Tafsiri ya Surat Hud amani iwe juu yake
Tafsiri ya Surat Hud amani iwe juu yake
Nayo iliteremka Makka
{الر كِتَابٌ أُحْكِمَتْ آيَاتُهُ ثُمَّ فُصِّلَتْ مِنْ لَدُنْ حَكِيمٍ خَبِيرٍ (1) أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّهَ إِنَّنِي لَكُمْ مِنْهُ نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ (2) وَأَنِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُمَتِّعْكُمْ مَتَاعًا حَسَنًا إِلَى أَجَلٍ مُسَمًّى وَيُؤْتِ كُلَّ ذِي فَضْلٍ فَضْلَهُ وَإِنْ تَوَلَّوْا فَإِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ كَبِيرٍ (3) إِلَى اللَّهِ مَرْجِعُكُمْ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (4)}.
1. Alif Lam Ra. Hiki ni Kitabu ambacho Aya zake zimefanywa kuwa sawa sawa, kisha zikapambanuliwa kwa kina, kilichotoka kwa Mwenye Hekima, Mwenye habari zote. 2. Ili msimuabudu isipokuwa Mwenyezi Mungu. Hakika mimi kwenu ni mwonyaji na mbashiri nitokaye kwake. 3. Na ili mumwombe msamaha Mola wenu Mlezi, kisha mtubie kwake. Atawastarehesha starehe nzuri mpaka muda maalumu. Na atampa kila mwenye fadhila, fadhila yake. Na wakikengeuka, basi mimi ninawahofia adhabu ya hiyo Siku Kubwa. 4. Marejeo yenu ni kwa Mwenyezi Mungu tu. Naye ni Muweza wa kila kitu.
#
{1} يقول تعالى: هذا {كتابٌ}: عظيم ونزل كريم، {أُحْكِمَتْ آياته}؛ أي: أتقنت وأحسنت، صادقةٌ أخبارها، عادلةٌ أوامرها ونواهيها، فصيحةٌ ألفاظهُ بهيةٌ معانيه، {ثم فُصِّلَتْ}؛ أي: ميزت وبينت بياناً في أعلى أنواع البيان، {من لَدُنْ حكيم}: يضع الأشياء مواضعها، وينزلها منازلها، لا يأمر ولا ينهى إلا بما تقتضيه حكمته، {خبيرٍ}: مطَّلع على الظواهر والبواطن؛ فإذا كان إحكامه وتفصيلُه من عند الله الحكيم الخبير؛ فلا تسألْ بعد هذا عن عظمته وجلالته واشتماله على كمال الحكمة وسعة الرحمة.
{1} Yeye Mtukufu anasema: Hiki ni
“Kitabu” kitukufu na uteremsho mtukufu, ambacho “Aya zake zimefanywa kuwa sawa sawa.” Yaani, zilifanywa kuwa kamilifu, nzuri, zenye habari za ukweli, zenye maamrisho na makatazo ya uadilifu, zenye maneno ya ufasaha na maana zake, "kisha zikapambanuliwa kwa kina." Yaani, zimepambanuliwa, na kubainishwa kunainisha kwa ya hali ya juu kabisa. "Kilichotoka kwa Mwenye Hekima" ambaye huviweka vitu pahali pake na kuviteremsha katika daraja zake. Haamrishi wala hakatazi isipokuwa kile ambacho hekima yake inataka. "Mwenye habari zote," anayajua ya dhahiri na ya ndani yote. Kwa hivyo, ikiwa kuzifanya kwake kuwa sawasawa, na kuzipambanua kwake kwa kina ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye hekima, Mwenye habari zote, basi usiulize baada ya haya kuhusu ukuu wake, utukufu wake, na kujumuisha kwa kwa hekima kamili na rehema pana.
#
{2} وإنما أنزل الله كتابه لأن لا تعبدوا إلاَّ اللهَ؛ أي: لأجل إخلاص الدين كلِّه لله، وأن لا يُشْرِكَ به أحدٌ من خلقه. {إنني لكم}: أيُّها الناس، {منه}؛ أي: من الله ربكم {نذيرٌ}: لمن تجرَّأ على المعاصي بعقاب الدنيا والآخرة، {وبشيرٌ}: للمطيعين لله بثواب الدُّنيا والآخرة.
{2} Na Mwenyezi Mungu alikiteremsha Kitabu chake ili msimwabudu isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. Yaani, ili afanyiwe dini yote yeye tu, na kwamba asishirikishwe na chochote miongoni mwa viumbe vyake. "Hakika Mimi kwenu" Enyi watu! "Kutoka kwa Mwenyezi Mungu" Mola wenu Mlezi ni "mwonyaji" kwa anayeyafanyia ujasiri maasia kwamba ataadhibiwa katika dunia na Akhera. "Mbashiri" kwa wale wanaomtii Mwenyezi Mungu kwamba watapata malipo katika dunia hii na akhera.
#
{3} {وأن استغفروا ربَّكم}: عن ما صدر منكم من الذُّنوب، {ثم توبوا إليه}: فيما تستقبلون من أعماركم بالرجوع إليه بالإنابة والرجوع عما يكرهه الله إلى ما يحبُّه ويرضاه. ثم ذكر ما يترتَّب على الاستغفار والتوبة، فقال: {يمتِّعْكم متاعاً حسناً}؛ أي: يعطيكم من رزقه ما تتمتَّعون به، وتنتفعون {إلى أجل مسمّى}؛ أي: إلى وقت وفاتكم. {ويؤت}: منكم {كلَّ ذي فضل فضلَه}؛ أي: يعطي أهل الإحسان والبر من فضله وبرِّه ما هو جزاءٌ لإحسانهم من حصول ما يحبُّون ودفع ما يكرهون. {وإن تَوَلَّوا}: عن ما دعوتكم إليه، بل أعرضتُم عنه، وربَّما كذَّبتم به، {فإني أخاف عليكم عذابَ يوم كبيرٍ}: وهو يوم القيامة، الذي يجمع الله فيه الأوَّلين والآخرين.
{3} "Na kwamba mumwombe msamaha Mola wenu Mlezi" kwa yale mliyoyafanya miongoni mwa madhambi. "Kisha mtubie kwake" katika maisha ya umri wenu yajayo kwa kumrudia na kuacha yale anayoyachukia Mwenyezi Mungu hadi kwa yale anayoyapenda na kuyaridhia. Kisha akataja yale yanayotokana na kuomba maghufira na toba, akasema, "Atawastarehesha starehe nzuri." Yaani, atawapa katika riziki yake kile mtakachostareheka kwacho, na kunufaika nacho "mpaka muda maalumu;" yaani, mpaka wakati wa kufa kwenu. "Na atampa" miongoni mwenu "kila mwenye fadhila, fadhila yake." Yaani, atawapa watu ukarimu na wema katika fadhila yake na wema wake kile ambacho ni malipo ya ukarimu wao, kama vile kupata yale wanayoyapenda na kuzuia yale wanayoyachukia. "Na wakikengeuka," dhidi ya yale niliyowalingania, na mkayapa mgongo, na hata pengine mkayakadhibisha, "basi mimi ninawahofia adhabu ya hiyo Siku Kubwa." Nayo ni Siku ya Qiyama ambayo Mwenyezi Mungu atawakusanya wa kwanza na wa mwisho ndani yake.
#
{4} فيجازيهم بأعمالهم إن خيراً؛ فخير، وإن شرًّا؛ فشر. وفي قوله: {وهو على كلِّ شيء قديرٌ}: كالدليل على إحياء الله الموتى؛ فإنه على كلِّ شيء قديرٌ ، ومن جملة الأشياء إحياء الموتى، وقد أخبر بذلك، وهو أصدق القائلين؛ فيجب وقوع ذلك عقلاً ونقلاً.
{4} Kisha atawalipa kwa matendo yao, ikiwa ni heri, basi kwa ya heri. Na kama ni maovu, basi ni kwa uovu.
Na katika kauli yake: "Naye ni Muweza wa kila kitu," ni ushahidi wa Mwenyezi Mungu juu ya kuwafufua wafu. Kwani Yeye ni Mwenye Uweza wa kila kitu. Na miongoni mwa vitu hivyo ni kuwafufua wafu. Naye tayari alikwisha julisha juu ya hilo, na Yeye ndiye mkweli zaidi wa wanaosema. Kwa hivyo, ni lazima hilo litokee, kiakili na kwa maandiko.
{أَلَا إِنَّهُمْ يَثْنُونَ صُدُورَهُمْ لِيَسْتَخْفُوا مِنْهُ أَلَا حِينَ يَسْتَغْشُونَ ثِيَابَهُمْ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ (5)}
5. Hebu angalia! Ati wanafunika vilivyomo vifuani mwao ili wamfiche Mwenyezi Mungu! Jueni kuwa wanapojigubika nguo zao, Yeye anajua yale wanayoyaficha na yale wanayoyaweka hadharani. Hakika Yeye ni Mwenye kujua zaidi yaliyomo vifuani.
#
{5} يخبر تعالى عن جهل المشركين وشدة ضلالهم أنهم {يَثْنون صدورَهم}؛ أي: يميلونها ليستخفوا من الله، فتقع صدورهم حاجبةً لعلم الله بأحوالهم وبصره لهيئاتهم. قال تعالى مبيناً خطأهم في هذا الظنِّ: {ألا حين يَسْتَغْشون ثيابهم}؛ أي: يتغطون بها، يعلمهم في تلك الحال التي هي من أخفى الأشياء، بل {يعلم ما يُسِرُّون}: من الأقوال والأفعال، {وما يُعْلِنون}: منها، بل ما هو أبلغُ من ذلك، وهو: {إنه عليمٌ بذات الصدور}؛ أي: بما فيها من الإرادات والوساوس والأفكار التي لم ينطقوا بها سرًّا ولا جهراً؛ فكيف تخفى عليه حالكم إذا ثنيتم صدوركم لتستخفوا منه؟!
ويُحتمل أنَّ المعنى في هذا: أن الله يذكر إعراض المكذِّبين للرسول، الغافلين عن دعوته، أنَّهم من شدَّة إعراضهم يَثْنون صدورهم؛ أي: يَحْدَوْدِبون حين يرون الرسول؛ لئلاَّ يراهم ويُسْمِعَهم دعوته ويعظَهم بما ينفعهم؛ فهل فوق هذا الإعراض شيء؟! ثم توعَّدهم بعلمه تعالى بجميع أحوالهم وأنهم لا يخفون عليه، وسيجازيهم بصنيعهم.
{5} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu ujinga wa washirikina na ukubwa wa upotovu wao kwamba "wanafunika vilivyomo vifuani mwao." Yaani, wanavigeuza ili wamfiche Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, vifua vyao vinakuwa vimezuiliwa mbali namna ya kwamba Mwenyezi Mungu hajui hali zao wala hawezi kuona sura zao.
Yeye Mtukufu Akasema akibainisha kosa lao katika dhana hii: "Jueni kuwa wanapojigubika nguo zao" anawajua katika hali hiyo ambayo ni miongoni mwa vitu vilivyofichikana zaidi. Bali "Anajua yale wanayoyaficha" miongoni mwa maneno na vitendo "na yale wanayoyaweka hadharani" miongoni mwa hayo. Bali hata yale yaliyo zaidi ya hayo, ambayo ni kwamba "Hakika Yeye ni Mwenye kujua zaidi yaliyomo vifuani." Yaani, yale yaliyo ndani yake miongoni mwa nia mbalimbali, na wasiwasi, na fikiria ambazo hawakuzitamka kwa siri au kwa sauti kubwa. Basi vipi hali yenu itafichikana kwake mnapovifunika vifua vyenu ili mjifiche kutoka kwake? Na inawezekana kwamba maana yake ni kwamba Mwenyezi Mungu anataja kupeana mgongo kwa wanaomkadhibisha Mtume, ambao wameghafilika na wito wake, kwamba kwa sababu ya ukubwa wa kupeana kwao mgongo wanavifunika vifua vyao. Yaani, wanajikunja wanapomuona Mtume, ili asiwaone na kuwaskizisha wito wake na kuwaaidhi kwa yenye kuwanufaisha. Basi Je, kuna kitu chochote juu ya kupeana mgongo huku? Kisha akawaonya kwamba Yeye Mtukufu anazijua hali zao zote na kwamba hawafichikani kwake, na atawalipa kwa matendo yao.
{وَمَا مِنْ دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ إِلَّا عَلَى اللَّهِ رِزْقُهَا وَيَعْلَمُ مُسْتَقَرَّهَا وَمُسْتَوْدَعَهَا كُلٌّ فِي كِتَابٍ مُبِينٍ (6)}.
6. Na hakuna mnyama yoyote katika ardhi isipokuwa riziki yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Naye anajua makao yake na mapitio yake. Yote hayo yamo katika Kitabu chenye kubainisha.
#
{6} أي: جميع ما دبَّ على وجه الأرض من آدميٍّ وحيوانٍ بَرِّيٍّ أو بحريٍّ؛ فالله تعالى قد تكفَّل بأرزاقهم وأقواتهم، فرزقُهم على الله. {ويعلم مستقرَّها ومستوْدَعَها}؛ أي: يعلم مستقرَّ هذه الدوابِّ، وهو المكان الذي تقيم فيه وتستقرُّ فيه وتأوي إليه، ومستودعُها المكانُ الذي تنتقل إليه في ذهابها ومجيئها وعوارض أحوالها. {كلٌّ}: من تفاصيل أحوالها {في كتابٍ مبينٍ}؛ أي: في اللوح المحفوظ، المحتوي على جميع الحوادث الواقعة، والتي تقع في السماوات والأرض، الجميع قد أحاط بها علم الله، وجرى بها قلمه، ونفذت فيها مشيئته ووسعها رزقه؛ فلتطمئنَّ القلوب إلى كفاية من تكفَّلَ بأرزاقها، وأحاط علماً بذواتها وصفاتها.
{6} Yaani, kila kitu kinachoenda juu ya uso wa ardhi kama vile binadamu na mnyama wa nchi kavu au wa baharini, Mwenyezi Mungu Mtukufu alichukua jukumu la kuwapa riziki na vyakula vyao vikuu; kwa hivyo, riziki yao iko juu ya Mwenyezi Mungu. "Naye anajua makao yake na mapitio yake;" yaani, anajua makao ya wanyama hawa ambako wanakaa na kujilinda hapo. Na mapitio yao ni mahali ambapo wanahamia katika kwenda kwao na kurudi kwao na mambo yote ya maisha yao yanayowapata. "Yote hayo" miongoni mwa maelezo ya kina ya hali zao "yamo katika Kitabu chenye kubainisha." Yaani, katika Ubao Uliohifadhiwa, ambao unajumuisha matukio yote yanayotokea na ambayo hutokea katika mbingu na ardhi, yote hayo yamezungukwa na elimu ya Mwenyezi Mungu, na yakaandikwa na kalamu yake, na yakatekelezeka kwa mapenzi yake, na yakazungukwa na riziki yake. Basi na zitulie nyoyo kwa sababu ya utoshelevu wa yule aliyechukua dhamana ya kuwaruzuku na akawazunguka wao na hata sifa zao kwa elimu yake.
{وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَكَانَ عَرْشُهُ عَلَى الْمَاءِ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا وَلَئِنْ قُلْتَ إِنَّكُمْ مَبْعُوثُونَ مِنْ بَعْدِ الْمَوْتِ لَيَقُولَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَذَا إِلَّا سِحْرٌ مُبِينٌ (7) وَلَئِنْ أَخَّرْنَا عَنْهُمُ الْعَذَابَ إِلَى أُمَّةٍ مَعْدُودَةٍ لَيَقُولُنَّ مَا يَحْبِسُهُ أَلَا يَوْمَ يَأْتِيهِمْ لَيْسَ مَصْرُوفًا عَنْهُمْ وَحَاقَ بِهِمْ مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ (8)}.
7. Na Yeye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Na Kiti chake cha Enzi kilikuwa juu ya maji, ili awajaribu ni nani kati yenu ndiye mzuri zaidi wa matendo. Na wewe ukisema, "Hakika nyinyi mtafufuliwa baada ya kufa." Hakika wale waliokufuru watasema, "Haya si isipokuwa uchawi ulio wazi." 8. Na hata tukiwacheleweshea adhabu mpaka muda uliokwisha hisabiwa, wao hakika watasema, "Ni nini kinachoizuia?" Jueni! Siku itakapowajia, basi haitaondolewa kwao. Na yatawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha.
#
{7} يخبر تعالى أنه {خَلَقَ السمواتِ والأرضَ في ستَّة أيام}: أولها يوم الأحد، وآخرُها يوم الجمعة. {و} حين خلق السماواتِ والأرضَ، {كان عرشُهُ على الماء}: فوق السماء السابعة؛ فبعد أن خلقَ السماوات والأرض؛ استوى على عرشه، يدبِّر الأمور ويصرِّفها كيف شاء من الأحكام القدريَّة والأحكام الشرعيَّة. ولهذا قال: {لِيَبْلُوَكم أيُّكم أحسنُ عملاً}؛ أي: ليمتَحِنَكم إذ خَلَقَ لكم ما في السماوات والأرض بأمره ونهيه، فينظر أيُّكم أحسنُ عملاً. قال الفضيل بن عِياض رحمه الله: أخلصُه وأصوبُه. قيل: يا أبا علي! ما أخلصه وأصوبه؟ فقال: إنَّ العمل إذا كان خالصاً ولم يكن صواباً؛ لم يُقْبَلْ، وإذا كان صواباً ولم يكن خالصاً؛ لم يُقْبَلْ، حتى يكون خالصاً صواباً. والخالص: أن يكون لوجه الله، والصواب: أن يكون متَّبِعاً فيه الشرع والسُّنة. وهذا كما قال تعالى: {وما خلقتُ الجِنَّ والإنس إلا ليعبدونِ}، وقال تعالى: {اللهُ الذي خلق سبع سمواتٍ ومن الأرض مثلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ الأمر بينَهنَّ لِتَعْلموا أنَّ الله على كلِّ شيءٍ قديرٌ وأن الله قد أحاطَ بكلِّ شيءٍ علماً}: فالله تعالى خلق الخلق لعبادته ومعرفته بأسمائه وصفاته، وأمرهم بذلك؛ فمن انقاد وأدَّى ما أمِرَ به؛ فهو من المفلحين، ومن أعرض عن ذلك؛ فأولئك هم الخاسرون، ولا بدَّ أن يجمَعَهم في دار يجازيهم على ما أمرهم به ونهاهم. ولهذا ذكر الله تكذيب المشركين بالجزاء، فقال: {ولئن قلتَ إنَّكم مبعوثون من بعدِ الموت لَيقولَنَّ الذين كفروا إنْ هذا إلاَّ سحرٌ مبينٌ}؛ أي: ولئن قلتَ لهؤلاء وأخبرتَهم بالبعث بعد الموت؛ لم يصدِّقوك، بل كذَّبوك أشدَّ التكذيب ، وقدحوا فيما جئت به، وقالوا: {إنْ هذا إلا سحرٌ مُبين}: ألا وهو الحقُّ المبين.
{7} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba "Yeye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita" ya kwanza yake ni Siku ya Jumapili, na ya mwisho yake ni siku ya Ijumaa. "Na" wakati alipoziumba mbingu na ardhi, "Na Kiti chake cha Enzi kilikuwa juu ya maji" juu ya mbingu ya saba. Na baada ya kuziumba mbingu na ardhi, aliinuka juu ya kiti Chake cha Enzi, akiendesha mambo, na kuyapeleka namna anavyotaka miongoni mwa hukumu za kimajaliwa na kisheria. Na ndiyo maana akasema, "ili awajaribu ni nani wenu ndiye mzuri zaidi wa matendo." Yaani, awape mtihani alipowaumbia vilivyomo mbinguni na ardhini kwa maamrisho yake na makatazo yake, ndiyo aone ni nani wenu ndiye mzuri zaidi wa matendo. Al-Fudhail bin Iyadh, Mwenyezi Mungu amrehemu, alisema, "Yapi, yale ambayo yalikusudiwa yeye tu, na yaliyo sahihi zaidi" Akaambiwa, "Ewe Abu Ali! Ni yapi yaliyokusudiwa yeye tu, na yaliyo sahihi zaidi?" Akasema, "Hakika, matendo yanapokuwa yamekusudiwa yeye tu, lakini hayakuwa sahihi, basi hayakubaliwi. Na ikiwa ni sahihi, lakini hayakukusudiwa yeye tu, basi hayakubaliwi mpaka yakusudiwe yeye tu na yawe sahihi. Na yale yaliyokusudiwa yeye ni yale ambayo yanatakwa kwayo uso wake. Nayo yaliyo sahihi ni kwamba afuate kwayo sheria na Sunna. Hayo ni kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Nami sikuwaumba majini na watu isipokuwa waniabudu Mimi." Na akasema Yeye Mtukufu, "Mwenyezi Mungu ndiye aliziumba mbingu saba, na ardhi kwa mfano wa hizo. Amri zake zinashuka baina yake, ili mjue kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu, na kwamba Mwenyezi Mungu amekizunguka kila kitu kwa elimu yake." Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu aliviumba viumbe ili vimuabudu Yeye na kuyajua majina yake na sifa zake, na akawaamrisha kufanya hivyo. Kwa hivyo, mwenye kufuata na akatekeleza yale aliyoamrishwa, basi yeye ni katika waliofaulu. Na mwenye kuyapa mgongo hayo, basi hao ndio waliohasirika. Na hakuna shaka lazima atawakusanya katika nyumba ambayo atawalipa kwa yale aliyowaamrisha na kuwakataza. Na ndiyo maana Yeye Mtukufu akataja kukadhibisha kwa washirikina malipo, akasema, "Na wewe ukisema, "Hakika nyinyi mtafufuliwa baada ya kufa." Hakika wale waliokufuru watasema, "Haya si isipokuwa uchawi ulio wazi." Yaani, ukiwaambia hawa na ukawajulisha kuhusu ufufuo baada ya kufa, hawakusadiki, bali wanakukadhibisha kukadhibisha kukubwa, na wanatia doa katika yale uliyokuja nayo, na wanasema, "Haya si isipokuwa uchawi ulio wazi." Lakini, haya ndiyo haki iliyo wazi.
#
{8} {ولئنْ أخَّرْنا عنهم العذابَ إلى أمَّةٍ معدودةٍ}؛ أي: إلى وقت مقدَّر فتباطؤوه، لقالوا من جهلهم وظلمهم: {ما يحبِسُه}؟! ومضمونُ هذا تكذيبُهم به؛ فإنهم يستدلُّون بعدم وقوعه بهم عاجلاً على كذب الرسول المخبر بوقوع العذاب؛ فما أبعد هذا الاستدلال. {ألا يوم يأتيهم} العذابُ {ليس مصروفاً عنهم}: فيتمكَّنون من النظر في أمرهم، {وحاق بهم}؛ أي: نزل {ما كانوا به يستهزِئون}: من العذاب حيثُ تهاونوا به، حتى جَزَموا بكذب مَنْ جاء به.
{8} "Na hata tukiwacheleweshea adhabu mpaka muda uliokwisha hisabiwa;" yaani, mpaka muda uliopimwa, nao wakaiona kuwa imechelewa. Basi wangesema kutokana na ujinga wao na udhalimu wao, "Ni nini kinachoizuia?" Na hili linajumuisha kukadhibisha kwao hilo. Kwa maana, wao wanatumia ushahidi wa kutowatokea kwake haraka kwamba Mtume anayejulisha kuwa adhabu itatokea ni mwongo. Lakini ni wa mbali ulioje ushahidi huu. "Jueni! Siku itakapowajia" adhabu hiyo, "basi haitaondolewa kwao" ili waweze kuyatazama mambo yao, "Na yatawafika." Yaani, yatawateremkia "yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha" miongoni mwa adhabu, kwa kuwa waliifanyia uzembe mpaka wakawa na uhakika na kwamba aliyekuja na hilo ni mwongo.
{وَلَئِنْ أَذَقْنَا الْإِنْسَانَ مِنَّا رَحْمَةً ثُمَّ نَزَعْنَاهَا مِنْهُ إِنَّهُ لَيَئُوسٌ كَفُورٌ (9) وَلَئِنْ أَذَقْنَاهُ نَعْمَاءَ بَعْدَ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُ لَيَقُولَنَّ ذَهَبَ السَّيِّئَاتُ عَنِّي إِنَّهُ لَفَرِحٌ فَخُورٌ (10) إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَئِكَ لَهُمْ مَغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ (11)}.
9. Na tukimwonjesha mtu rehema kutoka kwetu, kisha tukaiondoa kwake, yeye hakika ni mwenye kukata tamaa, mwingi wa kufuru. 10. Na tukimwonjesha neema baada ya madhara yaliyomgusa, hakika yeye husema, "Mabaya yamekwisha niondokea." Hakika yeye ni mwenye kufurahi, mwenye kujifahiri mno. 11. Isipokuwa wale waliosubiri na wakatenda mema. Hao wana maghufira na malipo makubwa.
#
{9 - 10} يخبر تعالى عن طبيعة الإنسان أنه جاهلٌ ظالمٌ: بأنَّ الله إذا أذاقه منه رحمةً كالصحة والرزق والأولاد ونحو ذلك، ثم نزعها منه؛ فإنَّه يستسلم لليأس وينقادُ للقنوط؛ فلا يرجو ثوابَ الله ولا يخطُرُ بباله أنَّ الله سيردُّها أو مثلها أو خيراً منها عليه، وأنَّه إذا أذاقه رحمةً من بعد ضرَّاء مسَّتْه، أنه يفرح ويَبْطَرُ ويظنُّ أنه سيدوم له ذلك الخير ويقول: {ذَهَبَ السيئاتُ عنِّي إنَّه لفرحٌ فخورٌ}؛ أي: يفرح بما أوتي مما يوافق هوى نفسه، فخورٌ بنعم الله على عباد الله، وذلك يحمله على الأشر والبطر والإعجاب بالنفس والتكبُّر على الخلق واحتقارهم وازدرائهم، وأيُّ عيبٍ أشدُّ من هذا؟!
{9 - 10} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu maumbile ya mwanadamu kwamba yeye ni mjinga na dhalimu. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu anapomwonjesha rehema kutoka Kwake, kama vile afya nzuri, riziki, watoto, na mfano wa hayo, kisha akaiondoa kwake, yeye hakika anajisalimisha kwa kukata tamaa na anafuata huko kukata kwake tamaa. Kwa hivyo hatarajii malipo ya Mwenyezi Mungu, wala haimjii katika akili yake kwamba Mwenyezi Mungu atairejesha kwake, au kitu mfano wake, au kitu bora zaidi kuliko hicho. Na kwamba akimwonjesha rehema baada ya dhara lililomgusa, yeye hufurahi na kujifahiri na kudhani kuwa heri hiyo itaendelea kudumu kwake. Na anasema, "Mabaya yamekwisha niondokea. Hakika yeye ni mwenye kufurahi, mwenye kujifahiri mno." Yaani, anafurahia kile alichopewa ambacho kinaafikiana na matamanio yake, na ni mwenye kujifahiri kwa neema za Mwenyezi Mungu juu ya waja wa Mwenyezi Mungu. Na hilo linamfanya kutenda maovu, majigambo, kujiona mwenyewe, na kuwafanyia kiburi viumbe, na kuwadharau, na kuwaona kuwa duni. Na ni kasoro gani iliyo kubwa zaidi kuliko hii?
#
{11} وهذه طبيعة الإنسان من حيث هو؛ إلا مَنْ وفَّقه الله وأخرجه من هذا الخُلُق الذميم إلى ضدِّه، وهم الذين صبَّروا أنفسهم عند الضراءِ فلم ييأسوا، وعند السراء فلم يبطروا، وعملوا الصالحات من واجبات ومستحبَّات. {أولئك لهم مغفرة}؛ لذنوبهم يزول بها عنهم كل محذور، {وأجر كبير}؛ وهو الفوز بجناتِ النعيم التي فيها ما تشتهيه الأنفس، وتلذُّ الأعين.
{11} Na hili ndilo umbile la mwanadamu jinsi alivyo, Isipokuwa yale ambayo Mwenyezi Mungu alimuwezesha na akamtoa katika tabia hii ya kukashifiwa hadi kwenda kinyume chake. Nao ni wale ambao wanajisubirisha katika nyakati za shida na hawakati tamaa, na wakati wa mazuri, na hawajivuni, na wakafanya mema miongoni mwa mambo ya wajibu na yale yanayopendekezwa. "Hao wana maghufira" juu ya dhambi zao na yatawaondokea kila yanayoepukwa. "Na malipo makubwa;" nayo ni kufuzu kufikia mabustani yenye neema ambayo ndani yake kuna yale ambayo nafsi zinayatamani na macho yanayafurahia.
{فَلَعَلَّكَ تَارِكٌ بَعْضَ مَا يُوحَى إِلَيْكَ وَضَائِقٌ بِهِ صَدْرُكَ أَنْ يَقُولُوا لَوْلَا أُنْزِلَ عَلَيْهِ كَنْزٌ أَوْ جَاءَ مَعَهُ مَلَكٌ إِنَّمَا أَنْتَ نَذِيرٌ وَاللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ (12) أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ قُلْ فَأْتُوا بِعَشْرِ سُوَرٍ مِثْلِهِ مُفْتَرَيَاتٍ وَادْعُوا مَنِ اسْتَطَعْتُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (13) فَإِلَّمْ يَسْتَجِيبُوا لَكُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّمَا أُنْزِلَ بِعِلْمِ اللَّهِ وَأَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ فَهَلْ أَنْتُمْ مُسْلِمُونَ (14)}.
12. Basi labda utaacha baadhi ya yale yaliyofunuliwa kwako, na kifua chako kikaona dhiki kwa hayo, kwa sababu wanasema, "Mbona hakuteremshiwa hazina, au Malaika akaja pamoja naye?" Hakika, wewe ni mwonyaji tu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mtegemewa kwa kila kitu. 13. Au wanasema, "Ameizua?" Sema, "Basi leteni Sura kumi zilizozuliwa mfano wake, na waiteni muwawezao isipokuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni wakweli." 14. Na wasipowaitikia, basi jueni ya kwamba
(hii Qur-ani) imeteremshwa kwa elimu ya Mwenyezi Mungu, na kwamba hakuna mungu isipokuwa Yeye. Basi je, nyinyi ni Waislamu?
#
{12} يقول تعالى مسلياً لنبيه محمد - صلى الله عليه وسلم - عن تكذيب المكذبين: {فلعلَّك تاركٌ بعضَ ما يوحى إليك وضائقٌ به صدرُك أن يقولوا لولا أنزِلَ عليه كنزٌ}؛ أي: لا ينبغي هذا لمثلك؛ أن قولهم يؤثِّر فيك ويصدُّك عما أنت عليه، فتترك بعضَ ما يوحى إليك، ويضيق صدرك لتعنُّتهم بقولهم: {لولا أُنزِلَ عليه كنزٌ أو جاء معه مَلَكٌ}: فإنَّ هذا القول ناشئ من تعنُّتٍ وظلم وعنادٍ وضلالٍ وجهلٍ بمواقع الحجج والأدلَّة؛ فامضِ على أمرك، ولا تصدَّك هذه الأقوالُ الركيكةُ التي لا تصدُرُ إلا من سفيهٍ، ولا يضيق لذلك صدرك؛ فهل أوردوا عليك حجَّة لا تستطيع حلَّها؟! أم قدحوا ببعض ما جئت به قدحاً يؤثِّر فيه وينقص قدره فيضيق صدرك لذلك؟! أم عليك حسابُهم ومُطَالَبٌ بهدايتهم جبراً؟! {إنما أنت نذيرٌ والله على كلِّ شيءٍ وكيلٌ}: فهو الوكيل عليهم، يحفظُ أعمالهم، ويجازيهم بها أتمَّ الجزاء.
{12} Yeye Mtukufu anasema akimliwaza Mtume wake Muhammad -rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie -
kukadhibisha kwa wakadhibishaji: "Basi labda utaacha baadhi ya yale yaliyofunuliwa kwako, na kifua chako kikaona dhiki kwa hayo, kwa sababu wanasema, "Mbona hakuteremshiwa hazina." Yaani, hili halimfailii mfano wako, kwamba maneno yao yanakushawishi na yanakuzuia na yale uliyo juu yake, basi ukayaacha baadhi ya yale yanayoteremshwa kwako, na moyo wako ukaona dhiki kwa sababu ya ukaidi wao juu ya kusema kwao “Mbona hakuteremshiwa hazina, au Malaika akaja pamoja naye?" Kwa maana, maneno haya yanatokana na ukaidi, na udhalimu, usugu, na upotofu, na kutojua pahali pa hoja na ushahidi. Kwa hivyo, endelea na jambo lako wala zisikuzuie kauli dhaifu ambazo hazitoki isipokuwa kwa mpumbavu tu, wala kisione kifua chako dhiki juu yake. Kwani je, walikuletea hoja yoyote ambayo huwezi kuibatilisha? Au walitia doa baadhi ya yale uliyokuja nayo kwa doa ambalo linaathiri ndani yake na kupunguza hadhi yake ndiyo kikakubana kifua chako kwa sababu ya hilo? Au ni juu yako hesabu yao na kwamba unalazimika kuwaongoa kwa nguvu? "Hakika, wewe ni mwonyaji tu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mtegemewa kwa kila kitu." Basi Yeye ndiye mlinzi juu yao, na anayahifadhi matendo yao, na atawalipa ujira kamili zaidi.
#
{13} {أم يقولون افتراه}؛ أي: افترى محمدٌ هذا القرآن، فأجابهم بقوله: {قلْ}: لهم: {فأتوا بعشر سورٍ مثله مفتريات وادعوا مَنِ استَطَعْتُم من دون الله إن كنتُم صادقين}؛ أي: إنه قد افتراه؛ فإنَّه لا فرق بينكم وبينه في الفصاحة والبلاغة، وأنتُم الأعداء حقًّا الحريصون بغاية ما يمكنكم على إبطال دعوته فإن كنتم صادقين فأتوا بعشر سورٍ مثله مفتريات!
{13} "Au wanasema: "Ameizua?" Yaani, Muhammad ameizua hii Qur’ani, kwa hivyo akawajibu kwa kauli yake, "Sema" ukiwaambia, "Basi leteni Sura kumi zilizozuliwa mfano wake, na waiteni muwawezao isipokuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni wakweli." Yaani, ikiwa ni ukweli kwamba ameizua. Kwani, hakuna tofauti baina yenu na yeye katika ufasaha na usemi mzuri, na tena nyinyi ni maadui wa kweli, mnaofanya bidii kiasi muwezavyo kuubatilisha wito wake. Kwa hivyo, ikiwa nyinyi ni wakweli, basi leteni Sura kumi za kuzuliwa mfano wake!
#
{14} {فإن لم يستجيبوا لكم}: على شيءٍ من ذلكم، {فاعلموا أنَّما أنزِلَ بعلم الله}: من عند الله ؛ لقيام الدليل والمقتضي وانتفاء المعارِض. {وأن لا إله إلا هو}؛ أي: واعلموا أنه لا إله إلا هو؛ أي: هو [وحده] المستحقُّ للألوهيَّة والعبادة. {فهل أنتم مسلمونَ}؛ أي: منقادون لألوهيته، مستسلمون لعبوديته.
وفي هذه الآيات إرشادٌ إلى أنه لا ينبغي للدَّاعي إلى الله أن يصدَّه اعتراضُ المعترضين ولا قدحُ القادحين، خصوصاً إذا كان القدح لا مستندَ له ولا يقدح فيما دعا إليه، وأنه لا يضيق صدرُه، بل يطمئنُّ بذلك، ماضياً على أمره، مقبلاً على شأنه، وأنه لا يجب إجابة اقتراحات المقترحين للأدلَّة التي يختارونها، بل يكفي إقامةُ الدليل السالم عن المعارض على جميع المسائل والمطالب.
