:
Tafsiri ya Surat Al-Bayyina
Tafsiri ya Surat Al-Bayyina
Ilishuka Madina
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu
: 1 - 8 #
{لَمْ يَكُنِ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ مُنْفَكِّينَ حَتَّى تَأْتِيَهُمُ الْبَيِّنَةُ (1) رَسُولٌ مِنَ اللَّهِ يَتْلُو صُحُفًا مُطَهَّرَةً (2) فِيهَا كُتُبٌ قَيِّمَةٌ (3) وَمَا تَفَرَّقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَةُ (4) وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ وَذَلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ (5) إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أُولَئِكَ هُمْ شَرُّ الْبَرِيَّةِ (6) إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَئِكَ هُمْ خَيْرُ الْبَرِيَّةِ (7) جَزَاؤُهُمْ عِنْدَ رَبِّهِمْ جَنَّاتُ عَدْنٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ذَلِكَ لِمَنْ خَشِيَ رَبَّهُ (8)}.
1. Hawakuwa waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina waache waliyo nayo mpaka iwajie bayana. 2. Yaani Mtume aliyetoka kwa Mwenyezi Mungu anayewasomea kurasa zilizotakasika. 3. Ndani yake mna maandiko yaliyonyooka. 4. Wala hawakufarikiana waliopewa Kitabu ila baada ya kuwajia hiyo bayana. 5. Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti. 6. Hakika waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina wataingia katika Moto wa Jahannamu wadumu milele humo. Hao ndio viumbe waovu kabisa. 7. Hakika walioamini na wakatenda mema, hao ndio bora wa viumbe. 8. Malipo yao kwa Mola wao Mlezi ni Bustani za daima, zipitazo mito kati yake. Wakae humo milele. Mwenyezi Mungu yu radhi nao, na wao wa radhi naye. Hayo ni kwa anayemwogopa Mola wake Mlezi.
#
{1} يقول تعالى: {لم يكنِ الذينَ كَفَروا من أهلِ الكتابِ}؛ أي: من اليهود والنصارى، {والمشركين}: من سائر أصناف الأمم، {مُنفَكِّينَ}: عن كفرهم وضلالهم الذي هم عليه؛ أي: لا يزالون في غيِّهم وضلالهم، لا يزيدهم مرور الأوقات إلاَّ كفراً، {حتَّى تأتِيَهُم البيِّنةُ}: الواضحة والبرهان الساطع.
{1} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hawakuwa waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu," yaani, kutoka kwa Mayahudi na Manaswara "na washirikina" kutoka katika kila namna ya mataifa; "waache waliyo nayo" ya ukafiri wao na upotofu wao "mpaka iwajie bayana" na hoja iliyo wazi.
#
{2 - 3} ثم فسَّر تلك البيِّنة، فقال: {رسولٌ من اللهِ}؛ أي: أرسله الله يدعو الناس إلى الحقِّ، وأنزل عليه كتاباً يتلوه ليعلِّم الناس الحكمة ويزكِّيهم ويخرجَهم من الظُّلُمات إلى النُّور، ولهذا قال: {يتلو صُحُفاً مطهَّرةً}؛ أي: محفوظةً من قربان الشياطين، لا يمسُّها إلاَّ المطهَّرون؛ لأنَّها أعلى ما يكون من الكلام، ولهذا قال عنها: {فيها}؛ أي: في تلك الصُّحف {كتبٌ قيِّمةٌ}؛ أي: أخبارٌ صادقةٌ وأوامرُ عادلةٌ تهدي إلى الحقِّ وإلى طريقٍ مستقيمٍ؛ فإذا جاءتهم هذه البيِّنة؛ فحينئذٍ يتبيَّن طالب الحقِّ ممَّن ليس له مقصدٌ في طلبه، فيهلك مَن هلك عن بيِّنة ويحيا من حيَّ عن بيِّنةٍ.
{2 - 3} Kisha akaeleza bayana hiyo kwa kusema: "Mtume aliyetoka kwa Mwenyezi Mungu" aliyemtuma kuwalingania watu kwenye haki, na akamteremshia kitabu ili akisome ili awafundishe watu hekima, awatakase, na awatoe gizani awapeleke kwenye nuru, na ndiyo maana akasema: "anayewasomea kurasa zilizotakasika." Yaani, zilizohifadhiwa kutokana na kukaribiwa na mashetani, na hawazigusi isipokuwa waliotakaswa. Kwa sababu ni usemi wa hali ya juu zaidi, na ndiyo maana akasema juu yake: "ndani yake" kurasa hizo "mna maandiko yaliyonyooka." Yaani, habari za ukweli na maamrisho ya uadilifu yanayoongoza kwenye haki na njia iliyonyooka. Kwa hivyo, bayana hii ikiwajia, hapo atabainika ni nani mtafuta haki na yule ambaye hana lengo la kuitafuta, kwa hivyo akaangamia mwenye kuangamia kwa ushahidi wa wazi, na akaishi hai mwenye kuishi kwa ushahidi wa wazi.
#
{4} وإذا لم يؤمن أهل الكتاب بهذا الرسول وينقادوا له؛ فليس ذلك ببدع من ضلالهم وعنادهم؛ فإنَّهم ما تفرَّقوا واختلفوا وصاروا أحزاباً {إلاَّ من بعدِ ما جاءتْهُمُ البيِّنَةُ}: التي توجب لأهلها الاجتماع والاتِّفاق، ولكنَّهم لرداءتهم ونذالتهم لم يزدهم الهدى إلا ضلالاً ولا البصيرة إلا عمىً.
