Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu
{اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ (1) خَلَقَ الْإِنْسَانَ مِنْ عَلَقٍ (2) اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ (3) الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ (4) عَلَّمَ الْإِنْسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ (5) كَلَّا إِنَّ الْإِنْسَانَ لَيَطْغَى (6) أَنْ رَآهُ اسْتَغْنَى (7) إِنَّ إِلَى رَبِّكَ الرُّجْعَى (8) أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَى (9) عَبْدًا إِذَا صَلَّى (10) أَرَأَيْتَ إِنْ كَانَ عَلَى الْهُدَى (11) أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَى (12) أَرَأَيْتَ إِنْ كَذَّبَ وَتَوَلَّى (13) أَلَمْ يَعْلَمْ بِأَنَّ اللَّهَ يَرَى (14) كَلَّا لَئِنْ لَمْ يَنْتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ (15) نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ (16) فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ (17) سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ (18) كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِبْ (19)}.
1. Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliyeumba. 2. Amemuumba binaadamu kwa tone la damu. 3. Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! 4. Ambaye amefundisha kwa kalamu. 5. Kamfundisha mtu aliyokuwa hayajui. 6. Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri. 7. Akijiona katajirika. 8. Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo. 9. Umemuona yule anayemkataza. 10. Mja anaposali? 11. Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu? 12. Au anaamrisha ucha Mungu? 13. Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma? 14. Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona? 15. Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele! 16. Shungi la uwongo, lenye makosa! 17. Basi na awaite wenzake! 18. Nasi tutawaita Mazabania! 19. Hasha! Usimtii! Nawe sujudu na ujongee!
#
{1} هذه السُّورة أول السُّور القرآنيَّة نزولاً على رسول الله - صلى الله عليه وسلم -؛ فإنَّها نزلت عليه في مبادئ النبوَّة؛ إذ كان لا يدري ما الكتاب ولا الإيمان، فجاءه جبريل عليه [الصلاة و] السلام بالرِّسالة، وأمره أن يقرأ، فامتنع وقال: ما أنا بقارئٍ! فلم يزل به حتى قرأ ؛ فأنزل اللَّه [عليه]: {اقرأ باسمِ ربِّك الذي خَلَقَ}: عموم الخلق.
{1} Sura hii ndiyo sura ya kwanza ya Qur-ani iliyoteremshwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie. Ilifunuliwa kwake mwanzoni mwa unabii. Hapo, alikuwa hajui Kitabu ni nini wala imani. Basi Jibril, rehema na amani zimshukie, akamjia na ujumbe, na akamuamuru kusoma,
lakini akakataa na akasema: 'Mimi sijui kusoma!' Basi akaendelea naye hivyo mpaka akasoma.
Basi Mwenyezi Mungu akamteremshia: "Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliyeumba" viumbe vyote kwa ujumla.
#
{2} ثم خصَّ الإنسان، وذكرَ ابتداءَ خلقِه {من عَلَقٍ}؛ فالذي خلق الإنسان واعتنى بتدبيره لا بدَّ أن يدبِّره بالأمر والنَّهي، وذلك بإرسال الرسل وإنزال الكتب ، ولهذا أتى بعد الأمر بالقراءة بخلقه للإنسان.
{2} Kisha akamtaja mwanadamu hasa, na akataja mwanzo wa kuumbwa kwake "kwa tone la damu." Basi aliyemuumba mwanadamu na akashughulikia suala la kumsimamia, ni lazima amsimamie kwa kumuamrisha na kumkataza, na hilo ni kwa kutuma Mitume na kuteremsha vitabu, na ndiyo maana akaamrisha kusoma baada ya kutaja kuumba kwake mwanadamu.
