَّ المسكين قد يكون له مالٌ لا يبلُغ كفايته ولا يخرجُ بذلك عن اسم المسكنة؛ لأنَّ الله أخبر أنَّ هؤلاء المساكين لهم سفينة.
ومنها: أنَّ القتل من أكبر الذنوب؛ لقوله في قتل الغلام: {لقد جئتَ شيئا نُكْراً}.
ومنها: أنَّ القتل قصاصاً غير مُنْكَرٍ؛ لقوله: {بغيرِ نفسٍ}.
ومنها: أنَّ العبد الصالح يحفظُهُ الله في نفسه وفي ذُرِّيَّتِهِ.
ومنها: أن خدمة الصالحين أو مَنْ يتعلَّق بهم أفضل من غيرها؛ لأنَّه علَّل استخراج كنزهما وإقامة جدارهما بأنَّ أباهما صالح.
ومنها: استعمال الأدب مع الله تعالى في الألفاظ؛ فإنَّ الخضر أضاف عَيْبَ السفينة إلى نفسه؛ بقوله: {فأردتُ أن أعيبها}، وأما الخيرُ؛ فأضافه إلى الله تعالى؛ لقوله: {فأراد ربُّك أن يَبْلُغا أشدَّهما ويستخرِجا كَنزَهما رحمةً من ربِّك}؛ كما قال إبراهيم عليه السلام: {وإذا مرضْتُ فهو يشفينِ}، وقالت الجنُّ: {وأنَّا لا ندري أشرٌّ أريدَ بِمَن في الأرض أم أرادَ بهم ربُّهم رَشَداً}؛ مع أنَّ الكلَّ بقضاء الله وقدره.
ومنها: أنَّه ينبغي للصاحب أن لا يفارِقَ صاحبه في حالةٍ من الأحوال ويترك صحبتَهُ حتى يُعْتِبَه ويُعْذِرَ منه؛ كما فعل الخضر مع موسى.
ومنها: أن موافقة الصاحب لصاحبه في غير الأمور المحذورة مدعاةٌ وسببٌ لبقاء الصحبة وتأكُّدها؛ كما أنَّ عدم الموافقة سببٌ لقطع المرافقة.
[ومنها: أن هذه القضايا التي أجراها الخضر هي قدر محض، أجراها اللَّه وجعلها على يد هذا العبد الصالح ليستدل العباد بذلك على ألطافه في أقضيته، وأنه يقدر على العبد أموراً يكرهها جداً وهي صلاح دينه، كما في قضية الغلام، أو وهي صلاح دنياه كما في قضية السفينة، فأراهم نموذجاً من لطفه وكرمه ليعرفوه، ويرضوا غاية الرضا بأقداره الكريهة].
{82}. ''Na ama ukuta ule" ambao niliusimamisha, ''huo ulikuwa ni wa vijana wawili mayatima kule mjini. Na chini yake ilikuwako hazina yao; na baba yao alikuwa ni mtu mwema." Yaani, hali yao inahitaji wafanyiwe upole na kuwarehemu, kwa sababu wao ni wachanga ambao walimpoteza baba yao, na Mwenyezi Mungu pia aliwahifadhi kwa sababu ya wema wa wazazi wao. ''Basi Mola wako Mlezi alitaka wafikie utu uzima wao na wajitolee hazina yao wenyewe." Na ndiyo maana niliubomoa ukuta huo, nikatoa hazina iliyokuwa chini yake, na nikaujenga tena, kisha nikairudisha hazina yao bure bila malipo. "Hii ikiwa ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi" ambayo Mwenyezi Mungu alimpa mja wake Al-Khidhr. "Wala mimi sikuyatenda hayo kwa amri yangu'' na kwa kutaka kwangu tu. Lakini hayo yalikuwa kutokana na rehema ya Mwenyezi Mungu na amri yake. ''Hiyo'' ambayo nimekufasiri "ndiyo tafsiri ya hayo ambayo wewe hukuweza kuyasubiria." Na katika kisa hiki cha ajabu na kitukufu, kunazo faida, hukumu,
na misingi mingi ambayo tutaonyesha baadhi yake kwa msaada wa Mwenyezi Mungu: Miongoni mwake ni ubora wa elimu na kusafiri kwa ajili ya kuitafuta, na kwamba hayo ndiyo mambo muhimu zaidi. Kwa maana, Musa, amani iwe juu yake, alisafiri kwenda umbali mrefu, na akapata uchovu katika kuitafuta, na akaacha kukaa pamoja na Wana wa Israili ili awafundishe na kuwaelekeza, na akachagua kusafiri ili kuongeza elimu kuliko hayo. Na miongoni mwake ni kuanza na kilicho muhimu zaidi kisha kinachokifuata kwa umuhimu. Kwa maana, kuzidisha elimu na elimu ya mwanadamu ni muhimu zaidi kuliko kuliacha hilo, na kushughulika na kufundisha pasi na kujiongezea elimu, na kuyachanganya mambo mawili haya ndio ukamilifu zaidi. Miongoni mwake ni kwamba inaruhusika kuwa na mtumishi nyumbani na safarini, ili atosheleze kazi mbalimbali na ili akupumzishe, kama alivyofanya Musa. Miongoni mwake ni kwamba mwenye kusafiri kwa ajili ya kutafuta elimu, au kushiriki katika jihadi au mengineyo ikiwa masilahi yatahitaji kujulisha anachotafuta na anakokwenda, basi hilo ni kamilizi zaidi kuliko kulificha. Kwa maana, katika kulidhihirisha kuna faida kama vile kujiandaa kwa ajili ya hili maandalizi mazuri, na ili kulifanya jambo kwa ufahamu, na kuonyesha hamu kubwa juu ya ibada hii tukufu. Kama Musa alivyosema, ''Sitaacha kuendelea mpaka nifike zinapokutana bahari mbili, au nitaendelea kwa muda mrefu.'' Na kama Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - alivyowajulisha maswahaba zake wakati alipotaka kwenda katika vita vya Tabuk kuhusu anakokwenda, pamoja na kwamba kawaida yake nikujulisha kuhusu jambo kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja, na hilo linafuatana na masilahi. Na miongoni mwake ni kufungamanisha uovu na sababu zake na Shetani kwa njia ya kushawishi na kupamba maovu. Hata kama yote hayo ni kutika hukumu na majaliwa ya Mwenyezi Mungu, kwa kauli ya kijana wa Musa, ''Na hakuna aliyenisahaulisha kulikumbuka isipokuwa Shetani tu." Na miongoni mwake ni kwamba inaruhusika kumjulisha mtu yale ambayo ni katika mambo ya kimaumbile kama vile uchovu, njaa, au kiu, ikiwa sio kwa njia ya hasira na yakawa ni ukweli. Kwa kauli ya Musa, "Kwa hakika tumepata machovu kweli kwa hii safari yetu." Na miongoni mwake ni kuwa inapendekezwa kwamba mtumishi wa mtu awe mwerevu, mwenye uelewa wa haraka, mwenye busara ili aweze kufikia kile anachotaka. Na miongoni mwake ni kwamba inapendekezwa kwa mtu kumlisha mtumishi wake kutoka katika chakula chake na kwamba wakile pamoja. Kwa sababu maana ya dhahiri ya kauli yake ''Tupe chakula chetu cha mchana'' inawafungamanisha wote nacho, na kwamba yeye Musa na kijana wake wote walikula kwacho. Miongoni mwake ni kwamba msaada unamshukia mja kulingana na kufanya kwake aliyoamrishwa, na kwamba mwenye kuafiki amri ya Mwenyezi Mungu husaidiwa kwa namna asiyosaidiwa asiyekuwa yeye. Kwa kauli yake, ''Hakika tumepata uchovu katika safari yetu hii.'' Na sehemu ya safari inayoashiriwa hapa ni ile sehemu yake waliyokuwa tayari wameshapita makutano ya bahari zile mbili. Na ama sehemu yake ya kwanza, hakulalamika kwa sababu yake uchovu wowote pamoja na urefu wake, kwa sababu ndiyo ilikuwa safari kwa uhakika. Na ama ya mwisho, basi la dhahiri ni kwamba ilikuwa baadhi ya siku, kwa sababu walimpoteza samaki wao walipokimbilia kwenye mwamba. Na la dhahiri ni kwamba walilala hapo, kisha wakaendelea kutembea kesho yake mpaka ilipokuwa ni wakati wa chakula cha mchana,
Musa akamwambia kijana wake: Tupe chakula chetu cha mchana. Basi hapo, ndipo akakumbuka kwamba alikisahau pale mahali ambapo palikuwa amepakusudia hasa. Na miongoni mwake ni kwamba mja huyo ambaye Musa alikutana naye hakuwa nabii, bali alikuwa mja mwema tu. Kwa sababu alimuelezea kwa sifa ya uja tu, na akataja neema ya Mwenyezi Mungu juu yake kwa rehema na elimu. Lakini hakutaja utume wake wala unabii wake. Na kama angekuwa nabii, basi angetaja hilo kama alivyowataja wengineo. Na ama kauli yake mwishoni mwa kisa hiki, ''Wala mimi sikutenda hayo kwa amri yangu,'' hiyo haionyeshi kuwa yeye ni nabii, lakini inaonyesha tu kwamba alifahamishwa na kuonyeshwa hayo na Mwenyezi Mungu, na wanavyofanyiwa hivyo wasiokuwa manabii pia. Kama alivyosema Yeye Mtukufu,
''Na tulimfunulia mama yake Musa kwa kumwambia: Mnyonyeshe." Na kauli yake,
"Na Mola wako Mlezi amemfunulia nyuki: Jitengenezee majumba yako.
