Tafsiri ya Surat Bani Israili
Tafsiri ya Surat Bani Israili
Nayo iliteremka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلًا مِنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ (1)}
1. Ametakasika yule aliyempeleka mja wake usiku mmoja kutoka katika Msikiti Mtakatifu mpaka Msikiti wa Al-Aqswa, ambao tumebariki kandoni mwake, ili tumuonyeshe katika Ishara zetu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia zaidi, Mwenye kuona zaidi.
#
{1} ينزِّه تعالى نفسه المقدَّسة ويعظِّمها لأنَّ له الأفعال العظيمة والمنن الجسيمة التي من جملتها أنه {أسرى بعبدِهِ}: ورسوله محمد - صلى الله عليه وسلم -، {من المسجد الحرام}: الذي هو أجلُّ المساجد على الإطلاق، {إلى المسجد الأقصى}: الذي هو من المساجد الفاضلة، وهو محلُّ الأنبياء، فأسرى به في ليلة واحدةٍ إلى مسافة بعيدةٍ جدًّا، ورجع في ليلته، وأراه الله من آياته ما ازداد به هدىً وبصيرةً وثباتاً وفرقاناً، وهذا من اعتنائه تعالى به ولطفه؛ حيث يسَّره لليسرى في جميع أموره، وخوَّله نعماً فاق بها الأوَّلين والآخرين. وظاهر الآية أنَّ الإسراء كان في أول الليل، وأنَّه من نفس المسجد الحرام، لكن ثبت في الصحيح أنه أُسْرِيَ به من بيت أم هانئ ؛ فعلى هذا تكون الفضيلة في المسجد الحرام لسائر الحرم؛ فكلُّه تضاعف فيه العبادة كتضاعفها في نفس المسجد، وأنَّ الإسراء بروحه وجسده معاً، وإلاَّ لم يكن في ذلك آيةٌ كبرى ومنقبةٌ عظيمة.
وقد تكاثرت الأحاديث الثابتة عن النبي - صلى الله عليه وسلم - في الإسراء وذكر تفاصيل ما رأى، وأنه أُسْرِيَ به إلى بيت المقدس، ثم عُرِج به من هناك إلى السماوات حتى وصل إلى ما فوق السماوات العُلى، ورأى الجنة والنار، والأنبياء على مراتبهم، وفُرِضَ عليه الصلواتُ خمسين، ثم ما زال يراجِعُ ربَّه بإشارة موسى الكليم حتى صارت خمساً في الفعل وخمسين في الأجر والثواب، وحاز من المفاخر تلك الليلة هو وأمتُه ما لا يعلم مقدارَه إلاَّ الله عز وجل. وذَكَرَهُ هنا وفي مقام الإنزال للقرآن ومقام التحدِّي بصفة العبوديَّة؛ لأنَّه نال هذه المقامات الكبار بتكميله لعبوديَّة ربه.
وقوله: {الذي بارَكْنا حوله}؛ أي: بكثرة الأشجار والأنهار والخصب الدائم، ومن بركته تفضيله على غيره من المساجد سوى المسجد الحرام ومسجد المدينة، وأنه يُطْلَبُ شدُّ الرحل إليه للعبادة والصلاة فيه، وأنَّ الله اختصَّه محلاًّ لكثيرٍ من أنبيائه وأصفيائه.
{1} Yeye Mtukufu anajitakasa nafsi yake Takatifu na kuitukuza kwa sababu ana vitendo vikuu na neema kubwa kubwa. Na miongoni mwake ni kuwa, "alimchukua mja wake" na mtume wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - "kutoka katika Msikiti Mtakatifu" ambao ndio msikiti mtukufu zaidi kuliko misikiti yote "mpaka Msikiti wa Al-Aqswa" ambao ni miongoni mwa Misikiti bora, na ni mahali pa Manabii. Basi akamchukua katika usiku mmoja kwenda katika masafa ya mbali sana, na akarudi usiku ule ule, na Mwenyezi Mungu akamwonyesha katika ishara zake ambazo zilimzidishia uwongofu, ufahamu, uthabiti, na upambanuzi. Na hii ni kutokana na uangalizi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu juu yake na upole wake. Kwa vile alimrahisishia katika mambo yake yote yakawa mepesi, na akampa neema alizopita kwazo wa mwanzo na wa mwisho. Na maana ya dhahiri ya Aya hii ni kuwa Israa ilifanyika mwanzoni mwa usiku, na ilitokea katika Msikiti ule ule Mtukufu. Lakini pia imethibiti katika hadithi Sahihi kwamba Israa ilitokea katika nyumba ya Ummu Hani, na kwa mujibu wa hili inakuwa fadhila iliyo katika Msikiti Mtakatifu ni sawa na ile ya sehemu nyinginezo zilizo ndani ya eneo takatifu. Kwa hivyo, eneo lote hilo, ibada huzidishwa maradufu, kama inavyozidishwa maradufu katika msikiti wenyewe. Na pia ilithibiti kwamba safari ya Israa ilikuwa kwa roho yake pamoja na kiwiliwili chake, vinginevyo kusingekuwa na muujiza mkubwa wala fadhila kubwa katika hilo. Zimekuja Hadiyth nyingi zilizothibiti juu ya Mtume – rehema na amani ziwe juu yake – kuhusu Safari ya Usiku, na akataja maelezo ya aliyoyaona, na kwamba alichukuliwa safari ya kwenda Jerusalem, kisha akachukuliwa kutoka huko. Mbinguni mpaka akafika vilio juu ya mbingu, na akaiona Pepo na Jahannamu, na Manabii kwa mpangilo wao. Na akafaradhishiwa swala hamsini, kisha hakuacha kurudi kwa Mola wake Mlezi kuomba kufanyiwa wepesi kwa Ishara ya Musa mneni wa Allah. Mpaka ikawa tano kwa vitendo na hamsini za malipo, na yeye na umma wake wakapata heshima kubwa usiku huo, kiasi ambacho hakuna ajuaye isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na Mwenyezi Mungu amemtaja Mtume hapa kwa sifa ya uja katika muktadha wa kuteremshwa kwa Qur-ani na muktadha wa kupeana changamoto, kwa sababu alivipata vyeo hivi vikubwa kwa sababu alikamilisha uja wake kwa Mola wake Mlezi. Na kauli yake, "ambao tumebariki kandoni mwake." Yaani, kwa wingi wa miti, mito, na rutuba ya kudumu. Na miongoni mwa baraka zake ni kupendelewa na kufadhilishwa kuliko misikiti mingine isipokuwa Msikiti Mtakatifu wa Makka na Msikiti wa Madina, na kwamba inatakiwa kufunga safari kwenda huko kwa ajili ya kufanya ibada na kuswalia humo, na kwamba Mwenyezi Mungu amepateua kuwa mahali pa wengi wa manabii na wateule wake.
{وَآتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَجَعَلْنَاهُ هُدًى لِبَنِي إِسْرَائِيلَ أَلَّا تَتَّخِذُوا مِنْ دُونِي وَكِيلًا (2) ذُرِّيَّةَ مَنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ إِنَّهُ كَانَ عَبْدًا شَكُورًا (3) وَقَضَيْنَا إِلَى بَنِي إِسْرَائِيلَ فِي الْكِتَابِ لَتُفْسِدُنَّ فِي الْأَرْضِ مَرَّتَيْنِ وَلَتَعْلُنَّ عُلُوًّا كَبِيرًا (4) فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ أُولَاهُمَا بَعَثْنَا عَلَيْكُمْ عِبَادًا لَنَا أُولِي بَأْسٍ شَدِيدٍ فَجَاسُوا خِلَالَ الدِّيَارِ وَكَانَ وَعْدًا مَفْعُولًا (5) ثُمَّ رَدَدْنَا لَكُمُ الْكَرَّةَ عَلَيْهِمْ وَأَمْدَدْنَاكُمْ بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَجَعَلْنَاكُمْ أَكْثَرَ نَفِيرًا (6) إِنْ أَحْسَنْتُمْ أَحْسَنْتُمْ لِأَنْفُسِكُمْ وَإِنْ أَسَأْتُمْ فَلَهَا فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ لِيَسُوءُوا وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُوا الْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا مَا عَلَوْا تَتْبِيرًا (7) عَسَى رَبُّكُمْ أَنْ يَرْحَمَكُمْ وَإِنْ عُدْتُمْ عُدْنَا وَجَعَلْنَا جَهَنَّمَ لِلْكَافِرِينَ حَصِيرًا (8)}.
2. Na tulimpa Musa Kitabu na tukakifanya kuwa ni uwongofu kwa Wana wa Israili.
(Tukawambia) kwamba msimfanye yeyote asiyekuwa mimi kuwa mtegemewa wenu. 3. Kizazi cha wale tuliowabeba pamoja na Nuhu. Hakika yeye alikuwa mja wa kushukuru sana. 4. Na tukawahukumia Wana wa Israili katika kitabu kwamba hakika mtafanya uharibifu katika ardhi mara mbili, na hakika mtapanda kiburi, kiburi kikubwa. 5. Na itakapokuja ahadi ya kwanza yake, tutawatumia waja wetu wenye nguvu kubwa. Watawaingilia ndani ya majumba. Na hii ilikuwa ahadi iliyotimizwa. 6. Kisha tukawarudishia nguvu zenu dhidi yao, na tukawasaidia kwa mali na wana, na tukawajalia mkawa wengi zaidi. 7. Mkifanya wema, mnafanyia wema nafsi zenu. Na mkifanya ubaya, basi mnajifanyia wenyewe. Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu na waingie msikitini kama walivyoingia mara ya kwanza na waharibu kila walichokiteka kwa uharibifu mkubwa. 8. Huenda Mola wenu Mlezi akawarehemu, na mkirudia, na sisi tutarudia. Na tumeifanya Jahannam kuwa ni gereza kwa ajili ya makafiri.
#
{2} كثيراً ما يَقْرِنُ الباري بين نبوَّة محمد - صلى الله عليه وسلم - ونبوَّة موسى - صلى الله عليه وسلم - وبين كتابيهما وشريعتيهما؛ لأنَّ كتابيهما أفضل الكتب، وشريعتيهما أكمل الشرائع، ونبوَّتيهما أعلى النبوَّات، وأتباعهما أكثر المؤمنين، ولهذا قال هنا: {وآتينا موسى الكتابَ}: الذي هو التوراة، {وجَعَلْناه هدىً لبني إسرائيل}: يهتدونَ به في ظُلُمات الجهل إلى العلم بالحقِّ. {ألاَّ تتَّخذوا مِن دوني وكيلاً}؛ أي: وقلنا لهم ذلك، وأنزلنا إليهم الكتاب لذلك؛ ليعبدوا الله وحده، ويُنيبوا إليه، ويتَّخذوه وحدَه وكيلاً ومدبراً لهم في أمر دينهم ودُنياهم، ولا يتعلَّقوا بغيره من المخلوقين الذين لا يملكون شيئاً ولا ينفعونَهم بشيءٍ.
{2} Yeye Muumba mara nyingi huunganisha kati ya unabii wa Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na unabii wa Musa - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na vitabu vyao na sheria zao; kwa sababu vitabu vyao ndivyo vitabu bora zaidi, na sheria zao ndizo sheria kamili zaidi, na unabii wao ndio unabii wa hali ya juu zaidi, na wafuasi wao ndio waumini wengi zaidi. Na ndiyo sababu akasema hapa, "Na tulimpa Musa Kitabu" ambacho ni Taurati. "Na tukakifanya kuwa ni uwongofu kwa Wana wa Israili" ili waongoke kwacho katika giza la ujinga hadi katika kuijua haki. "Kwamba msimfanye yeyote asiyekuwa mimi kuwa mwakilishi wenu." Yaani, tuliwaambia hayo, na tukawateremshia Kitabu kwa ajili ya hilo, ili wamwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na wamrudie, na wamfanye yeye peke yake kuwa ndiye mtegemewa wao, mwenye kuendesha mambo yao ya kidini na ya kidunia, na wala wasijifungamanishe na yeyote asiyekuwa yeye miongoni mwa viumbe ambao hawamiliki kitu na wala hawawafai kwa chochote.
#
{3} {ذُرِّيَّةَ مَنْ حَمَلْنا مع نوح}؛ أي: يا ذُرِّيَّة مَنْ مَنَنَّا عليهم وحملناهم مع نوح. {إنَّه كان عبداً شكوراً}: ففيه التنويه بالثناء على نوح عليه السلام بقيامه بشكر الله واتِّصافه بذلك، والحثِّ لذُرِّيَّتِهِ أن يقتدوا به في شكره ويتابعوه عليه، وأن يتذكَّروا نعمةَ الله عليهم إذْ أبقاهم، واستخلفهم في الأرض، وأغرق غيرهم.
{3} "Kizazi cha wale tuliowabeba pamoja na Nuhu." Yaani, enyi dhuria ya wale tuliowaneemesha na tunawabeba pamoja na Nuhu. "Hakika yeye alikuwa mja wa kushukuru sana." Na hili ndani yake kuna ishara ya kumsifu Nuhu - amani iwe juu yake - kwamba alikuwa akimshukuru Mwenyezi Mungu akawa anasifika kwa hilo. Na pia kuna kuwahimiza dhuria yake kwamba wamuige katika kushukuru kwake, na wamfuate katika hilo, na kwamba waikumbuke neema ya Mwenyezi Mungu juu yao kwa kuwa aliwabakisha, na akawafanya kushika nafasi katika ardhi na akawazamisha wengineo.
#
{4} {وقَضَيْنا إلى بني إسرائيل}؛ أي: تقدَّمنا وعَهِدْنا إليهم وأخبرناهم في كتابهم أنهم لا بدَّ أن يقعَ: منهم إفسادٌ في الأرض مرتين بعمل المعاصي والبَطَر لنعم الله والعلوِّ في الأرض والتكبُّر فيها، وأنَّه إذا وقع واحدةٌ منهما؛ سلَّطَ الله عليهم الأعداء وانتقم منهم، وهذا تحذيرٌ لهم وإنذارٌ لعلَّهم يرجعون فيتذكَّرون.
{4} "Na tukawahukumia Wana wa Israili." Yaani, tulichukua ahadi yao na tukawaambia katika kitabu chao kwamba lazima utatokea uharibifu miongoni mwa katika ardhi mara mbili kwa kufanya maasia, na kujivuna kwa sababu ya neema za Mwenyezi Mungu na kupanda kiburi katika ardhi na kutakabari humo, na kwamba moja tu ya hayo itakapofanyika, basi Mwenyezi Mungu atawapa mamlaka maadui zao dhidi yao na kuwaadhibu. Na hili ni tahadharisho kwao na onyo ili labda watarudi na kukumbuka.
#
{5} {فإذا جاء وَعْدُ أولاهما}؛ أي: أولى المرتين اللتين يفسدون فيهما؛ أي: إذا وقع منهم ذلك الفسادُ، {بَعَثْنا عليكم}: بعثاً قدريًّا وسلَّطنا عليكم تسليطاً كونيًّا جزائيًّا، {عباداً لنا أولي بأسٍ شديدٍ}؛ أي: ذوي شجاعة وعددٍ وعُدَّةٍ، فنصرهم اللهُ عليكم، فقتلوكم وسَبَوْا أولادكم ونهبوا أموالكم، وجاسوا {خلالَ الدِّيار}: فهتكوا الدُّور، ودخلوا المسجد الحرام، وأفسدوه. {وكان وعداً مفعولاً}: لا بدَّ من وقوعه لوجود سببه منهم. واختلف المفسِّرون في تعيين هؤلاء المسلَّطين؛ إلاَّ أنَّهم اتَّفقوا على أنَّهم قومٌ كفارٌ: إمَّا من أهل العراق، أو الجزيرة، أو غيرها؛ سلَّطهم الله على بني إسرائيل لما كَثُرَتْ فيهم المعاصي وتركوا كثيراً من شريعتهم وطَغَوا في الأرض.
{5} "Na itakapokuja ahadi ya kwanza yake." Yaani, mara ya kwanza kati ya mbili hizo ambazo watafanya uharibifu, yaani, wakati watakapoufanya uharibifu huo, "tutawatumia" kulingana na majaaliwa yaliyoandikwa kabla, na kuwapa mamlaka juu yenu pia kimajaaliwa ya kiadhabu. "Waja wetu wenye nguvu kubwa;" yaani, mashuja, wenye idadi kubwa na maandalizi mazuri, kisha Mwenyezi Mungu atawasaidia dhidi yenu, wawaue, wawateke wana wenu, wapore mali zenu, na wawaingilie "ndani ya majumba." Kwa hivyo waharibu nyumba hizo, waingie katika Msikiti Mtakatifu, na wauharibu. "Na hii ilikuwa ahadi iliyotimizwa" ambayo ilikuwa lazima itokee kwa sababu ilipatikana sababu ya kutokea kwake kutoka kwao. Wafasiri walitofautiana kuhusiana na hao waliopewa mamlaka dhidi ya Wana wa Israili, lakini walikubaliana kwamba walikuwa kaumu makafiri ima kutoka katika watu wa Iraq, au Al-Jazira, au sehemu nyingineyo. Mwenyezi Mungu aliwapa mamlaka juu ya wana wa Israili wakati kulikuwa na maasia mengi miongoni mwao na wakaacha sheria zao nyingi na wakavuka mipaka katika ardhi.
#
{6} {ثم رَدَدْنا لكمُ الكَرَّةَ عليهم}؛ أي: على هؤلاء الذين سُلطوا عليكم فأجْلَيْتموهم من دياركم، {وأمدَدْناكم بأموال وبنينَ}؛ أي: أكثرنا أرزاقكم وكثَّرناكم وقوَّيناكم عليهم، {وجعلناكُم أكثرَ نفيراً}: منهم، وذلك بسبب إحسانكم وخضوعكم لله.
{6} "Kisha tukakurudishia nguvu zenu dhidi yao." Yaani, dhidi ya wale waliopewa mamlaka dhidi yenu, kwa mkawaondoa katika makazi yenu. "Na tukawasaidia kwa mali na wana." Yaani, tukawazidishia riziki zenu, na tukawazidisha kwa idadi na tukawapa nguvu dhidi yao. "Na tukawajalia mkawa wengi zaidi" kuliko wao, kwa sababu ya hisani yenu na kunyenyekea kwenu kwa Mwenyezi Mungu.
#
{7} {إنْ أحسنتُم أحسنتُم لأنفسِكم}: لأنَّ النفع عائدٌ إليكم حتى في الدُّنيا كما شاهدتم من انتصِاركم على أعدائكم. {وإنْ أسأتُم فلها}؛ أي: فلأنفسكم يعود الضرر؛ كما أراكم الله من تسليط الأعداء. {فإذا جاء وعدُ الآخرة}؛ أي: المرَّة الأخرى التي تفسِدون فيها في الأرض؛ سلَّطْنا أيضاً عليكم الأعداء، {ليسوءوا وجوهكم}: بانتصارهم عليكم وسَبْيِكم، {ولِيَدْخُلوا المسجد كما دَخَلوه أوَّل مرَّةٍ}: والمراد بالمسجد مسجد بيت المقدس، {ولِيُتَبِّروا}؛ أي: يخرِّبوا ويدمِّروا {ما عَلَوْا}: عليه {تتبيراً}: فيخرِّبوا بيوتكم ومساجدكم وحروثكم.
{7} "Mkifanya wema mnafanyia wema nafsi zenu." Kwa maana faida yake itawarudia nyinyi wenyewe hata katika dunia hii, kama mlivyoona kutokana na ushindi wenu juu ya maadui zenu. "Na mkifanya ubaya, basi mnajifanyia wenyewe." Yaani, madhara yake yanawarudia nyinyi wenyewe, kama vile Mwenyezi Mungu alivyowaonyesha kwa kuwapa mamlaka maadui. "Na ikifika ahadi ya mwisho;" yaani, mara ya pili mtakapofanya uharibifu katika ardhi, tutawapa mamlaka maadui dhidi yenu tena, "ili waziharibu nyuso zenu" kwa kuwashinda nyinyi na kuwateka. "Na waingie msikitini kama walivyoingia mara ya kwanza." Makusudio ya msikiti hapa ni msikiti wa Bayt Al-Maqdis. "Na waharibu;" yaani, kubomoa na kuharibu "kile walichokiteka, kwa uharibifu mkubwa" kwa kubomoa nyumba zenu, misikiti yenu, na mashamba yenu.
#
{8} {عسى ربُّكم أن يرحَمَكم}: فيُديل لكم الكرة عليهم، فرحمهم وجعل لهم الدولة وتوعَّدهم على المعاصي، فقال: {وإنْ عُدتم}: إلى الإفساد في الأرض، {عُدْنا}: إلى عقوبتِكم، فعادوا لذلك، فسلَّط الله عليهم رسوله محمداً - صلى الله عليه وسلم -، فانتقم الله به منُهم؛ فهذا جزاء الدُّنيا، وما عند الله من النَّكال أعظمُ وأشنعُ، ولهذا قال: {وجَعَلْنا جهنَّم للكافرين حصيراً}: يصلونها ويلازِمونها لا يخرجون منها أبداً. وفي هذه الآيات التحذير لهذه الأمَّة من العمل بالمعاصي؛ لئلاَّ يصيبهم ما أصاب بني إسرائيل؛ فسنَّة الله واحدةٌ لا تبدَّل ولا تغيَّر، ومن نظر إلى تسليط الكفرة على المسلمين والظَّلَمة؛ عَرَفَ أنَّ ذلك من أجل ذنوبهم عقوبةً لهم، وأنَّهم إذا أقاموا كتاب الله وسنَّة رسوله؛ مكَّن لهم في الأرض، ونصرهم على أعدائهم.
{8}"Huenda Mola wenu Mlezi akawarehemu." Kwa hivyo aliwarudishia zamu dhidi yao. Basi akawarehemu na akawarudishia zamu lakini akawatishia kwamba wasiasi. Akasema, "na mkirudia" katika kufanya uharibifu katika ardhi, "tutarudia" kuwaadhibu. Kwa hivyo, wakalirudia hilo. Basi Mwenyezi Mungu akampa mamlaka Mtume wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - dhidi yao na Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa yeye. Haya ndiyo malipo ya duniani. Na ama adhabu iliyo mbele ya Mwenyezi Mungu ni kubwa na mbaya zaidi. Na kwa sababu hii akasema, "Na tumeifanya Jahannam kuwa ni gereza kwa ajili ya makafiri." Wataingia na kukaa humo na hawatatoka humo kamwe. Katika aya hizi, kuna onyo kwa umma huu juu ya kufanya maasia, ili wasipatwe na yale yaliyowapata Wana wa Israili. Kwa maana, desturi ya Mwenyezi Mungu ni moja, haibadiliki wala haigeuki. Na mwenye kutazama namna makafiri na madhalimu wamepewa mamlaka juu ya Waislamu, atatambua kuwa yote hayo ni kwa sababu ya madhambi yao, na hilo ni ili iwe ni adhabu kwao. Na kwamba wakisimamisha Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume wake, atawaimarisha katika ardhi na atawasaidia dhidi ya maadui zao.
{إِنَّ هَذَا الْقُرْآنَ يَهْدِي لِلَّتِي هِيَ أَقْوَمُ وَيُبَشِّرُ الْمُؤْمِنِينَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا كَبِيرًا (9) وَأَنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ أَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا (10)}.
9. Hakika hii Qur-ani inaongoa kwenye yale yaliyonyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba wana malipo makubwa. 10. Na ya kwamba wale wasioiamini Akhera tumewaandalia adhabu chungu.
#
{9 - 10} يخبر تعالى عن شرف القرآن وجلالته وأنَّه {يهدي للتي هي أقومُ}؛ أي: أعدلُ وأعلى من العقائد والأعمال والأخلاق؛ فمن اهتدى بما يدعو إليه القرآنُ؛ كان أكملَ الناس وأقومَهم وأهداهم في جميع الأمور. {ويبشِّرُ المؤمنين الذين يعملونَ الصَّالحاتِ}: من الواجبات والسُّنن، {أنَّ لهم أجراً كبيراً}: أعدَّه الله لهم في دار كرامته لا يعلم وصفَه إلاَّ هو. {وأنَّ الذين لا يؤمنون بالآخرةِ أعْتَدْنا لهم عذاباً أليماً}؛ فالقرآنُ مشتملٌ على البشارة والنِّذارة وذِكْرِ الأسباب التي تُنال بها البشارة، وهو الإيمان والعمل الصالح، والتي تستحقُّ بها النذارة، وهو ضدُّ ذلك.
{9-10} Yeye Mtukufu anajulisha juu ya heshima na utukufu wa Qur-ani na kwamba, "inaongoa kwenye yale yaliyonyooka kabisa." Yaani, maadilifu zaidi na ya juu zaidi miongoni mwa itikadi, matendo na tabia. Kwa hivyo yeyote atayeongoka kwa kile ambacho Qur-ani inalingania, anakuwa mkamilifu zaidi wa watu, na mnyoofu zaidi, na mwongofu zaidi katika mambo yote. "Na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema" miongoni mwa mambo ya wajibu na mambo yapendekezwayo, na "ya kwamba wana malipo makubwa;" ambayo Mwenyezi Mungu amewaandalia katika nyumba ya utukufu wake ambayo hajui maelezo yake na sifa zake isipokuwa yeye tu. "Na ya kwamba wale wasioiamini Akhera tumewaandalia adhabu chungu." Kwa maana Qur-ani ndani yake kuna bishara na maonyo. Na imetaja sababu ambazo bishara hupatikana kwazo, ambazo ni imani na matendo mema, na mambo ambayo kwayo anastahiki onyo, nayo ni kinyume cha hayo.
{وَيَدْعُ الْإِنْسَانُ بِالشَّرِّ دُعَاءَهُ بِالْخَيْرِ وَكَانَ الْإِنْسَانُ عَجُولًا (11)}.
11. Na mtu huomba maovu kama vile aombavyo heri, kwani mtu ni mwenye pupa mno.
#
{11} وهذا من جهل الإنسان وعجلته؛ حيث يدعو على نفسه وأولاده بالشرِّ عند الغضب، ويبادِرُ بذلك الدعاء كما يبادِرُ بالدُّعاء في الخير، ولكنَّ الله من لطفه يستجيبُ له في الخير ولا يستجيبُ له بالشر، ولو يُعَجِّلُ الله للناس الشرَّ استعجالهم بالخير لَقُضي إليهم أجلهم.
{11} Na hili ni katika ujinga wa mtu na haraka haraka zake, ambapo anajiapiza mwenyewe na watoto wake kwa maovu anapokasirika, na anaharakisha kuomba dua kama vile anavyoharakisha kuomba dua katika heri, lakini Mwenyezi Mungu kwa upole wake anamuitikia katika heri na hamuitikii katika maovu. Na kama Mwenyezi Mungu angeharakishia watu uovu kwa vile watu wanavyoharakisha heri, bila ya shaka ungelikwisha timizwa muda wao.
{وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ آيَتَيْنِ فَمَحَوْنَا آيَةَ اللَّيْلِ وَجَعَلْنَا آيَةَ النَّهَارِ مُبْصِرَةً لِتَبْتَغُوا فَضْلًا مِنْ رَبِّكُمْ وَلِتَعْلَمُوا عَدَدَ السِّنِينَ وَالْحِسَابَ وَكُلَّ شَيْءٍ فَصَّلْنَاهُ تَفْصِيلًا (12)}.
12. Na tumefanya usiku na mchana kuwa ishara mbili. Tena tukaifuta ishara ya usiku, na tukaifanya ishara ya mchana ni yenye mwangaza ili mtafute fadhila itokayo kwa Mola wenu Mlezi, na ili mpate kujua idadi ya miaka na hesabu. Na kila kitu tumekifafanua kwa kina waziwazi.
#
{12} يقول تعالى: {وجعلنا الليلَ والنهار آيتينِ}؛ أي: دالَّتين على كمال قدرة الله وسَعَة رحمته وأنَّه الذي لا تنبغي العبادة إلاَّ له. {فَمَحَوْنا آية الليل}؛ أي: جعلناه مظلماً للسكون فيه والراحة. {وجعلنا آيةَ النهارِ مبصرةً}؛ أي: مضيئة، {لتبتغوا فَضْلاً من ربِّكم}: في معايشكم وصنائعكم وتجاراتكم وأسفاركم، {ولتعلموا}: بتوالي الليل والنهار واختلاف القمر {عَدَدَ السنين والحسابَ}: فتبنون عليها ما تشاؤون من مصالحكم. {وكلَّ شيءٍ فصَّلْناه تفصيلاً}؛ أي: بيَّنَّا الآيات، وصرَّفناه لتتميز الأشياء، ويتبيَّن الحقُّ من الباطل؛ كما قال تعالى: {ما فرَّطْنا في الكتاب من شيءٍ}.
{12} Anasema Yeye Mtukufu, "Na tumefanya usiku na mchana kuwa ishara mbili" yenye kuashiria ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu na upana wa rehema yake, na kwamba Yeye tu ndiye anayestahiki kuabudiwa. "Tena tukaifuta ishara ya usiku;" yaani, tukaifanya kuwa na giza ili mtulie humo na mpate starehe. "Na tukaifanya ishara ya mchana ni yenye mwangaza, ili mtafute fadhila itokayo kwa Mola wenu Mlezi" katika maisha yenu, na shughuli zenu, na biashara zenu, na safari zenu, "na ili mpate kujua" kwa kufuatana usiku na mchana, na kutofautiana kwa mwezi, "idadi ya miaka na hesabu" ili mpate kujenga juu yake chochote mnachotaka katika masilahi yenu. "Na kila kitu tumekifafanua kwa kina waziwazi." Yaani, tumezibainisha ishara na kuzibadilishabadilisha ili mambo yaweze kupambanuka, na haki ibainike kutoka kwa batili, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema, "Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote."
{وَكُلَّ إِنْسَانٍ أَلْزَمْنَاهُ طَائِرَهُ فِي عُنُقِهِ وَنُخْرِجُ لَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ كِتَابًا يَلْقَاهُ مَنْشُورًا (13) اقْرَأْ كِتَابَكَ كَفَى بِنَفْسِكَ الْيَوْمَ عَلَيْكَ حَسِيبًا (14)}.
13. Na kila mtu tumemfungia matendo yake shingoni mwake. Na Siku ya Qiyama tutamtolea kitabu atakachokikuta ki wazi kimekunjuliwa. 14.
Ataambiwa: Soma kitabu chako! Nafsi yako inakutosha leo kukuhesabu.
#
{13 - 14} وهذا إخبارٌ عن كمال عدله: أنَّ كلَّ إنسان يُلْزِمُهُ طائِرَهُ في عنقِهِ؛ أي: ما عمل من خيرٍ وشرٍّ يجعله الله ملازماً له لا يتعدَّاه إلى غيره؛ فلا يحاسَبُ بعمل غيره ولا يحاسَبُ غيره بعمله. {ونخرِجُ له يوم القيامةِ كتاباً يلقاهُ منشوراً}: فيه عملُهُ من الخير والشرِّ حاضراً صغيرُهُ وكبيرُهُ، ويقال له: {اقرأ كتابَكَ كفى بنفسِكَ اليوم عليك حسيباً}: وهذا من أعظم العدل والإنصاف أن يقال للعبدِ: حاسِبْ نفسَكَ؛ ليعرف ما عليه من الحقِّ الموجب للعقاب.
