:
Tafsiri ya Surat Al-Adiyat
Tafsiri ya Surat Al-Adiyat
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
: 1 - 11 #
{وَالْعَادِيَاتِ ضَبْحًا (1) فَالْمُورِيَاتِ قَدْحًا (2) فَالْمُغِيرَاتِ صُبْحًا (3) فَأَثَرْنَ بِهِ نَقْعًا (4) فَوَسَطْنَ بِهِ جَمْعًا (5) إِنَّ الْإِنْسَانَ لِرَبِّهِ لَكَنُودٌ (6) وَإِنَّهُ عَلَى ذَلِكَ لَشَهِيدٌ (7) وَإِنَّهُ لِحُبِّ الْخَيْرِ لَشَدِيدٌ (8) أَفَلَا يَعْلَمُ إِذَا بُعْثِرَ مَا فِي الْقُبُورِ (9) وَحُصِّلَ مَا فِي الصُّدُورِ (10) إِنَّ رَبَّهُمْ بِهِمْ يَوْمَئِذٍ لَخَبِيرٌ (11)}.
1. Ninaapa kwa farasi wendao mbio wakipumua. 2. Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini. 3. Wakishambulia wakati wa asubuhi. 4. Huku wakitimua vumbi. 5. Na wakijitoma kati ya kundi. 6. Hakika mwanadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi! 7. Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo! 8. Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali! 9. Kwani hajui watakapofufuliwa waliomo makaburini? 10. Na yakakusanywa yaliomo vifuani? 11. Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na habari zao wote!
#
{1} أقسم [الله تبارك و] تعالى بالخيل؛ لما فيها من آياتِه الباهرة ونعَمِه الظَّاهرة ما هو معلومٌ للخلق، وأقسم تعالى بها في الحال التي لا يشاركُها فيه غيرها من أنواع الحيوانات، فقال: {والعادياتِ ضَبْحاً}؛ أي: العاديات عدواً بليغاً قويًّا يصدر عنه الضَّبحُ، وهو صوت نَفَسها في صدرها عند اشتداد عَدْوها.
{1} [Mwenyezi Mungu Mtakatifu] na Mtukufu aliapa kwa farasi; kwa sababu ya ishara zake zinazong'aa na neema zake za dhahiri zinazojulikana kwa viumbe, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akaapa kwa hao katika hali ambayo hakuna aina nyingine ya wanyama wanaoshiriki nao, akasema: "Ninaapa kwa farasi wendao mbio wakipumua" kwa pumzi inayosikika.
#
{2} {فالمورياتِ}: بحوافرهنَّ ما يطأنَ عليه من الأحجار، {قَدْحاً}؛ أي: تنقدح النار من صلابة حوافرهنَّ وقوتهنَّ إذا عَدَوْنَ.
{2} "Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini" juu ya mawe wanayoyakanyaga kwa sababu ya kwato zao ngumu.
#
{3} {فالمغيراتِ}: على الأعداء، {صبحاً}: وهذا أمرٌ أغلبيٌّ أنَّ الغارة تكون صباحاً.
{3} "Wakishambulia" maadui "wakati wa asubuhi."
#
{4 - 5} {فأثرنَ به}؛ أي: بعدوهنَّ وغارتهنَّ، {نقعاً}؛ أي: غباراً، {فوسطن به}؛ أي: براكبهنَّ {جمعاً}؛ أي: توسطن به جموع الأعداء الذين أغار عليهم.
{4 - 5} "Huku wakitimua vumbi" juu ya adui zao wanapowavamia. "Na wakijitoma kati ya kundi."
#
{6} والمقسَم عليه قوله: {إنَّ الإنسانَ لربِّه لَكَنودٌ}؛ أي: منوعٌ للخير الذي لله عليه ؛ فطبيعة الإنسان وجِبِلَّتُه أنَّ نفسه لا تسمح بما عليه من الحقوق فتؤديها كاملة موفرة، بل طبيعتها الكسل والمنع لما عليها من الحقوق الماليَّة والبدنيَّة؛ إلاَّ مَن هداه الله وخرج عن هذا الوصف إلى وصف السماح بأداء الحقوق.
{6} Kinachoapwa kwa sababu yake hapa ni kauli yake: “Hakika mwanadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!" Bali maumbile yake ni uvivu na kunyima haki za kimali na za kimwili zilizo juu yake. Isipokuwa wale ambao Mwenyezi Mungu amewaongoza na wakaondoka kwenye sifa hii hadi kwenye sifa ya kuruhusu kutimiza haki.