وفيها: أن هذا القرآن معجِزٌ بنفسه، لا يقدر أحدٌ من البشر أن يأتي بمثله، ولا بعشر سورٍ مثله، بل ولا بسورة من مثله؛ لأنَّ الأعداء البلغاء الفصحاء تحدَّاهم الله بذلك، فلم يعارضوه؛ لعلمهم أنَّهم لا قدرة فيهم على ذلك.
وفيها: أن مما يُطْلَبُ فيه العِلْمُ ولا يكفي غلبةَ الظنِّ، علمُ القرآن وعلمُ التوحيد؛ لقوله تعالى: {فاعلموا أنَّما أنزل بعلم الله وأن لا إله إلا هو}.
{14} "Na wasipowaitikia" juu ya lolote katika hayo, "basi jueni ya kwamba
(Qur-ani hii) imeteremshwa kwa elimu ya Mwenyezi Mungu" kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu, ushahidi unaohitaji hilo ulikwisha simama, na kizuizi kwamba hakuna upinzani wowote juu ya hilo, "na kwamba hakuna mungu isipokuwa Yeye." Yaani, jueni kwamba hakuna mungu isipokuwa Yeye. Yaani, Yeye peke yake ndiye anayestahiki uungu na kuabudiwa. "Basi je, nyinyi ni Waislamu?" Yaani, mmefuata uungu Wake, kujisalimisha kwa uja kwake. Katika aya hizi kuna mwongozo kwamba mwenye kulingania kwa Mwenyezi Mungu hafai kuzuiliwa na pingamizi za wale wanaompinga au kashfa za wanaomkosoa, hasa ikiwa kashfa hiyo haina msingi wowote, na haitii doa katika kile anachokiitia. Na kwamba, moyo wake usiwe na dhiki, bali atulie na hilo, na aendelee na jambo lake, na aelekee kwa mambo yake. Na kwamba, si lazima kuitikia mapendekezo ya wanaopendekeza kwa ushahidi wanaouchagua wao. Bali inatosha tu kusimamisha ushahidi ulio salama kutokana na upinzani wowote juu ya masuala na madai yote. Na ndani yake kuna kwamba Qur-ani hii ni muujiza yenyewe. Kwa sababu, hakuna yeyote anayeweza kuleta mfano wake wala sura kumi mfano wake, bali sura moja mfano wake. Kwa sababu, maadui wenye usemi bora zaidi na ufasaha, Mwenyezi Mungu aliwapa changamoto ya kufanya hivyo, lakini hawakumpinga. Kwa sababu, walijua kwamba hawana uwezo wa kufanya hivyo. Na ndani yake kuna kwamba, miongoni mwa mambo ambayo elimu yake inatafutwa na kwamba kuna tu na dhana kubwa ju yake haitoshi, ni elimu ya Qur-ani na elimu ya tauhidi. Kwa sababu ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, "basi jueni ya kwamba,
(Qur-ani hii) imeteremshwa kwa elimu ya Mwenyezi Mungu, na kwamba hakuna mungu isipokuwa Yeye."
{مَنْ كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَالَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لَا يُبْخَسُونَ (15) أُولَئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ إِلَّا النَّارُ وَحَبِطَ مَا صَنَعُوا فِيهَا وَبَاطِلٌ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (16)}.
15. Yule ambaye anataka uhai wa dunia na mapambo yake, tutawalipa humo matendo yao kamili. Na wao humo hawatapunjwa. 16. Hao ndio ambao hawana kitu katika Akhera isipokuwa Moto, na yataharibika yale waliyoyafanya humo, na yatabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.
#
{15} يقول تعالى: {من كان يريد الحياة الدُّنيا وزينتَها}؛ أي: كلُّ إرادته مقصورةٌ على الحياة الدُّنيا وعلى زينتها من النساء والبنين والقناطير المقنطرة من الذهب والفضة والخيل المسوَّمة والأنعام والحرث، قد صرف رغبته وسعيَهُ وعملَهُ في هذه الأشياء، ولم يجعلْ لدار القرار من إرادته شيئاً؛ فهذا لا يكون إلا كافراً؛ لأنَّه لو كان مؤمناً؛ لكان ما معه من الإيمان يمنعُه أن تكون جميع إرادتِهِ للدار الدُّنيا، بل نفس إيمانه وما تيسَّر له من الأعمال أثرٌ من آثار إرادتِهِ الدارَ الآخرة، ولكنْ، هذا الشقيُّ الذي كأنه خُلِقَ للدنيا وحدها، {نوفِّ إليهم أعمالهم فيها}؛ أي: نعطيهم ما قُسِمَ لهم في أمِّ الكتاب من ثواب الدُّنيا. {وهم فيها لا يُبْخَسون}؛ أي: لا يُنْقَصون شيئاً مما قُدِّرَ لهم، ولكنْ هذا منتهى نعيمهم.
{15} Yeye Mtukufu Anasema, "Yule ambaye anataka uhai wa dunia na mapambo yake." Yaani, utashi wake wote umefungika tu katika uhai wa dunia hii na mapambo yake, kama vile wanawake, watoto, na mirundi ya dhahabu na fedha, na farasi asili, na mifugo, na mashamba, ambaye ameuelekeza utashi wake na bidii yake na matendo yake kwa mambo haya, na wala hakuipa nyumba ya makazi ya kudumu chochote katika utashi wake; basi huyu hawi isipokuwa kafiri. Kwa sababu, kama angekuwa Muumini, basi Imani ambayo anayo ingemzuia kufanya utashi wake wote kuwa juu ya nyumba hii ya duniani. Bali imani yake yenyewe na vitendo alivyoweza kufanya kwa wepesi ni athari miongoni mwa kutaka kwake nyumba ya akhera. Lakini huyu aliyemo mashakani ambaye ni kana kwamba aliumbwa kwa ajili ya dunia hii peke yake, "tutawalipa humo matendo yao kamili." Yaani, tutawapa yale waliyogawiwa katika Kitabu Kikuu miongoni mwa malipo ya kidunia. "Na wao humo hawatapunjwa," yaani, hawatapunguzwa chochote katika yale waliyoandikiwa, lakini huu ndio mwisho wa starehe zao.
#
{16} {أولئك الذين ليس لهم في الآخرة إلاَّ النارُ}: خالدين فيها أبداً، لا يفتر عنهم العذاب، وقد حرموا جزيل الثواب. {وحَبِطَ ما صنعوا فيها}؛ أي: في الدنيا؛ أي: بطل، واضمحلَّ ما عملوه مما يكيدون به الحقَّ وأهله، وما عملوه من أعمال الخير التي لا أساس لها، ولا وجود لشرطها وهو الإيمان.
{16} "Hao ndio ambao hawana kitu katika Akhera isipokuwa Moto" Watadumu humo milele, na wala hawatapumzishwa adhabu, na tayari walikwisha nyimwa malipo makubwa. "Na yataharibika yale waliyoyafanya humo;" yaani, katika dunia. Yaani, yataharibika na kupotelea mbali yale waliyoyafanya miongoni mwa yale wanayoihadaa kwayo haki na watu wake, na yale waliyoyafanya ya heri ambayo hayana msingi, na wala hayana sharti lake ambayo ni imani.
{أَفَمَنْ كَانَ عَلَى بَيِّنَةٍ مِنْ رَبِّهِ وَيَتْلُوهُ شَاهِدٌ مِنْهُ وَمِنْ قَبْلِهِ كِتَابُ مُوسَى إِمَامًا وَرَحْمَةً أُولَئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ وَمَنْ يَكْفُرْ بِهِ مِنَ الْأَحْزَابِ فَالنَّارُ مَوْعِدُهُ فَلَا تَكُ فِي مِرْيَةٍ مِنْهُ إِنَّهُ الْحَقُّ مِنْ رَبِّكَ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ (17)}.
17. Basi je, yule ambaye ana ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wake Mlezi, na unaofuatwa na shahidi anayetoka kwake, na kabla yake kilikuwapo Kitabu cha Musa kilichokuwa mwongozi na rehema. Hao wanaiamini. Naye anayeikufuru katika makundi, basi Moto ndipo pahali pa miadi yake. Kwa hivyo, usiwe katika shaka juu yake. Hakika, hii ni haki itokayo kwa Mola wako Mlezi, lakini wengi wa watu hawaamini.
#
{17} يذكر تعالى حال رسوله محمد - صلى الله عليه وسلم - ومن قام مقامه من ورثته القائمين بدينه. وحججه الموقنين بذلك، وأنهم لا يوصف بهم غيرهم، ولا يكون أحدٌ مثلهم، فقال: {أفمن كان على بيِّنةٍ من ربِّه}: بالوحي الذي أنزل الله فيه المسائل المهمَّة ودلائلها الظاهرة، فتيقَّن تلك البيِّنة، {ويتلوه}؛ أي: يتلو هذه البينة والبرهان برهانٌ آخرُ، {شاهدٌ منه}: وهو شاهدُ الفطرة المستقيمة والعقل الصحيح، حين شهد حقيقةَ ما أوحاه الله وشَرَعَهُ وعَلِمَ بعقله حُسْنَهُ فازداد بذلك إيماناً إلى إيمانِهِ {و} ثَمَّ شاهدٌ ثالثٌ؛ وهو {كتابُ موسى}: التوراة التي جعلها الله {إماماً} للناس {ورحمةً} لهم، يشهد لهذا القرآن بالصدق ويوافقه فيما جاء به من الحقِّ؛ أي: أفمنْ كان بهذا الوصف، قد تواردتْ عليه شواهدُ الإيمان وقامتْ لديه أدلُة اليقين؛ كمن هو في الظُّلمات والجهالات ليس بخارج منها؟ لا يستوون عند الله ولا عند عباد الله. {أولئك}؛ أي: الذين وفِّقوا لقيام الأدلَّة عندهم، يؤمنون بالقرآن حقيقة، فيثمر لهم إيمانهم كلَّ خيرٍ في الدنيا والآخرة.
{ومن يكفُرْ به}؛ أي: القرآن، {من الأحزاب}؛ أي: سائر طوائف أهل الأرض المتحزِّبة على ردِّ الحق، {فالنار موعده}: لا بدَّ من وروده إليها، {فلا تكُ في مِريةٍ [منه]}؛ أي: في أدنى شكٍّ. {إنَّه الحقُّ من ربِّك ولكنَّ أكثر الناس لا يؤمنون}: إما جهلاً منهم وضلالاً، وإما ظلماً وعناداً وبغياً، وإلاَّ؛ فمن كان قصدُه حسناً وفَهْمُه مستقيماً؛ فلا بدَّ أن يؤمنَ به؛ لأنَّه يرى ما يدعوه إلى الإيمان من كلِّ وجه.
{17} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaitaja hali ya Mtume wake Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - na wale walioshika nafasi yake katika warithi wake ambao wanaisimamisha dini yake, na hoja zake, wale ambao wana yakini na hayo. Na kwamba, hakuna yeyote anayeweza kusifiwa kwa sifa zao na kwamba mtu yeyote hawezi kuwa mfano wao. Akasema, "Basi je, yule ambaye ana ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wake Mlezi" kwa wahyi aliouteremsha Mwenyezi Mungu ukiwa ndani yake na masuala muhimu na ushahidi wake ulio dhahiri, basi akawa na yakini na ushahidi huo ulio wazi, "na unaofuatwa." Yaani, ushahidi huu na hoja hii vikafuatwa na uthibitisho mwingine, ambao ni "na shahidi anayetoka kwake." Naye ni shahidi wa maumbile ya asili yaliyonyooka, na akili timamu, aliposhuhudia kwa uhakika yale aliyoyafunua Mwenyezi Mungu na sheria yake, na akajua kwa akili yake uzuri wake, kwa hivyo akazidi kwa sababu ya hilo imani juu ya imani "na" kisha kuna shahidi wa tatu. Nayo ni "Kitabu cha Musa," Taurati ambayo Mwenyezi Mungu aliifanya kuwa "mwongozi" kwa watu "na rehema" kikiishuhudilia Qur-ani hii kuwa ni ukweli na inaafikiana nayo katika yale iliyokuja nayo ya haki. Yaani, Je, kuna mtu mwenye sifa hizi, ambaye amekuwa akijiwa na ushahidi wa imani na hoja za yakini zikamsimamia, je yeye ni kama yule ambaye yuko katika giza mbalimbali na ujinga mwingi ambavyo hawezi kutoka nje yake? Hawawi sawa kwa Mwenyezi Mungu wala kwa waja wa Mwenyezi Mungu. "Hao;" Yaani, wale ambao waliwezeshwa kusimamiwa na ushahidi, hao wanaiamini Qur’ani kwa uhakika, kwa hivyo imani yao hiyo ikawasababishia heri katika dunia hii na Akhera. "Naye anayeikufuru" yaani, Qur’ani, "katika makundi." Yaani, makundi mengineyo yote ya watu wa ardhi wanaofanya makundi ya kuikataa haki, "basi Moto ndipo pahali pa miadi yake" ni lazima atauingia. "Kwa hivyo, usiwe katika shaka
[juu yake]" yaani, hata shaka kidogo tu. "Hakika, hii ni haki itokayo kwa Mola wako Mlezi, lakini wengi wa watu hawaamini." Ima kwa ujinga wao tu na upotofu, na ima kwa dhuluma, ukaidi, na kuvuka mipaka. Na kama sivyo, mwenye makusudio mazuri na ufahamu wake umenyooka, basi ni lazima aiamini; kwa sababu, anaona kile kinachomwita kwenye imani kutoka kila pembe.
{وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَى عَلَى اللَّهِ كَذِبًا أُولَئِكَ يُعْرَضُونَ عَلَى رَبِّهِمْ وَيَقُولُ الْأَشْهَادُ هَؤُلَاءِ الَّذِينَ كَذَبُوا عَلَى رَبِّهِمْ أَلَا لَعْنَةُ اللَّهِ عَلَى الظَّالِمِينَ (18) الَّذِينَ يَصُدُّونَ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا وَهُمْ بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ (19) أُولَئِكَ لَمْ يَكُونُوا مُعْجِزِينَ فِي الْأَرْضِ وَمَا كَانَ لَهُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ يُضَاعَفُ لَهُمُ الْعَذَابُ مَا كَانُوا يَسْتَطِيعُونَ السَّمْعَ وَمَا كَانُوا يُبْصِرُونَ (20) أُولَئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنْفُسَهُمْ وَضَلَّ عَنْهُمْ مَا كَانُوا يَفْتَرُونَ (21) لَا جَرَمَ أَنَّهُمْ فِي الْآخِرَةِ هُمُ الْأَخْسَرُونَ (22)}.
18. Na ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uongo? Hao wataletwa mbele ya Mola wao Mlezi, na mashahidi watasema, "Hawa ndio waliomdanganyishia Mola wao Mlezi. Sikilizeni! Laana ya Mwenyezi Mungu iwapate madhalimu." 19. Ambao wanazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, na wanaitakia ijipinde, nao wanakufuru Akhera. 20. Hao hawakuwa ni wa kushinda katika ardhi, wala hawana walinzi wowote kando na Mwenyezi Mungu. Watazidishiwa adhabu. Kwa kuwa, hawakuwa wakiweza kusikia wala hawakuwa wakiona. 21. Hao ndio waliozihasiri nafsi zao, na yakawapotea yale waliyokuwa wakiyazua. 22. Hakuna shaka kwamba wao katika Akhera ndio waliohasiri zaidi.
#
{18} يخبر تعالى أنه لا أحد {أظلمُ ممَّن افترى على الله كذباً}: ويدخل في هذا كلُّ من كذب على الله بنسبة الشريك له، أو وَصَفَه بما لا يَليق بجلاله، أو الإخبار عنه بما لم يقلْ، أو ادعاء النبوَّة، أو غير ذلك من الكذب على الله؛ فهؤلاء أعظم الناس ظلماٌ. {أولئك يُعْرَضونَ على ربِّهم}: ليجازِيَهم بظلمهم؛ فعندما يحكُم عليهم بالعقاب الشديد؛ {يقولُ الأشهادُ}؛ أي: الذين شهدوا عليهم بافترائهم وكذبهم: {هؤلاء الذين كَذَبوا على ربِّهم ألا لعنة الله على الظالمين}؛ أي: لعنة لا تنقطع؛ لأنَّ ظلمهم صار وصفاً لهم ملازماً، لا يقبل التخفيف.
{18} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba hakuna yeyote “aliye dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uongo?" Na anaingia katika hili kila mtu anayesema uongo juu ya Mwenyezi Mungu kwa kumnasibishia mshirika, au akamsifu kwa njia isiyoufailia utukufu Wake, au akajulisha juu Yake kwa yale ambayo hakuyasema, au akadai unabii au yasiyokuwa hayo miongoni mwa kumdanganyishia Mwenyezi Mungu. Basi hawa ndio watu madhalimu zaidi. "Hao wataletwa mbele ya Mola wao Mlezi" ili awalipe kwa dhuluma yao. Na atakapowahukumia adhabu kali, "mashahidi watasema;" yaani,
wale waliowashuhudia kuzua kwao na uongo wao: "Hawa ndio waliomdanganyishia Mola wao Mlezi. Sikilizeni! Laana ya Mwenyezi Mungu iwapate madhalimu." Yaani, laana isiyokoma. Kwa sababu, dhuluma yao imekwisha kuwa ni sifa yao isiyowaacha, na haiwezi kupunguzwa.
#
{19} ثم وصف ظلمهم فقال: {الذين يصدُّون عن سبيل الله}: فصدُّوا بأنفسهم عن سبيل الله، وهي سبيل الرسل التي دعوا الناس إليها، وصدُّوا غيرَهم عنها، فصاروا أئمة يدعون إلى النار {ويبغونَها}؛ أي: سبيل الله {عوجاً}؛ أي: يجتهدون في ميلها وتشيينها وتهجينها؛ لتصير عند الناس غير مستقيمة، فيحسِّنون الباطل؛ ويقبِّحون الحقَّ؛ قبَّحهم الله. {وهم بالآخرة هم كافرون}.
19. Kisha akaeleza dhuluma yao hiyo,
akasema: "Ambao wanazuilia njia ya Mwenyezi Mungu" Basi wao wenyewe wakajizuia na njia ya Mwenyezi Mungu. Nayo ni njia ya Mitume ambayo waliwalingania watu kwayo. Na pia waliwazuia wengine dhidi yake. Kwa hivyo, wakawa ni viongozi wanaolingania kwenye Moto "na wanaitakia;" yaani, Njia ya Mwenyezi Mungu "ijipinde." Yaani, wanajitahidi katika kuipinda, kuitia doa, na kuichanganya ili isiwe iliyonyooka kwa watu kwa hivyo wakapendelea batili, na kuichukia haki. Na mwenyezi mungu awalaani. "Nao wanakufuru Akhera."
#
{20} {أولئك لم يكونوا معجزِين في الأرض}؛ أي: ليسوا فائتين الله؛ لأنهم تحت قبضته وفي سلطانه، {وما كان لهم مِن دونِ الله من أولياء}: فيدفعون عنهم المكروهَ أو يحصِّلون لهم ما ينفعهم، بل تقطَّعت بهم الأسباب. {يضاعفُ لهم العذابُ}؛ أي: يغلَّظ ويزداد؛ لأنَّهم ضلوا بأنفسهم وأضلُّوا غيرهم. {ما كانوا يستطيعون السمع}؛ أي: من بغضهم للحقِّ ونفورهم عنه، ما كانوا يستطيعون أن يسمعوا آياتِ الله سماعاً ينتفعون به؛ {فما لهم عن التَّذْكِرَةِ معرضينَ. كأنَّهم حُمُرٌ مُسْتَنفِرَةٌ. فرَّتْ من قَسْوَرة}، {وما كانوا يبصِرون}؛ أي: ينظرون نظر عبرة وتفكُّر فيما ينفعهم، وإنما هم كالصمِّ البكم الذين لا يعقلون.
{20} "Hao hawakuwa ni wa kushinda katika ardhi;" yaani, hawawezi kumkwepa Mwenyezi Mungu; Kwa sababu wao wako katika mshiko wake na katika mamlaka yake, "wala hawana walinzi wowote kando na Mwenyezi Mungu." Basi wanawalinda ili wawazuilie machukizo au wawaletee yenye kuwanufaisha, bali mafungamano yao yalikatika. "Watazidishiwa adhabu;" yaani, watafanyiwa kuwa kali na kuzidishiwa. Kwa sababu walijipoteza wao wenyewe na wakawapoteza wengine, "Kwa kuwa, hawakuwa wakiweza kusikia." Yaani, kwa sababu ya kuchukia kwao haki na kujiweka kwao mbali nayo, hawakuweza kuzisikia Aya za Mwenyezi Mungu kusikia kwa kuwanufaisha. "Basi wana nini hata wanapuuza ukumbusho huu? Kama kwamba wao ni mapunda waliotimuliwa. Wanaomkimbia simba!" "Wala hawakuwa wakiona." Yaani, kuona kwa kuzingatia, na kutafakari juu ya yale yatakayowanufaisha, lakini wao ni kama viziwi, mabubu ambao hawatumii akili.
#
{21} {أولئك الذين خسروا أنفسهم}: حيث فوَّتوها أعظم الثواب واستحقُّوا أشدَّ العذاب، {وضلَّ عنهم ما كانوا يفترون}؛ أي: اضمحلَّ دينُهم الذي يدعون إليه ويحسِّنونه، ولم تغنِ عنهم آلهتُهم التي يعبدون من دون الله لمَّا جاء أمرُ ربِّك.
{21} "Hao ndio waliozihasiri nafsi zao" kwa kuwa walizikosesha malipo makubwa zaidi, na wakastahiki adhabu kali kabisa, "na yakawapotea yale waliyokuwa wakiyazua." Yaani, ilipotea Dini yao hiyo ambayo wanailingania na kuichukulia kuwa nzuri. na miungu yao wanayoiabudu badala ya Mwenyezi Mungu haikuwafaa kitu ilipokuja amri ya Mola wako Mlezi.
#
{22} {لا جرم}؛ أي: حقًّا وصدقاً، {أنهم في الآخرة هم الأخسرون}: حصر الخسار فيهم، بل جعل لهم منه أشدَّه؛ لشدة حسرتهم وحرمانهم وما يعانون من المشقَّة من العذاب، فنستجير بالله من حالهم.
{22} "Hakuna shaka;" Yaani, kwa haki na ukweli "kwamba wao katika Akhera ndio waliohasiri zaidi," na hasara ilifungiwa kwao tu. Bali aliwafanyia kubwa yake zaidi, kwa sababu ya ukubwa wa majuto yao, na kunyimwa kwao, na magumu wanayoyapata kutokana na adhabu. Basi tunatafuta kimbilio kwa Mwenyezi Mungu kutokana na hali yao hiyo.
Na alipotaja hali ya walio mashakani, Akataja sifa za waliofikia furaha, na malipo waliyo nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Akasema:
{إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَأَخْبَتُوا إِلَى رَبِّهِمْ أُولَئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ (23) مَثَلُ الْفَرِيقَيْنِ كَالْأَعْمَى وَالْأَصَمِّ وَالْبَصِيرِ وَالسَّمِيعِ هَلْ يَسْتَوِيَانِ مَثَلًا أَفَلَا تَذَكَّرُونَ (24)}.
23. Hakika, wale walioamini, na wakatenda mema, na wakanyenyekea kwa Mola wao Mlezi, hao ndio wenza wa Pepo, humo watadumu. 24. Mfano wa makundi mawili haya ni kama kipofu na kiziwi, na mwenye kuona na anayesikia. Je, wawili hawa wanakuwa sawa kwa kufananishwa? Basi, je, hamkumbuki?
#
{23} يقول تعالى: {إنَّ الذين آمنوا}: بقلوبهم؛ أي: صدقوا واعترفوا لما أمر الله بالإيمان به من أصول الدين وقواعده، {وعملوا الصالحات}: المشتملة على أعمال القلوب والجوارح وأقوال اللسان، {وأخْبَتوا إلى ربِّهم}؛ أي: خضعوا له واستكانوا لعظمته وذلوا لسلطانه، وأنابوا إليه بمحبته وخوفه ورجائه والتضرُّع إليه. {أولئك}: الذين جمعوا تلك الصفات، {أصحابُ الجنة هم فيها خالدون}: لأنهم لم يتركوا من الخير مطلباً إلا أدركوه، ولا خيراً إلا سَبَقوا إليه.
{23} Yeye Mtukufu anasema: "Hakika, wale walioamini" kwa nyoyo zao; yaani, walisadiki na wakakiri yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu kuamini katika misingi ya Dini na kanuni zake, "na wakatenda mema" yanayojumuisha matendo ya nyoyo na viungo na maneno ya ulimi, "na wakanyenyekea kwa Mola wao Mlezi." Yaani, walimnyenyekea, wakasalimu amri kwa sababu ya ukuu Wake, na wakajidhalilisha kwa sababu ya mamlaka yake, na wakamrudia kwa upendo, hofu, matumaini, na kumwomba dua Kwa unyenyekevu. "Hao" ambao walikusanya sifa hizo "hao ndio wenza wa Pepo, humo watadumu" kwa sababu hawakuacha njia ya kutafuta heri isipokuwa waliishika, wala heri yoyote isipokuwa waliikimbilia.
#
{24} {مَثَلُ الفريقين}؛ أي: فريق الأشقياء وفريق السعداء، {كالأعمى والأصمِّ}: هؤلاء الأشقياء. {والبصير والسميع}: مَثَل السعداء. {هل يستويان مثلاً}؟ لا يستوون مثلاً، بل بينهما من الفَرْق ما لا يأتي عليه الوصف. {أفلا تَذَكَّرون}: الأعمال التي تنفعكم فتفعلونها، والأعمال التي تضرُّكم فتتركونها.
{24} "Mfano wa makundi mawili haya;" yaani, kundi la walio mashakani na kundi la walio katika furaha, {ni kama kipofu na kiziwi." Hawa ndio walio mashakani. "Na mwenye kuona anayesikia" ndio mfano wa walio katika furaha. "Je, wawili hawa wanakuwa sawa kwa kufananishwa?" Wao si sawa kwa kufananishwa, lakini kati yao kuna tofauti ambayo haiwezi kuelezewa. "Basi, je, hamkumbuki?" matendo yenye kuwanufaisha basi mkayafanya, na matendo yenye kuwadhuru, basi mkayaacha.
{وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَى قَوْمِهِ إِنِّي لَكُمْ نَذِيرٌ مُبِينٌ (25) أَنْ لَا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّهَ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ أَلِيمٍ (26) فَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ قَوْمِهِ مَا نَرَاكَ إِلَّا بَشَرًا مِثْلَنَا وَمَا نَرَاكَ اتَّبَعَكَ إِلَّا الَّذِينَ هُمْ أَرَاذِلُنَا بَادِيَ الرَّأْيِ وَمَا نَرَى لَكُمْ عَلَيْنَا مِنْ فَضْلٍ بَلْ نَظُنُّكُمْ كَاذِبِينَ (27) قَالَ يَاقَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِنْ كُنْتُ عَلَى بَيِّنَةٍ مِنْ رَبِّي وَآتَانِي رَحْمَةً مِنْ عِنْدِهِ فَعُمِّيَتْ عَلَيْكُمْ أَنُلْزِمُكُمُوهَا وَأَنْتُمْ لَهَا كَارِهُونَ (28) وَيَاقَوْمِ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مَالًا إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى اللَّهِ وَمَا أَنَا بِطَارِدِ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّهُمْ مُلَاقُو رَبِّهِمْ وَلَكِنِّي أَرَاكُمْ قَوْمًا تَجْهَلُونَ (29) وَيَاقَوْمِ مَنْ يَنْصُرُنِي مِنَ اللَّهِ إِنْ طَرَدْتُهُمْ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ (30) وَلَا أَقُولُ لَكُمْ عِنْدِي خَزَائِنُ اللَّهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ إِنِّي مَلَكٌ وَلَا أَقُولُ لِلَّذِينَ تَزْدَرِي أَعْيُنُكُمْ لَنْ يُؤْتِيَهُمُ اللَّهُ خَيْرًا اللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا فِي أَنْفُسِهِمْ إِنِّي إِذًا لَمِنَ الظَّالِمِينَ (31) قَالُوا يَانُوحُ قَدْ جَادَلْتَنَا فَأَكْثَرْتَ جِدَالَنَا فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِنْ كُنْتَ مِنَ الصَّادِقِينَ (32) قَالَ إِنَّمَا يَأْتِيكُمْ بِهِ اللَّهُ إِنْ شَاءَ وَمَا أَنْتُمْ بِمُعْجِزِينَ (33) وَلَا يَنْفَعُكُمْ نُصْحِي إِنْ أَرَدْتُ أَنْ أَنْصَحَ لَكُمْ إِنْ كَانَ اللَّهُ يُرِيدُ أَنْ يُغْوِيَكُمْ هُوَ رَبُّكُمْ وَإِلَيْهِ {تُرْجَعُونَ (34) أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ قُلْ إِنِ افْتَرَيْتُهُ فَعَلَيَّ إِجْرَامِي وَأَنَا بَرِيءٌ مِمَّا تُجْرِمُونَ (35) وَأُوحِيَ إِلَى نُوحٍ أَنَّهُ لَنْ يُؤْمِنَ مِنْ قَوْمِكَ إِلَّا مَنْ قَدْ آمَنَ فَلَا تَبْتَئِسْ بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ (36) وَاصْنَعِ الْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا وَوَحْيِنَا وَلَا تُخَاطِبْنِي فِي الَّذِينَ ظَلَمُوا إِنَّهُمْ مُغْرَقُونَ (37) وَيَصْنَعُ الْفُلْكَ وَكُلَّمَا مَرَّ عَلَيْهِ مَلَأٌ مِنْ قَوْمِهِ سَخِرُوا مِنْهُ قَالَ إِنْ تَسْخَرُوا مِنَّا فَإِنَّا نَسْخَرُ مِنْكُمْ كَمَا تَسْخَرُونَ (38) فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَنْ يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَيَحِلُّ عَلَيْهِ عَذَابٌ مُقِيمٌ (39) حَتَّى إِذَا جَاءَ أَمْرُنَا وَفَارَ التَّنُّورُ قُلْنَا احْمِلْ فِيهَا مِنْ كُلٍّ زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ وَأَهْلَكَ إِلَّا مَنْ سَبَقَ عَلَيْهِ الْقَوْلُ وَمَنْ آمَنَ وَمَا آمَنَ مَعَهُ إِلَّا قَلِيلٌ (40) وَقَالَ ارْكَبُوا فِيهَا بِسْمِ اللَّهِ مَجْرَاهَا وَمُرْسَاهَا إِنَّ رَبِّي لَغَفُورٌ رَحِيمٌ (41) وَهِيَ تَجْرِي بِهِمْ فِي مَوْجٍ كَالْجِبَالِ وَنَادَى نُوحٌ ابْنَهُ وَكَانَ فِي مَعْزِلٍ يَابُنَيَّ ارْكَبْ مَعَنَا وَلَا تَكُنْ مَعَ الْكَافِرِينَ (42) قَالَ سَآوِي إِلَى جَبَلٍ يَعْصِمُنِي مِنَ الْمَاءِ قَالَ لَا عَاصِمَ الْيَوْمَ مِنْ أَمْرِ اللَّهِ إِلَّا مَنْ رَحِمَ وَحَالَ بَيْنَهُمَا الْمَوْجُ فَكَانَ مِنَ الْمُغْرَقِينَ (43) وَقِيلَ يَاأَرْضُ ابْلَعِي مَاءَكِ وَيَاسَمَاءُ أَقْلِعِي وَغِيضَ الْمَاءُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ وَاسْتَوَتْ عَلَى الْجُودِيِّ وَقِيلَ بُعْدًا لِلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ (44) وَنَادَى نُوحٌ رَبَّهُ فَقَالَ رَبِّ إِنَّ ابْنِي مِنْ أَهْلِي وَإِنَّ وَعْدَكَ الْحَقُّ وَأَنْتَ أَحْكَمُ الْحَاكِمِينَ (45) قَالَ يَانُوحُ إِنَّهُ لَيْسَ مِنْ أَهْلِكَ إِنَّهُ عَمَلٌ غَيْرُ صَالِحٍ فَلَا تَسْأَلْنِ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ إِنِّي أَعِظُكَ أَنْ تَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ (46) قَالَ رَبِّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ أَنْ أَسْأَلَكَ مَا لَيْسَ لِي بِهِ عِلْمٌ وَإِلَّا تَغْفِرْ لِي وَتَرْحَمْنِي أَكُنْ مِنَ الْخَاسِرِينَ (47) قِيلَ يَانُوحُ اهْبِطْ بِسَلَامٍ مِنَّا وَبَرَكَاتٍ عَلَيْكَ وَعَلَى أُمَمٍ مِمَّنْ مَعَكَ وَأُمَمٌ سَنُمَتِّعُهُمْ ثُمَّ يَمَسُّهُمْ مِنَّا عَذَابٌ أَلِيمٌ (48) تِلْكَ مِنْ أَنْبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهَا إِلَيْكَ مَا كُنْتَ تَعْلَمُهَا أَنْتَ وَلَا قَوْمُكَ مِنْ قَبْلِ هَذَا فَاصْبِرْ إِنَّ الْعَاقِبَةَ لِلْمُتَّقِينَ (49)}.
25. Na hakika, tulimtuma Nuhu kwa kaumu yake, akawaambia, "Hakika mimi ni mwonyaji aliye wazi kwenu." 26. Ya kwamba msimuabudu isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. Hakika mimi ninawahofia adhabu ya Siku Chungu. 27. Basi wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake, "Hatukuoni wewe isipokuwa ni mtu tu mfano wetu, wala hatukuoni wamekufuata isipokuwa wale wetu walio duni, watu wasiokuwa na maoni. Wala hatuwaoni nyinyi kuwa mna ubora wowote kutushinda sisi. Bali tunawadhania nyinyi kuwa ni waongo." 28. Akasema, "Enyi kaumu yangu! Hebu fikirini! Ikiwa mimi ninayo hoja wazi iliyotoka kwa Mola wangu Mlezi, na amenipa rehema kutoka kwake, nayo ikafichwa kwenu. Je, tuwalazimishe kuikubali ilhali nyinyi mnaichukia?" 29. "Na enyi kaumu yangu! Mimi siwaombi mali kwa ajili ya haya. Mimi sina ujira isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu; na mimi sitawafukuza walioamini. Hakika wao watakutana na Mola wao Mlezi, lakini mimi nawaona mnafanya ujinga. 30. Na enyi kaumu yangu! Ni nani atakayeninusuru kwa Mwenyezi Mungu nikiwafukuza hawa? Basi je, hamkumbuki? 31. Wala siwaambii kuwa nina hazina za Mwenyezi Mungu, wala kuwa mimi ninajua mambo ya ghaibu,
wala sisemi: Mimi ni Malaika. Wala sisemi kuhusu wale ambao yanawadharau macho yenu kuwa Mwenyezi Mungu hatawapa heri. Mwenyezi Mungu ndiye anayajua zaidi yaliyo katika nafsi zao. Hapo bila ya shaka nitakuwa miongoni mwa madhalimu. 32. Wakasema, "Ewe Nuhu! Umejadiliana nasi, na umekithirisha kutujadili. Basi tuletee hayo unayotuahidi, ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli." 33. Akasema, "Hakika Mwenyezi Mungu tu ndiye atakayewaletea akipenda. Wala nyinyi si wenye kumshinda." 34. "Wala nasaha yangu haitawafaa kitu nikitaka kuwanasihi, ikiwa Mwenyezi Mungu anataka kuwapoteza. Yeye ndiye Mola wenu Mlezi, na kwake mtarejeshwa." 35. Au ndio wanasema, "Ameizua?" Sema, "Ikiwa nimeizua, basi kosa hilo ni juu yangu, na mimi niko mbali sana na makosa myatendayo." 36. Na akafunuliwa Nuhu akaambiwa, "Hataamini yeyote katika kaumu yako isipokuwa wale waliokwisha amini. Basi usisikitike kwa yale waliyokuwa wakiyatenda." 37. "Na unda jahazi mbele ya macho yetu na kwa mujibu wa ufunuo wetu. Wala usiniongeleshe kuwatetea wale waliodhulumu. Kwani hao bila ya shaka watazamishwa." 38. Na akawa anaunda jahazi, na kila walipopita karibu nayo wakuu kutoka kwa kaumu yake, wanamkejeli. Yeye akasema, "Ikiwa nyinyi mnatukejeli, basi sisi pia tunawakejeli kama mnavyotukejeli." 39. "Nanyi mtakuja jua ni nani itakayemfikia adhabu ya kumhizi, na itakayemteremkia adhabu ya kudumu." 40. Mpaka ilipokuja amri yetu, na tanuri ikafoka maji, tulisema, "Pakia humo katika kila kitu, jozi mbili ya dume na jike, na ahali zako, isipokuwa wale ambao imekwisha wapitia hukumu, na watu walioamini." Na hawakuamini pamoja naye isipokuwa wachache tu. 41. Na akasema, "Pandeni humo kwa Bismillahi
(Kwa Jina la Mwenyezi Mungu), kwenda kwake na kusimama kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." 42. Ikawa inakwenda nao katika mawimbi kama milima.