" Na miongoni mwake ni kwamba elimu ambayo Mwenyezi Mungu anawafundisha waja wake ni ya aina mbili: elimu ya kujifundisha ambayo mja huipata kwa bidii yake na kujitahidi kwake, na aina nyingine ni elimu ya kupewa na Mwenyezi Mungu ambayo Mwenyezi Mungu humtunuku anayemneemesha kwayo katika waja wake. Kwa kauli yake, ''na tukamfunza mafunzo yaliyotoka kwetu." Na miongoni mwake ni kuwa na adabu mbele ya mwalimu na mwanafunzi kuzungumza naye kwa maneno ya upole zaidi, kama alivyosema Musa, amani iwe juu yake, "Je, nikufuate ili unifundishe kile ulichofundishwa cha uwongofu?" Akawa ameyatoa maneno kwa njia ya upole na kutafuta ushauri, na kwamba unaniruhusu kufanya hivyo au la? Na kukubali kwake kwamba ajifunze kutoka kwake. Haya ni tofauti na yale wayafanyayo wale ambao hawana adabu na wenye kiburi, ambao hawamuonyeshi mwalimu kwamba wanahitaji elimu yake. Lakini wanadai kwamba atashirikiana naye na hata anaweza kufikiria kuwa anamfundisha mwalimu wake ilhali yeye ni mjinga sana. Kwa hivyo, kujidhalilisha mbele ya mwalimu na kuonyesha kwamba anahitaji amfundishe ni katika mambo yenye manufaa zaidi kwa mwanafunzi. Na miongoni mwake ni kunyenyekea kwa yule alieye bora mbele ya yule aliye chini yake. Kwa maana, Musa bila shaka ni bora kuliko Al-Khidhr. Na miongoni mwake ni kwamba mwanachuoni bora anaweza kujifunza elimu ambayo hakuijua vilivyo kutoka kwa yule ambaye ni stadi ndani yake, hata kama atakuwa chini yake katika elimu kwa daraja nyingi. Kwa maana Musa, amani iwe juu yake, alikuwa katika Mitume wenye stahamala kubwa sana ambao Mwenyezi Mungu aliwapa elimu ambayo hakuwapa wengineo, lakini elimu hii maalumu, mja mwema Al-Khidhr alikuwa na kile ambacho Musa hawakuwa nacho. Basi ndiyo maana akafanya bidii ili ajifunze kutoka kwake. Na haipaswi kwa mwanachuoni katika elimu ya Fiqhi na hadithi akiwa na upungufu na kasoro katika elimu ya nahwu au swarf, au mfano wake miongoni mwa elimu tofautitofauti, asijifundishe kutoka kwa yule ambaye ni stadi katika hilo hata kama si mwanachuoni wa hadithi wala elimu ya Fiqhi. Na miongoni mwake ni kufungamanisha elimu na mengineyo miongoni mwa fadhila nyinginezo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kukubali hilo, na kumshukuru Mwenyezi Mungu juu yake, kauli yake, ''unifunze katika ule uwongofu uliofunzwa wewe?'' Yaani, katika yale ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu alikufundisha. Na katika hayo ni kwamba elimu yenye manufaa ni elimu inayoelekeza mtu katika mambo ya heri. Kwa hivyo, kila elimu yenye kuelekeleza sawasawa na yenye kuongoza kwenye heri na kutahadharisha na njia ya uovu njia ya kufanya hivyo, basi hiyo ni katika elimu yenye manufaa. Na chochote kisichokuwa hivyo, basi ima ni yenye madhara au haina faida, kwa kauli yake, "ili unifunze katika ule uwongofu uliofunzwa wewe?" Na miongoni mwake ni kwamba yeyote asiyekuwa na nguvu ya kusubiri juu ya kumpa usuhuba mwanachuoni na kusubiri juu ya elimu na kuwa imara sawasawa katika hilo, basi
[atakosa elimu nyingi kulingana na kutoweza kusubiri kwake katika hilo]. Kwa hivyo, yeyote asiyeweza kusubiri, hawezi kuipata elimu. Na yeyote mwenye kusubiri na akashikamana nayo, basi atapata kwayo kila kitu anachokifanyia bidii. Kama alivyosema Al-Khidhr huku akitaka Musa kumkubalia udhuru,
kwa kutaja kizuizi kilichomzuia Musa kujifunza elimu kutoka kwake: kwamba hakuweza kusubiri kuwa pamoja naye. Na miongoni mwake ni kwamba sababu kubwa ya kuweza kusubiri ni mtu kulijua sawasawa jambo hilo na kuwa na uzoefu na jambo hilo ambalo aliamrishwa alivumilie. Vinginevyo, yeyote asiyelijua au asiyejua kusudi lake, matokeo yake, wala faida yake na matunda yake, basi hatakuwa na sababu ya kusubiri juu yake. Kama alivyosema, ''Na utawezaje kusubiri yale usiyoyajua vilivyo undani wake?" Kwa hivyo akafanya sababu ya kutosubiri kwake kuwa ni kutojua kwake vyema jambo hilo. Na miongoni mwake ni amri ya kutoharakisha, kuthibitisha mambo, na kutoharakisha kutoa hukumu ya jambo mpaka mtu ajue linalotakikana na ni lipi hasa linalokusudiwa. Miongoni mwake ni kufungamanisha mambo ya baadaye ambayo ni katika matendo ya waja na mapenzi yake Mwenyezi Mungu,
na kwamba mtu asiseme chochote: Hakika mimi nitafanya hilo katika siku zijazo isipokuwa na aseme pia: Mwenyezi Mungu akipenda. Na miongoni mwake ni kwamba kuazimia kufanya kitu siyo sawa na kukifanya hasa. Kwa maana, Musa alisema, ''Inshaallah
(Mwenyezi Mungu) akipenda, utanipata ni mwenye kusubiri." Basi akaanza kuizoesha nafasi yake juu ya kusubiri lakini hakufanya hivyo. Na miongoni mwake ni kwamba ikiwa mwalimu ataona kwamba kuna masilahi katika kumzuia mwanafunzi kuuliza maswali mwanzoni juu ya baadhi ya vitu mpaka mwalimu mwenyewe awe ndiye anayemjulisha juu yake, basi inapaswa kufuata masilahi hayo, kama vile ikiwa uelewa wake ni mdogo, au akamkataza kuuliza mambo madogo ambayo mengineyo ni muhimu zaidi kuliko hayo au kwamba akili yake haiyafikii, au kuuliza swali ambalo halihusiani na jambo hilo. Na miongoni mwake, ni kuruhusiwa kusafiri baharini katika hali isipokuwa ile ambayo kuna hofu katika hilo. Na miongoni mwake ni kwamba mwenye kusahau halaumiwi kwa kusahau kwake, si kwa haki ya Mwenyezi Mungu, wala katika haki za waja wake, kwa kauli yake, "Usinichukulie kwa niliyosahau.'' Na miongoni mwake ni kwamba mtu anapaswa kuchukua katika tabia za watu na miamala yao kile cha chini zaidi na kile ambacho nafsi zao ziliweza kufanya, na wala haifai kuwatwika kile ambacho hawakiwezi au kuwafanyia ugumu na kuwachosha. Kwa maana, hili litasababisha wajitenge naye na kuchoka naye, lakini na achukue chepesi ili jambo hilo limuwiye jepesi. Na miongoni mwake ni kwamba hukumu za mambo zinahukumiwa kulingana na dhahiri zake, na zinafungamanishwa hivyo na hukumu za kidunia zinazohusiana na mali, damu, na mengineyo. Kwa maana, Musa, amani iwe juu yake, alimkataza Al-Khidhr kulitoboa lile jahazi na kumuua kijana yule, na kwamba mambo haya kwa dhahiri yake ni kwamba ni maovu, na Musa, amani iwe juu yake, hakuweza kukaa kimya juu yake katika hali isiyokuwa hii ya kuandamana kwake na Al-Khidhr. Kwa hivyo yeye, amani iwe juu yake, akaharakisha na kukimbilia kuyahukumu kulingana na hali yake ya ujumla, na wala hakuzingatia mambo hayo yaliyofungamana nayo ambayo yalimhitaji kusubiri na kutoharakisha kukataza. Miongoni mwake ni ile kanuni kubwa tukufu ambayo ni kwamba uovu mkubwa unaweza kuzuiwa kwa kutenda uovu mdogo, na yanazingatiwa masilahi makubwa zaidi kati ya masilahi mawili hayo kwa kukosa masilahi yaliyo chini kati ya hayo. Kwa maana, kumuua mvulana ni uovu, lakini kuishi kwake hadi awatie majaribio wazazi ili waiache dini yao ni uovu mkubwa kuliko huo. Na kuishi kwa mvulana huyo bila ya kumua na kuuhifadhi uhai wake, hata kama inafikiriwa kuwa ni heri, lakini heri katika kubakia dini ya wazazi wake na imani yao ni bora kuliko hiyo. Na ndiyo kwa sababu hiyo Al-Khidhr akamuua. Na chini ya kanuni hii, kuna matawi na faida mbazo hazihesabiwi. Kwa maana, suala la kushindana kwa masilahi na uharibifu yote yanaingia katika hili. Na miongoni mwake ni kwamba ni kanuni hii kuu pia ambayo ni kwamba matendo ya mtu ya katika mali ya wengine, ikiwa ni kwa masilahi bora na kuondoa uharibifu, basi hilo linaruhusiwa, hata kama ni bila ya ruhusa. Hata kama kazi yake hiyo itasababisha kuharibika kwa baadhi ya mali hiyo ya wengine, kama mja Al-Khidhr alivyolitoboa lile jahazi ili liwe na dosari ili lisalimike kutokana na kupokonywa na mfalme yule dhalimu. Kwa hivyo, lau lingechomeka, au kuzama, au mambo kama hayo katika nyumba ya mtu yoyote au mali zake, na ikawa katika kuharibu baadhi ya mali hiyo au kubomoa baadhi ya nyumba hiyo kuna usalama kwa sehemu iliyobakia, basi mtu anaruhusiwa kufanya hivyo, bali sheria imemruhusu kufanya hivyo ili kuhifadhi mali za wengine. Vivyo hivyo, ikiwa mtu dhalimu atataka kuchukua mali za wengine, na mtu akampa mali kiasi fulani ili kukomboa zilizobaki, basi hilo linaruhusiwa, hata kama ni bila ya ruhusa. Na miongoni mwake ni kwamba inaruhusiwa kufanya kazi baharini kama inavyoruhusiwa katika nchi kavu. Kwa kauli yake, "wafanyao kazi baharini,'' na hakuwakataza kazi yao hiyo. Na miongoni mwake ni kwamba masikini anaweza kuwa na mali ambazo hazimtoshelezi na wala hatoki kwa hilo nje ya jina la umasikini, kwa sababu Mwenyezi Mungu alijusha kwamba masikini hawa wana jahazi. Na miongoni mwake ni kwamba mauaji ni katika madhambi makubwa zaidi. Kwa kauli yake kuhusiana na kuuawa kwa kijana yule, "Ama hakika umefanya jambo baya kabisa!" Na miongoni mwake ni kwamba kuua kwa kisasi si jambo linalokatazwa. Kwa sababu ya kauli yake, ''wala hakuuwa." Na miongoni mwake ni kwamba mja mwema analindwa na Mwenyezi Mungu katika nafsi yake na katika kizazi chake. Na miongoni mwake ni kwamba kuwatumikia watu wema au wale wanaohusiana nao ni bora kuliko kufanya mengineyo, kwa sababu alitoa sababu ya kutoa hazina yao hiyo na kuusimamisha ukuta wao huo tena kwamba ni kwa kuwa baba yao alikuwa ni mwema. Na miongoni mwake ni kuwa na adabu mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika maneno. Kwa maana, Al-Khidr alifungamanisha kuitia kasoro jahazi ile na yeye mwenyewe, kwa kauli yake, "nilitaka kuitia dosari." Na ama heri, hiyo aliifungamanisha na Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kauli yake, ''Basi Mola wako Mlezi alitaka wafikie utu uzima wao na wajitolee hazina yao wenyewe, hii ikiwa ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi." Kama alivyosema Ibrahim, amani iwe juu yake, "Na ninapougua, ni Yeye ndiye anayeniponesha." Nao majini walisema, "Nasi hatujui kama wanatakiwa uovu wale wanaokaa kwenye ardhi au Mola wao Mlezi anawatakia uwongofu." Pamoja na kwamba yote hayo ni kwa majaliwa ya Mwenyezi Mungu na hatima yake. Na miongoni mwake ni kwamba rafiki asimwache mwenzake kwa hali yoyote ile na kuacha urafiki wake hadi atakapomlaumu na kumtaka mwenzake huyo amkubalie udhuru wake, kama vile alivyofanya Al-Khidhr alipokuwa pamoja na Musa. Na miongoni mwake ni kwamba kuafikiana kwa rafiki na mwenzake katika mambo yasiyokuwa ya haramu inachangia na ni sababu ya kubakia urafiki huo na kuusisitiza, kama vile kutoafikiana naye ni sababu ya kukatika kwa urafiki huo.