{4} Na ikiwa Watu wa Kitabu hawamuamini Mtume huyu na kumfuata, basi hilo si la kwanza katika upotofu wao na ukaidi wao. Kwani hawakufarikiana na kutofautiana na wakawa makundi "ila baada ya kuwajia hiyo bayana" inayohitaji watu wake kukusanyika pamoja na kuafikiana, lakini kwa sababu ya uduni wao na uovu wao, uwongofu huo haukuwaongeza isipokuwa upotovu, na ufahamu haukuwazidishia isipokuwa upofu.
#
{5} مع أنَّ الكتب كلَّها جاءت بأصل واحدٍ ودين واحدٍ؛ فما {أمِروا} في سائر الشرائع، إلا أن يعبدوا {اللهَ مخلصين له الدِّين}؛ أي: قاصدين بجميع عباداتهم الظَّاهرة والباطنة وجه الله وطلب الزُّلفى لديه، {حنفاءَ}؛ أي: معرضين مائلين عن سائر الأديان المخالفة لدين التَّوحيد، وخصَّ الصلاة والزَّكاة بالذِّكر مع أنَّهما داخلان في قوله: {ليعبدوا الله مخلصين له الدين}؛ لفضلهما وشرفهما وكونهما العبادتين اللتين مَن قام بهما قام بجميع شرائع الدين. {وذلك}؛ أي: التَّوحيد والإخلاص في الدِّين هو {دين القيِّمة}؛ أي: الدين المستقيم الموصل إلى جنَّات النَّعيم، وما سواه فطرقٌ موصلةٌ إلى الجحيم.
{5} Ingawa vitabu vyote vilitoka katika asili moja na dini moja; wao “hawakuamrishwa" katika sheria zote isipokuwa kumwabudu “Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini" na kukusudia katika ibada zao zote za nje na za ndani uso wa Mwenyezi Mungu na kutafuta kuwa karibu mno naye. "Wawe waongofu" kwa kuacha dini zote zinazopingana na dini ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu. Na hapa Mwenyezi Mungu ameitaja swala hasa na zaka ijapokuwa zimejumuishwa katika kauli yake: "ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini" kwa sababu ya fadhila zake na heshima zake na kwa kuwa ndizo ibada mbili ambazo yeyote anayezifanya, basi atatekeleza pia sheria zinginezo zote za dini. "Na hiyo" yaani, kumpwekesha na kumkusudia Yeye tu katika dini ndiyo "Dini madhubuti" yenye kufikisha kwenye mabustani ya neema, na nyinginezo ni njia zinazofikisha kwenye Jahannamu.
#
{6} ثم ذكر جزاء الكافرين بعدما جاءتهم البيِّنة، فقال: {إنَّ الذين كفروا من أهل الكتابِ والمشركينَ في نارِ جهنَّم}: قد أحاط بهم عذابها، واشتدَّ عليهم عقابها، {خالدين فيها}: لا يُفَتَّر عنهم العذاب، وهم فيها مبلسون. {أولئك هم شرُّ البريَّة}: لأنَّهم عرفوا الحقَّ، وتركوه، وخسروا الدُّنيا والآخرة.
{6} Kisha akataja malipo ya makafiri baada ya kuwajia hoja iliyo wazi, akasema: "Hakika waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina wataingia katika Moto wa Jahannamu" ambao adhabu yake kali imewazunguka "wadumu milele humo." Hawatapumzishwa mbali nayo na humo watakata tamaa mno. "Hao ndio viumbe waovu kabisa." Kwa sababu walijua haki, na wakaiacha, na wakaipoteza dunia na Akhera.
#
{7} {إنَّ الذين آمنوا وعملوا الصَّالحات أولئك هم خيرُ البريَّة}: لأنَّهم عبدوا الله وعرفوه، وفازوا بنعيم الدُّنيا والآخرة.
{7} "Hakika walioamini na wakatenda mema, hao ndio bora wa viumbe" kwa sababu walimwabudu Mwenyezi Mungu na wakamjua, na wakapata neema ya dunia na Akhera.
#
{8} {جزاؤهم عند ربِّهم جناتُ عدنٍ}؛ أي: جناتُ إقامةٍ لا ظعن فيها ولا رحيل ولا طلب لغايةٍ فوقَها، {تجري من تحتها الأنهارُ خالدين فيها أبداً رضيَ الله عنهم ورضوا عنه}: فرضي عنهم بما قاموا به من مراضيه، ورضوا عنه بما أعدَّ لهم من أنواع الكرامات [وجزيل المثوبات]. {ذلك}: الجزاء الحسن {لِمَنْ خشيَ ربَّه}؛ أي: لمن خاف الله فأحجم عن معاصيه، وقام بما أوجب عليه.
{8} "Malipo yao kwa Mola wao Mlezi ni Bustani za daima." Hawatatoka humo wala kutafuta kingine cha juu zaidi yake. "Zipitazo mito kati yake. Wakae humo milele. Mwenyezi Mungu yu radhi nao, na wao wa radhi naye." Aliwaridhia kwa yale waliyoyafanya ya kumridhisha, nao wakawa radhi naye kwa aina mbalimbali za mambo matukufu [na malipo mengi] aliyowaandalia. "Hayo" malipo mazuri "ni kwa anayemwogopa Mola wake Mlezi." Yaani, wenye kumhofu Mwenyezi Mungu, kwa hivyo wakajiepusha kumuasi, na wakafanya aliyowafaradhishia.
Imekamilika, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.
* * *