Na Nuhu akamwita mwanawe naye alikuwa mbali: Ewe mwanangu! Panda pamoja nasi, wala usiwe pamoja na makafiri. 43.
Akasema: Nitakimbilia mlimani unilinde na maji.
(Nuhu) akasema: Leo hakuna wa kulindwa na amri ya Mwenyezi Mungu isipokuwa yule aliyemrehemu mwenyewe. Na wimbi likawatenganisha, basi akawa katika waliozama. 44.
Na ikasemwa: Ewe ardhi! Meza maji yako. Na Ewe mbingu! Jizuie. Basi maji yakadidimia chini, na amri hiyo ikapitishwa, na
(jahazi) likasimama juu ya
(mlima) wa Al Juudiy.
Na ikasemwa: Wapotelee mbali kaumu madhalimu! 45.
Na Nuhu alimwomba Mola wake Mlezi: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mwanangu ni katika ahali zangu, na hakika ahadi yako ndiyo ya haki. Na Wewe ndiye hakimu bora zaidi ya mahakimu wote. 46.
Akasema: Ewe Nuhu! Huyu si katika ahali zako. Hakika yeye mwendo wake si mwema. Basi usiniombe jambo usilo na elimu nalo. Mimi nakuwaidhi usije ukawa miongoni mwa wajinga. 47.
Nuhu akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Mimi najikinga kwako nikuombe nisilo na elimu nalo. Na kama hunisamehe na ukanirehemu, nitakuwa katika waliohasiri. 48.
Ikasemwa: Ewe Nuhu! Shuka kwa salama itokayo kwetu, na baraka nyingi juu yako na juu ya umma miongoni mwa wale walio pamoja nawe. Na zitakuwapo umma tutakazozistarehesha, na kisha zitaguswa na adhabu chungu itokayo kwetu. 49. Hizi ni katika habari za ghaibu tunazokufunulia. Hukuwa ukizijua wewe, wala kaumu yako, kabla ya haya. Basi subiri! Hakika Mwisho ni wa wachamungu.
#
{25} أي: {ولقد أرسلْنا نوحاً}: أول المرسلين {إلى قومه}: يدعوهم إلى الله وينهاهم عن الشرك، فقال: {إني لكم نذيرٌ مبينٌ}؛ أي: بينتُ لكم ما أنذرتكم به بياناً زال به الإشكال.
{25} Yaani, "Na hakika tulimtuma Nuhu" ambaye alikuwa Mtume wa kwanza "kwa kaumu yake" akiwalingania kwa Mwenyezi Mungu na akiwakataza ushirikina. Akasema, "Hakika mimi kwenu ni mwonyaji aliye wazi." Yaani, niliwabainishia yale niliyowaonya kwa ubainisho ulioondoa mchanganyiko wote.
#
{26} {أن لا تعبُدوا إلاَّ الله}؛ أي: أخلصوا العبادة لله وحده، واتركوا كلَّ ما يُعبد من دون الله. {إني أخافُ عليكم عذابَ يوم أليم}: إنْ لم تقوموا بتوحيد الله وتطيعوني.
{26} "Ya kwamba msimuabudu isipokuwa Mwenyezi Mungu tu." Yaani, mfanyieni ibada Mwenyezi Mungu peke yake, na acheni kila kinachoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu. "Hakika mimi ninawahofia adhabu ya Siku Chungu" ikiwa hamtampwekesha Mwenyezi Mungu na mkanitii mimi.
#
{27} {فقال الملأ الذين كَفَروا من قومِهِ}؛ أي: الأشراف والرؤساء رادِّين لدعوة نوح عليه السلام كما جَرَتِ العادة لأمثالهم أنَّهم أول مَن ردَّ دعوة المرسلين {ما نراك إلا بشراً مثلَنا}: وهذا مانعٌ بزعمهم عن اتِّباعه، مع أنه في نفس الأمر هو الصوابُ الذي لا ينبغي غيره؛ لأنَّ البشر يتمكَّن البشرُ أن يتلقَّوا عنه ويراجعوه في كلِّ أمرٍ؛ بخلاف الملائكة. {وما نراك اتَّبعك إلا الذين هم أراذِلُنا}؛ أي: ما نرى اتَّبعك منَّا إلا الأراذلُ والسَّفَلة ـ بزعمهم ـ وهم في الحقيقة الأشرافُ وأهل العقول، الذين انقادوا للحقِّ، ولم يكونوا كالأراذل الذين يُقال لهم: الملأ، الذين اتَّبعوا كل شيطان مَريدٍ، واتَّخذوا آلهة من الحجر والشجر يتقرَّبون إليها ويسجدون لها؛ فهل ترى أرذل من هؤلاء وأخس؟! وقولهم: {بادِيَ الرأي}؛ أي: إنما اتَّبعوك من غير تفكُّر ورويَّة، بل بمجرَّد ما دعوتهم اتَّبعوك؛ يعنون بذلك أنهم ليسوا على بصيرةٍ من أمرهم، ولم يعلموا أنَّ الحقَّ المبينَ تدعو إليه بداهةُ العقول، وبمجرَّد ما يصل إلى أولي الألباب يعرفونه ويتحقَّقونه، لا كالأمور الخفيَّة التي تحتاج إلى تأمُّل وفكر طويل. {وما نرى لكم علينا من فضل}؛ أي: لستم أفضل منا فننقادُ لكم، {بل نظنُّكم كاذبين}: وكذبوا في قولهم هذا؛ فإنَّهم رأوا من الآيات التي جعلها الله مؤيِّدة لنوح ما يوجِبُ لهم الجزم التامَّ على صدقه.
{27} "Basi wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake." Yaani watukufu na viongozi wakiukataa wito wa Nuhu, amani iwe juu yake, kama ilivyokuwa desturi ya mfano wao baada yao kwamba wao ndio waliokuwa wa kwanza kukataa wito wa Mitume, “Hatukuoni wewe isipokuwa ni mtu tu mfano wetu" na hiki ni kizuizi dhidi ya kumfuata kulingana na madai yao ingawa katika jambo hilo lenyewe ndilo lililo sahihi ambalo halifai linginelo. Kwa sababu wanadamu wenzake wanaweza kujifunza kutoka kwake na kutafuta ushauri wake katika kila jambo, tofauti na malaika. "Wala hatukuoni wamekufuata isipokuwa wale wetu walio duni." Yaani, hatuoni yeyote miongoni mwetu akikufuata isipokuwa wadhalilifu watu duni sana - kulingana na madai yao - na kiuhakika wao ndio watukufu na watu wenye akili, ambao waliifuata haki, na hawakuwa kama watu wadharauliwao ambao wanaitwa 'wakuu' ambao walimfuata kila shetani aliyeasi, na wakajichukulia miungu ya mawe na miti wakijikurubisha kwayo na wakiisujudia. Je,
unadhani kuna mdharauliwa zaidi kuliko hao walio duni mno? Na kauli yao: "Watu wasiokuwa na maoni;" yaani, walikufuata tu bila ya kufikiria wala kuangalia. Bali mara tu ulipowaita, wakakufuata. Wanachomaanisha kwa hayo ni kuwa hao hawana ufahamu wa mambo yao, lakini hawakujua kwamba haki iliyo wazi zinaita kwayo akili za kawaida, na mara tu inapowafikia wenye ufahamu mkubwa, wanaijua na wanaithibitisha. Si kama mambo yaliyofichikana ambayo yanahitaji kuyaangalia na kutafakari kwa kurefu. "Wala hatuwaoni nyinyi kuwa mna ubora wowote kutushinda sisi." Yaani, nyinyi si bora kutuliko ili tuwafuate. "Bali tunawadhania nyinyi kuwa ni waongo." Lakini walisema uongo katika kauli yao hii. Kwa maana, waliona ishara nyingi ambazo Mwenyezi Mungu alimuunga mkono Nuhu kwazo jambo ambalo linalowahitaji wawe na uhakika kabisa juu ya ukweli wake.
#
{28} ولهذا {قال} لهم نوحٌ مجاوباً: {يا قوم أرأيتُم إن كنتُ على بيِّنةٍ من ربِّي}؛ أي: على يقين وجزم؛ يعني: وهو الرسول الكامل القدوة، الذي ينقاد له أولو الألباب، وتضمحِلُّ في جنب عقله عقول الفحول من الرجال، وهو الصادق حقًّا؛ فإذا قال: إني على بيِّنة من ربِّي؛ فحسبُك بهذا القول شهادةً له وتصديقاً. {وآتاني رحمةً من عنده}؛ أي: أوحى إليَّ وأرسلني ومنَّ عليَّ بالهداية، {فعُمِّيَتْ عليكم}؛ أي: خفيت عليكم وبها تثاقلتم، {أنُلْزِمُكموها}؛ أي: أنُكْرِهكم على ما تحقَّقناه، وشككتم أنتم فيه. وأنتم كارهونَ حتَّى حرصتُم على ردِّ ما جئتُ به، ليس ذلك ضارَّنا، وليس بقادح مِن يقيننا فيه، ولا قولكم وافتراؤكم علينا صادًّا لنا عمَّا كنَّا عليه، وإنَّما غايته أن يكون صادًّا لكم أنتم وموجباً لعدم انقيادكم للحقِّ الذي تزعمون أنَّه باطل؛ فإذا وصلت الحال إلى هذه الغاية؛ فلا نقدر على إكراهكم على ما أمر الله ولا إلزامكم ما نفرتُم عنه، ولهذا قال: {أنُلْزِمُكموها وأنتم لها كارهون}؟!
{28} Na ndiyo maana Nuhu "Akasema" akiwaambia: "Enyi kaumu yangu! Hebu fikirini! Ikiwa mimi ninayo hoja wazi iliyotoka kwa Mola wangu Mlezi." Yaani, kwenye yakini na uhakika. Yaani, kuwa yeye ni Mtume mkamilifu na kiigizo, ambaye watu wenye akili wanamfuata, na akili za wanaume wenye nguvu hufifia katika upande wa akili Yake, na kwamba Yeye ndiye mkweli kwa hakika.
Basi ikiwa atasema: Ninayo hoja iliyo wazi iliyotoka kwa Mola wangu Mlezi, basi kauli hii inakutosha kuwa ushahidi kwake na kumsadikisha. "Na amenipa rehema kutoka kwake;" yaani, amenifunulia wahyi na akanituma, na akanineemesha uwongofu, "nayo ikafichwa kwenu." Yaani, imefichikana kwenu na mkaona uzito kuuendea. "Je, tuwalazimishe kuikubali;" yaani, tuwalazimishe juu ya yale tuliyoyapata kuwa hakika, nanyi mkayatilia shaka hali ya kuwa mnayachukia hadi mkawa na hima kubwa katika kukataa yale niliyokuja nayo. Basi hilo halitudhuru, na wala halitii doa katika yakini yetu juu yake, wala kauli yenu na kuzua kwenu dhidi yetu haviwezi kutuzuia yale tuliyokuwa juu yake. Lakini kilele chake ni kwamba yatawazuia nyinyi na kuwasababishia kutofuata kwenu haki ambayo mnadai kuwa ni batili. Kwa hivyo, hali yenu ikifikia kiwango hiki, basi sisi hatuwezi kuwalazimisha juu ya yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu, wala kuwalazimisha yale mliyoyakimbia,
na ndiyo maana akasema: "Tuwalazimishe kuikubali ilhali nyinyi mnaichukia?"
#
{29} {ويا قوم لا أسألُكم عليه}؛ أي: على دعوتي إياكم {مالاً}: فتستثقلون المغرم، {إنْ أجرِيَ إلاَّ على الله}: وكأنهم طلبوا منه طردَ المؤمنين الضعفاء، فقال لهم: {وما أنا بطاردِ الذين آمنوا}؛ أي: ما ينبغي لي ولا يَليق بي ذلك، بل أتلقَّاهم بالرُّحب والإكرام والإعزاز والإعظام، {إنَّهم ملاقو ربِّهم}: فمثيبهم على إيمانهم وتقواهم بجنات النعيم. {ولكنِّي أراكم قوماً تجهلون}: حيث تأمرونني بطرد أولياء الله وإبعادهم عنِّي، وحيث رددتُم الحقَّ لأنهم أتباعه، وحيث استدللتم على بطلان الحقِّ بقولكم: إني بشرٌ مثلكم، وإنَّه ليس لنا عليكم من فضل.
{29} "Na enyi kaumu yangu! Mimi siwaombi juu ya haya" ya kuwalingania nyinyi "mali yoyote", ndiyo mkaona uzito wa gharama yake. "Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu." Na ni kama kwamba walimtaka awafukuze Waumini wanyonge,
lakini akawaambia: "Na mimi sitawafukuza walioamini." Yaani, halinifailii wala haliendani na mimi; bali ninawapokea kwa moyo mkunjufu na ukarimu, na utukufu, na heshima. "Hakika wao watakutana na Mola wao Mlezi" na atawalipa kwa imani yao na uchamungu wao kwa Pepo za neema. "Lakini mimi nakuoneni mnafanya ujinga," kwa maana, mnaniamrisha niwafukuze vipenzi wa Mwenyezi Mungu na kuwaweka mbali nami, na kwa sababu mliikataa haki kwa kuwa walinifuata,
na kwa kuwa mlitumia ushahidi wa kuonyesha ubatili wa haki kwa kauli yenu: Mimi ni binadamu mfano wenu, na kwamba hatuna ubora wowote juu yenu.
#
{30} {ويا قومِ مَن ينصُرني من الله إن طَرَدْتُهم}؛ أي: مَن يمنعني من عذابِهِ؛ فإنَّ طردهم موجب للعذاب والنَّكال الذي لا يمنعه من دون الله مانع. {أفلا تذكَّرونَ}: ما هو الأنفع لكم والأصلح وتدبَّرون الأمور؟!
{30} "Na enyi kaumu yangu! Ni nani atakayeninusuru kwa Mwenyezi Mungu nikiwafukuza hawa?" Yaani, ni nani atanilinda kutokana na adhabu yake? Kwa maana, kufukuza kunalazimu adhabu na mateso ambayo hakuna mwenye kuzuia awezaye kuyazuia isipokuwa Mwenyezi Mungu. "Basi je, hamkumbuki?" Yale ambayo ni yenye manufaa na bora zaidi kwenu, na myazingatie mambo?
#
{31} {ولا أقول لكم عندي خزائنُ الله ولا أعلم الغيبَ ولا أقولُ إني مَلَكٌ}؛ أي: غايتي أني رسولُ الله إليكم؛ أبشِّركم وأنذركم، وما عدا ذلك؛ فليس بيدي من الأمر شيء، فليست خزائن الله عندي أدبِّرها أنا وأعطي مَنْ أشاء وأحْرُمُ مَن أشاء. {ولا أعلمُ الغيبَ}: فأخبركم بسرائِرِكم وبواطنكم، {ولا أقولُ إني مَلَك}: والمعنى أني لا أدَّعي رتبةً فوق رتبتي، ولا منزلةً سوى المنزلة التي أنزلني الله بها، ولا أحكم على الناس بظنِّي، فلا {أقول للذين تَزْدَري أعيُنكم}؛ أي: الضعفاء المؤمنين الذين يحتقرهم الملأ الذين كفروا؛ {لن يؤتيهم الله خيراً اللهُ أعلم بما في أنفسِهم}: فإن كانوا صادقينَ في إيمانهم؛ فلهم الخير الكثير، وإن كانوا غير ذلك؛ فحسابهم على الله. {إني إذاً}؛ أي: إن قلتُ لكم شيئاً ممَّا تقدَّم، {لمن الظَّالمين}: وهذا تأييس منه عليه الصلاة والسلام لقومِهِ أن ينبذَ فقراء المؤمنين أو يمقتهم، وتقنيع لقومه بالطُّرق المقنعة للمنصف.
{31} "Wala siwaambii kuwa nina hazina za Mwenyezi Mungu, wala kuwa mimi ninajua mambo ya ghaibu,
wala sisemi: Mimi ni Malaika." Yaani, Mwisho wangu ni kuwa mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu. Ninawabashiria na ninawaonya, na mengine yasiyokuwa hayo, basi hakuna chochote katika hayo mkononi mwangu. Kwa maana sina hazina za Mwenyezi Mungu, ili niweze kuziendesha, na nimpe nimtakaye, na nimnyime nimtakaye. "Wala mimi sijui mambo ya ghaibu" ili nawajulishe siri zenu na mambo ya ndani yenu. "Wala sisemi Mimi ni Malaika." Maana yake ni kuwa sidai cheo juu ya cheo changu, wala daraja isiyokuwa ile daraja ambayo Mwenyezi Mungu aliniteremsha hapo, wala mimi siwahukumu watu kwa dhana yangu tu. Kwa hivyo, "Wala sisemi kuhusu wale ambao yanawadharau macho yenu." Yaani, Waumini wanyonge ambao wanadharauliwa na wakuu hao waliokufuru; "kuwa Mwenyezi Mungu hatawapa heri. Mwenyezi Mungu ndiye anayajua zaidi yaliyo katika nafsi zao." Kwa hivyo, ikiwa wao ni wakweli katika imani yao, basi wana heri nyingi. Na kama wao si hivyo, basi Hesabu yao iko kwa Mwenyezi Mungu. "Mimi Hapo bila ya shaka;" yaani, ikiwa nitawaambia kitu katika hayo yaliyotangulia "nitakuwa miongoni mwa madhalimu." Na hili ni kuwakatisha tamaa - yeye rehema na amani za mwenyezi mungu ziwe juu yake, - kaumu yake kuwafukuza Waumini maskini, au kuwachukia na kuwashawishi kaumu yake wa njia za kushawishi kwa yule ambaye ni mwadilifu.
#
{32} فلما رأوه لا ينكفُّ عما كان عليه من دعوتهم ولم يدرِكوا منه مطلوبَهم؛ {قالوا يا نوحُ قد جادَلْتنا فأكثرتَ جِدالنا فأتِنا بما تَعِدُنا} [من العذابِ] {إنْ كنتَ من الصادقين}: فما أجهلهم وأضلَّهم! حيثُ قالوا هذه المقالة لنبِّيهم الناصح؛ فهلاَّ قالوا إن كانوا صادقين: يا نوحُ! قد نصحتَنا وأشفقتَ علينا ودعوتَنا إلى أمرٍ لم يتبيَّن لنا فنريدُ منك أن تبيِّنه لنا لننقادَ لك، وإلاَّ فأنت مشكورٌ في نصحك؛ لكان هذا الجواب المنصف للذي قد دُعِيَ إلى أمرٍ خفي عليه، ولكنهم في قولهم كاذبون، وعلى نبيهم متجرِّئون، ولم يردُّوا ما قاله بأدنى شبهةٍ فضلاً عن أن يردُّوه بحجَّة، ولهذا عدلوا من جهلهم وظلمهم إلى الاستعجال بالعذاب وتعجيز الله.
{32} Basi walipomuona hayaachi yale aliyokuwa juu yake ya kuwalingania na hawakupata walichotaka kutoka kwake,
"Wakasema: Ewe Nuhu! Umejadiliana nasi, na umekithirisha kutujadili. Basi tuletee hayo unayotuahidi"
[ya adhabu], "ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli." Lakini ni wajinga kiasi gani hiki, na ni wapotofu kiasi gani hiki wawalipomwambia Mtume wao,
mshauri mwaminifu maneno haya! Kwa nini hawakusema ikiwa wao ni wakweli: Ewe Nuhu! Umetunasihi, na umetuonea huruma sana, na umetulingania kwa jambo ambalo halijakuwa wazi kwetu, kwa hivyo tunataka utufafanulie ili tukufuate, vinginevyo basi tunakushukuru kwa ushauri wako. Basi hili lingelikuwa ni jibu la uadilifu kwa yule aliyeitwa kufanya jambo lililofichika kwake, lakini wao katika hayo waliyoyasema walikuwa waongo, na wakawa wamemfanyia ujasiri Nabii wao. Na wala hawakukataa yale aliyoyasema kwa sababu ya shaka hata iliyo kidogo zaidi, achilia mbali kwamba wayakatee kwa hoja. Na ndiyo maana wakapinda kwa ujinga wao na dhuluma yao kwenda kujiharakishia adhabu na kumuona Mwenyezi Mungu kwamba hawezi.
#
{33} ولهذا أجابهم نوحٌ عليه السلام بقوله: {إنَّما يأتيكم به الله إن شاءَ}؛ أي: إن اقتضتْ مشيئته وحكمتُه أن يُنْزِلَه بكم؛ فعل ذلك، {وما أنتم بمعجِزين}: لله، وأنا ليس بيدي من الأمر شيءٌ.
{33} Na ndiyo maana Nuhu, amani iwe juu yake,
akawajibu kwa kusema: "Hakika Mwenyezi Mungu tu ndiye atakayewaletea akipenda." Yaani, ikiwa mapenzi yake na hekima yake yatataka kwamba aiteremshe kwenu, basi atafanya hivyo; "Wala nyinyi si wenye kumshinda" Mwenyezi Mungu, na mimi sina chochote mikononi mwangu katika jambo hili.
#
{34} {ولا ينفعكم نُصحي إنْ أردتُ أنْ أنصَحَ لكم إن كان الله يريدُ أن يُغْوِيَكم}؛ أي: إن إرادة الله غالبةٌ؛ فإنَّه إذا أراد أن يغوِيَكم لردِّكمُ الحقَّ؛ فلو حرصتُ غاية مجهودي ونصحتُ لكم أتمَّ النُّصح ـ وهو قد فعل عليه السلام ـ؛ فليس ذلك بنافع لكم شيئاً. {هو ربُّكم}: يفعلُ بكم ما يشاء ويحكُم فيكم بما يُريدُ، {وإليه تُرْجَعون}: فيجازيكم بأعمالكم.
{34} "Wala nasaha yangu haitawafaa kitu nikitaka kuwanasihi, ikiwa Mwenyezi Mungu anataka kuwapoteza." Yaani, utashi wa Mapenzi ya Mungu ndio wenye kushinda. Kwa maana, akitaka kuwapotosha kwa sababu ya kukataa kwenu haki, basi hata kama nikafanya hima uwezo wangu wote na nikawanasihi nasaha kamili zaidi, - na tayari alikwisha fanya hivyo, yeye amani iwe juu yake; - basi hilo halitawafaidi kitu. "Yeye ndiye Mola wenu Mlezi," anayewafanyia atakavyo na anawahukumu kwa kina anachotaka. "Na kwake mtarejeshwa" na atawalipa kwa matendo yenu.
#
{35} {أم يقولونَ افتراه}: هذا الضمير محتملٌ أن يعود إلى نوح كما كان السياق في قصتِهِ مع قومه، وأنَّ المعنى: إنَّ قومه يقولون: افترى على الله كذباً، وكَذَبَ بالوحي الذي يزعم أنَّه من الله، وأنَّ الله أمره أن يقول: {قلْ إنِ افتريتُه فعليَّ إجرامي وأنا بريء مما تُجْرِمون}؛ أي: كلٌّ عليه وزره، {ولا تَزِرُ وازرةٌ وِزْرَ أخرى}. ويُحتمل أن يكون عائداً إلى النبيِّ محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -، وتكون هذه الآية معترضةً في أثناء قصة نوح وقومه؛ لأنَّها من الأمور التي لا يعلمها إلا الأنبياء، فلما شرع الله في قصِّها على رسوله، وكانت من جملة الآيات الدالَّة على صدقه ورسالته؛ ذكر تكذيب قومه له، مع البيان التامِّ، فقال: {أم يقولونَ افتراه}؛ أي: هذا القرآن اختلقه محمدٌ من تلقاء نفسه؛ أي: فهذا من أعجب الأقوال وأبطلها؛ فإنَّهم يعلمون أنَّه لم يقرأ ولم يكتبْ ولم يرحلْ عنهم لدراسة على أهل الكتب، فجاء بهذا الكتاب الذي تحدَّاهم أن يأتوا بسورةٍ من مثله؛ فإذا زعموا مع هذا أنَّه افتراه؛ عُلِمَ أنَّهم معاندون، ولم يبقَ فائدةٌ في حجاجهم، بل اللائق في هذه الحال الإعراضُ عنهم، ولهذا قال: {قلْ إنِ افتريتُهُ فعليَّ إجرامي}؛ أي: ذنبي وكذبي. {وأنا بريءٌ مما تجرِمون}؛ أي: فلم تستلِجُّون في تكذيبي؟
{35} "Au ndio wanasema: Ameizua?" Kiwakilishi nafsi hiki 'a' kinaweza kumrudia Nuhu, kama ulivyokuwa muktadha katika hadithi yake na kaumu yake,
na kwamba maana yake ni: hakika kaumu yake wanasema: Amemzulia uongo Mwenyezi Mungu, na akaudanganyishia wahyi ambao anadai kuwa umetoka kwa Mwenyezi Mungu.
Na kwamba Mwenyezi Mungu alimuamrisha kwamba aseme: "Sema: Ikiwa nimeizua, basi kosa hilo ni juu yangu, na mimi niko mbali sana na makosa myatendayo." Yaani, kila mmoja atabeba mzigo wake, "Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine." Na inawezekana kwamba inamrudia Nabii Muhammad -rehema na amani ziwe juu yake - na aya hii imeingilia tu kati kwenye kisa cha Nuhu na kaumu yake. Kwa sababu, ni miongoni mwa mambo ambayo hawayajui isipokuwa manabii peke yao. Basi Mwenyezi Mungu alipoanza kumsimulia Mtume wake juu yake, na yakawa miongoni mwa ishara zinazoashiria ukweli wake na ujumbe wake, Akataja kukanushwa kwake na kaumu yake kwa maelezo kamili,
na akasema: "Au ndio wanasema: Ameizua?" Yaani, Qur-ani hii aliizua Muhammad mwenyewe tu. Basi haya ni katika kauli za kushangaza batili zaidi
na zilizo batili zaidi. Kwani, Wanajua kwamba yeye hakusoma, wala hakuandika, wala hakusafiri akawaacha akaenda kusoma kwa watu wa vitabu; basi ndiyo akaleta kitabu hiki ambacho kiliwapa changamoto ya kuleta sura moja mfano wake. Kwa hivyo, wakidai pamoja na haya kuwa yeye ndiye aliyeizua, basi itajulikana kuwa wao ni wakaidi tu, na hakutakuwa na faida yoyote katika kuhojiana nao. Bali katika hali hii, kinachofailiana nao zaidi ni kujitenga nao,
na kwa sababu ya hili ndiyo akasema: "Sema, "Ikiwa nimeizua, basi kosa hilo ni juu yangu." Yaani, dhambi yangu na uongo wangu. "Na mimi niko mbali sana na makosa myatendayo." Yaani, kwa nini mnang'ang'ania kunikadhibisha.
#
{36} وقوله: {وأوحي إلى نوح أنَّه لن يؤمِنَ مِن قومِكَ إلاَّ مَنْ قد آمنَ}؛ أي: قد قسوا {فلا تبتئِسْ بما كانوا يفعلون}؛ أي: فلا تحزنْ ولا تبالِ بهم وبأفعالهم؛ فإنَّ الله قد مَقَتَهم وأحقَّ عليهم عذابه الذي لا يردُّ.
{36} Na kauli yake: "Na akafunuliwa Nuhu akaambiwa, "Hataamini yeyote katika kaumu yako isipokuwa wale waliokwisha amini." Yaani, walikwisha kuwa sugu. "Basi usisikitike kwa yale waliyokuwa wakiyatenda." Yaani, usihuzunike wala usiwajali wao na matendo yao. Kwani, Mwenyezi Mungu alikwisha wachukia na akapitisha kuwa wanastahiki adhabu yao ambayo haizuiwi.
#
{37} {واصنع الفُلْكَ بأعيُننا ووَحْينا}؛ أي: بحفظنا ومرأىً منَّا وعلى مرضاتنا، {ولا تخاطِبْني في الذين ظلموا}؛ أي: لا تراجِعْني في إهلاكهم، {إنَّهم مُغْرَقون}؛ أي: قد حقَّ عليهم القولُ، ونَفَذَ فيهم القدرُ.
{37} "Na unda jahazi mbele ya macho yetu na kwa mujibu wa ufunuo wetu." Yaani, kwa ulinzi wetu, na kwa kuona kwetu, na kwa radhi yetu, "Wala usiniongeleshe kuwatetea wale waliodhulumu." Yaani, usinirejelee tena kuhusiana na kuwaangamiza, "kwani hao bila ya shaka watazamishwa." Yaani, neno limekwisha kuwa la uhakika juu yao, na majaliwa yakawatekelezekea.
#
{38} فامتثلَ أمر ربِّه، وجَعَلَ يصنع الفلك، {وكلما مرَّ عليه ملأ من قومِهِ}: ورأوا ما يصنع، {سَخِروا منه قال إن تَسْخَروا منَّا}: الآن، {فإنَّا نسخَرُ منكم كما تسخَرونَ}.
{38} Basi akaitekeleza amri ya Mola wake Mlezi, na akaanza kuijenga safina, "na kila walipopita karibu nayo wakuu kutoka kwa kaumu yake" na wakaona alivyokuwa akiiunda, "wanamkejeli.
Yeye akasema: ikiwa nyinyi mnatukejeli" sasa hivi; "basi sisi pia tunawakejeli kama mnavyotukejeli."
#
{39} {فسوفَ تعلمونَ مَن يأتيه عذابٌ يُخْزيه ويَحِلُّ عليه عذابٌ مقيمٌ}: نحنُ أم أنتم؟ وقد علموا ذلك حين حلَّ بهم العقاب.
{39} "Nanyi mtakuja jua ni nani itakayemfikia adhabu ya kumhizi, na itakayemteremkia adhabu ya kudumu." Sisi au nyinyi? Na hakika walilijua hilo wakati adhabu ilipowafika.
#
{40} {حتَّى إذا جاء أمرُنا}؛ أي: قدرُنا بوقتِ نزول العذاب بهم، {وفار التنُّور}؛ أي: أنزل الله السماء بالماء المنهمر، وفجَّر الأرض كلَّها عيوناً، حتى التنانير التي هي محلُّ النار في العادة وأبعد ما يكون عن الماء تفجَّرت، فالتقى الماءُ على أمرٍ قد قُدِرَ، {قُلْنا} لنوح: {احملْ فيها مِن كلٍّ زوجين اثنين}؛ أي: من كلِّ صنف من أصناف المخلوقات ذكر وأنثى؛ لتبقى مادَّة سائر الأجناس، وأما بقيَّة الأصناف الزائدة عن الزوجين؛ فلأنَّ السفينة لا تُطيق حملها، {وأهْلَكَ إلاَّ مَن سَبَقَ عليه القولُ}: ممَّن كان كافراً؛ كابنه الذي غرق. {ومَنْ آمن و} ـ الحال أنه ـ {ما آمَنَ معه إلا قليلٌ}.
{40} "Mpaka ilipokuja amri yetu;" yaani, majaliwa yetu wakati wa wao kushukiwa na adhabu, "na tanuri ikafoka maji." Yaani, Mwenyezi Mungu aliiteremsha mbingu kwa maji ya kumiminika kwa wingi, na akaipasua ardhi yote kwa chemchemi, kiasi kwamba pia tanuru, ambazo ndiyo kwa kawaida ndipo pahali pa moto na pahali ambapo huwa mbali zaidi na maji, zikalipuka maji, na maji yakakutana kwa jambo lililokwisha pitishwa.
"Tukamwambia" Nuhu: "Pakia humo katika kila kitu, jozi mbili ya dume na jike." Yaani, kutoka kwa kila aina ya viumbe, dume na jike ili asili ya sampuli zote za viumbe zibakie juu ya ardhi. Na ama sampuli zinginezo zinazozidi jozi, basi zitaangamia kwa sababu safina haiwezi kuzibeba. "Na ahali zako, isipokuwa wale ambao imekwisha wapitia hukumu;" yaani, wale waliokuwa makafiri, kama vile mtoto wake ambaye alizama. "Na watu walioamini." Na - hali ni kwamba - "hawakuamini pamoja naye isipokuwa wachache tu."
#
{41} {وقال} نوحٌ لمن أمره الله أن يحمِلَهم: {ارْكَبوا فيها بسم الله مَجْريها ومُرْساها}؛ أي: تجري على اسم الله وترسي [على اسم الله وتجري] بتسخيره وأمره. {إنَّ ربِّي لغفورٌ رحيمٌ}: حيث غَفَرَ لنا، ورَحِمنا، ونجَّانا من القوم الظالمين.
{41} "Na akasema" Nuhu akiwaambia wale ambao Mwenyezi Mungu alimuamrisha awabebe: "Pandeni humo kwa Bismillahi
(Kwa Jina la Mwenyezi Mungu), kwenda kwake na kusimama kwake." Yaani ikwende kwa jina la Mwenyezi Mungu na itie nanga
[kwa jina la Mwenyezi Mungu, na ikwende] kwa kutiishwa kwake na amri yake. "Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." Kwa kuwa alitusamehe, na akaturehemu, na akatuokoa sawasawa kutokana na kaumu madhalimu.
#
{42} ثم وصف جريانَها كأنَّا نشاهدها، فقال: {وهي تجري بهم}؛ أي: بنوح ومَنْ رَكِبَ معه {في موج كالجبال}: والله حافِظُها، وحافظُ أهلها، {ونادى نوحٌ ابنَه}: لما ركب ليركبَ معه، {وكان} ابنُه {في مَعْزِل}: عنهم حين ركبوا؛ أي: مبتعداً، وأراد منه أن يقرب ليركبَ، فقال له: {يا بنيَّ اركب معنا ولا تَكُن مع الكافرين}: فيصيُبك ما يصيبهم.
{42} Kisha akaeleza kwenda kwake kama kwamba tunaitazama,
akasema: "Ikawa inakwenda nao." Yaani, inakwenda na Nuhu na wale waliopanda humo pamoja naye "katika mawimbi kama milima." Na Mwenyezi Mungu akawa ndiye Mlinzi wake na Mlinzi wa watu wake. "Na Nuhu akamwita mwanawe" alipopanda ili apande humo pamoja naye. "Naye" yaani, mwanawe "alikuwa mbali" nao wakati walipopanda humo, na wakataka asonge karibu ili apande.
