Ilishuka Madina
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu
{قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ (1) مَلِكِ النَّاسِ (2) إِلَهِ النَّاسِ (3) مِنْ شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ (4) الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ (5) مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ (6)}.
1.
Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanadamu. 2. Mfalme wa wanadamu. 3. Mungu wa wanadamu. 4. Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas. 5. Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu. 6. Kutokana na majini na wanadamu.
#
{1 - 6} وهذه السورة مشتملةٌ على الاستعاذة بربِّ النَّاس ومالكهم وإلههم من الشيطان، الذي هو أصل الشُّرور كلِّها ومادتها، الذي من فتنته وشرِّه أنَّه يوسوس في صدور النَّاس؛ فيحسِّن لهم الشرَّ، ويريهم إيَّاه في صورة حسنةٍ، وينشِّط إرادتهم لفعله، ويثبِّطهم عن الخير ، ويريهم إيَّاه في صورةٍ غير صورتِه، وهو دائماً بهذه الحال، يوسوس ثم يخنُسُ؛ أي: يتأخَّر عن الوسوسة إذا ذكر العبد ربَّه واستعان [به] على دفعه؛ فينبغي له أن يستعين ويستعيذ ويعتصم بربوبيَّة الله للناس كلِّهم، وأنَّ الخلق كلَّهم داخلون تحت الرُّبوبيَّة والملك، فكلُّ دابَّةٍ هو آخذٌ بناصيتها، وبألوهيَّته التي خلقهم لأجلها؛ فلا تتمُّ لهم إلاَّ بدفع شرِّ عدوِّهم الذي يريد أن يقتَطِعَهم عنها ويحول بينهم وبينها، ويريد أن يجعلهم من حزبِه؛ لِيكونوا من أصحاب السعير، والوسواس كما يكون من الجنِّ يكون من الإنس، ولهذا قال: {من الجِنَّةِ والنَّاسِ}.
{1 - 6} Sura hii inajumuisha kutafuta hifadhi kwa Mola Mlezi wa watu, Mmilki wao, na Mungu wao kutokana na Shetani, ambaye ndiye asili na kiini cha maovu yote, ambaye katika majaribio yake na uovu wake ni kwamba anatia wasiwasi katika nyoyo za watu. Akawa anawafanyia uovu kuwa mzuri na akaukakamua utashi wao kuufanya, na anawakatisha tamaa ya kufanya wema, na anawaonyesha wema huo kwa sura isiyo yake, na yeye huwa katika hali hii kila wakati, akiwatia wasiwasi kisha anajifcha mja anapomkumbuka Mola wake Mlezi na akaomba kinga yake katika kumzuia. Kwa hivyo mja atafute msaada na atake hifadhi kwa umola wa Mwenyezi Mungu kwa watu wote, na kwamba viumbe vyote vimejumuishwa chini ya umola wake na ufalme wake. Kwa hivyo Yeye amekishika kila kiumbe kwa nywele za utosini, na kwa uungu wake ambao kwa ajili yake amewaumba. Hayawatimii isipokuwa kwa kuwazuilia shari ya adui yao, ambaye anataka kuwakata mbali nayo na kuwazuia mbali nayo, na anataka kuwafanya kuwa katika kundi lake. Ili wawe miongoni mwa wakazi wa Moto wenye mwako mkali. Na kama vile wasiwasi hutokana na majini, pia hutokana na watu, na ndiyo maana akasema "kutokana na majini na wanadamu."
Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, mwanzoni na mwishoni, kwa dhahiri na kwa siri, na tunamuomba Mwenyezi Mungu atutimizie neema zake, na atusamehe dhambi zetu ambazo zimetuzuilia baraka zake nyingi, na makosa na matamanio ambayo yazizuia nyoyo zetu kutafakari ishara zake. Tunatarajia na kutumaini kwamba asitunyime heri aliyo nayo kwa sababu ya uovu wetu. Kwani hawakati tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu isipokuwa watu makafiri, na wala hawakati tamaa na rehema yake isipokuwa waliopotea. Na rehema na amani ziwe juu ya Mtume wake Muhammad na ahali wake na maswahaba wake wote. Rehema na amani idumuyo milele, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, ambaye kwa neema yake matendo mema yanatimia. Imekamilika tafsiri ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa msaada wake na kuwezesha kwake kuzuri, kwa mkono wa mtungaji wake na mwandishi wake, Abdur-Rahman bin Naswir bin Abdalla, anayejulikana kama Ibn Saadi. [Mwenyezi Mungu amsamehe yeye, wazazi wake na Waislamu wote]. Kuandikwa kwake kulifanyika tarehe saba, mwezi wa Shaban mwaka wa 1345 Hijria. Mola wetu Mlezi, tukubalie na utusamehe. Hakika wewe ndiye Mwenye kusamehe mno, Mwingi wa kurehemu.