{13-14} Na huku ni kujulisha kuhusu ukamilifu wa uadilifu wake: kwamba kila mutu amemfungia matendo yake shingoni mwake. Yaani, matendo ya heri na maovu aliyokifanya, Mwenyezi Mungu atayafanya kuwa pamoja naye, hayatamruka yakamwendea mwingine. Kwa hivyo hatahesabiwa kwa matendo ya wengine, wala wengine hawatahesabiwa kwa matendo yake. "Na siku ya Qiyama tutamtolea kitabu atakachokutana nacho kimekunjuliwa," kikiwa na matendo yake ndani yake mema na maovu yamehudhuria, madogo na makubwa. Na ataambiwa, "Soma kitabu chako! Nafsi yako inakutosha leo kukuhesabu." Na hili ni katika uadilifu mkubwa zadi na haki, kwamba mja aambiwe, 'Jifanyie hesabu mwenyewe' ili apate kujua haki iliyo juu yake inayolazimu aadhibiwe.
{مَنِ اهْتَدَى فَإِنَّمَا يَهْتَدِي لِنَفْسِهِ وَمَنْ ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيْهَا وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَى وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّى نَبْعَثَ رَسُولًا (15)}
15. Anayeongoka, basi anaongoka kwa ajili ya nafsi yake. Na anayepotea, basi anapotea kwa hasara yake mwenyewe. Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine. Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumtume Mtume.
#
{15} أي: هدايةُ كلِّ أحدٍ وضلاله لنفسه. لا يحمل أحدٌ ذنب أحدٍ، ولا يدفع عنه مثقالَ ذرَّة من الشرِّ، والله تعالى أعدل العادلين، لا يعذِّب أحداً حتى تقوم عليه الحجَّة بالرسالة ثم يعاند الحجَّة، وأما من انقاد للحجَّة أو لم تبلُغْه حجَّة الله تعالى؛ فإنَّ الله تعالى لا يعذِّب به. استدل بهذه الآية على أنَّ أهل الفترات وأطفال المشركين لا يعذِّبُهم الله حتى يبعثَ إليهم رسولاً؛ لأنَّه منزَّه عن الظُّلم.
{15} Yaani, kuongoka kwa kila mmoja na kupotoka kwake kunairudia nafsi yake mwenyewe. Hakuna mtu yeyote atakayebeba dhambi ya mwingine, wala hawezi kumzuilia hata uzito wa chembe ya uovu. Kwa maana, Mwenyezi Mungu ndiye mwadilifu zaidi ya waadilifu wote. Hamuadhibu mtu yeyote mpaka hoja imsimamie kwa ujumbe, kisha yeye mwenyewe tu aipinge hoja hiyo kwa ukaidi. Na ama mwenye kufuata hoja au hakufikiwa na hoja yoyote ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi Mwenyezi Mungu hamwadhibu kwa dhambi hiyo. Aya hii ilitumiwa kama ushahidi kwamba watu wa nyakati ambazo hakukuwa na mtume yeyote, na watoto wa washirikina hawataadhibiwa na Mwenyezi Mungu mpaka awatumie mjumbe. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu ametakasika na kufanya dhuluma.
{وَإِذَا أَرَدْنَا أَنْ نُهْلِكَ قَرْيَةً أَمَرْنَا مُتْرَفِيهَا فَفَسَقُوا فِيهَا فَحَقَّ عَلَيْهَا الْقَوْلُ فَدَمَّرْنَاهَا تَدْمِيرًا (16) وَكَمْ أَهْلَكْنَا مِنَ الْقُرُونِ مِنْ بَعْدِ نُوحٍ وَكَفَى بِرَبِّكَ بِذُنُوبِ عِبَادِهِ خَبِيرًا بَصِيرًا (17)}
16. Na pindi tukitaka kuuteketeza mji, tunawaamrisha wale wana starehe na taanusi wake, lakini wao wakaendelea kutenda maovu humo. Basi hapo kauli ikathibiti juu ya mji huo, nasi tukauangamiza kwa maangamizo makubwa. 17. Na kaumu ngapi tumeziangamiza baada ya Nuhu! Na Mola wako Mlezi anatosha kabisa kuwa ni Mwenye kuzijua na kuziona dhambi za waja wake.
#
{16} يخبر تعالى أنه إذا أراد أن يُهْلِكَ قريةً من القرى الظالمة ويستأصلها بالعذاب؛ أمر مُتْرَفيها أمراً قدريًّا، ففسقوا فيها، واشتدَّ طغيانُهم؛ {فحقَّ عليها القولُ}؛ أي: كلمة العذاب التي لا مردَّ لها؛ {فدمَّرْناها تدميراً}
{16} Yeye mtukufu anajulisha kwamba anapotaka kuangamiza moja ya miji dhalimu na kuuondoa kabisa kwa adhabu, anawaamrisha wana starehe wake amri ya kimajaaliwa, lakini wakafanya maovu humo, na upindukiaji wao mipaka ukawa mkubwa, "Basi hapo kauli ikathibiti juu ya mji huo." Yaani, neno la adhabu lisiloweza kuzuilika, "Nasi tukauangamiza kwa maangamizo makubwa."
#
{17} وهؤلاء أمم كثيرةٌ أبادهم الله بالعذاب من بعد قوم نوح؛ كعاد وثمود وقوم لوط وغيرهم ممَّن عاقبهم الله لما كَثُر بغيُهم واشتدَّ كفرُهم؛ أنزل الله بهم عقابَه العظيم. {وكفى بربِّك بذُنوب عبادِهِ خبيراً بصيراً}: فلا يخافوا منه ظلماً، وأنه يعاقبهم على ما عملوه.
{17} Na hizi ni umma ningi ambazo Mwenyezi Mungu aliziangamiza kwa adhabu baada ya kaumu ya Nuhu, kama vile 'Aadi, Thamud, kaumu ya Lut' na wengineo ambao Mwenyezi Mungu aliwaadhibu wakati dhuluma yao ilipokithiri na ukafiri wao ukawa mkubwa, Mwenyezi Mungu akawateremshia adhabu yake kubwa. "Na Mola wako Mlezi anatosha kabisa kuwa ni Mwenye kuzijua na kuziona dhambi za waja wake." Basi wasihofu kwamba atawadhulumu, na kwamba atawaadhibu kwa sababu ya yale waliyoyatenda tu.
{مَنْ كَانَ يُرِيدُ الْعَاجِلَةَ عَجَّلْنَا لَهُ فِيهَا مَا نَشَاءُ لِمَنْ نُرِيدُ ثُمَّ جَعَلْنَا لَهُ جَهَنَّمَ يَصْلَاهَا مَذْمُومًا مَدْحُورًا (18) وَمَنْ أَرَادَ الْآخِرَةَ وَسَعَى لَهَا سَعْيَهَا وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَئِكَ كَانَ سَعْيُهُمْ مَشْكُورًا (19) كُلًّا نُمِدُّ هَؤُلَاءِ وَهَؤُلَاءِ مِنْ عَطَاءِ رَبِّكَ وَمَا كَانَ عَطَاءُ رَبِّكَ مَحْظُورًا (20) انْظُرْ كَيْفَ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَى بَعْضٍ وَلَلْآخِرَةُ أَكْبَرُ دَرَجَاتٍ وَأَكْبَرُ تَفْضِيلًا (21)}.
18. Anayetaka yapitayo upesi upesi, tutafanya haraka kumletea hapa hapa tunayoyataka kwa tumtakaye. Kisha tumemwekea Jahannamu, ataingia humo hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa na kufurushwa. 19. Na anayeitaka Akhera, na akaifanyia juhudi ipasavyo ilhali ni Muumini, basi hao juhudi zao zitakuwa ni za kushukuriwa. 20. Wote hao tunawakunjulia, hawa na hao, katika vipawa vya Mola wako Mlezi. Wala vipawa vya Mola wako Mlezi havizuiliki. 21. Angalia vipi tulivyowafadhilisha baadhi yao kuliko wengine wao. Na hakika Akhera ni yenye daraja kubwa zaidi na fadhila kubwa zaidi.
#
{18} يخبر تعالى أن {مَن كان يريدُ}: الدنيا {العاجلة} المنقضية الزائلة، فعمل لها وسعى، ونسي المبتدأ أو المنتهى: أنَّ الله يعجِّل له من حطامها ومتاعها ما يشاؤه ويريده، مما كَتَبَ الله له في اللوح المحفوظ، ولكنَّه متاعٌ غير نافع ولا دائم له، ثم يجعل له في الآخرة {جهنَّم يَصْلاها}؛ أي: يباشر عذابها، {مذموماً مدحوراً}؛ أي: في حالة الخِزْي والفضيحة والذمِّ من الله ومن خلقِهِ والبعد عن رحمةِ الله، فيجمعُ له بين العذاب والفضيحة.
{18} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba "anayetaka" dunia hii ambayo ni katika yale "yapitayo upesi upesi" itakayoisha na kuondoka, kwa hivyo akafanya matendo kwa ajili yake na akatia bidii katika hilo, na akasahau mwanzo au mwisho, basi Mwenyezi Mungu anamharakishia katika kumpa vitu vyake visivyo na thamani, na vitu vyake vinginevyo chochote anachopenda na anachotaka katika yale ambayo Mwenyezi Mungu alimwandikia katika Ubao Uliohifadhiwa, lakini ni vitu visivyo na manufaa wala vya kudumu navyo, na kisha amemuwekea katika Akhera, "Jahannamu; ataingia humo" na kukabiliana na adhabu yake, "hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa na kufurushwa." Yaani, katika hali ya hizaya, fedheha, na kashfa kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kutoka kwa viumbe vyake na kuwekwa mbali na rehema za Mwenyezi Mungu, kwa hivyo akawa amemjumuishia adhabu na fedheha.
#
{19} {ومن أراد الآخرةَ}: فرضِيَها وآثرها على الدُّنيا، {وسعى لها سَعْيَها}: الذي دعت إليه الكتب السماويَّة والآثار النبويَّة، فعمل بذلك على قدر إمكانه، {وهو مؤمنٌ}: بالله وملائكته وكتبه ورسله واليوم الآخر. {فأولئك كان سعيُهم مشكوراً}؛ أي: مقبولاً منمًّى مدَّخراً، لهم أجرهم وثوابهم عند ربهم.
{19} "Na anayeitaka Akhera" na akairidhia na akaipendelea kuliko dunia, "Na akaifanyia juhudi ipasavyo" kama vitabu vya mbinguni na hadithi za Nabii zilivyofundisha, kwa hivyo akafanya hivyo kulingana na awezavyo, "ilhali ni Muumini" anayemwamini Mwenyezi Mungu, Malaika wake, vitabu vyake, mitume wake, na Siku ya Mwisho. "Basi hao juhudi zao zitakuwa ni za kushukuriwa." Yaani, zitakubaliwa na kukuzwa kuwekewa akiba, kwani wana ujira wao na thawabu zao kwa Mola wao Mlezi.
#
{20} ومع هذا؛ فلا يفوتُهم نصيبُهم من الدُّنيا؛ فكلًّا يُمِدُّه الله منها؛ لأنَّه عطاؤه وإحسانه. {وما كان عطاءُ ربِّك محظوراً}؛ أي: ممنوعاً من أحدٍ، بل جميعُ الخلق راتِعون بفضلِهِ وإحسانِهِ.
{20} Pamoja na hayo, hawapotezi fungu lao katika dunia, kwa maana wote Mwenyezi Mungu huwapa kwayo, kwa sababu ni kipawa chake na ihsani yake. "Wala vipawa vya Mola wako Mlezi havizuiliki." Yaani, hazuiliwi hivyo mtu yeyote, bali viumbe vyote hufurahia fadhila yake na ihisani zake.
#
{21} {انظرْ كيف فضَّلْنا بعضَهم على بعضٍ}: في الدُّنيا بسَعة الأرزاق وقلَّتها، واليُسْر والعُسْر، والعلم والجهل، والعقل والسَّفَه، وغير ذلك من الأمور التي فضَّل الله العباد بعضهم على بعض بها. {وللآخرةُ أكبرُ درجاتٍ وأكبرُ تفضيلاً}: فلا نسبة لنعيم الدُّنيا ولذَّاتها إلى الآخرة بوجه من الوجوه؛ فكم بين من هو في الغرف العاليات واللَّذَّات المتنوِّعات والسرور والخيرات والأفراح ممَّن هو يتقلَّب في الجحيم، ويعذَّب بالعذاب الأليم، وقد حلَّ عليه سَخَطُ الربِّ الرحيم، وكلٌّ من الدارين بين أهلها من التفاوت ما لا يمكنُ أحداً عدُّه.
{21} "Angalia vipi tulivyowafadhili baadhi yao kuliko wengine wao" katika dunia kwa upana na ukunjufu wa riziki, na urahisi na ugumu, na elimu na ujinga, akili na upumbavu, na vitu vingine ambavyo Mwenyezi Mungu amewafadhilisha kwavyo waja baadhi ya kuliko wengine wao. "Na hakika Akhera ni yenye daraja kubwa zaidi na fadhila kubwa zaidi." Hakuna ulinganisho kati ya neema za dunia hii na starehe zake na Akhera kwa njia yoyote ile. Ni wangapi miongoni mwa waliomo katika vyumba vya juu na starehe mbalimbali, furaha, na heri mbalimbali na ni miongoni mwa wale ambao wanageukageuka ndani ya Jahiim, na anaadhibiwa kwa adhabu chungu, na tayari alikwisha fikiwa na ghadhabu ya Mola Mlezi Mwingi wa rehema. Na kila moja ya nyumba hizi mbili kati ya watu wake kuna tofauti ambayo hakuna mtu anayeweza kuihesabu.
{لَا تَجْعَلْ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ فَتَقْعُدَ مَذْمُومًا مَخْذُولًا (22)}.
22. Usimfanye mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, ukaja ukawa wa kulaumiwa uliyetupika.
#
{22} أي: لا تعتقدْ أنَّ أحداً من المخلوقين يستحقُّ شيئاً من العبادة، ولا تشركْ بالله أحداً منهم؛ فإنَّ ذلك داع للذمِّ والخذلان؛ فالله وملائكته ورسله قد نَهَوْا عن الشرك، وذمُّوا من عمله أشدَّ الذمِّ، ورتَّبوا عليه من الأسماء المذمومة والأوصاف المقبوحة ما كان به متعاطيه أشنعَ الخلق وصفاً وأقبحهم نعتاً، وله من الخِذْلان في أمر دينه ودنياه بحسب ما تركه من التعلُّق بربِّه؛ فمن تعلَّق بغيره؛ فهو مخذولٌ قد وُكِلَ إلى مَن تعلَّق به، ولا أحد من الخلق ينفع أحداً إلا بإذن الله؛ وكما أنَّ مَن جعل مع الله إلهاً آخر له الذمُّ والخذلان؛ فمن وحَّده وأخلص دينه لله، وتعلَّق به دون غيره؛ فإنَّه محمودٌ مُعانٌ في جميع أحواله.
{22} Yaani, usiitakidi kwamba kuna yeyote katika viumbe anayestahili chochote katika ibada, na wala usimshirikishe Mwenyezi Mungu na yeyote miongoni mwao. Kwa maana, hilo linasababisha kulaumiwa na kutupwa. Kwani Mwenyezi Mungu, Malaika wake, na Mitume wake walikataza ushirikina, na wakamlaumu mwenye kuufanya lawama kubwa zaidi, na wakaliwekea majina yanayolaumiwa na sifa mbaya ambazo yeyote mwenye kusifika nazo anakuwa ndiye mwenye kuelezeka kwa maelezo mabaya zaidi ya viumbe vyote na mwenye sifa mbaya zaidi kati yao, naye atatupwa katika mambo ya dini yake na dunia yake kulingana na kile alichoacha cha kujifungamanisha na Mola wake Mlezi. Na yeyote mwenye kufungamana na asiyekuwa Yeye, basi huyo ametupwa, na amekabidhiwa yule ambaye alijifungamanisha naye. Na hakuna hata mmoja wa viumbe anayeweza kumfaidi mtu yeyote isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na kama vile mwenye kufanya mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu ana lawama na kutupwa, basi mwenye kumpwekesha na akamfanyia Mwenyezi Mungu tu dini yake, na akafungamana naye na si mwingine, basi yeye atasifiwa, na kusaidiwa katika hali zake zote.
{وَقَضَى رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِنْدَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُلْ لَهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُلْ لَهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا (23) وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُلْ رَبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا (24)}.
23. Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata, Ah! Wala usiwakemee. Na uwaambie maneno ya heshima. 24. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea rehema.
Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyonilea utotoni.
#
{23} لما نهى تعالى عن الشرك به؛ أمر بالتوحيد، فقال: {وقضى ربُّك}: قضاء دينيًّا، وأمر أمراً شرعيًّا {أن لا تعبُدوا}: أحداً من أهل الأرض والسماوات الأحياء والأموات، {إلاَّ إيَّاه}: لأنَّه الواحد الأحد، الفرد الصمد، الذي له كلُّ صفة كمال، وله من تلك الصفة أعظمها، على وجهٍ لا يشبهه أحدٌ من خلقه، وهو المنعِمُ بالنعم الظاهرة والباطنة، الدافع لجميع النِّقم، الخالق، الرازق، المدبِّر لجميع الأمور؛ فهو المتفرِّد بذلك كلِّه، وغيره ليس له من ذلك شيء. ثم ذكر بعد حقِّه القيام بحقِّ الوالدين، فقال: {وبالوالدين إحساناً}؛ أي: أحسنوا إليهما بجميع وجوه الإحسان القوليِّ والفعليِّ؛ لأنهما سببُ وجود العبد، ولهما من المحبَّة للولد والإحسان إليه، والقرب ما يقتضي تأكُّد الحقِّ ووجوب البرِّ. {إمَّا يَبْلُغَنَّ عندَكَ الكِبَرَ أحدُهما أو كلاهما}؛ أي: إذا وصلا إلى هذا السنِّ الذي تضعُفُ فيه قواهما ويحتاجان من اللُّطف والإحسان ما هو معروفٌ، {فلا تَقُلْ لهما أفٍّ}: وهذا أدنى مراتب الأذى، نبَّه به على ما سواه، والمعنى: لا تؤذِهِما أدنى أذيَّة، {ولا تَنْهَرْهُما}؛ أي: تزجُرهما وتتكلَّم لهما كلاماً خشناً. {وقلْ لهما قولاً كريماً}: بلفظٍ يحبَّانه، وتأدَّب وتلطَّف بكلام ليِّن حسن يلذُّ على قلوبهما، وتطمئنُّ به نفوسهما، وذلك يختلفُ باختلاف الأحوال والعوائد والأزمان.
{23} Yeye Mtukufu alipokataza kumshirikisha na chochote, akaamrisha kupwekeshwa, akasema, " Na Mola wako Mlezi ameamrisha" yaani amri ya kisheria, "kuwa msimuabudu" yeyote katika wakazi wa ardhi na mbingu, walio hai na wafu, "isipokuwa Yeye tu" kwa sababu Yeye ni Mmoja, wa Pekee, Mkusudiwa, ambaye ana kila sifa ya ukamilifu, na katika sifa hiyo ana kubwa yake zaidi, kwa njia ambayo hakuna yeyote katika viumbe wake anayefanana naye. Naye ndiye anayeneemesha kwa neema za dhahiri na za ndani, mwenye kuzuia kila adhabu, Muumba, Mwenye kuruzuku, Mwendashaji wa mambo yote. Yeye ndiye ambaye ni wa pekee katika yote hayo, na wasiokuwa yeye hana chochote katika hayo. Kisha akataja baada ya haki yake, kutekeleza haki ya wazazi, akasema, "Na wazazi wawili muwatendee wema" yaani, watendeeni wema kwa nyanja zote za wema wa kimaneno na kimatendo. Kwa sababu wao ndio sababu ya kuwepo kwa mja, nao wanampenda na kumfanyia mwanao wema, na wako karibu sana naye, jambo ambalo linahitaji kuisisitiza haki zao na ulazima wa kuwafanyia wema. "Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili," yaani, wanapofikia umri huu ambao nguvu zao zinadhoofika na wanahitaji upole na ihsani kama inavyojulikana, "usiwaambie hata, 'Ah!'" Na hiki ndicho kiwango cha chini kabisa cha kuwaudhi, ambacho alikitumia kama mfano kwa mengineyo. Na maana yake ni kwamba usiwaudhi kwa hata udhia mdogo zaidi. "wala usiwakemee", na kuwaambia maneno makali. "Na uwaambie maneno ya heshima;" kwa maneno wanayoyapenda, na kuwa na adabu na upole kwa maneno laini, mazuri, yenye kuifurahisha mioyo yao, na kutuliza roho zao, na hayo yanatofautiana kulingana na hali tofauti tofauti, ada na nyakati mbalimbali.
#
{24} {واخفضْ لهما جناحَ الذُّلِّ من الرحمةِ}؛ أي: تواضع لهما ذُلًّا لهما ورحمةً واحتساباً للأجر، لا لأجل الخوف منهما أو الرجاء لما لهما ونحو ذلك من المقاصد التي لا يؤجَر عليها العبد. {وقل ربِّ ارحَمْهما}؛ أي: ادعُ لهما بالرحمة أحياءً وأمواتاً؛ جزاءً على تربيتهما إيَّاك صغيراً. وفُهِمَ من هذا أنَّه كلَّما ازدادت التربيةُ؛ ازداد الحقُّ. وكذلك من تولَّى تربية الإنسان في دينِهِ ودُنياه تربيةً صالحةً غير الأبوين؛ فإنَّ له على مَن ربَّاه حقَّ التربية.
{24} "Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea rehema" yaani, uwanyenyekee kwa kujidhalilisha kwao, na rehema, na kutarajia thawabu, siyo kwa kuwahofu au kutumaini kile walicho nacho na mfano wa hayo miongoni mwa makusudio ambayo mja hulipwa juu yake.
"Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu" yaani, waombee rehema wakiwa hai na wakiwa wamekufa, kama malipo kwa kukulea wewe ulipokuwa mdogo. Na inaeleweka kutokana na hili kwamba kila malezi yanavyozidi, ndiyo haki pia inazidi. Na vile vile mwenye kumlea mtu katika dini yake na dunia yake malezi mema asiyekuwa wazazi wake, basi ana haki ya malezi kwa yule ambaye yeye alimlea.
{رَبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَا فِي نُفُوسِكُمْ إِنْ تَكُونُوا صَالِحِينَ فَإِنَّهُ كَانَ لِلْأَوَّابِينَ غَفُورًا (25)}
25. Mola wenu Mlezi anajua kabisa yaliyo nyoyoni mwenu. Ikiwa nyinyi mtakuwa wema, basi hakika Yeye ni Mwenye kuwaghufiria wanaorudi sana kwake.
#
{25} أي: ربُّكم تعالى مطَّلع على ما أكنَّته سرائركم من خير وشرٍّ، وهو لا ينظر إلى أعمالكم وأبدانكم، وإنما ينظر إلى قلوبكم وما فيها من الخير والشر. {إن تكونوا صالحين}: بأن تكون إرادتُكم ومقاصدكم دائرةً على مرضاة الله، ورغبتكم فيما يقربكم إليه، وليس في قلوبكم إرادات مستقرة لغير الله. {فإنَّه كان للأوَّابين}؛ أي: الرجَّاعين إليه في جميع الأوقات؛ {غفوراً}: فمن اطَّلع الله على قلبه، وعلم أنه ليس فيه إلاَّ الإنابة إليه ومحبَّته ومحبَّة ما يقرِّب إليه؛ فإنَّه وإن جرى منه في بعض الأوقات ما هو مقتضى الطبائع البشريَّة؛ فإنَّ الله يعفو عنه، ويغفر له الأمور العارضة غير المستقرَّة.
{25} Yaani, Mola wenu Mlezi, Mtukufu anajua yaliyofikichika katika siri zenu za heri na shari, naye haangalii matendo yenu na miili yenu, bali anaangalia nyoyo zenu na yaliyomo ndani yake ya heri na shari. "Ikiwa nyinyi mtakuwa wema" kwa namna kwamba utashi wenu na makusudio yenu zinazungukia kwenye radhi za Mwenyezi Mungu, na hamu yenu ni katika kile kinachowaleta karibu naye, na wala hamna utashi thabiti wa asiyekuwa Mwenyezi Mungu katika mioyo yenu, "basi hakika Yeye ni Mwingi wa kuwaghufiria wanaomrudia sana." Kwa hivyo na anajua yule ambaye Mwenyezi Mungu ameuangalia moyo wake na akajua kwamba hakuna chochote ndani yake isipokuwa kutubia kwake, kumpenda, na kupenda kile kinachomfanya kuwa karibu naye. Basi yeye hata kama wakati mwingine akifanya kile kilicho katika maumbile yake ya kibinadamu, basi Mwenyezi Mungu humsamehe, na humghufiria mambo yaliyomkuta tu na si ada yake wala hayafanyi mara kwa mara.
{وَآتِ ذَا الْقُرْبَى حَقَّهُ وَالْمِسْكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَلَا تُبَذِّرْ تَبْذِيرًا (26) إِنَّ الْمُبَذِّرِينَ كَانُوا إِخْوَانَ الشَّيَاطِينِ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِرَبِّهِ كَفُورًا (27) وَإِمَّا تُعْرِضَنَّ عَنْهُمُ ابْتِغَاءَ رَحْمَةٍ مِنْ رَبِّكَ تَرْجُوهَا فَقُلْ لَهُمْ قَوْلًا مَيْسُورًا (28) وَلَا تَجْعَلْ يَدَكَ مَغْلُولَةً إِلَى عُنُقِكَ وَلَا تَبْسُطْهَا كُلَّ الْبَسْطِ فَتَقْعُدَ مَلُومًا مَحْسُورًا (29) إِنَّ رَبَّكَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَنْ يَشَاءُ وَيَقْدِرُ إِنَّهُ كَانَ بِعِبَادِهِ خَبِيرًا بَصِيرًا (30)}.
26. Na mpe aliye jamaa yako haki yake, na masikini, na msafiri; wala usitumie ovyo kwa fujo. 27. Hakika wabadhirifu ni ndugu wa Mashetani. Na Shetani ni mwenye kumkufuru mno Mola wake Mlezi. 28. Na ikiwa ukiwapa mgongo sawasawa, nawe unatafuta rehema kutoka kwa Mola wako Mlezi unayoitaraji, basi sema nao maneno laini. 29. Wala usiufanye mkono wako kama uliofungwa shingoni mwako, wala usiukunjue wote kabisa, ukabaki ukilaumiwa muflisi. 30. Hakika Mola wako Mlezi humkunjulia riziki amtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika Yeye kwa waja wake ni Mwenye kuwajua na kuwaona vyema.
#
{26 - 27} يقول تعالى: {وآت ذا القُربى حقَّه}: من البرِّ والإكرام الواجب والمسنون، وذلك الحقُّ يتفاوت بتفاوت الأحوال والأقارب والحاجة وعدمها والأزمنة، {والمسكينَ}: آته حقَّه من الزَّكاة ومن غيرها؛ لتزول مسكنتُه، {وابنَ السبيل}: وهو الغريب المنقطع به عن بلده، فيُعْطى الجميع من المال، على وجهٍ لا يضرُّ المعطي، ولا يكون زائداً على المقدار اللائق؛ فإنَّ ذلك تبذيرٌ، قد نهى الله عنه وأخبر: إنَّ المبذِّرين {إخوانُ الشياطين}: لأنَّ الشيطان لا يدعو إلاَّ إلى كلِّ خَصلة ذميمةٍ، فيدعو الإنسان إلى البخل والإمساك؛ فإذا عصاه؛ دعاه إلى الإسراف والتبذير، والله تعالى إنَّما يأمُرُ بأعدل الأمور وأقسطِها، ويمدحُ عليه؛ كما في قوله عن عباد الرحمن الأبرار: {والذين إذا أنفقوا لم يُسْرِفوا ولم يَقْتُروا وكان بين ذلك قَواماً}.
{26-27} Yeye Mtukufu anasema, "Na mpe aliye jamaa yako haki yake" kama vile kumfanyia wema, na kumkirimu kwa wajibu na kusiko kwa wajibu. Na haki hizo zinatofautiana kulingana na hali tofauti tofauti, jamaa, mahitaji, na kutohitaji, na nyakati. "Na maskini" mpe haki yake katika mali ya zakat yake na mali nynginezo, ili umaskini wake uishe. "Na msafiri aliyekatikiwa" ambaye hayukao katika mji wake. Kwa hivyo wote watapewa katika maili hiyo kwa njia ambayo haimdhuru mtoaji, na wala isiyozidi kiasi kinachofaa. Kwa maana, hilo kutumia ovyo kwa fujo ambako Mwenyezi Mungu alikataza na akasema kwamba hakika watumiao ovyo kwa fujo, "ni ndugu wa mashetani." Kwa sababu Shetani analingania katika sifa inayokashifiwa. Basi yeye humuita mtu katika ubahili na kushikilia mali bila ya kuitoa. Kwa hivyo, anapomuasi, anamuita katika kupitiliza kiasi na kutoa ovyo kwa fujo. Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu anaamrisha kutenda mambo yenye uadilifu mkubwa zaidi na ya haki zaidi, na anasifu juu yake, kama ilivyo katika kauli yake kuhusu waja wa Mwingi wa rehema walio wema. "Na wale ambao wanapotoa mali zao, hawatoi kwa kupitiliza kiasi wala hawafanyi ubahili, bali wanasimama sawasawa katikati baina ya hayo."
#
{29} وقال هنا: {ولا تجعل يَدَكَ مغلولةً إلى عنقك}: كناية عن شدة الإمساك والبخل، {ولا تَبْسُطْها كلَّ البسط}: فتنفق فيما لا ينبغي أو زيادة على ما ينبغي، {فتقعدَ}: إن فعلت ذلك {مَلوماً}؛ أي: تُلام على ما فعلتَ، {مَحْسوراً}؛ أي: حاسر اليد فارغها؛ فلا بقي ما في يدك من المال، ولا خَلَفَه مدحٌ وثناءٌ.
{29} Na akasema hapa, "Na usifanye mkono wako umefungwa shingoni mwako." Nayo ni sitiari ya ugumu wa kushikilia mali na ubahili. "Wala usiukunjue wote kabisa." Kwa hivyo ukatoa mali katika kile ambacho hupaswi au ukatoa zaidi ya kile unachopaswa; "ukabaki," ikiwa utafanya hivyo; "ukilaumiwa" juu ya yale uliyofanya, "muflisi" bila ya kubakia na mali mikononi mwako, na tena hata hukusifiwa kwa hilo.