Kisha akamwambia: "Ewe mwanangu! Panda pamoja nasi, wala usiwe pamoja na makafiri" yakakusibu yale yatakayowasibu.
#
{43} فقال ابنُه مكذِّباً لأبيهِ أنَّه لا ينجو إلاَّ مَنْ رَكِبَ [معه] السفينة: {سآوي إلى جبل يَعْصِمُني من الماء}؛ أي: سأرتقي جبلاً أمتنع به من الماء. فقال نوحٌ: {لا عاصِمَ اليوم من أمرِ الله إلاّ مَن رَحِمَ}: فلا يعصمُ أحداً جبلٌ ولا غيرُه، ولو تسبَّب بغاية ما يمكِنُه من الأسباب؛ لَمَا نجا إن لم يُنْجِهِ الله، {وحال بينَهما الموجُ فكانَ} الابنُ {من المغرَقين}.
43. Lakini mwanawe akasema, akimkadhibisha baba yake alipomwambia ya kwamba hataokoka isipokuwa yule aliyepanda safina
[pamoja naye]. "Nitakimbilia mlimani unilinde na maji." Yaani, nitapanda mlima fulani ili nijikinge nao kutokana na maji hayo.
Basi Nuhu akasema:
Leo hakuna wa kulindwa na amri ya Mwenyezi Mungu isipokuwa yule aliyemrehemu mwenyewe." Basi hakuna mlima wowote utakaomkinga yeyote wala kinginecho, hata kama atachukua sababu kubwa zaidi atakazoweza, basi hataweza kuokoka ikiwa Mwenyezi Mungu hatamwokoa. "Na wimbi likawatenganisha, basi akawa" mwanawe huyo "katika waliozama."
#
{44} فلمَّا أغرَقَهم الله ونجَّى نوحاً ومن معه؛ و {قيل يا أرضُ ابلَعي ماءَك}: الذي خرج منك، والذي نزل إليك، ابلعي الماء الذي على وجهك، {ويا سماءُ أقلِعي}: فامتَثَلَتا لأمر الله، فابتلعتِ الأرضُ ماءها، وأقلعتِ السماء فنضب الماء من الأرض، {وقُضِيَ الأمرُ}: بهلاك المكذِّبين ونجاة المؤمنين، {واسْتَوَت} السفينةُ {على الجوديِّ}؛ أي: أرست على ذلك الجبل المعروف في أرض الموصل، {وقيلَ بُعداً للقوم الظالمين}؛ أي: أُتْبِعوا بهلاكهم لعنةً وبُعداً وسُحْقاً لا يزال معهم.
{44} Basi Mwenyezi Mungu alipowazamisha na akamuokoa Nuhu na wale waliokuwa pamoja naye,
na "ikasemwa: Ewe ardhi! Meza maji yako" ambayo yalitoka kwako, na yale yaliyokuteremkia, yameze maji yaliyo juu ya uso wako. "Na Ewe mbingu! Jizuie" basi ardhi ikameza maji yake, na mbingu ikajizuia, na maji yakakauka katika ardhi. "Amri hiyo ikapitishwa" kwa kuwaangamiza wale waliokadhibisha na kuwaokoa Waumini "na
(jahazi) likasimama juu ya
(mlima) wa Al Juudiy." Yaani, ilitia nanga juu ya ule mlima huo mashuhuri katika ardhi ya Mosil
(huko Iraq).
"Na ikasemwa: Wapotelee mbali kaumu madhalimu!" Yaani, walifuatishwa laana pamoja na maangamizo yao na kuwekwa mbali ambayo hayaachi kuwaandama.
#
{45} {ونادى نوحٌ ربَّه فقالَ ربِّ إنَّ ابني من أهلي وإنَّ وعدَكَ الحقُّ}؛ [أي]: وقد قلتَ لي: فاحملْ فيها من كلٍّ زوجين اثنين وأهلَكَ، ولن تُخْلِفَ ما وَعَدْتَني به. لعلَّه عليه الصلاة والسلام ـ حملتْه الشفقةُ وأنَّ الله وعده بنجاة أهلِهِ ـ ظنَّ أنَّ الوعد لعمومهم؛ مَن آمن ومَن لم يؤمن؛ فلذلك دعا ربَّه بذلك الدُّعاء، ومع هذا؛ ففوَّض الأمر لحكمة الله البالغة.
{45} "Na Nuhu alimwomba Mola wake Mlezi akasena: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mwanangu ni katika ahali zangu, na hakika ahadi yako ndiyo ya haki."
[Yaani],
Na ulikuwa umeniambia: basi beba humo katika kila jozi mbili dume na jike na ahali zako, wala hutayavunja yale uliyoniahidi. Labda yeye - rehema na amani ziwe juu yake - alisukumwa na huruma kubwa, na kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa amemuahidi kuwaokoa ahali zake - na akadhani kwamba ahadi hiyo ilikuwa kwa ujumla wao; wale waliamini na wale ambao hawakuamini. Basi kwa sababu ya hilo, ndiyo akamwomba Mola wake Mlezi kwa dua hiyo, lakini pamoja na hayo, aliliachia jambo hilo hekima kuu ya Mwenyezi Mungu.
#
{46} فقال اللهُ له: {إنَّه ليس من أهلك}: الذين وعدتُك بإنجائهم، {إنَّه عملٌ غيرُ صالح}؛ أي: هذا الدُّعاء الذي دعيتَ به لنجاة كافر لا يؤمنُ بالله ولا رسوله، {فلا تَسْألْنِ ما ليس لك به علمٌ}؛ أي: ما لا تعلم عاقبته ومآله، وهل يكون خيراً أو غير خير. {إني أعظُك أن تكونَ من الجاهلين}؛ أي: إني أعظُك وعظاً تكون به من الكاملين، وتنجو به من صفات الجاهلين.
{46} Basi Mwenyezi Mungu akamwambia: "Huyu si katika ahali zako" ambao nilikuahidi kuwaokoa, "Hakika yeya mwendo wake si mwema." Yaani, Dua hii ambayo uliomba ilikuwa ya kumwokoa kafiri asiyemwamini Mwenyezi Mungu wala Mtume wake, "Basi usiniombe jambo usilo na elimu nalo." Yaani, yale usiyoyajua matokeo yake, na mwisho wake. Na je, utakuwa mwisho mwema au si mwema? "Mimi nakuwaidhi usije ukawa miongoni mwa wajinga." Yaani, Mimi ninakuwaidhi kwa waadhi ambao kwa huo utakuwa miongoni mwa watu kamili, na utajiepusha kwa huo kutokana na sifa za wajinga.
#
{47} فحينئذٍ ندمَ نوحٌ عليه السلام ندامةً شديدةً على ما صَدَرَ منه، و {قال ربِّ إنِّي أعوذُ بك أن أسألَكَ ما ليس لي به علمٌ وإلاَّ تَغْفِرْ لي وترحَمْني أكن من الخاسرينَ}: فبالمغفرة والرحمة ينجو العبدُ من أن يكون من الخاسرين. ودلَّ هذا على أنَّ نوحاً عليه السلام لم يكنْ عندَه علمٌ بأنَّ سؤاله لربِّه في نجاة ابنه محرَّمٌ داخلٌ في قوله: {ولا تخاطِبْني في الذين ظَلَموا إنَّهم مغرقونَ}، بل تعارض عندَه الأمران، وظنَّ دخوله في قوله: {وأهلَكَ}، وبعد هذا تبيَّن له أنَّه داخلٌ في المنهيِّ عن الدعاء لهم والمراجعة فيهم.
{47} Basi hapo Nuhu - amani iwe juu yake - akajuta kujuta kukubwa kwa yale aliyoyafanya,
na "akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Mimi najikinga kwako nikuombe nisilo na elimu nalo. Na kama hunisamehe na ukanirehemu, nitakuwa katika waliohasiri." Kwa hivyo, kwa njia ya msamaha na rehema, mja huokoka kutokana na kuwa miongoni mwa waliohasirika. Na hili liliashiria kuwa Nuhu - amani iwe juu yake -
alikuwa hajui kuwa kumwomba Mola wake Mlezi kuhusu kumuokoa mwanawe kuliharamishwa na kunaingia katika kauli yake: "Wala usiniongeleshe kuwatetea wale waliodhulumu. Kwani, hao bila ya shaka watazamishwa." Bali mambo hayo mawili yalihitilafiana kwake,
na akadhania kuwa alijumuishwa katika kauli yake: "Na ahali zako," lakini baada ya haya ikambainikia kuwa aliingia katika wale ambao ilikakatazwa kuwaombea dua, na kurejea kwa Mwenyezi Mungu kuhusiana nao.
#
{48} {قيل يا نوحُ اهبطْ بسلام منَّا وبركاتٍ عليك وعلى أمم ممَّن معكَ}: من الآدميين وغيرهم من الأزواج التي حملها معه، فبارك الله في الجميع، حتى ملؤوا أقطار الأرض ونواحيها {وأممٌ سنمتِّعهم}: في الدُّنيا، {ثم يمسُّهم منَّا عذابٌ أليمٌ}؛ أي: هذا الإنجاء ليس بمانع لنا من أنَّ مَنْ كَفَرَ بعد ذلك؛ أحلَلْنا به العقاب، وإنْ مُتِّعوا قليلاً؛ فسيؤخذون بعد ذلك.
{48} "Ikasemwa: Ewe Nuhu! Shuka kwa salama itokayo kwetu, na baraka nyingi juu yako na juu ya umma miongoni mwa wale walio pamoja nawe," miongoni mwa wanadamu na wasiokuwa wao katika zile jozi ambazo alizibeba pamoja naye. Basi Mwenyezi Mungu akawabariki wote mpaka wakajaza pande zote za ardhi. "Na zitakuwapo umma tutakazozistarehesha" katika duani hii "kisha zitaguswa na adhabu chungu itokayo kwetu" Yaani, ukombozi huu hautuzuii kwamba mwenye kukufuru baada ya hayo, tutamfikishia adhabu hata kama watastareheshwa kidogo, lakini wataadhibiwa baada ya hapo.
#
{49} قال الله لنبيِّه محمد - صلى الله عليه وسلم - بعدما قصَّ عليه هذه القصة المبسوطة التي لا يعلمها إلاَّ مَنْ مَنَّ عليه برسالته: {تلك من أنباء الغيبِ نوحيها إليكَ ما كنتَ تعلمُها أنت ولا قومُك مِن قَبْلِ هذا}: فيقولوا: إنَّه كان يعلمها؛ فاحمدِ الله واشكُرْه واصبرْ على ما أنت عليه من الدِّين القويم والصِّراط المستقيم والدَّعوة إلى الله. {إنَّ العاقبةَ للمتَّقين}: الذين يتَّقون الشرك وسائر المعاصي، فستكون لك العاقبةُ على قومِكَ كما كانت لنوح على قومِهِ.
{49} Mwenyezi Mungu akamwambia Nabii wake Muhammad -rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - baada ya kumsimulia kisa hiki kilichoelezwa kwa kina,
ambacho hakuna akijuaye isipokuwa yule aliyemneemesha kwa ujumbe wake: "Hizi ni katika habari za ghaibu tunazokufunulia. Hukuwa ukizijua wewe, wala kaumu yako,
kabla ya haya" ndiyo wakasema kwamba: Hakika alikuwa alikiyajua. Basi sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, na mshukuru, na subiri katika yale uliyo juu yake ya Dini iliyonyooka, na njia iliyonyooka, na kulingania kwa Mwenyezi Mungu. "Hakika Mwisho ni wa wachamungu" ambao wanajiepusha na ushirikina na maasi mengine yote, basi mwisho utakuwa wako dhidi ya kaumu yako kama ulivyokuwa wa Nuhu dhidi ya kaumu yake.
{وَإِلَى عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا قَالَ يَاقَوْمِ اعْبُدُوا اللَّهَ مَا لَكُمْ مِنْ إِلَهٍ غَيْرُهُ إِنْ أَنْتُمْ إِلَّا مُفْتَرُونَ (50) يَاقَوْمِ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى الَّذِي فَطَرَنِي أَفَلَا تَعْقِلُونَ (51) وَيَاقَوْمِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُمْ مِدْرَارًا وَيَزِدْكُمْ قُوَّةً إِلَى قُوَّتِكُمْ وَلَا تَتَوَلَّوْا مُجْرِمِينَ (52) قَالُوا يَاهُودُ مَا جِئْتَنَا بِبَيِّنَةٍ وَمَا نَحْنُ بِتَارِكِي آلِهَتِنَا عَنْ قَوْلِكَ وَمَا نَحْنُ لَكَ بِمُؤْمِنِينَ (53) إِنْ نَقُولُ إِلَّا اعْتَرَاكَ بَعْضُ آلِهَتِنَا بِسُوءٍ قَالَ إِنِّي أُشْهِدُ اللَّهَ وَاشْهَدُوا أَنِّي بَرِيءٌ مِمَّا تُشْرِكُونَ (54) مِنْ دُونِهِ فَكِيدُونِي جَمِيعًا ثُمَّ لَا تُنْظِرُونِ (55) إِنِّي تَوَكَّلْتُ عَلَى اللَّهِ رَبِّي وَرَبِّكُمْ مَا مِنْ دَابَّةٍ إِلَّا هُوَ آخِذٌ بِنَاصِيَتِهَا إِنَّ رَبِّي عَلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ (56) فَإِنْ تَوَلَّوْا فَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ مَا أُرْسِلْتُ بِهِ إِلَيْكُمْ وَيَسْتَخْلِفُ رَبِّي قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّونَهُ شَيْئًا إِنَّ رَبِّي عَلَى كُلِّ شَيْءٍ حَفِيظٌ (57) وَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا هُودًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِنَّا وَنَجَّيْنَاهُمْ مِنْ عَذَابٍ غَلِيظٍ (58) وَتِلْكَ عَادٌ جَحَدُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ وَعَصَوْا رُسُلَهُ وَاتَّبَعُوا أَمْرَ كُلِّ جَبَّارٍ عَنِيدٍ (59) وَأُتْبِعُوا فِي هَذِهِ الدُّنْيَا لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ أَلَا إِنَّ عَادًا كَفَرُوا رَبَّهُمْ أَلَا بُعْدًا لِعَادٍ قَوْمِ هُودٍ (60)}.
50. Na kwa kina 'Aadi tulimtuma ndugu yao Hud. Akasema, "Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu! Hamna mungu isipokuwa Yeye tu. Nyinyi si chochote isipokuwa ni wazushi tu." 51. "Enyi watu wangu! Siwaombi ujira kwa ajili ya haya. Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Yule aliyeniumba. Basi hamtumii akili?" 52. "Na enyi kaumu yangu! Mwombeni msamaha Mola wenu Mlezi, kisha mtubie kwake. Atawatumia mbingu zenye kunyesha mvua ya kumiminika, na atawazidishia nguvu juu ya nguvu zenu. Wala msigeuke mkawa wahalifu." 53. Wakasema, "Ewe Hud! Hujatuletea ushahidi ulio wazi. Wala sisi hatuiachi miungu yetu kwa kufuata kauli yako. Na wala sisi hatukuamini wewe." 54.
"Sisi tunasema: 'Baadhi ya miungu yetu imekusibu kwa baa.' Akasema, "Hakika, mimi ninamshuhudisha Mwenyezi Mungu, na nyinyi shuhudieni, ya kwamba mimi niko mbali na hao mnaowafanya washirika." 55. "Badala ya Yeye. Basi nyinyi nyote nipangieni njama, na kisha msinipe muhula!" 56. "Hakika mimi nimemtegemea Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Hakuna kiumbe yeyote isipokuwa Yeye anamwendesha atakavyo. Hakika Mola wangu Mlezi yuko kwenye njia iliyonyooka." 57. Na wakikengeuka, "basi hakika mimi nimekwisha wafikishia yale niliyotumwa nayo kwenu. Na Mola wangu Mlezi atawaleta watu wengine badala yenu, wala nyinyi hamumdhuru kitu Yeye. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kuhifadhi kila kitu." 58. Na ilipofika amri yetu, tulimwokoa Hud na wale walioamini pamoja naye, kwa rehema itokayo kwetu. Na tukawaokoa na adhabu kali. 59. Na hao ndio kina 'Aadi. Walizikufuru Ishara za Mola wao Mlezi, na wakawaasi Mitume wake, na wakafuata amri ya kila jabari mkaidi. 60. Na wakafuatishiwa laana katika dunia hii na Siku ya Qiyama. Basi tambueni mtanabahi kuwa hakika kina 'Aadi walimkufuru Mola wao Mlezi. Na tambueni mtanabahi kuwa hakika waliangamizwa kina 'Aadi, kaumu ya Hud.
#
{50} أي: {و} أرسلنا {إلى عادٍ}: وهم القبيلة المعروفة في الأحقاف من أرض اليمن، {أخاهم}: في النسب، {هوداً}: ليتمكَّنوا من الأخذ عنه والعلم بصدقه، فقال لهم: {اعبُدوا الله ما لكم من إلهٍ غيرُه إنْ أنتُم إلاَّ مفتَرون}؛ أي: أمرهم بعبادة الله وحده، ونهاهم عمَّا هم عليه من عبادة غير الله، وأخبرهم أنَّهم قد افتَرَوا على الله الكذب في عبادتهم لغيره وتجويزهم لذلك، ووَضَّحَ لهم وجوب عبادة الله وفساد عبادة ما سواه.
{50} Yaani, "Na" tulituma "kwa 'Aadi." Nao ni kabila linalojulikana kwamba walikuwa wakiishi katika Al-Ahqaf huko ardhi ya Yemen, "ndugu yao" kwa nasaba, "Hud" ili waweze kujifunza kwake, na waweze kuujua ukweli wake.
Basi akawaambia: "Mwabuduni Mwenyezi Mungu! Hamna mungu isipokuwa Yeye tu. Nyinyi si chochote isipokuwa ni wazushi tu." Yaani, aliwaamrisha kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na akawakataza yale wanayofanya miongoni mwa kumwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na akawajulisha kuwa walimsingizia Mwenyezi Mungu uongo katika kuabudu kwao asiyekuwa Yeye na kuruhusu kwao hilo, na akawawekea wazi ulazima wa kumwabudu Mwenyezi Mungu na uharibifu wa kuabudu kisichokuwa Yeye.
#
{51} ثم ذكر عدم المانع لهم من الانقياد، فقال: {يا قومِ لا أسألُكم عليه أجراً}؛ أي: غرامة من أموالكم على ما دعوتكم إليه فتقولوا: هذا يريدُ أن يأخذَ أموالنا، وإنما أدعوكم وأعلِّمكم مجاناً. {إن أجْرِيَ إلاَّ على الذي فطرني أفلا تعقلون}: ما أدعوكم إليه وأنَّه موجبٌ لقبوله، منتفٍ المانع عن ردِّه.
{51} Kisha akataja kuwa hakuna kinachowazuia kufuata,
akasema: "Enyi kaumu yangu! Siwaombi ujira kwa ajili ya haya." Yaani, siwaitishi gharama ya ninayowalingania kwayo kutoka katika mali zenu,
mkaja kusema: Huyu anataka kuchukua mali zetu, lakini ninawalingania na kuwafundisha bure. "Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Yule aliyeniumba. Basi hamtumii akili" juu ya kile ninachowalingania kwacho na kwamba ni lazima mkikubali, na hakina kizuizi chochote cha kukikataa?
#
{52} {ويا قوم استغفروا ربكم}: عما مضى منكم، {ثم توبوا إليه}: فيما تستقبلونه بالتوبة النَّصوح والإنابة إلى الله تعالى؛ فإنَّكم إذا فعلتم ذلك؛ {يُرْسِل السماءَ عليكُم مِدْراراً}: بكثرة الأمطار التي تَخْصُبُ بها الأرض ويكثر خيرها، {ويَزدْكم قوةً إلى قوَّتكم}: فإنَّهم كانوا من أقوى الناس، ولهذا قالوا: {من أشدُّ مِنَّا قوَّةً}، فوعدهم أنَّهم إن آمنوا زادهم قوَّةً إلى قوَّتهم، {ولا تتولَّوا}: عنه؛ أي: عن ربكم {مجرمين}؛ أي: مستكبرين عن عبادته، متجرِّئين على محارمه.
{52} "Na enyi kaumu yangu! Mwombeni msamaha Mola wenu Mlezi" kwa yale mliyoyatanguliza, "kisha mtubie kwake" kwa yale mtakayofanya kwa toba ya kweli na kurejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa maana, mkifanya hivyo, "Atawatumia mbingu zenye kunyesha mvua ya kumiminika;" yaani, kutakuwa na mvua nyingi ambayo kwayo ardhi itarutubika na heri yake itakithiri, "na atawazidishia nguvu juu ya nguvu zenu" kwa maana walikuwa miongoni mwa watu wenye nguvu zaidi.
Na ndiyo maana wakasema: "Nani mwenye nguvu kushinda sisi?" Basi akawaahidi kwamba wakiamini, atawazidishia nguvu juu ya nguvu zao, "Wala msigeuke" mkamuacha Mola wenu Mlezi "mkawa wahalifu." Yaani, wenye kutakabari mkaacha kumwabudu, na mkafanya ujasiri wa kufanya maharamisho yake.
#
{53} فقالوا رادِّين لقوله: {يا هودُ ما جئتَنا ببيِّنةٍ}: إن كان قصدُهم بالبينة البينة التي يقترحونها؛ فهذه غير لازمة للحقِّ، بل اللازم أن يأتي النبيُّ بآية تدلُّ على صحة ما جاء به، وإن كان قصدُهم أنه لم يأتهم ببيِّنة تشهدُ لما قاله بالصحة؛ فقد كذبوا في ذلك؛ فإنَّه ما جاء نبيٌّ لقومه إلاَّ وبعث الله على يديه من الآيات ما يؤمن على مثله البشر، ولو لم يكن له آية إلاَّ دعوتُه إياهم لإخلاص الدين لله وحده لا شريك له، والأمر بكلِّ عمل صالح وخُلُق جميل، والنهي عن كلِّ خُلُق ذميم من الشرك بالله والفواحش والظُّلم وأنواع المنكرات، مع ما هو مشتملٌ عليه هودٌ عليه السلام من الصفات التي لا تكون إلاَّ لخيار الخلق وأصدقهم، لكفى بها آيات وأدلة على صدقه، بل أهل العقول وأولو الألباب يرون أنَّ هذه الآية أكبر من مجرَّد الخوارق التي يراها بعض الناس هي المعجزات فقط.
ومن آياته وبيِّناته الدالة على صدقه أنَّه شخصٌ واحدٌ، ليس له أنصار ولا أعوان، وهو يصرخُ في قومه ويناديهم ويعجِزُهم ويقول لهم: إنِّي توكلتُ على الله ربِّي وربكم، {إنِّي أُشْهِدُ اللهَ واشْهَدوا أنِّي بريءٌ مما تشرِكونَ. من دونِهِ فكيدوني جميعاً ثم لا تُنظِرونِ}: وهم الأعداءُ الذين لهم السَّطوة والغَلَبة، ويريدون إطفاء ما معه من النور بأيِّ طريق كان، وهو غير مكترث منهم ولا مبال بهم، وهم عاجزون لا يقدرون أن ينالوه بشيءٍ من السُّوء، إنِّ في ذلك لآيات لقوم يعقلون. وقولهم: {وما نحنُ بتارِكي آلهتنا عن قولِكَ}؛ أي: لا نترك عبادةَ آلهتنا لمجرَّد قولِكَ الذي ما أقمتَ عليه بيِّنةً بزعمهم. {وما نحنُ لك بمؤمنينَ}: وهذا تأييس منهم لنبيِّهم هودٍ عليه السلام في إيمانهم، وأنهم لا يزالون في كفرهم يعمهون.
{53} Wakasema wakiikataa kauli yake: {Ewe Hud! Hujatuletea ushahidi ulio wazi." Ikiwa makusudio yao ni ushahdii ulio wazi wanaoupendekeza wao, basi hili si jambo la lazima ili ayasemayo yawe ndiyo haki. Bali la lazima ni kwamba nabii aje na ishara inayoashiria usahihi wa kile alichokuja nacho. Na kama makusudio yao ni kwamba hakuwajia na ushahidi unaoshuhudia usahihi wa kile alichokuja nacho, basi hakika walidanganya katika hilo. Kwa maana, hakuwahi kuja nabii yeyote kwa kaumu yake isipokuwa Mwenyezi Mungu alituma kwa mikono yake Ishara ambazo wanaadamu wanaamini mfano wake, na kama hangekuwa na ishara isipokuwa kuwalingania tu wampwekeshee Mwenyezi Mungu Dini bila ya mshirika yeyote, na kuamrisha kila tendo jema, na tabia nzuri, na kukataza kila tabia mbaya miongoni mwa kumshirikisha Mwenyezi Mungu na dhuluma na aina mbalimbali za maovu, pamoja na yale anayosifika kwayo Hud, amani iwe juu yake ya sifa ambazo haziwi isipokuwa viumbe bora zaidi na wakweli wao zaidi. Basi Haya yangetosha kuwa ishara na ushahidi juu ya ukweli wake. Bali watu wenye akili na ufahamu wanaona kwamba ishara hii ni kubwa zaidi kuliko mambo ya kimuujiza ambayo baadhi ya watu wanayaona kuwa ndiyo miujiza tu. Na miongoni mwa ishara zake na ushahidi wake ulio wazi unaoashiria ukweli wake ni kwamba alikuwa mtu mmoja tu bila ya wa kumnusuru wala wasaidizi, lakini yeye akawa anasema kwa sauti kubwa katika kaumu yake na kuwaita na kuwaona kwamba hawana uwezo.
Na anawaambia: Hakika mimi ninamtegemea Mwenyezi Mungu wangu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. "Hakika, mimi ninamshuhudisha Mwenyezi Mungu, na nyinyi shuhudieni, ya kwamba mimi niko mbali na hao mnaowafanya washirika. Badala ya Yeye. Basi nyinyi nyote nipangieni njama, na kisha msinipe muhula!" Ilhali wao ni maadui ambao wana uwezo na ushindi, na wanataka kuzima nuru aliyo nayo kwa njia yoyote ile, naye akawa hashughuliki nao wala kuwajali, nao wakawa wameshindwa na hawawezi kumfikishia mabaya yoyote. hakika katika hayo zimo ishara kwa kaumu wanaotumia akili.
Na kauli yao: "Wala sisi hatuiachi miungu yetu kwa kufuata kauli yako." Yaani, hatuachi kuabudu miungu yetu kwa sababu tu ya yale uliyoyasema, ambayo hukuyasimamishia ushahidi wowote - kulingana na madai yao. "Na wala sisi hatukuamini wewe" na huku ni kumkatisha kwao tamaa nabii wao Hud - amani iwe juu yake - katika kuamini kwao. Na kwamba hawataacha kuendelea kutangatanga kiupofu katika ukafiri wao.
#
{54} {إن نقولُ}: فيك {إلاَّ اعتراكَ بعضُ آلهتنا بسوءٍ}؛ أي: أصابتك بخبال وجنون، فصرتَ تَهْذي بما لا يُعْقَلُ؛ فسبحان من طبع على قلوب الظالمين! كيف جعلوا أصدقَ الخلق الذي جاء بأحقِّ الحقِّ بهذه المرتبة التي يستحي العاقل من حكايتها عنهم، لولا أنَّ الله حكاها عنهم؟!
{54} "Sisi tunasema" kukuhusu wewe: "Baadhi ya miungu yetu imekusibu kwa baa." Yaani imekusibu na ubaya na wendawazimu, basi ukawa unaropoka mambo yasiyoeleweka. Ametakasika yule aliyezifunga nyoyo za madhalimu! Ni vipi walimfanya kiumbe mkweli zaidi ambaye alikuja na haki ya haki zote katika daraja hili ambalo mtu mwenye akili timamu anaona haya kulieleza kutoka kwao, kama si tu kwamba Mwenyezi Mungu aliyasimulia kuwahusu?
#
{55} ولهذا بيَّن هودٌ عليه الصلاة والسلام أنه واثقٌ غاية الوثوق أنَّه لا يصيبُه منهم ولا من آلهتهم أذىً، فقال: {إنِّي أُشْهِدُ الله واشْهَدوا أنِّي بريءٌ مما تشركون. من دونِهِ فكيدوني جميعاً}؛ أي: اطلبوا لي الضَّرر كلُّكم بكلِّ طريق تتمكَّنون بها منِّي، {ثم لا تُنظِرونِ}؛ أي: لا تمهلوني.
55. Na ndiyo maana Hud -rehema na Amani zimshukie - akabainisha kuwa yeye ana imani kubwa zaidi kwamba hatapatwa na madhara yoyote kutoka kwao wala kutoka kwa miungu yao.
Kwa hivyo akasema: "Hakika, mimi ninamshuhudisha Mwenyezi Mungu, na nyinyi shuhudieni, ya kwamba mimi niko mbali na hao mnaowafanya washirika."
"Badala ya Yeye. Basi nyinyi nyote nipangieni njama." Yaani, nitafutieni madhara nyinyi nyote kwa kila njia muwezayo dhidi yangu, "kisha msinipe muhula."
#
{56} {إني توكلتُ على الله}؛ أي: اعتمدت في أمري كلِّه على الله، {ربِّي وربِّكم}؛ أي: هو خالق الجميع ومدبِّرنا وإيَّاكم، وهو الذي ربَّانا. {ما من دابَّةٍ إلاَّ هو آخذٌ بناصيتها}: فلا تتحرَّك ولا تسكُن إلا بإذنِهِ؛ فلو اجتمعتُم جميعاً على الإيقاع بي، والله لم يسلِّطْكم عليَّ؛ لم تقدِروا على ذلك؛ فإن سلَّطكم فلحكمةٍ أرادَها. {إنَّ ربِّي على صراطٍ مستقيم}؛ أي: على عدل وقِسْطٍ وحكمةٍ وحمدٍ في قضائه وقَدَرِهِ و [في] شرعِهِ وأمره وفي جزائه وثوابه وعقابه، لا تخرجُ أفعالُه عن الصراط المستقيم التي يُحْمَد، ويُثنى عليه بها.
{56} "Hakika mimi nimemtegemea Mwenyezi Mungu." Yaani, nimemtegemea Mwenyezi Mungu katika mambo yangu yote, "Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi." Yaani, Yeye ndiye Muumba wa kila kitu, na mwendeshaji wetu na nyinyi, naye ndiye aliyetulea. "Hakuna kiumbe yeyote isipokuwa Yeye anamwendesha atakavyo," basi hutafanya harakati zozote wala kutulia isipokuwa kwa idhini yake. Kwa hivyo, ikiwa mtakusanyika nyote pamoja ili kunishambulia, na Mwenyezi Mungu hakuwapa mamlaka dhidi yangu, basi hamtaweza hilo. lakini akiwapa mamlaka dhidi yangu, basi ni kwa sababu ya hekima aliyotaka. "Hakika Mola wangu Mlezi yuko kwenye njia iliyonyooka." Yaani, Yeye yuko kwenye uadilifu, na haki, na ni Mwenye hekima, na Mwenye kusifiwa katika hukumu zake na majaliwa Yake, na
[katika] sheria yake na amri yake, na katika malipo Yake, na thawabu zake na adhabu yake. Vitendo vyake havitoki katika njia iliyonyooka ambayo anahimidiwa na kusifiwa kwayo.
#
{57} {فإن تولَّوا}: عما دعوتُكم إليه، {فقد أبلغتكُم ما أُرْسِلْتُ به إليكم}: فلم يبقَ عليَّ تَبِعَةٌ من شأنكم، {ويستخلِفُ ربِّي قوماً غيركم}: يقومون بعبادته ولا يشرِكون به شيئاً، {ولا تضرُّونه شيئاً}: فإنَّ ضرركم إنما يعودُ إليكم ؛ فالله لا تضرُّه معصية العاصين ولا تنفعه طاعةُ الطائعين ، مَنْ عمل صالحاً؛ فلنفسه، ومَن أساء؛ فعليها. {إنَّ ربِّي على كلِّ شيء حفيظٌ}.
{57} "Na wakikengeuka" kutoka katika yale niliyowalingania "basi hakika mimi nimekwisha wafikishia yale niliyotumwa nayo kwenu." Basi haijabakia lawama yoyote juu yangu katika jambo lenu "wala nyinyi hamumdhuru kitu Yeye," kwa maana madhara yenu yanarudi tu kwenu. Kwani, Mwenyezi Mungu hayamdhuru maasia ya waasi, wala haumnufaishi utiifu wa watiifu. Mwenye kutenda mema, basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na mwenye kufanya ubaya, basi ni juu yake pia. "Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kuhifadhi kila kitu."
#
{58} {ولما جاء أمرُنا}؛ أي: عذابُنا بإرسال الريح العقيم التي ما تَذَرُ من شيء أتت عليه إلاَّ جَعَلَتْهُ كالرَّميم؛ {نجَّينا هوداً والذين آمنوا معه برحمةٍ منَّا ونَجَّيْناهم من عذاب غليظٍ}؛ أي: عظيم شديد أحلَّه الله بعادٍ فأصبحوا لا يُرى إلاَّ مساكنُهم.
{58} "Na ilipofika amri yetu;" yaani, adhabu yetu kwa kuutuma upepo tasa ambao hauachi chochote unachokifikia isipokuwa unakifanya kama kilichonyambuka, "tulimwokoa Hud na wale walioamini pamoja naye, kwa rehema itokayo kwetu. Na tukawaokoa na adhabu kali;" yaani, kubwa na kali. Mwenyezi Mungu aliifikisha kwa watu wa 'Aadi, kwa hivyo wakaishia hayaonekani isipokuwa maskani yao tu.
#
{59} {وتلك عادٌ}: الذين أوقع الله بهم ما أوقعَ بظُلْم منهم لأنهم {جَحَدوا بآيات ربِّهم}: ولهذا قالوا لهود: ما جئتَنا ببيِّنةٍ! فتبيَّن بهذا أنهم متيقِّنون لدعوته، وإنما عاندوا وجحدوا، {وعَصَوا رُسُلَه}؛ لأنَّ من عصى رسولاً؛ فقد عصى جميع المرسلين؛ لأنَّ دعوتهم واحدة، {واتَّبعوا أمر كلِّ جبارٍ}؛ أي: متسلِّط على عباد الله بالجبروت، {عنيدٍ}؛ أي: معاند لآيات الله، فعصَوْا كلَّ ناصح ومشفق عليهم، واتَّبعوا كلَّ غاشٍّ لهم يريد إهلاكَهم، لا جَرَمَ أهلكهم الله.
59. "Na hao ndio kina 'Aadi" ambao Mwenyezi Mungu aliwafikishia yale aliyowafikishia kwa sababu ya dhuluma yao, kwa sababu "Walizikufuru Ishara za Mola wao Mlezi.
" Na ndiyo maana wakamwambia Hud: Hukutujia na ushahidi wowote ulio wazi! Kwa hivyo, ikabainika kwa hili kuwa wao walikuwa na yakini juu ya ulinganizi wake, lakini walikaidi tu na wakakataa, "na wakawaasi Mitume wake." Kwa sababu, mwenye kumuasi Mtume mmoja, basi hakika ameshawaasi Mitume wote; kwa sababu, wito wao ni mmoja. "Na wakafuata amri ya kila jabari;" yaani, anayejipa mamlaka juu ya waja wa Mwenyezi Mungu kwa kuwakandamiza. "Mkaidi;" yaani, anayezikaidi ishara za Mwenyezi Mungu, na wakamuasi kila mshauri na mwenye kuwahurumia vikubwa, na wakamfuata kila mwenye kuwadanganya anayetaka kuwaangamiza. Basi hakuna shaka kwamba ndiyo sababu ya Mwenyezi Mungu kuwaangamiza.