[Na miongoni mwake ni kwamba mambo haya ambayo Al-Khidhr aliyafanya ni hatima tupu, ambayo Mwenyezi Mungu aliyapitisha na akayaweka mikononi mwa mja huyu mwema ili waja waweze kuchukua hayo kama ushahidi juu ya hukumu zake. Na kwamba anaweza kumwandikia mja mambo ambayo anayachukia sana, lakini hayo ndiyo yenye kumtengenezea dini yake. Kama ilivyo katika suala la kijana yule. Na hayo ndiyo yenye kuutengeneza vyema dunia yake, kama ilivyo katika suala la jahazi lile. Kwa hivyo aliwaonyesha mfano wa upole wake na ukarimu wake ili wapate kuujua, na waridhie kabisa na hukumu zake zinazochukiza].
{وَيَسْأَلُونَكَ عَنْ ذِي الْقَرْنَيْنِ قُلْ سَأَتْلُو عَلَيْكُمْ مِنْهُ ذِكْرًا (83) إِنَّا مَكَّنَّا لَهُ فِي الْأَرْضِ وَآتَيْنَاهُ مِنْ كُلِّ شَيْءٍ سَبَبًا (84) فَأَتْبَعَ سَبَبًا (85) حَتَّى إِذَا بَلَغَ مَغْرِبَ الشَّمْسِ وَجَدَهَا تَغْرُبُ فِي عَيْنٍ حَمِئَةٍ وَوَجَدَ عِنْدَهَا قَوْمًا قُلْنَا يَاذَا الْقَرْنَيْنِ إِمَّا أَنْ تُعَذِّبَ وَإِمَّا أَنْ تَتَّخِذَ فِيهِمْ حُسْنًا (86) قَالَ أَمَّا مَنْ ظَلَمَ فَسَوْفَ نُعَذِّبُهُ ثُمَّ يُرَدُّ إِلَى رَبِّهِ فَيُعَذِّبُهُ عَذَابًا نُكْرًا (87) وَأَمَّا مَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَهُ جَزَاءً الْحُسْنَى وَسَنَقُولُ لَهُ مِنْ أَمْرِنَا يُسْرًا (88)}.
83. Na wanakuuliza kuhusu Dhul-Qarnain.
Waambie: nitawasomea baadhi ya hadithi yake. 84. Hakika Sisi tulimuimarisha katika ardhi na tukampa katika njia za kila kitu. 85.Basi akaifuata njia. 86. Mpaka alipofika machweo ya jua, akaliona linatua katika chemchemi yenye matope meusi. Na pale akawakuta kaumu fulani.
Tukasema: Ewe Dhul-Qarnain, ima uwaadhibu au uwafanyie uzuri. 87.
Akasema: Ama aliyedhulumu, basi tutamuadhibu kisha atarudishwa kwa Mola wake Mlezi, naye atamuadhibu adhabu mbaya zaidi. 88. Na ama yule mwenye kuamini na akatenda mema, basi huyo ana malipo mazuri, nasi tutamwambia lililo jepesi katika amri yetu.
#
{83} كان أهل الكتاب أو المشركون سألوا رسولَ الله - صلى الله عليه وسلم - عن قصَّة ذي القرنين، فأمره الله أن يقول: {سأتلو عليكم منه ذِكْراً}: فيه نبأٌ مفيدٌ وخطابٌ عجيبٌ؛ أي: سأتلو عليكم من أحواله ما يُتَذَكَّر فيه ويكون عبرةً، وأما ما سوى ذلك من أحواله؛ فلم يَتْلُه عليهم.
{83} Watu wa Kitabu
(Mayahudi na Manaswara) walimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - juu ya kisa cha Dhul-Qarnain. Basi na Mwenyezi Mungu akamuamrisha kwamba aseme, ''Nitawasomea baadhi ya hadithi yake;" ndani yake kuna habari muhimu na mazungumzo ya ajabu. Nitawasomea katika hali zake zitakazokuwa makumbusho na mazingatio. Na ama mambo mengineyo katika hali zake, hayo hakuwasomea.
#
{84 - 85} {إنَّا مَكَّنَّا له في الأرض}؛ أي: مَلَّكَهُ الله تعالى ومكَّنه من النفوذ في أقطار الأرض وانقيادهم له. {وآتَيْناه من كلِّ شيءٍ سبباً. فأتبع سبباً}؛ أي: أعطاه الله من الأسباب الموصلة له لما وَصَلَ إليه ما به يستعين على قهر البلدان وسهولة الوصول إلى أقاصي العمران، وعَمِلَ بتلك الأسباب التي أعطاه الله إياها؛ أي: استعملها على وجهها؛ فليس كلُّ من عنده شيءٌ من الأسباب يسلُكُه، ولا كلُّ أحدٍ يكون قادراً على السبب؛ فإذا اجتمع القدرةُ على السبب الحقيقيِّ والعملُ به؛ حصل المقصودُ، وإن عُدِما أو أحدُهما؛ لم يحصُل، وهذه الأسبابُ التي أعطاه الله إيَّاها لم يُخْبِرْنا الله ولا رسولُهُ بها، ولم تتناقَلْها الأخبارُ على وجهٍ يفيدُ العلم؛ فلهذا لا يَسَعُنا غير السكوت عنها وعدم الالتفات لما يَذْكُرُهُ النقلة للإسرائيلياتِ ونحوها، ولكنَّنا نعلم بالجملة أنَّها أسبابٌ قويَّة كثيرةٌ داخليةٌ وخارجيةٌ، بها صار له جندٌ عظيمٌ ذو عَددٍ وعُددٍ ونظام، وبه تمكَّن من قهر الأعداء ومن تسهيل الوصول إلى مشارق الأرض ومغاربها وأنحائها.
{84-85} ''Hakika Sisi tulimuimarisha katika ardhi." Yaani, Mwenyezi Mungu Mtukufu alimmilikisha na akamuimarisha katika kuendesha pande za ardhi na watu hao wote kumtii yeye. ''Na tukampa katika njia za kila kitu." "Basi akaifuata njia.'' Yaani, Mwenyezi Mungu alimpa katika njia zilizomfikisha alichofikia, ambazo alijisaidia kwazo katika kushinda nchi, na zikampa wepesi wa kufika mwisho wa mafanikio. Na alizitumia njia hizo ambazo Mwenyezi Mungu alimpa katika matumizi yanayozifaa. Kwa maana, siyo kila mtu aliye na njia zozote zile, anazifuata, wala siyo kila mtu ana uwezo wa kuzifikia njia hizo. Kwa hivyo, unapokutana uwezo wa kufikia njia ya uhakika na kuifanyia kazi njia hiyo, basi jambo lililokusudiwa linapatikana. Na mawili hayo yakikosekana au mojawapo, basi hayafikiwi makusudio. Na njia hizi ambazo Mwenyezi Mungu alimpa, Yeye Mwenyezi Mungu hakutuambia kuzihusu, wala Mtume wake pia hakutuambia. Kwa hivyo habari zilizotufikia hazikuzifikisha kwa njia ambayo inaelimisha. Basi ndiyo sababu hatuwezi isipokuwa kunyamaza kimya kuhusiana nazo, na kutoyazingatia yale ambayo Wana wa Israili na mfano wao wanataja. Lakini tunajua kwa ujumla kwamba ni njia nyingi zenye nguvu, za ndani na za nje, ambazo kwazo aliweza kupata jeshi kubwa lenye idadi kubwa, na zama za nguvu, na nidhamu nzuri. Na kwazo aliweza kushinda maadui wake na zikamuwezesha kufika mashariki ya ardhi na magharibi yake, na pande zake zinginezo.
#
{86} فأعطاه الله ما بلغ به {مغربَ الشمس}، حتى رأى الشمس في مرأى العين كأنها {تَغْرُبُ في عينٍ حمئةٍ}؛ أي: سوداء، وهذا المعتاد لمن كان بينه وبين أفُقِ الشمس الغربيِّ ماءٌ؛ رآها تغرُبُ في نفس الماء، وإنْ كانت في غاية الارتفاع. {ووجَدَ عندها}؛ أي: عند مغربها {قوماً قُلْنا يا ذا القرنينِ إمَّا أن تُعَذِّبَ وإمَّا أن تَتَّخِذَ فيهم حُسْناً}؛ أي: إما أن تعذبهم بقتل أو ضرب أو أسرٍ ونحوه، وإما أن تُحْسِنَ إليهم؛ فخُيِّرَ بين الأمرين؛ لأنَّ الظاهر أنهم [إما] كفارٌ أو فساقٌ أو فيهم شيءٌ من ذلك؛ لأنَّهم لو كانوا مؤمنين غير فساق؛ لم يرخَّصْ له في تعذيبهم.
{86} Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akampa kile alichofika
kwacho "machweo ya jua," hadi akaliona jua kulingana na kuona kwa macho kana kwamba "linatua katika chemchemi yenye matope meusi." Na hili ni la kawaida kwa yule ambaye kuna maji baina yake na upeo wa jua wa magharibi. Aliliona likitua katika maji hayo, hata ingawa lilikuwa limeinuka juu sana. "Na pale akawakuta kaumu fulani.
Tukasema: Ewe Dhul-Qarnain, ima uwaadhibu" kwa kuwaua, au kuwapiga, au kuwateka au mfano wake, "au uwafanyie uzuri." Kwa hivyo akapewa chaguo kati ya mambo hayo mawili. Kwa sababu, ilionekana kwa dhahiri kwamba wao
[ima] ni makafiri au watu wavukao mipaka au ndani yao kuna mambo kama hayo. Kwa sababu wangekuwa waumini wasiovuka mipaka, basi asingeruhusiwa kuwaadhibu.