#
{28} وهذا الأمر بإيتاء ذي القربى مع القدرة والغنى، فأمَّا مع العُدْم أو تعسُّر النفقة الحاضرة؛ فأمر تعالى أن يُردُّوا ردًّا جميلاً، فقال: {وإمَّا تعرضَنَّ عنهم ابتغاءَ رحمةٍ من ربِّك ترجوها}؛ أي: تعرض عن إعطائِهِم إلى وقت آخر ترجو فيه من الله تيسير الأمر. {فقُلْ لهم قولاً ميسوراً}؛ أي: لطيفاً برفقٍ ووعد بالجميل عند سُنوح الفرصة واعتذارٍ بعدم الإمكان في الوقت الحاضر؛ لينقلبوا عنك مطمئنَّة خواطرهم؛ كما قال تعالى: {قولٌ معروفٌ ومغفرةٌ خيرٌ من صدقةٍ يَتْبَعُها أذى}: وهذا أيضاً من لطف الله تعالى بالعباد، أمرهم بانتظار الرحمة والرزق منه؛ لأنَّ انتظار ذلك عبادة، وكذلك وعدُهم بالصدقة والمعروف عند التيسُّر عبادةٌ حاضرةٌ؛ لأنَّ الهمَّ بفعل الحسنة حسنةٌ، ولهذا ينبغي للإنسان أن يفعل ما يَقْدِرُ عليه من الخير، وينوي فعل ما لم يقدِرْ عليه لِيُثاب على ذلك، ولعلَّ الله ييسِّر له بسبب رجائه.
{28} Amri hii ya kuwapa jamaa ni kulingana na uwezo na utajiri. Ama ikiwa mtu hana na ana uchache katika kutekeleza matumizi ya sasa, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaamuru warudishe majibu mazuri. Akasema, "Na ikiwa utawapa mgongo, nawe unatafuta rehema ya Mola wako Mlezi unayoitaraji." Yaani, ikiwa utawapa mgongo usiwape kitu hadi wakati mwingine ambao unatarajia Mwenyezi Mungu kufanya mambo kuwa mepesi. "Basi sema nao maneno laini." Yaani, kwa upole na kutokuwa mgumu, na kuwapa ahadi ya kuwafanyia mazuri fursa itatokea na uombe udhuru wa kutoweza kufanya hivyo kwa wakati huu, ili waondoke kutoka kwako hali ya kuwa mawazo yao yametulia. Kama Mwenyezi Mtukufu alivyosema, "Kauli njema na usamehevu ni bora kuliko sadaka inayofuatiliwa na maudhi." Hili pia ni katika upole wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake, ambapo aliwaamuru wasubiri rehema na riziki kutoka kwake, kwa sababu kungojea hilo ni ibada. Na vile vile ahadi yao ya kutoa sadaka na kufanya wema katika hali ya wepesi ni ibada ya sasa. Kwa sababu kuazimia kufanya matendo mazuri ni jambo zuri. Na kwa hivyo mtu anapaswa kufanya kile anachoweza kufanya ya heri, na akusudie kufanya kile asichoweza kufanya ili alipwe kwa hilo, na labda Mwenyezi Mungu anaweza kumrahisishia kwa sababu ya tumaini lake.
#
{30} ثم أخبر تعالى: أنَّ اللهَ {يبسُطُ الرزق لمن يشاء}: من عباده ويقدِرُه ويضيِّقه على من يشاء حكمةً منه. {إنَّه كان بعبادِهِ خبيراً بصيراً}: فيَجْزيهم على ما يعلمُهُ صالحاً لهم، ويدبِّرهم بلطفه وكرمه.
{30} Kisha Yeye Mtukufu akajulisha kwamba Mwenyezi Mungu, "humkunjulia riziki amtakaye" katika waja wake, na anaipima, na kuifanya kuwa finyu kwa amtakaye kwa sababu ya hekima itokayo kwake. "Hakika Yeye kwa waja wake ni Mwenye kuwajua na kuwaona." Kwa hivyo atawapa kwa kile anachojua kwamba ni chema kwao, na atawasimamia kwa upole wake ukarimu wake.
{وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُمْ خَشْيَةَ إِمْلَاقٍ نَحْنُ نَرْزُقُهُمْ وَإِيَّاكُمْ إِنَّ قَتْلَهُمْ كَانَ خِطْئًا كَبِيرًا (31)}.
31. Wala msiwaue wana wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua hao kulikuwa ni kosa kubwa.
#
{31} وهذا من رحمته بعباده؛ حيث كان أرحم بهم من والديهم، فنهى الوالدين أن يقتُلوا أولادهم خوفاً من الفقر والإملاق، وتكفَّل برزق الجميع، وأخبر أنَّ: {قَتْلَهم كان خِطْئاً كبيراً}؛ أي: من أعظم كبائر الذنوب؛ لزوال الرحمة من القلب، والعقوق العظيم، والتجرِّي على قتل الأطفال الذين لم يجرِ منهم ذنبٌ ولا معصيةٌ.
{31} Na hii ni katika rehema yake kwa waja wake, ambapo alikuwa na mwenye rehema kwao zaidi ya wazazi wao, kwa hivyo akawakataza wazazi kuwaua watoto wao kwa kuogopa umasikini, na akaweka dhamana ya kuwaruzuku wote. Na akajulisha kuwa, "Kuwaua hao kulikuwa ni kosa kubwa," yaani, moja ya madhambi makubwa, kwa sababu ya kuondolewa kwa rehema kutoka moyoni, na kutotii kukubwa sana, na kuthubutu kuwaua watoto ambao hawana dhambi yoyote wala hawakuasi.
{وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَا إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا (32)}.
32. Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya.
#
{32} والنهي عن قربانه أبلغ من النهي عن مجرَّد فعله؛ لأنَّ ذلك يشمل النهي عن جميع مقدّماته ودواعيه؛ فإنَّ من حام حول الحمى يوشك أن يقع فيه، خصوصاً هذا الأمر الذي في كثير من النفوس أقوى داع إليه، ووصف الله الزِّنا وقبْحه بأنه {كان فاحشةً}؛ أي: إثماً يُستفحش في الشرع والعقل والفِطَر؛ لتضمُّنه التجرِّي على الحرمة في حقِّ الله وحقِّ المرأة وحقِّ أهلها أو زوجها وإفساد الفراش واختلاط الأنساب وغير ذلك من المفاسد. وقوله: {وساء سبيلاً}؛ أي: بئس السبيل سبيلُ من تجرَّأ على هذا الذنب العظيم.
{32} Na kukataza kuikaribia zina kuna maana kubwa zaidi kuliko kukataza kuifanya tu, kwa sababu hilo linajumisha kukatazwa kwa matangulizi yake yote na sababu zake. Kwa maana, yeyote mwenye kuzunguka karibu na himaya, anakaribia kuanguka ndani yake, hasa jambo hili, ambalo ndani ya nafsi nyingi kuna sababu za nguvu za kuliitia. Na Mwenyezi Mungu aliuelezea uzinzi na ubaya wake kwamba ni, "uchafu." Yaani, dhambi inayojulikana uchafu wake katika sheria, na akili, na maumbile ya asili, kwa sababu unajumuisha kuthubutu kufanya maharamisho yanayohusiana na Mwenyezi Mungu, na mwanamke, na familia yake au mumewe, kuharibu malazi yao, na kuchanganya nasaba, na uharibifu mwingine. Na kauli yake, "na njia mbaya" yaani, njia mbaya zaidi ni njia ya mwenye kuthubutu kutenda dhambi hili kubwa.
{وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَمَنْ قُتِلَ مَظْلُومًا فَقَدْ جَعَلْنَا لِوَلِيِّهِ سُلْطَانًا فَلَا يُسْرِفْ فِي الْقَتْلِ إِنَّهُ كَانَ مَنْصُورًا (33)}.
33. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipokuwa kwa haki. Na aliyeuliwa kwa kudhulumiwa, basi hakika tumempa msimamizi wake mamlaka. Lakini asipitilize kiasi katika kuua. Kwani yeye anasaidiwa.
#
{33} وهذا شاملٌ لكلِّ نفس حرَّم الله قتلَها من صغير وكبير وذكر وأنثى وحرٍّ وعبد ومسلم وكافرٍ له عهد، {إلاَّ بالحق}: كالنفس بالنفس، والزاني المحصن، والتارك لدينه المفارق للجماعة، والباغي في حال بغيه إذا لم يندفع إلاَّ بالقتل. {ومَن قُتِلَ مظلوماً}؛ أي: بغير حقٍّ، {فقد جَعَلْنا لوليِّه}: وهو أقرب عَصَباته وورثتِهِ إليه {سلطاناً}؛ أي: حجة ظاهرة على القصاص من القاتل، وجعلنا له أيضاً تسلُّطاً قدريًّا على ذلك، وذلك حين تجتمع الشروط الموجبة للقصاص؛ كالعمد العدوان والمكافأة. {فلا يسرفْ}: الولي {في القتل إنَّه كان منصوراً}: والإسراف مجاوزةُ الحدِّ: إما أن يمثِّل بالقاتل، أو يقتُله بغير ما قَتَلَ به، أو يَقْتُلَ غير القاتل. وفي هذه الآية دليلٌ إلى أنَّ الحقَّ في القتل للوليِّ؛ فلا يُقْتَص إلاَّ بإذنه، وإن عفا؛ سقط القصاص، وأنَّ وليَّ المقتول يُعينه الله على القاتل ومن أعانه، حتى يتمكَّن من قتله.
{33} Na hili linajumuisha kila nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharamisha sawa iwe ni ndogo, kubwa, ya kiume, ya kike, huru, ya mtumwa, ya Mwislamu, na ya kafiri ambaye ana agano ya amani na Waislamu. "Isipokuwa kwa haki" kama vile kuua nafsi kwa sababu nafsi hiyo iliua pia, mzinzi aliyeoleka, mwenye kuiacha dini yake ya Uislamu na akajitenga na kundi la Waislamu, na wale wanaompiga vita kiongozi mkuu katika hali ya vita vyao ikiwa hawawezi kuzuilika isipokuwa kwa kuwaua. "Na aliyeuawa kwa kudhulumiwa." Yaani, bila haki, "basi hakika tumempa mamlaka" yaani hoja iliyo dhahiri ya kufanya kisasi kama vile kuua muuaji, "mrithi wake" naye ni yule aliye karibu zaidi na maiti miongoni mwa warithi wanaochukua mali iliyosalia au warithi wengineo. Na pia tumempa mamlaka ya kimajaaliwa juu ya hilo, wakati masharti ya adhabu ya kisasi yatakapotimizwa, kama vile mauaji ya makusudi, kukiuka mipaka, nafsi mbili hizo kutoshana. "Lakini asipitilize kiasi" mrithi huyo "katika kuua, kwani yeye anasaidiwa." Na kupitiliza kiasi ni kuvuka mipaka, ima kwa kumkatakata anayemuua huyo, au kumuua kwa kile ambacho hakumuua kwacho, au kumuua muuaji halisi. Na katika aya hii, kuna ushahidi kwamba haki ya kuua ni ya mrithi wake, kwa hivyo hairuhusiki kufanya kisasi isipokuwa kwa idhini yake .Na ikiwa atasamehe, basi adhabu ya kisasi hiyo itaanguka, na kwamba mrithi wa aliyeuawa anasaidiwa na Mwenyezi Mungu dhidi ya muuaji na wale waliomsaidia mpaka aweze kumuua naye pia.
{وَلَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ حَتَّى يَبْلُغَ أَشُدَّهُ وَأَوْفُوا بِالْعَهْدِ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْئُولًا (34)}.
34. Wala msiyakaribie mali ya yatima, isipokuwa kwa njia iliyo nzuri zaidi, mpaka afike utu uzimani. Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itaulizwa.
#
{34} وهذا من لطفه ورحمته باليتيم الذي فَقَدَ والده وهو صغيرٌ غير عارف بمصلحة نفسه ولا قائمٌ بها أنْ أمر أولياءه بحفظه وحفظ ماله وإصلاحه وأنْ لا يَقْرَبوهُ {إلاَّ بالتي هي أحسنُ}: من التِّجارة فيه وعدم تعريضه للأخطار والحرص على تنميته، وذلك ممتدٌّ إلى أن يبلغَ اليتيمُ {أشدَّه}؛ أي: بلوغه وعقله ورشده؛ فإذا بَلَغَ أشدَّه؛ زالت عنه الولايةُ، وصار وليَّ نفسه، ودفع إليه ماله؛ كما قال تعالى: {فإنْ آنَسْتُم منهم رُشْداً فادْفَعوا إليهم أموالَهم}، {وأوفوا بالعهدِ}: الذي عاهدتم الله عليه، والذي عاهدتم الخلق عليه. {إنَّ العهد كان مَسْؤولاً}؛ أي: مسؤولين عن الوفاء به وعدمه؛ فإن وفيتم؛ فلكم الثواب الجزيل، وإن لم تفعلوا ؛ فعليكم الإثم العظيم.
{34} Na hili ni katika upole wake na rehema yake kwa yatima yule ambaye alipoteza baba yake hali ya kuwa ni mdogo na bado hajajua masilahi yake mwenyewe na hata hawezi kuyatekeleza. Basi akamuamuru wasimamizi wake kumhifadhi na kuhifadhi mali yake na kuitengeneza, na kwamba wasiikaribie, "isipokuwa kwa kilicho kizuri zaidi" kama vile kuifanyia biashara, kutotia katika mambo hatari, na kufanya bidii ya kuikuza, na hayo yanafaa kuendelea hadi yatima atakapofikia "utu uzima wake." Yaani, atakapobaleghe na akapata akili komavu na akafanya mambo ya busara. Basi atakapofika utu uzima wake, ulezi ulio juu yake unaisha na anaweza sasa kujisimamia mwenyewe, na hapo atapewa mali yake. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Mkiwaona ni werevu, basi wapeni mali yao." "Na kutimiza agano" ambalo mlimpa Mwenyezi Mungu, na ambayo mliagana na viumbe. "Kwa hakika ahadi itaulizwa juu yake." Yaani, mtaulizwa ikiwa mliitimiza au la. Kwa hivyo, ikiwa mlitimiza, basi mna thawabu nyingi. Na kama hamkufanya hivyo, basi mna dhambi kubwa.
{وَأَوْفُوا الْكَيْلَ إِذَا كِلْتُمْ وَزِنُوا بِالْقِسْطَاسِ الْمُسْتَقِيمِ ذَلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا (35)}.
35. Na timizeni kipimo mnapopima. Na pimeni kwa mizani zilizo sawa. Hayo ni heri na yenye mwisho bora.
#
{35} وهذا أمرٌ بالعدل وإيفاء المكاييل والموازين بالقسط من غير بخسٍ ولا نقص. ويؤخذ من عموم المعنى، النهي عن كلِّ غشٍّ في ثمنٍ أو مثمَّنٍ أو معقودٍ عليه، والأمر بالنُّصح والصدق في المعاملة. {ذلك خيرٌ}: من عدمه، {وأحسنُ تأويلاً}؛ أي: أحسن عاقبة، به يسلم العبد من التَّبِعات، وبه تنزل البركة.
{35} Hili ni amri ya kufanya uadilifu na kutimiza vipimo vya wingi na vipimo vya uzito kwa haki bila ya kupunja wala kupunguza. Na inachukuliwa kutoka kwa maana yake ya jumla, kukataza kila ulaghai katika bei au bidhaa au chochote kinachofungiwa mkataba juu yake, na pia kuna amri ya kupena nasiha na kuwa mkweli katika miamala. "Hayo ni heri" kuliko kutofanya hivyo, "na yenye mwisho mzuri zaidi." Yaani, mwisho mwema, kwa hilo mja anasalimika kutokana lawama mbalimbali, na kwa hayo ndiyo baraka huteremka.
{وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا (36)}.
36. Wala usiyafuate usiyo na elimu nayo. Hakika kusikia, na kuona, na moyo hivyo vyote itaulizwa juu yake.
#
{36} أي: ولا تتَّبع ما ليس لك به علم، بل تثبَّت في كلِّ ما تقوله وتفعله؛ فلا تظنَّ ذلك يذهب لا لك ولا عليك. {إنَّ السمع والبصر والفؤاد كلُّ أولئك كان عنه مسؤولاً}: فحقيق بالعبد الذي يعرف أنه مسؤول عما قاله وفعله وعما استعمل به جوارحه التي خلقها الله لعبادته أن يُعِدَّ للسؤال جواباً، وذلك لا يكون إلاَّ باستعمالها بعبوديَّة الله، وإخلاص الدِّين له، وكفِّها عما يكرهه الله تعالى.
{36} Yaani, usifuate kile usichokijua, lakini thibitisha kwanza katika kila kitu unachosema na kufanya, na usifikiri kwamba hayo yataisha tu hivyo kwa njia ya kwamba si kwa manufaa yako wala ati hautalaumiwa. "Hakika kusikia, na kuona, na moyo vyote hivyo itaulizwa juu yake." Basi inampasa zaidi mja anayejua kwamba ataulizwa juu ya kile alichosema na kufanya na juu ya kile alichotumia viungo vyake ambavyo Mwenyezi Mungu aliviumba kwa ajili ya ibada yake kwamba aliandalie swali jibu. Na hilo haliwi kwa kuvitumia tu katika kumuabudu Mwenyezi Mungu, na kumfanyia yeye tu Dini, na kuvizuia kutokana na vyote ambavyo Mwenyezi Mungu Mtukufu anakichukia.
{وَلَا تَمْشِ فِي الْأَرْضِ مَرَحًا إِنَّكَ لَنْ تَخْرِقَ الْأَرْضَ وَلَنْ تَبْلُغَ الْجِبَالَ طُولًا (37) كُلُّ ذَلِكَ كَانَ سَيِّئُهُ عِنْدَ رَبِّكَ مَكْرُوهًا (38) ذَلِكَ مِمَّا أَوْحَى إِلَيْكَ رَبُّكَ مِنَ الْحِكْمَةِ وَلَا تَجْعَلْ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ فَتُلْقَى فِي جَهَنَّمَ مَلُومًا مَدْحُورًا (39)}.
37. Wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi na kamwe huwezi kufikia urefu wa milima. 38. Hayo yote ubaya wake ni wenye kuchukiza kwa Mola wako Mlezi. 39. Hayo ni katika hekima alizokufunulia Mola wako Mlezi. Wala usimweke pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwengine, ukaja ukatupwa katika Jahannamu ukilaumiwa na kufurushwa.
#
{37} يقول تعالى: {ولا تمشِ في الأرض مَرَحاً}؛ أي: كبراً وتيهاً وبطراً متكبِّراً على الحقِّ ومتعاظماً على الخلق. {إنَّك}: في فعلك ذلك {لن تَخْرِقَ الأرض ولن تبلُغَ الجبال طولاً}: في تكبُّرك بل تكون حقيراً عند الله، ومحتقراً عند الخلق، مبغوضاً، ممقوتاً، قد اكتسبت شرَّ الأخلاق، واكتسيت بأرذلها، من غير إدراك لبعض ما تروم.
{37} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, "wala usitembee katika ardhi kwa maringo" yaani, kwa kiburi, kuikataa haki kujiinua juu ya viumbe. "Hakika wewe" kwa kufanya hivyo, "na kamwe huwezi kufikia urefu wa milima" katika kufanya kwao kiburi, bali utadharauliwa kwa Mwenyezi Mungu, na pia utadharauliwa kwa waja wake, na kuchukiwa, kwa maana umeshakuwa na tabia mbaya zaidi, na ukavaa za chini zake zaidi tena bila ya kufikia hata baadhi ya yale unayotafuta.
#
{38} {كل ذلك}: المذكور الذي نهى الله عنه فيما تقدَّم من قوله: {لا تَجْعَلْ مع الله إلهاً آخر}، والنهي عن عقوق الوالدين، وما عُطِف على ذلك، {كان سَيِّئُهُ عند ربِّك مكروهاً}؛ أي: كل ذلك يسوء العاملين ويضرُّهم والله تعالى يكرهه ويأباه.
{38}"Haya yote" yaliyotajwa, ambayo Mwenyezi Mungu alikataza hapo awali katika kauli yake, "Usimfanye mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu." Na katazo la kuwaasi wazazi, na yote yaliyofungamanishwa na hayo, "ubaya wake ni wenye kuchukiza kwa Mola wako Mlezi." Yaani, yote hayo ni mabaya kwa mwenye kuyatenda na yanawadhuru, na Mwenyezi Mungu Mtukufu anayachukia na anayakataa.
#
{39} {ذلك} الذي بيَّنَّاه ووضَّحناه من هذه الأحكام الجليلة، {مما أوحى إليك ربُّك من الحكمة}: فإنَّ الحكمة الأمر بمحاسن الأعمال ومكارم الأخلاق والنهي عن أراذل الأخلاق وأسوأ الأعمال. وهذه الأعمال المذكورة في هذه الآيات من الحكمة العالية التي أوحاها ربُّ العالمين لسيِّد المرسلين في أشرف الكتب ليأمر بها أفضل الأمم؛ فهي من الحكمة التي من أوتيها؛ فقد أوتي خيراً كثيراً. ثم ختمها بالنهي عن عبادة غير الله كما افتتحها بذلك، فقال: {ولا تَجْعَلْ مع الله إلهاً آخر فَتُلقى في جهنَّم}؛ أي: خالداً مخلَّداً؛ فإنَّه من يُشْرِك بالله فقد حرَّم الله عليه الجنة ومأواه النار. {مَلوماً مَدْحوراً}؛ أي: قد لحقتك اللائمة واللعنة والذمُّ من الله وملائكته والناس أجمعين.
{39} "Hayo" ambayo tumeyaelezea na kuyaweza wazi miongoni mwa hukumu hizi kubwa, "ni katika hekima alizokufunulia Mola wako Mlezi." Kwa maana, hekima ni kuamrisha matendo mazuri na tabia nzuri, na kukataza tabia duni na matendo mabaya. Matendo haya yaliyotajwa katika Aya hizi ni katika hekima ya juu ambayo Mola Mlezi wa walimwengu wote alimfunulia bwana wa Mitume wote katika kitabu kitukufu zaidi, ili awaamuru hayo umma bora zaidi. Na hayo ni katika hekima ambayo mwenye kupewa, basi hakika amepewa heri nyingi. Kisha akazihitimisha Aya hizi kwa kukataza kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu kama alivyozifungua kwa hilo, akasema, "Wala usimweke pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwengine, ukaja ukatupwa katika Jahannamu." Yaani, ukadumu humo. Kwa maana, mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ameshamharamishia Pepo, na mahali pake ni Motoni. "Ukilaumiwa na kufurushwa;" yaani, utafuatwa na lawama, na laana, na kashfa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Malaika wake, na watu wote.
{أَفَأَصْفَاكُمْ رَبُّكُمْ بِالْبَنِينَ وَاتَّخَذَ مِنَ الْمَلَائِكَةِ إِنَاثًا إِنَّكُمْ لَتَقُولُونَ قَوْلًا عَظِيمًا (40)}.
40. Je, Mola wenu Mlezi amewateulia nyinyi wavulana, na Yeye akawafanya Malaika ni banati zake? Kwa hakika nyinyi mnasema kauli kubwa.
#
{40} وهذا إنكارٌ شديدٌ على من زَعَمَ أنَّ الله اتَّخذ من خلقه بنات، فقال: {أفأصفاكم ربُّكم بالبنين}؛ أي: اختار لكم الصَّفوة والقسم الكامل، {واتَّخذ}: لنفسه {من الملائكة إناثاً}: حيث زعموا أن الملائكة بنات الله. {إنَّكُم لَتَقُولُونَ قَولاً عَظِيماً}: فيه أعظم الجرأة على الله، حيث نسبتُم له الولد المتضمِّن لحاجته، واستغناء بعض المخلوقات عنه، وحكموا له بأردأ القسمين، وهن الإناث، وهو الذي خلقكم واصطفاكم بالذكور، فتعالى الله عما يقول الظالمون علوًّا كبيراً.
{40} Na hili ni katazo kubwa kwa mwenye kudai kwamba Mwenyezi Mungu amejifanyia mabinti kutoka kwa viumbe wake, akasema, "Je, Mola wenu Mlezi aliwateulia nyinyi wavulana." Yaani, aliwachagulia nyinyi walio bora zaidi na kundi lililo kamili, "naye akawafanya Malaika ni banati zake," ambapo washirikina walidai kwamba Malaika ni binti za Mwenyzi Mungu. "Kwa hakika nyinyi mnasema kauli kubwa" ambayo ndani yake kuna kumfanyia Mwenyezi Mungu ujasiri mkubwa zaidi, ambapo mlimnasibisha na mwana, jambo ambalo linamaanisha kwamba anahitaji kuwa na mwana, na kwamba baadhi ya viumbe hawamhitaji, na tena wakampa Yeye mgao duni zaidi katika migao hiyo miwili, ambao ni wanawake. Ilhali Yeye ndiye aliyewaumba nyinyi na akawateulia wanaume. Basi ametukuka juu kabisa na ambayo madhalimu wanayasema.
{وَلَقَدْ صَرَّفْنَا فِي هَذَا الْقُرْآنِ لِيَذَّكَّرُوا وَمَا يَزِيدُهُمْ إِلَّا نُفُورًا (41) قُلْ لَوْ كَانَ مَعَهُ آلِهَةٌ كَمَا يَقُولُونَ إِذًا لَابْتَغَوْا إِلَى ذِي الْعَرْشِ سَبِيلًا (42) سُبْحَانَهُ وَتَعَالَى عَمَّا يَقُولُونَ عُلُوًّا كَبِيرًا (43) تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالْأَرْضُ وَمَنْ فِيهِنَّ وَإِنْ مِنْ شَيْءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِ وَلَكِنْ لَا تَفْقَهُونَ تَسْبِيحَهُمْ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا (44)}.
41. Na tumekwisha bainisha katika Qur'ani hii ili wapate kukumbuka. Lakini haikuwazidisha ila kuwa mbali nayo. 42.
Sema: Lau kuwa wangelikuwa pamoja naye miungu mingine kama wasemavyo, basi wangelitafuta njia ya kumfikia Mwenye Kiti cha Enzi. 43. Subhanahu Wa Taa'la,
(Ametakasika na Ametukuka juu) kabisa na hayo wanayoyasema. 44. Zinamtakasa zote mbingu saba na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake. Na hapana kitu ila kinamtakasa kwa sifa zake. Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake. Hakika Yeye ni Mpole na Mwenye maghfira.
#
{41} يخبر تعالى أنه صرَّف لعباده في هذا القرآن؛ أي: نوَّع الأحكام ووضَّحها وأكثر من الأدلَّة والبراهين على ما دعا إليه، ووعظ وذكَّر لأجل أن يتذكَّروا ما ينفعهم فيَسْلُكوه وما يضرُّهم فيدعوه، ولكن أبى أكثر الناس {إلاَّ نفوراً} عن آيات الله؛ لبغضهم للحقِّ ومحبَّتهم ما كانوا عليه من الباطل، حتى تعصَّبوا لباطلهم، ولم يُعيروا آيات الله لهم سمعاً، ولا ألقَوْا لها بالاً.
{41} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba amekwisha wabainishia waja wake katika Qur-ani hii, kwa kuweka hukumu anuai na akaziweka wazi na akaziwekea ushahidi mwingi na hoja juu ya kile alicholingania, na akaaidhi, na akakumbusha ili wakumbuke yenye kuwafaidi, kwa hivyo wayafuate, na yenye kuwadhuru, kwa hivyo wakiache. Lakini walikataa wengi wa watu "isipokuwa kuwa mbali nayo" yaani ishara za Mwenyezi Mungu, kwa sababu ya kuchukia kwao haki na kupenda batili waliyokuwa wakiyafanya, mpaka wakatetea sana batili yao hiyo na wala hawakuzipa ishara za Mwenyezi Mungu sikio, wala hawakuzijali.
#
{42} ومن أعظم ما صرَّف فيه الآيات والأدلَّة التَّوحيد الذي هو أصل الأصول، فأمر به ونهى عن ضدِّه وأقام عليه من الحجج العقليَّة والنقليَّة شيئاً كثيراً؛ بحيث إنَّ من أصغى إلى بعضها لا تَدَعُ في قلبه شكًّا ولا ريباً، ومن الأدلَّة على ذلك هذا الدليل العقليُّ الذي ذكره هنا، فقال: {قل}: للمشركين الذين يجعلون مع الله إلهاً آخر: {لو كان معه آلهةٌ كما يقولون}؛ أي: على موجب زعمهم وافترائهم؛ {إذاً لابْتَغَوا إلى ذي العرش سبيلاً}؛ أي: لاتَّخذوا سبيلاً إلى الله بعبادته والإنابة إليه والتقرُّب وابتغاء الوسيلة؛ فكيف يجعل العبد الفقير الذي يرى شدَّة افتقاره لعبوديَّة ربِّه إلهاً مع الله؟! هل هذا إلاَّ من أظلم الظلم وأسفه السَّفَه؛ فعلى هذا المعنى تكون هذه الآية كقوله تعالى: {أولئك الذين يدعون يبتغون إلى ربهم الوسيلة أيهم أقرب}: وكقوله تعالى: {ويوم يَحْشُرُهم وما يعبُدون من دون الله فيقول أأنتُم أضللتُم عبادي هؤلاء أم هُم ضلُّوا السبيل قالوا سبحانك ما كان ينبغي لنا أن نتَّخذ من دونِكَ من أولياءَ}.
ويُحتمل أنَّ المعنى في قوله: {قُلْ لو كان معه آلهةٌ كما يقولون إذاً لابْتَغَوْا إلى ذي العرش سبيلاً}؛ أي: لطلبوا السبيل وسَعَوْا في مغالبة الله تعالى، فإما أن يعلوا عليه فيكون مَنْ علا وقَهَرَ هو الربَّ الإله، فأما وقد علموا أنهم يقرُّون أنَّ آلهتهم التي يدعون من دون الله مقهورةٌ مغلوبةٌ ليس لها من الأمر شيء؛ فلم اتَّخذوها وهي بهذه الحال؟! فيكون هذا كقوله تعالى: {ما اتَّخَذَ اللهُ من ولدٍ وما كان معه من إلهٍ إذاً لَذَهَبَ كلُّ إلهٍ بما خَلَقَ ولعلا بعضهم على بعض}.
{42} Na miongoni mwa mambo makubwa ambayo aliyawekea ishara na hoja anuwai ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu ambako ndiyo msingi wa misingi yote. Kwa hivyo akaliamrisha hilo na akakataza kinyume chake, na akalisimamishia hilo hoja za kiakili na za kimaandiko nyingi sana kiasi kwamba mwenye kusikiliza baadhi yake, haziachi moyoni mwake shaka yoyote wala kusitasita. Na katika ushahidi wa hilo ni ushahidi huu wa kiakili ambao alitaja hapa, akasema, "Sema" uwaambie washirikina hawa ambao wanamfanya mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu. "Lau kuwa wangelikuwa pamoja naye miungu mingine kama wasemavyo." Yaani, kulingana na madai yao na uzushi wao wa uongo, "basi wangelitafuta njia ya kumfikia Mwenye Kiti cha Enzi." Yaani, wangetafuta njia ya kumfikia Mwenyezi Mungu kwa kumwabudu, kurudi kwake, kumkaribia, na kutafuta njia ya kumfikia. Basi vipi atamchukua mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu mja maskini ambaye anaona ukubwa wa uhitaji wake kumuabudu Mola wake Mlezi? Je, haya si isipokuwa ni katika dhuluma kubwa zaidi na upumbavu mkubwa zaidi? Na kwa maana hii, aya hii inakuwa na maana kama kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Hao wanaowaomba, wao wenyewe wanatafuta njia ya kwendea kwa Mola wao Mlezi - hata miongoni mwao walio karibu mno" na ni kama kauli yake yeye Mtukufu, "Na siku atakapowakusanya wao na hao wanaowaabudu.