#
{60} {وأتبعوا في هذه الدُّنيا لعنةً}: فكل وقتٍ وجيل إلا ولأنبائهم القبيحة وأخبارهم الشنيعة ذِكْرٌ يذكَرون به وذمٌّ يلحقُهم. {ويوم القيامة}: لهم أيضاً لعنةٌ، {ألا إنَّ عاداً كفروا ربَّهم}؛ أي: جحدوا مَنْ خَلَقَهم ورَزَقَهم وربَّاهم. {ألا بعداً لعادٍ قوم هود}؛ أي: أبعدهم الله عن كلِّ خير، وقرَّبهم من كلِّ شرٍّ.
{60} "Na wakafuatishiwa laana katika dunia hii." Kwa hivyo, hakuna katika nyakati zote na kizazi isipokuwa kwa sababu ya habari zao mbaya na za kuchukiza wanatajwa kwa utajo kwa kukashifiwa kwao. "Na Siku ya Qiyama" pia watapata laana. "Basi tambueni mtanabahi kuwa hakika kina 'Aadi walimkufuru Mola wao Mlezi." Yaani, walimkataa yule aliyewaumba, na akawaruzuku, na akawalea. "Na tambueni mtanabahi kuwa hakika waliangamizwa kina 'Aadi, kaumu ya Hud." Yaani, Mwenyezi Mungu aliwaweka mbali na kila heri, na akawaleta karibu na kila uovu.
{وَإِلَى ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا قَالَ يَاقَوْمِ اعْبُدُوا اللَّهَ مَا لَكُمْ مِنْ إِلَهٍ غَيْرُهُ هُوَ أَنْشَأَكُمْ مِنَ الْأَرْضِ وَاسْتَعْمَرَكُمْ فِيهَا فَاسْتَغْفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ إِنَّ رَبِّي قَرِيبٌ مُجِيبٌ (61) قَالُوا يَاصَالِحُ قَدْ كُنْتَ فِينَا مَرْجُوًّا قَبْلَ هَذَا أَتَنْهَانَا أَنْ نَعْبُدَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا وَإِنَّنَا لَفِي شَكٍّ مِمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ مُرِيبٍ (62) قَالَ يَاقَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِنْ كُنْتُ عَلَى بَيِّنَةٍ مِنْ رَبِّي وَآتَانِي مِنْهُ رَحْمَةً فَمَنْ يَنْصُرُنِي مِنَ اللَّهِ إِنْ عَصَيْتُهُ فَمَا تَزِيدُونَنِي غَيْرَ تَخْسِيرٍ (63) وَيَاقَوْمِ هَذِهِ نَاقَةُ اللَّهِ لَكُمْ آيَةً فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللَّهِ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ قَرِيبٌ (64) فَعَقَرُوهَا فَقَالَ تَمَتَّعُوا فِي دَارِكُمْ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ ذَلِكَ وَعْدٌ غَيْرُ مَكْذُوبٍ (65) فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا صَالِحًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِنَّا وَمِنْ خِزْيِ يَوْمِئِذٍ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ الْقَوِيُّ الْعَزِيزُ (66) وَأَخَذَ الَّذِينَ ظَلَمُوا الصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دِيَارِهِمْ جَاثِمِينَ (67) كَأَنْ لَمْ يَغْنَوْا فِيهَا أَلَا إِنَّ ثَمُودَ كَفَرُوا رَبَّهُمْ أَلَا بُعْدًا لِثَمُودَ (68)}.
61. Na kina Thamud tuliwatumia ndugu yao Saleh.
Akasema: Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu yeyote isipokuwa Yeye. Yeye ndiye aliyewaumba kutoka katika ardhi, na akawaweka humo imara. Basi mwombeni msamaha, kisha mtubu kwake. Hakika Mola wangu Mlezi yupo karibu, anaitikia maombi. 62.
Wakasema: Ewe Saleh! Hakika kabla ya haya ulikuwa unatarajiwa heri kwetu. Je, unatukataza kuwaabudu wale ambao baba zetu walikuwa wakiwaabudu? Na hakika sisi tuna shaka na wasiwasi kwa hayo unayotuitia. 63.
Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwaonaje ikiwa ninao ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wangu Mlezi, naye akawa amenipa rehema kutoka kwake, je, ni nani atakayeninusuru kutokana na Mwenyezi Mungu nikimuasi? Basi nyinyi hamnizidishii isipokuwa kuhasirika tu. 64. Na enyi kaumu yangu! Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu kama Ishara kwenu. Basi mwacheni ale katika ardhi ya Mwenyezi Mungu, wala msimguse kwa ubaya, ikaja kuwaangamiza adhabu iliyo karibu. 65. Lakini wakamchinja. Basi
(Saleh) akasema: Stareheni katika makazi yenu muda wa siku tatu. Hiyo ni ahadi isiyokuwa ya uongo. 66. Basi ilipokuja amri yetu, tulimwokoa sawasawa Saleh na wale walioamini pamoja naye kwa rehema yetu kutokana na hizaya ya siku ile. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu, Mtukufu. 67. Na ukelele uliwaangamiza wale waliodhulumu, basi wakaishia majumbani mwao wamekufa kifudifudi! 68. Kama kwamba hawakuishi kwa ustawi huko. Hebu zingatieni! Hakika kina Thamud walimkufuru Mola wao Mlezi. Hebu zingatieni! Thamud walipotelea mbali!
#
{61} أي: {و} أرسلنا {إلى ثمودَ}: وهم عادٌ الثانية، المعروفون، الذين يسكنون الحِجْر ووادي القُرى، {أخاهم}: في النسب، {صالحاً}: عبد الله ورسوله - صلى الله عليه وسلم -، يدعوهم إلى عبادة الله وحده. فَـ {قَالَ يا قومِ اعبُدوا الله}؛ أي: وحِّدوه وأخلصوا له الدين، {ما لكُم من إلهٍ غيرُه}: لا من أهل السماء ولا من أهل الأرض، {هو أنشأكم من الأرض}؛ أي: خلقكم فيها، فقال: {واستعمَرَكم فيها}؛ أي: استخلفكم فيها وأنعم عليكم بالنِّعم الظاهرة والباطنة، ومكَّنكم في الأرض؛ تَبْنون وتغرسون وتزرعون وتحرثون ما شئتم وتنتفعون بمنافعها وتستغلون مصالحها؛ فكما أنَّه لا شريك له في جميع ذلك؛ فلا تشركوا به في عبادته. {فاستغفروه}: مما صَدَرَ منكم من الكفر والشِّرْك والمعاصي وأقلعوا عنها، {ثمَّ توبوا إليه}؛ أي: ارجِعوا إليه بالتوبة النصوح والإنابة. {إنَّ ربِّي قريبٌ مجيبٌ}؛ أي: قريبٌ ممَّن دعاه دعاء مسألة أو دعاء عبادة يجيبه بإعطائِهِ سؤاله وقَبول عبادتِهِ وإثابته عليها أجلَّ الثواب.
واعلم أنَّ قُرْبَهُ تعالى نوعان: عامٌّ وخاصٌّ: فالقربُ العامُّ: قربُه بعلمه من جميع الخلق، وهو المذكور في قوله تعالى: {ونحنُ أقربُ إليه من حبل الوريدِ}.
والقربُ الخاصُّ: قربُه من عابديه وسائليه ومحبِّيه، وهو المذكورُ في قوله تعالى: {فاسجُدْ واقْتَرِبْ}، وفي هذه الآية، وفي قوله: {وإذا سألك عبادي عنِّي فإنِّي قريبٌ أجيبُ دعوةَ الدَّاعي}، وهذا النوع قربٌ يقتضي إلطافه تعالى وإجابته لدعواتهم وتحقيقه لمراداتهم، ولهذا يقرن باسمه القريب اسمه المجيب.
{61} Yaani: {Na" tuliwatuma "kwa Thamud." Nao ni kina 'Aadi wa pili, wanaojulikana, ambao walikuwa wakiishi huko Al-Hijr na Wadi Al-Qura, "ndugu yao" kwa nasaba, "Saleh" mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - akiwalingania kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake. Basi "Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu." Yaani, mpwekesheni yeye na mumfanyie yeye tu Dini. "Nyinyi hamna Mungu yeyote isipokuwa Yeye" si katika wakazi wa mbinguni wala katika wakazi wa ardhini. "Yeye ndiye aliyewaumba kutoka katika ardhi." Yaani, aliwaumba humo,
na akasema: "Na akawaweka humo imara." Yaani, aliwafanya kuwa wafuatilizi humo na akawaneemesha kwa neema za dhahiri na zilizofichikana, na akawaimarisha katika ardhi. Mnaweza kujenga, na kupanda, na kulima chochote mnachotaka, na mnafaidika kwa manufaa yake na kutumia masilahi yake. Kwa hivyo, kama vile hana mshirika yeyote katika hayo yote, basi msishirikishe na wengine katika kumwabudu. "Basi mwombeni msamaha" kwa yale mliyofanya ya kufuru, na ushirikina, na maasia na achaneni nayo, "kisha mtubu kwake." Yaani, rejeeni kwake kwa toba ya kweli na kurudi katika utiifu. "Hakika Mola wangu Mlezi yupo karibu, anaitikia maombi." Yaani, yuko karibu na yule anayemwomba kwa dua ya kutaka kitu, au dua ya ibaada, naye humwitikia kwa kumpa ombi lake, na kuikubali ibada yake, na kumlipa kwayo malipo makubwa zaidi.
Na jua kuwa ukaribu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni aina mbili: wa jumla na makhsusi.
Basi ukaribu wa jumla ni ukaribu wake kwa elimu yake juu ya viumbe vyote ambao umetajwa katika kauli yake Mtukufu: "Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake." Na ukaribu mahususi ni Ukaribu wake kwa waja wake, wale wanaomuomba na wale wanaompenda.
Nao ndio uliotajwa katika kauli yake Mtukufu: "Basi sujudu na ujongee!" Na katika Aya hii,
na katika kauli yake: "Na waja wangu watakapokuuliza habari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji." Na aina hii ya ukaribu inalazimu upole wake yeye Mtukufu na kuitikia kwake dua zao, na kutimiza kwake matashi yao. Na ndiyo maana jina lake "Al-Qarib
(Aliye karibu)" huunganishwa na jina lake "Al-Mujib
(mwenye kuitikia)."
#
{62} فلما أمرهم نبيُّهم صالحٌ عليه السلام ورغَّبهم في الإخلاص لله وحده؛ ردُّوا عليه دعوته، وقابلوه أشنع المقابلة. و {قالوا يا صالحُ قد كنتَ فينا مرجُوًّا قبلَ هذا}؛ أي: قد كنَّا نرجوك ونؤمِّل فيك العقل والنفع، وهذا شهادةٌ منهم لنبيِّهم صالح: أنَّه ما زال معروفاً بمكارم الأخلاق ومحاسن الشيم، وأنَّه من خيار قومه، ولكنَّه لمَّا جاءهم بهذا الأمر الذي لا يوافِقُ أهواءهم الفاسدة؛ قالوا هذه المقالة التي مضمونُها أنَّك قد كنتَ كاملاً، والآن أخلفتَ ظنَّنا فيك، وصرتَ بحالةٍ لا يُرجى منك خيرٌ، وذنبه ما قالوه عنه، [وهو قولهم]: {أتَنْهانا أن نعبُدَ ما يعبُدُ آباؤنا}: وبزعمهم أنَّ هذا من أعظم القدح في صالح؛ كيف قَدَحَ في عقولهم وعقول آبائهم الضالِّين؟! وكيف ينهاهم عن عبادة مَنْ لا ينفع ولا يضرُّ ولا يغني شيئاً من الأحجار والأشجار ونحوها، وأمرهم بإخلاص الدِّين لله ربِّهم الذي لم تزلْ نِعَمُهُ عليهم تَتْرى وإحسانُهُ عليهم دائماً ينزِلُ، الذي ما بهم من نعمةٍ إلا منه، ولا يدفع عنهم السيئات إلا هو؟! {وإنَّنا لفي شكٍّ مما تدعونا إليه مُرِيبٍ}؛ أي: ما زلنا شاكِّين فيما دعوتَنا إليه شكًّا مؤثِّراً في قلوبنا الريب.
{62} Basi Nabii wao Saleh amani iwe juu yake alipowaamrisha na akawahimiza wamkusudie Mwenyezi Mungu peke yake, wakaukataa wito wake huo, na wakaukabili kuukabili kubaya zaidi.
Na "Wakasema: Ewe Saleh! Hakika kabla ya haya ulikuwa unatarajiwa heri kwetu." Yaani, tulikuwa tukikutarajia na kuwa na matumaini nawe kwamba una akili na manufaa. Na huu ni ushahidi kutoka kwao kwa Nabii wao Saleh kwamba hakuacha kujulikana kwa tabia njema na maadili ya hali ya juu, na kwamba yeye ni miongoni mwa walio bora zaidi wa kaumu yake, lakini alipowajia na jambo hili ambalo halikukubaliana na matamanio yao maovu. Wakasema maneno haya ambayo makusudio yake ni kwamba wewe hakika ulikuwa mkamilifu, na sasa umeyafelisha maoni yetu kuhusiana nawe, na umekuwa katika hali ambayo hakuna heri yoyote inayotarajiwa kutoka kwako. Na dhambi yake ni yale waliyosema juu yake,
[ambayo ni kauli yao]: "Je unatukataza kuwaabudu wale ambao baba zetu walikuwa wakiwaabudu?" Na kulingana na madai yao ni kwamba hilo ni miongoni mwa doa kubwa zaidi kwa Saleh. Vipi alikashifu akili zao na akili za baba zao wapotovu? Na vipi anawakataza kuwaabudu wale ambao hawanufaishii, wala hawadhuru, wala hawasaidii kitu, miongoni mwa mawe, na miti, na mfano wake, na akawaamrisha kumfanyia dini Mwenyezi Mungu tu, Mola wao Mlezi ambaye neema zake juu yao hazijaacha kufuatana, na kuteremka kwa wema wake juu yao kwa daima, na ambaye hakuna neema yoyote isipokuwa ni kutoka kwake, wala hakuna yeyote anayewazuia kutokana na mabaya isipokuwa Yeye? "Na hakika sisi tuna shaka na wasiwasi kwa hayo unayotuitia." Yaani, bado tuko katika shaka juu ya yale uliyotulingania. Nayo ni shaka inayotia kusitasita kukubwa mioyoni mwetu.
#
{63} وبزعمهم أنَّهم لو علموا صحَّة ما دعاهم إليه؛ لاتَّبعوه، وهم كَذَبَةٌ في ذلك، ولهذا بيَّن كذِبَهم في قوله: {قال يا قومِ أرأيتُم إن كنتُ على بيِّنةٍ من ربِّي}؛ أي: برهان ويقين منِّي، {وآتاني منه رحمةً}؛ أي: مَنَّ عليَّ برسالته ووحيه؛ أي: أفأتابعكم على ما أنتم عليه وما تدعونني إليه. {فمن ينصُرُني من الله إن عصيتُهُ فما تزيدونَني غير تخسيرٍ}؛ أي: غير خسار وتَباب وضرر.
{63} Na kwa madai yao kwamba lau wangelijua usahihi wa yale aliyowalingania, basi wangemfuata, na ilhali wao ni waongo katika hilo. Na ndiyo maana akaeleza uongo wao katika kauli yake.
"Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwaonaje ikiwa ninao ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wangu Mlezi" yaani niko na hoja na yakini {naye akawa amenipa rehema kutoka kwake" Yaani, amenineemesha kwa ujumbe wake na wahyi wake. Yaani, Je, niwafuate katika hayo mliyo juu yake na yale mnayoniitia? "Je, ni nani atakayeninusuru kutokana na Mwenyezi Mungu nikimuasi? Basi nyinyi hamnizidishii isipokuwa kuhasirika tu." Yaani, isipokuwa hasara tu, na maangamio, na madhara.
#
{64} {ويا قوم هذه ناقةُ الله لكم آيةً}: لها شِرْبٌ من البئر يوماً، ثم يشربون كلُّهم مِنْ ضَرْعها، ولهم شِرْبُ يوم معلوم، {فَذَروها تأكُلْ في أرض الله}؛ أي: ليس عليكم من مؤنتها وعلفها شيءٌ، {ولا تمسُّوها بسوءٍ}؛ أي: بعقرٍ؛ {فيأخُذَكم عذابٌ قريبٌ}.
{64} "Na Enyi kaumu yangu! Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu kama Ishara kwenu," anayo siku moja ya kunywa kisimani, kisha wote watakunywa katika kiwele chake, nao pia wana siku maalumu ya kunywa kisimani. "Basi mwacheni ale katika ardhi ya Mwenyezi Mungu." Yaani, hamlazimiki chochote katika kumsimamia wala kumlisha, "wala msimguse kwa ubaya." Yaani, kwa kumchinja "ikaja kuwaangamiza adhabu iliyo karibu."
#
{65} {فعقروها فقال}: لهم صالحٌ: {تمتَّعوا في دارِكُم ثلاثة أيَّام ذلك وعدٌ غير مكذوبٍ}: بل لا بدَّ من وقوعه.
{65} "Basi wakamchinja,
na" Salih "akasema: starehekeni katika makazi yenu siku tatu, hii ni ahadi isiyokuwa ya uongo;" bali ni lazima itatokea.
#
{66} {فلمَّا جاء أمرُنا}: بوقوع العذاب، {نجَّيْنا صالحاً والذين آمنوا معه برحمةٍ منَّا ومِنْ خِزْي يومِئِذٍ}؛ أي: نجيناهم من العذاب والخزي والفضيحة. {إنَّ ربَّك هو القويُّ العزيز}: ومن قوَّته وعزَّته أن أهلك الأممَ الطاغيةَ ونجَّى الرسلَ وأتباعهم.
{66} "Basi ilipokuja amri yetu" ya kutokea kwa adhabu, "tulimwokoa sawasawa Saleh na wale walioamini pamoja naye kwa rehema yetu kutokana na hizaya ya siku ile." Yaani, tuliwaokoa sawasawa na adhabu, na hizaya, na fedheha. "Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu, Mtukufu." Na katika nguvu zake na utukufu wake ni kuwa aliziangamiza umma waliopitiliza mipaka na akawaokoa Mitume na wafuasi wao.
#
{67} وأخذت {الذين ظلموا الصيحة}: فقطعت قلوبهم؛ {فأصبحوا في ديارهم جاثمين}؛ أي: خامدين لا حراك لهم.
{67} Na ukawaangamiza "ukelele wale waliodhulumu" na ukazikata nyoyo zao. "Basi wakaishia majumbani mwao wamekufa kifudifudi!" Yaani, huku wamezimika bila kuwa na harakati zozote.
#
{68} {كأن لم يَغْنَوْا فيها}؛ أي: كأنهم لما جاءهم العذاب ما تمتَّعوا في ديارهم ولا أنسوا فيها ولا تنعَّموا بها يوماً من الدَّهر، قد فارقهم النعيمُ، وتناولهم العذابُ السرمديُّ، الذي لا ينقطع، الذي كأنه لم يزل. {ألا إنَّ ثمودَ كَفَروا ربَّهم}؛ أي: جحدوه بعد أن جاءتهم الآيةُ المبصرةُ. {ألا بُعداً لِثمودَ}: فما أشقاهم وأذلَّهم! نستجير بالله من عذاب الدُّنيا وخزيها.
{68} "Kama kwamba hawakuishi kwa ustawi huko." Yaani, kana kwamba wakati ilipowajia adhabu, hawakuwa wamewahi kustarehe katika majumba yao, wala hawatulia humo, wala hawakuzifurahia hata kwa siku moja ya maisha. Starehe hiyo ikawa imewatoka, na ikawachukua adhabu ya Milele ambayo haikomi, ambayo ni kana kwamba haikuacha kuendelea. "Hebu zingatieni! Hakika kina Thamud walimkufuru Mola wao Mlezi." Yaani walimkataa baada ya kujiwa na Ishara yenye kuonyesha. "Hebu zingatieni! Thamud walipotelea mbali!" Basi ni mashaka makubwa vipi waliyo nayo! Na ni udhalilifu mkubwa vipi uliowapata! Tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na adhabu ya dunia hii na hizaya yake.
{وَلَقَدْ جَاءَتْ رُسُلُنَا إِبْرَاهِيمَ بِالْبُشْرَى قَالُوا سَلَامًا قَالَ سَلَامٌ فَمَا لَبِثَ أَنْ جَاءَ بِعِجْلٍ حَنِيذٍ (69) فَلَمَّا رَأَى أَيْدِيَهُمْ لَا تَصِلُ إِلَيْهِ نَكِرَهُمْ وَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً قَالُوا لَا تَخَفْ إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَى قَوْمِ لُوطٍ (70) وَامْرَأَتُهُ قَائِمَةٌ فَضَحِكَتْ فَبَشَّرْنَاهَا بِإِسْحَاقَ وَمِنْ وَرَاءِ إِسْحَاقَ يَعْقُوبَ (71) قَالَتْ يَاوَيْلَتَى أَأَلِدُ وَأَنَا عَجُوزٌ وَهَذَا بَعْلِي شَيْخًا إِنَّ هَذَا لَشَيْءٌ عَجِيبٌ (72) قَالُوا أَتَعْجَبِينَ مِنْ أَمْرِ اللَّهِ رَحْمَتُ اللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ عَلَيْكُمْ أَهْلَ الْبَيْتِ إِنَّهُ حَمِيدٌ مَجِيدٌ (73) فَلَمَّا ذَهَبَ عَنْ إِبْرَاهِيمَ الرَّوْعُ وَجَاءَتْهُ الْبُشْرَى يُجَادِلُنَا فِي قَوْمِ لُوطٍ (74) إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَحَلِيمٌ أَوَّاهٌ مُنِيبٌ (75) يَاإِبْرَاهِيمُ أَعْرِضْ عَنْ هَذَا إِنَّهُ قَدْ جَاءَ أَمْرُ رَبِّكَ وَإِنَّهُمْ آتِيهِمْ عَذَابٌ غَيْرُ مَرْدُودٍ (76) وَلَمَّا جَاءَتْ رُسُلُنَا لُوطًا سِيءَ بِهِمْ وَضَاقَ بِهِمْ ذَرْعًا وَقَالَ هَذَا يَوْمٌ عَصِيبٌ (77) وَجَاءَهُ قَوْمُهُ يُهْرَعُونَ إِلَيْهِ وَمِنْ قَبْلُ كَانُوا يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ قَالَ يَاقَوْمِ هَؤُلَاءِ بَنَاتِي هُنَّ أَطْهَرُ لَكُمْ فَاتَّقُوا اللَّهَ وَلَا تُخْزُونِ فِي ضَيْفِي أَلَيْسَ مِنْكُمْ رَجُلٌ رَشِيدٌ (78) قَالُوا لَقَدْ عَلِمْتَ مَا لَنَا فِي بَنَاتِكَ مِنْ حَقٍّ وَإِنَّكَ لَتَعْلَمُ مَا نُرِيدُ (79) قَالَ لَوْ أَنَّ لِي بِكُمْ قُوَّةً أَوْ آوِي إِلَى رُكْنٍ شَدِيدٍ (80) قَالُوا يَالُوطُ إِنَّا رُسُلُ رَبِّكَ لَنْ يَصِلُوا إِلَيْكَ فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِنَ اللَّيْلِ وَلَا يَلْتَفِتْ مِنْكُمْ أَحَدٌ إِلَّا امْرَأَتَكَ إِنَّهُ مُصِيبُهَا مَا أَصَابَهُمْ إِنَّ مَوْعِدَهُمُ الصُّبْحُ أَلَيْسَ الصُّبْحُ بِقَرِيبٍ (81) فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا جَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهَا حِجَارَةً مِنْ سِجِّيلٍ مَنْضُودٍ (82) مُسَوَّمَةً عِنْدَ رَبِّكَ وَمَا هِيَ مِنَ الظَّالِمِينَ بِبَعِيدٍ (83)}.
69. Na hakika wajumbe wetu walimjia Ibrahim kwa bishara njema, wakasema, "Salama!" Naye akasema, "Salama!" Kisha hakukaa isipokuwa mara hiyo akaja na ndama wa kuchoma. 70. Basi alipoiona mikono yao haimfikii, akawatilia shaka, na akawahofu. Wakasema, "Usihofu! Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya Lut." 71. Na mkewe alikuwa amesimama wima, akacheka. Basi tukambashiria kuhusu
(kuzaliwa kwa) Is-haq, na baada ya Is-haq Yaaqub. 72. Akasema, "Ole wangu! Mimi nizae ilhali mimi ni ajuza? Na tena huyu mume wangu ni mzee? Hakika haya ni mambo ya ajabu!" 73.
Wakasema: Je, unastaajabia amri ya Mwenyezi Mungu? Rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake ziwe juu yenu, enyi watu wa nyumba hii! Hakika Yeye ndiye Msifika, Mtukufu. 74. Basi hofu ilipomwondoka Ibrahim, na ikawa ile bishara imemfikia, alianza kujadiliana nasi juu ya kaumu ya Lut. 75. Hakika Ibrahim alikuwa mvumilivu sana, mwenye huzuni kubwa, na mwepesi wa kurejea kwa Mwenyezi Mungu. 76.
(Akaambiwa): Ewe Ibrahim! Achilia mbali haya! Hakika amri ya Mola wako Mlezi imekwisha kuja, na hakika hao itawafikia adhabu isiyorudishwa nyuma. 77. Na wajumbe wetu walipomjia Lut, yakamuwia mabaya kwa sababu yao na akaona dhiki kubwa kwa sababu yao.
Akasema: Hii si ni siku ngumu sana! 78. Wakamjia kaumu yake mbio mbio. Na kabla ya haya walikuwa wakitenda mabaya.
Yeye akasema: Enyi kaumu yangu! Hawa binti zangu, ndio wametakasika zaidi kwenu. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi mbele ya wageni wangu. Hivyo je, hakuna hata mtu mmoja miongoni mwenu aliyeongoka? 79.
Wakasema: Bila shaka umekwisha jua hatuna haki yoyote juu ya binti zako, na hakika wewe unayajua yale tunayoyataka. 80.
Akasema: Laiti ningelikuwa na nguvu kwenu, au nijilinde kwenye nguzo yenye nguvu! 81.
(Wajumbe) wakasema: Ewe Lut! Sisi ni wajumbe wa Mola wako Mlezi. Hawa hawatakufikia. basi wewe ondoka pamoja na ahali zako usiku ungalipo. Wala yeyote miongoni mwenu asitazame nyuma, isipokuwa mkeo, kwani yeye utamfika msiba utakaowafika hao. Hakika miadi yao ni asubuhi. Je, asubuhi si karibu? 82. Basi ilipokuja amri yetu, tuliigeuza nchi juu chini, na tukaiteremshia mvua ya changarawe za udongo mgumu uliokamatana wa Motoni. 83. Zilizotiwa alama kwa Mola wako Mlezi. Na haya hayako mbali na madhalimu wengineo.
#
{69} أي: {ولقد جاءتْ رُسُلُنا}: من الملائكة الكرام رسولَنا {إبراهيمَ} الخليل {بالبشرى}؛ أي: بالبشارة بالولد حين أرسلهم الله لإهلاك قوم لوط وأمَرَهم أنْ يمرُّوا على إبراهيم فيبشِّروه بإسحاق، فلما دخلوا عليه، {قالوا سلاماً قال سلامٌ}؛ أي: سلَّموا عليه وردَّ عليهم السلام. ففي هذا مشروعية السلام، وأنَّه لم يزْل من ملَّة إبراهيم عليه السلام، وأنَّ السلام قبل الكلام، وأنَّه ينبغي أن يكون الردُّ أبلغَ من الابتداء؛ لأنَّ سلامهم بالجملة الفعليَّة الدالَّة على التجدُّد، وردُّه بالجملة الاسمية الدالَّة على الثُّبوت والاستمرار، وبينهما فرقٌ كبيرٌ؛ كما هو معلومٌ في علم العربية. {فما لَبِثَ}: إبراهيمُ لما دخلوا عليه، {أن جاء بعجل حنيذ}؛ أي: بادر لبيته فاستحضر لأضيافه عجلاً مشويًّا على الرَّضْفِ سميناً، فقرَّبه إليهم فقال: ألا تأكلونَ.
{69} Yaani, "Na hakika wajumbe wetu walimjia;" yaani, wajumbe hao walikuwa Malaika watukufu, nao walimjia Mtume wetu "Ibrahim" Al-Khalil "kwa bishara njema." Yaani, kwa habari njema ya kupata mtoto wakati Mwenyezi Mungu alipowatuma kuwaangamiza kaumu ya Lut na akawaamuru kwamba wapitie kwa Ibrahimu na wampe bishara njema ya kuzaliwa kwa Is-haq. Basi walipoingia kwake, "wakasema, "Salama!" Naye akasema, "Salama!" Yaani, walimsalimia naye akawajibu salamu zao. Na katika hili kuna uhalali wa kutoa salamu, na kwamba haikuacha kuwa katika mila ya Ibrahim, amani iwe juu yake, na kwamba salamu huwa kabla ya mazungumzo, na kwamba inafaa jibu liwe bora zaidi kuliko kuanzisha salamu. Kwa sababu katika maamkizi yao walitumia sentensi ianzayo kwa kitenzi, kitu ambacho kinaonyesha upya, naye akajibu kwa sentensi ianzayo kwa nomino jambo linaloonyesha uthabiti na uendelevu, na kuna tofauti kubwa kati ya mawili hayo, kama inavyojulikana katika sayansi za lunga ya Kiarabu. "Kisha hakukaa" Ibrahimu walipoingia kwake "mara hiyo akaja na ndama wa kuchoma." Yaani, alikwenda haraka nyumbani na akawaletea wageni wake ndama wa kuchomewa kwenye mawe ya moto,
mnene; basi akamsongesha karibu nao na akasema: Mbona hamli?
#
{70} {فلمَّا رأى أيديَهم لا تصلُ إليه}؛ أي: إلى تلك الضيافة، {نَكِرَهُم وأوجس منهم خِيفةً}: وظنَّ أنهم أتوه بشرٍّ ومَكْروه، وذلك قبلَ أن يعرِفَ أمرَهم، فقالوا: {لا تخفْ إنَّا أرْسِلْنا إلى قوم لوطٍ}؛ أي: إنَّا رسلُ الله، أرسلنا الله إلى إهلاك قوم لوطٍ.
{70} "Basi alipoiona mikono yao haimfikii." Yaani, alipoona haikifikii chakula hicho "akawatilia shaka, na akawahofu" na akadhani ya kuwa yamekuja kwa ajili ya maovu na machukizo. Na hilo lilikuwa kabla ya kujua hali yao, wakasema, "Usihofu! Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya Lut." Yaani, hakika Sisi ni Mitume wa Mwenyezi Mungu, ametutuma kuwaangamiza kaumu ya Lut.
#
{71} وامرأة إبراهيم {قائمةٌ}: تخدُمُ أضيافَه، {فضَحِكَتْ}: حين سمعتْ بحالهم وما أرسلوا به تعجُّباً، {فبشَّرْناها بإسحاقَ ومن وراءِ إسحاق يعقوبَ}.
{71} Na mke wa Ibrahim "alikuwa amesimama wima" akiwahudumia wageni wake, "akacheka," wakati aliposikia hali yao na waliyokuwa wametumwa kufanya kwa mshangao. "Basi tukambashiria kuhusu
(kuzaliwa kwa) Is-haq, na baada ya Is-haq Yaaqub."
#
{72} فتعجَّبت من ذلك و {قالتْ يا وَيْلتا أألِدُ وأنا عجوزٌ وهذا بعلي شيخاً}: فهذان مانعان من وجود الولد. {إنَّ هذا لشيءٌ عجيبٌ}.
{72} Basi akastaajabishwa kwa sababu ya na hilo,
na akasema: “Ole wangu! Mimi nizae ilhali mimi ni ajuza? Na tena huyu mume wangu ni mzee?" Kwa maana, mawili haya yanazuia kupata mtoto. "Hakika haya ni mambo ya ajabu!"
#
{73} {قالوا أتَعْجَبين من أمرِ الله}: فإنَّ أمره لا عجب فيه؛ لنفوذ مشيئته التامَّة في كل شيءٍ؛ فلا يُستغرب على قدرته شيء، وخصوصاً فيما يدبِّره ويمضيه لأهل هذا البيت المبارك. {رحمةُ الله وبركاتُهُ} عليكم أهل البيت؛ أي: لا تزال رحمته وإحسانه وبركاته، وهي الزيادة من خيره وإحسانه وحلول الخير الإلهي على العبد. {عليكم أهلَ البيت إنَّه حميدٌ مجيدٌ}؛ أي: حميد الصفات؛ لأنَّ صفاته صفات كمال، حميدُ الأفعال؛ لأنَّ أفعاله إحسانٌ وجودٌ وبرٌّ وحكمةٌ وعدلٌ وقِسْطٌ. {مجيدٌ}: والمجد هو عظمة الصفات وسَعَتُها؛ فله صفات الكمال، وله من كلِّ صفةِ كمالٍ أكملُها وأتمُّها وأعمُّها.
{73} "Wakasema: Je, unastaajabia amri ya Mwenyezi Mungu?" Kwani, jambo lake halina cha kustaajabisha kwa sababu ya kutekelezeka kwa mapenzi yake kamili katika kila kitu. Kwa hivyo, hakuna kitu cha kushangaza kuhusu uwezo wake, hasa katika kile anachopanga na kuwapitishia watu wa nyumba hii iliyobarikiwa. "Rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake" ziwe juu yenu enyi watu wa nyumba hii. Yaani, hazitaacha kuwepo rehema zake, na ihsani yake na baraka Zake. Nayo ni ongezeko la heri yake na wema wake, na ihsani na kuwepo kwa heri ya kiungu juu ya mja. "Juu yenu, enyi watu wa nyumba hii! Hakika Yeye ndiye Msifika, Mtukufu." Yaani, yeye ni mwenye Sifa za kusifika kwa sababu sifa zake ni sifa za ukamilifu, na ni mwenye matendo ya kusifika. Kwa sababu, matendo yake ni wema, na ukarimu, na wema, na hekima, na uadilifu, na haki. "Msifika;" yaani, Mwenye Utukufu mkubwa wa sifa ambazo ni pana mno. Basi ana sifa za ukamilifu, na katika kila sifa ya ukamilifu ana kamilifu zaidi zake, na timilifu zaidi zake, na za jumla zaidi zake.
#
{74} {فلما ذَهَبَ عن إبراهيم الرَّوْعُ}: الذي أصابه من خيفة أضيافه، {وجاءتْه البُشرى}: بالولد؛ التفتَ حينئذٍ إلى مجادلة الرسل في إهلاك قوم لوطٍ، وقال لهم: {إنَّ فيها لوطاً. قالوا نحنُ أعلمُ بمَن فيها لَنُنَجِيَنَّه وأهْلَه إلاَّ امرأتَهُ}.
{74} "Basi hofu ilipomwondoka Ibrahim;" yaani, hofu iliyompata kutoka kwa wageni wake hao, "na ikawa ile bishara imemfikia" juu ya kuzaliwa kwa mtoto, hapo akageukia kuwajadili wajumbe hawa kuhusu kuangamizwa kwa kaumu ya Luti,
na akawaambia: "Hakika ndani yake yuko Luti.
Wao wakasema: Sisi tunajua zaidi ni nani yumo humo. Hakuna shaka tutamwokoa sawasawa yeye na ahali zake, isipokuwa mkewe."