#
{87} فكان عند ذي القرنين من السياسة الشرعيَّة ما استحقَّ به المدح والثناء؛ لتوفيق الله له لذلك، فقال: سأجعلهم قسمين: {أمَّا مَنْ ظَلَمَ}: بالكفر، {فسوف نعذِّبُه ثم يردُّ إلى ربِّه فيعذِّبه عذاباً نُكْراً}؛ أي: تحصُلُ له العقوبتان؛ عقوبة الدنيا، وعقوبة الآخرة.
{87} Naye Dhul-Qarnayn alikuwa na sera katika mambo ya kisheria ambayo kwayo alistahili kutajwa kwa uzuri na kusifiwa, kwa sababu Mwenyezi Mungu alimuwezesha kuyafikia hayo.
Akasema: Nitawafanya kuwa makundi mawili: ''Ama aliyedhulumu'' kwa ukafiri, ''basi tutamuadhibu, kisha atarudishwa kwa Mola wake Mlezi, naye atamuadhibu adhabu mbaya zaidi." Yaani,
atapata adhabu mbili: adhabu ya duniani na adhabu ya Akhera.
#
{88} {وأمَّا مَنْ آمن وعمل صالحاً فله جزاء الحُسْنى}؛ أي: فله الجنة والحالة الحسنة عند الله جزاءً يوم القيامة. {وسنقولُ له من أمرِنا يُسْراً}؛ أي: وسنُحْسِنُ إليه ونَلْطُفُ له بالقول ونيسِّر له المعاملة. وهذا يدلُّ على كونه من الملوك الصالحين [و] الأولياء العادلين العالمين؛ حيث وافق مرضاةَ الله في معاملة كلِّ أحدٍ بما يليق بحاله.
{88} "Na ama yule mwenye kuamini na akatenda mema, basi huyo ana malipo mazuri." Yaani, atapata Pepo na hali nzuri kwa Mwenyezi Mungu, yawe ndiyo malipo yake siku ya Qiyama. "Nasi tutamwambia lililo jepesi katika amri yetu." Yaani, tutamtendea mazuri, na kusema naye kwa upole, na kuamiliana naye kwa urahisi. Na hili linaonyesha kwamba yeye ni miongoni mwa wafalme wema
[na] vipenzi wa Mwenyezi Mungu waadilifu, wenye elimu, kwa maana aliafikiana na yanayomridhisha Mwenyezi Mungu katika kuamiliana na kila mtu kwa yale yanayoifailia hali yake.
{ثُمَّ أَتْبَعَ سَبَبًا (89) حَتَّى إِذَا بَلَغَ مَطْلِعَ الشَّمْسِ وَجَدَهَا تَطْلُعُ عَلَى قَوْمٍ لَمْ نَجْعَلْ لَهُمْ مِنْ دُونِهَا سِتْرًا (90) كَذَلِكَ وَقَدْ أَحَطْنَا بِمَا لَدَيْهِ خُبْرًا (91) ثُمَّ أَتْبَعَ سَبَبًا (92) حَتَّى إِذَا بَلَغَ بَيْنَ السَّدَّيْنِ وَجَدَ مِنْ دُونِهِمَا قَوْمًا لَا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ قَوْلًا (93) قَالُوا يَاذَا الْقَرْنَيْنِ إِنَّ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ فَهَلْ نَجْعَلُ لَكَ خَرْجًا عَلَى أَنْ تَجْعَلَ بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمْ سَدًّا (94) قَالَ مَا مَكَّنِّي فِيهِ رَبِّي خَيْرٌ فَأَعِينُونِي بِقُوَّةٍ أَجْعَلْ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُمْ رَدْمًا (95) آتُونِي زُبَرَ الْحَدِيدِ حَتَّى إِذَا سَاوَى بَيْنَ الصَّدَفَيْنِ قَالَ انْفُخُوا حَتَّى إِذَا جَعَلَهُ نَارًا قَالَ آتُونِي أُفْرِغْ عَلَيْهِ قِطْرًا (96) فَمَا اسْطَاعُوا أَنْ يَظْهَرُوهُ وَمَا اسْتَطَاعُوا لَهُ نَقْبًا (97) قَالَ هَذَا رَحْمَةٌ مِنْ رَبِّي فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ رَبِّي جَعَلَهُ دَكَّاءَ وَكَانَ وَعْدُ رَبِّي حَقًّا (98)}.
89. Kisha akaifuata njia. 90. Hata alipofika machomozeo ya jua, akaliona linawachomozea kaumu ambao hatukuwawekea pazia ya kuwakinga kutokana nalo. 91. Vivyo hivyo. Na Sisi tulizijua vilivyo habari zake zote. 92. Kisha akaifuata njia. 93. Hata alipofika katikati ya milima miwili, alikuta nyuma yake kaumu ambao walikaribia kutofahamu neno lolote. 94.
Wakasema: Ewe Dhul-Qarnain! Hakika Yaajuju na Maajuju wanafanya uharibifu katika ardhi. Basi je, tukupe ujira ili utie baina yetu na baina yao kizuizi? 95.
Akasema: yale ambayo Mola wangu Mlezi ameniimarisha ndani yake ndiyo bora zaidi. Lakini nisaidieni kwa nguvu. Nitaweka baina yenu na baina yao kizuizi imara. 96. Nileteeni vipande vya chuma. Hata alipoijaza sawasawa nafasi iliyo katikati ya milima miwili hiyo, akasema, "Pulizeni moto" mpaka alipokifanya kuwa moto, akasema, " Nileteeni shaba iliyoyeyuka niimimine juu ya chuma hicho." 97. Basi hawakuweza kukikwea, wala hawakuweza kukitoboa. 98. Akasema, "Hii ni rehema kutoka kwa
Mola wangu Mlezi. Na itakapokuja ahadi ya Mola wangu Mlezi, atakivunjavunja. Na ahadi ya Mola wangu Mlezi ni ya kweli."
#
{89} أي: لما وصل إلى مغرب الشمس؛ كرَّ راجعاً، قاصداً مطلعها، متَّبعاً للأسباب التي أعطاه الله.
{89} Yaani, alipofika machweo ya jua, akafunga safari ya kurudi, akaelekea machomozeo yake, akifuata njia ambazo Mwenyezi Mungu alimpa.
#
{90} فوصل إلى مطلع الشمس فـ {وجدها تطلُعُ على قومٍ لم نجعل لهم من دونِها سِتْراً}؛ أي: وجدها تطلُعُ على أناس ليس لهم سترٌ من الشمس: إما لعدم استعدادِهم في المساكن، وذلك لزيادة همجيَّتهم وتوحُّشهم وعدم تمدُّنهم، وإما لكون الشمس دائمة عندهم لا تغرُبُ [عنهم] غروباً يُذكر؛ كما يوجد ذلك في شرقيِّ إفريقيا الجنوبي، فوصل إلى موضع انقطع عنه علمُ أهل الأرض فضلاً عن وصولهم إياه بأبدانهم.
{90} Basi akafika machomozeo ya jua, kwa hivyo "akaliona linawachomozea kaumu ambao hatukuwawekea pazia ya kuwakinga kutokana nalo." Ima kwa sababu ya kutokuwa kwao na maandalizi kabambe katika makazi yao, kwa sababu ya ukatili wao mwingi na unyama wao, na kutokuwa na ustaarabu. Au ima kwa sababu jua liliwaka kwao daima bila ya kuchwea, kuchwea kunakoweza kutajwa, kama ilivyo katika mashariki mwa Afrika ya kusini. Kwa hivyo, akafikia mahali ambapo elimu ya watu walio katika ardhi haikufika huko, achilia mbali wao kufika huko kwa miili yao.
#
{91} ومع هذا؛ فكلُّ هذا بتقدير الله له وعلمه به، ولهذا قال: {كذلك وقَدْ أَحَطْنا [بما لديه خبراً}؛ أي:] بما عنده من الخير والأسباب العظيمة، وعِلْمُنا معه حيثما توجَّه وسار.
{91} Na pamoja ya haya, haya yote ni kwa majaliwa ya Mwenyezi Mungu na Yeye kuyajua, na ndiyo maana akasema, "Ndiyo kama hivyo. Na Sisi tulizijua vilivyo habari zake zote." Ya heri aliyo nayo, na njia kubwa, na elimu yetu iko pamoja naye popote anapoelekea.
#
{92 - 93} {ثم أتبع سبباً. حتى إذا بلغ بين السَّدَّيْن}: قال المفسِّرون: ذهب متوجِّهاً من المشرق قاصداً للشمال، فوصل إلى ما بين السدَّيْن، وهما سدَّان كانا معروفين في ذلك الزمان، سدَّان من سلاسل الجبال المتَّصلة يمنةً ويسرةً، حتى تتصل بالبحار ، بين يأجوجَ ومأجوجَ وبين الناس، {وجد}: من دون السدين {قوماً لا يكادون يفقهون قولاً}؛ لعُجْمَةِ ألسنتهم واستعجام أذهانِهِم وقلوبهم.
{92- 93} ''Kisha akaifuata njia.
'' "Hata alipofika katikati ya milima miwili" Wafasiri walisema: Alikwenda kutoka Mashariki kuelekea Kaskazini, na akafika katikati ya milima miwili. Nayo ilikuwa inajulikana katika wakati huo, miongoni mwa safu ya milima iliyounagana upande wa kulia na wa kushoto mpaka iungane na bahari, kati ya Yaajuju na Maajuju na watu, "alikuta" kati ya milima hiyo miwili "kaumu ambao walikaribia kutofahamu neno lolote." Kwa sababu ya ugeni wa lugha yao na kutofahamu kwa akili zao na nyoyo zao.
#
{94} وقد أعطى الله ذا القرنين من الأسباب العلميَّة ما فقه به ألسنة أولئك القوم وفقههم وراجعهم وراجعوه، فاشْتَكَوا إليه ضرر يأجوج ومأجوج، وهما أمَّتان عظيمتان من بني آدم، فقالوا: {إنَّ يأجوج ومأجوجَ مفسدون في الأرض}: بالقتل وأخذ الأموال وغير ذلك. {فهل نَجْعَلُ لك خَرْجاً}؛ أي: جُعْلاً؛ {على أن تجعلَ بيننا وبينَهم سدًّا}: ودلَّ ذلك على عدم اقتدارهم بأنفسهم على بنيان السدِّ، وعرفوا اقتدار ذي القرنين عليه، فبذلوا له أجرةً ليفعل ذلك، وذكروا له السببَ الداعي، وهو إفسادهم في الأرض.
