:
Tafsiri ya Surat Al-Falaq
Tafsiri ya Surat Al-Falaq
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu
: 1 - 5 #
{قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ (1) مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ (2) وَمِنْ شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ (3) وَمِنْ شَرِّ النَّفَّاثَاتِ فِي الْعُقَدِ (4) وَمِنْ شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ (5)}.
1. Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko. 2. Na shari ya alivyoviumba. 3. Na shari ya giza la usiku liingiapo. 4. Na shari ya wanaopulizia mafundoni. 5. Na shari ya hasidi anapohusudu.
#
{1} أي: {قل}: متعوِّذاً: {أعوذُ}؛ أي: ألجأ وألوذُ وأعتصمُ، {بربِّ الفلق}؛ أي: فالق الحبِّ والنَّوى، وفالق الأصباح.
{1} Yaani, "Sema" kwa kutafuta hifadhi: "Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko." Pia ilisemekana kwamba maana yake ni mpasuaji mbegu na kokwa zikachipua.
#
{2} {من شرِّ ما خَلَقَ}: وهذا يشمل جميع ما خلق الله من إنسٍ وجنٍّ وحيوانات؛ فيستعاذ بخالقها من الشرِّ الذي فيها.
{2} "Kutokana na shari ya alivyoviumba" Haya yanajumisha vyote alivyoviumba Mwenyezi Mungu, wakiwemo wanadamu, majini na wanyama. Kwa hivyo, inatafutwa kinga ya Muumba wake kutokana na shari iliyomo ndani ya vyote hivyo.
#
{3} ثم خصَّ بعدما عمَّ، فقال: {ومن شرِّ غاسقٍ إذا وَقَبَ}؛ أي: من شرِّ ما يكون في الليل حين يغشى النّاسَ، وتنتشر فيه كثيرٌ من الأرواح الشرِّيرة والحيوانات المؤذية.
{3} Kisha akasema maneno mahususi baada ya kusema maneno ya jumla "Na kutokana na shari ya giza la usiku liingiapo" na wakaenea humo pepo wengi waovu na wanyama wenye madhara.
#
{4} {ومن شرِّ النَّفَّاثات في العقد}؛ أي: ومن شرِّ السَّواحر اللاتي يَسْتَعِنَّ على سحرهنَّ بالنَّفْثِ في العقد التي يَعْقِدْنَها على السحر.
{4} "Na kutokana na shari ya wanaopulizia mafundoni." Nao ni wachawi wa kike wanaotafuta msaada juu ya uchawi wao kwa kupuliza mafundoni wanayofunga kwa ajili ya kufanya uchawi.
#
{5} {ومن شرِّ حاسدٍ إذا حَسَدَ}: والحاسدُ هو الذي يحبُّ زوال النِّعمة عن المحسود؛ فيسعى في زوالها بما يقدر عليه من الأسباب، فاحتيج إلى الاستعاذة بالله من شرِّه وإبطال كيده. ويدخل في الحاسد العاينُ؛ لأنَّه لا تصدر العين إلاَّ من حاسدٍ شرِّيرِ الطبع خبيث النفس. فهذه السورة تضمَّنت الاستعاذة من جميع أنواع الشُّرور عموماً وخصوصاً، ودلَّت على أنَّ السِّحر له حقيقةٌ؛ يُخشى من ضرره، ويستعاذ بالله منه ومن أهله.
{5} "Na kutokana na shari ya hasidi anapohusudu." Naye ni kila anayetaka neema iondolewe kwa yule anayemhusudu. Kwa hivyo akatafuta kuiondoa kwa kutumia njia yoyote awezayo. Basi ikahitaji kutafuta hifadhi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na uovu wake na kubatilisha njama yake. Pia anaingia hapa mtu mwenye kijicho. Kwa sababu kijicho hakitokei isipokuwa kwa mtu hasidi mwenye tabia ya uovu, mwenye nafsi chafu. Sura hii inajumuisha kutafuta hifadhi kutokana na kila aina ya uovu kwa ujumla na kwa njia mahususi. Na inaonyesha kwamba uchawi ni jambo la uhakika, unaoogopwa madhara yake, na mtu anapaswa kutafuta hifadhi kwa Mwenyezi Mungu kutokana nao na kutokana na watu wa uchawi.
* * *