#
{75} {إنَّ إبراهيم لحليمٌ}؛ أي: ذو خُلُق [حسنٍ] وسعة صدر وعدم غضب عند جهل الجاهلين، {أوَّاهٌ}؛ أي: متضرِّع إلى الله في جميع الأوقات، {منيبٌ}؛ أي: رجَّاع إلى الله بمعرفته ومحبَّته والإقبال عليه والإعراض عمَّن سِواه؛ فلذلك كان يجادِلُ عن مَنْ حَتَّم الله بهلاكهم.
{75} "Hakika Ibrahim alikuwa mvumilivu sana;" yaani, mwenye tabia
[nzuri], ana moyo mkunjufu, na kutokasirika juu ya ujinga wa wajinga, "mwenye huzuni kubwa." Yaani, mwenye kumwomba mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu katika kila wakati, "mwepesi wa kurejea kwa Mwenyezi Mungu." Yaani, mwenye kurudi sana kwa Mwenyezi Mungu kwa kumjua, na kumpenda, na kumwelekea yeye tu, na kujitenga na asiyekuwa yeye. Na ndiyo maana akawa anajadiliana kuhusu wale ambao Mwenyezi Mungu alikuwa amekwisha pitisha kwamba waangamizwe.
#
{76} فقيل له: {يا إبراهيمُ أعْرِضْ عن هذا}: الجدال. {إنَّه قد جاءَ أمرُ ربِّك}: بهلاكهم، {وإنَّهم آتيهم عذابٌ غيرُ مردودٍ}: فلا فائدة في جدالك.
{76} Basi akaambiwa: "Ewe Ibrahim! Achilia mbali haya " ya kujadili! "Hakika amri ya Mola wako Mlezi imekwisha kuja" juu ya kuwaangamiza hao. "Na hakika hao itawafikia adhabu isiyorudishwa nyuma." Basi hakuna faida yoyote katika kujadili kwako.
#
{77} {ولما جاءت رسُلُنا}؛ أي: الملائكة الذين صدروا من إبراهيم، لما أتوا {لوطاً سيء بهم}؛ أي: شقَّ عليه مجيئهم، {وضاق بهم ذَرْعاً وقال هذا يومٌ عصيبٌ}؛ أي: شديدٌ حرجٌ؛ لأنَّه علم أنَّ [قومَه] لا يتركونَهم؛ لأنَّهم في صور شباب جردٍ مردٍ في غاية الكمال والجمال.
{77} "Na wajumbe wetu walipomjia;" yaani, Malaika wale waliotoka kwa Ibrahim walipomjia "Lut, yakamuwia mabaya kwa sababu yao." Yaani, kuja kwao kulikuwa kugumu kwake, "na akaona dhiki kubwa kwa sababu yao.
" Na akasema: Hii si ni siku ngumu sana!" Yaani, ni ngumu sana Kwa sababu alijua kwamba
[kaumu yake] hawatawaacha. Kwa sababu, walikuwa katika sura za vijana wa kiume, barobaro, wakamilifu mno na wazuri sana.
#
{78} ولهذا وَقَعَ ما خطر بباله، فجاءه {قومُهُ يُهْرَعونَ إليه}؛ أي: يسرعون ويبادرون يريدون أضيافه بالفاحشة التي كانوا يعملونها، ولهذا قال: {ومِن قَبْلُ كانوا يعملون السِّيئاتِ}؛ أي: الفاحشة التي ما سبقهم عليها أحدٌ من العالمين. {قال يا قوم هؤلاءِ بناتي هُنَّ أطهرُ لكم}: من أضيافي ـ وهذا كما عَرَضَ سليمانُ - صلى الله عليه وسلم - على المرأتين أن يَشُقَّ الولد المختصم فيه لاستخراج الحقِّ ـ ولعلمه أنَّ بناته ممتنعٌ منالهنَّ ولا حقَّ لهم فيهنَّ، والمقصود الأعظم دفعُ هذه الفاحشة الكبرى. {فاتَّقوا الله ولا تُخْزونِ في ضيفي}؛ أي: إما أن تُراعوا تقوى الله، وإما أن تراعوني في ضَيْفي ولا تخزونِي عندهم. {أليس منكم رجلٌ رشيدٌ}: فينهاكم ويزجُرُكم. وهذا دليلٌ على مروجهم وانحلالهم من الخير والمروءة.
78. Na ndiyo maana yakatokea yale yaliyomjia moyoni, kwa hivyo wakaja "mbio mbio kwake." Yaani, wakaja mbio wakitaka kufanya uchafu na wageni wake hao. Uchafu ambao walikuwa wakiyafanya,
na ndio maana akasema: "Na kabla ya haya walikuwa wakitenda mabaya;" yaani, uasherati ambao hakuna yeyote katika walimwengu aliyewatangulia kufanya hivyo.
"Yeye akasema: Enyi kaumu yangu! Hawa binti zangu, ndio wametakasika zaidi kwenu" kuliko wageni wangu hawa- na hili ni kama Suleiman - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - alivyowaambia wanawake wawili wale kwamba atamgawanya mtoto yule ambaye walikuwa wanabishana juu yake ili ajue ukweli - na kwa sababu alijua kwamba mabinti zake hawangepatikana kwa urahisi na wala hawakuwa na haki yoyote kwao. Basi makusudio makubwa hapa yalikuwa kuzuia uchafu huu mkubwa. "Basi mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi mbele ya wageni wangu." Yaani, ima muwe na uchamungu, na ima muniheshimu katika wageni wangu na msinifedheheshe mbele yao. "Hivyo je, hakuna hata mtu mmoja miongoni mwenu aliyeongoka?" Basi akawakataza na kuwakemea, na huu ni ushahidi wa upotofu wao kutokuwa kwao na wema na uungwana.
#
{79} فـ {قَالُوا} له: {لقد علمتَ ما لنا في بناتِكَ من حقٍّ وإنَّك لتعلمُ ما نريدُ}؛ أي: لا نريد إلاَّ الرجال، ولا لنا رغبةٌ في النساء.
79.
Lakini "Wakasema" wakimwambia: "Bila shaka umekwisha jua hatuna haki yoyote juu ya binti zako, na hakika wewe unayajua yale tunayoyataka." Yaani, hatutaki isipokuwa wanaume tu, na hatuna hamu yoyote na wanawake.
#
{80} فاشتدَّ قلقُ لوطٍ عليه الصلاة والسلام و {قال لو أنَّ لي بكم قوَّةً أو آوي إلى ركنٍ شديدٍ}؛ كقبيلة مانعةٍ؛ لمنعتكم. وهذا بحسب الأسباب المحسوسة، وإلاَّ؛ فإنَّه يأوي إلى أقوى الأركان، وهو الله الذي لا يقوم لقوته أحدٌ.
{80} Kwa hivyo wasiwasi wa Lut - rehema na amani ziwe juu yake -
ukawa mkubwa sana na "akasema: Laiti ningelikuwa na nguvu kwenu, au nijilinde kwenye nguzo yenye nguvu!" Kama vile kabila lenye nguvu, basi ningewazuia. Na hili ni kulingana na sababu zinazohisika, vinginevyo yeye kwa hakika angeweza kuikimbilia nguzo yenye nguvu zaidi, yaani, Mwenyezi Mungu, ambaye hakuna awezaye kusimama mbele ya nguvu zake.
#
{81} ولهذا لمَّا بَلَغَ الأمرُ منتهاه واشتدَّ الكربُ؛ {قالوا} له: {إنَّا رسلُ ربِّك}؛ أي: أخبروه بحالهم ليطمئنَّ قلبُه، {لن يَصِلوا إليكَ}: بسوءٍ. ثم قال جبريل بجناحِهِ، فطمس أعينَهم، فانطلقوا يتوعَّدون لوطاً بمجيء الصبح، وأمر الملائكةُ لوطاً أن يَسْرِيَ بأهله {بِقِطْع من الليل}؛ أي: بجانب منه قبل الفجر بكثير؛ ليتمكَّنوا من البعدِ عن قريتهم، {ولا يلتفتْ منكُم أحدٌ}؛ أي: بادروا بالخروج، وليكن همُّكم النجاءَ، ولا تلتفِتوا إلى ما وراءكم، {إلاَّ امرأتَكَ إنَّه مصيبُها}: من العذاب {ما أصابهم}؛ لأنَّها تشارِكُ قومها في الإثم، فتدلُّهم على أضياف لوطٍ إذا نزل به أضيافٌ. {إنَّ موعِدَهم الصُّبحُ}: فكأنَّ لوطاً استعجلَ ذلك، فقيل له: {أليس الصبحُ بقريبٍ}.
{81} Na kwa sababu ya hayo,
jambo lake lilipofika mwisho wake na dhiki ikawa kubwa zaidi; "Wakamwambia: Hakika Sisi ni wajumbe wa Mola wako Mlezi." Yaani wakamwambia hali yao ili moyo wake utulie. "Hawa hawatakufikia" kwa madhara. Kisha Jibril akafanya kwa bawa lake, na akayapofua macho yao, kwa hivyo wakaondoka kwenda wakimtishia Luti kwamba warudi alfajiri. Na Malaika hao wakamuamuru Lut'i kwamba asafiri na ahali zake "usiku ungalipo" kabla ya mapambazuko Ili waweze kuwa mbali na kijiji chao. "Wala yeyote miongoni mwenu asitazame nyuma;" yaani, harakisheni kutoka, na iwe hamu yenu ni kuokoka, wala msigeuke kuyaangalia yale yaliyo nyuma yenu, "isipokuwa mkeo, kwani yeye utamfika msiba utakaowafika hao." Kwa sababu, yeye anashiriki katika dhambi hiyo na kaumu yake, kwa hivyo alikuwa akiwaonyesha kaumu yake wageni wa Luti wanapomjia wageni. "Hakika miadi yao ni asubuhi" na ni kana kwamba Luti alitaka hilo lifanyike kwa haraka,
basi akaambiwa: "Je, asubuhi si karibu?"
#
{82} {فلما جاء أمرُنا}: بنزولِ العذاب وإحلاله فيهم {جَعَلْنا}: ديارهم {عالِيَها سافِلَها}؛ أي: قلبناها عليهم، {وأمْطَرْنا عليها حجارةً من سِجِّيلٍ}؛ أي: من حجارة النار الشديدة الحرارة، {منضودٍ}؛ أي: متتابعة تتبع من شذَّ عن القرية.
{82} "Basi ilipokuja amri yetu" ya kuwateremshia adhabu na kuwafikishia, "tuliigeuza" majumba yao "juu yao yake kuwa chini yake na tukaiteremshia mvua ya changarawe." Yaani, mawe ya moto mkali sana, "uliokamatana," na yenye kufuatana, na kuwafuata wale wanaotoroka kutoka kijijini humo.
#
{83} {مسوَّمةً عند ربِّك}؛ أي: معلمة عليها علامة العذاب والغضب، {وما هي من الظالمينَ}: الذين يشابهون لفعل قوم لوطٍ، {ببعيد}: فليحذرِ العبادُ أن يفعلوا كفعلهم؛ لئلاَّ يصيبَهم ما أصابهم.
{83} "Zilizotiwa alama kwa Mola wako Mlezi." Yaani, zilikuwa na alama za adhabu na ghadhabu, "Na haya hayako mbali na madhalimu wengineo" ambao wanafanya matendo kama ya kaumu ya Luti. Basi na wajihadhari waja na kufanya kama walivyofanya hao Ili yasiwasibu yale yaliyowapata wale.
{وَإِلَى مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا قَالَ يَاقَوْمِ اعْبُدُوا اللَّهَ مَا لَكُمْ مِنْ إِلَهٍ غَيْرُهُ وَلَا تَنْقُصُوا الْمِكْيَالَ وَالْمِيزَانَ إِنِّي أَرَاكُمْ بِخَيْرٍ وَإِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ مُحِيطٍ (84) وَيَاقَوْمِ أَوْفُوا الْمِكْيَالَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ (85) بَقِيَّتُ اللَّهِ خَيْرٌ لَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ وَمَا أَنَا عَلَيْكُمْ بِحَفِيظٍ (86) قَالُوا يَاشُعَيْبُ أَصَلَاتُكَ تَأْمُرُكَ أَنْ نَتْرُكَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا أَوْ أَنْ نَفْعَلَ فِي أَمْوَالِنَا مَا نَشَاءُ إِنَّكَ لَأَنْتَ الْحَلِيمُ الرَّشِيدُ (87) قَالَ يَاقَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِنْ كُنْتُ عَلَى بَيِّنَةٍ مِنْ رَبِّي وَرَزَقَنِي مِنْهُ رِزْقًا حَسَنًا وَمَا أُرِيدُ أَنْ أُخَالِفَكُمْ إِلَى مَا أَنْهَاكُمْ عَنْهُ إِنْ أُرِيدُ إِلَّا الْإِصْلَاحَ مَا اسْتَطَعْتُ وَمَا تَوْفِيقِي إِلَّا بِاللَّهِ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ (88) وَيَاقَوْمِ لَا يَجْرِمَنَّكُمْ شِقَاقِي أَنْ يُصِيبَكُمْ مِثْلُ مَا أَصَابَ قَوْمَ نُوحٍ أَوْ قَوْمَ هُودٍ أَوْ قَوْمَ صَالِحٍ وَمَا قَوْمُ لُوطٍ مِنْكُمْ بِبَعِيدٍ (89) وَاسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ إِنَّ رَبِّي رَحِيمٌ وَدُودٌ (90) قَالُوا يَاشُعَيْبُ مَا نَفْقَهُ كَثِيرًا مِمَّا تَقُولُ وَإِنَّا لَنَرَاكَ فِينَا ضَعِيفًا وَلَوْلَا رَهْطُكَ لَرَجَمْنَاكَ وَمَا أَنْتَ عَلَيْنَا بِعَزِيزٍ (91) قَالَ يَاقَوْمِ أَرَهْطِي أَعَزُّ عَلَيْكُمْ مِنَ اللَّهِ وَاتَّخَذْتُمُوهُ وَرَاءَكُمْ ظِهْرِيًّا إِنَّ رَبِّي بِمَا تَعْمَلُونَ مُحِيطٌ (92) وَيَاقَوْمِ اعْمَلُوا عَلَى مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ سَوْفَ تَعْلَمُونَ مَنْ يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَمَنْ هُوَ كَاذِبٌ وَارْتَقِبُوا إِنِّي مَعَكُمْ رَقِيبٌ (93) وَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا شُعَيْبًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِنَّا وَأَخَذَتِ الَّذِينَ ظَلَمُوا الصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دِيَارِهِمْ جَاثِمِينَ (94) كَأَنْ لَمْ يَغْنَوْا فِيهَا أَلَا بُعْدًا لِمَدْيَنَ كَمَا بَعِدَتْ ثَمُودُ (95)}.
84. Na kwa watu wa Madyana tuliwatumia ndugu yao Shua'ib.
Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu yoyote isipokuwa Yeye, wala msipunguze vipimo na mizani. Mimi ninawaona mmo katika hali njema, nami ninawahofia adhabu ya Siku kubwa hiyo itakayowazunguka. 85. Na enyi kaumu yangu! Timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msienee katika ardhi mkifanya uharibifu. 86. Alivyowabakishia Mwenyezi Mungu ndiyo bora kwenu, ikiwa nyinyi ni Waumini. Wala mimi siye mlinzi wenu. 87.
Wakasema: Ewe Shua'ibu! Je, ni sala zako ndizo zinazokuamrisha tuyaache yale waliyokuwa wakiyaabudu baba zetu, au tuache kufanya tupendavyo katika mali zetu? Ama hakika wewe ni mstahamilivu kweli na mwongofu mno! 88.
Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwaonaje ikiwa ninao ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wangu Mlezi, na ikawa Yeye ameniruzuku riziki njema kutoka kwake? Wala mimi sitaki kuwahalifu nikafanya yale ninayowakataza. Sitaki isipokuwa kutengeneza kiasi ninavyoweza. Na sipati kuwezeshwa haya isipokuwa na Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye ninategemea, na kwake Yeye ninarudi. 89. Na enyi kaumu yangu! Kuhalifiana nami kusiwapelekee hata mkasibiwa na mfano wa yale waliyosibiwa kaumu ya Nuhu, au kaumu ya Hud, au kaumu ya Saleh. Na kaumu ya Lut si mbali nanyi. 90. Na ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi, tena tubuni kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kurehemu sana, Mwenye upendo mkubwa. 91.
Wakasema: Ewe Shu'aibu! Mengi katika hayo unayoyasema hatuyafahamu. Na sisi tunakuona dhaifu miongoni mwetu. Na lau kuwa si jamaa zako, tungekupiga mawe, wala wewe si mtukufu kwetu. 92.
Akasema: Enyi kaumu yangu! Kwani jamaa zangu ni watukufu zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu? Na Yeye mmemueka nyuma ya migongo yenu! Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kuyazunguka yote mnayoyatenda. 93. Na enyi kaumu yangu! Fanyeni katika mahali penu, na mimi pia ninafanya. Karibuni mtajua ni nani itakayemfikia adhabu ya kumhizi, na ni nani mwongo. Na ngojeni, mimi pia ninangoja pamoja nanyi. 94. Na amri yetu ilipokuja, tulimwokoa sawasawa Shu'aibu na wale walioamini pamoja naye kwa rehema kutoka kwetu. Na ukelele uliwanyakua wale waliodhulumu, na wakaishia wamekufa kifudifudi katika majumba yao! 95. Kama kwamba hawakuishi kwa ustawi humo. Zingatia ilivyoangamia Madyana, kama ilivyoangamia Thamud!
#
{84} أي: {و} أرسلنا {إلى مدينَ}: القبيلة المعروفة، الذين يسكنون مَدْيَنَ، في أدنى فلسطين، {أخاهم}: في النسب، {شُعيباً}: لأنَّهم يعرفونه ويتمكَّنون من الأخذ عنه، فقال لهم: {يا قومِ اعبُدوا الله ما لكم من إلهٍ غيرُه}؛ أي: أخلصوا له العبادة؛ فإنَّهم كانوا يشرِكون [به]، وكانوا مع شركهم يَبْخَسون المكيال والميزان، ولهذا نهاهم عن ذلك، فقال: {ولا تَنقُصوا المِكْيال والميزانَ}: بل أوفوا الكيل والميزان بالقسط. {إني أراكُم بخيرٍ}؛ أي: بنعمة كثيرةٍ وصحَّة وكثرة أموال وبنين؛ فاشكُروا الله على ما أعطاكم، ولا تكفروا بنعمة الله فيزيلها عنكم. {وإنِّي أخافُ عليكم عذابَ يوم محيطٍ}؛ أي: عذاباً يحيط بكم ولا يُبقي منكم باقيةً.
84. Yaani, "Na" tulituma "kwa watu wa Madyana" nalo ni kabila mashuhuri, ambao walikuwa wakiishi huko Madyana, katika pande za chini kabisa za Palestina, "ndugu yao" kwa nasaba "Shu'aib" kwa sababu walikuwa wanamjua, na wanaweza kujifunza kutoka kwake. Basi akawaambia, "Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu yoyote isipokuwa Yeye." Yaani, muabuduni yeye tu, kwa maana walikuwa wakimshirikisha, na walikuwa pamoja na ushirikina wao huo wakipunja katika vipimo na mizani, na ndio maana akawakataza kufanya hivyo.
Akasema: "wala msipunguze vipimo na mizani;" bali vitimizeni vipimo na mizani kwa uadilifu. "Mimi ninawaona mmo katika hali njema;" yaani, mko katika neema nyingi, na afya nzuri, na mali nyingi, na watoto. Basi mshukuruni Mwenyezi Mungu kwa hayo aliyowapa, wala msiikanushe neema ya Mwenyezi Mungu, akajaiondoa kwenu. "Nami ninawahofia adhabu ya Siku kubwa hiyo itakayowazunguka." Yaani, adhabu itakayowazunguka wala haitaacha yeyote mwenye kubakia.
#
{85} {ويا قوم أوفوا المكيالَ والميزان بالقِسْطِ}؛ أي: بالعدل الذي ترضَوْن أن تعطوه، {ولا تَبخَسوا الناس أشياءهم}؛ أي: لا تنقصوا من أشياء الناس، فتسرقوها بأخذها بنقص المكيال والميزان، {ولا تَعْثَوْا في الأرض مفسِدينَ}: فإنَّ الاستمرار على المعاصي يفسِدُ الأديان والعقائد والدِّين والدُّنيا ويهلِكُ الحرثَ والنسل.
{85} "Na enyi kaumu yangu! Timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu;" yaani, kwa uadilifu ambao nyinyi wenyewe mnaridhia mpewe, "wala msiwapunje watu vitu vyao." Yaani, msipunguze katika vitu vya watu mkawa mmeviiba kwa kuvichukua kwa kupunguza vipimo au mizani, "wala msienee katika ardhi mkifanya uharibifu." Kwa maana, kuendelea kufanya maasia kunaharibu dini na itikadi, na akhera na dunia, na kunaharibu mimea na viumbe.
#
{86} {بقيةُ الله خيرٌ لكم}؛ أي: يكفيكم ما أبقى الله لكم من الخير وما هو لكم؛ فلا تطمَعوا في أمرٍ لكم عنه غُنيةٌ وهو ضارٌّ لكم جدًّا، {إن كنتُم مؤمنينَ}: فاعملوا بمقتضى الإيمان. {وما أنا عليكم بحفيظٍ}؛ أي: لست بحافظٍ لأعمالكم ووكيل عليها، وإنَّما الذي يحفظها الله تعالى، وأمَّا أنا فأبلِّغكم ما أرسلتُ به.
{86} "Alivyowabakishia Mwenyezi Mungu ndiyo bora kwenu;" yaani, yanawatosha yale ambayo Mwenyezi Mungu amewaachia miongoni mwa heri na kile kilicho chenu. Basi msiwe na pupa juu ya kitu ambacho hamkihitaji, tena ni chenye kuwadhuru sana; "ikiwa nyinyi ni Waumini" basi fanyeni kulingana na matakwa ya Imani hiyo. "Wala mimi siye mlinzi wenu.
" Yaani: Mimi si mlinzi au msimamizi wa matendo yenu; bali anayevihifadhi ni Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ama mimi, ninawafikishia tu yale niliyotumwa nayo.
#
{87} {قالوا يا شُعيبُ أصلاتُكَ تأمُرُك أن نَتْرُكَ ما يعبدُ آباؤنا}؛ أي: قالوا ذلك على وجه التهكُّم بنبيِّهم والاستبعاد لإجابتهم له، ومعنى كلامهم: أنَّه لا موجب لنهيك لنا إلاَّ أنك تصلي لله وتتعبَّد له؛ أفإنْ كنتَ كذلك؛ أفيوجِبُ لنا أن نتركَ ما يعبدُ آباؤنا لقولٍ ليس عليه دليلٌ إلاَّ أنه موافقٌ لك؟! فكيف نتَّبعك ونترك آباءنا الأقدمين أولي العقول والألباب؟! وكذلك لا يوجِبُ قولُك لنا أن نفعلَ في أموالنا ما قلتَ لنا من وفاء الكيل والميزان وأداء الحقوق الواجبة فيها، بل لا نزالُ نفعل فيها ما شئنا؛ لأنَّها أموالُنا، فليس لك فيها تصرُّف، ولهذا قالوا في تهكُّمهم: {إنَّك لأنتَ الحليمُ الرشيدُ}؛ أي: أئنك أنت الذي الحلم والوَقارُ لك خُلُقٌ والرُّشْدُ لك سجيَّةٌ؛ فلا يصدُرُ عنك إلا رشدٌ، ولا تأمرُ إلاَّ برشدٍ، ولا تنهى إلاَّ عن غيٍّ؟! أي: ليس الأمر كذلك، وقصدُهم أنَّه موصوفٌ بعكس هذين الوصفين: بالسَّفه والغواية؛ أي: أن المعنى: كيف تكونُ أنت الحليم الرشيد، وآباؤنا هم السفهاء الغاوين؟! وهذا القول الذي أخرجوه بصيغة التهكُّم وأنَّ الأمر بعكسه ليس كما ظنُّوه، بل الأمر كما قالوه: إنَّ صلاته تأمُرُه أن ينهاهم عمَّا كان يعبدُ آباؤهم الضالُّون وأن يفعلوا في أموالهم ما يشاؤون؛ فإنَّ الصلاة تنهى عن الفحشاء والمنكر، وأيُّ فحشاء ومنكرٍ أكبر من عبادة غير الله، ومن منع حقوق عباد الله، أو سرقتها بالمكاييل والموازين، وهو عليه الصلاة والسلام الحليم الرشيد؟!
{87} "Wakasema: Ewe Shua'ibu! Je, ni sala zako ndizo zinazokuamrisha tuyaache yale waliyokuwa wakiyaabudu baba zetu?" Yaani, walisema hayo kwa njia ya kumkejeli Nabii wao na kulifanya kuwa mbali sana jambo la kuitikia kwa Nabii wao. Na maana ya maneno yao hayo ni kwamba, hakuna sababu ya wewe kukataza haya isipokuwa kwamba wewe unaswali na kumuabudu Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, ukiwa hivyo, je, inatulazimu kuyaacha yale waliokuwa baba zetu wakiwaabudu kwa sababu tu ya kauli ambayo hakuna ushahidi wowote juu yake isipokuwa tu kwamba inaafikiana nawe? Basi vipi tukufuate na kuwaacha baba zetu wa kale wenye akili na ufahamu? Na vile vile kauli yako hiyo haitulazimu kufanya katika mali zetu yale uliyotuambia ya kutimiza vipimo na mizani, na kutekeleza haki za wajibu ndani yake. Bali hatutaacha kuendelea kufanya ndani yake chochote tunachotaka. Kwa sababu hizo ni mali zetu, nawe huna uendeshaji wowote ndani yake.
Basi ndiyo maana wakasema katika kejeli zao: "hakika wewe ni mstahamilivu kweli na mwongofu mno!" Yaani, je, wewe ndiye yule ambaye ustahamilivu na heshima ni katika tabia zako, na uongofu ndiyo mwenendo wako? Basi hakitoki kwako isipokuwa uwongofu tu, wala huamrishi isipokuwa uwongofu tu, na wala hukatazi isipokuwa upotovu? Yaani,
mambo siyo hivyo na wanachomaanisha ni kwamba yeye anasifika kwa kinyume cha sifa hizi mbili: upumbavu na upotovu. Na maana yake ni kwamba, vipi utakuwa wewe ndiye mstahamilivu zaidi, mwongofu na baba zetu wawe ndio wapumbavu na wapotofu? Na kauli hii waliyoisema kwa mbinu ya kejeli, na kwamba mambo yake ni kinyume chake, si kama walivyodhania. Bali mambo yake ni kama walivyosema kwamba Swalah yake inamuamrisha awakataze yale waliyokuwa wakiabudu baba zao wapotofu na kwamba wafanye katika mali zao watakavyo. Kwa maana, Swala inakataza uchafu na maovu na ni uchafu upi na uovu ulio mkubwa zaidi kuliko kumwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na kuliko kuzuia haki za waja wa Mwenyezi Mungu, au kuziiba kwa vipimo na mizani, na bila shaka yeye - rehema na amani ziwe juu yake - ndiye mstahamilivu zaidi, mwongofu zaidi?
#
{88} {قال} لهم شعيبٌ: {يا قوم أرأيتُم إن كنتُ على بيِّنةٍ من ربِّي}؛ أي: يقين وطمأنينة في صحَّة ما جئت به، {ورَزَقَني منه رزقاً حسناً}؛ أي: أعطاني الله من أصناف المال ما أعطاني، {و} أنا لا {أريدُ أن أخالِفَكم إلى ما أنهاكم عنه}: فلستُ أريدُ أنْ أنهاكم عن البَخْس في المكيال والميزان وأفعله أنا حتى تتطرق إليَّ التُّهمة في ذلك، بل ما أنهاكم عن أمر إلا وأنا أول مبتدرٍ لتركِهِ. {إن أريدُ إلاَّ الإصلاح ما استطعتُ}؛ أي: ليس لي من المقاصد إلاَّ أن تَصْلُحَ أحوالكم وتستقيم منافعكم، وليس لي من المقاصد الخاصَّة لي وحدي شيءٌ بحسب استطاعتي. ولما كان هذا فيه نوعُ تزكيةٍ للنفس؛ دَفَعَ هذا بقوله: {وما توفيقي إلاَّ بالله}؛ أي: وما يحصل لي من التوفيق لفعل الخير و الانفكاك عن الشرِّ إلاَّ بالله تعالى، لا بحولي ولا بقوَّتي. {عليه توكلتُ}؛ أي: اعتمدتُ في أموري ووثقتُ في كفايته. {وإليه أنيبُ}: في أداء ما أمرني به من أنواع العبادات، وفي هذا التقرُّب إليه بسائر أفعال الخيرات، وبهذين الأمرين تستقيمُ أحوال العبد، وهما الاستعانةُ بربِّه والإنابة إليه؛ كما قال تعالى: {فاعبُدْه وتوكَّلْ عليه}. وقال: {إيَّاك نعبدُ وإيَّاك نستعينُ}.
{88} Shuaibu "akasema" akiwaambia, "Enyi kaumu yangu! Mwaonaje ikiwa ninao ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wangu Mlezi?" Yaani, yakini na utulivu juu ya usahihi wa yale niliyokuja nayo, "na ikawa Yeye ameniruzuku riziki njema kutoka kwake?" Yaani, Mwenyezi Mungu amenipa sampuli za mali alizonipa, "Na" mimi sitaki "kuwahalifu nikafanya yale ninayowakataza." Sitaki kuwakataza kupunja katika vipimo na mizani, kisha mimi mwenyewe ninaifanya hayo mpaka nikawa ninalaumiwa katika hilo. Bali mimi siwakatazi jambo lolote isipokuwa mimi ndiye mtu wa kwanza kuliacha. "Sitaki isipokuwa kutengeneza kiasi ninavyoweza;" yaani, sina malengo zaidi ya kwamba zitengenee hali zenu na yanyooke manufaa yenu, wala sina malengo yoyote ambayo ni mahususi kwangu peke yangu kwa kulingana na uwezo wangu. Na kwa kuwa hili lina aina fulani ya kujitakasa nafsi,
akalizuia hili kwa kauli yake: "Na sipati kuwezeshwa haya isipokuwa na Mwenyezi Mungu " Yaani, sipati kuwezeshwa kufanya heri na kujiepusha na maovu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, si kwa uwezo wangu wala kwa nguvu yangu. "Kwake Yeye ninategemea;" yaani, nimemtegemea katika mambo yangu na nina imani kwamba atanitosheleza. "Na kwake Yeye ninarudi" katika kutekeleza yale aliyoniamrisha miongoni mwa aina mbalimbali za ibada, na katika kujiweka karibu huku naye kwa vitendo vya heri vyote, na kwa mambo haya mawili ndiyo hali za mja zinanyooka, ambayo ni kutafuta msaada kutoka kwa Mola wake Mlezi na kurejea kwake.
Kama alivyosema yeye Mtukufu: "Basi muabudu Yeye na umtegemee Yeye.
" Na akasema: “Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada.”
#
{89} {ويا قوم لا يجرمنَّكم شِقاقي}؛ أي: لا تحملنَّكم مخالفتي ومشاقَّتي، {أن يصيبَكُم}: من العقوبات، {مثلُ ما أصاب قومَ نوحٍ أو قومَ هودٍ أو قومَ صالحٍ وما قومُ لوطٍ منكم ببعيد}: لا في الدار ولا في الزمان.
{89} "Na enyi kaumu yangu! Kuhalifiana nami kusiwapelekee hata mkasibiwa" na adhabu "na mfano wa yale waliyosibiwa kaumu ya Nuhu, au kaumu ya Hud, au kaumu ya Saleh. Na kaumu ya Lut si mbali nanyi. Si katika makazi wala katika zama.
#
{90} {واستغفِروا ربَّكم}: عما اقترفتم من الذُّنوب، {ثمَّ توبوا إليه}: فيما يستقبل من أعماركم بالتوبة النَّصوح والإنابة إليه بطاعته وترك مخالفته. {إنَّ ربِّي رحيمٌ ودودٌ}: لمن تاب وأناب؛ يرحمه فيغفر له ويتقبَّل توبته ويحبُّه.
ومعنى الودود من أسمائه تعالى: أنَّه يحبُّ عباده المؤمنين ويحبُّونه؛ فهو فعولٌ بمعنى فاعل ومعنى مفعول.
{90} "Na ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi" kwa yale mliyotenda miongi mwa madhambi, "tena tubuni kwake" kwa yale yatakayokuja katika maisha yenu kwa toba ya kweli, na kurejea Kwake kwa kumtii na kuacha kumhalifu. "Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kurehemu sana, Mwenye upendo mkubwa." Kwa mwenye kutubu na kurejea kwake atamrehemu, na kumsamehe, na atamkubalia toba yake, na atampenda. Maana ya jina Al-Wadud ambalo ni katika majina yake yeye Mtukufu ni kwamba yeye anawapenda waja Wake Waumini nao wanampenda. Basi ni nomino yenye maana ya mwenye kupenda na mpendwa.
#
{91} {قالوا يا شعيبُ ما نَفْقَهُ كثيراً مما تقولُ}؛ أي: تضجَّروا من نصائحِهِ ومواعظِهِ لهم، فقالوا: ما نفقهُ كثيراً مما تقولُ، وذلك لبُغْضِهم لما يقولُ ونفرتهم عنه. {وإنَّا لنراك فينا ضعيفاً}؛ أي: في نفسك، لست من الكبار والرؤساء، بل من المستضعفين. {ولولا رهطُكَ}؛ أي: جماعتك وقبيلتك، {لَرَجَمْناك وما أنت علينا بعزيز}؛ أي: ليس لك قَدْرٌ في صدورنا ولا احترامٌ في أنفسنا، وإنما احترمنا قبيلتك بتركنا إياك.
{91} "Wakasema: Ewe Shu'aibu! Mengi katika hayo unayoyasema hatuyafahamu." Yaani, walichoshwa na nasaha zake na kuwaaidhi kwake,
kwa hivyo wakasema: Hatufahamu mengi katika hayo unayoyasema. na hilo ni kwa sababu ya kuchukia kwao yale anayoyasema na kujiweka kwao mbali nayo. "Na hakika sisi tunakuona dhaifu miongoni mwetu;" yaani, wewe mwenyewe si katika wakubwa na viongozi, bali ni katika walio dhaifu. "Na lau kuwa si kundi lako;" yaani, kundi lako na kabila lako. "Tungekupiga mawe, wala wewe si mtukufu kwetu." Yaani, huna cheo chochote katika nyoyo zetu wala heshima katika nafsi zetu, bali tuliheshimu tu kabila lako ndio tukakuacha.
#
{92} {قال} لهم مترقِّقاً لهم: {يا قومِ أرَهْطي أعزُّ عليكم من الله}؛ أي: كيف تراعونني لأجل رَهْطي ولا تراعونني لله، فصار رَهْطي أعزَّ عليكم من الله. {واتَّخذتُموه وراءكم ظِهْرِيًّا}؛ أي: نبذتُم أمر الله وراء ظهوركم، ولم تُبالوا به، ولا خِفْتُم منه. {إنَّ ربِّي بما تعملون محيطٌ}: لا يخفى عليه من أعمالكم مثقالُ ذرَّة في الأرض ولا في السماء، فسيُجازيكم على ما عملتم أتمَّ الجزاء.
{92} "Akasema" akiwafanyia huruma, "Enyi kaumu yangu! Kwani jamaa zangu ni watukufu zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu." Yaani, vipi mnaniheshimu kwa sababu ya kundi langu na wala hamniheshimu kwa sababu ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo likawa kundi langu ni tukufu zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu? "Na Yeye mmemueka nyuma ya migongo yenu!" Yaani, mliitupa amri ya Mwenyezi Mungu nyuma ya migongo yenu, wala hamkuijali wala hamkumhofu. "Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kuyazunguka yote mnayoyatenda." Haifichiki kwake katika matendo yenu hata uzito wa chembe katika ardhi wala mbinguni, basi atawalipa kwa yale mliyoyatenda ujira kamili zaidi.