{94} Mwenyezi Mungu alimpa Dhul-Qarnain njia za kielimu ambazo kwazo aliweza kufahamu lugha za kaumu wale na ufahamu wao wa kisheria, na akawaongea na wao, nao wakamuongelesha. Kwa hivyo, wakamlalamikia kuhusu madhara yaliyofanywa na Yaajuju na Maajuju, ambao walikuwa umma mbili kubwa kubwa za wanadamu. Wakasema, "Hakika Yaajuju na Maajuju wanafanya uharibifu katika ardhi" kwa kuua na kuchukua mali na mengineyo. "Basi je, tukupe ujira ili utie baina yetu na baina yao kizuizi?" Na hilo lilionyesha kwamba wao wenyewe hawakuweza kukijenga kizuizi hicho, na wakajua uwezo wa Dhul-Qarnain wa kufanya hivyo. Kwa hivyo wakampa malipo ili afanye hivyo, na wakamtajia sababu ya hilo, ambayo ni uharibifu wao
(Yaajuju na Maajuju) katika ardhi.
#
{95} فلم يكن ذو القرنين ذا طمع ولا رغبةٍ في الدُّنيا ولا تاركاً لإصلاح أحوال الرعيَّة، بل قصدُهُ الإصلاح؛ فلذلك أجاب طلبتهم؛ لما فيها من المصلحة، ولم يأخذ منهم أجرةً، وشَكَرَ ربَّه على تمكينه واقتداره، فقال لهم: {ما مَكَّنِّي فيه ربِّي خيرٌ}؛ أي: مما تبذلون لي وتعطوني، وإنَّما أطلب منكم أن تعينوني بقوَّةٍ منكم بأيديكم؛ {أجْعَلْ بينَكم وبينهم رَدْماً}؛ أي: مانعاً من عبورهم عليكم.
{95} Lakini Dhul-Qarnain hakuwa na tamaa wala kupenda dunia wala hakuacha kurekebisha hali ya wale walio chini ya uchungaji wake. Bali makusudio yake yalikuwa ni kuwarakebisha na kuwatengeneza vyema. Na ndiyo maana aliwaitikia ombi lao hilo, kwa sababu ya masilahi yaliyo ndani yake, na wala hakuchukua malipo yoyote kutoka kwao, na akamshukuru Mola wake Mlezi kwa kumuimarisha na kumpa uwezo. Akawaambia, "yale ambayo Mola wangu Mlezi ameniimarisha ndani yake ndiyo bora zaidi." Yaani, kuliko hayo mnayotoa ili kunilipa. Lakini ninaomba tu mnisaidie kwa nguvu kwa mikono yenu. ''Nitaweka baina yenu na baina yao kizuizi imara" kitakachowazuia Yaajuju na Maajuju kukivuka na kuwajia.
#
{96} {آتوني زُبَرَ الحديدِ}؛ أي: قطع الحديد، فأعْطَوْه ذلك، {حتى إذا ساوى بين الصَّدَفين}؛ أي: الجبلين اللذين بُني بينهما السدُّ، {قال انفُخوا}: النار؛ أي أوقدوها إيقاداً عظيماً واستعملوا لها المنافيخ لتشتدَّ فتذيبَ النحاس، فلما ذاب النحاس الذي يريُد أن يُلْصِقَهُ بين زُبَرِ الحديد، {قال آتوني أفْرِغْ عليه قِطْراً}؛ أي: نحاساً مذاباً، فأفرغ عليه القطر، فاستحكم السدُّ استحكاماً هائلاً، وامتنع به من وراءه من الناس من ضرر يأجوج ومأجوج.
{96} "Nileteeni vipande vya chuma." Yaani, kipande cha chuma; nao wakampa. "Hata alipojaza sawasawa nafasi iliyo katikati ya milima miwili hiyo,
akasema: pulizeni moto" mkubwa, na tumieni vipulizio ili uwe mkali na uyeyushe shaba hiyo. Na ilipoyeyuka shaba hiyo ambayo alitaka kuiunganishia kati ya vipande vile vya chuma.
"Akasema: nileteeni shaba iliyoyeyuka niimimine juu ya chuma hicho." Kwa hivyo akaiminina shaba hiyo, na kizuizi hicho kikaimarika kuimarika kukubwa mno, na wakazuiwa kwacho watu walio nyuma yake kudhuriwa na Yaajuju na Maajuju.
#
{97} {فما اسطاعوا أن يظهروه وما استطاعوا له نَقْباً}؛ أي: فما لهم استطاعةٌ ولا قدرةٌ على الصعود عليه؛ لارتفاعِهِ، ولا على نقبِهِ؛ لإحكامِهِ وقوَّته.
{97} "Basi hawakuweza kukikwea, wala hawakuweza kukitoboa." Yaani, hawakuwa na uwezo wala nguvu wa kupanda juu yake kwa sababu ya urefu wake, na kina chake, na uimara wake, na nguvu yake.
#
{98} فلما فَعَلَ هذا الفعل الجميل والأثر الجليل؛ أضاف النعمةَ إلى موليها، وقال: {هذا رحمةٌ من ربِّي}؛ أي: من فضله وإحسانه عليَّ، وهذه حال الخلفاء والصالحين إذا منَّ الله عليهم بالنِّعم الجليلة؛ ازدادَ شكرُهُم وإقرارُهُم واعترافُهم بنعمة الله؛ كما قال سليمانُ عليه السلام لما حَضَرَ عنده عرشُ ملكة سبأ مع البعد العظيم؛ قال: {هذا من فضل ربِّي لِيَبْلُوَني أأشكُرُ أم أكْفُرُ}؛ بخلاف أهل التجبُّر والتكبُّر والعلوِّ في الأرض؛ فإنَّ النعم الكبار تزيدُهم أشراً وبطراً؛ كما قال قارونُ لما آتاه الله من الكنوز ما إنَّ مفاتِحَهُ لتنوءُ بالعُصْبَةِ أولي القوَّة؛ قال: {إنَّما أوتيتُهُ على علم عندي}. وقوله: {فإذا جاء وعدُ ربِّي}؛ أي: لخروج يأجوج ومأجوج. {جَعَلَه}؛ أي: ذلك السدَّ المحكم المتقن {دَكَّاءَ}؛ أي: دكَّه فانهدم، واستوى هو والأرض، {وكان وعدُ ربِّي حقًّا}.
{98} Alipofanya kitendo hiki kizuri na kumbukumbu iliyokuwa kubwa, akaifungamanisha neema hii na yule aliyemneemesha kwayo, akasema, "Hii ni rehema kutoka kwa Mola wangu Mlezi." Yaani, ni katika fadhila zake na wema wake juu yangu. Na hii ndiyo hali ya makhalifa na watu wema, Mwenyezi Mungu anapowaneemesha kwa neema kubwa, inazidi shukrani yao, kukiri kwao na kukubali kwao neema ya Mwenyezi Mungu. Kama vile Suleiman, amani iwe juu yake, aliposema wakati kilipohudhuria kiti cha enzi cha malkia wa Sabai pamoja na kwamba kilikuwa mbali sana, akasema, "Haya ni katika fadhila za Mola wangu Mlezi, ili anijaribu nitashukuru au nitakufuru" tofauti na watu wanaotakabari na kufanya kiburi katika ardhi. Kwa maana, neema kubwa huwazidishia hao uovu na kujiona, kama alivyosema Qaarun wakati Mwenyezi Mungu alipompa hazina ambazo funguo zake zinawatopeza watu wenye nguvu kuzichukua. Akasema, "Kwa hakika, nimepewa haya kwa sababu ya elimu niliyo nayo." Na kauli yake, "Na itakapokuja ahadi ya Mola wangu Mlezi'', ili watoke Yaajuju na Maajuju; "atakivunjavunja." Yaani, kizuizi hicho madhubuti na kitabomoka mpaka kiwe sawia na ardhi. "Na ahadi ya Mola wangu Mlezi ni ya kweli.''
{وَتَرَكْنَا بَعْضَهُمْ يَوْمَئِذٍ يَمُوجُ فِي بَعْضٍ وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَجَمَعْنَاهُمْ جَمْعًا (99)}.
99. Na tutawaacha siku hiyo wachanganyike wao kwa wao na litapulizwa baragumu, hapo tutawakusanya wote pamoja.
#
{99} يحتمل أنَّ الضمير يعودُ إلى يأجوج ومأجوج، وأنَّهم إذا خرجوا على الناس من كثرتهم واستيعابهم للأرض كلِّها يموجُ بعضُهم ببعضٍ؛ كما قال تعالى: {حتَّى إذا فُتِحَتْ يأجوجُ ومأجوجُ وهم من كُلِّ حَدَبٍ يَنسِلونَ}، ويُحتمل أن الضمير يعود إلى الخلائق يوم القيامة، وأنَّهم يجتمعون فيه، فيكثرون، ويموجُ بعضهم ببعض من الأهوال والزلازل العظام؛ بدليل قوله:
{99} Inawezekana kwamba neno "tutawaacha" linamaanisha Yaajuju na Maajuju, na kwamba watakapowatokea watu, kwa sababu ya wingi wao na kujaa kwao katika ardhi yote, wachanganyike wao kwa wao. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Hata watakapofunguliwa Yaajuju na Maajuju wakawa wanateremka kutoka kila mlima.'' Na inawezekana kwamba neno "tutawaacha" linawarudia viumbe wote Siku ya Qiyama, na kwamba watakusanyika ndani yake, na wawe wengi, na wasonganesongane wao kwa wao kwa sababu ya uzito na dhiki na mitetemeko mikubwa.
Kwa ushahidi wa kauli yake:
{وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَجَمَعْنَاهُمْ جَمْعًا (99) وَعَرَضْنَا جَهَنَّمَ يَوْمَئِذٍ لِلْكَافِرِينَ عَرْضًا (100) الَّذِينَ كَانَتْ أَعْيُنُهُمْ فِي غِطَاءٍ عَنْ ذِكْرِي وَكَانُوا لَا يَسْتَطِيعُونَ سَمْعًا (101)}.
99. Na tutawaacha baadhi yao siku hiyo wachanganyike wao kwa wao, na litapulizwa baragumu, hapo tutawakusanya wote pamoja. 100. Na siku hiyo tutawadhihirishia wazi Jahannamu makafiri waione. 101. Wale ambao macho yao yalikuwa paziani hawanikumbuki, na wakawa hawawezi kusikia.
#
{99} أي: إذا نفخ إسرافيل في الصور؛ أعاد الله الأرواح إلى الأجساد، ثمَّ حَشَرَهم وجمعهم لموقف القيامة، الأوَّلين منهم والآخرين، والكافرين والمؤمنين؛ ليُسألوا، ويُحاسبوا، ويُجزون بأعمالهم.
