:
Tafsiri ya Surat Quraysh
Tafsiri ya Surat Quraysh
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu
: 1 - 4 #
{لِإِيلَافِ قُرَيْشٍ (1) إِيلَافِهِمْ رِحْلَةَ الشِّتَاءِ وَالصَّيْفِ (2) فَلْيَعْبُدُوا رَبَّ هَذَا الْبَيْتِ (3) الَّذِي أَطْعَمَهُمْ مِنْ جُوعٍ وَآمَنَهُمْ مِنْ خَوْفٍ (4)}
1. Kwa walivyozoea Maqureshi. 2. Kuzoea kwao safari za siku za baridi na siku za joto. 3. Basi na wamuabudu Mola Mlezi wa Nyumba hii. 4. Ambaye anawalisha wasipate njaa, na anawalinda na hofu.
#
{1 - 4} قال كثيرٌ من المفسِّرين: إنَّ الجارَّ والمجرور متعلِّقٌ بالسورة التي قبلها؛ أي: فعلنا ما فعلنا بأصحاب الفيل؛ لأجل قريشٍ وأمنهم واستقامة مصالحهم وانتظام رحلتهم في الشتاء لليمن وفي الصيف للشام لأجل التِّجارة والمكاسب. فأهلك الله من أرادهم بسوءٍ، وعظم أمر الحرم وأهله في قلوب العرب، حتى احترموهم، ولم يعترضوا لهم في أيِّ سفرٍ أرادوا، ولهذا أمرهم الله بالشكر، فقال: {فَلْيَعْبُدوا ربَّ هذا البيتِ}؛ أي: ليوحِّدوه ويُخْلِصوا له العبادة، {الذي أطْعَمَهُم من جوعٍ وآمَنَهُم من خوفٍ}: فرغدُ الرِّزق والأمن من الخوف من أكبر النِّعم الدنيويَّة الموجبة لشكر الله تعالى. فلك اللهمَّ الحمد والشُّكر على نعمك الظَّاهرة والباطنة. وخصَّ الله الربوبيَّة بالبيت لفضله وشرفه، وإلاَّ؛ فهو ربُّ كلِّ شيءٍ.
{1 - 4} Wafasiri wengi walisema kwamba neno "kwa" na maneno ya baada yake yanahusiana na sura iliyoko kabla ya sura hii. Yaani, tuliwafanyia watu wa tembo yale tuliyowafanyia kwa ajili ya Maquraishi, usalama wao, kuweka sawa masilahi yao, na kuweka nidhamu iliyo kwa ajili ya safari zao wakati wa kipupwe kwenda Yemen na wakati wa kiangazi kwenda Sham, kwa ajili ya biashara na kuchuma. Basi Mwenyezi Mungu akawaangamiza wale waliowatakia mabaya, na akalifanya suala la Msikiti Mtakatifu na pia watu wake kuwa kubwa katika nyoyo za Waarabu, mpaka wakawaheshimu na hawakupingana nao katika safari yoyote waliyoitaka, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akawaamrisha kushukuru, akasema: "Basi na wamuabudu Mola Mlezi wa Nyumba hii" na wamkusudie Yeye tu katika ibada. "Ambaye anawalisha wasipate njaa, na anawalinda na hofu." Kwani wingi wa riziki na usalama kutokana na hofu ni miongoni mwa neema kubwa za kidunia zinazohitaji kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu. Basi ewe Mwenyezi Mungu sifa njema na shukrani ni zako kwa sababu ya neema zako zilizo dhahiri na zilizofichika. Na hapa Mwenyezi Mungu ametaja umola wake kwa Nyumba Tukufu kwa sababu ya fadhila zake na utukufu wake, vinginevyo; Yeye ndiye Mola Mlezi wa kila kitu.
* * *