Na akasema: Je, ni nyinyi mliowapoteza waja wangu hawa,
au wao wenyewe walipotea njia? Watasema: Subhanak
(Umetakasika na upungufu)! Haikutufailia sisi kujifanyia walinzi wowote badala yako." Na inawezekana kwamba maana ya kauli yake,
"Sema: Lau kuwa wangelikuwa pamoja naye miungu mingine kama wasemavyo, basi wangelitafuta njia ya kumfikia Mwenye Kiti cha Enzi." Yaani, wangetafuta njia na wakafanya bidii ya kumshinda Mwenyezi Mungu Mtukufu. Basi ikiwa wao watashinda atakuwa yeye aliye juu na aliye mshidi ndiye Mola Mlezi, Muabudiwa. Lakini kwa kuwa wao wenyewe wanakiri kwamba miungu yao ambayo wanaiomba badala ya Mwenyezi Mungu wameshindwa na hawana chochote katika jambo hilo, basi ni kwa nini waliwafanya kuwa miungu wao ilhali hii ndiyo hali yao? Basi maana hii inakuwa kama kauli yake, "Mwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hakuna mungu yeyote pamoja naye. Ingekuwa hivyo, basi kila mungu angelichukua alivyoumba, na baadhi yao wangeliwashinda wengine."
#
{43} {سبحانه وتعالى}؛ أي: تقدَّس وتنزَّه وعلت أوصافه، {عما يقولون}: من الشرك به واتِّخاذ الأنداد معه، {علوًّا كبيراً}: فعلا قدرُه وعظُم وجلَّت كبرياؤه التي لا تُقادر أن يكون معه آلهة؛ فقد ضلَّ مَن قال ذلك ضلالاً مبيناً وظلم ظلماً كبيراً، لقد تضاءلتْ لعظمتِهِ المخلوقاتُ العظيمةُ، وصغُرَتْ لدى كبريائِهِ السماواتُ السبع ومن فيهن والأرضون السبع ومن فيهن، والأرض جميعاً قبضتُه يوم القيامة والسماواتُ مطوياتٌ بيمينه، وافتقر إليه العالمُ العلويُّ والسفليُّ فقراً ذاتيًّا لا ينفكُّ عن أحدٍ منهم في وقتٍ من الأوقات، هذا الفقر بجميع وجوهه؛ فقرٌ من جهة الخلق والرزق والتدبير، وفقرٌ من جهة الاضطرار إلى أن يكون معبودَه ومحبوبَه الذي إليه يتقرَّبون، وإليه في كل حال يفزعون.
{43} "Subhanahu Wa Taa'la
(Ametakasika na Ametukuka juu kabisa) na sifa zake ziko juu zaidi "na hayo wanayoyasema," kwamba ana mshirika, na kumfanyia wenza pamoja naye. Yeye hadhi yake iko juu sana, na ukubwa wake ni mkuu, na mtukufu zaidi kiasi kwamba haiwezekani kuwepo na miungu pamoja naye. Kwa hivyo amekwisha potea mwenye kusema hivyo upotevu ulio wazi na akadhulumu dhuluma kubwa. Kwa maana, viumbe vyote vikubwa ni duni mbele ya ukuu wake, ni hata mbingu saba na vilivyo ndani yake na ardhi saba na vilivyo ndani yake ni vidogo mno mbele ya ukubwa wake. Na Siku ya Qiyama ardhi yote itakuwa mkononi mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kuume. Na ulimwengu wa juu na wa chini unamhitaji uhitaji wa kidhati ambao hauachani na yeyote kati yao wakati wowote ule. Nako ni kuhitaji kwa aina zake zote. Kuhitaji katika upande wa kuumbwa, kuruzukiwa, na kuendeshwa. Na kuhitaji katika upande wa ulazima ulioko kwamba awe yeye ndiye Muabudiwa wao, na Mpendwa wao ambaye wanajiweka karibu naye, na ambaye wanamkimbilia katika kila hali.
#
{44} ولهذا قال: {تسبِّحُ له السمواتُ السبع والأرض ومن فيهن وإن من شيءٍ}: من حيوانٍ ناطق وغير ناطقٍ، ومن أشجار ونبات وجامد، وحيٍّ وميت، {إلاَّ يسبِّحُ بحمدِهِ}: بلسان الحال ولسان المقال، {ولكنْ لا تفقَهون تسبيحَهم}؛ أي: تسبيح باقي المخلوقات التي على غير لغتكم، بل يحيطُ بها علاَّم الغيوب. {إنَّه كان حليماً غفوراً}: حيثُ لم يعاجِلْ بالعُقوبة مَن قال فيه قولاً تكاد السماواتُ والأرض تنفَطِر منه وتَخِرُّ له الجبال، ولكنَّه أمهلهم، وأنعم عليهم، وعافاهم، ورزقهم، ودعاهم إلى بابِهِ ليتوبوا من هذا الذنب العظيم؛ ليعطيهم الثواب الجزيل، ويغفر لهم ذنبهم؛ فلولا حلمُهُ ومغفرته؛ لسقطت السماوات على الأرض، ولما ترك على ظهرها من دابَّةٍ.
{44} Na ndiyo sababu akasema, "Zinamtakasa zote mbingu saba na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake ijapokuwa hakuna kitu" miongoni mwa wanyama anayezungumza na asiyezungumza, na miti, mimea na vyote visivyo hai na vilivyo hai, na wafu, "ila kinamtakasa kwa sifa zake," kwa hali zao mbali mbali na hata kwa maneno. "Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake." yaani, kutakasa ambako wanafanya viumbe wengineo ambao hawazungumzi lugha yako, lakini Yeye ajuaye zaidi ghaibu amevizunguka vyote. "Hakika Yeye ni Mstahamilivu na Mwenye kughufiria." Kwa maana hakumharakishia adhabu mwenye kusema kumhusu kauli ambayo mbingu na ardhi vinakaribia kupasuka kwa sababu yake na milima inakaribia kuangukia. Lakini yeye huwapa muhula na anawaneemesha, na anawapa salama, na anawaruzuku, na anawaita kwenye mlango wake ili watubie kutokana na dhambi hii kubwa, ili awape thawabu nyingi, na awasamehe dhambi zao. Na kama usingekuwa ustahamilivu wake na msamaha wake, mbingu zingeanguka juu ya ardhi, na asingeacha mnyama yeyote juu ya mgongo wake.
{وَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ جَعَلْنَا بَيْنَكَ وَبَيْنَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ حِجَابًا مَسْتُورًا (45) وَجَعَلْنَا عَلَى قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَنْ يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا وَإِذَا ذَكَرْتَ رَبَّكَ فِي الْقُرْآنِ وَحْدَهُ وَلَّوْا عَلَى أَدْبَارِهِمْ نُفُورًا (46) نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَسْتَمِعُونَ بِهِ إِذْ يَسْتَمِعُونَ إِلَيْكَ وَإِذْ هُمْ نَجْوَى إِذْ يَقُولُ الظَّالِمُونَ إِنْ تَتَّبِعُونَ إِلَّا رَجُلًا مَسْحُورًا (47) انْظُرْ كَيْفَ ضَرَبُوا لَكَ الْأَمْثَالَ فَضَلُّوا فَلَا يَسْتَطِيعُونَ سَبِيلًا (48)}.
45. Na unaposoma Qur-ani, tunaweka baina yako na wale wasioiamini Akhera pazia linalowafunika. 46. Na tunaweka vifuniko juu ya nyoyo zao wasije wakaifahamu, na tunaweka kwenye masikio yao uziwi. Na unapomtaja katika Qur-ani Mola wako Mlezi peke yake, basi wao hugeuka nyuma wakaenda zao. 47. Sisi tunajua vyema kabisa sababu wanayosikilizia wanapokusikiliza, na wanaponong'ona.
Wanaposema hao madhalimu: Nyinyi hamumfuati isipokuwa mwanamume aliyerogwa. 48. Tazama jinsi walivyokupigia mifano. Basi wakapotea. Kwa hivyo hawawezi kuipata njia.
#
{45} يخبر تعالى عن عقوبته للمكذِّبين بالحقِّ الذين ردُّوه وأعرضوا عنه أنَّه يَحول بينَهم وبين الإيمان، فقال: {وإذا قرأتَ القرآنَ}: الذي فيه الوعظُ والتَّذكير والهدى والإيمان والخير والعلم الكثيرُ؛ {جَعَلْنا بينَك وبين الذين لا يؤمنونَ بالآخرة حجاباً مستوراً}: يستُرهم عن فهمه حقيقةً وعن التحقُّق بحقائقه والانقياد إلى ما يدعو إليه من الخير.
{45} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu adhabu yake juu ya wale wanaokadhibisha haki, ambao waliikataa na wakaipa mgongo kwamba anawazuia wasiamini. Akasema, "Na unaposoma Qur-ani" ambayo ndani yake kuna mawaidha, ukumbusho, uwongofu, imani, heri, na elimu nyingi, "tunaweka baina yako na wale wasioiamini Akhera pazia linalowafunika," wasiielewe kwa kweli, wasithibitishe hakika zake, na wasifuate yale inayolingania ya heri.
#
{46} {وجَعَلْنا على قلوبِهِم أكِنَّةً}؛ أي: أغطية وأغشية لا يفقهون معها القرآن، بل يسمعونه سماعاً تقوم به عليهم الحجَّة، {وفي آذانهم وَقْراً}؛ أي: صمماً عن سماعه، {وإذا ذكرتَ ربَّك في القرآن وحدَه}: داعياً لتوحيده، ناهياً عن الشرك به؛ {وَلَّوا على أدبارِهِم نُفوراً}: من شدَّة بُغضهم له ومحبَّتهم لما هم عليه من الباطل؛ كما قال تعالى: {وإذا ذُكِرَ اللهُ وحدَه اشمأزَّت قلوبُ الذين لا يؤمنون بالآخرةِ وإذا ذُكِرَ الذين من دونِهِ إذا هم يستبشرونَ}.
{46} "Na tunaweka vifuniko juu ya nyoyo zao" kwa hivyo hawaielewi Qur-ani kwa sababu yake, lakini wanaisikiliza tu kusikiliza kwa kuwasimamishia hoja. "Na tunaweka kwenye masikio yao uziwi" kwa hivyo hawawezi kuisikia. "Na unapomtaja katika Qur-ani Mola wako Mlezi peke yake" ukilingania upweke wake, ukikataza kumshirikisha, "basi wao hugeuka nyuma wakaenda zao" kutokana na ukubwa wa kuichukia na kupenda kwao batili waliyo nayo. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Na anapotajwa Mwenyezi Mungu peke yake, nyoyo za wale wasioiamini Akhera huchafuka. Na wanapotajwa wenginewe wasiokuwa Yeye, basi tazama, wanafurahi mno."
#
{47} {نحنُ أعلم بما يستمعون به}؛ أي: إنَّما مَنَعْناهم من الانتفاع عند سماع القرآن لأنَّنا نعلم أن مقاصدهم سيِّئة؛ يريدون أن يعثروا على أقلِّ شيءٍ لِيَقْدَحوا به، وليس استماعُهم لأجل الاسترشاد وقَبول الحقِّ، وإنَّما هم معتمدون على عدم اتِّباعه، ومَنْ كان بهذه الحالة؛ لم يُفِدْهُ الاستماع شيئاً، ولهذا قال: {إذْ يستَمِعونَ إليك وإذْ هم نَجْوى}؛ أي: متناجين، {إذْ يقولُ الظالمونَ}: في مناجاتهم: {إنْ تَتَّبِعونَ إلاَّ رجلاً مسحوراً}: فإذا كانت هذه مناجاتُهم الظالمة فيما بينهم، وقد بَنَوْها على أنه مسحورٌ؛ فهم جازمون أنَّهم غير معتَبِرين لما قال، وأنَّه يَهْذي لا يدري ما يقول.
{47} "Sisi tunajua vyema kabisa sababu wanayosikilizia." Yaani, tuliwazuia wasinufaike wanaposikia Qur-ani kwa sababu tunajua kwamba nia zao ni mbaya. Wanataka waone jambo dogo tu ili waikashifu. Kwa hivyo kusikiliza kwao huko si kwa ajili ya kutafuta mwongozo na kuikubali haki. Lakini wamekusudia kutokuifuata. Na yule ambaye hali yake ni hii, basi hawezi kunufaika na kitu katika kuisikiliza, na ndiyo sababu akasema, "wanapokusikiliza, na wanaponong'ona. Wanaposema hao madhalimu" katika kunong'ona kwao, "Nyinyi hamumfuati isipokuwa mwanamume aliyerogwa." Kwa hivyo, ikiwa huku ndiko kunong'onezana kwao kwa kidhalimu, na tayari walikujenga juu ya itikadi yao kwamba amefanyiwa uchawi, basi wameshakata shauri kwamba hawatayazingatia ayasemayo, na kwamba anaropokwa tu na hajui anachosema.
#
{48} قال تعالى: {انظر}: متعجباً {كيف ضربوا لك الأمثال}: التي هي أضلُّ الأمثال وأبعدُها عن الصواب، {فضَلُّوا}: في ذلك، أو فصارت سبباً لضلالهم؛ لأنَّهم بَنَوا عليها أمرهم، والمبنيُّ على فاسدٍ أفسدُ منه. فلا يهتدون {سبيلاً}؛ أي: لا يهتدون أيَّ اهتداءٍ، فَنَصِيبُهُم الضلال المحضُ والظُّلم الصرف.
{48} Yeye Mtukufu akasema, "Tazama" kwa kushangaa "jinsi walivyokupigia mifano" ambayo ndiyo mifano potevu zaidi, na iliyo mbali zaidi na usahihi. "Basi wakapotea" katika hilo, au likawa hilo ndilo sababu ya kupotea kwao, kwa sababu walijengea jambo lao hilo juu yake. Na chenye kujengeka juu ya kibovu, basi hicho ni kibovu zaidi yake. Kwa hivyo hawaongoki wakaipata "njia," kwa namna yoyote ile. Kwa hivyo, fungu lao ni upotovu mtupu na dhuluma ya mwisho kabisa.
{وَقَالُوا أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا وَرُفَاتًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ خَلْقًا جَدِيدًا (49) قُلْ كُونُوا حِجَارَةً أَوْ حَدِيدًا (50) أَوْ خَلْقًا مِمَّا يَكْبُرُ فِي صُدُورِكُمْ فَسَيَقُولُونَ مَنْ يُعِيدُنَا قُلِ الَّذِي فَطَرَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ فَسَيُنْغِضُونَ إِلَيْكَ رُءُوسَهُمْ وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَنْ يَكُونَ قَرِيبًا (51) يَوْمَ يَدْعُوكُمْ فَتَسْتَجِيبُونَ بِحَمْدِهِ وَتَظُنُّونَ إِنْ لَبِثْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا (52)}.
49.
Na walisema: Je! Tutakapokuwa mifupa na mapande yaliyovurugika, tutafufuliwa kwa umbo jipya? 50.
Sema: Kuweni hata mawe na chuma. 51. Au umbo lolote mnaloliona kubwa katika vifua vyenu.
Watasema: Nani atakayeturudisha tena? Sema: Yule yule aliyewaumba mara ya kwanza! Watakutikisia vichwa vyao,
na watasema: Ni lini hayo? Sema: Labda huenda itakuwa hivi karibuni! 52. Siku atakapowaita, nanyi mtamuitikia kwa kumsifu, na mtaadhani kuwa hamkukaa isipokuwa muda mdogo tu.
#
{49} يخبر تعالى عن قول المنكرين للبعث وتكذيبهم به واستبعادهم بقولهم: {أإذا كُنَّا عظاماً ورُفاتاً}؛ أي: أجساداً بالية. {أإنَّا لَمبعوثون خلقاً جديداً}؛ أي: لا يكون ذلك، وهو محالٌ بزعمهم، فجهلوا أشدَّ الجهل؛ حيثُ كذَّبوا رسل الله، وجَحَدوا آيات الله، وقاسوا قدرةَ خالق السماواتِ والأرضِ بِقُدَرِهِمُ الضعيفة العاجزة، فلما رأوا أنَّ هذا ممتنعٌ عليهم لا يقدرون عليه؛ جعلوا قدرة الله كذلك؛ فسبحان مَنْ جَعَلَ خلقاً من خلقه يزعُمون أنَّهم أولو العقول والألباب مثالاً في جهل أظهر الأشياء وأجلاها وأوضحها براهين وأعلاها؛ لِيُري عباده أنه ما ثَمَّ إلا توفيقه وإعانتُه أو الهلاك والضلال، {ربَّنا لا تُزِغْ قلوبنا بعد إذْ هَدَيْتَنا وَهَبْ لنا من لَدُنْك رحمةً إنَّك أنت الوهاب}.
{49} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu maneno ya wanaokanusha kufufuliwa na kukadhibisha kwao hilo na kuona kwao kwamba hilo haliwezekani kwa kusema, "Tutakapokuwa mifupa na mapande yaliyovurugika." Yaani, miili iliyochakaa. "Tutafufuliwa kwa umbo jipya." Yaani, hilo halitatokea, na kwamba haliwezekani kulingana na madai yao, kwa hivyo ni wajinga mno. Ambapo waliwakadhibisha Mitume wa Mwenyezi Mungu, wakazikataa ishara za Mwenyezi Mungu, na wakapima uwezo wa Muumba wa mbingu na ardhi kwa uwezo wao dhaifu na usioweza kitu, na walipoona hawaliwezi hilo, wakaufanya uwezo wa Mwenyezi Mungu kuwa hivyo. Lakini ametakasika yule aliyewafanya viumbe miongoni mwa viumbe wake, ambao wanadai kuwa wao ndio wenye akili na ufahamu kuwa ni mfano wa kutojua mambo yaliyo dhahiri kabisa, na ya peupe yake zaidi, na yaliyo wazi yake zaidi kwa hoja, ili kuwaonyesha waja wake kwamba hakuna kufaulu isipokuwa kwa kuwezesha kwake, na usaidizi wake au kuangamia na kupotea. "Mola wetu Mlezi! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kwisha tuongoa, na utupe rehema itokayo kwako. Hakika Wewe ndiye Mwenye kutunuku."
#
{50 - 51} ولهذا أمر رسوله - صلى الله عليه وسلم - أن يقول لهؤلاء المنكرين للبعث استبعاداً: {قُلْ كونوا حجارة أو حديداً. أو خلقاً مما يكبر}؛ أي: يعظُم {في صدورِكم}: لتسلموا بذلك - على زعمكم - من أن تنالكم قدرة الله أو تنفذَ فيكم مشيئتُه؛ فإنكم غير معجزين الله في أيِّ حالة تكونون وعلى أيِّ وصفٍ تتحوَّلون، وليس لكم في أنفسكم تدبيرٌ في حالة الحياة وبعد الممات؛ فدعوا التدبير والتصريف لِمَنْ هو على كلِّ شيء قدير وبكلِّ شيء محيط. {فسيقولون}: حين تُقيم عليهم الحجَّة في البعث: {من يعيدنا قل الذي فَطَرَكم أول مرة}: فكما فطركم ولم تكونوا شيئاً مذكوراً؛ فإنَّه سيعيدكم خلقاً جديداً؛ {كما بَدَأنا أوَّلَ خلقٍ نعيدُه}، {فسيُنْغِضونَ إليك رؤوسهم}؛ أي: يهزُّونها إنكاراً وتعجُّباً مما قلت. {ويقولون متى هو}؛ أي: متى وقتُ البعث الذي تزعمه على قولك؟ لا إقراراً منهم لأصل البعث، بل ذلك سفهٌ منهم وتعجيزٌ. {قل عسى أن يكونَ قريباً}: فليس في تعيين وقتِهِ فائدةٌ، وإنَّما الفائدة والمدار على تقريره والإقرار به وإثباته، وإلاَّ؛ فكلُّ ما هو آتٍ؛ فإنَّه قريب.
{50 - 51} Na kwa sababu hiyo alimwamrisha Mtume wake -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - kwamba awaambie hawa waliokanusha kufufuliwa kwa kuona kwamba hilo haliwezekani.
"Sema: kuweni hata mawe na chuma. Au umbo lolote mnaloliona kubwa katika vifua vyenu." Ili msalimike kwa hilo - kwa madai yenu - kwamba nguvu za Mwenyezi Mungu hazitawafikia wala kwamba mapenzi yake hayatatekelezeka kwenu. Hakika nyinyi hamwezi kumshinda Mwenyezi Mungu katika hali yenu yoyote na katika sifa yoyote mnayoibadilikia. Nanyi wenyewe hamuwezi hata kuendesha chochote katika hali ya uhai wenu wala baada ya kifo. Basi acheni uendeshaji wa mambo na ubadilishaji wa mambo kwa Yule ambaye ni Muweza wa kila kitu na aliyezunguka kila kitu. "Watasema" wakati unapowasimamishia hoja juu ya ufufuo,
"Ni nani atakayeturudisha tena? Sema: Yule yule aliyewaumba mara ya kwanza!" Kama alivyowaumba na hamkuwa chochote cha kukumbukwa, basi hakika yeye atawarudisha umbo jipya; "kama tulivyoanza umbo la kwanza, tutalirudisha tena." "Watakutikisia vichwa vyao" kwa kukataa na kushangazwa na kile ulichosema.
"Watasema: Ni lini hayo?" Yaani, itakuwa lini saa ya kufufuliwa hiyo ambayo unadai kwa mujibu wa kauli yako? Si kwa kukiri asili ya ufufuo, bali huo ni upumbavu na kutaka kwao kushinda.
"Sema: Labda itakuwa hivi karibuni" Na hakuna faida yoyote katika kubainisha wakati wake hasa, bali manufaa na mazingatio ni katika kuamini uhakika wa kutokea kwake na kulikubali hilo, na kulithibitisha, vinginevyo, kila kitu kinachokuja, basi hicho kiko karibu.
#
{52} {يوم يدعوكم}: للبعث والنُّشور وينفُخ في الصور، {فتستجيبونَ بحمدِهِ}؛ أي: تنقادون لأمرِهِ ولا تستعصونَ عليه. وقوله: {بحمده}؛ أي: هو المحمود تعالى على فعله، ويجزي به العباد إذا جمعهم ليوم التَّنادِ، {وتظنُّونَ إن لَبِثْتُم إلاَّ قليلاً}: من سرعة وقوعه، وأنَّ الذي مرَّ عليكم من النعيم كأنَّه ما كان؛ فهذا الذي يقول عنه المنكرون: متى هو؟ يندمون غاية الندم عند ورودِهِ، ويُقال لهم: هذا الذي كنتُم به تكذِّبون.
{52} "Siku atakapowaita" kwa ajili ya kufufuliwa na kutolewa makaburini, na litapulizwa baragumu, "Nanyi mtamuitikia kwa kumsifu." Yaani, mtafuata amri yake wala hamtamuwiya wagumu. Na kauli yake, "kwa kumsifu." Yaani, Yeye Mtukufu ndiye mwenye kusifiwa kwa vitendo vyake, na atawalipa waja wake atakapowakusanya kwa ajili ya Siku ya Wito. "Na mtadhani kuwa hamkukaa isipokuwa muda mdogo tu;" kwa sababu ya kasi kubwa ya kutokea kwake, na kwamba starehe mlizokuwa nazo ni kana kwamba hazikuwahi kutokea.
Basi hii ambayo wakadhibishaji wanasema juu yake: Ni lini hayo? Basi watajuta sana itakapotokea,
na wataambiwa: Haya ndiyo mliyokuwa mkiyakadhibisha.
{وَقُلْ لِعِبَادِي يَقُولُوا الَّتِي هِيَ أَحْسَنُ إِنَّ الشَّيْطَانَ يَنْزَغُ بَيْنَهُمْ إِنَّ الشَّيْطَانَ كَانَ لِلْإِنْسَانِ عَدُوًّا مُبِينًا (53) رَبُّكُمْ أَعْلَمُ بِكُمْ إِنْ يَشَأْ يَرْحَمْكُمْ أَوْ إِنْ يَشَأْ يُعَذِّبْكُمْ وَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ وَكِيلًا (54) وَرَبُّكَ أَعْلَمُ بِمَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَقَدْ فَضَّلْنَا بَعْضَ النَّبِيِّينَ عَلَى بَعْضٍ وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا (55)}.
53. Waambie waja wangu waseme maneno mazuri, kwa maana hakika Shetani huchochea ugomvi baina yao. Hakika Shetani ni adui aliye dhahiri kwa mwanadamu. 54. Mola wenu Mlezi anawajua vilivyo. Akitaka, atawarehemu, na akitaka, atawaadhibu. Na hatukukutuma ili uwe msimamizi wao. 55. Na Mola wako Mlezi anawajua vilivyo waliomo mbinguni na katika ardhi. Na hakika tumewafadhilisha baadhi ya Manabii kuliko wengine, na Daudi tulimpa Zaburi.
#
{53} وهذا من لطفِهِ بعباده؛ حيثُ أمرهم بأحسن الأخلاق والأعمال والأقوال الموجبة للسعادة في الدُّنيا والآخرة، فقال: {وقُلْ لعبادي يقولوا التي هي أحسنُ}: وهذا أمرٌ بكلِّ كلام يقرِّب إلى الله؛ من قراءةٍ وذكرٍ وعلم وأمرٍ بمعروف ونهي عن منكرٍ وكلام حسنٍ لطيفٍ مع الخلق على اختلاف مراتبهم ومنازلهم، وأنه إذا دار الأمر بين أمرين حسنين؛ فإنَّه يؤمَر بإيثار أحسَنِهما إن لم يمكن الجمعُ بينَهما، والقول الحسنُ داعٍ لكلِّ خلقٍ جميل وعمل صالح؛ فإنَّ مَن مَلَكَ لسانه؛ مَلَكَ جميع أمره. وقوله: {إنَّ الشيطانَ يَنْزَغُ بينهم}؛ أي: يسعى بين العباد بما يُفْسِدُ عليهم دينهم ودنياهم؛ فدواءُ هذا أن لا يُطيعوه في الأقوال غير الحسنة التي يدعوهم إليها، وأن يَلينوا فيما بينَهم؛ لينقمعَ الشيطانُ الذي ينزغ بينهم؛ فإنَّه عدوُّهم الحقيقيُّ الذي ينبغي لهم أن يحاربوه؛ فإنَّه يدعوهم ليكونوا من أصحاب السعير، وأما إخوانهم؛ فإنَّهم وإنْ نزغ الشيطان فيما بينهم وسعى في العداوة؛ فإنَّ الحزم كلَّ الحزم السعيُ في ضدِّ عدوِّهم، وأن يَقْمَعوا أنفسهم الأمَّارة بالسوء، التي يدخُل الشيطان من قِبَلِها؛ فبذلك يطيعون ربَّهم، ويستقيم أمرهم، ويُهْدَون لرشدهم.
{53} Na haya ni katika upole wake kwa waja wake, ambapo aliwaamrisha wawe na maadili mema, vitendo na maneno yenye kuleta furaha duniani na akhera. Akasema, "Na waambie waja wangu waseme yaliyo bora zaidi." Hii ni ya kwamba waseme kila neno yenye kumleta mtu karibu na Mwenyezi Mungu, kama vile kusoma, kufanya dhikri, elimu, kuamrisha mema na kukataza maovu, na kusema kwa uzuri na upole na watu bila ya kujali nyadhifa zao na vyeo vyao, na kwamba ikiwa jambo linazunguka baina ya mambo mawili mazuri, basi ameamrishwa kulipendelea lililo zuri zaidi kati ya mawili hayo ikiwa haiwezekani kufanya uwiyano kati yake, na kauli nzuri ni sababu ya kila tabia nzuri na matendo mema. Kwani mwenye kuutawala ulimi wake, atatawala mambo yake yote. Na kauli yake, “Kwa maana hakika Shetani huchochea ugomvi baina yao." Yaani anafanya bidii kati ya waja ili kuwaharibia dini yao na maisha yao ya kidunia. Na dawa ya hayo ni kwamba wasimtii katika maneno mabaya anayowaitia, na kwamba wawe wapole wao kwa wao, ili akomeke shetani anayechochea ugomvi kati yao. Kwa maana yeye ndiye adui wao wa kweli ambaye wanapaswa kupigana naye. Kwa maana, anawaita ili wawe katika wenza wa Moto. Na ama ndugu zao, hata kama Shetani anapotaka kuchochea kati yao na akafanya bidii ya kuweka uadui kati yao, basi na liwe azimio lao lote ni kujitahidi dhidi ya adui yao huyu, na kuzikomesha nafsi zao ziamrishazo mabaya, ambazo Shetani huingilia humo. Na kwa hayo watakuwa wamemtii Mola wao Mlezi, na mambo yao yatanyooka, na wataongolewa kwenye uongofu wao.
#
{54} {ربُّكم أعلم بكم}: من أنفسكم؛ فلذلك لا يريد لكم إلاَّ ما هو الخير، ولا يأمركم إلاَّ بما فيه مصلحة لكم، وقد تريدون شيئاً الخيرُ في عكسه. {إن يَشَأْ يَرْحَمْكُم أو إن يَشَأ يُعَذِّبْكم}: فيوفِّق مَن شاء لأسباب الرحمة، ويخذُلُ من شاء فَيَضِلُّ عنها فيستحقُّ العذاب. {وما أرسلناك عليهم وكيلاً}: تُدبِّرُ أمرهم وتقوم بمجازاتهم، وإنَّما الله هو الوكيل، وأنت مبلغٌ هادٍ إلى صراط مستقيم.
{54} "Mola wenu Mlezi anawajua vilivyo" kuwaliko hata nyinyi wenyewe. Ndiyo maana, hawawatakii isipokuwa heri, wala hawaamrishi isipokuwa yenye masilahi kwenu, na mnaweza kutaka jambo ambalo heri iko katika kinyume chake. "Akitaka, atawarehemu, na akitaka, atawaadhibu." Atamuwezesha amtakaye kufikia njia za rehema, na atamwacha amtakaye, basi atapotea asizifikie kwa hivyo akastahili adhabu. "Na hatukukutuma ili uwe msimamizi wao," ili uwaendeshee mambo yao na, na uwalipe. Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Msimamizi wao, nawe ni mfikishaji tu anayeongoza kwenye njia iliyonyooka.