{99} Yaani, Israfil atakapolipuliza katika baragumu, Mwenyezi Mungu atazirudisha roho zote katika viwiliwili, kisha atawakusanya katika pahali pa kusimama katika Siku ya Qiyama. Atawakusanya wa kwanza katika wao na wa mwisho, makafiri na waumini ili waulizwe, na wahesabiwe, na walipwe kwa matendo yao.
#
{100} فأما الكافرون على اختلافهم؛ فإنَّ جهنم جزاؤهم خالدين فيها أبداً، ولهذا قال: {وعَرَضْنا جهنَّم يومئذٍ للكافرينَ عرضاً}؛ كما قال تعالى: {وإذا الجحيمُ سعرت}؛ أي: عُرِضَتْ لهم لتكون مأواهم ومنزلهم، وليتمتَّعوا بأغلالها وسعيرها وحميمها وزمهريرها، وليذوقوا من العقاب ما تبكم له القلوبُ، وتصمُّ الآذان.
{100} Ama makafiri pamoja na utofauti wa itikadi zao, hao malipo yao yatakuwa Jahannamu, watadumu humo milele. Na ndiyo maana akasema, "Na siku hiyo tutawadhihirishia wazi Jahannamu makafiri waione." Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema, "Na Jahim itakapozidishwa kuwashwa" ili iwe makao yao na mashukio yao, na ili wafurahie kwa pingu zake, na mwako wake mkali, na maji yake ya moto, baridi yake kali, ili waonje adhabu ambayo mioyo itakuwa bubu kutokana nayo, na masikio yao yawe na uziwi.
#
{101} وهذا آثار أعمالهم وجزاء أفعالهم؛ فإنَّهم في الدُّنيا كانت أعينُهم في غطاءٍ عن ذكر الله؛ أي: معرضين عن الذكر الحكيم والقرآن الكريم، {وقالوا قلوبُنا في أكِنَّةٍ مما تَدْعونا إليه}، وفي أعينهم أغطيةٌ تمنعهم من رؤية آيات الله النافعة؛ كما قال تعالى: {وعلى أبصارِهم غِشاوةٌ}. {وكانوا لا يستطيعونَ سمعاً}؛ أي: لا يقدرون على سمع آيات الله، الموصلة إلى الإيمان؛ لبغضهم القرآن والرسول؛ فإنَّ المبغِضَ لا يستطيع أن يلقي سمعه إلى كلام من أبغضه؛ فإذا انحجبتْ عنهم طرقُ العلم والخير؛ فليس لهم سمعٌ ولا بصرٌ ولا عقلٌ نافعٌ؛ فقد كفروا بالله، وجحدوا آياته، وكذَّبوا رسله، فاستحقُّوا جهنَّم، وساءت مصيراً.
{101} Na hizi ndizo athari za matendo yao na malipo ya vitendo vyao. Kwa maana, wao katika dunia hii, macho yao yalikuwa yamefunikwa kutokana na kumkumbuka Mwenyezi Mungu, wakawa wamelipa mgongo jambo la kumkumbuka Mwenyezi Mungu, Mwenye hekima, na Qur-ani Tukufu.
''Na wakasema: nyoyo zetu ziko katika vifuniko kwa yale unayotuitia.'' Na machoni mwao kuna vizibo vinavyowazuia kuona ishara za Mwenyezi Mungu zenye manufaa. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na kwenye macho yao kuna vifuniko.'' "Na wakawa hawawezi kusikia" ishara za Mwenyezi Mungu zinazofikisha katika Imani; kwa kuwa waliichukia Qur-ani na Mtume. Kwa maana, mwenye kuchukia hawezi kuyapa masikio yake maneno ya yule ambaye yeye anamchukia. Kwa hivyo, zinapozuilika njia za kupata elimu na heri, basi hawana uwezo wa kusikia wala kuona wala hawana akili yenye kunufaisha. Kwa kuwa walimkufuru Mwenyezi Mungu, na wakazikataa Ishara zake, na wakawakadhibisha Mitume wake, basi wakastahiki Jahannam, na hayo ndiyo maishio mabaya mno.
{أَفَحَسِبَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنْ يَتَّخِذُوا عِبَادِي مِنْ دُونِي أَوْلِيَاءَ إِنَّا أَعْتَدْنَا جَهَنَّمَ لِلْكَافِرِينَ نُزُلًا (102)}
102. Je, wanadhani wale waliokufuru kwamba watawafanya waja wangu kuwa vipenzi wao badala yangu Mimi? Hakika Sisi tumeiandaa Jahannamu iwe ndipo pahali pa kuteremkia pa makafiri.
#
{102} وهذا برهانٌ وبيانٌ لبطلان دعوى المشركين الكافرين، الذين اتَّخذوا بعض الأنبياء والأولياء شركاء لله يعبُدونهم، ويزعمون أنَّهم يكونون لهم أولياء، ينجُّونهم من عذاب الله، ويُنيلونهم ثوابه، وهم قد كفروا بالله وبرسوله ، يقول الله لهم على وجه الاستفهام والإنكار المتقرِّر بطلانه في العقول: {أفَحَسِبَ الذين كفروا أن يَتَّخِذوا عبادي من دوني أولياءَ}؛ أي: لا يكون ذلك، ولا يوالي وليُّ الله معادياً لله أبداً؛ فإنَّ الأولياء موافقون لله في محبَّته ورضاه وسخطه وبغضه، فيكون على هذا المعنى مشابهاً لقوله تعالى: {ويوم يَحْشُرُهم جميعاً ثم يقولُ للملائكةِ أهؤلاءِ إيَّاكُم كانوا يعبُدونَ * قالوا سبحانك أنت وَلِيُّنا من دونِهِم}؛ فمن زعم أنه يتَّخِذُ وليَّ الله وليًّا له وهو معادٍ لله؛ فهو كاذبٌ. ويُحتمل ـ وهو الظاهر ـ أنَّ المعنى: أفحسِبَ الكفارُ بالله المنابذون لرسلِهِ أن يتَّخذوا من دونِ الله أولياء ينصرونهم وينفعونهم من دونِ الله ويدفعونَ عنهم الأذى؟ هذا حسبانٌ باطلٌ وظنٌّ فاسدٌ؛ فإنَّ جميع المخلوقين ليس بيدهم من النفع والضرِّ شيءٌ، ويكون هذا كقوله تعالى: {قل ادْعوا الذين زَعَمْتُم من دونِهِ فلا يملِكونَ كَشْفَ الضُّرِّ عنكم ولا تحويلاً}، {ولا يملِكُ الذين يدعونَ من دونِهِ الشفاعةَ}. ونحو ذلك من الآيات التي يَذْكُرُ الله فيها أن المتَّخِذ من دونه وليًّا ينصُرُه ويواليه ضالٌّ خائبُ الرجاء غير نائل لبعض مقصودِهِ. {إنَّا أعْتَدْنا جهنَّمَ للكافرين نُزُلاً}؛ أي: ضيافة وقِرىً؛ فبئس النُّزل نُزُلهم، وبئست جهنم ضيافتهم.
{102} Na huu ni uthibitisho na ubainisho wa ubatili wa madai ya washirikina makafiri, ambao waliwachukua baadhi ya manabii na vipenzi wa Mwenyezi Mungu kuwa washirika wa Mwenyezi Mungu wakawa wanawaabudu. Na wakadai kwamba watakuwa vipenzi walinzi wao, ili wawaokoe kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na wawape thawabu zake, nao walimkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Basi Mwenyezi Mungu anawaambia kwa njia ya kuuliza na kukanusha kusikopingika kwa maana huo ni ubatili wake katika akili, "Je, wanadhani wale waliokufuru kwamba watawafanya waja wangu kuwa vipenzi wao?" Yaani, hilo haliwi, na wala kipenzi cha Mwenyezi Mungu kamwe hawezi kumfanya adui wa Mwenyezi Mungu. Kwa maana vipenzi wake wanakubaliana na Mwenyezi Mungu katika upendo wake, kuridhia kwake, hasira zake na chuki yake. Na kwa maana hii, aya hii inakuwa sawa na kauli yake yeye Mtukufu, "Na siku atakayowakusanya wote,
kisha atawaambia Malaika: Je,
hawa walikuwa wakiwaabudu nyinyi? Watasema: Subhanak
(Umetakasika). Wewe ndiye kipenzi chetu, si hao." Kwa hivyo, yeyote yule anayedai kwamba amemchukua kipenzi cha Mwenyezi Mungu kuwa ni kipenzi wake ilhali yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu, basi yeye ni mwongo. Na inawezekana kwamba - nayo hii ndiyo maana ya dhahiri -
maana yake ni kuwa: Je, wale waliomkufuru Mwenyezi Mungu na kuwafanyia uadui Mitume wake kuwa watawafanya badala ya Mwenyezi Mungu, vipenzi wa kuwanusuru na kuwanufaisha kando na Mwenyezi Mungu na kuwazuia madhara? Hii ni dhana batili na mbovu. Kwa maana, viumbe vyote havina chochote mikononi mwao cha kunufaisha na kudhuru. Na hii ni kama kauli yake yeye Mtukufu,
"Sema: Waombeni hao mnaowadaia badala yake Yeye. Hawawezi kuwaondolea madhara, wala kuyaweka pengine." "Wala hao ambao wao wanawaomba badala yake Yeye hawana uwezo wa kumwombea mtu." Na mfano wa hizo miongoni mwa Aya ambazo Mwenyezi Mungu anataja ndani yake kwamba yule anayechukuwa badala yake kipenzi ili amnusuru na kumlinda, ni mpotevu ambaye ameambulia patupu katika matarajio yake, ambaye hawezi pata baadhi ya makusudio yake. "Hakika Sisi tumeiandaa Jahannamu iwe ndipo pahali pa kuteremkia pa makafiri;" kama wageni na makaribisho kwao. Basi mashukio maovu mno ni mashukio yao hayo. Na makaribisho maovu mno ni hayo yao ya Jahannam.
{قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُمْ بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا (103) الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا (104) أُولَئِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ وَلِقَائِهِ فَحَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَلَا نُقِيمُ لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَزْنًا (105) ذَلِكَ جَزَاؤُهُمْ جَهَنَّمُ بِمَا كَفَرُوا وَاتَّخَذُوا آيَاتِي وَرُسُلِي هُزُوًا (106)}.
103.
Sema: Je, tuwatajieni wenye hasara mno katika vitendo vyao? 104. Ni wale ambao juhudi yao katika uhai wa dunia ilipotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya matendo mazuri. 105. Hao ni wale waliozikufuru Ishara za Mola wao Mlezi na kukutana naye. Kwa hivyo matendo yao yakapotea bure, na wala Siku ya Qiyama hatutawasimamishia mizani yoyote. 106. Hayo ndiyo malipo yao, Jahannam, kwa walivyokufuru na wakafanyia stihizai Ishara zangu na Mitume wangu.