#
{93} {و} لما أعيَوْه وعجز عنهم؛ قال: {يا قوم اعملوا على مكانتِكُم}؛ أي: على حالتكم ودينكم. {إنِّي عامل سوف تعلمونَ من يأتيه عذابٌ يُخزيه}: ويحلُّ عليه عذابٌ مقيمٌ، أنا أم أنتم، وقد علموا ذلك حين وقع عليهم العذابُ، {وارتقِبوا}: ما يحلُّ بي. {إنِّي معكم رقيبٌ} ما يَحِلُّ بكم.
93. "Na" walipomchosha, naye akawa hawawezi,
Akasema: "Na enyi kaumu yangu! Fanyeni katika mahali penu." Yaani, katika hali yenu na dini yenu. "Karibuni mtajua ni nani itakayemfikia adhabu ya kumhizi" na ya kudumu, mimi au nyinyi. Na hakika walilijua hilo wakati adhabu ilipowashukia. "Na ngojeni" yale yatakayonipata "mimi pia ninangoja pamoja nanyi" kuona yale yatakayowafikia.
#
{94} {ولما جاء أمرُنا}: بإهلاك قوم شعيب، {نجَّيْنا شُعيباً والذين آمنوا معه برحمةٍ منَّا وأخذتِ الذين ظلموا الصيحةُ فأصبحوا في ديارِهم جاثمينَ}: لا تَسْمَعُ لهم صوتاً، ولا ترى منهم حركةً.
{94} "Na amri yetu ilipokuja" ya kuwaangamiza kaumu ya Shu'aib, "tulimwokoa Shu'aibu na wale walioamini pamoja naye kwa rehema kutoka kwetu. Na ukelele uliwanyakua wale waliodhulumu, na wakaishia wamekufa kifudifudi katika majumba yao!" Hungaweza kusikia sauti yoyote kutoka kwao, wala hungeweza kuona harakati yoyote kutoka kwao.
#
{95} {كأن لم يَغْنَوْا فيها}؛ أي: كأنهم ما أقاموا في ديارهم ولا تنَّعموا فيها حين أتاهم العذاب. {ألا بعداً لمدين}: إذْ أهلكها اللهُ وأخزاها، {كما بَعِدَتْ ثمودُ}؛ أي: قد اشتركت هاتان القبيلتان في السَّحق والبُعد والهلاك.
وشعيبٌ عليه السلام كان يسمى خطيب الأنبياء؛ لحسن مراجعته لقومه. وفي قصته من الفوائد والعبر شيء كثير:
منها: أن الكفار كما يعاقَبون ويخاطَبون بأصل الإسلام؛ فكذلك بشرائعه وفروعه؛ لأنَّ شعيباً دعا قومه إلى التوحيد وإلى إيفاء المكيال والميزان، وجعل الوعيد مرتباً على مجموع ذلك.
ومنها: أن نقصَ المكاييل والموازين من كبائر الذُّنوب وتخشى العقوبة العاجلة على من تعاطى ذلك، وأنَّ ذلك من سرقة أموال الناس، وإذا كان سرقتهم في المكاييل والموازين موجبةً للوعيد؛ فسرِقَتُهم على وجه القهر والغلبة من باب أولى وأحرى.
ومنها: أنَّ الجزاء من جنس العمل؛ فمن بَخَسَ أموال الناس يريد زيادة ماله؛ عوقِبَ بنقيض ذلك، وكان سبباً لزوال الخير الذي عنده من الرزق؛ لقوله: {إني أراكم بخيرٍ}؛ أي: فلا تتسبَّبوا إلى زواله بفعلكم.
ومنها: أن على العبد أن يَقْنَعَ بما آتاه الله ويَقْنَعَ بالحلال عن الحرام وبالمكاسب المباحة عن المكاسب المحرمة، وأنَّ ذلك خيرٌ له؛ لقوله: {بقيَّةُ الله خيرٌ لكم}؛ ففي ذلك من البركة وزيادة الرزق ما ليس في التكالب على الأسباب المحرَّمة من المَحْق وضدِّ البركة.
ومنها: أن ذلك من لوازم الإيمان وآثاره؛ فإنَّه رتب العمل به على وجود الإيمان، فدلَّ على أنَّه إذا لم يوجد العمل؛ فالإيمان ناقصٌ أو معدومٌ.
ومنها: أنَّ الصلاة لم تزل مشروعة للأنبياء المتقدِّمين، وأنَّها من أفضل الأعمال، حتى إنه متقرِّر عند الكفار فضلها وتقديمها على سائر الأعمال، وأنها تنهى عن الفحشاء والمنكر، وهي ميزانٌ للإيمان وشرائعه؛ فبإقامتها تكمُلُ أحوال العبدِ، وبعدم إقامتها تختلُّ أحواله الدينيَّة.
ومنها: أنَّ المال الذي يرزقُهُ الله الإنسان، وإنْ كان الله قد خوَّله إياه؛ فليس له أن يصنع فيه ما يشاء؛ فإنه أمانةٌ عنده، عليه أن يقيم حقَّ الله فيه بأداء ما فيه من الحقوق والامتناع من المكاسب التي حرَّمها الله ورسوله، لا كما يزعمه الكفار ومن أشبههم؛ أنَّ أموالهم لهم أن يصنعوا فيها ما يشاؤون ويختارون، سواءٌ وافقَ حكمَ الله أو خالفه.
ومنها: أن من تَكْمِلَةِ دعوة الداعي وتمامها: أن يكونَ أول مبادرٍ لما يأمر غيره به وأول منتهٍ عما ينهى غيره عنه؛ كما قال شعيبٌ عليه السلام: {وما أريدُ أنْ أخالِفَكم إلى ما أنهاكم عنه}، ولقوله تعالى: {يا أيُّها الذين آمنوا لم تقولونَ ما لا تفعلونَ [كَبُرَ مقتًا عند اللهِ أن تقولوا ما لا تفعلون]}.
ومنها: أن وظيفة الرسل وسنَّتهم وملَّتهم إرادةُ الإصلاح بحسب القدرة والإمكان، فيأتون بتحصيل المصالح وتكميلها أو بتحصيل ما يُقْدَرُ عليه منها، وبدفع المفاسدِ وتقليلها، ويراعون المصالح العامة على المصالح الخاصة.
وحقيقة المصلحة هي التي تَصْلُح بها أحوال العباد، وتستقيم بها أمورهم الدينيَّة والدنيويَّة.
ومنها: أنَّ مَن قام بما يقدِرُ عليه من الإصلاح؛ لم يكن مَلوماً ولا مَذْموماً في عدم فعله ما لا يقدِرُ عليه؛ فعلى العبدِ أن يُقيم من الإصلاح في نفسه وفي غيره ما يقدِرُ عليه.
ومنها: أنَّ العبد ينبغي له أن لا يتَّكل على نفسه طرفة عين، بل لا يزال مستعيناً بربِّه، متوكِّلاً عليه، سائلاً له التوفيق، وإذا حصل له شيءٌ من التوفيق؛ فلينسبه لِموليهِ ومُسْديه ولا يُعْجَب بنفسه؛ لقوله: {وما توفيقي إلاَّ بالله عليه توكلتُ وإليه أُنيبُ}.
ومنها: الترهيب بأخذات الأمم، وما جرى عليهم، وأنه ينبغي أنْ تُذْكَرَ القَصصُ التي فيها إيقاعُ العقوبات بالمجرمين في سياق الوعظ والزجر؛ كما أنه ينبغي ذِكْرُ ما أكرم الله به أهل التقوى عند الترغيب والحثِّ على التقوى.
ومنها: أن التائب من الذنب كما يُسمح له عن ذنبه ويُعفى عنه؛ فإنَّ الله تعالى يحبُّه ويودُّه، ولا عبرة بقول من يقول: إنَّ التائبَ إذا تاب؛ فحسبُه أن يُغْفَرَ له ويعودَ عليه العفو، وأما عَوْدُ الودِّ والحبِّ؛ فإنه لا يعودُ؛ فإنَّ الله قال: {واستغفِروا ربَّكم ثمَّ توبوا إليه إنَّ ربي رحيمٌ ودودٌ}.
ومنها: أنَّ الله يدفع عن المؤمنين بأسبابٍ كثيرةٍ قد يعلمون بعضها وقد لا يعلمون شيئاً منها، وربما دَفَعَ عنهم بسبب قبيلتهم وأهل وطنهم الكفار؛ كما دفع الله عن شعيبٍ رجمَ قومِهِ بسبب رهطِهِ.
وأنَّ هذه الروابط التي يحصُلُ بها الدفع عن الإسلام والمسلمين لا بأس بالسعي فيها، بل ربَّما تعيَّن ذلك؛ لأنَّ الإصلاح مطلوبٌ على حسب القدرة والإمكان؛ فعلى هذا لو ساعد المسلمون الذين تحت ولاية الكفار، وعملوا على جعل الولاية جمهوريَّةً يتمكَّن فيها الأفرادُ والشعوبُ من حقوقهم الدينيَّة والدنيويَّة؛ لكان أولى من استسلامهم لدولةٍ تقضي على حقوقهم الدينيَّة والدنيويَّة، وتحرص على إبادتها وجعلهم عَمَلَةً وخدماً لهم. نعم؛ إنْ أمكن أن تكون الدولة للمسلمين وهم الحكام؛ فهو المتعيِّن، ولكن لعدم إمكان هذه المرتبة؛ فالمرتبة التي فيها دفعٌ ووقايةٌ للدين والدنيا مقدمة. والله أعلم.
{95} "Kama kwamba hawakuishi kwa ustawi humo." Yaani, ni kana kwamba hawakukaa katika makazo yao wala hawakufurahia humo wakati adhabu ilipowajia. "Zingatia ilivyoangamia Madyana," wakati Mwenyezi Mungu alipoiangamiza na kuihizi, "kama ilivyoangamia Thamud." Yaani, makabila haya mawili yalishiriki katika kufutiliwa mbali na kuangamia. Naye Shu'aib - amani iwe juu yake - alikuwa akiitwa mhubiri wa manabii, kwa sababu ya kuwashawishi kwake kaumu yake kwa uzuri.
Na kuna faida na mafunzo mengi katika kisa chake: Miongoni mwake ni kwamba, makafiri namna watakavyoadhibiwa juu ya kuacha msingi wa Uislamu, basi vile vile wataadhibiwa kwa kuacha sheria zake na matawi yake. Kwa sababu, Shu'aib aliwalingania kaumu yake kwenye tauhidi na kutimiza vipimo na mizani, na akatoa ahadi ya adhabu juu ya kuacha jumla ya hayo. Miongoni mwake ni kwamba, kupunguza vipimo na mizani ni katika madhambi makubwa na anahofiwa adhabu ya haraka mwenye kufanya hivyo, na kwamba hayo ni katika kuiba mali za watu. Na ikiwa wizi wao katika vipimo na mizani unasababisha ahadi ya adhabu, basi kuiba kwao kwa njia ya nguvu na ushindi ni jambo wanalostahiki na kufailia zaidi kuadhibiwa. Miongoni mwake ni kwamba malipo ni ya aina sawa na matendo. Kwa hivyo, mwenye kupunja mali za watu akitaka kuongeza mali yake, basi anaadhibiwa kwa kinyume cha hilo, na linakuwa ndiyo sababu ya kutoweka kwa heri ya riziki aliyokuwa nayo. Kwa kauli yake "hakika mimi ninawaona mmo katika hali njema." Yaani, kwa hivyo msisababishe kutoweka kwake kwa matendo yenu. Miongoni mwake ni kwamba, ni lazima kwa mja aridhike na yale aliyopewa na Mwenyezi Mungu na aridhike na yale ya halali juu ya yale yaliyoharamishwa, na machumo yanayoruhusiwa juu ya yale yaliyoharamishwa, na kwamba hayo ni bora kwake. Kwa sababu ya kauli yake, "Alivyowabakishia Mwenyezi Mungu ndiyo bora kwenu" kwa maana katika hayo kuna baraka nyingi na kuongezeka kwa riziki katika hilo ambazo haziko katika kupigania mambo yaliyoharamishwa kama vile kuondolewa baraka na ni kinyume cha baraka. Miongoni mwake ni kwamba, hilo ni katika yale yanayofungamana na imani na athari zake, kwa maana alifungamanisha kuyafanya juu ya kuwepo imani, kwa hivyo likaashiria kwamba ikiwa mateso hayapo, basi Imani ni pungufu au haipo kabisa. Miongoni mwake ni kwamba, Swala haikuacha kuwa ni ibada inayoruhisiwa kwa Mitume wa zamani, na kwamba ni miongoni mwa matendo bora zaidi, kiasi kwamba ubora wake umethibiti kwa makafiri na kupewa kwake kipaumbele kuliko matendo mengine yote, na kwamba inakataza uchafu na uovu, nayo ndiyo mizani ya imani na sheria zake. Kwa hivyo kwa kuisimamisha, hali za mja zinakamilika, na kwa kutoisimamisha, hali zake za kidini yanakuwa na kasoro. Miongoni mwake ni kwamba, mali ambayo Mwenyezi Mungu humruzuku mtu, hata kama Mwenyezi Mungu amempa, basi hana haki ya kufanya humo chochote anachotaka. Kwani, ni amana kwake, na ni lazima aisimamishe haki ya Mwenyezi Mungu kwa kutekeleza haki zilizoko ndani yake na kujiepusha na mapato ambayo Mwenyezi Mungu na Mtume wake wameharamisha, si kama wanavyodai makafiri na mwenye kufanana nao, kwamba mali zao wanaweza kufanya humo chochote wanachotaka na kuchagua, sawa iafikiane na hukumu ya Mwenyezi Mungu au ihalifiane nayo. Miongoni mwake ni kwamba, katika kinachokamilisha ulinganizi wa mlinganiaji na kukitimiza ni kwamba awe wa kwanza kuyafanya yale anayoamrisha wengine wayafanye na wa kwanza kuacha yale ambayo anawakataza wengine. Kama alivyosema Shu'aib,
amani iwe juu yake: "Wala mimi sitaki niwahalifu nikafanya yale ninayowakataza." Na kwa kauli yake Mtukufu "Enyi mlioamini! Kwa nini mnasema msiyoyatenda?
[Yanachukiza vikubwa mno kwa Mwenyezi Mungu kuwa mnasema msiyoyatenda]." Miongoni mwake ni kwamba kazi ya Mitume, na desturi yao, na mila yao ni kutafuta kurekebisha kulingana na uwezo na uwezekano, ili wafikie kuleta masilahi na kuyakamilisha au kuleta kile kinachoweza kufikiwa katika hayo, na kuzuia maovu na kuyapunguza, na wanayazingatia masilahi ya umma kuliko masilahi kibinafsi. Na uhakika wa masilahi ni yale ambayo kwayo hali za waja zinatengenea, na mambo yao ya kidini na ya kidunia yananyooka kwayo. Miongoni mwake ni kwamba, mwenye kufanya analoweza kufanya la kutengeneza, basi hatalaumiwa wala kushutumiwa katika kutofanya kwake asichoweza kufanya. Kwa hivyo, ni juu ya mja kusimamisha mambo ya kutengeneza katika nafsi yake na kwa wengine kulingana na awezavyo. Miongoni mwake ni kwamba, mja hafai kuitegemea nafsi yake kiasi cha kupepesa jicho, bali asiache kuendelea kuomba msaada kutoka kwa Mola wake Mlezi, na kumtegemea Yeye, na kumwomba mafanikio. Na anapofikiwa na kitu katika mafanikio, basi na akinasibishe na bwana wake na yule aliyekileta, wala asijinasibishie yeye mwenyewe.
Kwa mujibu wa kauli yake: "Na sipati kuwezeshwa haya isipokuwa na Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye ninategemea, na kwake Yeye ninarudi." Miongoni mwake ni vitisho kwa maangamivu ya umma mbalimbali, na yale yaliyowapata, na kwamba inapasa kutaja visa ambavyo ndani yake kuna kuwaadhibu wahalifu katika muktadha wa mawaidha na makaripio. Na vile inapasa kutaja kile ambacho Mwenyezi Mungu aliwakirimia kwacho watu wachamungu wakati wa kutia moyo na kuhimiza juu ya uchamungu. Miongoni mwake ni kwamba, mwenye kutubia dhambi kama vile anavyosamehewa dhambi yake na kuachiliwa, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu anampenda na anamuenzi sana,
na wala hayaangaliwi maneno ya wale wanaosema: hakika mwenye kutubia anapotubu, basi inamtosha tu kusamehewa na kuachiliwa. Na ama kumuenzi na kumpenda, basi hilo halipati. Lakini ukweli si hivyo, kwa maana Mwenyezi Mungu alisema, "Na ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi, tena tubuni kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kurehemu sana, Mwenye upendo mkubwa." Miongoni mwake ni kwamba, Mwenyezi Mungu huwalinda Waumini kwa sababu nyingi, baadhi yake wanaweza zijua na hata pengine wanaweza kosa kujua chochote katika hizo. Na pengine akawalinda kwa sababu ya kabila lao na makafiri wa nchi yao, kama Mwenyezi Mungu alivyomlinda Shu'aib kutokana na kupigwa mawe na kaumu yake kwa sababu ya kundi lake. Na kwamba, hakuna ubaya wowote katika kujitahidi katika mafungamano haya ambayo kwayo mtu anaweza kuulinda Uislamu na Waislamu, bali pengine hilo likawa lazima. Kwa sababu kutengeneza kunahitajika kulingana na uwezo na uwezekano. Kwa hivyo, lau kuwa Waislamu watawasaidia wale walio chini ya uongozi wa makafiri, na wakajitahidi kuufanya uongozi huo kuwa jamhuri ambayo watu binafsi na makabila wataweza kutekeleza haki zao za kidini na za kidunia, basi ingelikuwa bora kwao kuliko kujisalimisha kwa nchi ambayo inaondoa haki zao za kidini na za kidunia, na wanawania kuwaangamiza na kuwafanya watenda kazi na watumishi wao. Ndiyo, ikiwezekana nchi hiyo iwe ya Waislamu na wao ndio watawala, basi hilo ndilo la lazima kufanywa. Lakini kwa sababu cheo kutowezekana kwa daraja hii, basi daraja ambayo ndani yake kuna kuizuia na kuilinda dini na dunia itatangulizwa. Na mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi.
{وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَى بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍ مُبِينٍ (96) إِلَى فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَاتَّبَعُوا أَمْرَ فِرْعَوْنَ وَمَا أَمْرُ فِرْعَوْنَ بِرَشِيدٍ (97) يَقْدُمُ قَوْمَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَأَوْرَدَهُمُ النَّارَ وَبِئْسَ الْوِرْدُ الْمَوْرُودُ (98) وَأُتْبِعُوا فِي هَذِهِ لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ بِئْسَ الرِّفْدُ الْمَرْفُودُ (99) ذَلِكَ مِنْ أَنْبَاءِ الْقُرَى نَقُصُّهُ عَلَيْكَ مِنْهَا قَائِمٌ وَحَصِيدٌ (100) وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَكِنْ ظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ فَمَا أَغْنَتْ عَنْهُمْ آلِهَتُهُمُ الَّتِي يَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ مِنْ شَيْءٍ لَمَّا جَاءَ أَمْرُ رَبِّكَ وَمَا زَادُوهُمْ غَيْرَ تَتْبِيبٍ (101)}.
96. Na hakika tulimtuma Musa pamoja na Ishara zetu na uthibitisho ulio wazi. 97. Kwa Firauni na waheshimiwa wake. Lakini wao wakafuata amri ya Firauni, na amri ya Firauni haikuwa yenye uwongofu. 98. Siku ya Qiyama atawatangulia kaumu yake na atawaingiza Motoni. Na muingio mbaya zaidi ulioje huo unaoingiwa! 99. Nao walifuatishwa laana hapa
(duniani) na Siku ya Qiyama. Ni kipawa kibaya zaidi kilichoje walichopewa! 100. Hizi ni katika habari za miji, tunakusimulia. Mingine ipo bado na mingine ilifyekwa. 101. Na Sisi hatukuwadhulumu, lakini wao wenyewe walizidhulumu nafsi zao. Na miungu yao waliyokuwa wakiiomba badala ya Mwenyezi Mungu haikuwafaa kitu ilipokuja amri ya Mola wako Mlezi. Na hiyo miungu haikuwazidishia isipokuwa maangamio tu.
#
{96} يقول تعالى: {ولقد أرسلنا موسى}: ابن عمران {بآياتنا}: الدالَّة على صدق ما جاء به؛ كالعصا واليد ونحوهما من الآيات التي أجراها الله على يدي موسى عليه السلام، {وسلطانٍ مُبينٍ}؛ أي: حجة ظاهرة بيِّنة ظهرتْ ظهور الشمس.
{96} Yeye Mtukufu Anasema: "Na hakika tulimtuma Musa" Ibn Imran "pamoja na Ishara zetu" zikionyesha ukweli wa yale aliyokuja nayo, kama vile fimbo, na mkono, na ishara nyinginezo miongoni mwa ishara ambazo Mwenyezi Mungu alizifanya juu ya mkono wa Musa - amani iwe juu yake - "na uthibitisho ulio wazi." Yaani, hoja iliyo dhahiri kwa kudhihirika kwa jua
#
{97} {إلى فرعونَ وملئِهِ}؛ أي: أشراف قومه؛ لأنَّهم المتبوعون، وغيرهم تَبَع لهم، فلم ينقادوا لما مع موسى من الآيات التي أراهم إيَّاها كما تقدم بسطُها في سورة الأعراف، ولكنهم {اتَّبعوا أمرَ فرعون وما أمرُ فرعونَ برشيدٍ}: بل هو ضالٌّ غاوٍ لا يأمر إلا بما هو ضررٌ محضٌ.
{97} "Kwa Firauni na waheshimiwa wake;" yaani, watukufu wa kaumu yake. Kwa sababu hao ndio wanaofuatwa, na wengineo ni wafuasi wao. Lakini hawakufuata yale aliyokuwa nayo Musa miongoni mwa ishara ambazo aliwaonyesha, kama ilivyoelezwa hapo awali kwa kina katika Surat Al-A'raf. Bali wao "wakafuata amri ya Firauni, na amri ya Firauni haikuwa yenye uwongofu." Bali yeye ni mpotevu, mkengeufu na haamrishi isipokuwa yale ambayo ni madhara matupu.
#
{98} لا جرم لمَّا اتَّبعه قومُه؛ أرداهم وأهلكهم؛ {يَقْدُمُ قومَه يوم القيامة فأوردَهم النارَ وبئس الوِرْدُ المورودُ}.
{98} Ndiyo Hakuna shaka kwamba kaumu yake walipomfuata, aliwatokomeza na kuwaangamiza. "Siku ya Qiyama atawatangulia kaumu yake na atawaingiza Motoni. Na muingio mbaya zaidi ulioje huo unaoingiwa!"
#
{99} {وأُتْبِعوا في هذه}؛ أي: في الدنيا {لعنةً ويوم القيامةِ}؛ أي: يلعنهم الله وملائكته والناسُ أجمعون في الدنيا والآخرة. {بئس الرِّفْدُ المرفودُ}؛ أي: بئس ما اجتمع لهم، وترادَفَ عليهم من عذاب الله ولعنة الدُّنيا والآخرة.
{99} "Nao walifuatishwa;" yaani, duniani "laana na Siku ya Kiyama." Yaani, anawalaani Mwenyezi Mungu, na Malaika wake na watu wote katika dunia na Akhera. "Ni kipawa kibaya zaidi kilichoje walichopewa!" Yaani, ni mabaya zaidi yale yaliyowakusanyikia na yakafuatana juu yao miongoni mwa adhabu ya Mwenyezi Mungu na laana ya duniani na Akhera.
#
{100} ولما ذكر قصص هؤلاء الأمم مع رسلهم؛ قال الله تعالى لرسوله: {ذلك من أنباءِ القُرى نقصُّه عليك}: لتنذر به ويكونَ آية على رسالتك وموعظةً وذكرى للمؤمنين. {منها قائمٌ}: لم يتلفْ بل بقي من آثار ديارهم ما يدلُّ عليهم. {و} منها {حصيدٌ}: قد تهدَّمت مساكنهم، واضمحلَّت منازلهم فلم يبقَ لها أثرٌ.
{100} Na alipotaja visa vya umma hizi pamoja na Mitume wao,
Mwenyezi Mungu Mtukufu akamwambia Mtume wake: "Hizi ni katika habari za miji, tunakusimulia" ili uonye kwazo na ziwe ni Ishara juu ya ujumbe wako na mawaidha na ukumbusho kwa Waumini. "Mingine ipo bado" haikuharibika, bali zimebakia athari za makazi yao tu zinazoashiria juu yake. "Na" miongoni mwake "ilifyekwa," tayari makazi yao yameharibika, na majumba yao yakapotelea mbali, na hakuna athari yao yoyote iliyobakia.
#
{101} {وما ظَلَمْناهم}: بأخذهم بأنواع العقوبات، {ولكن ظَلَموا أنفسَهم}: بالشرك والكفر والعناد. {فما أغنتْ عنهم آلهتُهم التي يَدْعون من دون الله من شيءٍ لمَّا جاء أمرُ ربِّك}: وهكذا كلُّ من التجأ إلى غير الله؛ لم ينفعْه ذلك عند نزول الشدائد. {وما زادوهم غير تَتْبيبٍ}؛ أي: خسار ودمار بالضدِّ مما خطر ببالهم.
{101} "Na Sisi hatukuwadhulumu" kwa kuwachukua kwa adhabu mbali mbali, "lakini wao wenyewe walizidhulumu nafsi zao" kwa ushirikina, na ukafiri, na ukaidi. "Na miungu yao waliyokuwa wakiiomba badala ya Mwenyezi Mungu haikuwafaa kitu ilipokuja amri ya Mola wako Mlezi." Na vile vile kila anayekimbilia kwa asiyekuwa Mwenyezi Nungu, haliwezi hilo kumsaidia wakati mashaka yatakapomteremkia. "Na hiyo miungu haikuwazidishia isipokuwa maangamio tu." Yaani, hasara na uharibifu, kinyume na yale yalyokuwa katika akili zao.
{وَكَذَلِكَ أَخْذُ رَبِّكَ إِذَا أَخَذَ الْقُرَى وَهِيَ ظَالِمَةٌ إِنَّ أَخْذَهُ أَلِيمٌ شَدِيدٌ (102)}.
102. Na hivyo ndivyo ulivyo mshiko wa Mola wako Mlezi anapoishika miji inapokuwa imedhulumu. Hakika mshiko wake ni mchungu na mkali.
#
{102} أي: يقصِمُهم بالعذاب، ويبيدهم، ولا ينفعهم ما كانوا يَدْعون من دون الله من شيءٍ.
{102} Yaani anawateketeza kwa adhabu na kuwaangamiza, na wala yale waliyokuwa wakiyaomba badala ya Mwenyezi Mungu hayawafai kitu.
{إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَةً لِمَنْ خَافَ عَذَابَ الْآخِرَةِ ذَلِكَ يَوْمٌ مَجْمُوعٌ لَهُ النَّاسُ وَذَلِكَ يَوْمٌ مَشْهُودٌ (103) وَمَا نُؤَخِّرُهُ إِلَّا لِأَجَلٍ مَعْدُودٍ (104) يَوْمَ يَأْتِ لَا تَكَلَّمُ نَفْسٌ إِلَّا بِإِذْنِهِ فَمِنْهُمْ شَقِيٌّ وَسَعِيدٌ (105) فَأَمَّا الَّذِينَ شَقُوا فَفِي النَّارِ لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَشَهِيقٌ (106) خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ إِنَّ رَبَّكَ فَعَّالٌ لِمَا يُرِيدُ (107) وَأَمَّا الَّذِينَ سُعِدُوا فَفِي الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ عَطَاءً غَيْرَ مَجْذُوذٍ (108)}.
103. Hakika katika hayo ipo ishara kwa yule anayehofu adhabu ya Akhera. Hiyo ndiyo Siku itakayokusanyiwa watu, na hiyo ndiyo Siku itakayoshuhudiwa 104. Na wala hatuiahirishi isipokuwa kwa muda unaohisabiwa. 105. Siku hiyo itakapokuja, nafsi yoyote haizungumza isipokuwa kwa idhini yake. Basi miongoni mwao watakuwamo waliomo mashakani na wenye furaha. 106. Ama wale wale walijitia mashakani, hao watakuwa Motoni, humo watavuta pumzi na kuitoa kwa ugumu mkubwa. 107. Watadumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipokuwa atakavyo Mola wako Mlezi. Hakika Mola wako Mlezi hutenda atakavyo. 108. Na ama wale waliofurahishwa, wao watakuwa katika Pepo wakidumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipokuwa atakavyo Mola wako Mlezi. Hicho ni kipawa kisicho na kikomo.
#
{103} {إن في ذلك}: المذكور من أخذه للظالمين بأنواع العقوبات، {لآية لمَنْ خاف عذابَ الآخرة}؛ أي: لعبرةً ودليلاً على أنَّ أهل الظُّلم والإجرام لهم العقوبة الدنيويَّة والعقوبة الأخرويَّة. ثم انتقل من هذا إلى وصفِ الآخرة، فقال: {ذلك يومٌ مجموع له الناس}؛ أي: جُمِعوا لأجل ذلك اليوم للمجازاة وليظهر لهم من عظمة الله وسلطانه وعدله العظيم ما به يعرِفونه حقَّ المعرفة. {وذلك يومٌ مشهودٌ}؛ أي: يشهده الله وملائكتُه وجميعُ المخلوقين.
{103} "Hakika katika hayo" yaliyotajwa miongoni mwa kuwaadhibu kwake madhalimu kwa aina mbali mbali za adhabu, "ipo ishara kwa yule anayehofu adhabu ya Akhera." Yaani, kuna mazingatio na ushahidi kwamba madhalimu na wahalifu wana adhabu ya kidunia na adhabu ya kiakhera. Kisha akatoka katika haya hadi katika kuielekeza Akhera,
akasema: "Hiyo ndiyo Siku itakayokusanyiwa watu;" yaani, watakusanywa kwa ajili ya siku hiyo kwa ajili ya malipo na ili uwadhihirikie ukuu wa Mwenyezi Mungu, na mamlaka yake, na uadilifu wake mkuu jambo ambalo kwalo watajua kujua kwa haki "na hiyo ndiyo Siku itakayoshuhudiwa." Yaani, ataishuhudia Mwenyezi Mungu na Malaika wake na viumbe vyote.
#
{104} {وما نؤخِّرُه}؛ أي: إتيان يوم القيامة، {إلاَّ لأجل مَعْدودٍ}: إذا انقضى أجل الدُّنيا، وما قدر الله فيها من الخلق؛ فحينئذٍ ينقلهم إلى الدار الأخرى، ويُجري عليهم أحكامه الجزائيَّة، كما أجرى عليهم في الدُّنيا أحكامه الشرعيَّة.
{104} "Wala hatuiahirishi;" Yaani, kufika kwa Siku ya Qiyama, "isipokuwa kwa muda unaohesabiwa." Utakapokwisha muda wa dunia hii, na yale aliyopitisha Mwenyezi Mungu kuumba ndani yake, basi hapo atawahamisha hadi kwenye ile nyumba nyingine, na atawapitishia hukumu zake za malipo, kama vile alivyowapitishia hukumu zake za kisheria katika dunia hii.
#
{105} {يومَ يأتِ}: ذلك اليومُ ويجتمعُ الخلق، {لا تَكَلَّمُ نفسٌ إلا بإذنِهِ}: حتى الأنبياء والملائكة الكرام لا يشفعون إلا بإذنِهِ. {فمنهم}؛ أي: الخلق {شقيٌّ وسعيدٌ}: فالأشقياء هم الذين كفروا بالله، وكذَّبوا رسله وعَصَوا أمره، والسعداء هم المؤمنون المتَّقون.
{105} "Siku hiyo itakapokuja" siku ambayo viumbe vitakusanywa, "nafsi yoyote haizungumza isipokuwa kwa idhini yake," hata Manabii na Malaika watukufu hawatafanya uombezi isipokuwa kwa idhini yake. "Basi miongoni mwao;" yaani, miongoni mwa viumbe "watakuwamo waliomo mashakani na wenye furaha." Kwa hivyo, wale waliomo mashakani ndio wale waliomkufuru Mwenyezi Mungu, na wakawakadhibisha Mitume wake, na wakaasi amri yake, nao wenye furaha ni Waumini wachamungu.
#
{106} وأما جزاؤهم: {فأما الذين شَقُوا}؛ أي: حصلت لهم الشقاوة والخزي والفضيحة {ففي النار}: منغمسون في عذابها مشتدٌّ عليهم عقابها. {لهم فيها}: من شدَّة ما هم فيه {زفيرٌ وشهيقٌ}: وهو أشنع الأصوات وأقبحُها.
{106} Ama malipo yao, "Ama wale wale walijitia mashakani;" yaani, waliopatwa na mashaka, hizaya, na fedheha "hao watakuwa Motoni" wanatumbukizwa katika adhabu yake, na mateso yake yatakuwa makali mno kwao. "Humo watavuta pumzi na kuitoa kwa ugumu mkubwa" kwa sababu ya uzito wa yale wanayoyapata. Nazo ndizo sauti mbovu na mbaya zaidi.
#
{107} {خالدين فيها}؛ أي: في النار التي هذا عذابُها، {ما دامتِ السمواتُ والأرضُ إلاَّ ما شاء ربُّك}؛ أي: خالدين فيها أبداً إلاَّ المدَّة التي شاء الله أن لا يكونوا فيها، وذلك قبل دخولها؛ كما قاله جمهور المفسرين؛ فالاستثناء على هذا راجعٌ إلى ما قبل دخولها؛ فهم خالدون فيها جميع الأزمان سوى الزمن الذي قبل الدخول فيها. {إنَّ ربَّك فعَّالٌ لما يريد}: فكل ما أراد فعله واقتضته حكمتُه؛ فَعَلَه تبارك وتعالى، لا يردُّه أحدٌ عن مُراده.
{107} "Watadumu humo; yaani, katika Moto ambao hii ndiyo adhabu yake, "muda wa kudumu mbingu na ardhi isipokuwa atakavyo Mola wako Mlezi." Yaani, watadumu humo milele isipokuwa muda atakaotaka Mwenyezi Mungu wasiwe humo. Na hilo ni kabla ya kuingia humo, kama walivyosema wengi wa wafasiri. Na muda wa kutodumu humo ni ule wa kabla ya kuingia humo. Kwa hivyo, watadumu humo nyakati zote isipokuwa muda ule wa kabla ya kuingia humo. "Hakika Mola wako Mlezi hutenda atakavyo" kwani kila anachotaka kukifanya na hekima yake ikwa inahitaji hivyo, hukifanya yeye Mwingi wa baraka, Mtukufu, na hakuna yeyote anayeweza kumzuia anachotaka.
#
{108} {وأما الذين سُعِدوا}؛ أي: حصلت لهم السعادة والفلاح والفوز، {ففي الجنَّة خالدين فيها ما دامت السمواتُ والأرض إلاَّ ما شاء ربُّك}: ثمَّ أكَّد ذلك بقوله: {عطاءً غير مجذوذٍ}؛ أي: ما أعطاهم الله من النعيم المقيم واللَّذة العالية؛ فإنَّه دائمٌ مستمرٌّ غير منقطع بوقت من الأوقات. نسأل الله الكريم من فضله.
