:
Tafsiri ya Surat An-Nasr
Tafsiri ya Surat An-Nasr
Ilishuka Madina
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu
: 1 - 3 #
{إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّهِ وَالْفَتْحُ (1) وَرَأَيْتَ النَّاسَ يَدْخُلُونَ فِي دِينِ اللَّهِ أَفْوَاجًا (2) فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَاسْتَغْفِرْهُ إِنَّهُ كَانَ تَوَّابًا (3)}.
1. Itakapokuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi. 2. Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi. 3. Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha; hakika Yeye ndiye anayepokea toba.
#
{1 - 3} في هذه السورة الكريمة: بشارةٌ، وأمرٌ لرسوله عند حصولها، وإشارةٌ، وتنبيهٌ على ما يترتَّب على ذلك: فالبشارةُ هي البشارة بنصر الله لرسوله، وفتحه مكَّة، ودخول الناس {في دين الله أفواجاً} بحيث يكون كثيرٌ منهم من أهله وأنصاره بعد أن كانوا من أعدائه، وقد وقع هذا المبشَّر به. وأما الأمر بعد حصول النَّصر والفتح؛ فأمر [اللَّهُ] رسولَه أن يشكره على ذلك، ويسبِّح بحمده، ويستغفره. وأما الإشارة؛ فإن في ذلك إشارتين: إشارة أنَّ النَّصر يستمرُّ للدين ويزداد عند حصول التَّسبيح بحمد الله واستغفاره من رسوله؛ فإن هذا من الشُّكر، والله يقول: {لئن شكرتُمْ لأزيدَنَّكم}: وقد وُجِدَ ذلك في زمن الخلفاء الراشدين وبعدهم في هذه الأمَّة، لم يزل نصر الله مستمرًّا حتى وصل الإسلام إلى ما لم يصل إليه دينٌ من الأديان، ودخل فيه من لم يدخل في غيره، حتى حدث من الأمة من مخالفة أمر الله ما حدث، فابتُلوا بتفرُّق الكلمة وتشتُّت الأمر، فحصل ما حصل، ومع هذا؛ فلهذه الأمَّة وهذا الدِّين من رحمة الله ولطفه ما لا يخطر بالبال أو يدور في الخيال. وأما الإشارة الثانية؛ فهي الإشارة إلى أنَّ أجلَ رسول الله - صلى الله عليه وسلم - قد قرب ودنا، ووجه ذلك أنَّ عمره عمرٌ فاضلٌ، أقسم الله به، وقد عُهِدَ أنَّ الأمور الفاضلة تُخْتَم بالاستغفار؛ كالصلاة والحجِّ وغير ذلك، فأمر الله لرسوله بالحمد والاستغفار في هذه الحال إشارةٌ إلى أنَّ أجله قد انتهى؛ فلْيستعدَّ ويتهيَّأ للقاء ربِّه ويختم عمره بأفضل ما يجده صلوات الله وسلامه عليه، فكان [- صلى الله عليه وسلم -] يتأوَّل القرآن ويقول ذلك في صلاته؛ يكثر أن يقول في ركوعه وسجوده: «سبحانك اللهمَّ ربَّنا وبحمدك، اللهمَّ! اغفر لي».
{1 - 3} Katika Sura hii tukufu kuna bishara njema, amri kwa Mtume wake itakapotokea, na ishara na tanbihi juu ya yatakayotokea kutokana na hayo. Bishara njema hiyo ni bishara njema ya nusura ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake, na kuiteka kwake Makka, na kuingia kwa watu "katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi" hapo wakawa wengi wake ni katika watu wake na wasaidizi wake baada ya kwamba walikuwa katika adui zake. Na bishara hii tayari ilishatokea. Ama amri aliyoamrishwa baada ya nusura na ushindi wa Makka ni ile amri ambayo [Mwenyezi Mungu] alimuamuru Mtume wake kumshukuru kwa hayo, na kumtakasa kwa sifa zake, na kumuomba msamaha. Na ama bishara njema, hiyo ndani yake kuna ishara mbili: ishara kwamba nusura ya dini itaendelea na kuongezeka wakati wa kumtakasa Mwenyezi Mungu kwa sifa zake na Mtume wake kumuomba msamaha. Kwani hayo ni katika shukurani, na Mwenyezi Mungu anasema: "Mkishukuru nitakuzidishieni." Haya tayari yalishapatikana katika zama za Makhalifa waongofu na baada yao katika umma huu. Nusura ya Mwenyezi Mungu iliendelea mpaka Uislamu ukafika pale ambapo dini nyingine yoyote ile haikuwahi kufika, na wakaingia ndani yake wale ambao hawakuingia katika dini nyingineyo, hadi yalipotokea yaliyotokea katika umma huu ya kuhalifu amri ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo wakapewa mtihani wa kufarikiana kwa neno lao na jambo lao kutawanyika. Lakini licha ya hili, umma huu na dini hii vina rehema na upole wa Mwenyezi Mungu ambao hautokei akilini mwa mtu yeyote wala katika fikira yake. Na ama bishara njema ya pili ni ishara ya kwamba maisha ya Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani zimshukie - yamekaribia kwisha. Na sababu ya hilo ni kuwa maisha yake ni maisha bora, ambayo Mwenyezi Mungu ameapa kwayo, na imekuwa kawaida kwamba mambo bora yanafungwa kwa msamaha; kama vile swala, Hija, na mengineyo. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu kumwamrisha Mtume wake kumsifu na kuomba msamaha katika hali hii ni ishara ya kwamba wakati wake umefika mwisho. Basi na ajiandae na kukutana na Mola wake Mlezi na amalizie maisha yake kwa bora zaidi anayoweza kuyapata - rehema na amani ziwe juu yake. Kwa hivyo Mtume - rehema na amani ziwe juu yake - akawa anafasiri Qur-ani na anasema hivyo katika swala yake. Mara nyingi alikuwa akisema katika kurukuu kwake na kusujudu kwake: "Umetakasika, ewe Mwenyezi Mungu, Mola wetu Mlezi, na sifa njema ni zako. Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe."
* * *