Tafsiri ya Surat Az-Zalzala
Tafsiri ya Surat Az-Zalzala
Ilishuka Madina
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu
{إِذَا زُلْزِلَتِ الْأَرْضُ زِلْزَالَهَا (1) وَأَخْرَجَتِ الْأَرْضُ أَثْقَالَهَا (2) وَقَالَ الْإِنْسَانُ مَا لَهَا (3) يَوْمَئِذٍ تُحَدِّثُ أَخْبَارَهَا (4) بِأَنَّ رَبَّكَ أَوْحَى لَهَا (5) يَوْمَئِذٍ يَصْدُرُ النَّاسُ أَشْتَاتًا لِيُرَوْا أَعْمَالَهُمْ (6) فَمَنْ يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ (7) وَمَنْ يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ (8)}.
1. Itakapotetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake! 2. Na itakapotoa ardhi mizigo yake! 3.
Na mtu akasema: Ina nini? 4. Siku hiyo itahadithia habari zake. 5. Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia! 6. Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao! 7. Basi anayetenda chembe ya wema, atauona! 8. Na anayetenda chembe ya uovu atauona!
#
{1 - 2} يخبر تعالى عمَّا يكون يوم القيامة، وأنَّ الأرض تتزلزل وترجف وترتجُّ حتى يسقطَ ما عليها من بناءٍ ومَعْلَمٍ ، فتندكُّ جبالها، وتسوَّى تلالُها، وتكون قاعاً صفصفاً لا عوج فيه ولا أمتا، {وأخرجت الأرضُ أثقالها}؛ أي: ما في بطنها من الأموات والكنوز.
{1 - 2} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha yatakayotokea Siku ya Kiyama, na kwamba ardhi itatetemeka na kutikisika mpaka majengo yote na alama zilizo juu yake zitaanguka chini, na milima yake itapasuka, na vilima vyake vitasawazishwa na itakuwa tambarare uwanda isiyo na mwinuko wala mdidimio. "Na itakapotoa ardhi mizigo yake" iliyo ndani yake, yaani wafu na hazina.
#
{3} {وقال الإنسان}: إذا رأى ما عراها من الأمر العظيم [مستعظمًا لذلك]: {ما لها}؛ أي: أيُّ شيء عرض لها؟!
{3} "Na mtu akasema" atakapoyaona itakayoyafichua katika mambo makubwa
[akiyaona kwamba ni makubwa mno]: "Ina nini?"
#
{4 - 5} {يومئذٍ تحدِّث}: الأرض {أخبارَها}؛ أي: تشهد على العاملين بما عملوا على ظهرها من خيرٍ وشرٍّ؛ فإن الأرض من جملة الشهود الذين يشهدون على العباد بأعمالهم. ذلك {بأنَّ ربَّك أوحى لها}؛ أي: أمرها أن تخبر بما عمل عليها؛ فلا تعصي لأمره.
{4 - 5} "Siku hiyo" ardhi "itahadithia habari zake" ikishuhudia juu ya watendaji kwa yale ya heri na uovu waliyoyafanya juu ya mgongo wake. Kwani ardhi ni miongoni mwa mashahidi watakaoshuhudia juu ya waja kwa vitendo vyao. Hayo ni "kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia!" Yaani aliiamuru ieleze yaliyofanywa juu yake, na wala haitaasi amri yake.
#
{6} {يومئذٍ يَصْدُرُ الناسُ}: من موقف القيامة [حين يقضي اللَّهُ بينهم] {أشتاتاً}؛ أي: فرقاً متفاوتين، {لِيُرَوْا أعمالَهم}؛ أي: ليريهم الله ما عملوا من السيئات والحسنات ، ويريهم جزاءه موفراً.
{6} "Siku hiyo watu watatoka" kwenye mahali pa Kiyama
[Mwenyezi Mungu atakapohukumu kati yao] "kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao" mabaya na mema, na awaonyeshe malipo yao ya kutimia.
#
{7 - 8} {فمَن يعملْ مثقال ذرَّةٍ خيراً يَرَهُ. ومَن يعملْ مثقال ذرَّةٍ شرًّا يَرَهُ}: وهذا شامل عامٌّ للخير والشرِّ كلِّه؛ لأنَّه إذا رأى مثقال الذَّرَّة التي هي أحقر الأشياء، وجوزي عليها؛ فما فوق ذلك من باب أولى وأحرى؛ كما قال تعالى: {يومَ تجدُ كلُّ نفسٍ ما عملتْ من خيرٍ محضَراً وما عملتْ من سوءٍ تودُّ لو أنَّ بينها وبينه أمداً بعيداً}، {ووجدوا ما عملوا حاضراً}، وهذا فيه الترغيب في فعل الخير، ولو قليلاً، والترهيب من فعل الشر، ولو حقيراً.
{7-8} "Basi anayetenda chembe ya wema, atauona! Na anayetenda chembe ya uovu atauona!" Hili linajumuisha wema na uovu wote. Kwa sababu akiuona uzito wa chembe ambayo ndicho kitu duni zaidi, na akalipwa kwacho, basi kilicho juu ya hicho kinafaa na kustahiki zaidi,
kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Siku ambayo kila nafsi itakuta mema iliyoyafanya yamehudhurishwa, na pia ubaya ilioufanya. Itapenda nafsi lau kungekuwako masafa marefu baina ya ubaya huo na yeye." Pia akasema "Na watayakuta yote waliyoyatenda yamehudhuria hapo." Katika haya kuna kupeana moyo wa kutenda mema, hata ikiwa ni kidogo, na kutishia dhidi ya kufanya maovu, hata yakiwa ni madogo vipi.