{108} "Na ama wale waliofurahishwa;" yaani, waliopata furaha, mafanikio, na kufuzu, "wao watakuwa katika Pepo wakidumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipokuwa atakavyo Mola wako Mlezi." Kisha akasisitiza hilo kwa kauli yake, "Hicho ni kipawa kisicho na kikomo." Yaani, yale aliyowapa Mwenyezi Mungu miongoni mwa raha ya milele na utamu wa hali ya juu zaidi ni ya kudumu na kuendelea, hayatakatika katika wakati wowote ule. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atujalie katika fadhila zake.
{فَلَا تَكُ فِي مِرْيَةٍ مِمَّا يَعْبُدُ هَؤُلَاءِ مَا يَعْبُدُونَ إِلَّا كَمَا يَعْبُدُ آبَاؤُهُمْ مِنْ قَبْلُ وَإِنَّا لَمُوَفُّوهُمْ نَصِيبَهُمْ غَيْرَ مَنْقُوصٍ (109)}.
109. Basi usiwe katika shaka juu ya yale wanayoyaabudu hawa. Hawaabudu isipokuwa kama walivyoabudu baba zao zamani. Na hakika Sisi tutawatimilizia fungu lao bila ya kupunguzwa.
#
{109} يقول الله تعالى لرسوله محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -: {فلا تكُ في مِرْيَةٍ ممَّا يعبدُ هؤلاء}: المشركون؛ أي: لا تشكَّ في حالهم، وأنَّ ما هم عليه باطلٌ؛ فليس لهم دليلٌ شرعيٌّ ولا عقليٌّ، وإنما دليلُهم وشبهتهم أنهم يعبُدون كما يعبُدُ آباؤهم من قبلُ، ومن المعلوم أن هذا ليس بشبهةٍ فضلاً عن أن يكون دليلاً؛ لأنَّ أقوال ما عدا الأنبياء يحتجُّ لها لا يحتج بها، خصوصاً أمثال هؤلاء الضالين، الذين كثر خطؤهم وفساد أقوالهم في أصول الدين؛ فإنَّ أقوالهم وإن اتَّفقوا عليها؛ فإنَّها خطأ وضلال {وإنَّا لَمُوفُّوهم نصيبَهم غير منقوص}؛ أي: لا بدَّ أن ينالهم نصيبُهم من الدُّنيا مما كتب لهم، وإن كَثُر ذلك النصيب أو راق في عينك؛ فإنَّه لا يدلُّ على صلاح حالهم؛ فإنَّ الله يعطي الدُّنيا من يحبُّ ومن لا يحبُّ، ولا يعطي الإيمان والدين الصحيح إلاَّ من يُحِبُّ. والحاصلُ أنَّه لا يُغترُّ باتفاق الضالين على قول الضالين من آبائهم الأقدمين، ولا على ما خوَّلهم الله، وآتاهم من الدنيا.
{109} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Mtume wake Muhammad -
rehema na amani za mwenyezi mungu zimshukie: - "Basi usiwe katika shaka juu ya yale wanayoyaabudu hao" washirikina. Yaani, usiwe na shaka na hali yao, na kwamba hilo walifanyalo ni batili. Kwani, hawana ushahidi wowote wa kisheria wala wa kiakili, lakini ushahidi wao na mchanganyiko wao ni kuwa wanaabudu kama walivyoabudu baba zao kabla. Na inavyojulikana ni kuwa, hili si mchanganyiko, achilia mbali kutosha kuwa ushahidi. Kwa sababu, maneno ya wasiokuwa Mitume yanatafutiwa ushahidi wala hayatumiki kama ushahidi, hasa mfano wa hawa watu wapotofu, ambao makosa yao na uharibifu wao ni mwingi katika misingi ya dini. Kwa maana, maneno yao, hata kama watakubaliana juu yake, hayo kwa hakika ni makosa na upotofu "Na hakika Sisi tutawatimilizia fungu lao bila ya kupunguzwa." Yaani, ni lazima litawapata fungu lao waliloandikiwa katika dunia hii, hata kama fungu hilo ni nyingi au ni la kupendeza machoni pako, basi hilo halionyeshi utengenevu wa hali yao. Kwa maana Mwenyezi Mungu humpa dunia yule ambaye Yeye anampenda na asiyempenda, lakini hampi imani na Dini sahihi isipokuwa yule ambaye Yeye anampenda. La msingi ni kwamba asidanganywe na makubaliano ya wapotofu juu ya maneno ya wale waliopotoka miongoni mwa baba zao wa zamani, wala juu ya yale aliyowapa Mwenyezi Mungu na akawapa katika dunia hii.
{وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَاخْتُلِفَ فِيهِ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِنْ رَبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ وَإِنَّهُمْ لَفِي شَكٍّ مِنْهُ مُرِيبٍ (110) وَإِنَّ كُلًّا لَمَّا لَيُوَفِّيَنَّهُمْ رَبُّكَ أَعْمَالَهُمْ إِنَّهُ بِمَا يَعْمَلُونَ خَبِيرٌ (111) فَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ وَمَنْ تَابَ مَعَكَ وَلَا تَطْغَوْا إِنَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ (112) وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنْصَرُونَ (113)}.
110. Na hakika tulimpa Musa Kitabu, lakini kukazuka kuhitilafiana ndani yake. Na lau kuwa si neno lililokwisha tangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi, bila ya shaka ingelihukumiwa baina yao. Na hakika wao wamo katika shaka juu yake inayowahangaisha. 111. Na hakika Mola wako Mlezi atawatimilizia malipo ya matendo yao wote. Hakika Yeye anayo habari ya wayatendayo. 112. Basi, nyooka kama ulivyoamrishwa, wewe na wale wanaotubia kwa Mwenyezi Mungu pamoja nawe, wala msivuke mipaka. Hakika Yeye anayaona yote myatendayo. 113. Wala msiwategemee wale waliodhulumu, mkaja kuguswa na Moto. Wala nyinyi hamna walinzi wowote kando na Mwenyezi Mungu, wala tena hamtanusuriwa.
#
{110} يخبر تعالى أنه آتى موسى الكتاب الذي هو التوراة، الموجب للاتفاق على أوامره ونواهيه والاجتماع، ولكن مع هذا؛ فإنَّ المنتسبين إليه اختلفوا فيه اختلافاً أضرَّ بعقائدهم وبجامعتهم الدينيَّة. {ولولا كلمةٌ سبقتْ من ربِّك}: بتأخيرهم وعدم معاجلتهم بالعذاب، {لَقُضِيَ بينَهم}: بإحلال العقوبة بالظَّالم، ولكنَّه تعالى اقتضت حكمته أن أخَّر القضاء بينَهم إلى يوم القيامة، وبَقوا في شكٍّ مريبٍ. وإذا كانت هذه حالُهم مع كتابهم؛ فمع القرآن الذي أوحاه الله إليك غير مستغربٍ من طائفة اليهود أن لا يؤمنوا به، وأن يكونوا في شكٍّ منه مريب.
{110} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba alimpa Musa Kitabu, ambacho ni Taurati, jambo linalolazimu kukubaliana juu ya amri zake na makatazo yake na kukusanyika pamoja, lakini pamoja na haya, wale wanaojinasibisha nacho walitofautiana ndani yake kutofautiana kulikozidhuru itikadi zao na umoja wao wa kidini. "Na lau kuwa si neno lililokwisha tangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi" kwa kuwachelewesha na kutowaharakishia adhabu, "bila ya shaka ingelihukumiwa baina yao" kwa kumfikishia dhalimu adhabu, lakini hekima yake Yeye Mtukufu ilihitaji kuchelewesha kupitisha hukumu baina yao mpaka Siku ya Qiyama, kwa hivyo wakabakia katika shaka inayotia wasiwasi. Na ikiwa hii ndiyo hali yao kuhusiana na kitabu chao, basi hali yao kuhusiana na Qur’an ambayo Mwenyezi Mungu aliiteremsha haishangazi kwamba kundi la Mayahudi lisimuamini, na kwamba wana shaka itiayo wasiwasi juu yake.
#
{111} {وإن كُلاًّ لَمَّا لَيُوَفِّيَنَّهُم ربُّك أعمالَهم}؛ أي: لا بدَّ أن يقضي الله بينهم يوم القيامة بحكمه العدل، فيجازي كلاًّ بما يستحقُّه. {إنه بما يعملون}: من خير وشرٍّ، {خبيرٌ}: فلا يَخْفى عليه شيء من أعمالهم؛ دقيقِها وجليلِها.
{111} "Na hakika Mola wako Mlezi atawatimilizia malipo ya matendo yao wote." Yaani, lazima Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao Siku ya Qiyama kwa hukumu yake ya uadilifu, na amlipe kila mmoja anachostahiki. {Hakika Yeye anayo habari ya wayatendayo" miongoni mwa ya heri na ya shari. Kwa hivyo, hakuna kitu kinachofichika kwake katika matendo yao, ya siri zaidi na ya dhahiri mno.
#
{112} ثم لما أخبر بعدم استقامتهم التي أوجبتِ اختلافَهم وافتراقَهم؛ أمر نبيَّه محمداً - صلى الله عليه وسلم - ومَنْ معه من المؤمنين أن يستقيموا كما أمِروا، فيسلكوا ما شرعه الله من الشرائع، ويعتقِدوا ما أخبر الله به من العقائد الصحيحة، ولا يَزيغوا عن ذلك يمنةً ولا يسرةً، ويدوموا على ذلك، ولا يَطْغَوْا بأنْ يتجاوزوا ما حدَّه الله لهم من الاستقامة، وقوله: {إنَّه بما تعملون بصيرٌ}؛ أي: لا يخفى عليه من أعمالكم شيء، وسيجازيكم عليها. ففيه ترغيبٌ لسلوك الاستقامة وترهيبٌ من ضدِّها.
{112} Kisha alipojulisha kuhusu kutonyooka kwao ambako kuliwasababishia kutofautiana na kutengana, akamuamrisha Nabii wake Muhammad - rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - na wale walio pamoja naye miongoni mwa Waumini kwamba wanyooke kama walivyoamrishwa, kwa kufuata sheria alizoziweka Mwenyezi Mungu, na waitakidi yale aliyojulisha Mwenyezi Mungu miongoni mwa itikaki mbalimbali sahihi, wala wasikengeuke wakaacha hayo kwenda kulia wala kushoto, na kwamba wadumu hivyo, wala wasivuke mipaka ya unyoofu aliyowawekea Mwenyezi Mungu.
Na kauli yake: "Hakika Yeye anayaona yote myatendayo." Yaani, hakifichiki kwake chochote katika matendo yenu, na atawalipa kwa hayo; basi ndani yake kuna himizo juu ya kufuata unyoofu na kuhofisha dhidi ya kufuata kinyume chake.
#
{113} ولهذا حذَّرهم عن الميل إلى من تعدَّى الاستقامة، فقال: {ولا تَرْكَنوا}؛ [أي: لا تميلوا] {إلى الذين ظلموا}: فإنَّكم إذا ملتم إليهم وافقتموهم على ظلمهم أو رضيتم ما هم عليه من الظُّلم؛ {فَتَمَسَّكُم النارُ}: إن فعلتُم ذلك. {وما لكم من دون الله من أولياء}: يمنعونكم من عذاب الله، ولا يحصِّلون لكم شيئاً من ثواب الله. {ثم لا تُنصرون}؛ أي: لا يدفع عنكم العذابُ إذا مسَّكم.
ففي هذه الآية التحذير من الركون إلى كلِّ ظالم، والمرادُ بالرُّكون: الميل والانضمام إليه بظلمه وموافقته على ذلك والرضا بما هو عليه من الظلم، وإذا كان هذا الوعيد في الركون إلى الظلمة؛ فكيف حال الظلمة بأنفسهم؟! نسأل الله العافية من الظلم.
{113} Na ndiyo maana akawatahadharisha dhidi ya kuelekea upande wa wale waliopindukia unyoofu,
kwa hivyo akasema: "Wala msiwategemee"
[Yaani msielekee upande wa] "wale waliodhulumu." Kwani, mkielekea upande wao na mkakubaliana nao katika dhuluma yao au mkaridhia dhuluma wafanyayo hiyo, basi "mkaja kuguswa na Moto" mkifanya hivyo. "Wala nyinyi hamna walinzi wowote kando na Mwenyezi Mungu" watakaowakinga kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu, wala hawatawapatia chochote katika malipo ya Mwenyezi Mungu. "Wala tena hamtanusuriwa;" yaani, hakuna atakayewazuilia adhabu itakapowagusa. Basi katika Aya hii, kuna tahadharisho dhidi ya kumtegemea kila dhalimu. Na maana ya kuegemea ni kuelekea upande wake na kuungana naye katika dhuluma yake na kukubaliana naye katika hilo na kuridhia dhuluma hiyo anayofanya. Na ikiwa ahadi hii ya adhabu ni kuhusiana na kuwaelekea madhalimu, basi vipi hali ya madhalimu wenyewe? Tunamuomba Mwenyezi Mungu salama kutokana na dhuluma.
{وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِنَ اللَّيْلِ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ذَلِكَ ذِكْرَى لِلذَّاكِرِينَ (114) وَاصْبِرْ فَإِنَّ اللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ (115)}.
114. Na simamisha Swala katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zilizo karibu na mchana. Hakika mazuri huondoa mabaya. Huu ni ukumbusho kwa wanaokumbuka. 115. Na subiri, kwani hakika Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wafanyao mazuri.
#
{114} يأمر تعالى بإقامة الصلاة كاملة {طَرَفي النهار}؛ أي: أوله وآخره، ويدخل في هذا صلاة الفجر وصلاتا الظهر والعصر، {وزُلَفاً من الليل}: ويدخل في ذلك صلاة المغرب والعشاء، ويتناول ذلك قيام الليل؛ فإنَّها مما تُزْلِفُ العبد وتقرِّبه إلى الله تعالى. {إنَّ الحسنات يُذْهِبْنَ السيِّئاتِ}؛ أي: فهذه الصلوات الخمس وما ألحق بها من التطوُّعات من أكبر الحسنات، وهي مع أنها حسنات تقرِّب إلى الله وتوجِبُ الثواب؛ فإنَّها تُذْهِبُ السيِّئات وتمحوها، والمرادُ بذلك الصغائر؛ كما قيَّدتها الأحاديث الصحيحة عن النبيِّ - صلى الله عليه وسلم -؛ مثل قوله: «الصلوات الخمس، والجمعة إلى الجمعة، ورمضان إلى رمضان؛ مكفراتٌ لما بينهنَّ ما اجتُنِبَتِ الكبائر» ، بل كما قيَّدتها الآية التي في سورة النساء، وهي قوله عزَّ وجلَّ: {إن تَجْتَنِبوا كبائِرَ ما تُنْهَوْنَ عنه نكفِّر عنكم سيئاتِكم وندخِلْكم مُدْخلاً كريماً}. {ذلك}: لعل الإشارة لكلِّ ما تقدَّم؛ من لزوم الاستقامة على الصراط المستقيم، وعدم مجاوزته وتعدِّيه، وعدم الرُّكون إلى الذين ظلموا، والأمر بإقامة الصلاة، وبيان أنَّ الحسنات يُذْهِبْنَ السيئات؛ الجميع {ذكرى للذاكرينَ}: يفهمون بها ما أمرهم الله به ونهاهم، ويمتثلون لتلك الأوامر الحسنة المثمِرَة للخيرات الدَّافعة للشُّرور والسيئات.
{114} Yeye Mtukufu anaamuru kwamba sala isimamishwe kikamilifu "katika ncha mbili za mchana." Yaani, mwanzo wake na mwisho wake, na inaingia katika hili swala ya alfajiri, adhuhuri na alasiri, "na nyakati za usiku zilizo karibu na mchana" na inaingia katika hilo swala ya maghrib na ishaa, na pia inajumuisha swala ya usiku
(Tahajjud), kwani ni katika yale yanayomsongeza na kumleta mja karibu zaidi na Mwenyezi Mungu. "Hakika mzuri huondoa mabaya;" yaani, Sala hizi tano na sala za hiari zinazoambatana nazo ni miongoni mwa matendo mazuri zaidi, na ingawa ni matendo mazuri, yanamuweka mtu karibu na Mwenyezi Mungu na yanasababisha malipo mazuri. Kwa maana, yanaondoa matendo mabaya na kuyafuta, na yanayokusudiwa na hilo ni madhambi madogo, kama hadithi sahihi zilivyozuilia hivyo kutoka kwa Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie. - Kama vile kauli yake,
“Swala tano za kila siku, na Ijumaa hadi Ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani ni kafara ya yale yaliyo baina yake maadamu madhambi makubwa yataepukika.” Bali, vile vile kama ilivyofungia hivyo ile aya ya Surat An-Nisa,
ambayo ni kauli yake Yeye Mwenye Nguvu Mtukufu: “Mkiyaepuka makubwa mnayokatazwa, tutawafutia mabaya yenu madogo, na tutawaingiza mahali patukufu." "Huu," na huenda ishara hii inarejelea yote yaliyotangulia hapo awali, ya kudumu katika unyoofu kwenye njia iliyonyooka, na kutoivuka, na kutowategemea wale waliodhulumu, na amri ya kusimamisha Swala, na kubainisha kwamba matendo mazuri yanaondoa mabaya, yote hayo ni "ukumbusho kwa wanaokumbuka." Kwa huo, wanayafahamu yale aliyowaamrisha Mwenyezi Mungu na kuwakataza, na wanatekeleza maamrisho hayo mazuri yenye kuzaa heri yenye kuepusha maovu na mabaya.
#
{115} ولكن تلك الأمور تحتاج إلى مجاهدة النفس والصبر عليها، ولهذا قال: {واصبِرْ}؛ أي: احبس نفسك على طاعة اللَّه وعن معصيته وإلزامها لذلك واستمرَّ ولا تضجر. {فإنَّ اللَّه لا يُضيعُ أجْرَ المحسنينَ}: بل يتقبَّل اللَّه عنهم أحسن الذي عملوا ويَجْزيهم أجْرَهم بأحسن ما كانوا يعملون.
وفي هذا ترغيبٌ عظيمٌ للزوم الصبر بتشويق النفس الضعيفة إلى ثواب الله كلَّما وَنَتْ وَفَتَرَتْ.
115. Lakini mambo haya yanahitaji juhudi na subira juu yake,
na ndiyo maana akasema: "Na subiri." Yaani, izuie nafsi yako katika kumtii Mwenyezi Mungu na kujiepusha na kumuasi na kuilazimisha kufanya hivyo, na endelea na usinung'unike. "Kwani, hakika Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wafanyao mazuri." Bali Mwenyezi Mungu anapokea kutoka kwao bora zaidi ya waliyokuwa wakiyatenda, na anawalipa malipo yao kwa uzuri zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda. Na katika hili kuna himizo kubwa juu ya kushikamana na subira kwa kuipa shauku nafsi dhaifu juu ya malipo ya Mwenyezi Mungu kila inapodhoofika na kuchoka.
{فَلَوْلَا كَانَ مِنَ الْقُرُونِ مِنْ قَبْلِكُمْ أُولُو بَقِيَّةٍ يَنْهَوْنَ عَنِ الْفَسَادِ فِي الْأَرْضِ إِلَّا قَلِيلًا مِمَّنْ أَنْجَيْنَا مِنْهُمْ وَاتَّبَعَ الَّذِينَ ظَلَمُوا مَا أُتْرِفُوا فِيهِ وَكَانُوا مُجْرِمِينَ (116)}.
116. Basi mbona hawakuwamo katika vizazi vya kabla yenu wenye vyeo na wasaa wanaokataza uharibifu katika nchi, isipokuwa wachache tu, miongoni mwa wale tuliowaokoa miongoni mwao? Na wale waliodhulumu walifuata yale waliyostareheshwa kwayo, na walikuwa wahalifu.
#
{116} لمَّا ذكر تعالى إهلاك الأمم المكذِّبة للرسل، وأنَّ أكثرهم منحرفون عن أهل الكتب الإلهية، وذلك كلُّه يقضي على الأديان بالذَّهاب والاضمحلال؛ ذكر أنَّه لولا أنه جعل في القرون الماضية بقايا من أهل الخير، يدعون إلى الهدى وينهون عن الفساد والرَّدى، فحصل من نفعهم، وأبقيت به الأديان، ولكنَّهم قليلون جدًّا ، وغاية الأمر أنَّهم نجوا باتِّباعهم المرسلين، وقيامهم بما قاموا به من دينهم، وبكون حجَّة الله أجراها على أيديهم؛ ليهلك من هَلَكَ عن بيِّنة ويحيا من حَيَّ عن بيَّنة {و} لكن {اتَّبع الذين ظلموا ما أُتْرِفوا فيه}؛ أي: اتَّبعوا ما هم فيه من النعيم والترف، ولم يبغوا به بدلاً. {وكانوا مجرمين}؛ أي: ظالمين باتِّباعهم ما أترِفوا فيه، فلذلك حقَّ عليهم العقابُ واستأصلهم العذابُ.
وفي هذا حثٌّ لهذه الأمة أن يكون فيهم بقايا؛ مصلحون لما أفسد الناس، قائمون بدين الله، يدعون من ضلَّ إلى الهدى، ويصبرون منهم على الأذى، ويبصِّرونهم من العمى، وهذه الحالة أعلى حالة يرغب فيها الراغبون، وصاحبها يكون إماماً في الدين؛ إذا جعل عمله خالصاً لربِّ العالمين.
{116} Yeye Mtukufu alipotaja kuangamizwa kwa umma waliowakadhibisha Mitume, na kwamba wengi wao walipotoka wakawaacha watu wa Vitabu vya Mwenyezi Mungu, na hayo yote yanaziangamiza dini na kuzipoteza. Akataja kwamba lau angeweka katika vizazi vilivyopita wenye vyeo na wasaa walio wema ili wawalinganie kwenye uongofu na kukataza uharibifu na kuangamia, na manufaa yao yakapatikana na dini zikabakia wa sababu ya hayo, lakini wao walikuwa wachache sana. Na uhakika wa jambo ni kuwa, wao waliokoka kwa kuwafuata Mitume, na wakayafanya yale waliyoyafanya katika dini yao, na kuwa ni hoja ya Mwenyezi Mungu alioifanyisha katika mikono yao ili aangamie mwenye kuangamia kwa hoja iliyo wazi, na aishi anayeishi kwa hoja iliyo wazi "na" lakini "wale waliodhulumu walifuata yale waliyostareheshwa kwayo." Yaani, walifuata yale waliyo ndani yake ya neema na anasa, wala hawakutafuta badala yake. "Na walikuwa wahalifu;" yaani, walikuwa madhalimu kwa kufuata yale waliyostareheshwa kwayo. Na kwa sababu hiyo walistahiki mateso na adhabu ikawaangamiza. Na katika hili kuna himizo kwa umma huu kwamba kuwe wana ufahamu na heri miongoni mwao wenye kutengeneza yale waliyoyaharibu watu, na kuisimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu, na kumlingania aliyepotea kwenye uwongofu, kuwa na subira juu ya udhia wao, na kuwaonyesha heri kutokana na upofu. Na hali hii ndiyo hali ya juu zaidi wanayoitaka wenye kutaka, na mwenyewe huwa ni imamu katika dini, ikiwa atayafanya matendo yake kwa ajili ya Mola Mlezi wa walimwengu wote peke yake.
{وَمَا كَانَ رَبُّكَ لِيُهْلِكَ الْقُرَى بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا مُصْلِحُونَ (117)}.
117. Wala hakuwa Mola wako Mlezi wa kuiangamiza miji kwa dhuluma tu ilhali watu wake ni watenda mema.
#
{117} أي: وما كان الله ليهلك القرى بظُلم منه لهم والحالُ أنَّهم {مصلحون}؛ أي: مقيمون على الصلاح مستمرون عليه؛ فما كان الله ليهلكهم إلا إذا ظلموا، وقامت عليهم حجَّة الله.
ويُحتمل أنَّ المعنى: وما كان ربُّك لِيُهْلِكَ القرى بظلمهم السابق إذا رجعوا وأصلحوا عملهم؛ فإنَّ الله يعفو عنهم، ويمحو ما تقدَّم من ظلمهم.
{117} Yaani, Mwenyezi Mungu hakuwa ni wa kuiangamiza miji kwa dhuluma kutoka kwake ilhali wao, "ni watenda mema." Yaani, wameshikamana kutengeneza mambo kuwa mazuri na wanadumu katika hilo. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu hakuwa ni wa kuwaangamiza isipokuwa ikiwa watadhulumu na ikawasimamia hoja ya Mwenyezi Mungu juu yao. Na inawezekana kwamba maana yake ni kuwa Mola wako Mlezi hakuwa ni wa kuiangamiza miji kwa dhuluma yao iliyotangulia ikiwa watarejea na kurekebisha matendo yao. Kwa maana, Mwenyezi Mungu atawasamehe na kuwafutia dhuluma yao iliyotangulia.
{وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ النَّاسَ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَا يَزَالُونَ مُخْتَلِفِينَ (118) إِلَّا مَنْ رَحِمَ رَبُّكَ وَلِذَلِكَ خَلَقَهُمْ وَتَمَّتْ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ (119)}
118. Na Mola wako Mlezi angelitaka, angewafanya watu wote wakawa umma mmoja. Lakini hawaachi kuhitalifiana. 119. Isipokuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu. Na kwa hiyo ndiyo Mwenyezi Mungu amewaumba. Na lilitimia neno la Mola wako Mlezi kwamba hakika nitaijaza Jahannam kwa majini na watu kwa pamoja.
#
{118} يخبر تعالى أنه لو شاء لجعل الناس أمَّة واحدة على الدين الإسلامي؛ فإنَّ مشيئته غير قاصرة، ولا يمتنعُ عليه شيءٌ،، ولكنَّه اقتضت حكمته أن لا يزالون مختلفين، مخالفين للصراط المستقيم، متَّبعين السبل الموصلة إلى النار، كلٌّ يرى الحقَّ فيما قاله والضَّلال في قول غيره.
{118} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba lau angetaka, angewafanya watu kuwa umma mmoja kwenye kufuata dini ya Uislamu. Kwani, utashi wake hauna mipaka, na hakuna kinachozuilika Kwake. Bali hekima yake ilihitaji kwamba wasiache kuendelea kutofautiana, wakiihalifu njia iliyonyooka, wakifuata njia zifikishazo Motoni, kila mmoja akiuona ukweli kuwa uko katika yale aliyosema na kwamba upotovu uko katika maneno ya wengineo.
#
{119} {إلاَّ مَن رَحِمَ ربُّك}: فهداهم إلى العلم بالحقِّ والعمل به والاتفاق عليه؛ فهؤلاء سبقت لهم سابقةُ السعادة وتداركتْهم العنايةُ الربَّانية والتوفيق الإلهيُّ، وأما من عداهم؛ فهم مخذولون مَوْكولون إلى أنفسهم. وقوله: {ولذلك خَلَقَهم}؛ أي: اقتضت حكمته أنَّه خلقهم ليكون منهم السعداء والأشقياء والمتفقون والمختلفون والفريق الذي هدى الله والفريق الذي حقت عليهم الضلالة؛ ليتبيَّن للعباد عدلُه وحكمتُه، وليُظْهِر ما كمن في الطباع البشرية من الخير والشرِّ، وليقوم سوقُ الجهاد والعبادات التي لا تتمُّ ولا تستقيم إلا بالامتحان والابتلاء، {و} لأنَّه {تمَّتْ كلمةُ ربِّك لأملأنَّ جهنَّم من الجِنَّة والناس أجمعينَ}: فلا بدَّ أن ييسِّر للنار أهلاً يعملون بأعمالها الموصلة إليها.
{119} "Isipokuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu." Basi akawaongoa kwenye elimu ya Haki, na kuifanyia kazi, na kuafikiana juu yake. Basi hawa yalikwisha watangulia matangulizi ya furaha na wakafikiwa na uangalizi wa kiungu, na kuwezeshwa wa kiungu. Na ama wale wasiokuwa wao, hao waliachiliwa mbali wajisimamie wenyewe.
Na kauli yake: "Na kwa hiyo ndiyo Mwenyezi Mungu amewaumba." Yaani, ilihitaji Hekima yake kuwa aliwaumba ili miongoni mwao kuwe na wenye furaha na walioko mashakani, na wenye kuafikiana na wenye kuhitalifiana, kundi aliloliongoa Mwenyezi Mungu, na kundi ambalo upotevu uliwathibitikia, ili iwabainikie waja uadilifu wake na hekima Yake, na ili ayadhihirishe mazuri na maovu yaliyokuwa yamejificha katika maumbile ya wanadamu, na lisimame suala la jihadi na ibada zisizoweza kukamilika wala kunyooka isipokuwa kwa njia ya mitihani na majaribio "na" kwa sababu "lilitimia neno la Mola wako Mlezi kwamba hakika nitaijaza Jahannam kwa majini na watu kwa pamoja." Basi ni lazima ausahilishie Moto huo wastahiki wake wanaofanya matendo yake yafikishayo humo.
{وَكُلًّا نَقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنْبَاءِ الرُّسُلِ مَا نُثَبِّتُ بِهِ فُؤَادَكَ وَجَاءَكَ فِي هَذِهِ الْحَقُّ وَمَوْعِظَةٌ وَذِكْرَى لِلْمُؤْمِنِينَ (120) وَقُلْ لِلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ اعْمَلُوا عَلَى مَكَانَتِكُمْ إِنَّا عَامِلُونَ (121) وَانْتَظِرُوا إِنَّا مُنْتَظِرُونَ (122) وَلِلَّهِ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَإِلَيْهِ يُرْجَعُ الْأَمْرُ كُلُّهُ فَاعْبُدْهُ وَتَوَكَّلْ عَلَيْهِ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ (123)}.
120. Na yote tunayokusimulia katika habari za Mitume yale tunayokuimarisha kwayo moyo wako. Na katika haya imekujia haki na mawaidha na ukumbusho kwa Waumini. 121. Na waambie wale wasioamini, "Fanyieni mahali penu, nasi hakika pia tunafanya." 122. Na ngojeni, na sisi hakika tunangoja. 123. Na ni ya Mwenyezi Mungu tu ghaibu ya mbinguni na ardhi, na mambo yote yatarejeshwa kwake. Basi muabudu Yeye na umtegemee Yeye. Na Mola wako Mlezi haghafiliki na yale mnayoyatenda.
#
{120} لما ذكر في هذه السورة من أخبار الأنبياء ما ذَكَرَ؛ ذَكَرَ الحكمة في ذِكْر ذلك، فقال: {وكلًّا نَقُصُّ عليك من أنباء الرُّسل ما نثبِّتُ به فؤادك}؛ أي: قلبك؛ ليطمئن، ويثبت، ويصبر كما صبر أولو العزم من الرسل؛ فإنَّ النفوس تأنَس بالاقتداء وتنشَط على الأعمال، وتريد المنافسة لغيرها، ويتأيَّد الحقُّ بذِكْر شواهده وكثرة من قام به. {وجاءك في هذه}: السورة {الحقُّ}: اليقينُ فلا شكَّ فيه بوجهٍ من الوجوه؛ فالعلم بذلك من العلم بالحقِّ الذي هو أكبر فضائل النفوس. {وموعظةٌ وذِكرى للمؤمنينَ}؛ أي: يتَّعظون به فيرتدعون عن الأمور المكروهة ويتذكَّرون الأمور المحبوبة لله فيفعلونها.
{120} Alipotaja katika Sura hii habari za manabii yale aliyotaja, akataja hekima ya kuyataja hayo. Kwa hivyo,
akasema: "Na yote tunayokusimulia katika habari za Mitume yale tunayokuimarisha kwayo moyo wako." Yaani, ili moyo wako utulie, na kuimarika, na usubiri kama wale waliokuwa na azimio kubwa miongoni mwa Mitume walivyokuwa na subira. Kwa maana, nafsi hutulia kwa kuiga wengine, na hupata nguvu ya kufanya matendo, na kutaka kushindana na wengine. Nao ukweli unaungwa mkono kwa kutaja ushahidi wake na idadi nyingi ya wale walioitekeleza. "Na katika haya" yaliyo katika sura hii "imekujia haki" ya yakini, basi hakuna shaka ndani yake kwa namna yoyote ile. Kwa hivyo, kujua haya ni katika kujua haki ambayo ndiyo sifa kuu zaidi ya nafsi. "Mawaidha na ukumbusho kwa Waumini;" yaani, ili waaidhike kwayo kwa hivyo wakakomeka na mambo yanayochukiza, na wanayakumbuka mambo yanayopendwa na Mwenyezi Mungu, kwa hivyo wakayafanya.
#
{121} وأما من ليس من أهل الإيمان؛ فلا تنفعُهم المواعظُ وأنواع التذكير، ولهذا قال: {وقلْ للذينَ لا يؤمنون}: بعدما قامت عليهم الآيات: {اعْمَلوا على مكانتِكُم}؛ أي: حالتكم التي أنتم عليها، {إنَّا عاملونَ}: على ما كنَّا عليه.
{121} Na ama yule ambaye siyo miongoni mwa wenye imani, basi mawaidha hayawafai, na hata aina mbalimbali za ukumbusho. Na ndiyo maana akasema,
"Na waambie wale wasioamini" baada ya kusimamiwa na ishara mbalimbali: "Fanyieni mahali penu;" yaani, katika hali yenu mliyomo, "nasi hakika pia tunafanya" katika hali yetu tuliyomo.
#
{122} {وانتظروا}: ما يحِلُّ بنا، {إنا منتظرون}: ما يحلُّ بكم.
{122} "Na ngojeni" yale yatakayotufika "na sisi hakika tunangoja" yale yatakayowafika nyinyi.
#
{123} وقد فصَل الله بين الفريقين، وأرى عبادَه نَصْرَه لعبادِه المؤمنين، وقَمْعَه لأعداء الله المكذبين. {ولله غيبُ السمواتِ والأرض}؛ أي: ما غاب فيهما من الخفايا والأمور الغيبيَّة، {وإليه يُرْجَعُ الأمرُ كلُّه}: من الأعمال والعمال، فيميز الخبيثُ من الطيِّب، {فاعبُدْه وتوكَّلْ عليه}؛ أي: قم بعبادته، وهي جميع ما أمر الله به مما تقدر عليه. {وتوكَّلْ على الله}: في ذلك.
{وما ربُّك بغافل عما تعملون}: من الخير والشرِّ، بل قد أحاط علمُه بذلك، وجرى به قلمه، وسيجري عليه حكمه وجزاؤه.
{123} Na Mwenyezi Mungu alikwisha pambanua kati ya makundi mawili haya, na akawaonyesha waja Wake nusura yake kwa waje wake Waumini, na ushindi wake dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu wanaomkadhibisha. "Na ni ya Mwenyezi Mungu tu ghaibu ya mbinguni na ardhi;" yaani, yaliyofichikana humo miongoni mwa mambo ya siri na mambo ya ghaibu "na mambo yote yatarejeshwa kwake" miongoni mwa matendo na watendao matendo, kisha apambanue kati ya maovu na mazuri, "Basi muabudu Yeye na umtegemee Yeye." Yaani, mwabuduni Yeye, na hilo ni kwa kufanya mambo yote ambayo Mwenyezi Mungu aliamrisha katika yale unayoweza. "Na mtegemee Mwenyezi Mungu" katika hayo. "Na Mola wako Mlezi haghafiliki na yale mnayoyatenda" ya heri na maovu, bali ameyazunguka hayo yote kwa elimu yake, tayari kalamu yake ilikwisha yaandika, na itapita juu yake hukumu yake na malipo Yake.
Imekamilika tafsiri ya Surat Hud. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu mola Mlezi wa walimwengu wote, na Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Muhammad. Uandishi wake ulikamilika siku ya Jumamosi, tarehe 21 ya mwezi wa Rabi’ al-Akhir katika mwaka wa 1347.
* * *