#
{55} {وربُّك أعلمُ بمن في السمواتِ والأرض}: من جميع أصناف الخلائق، فيعطي كلاًّ منهم ما يستحقُّه وتقتضيه حكمتُه، ويفضِّل بعضَهم على بعض في جميع الخصال الحسيَّة والمعنويَّة؛ كما فضَّل بعض النبيِّين المشتركين بوحيه على بعضٍ، بالفضائل والخصائص الرَّاجعة إلى ما مَنَّ به عليهم، من الأوصاف الممدوحة، والأخلاق المرضيَّة والأعمال الصالحة وكَثْرة الأتباع ونزول الكتب على بعضهم، المشتملة على الأحكام الشرعيَّة والعقائد المرضيَّة؛ كما أنزل على داود زَبوراً، وهو الكتاب المعروف؛ فإذا كان تعالى قد فضَّل بعضَهم على بعضٍ وآتى بعضهم كتباً؛ فِلمَ ينكِرُ المكذِّبون لمحمدٍ - صلى الله عليه وسلم - ما أنزله الله عليه وما فضَّله به من النبوَّة والكتاب؟
{55} "Na Mola wako Mlezi anawajua vilivyo waliomo mbinguni na katika ardhi" miongoni mwa kila aina ya viumbe, basi humpa kila mmoja wao anachostahiki na kinachohitajiwa na hekima yake, na huwafadhilisha baadhi yao kuliko wengine katika sifa zote za kihisia na zisizo za kihisia. Kama vile alivyowafadhilisha baadhi ya Manabii walioshiriki katika ufunuo wake juu ya wengine kwa fadhila na sifa mbalimbali kutokana na yale aliyowaneemesha kwayo miongoni mwa sifa za kusifiwa, tabia za kuridhisha, matendo mema, idadi kubwa ya wafuasi, na baadhi yao kuteremshiwa vitabu vilivyo na hukumu za kisheria na itikadi zinazoridhiwa, kama alivyomteremsha Daudi Zaburi. Nacho ni kitabu kinachojulikana sana. Na ikiwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na akawapa baadhi yao vitabu, basi kwa nini wanaomkadhibisha Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - wanakanusha yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu juu yake na yale aliyomfadhilisha kwayo ya unabii na Kitabu?
{قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُمْ مِنْ دُونِهِ فَلَا يَمْلِكُونَ كَشْفَ الضُّرِّ عَنْكُمْ وَلَا تَحْوِيلًا (56) أُولَئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَى رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحْذُورًا (57)}.
56.
Sema: Waombeni hao mnaowadai badala yake Yeye. Hawawezi kuwaondolea madhara, wala kuyaweka pengine. 57. Hao ambao wao wanaowaomba, wao wenyewe wanatafuta njia ya kwendea kwa Mola wao Mlezi hata miongoni mwao walio karibu mno, na wanataraji rehema zake, na wanaihofu adhabu yake. Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi yafaa kutahadhariwa.
#
{56} يقول تعالى: {قل} للمشركين بالله الذين اتَّخذوا من دونه أنداداً يعبُدونهم كما يعبدون الله، ويدعونهم كما يدعونَه ملزِماً لهم بتصحيح ما زعموه، واعتقدوه إن كانوا صادقين: {ادعوا الذين زعمتُم}: آلهة من دون اللَّه، فانظروا هل يَنْفَعونكم أو يدفَعون عنكم الضُّرَّ؟ فإنهم لا {يملِكونَ كشفَ الضُّرِّ عنكم}: من مرضٍ أو فقرٍ أو شدَّةٍ ونحو ذلك؛ فلا يدفعونَه بالكُلِّيَّة. ولا يملكون أيضاً تَحْويله من شخص إلى آخر، ومن شدَّة إلى ما دونها؛ فإذا كانوا بهذه الصفة؛ فلأيِّ شيءٍ تدعونَهم من دون الله؛ فإنَّهم لا كمالَ لهم ولا فعال نافعة؛ فاتِّخاذُهم نقصٌ في الدين والعقل وسَفَهٌ في الرأي.
ومن العجب أنَّ السَّفه عند الاعتياد والممارسة وتلقِّيه عن الآباء الضالِّين بالقبول يراه صاحبه هو الرأي السديد والعقل المفيد، ويرى إخلاصَ الدِّين لله الواحد الأحد الكامل المنعم بجميع النعم الظاهرة والباطنة هو السَّفه والأمر المتعجَّب منه؛ كما قال المشركون: {أجعلَ الآلهةَ إلهاً واحداً إنَّ هذا لشيءٌ عُجابٌ}.
{56} Mwenyezi Mungu aliyetukuka anasema, "Sema" kuwaambia wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, ambao walifanya wenza badala yake, wakawaabudu kama wanavyomuabudu Mwenyezi Mungu, na wanawaomba kama wanavyomuomba, huku akiwalazimisha kusahihisha wanayodai hayo, na waliyoyaitakidi ikiwa ni wakweli, "Waombeni hao mnaowadai" kuwa ni miungu badala yake Yeye, basi angalieni watawanufaisha au wanaweza kuwazuilia madhara yoyote? Hao, "Hawawezi kuwaondolea madhara" kama vile magonjwa, ufukara, ugumu na mfano wake. Hawawezi kuyazuia kabisa, wala hawana uwezo wa kuhamisha kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine, au kutoka kwa ugumu moja hadi kwa kilicho kidogo zaidi yake. Basi ikiwa hii ndiyo sifa yao, kwa nini mnawaomba badala ya Mwenyezi Mungu? Kwani wao hawana ukamilifu wala kitendo chenye manufaa. Basi kuwafanya miungu ni upungufu katika dini na akili na ni upumbavu katika rai. Na katika yanayoshangaza ni kwamba upumbavu unapokuwa ndiyo ada, na ukazoewa, na ukachukuliwa kutoka kwa akina baba wapotovu, huonwa na mwenye kuwa na rai iliyo sawasawa na akili yenye manufaa, na anaona kuwa mumfanyie dini Mwenyezi Mungu tu, ambaye ni Mmoja tu, wa pekee, Mkamilifu, Mneemeshaji kwa neema zote za dhahiri na zilizofichikana kwamba ni upumbavu na jambo la kustaajabisha, kama walivyosema washirikina, "Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu."
#
{57} ثم أخبر أيضاً أنَّ الذين يعبُدونهم من دون الله في شغل شاغل عنهم باهتمامهم بالافتقار إلى الله وابتغاء الوسيلة إليه؛ فقال: {أولئك الذين يَدْعونَ}: من الأنبياء والصالحين والملائكة، {يَبْتَغون إلى ربِّهم الوسيلةَ أيُّهم أقربُ}؛ أي: يتنافسون في القرب من ربِّهم، ويبذُلون ما يقدرون عليه من الأعمال الصالحة المقرِّبة إلى الله تعالى وإلى رحمتِه، {ويخافون عذابَه}: فيجتنبون كلَّ ما يوصِلُ إلى العذاب. {إنَّ عذاب ربِّك كان محذوراً}؛ أي: هو الذي ينبغي شدَّة الحذر منه والتوقِّي من أسبابه. وهذه الأمور الثلاثةُ الخوف والرجاء والمحبَّة التي وَصَفَ الله بها هؤلاء المقرَّبين عنده هي الأصل والمادَّة في كلِّ خير؛ فمن تَمَّتْ له؛ تَمَّتْ له أموره، وإذا خلا القلبُ منها؛ ترحَّلت عنه الخيرات، وأحاطت به الشرور.
وعلامة المحبَّة ما ذَكَرَهُ الله أن يجتهد العبدُ في كلِّ عَمَلٍ يقرِّبُه إلى الله، وينافس في قربه بإخلاص الأعمال كلِّها لله، والنُّصح فيها وإيقاعها في أكمل الوجوه المقدور عليها؛ فمن زعم أنه يحبُّ الله بغير ذلك؛ فهو كاذب.
{57} Kisha akajulisha pia kwamba wao wanawaabudu badala ya Mwenyezi Mungu wako katika shughuli inayowafanya kuwasahau kwa sababu wanajali sana uhitaji wao kwa Mwenyezi Mungu na kutafuta njia ya kumfikia. Akasema,
“Hao ambao wao wanaowaomba” miongoni mwa Manabii, watu wema, na Malaika, "wao wenyewe wanatafuta njia ya kwendea kwa Mola wao Mlezi hata miongoni mwao walio karibu mno." Yaani, wanashindana katika kuwa karibu na Mola wao Mlezi, na wanafanya yale wanayoweza miongoni mwa matendo mema ambayo yatawaweka karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu na rehema zake, "na wanaihofu adhabu yake" basi wanajiepusha na kila kitu chenye kufikisha kwenye adhabu yake. "Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi yafaa kutahadhariwa" na kujiepusha na sababu zake.
Na mambo haya matatu: hofu, matumaini, na upendo, ambayo Mwenyezi Mungu aliwaelezea hawa walio karibu naye, ndiyo msingi na kiini cha heri yote. Kwa hivyo, aliye nayo, basi mambo yake yanakuwa yamekamilika. Na ikiwa moyo hautakuwa nayo, basi heri zinauondoka, na unazungukwa na maovu. Na alama ya upendo ni kama alivyotaja Mwenyezi Mungu kwamba mja ajitahidi katika kila tendo linalomkurubisha kwa Mwenyezi Mungu, na kushindana katika kujikurubisha kwake kwa kumtaka Mwenyezi Mungu tu katika matendo yote, kuyafanya kuwa safi na kuyatekeleza kwa njia ya ukamilifu zaidi iwezekanayo. Kwa hivyo, mwenye kudai kwamba anampenda Mwenyezi Mungu na akafanya yasiyokuwa haya, basi yeye ni mwongo.
{وَإِنْ مِنْ قَرْيَةٍ إِلَّا نَحْنُ مُهْلِكُوهَا قَبْلَ يَوْمِ الْقِيَامَةِ أَوْ مُعَذِّبُوهَا عَذَابًا شَدِيدًا كَانَ ذَلِكَ فِي الْكِتَابِ مَسْطُورًا (58)}.
58. Na hapana mji wowote ila Sisi tutauteketeza kabla ya Siku ya Kiyama, au tutaupa adhabu kali. Haya yamekwisha andikwa katika Kitabu.
#
{58} أي: ما من قريةٍ من القُرى المكذِّبة للرسل إلاَّ لا بدَّ أن يصيبهم هلاكٌ قبل يوم القيامة أو عذابٌ شديدٌ، كتابٌ كتبه الله وقضاءٌ أبرمه لا بدَّ من وقوعه؛ فليبادر المكذِّبون بالإنابة إلى الله وتصديق رُسُلِهِ قبل أن تتمَّ عليهم كلمةُ العذاب ويحقَّ عليهم القول.
{58} Yaani, hakuna mji wowote miongoni mwa miji iliyokadhibisha Mitume isipokuwa ni lazima waangamizwe kabla ya Siku ya Qiyama au wafikiwe na adhabu kali. Hilo ni andiko aliloandika Mwenyezi Mungu na hukumu aliyoihitimisha ambayo ni lazima itokee. Basi na waharakishe hao wanaokadhibisha kurejea kwa Mwenyezi Mungu na kuwasadiki Mitume wake kabla neno la adhabu kutimia juu yao, na kauli kuwastahili.
{وَمَا مَنَعَنَا أَنْ نُرْسِلَ بِالْآيَاتِ إِلَّا أَنْ كَذَّبَ بِهَا الْأَوَّلُونَ وَآتَيْنَا ثَمُودَ النَّاقَةَ مُبْصِرَةً فَظَلَمُوا بِهَا وَمَا نُرْسِلُ بِالْآيَاتِ إِلَّا تَخْوِيفًا (59) وَإِذْ قُلْنَا لَكَ إِنَّ رَبَّكَ أَحَاطَ بِالنَّاسِ وَمَا جَعَلْنَا الرُّؤْيَا الَّتِي أَرَيْنَاكَ إِلَّا فِتْنَةً لِلنَّاسِ وَالشَّجَرَةَ الْمَلْعُونَةَ فِي الْقُرْآنِ وَنُخَوِّفُهُمْ فَمَا يَزِيدُهُمْ إِلَّا طُغْيَانًا كَبِيرًا (60)}.
59. Na hapana kinachotuzuia kupeleka miujiza ila ni kuwa watu wa zamani waliikanusha. Na tuliwapa Wathamudi ngamia jike kuwa ni Ishara iliyo dhaahiri, lakini walidhulumu kwaye. Nasi hatutumii Ishara isipokuwa kwa ajili ya kuhofisha. 60.
Na tulipokwambia: Hakika Mola wako Mlezi amekwisha wazunguka hao watu. Na hatukuifanya ndoto tuliyokuonyesha isipokuwa ni kuwajaribu watu, na mti uliolaaniwa katika Qur-ani. Na tunawahofisha, lakini haiwazidishii isipokuwa uasi mkubwa.
#
{59} يذكر تعالى رحمته بعدم إنزاله الآيات التي يقترحُ بها المكذِّبون، وأنَّه ما منعه أن يرسِلَها إلاَّ خوفاً من تكذيبهم لها؛ فإذا كذَّبوا بها؛ عاجَلَهم العقابُ وحلَّ بهم من غير تأخيرٍ كما فعل بالأولين الذين كذبوا بها، ومن أعظم الآيات الآيةُ التي أرسلها الله إلى ثمود، وهي الناقة العظيمةُ الباهرة التي كانت تصدُرُ عنها جميع القبيلة بأجمعها، ومع ذلك كذَّبوا بها، فأصابهم ما قصَّ الله علينا في كتابه. وهؤلاء كذلك؛ لو جاءتهم الآيات الكبار؛ لم يؤمنوا؛ فإنَّه ما منعهم من الإيمان خفاءُ ما جاء به الرسول واشتباهه هل هو حقٌّ أو باطل؟ فإنه قد جاء من البراهين الكثيرة ما دلَّ على صحَّة ما جاء به الموجب لهداية مَنْ طلب الهداية؛ فغيرُها مثلُها، فلا بدَّ أن يسلكوا بها ما سلكوا بغيرها، فتركُ إنزالها والحالة هذه خيرٌ لهم وأنفع. وقوله: {وما نرسل بالآيات إلا تخويفاً}؛ أي: لم يكن القصدُ بها أن تكون داعيةً وموجبةً للإيمان الذي لا يحصُلُ إلاَّ بها، بل المقصود منها التخويف والترهيب؛ ليرتدِعوا عن ما هم عليه.
{59} Yeye Mtukufu anataja rehema yake ya kutoteremsha ishara wanazopendekeza hao wanaokadhibisha, na kwamba halikumzuia Yeye kuzituma isipokuwa kwa kuhofia waje kuzikadhibisha. Na wakizikadhibisha, adhabu inawapata haraka bila ya kuchelewa, kama ilivyowafanya wa mwanzo ambao walizikadhibisha. Na miongoni mwa ishara kubwa zaidi ni ile ishara aliyoituma Mwenyezi Mungu kwa Thamud, ambaye ni ngamia jike mkubwa mwenye kung’aa sana, ambaye kabila zima lilikuwa linakunywa maziwa kutoka kwake lakini wakaikadhibisha ishara hiyo, basi wakapatwa na yale aliyotuhadithia Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake. Na hawa pia, lau zitawajia ishara kubwa kubwa, hawataamini. Kwa maana,
hakikuwazuia kuamini kuficha kwa yale waliyokuja nayo Mtume na kuchanganyika kwake: ni haki au batili? Kwani zimekuja hoja nyingi zinazoashiria usahihi wa yale aliyowajia nayo, jambo lanalosababisha aongoke anayetafuta uwongofu, na ishara zinginezo ni mfano wa hizo tu, na ni lazima watazitendea kama walivyozitendea zinginezo. Kwa hivyo kuacha kuziteremsha ilhali hii ndiyo hali, ni bora kwao na ni la manufaa zaidi. Na kauli yake,
“Nasi hatutumi Ishara isipokuwa kwa ajili ya kuhadharisha.” Yaani, hazikukusudiwa kuwa sababu ya kuamini kwao ambako hakuwezi kupatikana bila ya hizo, bali zilikusudiwa kuhofisha na kutishia, ili wakomeke na yale waliyonayo.
#
{60} {وإذ قلنا لك إنَّ ربَّك أحاط بالناس}: علماً وقدرةً؛ فليس لهم ملجأ يلجؤون إليه ولا ملاذٌ يلوذون به عنه، وهذا كافٍ لمن له عقلٌ في الانكفاف عما يكرهه الله الذي أحاط بالناس، {وما جَعَلْنا الرؤيا التي أرَيْناك}: أكثر المفسرين على أنَّها ليلة الإسراء، {والشجرةَ الملعونةَ}: التي ذكرت {في القرآن}: وهي شجرة الزقُّوم التي تَنْبُتُ في أصل الجحيم.
والمعنى: إذا كان هذان الأمران قد صارا فتنةً للناس، حتى استلجَّ الكفَّار بكفرهم وازداد شرُّهم، وبعض مَن كان إيمانُهُ ضعيفاً رجع عنه، بسبب أنَّ ما أخبرهم به من الأمور التي كانت ليلة الإسراء، ومن الإسراء من المسجد الحرام إلى المسجد الأقصى كان خارقاً للعادة، والإخبار بوجود شجرةٍ تَنْبُتُ في أصل الجحيم أيضاً من الخوارق؛ فهذا الذي أوجب لهم التكذيب؛ فكيفَ لو شاهدوا الآيات العظيمة والخوارق الجسيمة؟! أليس ذلك أولى أن يزداد بسببه شرُّهم؛ فلذلك رحمهم الله وصرفها عنهم. ومن هنا تعلمُ أنَّ عدم التصريح في الكتاب والسنة بذكر الأمورِ العظيمة التي حَدَثَتْ في الأزمنة المتأخِّرة أولى وأحسن؛ لأنَّ الأمور التي لم يشاهِدِ الناس لها نظيراً ربَّما لا تقبلها عقولُهم، [لو أُخْبِرُوا بها قبل وُقُوعِها] فيكون ذلك ريباً في قلوب بعض المؤمنين ومانعاً يمنعُ من لم يدخُل الإسلام ومنفراً عنه، بل ذكر الله ألفاظاً عامَّة تتناول جميع ما يكون. والله أعلم. {ونخوِّفُهم}: بالآيات، {فما يزيدهم}: التخويف {إلاَّ طغياناً كبيراً}: وهذا أبلغ ما يكون في التحلِّي بالشرِّ ومحبَّته وبغض الخير وعدم الانقياد له.
{60} "Na tulipokwambia: Hakika Mola wako Mlezi amekwisha wazunguka hao watu" kwa elimu na uwezo. Hawana kimbilio la kukimbilia kutoka kwake. Na hili linamtosha mwenye akili kuachana na yale anayoyachukia Mwenyezi Mungu ambaye amewazunguka watu. "Na hatukuifanya ndoto tuliyokuonyesha" wengi wa wafasiri wanaona kuwa ni usiku wa Safari ya Al-Isra, "na mti ule uliolaaniwa" ambao ulitajwa "katika Qur-ani" nao ni mti wa Zakumu unaotoka katikati ya Jahim. Maana yake ni kwamba ikiwa mambo haya mawili yamekuwa ni fitna kwa watu, hata makafiri wakawa na ujasiri wa kufanya ukafiri wao na uovu wao ukaongezeka, na baadhi ya wale ambao imani yao ilikuwa dhaifu wakatoka katika imani yao, kwa sababu ya yale aliyowaambia kuhusu mambo yaliyotokea usiku wa Safari ya Al-Isra, na kusafiri kwake usiku kutoka Msikiti Mtukufu hadi Msikiti wa Al-Aqsa, hayakuwa ya kawaida. Na kujulisha kwake pia kwamba kuna mti unaoota katikati ya Moto wa Jahiim kulikuwa jambo lisilo la kawaida. Basi hayo ndiyo yaliyowafanya kukadhibisha. Basi ingekuwaje ikiwa wangeona ishara kubwa kubwa na miujiza mikubwa? Je, hayo si uwezekano mkubwa wa kwamba wataongeza uovu wao kwa sababu yake? Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawarehemu na akawaondolea hayo. Na kwa sababu ya hili, utajua kwamba kutotaja kwa uwazi katika Qur-ani na Sunnah mambo makubwa yaliyotokea siku zama za mwisho ni bora zaidi. Kwa sababu mambo ambayo watu hawajawahi kushuhudia mfano wake huenda yasikubaliwe na akili zao,
[kama wangeambiwa hayo kabla ya kutokea kwake], na yakatia shaka katika nyoyo za baadhi ya waumini na kizuizi kinachozuia yule ambaye hajaingia katika Uislamu na kumfanya kujitenga mbali na Uislamu. Badala yake, Mwenyezi Mungu alitaja maneno ya jumla yenye kujumuisha kila kitu kitakachokuwepo. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi. "Na tunawahofisha" kwa ishara mbalimbali "lakini haiwazidishii" hiyo hofu "isipokuwa uasi mkubwa." Na hali hii ndiyo mbaya zaidi ya kufanya uovu na kuupenda, na kuichukia heri na kutoifuata.
{وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ قَالَ أَأَسْجُدُ لِمَنْ خَلَقْتَ طِينًا (61) قَالَ أَرَأَيْتَكَ هَذَا الَّذِي كَرَّمْتَ عَلَيَّ لَئِنْ أَخَّرْتَنِ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَأَحْتَنِكَنَّ ذُرِّيَّتَهُ إِلَّا قَلِيلًا (62) قَالَ اذْهَبْ فَمَنْ تَبِعَكَ مِنْهُمْ فَإِنَّ جَهَنَّمَ جَزَاؤُكُمْ جَزَاءً مَوْفُورًا (63) وَاسْتَفْزِزْ مَنِ اسْتَطَعْتَ مِنْهُمْ بِصَوْتِكَ وَأَجْلِبْ عَلَيْهِمْ بِخَيْلِكَ وَرَجِلِكَ وَشَارِكْهُمْ فِي الْأَمْوَالِ وَالْأَوْلَادِ وَعِدْهُمْ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلَّا غُرُورًا (64) إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ وَكَفَى بِرَبِّكَ وَكِيلًا (65)}.
61. Na pale tulipowaambia Malaika, "Msujudieni Adam." Wakamsujudia isipokuwa Iblisi. Akasema, "Je, nimsujudie uliyemuumba kwa udongo?" 62. Akasema, "Hebu unamuona huyu uliyemtukuza zaidi yangu, ukiniahirisha mpaka Siku ya Qiyama, hapana shaka nitawaangamiza dhuria zake isipokuwa wachache tu." 63. Akasema Mwenyezi Mungu, "Nenda! Na atakayekufuata katika wao, basi hakika Jahannamu itakuwa ndiyo malipo yenu, malipo yaliyo mengi." 64. Na wachochee uwawezao katika wao kwa sauti yako, na wakusanyie jeshi lako la wapandao farasi na waendao kwa miguu. Na shirikiana nao katika mali na wana, na waahidi. Na Shetani hawapi ahadi isipokuwa ya udanganyifu. 65. Hakika wewe huna mamlaka yoyote juu ya waja wangu. Na Mola wako Mlezi anatosha kuwa ni Mtegemewa.
#
{61} ينبِّه تبارك وتعالى عباده على شدَّة عداوة الشيطان وحرصه على إضلالهم، وأنَّه لما خَلَقَ الله آدم؛ استكبر عن السجود له و {قال} متكبِّراً: {أأسجُدُ لمن خلقتَ طيناً}؛ أي: من طين، وبزعمه أنَّه خيرٌ منه؛ لأنه خُلِقَ من نارٍ، وقد تقدَّم فساد هذا القياس الباطل من عدة أوجه.
{61} Yeye Mwingi wa baraka anatanabahisha waja wake juu ya ukubwa wa uadui wa Shetani na kufanya kwake bidii kubwa kuwapotosha, na kwamba Mwenyezi Mungu alipomuumba Adam, akajivuna kumsujudia. Na "Akasema" kwa kiburi, "Je, nimsujudie uliyemuumba kwa udongo?" Akadai kuwa yeye ni bora kuliko Adam, kwa sababu aliumbwa kutokana na moto, na tayari ilikwisha tangulia kubainisha ubovu wa ulinganisho huu batili kwa njia nyingi.
#
{62} فلما تبين لإبليس تفضيل الله لآدم؛ {قال} مخاطباً لله: {أرأيتَكَ هذا الذي كرَّمْتَ عليَّ لئنْ أخَّرْتَنِ إلى يوم القيامةِ لأحتَنِكَنَّ ذُرِّيَّتَهُ}؛ أي: لأستأصلَنَّهم بالإضلال ولأغْوِيَنَّهم، {إلاَّ قليلاً}: عرف الخبيثُ أنَّه لا بدَّ أن يكون منهم من يعاديه ويعصيه.
{62} Ilipombainikia Ibilis kwamba Mwenyezi Mungu amemfadhilisha Adam, "akasema" akimwambia Mwenyezi Mungu, "Hebu unamuona huyu uliyemtukuza zaidi yangu, ukiniahirisha mpaka Siku ya Qiyama, hapana shaka nitawaangamiza dhuria zake," kwa kuwapotosha na kuwadanganya; "isipokuwa wachache tu." Yeye mwovu alijua ya kwamba lazima watakuwapo baadhi yao watakaomfanya kuwa adui yao na kumuasi.
#
{63} فقال الله له: {اذهبْ فمن تبعك منهم}: واختارك على ربِّه ووليِّه الحقِّ. {فإنَّ جهنَّم جزاؤكم جزاءً موفوراً}؛ أي: مدَّخراً لكم موفَّراً جزاء أعمالكم.
{63} Mwenyezi Mungu akamwambia, "Nenda! Na atakayekufuata katika wao," na akachagua wewe badala ya Mola wake Mlezi, na mlinzi wake wa haki; "Basi hakika Jahannamu itakuwa ndiyo malipo yenu, malipo yaliyo mengi" kwa matendo yenu.
#
{64} ثم أمره الله أن يفعلَ كلَّ ما يقدِرُ عليه من إضلالهم، فقال: {واستفزِزْ من استطعتَ منهم بصوتِكَ}: ويدخل في هذا كلُّ داعٍ إلى المعصية، {وأجْلِبْ عليهم بخيلِكَ ورَجِلكَ}: ويدخل فيه كلُّ راكبٍ وماشٍ في معصية الله؛ فهو من خيل الشيطان ورَجِلِهِ. والمقصود أنَّ الله ابتلى العباد بهذا العدوِّ المبين الداعي لهم إلى معصية الله بأقواله وأفعاله. {وشارِكْهم في الأموال والأولاد}: وذلك شاملٌ لكلِّ معصية تعلَّقت بأموالهم وأولادهم من منع الزكاة والكفَّارات والحقوق الواجبة، وعدم تأديب الأولاد وتربيتهم على الخير وترك الشرِّ، وأخذ الأموال بغير حقِّها أو وضعها بغير حقِّها أو استعمال المكاسب الرديَّة، بل ذَكَرَ كثيرٌ من المفسِّرين أنه يدخُلُ في مشاركة الشيطان في الأموال والأولادِ تركُ التسمية عند الطعام والشراب والجماع، وأنَّه إذا لم يُسَمِّ الله في ذلك؛ شارك فيه الشيطان؛ كما ورد فيه الحديث. {وعِدْهم}: الأوعادَ المزخْرَفَة التي لا حقيقة لها، ولهذا قال: {وما يَعِدُهُم الشيطانُ إلاَّ غروراً}؛ أي: باطلاً مضمحلًّا؛ كأن يزيِّن لهم المعاصي والعقائد الفاسدة، ويعدهم عليها الأجر؛ لأنَّهم يظنُّون أنَّهم على الحق، وقال تعالى: {الشيطان يَعِدُكُم الفقر ويأمُرُكم بالفحشاءِ والله يَعِدُكُم مغفرةً منه وفضلاً}.
{64} Kisha Mwenyezi Mungu akamwamuru afanye kila awezalo katika kuwapoteza, akasema, "Na wachochee uwawezao katika wao kwa sauti yako" na anaingia katika hili kila anayelingania katika maasia. "Na wakusanyie jeshi lako la wapandao farasi na waendao kwa miguu." Na inaingia katika hili kila mpandaji na mtembeaji katika kumuasi Mwenyezi Mungu. Basi yeye ni miongoni mwa jeshi lake la wapandao farasi na waendao kwa miguu. Kinachokusudiwa ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwajaribu waja wake kwa adui huyu wa wazi anayewalingania katika kumuasi Mwenyezi Mungu kwa maneno yake na matendo yake. "Na shirikiana nao katika mali na wana." Haya yanajumuisha kila dhambi linalohusiana na mali yao na watoto wao, kama vile kukataa kutoa zaka, fidia mbalimbali, na haki za faradhi, kutowapa adabu nzuri watoto na kuwalea katika heri na kuacha maovu, kuchukua mali bila ya haki au kuitumia kwa yasiyo ya haki, au kutumia mapato mabaya. Basi wengi katika wafasiri walitaja kuwa hilo kumshirikisha Shetani katika mali na watoto, kunajumuisha kuacha kutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kula, kunywa, au kufanya tendo la ndoa, na kwamba ikiwa hatalitaja jina la Mwenyezi Mungu katika hayo, basi Shetani atashirikiana naye, kama ilivyokuja katika Hadithi. "Na waahidi" ahadi za uongo ambazo hazina uhakika wowote. Na ndiyo maana akasema, "Na Shetani hawapi ahidi isipokuwa ya udanganyifu" yenye kupotelea mbali, kama vile kuwapambia maasia na itikadi potovu, na akawaahidi malipo juu yake, kwa sababu wanadhani kwamba wako katika haki. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, “Shetani anawatia hofu ya ufukara na anawaamrisha mambo machafu. Na Mwenyezi Mungu anawaahidi msamaha na fadhila zitokazo kwake."
#
{65} ولما أخبر عما يريد الشيطان أن يفعل بالعباد؛ ذَكَرَ ما يُعْتَصَمُ به من فتنته، وهو عبوديَّة الله والقيام بالإيمان والتوكُّل، فقال: {إنَّ عبادي ليس لك عليهم سلطانٌ}؛ أي: تسلُّط وإغواءٌ، بل الله يدفع عنهم بقيامهم بعبوديَّته كلَّ شرٍّ، ويحفظُهم من الشيطان الرجيم، ويقوم بكفايتهم. {وكفى بربِّك وكيلاً}: لمن توكَّل عليه، وأدَّى ما أمر به.
{65} Na alipojulisha kuhusu yale anayotaka Shetani kuwafanyia waja wake, akataja yale yatakayowakinga kutokana na majaribio yake, nayo ni kumuabudu Mwenyezi Mungu na kumuamini na kumtegemea. Akasema, "Hakika wewe huna mamlaka yoyote juu ya waja wangu" ya kuwapoteza. Bali Mwenyezi Mungu anawalinda kutokana na kila uovu kwa sababu ya kumuabudu kwao na anawakinga kutokana na Shetani aliyelaaniwa, na huwatosheleza. "Na Mola wako Mlezi anatosha kuwa ni Mtegemewa" kwa mwenye kumtegemea Yeye, na akafanya aliyoamrishwa.
{رَبُّكُمُ الَّذِي يُزْجِي لَكُمُ الْفُلْكَ فِي الْبَحْرِ لِتَبْتَغُوا مِنْ فَضْلِهِ إِنَّهُ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا (66) وَإِذَا مَسَّكُمُ الضُّرُّ فِي الْبَحْرِ ضَلَّ مَنْ تَدْعُونَ إِلَّا إِيَّاهُ فَلَمَّا نَجَّاكُمْ إِلَى الْبَرِّ أَعْرَضْتُمْ وَكَانَ الْإِنْسَانُ كَفُورًا (67) أَفَأَمِنْتُمْ أَنْ يَخْسِفَ بِكُمْ جَانِبَ الْبَرِّ أَوْ يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ثُمَّ لَا تَجِدُوا لَكُمْ وَكِيلًا (68) أَمْ أَمِنْتُمْ أَنْ يُعِيدَكُمْ فِيهِ تَارَةً أُخْرَى فَيُرْسِلَ عَلَيْكُمْ قَاصِفًا مِنَ الرِّيحِ فَيُغْرِقَكُمْ بِمَا كَفَرْتُمْ ثُمَّ لَا تَجِدُوا لَكُمْ عَلَيْنَا بِهِ تَبِيعًا (69)}.
