Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu
{إِنَّا أَنْزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ (1) وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ (2) لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِنْ أَلْفِ شَهْرٍ (3) تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِمْ مِنْ كُلِّ أَمْرٍ (4) سَلَامٌ هِيَ حَتَّى مَطْلَعِ الْفَجْرِ (5)}.
1. Hakika Sisi tumeiteremsha Qur-ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu. 2. Na nini kitachokujulisha nini Laylatul Qadri? 3. Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu. 4. Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo. 5. Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.
#
{1} يقول تعالى مبيناً لفضل القرآن وعلوِّ قدره: {إنَّا أنزَلْناهُ في ليلةِ القَدْرِ}: [كما قال تعالى: {إنّا أنزلناه في ليلةٍ مباركة}] وذلك أنَّ الله تعالى ابتدأ بإنزال القرآن في رمضان في ليلة القدر، ورحم الله بها العباد رحمةً عامّةً لا يقدر العباد لها شكراً، وسميت ليلة القدر لعظم قدرها وفضلها عند الله، ولأنَّه يقدِّر فيها ما يكون في العام من الآجال والأرزاق والمقادير القدريَّة.
{1} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu akibainisha ubora wa Qur-
ani na daraja yake ya juu: "Hakika Sisi tumeiteremsha Qur-ani katika Laylatul Qadri
(Usiku wa Cheo Kitukufu)."
[Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: "Hakika tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa."] Na hilo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu alianza kuteremsha Qur-ani katika mwezi wa Ramadhani katika usiku wa huu wa Cheo, na Mwenyezi Mungu akawarehemu waja wake kwa rehema za jumla, ambazo waja hawawezi kuzishukuru. Na imeitwa Laylat al-Qadr kutokana na cheo chake kikubwa na ubora wake mbele ya Mwenyezi Mungu, na kwa sababu Yeye hupitisha ndani yake kitakachotokea katika mwaka mzima miongoni mwa umri mbalimbali, riziki, mipango mbalimbali ya kimungu.
#
{2} ثم فخَّم شأنها وعظَّم مقدارها، فقال: {وما أدراكَ ما ليلةُ القَدْرِ}؛ أي: فإنَّ شأنها جليلٌ، وخطرها عظيمٌ.
{2} Kisha akasisitiza ukubwa wake na kutukuza cheo chake,
akasema: "Na nini kitachokujulisha nini Laylatul Qadri?" Yaani, jambo lake ni kubwa na hatari yake ni kuu.
#
{3} {ليلةُ القدرِ خيرٌ من ألفِ شهرٍ}؛ أي: تعادل من فضلها ألف شهرٍ، فالعمل الذي يقع فيها خيرٌ من العمل في ألف شهرٍ خاليةٍ منها، وهذا مما تتحيَّر فيه الألباب، وتندهش له العقول؛ حيث منَّ [تبارك و] تعالى على هذه الأمَّة الضعيفة، القوَّة والقوى بليلةٍ يكون العمل فيها يقابل ويزيد على ألف شهر، عمر رجل معمَّرٍ عمراً طويلاً نيفاً وثمانين سنةً.
{3} "Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu moja." Yaani, ni sawa na miezi elfu moja katika fadhila zake. Kwa hivyo matendo yanayofanywa ndani yake ni bora zaidi kuliko matendo yanayofanywa ndani ya miezi elfu moja isiyokuwa huo. Na hili ni katika mambo ambayo akili zinachanganyikiwa kwa sababu yake na kustaajabu. Kwa kuwa
[Mwenyezi Mungu mtakatifu] Mtukufu aliuneemesha umma huu dhaifu, nguvu na uwezo katika usiku mmoja tu ambao matendo ya ndani yake ni sawa na au yanazidi matendo ya miezi elfu moja, muda wa maisha ya mtu aliyeishi kwa muda mrefu, miaka themanini na zaidi.
#
{4} {تَنَزَّلُ الملائكةُ والرُّوحُ فيها}؛ أي: يكثر نزولهم فيها، {من كلِّ أمرٍ}.
{4} "Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo" kwa wingi "kwa kila jambo."
#
{5} {سلامٌ هي}؛ أي: سالمةٌ من كل آفةٍ وشرٍّ، وذلك لكثرة خيرها، {حتَّى مطلعِ الفجرِ}؛ أي: مبتداها من غروب الشمس ومنتهاها طلوع الفجر. وقد تواترت الأحاديث في فضلها ، وأنَّها في رمضان، وفي العشر الأواخر منه، خصوصاً في أوتاره، وهي باقيةٌ في كلِّ سنةٍ إلى قيام الساعة، ولهذا كان النبيُّ - صلى الله عليه وسلم - يعتكف ويكثرُ من التعبُّد في العشر الأواخر من رمضان رجاء ليلة القدر. والله أعلم.
{5} "Amani usiku huo" kutokana na kila balaa na uovu, kwa hilo ni kwa sababu ya wingi wa heri zake, "mpaka mapambazuko ya alfajiri." Yaani, huanza kwa kuzama kwa jua na kuisha alfajiri. Zimeripotiwa hadithi nyingi za Mtume kuhusu fadhila zake, na kwamba ni katika Ramadhani na katika siku kumi za mwisho za Ramadhani, hasa katika siku za witiri
(zisizogawanyika mara mbili sawasawa), nao utaendelea kuwepo kila mwaka hadi Saa ya Kiyama, na ndiyo maana Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - alikuwa akifanya itikafu na kufanya ibada kwa nyingi katika kumi la mwisho la Ramadhani, akitarajia kupata Laylat Al-Qadr. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.
* * *