#
{103} أي: قل يا محمدُ للناس على وجه التحذير والإنذار: هل أخبِرُكُم بأخسر الناس {أعمالاً} على الإطلاق؟
103. Yaani, sema, ewe Muhammad,
uwaambie watu kwa namna ya kuwatahadharisha na kuwaonya: Je, niwaambieni watu wenye hasara kubwa zaidi kuliko wote "katika vitendo vyao?"
#
{104} {الذين ضلَّ سعيُهم في الحياة الدُّنيا}؛ أي: بطل واضمحلَّ كلُّ ما عملوه من عمل، {وهم يحسبون أنَّهم} محسنونَ في صنعه؛ فكيف بأعمالهم التي يعلمون أنها باطلةٌ وأنَّها محادَّةٌ لله ورسله ومعاداة؟!
{104} "Ni wale ambao juhudi yao katika uhai wa dunia ilipotea bure." Yaani, yalibatilika na kupotelea mbali matendo yao yote waliyoyatenda. "Nao wanadhani kwamba" wanafanya vizuri katika matendo yao. Basi vipi kuhusu matendo yao ambayo wanajua vyema kwamba ni batili na kwamba yanapingana na Mwenyezi Mungu na mitume wake na kuwafanyia uadui?
#
{105} فمن هم هؤلاء الذين خسرت أعمالُهم فخسروا أنفسهم يوم القيامة وأهليهم يوم القيامة ألا ذلك هو الخسران المبين؟ {أولئك الذين كفروا بآياتِ ربهم ولقائِهِ}؛ أي: جحدوا الآيات القرآنيَّة والآيات العيانيَّة الدالَّة على وجوب الإيمان به وملائكته ورسله وكتبه واليوم الآخر. {فحبِطَت}: بسبب ذلك {أعمالُهم فلا نقيمُ لهم يوم القيامة وَزْناً}: لأنَّ الوزن فائدته مقابلةُ الحسناتِ بالسيئاتِ والنظر في الراجح منها والمرجوح، وهؤلاء لا حسنات لهم؛ لعدم شرطها، وهو الإيمان؛ كما قال تعالى: {ومَن يعملْ من الصالحاتِ وهو مؤمنٌ فلا يخافُ ظلماً ولا هضماً}، لكنْ تعدُّ أعمالهم، وتُحصى ويقرَّرون بها، ويُخْزَوْن بها على رؤوس الأشهاد ثم يعذَّبون عليها.
{105} Basi ni akina nani hawa ambao vitendo vyao vilihasiri, kwa hivyo zikahasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Qiyama? Tambueni kuwa hiyo ndiyo hasara iliyo dhahiri. "Hao ni wale waliozikufuru Ishara za Mola wao Mlezi na kukutana naye." Yaani, walizikanusha ishara za kiqur-ani na ishara za kuonekana moja kwa moja zinazoonyesha ulazima wa kumwamini Yeye, na Malaika wake, na Mitume wake, na Vitabu vyake, na Siku ya Mwisho. "Kwa hivyo matendo yao yakapotea bure" kwa sababu ya hayo "na wala Siku ya Qiyama hatutawasimamishia mizani yoyote." Kwa sababu faida ya mizani ni kulinganisha kati ya matendo mema na mabaya, na kutazama yaliyo mazito kati yake na yale yaliyoshindwa uzito. Na hawa hawana matendo mema yoyote; kwa sababu walikosa sharti lake, ambalo ni imani. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema, "Na anayetenda mema, naye ni Muumini, basi hatahofu kudhulumiwa wala kupunjwa." Lakini matendo yao yatahesabiwa, na kudhibitiwa, na watafanywa kuyakiri na watafedheheshwa kwayo mbele ya mashahidi kisha wataadhibiwa kwayo.
#
{106} ولهذا قال: {ذلك جزاؤُهم}؛ أي: حبوط أعمالهم، وأنَّه لا يُقام لهم يوم القيامة وزنٌ؛ لحقارتهم وخسَّتهم بكفرهم بآيات الله واتِّخاذهم آياتِهِ ورسلِهِ هزواً يستهزئون بها ويسخَرون [منها] ، مع أنَّ الواجب في آيات الله ورسله الإيمانُ التامُّ بها والتعظيم لها والقيام بها أتمَّ القيام، وهؤلاء عكسوا القضيَّة، فانعكس أمرُهم وتعسوا وانتكسوا في العذاب.
{106} Na ndiyo maana akasema, "Hayo ndiyo malipo yao." Yaani, kuharibika kwa matendo yao, na kwamba hawatasimamishiwa mizani yoyote Siku ya Qiyama; kwa sababu uduni wao na kutokuwa kitu kwao kwa sababu walizikufuru ishara za Mwenyezi Mungu na kuzichukulia mzaha ishara zake na Mitume wake, pamoja na kwamba lililo la wajibu katika ishara za Mwenyezi Mungu na Mitume wake ni kuziamini kikamilifu na kuzitukuza na kuzitekeleza kikamilifu. Lakini hawa waliligeuza suala hili kinyume. Kwa hivyo jambo lao likawa kinyume, na wakaangamia, na kuhuzunika na kuadhibiwa katika adhabu.
Na alipobainisha hatima ya makafiri na matendo yao, akabainisha matendo ya waumini na hatima yao, akasema:
{إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَانَتْ لَهُمْ جَنَّاتُ الْفِرْدَوْسِ نُزُلًا (107) خَالِدِينَ فِيهَا لَا يَبْغُونَ عَنْهَا حِوَلًا (108)}.
107. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi. 108. Watadumu humo; hawatataka kuondoka humo.
#
{107} أي: {إنَّ الذين آمنوا}: بقلوبهم، {وعملوا الصالحات}: بجوارحهم، وشمل هذا الوصف جميع الدين؛ عقائده وأعماله، أصوله وفروعه الظاهرة والباطنة؛ فهؤلاء على اختلاف طبقاتهم من الإيمان والعمل الصالح، {لهم جناتُ الفردوس}: يُحتمل أن المراد بجنات الفردوس أعلى الجنة ووسطها وأفضلها، وأنَّ هذا الثواب لمن كمَّل الإيمان والعمل الصالح، وهم الأنبياء والمقرَّبون، ويُحتمل أن يُراد بها جميع منازل الجنان، فيشمل هذا الثواب جميع طبقات أهل الإيمان من المقرَّبين والأبرار والمقتصدين؛ كلٌّ بحسب حاله، وهذا [أَوْلى] المعنيين؛ لعمومه، ولذكر الجنة بلفظ الجمع المضاف إلى الفردوس، وأنَّ الفردوس يُطلق على البستان المحتوي على الكرم أو الأشجار الملتفَّة، وهذا صادق على جميع الجنة؛ فجنَّة الفردوس نُزُلٌ وضيافةٌ لأهل الإيمان والعمل الصالح، وأيُّ ضيافة أجلُّ وأكبر وأعظم من هذه الضيافة، المحتوية على كلِّ نعيم للقلوب والأرواح والأبدان؟! وفيها ما تشتهيه الأنفس وتلذُّ الأعينُ، من المنازل الأنيقة والرياض الناضرة والأشجار المثمرة والطيور المغرِّدة المشجية والمآكل اللذيذة والمشارب الشهيَّة والنساء الحسان والخدم والولدان والأنهار السارحة والمناظر الرائقة والجمال الحسيِّ والمعنويِّ والنعمة الدائمة، وأعلى ذلك وأفضله وأجلُّه التنعُّم بالقرب من الرحمن ونيل رضاه الذي هو أكبر نعيم الجنان، والتمتُّع برؤية وجهه الكريم وسماع كلام الرءوف الرحيم فلله تلك الضيافة؛ ما أجلها وأجملها وأدومها وأكملها! وهي أعظم من أن يحيطَ بها وصفُ أحدٍ من الخلائق، أو تخطر على القلوب؛ فلو عَلِمَ العبادُ بعض ذلك النعيم علماً حقيقياً يصل إلى قلوبهم لطارت إليها قلوبُهم بالأشواق، ولتقطَّعت أرواحهم من ألم الفراق، ولساروا إليها زرافاتٍ ووحداناً، ولم يؤثروا عليها دنيا فانيةً ولذاتٍ منغصةً متلاشيةً، ولم يفوِّتوا أوقاتاً تذهب ضائعةً خاسرةً، يقابل كلَّ لحظة منها من النعيم من الحقب آلافٌ مؤلَّفة، ولكنَّ الغفلة شملت، والإيمان ضَعُف، والعلم قلَّ، والإرادة وَهَتْ ، فكان ما كان؛ فلا حول ولا قوَّةَ إلاَّ بالله العليِّ العظيم.
{107} Yaani, "hakika wale walioamini" kwa mioyo yao, "na wakatenda mema" kwa viungo vyao. Na sifa hiyo inajumuisha dini yote. Itikadi zake na matendo yake, misingi yake na matawi yake ya dhahiri na ya ndani. Basi hawa pamoja na utofauti ulioko katika daraja zao za imani na matendo mema, "mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi." Inawezekana kwamba kilichokusudiwa na Pepo za Firdaus ni Pepo za juu zaidi, na bora zaidi kati yake, na kwamba thawabu hizi ni kwa yule aliyekamilisha imani na matendo mema, na wao ni Manabii na wa wale walio karibu zaidi na Mwenyezi Mungu. Na inawezekana kwamba maana yake ni daraja zote za Pepo. Basi thawabu hizi zinajumuisha daraja zote za watu wa imani miongoni mwa wale walio karibu zaidi na Mwenyezi Mungu, na wema, na wale wa katikati, kila mmoja kulingana na hali yake, na hii
[ndiyo bora zaidi] ya maana hizo mbili kwa sababu ya ujumla wake, na kwa sababu ya kuitaja Pepo kwa hali ya wingi huku imeunganishwa kwa Firdaus, na kwamba Firdaus hiyo inaitwa kwayo bustani iliyo na ukarimu au miti iliyoshikana. Na hili ni sahihi kuhusiana na Pepo. Kwa hivyo, Pepo ya Firdaus ndiyo mashukio na mahali pa ugeni kwa wenye imani na matendo mema. Na ni ugeni gani bora zaidi, mkubwa zaidi, mkuu zaidi kuliko ugeni huu wenye kila starehe ya mioyo na roho na viwiliwili? Ndani yake kuna yale ambayo nafsi hutamani na macho hufurahia, kama vile nyumba za kifahari, na bustani za kupendeza, na miti ya matunda, na ndege waimbao nyimbo nzuri nzuri, na vyakula na vinywaji vitamu, na wanawake wazuri, na watumishi, na watoto wadogo, na mito ipitayo, na mambo ya kutazamwa mazuri, na uzuri wa kihisia na usio wa kihisia, na neema ya kudumu, na ya juu zaidi. Na bora ya hayo yote na tukufu yake zaidi ni kufurahia kuwa karibu na Mwenye rehema na kupata ridhaa yake, ambayo ndiyo neema kubwa zaidi ya Peponi, na kufurahia kuona uso wake mtukufu na kusikia maneno ya Mwenye huruma kubwa, Mwingi wa kurehemu. Na ugeni huo ni kwa Mwenyezi Mungu. Ni ugeni mtukufu ulioje, na mzuri zaidi, na wa kudumu zaidi, na mkamilifu zaidi! Nao ni kubwa sana kuzungukwa na maelezo ya mmoja wa viumbe, au hata kupita ndani ya mioyo. Na ikiwa waja wangejua baadhi ya neema hizo kwa elimu ya uhakika yenye kufika katika mioyo yao, basi mioyo yao ingepeperuka kuiendea kwa sababu ya shauku kubwa, na roho zao zingekatika kwa sababu ya uchungu wa kutengana nayo, na wangeindea kwa makundi na mmoja mmoja, na wala hawangeipendelea dunia ya kuisha na starehe za kukatika na kuondoka badala yake. Na hawangeharibu nyakati zikipotea tu katika hasara, kwa kuwa kila muda mfupi katika dunia wa furaha unalingana na maelfu ya miaka mingi huko, lakini kwa kuwa kughafilika kumeenea, na imani ilidhoofika, na elimu ilipunguka, na utashi ulififia, ndiyo maana yakawa hayo yaliyokuwa. Basi hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, aliye juu, Mtukufu.