66. Mola wenu Mlezi ndiye anayewaendeshea marikebu katika bahari ili mtafute katika fadhila zake. Hakika Yeye ni Mwingi kuwarehemu nyinyi. 67. Na inapowakuta taabu katika bahari, hao mnaowaomba wanapotea, isipokuwa Yeye tu. Na anapowaokoa mkafika nchi kavu, mnageuka. Ama mwanadamu ni mwingi wa kukufuru. 68. Je, mna amani ya kuwa hatawadidimiza katika upande wowote katika nchi kavu, au kwamba hatawatumia tufani la kokoto? Kisha msipate yeyote wa kumtegemea. 69. Au mna amani ya kuwa hatawarudisha humo mara nyingine na akawatumia kimbunga cha upepo akawazamisha kwa mlivyokufuru, na kisha msipate wa kuwanusuru kutokana nasi.
#
{66} يذكر تعالى نعمته على العباد بما سخَّر لهم من الفُلك والسفن والمراكب، وألهمهم كيفيَّة صنعتها وسخَّر لها البحر الملتطم يحملها على ظهره؛ لينتفع العباد بها في الركوب والحمل للأمتعة والتجارة، وهذا من رحمته بعباده؛ فإنَّه لم يزْل بهم رحيماً رءوفاً، يؤتيهم من كلِّ ما تعلَّقت به إرادتهم ومنافعهم.
{66} Mwenyezi Mungu Mtukufu anataja neema zake juu ya waja wake kwa yale aliyowatiishia kama vile majahazi, safina na vipando vingine, na akawafunulia wahyi namna ya kuzitengeneza, na akazitiishia bahari iliyovurugika, na yenye kuwabeba juu ya mgongo wake, ili waja wake wanufaike nayo kwa kuyapanda na kubeba mizigo na biashara, na hii ni kutokana na rehema yake kwa waja wake. Kwa maana hajaacha kuwa mwingi rehema na mpole kwao, na huwapa katika kila kitu ambacho kinafungamana na utashi yao na manufaa yao.
#
{67} ومن رحمته الدالَّة على أنَّه وحده المعبود دون ما سواه أنَّهم إذا مسَّهم الضُّرُّ في البحر، فخافوا من الهلاك لتراكُم الأمواج؛ ضلَّ عنهم ما كانوا يدعون من دون الله في حال الرَّخاء من الأحياء والأموات، فكأنُّهم لم يكونوا يدعونهم في وقتٍ من الأوقات؛ لعلمهم أنَّهم ضعفاء عاجزون عن كشف الضُّرِّ، وصرخوا بدعوة فاطر الأرض والسماوات، الذي تستغيث به في شدائدها جميعُ المخلوقات، وأخلصوا له الدعاء والتضرُّع في هذه الحال، فلما كَشَفَ الله عنهم الضُّرَّ ونجَّاهم إلى البَرِّ؛ نسوا ما كانوا يدعون إليه من قبل، وأشركوا به مَنْ لا ينفع ولا يضرُّ ولا يعطي ولا يمنع، وأعرضوا عن الإخلاص لربِّهم ومليكهم.
وهذا من جهل الإنسان وكفرِهِ؛ فإنَّ الإنسان كفورٌ للنِّعم؛ إلاَّ مَن هدى الله فمنَّ عليه بالعقل السليم واهتدى إلى الصراط المستقيم؛ فإنَّه يعلم أنَّ الذي يكشف الشدائد، وينجِّي من الأهوال هو الذي يستحقُّ أن يُفْرَدَ، وتُخْلَصَ له سائر الأعمال في الشدَّة والرَّخاء واليُسر والعُسر، وأما من خُذِلَ ووُكِلَ إلى عقله الضعيف؛ فإنَّه لم يلحَظْ وقت الشدَّة إلاَّ مصلحته الحاضرة وإنجاءه في كلِّ تلك الحال، فلما حصلتْ له النجاةُ وزالت عنه المشقَّة؛ ظنَّ بجهله أنَّه قد أعجز الله، ولم يَخْطُرْ بقلبه شيء من العواقب الدنيويَّة فضلاً عن أمور الآخرة.
{67} Na miongoni mwa rehema zake zinazoashiria kuwa Yeye pekee ndiye anayeabudiwa na si mwingine ni kwamba yakiwapata madhara baharini, na wakahofu kuangamia kwa sababu ya kurundikana kwa mawimbi, wanatoweka wale ambao wao walikuwa wakiwaomba kama vile walio hai na wafu, badala ya Mwenyezi Mungu wakiwa katika nyakati nzuri. Na ni kana kwamba hawakuwahi kuwaomba wakati wowote ule, kwa kuwa walijua kwamba wao ni dhaifu na hawawezi kuondoa madhara, hivyo wakapiga kelele wakimuomba Muumba wa ardhi na mbingu, ambaye viumbe vyote vinamtafuta msaada katika shida zao, na wakamsafishia yeye tu dua na kumnyenyekea katika hali hii. Basi pindi Mwenyezi Mungu alipowaondolea madhara hayo na akawaokoa na wakawa katika nchi kavu, wakasahau yale waliyokuwa wakiyaomba kabla, na wakamshirikisha na wale wasionufaisha, wala hawadhuru, wala hawapeani, wala hawanyimi, na wakaacha kumsafishia matendo Mola wao Mlezi na Mfalme wao. Na haya ni katika ujinga wa mtu na ukafiri wake. Kwa maana mtu ni mwenye kukufuru sana neema isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa, basi akamneemesha akili timamu na akaongoka kwenye njia iliyonyooka. Yeye, anajua kwamba mwenye kuondosha dhiki na kuokoa kutokana na mambo ya kutisha ndiye anayestahiki kupwekeshwa, na kumsafishia yeye tu matendo katia dhiki, faraja, wepesi na ugumu. Na ama aliyeachiliwa mbali, na akaachwa kusimamiwa na akili dhaifu, yeye hakuona katika wakati wa dhiki isipokuwa manufaa yake ya sasa na kuokoka kutoka katika hali hiyo yote, na pindi alipookoka na shida hiyo ikamuondoka, akadhani kwa ujinga wake kwamba amemshinda Mwenyezi Mungu, na wala haikumjia katika akili yake matokeo yoyote ya kidunia, sembuse mambo ya akhera.
#
{68 - 69} ولهذا ذكَّرهم الله بقولِهِ: {أفأمِنتُم أن يخسِفَ بكم جانبَ البَرِّ أو يرسلَ عليكم حاصباً}؛ أي: فهو على كل شيء قديرٌ، إن شاء أنزل عليكم عذاباً من أسفلَ منكم بالخسفِ، أو من فوقِكم بالحاصب، وهو العذابُ الذي يَحصُبُهم فيصبحوا هالكين؛ فلا تظنُّوا أنَّ الهلاك لا يكون إلا في البحر، وإنْ ظننتُم ذلك؛ فأنتم آمنون من {أن يعيدكم}: في البحر؛ {تارةً أخرى فيرسل عليكم قاصِفاً من الريح}؛ أي: ريحاً شديدةً جدًّا تقصف ما أتت عليه، {فيغرِقَكم بما كفرتم ثم لا تَجِدوا لكم علينا به تبيعاً}؛ أي: تبعة ومطالبة؛ فإنَّ الله لم يظلمْكُم مثقال ذرَّة.
{68 - 69} Na kwa sababu hii, Mwenyezi Mungu akawakumbusha kwa kauli yake, "Je, mna amani ya kuwa hatawadidimisha upande wowote katika nchi kavu, au kwamba hatawatumia tufani la kokoto?" Kwa maana Yeye ni Muweza juu ya kila kitu. Akitaka, atawateremshia adhabu kutokea chini yenu kwa kuwadidimiza, au kutokea juu yenu kwa tufani la kokoto na iwaache wameangamia. Basi msidhani kwamba kuangamia hakutokei isipokuwa baharini. Na ikiwa mnadhani hivyo, basi kwani mna amani kuwa, "Hatawarudisha" baharini "mara nyingine na akawatumia kimbunga cha upepo." Yaani, upepo mkali sana utakaoharibu chochote unachokifikia, "akawazamisha kwa mlivyokufuru, na kisha msipate wa kuwanusuru kutokana nasi." Kwa maana Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu hata uzito wa chembe.
{وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِي آدَمَ وَحَمَلْنَاهُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَرَزَقْنَاهُمْ مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَى كَثِيرٍ مِمَّنْ خَلَقْنَا تَفْضِيلًا (70)}.
70. Na hakika tumewatukuza wanadamu, na tukawabeba katika nchi kavu na baharini, na tukawaruzuku katika vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa wale tuliowaumba.
#
{70} وهذا من كرمِهِ عليهم وإحسانه الذي لا يقادَرُ قَدْرُهُ؛ حيث كرَّم بني آدم بجميع وجوه الإكرام، فكرَّمهم بالعلم والعقل وإرسال الرسل وإنزال الكتب، وجعل منهم الأولياءَ والأصفياء، وأنعم عليهم بالنِّعم الظاهرة والباطنة، {وحَمَلْناهم في البرِّ}: على الركاب من الإبل والبغال والحمير والمراكب البريَّة. وفي {البحر}: في السفن والمراكب، {ورَزَقْناهم من الطيبات}: من المآكل والمشاربِ والملابس والمناكح؛ فما من طيب تتعلَّق به حوائجهم إلاَّ وقد أكرمهم الله به ويسَّره لهم غاية التيسيرِ، {وفضَّلْناهم على كثيرٍ ممَّن خَلَقْنا تفضيلاً}: بما خصَّهم به من المناقب وفضَّلهم به من الفضائل التي ليست لغيرهم من أنواع المخلوقات، أفلا يقومون بشكر مَنْ أولى النعم ودَفَعَ النِّقم ولا تحجبهم النِّعم عن المنعم فيشتغلوا بها عن عبادة ربِّهم، بل ربَّما استعانوا بها على معاصيه؟!
{70} Na hili ni katika ukarimu wake kwao na wema wake, ambao thamani yake haina kipimo. Ambapo aliwatukuza wanadamu kwa kila njia za kutukuza. Basi akawatukuza kwa elimu na akili, na kuwatuma Mitume, na kuwateremshia vitabu, na akawafanya vipenzi vyake miongoni mwake, na wateule, na akawaneemesha kwa neema zilizo wazi na zilizofichika. "Na tukawabeba katika nchi kavu" juu ya vipando kama vile ngamia, nyumbu, na punda, na vipando vinginevyo vya nchi kavu. Na "baharini" katika majahazi na meli "na tukawaruzuku katika vitu vizuri vizuri" kama vile vyakula, vinywaji, nguo, na mambo ya ndoa. Basi hakuna chochote kizuri kinachohusiana na mahitaji yao isipokuwa Mwenyezi Mungu amewatukuza kwacho na amewarahishia hilo kabisa "na tukawafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa wale tuliowaumba," kwa mambo maalumu aliyowapa kama vile sifa nzuri, na akawafadhilisha kwazo kwa namna ambayo hakuna wengine walizo nazo miongoni mwa aina mbalimbali za viumbe. Je, basi hawatamshukuru aliyewafikishia neema hizi na akawazuilia maangamivu? Na wala zisiwazuie neema hizo dhidi ya aliyezineemesha kwa hivyo zikawashughulisha wasimuabudu Mola wao Mlezi. Bali huenda wakazitumia neema kuwasaidia katika kumuasi.
{يَوْمَ نَدْعُو كُلَّ أُنَاسٍ بِإِمَامِهِمْ فَمَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ فَأُولَئِكَ يَقْرَءُونَ كِتَابَهُمْ وَلَا يُظْلَمُونَ فَتِيلًا (71) وَمَنْ كَانَ فِي هَذِهِ أَعْمَى فَهُوَ فِي الْآخِرَةِ أَعْمَى وَأَضَلُّ سَبِيلًا (72)}.
71. Siku tutakapowaita kila kikundi cha watu kwa mujibu wa wakifuatacho, basi atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, basi hao watasoma kitabu chao wala hawatadhulumiwa hata chembe. 72. Na yule ambaye ni kipofu hapa, basi atakuwa kipofu Akhera, na atakuwa ndiye mpotovu zaidi wa Njia.
#
{71} يخبر تعالى عن حال الخلق يوم القيامة، وأنه يدعو كلَّ أناس معهم إمامهم وهاديهم إلى الرُّشد، وهم الرسل ونوابهم، فتعرض كلُّ أمة، ويحضرها رسولهم الذي دعاهم، وتعرض أعمالهم على الكتاب الذي يدعو إليه الرسول هل هي موافقة له أم لا؟ فينقسمون بهذا قسمين: {فمن أوتي كتابه بيمينه}: لكونه اتَّبع إمامه الهادي إلى صراطٍ مستقيم، واهتدى بكتابه، فكثرت حسناتُه، وقلَّت سيئاتُه؛ {فأولئك يقرؤون كتابهم}: قراءة سرورٍ وبهجة على ما يرون فيها مما يفرِحُهم ويسرُّهم، {ولا يُظلمون فتيلاً}: ممّا عملوه من الحسنات.
{71} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu hali ya viumbe Siku ya Qiyama, na kwamba atawaita kila kikundi cha watu pamoja na imamu wao na mwongozi wao kwenye njia iliyonyooka, na wao ni Mitume na wawakilishi wao. Kwa hivyo kila umma watahudhurishwa, na atakuwepo Mtume wao aliyewalingania, na matendo yao yatawasilishwa mbele ya Kitabu alicholingania Mtume wao, je yanaafikiana nacho au hapana? Kisha watagawanyika katika makundi mawili, "basi atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia," kwa sababu alimfuata imamu wake, kiongozi kwenye njia iliyonyooka, na akaongoka kwa kitabu chake, basi mazuri yake yakakithiri, na maovu yake yakawa machache. "Basi hao watasoma kitabu chao" kisomo cha furaha na uzuri kwa sababu ya yale wanayoyaona humo, katika yale yenye kuwafurahisha, "wala hawatadhulumiwa hata chembe."
#
{72} {ومن كان في هذه}: الدنيا {أعمى}: عن الحقِّ؛ فلم يقبَلْه ولم ينقدْ له، بل اتَّبع الضلال، {فهو في الآخرة أعمى}: عن سلوك طريق الجنَّة كما لم يسلكه في الدنيا، {وأضلُّ سبيلاً}: فإنَّ الجزاء من جنس العمل، وكما تَدين تُدان.
وفي هذه الآية دليل على أنَّ كلَّ أمة تُدعى إلى دينها وكتابها وهل عملت به أم لا؟ وأنهم لا يؤاخذون بشرع نبيٍّ لم يؤمروا باتِّباعه، وأنَّ الله لا يعذِّب أحداً إلاَّ بعد قيام الحجَّة عليه ومخالفته لها، وأنَّ أهل الخير يعطَوْن كتبهم بأيمانهم، ويحصُلُ لهم من الفرح والسرور شيءٌ عظيم، وأنَّ أهل الشرِّ بعكس ذلك، وأنهم لا يقدِرون على قراءة كتبهم من شدَّة غمِّهم وحزنهم وثبورهم.
{72} "Na yule ambaye ni kipofu hapa" duniani asiijue na kuikubali haki, wala kuifuata, bali alifuata upotofu, "basi atakuwa kipofu Akhera" asiweze kushika njia ya peponi kwa vile hakuishika duniani, "na atakuwa ndiye mpotovu zaidi wa Njia." Kwa kuwa malipo ni kwa aina sawa na matendo. Na kama unavyotenda, ndivyo utakavyotendewa. Na katika Aya hii, kuna ushahidi kwamba kila umma utaitwa kwenye dini yake na kitabu chake. Na je, ulitenda kwa kufuata hayo au la? Na kwamba hawataadhibiwa kwa sheria ya Nabii ambaye hawakuamrishwa kuifuata, na kwamba Mwenyezi Mungu hamuadhibu yeyote isipokuwa baada ya kusimama hoja juu yake naye akaihalifu. Na kwamba watu wema watapewa vitabu vyao kwa mikono yao ya kulia, na watapata furaha nyingi, na kwamba watu waovu wako kinyume na hayo, na kwamba hawataweza kusoma vitabu vyao kwa sababu ya ukubwa wa dhiki yao, na huzuni yao, na kuangamia kwao.
{وَإِنْ كَادُوا لَيَفْتِنُونَكَ عَنِ الَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ لِتَفْتَرِيَ عَلَيْنَا غَيْرَهُ وَإِذًا لَاتَّخَذُوكَ خَلِيلًا (73) وَلَوْلَا أَنْ ثَبَّتْنَاكَ لَقَدْ كِدْتَ تَرْكَنُ إِلَيْهِمْ شَيْئًا قَلِيلًا (74) إِذًا لَأَذَقْنَاكَ ضِعْفَ الْحَيَاةِ وَضِعْفَ الْمَمَاتِ ثُمَّ لَا تَجِدُ لَكَ عَلَيْنَا نَصِيرًا (75) وَإِنْ كَادُوا لَيَسْتَفِزُّونَكَ مِنَ الْأَرْضِ لِيُخْرِجُوكَ مِنْهَا وَإِذًا لَا يَلْبَثُونَ خِلَافَكَ إِلَّا قَلِيلًا (76) سُنَّةَ مَنْ قَدْ أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ مِنْ رُسُلِنَا وَلَا تَجِدُ لِسُنَّتِنَا تَحْوِيلًا (77)}.
73. Na hakika walikaribia kukushawishi uache hayo tuliyokufunulia ili utuzulie mengineyo. Na hapo, ndipo wangelikufanya mwandani. 74. Na lau kuwa hatukukuweka imara, ungelikaribia kuwaegemea kidogo. 75. Hapo basi bila ya shaka, tungelikuonjesha adhabu maradufu ya uhai, na adhabu maradufu ya kifo. Kisha usingepata yeyote wa kukunusuru kutokana nasi. 76. Na walitaka kukukera ili wakutoe nchini. Na hapo, wao wasingelibakia humo isipokuwa kwa muda mchache tu. 77. Hiyo ndiyo desturi ya Mitume tuliowatuma kabla yako. Wala hutapata mabadiliko katika desturi yetu.
#
{73} يذكر تعالى منَّته على رسوله محمدٍ - صلى الله عليه وسلم - وحفظه له من أعدائه الحريصين على فتنته بكل طريق، فقال: {وإن كادوا لَيَفْتِنونك عن الذي أوحينا إليك لتفتريَ علينا}؛ أي: قد كادوا لك أمراً لم يُدْرِكوه، وتحيَّلوا لك على أن تفتري على الله غير الذي أنزلنا إليك، فتجيء بما يوافقُ أهواءهم، وتدعُ ما أنزل الله إليك. {وإذاً}: لو فعلت ما يهوون؛ {لاتَّخذوك خليلاً}؛ أي: حبيباً صفيًّا أعزَّ عليهم من أحبابهم لما جَبَلَكَ الله عليه من مكارم الأخلاق ومحاسن الآداب المحبَّبة للقريب والبعيد والصديق والعدوِّ، ولكن لتعلم أنَّهم لم يعادوك وينابذوك العداوة إلاَّ للحقِّ الذي جئتَ به لا لِذَاتك؛ كما قال تعالى: {قد نعلمُ إنَّه لَيَحْزُنُك الذي يقولون فإنَّهم لا يكذِّبونَكَ ولكنَّ الظالمين بآيات الله يجحدونَ}.
{73} Yeye Mtukufu anataja neema yake kwa Mtume wake Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – na kumhifadhi kwake kutokana na maadui zake ambao walikuwa na bidii ya kumjaribu kwa kila njia. Akasema, "Na hakika walikaribia kukushawishi uache hayo tuliyokufunulia ili utuzulie mengineyo." Yaani, walikupangia jambo baya ambalo hawakufanikiwa kulifikia, na wakakuhadaa ili umzulie Mwenyezi Mungu mambo ambayo hakukuteremshia, ili useme yale yanayoafikiana na matamanio yao, na uyaache yale aliyokuteremshia Mwenyezi Mungu. "Na hapo" lau ungefanya yale wanayotamani, "ndipo wangelikufanya mwandani" na kipenzi zaidi kwao kuliko wapenzi wao, kwa sababu ya maadili mema na tabia njema alizokuumba nazo Mwenyezi Mungu, ambazo zinamvutia walio karibu na walio mbali, rafiki na adui. Lakini ujue ya kwamba hawakukufanyia uadui na kukukanusha kwa uadui, isipokuwa kwa sababu ya haki ambayo ulikuja nayo, si kwa ajili yako mwenyewe, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, “Hakika tunajua ya kwamba yanakuhuzunisha hayo wanayoyasema. Basi hakika wao hawakukadhibishi wewe, lakini hao madhalimu wanazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu."
#
{74} {و} مع هذا {لولا أن ثَبَّتْناك}: على الحقِّ وامتنَّنا عليك بعدم الإجابة لداعيهم، {لقد كدتَ تركنُ إليهم شيئاً قليلاً}: من كثرة المعالجة ومحبَّتك لهدايتهم.
{74} "Na" pamoja na haya, "lau kuwa hatukukuweka imara" juu ya haki na tukakuneemesha kwa kutomuitikia mwitaji wao, "ungelikaribia kuwaegemea kidogo" kwa sababu ya kuwafuatilia kwako kwa wingi na kupenda kwako waongoke.
#
{75} {إذاً}: لو ركنت إليهم بما يهوون، {لأذقناك ضعفَ الحياة وضعفَ المماتِ}؛ أي: لأصبناك بعذابٍ مضاعفٍ في الدُّنيا والآخرة، وذلك لكمال نعمة الله عليك وكمال معرفتك. {ثمَّ لا تَجِدُ لك علينا نصيراً}: ينقذك مما يحلُّ بك من العذاب، ولكن الله تعالى عَصَمَكَ من أسباب الشَّرِّ ومن الشَّرِّ، فثبَّتك وهداك الصراط المستقيم، ولم تركَنْ إليهم بوجه من الوجوه؛ فله عليك أتمُّ نعمةٍ وأبلغ منحةٍ.
{75} "Hapo basi" lau ungeliegemea kwao kwa yale wanayoyatamani hao, "bila ya shaka, tungelikuonjesha adhabu maradufu ya uhai, na adhabu maradufu ya kifo." Yaani, tungekutia adhabu maradufu duniani na Akhera. Na hilo ni kwa sababu ya ukamilifu wa neema ya Mwenyezi Mungu juu yako na kujua kwako hayo kikamilifu. "Kisha usingepata yeyote wa kukunusuru kutokana nasi" kutokana na adhabu ambayo inngekupata. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu akakulinda kutokana na sababu za maovu na hata maovu yenyewe. Basi akakuimarisha na akakuongoa kwenye njia iliyonyooka, wala hukuwategemea kwa njia yoyote ile. Basi Yeye anazo neema kamili zaidi na kipawa kikubwa zaidi juu yako.
#
{76 - 77} {وإن كادوا لَيَسْتَفِزُّونك من الأرض لِيُخْرِجوك منها}؛ أي: من بغضهم لمقامك بين أظهرهم، قد كادوا أن يخرجوك من الأرضِ ويُجْلوك عنها، ولو فعلوا ذلك؛ لم يلبثوا بعدك فيها إلاَّ قليلاً، حتى تحلَّ بهم العقوبة؛ كما هي سنة الله التي لا تحول ولا تبدل في جميع الأمم، كل أمة كذبت رسولها وأخرجته؛ عاجلها الله بالعقوبة، ولمَّا مكر به الذين كفروا وأخرجوه؛ لم يلبثوا إلاَّ قليلاً حتَّى أوقع الله بهم ببدرٍ، وقَتَلَ صناديدهم، وفَضَّ بيضتهم؛ فله الحمد.
وفي هذه الآيات دليلٌ على شدة افتقار العبد إلى تثبيت الله إياه، وأنَّه [ينبغي له أن] لا يزال متملِّقاً لربِّه أن يثبته على الإيمان ساعياً في كلِّ سبب موصل إلى ذلك؛ لأنَّ النبيَّ - صلى الله عليه وسلم - - وهو أكمل الخلق - قال الله له: {ولولا أن ثَبَّتْناك لقد كِدت تَرْكَنُ إليهم شيئاً قليلاً}؛ فكيف بغيره؟!
وفيها: تذكيرُ الله لرسوله منَّته عليه وعصمته من الشرِّ، فدلَّ ذلك على أنَّ الله يحبُّ من عباده أن يتفطَّنوا لإنعامه عليهم عند وجود أسباب الشرِّ بالعصمة منه والثبات على الإيمان.
وفيها: أنه بحسب علوِّ مرتبة العبد وتواتُرِ النِّعم عليه من الله يَعْظُمُ إثمُهُ ويتضاعفُ جرمُهُ إذا فعل ما يُلام عليه؛ لأنَّ الله ذكَّر رسوله لو فعل - وحاشاه من ذلك - بقوله: {إذاً لأذَقْناك ضعفَ الحياة وضعفَ الممات ثم لا تجِدُ لك علينا نصيراً}.
وفيها: أنَّ الله إذا أراد إهلاك أمَّة؛ تضاعف جُرمها وعَظُم وكَبُر، فيحقُّ عليها القولُ من الله، فيوقع بها العقاب؛ كما هي سنَّته في الأمم إذا أخرجوا رسولهم.
{76 - 77} "Na walitaka kukukera ili wakutoe nchini." Yaani, kwa sababu ya kuchukia kwao kuishi kwako pamoja nao, walikuwa karibu zaidi kukutoa nchini na kukuhamisha kutoka humo. Na kama wangefanya hivyo, wasingalikaa humo baada yako isipokuwa muda mfupi tu kabla ya kujiwa na adhabu, kama ilivyo desturi ya Mwenyezi Mungu ambayo haigeuki wala haibadiliki katika umma zote, kila umma uliomkadhibisha Mtume wake na ukamfukuza, Mwenyezi Mungu aliwaharakishia adhabu. Na wale waliokufuru walipompangia njama na wakamfukuza, hawakukaa isipokuwa muda mfupi tu kabla ya Mwenyezi Mungu kuwaadhibu huko Badr, na akawaua wakuu wao, na akatawanya umoja wao. Basi sifa njema zote ni zake. Na katika aya hizi, kuna ushahidi juu ya uhitaji mkubwa zaidi wa mja juu ya kuimarishwa na Mwenyezi Mungu, na kwamba
[anapaswa] kuendelea kumuomba Mola wake Mlezi kwamba amuimarishe katika imani, akijitahidi kufanya kila sababu inayofikisha katika hilo. Kwa sababu Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – pamoja na kwamba yeye ndiye mkamilifu zaidi wa viumbe - Mwenyezi Mungu alimwambia, "na lau kuwa hatukukuweka imara, ungelikaribia kuwaegemea kidogo." Basi vipi kuhusu watu wengine? Na ndani yake pia Mwenyezi Mungu anamkumbusha Mtume wake neema yake juu yake na humkinga kwake kutokana na maovu. Kwa hivyo, hilo likaashiria kuwa Mwenyezi Mungu anapenda kwamba waja wake wawe na habari ya neema zake juu yao pindi zinapopatikana sababu za maovu kwa kutafuta kinga kutoka kwake na kukaa imara katika imani. Na ndani yake kuna kwamba kulingana na cheo cha mja na wingi wa kumshukia neema juu yake kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ndiyo dhambi zake zinakuwa kubwa na uhalifu wake unaongezeka maradufu ikiwa akifanya anacholaumiwa juu yake. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alimkumbusha Mtume wake kwamba kama angefanya hivyo - na aepushwe na hilo - kwa kwa kauli yake,
“bila ya shaka, tungelikuonjesha adhabu maradufu ya uhai, na adhabu maradufu ya kifo. Kisha usingepata yeyote wa kukunusuru kutokana nasi.” Na ndani yake kuna kwamba Mwenyezi Mungu akitaka kuuangamiza umma, uhalifu wake huongezeka na kuwa mkubwa zaidi na zaidi, kwa hivyo ukawa unastahiki neno la adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwa hivyo anauadhibu kama ilivyo desturi yake katika umma zote wanapomfukuza Mtume wao.
{أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَى غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ الْفَجْرِ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا (78) وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَكَ عَسَى أَنْ يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَحْمُودًا (79) وَقُلْ رَبِّ أَدْخِلْنِي مُدْخَلَ صِدْقٍ وَأَخْرِجْنِي مُخْرَجَ صِدْقٍ وَاجْعَلْ لِي مِنْ لَدُنْكَ سُلْطَانًا نَصِيرًا (80) وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا (81)}.
78. Simamisha Swala jua linapopinduka mpaka giza la usiku, na Qur-ani ya alfajiri. Hakika Qur-ani ya alfajiri inashuhudiwa daima. 79. Na amka usiku kwa ibada, ni ziada ya sunna hasa kwako wewe. Huenda Mola wako Mlezi akakunyanyua cheo kinachosifika. 80. Na sema, "Mola wangu Mlezi! Niingize muingizo mwema, na unitoe kutoka kwema. Na unipe nguvu zinazotoka kwako zinisaidie." 81. Na sema, "Haki imefika, na batili imetoweka. Hakika batili lazima itoweke!"
#
{78} يأمر تعالى نبيَّه محمداً - صلى الله عليه وسلم - بإقامة الصلاة تامَّة ظاهراً وباطناً في أوقاتها، {لِدُلوك الشمس}؛ أي: ميلانها إلى الأُفقِ الغربيِّ بعد الزوال، فيدخُلُ في ذلك صلاة الظهر وصلاة العصر {إلى غَسَقِ الليل}؛ أي: ظلمتِهِ، فدخل في ذلك صلاة المغرب وصلاة العشاء، {وقرآنَ الفجْرِ}؛ أي: صلاة الفجر، وسمِّيت قرآناً لمشروعيَّة إطالة القرآن فيها أطول من غيرها، ولفضل القراءة؛ حيث يشهدها الله وملائكةُ الليلِ وملائكة النهار.
ففي هذه الآية ذكرُ الأوقات الخمسة للصَّلوات المكتوبات، وأن الصَّلوات الموقعة فيه فرائضُ؛ لتخصيصها بالأمر.
وفيها أنَّ الوقت شرطٌ لصحَّة الصلاة، وأنَّه سببٌ لوجوبها؛ لأنَّ الله أمر بإقامتها لهذه الأوقات، وأنَّ الظهر والعصر يُجمعان، والمغرب والعشاء كذلك؛ للعذر؛ لأنَّ الله جمع وقتهما جميعاً.
وفيه فضيلةُ صلاة الفجر، وفضيلة إطالة القراءة فيها، وأنَّ القراءة فيها ركنٌ؛ لأنَّ العبادة إذا سُمِّيت ببعض أجزائها؛ دلَّ على فرضيَّة ذلك.
