Tafsiri ya Surat At-Takathur
Tafsiri ya Surat At-Takathur
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu
{أَلْهَاكُمُ التَّكَاثُرُ (1) حَتَّى زُرْتُمُ الْمَقَابِرَ (2) كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ (3) ثُمَّ كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ (4) كَلَّا لَوْ تَعْلَمُونَ عِلْمَ الْيَقِينِ (5) لَتَرَوُنَّ الْجَحِيمَ (6) ثُمَّ لَتَرَوُنَّهَا عَيْنَ الْيَقِينِ (7) ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ (8)}.
1. Kumekushughulisheni kutafuta wingi. 2. Mpaka mje makaburini! 3. Sivyo hivyo! Mtakuja jua! 4. Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua! 5. Sivyo hivyo! Lau mngelijua kwa ujuzi wa yakini. 6. Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu! 7. Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini. 8. Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema.
#
{1} يقول تعالى موبِّخاً عباده عن اشتغالهم عمَّا خُلِقوا له من عبادته وحده لا شريك له ومعرفته والإنابة إليه وتقديم محبَّته على كلِّ شيءٍ: {ألْهاكُمُ}: عن ذلك المذكور، {التَّكاثُرُ}: ولم يذكر المُتَكاثَرَ به؛ ليشمل ذلك كلَّ ما يَتَكاثَرُ به المتكاثرون ويفتخر به المفتخرون؛ من [التكاثر في] الأموال والأولاد والأنصار والجُنود والخدم والجاه وغير ذلك ممَّا يقصد منه مكاثرة كلِّ واحدٍ للآخر، وليس المقصود منه وجه الله.
{1} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu akiwakemea waja wake kwa kujishughulisha kwao mbali na kile walichoumbwa kwa ajili yake cha kumuabudu Yeye peke yake bila mshirika, na kumjua Yeye, na kurejea kwake,
na kutanguliza mapenzi yake juu ya kila kitu: "Kumekushughulisheni" mbali na hicho kilichotajwa, "kutafuta wingi." Hapa hakutaja kile kilichowashughulisha ili hilo lijumuishe kila kitu ambacho watu wanachokitafuta kiwe kingi wakajifahiri kwacho wenye kujifahiri, kama vile kutafuta wingi wa mali, watoto, wasaidizi, askari, watumishi, heshima na mambo mengineyo ambayo kila mtu anakusudia kwayo kutafuta wingi zaidi ya wenzake, na hawakusudii kwayo uso wa Mwenyezi Mungu.
#
{2} فاستمرَّت غفلتكم ولهوتكم وتشاغلكم {حتَّى زُرْتُمُ المقابرَ}: فانكشف حينئذٍ لكم الغطاءُ، ولكنْ بعدَما تعذَّر عليكم استئنافه. ودلَّ قولُه: {حتَّى زرتُم المقابر}: أنَّ البرزخ دارٌ المقصود منها النفوذ إلى الدار الآخرة ؛ لأن الله سمَّاهم زائرين، ولم يسمِّهم مقيمين، فدلَّ ذلك على البعث والجزاء على الأعمال في دار باقيةٍ غير فانيةٍ.
{2} Basi mghafala wenu, na pumbao yenu, na shughuli zenu zikaendelea "Mpaka mje makaburini" ndipo hapo mkafunukiwa na kifuniko, lakini baada ya kutoweza kwenu kukirudisha.
Na iliashiria kauli yake: “Mpaka mje makaburini" kwamba maisha ya kaburini ni maskani ambayo yalikusudiwa kupitia humo ndiyo mtu afike akhera. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwaita wageni, wala hakuwaita wakaaji wa hapo, basi hilo likaashiria kwamba kutakuwepo ufufuo na malipo juu ya vitendo katika makazi ya kudumu, yasiyokwisha.
#
{3 - 6} ولهذا توعَّدهم: {كلاَّ سوف تعلمون. ثم كلاَّ سوف تعلمون. كلاَّ لو تعلمونَ علمَ اليقينِ}؛ أي: لو تعلمون ما أمامكم علماً يصلُ إلى القلوب؛ لما ألهاكم التَّكاثر، ولبادرتم إلى الأعمال الصالحة، ولكن عدم العلم الحقيقيِّ صيَّركم إلى ما ترون، {لَتَرَوُنَّ الجحيم}؛ أي: لَتَرِدُنَّ القيامة، فلَتَرَوُنَّ الجحيم التي أعدَّها الله للكافرين.
{3 - 6} Ndiyo maana akawatishia: "Sivyo hivyo! Mtakuja jua! Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua! Sivyo hivyo! Lau mngelijua kwa ujuzi wa yakini.
" Yaani: Lau mngeyajua yale yaliyo mbele yenu kwa elimu yenye kuzifikia nyoyo zenu; basi kutafuta wingi hakungekushughulisheni, na mngeharakisha kufanya matendo mema, lakini ukosefu wa elimu ya uhakika umekufikisheni kwenye hayo mnayoyaona. "Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu" ambayo Mwenyezi Mungu ameitayarisha kwa ajili ya makafiri mtakapofika siku ya Kiyama.
#
{7} {ثمَّ لَتَرَوُنَّها عين اليقين}؛ أي: رؤيةً بصريةً؛ كما قال تعالى: {ورأى المجرمون النَّارَ فظَنُّوا أنَّهم مُواقِعوها ولمْ يَجِدوا عنها مَصْرِفاً}.
{7} "Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini.
" Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: "Na wahalifu watauona Moto na watajua ya kwamba wao lazima wataingia humo; wala hawatapata pa kuuepukia."
#
{8} {ثم لَتُسْألُنَّ يومئذٍ عن النَّعيم}: الذي تنعَّمتم به في دار الدُّنيا؛ هل قمتم بشكره، وأدَّيتم حقَّ الله فيه، ولم تستعينوا به على معاصيه؛ فينعِّمكم نعيماً أعلى منه وأفضل؟ أم اغتررتُم به، ولم تقوموا بشكره، بل ربَّما استعنتم به على المعاصي ؛ فيعاقبكم على ذلك؟ قال تعالى: {ويومَ يُعْرَضُ الذين كفروا على النارِ أذْهَبْتُم طيباتِكم في حياتكم الدُّنيا واستمتعتم بها فاليوم تُجْزَوْنَ عذاب الهُونِ ... } الآية.
{8} "Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema" mlizokuwa mkijistarehesha kwazo katika maskani ya dunia. Je, mlizishukuru, na mkatimiza haki ya Mwenyezi Mungu ndani yake, na hamkuzitumia katka kumuasi, basi akupeni neema iliyo juu kuliko hiyo na iliyo bora zaidi? Au je, mlidanganywa nazo na hamkumshukuru? Bali labda mlizitumia katika kumuasi,
ndiyo akuadhibuni kwa hayo? Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na siku watakapoletwa wale waliokufuru kwenye Moto wataambiwa: Nyinyi mlitwaa vitu vyenu vizuri katika uhai wa duniani, na mkastareheka navyo. Basi leo ndiyo mnalipwa adhabu ya fedheha..." hadi mwisho wa Aya.
* * *