Tafsiri ya Surat Al-Ikhlas
Tafsiri ya Surat Al-Ikhlas
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu
{قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ (1) اللَّهُ الصَّمَدُ (2) لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ (3) وَلَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُوًا أَحَدٌ (4)}
1.
Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. 2. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. 3. Hakuzaa wala hakuzaliwa. 4. Wala hana anayefanana naye hata mmoja.
#
{1} أي: {قُلْ}: قولاً جازماً به، معتقداً له، عارفاً بمعناه: {هو اللَّه أحدٌ}؛ أي: قد انحصرت فيه الأحديَّة؛ فهو الأحد المنفرد بالكمال، الذي له الأسماء الحسنى والصفات الكاملة العليا والأفعال المقدَّسة، الذي لا نظير له ولا مثيل.
{1} Yaani, "Sema" kauli uliyo na uthabiti nayo, ukiitakidi,
huku ukijua maana yake: "Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee" na hakuna mwingine kando naye katika upekee na katika ukamilifu, ambaye ana majina mazuri zaidi, sifa kamilifu za juu kabisa, na vitendo vitakatifu, ambaye hana aliyelingana naye wala anayefanana naye.
#
{2} {اللهُ الصمدُ}؛ أي: المقصود في جميع الحوائج؛ فأهل العالم العلويِّ والسفليِّ مفتقرون إليه غاية الافتقار، يسألونَه حوائجَهم، ويرغَبون إليه في مهمَّاتهم؛ لأنَّه الكامل في أوصافه، العليم الذي قد كمل في علمه، الحليم الذي [قد] كمل في حلمه، الرحيم الذي كمل في رحمته، الذي وسعت رحمتُه كلَّ شيءٍ ... وهكذا سائر أوصافه.
{2} "Mwenyezi Mungu Mkusudiwa" katika mahitaji yote. Wakazi wa ulimwengu wa juu na wa chini wanamuhitaji sana Yeye. Wanamwomba mahitaji yao na kumkimbilia katika mambo yao. Kwa sababu Yeye ndiye Mkamilifu katika sifa zake, ajuaye zaidi ambaye ni mkamilifu katika elimu yake, Mvumilivu zaidi ambaye
[amekamilika] katika ustahimilivu wake, Mwingi wa kurehemu ambaye ni mkamilifu katika rehema yake, ambaye rehema yake imekienea kila kitu... na vivyo hivyo katika sifa zake zote.
#
{3} ومن كماله أنَّه {لم يَلِدْ ولم يولَدْ}؛ لكمال غناه.
{3} Miongoni mwa ukamilifu wake ni kwamba "Hakuzaa wala hakuzaliwa" kwa sababu ya ukamilifu wa kujitosheleza kwake.
#
{4} {ولم يكن له كُفُواً أحدٌ}: لا في أسمائه، ولا في صفاته ، ولا في أفعاله؛ تبارك وتعالى.
فهذه السورة مشتملةٌ على توحيد الأسماء والصفات.
{4} "Wala hana anayefanana naye hata mmoja" si katika majina yake, wala katika sifa zake, wala katika vitendo vyake. Ni Mtakatifu, Mtukufu. Sura hii inajumuisha kuyapwekesha majina ya Mwenyezi Mungu na sifa zake.
* * *