{78} Yeye Mtukufu anamwamrisha Mtume wake Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kusimamisha Swala kamili, kwa dhahiri na kwa siri katika nyakati zake zilizowekwa, "jua linapopinduka." Yaani, linapoelekea kwenye upeo wa magharibi baada ya kukengeuka kwake. Na inaingia katika hilo swala ya adhuhuri na swala ya alasiri "mpaka giza la usiku." Na inaingia katika hilo swala ya Maghribi na swala ya Ishaa, "Na Qur-rani ya Al-fajiri." Yaani, swala ya alfajiri. Nayo iliitwa Qur-ani kwa sababu inaruhusiwa kurefusha kisomo cha Qur-ani ndani yake kuliko swala zinginezo, na kwa sababu ya fadhila ya kusoma Qur-ani, ambacho Mwenyezi Mungu anakishuhudia, na Malaika wa usiku na Malaika wa mchana. Basi katika Aya hii zimetajwa nyakati tano za swala tano za faradhi zilizoandikwa, na kwamba zinazofanywa nyakati hizo ni faradhi, kwa sababu ya kutajwa hizo tu katika amri hii. Na ndani yake pia kuna kwamba kuingia kwa wakati ni sharti ya swala kuwa sahihi, na kwamba ndiyo sababu ya kuifanya iwe wajibu. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliamuru kuisimamisha katika nyakati hizi. Na ndani yake pia kuna kwamba Adhuhuri na Alasiri huchanganywa pamoja, na Magharibi na Ishaa pia huchanganywa pamoja kama kuna udhuru wa kufanya hivyo. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alijumuisha nyakati zake pamoja. Na ndani yake pia kuna fadhila ya swala ya Alfajiri, na fadhila ya kurefusha kisomo cha Qur-ani ndani yake, na kwamba kusoma Qur-ani ndani yake ni nguzo yake. Kwa sababu ikiwa ibada itaitwa kwa baadhi ya sehemu zake, basi hilo litaonyesha ulazima wa sehemu hiyo.
#
{79} وقوله: {ومن الليل فتهجَّدْ به}؛ أي: صلِّ به في سائر أوقاته، {نافلةً لك}؛ أي: لتكون صلاة الليل زيادةً لك في علوِّ القدر ورفع الدرجات؛ بخلاف غيرك؛ فإنَّها تكون كفَّارة لسيِّئاته. ويُحتمل أن يكون المعنى أنَّ الصلوات الخمس فرضٌ عليك وعلى المؤمنين؛ بخلاف صلاة الليل؛ فإنها فرض عليك بالخصوص؛ لكرامتك على الله أن جَعَلَ وظيفتك أكثر من غيرك، وليكثر ثوابك، وتنال بذلك المقام المحمود، وهو المقام الذي يحمده فيه الأوَّلون والآخرون، مقام الشفاعة العظمى، حين يستشفع الخلائق بآدم ثم بنوح ثم إبراهيم ثم موسى ثم عيسى، وكلُّهم يعتذر ويتأخَّر عنها، حتى يستشفعوا بسيِّد ولد آدم ليرحمهم الله من همِّ الموقف وكربِهِ، فيشفع عند ربِّه، فيشفِّعه ويُقيمه مقاماً يغبطه به الأوَّلون والآخرون، وتكون له المنَّة على جميع الخلق.
{79} Na kauli yake, "Na amka usiku kwa ibada." Yaani, swali katika wakati wake wowote. "Ni ziada ya sunna hasa kwako wewe," ili swala hii ya usiku ikuzidishie utukufu na kunyanyuliwa daraja. Tofauti na wengine, hiyo kwao itakuwa ni kafara ya matendo yao mabaya. Na inawezekana kwamba maana yake ni kwamba swala tano za kila siku ni wajibu kwako na kwa Waumini. Tofauti na swala ya usiku, hiyo ni wajibu kwako tu hasa. Kwa sababu ya utukufu wako mbele ya Mwenyezi Mungu, akaufanya wajibu wako kuwa mkubwa zaidi kuliko wengine, na ili malipo yako yawe mengi, kwa hivyo upate nafasi ya kusifiwa, ambayo ni nafasi ambayo watamsifu kwayo watu wa mwanzo na wa mwisho. Nafasi ya uombezi mkubwa, wakati viumbe vitakapoomba kuombewa msamaha na Adam, kisha Nuhu, kisha Ibrahim, kisha Musa na Isa, na wote watatoa udhuru wa kutoweza kufanya hivyo na asifanye hivyo, mpaka watakapoomba uombezi kwa bwana wa wana wa Adam ambaye ni yeye mtume Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ili Mwenyezi Mungu awarehemu kutokana na wasiwasi kubwa na dhiki ya hali ngumu watakayokuwamo. Kisha atawafanyia uombezi kwa Mola wake Mlezi, naye atakubaliwa uombezi wake na atamsimamisha mahali ambapo wa mwanzo na wa mwisho watamuonea gere, na atakuwa amewasababishia viumbe wote kupata neema kubwa sana.
#
{80} وقوله: {وقل ربِّ أدخِلْني مُدْخَلَ صدقٍ وأخرِجْني مُخْرَجَ صدقٍ}؛ أي: اجعل مداخلي ومخارجي كلَّها في طاعتك وعلى مرضاتك، وذلك لتضمُّنها الإخلاص وموافقته الأمر. {واجعل لي من لدنك سلطاناً نصيراً}؛ أي: حجة ظاهرة وبرهاناً قاطعاً على جميع ما آتيه وما أذره، وهذا أعلى حالة يُنْزِلُها الله العبد، أنْ تكون أحوالُهُ كلُّها خيراً ومقربةً له إلى ربِّه، وأن يكون له على كلِّ حالة من أحواله دليلٌ ظاهرٌ، وذلك متضمِّن للعلم النافع والعمل الصالح للعلم بالمسائل والدلائل.
{80} Na kauli yake,
"Na sema: Mola wangu Mlezi! Niingize muingizo mwema, na unitoe kutoka kwema." Yaani, fanya maingilio yangu yote na matokeo yangu yote yawe katika utiifu kwako na katika radhi zako, kwa sababu kuyafanya kwa kukusudiwa wewe tu na kuafikiana kwake na amri yako. "Na unipe nguvu zinazotoka kwako zinisaidie." Yaani, ni hoja iliyo dhahiri na ushahidi wa yakini kwa kila nifanyacho na nikiachacho. Na hii ndiyo hali ya juu kabisa anayomfikisha Mwenyezi Mungu mja, kwamba hali zake zote ziwe ni heri na zenye kumuweka karibu na Mola wake Mlezi, na kwamba awe na ushahidi dhahiri katika kila hali zake. Na hilo linajumuisha kuwa na elimu yenye manufaa na matendo mema kwa kujua masuala na ushahidi wake.
#
{81} وقوله: {وقل جاء الحقُّ وزَهَقَ الباطل}: والحقُّ هو ما أوحاه الله إلى رسوله محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -، فأمره الله أن يقولَ ويعلِنَ: قد جاء الحقُّ الذي لا يقوم له شيءٌ، وزَهَقَ الباطلُ؛ أي: اضمحل وتلاشى. {إنَّ الباطل كان زَهوقاً}؛ أي: هذا وصف الباطل، ولكنَّه قد يكون له صولةٌ وروجان إذا لم يقابلْه الحقُّ، فعند مجيء الحقِّ؛ يضمحلُّ الباطل فلا يبقى له حراك، ولهذا لا يروج الباطل إلاَّ في الأزمان والأمكنة الخالية من العلم بآيات الله وبيناته. وقوله:
{81} Na kauli yake,
"Na sema: Haki, imefika, na batili imetoweka." Na haki ni yale aliyomfunulia Mwenyezi Mungu Mtume wake Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, -
na akamwamuru kuisema na kuitangaza kwamba: Hakika haki imekuja, ambayo hakuna kitu kinachoweza kusimama mbele yake, na batili imetoweka. Yaani, imeisha na kutoweka. "Hakika batili lazima itoweke!" Yaani, hii ndiyo sifa ya batili. Lakini inaweza kuwa na nguvu na umaarufu ikiwa haki haikabiliani nayo. Na pindi haki inapokuja, batili inatoweka, kwa hivyo haibaki kuwa na harakati yoyote. Na ndiyo maana batili haiwi maarufu isipokuwa katika nyakati fulani tu na maeneo ambayo hayana elimu juu ya ishara za Mwenyezi Mungu na hoja zake zilizo wazi. Na kauli yake,
{وَنُنَزِّلُ مِنَ الْقُرْآنِ مَا هُوَ شِفَاءٌ وَرَحْمَةٌ لِلْمُؤْمِنِينَ وَلَا يَزِيدُ الظَّالِمِينَ إِلَّا خَسَارًا (82)}.
82. Na tunateremsha katika Qur-ani yale ambayo ni uponyaji na rehema kwa Waumini. Wala hayawazidishii madhalimu isipokuwa hasara.
#
{82} فالقرآن مشتملٌ على الشفاء والرحمة، وليس ذلك لكلِّ أحدٍ، وإنَّما ذلك للمؤمنين به المصدِّقين بآياته العالمين به، وأما الظَّالمون بعدم التصديق به أو عدم العمل به؛ فلا تزيدُهم آياته إلا خساراً؛ إذ به تقومُ عليهم الحجَّة؛ فالشفاء الذي تضمنَّه القرآن عامٌّ لشفاء القلوب من الشُّبه والجهالة والآراء الفاسدة والانحراف السيئ والقصود السيئة؛ فإنه مشتملٌ على العلم اليقيني الذي تزول به كلُّ شبهة وجهالة، والوعظ والتذكير الذي يزول به كلُّ شهوة تخالف أمر الله، ولشفاء الأبدان من آلامها وأسقامها، وأما الرحمة؛ فإنَّ ما فيه من الأسباب والوسائل التي يحثُّ عليها متى فعلها العبد، فاز بالرحمة والسعادة الأبديَّة والثواب العاجل والآجل.
{82} Qur-ani inajumuisha uponyaji na rehema, lakini hilo si kwa kila mmoja. Bali ni kwa wale wanaoiamini na kusadiki ishara zake na kuzijua. Na ama madhalimu ambao hawaiamini au hawaifanyi kazi, basi Aya zake haziwazidishi isipokuwa hasara tu. Kwa sababu, kwazo hoja inasimama juu yao. Kwa hivyo, uponyaji ambao Qur-ani imeujumuisha ndani yake ni jumla kwa ajili ya kuponya nyoyo kutokana na fikira potofu, ujinga, maoni potovu, ukengeufu mbaya, na nia mbaya. Kwa maana, inajumuisha elimu ya yakini ambayo kwayo zinaisha kila fikira potofu na ujinga, na yanapatikana mawaidha na ukumbusho ambao kwa hayo yanaisha kila matamanio yanayohalifu amri ya Mwenyezi Mungu. Nayo pia ina uponyaji wa miili kutokana na maumivu yake na maradhi yake. Na ama rehema, kutokana na sababu na njia ambazo inazihimiza, kila wakati mja anapozifanya, anapata rehema, furaha ya milele, na malipo ya haraka na ya baadaye.
{وَإِذَا أَنْعَمْنَا عَلَى الْإِنْسَانِ أَعْرَضَ وَنَأَى بِجَانِبِهِ وَإِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ كَانَ يَئُوسًا (83)}.
83. Na tunapomneemesha mtu, hugeuka na kujitenga kando. Na yanapomgusa maovu, hukata tamaa.
#
{83} هذه طبيعة الإنسان من حيث هو، إلاَّ مَن هداه الله؛ فإنَّ الإنسان عند إنعام الله عليه يفرح بالنِّعم، ويبطَرُ بها، ويعرِضُ، وينأى بجانبِهِ عن ربِّه؛ فلا يشكُرُه، ولا يذكُرُه. {وإذا مسَّه الشرُّ}: كالمرض ونحوه، {كان يؤوساً}: من الخير، قد قطع عن ربِّه رجاءه، وظنَّ أنَّ ما هو فيه دائمٌ أبداً، وأمَّا مَنْ هداه الله؛ فإنَّه عند النعم يخضعُ لربِّه، ويشكر نعمته، وعند الضرَّاء يتضرَّع، ويرجو من الله عافيته وإزالة ما يقعُ فيه، وبذلك يخفُّ عليه البلاء.
{83} Haya ndiyo maumbile ya asili ya mtu kama alivyo, isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu alimuongoa. Kwa maana mtu anaponeemeshwa na Mwenyezi Mungu, hufurahia neema hizo, na huzifanyia kiburi na hukengeuka na kujiweka mbali na Mola wake Mlezi. Hamshukuru, wala hamtaji. "Na yanapomgusa maovu" kama vile maradhi na mengineyo, "Hukata tamaa" ya kupata heri, na akawa amekata matumaini yake kwa Mola wake Mlezi, na akadhani kwamba yale aliyomo yatadumu milele. Na ama yule ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa, yeye wakati anaponeemeshwa, humnyenyekea Mola wake Mlezi na anamshukuru kwa neema zake. Na wakati wa shida, huomba dua kwa unyenyekevu, na kutaraji salama kutoka kwa Mwenyezi Mungu kumuondolea yale yanayompata, na kwa hayo dhiki hiyo inakuwa nyepesi kwake.
{قُلْ كُلٌّ يَعْمَلُ عَلَى شَاكِلَتِهِ فَرَبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَنْ هُوَ أَهْدَى سَبِيلًا (84)}.
84. Sema, "Kila mmoja anafanya kwa namna yake. Na Mola wenu Mlezi ndiye anayejua zaidi yule aliyeongoka katika njia."
#
{84} أي: {قل كُلٌّ}: من الناس، {يعملُ على شاكلتِهِ}؛ أي: على ما يَليق به من الأحوال: إن كانوا من الصفوة الأبرار؛ لم يشاكِلْهم إلا عملهم لربِّ العالمين، ومن كانوا من غيرِهِم من المخذولين؛ لم يناسِبْهم إلاَّ العمل للمخلوقين، ولم يوافِقْهم إلاَّ ما وافق أغراضهم. وربك {أعلم بمن هو أهدى سبيلاً}: فيعلمُ مَنْ يَصْلُحُ للهداية فيهديه، ومن لا يَصْلُحُ لها فيخذله ولا يهديه.
{84} Yaani, "Sema kila mmoja" katika watu, "anafanya kwa namna yake." Yaani, kulingana na hali zinazomfaa; ikiwa ni miongoni mwa watu wema wa hali ya juu, haiwi hali yao isipokuwa kumfanyia matendo Mola Mlezi wa walimwengu wote. Na ama wale wengineo, miongoni mwa walioachiliwa mbali, basi haiwafailii isipokuwa kuwafanyia matendo viumbe, na hawawezeshwi isipokuwa yale yalioafikiana na malengo yao. Na Mola wako Mlezi "ndiye anayejua zaidi yule aliyeongoka katika njia." Anamjua anayefaa kuongoka, na anamuongoa, na yule asiyeufailia, na humuachilia mbali na wala hamuongoi.
{وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي وَمَا أُوتِيتُمْ مِنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا (85)}
85. Na wanakuuliza habari za Roho. Sema, "Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika elimu isipokuwa kidogo tu."
#
{85} وهذا متضمِّن لردع من يسأل المسائل التي لا يُقْصَدُ بها إلاَّ التعنُّت والتَّعجيز، ويدع السؤال عن المهمِّ، فيسألون عن الرُّوح التي هي من الأمور الخفيَّة التي لا يتقنُ وصفها وكيفيتها كلُّ أحدٍ، وهم قاصرون في العلم الذي يحتاجُ إليه العباد، ولهذا أمر الله رسوله أن يُجيبَ سؤالهم بقوله: {قل الرُّوحُ من أمر ربِّي}؛ أي: من جملة مخلوقاته التي أمرها أن تكونَ فكانَتْ، فليس في السؤال عنها كبيرُ فائدةٍ مع عدم علمِكُم بغيرها.
وفي هذه الآية دليلٌ على أنَّ المسؤول إذا سُئِلَ عن أمرٍ، الأَوْلَى بالسائل غيره أنْ يعرِضَ عن جوابه، ويدلَّه على ما يحتاجُ إليه، ويرشِدَه إلى ما ينفعه.
{85} Hili linajumusiha kumkomesha mwenye kuuliza maswali ambayo hayakusudiwi kwayo isipokuwa ukaidi na kutaka kumshinda aliyeulizwa, na akaacha kuuliza yaliyo muhimu. Hao waliuliza kuhusu roho, ambayo ni katika mambo yaliyofichika ambayo kila mmoja hawezi kuielezea namna ilivyo kihalisia, ilhali hata wana upungufu mkubwa katika elimu wanayohitaji waja kuijua. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake kulijibu swali lao kwa kauli yake,
“Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi.” Yaani, ni katika jumla ya viumbe vyake aliowaamrisha wawe, na ikawa. Basi hakuna faida kubwa katika kuuliza juu yake, pamoja na kutojua kwenu mengineyo. Na Aya hii ina ushahidi kwamba anayeulizwa akiulizwa kuhusu jambo ambalo ilikuwa bora kwa mtu kuuliza juu ya jambo linginelo, basi na ampuuze wala asimjibu, na amuelekeze kwenye yale anayoyahitaji, na amuongoze katika yale yatakayomnufaisha.
{وَلَئِنْ شِئْنَا لَنَذْهَبَنَّ بِالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ ثُمَّ لَا تَجِدُ لَكَ بِهِ عَلَيْنَا وَكِيلًا (86) إِلَّا رَحْمَةً مِنْ رَبِّكَ إِنَّ فَضْلَهُ كَانَ عَلَيْكَ كَبِيرًا (87)}
86. Na tungelipenda, tungeliyaondoa yale tuliyokufunulia. Kisha usingelipata mwakilishi wa kukupigania kwetu kwa haya. 87. Isipokuwa iwe rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika fadhila yake kwako ni kubwa.
#
{86 - 87} يخبر تعالى أنَّ القرآن والوحي الذي أوحاه إلى رسوله رحمةٌ منه عليه وعلى عبادِهِ، وهو أكبر النعم على الإطلاق على رسوله؛ فإنَّ فضل الله عليه كبيرٌ لا يقادَرُ قدرُهُ؛ فالذي تفضَّل به عليك قادرٌ على أن يَذْهَبَ به ثم لا تجِدُ رادًّا يردُّه ولا وكيلاً يتوجَّه عند الله فيه؛ فَلْتَغْتَبِطْ به وتَقَرَّ به عينُك، ولا يحزنك تكذيبُ المكذبين واستهزاءُ الضالين؛ فإنَّهم عرضت عليهم أجلُّ النعم فردُّوها لهوانهم على الله وخِذْلانِهِ لهم.
{86 - 87} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba Qur-ani na wahyi ambao uliteremshwa kwa Mtume wake ni rehema kutoka kwake na juu ya waja wake, na ndiyo neema kubwa kuliko zote kwa Mtume wake. Kwa maana, neema ya Mwenyezi Mungu juu yake ni kubwa na haiwezi kupimwa kiasi chake. Basi yule aliyekuneemesha kwazo ana uwezo wa kuiondoa, kisha huwezi kutapata wa kurudisha anayeweza kuirudisha wala mwakilishi mwenye kumuelekeza kwa Mwenyezi Mungu kuhusiana nayo. Basi lifurahie hilo na jicho lako liburudike kwalo, wala usihuzunishwe na kukadhibisha kwa wanaokadhibisha, na stihizai ya wapotovu. Kwa maana, walipewa neema kubwa zaidi lakini wakazikataa kwa sababu ya uduni wao kwa Mwenyezi Mungu na kuwaachilia mbali kwake.
{قُلْ لَئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنْسُ وَالْجِنُّ عَلَى أَنْ يَأْتُوا بِمِثْلِ هَذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا (88)}.
88.
Sema: Wangelikusanyika watu na majini ili walete mfano wa Qur-ani hii, basi hawawezi kuleta mfano wake, hata kama wakisaidiana wao kwa wao.
#
{88} وهذا دليلٌ قاطعٌ وبرهانٌ ساطعٌ على صحَّة ما جاء به الرسول وصدقه؛ حيث تحدَّى الله الإنس والجنَّ أن يأتوا بمثله، وأخبر أنهم لا يأتون بمثله، ولو تعاونوا كلُّهم على ذلك؛ لم يقدِروا عليه، ووقع كما أخبر اللهُ؛ فإنَّ دواعي أعدائه المكذِّبين به متوفِّرة على ردِّ ما جاء به بأيِّ وجهٍ كان، وهُمْ أهلُ اللسان والفصاحة؛ فلو كان عندَهم أدنى تأهُّل وتمكُّن من ذلك؛ لفعلوه، فعُلِمَ بذلك أنهم أذعنوا غاية الإذعان طوعاً وكرهاً، وعَجَزوا عن معارضتِهِ، وكيف يقدِرُ المخلوق من ترابٍ، الناقصُ من جميع الوجوه، الذي ليس له علمٌ ولا قدرةٌ ولا إرادةٌ ولا مشيئةٌ ولا كلامٌ ولا كمالٌ إلاَّ من ربِّه؛ أن يعارِضَ كلامَ ربِّ الأرض والسماوات، المطَّلع على سائر الخفيَّات، الذي له الكمالُ المطلقُ والحمدُ المطلقُ والمجدُ العظيمُ، الذي لو أنَّ البحر يمدُّه من بعده سبعةُ أبحر مداداً والأشجارَ كلَّها أقلامٌ؛ لَنَفِدَ المداد وفنيتِ الأقلام ولم تَنْفَدْ كلماتُ الله؛ فكما أنَّه ليس أحدٌ من المخلوقين مماثلاً لله في أوصافه؛ فكلامُهُ من أوصافه التي لا يماثِلُه فيها أحدٌ؛ فليس كمثلِهِ شيءٌ في ذاتِهِ وأسمائِهِ وصفاتِهِ وأفعالِهِ تبارك وتعالى؛ فتبًّا لمن اشتبه عليه كلامُ الخالق بكلام المخلوقِ، وزعم أنَّ محمداً - صلى الله عليه وسلم - افتراه على الله، واختلقه من نفسه.
{88} Na huu ni ushahidi wa uhakika na hoja ya wazi juu ya usahihi na ukweli wa yale aliyoyaleta Mtume, ambapo Mwenyezi Mungu aliwapa changamoto wanadamu na majini walete kitu mfano wake, na akawaambia kwamba hawatatoa mfano wake, hata kama wangesaidiana wote katika kufanya hivyo, basi hawangeweza kufanya hivyo, na kweli ikawa kama Mwenyezi Mungu alivyojulisha. Kwani sababu za maadui zake wanaomkadhibisha zilipatikana ili kukanusha kwa njia yoyote ile yale aliyoyaleta, nao ni watu wa lugha hiyo wenye ufasaha mkubwa. Na ikiwa wangekuwa wamejiandaa na uwezo mdogo zaidi wa kufanya hivyo, wangelifanya hivyo. Kwa hivyo ikajulikana kwa hilo kwamba walijisalimisha kabisa kwa hiari na kwa kutopenda, na wakashindwa kuipinga. Na vipi anaweza kiumbe kilichoumbwa kwa udongo, chenye upungufu kwa kila namna, kisicho na elimu, uwezo, wala utashi wala kupenda wala uwezo wa kuzungumza wala ukamilifu isipokuwa kutoka kwa Mola wake Mlezi kupinga maneno ya Mola Mlezi wa ardhi na mbingu, ambaye anajua kila kitu kilichofichika, ambaye ni wake ukamilifu wote, sifa njema zote, na utukufu mkubwa, ambaye, kama angeongeza juu yake bahari nyingine saba zikawa ni wino, nayo miti yote ikawa kalamu, basi wino huo ungeisha, na kalamu hizo zikaisha, na maneno ya Mwenyezi Mungu hayangeisha. Kwa hivyo, kama vile hakuna kiumbe chochote kinachofanana na Mwenyezi Mungu katika sifa zake, basi maneno yake ni katika sifa zake ambazo hakuna yeyote anayelingana naye katika hayo. Kwani hakuna kitu kama mfano wake katika dhati yake, majina yake, sifa zake, vitendo vyake, Yeye mwingi wa baraka, Mtukufu. Basi laana iwe juu ya mwenye kuchanganyikiwa kuhusiana na maneno ya Muumba na maneno ya viumbe, na akadai kuwa Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alimzulia Mwenyezi Mungu uongo, na akayasema hayo yeye mwenyewe tu.
{وَلَقَدْ صَرَّفْنَا لِلنَّاسِ فِي هَذَا الْقُرْآنِ مِنْ كُلِّ مَثَلٍ فَأَبَى أَكْثَرُ النَّاسِ إِلَّا كُفُورًا (89) وَقَالُوا لَنْ نُؤْمِنَ لَكَ حَتَّى تَفْجُرَ لَنَا مِنَ الْأَرْضِ يَنْبُوعًا (90) أَوْ تَكُونَ لَكَ جَنَّةٌ مِنْ نَخِيلٍ وَعِنَبٍ فَتُفَجِّرَ الْأَنْهَارَ خِلَالَهَا تَفْجِيرًا (91) أَوْ تُسْقِطَ السَّمَاءَ كَمَا زَعَمْتَ عَلَيْنَا كِسَفًا أَوْ تَأْتِيَ بِاللَّهِ وَالْمَلَائِكَةِ قَبِيلًا (92) أَوْ يَكُونَ لَكَ بَيْتٌ مِنْ زُخْرُفٍ أَوْ تَرْقَى فِي السَّمَاءِ وَلَنْ نُؤْمِنَ لِرُقِيِّكَ حَتَّى تُنَزِّلَ عَلَيْنَا كِتَابًا نَقْرَؤُهُ قُلْ سُبْحَانَ رَبِّي هَلْ كُنْتُ إِلَّا بَشَرًا رَسُولًا (93) وَمَا مَنَعَ النَّاسَ أَنْ يُؤْمِنُوا إِذْ جَاءَهُمُ الْهُدَى إِلَّا أَنْ قَالُوا أَبَعَثَ اللَّهُ بَشَرًا رَسُولًا (94) قُلْ لَوْ كَانَ فِي الْأَرْضِ مَلَائِكَةٌ يَمْشُونَ مُطْمَئِنِّينَ لَنَزَّلْنَا عَلَيْهِمْ مِنَ السَّمَاءِ مَلَكًا رَسُولًا (95) قُلْ كَفَى بِاللَّهِ شَهِيدًا بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ إِنَّهُ كَانَ بِعِبَادِهِ خَبِيرًا بَصِيرًا (96)}.
89. Na hakika tumewaeleza watu katika Qur-ani hii kwa kila mfano. Lakini wengi wa watu wakakataa isipokuwa kukufuru tu. 90. Na walisema, "Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemchemi katika ardhi hii." 91. Au uwe na bustani ya mitende na mizabibu, na utupitishie mito kati yake ikimiminika. 92. Au utuangushie mbingu vipande vipande kama ulivyodai, au utuletee Mwenyezi Mungu na Malaika uso kwa uso. 93. Au uwe na nyumba iliyopambwa, au upae mbinguni. Wala hatutaamini kupaa kwako huko mpaka ututeremshie kitabu tukisome. Sema, "Subhana Rabbi
(Ametakasika Mola wangu Mlezi)! Kwani mimi ni nani isipokuwa ni mtu tu na Mtume? 94. Na hakikuwazuilia watu kuamini ulipowajia uwongofu isipokuwa ni kwamba walisema, "Je, mwenyezi Mungu alimtuma mtu kuwa ni Mtume?" 95. Sema, "Ingelikuwa katika ardhi wapo Malaika wanatembea kwa utulivu wao, basi bila ya shaka tungeliwateremshia Malaika kuwa ni Mtume wao." 96. Sema, "Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi baina yangu na nyinyi. Hakika Yeye ana habari zote za waja wake na anawaona vyema."
#
{89 - 93} يقول تعالى: {ولقد صرَّفْنا للناس في هذا القرآن من كلِّ مثل}؛ أي: نوَّعنا فيه المواعظ والأمثال، وثنَّيْنا فيه المعاني التي يضطرُّ إليها العبادُ لأجل أن يتذكَّروا ويتَّقوا، فلم يتذكَّر إلا القليلُ منهم، الذين سبقت لهم من الله سابقةُ السعادة، وأعانهم الله بتوفيقه، وأما أكثر الناس؛ فأبَوْا إلا كُفوراً لهذه النعمة التي هي أكبرُ من جميع النعم، وجعلوا يتعنَّتون عليه آياتٍ غيرَ آياتِهِ يخترِعونها من تِلقاء أنفسهم الظالمة الجاهلة، فيقولون لرسول الله - صلى الله عليه وسلم - الذي أتى بهذا القرآن المشتمل على كل برهان وآية: {لن نؤمنَ لك حتَّى تَفْجُرَ لنا من الأرض يَنبوعاً}؛ أي: أنهاراً جاريةً، {أو تكونَ لك جنَّةٌ من نخيل وعنبٍ}: فتستغني بها عن المشي في الأسواق والذَّهاب والمجيء، {أو تُسْقِطَ السماء كما زَعَمْتَ علينا كِسَفاً}؛ أي: قطعاً من العذاب، {أو تأتيَ بالله والملائكةِ قَبيلاً}؛ أي؛ جميعاً أو مقابلةً ومعاينةً يشهدون لك بما جئت به، {أو يكونَ لك بيتٌ من زخرفٍ}؛ أي: مزخرف بالذهب وغيره، {أو تَرْقى في السماء}: رُقِيًّا حسيًّا. {و} مع هذا فلن {نؤمنَ لِرُقِيِّكَ حتى تنزِّلَ علينا كتاباً نقرَؤه}. ولما كانتْ هذه تعنُّتات وتعجيزات وكلام أسفه الناس وأظلمهم، المتضمِّنة لردِّ الحقِّ وسوء أدبٍ مع الله، وأن الرسول - صلى الله عليه وسلم - هو الذي يأتي بالآيات؛ أمره الله أن ينزِّهَهُ، فقال: {قل سبحانَ ربِّي}: عمَّا تقولون علواً كبيراً، وسبحانه أن تكونَ أحكامُهُ وآياتُهُ تابعةً لأهوائهم الفاسدة وآرائهم الضالَّة. {هل كنتُ إلاَّ بشراً رسولاً}: ليس بيده شيء من الأمر.