#
{7} {وإنَّه على ذلك لَشهيدٌ}؛ أي: إن الإنسانَ على ما يعرفُ من نفسه من المنع والكَنَد لشاهدٌ بذلك لا يجحده ولا ينكره؛ لأنَّ ذلك [أمرٌ] بيِّن واضحٌ، ويحتمل أنَّ الضمير عائدٌ إلى الله [تعالى]؛ أي: إنَّ العبد لربِّه لكنودٌ، والله شهيدٌ على ذلك؛ ففيه الوعيد والتهديد الشديد لمَن هو لربِّه كنودٌ بأنَّ الله عليه شهيدٌ.
{7} "Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo." Yaani mtu, licha ya yale anayoyajua yeye mwenyewe ya kuzuia na kutotosheka, ni shahidi mno wa hili na halikatai wala halikanushi. Kwa sababu hilo ni jambo lililo wazi, na inawezekana kwamba maana ya "Yeye" ni Mwenyezi Mungu. Yaani hakika mja ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi, naye Mwenyezi Mungu ni shahidi mno wa hilo. Kwa hivyo maana hii inakuwa na tishio kali kwa yule ambaye ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi kwamba Mwenyezi Mungu ni shahidi mno juu yake.
#
{8} {وإنه}؛ أي: الإنسان {لحبِّ الخير}؛ أي: المال، {لشديدٌ}؛ أي: كثير الحبِّ للمال، وحبُّه لذلك هو الذي أوجب له ترك الحقوق الواجبة عليه؛ قَدَّمَ شهوة نفسه على رضا ربِّه، وكلُّ هذا لأنَّه قصر نظره على هذه الدار، وغفل عن الآخرة.
{8} "Naye;" yaani mwanadamu, "hakika ana nguvu za kupenda mali." Kuipenda kwake huku ndiko kulikomfanya kuacha kutekeleza haki zinazomstahiki kutekeleza. Kwa hivyo akatanguliza matamanio yake kuliko radhi za Mola wake Mlezi, na yote hayo ni kwa sababu aliyaelekeza macho yake katika nyumba hii peke yake, na akapuuza maisha ya Akhera.
#
{9 - 10} ولهذا قال حاثًّا له على خوف يوم الوعيد: {أفلا يعلمُ}؛ أي: هلاّ يعلم هذا المغتر، {إذا بُعْثِرَ ما في القبورِ}؛ أي: أخرج الله الأموات من قبورهم لحشرهم ونشورهم، {وحُصِّل ما في الصُّدور}؛ أي: ظهر وبان ما فيها وما استتر في الصدور من كمائن الخير والشرِّ، فصار السرُّ علانيةً والباطن ظاهراً، وبان على وجوه الخلق نتيجة أعمالهم.
{9 - 10} Ndiyo maana akasema akimhimiza kuiogopa Siku ya Miadi, "Kwani hajui" huyu aliyedanganyika, “watakapofufuliwa waliomo makaburini?" Yaani, Mwenyezi Mungu atakapowatoa wafu makaburini mwao ili awakusanye na kuwafufua, "Na yakakusanywa yaliyomo vifuani" ya heri na ouvu, kwa hivyo siri ikawa kama jambo la dhahiri, nalo la ndani likadhihirika, na matokeo ya matendo yao yakawa wazi mbele ya nyuso za viumbe?
#
{11} {إنَّ ربَّهم بهم يومئذٍ لخبيرٌ}؛ أي: مطلع على أعمالهم الظاهرة والباطنة، الخفيَّة والجليَّة، ومجازيهم عليها، وخصَّ خبرهم بذلك اليوم مع أنه خبيرٌ بهم كلَّ وقتٍ؛ لأنَّ المراد بهذا الجزاء على الأعمال الناشئ عن علم الله واطِّلاعه.
{11} "Kwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na habari zao wote" za dhahiri na zilizofichika, na atawalipa kwa hayo. Na ametaja kwamba anazo habari zote siku hii haswa pamoja na kwamba Yeye anazijua kila wakati, kwa sababu kinachokusudiwa hapa ni kulipa juu ya matendo yanayotokana na elimu na ujuzi wa Mwenyezi Mungu.
* * *