Tafsiri ya Surat Al-Humaza
Tafsiri ya Surat Al-Humaza
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu
{وَيْلٌ لِكُلِّ هُمَزَةٍ لُمَزَةٍ (1) الَّذِي جَمَعَ مَالًا وَعَدَّدَهُ (2) يَحْسَبُ أَنَّ مَالَهُ أَخْلَدَهُ (3) كَلَّا لَيُنْبَذَنَّ فِي الْحُطَمَةِ (4) وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْحُطَمَةُ (5) نَارُ اللَّهِ الْمُوقَدَةُ (6) الَّتِي تَطَّلِعُ عَلَى الْأَفْئِدَةِ (7) إِنَّهَا عَلَيْهِمْ مُؤْصَدَةٌ (8) فِي عَمَدٍ مُمَدَّدَةٍ (9)}
1. Ole wake kila safihi, msengenyaji! 2. Aliyekusanya mali na kuyahesabu. 3. Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele! 4. Hasha! Atavurumishwa katika Hut'ama. 5. Na nani atakujuvya ni nini Hut'ama? 6. Moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa. 7. Ambao unapanda nyoyoni. 8. Hakika huo utafungiwa nao. 9. Kwenye nguzo zilizonyooshwa.
#
{1} {ويلٌ}؛ أي: وعيدٌ ووبالٌ وشدَّة عذابٍ، {لكلِّ هُمَزَةٍ لُمَزَةٍ}؛ أي: الذي يهمز الناس بفعله ويلمزهم بقوله؛ فالهمَّاز: الذي يَعيبُ الناس ويطعُنُ عليهم بالإشارة والفعل، واللَّمَّاز: الذي يعيبهم بقوله.
{1} "Ole wake." Yaani, hili ni tishio kali la adhabu kwa "kila safihi, msengenyaji" ambaye huwabeza watu kwa vitendo vyake na kuwatweza kwa maneno yake.
#
{2} ومن صفة هذا الهمَّازِ [اللَّمَّازِ] أنَّه لا همَّ له سوى جمع المال وتعديده والغبطة به، وليس له رغبةٌ في إنفاقه في طرق الخيرات وصلة الأرحام ونحو ذلك.
{2} Miongoni mwa sifa za mtwezaji huyu kwa vitendo na kauli ni kuwa hana jambo muhimu isipokuwa kukusanya mali, kuzihesabu na kufurahia kwazo, na hana hamu ya kuzitumia katika mambo ya heri, kudumisha mafungamano ya kifamilia na mfano wa hayo.
#
{3} {يحسبُ}: بجهله {أنَّ ماله أخْلَدَهُ}: في الدُّنيا، فلذلك كان كدُّه وسعيه [كلُّه] في تنمية ماله، الذي يظنُّ أنَّه ينمي عمره، ولم يدرِ أن البخل يقصف الأعمار ويخرب الديار، وأن البرَّ يزيد في العمر.
{3} "Anadhani" kutokana na ujinga wake "ya kuwa mali yake yatambakisha milele" katika dunia hii, na ndiyo maana taabu yake na juhudi zake zote zilikuwa katika kukuza mali yake, ambayo anadhania kuwa inamwongezea umri wake, wala hakutambua kwamba ubahili huharibu umri na kubomoa makazi, na kwamba wema huongeza umri.
#
{4 - 7} {كلاَّ لَيُنبَذَنَّ}؛ أي: ليطرحنَّ {في الحُطَمَةِ. وما أدراك ما الحُطَمَةُ}: تعظيمٌ لها وتهويلٌ لشأنها. ثم فسَّرها بقوله: {نار الله الموقَدة}: التي وقودها الناس والحجارة، {التي}: من شدَّتها {تطَّلع على الأفئدة}؛ أي: تنفذ من الأجسام إلى القلوب.
{4 - 7} "Hasha! Atavurumishwa katika Hut'ama.Na nani atakujuvya ni nini Hut'ama?" Hii ni mbinu ya kuonyesha ukubwa na ukali wa jambo lake.
Kisha akaifafanua kwa kauli yake: "Moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa." Ambao kuni zake ni watu na mawe. "Ambao" kutokana na ukali wake "unapanda nyoyoni."
#
{8 - 9} ومع هذه الحرارة البليغة، هم محبوسون فيها، قد أيسوا من الخروج منها، ولهذا قال: {إنَّها عليهم مؤصدةٌ}؛ أي: مغلقة، {في عَمَدٍ}: من خلف الأبواب، {ممدَّدةٍ}: لئلا يخرجوا منها؛ {كلَّما أرادوا أن يخرجوا منها أعيدوا فيها}، نعوذ بالله من ذلك، ونسأله العفو والعافية.
{8 - 9} Na pamoja na joto hili kali, watanaswa humo, na watakuwa wamekata tamaa mno ya kutoka humo,
na ndiyo maana akasema: "Hakika huo utafungiwa nao. Kwenye nguzo zilizonyooshwa" nyuma ya milango yake; ili wasitoke humo. "Kila wakitaka kutoka humo, watarudishwa humo humo." Tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na hayo, na tunamuomba msamaha na salama.
* * *