{89-93} Yeye Mtukufu anasema, "Na hakika tumewaeleza watu katika Qur-ani hii kwa kila mfano." Yaani, tumeeleza ndani yake aina mbalimbali za mawaidha na mifano, na tumerudiarudia humo maana ambazo waja wanazihitaji ili wazikumbuke na kumcha Mungu, lakini hawakukumbuka isipokuwa wachache tu miongoni mwao, wale ambao walikwisha andikiwa na Mwenyezi Mungu kwamba watakuwa wenye furaha, na Mwenyezi Mungu akawasaidia kwa kuwawezesha kufikia hayo. Ama wengi wa watu, hao walikataa isipokuwa kukufuru neema hii ambayo ndiyo kubwa zaidi kuliko neema zote, na wakaanza kumfanyia ukaidi kwa kutaka ishara zisizokuwa ishara zake, ambazo wanazizua kwa nafsi zao dhalimu zisizojua kitu. Wakamwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ambaye alikuja na Qur-ani hii yenye kila hoja na ishara, "Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemchemi katika ardhi hii." Yaani, mito itiririkayo. "Au uwe na bustani ya mitende na mizabibu," ikawa inakutosheleza kwenda na kurudi sokoni. "Au utuangushie mbingu vipande vipande kama ulivyodai." Yaani, kipande cha adhabu. "Au utuletee Mwenyezi Mungu na Malaika uso kwa uso," ili wakushuhudilie hayo uliyokuja nayo. "Au uwe na nyumba iliyopambwa" kwa dhahabu na vitu vingine. "Au upae mbinguni" kwa mwili wako. "Na" pamoja na haya, "hatutaamini kupaa kwako huko mpaka ututeremshie kitabu tukisome." Na kwa kuwa haya ni ukaidi, na kutaka kumfanya Mwenyezi Mungu kana kwamba hana uwezo, na ni maneno ambayo husemwa na watu wajinga zaidi na madhalimu zaidi, ambayo yanajumuisha kukataa haki na kuwa na tabia mbaya mbele ya Mwenyezi Mungu, na kwamba Mtume -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - ndiye anayeleta tu ishara. Mwenyezi Mungu akamwamrisha amtakase, akasema,
"Sema: Ametakasika Mola wangu Mlezi," kutokana na hayo mnayoyasema na yuko juu sana. Na ametakasika kutokana kwamba hukumu zake na ishara zake zifuatane na matamanio yao mabovu na rai zao potovu. "Je, kwani mimi ni nani isipokuwa ni mtu tu na Mtume," ambaye hana chochote mkononi mwake katika jambo hili?
#
{94} وهذا السبب الذي منع أكثر الناس من الإيمان؛ حيث كانت الرسل التي تُرْسَلُ إليهم من جنسهم بشراً، وهذا من رحمته بهم أن أرسل إليهم بشراً منهم؛ فإنَّهم لا يطيقون التلقي من الملائكة.
{94} Na hii ndiyo sababu iliyowazuia wengi wa watu kuamini. Ambapo Mitume waliotumiwa wao walikuwa ni watu wa aina zao, na hii ni katika rehema yake kwao kwamba aliwatumia watu kutoka miongoni mwao. Kwa maana, hawawezi kustahimili kupokea kutoka kwa malaika.
#
{95} فلو {كانَ في الأرض ملائكةٌ يمشونَ مطمئنِّين}: يَثْبُتون على رؤية الملائكة والتلقيِّ عنهم؛ {لَنَزَّلْنا عليهم من السماءِ مَلَكاً رسولاً}: ليمكِنَهم التلقي عنه.
{95} Na "Ingelikuwa katika ardhi wapo Malaika wanatembea kwa utulivu wao;" nao wanaweza kubaki madhubuti katika kuwaona na kupokea kutoka kwa Malaika, "Basi bila ya shaka tungeliwateremshia Malaika kuwa ni Mtume wao," ili waweze kupokea kutoka kwake.
#
{96} {قل كفى بالله شهيداً بيني وبينكم إنَّه كان بعبادِهِ خبيراً بصيراً}: فمن شهادتِهِ لرسولِهِ ما أيَّدَه به من المعجزات، وما أنزل عليه من الآيات، ونصره على مَنْ عاداه وناوأه؛ فلو تقوَّل عليه بعض الأقاويل؛ لأخَذَ منه باليمين، ثم لقطع منه الوتينَ؛ فإنَّه خبيرٌ بصيرٌ، لا تخفى عليه من أحوال العبادِ خافيةٌ.
{96} "Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi. Hakika Yeye ana habari zote za waja wake na anawaona vyema." Na katika ushahidi wake kwa Mtume wake ni miujiza aliyomsaidia nayo na Aya alizomteremshia, na nusura aliyompa dhidi ya wale waliomkaidi na kumfanyia uadui. Na lau kama angelimzulia baadhi ya maneno tu. Basi bila ya shaka angelimshika kwa mkono wa kulia. Kisha kwa hakika angelimkata mshipa mkubwa wa moyo! Kwani Yeye ni Mwenye habari zote, Mwenye kuona vyema, na hakuna chenye kufichika chochote kinachofichikana kwake kuhusu hali za waja wake.
{وَمَنْ يَهْدِ اللَّهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِ وَمَنْ يُضْلِلْ فَلَنْ تَجِدَ لَهُمْ أَوْلِيَاءَ مِنْ دُونِهِ وَنَحْشُرُهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَى وُجُوهِهِمْ عُمْيًا وَبُكْمًا وَصُمًّا مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ كُلَّمَا خَبَتْ زِدْنَاهُمْ سَعِيرًا (97) ذَلِكَ جَزَاؤُهُمْ بِأَنَّهُمْ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا وَقَالُوا أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا وَرُفَاتًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ خَلْقًا جَدِيدًا (98) أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّهَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ قَادِرٌ عَلَى أَنْ يَخْلُقَ مِثْلَهُمْ وَجَعَلَ لَهُمْ أَجَلًا لَا رَيْبَ فِيهِ فَأَبَى الظَّالِمُونَ إِلَّا كُفُورًا (99) قُلْ لَوْ أَنْتُمْ تَمْلِكُونَ خَزَائِنَ رَحْمَةِ رَبِّي إِذًا لَأَمْسَكْتُمْ خَشْيَةَ الْإِنْفَاقِ وَكَانَ الْإِنْسَانُ قَتُورًا (100)}.
97. Na yule ambaye Mwenyezi Mungu anamuongoa, basi huyo ndiye aliyeongoka. Na yule ambaye anampotoa, basi hutawapatia walinzi wowote badala yake. Na tutawakusanya Siku ya Qiyama hali ya kuwa wanakokotwa juu ya nyuso zao, huku ni vipofu, mabubu, na viziwi. Na makazi yao ni Jahannamu. Kila ukifanya kuzimika, tutazidi kuuchochea uwake kwa nguvu. 98. Hayo ni malipo yao kwa sababu walizikataa ishara zetu,
na wakasema: Hivyo tukisha kuwa mifupa na mapande yaliyovurugika tutafufuliwa kwa umbo jipya? 99. Kwani hawakuona ya kwamba Mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na ardhi ni Mwenye kuweza kuumba mfano wao? Na Yeye amewawekea muda usio na shaka yoyote. Lakini madhalimu walikataa isipokuwa kukufuru tu. 100. Sema, "Lau kuwa nyinyi mnazimiliki hazina za rehema za Mola wangu Mlezi, basi hapana shaka mngelizuia kwa sababu ya kuhofu kuzitumia. Na mtu tangu hapo tabia yake ni mchoyo mno!
#
{97} يخبر تعالى أنَّه المنفرد بالهداية والإضلال؛ فمن يهدِهِ فييسِّره لليسرى ويجنِّبه العسرى؛ فهو المهتدي على الحقيقة، ومن يُضْلِلْه فيخذله ويَكِله إلى نفسه: فلا هادي له من دون الله، وليس له وليٌّ ينصره من عذاب الله حين يحشُرُهم الله على وجوهِهِم، خزياً عُمياً وبُكماً، لا يبصرون، ولا ينطقون. {مأواهم}؛ أي: مقرُّهم ودارهم {جهنَّمُ}: التي جمعت كلَّ همٍّ وغمٍّ وعذابٍ. {كلَّما خَبَتْ}؛ أي: تهيّأت للانطفاء، {زِدْناهم سعيراً}؛ أي: سَعَّرْناها بهم، لا يُفَتَّرُ عنهم العذابُ، ولا يُقضى عليهم فيموتوا، ولا يخفف عنهم من عذابها.
{97} Yeye aliyetukuka anajulisha kwamba Yeye ndiye Pekee mwenye kuongoa na kupotosha. Kwa hivyo, yeyote ambaye yeye atamuongoa na akamrahisishia yakawa mepesi na akamuepusha na ugumu, basi kwa hakika huyo ndiye aliyeongoka. Na yule ambaye yeye atampotosha na akamuachilia mbali, na kumuachia nafsi yake, basi hana yeyote wa kumwongoa kando na Mwenyezi Mungu, na wala hana mlinzi yeyote wa kumuokoa kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu wakati atakapowakusanya juu ya nyuso zao huku wamehizika, ni vipofu na mabubu, hawaoni wala hawasemi. "Na makazi yao ni Jahannamu," ambayo imekusanya kila wasiwasi kubwa, dhiki na adhabu. "Kila ukifanya kuzimika, tutazidi kuuchochea uwake kwa nguvu," wala hawatapumzishwa na adhabu hiyo, wala hawatahukumiwa ili wafe, wala hawatapunguziwa adhabu yake.
#
{98} ولم يظلِمْهم الله تعالى، بل جازاهم بما كفروا بآياته وأنكروا البعثَ الذي أخبرت به الرُّسل، ونطقتْ به الكتب، وعجَّزوا ربَّهم؛ فأنكروا تمام قدرته، {وقالوا أإذا كنَّا عظامًا ورُفاتاً أإنَّا لَمَبْعوثونَ خلقاً جديداً}؛ أي: لا يكون هذا؛ لأنَّه في غاية البعد عند عقولهم الفاسدة.
{98} Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, bali aliwalipa kwa sababu ya kuzikufuru kwao Aya zake, na wakapinga ufufuo waliojulishwa na mitume wao, na vitabu vilivyozungumza kuuhusu, na wakamfanya Mola wao Mlezi kana kwamba hawezi kitu, na wakapinga ukamilifu wa uwezo wake.
"Na wakasema: Hivyo tukisha kuwa mifupa na mapande yaliyovurugika tutafufuliwa kwa umbo jipya?" Yaani, hili halitakuwa. Kwa sababu ndilo lisolowezekana kabisa kulingana na akili zao potovu.
#
{99} {أوَلَمْ يَرَوْا أنَّ الله الذي خلق السمواتِ والأرض}: وهي أكبر من خلق الناس، {قادرٌ على أن يَخْلُقَ مثلَهم}: بلى إنَّه على ذلك قدير. {و} لكنه قد جَعَلَ لذلك {أجلاً لا رَيْبَ فِيهِ}: ولا شكَّ وإلا فلو شاء لجاءهم به بغتة ومع إقامته الحجج والأدلة على البعث؛ {فأبى الظَّالمونَ إلاَّ كُفوراً}: ظُلْماً منهم وافتراءً.
{99} "Kwani hawakuona ya kwamba Mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na ardhi" ambazo ni kubwa zaidi kuliko kuumbwa kwa watu, "Ni Mwenye kuweza kuumba mfano wao?" Hakika Yeye ni Muweza wa hayo. "Na" lakini ameliwekea hilo "muda usio na shaka yoyote." Na lau si hivyo, basi angelitaka, angeliwaletea kwa ghafla. Na pamoja na kwamba alikwisha simamisha hoja na ushahidi juu ya ufufuo. "Lakini madhalimu walikataa isipokuwa kukufuru tu" kwa dhuluma na uzushi.
#
{100} {قل لو أنتم تملِكونَ خزائنَ رحمةِ ربِّي}: التي لا تَنْفَدُ ولا تبيد، {إذاً لأمْسَكْتم خشية الإنفاق}؛ أي: خشية أن يَنْفَدَ ما تنفِقون منه، مع أنَّه من المحال أن تَنْفَدَ خزائنُ الله، ولكنَّ الإنسان مطبوعٌ على الشحِّ والبخل.
{100} "Sema: Lau kuwa nyinyi mnazimiliki hazina za rehema za Mola wangu Mlezi" ambazo haziishi wala hazitoweki, "Basi hapana shaka mngelizuia kwa sababu ya kuhofu kuzitumia." Pamoja na kwamba haiwezekani kwa hazina za Mwenyezi Mungu kuisha, lakini mtu ameumbwa mwenye uchoyo na ubahili.
{وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى تِسْعَ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ فَاسْأَلْ بَنِي إِسْرَائِيلَ إِذْ جَاءَهُمْ فَقَالَ لَهُ فِرْعَوْنُ إِنِّي لَأَظُنُّكَ يَامُوسَى مَسْحُورًا (101) قَالَ لَقَدْ عَلِمْتَ مَا أَنْزَلَ هَؤُلَاءِ إِلَّا رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ بَصَائِرَ وَإِنِّي لَأَظُنُّكَ يَافِرْعَوْنُ مَثْبُورًا (102) فَأَرَادَ أَنْ يَسْتَفِزَّهُمْ مِنَ الْأَرْضِ فَأَغْرَقْنَاهُ وَمَنْ مَعَهُ جَمِيعًا (103) وَقُلْنَا مِنْ بَعْدِهِ لِبَنِي إِسْرَائِيلَ اسْكُنُوا الْأَرْضَ فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ جِئْنَا بِكُمْ لَفِيفًا (104)}.
101. Na kwa yakini tulimpa Musa ishara tisa zilizo wazi. Basi waulize Wana wa Israili alipowafikia, na Firauni akamwaambia, "Hakika mimi ninakuona wewe Musa umerogwa!" 102. Musa akasema, "Wewe unajua bila ya shaka kuwa haya hakuyateremsha isipokuwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ili kuwa ni ushahidi wa kuonekana. Na hakika mimi bila ya shaka nakuona wewe, Firauni, kuwa utaangamizwa." 103. Basi Firauni akataka kuwafukuza katika nchi. Kwa hivyo tukamzamisha yeye na wale waliokuwa pamoja naye wote. 104. Na tukawaambia baada yake Wana wa Israili, "Kaeni katika nchi. Na itapokuja ahadi ya Akhera, tutawaleta nyote pamoja."
#
{101} أي: لستَ أيُّها الرسول المؤيَّد بالآيات أولَ رسول كذَّبه الناس؛ فلقد أرسلْنا قبلَكَ موسى بن عمران الكليم إلى فرعون وقومِهِ وَآتيناه {تسعَ آياتٍ بيِّناتٍ}: كلُّ واحدة منها تكفي لمن قصدُهُ اتِّباع الحقِّ كالحيَّة والعصا والطُّوفان والجرادِ والقُمَّل والضفادع والدَّم والرجز وفلق البحر؛ فإنْ شككتَ في شيء من ذلك؛ {فاسألْ بني إسرائيلَ إذْ جاءَهم فقال له فرعونُ}: مع هذه الآيات: {إني لأظنُّك يا موسى مسحوراً}.
{101} Yaani: Wewe, ewe Mtume unayeungwa mkono na ishara mbalimbali, si Mtume wa kwanza ambaye watu walimkadhibisha; Hakika kabla yako tulimtuma Musa bin Imran aliyezungumza moja kwa moja na Mwenyezi Mungu aende kwa Firauni na watu wake, na tukampa, "Ishara tisa zilizo wazi." Kila mojawapo yake ilikuwa inatosha kwa mwenye kukusudia kufuata haki, kama vile nyoka, fimbo, gharika, nzige, chawa, vyura, damu, adhabu na kuipasua baharini. Kwa hivyo, ikiwa una shaka yoyote juu ya chochote miongoni mwa haya, "Basi waulize wana wa Israili alipowafikia, na Firauni akamwaambia" pamoja na ishara hizi "Hakika mimi ninakuona wewe Musa umerogwa!"
#
{102} فَـ {قَالَ} له موسى: {لقد علمتَ}: يا فرعونُ، {ما أنزلَ هؤلاء}: الآيات. {إلاَّ ربُّ السمواتِ والأرضِ بصائرَ}: منه لعباده؛ فليس قولُكَ هذا بالحقيقة، وإنَّما قلت ذلك ترويجاً على قومك واستخفافاً لهم. {وإنِّي لأظنُّك يا فرعونُ مَثْبوراً}؛ أي: ممقوتاً، مُلْقىً في العذاب، لك الويل والذمُّ واللعنة.
102} Na "Akasema" Musa akimwambia, "Wewe unajua bila ya shaka" ewe Firauni, "kuwa haya hakuyateremsha;" yaani, ishara hizi "isipokuwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ili kuwa ni ushahidi wa kuonekana," kutoka kwake kuwajia waja wake. Kauli yako hii si ya kweli, bali ulisema hivyo ili kuwachochea kaumu yako na kuwadharau. "Na hakika mimi ninaona kuwa wewe, ewe Firauni, kuwa utaangamizwa" na kutupwa katika adhabu, kwa kuwa utakuwa na adhabu kali, shutuma, na laana.
#
{103 - 104} {فأراد}: فرعون {أن يَسْتَفِزَّهم من الأرضِ}؛ أي: يُجْلِيَهم ويخرِجَهم منها، {فأغْرَقْناه ومن معه جميعاً}: وأورثنا بني إسرائيل أرضَهم وديارهم، ولهذا قال: {وقُلْنا من بعدِهِ لبني إسرائيلَ اسكُنوا الأرضَ فإذا جاء وعْدُ الآخرة جئنا بكم لفيفاً}؛ أي: جميعاً؛ لِيُجازِي كلَّ عامل بعمله.
{103-104} "Basi akataka" Firauni "kuwafukuza katika nchi. Kwa hivyo tukamzamisha yeye na wale waliokuwa pamoja naye wote." Na tukawarithisha Wana wa Israili ardhi yao na makazi yao. Na ndiyo maana akasema,
"Na tukawaambia baada yake Wana wa Israili: Kaeni katika nchi. Na itakapokuja ahadi ya Akhera, tutawaleta nyote pamoja," ili kila mtendaji alipwe kwa matendo yake.
{وَبِالْحَقِّ أَنْزَلْنَاهُ وَبِالْحَقِّ نَزَلَ وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا مُبَشِّرًا وَنَذِيرًا (105)}.
105. Na kwa Haki tumeiteremsha, na kwa Haki imeteremka. Na hatukukutuma isipokuwa uwe mbashiri na mwonyaji.
#
{105} أي: وبالحقِّ أنزلنا هذا القرآن الكريم لأمر العبادِ ونهيهم وثوابهم وعقابهم، {وبالحقِّ نزل}؛ أي: بالصدق والعدل والحفظ من كلِّ شيطان رجيم. {وما أرْسَلْناك إلاَّ مبشِّراً}: من أطاع الله بالثواب العاجل والآجل، {ونَذيراً}: لمن عصى الله بالعقاب العاجل والآجل، ويلزم من ذلك بيانُ ما يبشِّر به وينذر.
{105} Yaani, tumeiteremsha Qur-ani hii Tukufu kwa haki ili kuwaamrisha waja na kuwakataza, na kuwalipa thawabu na kuwaadhibu. "Na kwa haki imeteremka." Yaani, kwa ukweli, uadilifu, na huku imehifadhiwa kutoka na kila shetani aliyelaaniwa. "Na hatukukutuma isipokuwa uwe mbashiri" kwa anayemtii Mwenyezi Mungu kwa malipo ya thawabu za haraka na za baadaye hapa duniani na Akhera. "Na mwonyaji" kwa anayemuasi Mwenyezi Mungu kwa adhabu ya haraka na ya baadaye. Na hayo yanalazimu abainishe yale anayoleta bishara njema juu yake, na yale anayoonya dhidi yake.
{وَقُرْآنًا فَرَقْنَاهُ لِتَقْرَأَهُ عَلَى النَّاسِ عَلَى مُكْثٍ وَنَزَّلْنَاهُ تَنْزِيلًا (106) قُلْ آمِنُوا بِهِ أَوْ لَا تُؤْمِنُوا إِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ مِنْ قَبْلِهِ إِذَا يُتْلَى عَلَيْهِمْ يَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ سُجَّدًا (107) وَيَقُولُونَ سُبْحَانَ رَبِّنَا إِنْ كَانَ وَعْدُ رَبِّنَا لَمَفْعُولًا (108) وَيَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ يَبْكُونَ وَيَزِيدُهُمْ خُشُوعًا (109)}.
106. Na Qur-ani tumeigawanya sehemu mbalimbali ili uwasomee watu kwa kituo, na tumeiteremsha kidogo kidogo. 107. Sema, "Iaminini au msiiamini. Hakika wale waliopewa elimu kabla yake, wanaposomewa hii, huanguka kifudifudi wanasujudu. 108. "Na wanasema, 'Subhana Rabbina
(Ametakasika Mola wetu Mlezi)! Hakika ahadi ya Mola wetu Mlezi lazima itimizwe!' 109. "Na huanguka kifudifudi na huku wanalia, na inawazidisha unyenyekevu."
#
{106} أي: وأنزلنا هذا القرآن مفرَّفاً فارِقاً بين الهدى والضَّلال والحقِّ والباطل؛ {لتقرأه على الناس على مكث}؛ أي: على مَهْل؛ ليتدبَّروه، ويتفكَّروا في معانيه ويستخرجوا علومَه، {ونزَّلْناه تنزيلاً}؛ أي: شيئاً فشيئاً مفرَّقاً في ثلاث وعشرين سنة. {ولا يأتونَكَ بمَثَلٍ إلاَّ جِئْناكَ بالحقِّ وأحسنَ تفسيراً}.
{106} Yaani, tuliiteremsha Qur-ani hii kidogo kiodogo, akipambanua baina ya uwongofu na upotovu, haki na batili "ili uwasomee watu kwa kituo." Yaani, polepole, ili waweze kuizingatia, na watafakari maana zake, na watoe humo elimu zake. "Na tumeiteremsha kidogo kidogo" katika muda wa miaka ishirini na tatu. "Wala hawatakuletea mfano wowote, isipokuwa na Sisi tutakuletea
(jawabu la) haki, na tafsiri iliyo nzuri zaidi."
#
{107} فإذا تبيَّن أنَّه الحقُّ الذي لا شكَّ فيه ولا ريب بوجهٍ من الوجوه، فَـ {قُلْ} لمن كَذَّب به وأعرض عنه: {آمِنوا به أو لا تُؤمنوا}: فليس لله حاجةٌ فيكم ولستُم بضارِّيه شيئاً، وإنَّما ضرر ذلك عليكُم؛ فإنَّ لله عباداً غيركم، وهم الذين آتاهُمُ الله العلم النافع؛ {إذا يُتْلَى عَلَيْهِم يَخِرُّونَ للأذقَانِ سُجَّداً}؛ أي: يتأثرون به غاية التأثر ويخضعون له.
{107} Basi ikishabainika kwamba hii ndiyo haki isiyo na shaka yoyote wala kusitasita kwa namna yoyote ile, basi "Sema" umwambie mwenye kuikadhibisha na akajitenga nayo, "Iaminini au msiiamini." Mwenyezi Mungu hana haja na nyinyi na wala nyinyi hamuwezi kumdhuru hata kidogo, lakini madhara ya hayo ni juu yenu wenyewe. Kwa maana, Mwenyezi Mungu anao waja wasiokuwa nyinyi, na hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu aliwapa elimu yenye manufaa. "Wanaposomewa hii, huanguka kifudifudi wanasujudu." Yaani, wanaathiriwa sana nayo na wanainyenyekea.
#
{108} {ويقولون سبحانَ ربِّنا}: عما لا يَليقُ بجلالِهِ مما نَسَبَهُ إليه المشركون. {إنْ كان وعدُ ربِّنا}: بالبعث والجزاء بالأعمال، {لَمَفْعولاً}: لا خُلْفَ فيه ولا شكَّ.
{108} "Na wanasema: Ametakasika Mola wetu Mlezi," kutokana na yale yasiyoufailia utukufu wake miongoni mwa yale ambayo washirikina walimnasibisha nayo. "Hakika ahadi ya Mola wetu Mlezi" ya kuwafufua viumbe na kuwalipa kwa matendo yao "lazima itimizwe" na haitavunjika wala haina shaka yoyote juu yake.
#
{109} {ويخرون للأذقانِ}؛ أي: على وجوههم، {يبكونَ ويزيدُهُم}: القرآن {خشوعاً}: وهؤلاء كالذين منَّ الله عليهم من مؤمني أهل الكتاب؛ كعبد الله بن سلام، وغيره ممَّن أسلم في وقت النبيِّ - صلى الله عليه وسلم - وبعد ذلك.
{109} "Na huanguka kifudifudi huku wanalia, na inawazidisha" Qur-ani hii "unyenyekevu." Na hawa ni kama wale ambao Mwenyezi Mungu aliwaneemesha miongoni mwa waumini wa Watu wa Kitabu, kama vile Abdullah bin Salam na wengineo waliosilimu wakati wa Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – na baada ya hapo.
{قُلِ ادْعُوا اللَّهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَنَ أَيًّا مَا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَى وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا وَابْتَغِ بَيْنَ ذَلِكَ سَبِيلًا (110) وَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي لَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُنْ لَهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ وَلِيٌّ مِنَ الذُّلِّ وَكَبِّرْهُ تَكْبِيرًا (111)}.
110. Sema, "Mwombeni Allah
(Mwenyezi Mungu), au mwombeni Ar-Rahman
(Mwingi wa rehema), kwa jina lolote mnalomwita. Hakika, Yeye ana majina mazuri zaidi. Wala usiswali Swala yako kwa sauti kubwa sana, wala usiifiche kwa sauti ndogo sana, bali shika njia ya kati na kati ya hizo." 111. Na sema, "Alhamdulillah
(sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu) ambaye hakujifanyia mwana yeyote, wala hana mshirika yeyote katika ufalme, wala hana mlinzi yeyote wa kumsaidia kwa sababu ya udhaifu wake. Na mtukuze kwa utukufu mkubwa.
#
{110} يقول تعالى لعباده: {ادعوا الله أوِ ادْعوا الرحمن}؛ أي: أيهما شئتم. {أيًّا ما تدعوا فله الأسماءُ الحسنى}؛ أي: ليس له اسمٌ غير حسنٍ؛ أي: حتى ينهى عن دعائه به؛ [بل] أيُّ اسم دعوتُموه به؛ حَصَلَ به المقصودُ، والذي ينبغي أن يُدعى في كلِّ مطلوب بما يناسِبُ ذلك الاسم. {ولا تَجْهَرْ بصلاتك}؛ أي: قراءتك، {ولا تُخافِتْ بها}؛ فإنَّ في كلٍّ من الأمرين محذوراً، أمّا الجهرُ؛ فإنَّ المشركين المكذِّبين به إذا سمعوه، سبُّوه، وسبُّوا مَنْ جاء به. وأما المخافتةُ؛ فإنَّه لا يحصُلُ المقصود لمن أراد استماعَه مع الإخفاء. {وابتغ بينَ ذلك}؛ أي: بين الجهر والإخفات {سبيلاً}؛ أي: تتوسَّط فيما بينهما.
{110} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaambia waja wake, "Mwombeni Allah
(Mwenyezi Mungu), au mwombeni Ar-Rahman
(Mwingi wa rehema)." Yaani, kwa jina lolote mtakalo katika hayo. "Kwa jina lolote mnalomwita, kwani Yeye ana majina mazuri zaidi." Yaani, hana jina isipokuwa jina zuri tu, ndiyo akataze kwamba msimuombe kwa jina hilo.
[Bali] kila jina mtakalomuita kwalo, basi makusudio yatafikiwa. Lakini inafaa zaidi kwamba aombwe kwa jina linalofailiana zaidi na kila hali. "Wala usiswali kwa sauti kubwa mno wala usiifiche kwa sauti ndogo mno." Kwa maana, kila moja ya mawili hayo yamekatazwa. Ama kuswali kwa sauti kubwa mno, wakati washirikina wanaoikadhibisha Qur-ani watakapoisikia, wataitukana na kumtukana pia aliyeileta. Na ama kuswali kwa sauti ya chini mno, basi hilo haliwezi kufikisha katika makusudio kwa atakayetaka kuisikia. "Bali shika njia ya kati na kati ya hizo."
#
{111} {وقل الحمد لله}: الذي له الكمالُ والثناءُ والحمدُ والمجدُ من جميع الوجوه، المنزَّه عن كلِّ آفة ونقص. {الذي لم يتَّخِذْ ولداً ولم يكُن له شريكٌ في الملك}: بل الملكُ كلُّه لله الواحد القهار؛ فالعالم العلويُّ والسفليُّ كلُّهم مملوكون لله، ليس لأحدٍ من الملك شيء. {ولم يَكُن له وليٌّ من الذُّلِّ}؛ أي: لا يتولى أحداً من خلقه ليتعزز به ويعاونه، فإنه الغني الحميد، الذي لا يحتاج إلى أحدٍ من المخلوقات في الأرض ولا في السماوات، ولكنَّه يتخذ أولياءه إحساناً منه إليهم ورحمة بهم، {الله وليُّ الذينَ آمنوا يُخْرِجُهم من الظُّلُماتِ إلى النُّور}. {وكبِّرْه تكبيراً}؛ أي: عظِّمه وأجلَّه بالإخبار بأوصافه العظيمة، وبالثَّناء عليه بأسمائِهِ الحسنى، وبتمجيدِهِ بأفعاله المقدَّسة، وبتعظيمه وإجلاله بعبادتِهِ وحدَه لا شريك له، وإخلاص الدِّين كلِّه له.
{111} "Na sema, "Alhamdulillah
(sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu)" ambaye ana ukamilifu, na sifa njema, kuhimidiwa, na utukufu kwa namna zote. Naye ametakasika kutokana na kila balaa na kasoro. "Ambaye hakujifanyia mwana yeyote, wala hana mshirika yeyote katika ufalme;" bali ufalme wote ni wa Mwnyezi Mungu, Mmoja, Mshindi. Kwa maana, ulimwengu wa juu na wa chini wote unamilikiwa na Mwenyezi Mungu, na hakuna yeyote aliye na kitu chochote katika umiliki huo, "wala hana mlinzi yeyote wa kumsaidia kwa sababu ya udhaifu wake." Kwa hivyo, hamfanyi yeyote urafiki katika viumbe vyake ili ajiimarishe naye na ili amsaidie. Kwa maana, Yeye ndiye asiyemhitaji yeyote, Msifika, asiyehitaji chochote katika viumbe wake katika ardhi wala mbinguni, lakini hufanya vipenzi katika viumbe wake ili kuwafanyia wema na kuwarehemu. "Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa wale walioamini. Huwatoa gizani na kuwaingiza katika nuru. "Na mtukuze kwa utukufu mkubwa." Yaani, mfanye ndiye mkuu na umtukuze kwa kujulisha kuhusu sifa zake kubwa, na umsifu kwa majina yake mazuri zaidi, na kwa kumtukuza kwa matendo yake matakatifu, na kwa kumfanya mkuu na kumtukuza kwa kumwabudu Yeye peke yake bila ya mshirika yeyote, na kumfanyia yeye tu dini yote.
Imekamilika tafsiri ya Surat Al-Isra kupitia mkono wa mwandishi wake Abdur-Rahman bin Nasir bin Abdullah bin Saadi, na kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, na neema na sifa nzuri. Mwenyezi Mungu amsamehe yeye na wazazi wake na waislamu wote. Amin. Na rehema na amani nyingi za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mtume wake Muhammad. Tarehe 7 Jumada Al-Uula, 1344 Hijria. Na niliyatoa haya kutoka katika maandishi ya mwandishi wake kwa kalamu ya maskini kwa Mola wake Mlezi, Suleiman Al-Hamad Al-Bassam, Mwenyezi Mungu amsamehe yeye, wazazi wake na Waislamu wote. Amin. Na rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Muhammad na watu wa familia yake na Maswahaba wake wote. Amin, tena amin.