#
{108} وقوله: {خالدين فيها}: هذا هو تمام النعيم، أنَّ فيها النعيم الكامل، ومن تمامه أنه لا ينقطع، {لا يبغون عنها حِوَلاً}؛ أي: تحوُّلاً ولا انتقالاً؛ لأنَّهم لا يرون إلاَّ ما يعجِبُهم ويبهِجُهم ويسرُّهم ويفرحهم، ولا يرون نعيماً فوق ما هم فيه.
{108} Na kauli yake, "watadumu humo" huu ndio utimilifu wa neema, kwamba kuna neema kamilifu ndani yake. Na katika ukamilifu wake ni kwamba haikatiki. "Hawatataka kuondoka humo." Yaani, hawatataka kuondoka wala kuhama, kwa sababu hawaoni humo isipokuwa yenye kuwapendeza tu, na kuwafurahisha, na wala hawaoni neema yoyote iliyo juu zaidi ya ile waliyo ndani yake.
{قُلْ لَوْ كَانَ الْبَحْرُ مِدَادًا لِكَلِمَاتِ رَبِّي لَنَفِدَ الْبَحْرُ قَبْلَ أَنْ تَنْفَدَ كَلِمَاتُ رَبِّي وَلَوْ جِئْنَا بِمِثْلِهِ مَدَدًا (109)}.
109.
Sema: Lau kuwa bahari ingekuwa ndiyo wino kwa maneno ya Mola wangu Mlezi, basi bahari ingelimalizika kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu Mlezi, hata tungeliileta mfano wa hiyo kuongezea.
#
{109} أي: قل لهم مخبراً عن عظمة الباري وسعةِ صفاتِهِ وأنها لا يحيطُ العباد بشيء منها: {لو كان البحرُ}؛ أي: هذه الأبحر الموجودة في العالم {مداداً لكلماتِ ربِّي}؛ أي: وأشجارُ الدُّنيا من أولها إلى آخرها من أشجار البلدان والبراري والبحار أقلامٌ، {لَنَفِدَ البحرُ}: وتكسرت الأقلام {قبل أن تنفَدَ كلماتُ ربِّي}: وهذا شيءٌ عظيمٌ لا يحيط به أحدٌ، وفي الآية الأخرى: {ولو أنَّ ما في الأرض من شجرةٍ أقلامٌ والبحرُ يمدُّه من بعدِهِ سبعةُ أبحرٍ ما نَفِدَتْ كلماتُ الله إنَّ الله عزيزٌ حكيمٌ}: وهذا من باب تقريب المعنى إلى الأذهان؛ لأنَّ هذه الأشياء مخلوقةٌ، وجميع المخلوقات منقضيةٌ منتهيةٌ، وأما كلام الله؛ فإنَّه من جملة صفاتِهِ، وصفاتُهُ غير مخلوقة ولا لها حدٌّ ولا منتهى؛ فأيُّ سعة وعظمة تصورتْها القلوب؛ فالله فوق ذلك، وهكذا سائر صفات الله تعالى؛ كعلمه وحكمته وقدرته ورحمته؛ فلو جُمِعَ علمُ الخلائق من الأوَّلين والآخرين أهل السماوات وأهل الأرض؛ لكان بالنسبة إلى علم العظيم أقلَّ من نسبة عصفورٍ وقع على حافَّة البحر، فأخذ بمنقارِهِ من البحر بالنسبة للبحر وعظمتِهِ، ذلك بأنَّ الله له الصفات العظيمة الواسعة الكاملة، وأنَّ إلى ربِّك المنتهى.
{109} Yaani, waambie ukiwajulisha kuhusu ukuu wa Muumba na upana wa sifa zake na kwamba waja hawazunguki chochote kwazo, "Lau kuwa bahari" zinazopatikana katika ulimwengu "ingekuwa ndiyo wino kwa maneno ya Mola wangu Mlezi" na miti ya dunia hii tangu mwanzo wake hadi mwisho wake miongoni mwa miti ya nchi zote, na ya majangwani na ya baharini ndizo kalamu, "basi bahari ingelimalizika" na kalamu hizo zingevunjwa "kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu Mlezi." Na hili ni jambo kubwa ambalo hakuna yeyote anayeweza kulizunguka. Na katika aya nyingine, "Na lau kuwa miti yote iliyomo duniani ikawa ni kalamu, na bahari
(ikawa wino), na ikaongezewa juu yake bahari nyingine saba, maneno ya Mwenyezi Mungu yasingelikwisha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima." Hii ni njia ya kuleta maana karibu na akili. Kwa sababu vitu hivi vimeumbwa, na viumbe vyote vitatoweka na kuisha. Na ama maneno ya Mwenyezi Mungu, hayo ni katika sifa zake yeye Mtukufu, na sifa zake hazikuumbwa, wala hazina kikomo, wala mwisho. Basi upana wowote na ukuu wowote unaofikiriwa na mioyo, basi Mwenyezi Mungu yuko juu ya hivyo, na vivyo hivyo sifa zinginezo za Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama vile elimu yake, hekima yake, uwezo wake, na rehema zake. Na ikiwa elimu ya viumbe ingekusanywa kutoka kwa wa mwanzo na wa mwisho, wakazi wa mbinguni na wakazi wa duniani, basi ingekuwa kwa kulinganisha na elimu ya Mkuu kidogo kuliko kama vile ndege mdogo anaposimama kwenye ukingo wa bahari, kisha akachukua kwa mdomo wake maji kutoka baharini humo kwa kulinganisha na bahari hiyo na ukuu wake, kwa sababu Mwenyezi Mungu ana sifa kuu, pana na kamili, na kwamba kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho.
{قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِثْلُكُمْ يُوحَى إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَهُكُمْ إِلَهٌ وَاحِدٌ فَمَنْ كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا (110)}.
110. Sema, "Hakika mimi ni mwanadamu tu kama nyinyi. Ninaletewa Wahyi kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Kwa hivyo, mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi, basi na atende matendo mema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi."
#
{110} أي: قل يا محمدُ للكفار وغيرهم: {إنَّما أنا بشرٌ مثلُكم}؛ أي: لست بإله، ولا لي شركةٌ في الملك، ولا علمٌ بالغيب، ولا عندي خزائن الله، وإنَّما أنا بشرٌ مثلكم، عبدٌ من عبيد ربي. {يوحى إليَّ أنَّما إلهكم إلهٌ واحدٌ}؛ أي: فُضِّلْتُ عليكم بالوحي الذي يوحيه الله إليَّ، الذي أجلُّه الإخبار لكم، {أنَّما إلهكم إلهٌ واحدٌ}؛ أي: لا شريك له ولا أحد يستحقُّ من العبادة مثقال ذرَّة [غيره]، وأدعوكم إلى العمل الذي يقرِّبُكم منه ويُنيلكم ثوابه ويدفع عنكم عقابه، ولهذا قال: {فَمَن كان يَرْجو لقاءَ ربِّه فليعملْ عملاً صالحاً}: وهو الموافق لشرع الله من واجب ومستحبٍّ، {ولا يُشْرِكْ بعبادةِ ربِّه أحداً}؛ أي: لا يرائي بعمله، بل يعمله خالصاً لوجه الله تعالى؛ فهذا الذي جمع بين الإخلاص والمتابعة هو الذي ينال ما يرجو ويطلب، وأما مَنْ عدا ذلك؛ فإنَّه خاسرٌ في دنياه وأخراه، وقد فاته القرب من مولاه ونيل رضاه.
{110} Yaani, waambie ewe Muhammad makafiri na wegineo, "Hakika, mimi ni mwanadamu tu kama nyingi" na mimi si mungu, wala sina ushirika wowote katika ufalme wa Mwenyezi Mungu, wala sijui elimu ya ghaibu, wala sina hazina za Mwenyezi Mungu. Lakini mimi hakika ni mwanadamu tu kama nyinyi, na mja miongoni mwa waja wa Mola wangu Mlezi. "Ninaletewa Wahyi kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu." Yaani, nimeboreshwa juu yenu kwa ufunuo ambao Mwenyezi Mungu ananifunulia mimi, ambao mkubwa wake zaidi ni kuwaambia kwamba, "Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu" hana mshirika yeyote wala hakuna yeyote anayestahili kuabudu uzito wa chembe
[isipokuwa yeye tu], na ninawaita kwenye matendo ambayo inawaleta karibu naye, kuwapa thawabu zake na inawaondolea adhabu yake. Na ndiyo maana akasema, "Kwa hivyo, mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi, basi na atende matendo mema." Nayo ni yale matendo ambayo yanaafikiana na sheria ya Mwenyezi Mungu miongoni mwa mambo ya wajibu na yale yaliyopendekezwa. "Wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi." Yaani, asijioneshe kwa matendo yake, lakini ayafanye kwa kuukusudia uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu tu. Basi huyu aliyeunganisha kati ya kumkusudia Mwenyezi Mungu tu na kufuata sheria ya sawasawa ndiye atakayepata kile anachotarajia na anachotafuta. Na ama asiyekuwa kama huyu, basi yeye amehasiri katika dunia yake na akhera yake, na ameshapoteza kuwa karibu na Mola wake na kupata radhi zake.
Mwisho wa Tafsiri ya Surat Al-Kahf. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu.
* * *