#
{3 - 5} ثم قال: {اقرأ وربُّك الأكرمُ}؛ أي: كثير الصِّفات، واسعها، كثير الكرم والإحسان، واسع الجود، الذي من كرمه أن علَّم أنواع العلوم ، و {علَّم بالقلم. علَّم الإنسانَ ما لمْ يعلمْ}: فإنَّه تعالى أخرجه من بطن أمِّه لا يعلم شيئاً، وجعل له السَّمع والبصر والفؤاد، ويسَّر له أسباب العلم؛ فعلَّمه القرآن، وعلَّمه الحكمة، وعلَّمه بالقلم، [الذي به تُحفظ العلوم] وتُضبط الحقوق، وتكون رسلاً للنَّاس تنوب منابَ خطابهم؛ فلله الحمد والمنَّة الذي أنعم على عباده بهذه النِّعم، التي لا يقدرون لها على جزاءٍ ولا شكورٍ، ثمَّ منَّ عليهم بالغنى وسعة الرزق.
{3 - 5} Kisha akasema: "Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!" Yaani, ana sifa nyingi za upana, ni mwingi wa ukarimu na hisani, na ni Mpaji kwa wingi, ambaye katika ukarimu wake ni kwamba alifundisha aina mbalimbali za elimu, na "Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyokuwa hayajui." Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu alimtoa tumboni mwa mama yake ilhali hajui chochote, na akampa uwezo wa kusikia, kuona, na ufahamu wa moyo, na akamwepesishia njia za elimu. Basi akamfundisha Qur-ani, akamfundisha hekima, na akamfundisha kwa kalamu,
[ambayo kwayo zinahifadhiwa elimu] na haki zinawekwa sawasawa, na zinakuwa ni Mitume kwa watu zinazowakilisha mahali pa kuzungumza kwao. Basi sifa njema na neema ni za Mwenyezi Mungu ambaye amewajaalia neema hizi waja wake, ambazo hawawezi kuzilipa wala kushukuru, kisha akawaruzuku mali na riziki nyingi.
#
{6 - 8} ولكن الإنسان لجهله وظلمه؛ إذا رأى نفسه غنيًّا؛ طغى، وبغى، وتجبَّر عن الهدى، ونسي أنَّ لربِّه {الرُّجعى}: ولم يخف الجزاء، بل ربَّما وصلت به الحال أنَّه يترك الهدى بنفسه ويدعو غيره إلى تركه، فينهى عن الصَّلاة التي هي أفضل أعمال الإيمان.
{6 - 8} Lakini mwanadamu, kwa sababu ya ujinga wake na udhalimu wake; akijiona kajitosheleza; kwa hivyo akavuka mipaka, akafanya udhalimu, akajivuna kufuata uwongofu na akasahau kuwa kwa Mola wake Mlezi "ndio marejeo" na wala hakuogopa malipo. Bali huenda akafikia kiwango kwamba yeye mwenyewe aliacha uwongofu na tena akawalingania wengine kuuacha, akawa anakataza watu swala ambayo ndilo tendo bora zaidi la imani.
#
{9 - 14} يقول الله لهذا المتمرِّد العاتي: {أرأيتَ}: أيُّها الناهي للعبد إذا صلَّى، {إنْ كانَ}: العبد المصلِّي {على الهُدى}: العلم بالحقِّ والعمل به، {أو أمر}: غيره {بالتَّقوى}: فهل يحسُنُ أن يُنْهى مَن هذا وصفه؟! أليس نهيه من أعظم المحادَّة لله والمحاربة للحقِّ؟! فإنَّ النَّهي لا يتوجَّه إلاَّ لمن هو في نفسه على غير الهدى، أو كان يأمر غيره بخلاف التقوى، {أرأيتَ إن كذَّبَ}: النَّاهي بالحقِّ، {وتولَّى}: عن الأمر؟ أما يخاف الله ويخشى عقابه؟! {ألمْ يعلمْ بأنَّ اللهَ يرى}: ما يعمل ويفعل.
{9 - 14} Mwenyezi Mungu anamwambia muasi huyu mkaidi: "Umeona" ewe mwenye kumkataza mja anaposwali, "kama yeye" anayeswali "yuko juu ya uwongofu" kujua haki na kuifanyia kazi. "Au anaamrisha" wengine "ucha Mungu?" Basi je ni vyema kumkataza yule ambaye anasifika kwa haya? Je, kumkataza si mojawapo ya matendo makuu ya kumpinga Mwenyezi Mungu na kupigana na haki? Kwani katazo halielekezwi isipokuwa kwa yule ambaye hayuko kwenye uwongofu, au anayeamrisha wengine kinyume cha ucha Mungu. "Umeona" huyu mwenye kukataza haki "kama yeye akikanusha na anarudi nyuma" akaacha amri. Kwani hamuogopi Mwenyezi Mungu na akahofu adhabu yake? "Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona" anayoyafanya na kuyatenda?
