Tafsiri ya Surat Al-Masad
Tafsiri ya Surat Al-Masad
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu
{تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ (1) مَا أَغْنَى عَنْهُ مَالُهُ وَمَا كَسَبَ (2) سَيَصْلَى نَارًا ذَاتَ لَهَبٍ (3) وَامْرَأَتُهُ حَمَّالَةَ الْحَطَبِ (4) فِي جِيدِهَا حَبْلٌ مِنْ مَسَدٍ (5)}.
1. Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia. 2. Hayatamfaa mali yake, wala alivyovichuma. 3. Atauingia Moto wenye mwako. 4. Na mkewe, mchukuzi wa kuni. 5. Shingoni mwake iko kamba iliyosokotwa.
Abu Lahab ni ami yake Mtume – rehema na amani ziwe juu yake – na alikuwa na uadui na maudhi makali sana kwake. Hakuwa na dini ndani yake, wala hakuulinda undugu wake. Mwenyezi Mungu amlaani. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamkashifu kwa kashfa hii kubwa ambayo ni fedheha kwake mpaka Siku ya Kiyama.
#
{1} {تَبَّتْ يَدا أبي لَهَبٍ}؛ أي: خسرت يداه وشقي، {وتبَّ}: فلم يربح.
{1} "Imeangamia mikono ya Abu Lahab" na akawa mashakani "na yeye pia ameangamia" na wala hakupata faida.
#
{2} {ما أغنى عنه مالُه}: الذي كان عنده؛ فأطغاه ، ولا {ما كسبَ}: فلم يردَّ عنه شيئاً من عذاب الله إذ نزل به.
{2} "Hayatamfaa mali yake" alichokuwa nayo; basi yakamfanya kuvuka mipaka, wala "alivyovichuma." Kwani havikumwondolea chochote katika adhabu ya Mwenyezi Mungu ilipomfikia.
#
{3 - 5} {سيصلى ناراً ذات لهبٍ}؛ أي: ستحيط به النَّار من كلِّ جانبٍ، هو {وامرأتُه حَمَّالةَ الحطبِ}: وكانت أيضاً شديدة الأذيَّة لرسول الله - صلى الله عليه وسلم -؛ تتعاون هي وزوجها على الإثم والعدوان، وتلقي الشرَّ، وتسعى غاية ما تقدر عليه في أذيَّة الرسول - صلى الله عليه وسلم -، وتجمع على ظهرها الأوزار ؛ بمنزلة من يجمع حطباً، قد أعدَّ له في عنقه حبلاً {من مسدٍ}؛ أي: من ليف، أو أنها تحمل في النار الحطب على زوجها متقلِّدةً في عنقها حبلاً من مسدٍ.
وعلى كلٍّ؛ ففي هذه السورة آيةٌ باهرةٌ من آيات الله؛ فإنَّ الله أنزل هذه السورة وأبو لهب وامرأته لم يهلكا، وأخبر أنَّهما سيعذَّبان في النار ولا بدَّ، ومن لازم ذلك أنَّهما لا يسلمان، فوقع كما أخبر عالم الغيب والشهادة.
{3 - 5} "Atauingia Moto wenye mwako" Moto huo utamzunguka kutokea pande zote, yeye "na mkewe, mchukuzi wa kuni." Yeye pia alikuwa na maudhi makubwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake. Alikuwa akiasaidiana na mumewe katika madhambi, uadui, kufanya maovu, na akawa anajitahidi kiasi awezavyo kumdhuru Mtume – rehema na amani ziwe juu yake. Atakusanya mizigo mgongoni kwake kama mtu aliyekusanya kuni. Ameandaliwa kamba "iliyosokotwa" kutiwa shingoni mwake. Pia imesemwa kwamba maana yake ni kwamba atabeba kuni katika moto azitie juu ya mumewe, huku amevaa kamba iliyosokotwa kwenye shingo yake. Kwa namna yoyote ile, katika Sura hii kuna ishara ya wazi wazi kutoka katika ishara za Mwenyezi Mungu. Kwani Mwenyezi Mungu aliteremsha Sura hii na hali Abu Lahab na mkewe bado hawajaangamia, na akajulisha kwamba bila shaka wataadhibiwa Motoni, na hakuna budi. Na kinachotakiwa kutokana na hilo ni kwamba hawatakuwa salama. Basi ikawa kama alivyojulisha Mjuzi wa yaliyofichikana na yanayoonekana.
* * *