Tafsiri ya Surat Al-Qari'a
Tafsiri ya Surat Al-Qari'a
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu
{الْقَارِعَةُ (1) مَا الْقَارِعَةُ (2) وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْقَارِعَةُ (3) يَوْمَ يَكُونُ النَّاسُ كَالْفَرَاشِ الْمَبْثُوثِ (4) وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ الْمَنْفُوشِ (5) فَأَمَّا مَنْ ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ (6) فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَاضِيَةٍ (7) وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ (8) فَأُمُّهُ هَاوِيَةٌ (9) وَمَا أَدْرَاكَ مَا هِيَهْ (10) نَارٌ حَامِيَةٌ (11)}.
1. Inayogonga! 2. Nini Inayogonga? 3. Na ni nini kitachokujulisha nini Inayogonga? 4. Siku ambayo watu watakuwa kama nondo waliotawanywa; 5. Na milima itakuwa kama sufi zilizochambuliwa! 6. Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito. 7. Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza. 8. Na yule ambaye mizani zake zitakuwa hafifu. 9. Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya! 10. Na nini kitachokujulisha nini hiyo? 11. Ni Moto mkali!
#
{1 - 3} {القارعةُ}: من أسماء يوم القيامة، سمِّيت بذلك لأنَّها تقرع الناس وتزعِجُهم بأهوالها، ولهذا عظَّم أمرها وفخَّمه بقوله: {القارعةُ. ما القارعةُ. وما أدراكَ ما القارعةُ}.
{1 - 3} "Al-Qari'a"
(Inayogonga!) ni katika majina ya Siku ya Kiyama, iliitwa hivyo kwa sababu itawagonga watu na kuwasumbua kwa hali zake nzito, na ndiyo maana akasisitiza ukubwa wake kwa kauli yake "Inayogonga! Ni nini Inayogonga? Na nini kitachokujulisha nini Inayogonga?"
#
{4} {يومَ يكونُ الناسُ}: من شدَّة الفزع والهول، {كالفراشِ المبثوثِ}؛ أي: كالجراد المنتشر الذي يموج بعضه في بعض، والفراش هي الحيوانات التي تكون في الليل يموج بعضها ببعض، لا تدري أين توجَّه؛ فإذا أوقد لها نارٌ؛ تهافتت إليها لضعف إدراكها، فهذه حال الناس أهل العقول.
{4} "Siku ambayo watu watakuwa" kutokana na hofu na hali nzito "kama nondo waliotawanywa" wanaoingiana wao kwa wao, huwezi kujua wanaelekea wapi, na pindi wanapoashiwa moto, wakaukimbilia kwa sababu ya ufahamu wao dhaifu, na hii ndiyo hali ya watu wenye akili timamu
(siku ya Kiyama).
#
{5} وأما الجبال الصمُّ الصلابُ؛ فتكون {كالعهنِ المنفوشِ}؛ أي: كالصُّوف المنفوش الذي بقي ضعيفاً جدًّا تطير به أدنى ريح؛ قال تعالى: {وترى الجبال تحسبُها جامدةً وهي تمرُّ مرَّ السحابِ}، ثم بعد ذلك تكون هباءً منثوراً، فتضمحلُّ ولا يبقى منها شيءٌ يشاهَد. فحينئذٍ تُنْصَبُ الموازينُ، وينقسم الناس قسمين: سعداء وأشقياء:
{5} Ama milima migumu na imara, hiyo itakuwa "kama sufi zilizochambuliwa." Yaani, kama sufi iliyopeperushwa ambayo inabaki kuwa dhaifu sana na kupeperushwa na upepo mdogo tu.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na utaiona milima unaidhania imetulia; nayo inakwenda kama mwendo wa mawingu" kisha baada ya hayo inakuwa mavumbi yaliyotawanyika, kisha itapotelea mbali na hakuna chochote chake kitakachobakia cha kuonekana. Hapo, mizani zitawekwa mbele,
na watu watagawanyika katika makundi mawili: watu wa furahani na wa mashakani.
#
{6 - 7} {فأمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوازينُه}؛ أي: رجحت حسناتُه على سيئاتِه، {فهو في عيشةٍ راضيةٍ}: في جنَّات النعيم.
{6 - 7} "Basi yule ambaye mizani zake zitakuwa nzito" kwa namna ya kwamba mazuri yake ni mazito kuliko maovu yake, "huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza" katika Bustani za neema.
#
{8 - 11} {وأمَّا من خفَّت مَوازينُه}: بأن لم تكنْ له حسناتٌ تقاوم سيئاتِه، {فأمُّه هاويةٌ}؛ أي: مأواهُ ومسكنُه النارُ التي من أسمائها الهاوية، تكون له بمنزلة الأمِّ الملازمة؛ كما قال تعالى: {إنَّ عذابَها كانَ غَراماً}. وقيل: إنَّ معنى ذلك: فأمُّ دماغه هاويةٌ في النار؛ أي: يُلقى في النار على رأسه، {وما أدراكَ ما هِيَهْ}: وهذا تعظيمٌ لأمرها. ثم فسَّرها بقوله: {نارٌ حاميةٌ}؛ أي: شديدةُ الحرارة، قد زادت حرارتها على حرارة نار الدنيا بسبعين ضعفاً. نستجير بالله منها.
{8 - 11} "Na yule ambaye mizani zake zitakuwa hafifu" kwa sababu hakuwa na matendo mazuri yanayoweza kushinda maovu yake, "huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya" adumu humo milele,
kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: "Hakika adhabu yake ikimpata mtu haimwachi." Pia ilisemwa kwamba maana yake atatupwa motoni juu ya kichwa chake. "Na nini kitachokujulisha ni nini hiyo?" Huku ni kuonyesha ukubwa wa jambo lake.
Kisha akalifafanua hilo kwa kauli yake: "Ni Moto mkali" ambao joto lake ni kubwa mara sabini kuliko joto la moto wa duniani. Tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana nao.
* * *