#
{15 - 16} ثم توعَّده إن استمرَّ على حاله، فقال: {[كلاَّ] لئن لم ينتَهِ}: عمَّا يقول ويفعل، {لَنَسْفَعَاً بالنَّاصيةِ}؛ أي؛ لَنأخُذنَّ بناصيته أخذاً عنيفاً، وهي حقيقةٌ بذلك؛ فإنَّها {ناصيةٌ كاذبةٌ خاطئةٌ}؛ أي: كاذبةٌ في قولها، خاطئةٌ في فعلها.
{15 - 16} Kisha akamtishia ikiwa ataendelea kuwa hivyo,
akasema: "Kwani! Kama haachi" hayo anayoyasema na kuyatenda, "tutamkokota kwa shungi la nywele" kwa ukali, nalo ni jambo la uhakika. Kwa maana ni "Shungi la uongo, lenye makosa." Ni la uongo katika kile linachosema, na lenye makosa katika kile linachofanya.
#
{17 - 18} {فَلْيَدْعُ}: هذا الذي حقَّ عليه العذابُ {نادِيَهُ}؛ أي: أهل مجلسه وأصحابه ومن حوله ليُعينوه على ما نزل به، {سنَدْعو الزَّبانيةَ}؛ أي: خزنة جهنَّم لأخذه وعقوبته. فلينظر أيُّ الفريقين أقوى وأقدر. فهذه حالة الناهي وما توعد به من العقوبة.
{17 - 18} "Basi na awaite" huyu aliyestahiki adhabu "wenzake." Yaani, watu wa baraza lake, na sahibu zake, na wote walio karibu naye ili wamsaidie katika yale yaliyomfika. "Nasi tutawaita Mazabania!" Yaani, walinzi wa Jahannam ili wamchukue na kumuadhibu. Basi na atazame ni lipi kati ya vikundi viwili hivi ni lenye nguvu na uwezo zaidi. Basi hii ndiyo hali ya mkatazaji huyu na adhabu anayoahidiwa.
#
{19} وأمَّا حالة المنهيِّ؛ فأمره الله أن لا يصغي إلى هذا الناهي، ولا ينقاد لنهيه، فقال: {كلاَّ لا تُطِعْهُ}؛ أي: فإنَّه لا يأمر إلاَّ بما فيه الخسار ، {واسجُدْ}: لربِّك، {واقْتَرِبْ}: منه في السُّجود وغيره من أنواع الطاعات والقُرُبات؛ فإنَّها كلها تدني من رضاه وتقرِّب منه. وهذا عامٌّ لكلِّ ناهٍ عن الخير ولكلِّ منهيٍّ عنه، وإن كانت نازلةً في شأنِ أبي جهل حين نهى رسول الله - صلى الله عليه وسلم - عن الصلاة وعذَّبه وآذاه.
{19} Ama hali ya anayekatazwa, Mwenyezi Mungu alimuamrisha kwamba asimsikilize huyu anayemkataza, wala asifuate makatazo yake,
akasema: "Hasha! Usimtii!" Kwani haamrishi isipokuwa yenye hasara. "Nawe sujudu" kwa ajili ya Mola wako Mlezi, "na jikurubishe" kwake katika kusujudu na aina nyenginezo za utiifu na kujikurubisha kwake. Hayo yote humleta mtu karibu na radhi zake na kumleta karibu naye. Hili ni la jumla kwa kila mwenye kukataza heri na kwa kila mwenye kukatazwa heri, hata ikiwa sura hii iliteremka kwa sababu ya kisa cha Abu Jahl pale alipomkataa Mtume wa Mwenyezi - rehema na amani zimshukie – kuswali, akamtesa na kumuudhi.
Imekamilika, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
* * *